Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu, libarikiwe, karibu katika kujifunza maandiko.
Leo tutajifunza swali la msingi na la muhimu, linalozunguka katika vichwa vya watu wengi, walio wakristo na wasio wa kristo, na swali lenyewe ndio hili> Je chanjo ya Korona/corona ndio chapa ya mnyama yenyewe au ni kitu kingine?
Ili kupata jibu la swali hili vizuri, ni vyema kwanza kujua maana ya chapa na lengo la chapa!. Chapa maana yake ni lebo, au utambulisho. Kitu kilichotiwa chapa maana yake kimewekwa utambulisho wa hicho kitu, kwamfano bidhaa Fulani inayouzwa katika duka, ni lazima iwe na chapa au lebo, lengo la hiyo lebo/chapa ni kuitambulisha ile bidhaa Mmiliki wake pamoja na asili yake na vile vile ni nembo ya hati miliki ya wenye bidhaa.
Na kawaida chapa, au nembo ya bidhaa inawekwa mwishoni kabisa mwa bidhaa ile inapokamilika kutengenezwa, na huwa haiwekwagi mwanzoni mwa bidhaa ile inapotengenezwa.
Kadhalika, biblia imetabiri, kipindi kifupi sana kabla ya dunia kuisha, Shetani atawatia alama/nembo watu wake. Ili kwamba ithibitike kuwa wao ni milki yake ya halali, na hatua ya kutiwa chapa ni hatua ya mwisho kabisa ya uthibitisho wa mtu kwa shetani. Maana yake ni kwamba mpaka mtu aipokee chapa, tayari alikuwa katika kuandaliwa na shetani muda mrefu, hivyo sio jambo la kufumba na kufumbua tu.
Maana yake ni kwamba wote watakaoipokea chapa, ni sawa na mtu aliyemaliza kuiandika barua, anamalizia na sahihi tu pale chini!, ile sahihi ndio chapa!, lakini habari yenyewe sio ile sahihi bali ni ule ujumbe!.. kadhalika chapa!, ni sahihi tu ya uhalali wa mtu kwa shetani. Msingi huu utatusaidia kujua kuwa chapa ya mnyama sio jambo la kwanza kumtambulisha mtu kuwa ni milki ya shetani, bali ni jambo la mwisho!. Kwasababu kama ingekuwa ni jambo la kwanza, wapo watu waliokufa na hali hawana hiyo chapa ya mnyama na bado walikuwa ni milki ya shetani, na siku ya mwisho wataingia katika ziwa la moto!. Hivyo jambo la kuogopa sasa sio hiyo chapa inayokuja ambayo ni 666, bali ni kujiupusha na shetani muda huu na kazi zake zote, kwa kumpokea Bwana Yesu, na kubatizwa katika ubatizo sahihi na kuishi maisha matakatifu.
Kwa kufanya hivyo utakuwa umejitoa kabisa kwenye mkondo wa watu wa Yule mwovu, na wanaotengenezwa kuwa wake, na mwisho kutiwa chapa yake.
Sasa tukirudi kwenye swali letu, linalouliza, Je! Chanjo ya Corona ni alama ya mnyama au ni kitu kingine?. Jibu ni kwamba chanjo ya corona sio chapa ya mnyama!.. Isipokuwa inatangaza ujio wa chapa ya mnyama.
Katika maandiko tunasoma kulikuwepo na matukio ambayo yalikuwa yanatangulia kutokea, ambayo yalikuwa yanatangaza ujio wa tukio Fulani kubwa mbeleni. Kwamfano utaona janga mafuriko ya gharika ya Nuhu, ambayo yalitokea duniani kutokana na maasi ya wanadamu, na janga lile likafuta idadi kubwa karibia yote ya watu duniani… Kwa janga lile kubwa ijapokuwa liliangamiza na kubakisha watu nane tu!.. Lakini bado mwisho wa dunia ulikuwa haujafika!.
Lakini tukio lile lilikuwa linatangaza au kuhubiri jinsi mwisho wa dunia utakavyokuwa… Kwamba siku moja kabla mwisho wa dunia kufika, siku hizo zitafanana sana na siku za Nuhu,.. maasi yataongezeka, na vile vile dunia itaharibiwa yote kwa moto (2Petro 3:6), kama ilivyoharibiwa kwa maji kipindi cha Nuhu.
Mathayo 24:37 “Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
38 Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina,
39 wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu”
Vile vile hii chanjo ya korona sio chapa ya mnyama, bali inatangaza habari za chapa ya mnyama ambayo ipo mbioni kuja.. Kama vile gharika ya Nuhu inavyotangaza au kuhubiri gharika ya moto inatakayokuja mwisho wa dunia.
Kwahiyo tunaweza kuisema hii mithali na sisi “kama ilivyokuwa siku za chanjo ya Korona”.. “ndivyo itakavyokuwa siku za chapa ya mnyama”.. Kama ilivyokuwa siku za chanjo ya Korona, watu walikuwa hawawezi kusafiri sehemu baadhi, au kufanya shughuli Fulani bila kuwa na hiyo chanjo, ndivyo itakavyokuwa siku za ile chapa ya mnyama zitakapotimia.. katika siku hizo watu hawataweza kununua wala kuuza, wala kufanya biashara yoyote bila kuwa na chapa hiyo ya mnyama katika vipaji vya nyuso zao na katika mikono yao ya kuume.
Kwahiyo Chanjo ya Korona, wala ugonjwa wa korona sio chapa ya mnyama.
Sasa unaweza kuuliza ni kwanini isiwe chapa ya mnyama?. Maandiko yametupa majibu yote jinsi chapa ya mnyama itakavyokuwa na itakavyotenda kazi. Hivyo tukitumia maandiko tunaweza kupata majibu yote na kutusaidia kutoyumbishwa na upepo wowote wa elimu unaokuja mbele yetu sawa sawa na Waefeso 4: 14…
Waefeso 4: 14 “ ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu” (www wingulamashahidi org)
Sasa mambo yafuatayo ndiyo yatakayoitambulisha Chapa ya Mnyama.
Hili ni jambo la kwanza ambalo kila mkristo anapaswa alifahamu. Chapa ya mnyama haiwezi kufanya kazi kabla ya kanisa la Kristo kunyakuliwa. Baada ya watakatifu kuondolewa duniani kwa tendo maarufu lijulikanalo kama unyako, ndipo chapa ya mnyama itakapoanza kutenda kazi..
Na sasa (wakati huu tunaoishi) kanisa bado halijanyakuliwa, watakatifu bado wapo duniani. Na maandiko yanasema kanisa la Kristo ndilo linaloizuia ile siku isifike, kwasababu ndilo lenye Roho Mtakatifu.. Hivyo siku litakapoondolewa ndipo yule mpinga-kristo atanyanyuka na kuihimiza chapa yake..
2Wathesalonike 2:5 “Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?
6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.
7 Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa. 8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake”
Hili ni jambo la pili ambalo kila mkristo anapaswa alifahamu….
Huyu mpinga-Kristo biblia inamtaja kama ASI, au MWANA WA UHARIBIFU.
Maandiko yanasema hivyo katika kitabu cha…
2Wathesalonike 2:3 “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; AKAFUNULIWA YULE MTU WA KUASI, MWANA WA UHARIBIFU;
4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.
5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?
6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake”.
Na mpaka sasa ofisi atakayotokea Mpinga-kristo imeshajulikana (ni ofisi ya kipapa, kulingana na maandiko), lakini kwamba ni papa yupi, bado haijajulikana.. Na wakati chapa ya mnyama inazinduliwa duniani kote, biblia inasema mpinga kristo atakuwa ameshapata nguvu duniani kote, na kupewa nguvu na mataifa yote, na ndiye atakayeiratibu na kuihimiza, na vile vile atakuwa ameshajiweka tayari kutaka kuabudiwa kama Mungu. Jambo ambalo mpaka sasa halijatimia…ingawa lipo mbioni sana kutimia baada ya unyakuo wa kanisa kupita.
Hili ni jambo la tatu na la muhimu pia kila mkristo kufahamu. Dhiki kuu ya mpinga Kristo itadumu kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu, yaani miezi 42 (Ufunuo 13:5). Na tendo la watu kulazimishwa kuipokea chapa, litakuwa ni tendo la haraka sana na lenye kuchukua muda mfupi, ili kuiruhusu ile dhiki kwa miaka mitatu na nusu. Maana yake ni kwamba wakati chapa inazinduliwa, kitakuwa ni kitendo cha muda mfupi na cha shinikizo kubwa sana..haitachukua miaka au mwezi, kukamilisha zoezi hilo.. kama sasa inavyofanyika katika chanjo.
Sasa hebu jiulize, tangu huu ugonjwa wa Korona umetokea ni miaka mingapi imepita?.. Na tangu chanjo ziache kutolewa ni muda gani umepita?, na mpaka zoezi hili limalizike kwa watu wote, maana yake kila mtu awe amechagua kupokea au kutokupokea itachukua muda gani?, huoni ni jambo ambalo litachukua muda mrefu sana, pengine hata linaweza kuchukua miaka zaidi ya miaka miwili au mitatu mbeleni au hata zaidi ya hapo?..Sasa endapo likichukua miaka miwili mbeleni muda wa dhiki kuu utapatikana wapi?, muda wa vile vitasa saba vya ufunuo 16 utapatikana wapi?.
Umeona?.. kwahiyo hii chanjo sio chapa ya mnyama?.. chapa ya mnyama itakapoanza kufanya kazi itakuwa ni kipindi kifupi sana, kila mtu duniani ambaye hakwenda kwenye unyakuo atakuwa ameshachagua aidha kuipokea au kutoipokea, pengine zoezi hilo litaendeshwa chini ya mwezi mmoja tu!.. ili kuruhusu muda wa dhiki kuu ya miaka mitatu na nusu kwa wale ambao wataikataa. (tembelea www wingulamashahidi org)
Hili ni jambo la Nne na la mwisho ambalo kila mkristo anapaswa alifahamu. Chapa haitaletwa duniani kutokana na matatizo ya kiafya wala kiuchumi. Hapana!… Sababu kubwa ya chapa ya mnyama italetwa kutokana na masuala ya kiimani.. Yaani kile watu wanachokiamini na kukiabudu!… (Hicho ndicho kiini cha ile chapa).
Maana yake ni kwamba kipindi kifupi sana kabla ya chapa hiyo kuzinduliwa, shetani atanyanyua majanga na matatizo mengi ambayo yatakuwa yanasababishwa na imani za watu, vikundi kama vya kigaidi kama ISIS, BOKOHARAM, ANTI-BALAKA, ALQAEDA, ALSHABAAB n.k vitanyanyuka kwa kasi na kuleta shida kubwa sana duniani kote..vile vile manabii wengi wa uongo wataleta shida kubwa sana duniani kwa kufanya vitu vya ajabu na vyenye kutishia amani ya dunia.
Kutokana na hilo basi, dunia itatafuta mtu mmoja na taasisi moja maarufu ambayo inaweza kutoa mashauri na hata kutatua hayo matatizo, ndipo hapo atatafutwa mtu wa kidini mwenye ushawishi mkubwa kuliko wote, na mwenye nguvu kiusemi. Na huyo dunia nzima itamwamini na kumpa nguvu. Kiongozi huyo wa juu sana wa kidini, ndipo atakuja na wazo la namna ya kushughulikia kutatua matatizo hayo ya kiimani, ndipo atatoa wazo la kila mtu kusajiliwa katika Kanisa, au msikiti, au taasisi yoyote ambayo ipo chini ya mfumo wake huo. (www wingulamashahidi org)
Na yeyote ambaye atakosa au kuukataa huo utambulisho basi hataweza kuuza wala kununua wala kufanya shughuli yoyote, na zaidi ya yote ndiye atakayeonekana anachafua amani ya dunia. Na hivyo atakamatwa kwa kipindi kifupi sana na kupelekwa katika magereza maalumu, ambapo huko atapitia dhiki ambayo biblia inasema haijawahi kuwepo wala haitakuwepo baada ya hapo, kwa muda wa miaka mitatu na nusu na ndipo atakufa… Wakati wengine waliosalia ambao wameipokea chapa ya mnyama, wakingoja kuingia katika mapigo ya vitasa saba (tunayoyasoma katika Ufunuo 16). Kumbuka haya yote yatatokea baada ya kanisa kunyakuliwa juu mbinguni.
Huu ni mhutasari tu wa Chapa ya Mnyama jinsi utakavyokuwa, kwa maelezo marefu juu ya chapa hii ya mnyama, unaweza kuwasiliana nasi inbox kwa namba hizi 0693036618/0789001312. (www wingulamashahidi org)
Hivyo kwa hitimisho ni kwamba chanjo ya korona si chapa ya mnyama, lakini inatangaza ujio wa chapa ya mnyama. Na ugonjwa wa Korona haujatengenezwa na wanadamu, bali ni Tauni kutoka kwa Mungu (sawasawa na Luka 21:11), ambapo ugonjwa huu ni dalili mojawapo kubwa sana ya kurudi kwa Kristo.
Dalili zote za kurudi kwa Yesu zimeshatimia… unyakuo upo karibu sana, je! Umempokea Yesu?..kwa kutubu dhambi zako zote na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu?, kama bado kumbuka kuwa unyakuo utakapopita, utaachwa, na hutaachwa kwasababu unachapa ya mnyama, hapana utaachwa kwasababu tayari wewe ni wa Yule mwovu hata bila chapa!,.. Chapa itakuwa ni muhuri tu wa kuhitimisha kwamba wewe ni milki ya shetani.. Hivyo si wakati wa kuifikiri chapa na kuiogopa!, kitu cha kuogopa sasa ni dhambi..Hicho ndio cha kuogopa na kukikimbia, na kwa nguvu zetu hatuwezi kuikwepa wala kuishinda dhambi bali kwa kumpokea na kumwamini Yesu.
Bwana atubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Kwanini Bwana aliwalenga mbwa na nguruwe tu katika Mathayo 7:6?
SWALI: Biblia inasema mshahara wa dhambi ni Mauti, (Warumi 6:23) je wote wanaokumbwa na mauti sasa ni kutokana na dhambi zao?
Jibu: Ni vizuri kufahamu kuwa katika maandiko kuna Mauti za aina mbili. Mauti ya kwanza ni mwili uliokufa na kutupwa katika kaburi!, na mauti ya pili ni roho kutupwa katika ziwa la moto.
Bwana Yesu alisema maneno haya..
Mathayo 10:28 “Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum”
Umeona?, mwili unaangamizwa katika dunia hii, ndio hapo mtu anakufa na mwili wake kuzikwa, lakini roho ni katika jehanamu ya moto… Hii mauti ya pili ya kuiangamiza roho katika ziwa la moto, ndio mshahara wa dhambi biblia inayoizungumzia katika Warumi 6:23
Warumi 6:23 “KWA MAANA MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”
Hivyo mshahara wa dhambi ni Mauti ya Pili, na si ya kwanza, Katika mauti ya kwanza watakatifu wengi wamekufa, wataendelea kufa wengi.. lakini watafufuliwa na kuurithi uzima wa milele, hivyo biblia haikumaanisha kabisa mauti ya mwili huu kuwa ndio mshahara wa dhambi, vinginevyo mpaka sasa kungekuwa hakuna mwenye haki. Maana watakatifu wote waliotangulia tayari wamekufa!. Kwahiyo mauti iliyomaanishwa hapo katika Warumi 6:23 ni MAUTI YA PILI, yaani lile ziwa la moto, mahali roho ya wanadamu waovu zitakapoangamizwa..
Sasa labda unaweza kuuliza ni wapi tena katika maandiko, pametajwa mauti hii ya pili kuwa ni katika ziwa la moto..
Tusome..
Ufunuo 20:14 “Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”
Hivyo hatuna budi kujitenga na dhambi!, kwa kadri tuwezavyo ili tusije tukakubwa na mauti ya pili kwa kutupwa katika lile ziwa la moto, kama maandiko yanavyosema..
Ufunuo 2:11 “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya MAUTI YA PILI”.
Lakini kama hatutaishinda dhambi, kwa kumwamini Yesu, na kutubu na kubatizwa katika ubatizo sahihi na wa kimaandiko, basi tufahamu kuwa, mshahara wake utakuwa ni Mauti ya piil, ambayo ndio ziwa la moto..kama Bwana alivyosema..
Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, SEHEMU YAO NI KATIKA LILE ZIWA LIWAKALO MOTO NA KIBERITI. HII NDIYO MAUTI YA PILI”.
Je umempokea Yesu?, kama bado unangoja nini?, je unatamani kukumbwa na mauti ya pili?.. je unatamani kuingia jehanamu ya moto..mahali ambapo utateswa usiku na mchana, kwa maangamizi ya milele?
Fahamu kuwa tunaishi katika siku za mwisho na Bwana Yesu yupo mlangoni sana kurudi!.. siku yoyote parapanda inalia na ngano zitakusanywa ghalani, na magugu yote yatakusanywa na kwenda kuchomwa moto.
Bwana azidi kutubariki.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
SWALI: Kwanini Bwana Yesu alitokea katika ukoo wa Yuda na sio kwenye koo nyingine kama vile Yusufu?
JIBU: Hatma ya yale makabila 12, na tabia zao tunaona kwa mara ya kwanza zikifunuliwa na Yakobo Baba yao siku ile alipokuwa anakaribia kufa, alipowaita na kuwabariki. ukisoma pale utaona kila mtoto alinenewa habari zake. Kwasasa hatuwezi kuziandika zote hapa lakini kwa muda wako soma Mwanzo 49:1-28. Utaona.
Sasa, kulingana na tabiri zile ni kabila moja la Yuda, ndio lilibeba, vimelea vikuu sana, vimstahili Kristo.
Kwamfano pale makabila hayo yalipofananishwa na Wanyama, utaona Ni Yuda peke yake ndiye aliyefananishwa na SIMBA. Wakati wengine kama vile Naflati lilifananishwa na Ayala, Isakari kama na Punda, Dani kama na nyoka aumaye, Benyamini kama mbwa-mwitu mkali. Yusufu kama mti mchanga uzaao. Lakini Yuda ni kama SIMBA .
Na sikuzote simba anajulikana kama ni mfalme wa pori, tena jasiri.
Mwanzo 49:8 “Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia.
9 Yuda ni mwana-simba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakaye mwamsha?
10 Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.
11 Atafunga punda wake katika mzabibu, Na mwana-punda wake katika mzabibu mzuri. Amefua nguo zake kwa mvinyo, Na mavazi yake kwa damu ya zabibu.
12 Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa”.
Vilevile kama tunavyosoma utabiri wake, utaona anaambiwa, FIMBO YA ENZI, haitaondoka kwake, ikimaanisha kuwa fimbo ya kifalme, itakuwa katika uzao wake daima. Yaani kabila hili la Yuda litakuwa ni kabila la kifalme.
Mambo ambayo yanabeba kabisa tabia zote za masihi atakayekuja. Kwamba ni lazima AWE simba, jasiri, mwenye nguvu, na hodari.. Na ndio maana hatushangai kwanini Bwana Yesu alijiita Simba wa Yuda (Ufunuo 5:5).
Vilevile ni lazima awe Mfalme mkuu sana mwenye nguvu sawasawa na unabii wa (Isaya 9:6). Hivyo kabila lenye enzi za kifalme lilikuwa ni hili na tunathibitisha hilo tangu enzi wa Daudi.
Hivyo hiyo ndio sababu kwanini Bwana Yesu hakutokea kabila lingine lolote Zaidi ya kabila la Yuda, Kwasababu, ilimpasa awe juu ya yote..Lakini kama angetokea kabila ya Yusufu ambalo limetajwa kama kabila lenye mafanikio makubwa, ni wazi kuwa kusingekuwa na vimelea vyovyote vya kifalme kwake.. Jambo ambalo haliwezekani kwa Kristo. Yeye ni lazima awe juu, atawale kama Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana. Hivyo ni lazima tabia hizo zianze kuonekana tokea mbali sana, kwenye vizazi vya vya nyuma, hadi kumfikia yeye.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Shalom, ulishawahi kuutafakari vizuri huu mstari?
Yohana 17:14 “Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.
15 MIMI SIOMBI KWAMBA UWATOE KATIKA ULIMWENGU; bali uwalinde na yule mwovu”.
Embu takafakari, Bwana Yesu anasema sisi(watakatifu), sio wa ulimwengu huu, akiwa na maana kuwa hapa dunia hapatustahili kwa namna yoyote ile, kwasababu sio mahali petu, tunapaswa tukishamwamini tu yeye, tuondolewe, twende zetu mbinguni nyumbani kwetu, lakini wakati huo huo bado anasema, “Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwenguni”..
Yaani kwa lugha nyepesi tunaweza kusema, unapelekwa kwenye nyumba ya mtu mwingine, ambaye itikadi zake na za kwako haziendani kabisa, Na pale unapojaribu kutoka na kurudi nyumbani kwako, unazuiwa,unaambiwa uendelee kubaki pale pale, hakuna kuondoka. Si kazi rahisi kama unavyodhani.
Ndicho anachokifanya Mungu sasa kwa watoto wake, na anafanya hivyo kwa makusudi maalumu. Na makusudi yenyewe ni ili sisi tuiangaze NURU yake kwa walimwengu. ukiokoka, jiandae kuendelea kuishi katika mazingira haya haya ya walimwengu kwa kipindi Fulani kirefu tu.. tukisema ulimwenguni tunamaanisha miongoni mwa waovu, Hilo huwezi kuliepuka. Ni mara chache sana itatokea Mungu kukuweka katika mazingira ambayo utaishi na wapendwa wenzako, mnaoendana.
Utawekwa katikati ya watu wasioendana na wewe kabisa, ukaishi nao, Na pengine umemwomba Mungu mara nyingi akuondoe hapo, lakini unashangaa, ombi hilo halijibiwi,lakini mengine yanajibiwa. Ukiona hivyo likumbuke tu hilo Neno la Bwana Yesu.. “Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwenguni, bali uwalinde na yule mwovu”..
Pengine umeokoka, lakini mazingira ya kazini kwako, hayana utukufu kabisa, umezungukwa na watu waovu na wenye mizaha kila namna, na umemwomba Mungu sana, akufungulie mlango wa kazi nyingine nzuri zaidi yenye wapendwa wenzako. Ndugu kama umeomba sana na bado hujaona jibu lolote, ufahamu kuwa umewekwa ulimwenguni Huwezi kuondolewa, unachopaswa kufanya ni kuyatenda mapenzi ya Mungu hapo hapo ulipo, kwasababu huwezi jua kuwa ni Mungu kakuweka hapo ili awaokoe wengine kwa ile nuru yako unayoangaza.
Mtazame Danieli, alipopelekwa kwenye ufalme wa Nebukadreza, alikutana na mambo mengi sana ya kipagani, yanayokinzana na dini ya kiyahudi kwa kila kitu, lakini katika upagani wote ule, alimcha Mungu, na kumdhihirisha, na mwisho wa siku Mungu wake akatukuzwa katikati ya mataifa yote ulimwenguni kupitia yeye.
Hivyo na wewe uliyeokoka, inawezakana kabisa mazingira uliyopo, yasiwe mazuri, unatamani hata unyakuo upite leo uende zako mbinguni, au umetamani Mungu akuchukue uende ukaishi naye milele mbinguni, au unatamani walau akuweke katika mazingira mazuri yenye utulivu Fulani wa kiroho. Jambo unaloliomba ni kweli kabisa ni la ki-Mungu, na ni kweli ingepaswa iwe hivyo. Lakini usivunje moyo pia unapoona ombi hilo halijajibiwa kama ulivyotamani, badala yake, endelea kuyatenda mapenzi ya Mungu hapo mahali ulipo, wahubirie wengine habari njema, wakumbushe juu ya tumaini la uzima wa milele, na mwisho wa siku utakuwa umelitimiza kusudi la Mungu alilolikusudia katika maisha yako. Kwasababu Bwana Yesu hakuomba tuondolewe ulimwengu kwenye maudhi na makwazo, japokuwa alijua kabisa kuwa sisi sio wa ulimwengu huu. Bali alitaka tuendee kuishi nao kwa makusudi hayo waione nuru yake kwa kupitia sisi.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
AHADI YA ROHO ILIYOSALIA SASA KWA KIPINDI CHETU.
ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.
KWANINI MIMI?
Je aliyezungumza na Musa kule jangwani ni Mungu mwenyewe au malaika wake?
KWASABABU MUDA TULIOBAKIWA NAO SI MWINGI.
Wazimu ni “ugonjwa wa akili”.. Mtu mwenye wazimu ni mtu mwenye matatizo ya akili. Kwahiyo katika maandiko popote palipoandikwa neno wazimu, pamemaanisha mtu mwenye shida ya akili. Na wazimu huu upo katika mwili na vile vile upo katika roho.
Katika mwili ni ile hali mtu anakuwa hajitambui, yaani kwaufupi anakuwa kama kichaa. Mfano wa wazimu wa mwilini katika biblia… ni wakati ule Daudi alipojigeuza na kujifanya mwenye wazimu..
1Samweli 21:12 “Naye Daudi akayatia maneno hayo moyoni mwake, akamwogopa sana Akishi, mfalme wa Gathi.
13 Akaubadilisha mwenendo wake mbele yao, akajifanya mwenye WAZIMU mikononi mwao, akakuna-kuna katika mbao za mlango, na kuyaacha mate yake kuanguka juu ya ndevu zake.
14 Ndipo huyo Akishi akawaambia watumishi wake, Angalieni, mwaona ya kuwa mtu huyu ANA WAZIMU; basi, maana yake nini kumleta kwangu?
15 Je! Mimi nina haja ya watu wenye wazimu, hata mmemleta kiumbe hiki ili aonyeshe WAZIMU WAKE machoni pangu? Je! Huyu ataingia nyumbani mwangu?”
Lakini wazimu katika roho ni ile hali ambayo mtu anakuwa hajitambui katika roho, anakuwa anaonyesha tabia za utahira katika mambo ya rohoni, hawezi kuyaelewa wala kuyapambanua, anakuwa anafanya mambo ya ajabu ajabu tu katika roho, sawa na mtu mwenye wazimu katika mwili, mifano wa watu kwenye maandiko waliokuwa na wazimu wa rohoni ni Balaamu na Kaini.
Balaamu alifikia hatua ya kuongea na punda, halafu hata hashangai!, wala kujiuliza!…Inakuwaje kuwaje punda anaongea…na yeye bila kufikiri akawa anajibizana na punda!, jambo ambalo ni la kiwazimu.. mtu mwenye akili zake timamu za kiroho, hawezi kuonyesha hizo tabia…
Hesabu 22:27 “Yule punda akamwona malaika wa Bwana, akajilaza chini ya Balaamu; hasira yake Balaamu ikawaka, akampiga punda kwa fimbo yake.
28 Bwana akakifunua kinywa cha yule punda, naye akamwambia Balaamu, Nimekutenda nini, hata ukanipiga mara tatu hizi?
29 Balaamu akamwambia punda; Kwa sababu umenidhihaki; laiti ningekuwa na upanga mkononi mwangu ningekuua sasa hivi”.
Hivyo Balaamu alikuwa ni mfano wa watu wenye wazimu wa rohoni, na hata biblia inasema hivyo katika…
2Petro 2:15 “wakiiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaamu, mwana wa Beori, aliyependa ujira wa udhalimu”.
lakini alikaripiwa kwa uhalifu wake mwenyewe; punda, asiyeweza kusema, akinena kwa sauti ya kibinadamu, aliuzuia WAZIMU WA NABII YULE”.
Vile vile, Kaini alikuwa na wazimu, kwasababu mtu mwenye akili timamu za rohoni, hawezi kujibizana na muumba wake, lakini Kaini aliweza kufanya hivyo..
Mistari mingine inayozungumzia wazimu wa rohoni ni pamoja na 1Timotheo 6:4, kumbukumbu 28:28, Zekaria 12:4, na Yeremia 25:16.
Bwana atusaidie na kutuepusha na wazimu, hususani wa kiroho ambao ndio mbaya zaidi..kwasababu huo unatufanya tusiweze kupambanua wala kuelewa mambo ya rohoni. Ambayo madhara yake ni kifo kiroho. Tusiwe kama Kaini au Balaamu.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Jina la Mwokozi Yesu, libarikiwe.
Karibu tujifunze maandiko, Neno la Mungu wetu ambalo ndio taa iongozayo miguu yetu, na Mwanga wa njia yetu (Zab.119:105).
Safari ya wana wa Israeli ni funzo tosha, kwetu sisi tunaosafiri kutoka katika ulimwengu kwenda Kaanani yetu (yaani mbinguni). Hivyo tukijifunza kwa undani, jinsi safari ile ilivyokuwa tutaweza kujua tahadhari na sisi tunazopaswa kuzichukua katika safari yetu ya kwenda mbinguni.
Maandiko yanasema wana wa Israeli, walitolewa Misri kwa mkono hodari, lakini walipokuwa jangwani katika safari yao ya kwenda Kaanani, walikutana na changamoto chache, ambazo hizo ziliwafanya wamnung’unikie Mungu, na hata kufikia hatua ya kutamani tena kurudi Misri, walikotoka.
Hesabu 14:3 “Mbona Bwana anatuleta mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watakuwa mateka; JE! SI AFADHALI TURUDI MISRI?
4 Wakaambiana, NA TUMWEKE MTU MMOJA AWE AKIDA, TUKARUDI MISRI”.
Hesabu 11:4 “Kisha mkutano wa wafuasi waliokuwa kati yao, wakashikwa na tamaa; wana wa Israeli nao wakalia tena, wakasema, N’nani atakayetupa nyama tule?
5 Twakumbuka samaki tuliokula huko Misri bure; na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu, na vitunguu saumu;
6 lakini sasa roho zetu zimekauka; hapana kitu cho chote; hatuna kitu cha kutumaini isipokuwa hii mana tu. ”.
Na maandiko yanasema kwa kunung’unika huko, na kwa kutamani huko kurudi Misri, tayari walisharejea Misri katika mioyo yao, ijapokuwa katika mwili bado wapo jangwani.
Matendo 7:39 “Mtu huyo baba zetu hawakutaka kumtii, bali wakamsukumia mbali, NA KWA MIOYO YAO WAKAREJEA MISRI,
40 wakamwambia Haruni, Tufanyie miungu, watakaotutangulia; maana huyo Musa, ALIYETUTOA KATIKA NCHI YA MISRI, hatujui lililompata”.
Ndio maana katika wote walionung’unika na kutamani kurudi Misri, hakuna hata mmoja aliyeingia nchi ya Kaanani, wote walikufa jangwani. Kwanini?, kwasababu katika mwili walikuwa wametoka Misri lakini katika roho/moyo walikuwa wapo Misri. Na kwasababu nia ya ndani inazungumza Zaidi kuliko mwonekano wa nje, wakaangamia wote jangwani bila kufika kule wanakokwenda.
Kadhalika mtu mwingine tunayeweza kujifunza kwake ni Mke wa Lutu, ambaye Bwana alisema “mkumbukeni huyo”(Luka 17:32).
Mke wa Lutu ni kweli alikuwa ameshaanza safari ya kutoka Sodoma, na Zaidi ya yote ameshaokoka kabisa(na inavyoelekea wakati anatoka alitoka kwa Amani na furaha kabisa kama wana wa Israeli walivyotoka Misri).. lakini biblia inasema alipofika mbele katika safari ile ALIGEUKA NYUMA!!..
Maana yake ni kwamba, mawazo yake, fikra zake, tamaa zake, zikatamani tena ya Sodoma alikotoka… Labda alifika mahali akaanza kumlalamikia sana Lutu, na Mungu, kwanini katoka kule, sehemu nzuri na wanakwenda sehemu mbaya.. na kwa kosa hilo tu (la kurejea Sodoma kwa moyo wake).. mbele za Mungu alionekana tayari kastahili adhabu sawa na watu wa Sodoma na Gomora, haijalishi mwili wake haupo Sodoma. Na hivyo akageuka kuwa nguzo ya chumvi.
Ni kweli alikuwa ametoka, ameokoka, mwili wake haupo tena Sodoma, lakini Moyo wake upo Sodoma.. Na pasipo kujua kuwa moyo wa mwanadamu unanena zaidi kuliko kitu kingine chochote cha nje..akapumbazika na hivyo akajikuta anaangamia tu sawa na watu wa Sodoma.
Sasa mambo haya yaliyoandikwa katika biblia yanayowahusu wana wa Israeli na Mke wa Luthu, maandiko yanasema hayajaandikwa tu kutufurahisha! Au kutuhuzunisha, bali yaliandikwa kwaajili yetu ili sisi tusijifunze tusirudie makosa kama yao.
1Wakorintho 10:6 “Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.
7 Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze.
8 Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu.
9 Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka.
10 Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu.
11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.
12 Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke”.
Ndugu Dada/kaka.. kumbuka unapookoka, ni sawa na umeanza safari yako ya kutoka Misri, au Sodoma… Ulimwengu huu umefananishwa na Sodoma na Misri (Ufunuo 11:8). Hivyo hatuna budi kutoka Misri kweli kweli kwa miili yetu na mioyo yetu!.. sio tu kwa miili bali pia kwa mioyo yetu!.
Maana yake ni kwamba tunapomkiri Yesu, hatuna budi tuukatae ulimwengu kimwili na kiroho, tunapaswa tuache ulevi, mwilini na rohoni, tunapaswa tuache uasherati wa mwilini na wa rohoni, kama Bwana alivyosema katika…
Mathayo 5:27 “Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;
28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake”.
Hivyo tukisema hatuzini tu, na huku mioyoni tunaziwasha tamaa, hapo bado mioyo yetu ipo Misri, ijapokuwa kimwili tumetoka Misri, Tunapookoka na kusema si wauaji, si watoaji mimba, lakini mioyoni mwetu tunavinyongo na chuki kwa ndugu zetu na adui zetu, sisi bado ni wauaji tu (Mathayo 5:21-22) na bado tupo Misri kiroho, ingawa kimwili tunaelekea kaanani ambayo hatutaifikia..
Kadhalika ukiwa Misri na moyo wako upo kaanani, hapo bado upo Misri, haikusaidii chochote! Unapaswa utoke Misri, maana yake ni kwamba upo katika ulimwengu lakini una hamu ya kufika mbinguni, kila siku unasema siku moja nitaokoka, siku moja nitabadilika, siku moja nitaacha kuvaa vimini, siku moja nitaacha kujiuza, siku moja nitaacha ulevi.. Fahamu kuwa hiyo siku haitafika, na utakufa ukiwa bado Sodoma. Huu ni wakati wa kujiokoa roho zetu. Kwa kuamua kuokoka kweli kweli na si kuwa vuguvugu. Kwasbabu Bwana alisema watu wote walio vuguvugu atawatapika watoke katika kinywa chake.. (Ufunuo 3:15)
Bwana atusaidie tuokoke kweli kweli, tutoke Misri na Sodoma kiroho na kimwili..
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Ni kweli Paulo alipuuzia maonyo aliyopewa ya kwenda Yerusalemu?
Nakusalimu katika jina kuu sana la Bwana wetu Yesu Kristo, Ni siku nyingine tena tumepewa neema ya kuiona, hivyo nasi hatuna budi kutumia nafasi hiyo kujifunza maneno yake maadamu tumepewa nafasi hiyo.
Tukiwa hapa duniani ni lazima tujue kuwa upo ufalme ambao Bwana Yesu alienda kutuandalia huko mbinguni. Lakini kwa bahati mbaya ufalme huo hautakuwa wa watu wote, watakaopewa neema ya kuingia huko. Wengine watakuwa waalikwa tu, lakini hawatakuwa wafalme na makuhani, bali ni Bibi-arusi tu wa Kristo peke yake, na ndugu za mfalme ndio watakaokuwa na ufalme huko mbeleni. Soma (Mathayo 22:1-13)
Na hao Yesu alisema watakuwa ni watu “waliodumu naye katika Majaribu yake”
Luka 22:28 “Nanyi ndinyi mliodumu pamoja nami katika majaribu yangu.
29 Nami nawawekea ninyi ufalme, kama vile Baba yangu alivyoniwekea mimi”.
Umeona, wale waliodumu naye katika majaribu yake tangu, kuzaliwa kwake, mpaka anaanza hudumu, na hadi kufa kwake. Na hao si wengine zaidi ya akina Mariamu, ma mitume na wengine baadhi waliomfuata Yesu kila mahali alipokwenda kama vile Mathiya. Na sisi tuliotokea kipindi hichi ambao tutashiriki kama wao hapa duniani kwasasa.
Sasa leo tutamwangalia mtu mwingine mmoja, ambaye naye alishikiriki, kwa sehemu katika majaribu ya Yesu, na kwa kupitia yeye, tutajifunza na sisi tufanye nini ili, tuwe na nafasi katika ufalme huo mkuu sana. Na mtu mwenyewe si mwingine zaidi ya Simoni Mkirene.
Utakumbuka wakati ambao Bwana Yesu anakaribia kwenda kusulibiwa, baada ya kupigwa sana, kutemewa mate, kupigwa makofi, kuvikwa taji la miiba n.k., hali yake haikuwa nzuri kabisa. Biblia inasema aliharibiwa kuliko mtu yeyote duniani, hakuwa tena kama mwanadamu ukimtazama, kwa mapigo aliyoyapata (Isaya 52:14).
Lakini wale askari bado waliona hiyo haitoshi, wakamtwika msalaba wake, ili aubebe mpaka Goligotha, lakini alipojitahidi kuubeba mwendo kadhaa, hakuweza kutembea kabisa, mwendo wake ulikuwa ni mdogo sana, hakuwa na nguvu ya kuunyanyua msalaba kwasababu aliumizwa sana, Pengine wakawa wanampiga kwa mijeledi kama punda, walau waone kama ataongeza mwendo, lakini hakukuwa na mwitikio wowote katika hilo, ni jinsi gani Bwana alivyochoka..
Hatimaye wakaona, atawacheleweshea tu muda, hivyo ikawabidi watafute njia mbadala. Hapo ndipo wakaangalia kulia na kushoto miongoni mwa watu waliokuwa pale, lakini hawakuona hata mmoja aliyeweza kuunyanyua msalaba ule. Tengeneza picha biblia inasema, kulikuwa na mkutano mkubwa sana wa watu waliokuwa wanamfuata Yesu kwa nyuma hiyo siku, lakini askari hawakuona hata mmoja miongoni mwao mwenye uwezo wa kuubeba msalaba wa Yesu. Wengi wao walikuwa ni watakazamaji tu, wengine walalamikaji, wengine wahurumiaji tu, hakuna hata mmoja aliyeweza kusogeza hata shingo yake, kuimsaidia Yesu.
Lakini kwa bahati nzuri kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa anatokea SHAMBA, ambaye hakuwa hata na habari za kusulibiwa kwa Yesu, lakini askari wakamwona huyo ndiye anayefaa, wakamkamata kwa lazima, wakamshurutisha aunyanyue ule msalaba mzito mabegani mwake mpaka Goligotha.
Luka 23:26 “Na walipokuwa wakimwondoa walimkamata mtu mmoja, Simoni Mkirene, aliyekuwa ametoka shamba, wakamtwika msalaba, auchukue nyuma yake Yesu.
27 Mkutano mkubwa wa watu wakamfuata, na wanawake waliokuwa wakijipiga vifua na kumwombolezea”.
Sasa jiulize ni kwanini awe ni huyu mtu aliyetoka SHAMBA na si wale wengine? Ni kwasababu askari walimwona ni mtu wa KAZI, aliyezoelea utumishi, mtu wa kupiga majembe, mtu wa kukata mashoka huko misituni, hivyo wakimkatama huyo amsaidie ili safari ile ndefu ya msalaba mzito isiishe katikati bali itawafikisha Goligotha walipokusudia. Na kweli ikawa hivyo.
Jiulize tena kwa upande wa pili, Bwana Yesu alijisikiaje moyoni mwake kwa mtu kama huyu. Akiona katwikwa mzigo ule uzito asiostahili kuubeba, ni wazi kuwa moyo wake ulimhurumia, kwa kila jasho alilokuwa analitoa nyuma yake, wakipandisha kilima kile kirefu hadi Kalvari. Unategemea vipi mtu kama huyu asiwe sehemu ya Ufalme aliokwenda kuwaandalia watakatifu wake mbinguni. Ikiwa tu Yule mwizi pale msalabani hakufanya chochote chema, wala hakumsaidia Yesu kwa lolote lakini alipoomba tu aliambiwa usiku ya leo utakuwa pamoja nami peponi, Si zaidi kwa mtu kama huyu ambaye alikuwa sehemu ya majaribu ya Yesu Kristo duniani?
Marko 15:21 “Wakamshurutisha mtu aliyekuwa akipita, akitoka mashamba, Simoni Mkirene, baba yao Iskanda na Rufo, ili auchukue msalaba wake.
22 Wakamleta mpaka mahali paitwapo Golgotha, yaani, Fuvu la kichwa”.
Ni nini tunajifunza?
Bwana hawezi kutupa sehemu ya msalaba wake, ikiwa sisi si watu wa SHAMBA. Si watu wa kuzoelea kazi ya Mungu, Kwasababu ataona kama tutaishia njiani, tukautupa msalaba wake tukakimbia, tusilitimize kusudi lake, kwasababu ni watu laini laini.
Kuwa mtu wa shamba ni pamoja na kuwa mtu wa kulitendea kazi Neno la Mungu, na sio kuwa msikiaji tu au msomaji tu. Kama wale makutano ambao walikuwa wanafuata tu kwa nyuma, lakini wasifanye chochote kwa ajili ya Kristo.
Kuwa mtu wa shamba ni pamoja na kujitoa kwa ajili ya Kazi ya Kristo, kwa vile vidogo ulivyojaliwa, kwa karama Mungu aliyoiweka ndani yako.
Kuwa mtu wa shamba ni pamoja na kujizoesha kuishi maisha ya Utauwa(1Timotheo 4:7-8). Yaani kuwa mwombaji, mfungaji, na mshuhudiaji wa habari njema.
Hapo ndipo Bwana ataona sababu ya kukupa wewe neema ya kuubeba msalaba wake. Na faida yake ni kuwa utakuwa sehemu ya ufalme huko mbinguni alipokwenda kutuandalia. Kwasababu ufalme huo ni kwa wale tu walioshiriki taabu yake wakiwa hapa duniani.
Hivyo sisi sote kuanzia sasa, tuwe wakakamavu rohoni, tuwe hodari kama Simoni, sio walegevu walegevu, wasikiaji tu lakini sio watekelezaji wa kile tunachokisikia, vitu vidogo vidogo tu vinatutoa katika mstari wa wokovu, bali kila siku tutafute ni nini mapenzi ya Mungu.
Bwana akubariki sana, na nikutakie mafanikio mengi katika safari yako ya wokovu hapa duniani.
Shalom
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Tofauti kati ya ufalme wa mbinguni na ufalme wa Mungu ni ipi?
Shalom, karibu tujifunze maandiko.
Kama kuna njia tunaiendea ambayo itakuja kuleta majuto mbele yetu, basi Mungu wetu huwa anatangulia kututahadharisha kabla ya hatari yenyewe kutufikia!..Lengo ni tuiache hiyo njia ili madhara yasitukute!
Lakini jambo la kuogopesha ni kwamba mara nyingi Mungu hatumii tu mambo makubwa kututahadharisha, au kuzungumza na sisi, bali pia anatumia vitu vidogo, na vilivyo dharaulika, na visivyo na heshima kuzungumza na sisi au kututahadharisha..
Wakati Fulani Mungu alitumia Punda kumtahadharisha Balaamu, hatari iliyopo mbele yake.. Ghafla akiwa njiani kuelekea kufanya jambo ambalo ni kinyume na mapenzi ya Mungu, punda wake aliyempanda alifunga breki ghafla wakiwa katikati ya safari!.. Na kwasababu alimdharau mnyama Yule pasipo kujua kuwa kusimama kule kwa punda wake kusikokuwa kwa kawaida, inawezekana kuna jambo, lakini yeye hakulitafakari hilo..badala yake aliona ni punda tu!, na kuanza kumpiga!.. Kumbe Mungu alimtumia punda kuyanusuru maisha yake asiende kufa!! (habari hiyo kwa urefu unaweza kuisoma katika kitabu cha Hesabu 22).
Sio huyo tu!, tunaweza kujifunza kwa mtu mwingine ambaye alitahadharishwa na mnyama lakini hakusikia.. Na huyo si mwingine zaidi ya Petro.
Wakati Fulani Petro alifikia hatua ya kufanya jambo la hatari la kumkana Bwana, na wakati anaanza tu! Kumkana kwa mara ya kwanza.. Maandiko yanasema Jogoo aliwika!, sasa sauti ile ya jogoo!, haikuwa ya kawaida.. Petro aliona ni sauti ya kawaida tu!, kumbe ni Roho Mtakatifu aliingia ndani ya jogoo na kumfanya awike muda ule, ili kumtahadharisha Petro kuwa anakoelekea sio kuzuri, lakini Petro hakuelewa chochote, akaendelea kumkana Bwana kwa mara nyingine ya pili na ya tatu!, lakini Mungu jinsi alivyo wa huruma akazungumza naye tena kupitia Yule Yule jogoo ili kwamba aache hiyo njia, atubu lakini tunaona jogoo alipowika tena mara ya pili bado Petro hakuelewa wala kukumbuka.. Mpaka Bwana alipomgeukia na kumtazama, ndipo Petro akafahamu na kukumbuka, na kwenda kutubu…Kama tu Balaamu baada ya kufumbuliwa macho na kumwona Yule malaika, ndio akatambua!.
Marko 14: 66 “Na Petro alikuwa chini behewani; akaja mmoja wa vijakazi wa Kuhani Mkuu,
67 akamwona Petro akikota moto; akamkazia macho, akasema, Wewe nawe ulikuwapo pamoja na yule Mnazareti, Yesu.
68 Akakana, akasema, Sijui wala sisikii unayoyasema wewe. Akatoka nje hata ukumbini; JOGOO AKAWIKA.
69 Na yule kijakazi akamwona tena, akaanza tena kuwaambia waliosimama pale, Huyu ni mmoja wao.
70 Akakana tena. Kitambo kidogo tena wale waliosimama pale wakamwambia Petro, Hakika u mmoja wao, kwa sababu u Mgalilaya wewe.
71 Akaanza kulaani na kuapiza, Simjui mtu huyu mnayemnena.
72 NA MARA JOGOO AKAWIKA MARA YA PILI. Petro akalikumbuka lile neno aliloambiwa na Yesu, Kabla ya kuwika jogoo mara mbili, utanikana mara tatu. Na alipolifikiri, akalia”
Sasa ili tuzidi kuelewa vizuri baada ya jogoo kuwika mara ya pili ni nini kilitokea… hebu tusome tena habari hiyo katika kitabu cha Luka..
Luka 22:59 “Halafu, yapata saa moja, mtu mwingine alikaza kusema, Hakika na huyu alikuwa pamoja naye, kwa kuwa yeye pia ni Mgalilaya.
60 Petro akasema, Ee mtu, sijui usemalo. Na papo hapo alipokuwa katika kusema, jogoo aliwika.
61 BWANA AKAGEUKA AKAMTAZAMA PETRO. Petro akalikumbuka lile neno la Bwana jinsi alivyomwambia, Leo kabla hajawika jogoo utanikana mara tatu.
62 Akatoka nje akalia kwa majonzi”
Umeona hapo?.. Bwana alipomtazama Petro, ndipo Petro akakumbuka kuwa Bwana alimwambia na vile vile akafahamu kuwa sauti ile ya jogoo ilikuwa ni ya kumtahadharisha aache kumkana Bwana, Njia aliyokuwa anaieleka sio salama, maneno aliyokuwa anayatamka ni hatari, mwisho wake ni uharibifu!…
Laiti kama Bwana asingemgeukia Petro, au asingemwambia unabii ule, pengine Petro angeendelea kumkana Bwana hata kwa mara ya nne na tano.. na usalama wa Petro ungeendelea kuwa chini, kwasababu wale watu tayari walikuwa wameshamjua na labda wangemkamata!..na kumdhuru katika hali yake ile ile ya kumkana Bwana, lakini baada ya Bwana kumtazama, akajua kosa lake na akatoka kule behewani..Akatoka nje!, kutubu, hakuendelea kukaa kule ndani!
Ndugu, jambo hilo hilo linaendelea sasa, Ipo sauti ya Mungu inayotuonya katika mambo mengi tunayoyafanya!..Yule mhubiri unayemdharau na kumwona si kitu, ni huyo huyo Mungu anamtumia kuzungumza na wewe, hata mara tatu au nne, tofauti na Yule unayemdhania sana.. Wakati wewe unategemea kwenda kusikia sauti ya Mungu kwa mtu Fulani ambaye umemkuza sana katika kichwa chako, kumbe Mungu hatumii hiyo njia sana.
Mungu alimtumia Punda kumtahadharisha Balaamu, kadhalika alimtumia jogoo kumtahadharisha Petro, ambaye alikuwa ni mtume wake aliyemchagua yeye, ambaye leo hii ni nguzo katika Imani.. Atashindwaje kututahadharisha wewe na mimi kupitia mjusi au bata?. Anaweza kufanya hivyo!. Ni kuzidi kuwa wanyenyekevu tu na kuongoza umakini tu!. Na sio tu kututahadharisha, bali pia kuzungumza na sisi.
Unapopita mahali na kusikia mahubiri yanayomtaja Yesu Kristo wa kwenye biblia, usidharau chochote kile!, hata kama wewe una maarifa mengi kuzidi hapo unaposikia, tega sikio lako kwa makini sana, kwasababu kuna uwezekano Mungu anasema na wewe hapo!, haijalishi Yule anayehubiri ni mdhaifu na wewe ni Mchungaji au mtumishi!.. na wajibu wako kujinyenyekeza kwasababu, Mungu anatumia chochote kuzungumza na sisi, hivyo hatujui ni kwa njia gani atatumia kusema na sisi, ni kuwa tayari tu muda wote na kwa chochote.
Bwana atusaidie na kutubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
TUSIRUHUSU MAMBO YA KUSUBIRISHA, YAVURUGE MUDA WETU NA MUNGU.
Nakusalimu katika jina la Mkuu ya uzima, Mfalme wa wafalme, Bwana wetu Yesu Kristo. Sifa heshima na utukufu vina yeye milele na milele Amina.
Karibu tujifunze biblia. Leo tutatazama viashiria vikuu vitakavyomtambulisha huyo mpinga—kristo ambaye anatarajiwa kuja duniani. Kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na mikanganyiko mwingi, kuhusiana na ujio wake, na chapa yake ya 666, na hiyo imepelekea wengine kudhania kuwa mpinga-Kristo ni mkuu wa freemason atatokea kuzimu au ni ugonjwa wa Corona, kwamba mtu akichanjwa tayari ameshaipokea hiyo chapa ya 666. Lakini je! Biblia inatufundisha hivyo?
Ni kweli Bwana Yesu alisema wapinga-kristo wengi watatokea duniani, ambao kimsingi hadi sasa wapo wengi, lakini yupo mmoja ambaye atakuja. Ili kuleta uharibifu huku ulimwenguni (Soma 1Yohana 2:18). Ambaye ndio huyo tutakayekwenda kusoma tabia zake, na kwamba tukiona hizo zote zipo ndani yake, basi tujue ule mwisho umefika, tayari ameshafunuliwa, dunia imebadikiwa na kipindi kifupi sana zisichozidi miaka 7 (2Wathesalonike 2:1-6).
Zifuatazo ni tabia zitakazomtambulisha.
1) ATATOKEA KATIKA DINI KONGWE.
Mpinga-kristo tofauti na watu wanavyodhani kwamba atazuka tu ghafla kama mwanaharakati Fulani, pasipokuwa na chanzo, hapana, biblia inatuonyesha atatokea katika utawala utakaokuwa unaongoza ulimwengu wakati huo, ambao ulishawahi kuongoza pia hapo kabla, Na utawala wenyewe ni Rumi-ya-rohoni, na utakuja kupata nguvu tena kipindi cha kukaribia mwisho wa dunia, na utafanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu tu, yaani kwa maelezo mafupi ni kuwa mpinga-Kristo hatotokea mahali pengine isipokuwa katika ofisi ya UPAPA.
Ufunuo 17:11 “Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu”
2) DUNIA NZIMA ITAMSTAAJABIA:
Tabia nyingine ni kuwa dunia nzima itamstaajabia, kustaajabia maana yake ni kushangazwa na matendo yake, na ukuu wake, ikiwa na maana atakubalika sana na makundi yote, biblia inasema mataifa yatakubaliana naye, na watu wa itikadi zote, na kabila zote, na jamii zote za watu ulimwenguni. Hakuna hata mmoja atakayemwona kuwa ni mtu mwovu, isipokuwa tu wale masalia machache yatakayokuwa yamebaki duniani wakati huo.
Ufunuo 13:3 “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule….
8 Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia”.
Lakini sio Corona, au mtu Fulani mbaya, mwenye mapembe ambaye, leo hii anaogopeka, hapana mpinga-Kristo ataonekana ni mkombozi wa ulimwengu wakati huo.
3) ATAITWA MTU WA AMANI:
Sio mtu wa vurugu, au mchinjaji, kwani mikakati atakayokuwa ameipanga na ulmwengu, italenga katika kuleta amani ya dunia, na hivyo jambo lolote atakalolianzisha, au mfumo wowote atakaouleta duniani utapokewa na mataifa yote kwa moyo mmoja, na huko huko atapatia nguvu ya kuileta chapa yake yenye 666 ndani yake, na kwamba hakuna mtu yeyote atakayeruhusiwa kuuza au kununua asipokuwa nayo.
Danieli 11: 21 “Kisha badala yake atasimama mmoja, mtu astahiliye kudharauliwa, ambaye hawakumpa heshima ya ufalme; naye atakuja wakati wa amani, naye ataupata ufalme kwa kujipendekeza.
22 Na wale wenye silaha mfano wa gharika watagharikishwa mbele yake, na kuvunjika, naam, mkuu wa maagano pia”.
4) ATAKUJA NA ISHARA NA MIUJIZA YA UONGO:
Mpinga-Kristo atakuwa na uwezo pia wa kufanya miujiza, Kwasababu roho ya shetani itakuwa nyuma yake, mfano wa Yane na Yambre kipindi kile walipokuwa wakishindana na Musa, ambao tunaona nao pia shetani aliwapa uwezo wa kufanya miujiza,. Ili tu kushindana na kuwapinga watakatifu wa Mungu. Hivyo mpinga-Kristo naye atakuwa na uwezo huo wa shetani,lengo likiwa ni kuwachukua wale ambao watadhani ni yeye ni mpinga Kristo.
2Wathesalonike 2:8 “ Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;
9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;
10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
11 Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo;
12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu”
5) ATATAKA KUABUDIWA KAMA MUNGU.
Kwasababu atakuwa ni mtu wa rohoni, na vilevile mtu wa mwilini, lengo lake litakuwa ni kufikia kilele cha kiti cha enzi cha Mungu duniani. Atataka watu wamwone yeye kama Mungu,.Hivyo atajiinua juu ya dini zote, na madhehebu na imani zote duniani, ili apewe sifa na utukufu kana kwamba ni yeye ni Kristo.
2Wathesalonike 2:3 “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;
4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu”.
6) ATATOA MANENO YA MAKUFURU.
Kutaka kuwa kama Mungu tu peke yake haitoshi, bado atakuwa anaitukana njia ya wokovu, Ataukandamiza ukristo wa kweli pia, atadiriki kumtakana Mungu anayeabudiwa na watakatifu. Ili tu aonekane yeye ndio kila kitu.
Ufunuo 13:5 “Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.
6 Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni.
7 Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa”
7) HESABU YA JINA LAKE ITAKUWA NI 666.
Vilevile jina lake litakuwa ni hesabu ya 666. Yaani ukizihesabu tarakimu za jina lake, ni lazima ziishie na jumla ya 666
Ufunuo 13:16 “Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;
17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.
18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.
Sasa haya yote kwa jumla ukiyaona kwa wakati mmoja ndani ya huyo mtu mmoja, basi ujue huyo ndiye mpinga-Kristo mwenyewe, ambaye ataipelekea duniani ifikie kiama chake. Wakati huo ukifika dunia haitakuwa na zaidi ya miaka 7 tu mpaka itakapoisha, Na kulingana na maandiko watakaokumbana na kazi zake ni wale wote ambao hawatakwenda katika unyakuo, ambao hivi karibuni unakwenda kutokea.
Huyu mpinga-Kristo ataleta dhiki kubwa sana kwa wale watakaoachwa katika unyakuo. Kwasababu hutaruhusiwa kuuza wala kununua kama huna chapa yake. Ni dhiki ambayo watu watatamani vifo lakini vifo vitawakimbia.
Dalili zote zimeshatimia, Na huyu mtu wakati huu pengine anaishi duniani, ndio, anaishi duniani, kwasababu atatokea katika dini kongwe duniani, ya kirumi, katika kiti cha UPAPA,.kinachongojewa tu ni unyakuo wa kanisa, na baada ya hapo, aanze kutenda kazi yake ya kuuharibu ulimwengu. Huyu ndio lile Chukizo lenyewe la uharibifu linalozungumziwa katika maandiko.
Ndugu Je! Hadi sasa upo upande gani, Yesu akirudi leo utakuwa mgeni wa nani huko uendako?. Jibu unalo.
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tuyatafakari pamoja maneno ya uzima ya Mungu wetu.
Kuna wakati mtume Petro alialikwa kama mgeni, nyumbani kwa mtu mmoja aliyeitwa Simoni, Lakini siku moja alisikia njaa sana, Na njaa ile inaonekana haikuwa ya kawaida, pengine Petro hakula kitu chochote tangu jana yake, hivyo ulipofika muda wa chakula ikambidi akatafute kitu cha kula, lakini biblia inatuambia muda huo ndio walikuwa katika maandalizi kwamaana ilikuwa ni saa sita mchana..
Lakini tunaona Petro hakusubiri mpaka chakula kiive, ale kwanza ndio aendelee na shughuli zake za ibada, bali alitumia muda huo kuingia uweponi mwa Mungu ili aombe katika njaa yake, aliendelea hivyo mpaka alipozimia katika maono, ndipo Mungu akatumia Ono linalofanana na njaa yake kumfunulia Siri kubwa sana ya ukombozi, ambayo haikuwahi kufunuliwa kwa vizazi vyovyote vilivyomtangulia. Na siri yenyewe ilikuwa ni kuhusu “Ukombozi wetu sisi watu wa mataifa”
Matendo 10:9 “Hata siku ya pili, walipokuwa wakisafiri na kuukaribia mji, Petro alipanda juu darini, kwenda kuomba, yapata saa sita ya mchana;
10 akaumwa na njaa sana, akataka kula; lakini walipokuwa wakiandaa, roho yake ikazimia,
11 akaona mbingu zimefunuka, na chombo kikishuka kama nguo kubwa, inatelemshwa kwa pembe zake nne hata nchi;
12 ambayo ndani yake walikuwamo aina zote za wanyama wenye miguu minne, na hao watambaao, na ndege wa angani.
13 Kisha sauti ikamjia, kusema, Ondoka, Petro, uchinje ule”.
Sasa nachotaka tuone ni kuwa, wakati wa kusubiria huduma, Petro hakuona vyema muda huo upite hivi hivi tu, ni heri autimie kwa Bwana, hata kama atakuwa katika njaa.
Hata sasa, sisi kama watumishi wa Mungu, sisi kama wakristo, tunavurugiwa muda wetu kwa Mungu, kwasababu tu ya huduma tunazozisubiria za kimwili,. Na hiyo imetufanya tukose kuzijua siri nyingi za Mungu katika maisha yetu, na kanisa.
Wakati tunasubiri kwenda masomoni, kwanini tusitumie muda huo hapo katikati kuutafuta uso wa Mungu, au kuifanya kazi yake, kwanini tusitumie kuhudhuria mikesha, au kumfanyia Mungu ibada, nani ajuaye atatuonyesha njia iliyo bora zaidi, kuliko hiyo tuliyokuwa tunaiendea?.
Wakati tumemaliza chuo tunasubiria kupata kazi, ni sawa na kusema njaa ya kazi imekushika, kwanini usiende kuhubiri injili na wengine mitaani, kuliko muda wote, kuwaza ufanye hiki au kile ili utoke, hujui kuwa unapoteza muda wako mwingi kusubiria na wakati mwingine inapita hata miezi au miaka, ukisumbukia tu hicho hicho kitu kimoja ambacho bado hujakipata, kwanini usitumie muda huo ukiwa nyumbani, kuhudumu nyumbani kwa Mungu.
Wakati unasubiria kuolewa, njaa ya kuolewa imekukamata, pengine umri umeenda sana, ujana unakukimbia, Embu fanya kama Petro, wakati Mungu anakuandalia mume wako, au mke wako, tumia muda huo kujishughulisha na masuala ya Mungu, usipoteze muda wako mrefu kutanga tanga huku na huko, au kujiweka hivi au vile, vitakupotezea tu muda, wakati muda huo Mungu angekuwa anakufunulia mambo makubwa na ya ajabu.
Wakati njaa ya mafanikio imekushika, unasubiria siku ya kupewa mkopo ifike, au kupandishwa cheo, au kupata promosheni, kwanini usijishughulishe na mambo ya ufalme wa mbinguni?, kuliko kutwa kuchwa, unapambana umpendeze huyu au Yule, ili upate upendeleo, unakosa hata muda na Mungu wako, upo buzy kusubiria kitu ambacho bado kipo kwenye maandalizi.
Hivyo, tujifunze kuutumia muda wetu vizuri kama mitume, kwasababu hapa duniani, mambo ya kusubirisha yapo mengi. Na huwa yanavuruga akili kweli, na kupotezesha muda sana, kwa mfano unapoona wengine wamepata kazi wewe huna, fikra zako zote ni rahisi kuelekea kwenye njia mbalimbali, ili tu na wewe ukipate kwa haraka kama wao walivyopata, na hapo ndipo kumsahau Mungu kunapokuja, au kupunguza muda wako na Mungu kunapokuja. Kwasababu unapigana ili na wewe usipitwe nyuma Hivyo, hali kama hiyo ikikukuta wakumbuke mitume, Kwasababu hata wao walikuwa na sababu zote za kusubiri, lakini walitumia muda wao wa hapo katikati vizuri na ndio maana mpaka leo hii tunafaidi matunda ya kujitoa kwao.
Vivyo hivyo na sisi tusiruhusu hata kidogo mambo ya kusubirisha yatuvurugie muda wetu na Bwana. Tusiruhusu njaa zetu, zimweke Mungu nyuma.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo: