Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani

Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani

SWALI: Nini maana ya huu mstari?

Mithali  11: 26 “Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani; Auzaye nafaka, baraka itakuwa kichwani pake”.


JIBU: Kuna wakati sukari ilikuwa adimu sana katika taifa letu, baadhi ya wafanyabiashara wakubwa walipoona janga hilo limetokea, wakanunua sukari nyingi, tani kwa matani, wakazificha, hivyo ikaifanya sukari (hata hiyo kidogo iliyokuwepo) kuwa adimu zaidi.. Lengo lao ni sukari izidi kupanda bei ili waiuze kwa bei ya juu sana wapate faida kubwa.

Lakini jambo hili liliwaathiri watu wengi, hususani wafanyabishara wadogo wanaotegemea sukari  kuzalisha bidhaa zao, pamoja na watu wa hali ya chini wasioweza kununua sukari kwa bei ya juu. Matokeo yake ikawa ni watu kulaumu na kuwakasirikia sana wanaofanya vitendo hivyo.

Au wakati ambapo maji ni adimu, baadhi ya watu hupadisha bei, kwa lengo la kujipatia faida kubwa zaidi, watakaa na maji yao kwenye visima mpaka atakapotekea mwenye bei kubwa. Watu wa namna hii ukichunguza utaona wanaishia kulaaniwa sana na watu wanaowazunguka.

Ndio maana ya huo mstari “Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani; Auzaye nafaka, baraka itakuwa kichwani pake”..

watu watampenda na kumbariki Yule ambaye atawauzia huduma yake kama ilivyo desturi ya sikuzote.

1Yohana 3:17  “Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo?”

Na rohoni pia ni vivyo hivyo,..Wakati tuliopo sasa maandiko yalitabiri ni wakati wa njaa kubwa sana ya kiroho, watu wakizunguka huko na kule kutafuta Neno la kweli la Mungu (Amosi 8:11-12). Lakini inasikitisha kuona baadhi ya watu wakificha maarifa, au huduma, kisa tu, hawalipwi vizuri..kumuona mtume/nabii ni sh. Laki moja. Kununua kitabu cha mhubiri Fulani ni sh.elfu themanini. Badala tuuze kwa bei nafuu, tunauza kibiashara, kisa tunafahamu ni lazima tu vitanunuliwa kwasababu sisi ni maarufu.

Bwana atusaidie. Tutoe nafaka tusiizuie

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Maana ya huu mstari ni ipi? Mithali 14:4 ‘Zizi ni safi ambapo hapana ngombe;bali nguvu za ngombe zaleta faida nyingi’.

Kusemethi ni nini katika biblia?

Uga ni nini? Na kazi yake ni ipi kibiblia?

KWA KUWA WASEMA MIMI NI TAJIRI.

Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe;(Mithali 16:2)

Gengeni ni wapi, wale nguruwe walipoteremkia? (Marko 5:13)

KWA WINGI WA WASHAURI HUJA WOKOVU.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments