Jiepusha na dhambi ya wivu/husuda ambayo mwisho wake ni mauaji.
Silaha moja kubwa shetani anayoitumia kuwadhuru watu ni wivu…mtu mwenye wivu ni rahisi kutumiwa na shetani kwa viwango vikubwa sana… Mauaji mengi yanasababishwa na wivu, uchawi mwingi unatokana na wivu, hila nyingi zinatokana na wivu..na mambo yote mabaya yanatokana na wivu.
Hivyo ni muhimu kujifunza kutokuwa na wivu ili tusiwe kifaa cha kutumiwa na shetani kuwadhuru wengine.
Roho ya wivu ndiyo iliyowafanya Mafarisayo na Masadukayo wamchukie Bwana, pale walipoona Bwana anatenda miujiza ambayo wao hawawezi kuitenda, pale walipoona Bwana anawarejeza watu wengi kwa Mungu kuliko wao…Na mioyoni Roho Mtakatifu alikuwa akiwashuhudia kabisa kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu…na walikuwa wanajua kabisa katumwa na Mungu lakini kwasababu ya wivu..wakawa wanajitoa ufahamu na kumkufuru.. Soma..
Mathayo 22:15 “Ndipo Mafarisayo wakaenda zao, wakafanya shauri, jinsi ya kumtega kwa maneno.
16 Wakatuma kwake wanafunzi wao pamoja na Maherodi, wakasema, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, na njia ya Mungu waifundisha katika kweli, wala hujali cheo cha mtu awaye yote, kwa maana hutazami sura za watu”.
Unaona, walijua kabisa Kristo alikuwa mtu wa kweli aliyetumwa na Mungu..
Soma tena.. Yohana 3:1-3 utalithibitisha hilo…
Yohana 3:1 “Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi.
2 Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye”.
Lakini pamoja na hayo yote nguvu ya wivu ilikuwa kubwa ndani yao ikazidi nguvu ya kumpenda..na hatimaye wakafanya hila mpaka za kutaka kwenda kumsulubisha mfalme wao..Walimsulubisha moyoni wakijua kabisa huyu ni mwana wa Mungu aliyetumwa kutoka mbinguni…Hilo halikuwa na shaka mioyoni mwao. Walijua kabisa ndiye mfalme aliyetabiriwa kuja ulimwenguni.
Na hata walipompeleka kwa Pilato..Haraka sana Pilato ambaye hakuwa Myahudi akajua kuwa hakukuwa na kosa lolote alilolifanya Bwana Yesu ambalo linastahili yeye kusulubiwa lakini ni kwasababu tu ya wivu…Hawa wayahudi wamesikia tu wivu alivyojiita yeye ni mwana wa Mungu..Hilo tu! Wala hakuna lingine…walimwonea wivu kwa miujiza aliyokuwa anaitenda ambayo wao walishindwa kuitenda na wala hakuna lingine, na jinsi anavyowajalia watu wengi kupata wokovu…Kwahiyo hata Pilato aliliona hilo kama biblia inavyosema katika..
Marko 15:9 “Pilato akawajibu, akisema, Je! Mnataka niwafungulie mfalme wa Wayahudi?
10 Kwa maana alitambua ya kuwa wakuu wa makuhani wamemtoa kwa HUSUDA.
11 Lakini wakuu wa makuhani wakawataharakisha makutano, kwamba afadhali awafungulie Baraba”.
Sasa neno ‘HUSUDA’ maana yake ni ‘WIVU’ soma tena (Mathayo 27:17-18)..Kwahiyo unaona Pilato alishawajua kabisa hawa watu ni wivu ndio uliowafanya watake kumwua Yesu na wala hakuna lingine..alijua kabisa mioyoni mwako wanamwamini Yesu na kwamba “Yesu katoka kwa Mungu, na ni mfalme wao” lakini kwa kuwa wamemwonea wivu ndio maana wanataka afe…Ndio maana Pilato alikuwa akiwauliza kwa kurudia rudia.. “kama kweli wamemaanisha kumuua mfalme wao”
Yohana 19:13 “Basi Pilato, aliposikia maneno hayo, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo Sakafu ya Mawe, au kwa Kiebrania, Gabatha.
14 Nayo ilikuwa Maandalio ya pasaka, yapata saa sita. Akawaambia Wayahudi, TAZAMA, MFALME WENU!
15 Basi wale wakapiga kelele, Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe! Pilato akawaambia, JE! NIMSULIBISHE MFALME WENU! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalme ila Kaisari”.
Wivu ni mbaya sana unakufanya umkane Mtu, hata kama unamwamini na kumpenda…
Na ndio maana mwishoni kabisa baada ya kusulubishwa Bwana Yesu, Pilato aliandika anwani juu ya msalaba wa Bwana Yesu kwa lazima.. “Yesu Mnazareti, Mfalme wa Wayahudi”
Yohana 19:19 “Naye Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI.
20 Basi anwani hiyo waliisoma wengi katika Wayahudi; maana mahali pale aliposulibiwa Yesu palikuwa karibu na mji; nayo iliandikwa kwa Kiebrania, na Kirumi, na Kiyunani.
21 Basi wakuu wa makuhani na Wayahudi wakamwambia Pilato, Usiandike, Mfalme wa Wayahudi; bali ya kwamba yule alisema, Mimi ni mfalme wa Wayahudi.
22 PILATO AKAJIBU, NILIYOANDIKA NIMEYAANDIKA”.
Unaona hapo?..Pilato aling’ang’ania kuandika anwani ile kwa lazima?…kwanini?..ni kwasababu anaujua unafiki wa mafarisayo..mioyoni mwao walimwamini lakini mdomoni walimkana na kumtukana na kumsulubisha na hiyo yote ni kwasababu ya wivu tu!. Na ndio maana Pilato akaandika anwani ile.
Yohana 12:42 “Walakini hata katika wakuu walikuwamo wengi waliomwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumkiri, wasije wakatengwa na sinagogi”.
Sasa sio wote kabisa waliomwamini, Bwana Yesu…wapo ambao ni kweli hawakumwamini kabisa pamoja na ishara zote zile alizozifanya…lakini asilimia kubwa ya mafarisayo na wakuu wa makuhani walimwamini Bwana mioyoni mwao lakini WIVU ukawasababisha kumsulubisha Bwana, na sio Bwana tu bali hata mitume wake walisumbuliwa na mafarisayo hao hao..na yote hiyo ni kutokana na wivu tu.
Matendo 5:16 “Nayo makutano ya watu wa miji iliyoko kandokando ya Yerusalemu wakakutanika, wakileta wagonjwa, nao walioudhiwa na pepo wachafu; nao wote wakaponywa.
17 Akaondoka Kuhani Mkuu na wote waliokuwa pamoja naye, (hao ndio walio wa madhehebu ya Masadukayo), WAMEJAA WIVU,
18 wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza;”
Hiyo ndiyo silaha shetani aliyotumia kumpeleka Bwana msalabani…Na silaha hiyo hiyo anaitumia leo kuangamiza watu..Je! na wewe una wivu?…kama unaingiwa na wivu ndugu yako akipata jambo Fulani ambalo wewe huna ujue unakaribia kufanyika chombo cha shetani kumwangamiza, kama unasikia wivu jambo Fulani zuri ndugu yako, au jamii yako, au rafiki yako analolifanya, kama unasikia wivu, mwingine anapooa, au anapoolewa au anapofanya hiki au kile..au anapotoka hatua moja mpaka nyingine…kuna hatari kubwa ya kufanyika chombo cha shetani. Na wivu ukizidi sana unakuwa huna tena huruma..unakuwa unatamani kifo kwa huyo ndugu yako kama vile Kaini, alivyomwonea wivu ndugu yake mpaka akaenda kumwua.
Hivyo ni kwa namna gani utashinda Wivu?
Kwanza ni kwa kumpa Yesu Kristo maisha yako?..Unapookoka Bwana anakufanya kuwa kiumbe kipya, na ya kale yote yanakuwa yamepita, unakuwa umefanyika kiumbe kipya…Ule utu wa zamani, Bwana anauzika, Nia yako Bwana anaigueza kutoka kutazama vitu vya ulimwengu huu vinavyopita na kutazama mambo ya ulimwengu ujao ya milele yasiyoharibika..Hivyo kunakuwa hakuna shughuli yoyote ya kidunia ambayo itaweza kukupa wivu ndani ya moyo wako kwasababu nia yako imeshageuzwa na kuutazama ulimwengu ujao ambao utajiri wake na hazina yako hauna mwisho.
Pili baada ya kuokoka unapaswa uanze kujiwekea hazina yako mbinguni, Biblia inasema hazina yako ilipo ndipo na moyo wako utakapokuwepo…Hazina yako ikiwa kubwa katika mambo ya ulimwengu huu na moyo wako lazima utakuwa huko huko, hilo haliepukiki, kama ndoto zako kubwa kuliko zote ni wewe kupata mali nyingi sana ili hatimaye watu wote waje kukuona na kukuangukia na kukuheshimu, hapo roho ya wivu hauwezi kuiepuka, kwasababu atakapotokea mtu kakuzidi kidogo tu au unamwona ananyanyuka utamwonea wivu. Ndicho kilichowakuta mafarisayo na masadukayo, walikuwa na ndoto kubwa za wao waonekane wapo juu ya watu wote, na alipotokea mwingine mwenye nguvu kuliko wao wakaishia kumwonea wivu.
Lakini kama hazina yako ipo mbinguni, kwamba ndoto yako kubwa ni siku ile uirithi mbingu kwa daraja la kwanza, na kuwa na thawabu kubwa kule, kamwe hutakaa umwonee mtu wivu kwa vitu vya kidunia vinavyopita…Hazina yako inapoongezeka mbinguni, mawazo yako, akili yako, na moyo wako wote unakuwa kule, unakuwa kila siku unatafakari utukufu na thawabu zinazokungoja kule, na hivyo habari ya kuanza kuona wivu kwa vitu vya kidunia unakuwa huna..
Na hazina ya mbinguni unaitengeneza kwa kumpendeza Mungu na kwa kuifanya kazi yake…Na kazi yake sio kuhubiri tu, bali hata ile ya kuosha choo cha nyumba ya Mungu ni kazi yake yenye thawabu kubwa kule, hata ile ya kuwaombea watakatifu ni kazi yake yenye thawabu kubwa sana…n.k Unapofanya hayo bila ulegevu Roho Mtakatifu kila siku atakuwa anakushuhudia ndani yako kwamba thawabu yako ni kubwa mbinguni, na inazidi kuongezeka siku baada ya siku, hivyo kamwe huwezi kumwonea wivu mtu aliyeoa/ kuolewa na wewe hujaolewa, au jirani yako ambaye ni bilionea..
Ufunuo 2:17 “Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea………
26 Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,
27 naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu”……
Ufunuo 3:5 “Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake”………..
12 Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya…….
21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi”.N.k
Bwana akubariki sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Jini Mahaba yupo kibiblia?, Mtu mwenye jini mahaba anakuwaje?
Moja ya elimu inayowachanganya wengi na inayopotoshwa ni Elimu juu ya mapepo..
Mapepo kwa lugha nyingine wanaiwa majini…Ni kitu kimoja kinachojulikana kwa majina mawili tofauti, ni kama MWANADAMU na MTU. Hayo ni majina mawili tofauti lakini yanaelezea kitu kimoja.
Sasa mapepo ni roho za malaika walioasi mbinguni, ambao walitupwa chini pamoja na kiongozi wao mkuu shetani. Baada ya kutupwa chini ndio yakaitwa mapepo.
Mapepo hayo yanaweza kumwingia mtu na kumfanya awe na tabia yoyote ile wanayotaka wao. Mapepo haya yanaweza kumwingia mtu na kumfanya awe mwizi, mengine yanaweza kumfanya mtu awe mlevi, mengine yanaweza kumfanya mtu awe mzinifu au mwenye tabia ya zinaa.
Sasa mapepo ambayo yanawafanya watu wabadilike tabia na kuwa wazinifu au kuhisi wanafanya mapenzi na watu wakati wa kulala ndio hayo WATU wanayoyaita MAJINI MAHABA. Lakini kiuhalisia mapepo hayo hayana jinsia yoyote kwasababu ni roho. Na haya yanapomwingia mtu yoyote ambaye hajaokoka.(yaani ambaye hajampokea Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yake) yanamfanya anakuwa mtumwa wa dhambi hiyo ya zinaa katika ndoto au katika maisha yake ya kawaida..Kwa mtu wa kawaida huwa hayamtokei kwa wazi lakini kwa wale ambao wamekufa kabisa kiroho na wamejiuza kwa shetani huwa yanaweza kujidhihirisha kwa macho kabisa..
Lakini kumbuka shetani siku zote ni mwongo pamoja na mapepo yake yote, biblia inasema shetani anao uwezo wa kujigeuza na kuwa hata malaika wa Nuru (Kasome 2Wakoritho 11:14), hivyo sio ajabu kuweza kujigeuza na kuwa hata mwanamke mzuri au mwanamume mzuri wa kuvutia, lakini ndani yake ni pepo mbaya na mchafu. Watu wengi wanadanganyia na kufikiri kuna mapepo ya kike..Ndugu usidanganyike hakuna kitu kama hicho…hayo ni maroho tu hayana jinsi, shetani ni baba wa uongo siku zote.
Kwa asili roho hizi za mapepo huwa hazimtokei mtu kwa wazi kama tulivyotangulia kujifunza hapo juu, isipokuwa kwa mtu ambaye tayari amejiuza kwa shetani moja kwa moja, hususani kama mtu ni mshirikina, au mganga au mchawi kabisa, huyu anaweza kuziona kwa macho..Lakini kwa wengine ambao wapo nusunusu, vuguvugu..roho hizi zinawaendesha katika ndoto tu na katika tabia zao. Katika ndoto wanakuwa wanaota wanafanya zinaa na katika tabia wanakuwa wanatabia zilizokithiri za uasherati mpaka wengine kuwafanya kuwa mashoga au wasagaji, au walawiti au wafiraji.
Na zifuatazo ni njia mapepo haya yanayozitumia kuingia ndani ya watu.
Kujitazama kwenye kioo hakuna uhusiano wowote na kuingiwa na roho hizo..Isipokuwa mtu mwenye tabia ya kujipamba, na kujichubua, kusuka suka, kuchonga nyusi anakuwa na tabia ya kujiangalia kwenye kioo mara kwa mara..hivyo hiyo tabia ya kujipamba na kuchonga nyusi ndio mlango wa mapepo hayo kuingia lakini sio kujitazama kwenye kioo.
Biblia inasema katika..
Ufunuo 21:27 “Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo”.
Kilicho kinyonge kinachozungumziwa hapo ndio hicho chenye roho ya mapepo ndani yake..Kwasababu mtu mwenye roho ya mapepo atakuwa na tabia tu fulani chafu ambazo watu wenye tabia hizo biblia inasema hawataurithi uzima wa milele. Mtu mwenye pepo la zinaa/jini mahaba ni lazima atakuwa mzinifu na mbinguni hawataingia wazinifu..Mtu mwenye pepo la ulevi ni lazima atakuwa tu mlevi na mbinguni hawataingia walevi.
Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili..”
Mbinguni wataingia tu watu wenye Roho Mtakatifu..ambao ni watakatifu.
Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; “
Kwanza ni kwa kumpa Yesu Kristo maisha yako, unatubu kwa kudhamiria kabisa kuacha dhambi na kisha unajiepusha na milango kujitenga na milango hiyo sita hapo juu tuliyoiona ambayo ndio mlango ya kuingiwa na roho hizo chafu. Na roho hizo zitakuacha kabisa na utakuwa huru.
Bwana akubariki
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Je ni kweli kuna samaki nguva?..Je kwenye biblia nguva katajwa?
Jibu: Ukweli ni kwamba hakuna mahali popote katika biblia palipotajwa uwepo wa samaki aina ya nguva. Maana yake ni kwamba hakuna kiumbe cha namna hiyo kilichoumbwa na Mwenyezi Mungu.
Lakini utauliza je! hicho wanachokiona watu ni nini? ambacho kimaumbile kinaonekana nusu mtu nusu samaki?
Jibu ni kwamba vinavyoonekana na watu vyenye umbo kama hilo ni roho za mapepo. Kumbuka biblia inasema shetani anao uwezo wa kujigeuza na kuwa hata Malaika wa Nuru (Kasome 2Wakorintho 11:14), sasa si zaidi kujigeuza na kuwa kiumbe kiumbe kingine chochote chenye umbo la ajabu?. Anao huo uwezo, anaweza kujiguza na kuwa kama nusu mtu nusu mbuzi, anaweza kujigeuza na kuwa nusu mtu nusu nyoka, vivyo hivyo anao uwezo wa kujigeuza na kuwa nusu mtu nusu samaki (ambao ndio hao wanaojulikana kama nguva).
Sasa shetani na mapepo yake wote wanao huo uwezo wa kujigueza na kuwa hivyo viumbe vya ajabu..Na lengo lao ni lile lile moja..Kuwapoteza wanadamu na kuwaweka mbali na kweli ya Mungu, na hatimaye wafe katika dhambi zao na kuingia Jehanamu ya moto, wala hana lingine. Hivyo shetani kila siku anabuni njia mpya za kuwafanya watu wawe wabaya zaidi na kuzidi kuuamini uongo wake.
Sasa haya mapepo ambayo yanajigeuza maumbile..huwa hayawatokei wala hayawaingii watu waliookoka (Yaani waliomwamini Yesu Kristo na kuoshwa dhambi zao kwa damu yake). Huwa yanawatokea na kuwaingia watu ambao katika roho wapo dhaifu sana, na hao ni wale wote ambao wapo nje ya Neema ya Yesu Kristo. Huwa yanawajia katika ndoto, kuwahimiza kufanya jambo fulani lililo kinyume na neno la Mungu au kuwapa hisia ambayo ni kinyume na Neno la Mungu..
Na hisi kubwa na ya kwanza yanayopeleka kwa mtu ni hisia ya ZINAA na UASHERATI. Kwasababu hiyo ndio dhambi ya kwanza ambayo shetani anatumia kumwangusha nayo mwanadamu na ndio Dhambi ya asili.
Hisia ya pili ni.. kutenda mabaya, aidha kuabudu sanamu, au miungu, kuwa mshirikina, au wakati mwingine yanamletea mtu hisia za kuwa na chuki na jamii ya watu fulani, au mtu fulani na kumpeleka hata kutamani kuua, au kuiba au kudhuru. Hiyo ndio kazi ya mapepo hayo yanapomwingia mtu ndani yake…na haya yana majina mengi (wengine wanayaita majini, wengine vibwengo n.k)..lakini ndio hayo hayo mapepo…
Mapepo haya yakiwemo hayo yanayojigeza na kuwa huo mfano wa nguvu, huwa hayamtokea mtu kwa macho, yanakuwa ni roho ambazo zinamwingia mtu au zinatembea na mtu, na mtu anaweza kuziona tu katika ndoto..lakini si katika macho ya asili..Lakini pia kama mtu huyo hali yake ya roho ipo chini sana yanaweza kumtokea kabisa na akayaona dhahiri, wengi wa wanaoyaona hayo ni wale ambao ni wachawi au waganga, au washirikina…ambao wameshajiuza kwa shetani kikabisa.
Kwahiyo nguva si kiumbe kilichoumbwa ambacho kinaishi baharini, bali ni roho za mapepo, kama umewahi kuota upo na nguva au umewahi kumwona..Basi tambua kuwa hali yako katika roho ipo chini sana na ni hatari.
Hivyo suluhisho ni kumpa Yesu maisha yako, unapoamua kugeuka na kutubu kwa kumaanisha kuacha dhambi na maisha ya machafu uliyokuwa unaishi huko nyuma, na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi, roho hizo zitakuacha hata pasipo kwenda kuwekewa mikono na mtu yoyote na utakuwa huru mbali na utumwa wa roho za mapepo.
Bwana akubariki sana.
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Yakobo 5:7 “Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.
8 Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia”.
Kwanini mtume huyu alifananisha kumngojea Bwana na uvumilivu na wa mkulima anayengojea mazao ya nchi, mpaka atakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.?
Hii Mvua ya kwanza na mvua ya mwisho ni ipi?
Mvua ya kwanza kwa jina lingine ni mvua ya masika, na mvua ya mwisho ni mvua ya vuli..Israeli tangu zamani hadi sasa ni nchi ya jangwa, sio kama huku kwetu kwenye ukanda wa kitropiki, ardhi ina unyevunyevu wakati wowote, kiasi kwamba hata ukitaka kuchimba kisima popote unakutana maji chini..Jambo hilo huwezi kulikuta katika nchi za jangwa kama vile Israeli..
Hivyo wakulima walikuwa wanategemea sana misimu ya mvua ili kulima na kupanda, wakati mwingine wowote ilikuwa haiwezakani kutokana na kwamba ardhi kuwa kame na ngumu.
Hivyo wakulima ilikuwa inawapasa wangojee wakati wa mvua tu, ndipo wafanye kazi za ukulima, Kwasababu hata mito haikuwepo, na hata kama ipo basi haijitoshelezi yote kwa kilimo cha umwagiliaji..Na hiyo ilikuwa inawafanya wasubirie tu wakati wa mvua, na utakapofika huwa basi wanafanya kazi kama vichaa kwa uvumilivu wote na kwa subira yote kwasababu wanajua upo wakati ambao hawataweza kufanya kazi tena.. Sasa kulingana na Jeografia ya Israeli, mvua ya masika kwao ilikuwa inaanza mwezi wa 10-11, na vuli mwezi 3-4, tofauti na huku kwetu ambapo ni kinyume chake.
Sasa masika ilikuwa ikishaanza tu wakulima wote wanatoka wanaingia mashambani na kuanza kuandaa mashamba na kupanda mbegu zao, na kuzipalilia…Mpaka itakapoisha, Lakini baadaye tena mvua nyingine ndogo ndogo zilikuwa zinaendelea si kali kama zile za Masika ndio hizo za Vuli, ili kustawisha tu mazao, na kuifanya ardhi isipoteze unyevu wake, mpaka misimu yote ya mvua itakapoisha moja kwa moja
Sasa ndio hapa Mtume Yakobo anafanisha kumngojea kwetu Bwana kama mkulima aliye katika msimu wa kilimo chake anavyovumilia mpaka mazao yake yatakapopata mvua zote mbili yaani ya kwanza na ya mwisho… Na akishamaliza basi huvuna na kuyaweka ghalani, jasho lake, na taabu yake sasa inakuwa imekwisha..
HIVYO,MVUA YA KWANZA, NA YA MWISHO ROHONI INAFUNUA NINI?
Vivyo hivyo na sisi tunaomgonjea Bwana, Tulishanyeshewa mvua ya kwanza, siku ile ya Pentekoste takribani miaka 2000 iliyopita, Kazi ikaanza..sasa kuanzia huo wakati tumekuwa tukilima, na kupanda, na kupalilia shamba la Bwana..Lakini pia iliahidiwa mvua nyingine itakayokuja huko mbeleni ambayo itakayokamilisha taabu yetu ya ulimaji..
Ndugu kama hujui ni kuwa tayari tumeshaingia katika kipindi cha msimu wa mwisho wa mvua ambayo ndio ile mvua ya mwisho ya vuli (rohoni), Na mvua hii ilianza mwaka wa 1906, Huu ni wakati ambapo kwa mara nyingine tena Mungu aliijilia dunia kwa vipawa na karama za roho, na kazi zile zile zilikuwa zinatendeka wakati ule wa Pentekoste ya mitume miaka 2000 iliyopita, mambo ambayo hapo katikati yalikuwa hayafanyiki, wala hayaonekani.. Hivyo kuanzia wakati huo ndio, Karama zile zote za rohoni zilianza kurejeshwa katika kanisa tena upya, vilevile Mungu akanyanyua watumishi wake wengi waaminifu kulithibitisha hilo kuwa wakati huo umeanza watu hao ikiwemo (William Seymor, baadaye William marrion Branham, Billy Granham, Oral Roberts, TL Osborn na wengineo wengi)
Tangu huu wakati injili ilianza kuhubiriwa kwa nguvu na ujumbe ulikuwa ni huu…WAKATI WA MAVUNO UMEKARIBIA!! BWANA ANAKARIBIA KULICHUKUA KANISA LAKE..
Wote hawa walikuwa na ujumbe huo, wote walijua tupo katika wakati ule wa MVUA YA MWISHO, wa mvua ya vuli..Na mpaka sasa ndipo mvua hiyo inakaribia kufika ukingoni kabisa… kwenda kugota..Na ikishagota, basi hakutakuwa ni mvua nyingine tena milele..
Ndugu hii neema unayoiona, unapoona unahubiriwa injili kirahisi hivi, Neno la Mungu limezagaa kila mahali, lakini unalipuuzia usidhani ilikuwa hivyo kipindi cha karne ya 19 kushuka huko chini..Hii miujiza unayoina na karama za rohoni unazoziona usidhani zilikuwepo muda wowote wa kanisa… Wewe Mungu amekupa neema ya kuishi katika msimu huu wa mvua ya Vuli rohoni, ambayo ipo karibuni kuisha..Lakini unaichezea hii nafasi..Upo wakati utaitamani lakini mlango wa neema utakuwa umeshafungwa..
Kipindi si kirefu, kanisa litanyakuliwa, wala hakuna mtu atakayesema mimi sikuambiwa wala sikujua, wakati huo Bwana atakusanya mavuno yake na kuyaweka ghalani na magugu kuyatupa motoni..Wote tunafahamu, hali ilivyo sasa, magonjwa ya kutisha yanavyozidi kuzuka, tetesi za vita, matetemeko,manabii wa uongo, watu kupenda fedha, watu kupenda anasa kuliko kumpenda Mungu, ushoga kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, n.k. yote hayo yaliandikwa na tukaambiwa hizo ndio zitakuwa dalili kuu zitakazotutambulisha kuwa Kristo yupo mlangoni kurudi..
Lakini sisi tuliompokea tumeambiwa, tuyaonapo hayo..Basi ndio tunyanyue vichwa vyetu juu, kwasababu ukombozi wetu umekaribia..
Mvua hii ya neema ipo ukingoni, mkaribishe Bwana moyoni mwako kabla haijakoma kabisa moyoni mwako..Sisi sio wa kuambiwa tena tuvumilie kwasababu sisi tupo tayari wakati wa mavuno, waliokuwa wanapaswa wavulie ni wale wa makanisa mengine lakini sio sisi wa kanisa la mwisho la LAODIKIA.
Shalom.
Tafadhali “Share” Ujumbe huu na kwa wengine. Pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email, au Whatsapp au inbox yako ya faceboook, basi utujuze inbox nasi tutafanya hivyo. Vilevile usiache kutembelea website yetu hii (www wingulamashahidi org) kwa mafunzo zaidi.
Bwana akubariki sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?
Karibu tujikumbushe machache juu ya ujio wa Bwana Yesu, jinsi utakavyokuwa.
Bwana Yesu alikuja mara ya kwanza miaka ile 2,000 iliyopita…Alizaliwa na Bikira Mariamu, akasulubiwa na wayahudi, akazikwa, akafufuka baada ya siku tatu, na akapaa juu mbinguni kwa Baba…Mpaka muda huu tunapozungumza yupo mbingu za mbingu, amepokea Enzi na mamlaka yote ya mbinguni na duniani(1Timotheo 6:16). Lakini huko amekwenda kutuandalia makao (yaani nafasi zetu).
Baada ya muda mfupi atarudi tena kutuchukua tuende naye kwake, ili alipo nasi pia tuwepo..(Yohana 14:3).
Sasa siku ya kuja kutuchukua itakapofika, siku hiyo ndiyo inayoitwa SIKU YA UNYAKUO, Hatashuka duniani, bali atabaki pale mawinguni na atatuita sisi juu tupae kumfuata kule aliko..Siku hiyo tutaisikia sauti ya parapanda na muda huo huo uweza wa ajabu utashuka juu yetu ambapo kufumba na kufumbua tutajikuta miili hii yetu ya udhaifu imebadilika na kuwa kama wa kwake Bwana wetu Yesu. Na tutapaa juu, tutaicha hii ardhi kwa mara ya kwanza na kwenda juu sana…
Watu wa ulimwengu waliomkataa hawatamwona atakapotuita juu…watakaomwona ni wale tu ambao watanyakuliwa…kama vile alivyofufuka mara ya kwanza ni mitume wake tu na wafuasi wake wachache ndio waliomwona na wengine wote Mafarisayo na masadukayo hawakumwona, wala Pilato aliyemsulubisha hakujua chochote..ndivyo siku hiyo itakavyokuwa, wale wakristo ambao wameishikilia Imani mpaka siku hiyo itakapofika ndio watakaomwona Bwana mawinguni, na ndio watakaoisikia parapanda siku hiyo..
Sasa wafu ambao walitangulia kufa katika Kristo hawatasahaulika nao pia, kwasababu wao ndio watakaokuwa wa kwanza kuona tukio zima jinsi litakavyoendelea kwasababu watufufuliwa kwanza, kisha baadaye wataungana na sisi tulio hai na wote kwa pamoja tutavikwa miili ya utukufu. (kasome 1Wathesalonike 4:15)..
Na hali kadhalika wafu hao ambao watafufuka sio watu wote watawaona..hapana, watu wengine wakidunia watahisi tu labda kumetokea tetemeko la ardhi kama ilivyotokea siku ile Bwana aliyofufuka, lakini hawatamwona mtu yoyote….Watakaowaona wafu waliofufuliwa ni wale tu ambao wataungana nao kwenda kumlaki Bwana mawinguni.
Sasa Mbinguni, kutakuwa na karamu inaendelea kwa muda wa miaka saba, kutakuwa na raha isiyo na kifani..ambapo wakati huo duniani itakuwa inapitia kipindi cha dhiki kuu, na udhihirisho wa Mpinga-Kristo kwa watu waliosalia bila kwenda kwenye unyakuo, wachache watagundua Kristo amesharudi na wameachwa, wengi hawataamini na kuhisi ni uzushi tu umezuka..na hivyo watadanganyika kwa uongo wa mpinga-kristo na kuipokea chapa, na hatimaye kufa katika siku ya hasira ya Bwana ambapo Mungu mwenyewe ataiadhibu dunia kwa maovu yake kwa kupitia mapigo yale ya vitasa saba (Ufunuo 16).
Baada ya mambo hayo kuisha, Bwana kujilipizia kisasi kwa watenda maovu… Kristo pamoja na wale watakatifu wake ambao walikuwa wapo mbinguni katika karamu, watakuja duniani kwaajili ya ile vita ya Harmagedoni na kwa ajili ya kuanza utawala wa miaka 1,000..Wakati huo atakapokuja..wale watu wachache sana ambao wamebaki duniani ndio watakaomwona akija mawinguni kwa nguvu na utukufu mwingi.… atashuka na kulimalizia kundi dogo lililosalia katika vita vile vya Harmagedoni.. Hapo ndipo lile neno litakapotimia kwamba “kila jicho litamwona”…wataomboleza na kulia na kushikwa na hofu kuu, watakapomwona Kristo sio yule waliokuwa wanamwona kwenye picha au waliokuwa wanamsoma kwenye kitabu akija kwa upole na unyonge, wakati huu watamwona akija kwa utukufu mwingi kama umeme na ghadhabu nyingi.
Mathayo 24:30 “ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi”.
Baada ya hapo utawala wa miaka 1,000 utaanza…na baada ya utawala huo itakuja mbingu mpya na nchi mpya, ambapo huko kutakuwa hakuna kufa, wala kuzeeka, wala kujaribiwa, wala kuteswa…Mambo ya kwanza yamekwisha kupita, atayafanya yote kuwa mapya..watakatifu wataishi na Bwana milele, katika utukufu usio na mwisho..Muda utasimama kutakuwa hakuna kuhesabu miaka, kwasababu maisha yatakuwa ni ya umilele.
Ufunuo 21:4 “Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.”
Bwana atausaidie tuwe miongoni mwa wale watakaokuwa wamealikwa katika karamu ya mwanakondoo mbinguni..
Ufunuo 19:9 “Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo…”.
Wafu wafao sasa katika dhambi, hawatafufuliwa siku ya unyakuo itakapofika..watabaki kuzimu sehemu ya mateso..na siku moja watakuja kufufuliwa na kuhukumiwa kila mmoja kulingana na matendo yake(Ufunuo 20:13)..na baada ya kuhukumiwa watahamishwa kutoka kuzimu walipokuwepo na watakwenda kutupwa katika ziwa la moto lenye mateso makali Zaidi kuliko kule kuzimu walipokuwepo. Na huo ndio utakuwa mwisho wao.
Sio hilo tu, kwa wale waliokutwa wakiwa hai na wameachwa kwenye unyakuo na kuipokea chapa ya mpinga-kristo, hatapona hata mmoja wote baada ya kipindi kifupi watapitia mapigo makali ambayo yataletwa na Mungu mwenyewe kupitia vile vitasa 7..wakati wenzao waliokufa katika dhambi wakiwa jehanamu wanateseka wao watakuwa wanapitia mateso ya ghadhabu ya Mungu huku duniani, maji yote ya duniani yatageuzwa kuwa damu watu watasikia kiu mpaka kufikia hatua ya kuyanywa maji ya damu na kufa,(ili Mungu kuwalipizia kisasi kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu wake hivyo Mungu amewarushia hiyo damu wainywe), siku hizo jua litashushwa na kuwa kama moto juu ya wanadamu, mvua zitasimama kunyesha, na badala yake vitu vya ajabu vitaanza kuanguka kutoka mbinguni, na Bwana atawafanya watu wawe hawaelewani wao kwa wao hivyo kutakuwa na mapambano na vita vikuu,
Na katikati ya mateso hayo ya jua hilo kali, na kukosekana kwa maji na chakula duniani, Bwana ataleta magonjwa ya ajabu ya majipu ya ajabu juu ya wanadamu wote waliopokea chapa ya mnyama..kwahiyo mtu atakayeukosa unyakuo atakuwa hatna tofauti sana na mtu aliyekufa na kwenda kuzimu kutokana na mateso atakayoyapata akiwa hapa duniani.
Ufunuo 16:1 “Nikasikia sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Enendeni, mkavimimine vile vitasa saba vya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi.
2 Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na jipu baya, bovu, JUU YA WALE WATU WENYE CHAPA YA HUYO MNYAMA, NA WALE WENYE KUISUJUDIA SANAMU YAKE.
3 Na huyo wa pili akakimimina kitasa chake juu ya bahari, ikawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa.
Na baada ya kupitia mapigo hayo yote pamoja na kuuawa na mwanakondoo watakufa wote na kuungana na wenzao walioko jehanamu..wote kwa pamoja wakisubiria hukumu ya kutupwa katika ziwa la moto.
Hivyo unyakuo sio wa kukosa hata kidogo, Ni heri tukose hayo mengine yote lakini si unyakuo…Bwana atusaidie atukute tukiwa tunakesha katika roho kama alivyosema…
Marko 13:32 “Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba.
33 Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo.
34 Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe.
35 Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi;
36 asije akawasili ghafula akawakuta mmelala.
37 Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni”
Ulevi ni usingizi, uasherati ni usingizi, wizi ni usingizi, usengenyaji ni usingizi, kiburi, hasira, matukano,rushwa, utapeli,uongo, uuaji, moyo unaowaza mabaya, na mambo yanayofanana na hayo.
Bwana atubariki.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Kwanini Mungu aliikubali sadaka ya Yeftha ya kumtoa binti yake kafara?
SWALI: Mimi Nina MUNGU Wangu ambae Ni ALLAH subhanallah…sasa kwanini nimkabidhi maisha Yesu wakati naye alizaliwa Kama mimi?
JIBU: Mama yako alizaliwa kama wewe…lakini ilifika wakati Mwenyezi Mungu aliyakabidhisha maisha yako kwake. Ili uwe salama, ulindwe, uhifadhiwe, ulishwe na upendwe..na pamoja na hayo ufundishwe kanuni za maisha ambazo peke yako bila wazazi au mlezi usingeweza kujifunza.
Vivyo hivyo ulipaswa ukae chini ya sheria za wazazi wako ndipo uweze kufanikiwa, endapo ungekuika sheria hizo basi maishani usingefanikiwa….Na kama sio Mwenyezi Mungu kuyakabidhisha maisha yako kwa wazazi wako ambao wamezaliwa kama wewe, maisha yako yangukuwa magumu sana hapa duniani au hata pengine usingezaliwa kabisa au kama ungezaliwa ungekufa.
Vivyo hivyo Yesu alizaliwa kama sisi tulivyozaliwa, (Ingawa hakuzaliwa na dhambi ya asili kama sisi, kwasababu mimba yake ilitungishwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu), na katika nyakati hizi za uovu na mateso na dhiki za ulimwengu.
Mungu kwa huruma zake na kwa jinsi anavyotupenda akamtuma huyu Yesu Kristo, ili awe kama mzazi kwetu kwasababu sisi wenyewe hatutaweza kwa nguvu zetu na kwa akili zetu kujiongoza..Ndio maana hatuna budi wote tuyakabidhi maisha yetu kwake ili tuwe salama sasa na ahera.
Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
17 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu”
Yesu anapoingia maishani mwetu, anatupa furaha, faraja, amani, upendo na tunapata ulinzi dhidi ya Adui shetani na mapepo yake yote, siku zote za maisha yetu na tumaini la uzima wa milele.
Bwana Yesu akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
https://wingulamashahidi.org/2018/07/04/5-swali-je-kuna-dhambi-kubwa-na-ndogo-na-kama-hakuna-je-mtu-aliyeua-na-aliyetukana-je-watapata-adhabu-sawa/
Mwisho wa dunia utakuwaje?
Mwisho wa dunia maana yake ni hatua ambayo ustaarabu wa dunia utaifkia mwisho…Na mwisho wa dunia utahitimishwa na tukio moja kuu la vita vya HARMAGEDONI. Vita hivyo vitamaliza ustaarabu wote wa wanadamu…zitakuwepo vita ndogo ndogo zitakazotangulia, lakini vita hii kubwa ya mwisho ujulikanayo kama Harmagedon ndiyo itakayomaliza ustaarabu wote wa wanadamu.
Vita hii Biblia inaitaja kuwa ni vita kati ya Mungu mwenyezi na Wafalme wa Dunia..
Ufunuo 16:14 “Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.
15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)
16 Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni”
Vita hiyo Mwanakondoo yaani Yesu Kristo ataimaliza ndani ya muda mfupi sana kwa ushindi mnono..kwasababu yeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme.
Siku hiyo pia kutakuwa na tetemeko kubwa la nchi ambalo mfano wake haujawahi kutokea na visiwa vitahama na ustaarabu wa dunia ndio utakuwa umefikia mwisho.
Ufunuo 6:12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,
13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.
14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.
15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.
17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?
Biblia inasema wasemapo amani! amani! ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla
1Wathesalonike 5:3 “Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa”
Kwahivyo tunaonywa tusidanganyike na amani hii ya dunia inayodanganya…Amani ya kweli ipo kwa Yesu tu!..nchi inaweza kutangaza kuwa tupo katika kipindi cha amani lakini kumbe ndio tupo mwishoni kabisa mwa nyakati.
Mkabidhi Yesu maisha yako kama hujafanya hivyo, kwasababu yeye ndiye njia ya kufika mbinguni na kuepukana na ghadhabu ya Mungu inayokaribia kumwangwa duniani kote katika siku hizi za mwisho, zinazoonekana zenye amani tele.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Nini maana ya “Siku moja nyuani mwa Bwana ni bora kuliko miaka elfu”?
Ni mistari ipi shetani anapenda kuitumia kuwaangusha watu waliosimama?
Shetani akitaka kumwangamiza mtu aliye mwamini Mungu, anachofanya ni anamchukua na kumpeleka juu sana,.. hamwachi pale alipo, kwasababu anajua mtu aliye chini hata akinguka, ataumia kidogo tu, lakini bado akawa na uwezo wa kusimama na kuendelea mbele tena..Badala yake anachokifanya yeye ni anamchukua na kumpelekea juu sana kwenye kilele cha mnara, mahali ambapo anajua akifanya kosa kidogo tu, na kuteleza basi habari yake ndio inakuwa imeishia pale pale…
Ndivyo alivyofanya kwa Bwana wetu Yesu, alimnyanyua na kumpeleka juu sana kwenye kilele cha hekalu,..Na wakati anampandisha, akaanza kumuhubiria Zaburi ya 91 moyoni mwake (Hii ndio zaburi shetani anayoitumia sana kama silaha yake)…
Inayozungumzia jinsi Mtu yule aliyekubaliwa na Mungu anavyopokea ulinzi wa kipekee kutoka kwa Mungu, haijalishi itakuwa ni wakati wa mchana au wa usiku, haijalisha atakuwa anazungukwa na magonjwa ya hatari kiasi gani ambayo ni tuishio katika dunia yaliyowaangamiza watu makumi elfu, lakini kwake yeye hayatamgusa hata moja..Jinsi mtu huyo anavyofunikwa chini ya mbawa zake ili mabaya yasimpate.. jinsi atakavyowekwa mahali pa juu..jinsi atakavyowakanyaga simba na majoka, na jinsi Mungu atakavyomtumia malaika zake wamlindie njia zake zote, asiteleze….
Kwa muda wako pitia zaburi yote ya 91, uone jinsi inavyouzungumzia ulinzi wa kipekee anaoupokea Mtu yule aliyekubalika na Mungu..lakini hapa tutatazama tu vifungu vichache..
Zaburi 91:10 “Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.
11 KWA KUWA ATAKUAGIZIA MALAIKA ZAKE WAKULINDE KATIKA NJIA ZAKO ZOTE.
12 MIKONONI MWAO WATAKUCHUKUA, USIJE UKAJIKWAA MGUU WAKO KATIKA JIWE.
13 Utawakanyaga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.
14 Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.
15 Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;
16 Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu”.
Unaona? sasa Wakati anampandisha juu sana, alikuwa anamthibitishia mistari hiyo kichwani pake..Na kweli shetani alichokuwa anamwambia Bwana ni sahihi kabisa, lakini sio katika mazingira yale..Na alipomfikisha pale juu sasa, ndipo akamwambia huu ni wakati wa wewe kujitupa chini kwasababu Bwana Mungu wako amekupenda na kukuthibitisha, hakuna baya lolote litakaloweza kukupata …. Hivyo usiogope kujitupa chini kwasababu malaika zake wapo kila mahali ili Wakulinde katika njia zako zote. Na Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe
Unaweza kudhani alimaanisha jitupe tu chini kikawaida peke yake, La, sio hivyo tu.. shetani alimaanisha pia dondoka, kutoka katika msimamo wako wa Imani kidogo tu. Ukifanya hivyo Mungu wa mbinguni hatakuacha uangamie kabisa kwani atakutumia malaika zake ili kukurudisha pale ulipokuwa.
Lakini shetani alijua kitakachofuata baada ya pale ni nini..kwasababu alishawahi kuwaangusha watu wengi kwa njia hiyo hiyo akadhani itakuwa hivyo pia na kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Lakini Bwana alimwambia Neno fupi tu..Imeandikwa “Usimjaribu Bwana Mungu wako”.
Kama wewe ni umesimama katika wokovu, nataka nikuambie, katika mahali ambapo unapaswa uwe napo makini basi ni hapa..
Kwenye mahubiri yanayokuaminisha kwamba wewe umekubaliwa na Mungu wakati wote.., na hivyo unaoulinzi wa kipekee kutoka kwake.. kama hujui hiyo ndio mistari shetani anayoipenda kuitumia kuliko mistari mingine yeyote ili kukuangusha wewe uliyesimama..
Ni kweli Mungu ameahidi kufanya hivyo lakini ni kwanini aje kukuhubiria hivyo hivyo kila siku , hakuhubirii habari nyingine za kumcha Mungu? …Jiulize kwanini shetani hakumwambia Bwana, kwa maana imeandikwa mpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako wote, kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote…Badala yake anamwambia kwa kuwa imeandikwa atakuagiza malaika zake wakulinde, usiteleze….Utaona Ni mistari ya kusifiwa tu, na kufarijiwa tu na ya kutoa sifa tu ili ujione wewe ni kitu Fulani mbele za Mungu…hata kama utakuwa katika mahusiano mabaya na Mungu, atakuletea tu hiyo mistari..
Na kibaya Zaidi siku hizi za mwisho mafundisho ya namna hii ndio yanapewa kipaumbele, pale tunapohubiriwa kwamba Mungu ametukubali, Mungu ametuweka juu, hatutakwenda chini, maadui zetu watashindana wala hawatashinda, watakuja kwa njia moja lakini watatoweka kwa njia saba….mahubiri kama haya tunayapenda, ni kweli ni maneno ya Mungu lakini kumbuka hayo ndiyo yanayokupeleka katika kilele cha hekalu ili kukuangamiza kama hutakuwa makini..
Sasa ukiwa katika kilele cha mahubiri kama hayo, hutaki kusikia kingine chochote, hapo ndipo ibilisi anakuletea mambo maovu, kwasababu shetani alishakujaza ujasiri wote kuwa wewe ni mteule wa Mungu, huwezi kupotea?, Inakuwa ni rahisi kwako wewe kwenda kufanya uzinzi, kwasababu shetani ndani anakuhubiria na kukwambia Mungu anaelewa, bado anakupenda, ulishaokoka,atakulinda..Mungu haangalii mavazi yako, haangalii vimini vyako, anaangalia moyo wako, wewe ni mshindi tayari usikubali kushindwa…hata ukiendelea tu kuvaa uchi uchi na kutembea barabarani, haina shida wewe ni mtoto wa Mungu.
Kumbe hujui ndio ndio unaukaribia mwisho wako..Ukiingia huko ndio moja kwa moja, utakuwa umeshateleza na kuanguka kama yeye alivyoanguka alivyoasi zamani, Na mpaka utakapofika chini tayari umeshakuwa mfu rohoni..hufai tena.
Hizi ni siku za mwisho. Utakatifu hauhubiriwi, bali maneno ya kututia faraja tu, ya kutufanya tujione kuwa sisi tumekubaliwa na Mungu, ili kwamba tuendelee kustarehe katika dhambi zetu..
Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, NA HUO UTAKATIFU, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”
Bwana atusaidie.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.
JE! UMEFANYIKA KUWA MWANAFUNZI WA BWANA?
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 6
MJUMBE WA AGANO.
NIFANYE NINI ILI NILITIMIZE KUSUDI LA MUNGU.
Je kuna uislamu katika biblia? na je Muhamadi katika biblia katajwa wapi?
Japokuwa Kristo anafahamika na kutajwa katika dini nyingi tofauti tofauti ulimwenguni ikiwemo uislamu lakini Biblia haijataja dini ya kiislamu ndani yake wala haijamtaja popote mtume wa waislamu ajulikanaye kama Muhamad.
Mstari ufuatao ndio unaotumiwa na wafuasi wa dini ya kiislamu kuamini kuwa Muhamad alitabiriwa katika biblia..
Kumbukumbu 18:15 “Bwana, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye.
16 Kama vile ulivyotaka kwa Bwana, Mungu wako, huko Horebu, siku ya kusanyiko, ukisema, Nisisikie tena sauti ya Bwana, Mungu wangu, wala nisiuone tena moto huu mkubwa, nisije nikafa.
17 Bwana akaniambia, Wametenda vema kusema walivyosema. Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.
19 Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake.
20 Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa.
21 Nawe ukisema moyoni mwako, Tutajuaje neno asilolinena Bwana?
22 Atakaponena nabii kwa jina la Bwana, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena Bwana; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope”
Lakini mstari huo haumzungumzii nabii wao anayeitwa Muhamad bali unamzungumzia Yesu Kristo. Yeye ndiye maneno hayo yanamhusu ambaye Mungu alitia maneno yake kinywani mwake, kwa ishara na uweza mwingi alizungumza vitu na kutabiri na vikaja kutimia na vingine vitatimia siku za mwisho karibia na kurudi kwake..na ndiye aliyepewa Huduma kama Musa ukisoma hapo ya kuwatoa watu katika utumwa wa dhambi.
Soma,
Waebrania 3:1 “Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu,
2 aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama Musa naye alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu.
3 Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahili utukufu zaidi kuliko Musa, kama vile yeye aitengenezaye nyumba alivyo na heshima zaidi ya hiyo nyumba”
Huyu Yesu pia, kama maandiko yanavyosema hapo juu atatoka katikati ya jamii ya wana wa Israeli (ambao ndio ndugu zake Musa waliokuwa wanazungumziwa hapo)..Hivyo Muhamadi hakuwa mwisraeli bali alikuwa mtu wa Taifa lingine, na wala hajakidhi sifa hata moja hapo juu.
Kwa ishara na ajabu nyingi Yesu alithibitishwa na Mungu na kwasasa amekabidhiwa mamlaka yote ya mbinguni na duniani, na hakuna mtu anayeweza kufika kwa Baba isipokuwa kwa njia yake yeye.
Hivyo tunaonywa tusidanganyike kwa maneno ya watu wasio na elimu kamili ya kumjua Mungu, ambao wanatumika na roho zidanganyazo aidha kwa kujua au kwakutokujua…Roho hizi kazi yake ni kuyageuza maandiko ili kuwafanya watu wasimwamini Yesu Kristo hata kidogo, na hilo ndio lengo kuu la shetani..ili hatimaye wafe katika kutokuamini kwao na waende jehanamu ya moto..Hivyo tunaonywa tujihadhari sana.. kama biblia inavyosema katika kitabu cha Wakolosai..
Wakolosai 2:8 “Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.
9 Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.
10 Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka”.
Sasa utauliza waislamu wote ni wabaya? Hapana!..Sio watu wote wabaya..kama vile ilivyo sio wakristo wote wazuri….Kuna baadhi ambao hawaujui ukweli bado lakini siku wakiujua watatoka katika makosa hayo…Hivyo ni wajibu wetu kuwafundisha katika njia sahihi ili watoke katika mitego hiyo ya ibilisi na si kuwachukia, wala kuwatupia maneno ya dhihaka na laana, Kwasababu ndivyo Kristo anavyotufundisha kwamba tuwapende watu wote bila kuchagua, na Kristo alikufa kwaajili ya watu wote.
Ubarikiwe.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Kwanini Shetani ni joka wa zamani?
Shalom, ni kwa neema za Mungu wetu tumeliona tena jua leo..wapo ambao hawakupata nafasi hiyo, hivyo hatuna budi kumshukuru sana Mungu wetu. Karibu tujifunze Neno la Mungu chakula cha kweli cha roho zetu.
Biblia inasema katika..
Ufunuo 20:1 “Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake.
2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu;”
Shetani anajulikana kama joka wa zamani..ikiwa na maana kuwa ameishi muda mrefu, na ameishi katika hali hiyo hiyo ya ujoka tangu zamani…Na kama unavyojua kitu chochote ambacho kimeishi muda mrefu, kwa mfano mtu aliyeishi muda mrefu ni lazima atakuwa anajua mambo mengi…wazee wenye umri mkubwa wanakuwa wanajua mambo mengi zaidi kuliko vijana..
Kwasababu wamekumbana na mambo mengi katika maisha yao na wamejifunza mambo mengi, wamejifunza kutokana na makosa yao na kutokana na makosa ya watu wengine…hivyo hawawezi kufananishwa hata kidogo na watoto waliozaliwa hivi karibuni.
Vivyo hivyo shetani naye anajulikana kama joka wa zamani…
maana yake ni kwamba anajua mambo mengi sana yamhusuyo mwanadamu…alikuwepo tangu Edeni, anamjua Adamu kwa sura na tabia hajamsahau,..anamjua Hawa…anamjua Nuhu, na alikuwa anashuhudia jinsi dunia ilivyokuwa inaangamizwa kwa gharika…alikuwepo anatazama…Bado anaikumbuka sura ya Ibrahimu na ya Sara…anakumbuka ni wapi walipomsumbua katika maisha yao..Anamkumbuka Musa..na bado anazijua tabia zake zote na anaujua udhaifu wake..Anayo sura ya Danieli na ya Nebukadneza, na ya Eliya kichwani mwake na anazikumbuka tabia zao…Na zaidi ya yote anamfahamu sana Mkuu wa Uzima Yesu Kristo, anakumbuka matukio yote tangu anazaliwa mpaka alipokuwepo kule jangwani akimjaribu, na alipokufa na kufufuka, anajua nguvu zake na mamlaka yake aliyonayo sasa…
Vivyo hivyo anawajua watu, anawajua watu na tabia zao, anajua wanapenda nini, na hawapendi nini…Ameviona vizazi vyote tangu Adamu mpaka sasa…Hebu jiulize wewe tu mpaka umri ulioufikia sasa ambao pengine haujazidi hata miaka 60 lakini tayari umeshajua tabia za baadhi ya watu na baadhi ya makabila kiasi kwamba pengine hata ukimwona tu mtu Fulani tayari umeshajua kundi la kumweka hata kabla ya kuendelea mbele sana…Sasa kama wewe na miaka yako hiyo 50 tu tayari unajua jamii za watu na tabia zao…Unafikiri shetani atakuwa anawajua wanadamu kwa kiwango gani?..maana yeye tangu Edeni mpaka leo yupo.
Nataka nikuambia anawajua wanadamu vizuri..anajua ni wapi pa kuwashikia watoto, watu wazima na wazee…kwasababu mwanadamu ni Yule Yule…na biblia inasema hakuna jipya chini ya jua…anajua namna ya kummaliza mtu mchanga kiroho pindi tu anapotaka kujaribu kumtafuta Mungu…kwasababu alishajaribu kwa watu kadhaa huko nyuma wa vizazi vilivyopita na akafanikiwa…Anajua ni jinsi gani anaweza kuwaangusha watumishi wa Mungu..kwasababu alishajaribu huko nyuma na akafanikiwa kwa baadhi hivyo anatumia huo huo uzoefu kwa watu wa vizazi vyote. Anajua jinsi ya kuwazuia watu wasisali, wasimtafute Mungu n.k kwasababu alishaijaribu hiyo njia huko nyuma na ikafanya kazi.
Ndugu mpendwa usipoingia ndani ya Yesu kisawasawa hutamweza shetani kwa vyovyote vile anazo akili nyingi za kukuzidi wewe na mimi, ukisema humtaki Bwana Yesu na kwamba unaweza kujizuia usizini bila hata ya kuwa ndani ya Kristo, unapoteza muda wako! Siku moja utazini tu..alishawajaribu watu kama nyie huko nyuma na akawanasa hivyo wewe sio wa kwanza kuwaza hivyo au kujaribu hivyo..Ukisema naweza kufanya hichi chema au kile bila kuwa ndani ya Yesu..nataka nikuambie ni muda tu unaupoteza..watu kama nyie shetani alishawatafutia suluhisho lake pengine hata zaidi ya miaka 2000 iliyopita huko nyuma…wewe unaweza kukiri ni wa kwanza lakini kumbe hata ni wa milioni 10 kwenye kalenda zake na orodha zake za watu waliojaribu kufanya kama wewe huku wakiwa nje ya Kristo na akawashinda..
Hivyo wewe uliyezaliwa juzi huwezi kumzidi hekima Yule aliyekuwepo miaka mingi iliyopita huko nyuma…(Hujui ni kwanini shetani anaitwa mungu wa ulimwengu huu? Ni kwasababu anajua mambo ya wanadamu sana kuliko mwanadamu yoyote yule).
Ndio maana Bwana Yesu alimwambia kwamba siku zote anayawaza yaliyo ya wanadamu na si ya Mungu.. Kwanini? kwasababu anakesha kumsoma mwanadamu na namna ya kumtawala. Kasome (Mathayo 16:23)..
Hivyo utauliza kama shetani anayajua mambo ya wanadamu kiasi hicho, kiasi kwamba hakuna upenyo wa kuweza kumzidi ni nani basi atasalimika?
Jibu ni kwamba pamoja na ukongwe wake wote wa kuwafahamu wanadamu, yupo mmoja ambaye ni mkongwe zaidi yake..Na huyo si mwingine zaidi ya Mungu mwenyezi aliye Baba yetu ambaye tunamwabudu sisi kupitia Yesu Kristo(Danieli 7:9). Huyo anajulikana kama MZEE WA SIKU.
Danieli 7:13 “Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia HUYO MZEE WA SIKU, wakamleta karibu naye.
14 Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa”.
Baba yetu anatujua kuliko shetani anavyotujua..shetani anauzoefu wa kutuangusha lakini Hekima iliyo kwa Mungu inauwezo hata wa kuyajua mawazo yake na nia yake na mipango yake, na kuyaangusha chini mawazo yake..chochote anachotaka kukifikiria kwa uzoefu wake, sisi tulio ndani ya Kristo tayari tunauwezo wa kuitegua mitego yake..hekima ile ya Kiungu inaingia ndani yetu ambayo inatupa uwezo wa kuzitambua na kuziangusha fikra zote za shetani. Lakini hekima hiyo wanapewa wale tu wanaomwamini mwanae mpendwa Yesu Kristo.
Wengine wote walio nje ya Kristo kamwe hawataweza kumshinda Yule joka wa zamani ambaye ni Ibilisi..watapelekwa kule shetani anakotaka waende..hata kama hawataki, ndio maana mtu ambaye hajaokoka kisawasawa kamwe hawezi kuwa na Amani, na hawezi kuishinda dhambi, na mapenzi ya ulimwengu huu ndio anayoyatenda…wakati mwingine anapanga hiki lakini mwishoni kinaishia kuwa kingine…kwanini? Ni kwasababu anataka kujiongoza mwenyewe na kudhani anaweza kufanikiwa kwa nguvu zake na akili zake.
Hivyo kama hujaokoka, bado tumaini la kumshinda Yule joka lipo, Hekima ya kiMungu inataka kuingia leo ndani yako…usimsikilize shetani anayekuwambia akilini mwako sasahivi kwamba huwezi kuokoka kwamba unadhambi nyingi na Mungu hawezi kukusamehe…ndivyo alivyowaambia watu wengi wa vizazi vya nyuma na kuwaangusha..anatumia ukongwe wake tu…lakini wewe leo mkatae na mkane kwa vitendo…Amua leo kuacha dhambi, na kutubu, amua kuacha kwenda disko, amua kuacha kusengenya, amua kuacha ulevi na uasherati na Bwana atakupenda sana…Na hekima ya ajabu itokayo kwa yule MZEE WA SIKU, (YEHOVA) Mungu wetu,itaingia ndani yako itakayoweza kutambua mitego yake na hila zake…
Mithali 2:6 “Kwa kuwa Bwana huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;
7 Huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili; Yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu;
8 Apate kuyalinda mapito ya hukumu, Na kuhifadhi njia ya watakatifu wake.
9 Ndipo utakapofahamu haki na hukumu, Na adili, na kila njia njema.
10 Maana hekima itaingia moyoni mwako, Na maarifa yatakupendeza nafsi yako;”
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 78900131
Mada Nyinginezo:
ANGUKO LA UFALME WA SHETANI:
ZIFAHAMU HUDUMA KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.
NI NANI ALIYEWALOGA?
JINSI NEEMA YA MUNGU ILIVYOKUWA KUBWA KWA MKE WA LUTU.
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
CHUKIZO LA UHARIBIFU