MUNGU ATAKUUA UKIWA MBAYA MACHONI PAKE.

MUNGU ATAKUUA UKIWA MBAYA MACHONI PAKE.

Mwanzo 38:6 “Yuda akamwoza mke Eri, mzaliwa wake wa kwanza, na jina lake huyo mke ni Tamari.

7 Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa Bwana; na Bwana akamwua”.

Lazima tukumbuke kuwa Mungu anatazama matendo ya kila mmoja wetu katika hii dunia, Na pale yanapovuka mipaka yake aliyoiweka tujue kuwa tunayahatarisha maisha yetu sisi wenyewe.

Vifuatavyo ni vitu ambavyo, havimpendezi Mungu, na kama vipo ndani yako, basi hakikisha vinaondoka mapema sana. Tulishajifunza huko nyuma lakini ni vizuri tujikumbushe tena, ili visiondoke mioyoni mwetu. Tunavisoma katika..

Mithali 6:16 “Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.

17 Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;

18 Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu;

19 Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.

MACHO YA KIBURI:

Kiburi ni kujiona wewe ni bora kuliko wengine, upo juu wa wengine wote, hivyo unawadharau , hutaki kurekebishwa, hutaki kuonywa, hutaki kuwasaidia wengine. watu wa namna hii, ni machukizo mbele za Mungu, katika biblia kulikuwa na mtu aliyeitwa Nabali, ni mfano wa mtu aliyekuwa na kiburi, japokuwa alisaidiwa na Daudi kuangaliwa mifugo yake, lakini bado alimdharau na kumtukana, kisa tu ana mali, na mafanikio, na mwisho wa siku Mungu akamuua. (1Samweli 25:1-38)

Kiburi pia kinachozungumziwa hapo ni kiburi cha uzima. Kisa una afya, ni mzuri, una nguvu, una mafanikio, basi ukielezwa habari za Mungu, wewe ni kudharau, na kudhihaki, na kukebehi, unasema watu wanaomtafuta Mungu ni watu wajinga, wavivu, hawana akili. Kama wewe ni mmoja wapo wa hili kundi la watu, jirekebishe mapema sana, upo hatiani kuuliwa na Mungu.

ULIMI WA UONGO: 

Kilichomfanya shetani apewe adhabu ya kutupwa katika ziwa la moto, ni pamoja na uongo aliokuwa nao tangu mwanzo. Bwana Yesu alisema..

Yohana 8:44 “Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; KWA SABABU YEYE NI MWONGO, NA BABA WA HUO”.

Embu fikiria na wewe pale unapokuwa mwongo mwongo kwa kila jambo, unadhani Mungu atapendezwa na wewe? Hawezi kinyume chake unajitafutia kifo tu na hukumu. Uongo unaharibu mahusiano ya mtu na Mungu kwa kiasi kikubwa sana. Tuziponye ndimi zetu.

MIKONO IMWAGAYO DAMU ISIYO NA HATIA:

Kundi lingine ambalo Mungu halipendi kabisa, ni la wauaji. Wengi wanadhani kuwa muuaji ni mpaka utimilize  tendo lenyewe. Hapana, kitendo tu cha kusema nashika silaha,nashika kisu, panga, n.k. na kwenda kuvamia kuiba, tayari wewe ni muuaji, kwasababu hiyo silaha uliyobeba tayari ulishawaza kichwani mwako, endapo ikitokea shida utaitumia kujihamu, ikiwezekana hata kuua. Mambo kama hayo, yanavuta kifo chako cha kiroho na kimwili kwa haraka sana.(Mathayo 5:21-22). Acha matendo yenye harufu za uuaji nyuma yake. Zitakupunguzia maisha yako hapa duniani.

MOYO UWAZAO MAWAZO MABAYA:

Ni moyo ambao hauna fikra chanya kwa Mungu, au katika kuuendeleza ufalme wa Mungu. Badala yake ni moyo ambao unawaza uzinzi wakati wote, unafikiria mbinu ambazo unaweza kupata pesa ukatumie katika anasa. Moyo ambao unaamka asubuhi unafikiri ukafanye kazi ile baadaye ukamalizie siku yote baa.

Moyo ambao unafikiria utapeli, uporaji, dhulma, hauna nafasi hata mara moja kufikiria hatma ya maisha yake ya baadaye, haumfikirii muumba wake, haufikirii kumtolea Mungu, haufikirii kuifanya kazi ya Mungu. Watu kama hawa Mungu anawaua mapema sana, aidha rohoni au mwilini.

MIGUU ILIYO MYEPESI KUKIMBILIA MAOVU;

Kwa kawaida mwanadamu yoyote ni lazima aone ugumu Fulani, katika kutekeleza jambo ambalo sio la haki, ni lazima ashtuke pale anapoletewa habari ya kwenda kuzini na mke wa mtu, anapoambiwa tule rushwa n.k. Lakini kama wewe ni mwepesi wa kukimbilia maovu, mtu anakwambia twende Disko na wewe unakurupuka kuongozana naye, twende tukaibe, unakurupuka kuenda, twende tukazini mume wangu kasafiri, na wewe unaenda, Ujue mwisho wako utakuwa ni mbaya sana, kwasababu miguu hiyo ni mepesi kukimbilia maovu. (Mithali 1:16 , 7:5-27)

SHAHIDI WA UONGO ASEMAYE UONGO;

Huyu ni zaidi ya mtu anayesema uongo. Huyu anaushuhudia kabisa uongo  kuwa ni kweli. Kipindi kile Yezebeli aliajiri watu wamshuhudie uongo Nabothi kwamba amemkufuru Mungu, ili watu wampige mawe afe ili arithi kiwanja chake 1Wafalme 21:1-16

Hata leo hii, wapo watu ni hodari wa kushuhudia uongo, wanafundishwa kusema uongo ili wasitiri dhambi zao, au za wengine, hilo ni jambo baya sana, ambalo linamchukiza Mungu. Bwana atusaidie tusifanyike mashahidi wa uongo.

NAYE APANDAYE MBEGU ZA FITINA KATI YA NDUGU:

La mwisho ndio hili, unatunga uchonganishi katikati ya ndugu wanaomwamini Mungu, ili wachukiane, wagombane, wasiongee, unavunja umoja wao na upendo wao, ambao Bwana Yesu aliwaombea wawe nao katika Yohana 17. Lakini wewe furaha yako ni kuona hivyo. Jambo hilo linamchukiza sana Mungu.

Wakati Mungu anasema,Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu. Wewe unakuwa mchonganishi..kinyume chake ni kuwa utaitwa mwana wa Ibilisi.

Hivyo tunapoishi hapa duniani tuwe watu wenye Hofu ya Mungu. Tusiishi kana kwamba Mungu hatuoni.. Anatuona, na tunavyozidi kuwa wabaya ndivyo tunavyoyaweka maisha yetu hatarini. Ni wazi kuwa mtoto wa Yuda, alifanya mojawapo ya dhambi hizo na ndio maana Mungu akamuua. Vivyo hivyo na sisi tujichunguze kama mambo hayo yapo basi tuyaweke mbali na sisi.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine

Mada Nyinginezo:

TABIA KUU TATU ZA WAHUBIRI WALIORUDI NYUMA NA KUMWACHA MUNGU.

VIKAANGUKA MACHONI PAKE VITU KAMA MAGAMBA.

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

Rudi nyumbani:

Print this post

Je! kuna madhara kuchukiwa na kila mtu kwasababu huna mali?. Kama biblia inavyosema katika Mithali 14:20?.

Jibu: Tusome,

Mithali 14:20 “Maskini huchukiwa hata na jirani yake; Bali tajiri ana rafiki wengi”.

Na  pia

Mithali 19:4 Inasema  “Utajiri huongeza rafiki wengi; Bali maskini hutengwa na rafiki yake”.


Hizi ni Mithali ziliyoandikwa na Mfalme Sulemani, kwa hekima alizopewa na Mungu, na zipo Mithali nyingine nyingi alizoandika kwa mafunzo na maonyo. Lakini tofauti na inavyodhaniwa na wengi, Kuwa kila Mithali Sulemani aliyoiandika ilikuwa ni agizo! Hapana!. Sio kila mithali tunayoisoma katika kitabu cha Mithali ilikuwa ni agizo!. Mithali nyingi Sulemani alizoziandika zilikuwa zinahusu uhalisia wa jambo Fulani, na si agizo la jambo Fulani.

Kwamfano mimi leo nikisema “Watu wengi walio wapole wanaonewa na kudhulumiwa”. Hapo sijatoa agizo kwamba wapole wasiendelee kuwa wapole tena, waanze kuwa wakali na wakorofi. bali nimezungumza “uhalisia, jambo fulani ambalo lipo!”. Na huo umetokana na mimi kuchunguza mpaka nikaja na jawabu hilo.

Kadhalika Mithali nyingi Sulemani alizoziandika hazikuwa ni maagizo, bali ni uhalisia wa mambo fulani, ambayo yapo!!!  na huo unatokana na uchunguzi alioufanya!..Na mfano mmojawapo alioutoa ambao ulikuwa ni uhalisia na si agizo ndio huu tunaousoma..

Mithali 14:20 “Maskini huchukiwa hata na jirani yake; Bali tajiri ana rafiki wengi”.

Sasa hapa sio kwamba Sulemani, alitoa agizo kwamba.. “kuwa maskini watafute utajiri ili wawe na marafiki wengi”. Hapana hakumaanisha hivyo, Kwasababu ingekuwa ndivyo mbeleni asingekuja kusema tena haya maneno..

Mithali 28:6 “Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake, Kuliko mpotofu wa njia angawa ni tajiri”

Umeona! alisema maneno kwasababu alichunguza na kuona kuwa Walikuwepo Maskini wenye busara na hekima, ambao katika haki yao yote bado hawakupendwa, walichukiwa… Na hapo hapo akaona walikuwepo matajiri wengi ambao katika udhalimu wao walipendwa na wengi. Jambo ambalo ni kawaida hata sasa, mtu aliye na mali hata kama ni mali za haramu atapata marafiki wengi!..(lakini ni marafiki wasiofaa)

Hebu tusome tena mahali pengine Sulemani alipochunguza jambo kama hilo..

Mhubiri 9:14 “Palikuwa na mji mdogo, na watu ndani yake walikuwa wachache; akaja mfalme mkuu juu yake, akauhusuru, akajenga ngome kubwa ili kuupiga.

15 Basi, kulionekana humo MTU MASKINI MWENYE HEKIMA, naye kwa hekima yake akauokoa mji ule lakini hata hivyo HAPAKUWA NA MTU YE YOTE ALIYEMKUMBUKA YULE MTU MASKINI.

16 NDIPO NILIPOSEMA, BORA HEKIMA KULIKO NGUVU; walakini hekima ya maskini hudharauliwa, wala maneno yake hayasikilizwi.

17 Maneno ya wenye hekima yanenwayo taratibu husikiwa, Zaidi ya mlio wake atawalaye katikati ya wapumbavu.

18 Hekima NDIYO BORA KUPITA SILAHA ZA VITA; Lakini mkosaji mmoja huharibu mema mengi”

Umeona hapo?.. Sulemani anamsifu Maskini mwenye hekima, ambaye kwa hekima yake ameuokoa mji, anasema “Bora hekima kuliko nguvu, na hekima ni bora kuliko silaha za vita”.

Mithali 16:16 “Si afadhali kupata hekima kuliko dhahabu? Naam, yafaa kuchagua ufahamu kuliko fedha.

Na japokuwa anamwona maskini huyo hakumbukwi, wala hatapendwa na wengi, wala marafiki wengi, wala hakuna mtu aliyemkumbuka.. Lakini kwa hekima yake ameuokoa mji, na hivyo ipo thawabu yake baada ya maisha haya…

Mhubiri 4:13 “Heri kijana maskini mwenye hekima Kuliko mfalme mzee mpumbavu”.

Kwahiyo  ni vizuri kuzichambua vyema hekima za Sulemani na kuzielewa, kwasababu si kila kitu kilichoandikwa kule ni agizo!..

Tukirudi katika ukristo pia hatujaahidiwa kwamba tukimpokea Yesu tutakuwa na marafiki wengi, au ndio tutapendwa na watu wengi..la! kinyume chake ndio tutachukiwa.. Na kuchukiwa huko sio laana!, bali ndio muhuri wa wito wetu.

Luka 21:16  “Nanyi mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu, nao watawafisha baadhi yenu.

17  Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu”

Vile vile hatujaahidiwa kuwa tunapozaliwa mara ya pili ndio hatutapitia dhiki za hapa na pale.. vipindi vya dhiki vitakuwepo, lakini Bwana ameahidi kuwa atakuwa na sisi hatatuacha.

Bwana Yesu alisema maneno haya..

Ufunuo 2:9 “Naijua dhiki yako NA UMASKINI WAKO, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.

10  Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima”

Mathayo 16:2  “Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi”.

Bwana atubariki na kutusaidia.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine


Mada Nyinginezo:

WAOMBEENI WANAOWAUDHI.

LISHIKILIE SANA LILE AGIZO LA KWANZA.

Mego ni nini kama tunavyosoma katika biblia? (Mithali 17:1)

Mpumbavu ni nani katika biblia? (Zaburi 14:1, Mithali 10:14)

Nini maana ya Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu?

Rudi nyumbani

Print this post

Ni yupi aliyekuwa mkwe wa Musa kati ya Reueli na Yethro?

JIBU: Ukisoma katika kitabu cha Kutoka, utaona kuna habari kama inajichanganya kuhusiana na baba-mkwe halisi wa Musa, Kwamfano Kutoka 2:18 Inasema aliitwa Reueli, lakini sehemu nyingine zote zilizosalia kama vile Kutoka 3:1,4:18, inamtaja kama ni Yethro. Je  kuna makosa ya kiuandishi?

Embu tusome baadhi ya vifungu hivyo;

Kutoka 2:15 “Basi Farao alipopata habari, akataka kumwua Musa; lakini Musa akakimbia mbele ya Farao, akakaa katika nchi ya Midiani; akaketi karibu na kisima.

16 Basi kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja wakateka maji, wakazijaza birika maji, wapate kunywesha kundi la baba yao.

17 Wachungaji wakaja wakawafukuza; lakini Musa akasimama, akawasaidia, akalinywesha kundi lao.

18 Walipofika kwa Reueli baba yao, akasema, Imekuwaje hata mkarejea mapema leo?

19 Wakasema, Mmisri mmoja alituokoa katika mikono ya wachungaji, tena zaidi ya hayo, akatutekea maji, akalinywesha kundi.

20 Akawaambia binti zake, Yuko wapi basi? Mbona mmemwacha mtu huyo? Mwiteni, ale chakula.

21 Musa akawa radhi kukaa kwake mtu yule, naye akampa Musa binti yake, Sipora.

Kutoka 3:1 “Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu”.

Jibu ni kuwa hakuna hitilafu, yoyote ya kiuandishi isipokuwa zamani ilikuwa ni jambo la kawaida mtu mmoja kuwa na jina zaidi ya moja, Kwamfano tukimtazama Yakobo, Mungu alimwambia utaitwa Israeli, Hivyo majina yake yote mawili utayakuta yakiandikwa sehemu mbalimbali katika biblia Lakini mtu ni Yule Yule mmoja.

Vivyo hivyo na Yethro mkwewe Musa, aliitwa pia Reueli, na kwasababu alikuwa ni kuhani, hatushangai kuona akiwa na majina mawili, moja la kwake la asili na lingine la kikuhani.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine

Mada Nyinginezo:

UTAJI ULIOKUWA JUU YA USO WA MUSA.

Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1

NJIA YA KUPATA WOKOVU.

JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI, AU KUTOA TALAKA?

USIKATE TAMAA UNAPOPITIA MAGONJWA.

Rudi nyumbani

Print this post

TABIA ZA WATAKAOMKARIBIA SANA MUNGU SIKU ILE.

Kwa mara ya kwanza Yohana alionyeshwa maono ya jinsi mbinguni kulivyo, na mfumo wake mzima wa utawala ulivyojiunda.

Tukisoma mambo yale tusidhani, Mungu alikuwa anamuonyesha Yohana sinema tu ya mbinguni jinsi kulivyo, Hapana zipo siri kubwa sana zinazotuhusu sisi, endapo tutazitambua.

Leo kwa ufupi tutazama ngazi hizo, na ni jinsi gani zilivyoficha siri za sisi kumkaribia Mungu..

Ukisoma kile kitabu cha Ufunuo, sura ya 4 yote, utaona Yohana alionyeshwa mbingu zikifunga. Na moja kwa moja macho yake yakakiona kile kiti cha Enzi cha Mungu kilichojaa utukufu mwingi.

Lakini kiti hichi hakikusimama peke yake, bali alionyeshwa pia viti 24 ambavyo vimekizunguka kile kiti cha enzi ambavyo vimekaliwa na wale wazee 24, na katikati ya vile viti 24 aliona pia wenye uhai 4 ambao wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi. Na nyuma ya wale wazee 24 kulikuwa maelfu kwa maelfu ya malaika mbinguni  wamemzunguka Mungu, wakimsifu na kumtukuza. Soma Ufunuo sura ya 4 yote.

Embu tusome baadhi ya vifungu kidogo; Tafadhali soma kwa utulivu,usiviruke.

Ufunuo 4:1 “Baada ya hayo naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo.

2 Na mara nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya kile kiti;

3 na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi.

4 Na viti ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wanne, wameketi, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu.

5 Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti na ngurumo. Na taa saba za moto zilikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu.

6 Na mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na mfano wa bahari ya kioo, kama bilauri; na katikati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, walikuwako wenye uhai wanne, wamejaa macho mbele na nyuma”.

Ufunuo 5:11 “Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,

12 wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.

13 Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele.

14 Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu.

Sasa ni vizuri ukajiuliza kwanini walivyozidi kumkaribia Mungu, walionekana na maumbile tofauti tofauti. Ikumbukwe kuwa hao wote wanaozungumziwa hapo ni malaika, hakuna mwanadamu hata mmoja. Jiulize ni kwanini wawe ni wazee, na si vijana, na vilevile kwanini wale wenye Uhai wanne wawe na maumbile kama yale na si vinginevyo.?

Hiyo ni kufunua kuwa rohoni, na sisi tukitaka kumkaribia sana Mungu, basi hatuna budi kupitia hatua kama za wale wanaoonekana wapo karibu sana na Mungu.

Kwamfano tukiwatazama wale wazee 24, wanafunua kuwa ili mtu aweze kumkaribia Mungu sana, ni lazima awe ni mzee rohoni, awe amekomaa siku za wokovu ndani yake. Awe kama Ibrahimu, awe kama Henoko aliyetembea na Mungu kwa miaka 300 bila kumwacha, awe kama Eliya aliyemtumikia Mungu mpaka uzee wake, awe kama Ayubu, Hana, na Simoni, Zekaria na Elizabeti. Ambao hao walitembea katika haki yote na Mungu wao bila kumwacha. Watu wa namna hiyo, wanapomaliza siku zao hapa duniani, na wametembea na Mungu tangu ujana wao, mpaka kufa kwao, basi ni wazee rohoni. Na hivyo watakapovuka kule ng’ambo watakuwa karibu sana na Mungu.

Kwasababu Mungu naye, anajitambulisha kama mzee wa siku (Danieli 7:9). Hivyo na wale watakaomkaribia ni lazima wawe wameshiba siku za wokovu, Lakini ikiwa wewe unataka kuwa mkristo tu wa kufa ili uende mbinguni, hutaki kutenda mapenzi ya Mungu angali ukiwa hapa duniani, hutaki kukua kiroho, ujue kuwa ukifa leo hii, kamwe hutakaa umkaribie Mungu kule mbinguni, utakuwa mtu baki tu, haijalishi umeikwepa hukumu

Kwa urefu wa somo hilo fungua link hii>>

https://wingulamashahidi.org/2021/02/22/tutamkaribia-mungu-kwa-idadi-ya-mvi-zetu-rohoni/

Sasa tupige hatua mbele kidogo, kumbuka hawa malaika 24 ambao walifanana sana na wanadamu wazee 24 ni kweli walikuwa karibu na sana na Mungu, lakini wapo waliokuwa karibu zaidi ya Mungu kuliko wao. Na hao si wengine zaidi ya wale wenye uhai 4.

Wenye Uhai 4 walisimama moja kwa moja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, mbele ya wale wazee 24, Ndio makerubi wa Mungu. Hawa walikuwa na nyuso 4 kila mmoja. Uso wa kwanza upande wa kulia ulikuwa ni wa simba, upande wa kushoto ulikuwa ni wa ndama, upande wa nyuma ulikuwa ni wa Tai, na upande wa  mbele ulikuwa ni kama wa binadamu. Ndivyo Ezekieli alivyoonyesha kwa uwazi wote viumbe hai hao  jinsi walivyo (Ezekieli 1:1-26)

Japokuwa Yohana alionyeshwa upande mmoja mmoja wa kila kiumbe hai huyo kwasababu kulikuwa na sababu ya yeye kuonyeshwa vile, Lakini wote hao walikuwa na sura 4 kila mmoja wao (Soma Ufunuo 4).

Sasa kama tulivyotangulia kusema, haikuwa sinema tu, kwamba Mungu anataka kutuonyesha viumbe hao jinsi walivyo wa ajabu hapana. Bali alikuwa anatuonyesha kuwa na sisi tukitaka kumkaribia zaidi yeye. Ni lazima tuwe kama wao Rohoni, kwamba ni lazima uwe na sura hizo nne, ili ukidhi vigezo vya kuwa karibu sana na Mungu. hivyo tu.

Na leo kwa ufupi tutatazama kila uso wa hao makerubi, unawakilisha nini kwa leo. Tukianzana na ule..

USO WA SIMBA:

Kama tunavyojua simba ni mnyama jasiri asiye na woga,

Mithali 30:29 “Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza, Naam, wanne walio na mwendo mzuri.

30 Simba aliye hodari kupita wanyama wote; Wala hajiepushi na aliye yote;”

Kuonyesha kuwa kama mkristo, ni lazima uvae sura ya ujasiri kwa ajili ya imani yako na injili, kama Yesu Kristo alivyokuwa, na ndio maana anaitwa Simba wa Yuda (Ufunuo 5:6). Yeye hakuogopa mwanadamu yoyote, ilipofika suala la wokovu hata Herode alipotaka kumkamata, aliwaambiwa wale watu akisema “mwambieni Yule MBWEHA”!.. kuonyesha kuwa yeye hababaishwi na mwanadamu yoyote kuhubiri injili.

Vilevile na sisi ni lazima tuwe kama simba tukiwa hapa duniani kwasababu shetani naye hatufuati kama kondoo, bali kama Simba, biblia inasema hivyo katika 1Petro 5:8, Unategemea vipi na sisi tumwendee kwa upole katika kuuharibu ufalme wake?

USO WA NDAMA:

Upande wa kushoto wa vile viumbe walikuwa na uso wa ndama. Kama tunavyojua ndama ni wanyama wa kafara, wa kuchinjwa, wa kuchukua  dhambi za watu n.k. Hivyo hiyo ni kuonyesha kuwa unapokuwa mkristo ni lazima uso wa ndama/mwana kondoo, uwe nao pia. Yaani ukubali kuteseka kila siku kwa ajili ya manufaa ya wengine, na si yako tu peke yako. Ukubali hata kujinyima kwa ajili ya injili,

Paulo alisema..”Ninakufa kila siku”.. 1Wakor 15:31. Hata Bwana wetu Yesu Kristo alikuwa tayari kuutoa uhai wake kwa ajili yetu, ili sisi tupate ondoleo la dhambi. Vivyo hivyo na sisi kama wakristo, tunapaswa tuwe na uso huu wa ndama ndani yetu. Tuwe tayari kufa kila siku kwa ajili ya injili ya Kristo. Kujitoa ikiwemo na mali zetu  na nguvu zetu kwa ajili ya injili., kama alivyofanya Kristo na mitume wake.

USO WA TAI:

Wenye uhai 4 walikuwa na uso wa Tai kwa nyuma. Tai ni ndege anayeiona mbali sana, Jicho lake linaweza kuona chakula kutokea mbali sana, mahali ambapo wewe huwezi hata kumuona juu. Na sio tu chakula, bali pia maadui.

Na ndio maana Bwana Yesu alisema katika siku za mwisho, ni Tai tu ndio watakaoweza kuona chakula cha kweli cha roho kilipo. Wengine wote watakuwa kama kuku, wakisikia Kristo yupo huku wanakimbilia, yupo kule wanakimbilia, manabii wa uongo na imani potofu zikiwachanganya, wanabahatisha kwasababu macho yao hayawezi kuona mbali.

Luka 17:37 “Wakajibu, wakamwuliza, Wapi, Bwana? Akawaambia, Ulipo mzoga, ndipo watakapokutanika tai”.

USO WA MWANADAMU:

Wenye uhai 4 hawa walikuwa pia na nyuso wa binadamu kwa mbele.

Kumbuka mwanadamu, ndiye aliyejuu ya zaidi ya wanyama wote ambao Mungu alishawahi kuwaumba. Mwanadamu anao ujuzi, hekima, utashi, fikra, elimu, ujuzi, maarifa. Kwa kutumia tu utashi aliopewa na Mungu anaweza kubuni na kuvumbua mambo makubwa sana, ambayo yanaweza kumletea matokeo chanya au matokeo hasi. Inategemea na dhima yake ni nini.

Hivyo, Na sisi pia ni lazima tutumie utashi wetu tuliopewa na Mungu, kumpendeza Mungu. Sio kila mahali, tutatumia maombi tu peke yake hapana. Wakati ule Mungu anampa Musa maagizo ya kutengeneza vitu vya hemani, alimwambia akamtafute mtu aliyeitwa Bazaleli, ambaye Mungu atampa  ujuzi na utashi wa uchongaji wa vitu hivyo.

Kutoka 31:1 “Bwana akanena na Musa, na kumwambia,

2 Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda;

3 nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina,

4 ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba”,

Tujiulize je! Sisi tulishawahi kumbunia nini Mungu?  Watu wa ulimwengu wanatushinda, wao kila siku wanambunia mungu wao shetani, mambo mapya kila siku, mengi ya kuwavutia wao, wanamtungia kila aina ya nyimbo za miundo tofauti tofauti, lakini sisi kama wakristo, ujuzi wetu tuliopewa na Mungu tumeuweka kapuni, tukimwimbia Mungu badala tufikirie ni jinsi gani nyimbo zetu zitakuwa zimejaa Roho, sisi tunawaiga wale wa kidunia staili zao.

Bwana atusaidie sana.

Hivyo Bwana atusaidie sana. Nyuso zote hizo 4 tuwe nazo. Yaani tuwe jasiri kama Simba, tuwe wa kujitoa kama ndama, tuwe na jicho la kuona mbali chakula chetu kilipo kama Tai, na pia tuwe na hekima na ujuzi kama mwanadamu.

Tukiweza hayo, basi tujue kuwa tutakuwa karibu sana Mungu, kuliko tunavyodhani, kwasababu shetani anakuwa hana upenyo wa kutuingilia. Kwasababu kila upande kuna uso tunamwona.

Mwisho, kabisa, upako wa wenye uhai hawa wanne ulitembea pia katika nyakati saba za kanisa. Hivyo kama utapenda kufahamu kwa urefu juu ya nyakati hizo na jinsi mihuri ile ilivyofunguliwa basi fungua link hii utakutana na mfufulilizo wa maelezo hayo.

https://wingulamashahidi.org/2018/07/19/mihuri-saba/

Bwana akubariki sana.

Je! Umeokoka ndugu? Je! Una habari kuwa tunaishi katika kipindi ambacho tutashuhudia tukio la kurudi kwa pili kwa Kristo duniani?  Unalifahamu hilo? Kwasababu hakuna dalili hata moja Kristo aliyoizungumzia haijatimia. Ni heri ukayasalimisha maisha yako leo kwake, ili siku ile isikukute pabaya.

Tubu kwa kumaanisha kabisa, kisha kabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo upate ondoleo la dhambi zako.

Jina la Bwana libarikiwe.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine

Mada Nyinginezo:

UNYAKUO.

UFUNUO: Mlango wa 4

PINDO LA VAZI LAKE SASA LIMEREFUSHWA.

IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.

KAMA MKRISTO FAHAMU ZIPO HATUA UTAPIGISHWA NA MUNGU.

NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.

Rudi nyumbani

Print this post

Mahali pa juu palikuwa ni wapi kama tunavyosoma katika biblia?

“Mahali pa juu” ni mahali palipoinuka ambapo watu walikwenda kutengeneza madhabahu na kutoa dhabihu zao.. Mahali hapo panaweza kuwa ni mlimani au mahali  penye mwinuko. Ilikuwa ni heshima kwa Mungu kutengeneza madhabahu mahali palipoinuka, kuonyesha kuwa yeye ni juu ya yote.

Ibrahimu ni moja ya watu wa kwanza kutenengeneza madhabahu mahali pa juu.. Wakati anamtoa Isaka mwanawe, alipanda juu ya Moria, na kutengeneza madhabahu pale, sasa mahali pale alipojenga madhabahu ile ndio mfano wa “mahali pa juu”..

Ifuatayo ni baadhi ya mifano michache juu ya mahali pa juu…

1Samweli 9:11 “Hata walipokwea kwenda mjini, wakakutana na wasichana, wanatoka kwenda kuteka maji; wakawaambia, Je! Mwonaji yuko?

12 Nao wakawajibu, wakasema, Yuko; tazama, yuko huko mbele yako; fanyeni haraka sasa, maana hivi leo amekuja mjini; kwa sababu WATU WANA DHABIHU LEO KATIKA MAHALI PA JUU”

Na pia tunaona kabla Mfalme Sulemani kujenga hekalu lile juu ya mlima Moria, naye pia alikuwa anatoa dhabihuu katika mahali pa juu..

1Wafalme 3:2 “Ila watu walikuwa wakichinja dhabihu katika MAHALI PA JUU, kwa sababu haikuwapo nyumba iliyojengwa kwa jina la Bwana, hata siku zile.

3 Sulemani naye akampenda Bwana, akienda katika amri za Daudi babaye, ila hutoa dhabihu na kufukiza uvumba katika MAHALI PA JUU”

Mistari mingine inayozungumzia mahali pa juu ni pamoja 1Nyakati 16:39, 1Nyakati 21:29.

Lakini pamoja na hayo, walikuwepo pia watu waliotengeneza madhahabu katika mahali pa juu kwaajili ya miungu yao… popote walipopaona pameinuka walizitengeneza madhabahu hizo, na kuitolea dhabihu miungu hiyo, jambo ambalo lilikuwa ni chukizo kubwa sana kwa Bwana.

1Wafalme 14:22 “Basi Yuda wakafanya maovu machoni pa Bwana; wakamtia wivu, kwa makosa yao waliyoyakosa, kuliko yote waliyoyafanya baba zao.

23 Maana hao pia wakajijengea MAHALI PA JUU, na nguzo, na maashera, juu ya kila kilima kirefu, na chini ya kila mti wenye majani mabichi”.

Unaweza pia kusoma 2Wafalme 16:4, 2Wafalme 17:9-11,29, utaona jambo hilo hilo..

Swali ni je! Mahali petu pa juu pa leo ni wapi?..mahali ambapo tunaweza kumtengenezea Mungu wetu madhahabu inayompa heshima yeye?.

Tusome,

Yohana 4:19  “Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii!

20  Baba zetu waliabudu katika MLIMA HUU, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia.

21  Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu.

22  Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.

23  LAKINI SAA INAKUJA, NAYO SASA IPO, AMBAYO WAABUDUO HALISI WATAMWABUDU BABA KATIKA ROHO NA KWELI. KWA MAANA BABA AWATAFUTA WATU KAMA HAO WAMWABUDU

24  Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli”

Umeona mahali petu palipoinuka leo ni wapi?..Si milimani, wala si mahali penye miinuko, bali ni katika roho zetu. Huko ndiko madhabahu za Mungu aliye juu zinapotengenezwa.

Je ndani ya roho yako ipo madhabahu ya Mungu?..au ya miungu?..Haijalishi utakuwa unakwenda kanisani, au unatoa sadaka lakini kama mahali pa juu (yaani ndani ya roho yako), hakuna madhabahu ya Mungu, basi fahamu kuwa bado unaitumikia miungu migeni. Kama moyoni mwako kuna anasa, ulevi, wizi, uasherati, na mengineyo, bado wewe ni najisi mbele za Bwana.

Mathayo 15:19  “Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano”.

Bwana atusaidie tumjengee madhabahu bora katika roho zetu.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine


Mada Nyinginezo:

Nini maana ya “heri mtu asiyekaa barazani pa wenye mizaha?”

Kwanini madhabahu zilitengenezwa kwa mawe yasiyochongwa?

Mungu anaposema “nitaliweka jina langu” ana maana gani?

Swali: Kurushwa upesi kunakozungumziwa katika Danieli 9:21 ndio kupi?

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

Rudi nyumbani

Print this post

KANSA/SARATANI INATIBIKA.

Ni kweli Mungu amewapa wanadamu maarifa, ili yale yanayowezekana katika uwezo wao yatendeke, lakini  ipo wazi kuwa si kila tatizo mwanadamu anaweza kulitatua haijalishi ataonyesha bidii kubwa kiasi gani.

Yapo magonjwa ambayo, sisi kama wanadamu hatuwezi kuyatibu, isipokuwa Mungu tu peke yake.

Yeye mwenyewe alisema..

Yeremia 32:27 “Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza”?

Na sehemu nyingine pia Yesu alisema..

Mathayo 19:26b … Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu YOTE YAWEZEKANA.

Ikiwa na maana hakuna moja linaloshindikana kwake.

Huo ugonjwa wa Satarani, iwe ni ya koo, au ya damu, au ya ngozi, au ya matiti, au ya Shingo ya mfuko wa kizazi, au ya utumbo, au kongosho, au ini, au Mapafu ,au ubongo, au macho, au mifupa, au misuli, au Matezi n.k

Yote hayo, si kitu kwa Mungu. Kumbuka Sababu nyingine kubwa iliyomleta Bwana Yesu duniani, ilikuwa ni kutuponya magonjwa yetu. Na ndio maana ilimgharimu ateseke sana pale msalabani kwa mateso mengi, ili kwa kupigwa kwake kule wewe na mimi tupone.

1Petro 2:24 “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa”.

Mathayo 8:16 “Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya WOTE waliokuwa hawawezi,

17 ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu”.

Hivyo, anachotaka kwanza kwako, ni wewe umwamini kwa moyo wako wote. Utubu dhambi zako zote, ikiwa ulikuwa bado hujamkaribisha katika maisha yako, Kisha baada ya hapo ndipo akuponye magonjwa yako yote kama alivyoahidi katika Zaburi 103:3.

 “Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,”

Hivyo ukiwa upo tayari leo, kutubu dhambi zako, na kumkaribisha Bwana Yesu katika maisha yako. Basi, fuatisha sala hii ndani ya moyo wako kwa imani, ukimaanisha kabisa kumgeukia yeye, na kwamba unamuahidi kuwa akishakuponya utamtumikia yeye daima. Ikiwa upo tayari basi hapo ulipo ikiwa upo katika mahali pa utulivu, unaweza kupiga magoti yako, kisha sema sala hii kwa Imani;

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU  MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa kama utakuwa umesema sala hiyo kwa Imani, na kwa kumaanisha kabisa kutoka katika moyo wako. Basi Kristo Yesu ameshakusamehe, hivyo kuwa na amani, na kuanzia sasa uwezo wa kukuponya anao.

Basi nitakwenda kukuombea ugonjwa wako, Kisha Bwana atakufanyia uponyaji.

“Bwana Yesu, nakushukuru wa mwana wako huyu, ambaye ameona kuwa hakuna kimbilio lingine isipokuwa wewe. Naomba Bwana ukamponye magonjwa yake yote yanayomsumbua, iwe ni saratani, au mengine yoyote. Haijalishi madaktari wamesema amebakiwa na wiki mbili aishi au miaka 10. Tunafahamu kuwa wewe ndiye mponyaji. Hivyo nakuombwa Bwana, umponye Mama/dada/baba/kijana/mtoto huyu, anayesoma ujumbe huu. Na kuanzia sasa akawe mzima na huru, akakutumikie na kulitangaza jina  lako daima kwa watu wote.

Asante Bwana kwa kumponya. Amen”.

Hivyo, kuanzia sasa, uponyaji wako umeshaingia katika mwili wako. Maombi tuliyoyaomba ni mafupi tu, lakini uamini kuwa tayari yameshaumba uponyaji katika mwili wako. Hivyo nachotaka kwako kuanzia sasa, utazame, mahali unapoumwa, na pia anza kufanya mazoezi, au pashughulishe pale ambapo ulikuwa huwezi kufanya chochote, au maajabu ya Yesu Kristo utayaona.

Bwana akubariki sana.

Kwa mawasiliano ili kujifunza zaidi biblia/ Ushauri/ Maombezi/ Shuhuda/Ibada, basi wasiliana nasi kwa namba hizi +255789001312/ +255693036618

Bwana akubariki.

Yerema 30: 17a “Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana,..”

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:

Mada Nyinginezo:

YESU MPONYAJI.

JE! UKIMWI UNATIBIKA?

SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.

USIKATE TAMAA UNAPOPITIA MAGONJWA.

NITAUPATAJE UPENDO WA KI-MUNGU NDANI YANGU?

Rudi nyumbani

Print this post

JE! NA SISI NI SHABA ILIAYO NA UPATU UVUMAO?

Jina la Bwana wetu na mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe daima.. Karibu tujifunze maneno ya uzima.

Mtume Paulo aliandika hivi;

1 Wakorintho 13:1 “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, KAMA SINA UPENDO, NIMEKUWA SHABA ILIAYO NA UPATU UVUMAO.

2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.

3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu”.

Kifaa chochote cha shaba kikigongwa, au kupulizwa, huwa kinatoa sauti Fulani, kwamfano zile kengele kubwa za kanisani, huwa zinapogongwa basi sauti yake inaweza kusikika mbali kidogo, lakini hasara yake ni kuwa, sauti zile huwezi kuzisikia kwa muda mrefu, zitaenda kwa muda tu na baada ya sikunde tatu au nne zitakwisha kabisa nguvu yake, ni baada ya hapo utaona ukimya mkubwa, hadi zitakapogongwa tena.

Vivyo hivyo na upatu. Upatu ni chombo ambacho kinamuundo wa sahani pana, ambazo kimsingi zinakuwa mbili, sasa hizo sahani zikishagonganishwa pamoja nazo huwa zinatoa sauti Fulani.. Na zenyewe vivyo hivyo, , unaweza kudhani sauti zao zitadumu kwa muda mrefu, lakini baada ya sekunde kadhaa zitaendelea kama mwangwi tu, na mwisho wa siku  zitafifia na baadaye kurudia ukimya wake tena kama mwanzo.

Ndivyo Mtume Paulo alivyoliona kanisa la Korintho na kuwaongezea habari hiyo, aliliona ni kanisa lililokuwa na bidii kubwa sana katika vipawa na karama za Rohoni, Mtume Paulo akilizungumzia hilo katika sura iliyotangulia ya 12. Linanena kwa lugha sana, lina karama zote za Roho, lakini limesahau UPENDO ambao ndio kiini cha Ukristo.

Akawaambia, mtu unaweza ukawa na vyote hivyo, unaweza hata ukautoa mwili wako kuungua moto, lakini kama huna Upendo wa kweli wa Ki-Mungu ndani yako wewe ni sawa na shaba iliayo na upatu uvumao, yaani hayo matendo yako yote hayatakufikisha mbali.. Kama utaotoa mwili wako uungue moto kwa nia ya kujionyesha wewe ni shujaa, au upate sifa, lakini huna Upendo wa kweli na Yule mtu kama jirani yako, wewe sio kitu, akiwa na maana, vitendo vyako vyote hivyo havitakufikisha mbali, mambo hayo yatabatilika tu baada ya muda Fulani kupita.

Na ndo maaana leo hii unaweza kuona kuna watu wakishafanyiwa jambo Fulani na Mungu, basi siku za kwanza kwanza wanajitoa kweli kweli kwake, lakini ukishapita muda fulani utaona wanapoa au wanauacha wokovu kabisa..Sasa hao ndipo ile Shaba iliayo na upatu uvumao, kwasababu kilichowafanya wamfuate Mungu haukuwa UPENDO wao kwake, bali kwasababu walifanyiwa/ watafanyiwa jambo Fulani na Mungu..Hawajui kuwa tabia moja ya  upendo  ni uvumilivu,

Paulo aliendelea kusema..

1Wakorintho 13:4 “Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;

5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;

6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;

7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.

8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika”.

Kumbuka Mungu alitupenda BILA SABABU YOYOTE. Sio kwamba tulikuwa wema, au tulistahili, au tulimpa fedha, au chochote, hapana Yeye alitupenda tu, na sisi anataka tuwe na Upendo kama huo kwake, na kwa wanadamu wenzetu. Huo ndio unaoitwa UPENDO wa AGAPE (Upendo wa Ki-Mungu). Tunakuwa tayari kuwasaidia wengine kiroho, hata kama wanatupenda au hawatupendi, wanatusaidia au hawatusaidii. Ndivyo Mungu anavyotaka. Yeye anawanyeshea mvua yake waovu na wema.

Lakini tukikosa hayo yote, na huku tunataka kujaribu kumtumikia Mungu, na huku hatutaki kuwa kuvumilia, hatutaki kumwamini, hatutaki kuacha husuda, na majivuno  hatutaki kufadhili, tujue tu hizo ni mbio za sakafuni, hazitusaidii chochote.

Hata kama tutakuwa tunaona maono mengi makubwa kiasi gani, , bado mbele za Mungu sisi sio kitu.

Kuna mchungaji mmoja huko Jamaika, alikuwa sio tu ni mchungaji mwenye kanisa kubwa, lakini pia alikuwa ni mtu mwenye Karama kali sana ya kinabii, kiasi kwamba, aliposimama madhabahuni, kabla mtu hajaingia kanisani akiwa pale mlangoni tu, aliweza kumtambua na kumwambia, Fulani kwanini jana ulimdanganya mke wako na kuwambia hiki na hiki.. Na saa hiyo hiyo Yule mtu alidondoka kwa machozi mengi akilia na kuomboleza amemkosea Mungu. Mchungaji huyu aliogopeka na kuonekana ni mtakatifu sana.

Lakini siku moja, wakiwa katika ibada ya nguvu sana, na Roho Mtakatifu alishuka katikati yao, alisikia kuhukumiwa moyoni, ndipo akasimama huku akilia na kuliambia kanisa, leo ninatubu dhambi zangu, kwasababu nimekuwa nikilificha kanisa na Roho Mtakatifu, kwa tabia yangu ya Ushoga, ambayo nimekuwa nayo kwa muda mrefu, na nimeshazini na wanaume wengi sana.

Kanisa liliposikia vile liliishiwa nguvu, mpaka wakataka kusitisha karama zote za kinabii katika kanisa, kanisa liwe linaendelea tu hivyo hivyo bila karama yoyote ya Roho.

Unaona! Tatizo sio karama, tatizo ni upendo (Hofu )  wa mtu aliokuwa nao kwa Mungu. Huyu nabii alikuwa ni Upatu uvumao. Hata sasa tunapaswa tujihakiki sana, sisi kama wachungaji, manabii, wainjilisti, na vilevile washirika. Je! Utumishi wetu unaendana na Upendo halisi wa Mungu?. Tusije tukawa ni watu wa kutaabika usiku na mchana, tunatumika kwa nguvu nyingi, tunaona Mungu akiwafungua na kuwaponya wengi, kumbe nyuma ya pazia Mungu anatuona tunafanya kazi bure.

Bwana atusaidie tuupe Upendo kipaumbele cha kwanza. Kwasababu tukimpenda Mungu, hatutaona sababu ya kumvunja moyo kwa matendo yasiyompendeza.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:

Mada Nyinginezo:

UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?

NGAZI 7 AMBAZO MKRISTO NI LAZIMA AZIPANDE KUUFIKIA UKAMILIFU.

NJIA YA KUPATA WOKOVU.

JE UPENDO WAKO UMEPOA?

UFUNUO: Mlango wa 3 part 3

Rudi nyumbani

Print this post

USIWE MSIKIAJI TU! BALI MTENDAJI.


Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia..

Neno la Mungu wetu linafananishwa na vitu vingi katika biblia, kuna mahali linafananishwa na “Taa” (Zab.119:105)”, sehemu nyingine linafananishwa na Upanga wa roho (Waebrania 4:12, Waefeso 6:17)” Na kuna sehemu linafananishwa na “Kioo”. Na leo tutajifunza ni kwa namna gani linafananishwa na kioo, ili tuelewe tabia nyingine ya Neno la Mungu.

Kama tunavyojua kioo kazi yake ni kuakisi taswira ya kitu. Kwa mfano mtu anapotaka kujijua yupoje kimwonekano, hususani uso wake, hakuna namna anaweza kujua uso wake upoje, bila kutumia kioo. Akitaka kujua uso wake upoje na sehemu gani na gani afanye marekebisho ni lazima atatumia kioo kama yupo peke yake.

Kikawaida mtu mwenye busara, anapoamka asubuhi, baada ya kufanya usafi wa mwili wake, kabla hajatoa mguu wake kutoka nje, kwenda kwenye shughuli zake ni lazima ajitazame kwenye kioo.. Ili ajihakiki kama uso wake upo sawa au la!, atajihakiki kama nywele zake zimechanika vizuri, isije kuwa upande mmoja kitana hakijapita vizuri, vile vile atajihakiki hakuna tongotongo lililobaki machoni n.k Hivyo kama kuna kasoro yoyote, atairekebisha pale pale akiwa na kioo chake kabla hajaondoka, kwasababu kioo hakidanganyi!..

Lakini mtu asiyejali, anapoamka asubuhi anaweza kujiangalia mara moja kwenye kioo, akajiona kasoro zake kwamba hajachana nywele, wala hajajipaka mafuta usoni… na kwa kupuuzia atasema nitarekebisha hizo kasoro ndogo muda mfupi  kabla sijaondoka.. watu wa namna hiyo  kama ukichunguza, mara nyingi wanajikuta wanaondoka pasipo kuchana nywele, au kuosha uso vizuri, au kupaka mafuta… Na Utaona baadaye wakishafika mbali  na kupita karibu na kioo chochote huko mjini ndio wanakumbuka aa! kumbe hizi nywele sikuzichana tena!…. Au..aaa nilisahauje tena kupaka mafuta usoni, na tayari nilikuwa nimeshayaandaa pale?.

Sasa hiyo ni kwasababu gani?. Ni kwasababu walijitazama kwenye kioo, na badala ya kurekebisha kasoro zao wakati ule ule walipokuwa wanajitazama kwenye kioo, wakapuuzia wakijitumainisha kuzirekebisha baadaye!. Na mwisho wa siku wanajisahau kuwa bado hawajachana nywele, au kupaka mafuta.na wanajikuta wanaondoka hivyo hivyo.. (majuto ni baadaye wameshafika mbali)

Na ndio Neno la Mungu lipo hivyo hivyo, pindi tunapolisikia Lile ndio KIOO chetu!!.. Linatuonyesha kasoro zetu!… kasoro ambazo hatuwezi kuziona kwa macho! Lenyewe linatuonyesha.. Na lengo la kutufumbulia kasoro zetu, ni ili sisi tuzirekebisha Papo kwa Hapo, na wala si kusubiri kesho au baadaye!.. Hapana bali papo kwa hapo.. Maana yake tunapolisikia Neno la Mungu tunalitendea kazi saa hiyo hiyo, hatuliweki kiporo.. Hiyo ndio tabia ya Neno la Mungu!. Hebu tusome mistari ifuatayo…

Yakobo 1:22  “Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.

23  Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo.

24  Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo.

25  Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake”

Umeona hapo?.. “Anajiangalia, kisha anaenda zake na kusahau alivyo”

Neno la Mungu linapokuja mbele yetu, na kuzifunua kasoro zetu, hata kufikia kukubali  kuwa sisi ni wakosaji… hapo ni sawa na kioo kimewekwa mbele yetu kutuonyesha kasoro zetu. Na hivyo Mungu wetu anachokitegemea kwetu ni sisi kujirekebisha wakati ule ule, na si kusubiri baadaye…

kwasababu tukisubiri baadaye, tutajikuta unarudia kujiona tupo sawa! hatuna kasoro yoyote..(Unajikuta unajisahau kuwa wewe ni mtu wa namna gani)..utajiona huna kasoro zozote. Na ndicho kinachowatokea wengi leo. Utaona mtu kasikia injili leo, na kweli imemchoma na kapata kila sababu za kutubu!. Lakini moyoni mwake hayupo tayari kutubu pale pale, anasema atatubu tu!.. pasipo kujua kuwa kioo kipo mbele yake kwa wakati huo, kikishaondoka hapo, kinachofuata ni kujisahau tu yeye ni mtu wa namna gani.

Ndio maana biblia imetuonya hapo juu.. kuwa tusiwe wasikiaji tu!, bali watendaji wa Neno.

Je na wewe ni msikiaji tu? Au ni mtendaji pia!.. Ni maneno mangapi ya Mungu umeyatendea kazi  saa hiyo hiyo baada ya kuyasikia?. Je! Siku ile uliposikia na kushuhudiwa kuwa wazinzi wote watatupwa katika lile ziwa la moto, ulichukua hatua gani?. Je uliacha uzinzi kwa vitendo au kwa mdomo tu!..Je siku ile Neno la Mungu lilipokushuhudia moyoni mwako kuwa fashion, na mavazi yasiyo ya kujisitiri ni dhambi mbele za Mungu, ulichukua hatua gani??. Uliyaacha siku hiyo hiyo au ulisema nitayaacha siku moja!!..

Kumbuka biblia inasema saa ya wokovu ni sasa, na wakati uliokubalika ndio huu. Inawezekana na leo tena umepata nafasi ya kusikia maneno yale yale ya Bwana, kuwa wazinzi, waasherati, wezi, wanaovaa mavazi ya nusu tupu na ya kuonyesha maungo, wanaotazama picha za ngono mitandaoni, wanaojichua, wanaoupenda ulimwengu kuliko kumpenda Mungu..n.k wote hao hawataurithi uzima wa milele. Hichi ni kioo kimewekwa mbele yako!.. kinakuonyesha kasoro zako, ni heri ukazirekebisha sasa, usingoje kesho wala baadaye.

Kama unataka kuzirekebisha sasa, hapo ulipo anguka piga magoti, na kisha kiri mbele za Baba wa mbinguni kuwa umekosa, na tubu kwa kudhamiria kutozifanya tena, kama ulikuwa unafanya uzinzi na uasherati unaachana na mtandao wote uliokuwa unafanya nao uasherati, kama ulikuwa unavaa nguo za kizinzi, unazichoma sasa hivi baada ya toba yako, wala usimpe mtu mwingine na wala usizingojeshe kesho, vivyo hivyo na mambo mengine yote..unayaacha kwa vitendo, angali bado kioo kipo mbele yako sasa.

Na baada ya kutubu hivyo, hatua inayofuata ni ya muhimu sana, nayo si nyingine zaidi ya ubatizo!. Ubatizo sahihi ni ule wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo kulingana na Matendo 2:38, Na baada ya kubatizwa Roho Mtakatifu atakusaidia kufanya yaliyosalia, kwasababu tayari wewe utakuwa milki yake halali.

Bwana akubariki na Bwana atusaidie.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:


Mada Nyinginezo:

MUUNGANO WA DINI NA MADHEHEBU YOTE, UMEKARIBIA.

NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE

UFUNUO: Mlango wa 1

Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?

WAKATI WA JIONI KUTAKUWAKO NA NURU.

Rudi nyumbani

Print this post

Baghairi ni nini kama tunavyosoma katika 2Wakorintho 11:28?

Baghairi ni neno la kiunganishi lenye maana ya… “Mbali na”. Kwamfano nikitaka kusema.. “Mbali na yote ninayoyapitia bado nitasimama imara katika Imani”..naweza kuisema sentensi hiyo kama ifuatavyo “Baghairi ya yote ninayoyapitia bado nitasimama imara katika Imani”

Sasa katika biblia hilo neno limeonekana mara moja tu!. Katika kile kitabu cha 1Wakorintho 11:28

1Wakorintho 11:27 “katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi.

28 BAGHAIRI ya mambo ya nje, yako yanijiayo kila siku, ndiyo maangalizi ya makanisa yote.”

Jambo dogo tunaloweza kujifunza kupitia mstari huo, ni kwamba.. Mtume Paulo, pamoja na wakristo wa kwanza walipitia dhiki nyingi, kwaajili ya Injili na wala hawakuikana imani, Ndio maana ukianzia juu kidogo, mwa mstari huo, utaona hilo jambo…

Waebrani 13:23 “Wao ni wahudumu wa Kristo? (Nanena kiwazimu), mimi ni zaidi; katika taabu kuzidi sana;

katika vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi.

24 Kwa Wayahudi mara tano nalipata mapigo arobaini kasoro moja.

25 Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini;

26 katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang’anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo;

27 katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga

mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi.

28 Baghairi ya mambo ya nje, yako yanijiayo kila siku, ndiyo maangalizi ya makanisa yote”.

Bwana atusaidie tuzidi kujikana na kujitoa kwaajili ya injili.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:


Mada Nyinginezo:

Biblia ina maana gani inaposema akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko?

Neno Bildi linamaanisha nini kwenye biblia(Matendo 27:28) ?

Santuri ni nini? (Danieli 3:5,10)

Je ni kweli imani ya mtu ndiyo itakayomuokoa, na si kitu kingine?

LANGO LIMEBADILIKA.

Rudi nyumbani

Print this post

Je! Mfalme Abiya na Mfalme Asa walikuwa ni ndugu?

Katika 1Wafalme 15:2 na 1Wafalme 15:10 tunaona wote mama yao ni mmoja, ambaye ni Maaka, binti Absalomu. Lakini Mstari wa 8 unasema ni mtu na mwanawe.

Jibu: Tusome,

1Wafalme 15:1 “Mwaka wa kumi na nane wa mfalme Yeroboamu mwana wa Nebati, ABIYA alianza kutawala juu ya Yuda

2 Miaka mitatu akatawala huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa MAAKA, BINTI ABSALOMU…………..

8 Abiya akalala na baba zake, wakamzika mjini mwa Daudi. Akatawala Asa mwanawe mahali pake.

9 Mwaka wa ishirini wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, ASA ALIANZA KUTAWALA JUU YA YUDA.

10 Akatawala miaka arobaini na mmoja huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa MAAKA, BINTI ABSALOMU”

Ni muhimu kufahamu kuwa katika biblia, hakuna Neno “BABU” wala “BIBI”. Neno bibi katika biblia lilitumika tu kuwakilisha “Mwanamke mstahiki” kama vile bibi-arusi, au mwanamke mwenye hadhi Fulani (soma Esta1:18, Mwanzo 16:9) lakini sio “mama wa mama” kama leo hii tunavyolitumia, kwamba  wale waliowazaa mama zetu au baba zetu tunawaita “Bibi” au wale mababa waliowazaa baba zetu tunawaita “Babu”. Katika biblia hilo jambo halipo… Yule aliyemzaa baba anaitwa hivyo hivyo “Baba” na Yule aliyemzaa mama anaitwa hivyo hivyo “mama”..haijalishi ni vizazi vingapi vitapita, Yule babu wa babu wa babu, bado ataitwa baba tu!

Kwamfano utaona Mfalme Hezekia katika biblia ambaye alikuwa ni kitukuu cha 13 cha Mfalme Daudi, Lakini Mungu anamtaja kama Daudi ni baba yake na si babu yake. (soma 2Wafalme 20:5) unaweza kusoma pia,  2Nyakati 21:12, kutoka 3:15, Hesabu 32:8, kumbukumbu 1:8, Yoshua 24:2, Waamuzi 2:1, 1Samweli 12:6. N.k. Utaona jambo hilo hilo..

Kwahiyo tukirudi kwenye swali letu, ni kwamba huyu Maaka alikuwa ni mama wa Mfalme Abiya na ni bibi wa mfalme Asa, kwasababu Asa alikuwa ni mtoto wa Mfalme Abiya kama tunavyosoma hapo katika mstari wa 8.

1Wafalme 15:8 “Abiya akalala na baba zake, wakamzika mjini mwa Daudi. Akatawala Asa mwanawe mahali pake”

Kwahiyo biblia ingeweza kumtaja Maaka kama ni bibi wa Asa, badala ya mama lakini haina hilo neno bibi, halipo bali “mama” ndio maana unaona imewataja wote wawili (Abiya na Asa) kwamba mama yao ni mmoja, anayeitwa Maaka.  Na kama ukizidi kuendelea kusoma habari hiyo utaona, huyu Asa alipoingia tu katika ufalme alimtoa bibi yake huyo katika umalkia kwasababu alikuwa ni mwovu mbele za Bwana, kwa namna ya kawaida ni ngumu mtu kumtoa kwenye umalkia mama yake mzazi kwasababu huwa kunakuwa na uhusiano mkubwa sana wa tabia ya mtoto wa kiume na mama yake.

Sasa kwanini Biblia isitumie maneno “Babu” au “Bibi” na badala yake inatumia tu Baba au Mama, haijalishi ni vizazi vingapi vimepita?

Ni kwasababu Mungu anataka kutufundisha jambo Fulani la kiroho, kwamba na yeye mwenyewe si BABU yetu, bali ni BABA YETU haijalishi ni vizazi vingapi kabla yetu.

Kwa ufupi Mungu hana “wajukuu”. Huwezi kusema mimi ni mjukuu wa Mungu, sisi wote ni watoto wa Mungu, na Mungu wetu ni Baba yetu.. ndio maana kaondoa cheo cha “Ubabu” katika maandiko yake.

Mwanao utakayemzaa hatakuita wewe baba, na Mungu amwite Babu, bali atakuita wewe “baba” na Mungu atamwita “BABA” ya herufi kubwa!!. Kwasababu wewe ni kivuli tu! Cha Baba halisi aliye mbinguni.

Waefeso 3:14 “Kwa hiyo nampigia Baba magoti, ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa”.

Maana yake ni kwamba kwa chochote kile unachokifanya anakuchukulia wewe kama mwanae, na baba yako wa kimwili anamchukulia kama mwanae..hivyo katika roho wewe na baba yako wa kimwili ni mtu na kaka yake, hana upendeleo!!. Ukifanya linalostahili makosa atakuadhibu kama mwanae, na si kama mjukuu na baba yako vile vile atamwadhibu kama mwanae.. Kadhalika mkifanya mambo mazuri wote anawapa thawabu kama wanae.

Lakini kumbuka si wote katika hii dunia, Mungu ni Baba yao… wengi bado hawajafanyika watoto wa Mungu, tofauti na inavyoaminika na wengi leo kwamba sisi wote ni watoto wa Mungu! La huo sio ukweli hata kidogo.. wengi ni watu tu walioumbwa na Mungu!, lakini si watoto wa Mungu. Biblia inasema ili tufanyike watoto wa Mungu ni lazima tupasi huu mtihani hapa chini…

Yohana 1:11  “Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.

12  BALI WOTE WALIOMPOKEA ALIWAPA UWEZO WA KUFANYIKA WATOTO WA MUNGU, NDIO WALE WALIAMINIO JINA LAKE;

13  waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu”

Swali ni je!.. Umempokea?..ili upewe huo uwezo wa kufanyika mwana?..

Kama hujampokea fahamu kuwa bado wewe sio mtoto wa Mungu, huwezi kuwa mrithi wa ufalme wa mbinguni. Kwasababu katika hali ya kawaida watu hawawarithishi watu wasio watoto wao mali zao. Vivyo hivyo Mungu hawezi kuwarithisha wale wasio wanawe urithi wake.

Kama unatamani kwenda mbinguni na kuurithi uzima wa milele, leo hii mpokee Yesu maishani mwako, na dhamiria kuacha dhambi na katafute kubatizwa ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu (Matendo 2:38). Na baada ya hapo, Roho Mtakatifu atakayeingia ndani yako atakupa uwezo wa kufanyika mwana, na Mungu kwako atakuwa Baba.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:


Mada Nyinginezo:

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

KWANINI UNAPASWA UWE BIBI ARUSI NYAKATI HIZI ZA MAJERUHI?

Kwa jina lake Ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa.

Mbari ni nini kibiblia?

HAKUNA MTU ANIONDOLEAYE, BALI MIMI NAUTOA MWENYEWE

Rudi nyumbani

Print this post