SWALI: Kitabu cha Henoko ndio kitabu kipi hicho, Je! Sisi kama wakristo tunapaswa kukiamini?
JIBU: Kitabu cha Henoko ni moja ya vitabu vya Apokrifa ambavyo viliandika kati ya miaka 200 kabla ya Kristo(KK), na miaka 400 baada ya Kristo(WK). Vitabu hivi vinaaminiwa na baadhi ya wakristo kuwa vilihifadhiwa kwa siri, kutokana na kuwa vilikuwa na siri za ndani sana kuhusu Mungu na historia ya ulimwengu kwa ujumla, kiasi kwamba havikuweza kujumuishwa moja kwa moja kwenye biblia yenye vitabu 66 ambayo tunayo hivi sasa.
Lakini si kweli, vitabu hivi havikujumuishwa katika biblia takatifu kwasababu vilikuwa na siri za Mungu hapana badala yake vilionekana kujaa habari nyingi za kutungwa, ambazo zinakinzana na misingi ya imani ya Kikristo.
Sasa tukirudi katika hichi kitabu cha Henoko, kiligunduliwa kwenye miaka ya 1700 huko Ethiopia, baadaye kikasafirishwa mpaka Uingereza kwa ajili ya kutafsiriwa katika lugha nyingine, Kitabu hichi kilijulikana kama Henoko wa Kwanza (1Henoko), kwasababu kulikuja kuwa pia na matoleo mengine yaliyofuata baadaye.
Vipande vya nyaraka vya kitabu hichi pia viligunduliwa huko Israeli mnao mwaka 1947, kwenye mapango yalikuwa katika fukwe za bahari ya chumvi (dead sea), Na kwenye mapango hayo kulionekana pia machapishi ya vitabu vyote vya agano la kale isipokuwa tu kitabu cha Esta, inasadikika ni vitabu ambavyo vilikuwa vimehifadhiwa huko na watu wa kale ambao waliishi kabla hata ya Kristo kuja duniani.
Sasa kitabu hiki kinamueleza Henoko ambaye alikuwa ni mtu wa saba kutoka Adamu kama tunavyosoma katika biblia Mwanzo 5:18-24…Henoko hakuonja mauti kama ilivyokuwa kwa wanadamu wengine, bali alinyakuliwa kama Eliya. Hiyo imekuwa ikawafanya watu wengi waamini kuwa mtu huyu alipewa siri nyingi za rohoni na kuziandika kwa ajili ya watu wa baadaye.
Hivyo kitabu hichi kilipogunduliwa, kilidhaniwa kuwa mwandishi wake ni Henoko, japo hilo jambo halikuthibitika kuwa ni kweli. Kitabu hichi kimejaa historia zinaeleza visa vya dunia ya kwanza kugharikishwa na maji, kinasema baadhi malaika wa Mungu ambao walikuwa ni waangalizi wa huku ulimwenguni, ambao idadi yao ilikuwa ni 200 waliwaona binti za wanadamu, kisha wakawatamani, , hivyo wakashauriana washuke duniani wajitwalie wake, waishi nao, na kweli wakafanya hivyo wakashuka duniani wakawapa mimba wanawake, ndio wakazaa wale majitu ambayo tunayasoma katika Mwanzo 6
Zaidi ya yote, malaika hawa kwa kuwa walikuwa na ujuzi, wakawafundisha wanadamu, kubuni silaha za chuma, kufanya uharibifu, wengine wakawafundisha wanadamu kufanya uchawi, na wengine kusoma nyota za mbinguni. Pamoja na hayo watoto wao waliowazaa wakawa wakatili kupita kiasi, ndio wale wanefili, wakawa wanaharibu kila kitu ikiwemo mimea, wanyama, mpaka wanadamu. Urefu wa majitu hayo ulikuwa ni futi 4500, sawa na Jengo la ghorofa 415. Jambo ambalo ni ngumu kusadikika, Hakuna kiumbe cha namna hiyo kinaweza kuzaliwa na mwanamke. Japo wanefili kweli walikuwa ni wakubwa lakini sio kwa kiwango hicho.
Baadaye baadhi ya malaika wa mbinguni wakampelekea Mungu habari zao, lakini Mungu akakataa kuwasamehe, akawafunga katika vifungo vya giza, ndio hapo Mungu akamwambia Henoko kuwa atakwenda kuiangamiza dunia kwa gharika. Hii ndio habari ambayo inafahamika sana
Zipo habari nyingine katika kitabu hicho ambazo kiuhalisia hazina uhalisia wowote na maandiko.
Tunapaswa tujue vitabu hivi vimejaa hadithi nyingi za kutungwa, ambazo ni sumu kwa Mkristo, na ndio maana huwezi kuziona vikijumuishwa katika biblia yenye vitabu 66 vilivyovuviwa na Roho Mtakatifu, kwasababu vinakinzana na misingi ya kweli ya maandiko.
Bwana Yesu alisema..
Mathayo 22:29 “Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.
30 Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni”.
Unaona? Hakuna andiko lolote linaloonyesha kuwa malaika wanaoa, au wanazaliana, malaika hawakuumbiwa viungo vya uzazi kama tulivyonavyo sisi, hawahitaji kuzaliana, wao tayari walishaumbwa, ndivyo walivyo na idadi yao tayari ipo kamili, Lakini kusema walishuka duniani, ni fundisho la uongo ambalo wakristo wengi wanaliamini mpaka leo, na chanzo chake walikitoa katika hichi kitabu cha Henoko.
Waliowaona binti za wanadamu wakawatamani, walikuwa ni watakatifu wa Mungu, ambao hao hawakujichanganya na mambo ya ulimwengu tangu mwanzo, bali walitumia sehemu kubwa ya maisha yao, kuliita jina la Bwana na kumwabudu Mungu soma Mwanzo 4:26 utalithibitisha hilo ndio ule uzao wote wa Sethi (Wakina Henoko, Methusela, Na Nuhu).. Lakini binti za wanadamu walikuwa ni watu wa kidunia tu, ambao walitokea katika ule uzao wa Kaini..hao ndio tangu mwanzo walikuwa na ujuzi mkubwa, na hodari na pia wakatili ukisoma pale Mwanzo 4:16-23 utaona ni jinsi gani, uzao wa Kaini ulivyokuwa hodari, wenye ujuzi mwingine, lakini pia mwovu kwa uuaji, kama Baba yao alivyokuwa.
Baadaye sasa walipojichanganya mbegu ndipo Mungu akakasirika, akaghahiri na kuuangamiza ulimwengu wote, ni sawa na leo hii, Mungu aone, watakatifu wake wote, wanaiga na kufanya mambo ya ulimwengu, wanawake wanavaa vimini, wanatembea nusu uchi barabarani, wanaume watakatifu wanakuwa mashoga n.k. kiasi kwamba huwezi kuona tofauti yoyote kati yao na ulimwenguni, hapo kinachofuata ni Mungu kuuteketeza ulimwengu, ndivyo ilivyokuwa kwa watu wa kipindi kile. Watakatifu walijitofautisha kabisa na wana wa ulimwengu..
Hivyo hakuna sababu ya mkristo kuamini, moja kwa moja vyanzo ambavyo havipo katika biblia, kwasababu vingi kati ya hivyo vinakasoro nyingi na vimejaa hadithi nyingi zilizotungwa na wanadamu lakini sio kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu.
Kwamfano kwasasa Kanisa Katoliki, limeamua kuchukua baadhi ya hivi vitabu vya Apokrifa na kuviongezea kwenye biblia takatifu yenye vitabu 66, kufikia 73. Vitabu vyenyewe ikiwemo Yudithi, Baruku, Yoshua bin Sira, Wamakabayo 1&2, Hekima.
Vitabu hivi vinakinzana na misingi ya imani, kwamfano, vinafundisha kwenda toharani, yaani mtu mwenye dhambi anaweza kwenda mbinguni tena, lakini baada ya kupitishwa mahali panapoitwa toharani ili kutakaswa,.,Fundisho lingine ni kuwa Mungu, anasikia maombi ya wafu, mambo ambayo ni uongo, biblia inasema, mtu ameandikiwa kuishi mara moja na baada ya kifo ni hukumu (Waebrania 9:27).
Kwahiyo, vitabu vya Aprokifa, sio vya kuviamini, kama uaminivyo biblia, iwe ni kitabu cha Henoko, au kingine chochote kile nje ya vitabu 66 vya biblia sio vya kuiamini vinamakosa mengi na wakati mwingine vimejaa uongo mwingi, ambao unapotosha kabisa.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Kitabu cha YASHARI kinachozungumziwa katika 2Samweli 1:17-18, ni kitabu gani?
SWALI: Je Mungu aliumba watu wengine kabla ya Adamu?, maana tunasoma katika Mwanzo 1:27, alimwumba mwanamke na mwanamke, na tena tunaona anaumba tena mtu mwingine (Adamu) katika Mwanzo 2:7.
Jibu: Kitabu cha Mwanzo Mlango wa Kwanza kimezungumzia uumbaji wa Mungu kwa muhtasari (yaani kwa ufupi), lakini tunapokwenda katika Mlango wa pili, ndio tunaona uumbaji ukielezewa kwa urefu zaidi. Kwahiyo mlango wa kwanza ni muhtasari wa uumbaji, ndio maana utaona vitu vinaelezewa kwa ufupi tu…Kwamfano utaona Mungu anasema..
Mwanzo 1:11 “Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo
12 Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema,
13 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu.”
Hapo, uumbaji wa miti na mimea umeelezewa kwa kifupi sana, haijaelezwa ilitokeaje tokeaje… sasa ili tujue kwa undani zaidi, hiyo miti ilitokeaje tokeaje, ndipo tunakwenda katika mlango wa 2 wa kitabu hicho hicho cha mwanzo, tunaona ikielezewa vizuri zaidi..
Mwanzo 2:4 “Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa. Siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi
5 hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi;
6 ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi”
Unaona?..Kumbe Mungu aliposema nchi itoe majani na mche utoao mbegu, siku ile ile aliinyeshea nchi mvua na ndipo nchi ikazaa miti na mimea kadha wa kadha… Maana yake hakusema tu itokee halafu ikatokea kama tulivyosoma hapo katika hiyo Mwanzo 1:11, bali kulikuwa na hatua (process). Ambazo ndizo tulizokuja kuzisoma katika hiyo Mwanzo mlango wa pili.
Kadhalika Mungu aliposema katika Mwanzo 1:27 kwamba… “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba”.
Tunaona hapo uumbaji wa mtu umeelezwa kwa ufupi tu, haijaeleza ni jinsi gani huyo mtu alivyoumbwa, mwanaume na mwanamke walitokeaje tokeaji …je! Wote waliumbwa pamoja?..na je waliumbwa kwa malighafi gani?. Sasa majibu ya maswali hayo ndio tunayapata katika Mlango wa pili wa kitabu hicho hicho.. tusome,
Mwanzo 2:4 “Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa. Siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi
5 hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi;
6 ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi.
7 BWANA MUNGU AKAMFANYA MTU KWA MAVUMBI YA ARDHI, AKAMPULIZIA PUANI PUMZI YA UHAI; MTU AKAWA NAFSI HAI.
8 Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya”.
Umeona hapo, biblia inasema Bwana Mungu akamfanya mtu kutoka kwenye mavumbi ya ardhi, jambo ambalo halikutajwa katika ile Mwanzo 1:27, na ukiendelea kusoma katika Mwanzo 2:18-24, utaona jinsi uumbaji wa mwanamke ulivyokuwa, kwamba alitwaliwa kutoka kwa mwanaume (ubavuni mwa mwanaume), jambo ambalo halikuelezwa katika ile Mwanzo 1:27.
Kwahiyo kitabu cha Mwanzo mlango wa kwanza ni muhtasari tu wa uumbaji, umeelezea kwa ufupi sana, na mlango wa pili ndio umeelezea kwa undani kidogo. Ni sawa na unaposoma kitabu Fulani labda cha jeografia, unapokifungua mwanzo kabisa utakutana na “yaliyomo”/“table of content”. Lengo la lile ni kukupa muhtasari na kukuongoza utakachokwenda kukisoma.. Na utaona kila kichwa kimeelezea kwa ufupi sana, lakini utakapokwenda katika kurasa zenyewe utaona mada zimeelezewa kwa urefu sana. Ndicho kilichopo katika kitabu cha Mwanzo mlango wa Kwanza..na wa pili..
Hivyo si kweli kwamba kuna watu wengine waliumbwa kabla ya Adamu. Adamu na Hawa ndio wanadamu wa kwanza kuumbwa.. Na walipoasi waliondolewa katika ile bustani ya Mungu Edeni, na kuanzia huo wakati, wote tunaozaliwa tunakuwa tunalibeba anguko lake. Mpaka tutakapozaliwa mara ya pili katika uzao wa Adamu wa pili Yesu Kristo, ambaye yeye hakutenda dhambi hata mara moja, ambaye alijaribiwa kama Adamu lakini hakutenda dhambi, huyo pekee ndiye amewekwa kuwa ukombozi kwetu.
Kila amwaminiye maandiko yanasema atapata ondoleo la dhambi zake, naye atakuwa haishi chini ya laana bali chini ya Baraka, lakini wote wasiomwamini hawatapata ondoleo la dhambi zao, na siku ya mwisho watatupwa katika ziwa lile la moto, aliloandaliwa shetani na malaika zake.
Je wewe ni mmoja wa waliomwamini au ambao hawajamwamini?.. Kama bado tambua kuwa upo chini ya laana ya anguko la Adamu, na hakuna namna yoyote unaweza kuhesabiwa haki bila kumpokea Yesu maishani mwako, haijalishi utafanya mangapi mazuri, kama humtaki Yesu hutamwona Mungu, kwasababu yeye ndiye Njia ya kufika mbinguni, wala hakuna mwingine.
Hivyo mpokee leo kwa kutubu dhambi zako zote, na kwa kudhamiria kuziacha kabisa na baada ya toba yako hiyo, nenda katafute ubatizo sahihi, kumbuka ubatizo sahihi ni ule wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo ambalo ndio jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Kwa kukamilisha hatua hizo tatu, yaani Imani, ubatizo na kupokea Ujazo wa Roho Mtakatifu, utakuwa umeukamilisha wokovu wako na Roho Mtakatifu atakuongoza katika kuijua kweli yote na kukupa nguvu za kuishinda dhambi.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Rudi nyumbani
Jibu: Tusome,
Mathayo 5:18 “Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie”.
Yodi ni neno lililotumika katika lugha ya Kiswahili cha zamani, lenye maana ya “herufi ndogo”.. kwa lugha ya kiingereza ni “small letter”. Katika sentensi yoyote huwa kunakuwa na herufi kubwa na herufi ndogo, sasa zile ndogo ndio zinazoitwa “yodi”.. Mfano tunaposema neno “Yesu ni Mungu”..Herufi kubwa hapo ni hiyo “Y” na “M” lakini hizo nyingine zote zilizosalia kama “e” “s” “u” “n” “i” “u” ni YODI.
Kwahiyo Bwana Yesu aliposema kwamba hakuna hata “yodi” moja wala nukta itakayoondolewa hata yote yatimie maana yake.. ni kwamba hakuna herufi yoyote (hata ile iliyo ndogo kuliko zote, ‘yodi’) itakayobadilishwa katika maneno ya torati, kwasababu maneno ya Mungu hayabadilii. Ndio maana ukianzia juu kidogo utaona anasema hakuja kuitangua torati bali kuitimiliza..
Mathayo 5:17 “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
18 Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie”.
Mathayo 24:35 “Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe”.
Pale torati iliposema “usizini”..Bwana Yesu hakuja kulibadilisha hilo andiko, bali alikuja kulitimiliza kwa kusema “mtu amtazamaye mwanamke amekwisha kuzini naye nafsini mwake”. Hapo hajaondoa chochote, bali ameongezea dawa. Torati inaposema “usiue” Bwana Yesu alisema “amwoneaye ndugu yake hasira hana tofauti na muuaji, hivyo itampasa hukumu tu kama muuaji”. Hapo hajaitangua wala kulibadilisha bali ameitimiliza, na sheria nyingine zote za kwenye torati ni hivyo hivyo..
Je wewe bado una chuki kwa ndugu zako au maadui zako?,ukijitumainisha kwamba wewe si muuaji?.. bado unatamani ukijitumainisha kwamba wewe sio mzinzi??, bado unavaa nusu uchi,na suruali ukijitumainisha kwamba wewe si kahaba?? (kasome Mithali 7:10 ujipime kama wewe ni kahaba au la kwa mavazi yako), bado unajichua na kunatazama pornography ukijitumainisha kwamba wewe si mwasherati?, bado ni mshabiki wa mambo ya kidunia kuliko kitu kingine chochote ukijitumainisha kwamba wewe si wa kidunia??.
Kama unafanya mojawapo ya hayo, au yote, wakati wa kumkaribisha Mwokozi ndani ya maisha yako ni huu?..Usingoje kesho wala baadaye, saa ya wokovu ni sasa, na wakati uliokubaliwa ndio huu.. wakati wa kukimbilia Kalvari, Bwana akuokoe na kukutua mzigo ndio huu, sio kesho, kwasababu hujui kesho yako itakuwaje, labda leo ndio mwisho wako wa kuishi duniani, au leo ndio siku parapanda ya mwisho itakapolia, jiulize, unyakuo leo ukipita utakuwa wapi??.. Hivyo fanya uamuzi wa kumgeukia Yesu leo kwa kutubu dhambi zako zote kwake, na kwenda kubatizwa katika ubatizo wake wa maji tele (Yohana 3:23), na kwa jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38), na Bwana atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu, atakayekuongoza katika kweli yote ya maandiko.
Maran atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Mlima Gerizimu na Ebali ni ipi, na umuhimu wao rohoni ni upi?
SWALI: Warumi 5:7 “Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema”.
Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu, Naomba ufafanuzi wa hilo andiko na pia nipate kujua tofauti kati ya mtu mwenye haki na mtu mwema.
JIBU: Pamoja na kwamba Bwana Yesu kuja hapa duniani kuwaokoa watu waliopotea kabisa, (yaani watu wenye dhambi wasio na vimelea vyovyote wa utu, kama vile wauaji, wahalifu, mafisadi n.k.) alikuja pia kuwaokoa watu walio wema.
Sasa tukirudi kwenye mstari huo tunaona mwandishi anajaribu kutofautisha kati ya mtu mwema na mtu mwenye haki.
Mtu mwenye haki ni yupi?
Mtu mwenye haki ni mtu mkamilifu sana, asiyekuwa na kosa lolote mbele za Mungu, Mtu wa namna hii kiuhalisia hajawahi kuwepo tangu duniani iumbwe. Kama wangekuwepo hakukuwa na sababu ya Yesu Kristo kushuka hapa duniani, na kufa kwa ajili yao, wapate wokovu, ya nini sasa? Wakati tayari wanaoukamilifu wote ndani yao..hakuna doa lolote ndani yao?
Na ndio maana hapo inasema.. ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki..
Lakini mtu mwema, ni mtu ambaye sio mwovu sana, ni mtu ambaye anajaribu kuishi maisha ya kawaida tu katika jamii, anajiheshimu, anawasaidia wengine, anao utu, anajitahidi kutenda mema kwa bidii na kufanya mambo yake kwa utulivu bila kuvunja sheria yoyote ya jamii husika au nchi n.k. Lakini katika jitihada zake zote, bado hajaweza kufikia kipimo cha yeye kuwa mtu mwenye haki mbele za Mungu..Yaani nguvu zake bado hazijajitosheleza kumfanya awe mkamilifu..hao ndio watu wema mwandishi anaowazungumzia hapo. Na ndio maana ukianzia mstari wa juu anasema;
Warumi 5:6 “Kwa maana HAPO TULIPOKUWA HATUNA NGUVU, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu.
7 Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema”.
Unaona anasema “hapo tulipokuwa hatuna nguvu”, ikiwa na maana tulishajaribu kujitahidi kwa nguvu zetu na kwa matendo yetu kumpendeza Mungu lakini bado tukashindwa kuufikia ule ukamilifu…Na ndio Kristo alikuja kutufia pale msalabani, ili sasa kwa kumwamini tu yeye, tuhesabiwe haki mbele za Mungu.
Hivyo kwa kuhitimisha ni kuwa, kama tungekuwa wenye haki, basi Kristo asingekuja duniani, lakini kwasababu sote tumepungukiwa na utukufu wa Mungu, (nikiwa na maana watu waovu sana na wa kawaida), Sote tunamuhitaji Kristo ayabadilishe maisha yetu. Kwasababu pasipo yeye, haijalishi tuna dini nzuri kiasi gani, tunafanya mazuri kiasi gani, tunasaidia maskini wengi kiasi, bado hutuwezi kumpendeza Mungu, bila Kristo. Kwasababu hayo tayari yalishashindikana tangu zamani.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
USIOMBE MAOMBI YASIYOKUWA NA MAJIBU NA WALA USIMTUKANE MUNGU.
Yeremia 8:7 “Naam, koikoi angani ajua nyakati zake zilizoamriwa; na hua na mbayuwayu na korongo huangalia wakati wa kuja kwao; bali watu wangu hawazijui amri za Bwana”.
Koikoi, mbayuwayu na korongo ni ndege wa ajabu sana, ni ndege wenye uwezo wa kusoma majira ya dunia, Na hiyo imewasaidia sana, kuishi maisha ya salama salmini huku duniani, pasipo kukumbana na changamoto zozote zisizo na maana.
Hawa ni ndege ambao kikikaribia kipindi cha baridi wanahama wote waeneo yao wanayoishi kwa muda, na kusafiri umbali mrefu sana, kwenye pembe ya pili ya dunia kutafuta msimu tulivu aidha wa vuli au wa joto ulipo wakatulie, kisha baadaye hali ya baridi ikishakwisha wanarudi katika makazi yao ya awali kuendelea na maisha yao ya kawaida.
Kumbuka baridi tunayoizungumzia ni ile baridi haswaa, ya kutengeneza barafu iliyopo huko nchi za ulaya, ambayo hata mtu wa kawaida akikaa nje masaa machache tu anageuka kuwa jiwe la barafu, haijalishi atavaa masweta makubwa kiasi gani.. Baridi ya namna hiyo watu wanaoishi huko wanatumia muda wao mwingi kuwepo ndani, na hata kazi zao wanazifanyia ndani katika nyumba zilizojengwa kitaalamu kuhifadhi joto ndani, kwani nyumba za kawaida kama hizi zetu, kule hazijengwi kwasababu zinapitisha baridi, kiasi kwamba ukibaki ndani yake, ukakaa huko mpaka asubuhi ukiamka umeganda. Huku kwetu Afrika hatuna baridi ya namna hiyo.
Sasa, ndege hawa, wanaelewa kabisa kwa namna ya kawaida hawawezi kuishi katika mazingira hayo ya baridi kali, kwasababu hata viota vyao vitaganda.. Sasa ili kulitatua hilo tatizo inawagharimu wahame kwa muda, ndio hapo wanasafiri maelfu ya kilometa wanakuja mpaka huku kwetu Afrika, au nchi nyingine zenye joto, wanakaa huko mpaka msimu wa baridi utakaposhakwisha kule Ulaya ndio wanarudi sasa, kuendeleza maisha yao ya sikuzote.
Sasa Mungu ametumia mfano wa ndege hawa wasio na akili, kutushangaa sisi wanadamu wenye akili timamu kwanini hatujui hukumu zake alizoziweka hapa duniani..anasema..
“Naam, koikoi angani ajua nyakati zake zilizoamriwa; na hua na mbayuwayu na korongo huangalia wakati wa kuja kwao; bali watu wangu hawazijui amri za Bwana”
Hii ikiwa na maana tunashindwa kujua wakati wa neema ni upi, na wakati wa hukumu za Mungu ni upi.. Sisi tupo tu hatujui majira yetu, tunadhani wakati wote, hii neema ya wokovu itaendelea kuwepo, tunadhani wakati wote, hali itakuwa kama ilivyo sasa hivi, utahubiriwa injili kama unavyohubiriwa sasa hivi..
Ndugu yangu, fahamu kuwa neema hii inakwenda kuisha siku sio nyingi, Dhiki kubwa ambayo haijawahi kutokea tangu dunia iumbwe na wala haitakaa iwepo itakwenda kutokea ulimwenguni kote..Dalili zote zinaonyesha, pengine katika wakati wetu huu tunaoishi tutayashuhudia hayo..Haya majira ya neema ndio yanaishia hivyo, muda huu tulionao ni wa nyongeza tu, dunia ingepaswa iwe imeshakwisha tangu zamani, lakini kwasababu tu ile nuru ndogo ya jioni ipo ndio maana unaona mambo bado yapo hivi..
Tumeshafikia wakati ambao Yesu hatuhubirii tena injili ya kutuvuta kwenye wokovu, kama ilivyokuwa zamani bali anatuhubiria injili ya kuthibitisha ulichokiamini. Sikiliza anavyosema..
Ufunuo 22:10 “Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia.
11 Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.
12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo”.
Unaona, hiyo yote ni kwasababu ya unafki tulionao sasa, kwasababu kama tunaweza kuyatambua majira ya nchi, kwamba huu ni msimu wa masika na hivyo tunaanza kuyaandaa mashamba yetu kabla ya mvua kunyesha, au tunahama mabondeni mapema mafuriko yasitukute, inakuwaje basi, tunashindwa kuzitambua siku hizi kuwa ni siku za mwisho? Korona inakufundisha nini? Vimbunga vinakufundisha nini, Hili wimbi la manabii wa uongo unaloliona leo hii limezuka duniani kwa ghafla linakufundisha nini? . Bado tu huoni, hizo ni dalili za wazi kabisa ambazo zinatutambulisha kuwa tukio la unyakuo lipo karibu?
Yesu alisema..
Luka 12:54 “Akawaambia makutano pia, Kila mwonapo wingu likizuka pande za magharibi mara husema, Mvua inakuja; ikawa hivyo.
55 Na kila ivumapo kaskazi, husema, Kutakuwa na joto; na ndivyo ilivyo.
56 Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa nchi na mbingu; imekuwaje, basi, kuwa hamjui kutambua majira haya”?
Itakuwa ni ajabu sana tukishindwa akili na akina koikoi. Tujitathimini sana, tuamke katika usingizi huu mzito, hukumu ya Mungu juu ya ulimwengu wote ipo karibu. Kama upo nje ya safina, anza safari upesi, mkimbilie Kristo kwa kumaanisha kabisa kwa moyo wako wote akuokoe, kwasababu hatuna muda mrefu hapa duniani,
mbingu na nchi zitapita lakini maneno ya Bwana Yesu hayatapita milele.
Mbingu ipo,lakini pia kuzimu ipo, uchaguzi ni wa wako,
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Moyo ni neno ambalo linaweza kuwakilisha aidha nafsi ya mtu au roho ya mtu, inategemea na linapotumika.
Kwa kawaida hakuna lugha ya kuielezea nafsi ya mtu jinsi ilivyo, au roho ya Mtu jinsi ilivyo, kwamba inafananaje, au iko namna gani, hivyo lugha nyepesi ambayo inaweza kuwakilisha vitu hivyo viwili (yaani Roho na Nafsi) ni Moyo.
Kama vile tunavyokosa lugha ya kuzielezea nguvu za Mungu zikoje zikoje, au uweza wake ukoje ukoje, una rangi gani, una mwonekano gani, au unafanyaje kazi, hivyo tunaishia tu kusema “mkono wa Mungu umefanya hichi au kile”… tukimaanisha kwamba Nguvu za Mungu zimetenda hayo au uweza wa Mungu umefanya hayo. Hapo tumetumia kiungo cha mwili kuwakilisha kitu Fulani cha rohoni kisichoonekana. Na lengo la kufanya hivyo ni ile kitu kile kiweze kueleweka zaidi na kuleta maana.
Ingawa si wakati wote tutaziwakilisha nguvu za Mungu kwa “mkono wake” lakini pia tukitumia “mkono wa Mungu ” kuwakilisha “nguvu za Mungu” tutakuwa hatujakosea.
Na ni kwanini tunatumia kiungo mkono na si mguu??… Kwasababu mkono ndio unaofanya mambo yote, mkono ndio unaotumika kutia sahihi ya jambo Fulani liwe baya au zuri.. Hivyo mkono siku zote unawakilisha mamlaka ya Mtu au nguvu zake.
Kadhalika ili ipatikane lugha rahisi ya kuwakilisha roho ya mwanadamu au nafsi yake, ambayo haionekani kwa macho, ndipo lilipotumika neno “moyo” kama mbadala, Kwamfano badala ya kusema “Nina huzuni nyingi rohoni” unaweza kusema “nina huzuni nyingi moyoni”. Au badala ya kusema “nafsi yangu ina huzuni” unaweza kusema “moyo wangu una huzuni” ni kitu kile kile.
Sasa kwanini kitumike kiungo moyo na si kiungo kingine kama figo:
Kama tunavyojua kiungo pekee kinachoendesha na kuzungusha damu katika miili yetu ni moyo. Na ndio kiungo pekee ambacho ni chepesi kuitikia mabadiliko yoyote ya hisia za mwili. Utaona likitokea jambo la kushtusha ghafla, mapigo ya moyo yataanza kwenda kasi!..pakitokea hali ya utulivu sana, mapigo ya moyo yanashuka.. Ni ngumu mtu ashtushwe halafu asikie maini, au figo zinabadilika tabia.. Moyo ni kama vile mtu mwingine wa pili, anaishi ndani ya mwili.
Hivyo tabia hiyo ya kipekee ya kiungo hicho ambacho kipo ndani ya mwili lakini kina uwezo wa kuitikia na kuelewa mambo yanayoendelea nje ya mwili, na zaidi ya yote ndicho kinachozungusha uhai ndani ya mwili, imekifanya kifananishwe na roho au nafsi ya mtu.
Kwahiyo popote pale katika maandiko neno hilo “moyo” linapotumika.. basi fahamu kuwa linawakilisha aidha “nafsi ” au “roho”. Kujua tofauti iliyopo kati ya nafsi na roho unaweza kufungua hapa >> Tofauti ya Nafsi, mwili na roho
Je umempokea Yesu?. Je umempenda Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nguvu zako zote? Au unautumikia ulimwengu na fahari zake?..Kumbuka biblia inasema..
Mathayo 6:21 “kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako”.
Moyo wako upo wapi leo? Kama upo kwa Bwana ni vyema..lakini kama upo katika ulimwengu na fahari zake, kumbuka maandiko yanasema…
Yakobo 4:4 “Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu”
Ndugu kitendo cha kuipenda dunia tu tayari wewe ni adui wa Mungu, haihitaji useme kwamba wewe ni adui wa Mungu, hapana! Kitendo cha wewe kupenda fasheni tu, kitendo cha wewe kupenda kuvaa nusu uchi, kitendo cha wewe kuwa mshabiki wa mipira, kitendo cha wewe kupenda kutazama tamthilia na filamu za kidunia, tayari umejifanya kuwa adui wa Mungu. Na maadui wa Mungu wote! Sehemu yao itakuwa ni lile ziwa la Moto..(Luka 19:27).
Kama utapenda kumpokea leo Yesu, mlango wa neema upo wazi, ila hautakuwa hivyo siku zote..ipo siku utafungwa, tukiwa hapa hapa duniani, utafungwa kwa tendo linalojulikana kama unyakuo. Baada ya unyakuo kupita, kitakachokuwa kimebakia duniani ni dhiki kuu tu!, na baada ya hapo ni mapigo ya vitasa saba kama tunavyosoma katika Ufunuo 16. Duniani patakuwa si mahali salama kabisa. Hivyo kama upo tayari kumpokea Yesu maishani mwako leo, hapo ulipo jitenge kwa dakika chache tafuta sehemu ya utulivu kisha Ungama dhambi zako kwa kumaanisha kukiri makosa yako na kuyaacha. Baada ya hapo, acha vyote kwa vitendo ulivyokuwa unavifanya… Acha udunia wote!! Na hatua ya mwisho tafuta ubatizo sahihi kukamilisha wokovu wako, Ubatizo sahihi ni wa kuzamishwa kwenye maji mengi na kwa jina la Yesu, kulingana na maandiko (Matendo 2:38)
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Shalom, karibu tujifunze maneno ya uzima.
Wengi wetu tunadhani Bwana Yesu alizaliwa akiwa na ufahamu kamili wa kila kitu, au ujuzi wa mambo yote, Hapana alizaliwa akiwa kama sisi kabisa, hajui kitu chochote, japo alikuwa ni Mungu kweli katika mwili.
Ilipasa iwe hivyo, ili kutimiza kusudi la Mungu, la kumfananisha na sisi katika mambo yote ili awe kielelezo cha sisi kuifuata njia yake. Hivyo kwa kuyatazama tu Maisha ya Bwana Yesu tunaweza kujifunza mambo ambayo hata sisi wenyewe tunaweza kuyafanya.
Mpaka Bwana kufikia hatua ya kufahamu siri nyingi sana za Mungu, halikuwa ni jambo alilozaliwa nalo, hapana, biblia inasema..
“Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu”.
Kuendelea katika hekima na Kimo, maana yake ni kukua kila siku katika hekima ya kumjua Mungu, yaani kutoka kiwango kimoja hadi kingine, hatua moja hadi nyingi.. Na hilo halikuja tu hivi hivi, Bali alikuwa na bidii tangu akiwa mtoto, ya kujifunza maneno ya Mungu, kwa kuwatafuta waalimu ili wamsaidie, Na alipokutana nao alikuwa akiwauliza maswali pale ambapo alikuwa haelewi na kutoa maoni yake pale ambapo alikuwa anapaelewa zaidi,..Jambo hilo unaweza kulisoma katika…
Luka 3:46 “Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.
47 Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake.
48 Na walipomwona walishangaa, na mama yake akamwambia, Mwanangu, mbona umetutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni.
49 Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu?
50 Nao hawakuelewa na neno hilo alilowaambia.
51 Akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii; na mamaye aliyaweka hayo yote moyoni mwake.
52 Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu”.
Jaribu kutafakari, kijana wa miaka 12 anatumia siku tatu usiku na mchana, kakaa tu kanisani, akijifunza Biblia, na hiyo ni desturi yake ya mara kwa mara.. Unategemea vipi kijana kama huyo akiwa mtu mzima, atakuwa sawa na watu wengine?
Ni lazima tu, atakuwa katika maarifa ya kumjua Mungu kwa kasi, na ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana, mambo yote hayakumjia tu ghafla ndani yake, labda kazaliwa nacho, hivyo hakuwa na haja ya kuongeza maarifa au kujifunza hapana.
Leo hii, utaona mkristo, hana habari ya kujifunza Biblia, hata akienda kujifunza haulizi maswali, wachungaji wake, au manabii wake, au waalimu wake, yeye ni kusikiliza tu na kuondoka, akiambiwa jambo Fulani hata kama ni gheni kwake, atalipokea tu na kusema AMEN! Baba..Basi..
Kwa mtu ambaye ni msomaji wa biblia, ni lazima tu atakutana na mambo mengi sana yasiyoeleweka, Na Mungu ameyaficha hivyo makusudi, ili atujengee tabia ya kupenda kutafuta, na mwisho wa siku ampe majibu.. Lakini kama utasoma tu biblia kwa kujiburudisha, au kutimiza ratiba, ufahamu kuwa huo sio mpango wa Mungu.
Mungu anataka tujifunze biblia sio, tuisome kama gazeti, Biblia ni kitabu cha mafumbo, hakuna namna mkristo akose maswali ya kumuuliza Mungu..hilo haliwezekani..Embu kaa chini usome kitabu chochote kwa kumaanisha halafu uniambie kama ni mambo yote yaliyopo kule umeyaelewa..Hilo halipo..
Lakini Yesu hakuona aibu ya kutaka kujifunza pale ambapo alikuwa haelewi, na alitumia fursa hiyo vizuri kuwafuata waalimu wake wa torati…Vivyo hivyo na wewe kama unataka kukua katika hekima na Kimo katika kumjua Mungu, wafuate wale waliokutangulia katika Imani, yaani wachungaji wako, manabii wako, mitume wako, waalimu wako, waulize maswali kwa yale uliyojifunza katika biblia..ukiona majibu yao hayajakuridhisha..tafuta tena wachungaji wengine, kawaulize, maswali, hivyo hivyo mpaka Roho Mtakatifu atakufunulia jibu sahihi..
Japo Bwana Yesu alikaa chini ya waalimu, lakini mwisho wa siku yeye ndiye aliyekuwa MWALIMU WA WAALIMU… Alikuwa ni RABI, Alijua siri nyingi za ufalme wa mbinguni, kuliko watu wote waliokuwa duniani, sio tu wale walioishi naye, mpaka pia wale waliomtangulia.
Hata wewe ukiwa ni mtu wa kutoridhika na hali ya ufahamu wako kuhusu Mungu, ukaanza kujifunza, uwe na uhakika kuwa upo wakati, utakuwa ni mtu wa viwango vya mbali sana, na Mungu atajifunua kwako kwa namna ambazo wewe mwenyewe utashangaa.
Anza sasa, kumtafuta Mungu wako, kwa bidii kama za Bwana wetu YESU KRISTO.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Nini maana ya mhubiri 9:11? si wenye mbio washindao katika michezo?
Shalom, karibu tujifunze Neno la Mungu, lakini kabla hatujaendelea, ningependa kwanza uzitafakari hizi habari mbili, kwasababu ndio kiini cha somo letu kilipo, zingatia sana sana hiyo mistari iliyowekwa katika herufi kubwa.
Luka 5:4 “Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, TWEKA MPAKA KILINDINI, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.
5 Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.
6 Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika;
7 wakawapungia mikono washirika wao waliokuwa katika chombo cha pili, waje kuwasaidia; wakaja, wakavijaza vyombo vyote viwili, hata vikataka kuzama”.
Pia, soma..
Yohana 21:3 “Simoni Petro aliwaambia, Naenda kuvua samaki. Nao wakamwambia, Sisi nasi tutakwenda nawe. Basi wakaondoka, wakapanda chomboni; ila usiku ule hawakupata kitu.
4 Hata asubuhi kulipokucha, Yesu alisimama ufuoni; walakini wanafunzi hawakujua ya kuwa ni Yesu.
5 Basi Yesu akawaambia, Wanangu, mna kitoweo? Wakamjibu, La.
6 Akawaambia, LITUPENI JARIFE UPANDE WA KUUME WA CHOMBO, nanyi mtapata. Basi wakatupa; wala sasa hawakuweza kulivuta tena kwa sababu ya wingi wa samaki”.
Nataka ufananishe hizo habari mbili, utaona mara ya kwanza Kristo anakutana na akina Petro baada ya kuwahubiria aliwapa maagizo ya kwenda kuvua samaki, akamwambia atweke mpaka vilindini, akiwa na maana waanze safari ya kutoka pale walipo, waende mbali sana kwenye bahari kuu (Ndipo vilindini) ili wakavue samaki zao. Hatujui walisafiri umbali wa kilometa ngapi, lakini mpaka mtu ufike vilindini, ni sharti uende mbali sana na fukwe..Na walipofika wakazishusha nyavu zao kwa Neno la Bwana, kisha wakapata samaki wengi sana, mpaka nyavu zikawa zinakaribia kukatika kama tunavyosoma hiyo habari.
Lakini tunaona pia katika tukio lingine ambalo ni baada ya Kristo kufufuka, aliwaona tena wakihangaika usiku kuchwa kama pale mwanzo wakitafuta samaki wasipate.. Pengine safari hii Petro alitazamia ataambiwa “atweke mpaka vilindini” kama alivyoambiwa hapo kwanza, wakavue, lakini maagizo yalikuwa ni tofauti kabisa, bali palepale UFUKWENI walipokuwepo wametegesha vyombo vyao, Kristo aliwapa maagizo, wazitupe nyavu zao upande wa pili tu wa chombo. Ndipo walipofanya vile walipata samaki wengi sana tena wakubwa, kiasi cha kuwafanya hata wao washindwe kulivuta lile jarife pale pwani walipokuwepo.
Ni nini Kristo alitaka wanafunzi wake na sisi sote tujue?
Kuna majira Kristo atakupa maagizo ya kukihangaikia kidogo kile unachokihitaji, na mwisho wa siku atakufanyia muujiza mkubwa sana katika jambo hilo.. Lakini pia kuna wakati hatokuagiza ukihangaikie hata kidogo, bali hapo hapo ulipo, atakupatia, kuhangaika kwako wewe kutakuwa ni kukusanya tu.
Mambo haya mawili ni vizuri ukayafahamu, wewe uliyeokoka, kwasababu wapo watu wanadhani, Mungu wa “Mana” amekufa, hawezi kutenda kazi tena leo hii, wanadhani njia pekee aliyobakiwa nayo ya Mungu kukubariki, au kukutendea miujiza ni lazima ukajitaabishe huko vilindini! Basi. Nataka nikuambie hilo kweli linawezekana, na likaja kama agizo la Mungu, lakini pia lile lingine nalo linawezekana, tena sana.
Bwana Yesu alisema maneno haya..
Mathayo 6:25 “Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
26 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?
27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti
29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.
30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?
31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake”.
Hivyo usilipindue Neno la Kristo, kwa kuegemea upande mmoja tu, Yote yawezekana kwa Mungu (Mathayo 19:26), na vilevile Bwana Yesu alisema yote yawezekana kwake yeye aaminiye, sio Mungu tu peke yake, hata kwa mtu yeyote atakayemwamini Mungu, yatawezekana kwake (Marko 9:23). Hivyo ukimwamini Mungu katika njia ile atajifunua kwako katika hiyo, halikadhali ukimwamini katika njia ile nyingine atajifunua kwako katika hiyo. Hakuna formula kwa Mungu. Yeye sio mwanadamu. Ni Mungu wa milimani, pia ni Mungu wa mabondeni,.Njia zake hazitafutikani,
Warumi 11:33 “Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!”
Hivyo huna haja, ya kuogopa lolote, unachopaswa kufanya ni kuhakikisha unatembea naye katika njia zako zote, popote pale ulipo, uwe ni katika vilindi au katika fukwe, matokeo yatakuwa ni yale yale. Mwamini tu, huku ukimtumikia kwa moyo wako wote.
Mtafute Mungu ndugu yangu, hizi ni siku za mwisho, Usitoe kisingizio cha kusema nipo busy, siwezi kuomba, siwezi kwenda ibadani, siwezi kusoma Neno, nina majukumu ya kifamilia, hicho kisingizio hakitakuwa na mashiko siku ile ya mwisho utakaposimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu. Kwasababu wataletwa wenzako kama wewe ambao walikuwa buzy kuliko wewe mmojawapo ni Danieli, lakini watakuambia hatukuacha kumtafuta muumba wetu.
Je! Na wewe unatembeaje na Mungu wako, ukiwa hapa duniani?. Je umemkabidhi Maisha yako? Kama sivyo ni heri ukampokea leo kwasababu hakuna anayejua kesho kutatokea nini. Ondoa hofu ya Maisha, anza kumwamini Mungu, na atakuonekania katika mambo yako yote.
Zaburi 27:1 “Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani”?
Zaburi 23:1 “Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
3 Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji”.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
TUNALINDWA NA NGUVU ZA MUNGU.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.
Chamchela ni nini kwenye biblia?(Zaburi 58:9, Amosi 1:14)
NITAUPATAJE UPENDO WA KI-MUNGU NDANI YANGU?
Tofauti kati ya mtume na mwanafunzi ni ipi kibiblia?
SWALI: Tofauti kati ya mtume na mwanafunzi ni ipi?
Kwanini kuna mahali Bwana Yesu anawaita wale aliowaita mitume, na sehemu nyingine anawaita wanafunzi, tofauti yao ni ipi? Au ni kitu kimoja?
JIBU: Si kila mwanafunzi ni mtume, lakini kila mtume ni lazima awe mwanafunzi wa Yesu.
Mwanafunzi ni mtu ambaye anaketi chini kufundishwa, kupewa ujuzi au utashi au maarifa ya kumsaidia kuishi au kufanya jambo Fulani, Na Bwana Yesu naye alikuwa na watu wa namna hiyo hiyo,
Lakini kumbuka si wote waliomfuata waliitwa wanafunzi wake, isipokuwa wale tu waliokidhi vigezo vyake alivyoviweka, na vigezo vyenyewe ndio hivi;
Luka 14:25 “Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia,
26 Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
27 Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
28 Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?
29 Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki,
30 wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.”.
Lakini Mtume maana yake ni “aliyetumwa”, Wale walioitwa na Bwana Yesu na kuandaliwa kwa jukumu Fulani maalumu waliitwa mitume, ambao walikuwa kumi na mbili tu kwa wakati ule. Na kusudi lenyewe waliloitiwa lilikuwa hili;
Mathayo 28:19 “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa Dahari”.
Mitume pia waliendelea kuitwa na Kristo hata baada ya yeye kuondoka duniani.. Mfano utawaona mitume kama Paulo, Barnaba, na Epafrodito (Wafilipi 2:25)
Hata kwa wakati huu wa sasa, watumishi wote wa Mungu wanaofanya kazi kama waliyoifanya mitume, Yesu anawatambua kama mitume wake, hawa ni Zaidi ya wanafunzi, kwasababu hawawi wakristo tu peke yake, bali Zaidi wanajitaabisha kwa ajili ya ufalme wa mbinguni.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
JINSI MTUME PAULO ALIVYOUTHAMINI WITO WAKE, JUU YA WENYE VYEO.
Nini maana ya “Tumejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii”?
Jibu: Tusome kuanzia juu kidogo,
Mathayo 6:1“ Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.
2 Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu
3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;
4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.
Kwa namna ya kawaida haiwezekani kufanya jambo mkono wako mmoja usiwe na mawasiliano ufanyalo mkono wako wa pili, Kwasababu mwili wako wote umeungamanishwa na kuwa kitu kimoja. Kwahiyo Bwana Yesu alipotoa huo mfano hakumaanisha kuwa tutafute namna ambayo wakati tunatoa sadaka mkono wa kushoto usijue ufanyalo mkono wa kulia. Bali alitumia huo mfano kama kionjo tu!. Ambacho kingetusaidia kuelewa kwa kina anachotaka kumaanisha.
Kwamba sadaka zetu ziwe za siri za hali ya juu, zisiwe za kutangaza tangaza, kiasi kwamba hata wewe mwenyewe kwenye nafsi yako (mwili wako) huitangazi tangazi…Unakuwa unaitoa na kuisahau..
Luka 18:10 “ Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru.
Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.
12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma; HUTOA ZAKA KATIKA MAPATO YANGU YOTE.
13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.
14 Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa”.
Sasa sio kwamba huyo mtoza ushuru hapo juu, hakuwa anatoa zaka, au sadaka.. Alikuwa anazitoa, pengine zaidi hata ya huyo Farisayo, lakini kila alipotoa katika nafsi yake anakuwa anazisahau, hajinyanyui mbele za Mungu, wala hazitaji taji mbele za Mungu, kila siku anajiona kama hajamtolea, anakuwa hazihesabu, anajiona kama bado ana deni kubwa la kumtolea Mungu…. Hivyo hiyo ikamfanya awe wa haki zaidi kuliko ya yule Farisayo, ambaye alikuwa anajiinua inua katika nafsi yake.
Lakini zama hizi ni kinyume chake, hebu mtu amtolee Mungu sadaka Fulani, labda kiwango Fulani cha fedha, utaona jinsi atakavyotangaza kwa watu, atawejiwekea mazingira kila mtu ajue, na hata wakati mwingine kunung’unika nung’unika, anapoona jambo Fulani halipo sawa (kila mara utasikia anataja..sadaka zetu zinafanyiwa hichi au kile!!).. na hata akifaulu hilo (akawa hanung’uniki), utaona anavyojinyanyua kila siku mbele za Mungu katika sala zake.. Akisali utasikia, mwezi uliopita nilikutolea sadaka hii!..wiki iliyopita nikakutolea tena.. jambo hilo atalirudia rudia mara nyingi…kila sadaka anayotoa anaihesabu na anaona ni kama anamnufaisha Mungu kwa sadaka zake na wala si kama ni wajibu wake.
Lakini wakati huo huo yupo mwingine ambaye hawezi kupitisha wiki, hajamtolea Mungu sadaka nono, na kila anapopiga magoti mbele za Mungu anajiona kama hajawahi kumtolea chochote. Sadaka aliyoitoa wiki iliyopita hata haikumbuki! (Huyo ndio mfano wa mtu yule anayetoa sadaka ambayo hata mkono wake mmoja haujui ifanyacho mkono wake wa pili).
Hivyo Neno hilo ni kutufundisha tu, jinsi ya kuenenda mbele za Mungu, ili tupate thawabu, tufahamu kuwa tunapomtolea Mungu, au tunapowapa vitu watu, tusijionyeshe mbele za watu wala mbele za Mungu, Ukishatoa sahau kama umetoa, zaidi ya yote tutafute kumtolea tena na tena.. Ndivyo tutakavyopata thawabu kutoka kwa Mungu, lakini kinyume cha hapo, Bwana Yesu alisema, tumekwisha kupata thawabu zetu.
Bwana atubariki na kutusaidia.
Kumbuka, kama unaisikia injili leo na kuipinga, kama unahubiriwa uache uzinzi, na hutaki kuamua kuacha makusudi, kama unahubiriwa uache ulevi, na wizi na mambo yote machafu hutaki na unatafuta kumtolea Mungu sadaka, biblia inasema “kutii ni bora kuliko dhabihu (1Samweli 15:22)”.. na pia inasema…
Mhubiri 5:1 “Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa Mungu; Maana ni heri kukaribia ili usikie, Kuliko kutoa kafara ya wapumbavu; Ambao hawajui kuwa wafanya mabaya”.
Na pia inasema “Sadaka ya wasio haki ni chukizo;..(Mithali 15:8)” Na tena…
Kumbukumbu 23: 8 “Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya Bwana, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako, yote mawili”.
Usichukue mshahara wako wa kazi ya Bar na kumpelekea Mungu, ukidhani inamfurahisha sana hiyo sadaka.. Yeye anaihitaji roho yako ipate wokovu na si fedha yako. Sadaka ni matokeo ya shukrani, sasa utamshukuru vipi mtu ambaye umemkataa moyoni mwako?..si utakuwa ni mnafiki na kumfanya ahuzunike juu yako?.
Hivyo kama hujampokea Yesu, leo unayo nafasi, kabla ya kufikiria kwenda kumtolea Mungu, fikiria kwanza kuondoa roho ya uasherati, ulevi, kujichua, wizi na nyinginezo ndani yako. Baada ya hapo ndipo fikiria kwenda kumtolea Mungu, na unapomtolea hakikisha hujinyanyui mbele zake.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo: