Title August 2020

 Behewa ni nini?

Behewa kwa jina lingine ni UA, ni eneo la wazi lililokuwa limezungushiwa fensi mbele ya Hema ya kukutania , kwa ajili ya makuhani kutoa sadaka za kuteketezwa, na kufanya shughuli za kikuhani tazama picha juu..

Lakini  baadaye Hekalu lilipokuja kutengenezwa na Sulemani pale Yerusalemu, eneo la behewa/Ua lilizungushiwa ukuta, na pakawa na behewa kuu mbili, 1) ya ndani 2) na ya nje, ili ya ndani ikabakia kuwa ya makuhani tu, kufanya mambo ya upatanisho na sadaka za kuteketezwa, Na ile ya nje ikabakia kuwa ya Wayahudi  wote kukutanika kuabudu..Tazama picha chini..

hekalu la sulemani

Lakini pia behewa, kwenye biblia haikumaanisha tu ni lazima iwe mbele ya hema ya kukutania au mbele ya Hekalu la Mungu, biblia inayonyesha pia, zilikuwa pia kwenye majumba ya kifalme na ya kikuhani.

1Wafalme 7:1 “Naye Sulemani alikuwa katika kuijenga nyumba yake mwenyewe miaka kumi na mitatu, akaimaliza nyumba yake yote….11 Na juu kulikuwa na mawe ya thamani, mawe ya kuchongwa, sawasawa na cheo, na mierezi.

12 Na behewa kubwa pande zote ilikuwa na safu tatu za mawe ya kuchongwa, na safu moja ya mihimili ya mierezi; mfano wa behewa ya ndani ya nyumba ya Bwana, na ukumbi wa nyumba”.

Mathayo 16:3 “Wakati ule wakuu wa makuhani, na wazee wa watu, wakakusanyika katika behewa ya Kuhani Mkuu, jina lake Kayafa”;

Lakini pia katika kitabu cha ufunuo tunasoma, kuwa wakati wa mwisho, behewa/ua iliyo nje ya hekalu ambalo litakuja kujengwa na Wayahudi pale Yerusalemu siku za mwisho, litamilikiwa na watu wa mataifa kwa muda wa miezi 42..

Ufunuo 11:1 “Nikapewa mwanzi kama fimbo; na mmoja akaniambia, Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wasujuduo humo.

2 Na behewa iliyo nje ya hekalu uiache nje wala usiipime, kwa maana Mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arobaini na miwili”.

Ili kufahamu habari kamili, sababu na maana yake rohoni ya mambo hayo fungua vichwa vingine vya masomo tulivyovirodhesha chini.

Kwa mawasiliano/mafundisho zaidi kwa njia ya whatsapp, tutumie ujumbe kwenye namba hizi: +255789001312/ +255693036618

  Au Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo

Konzo la Ng’ombe ni nini? (Waamuzi 3:31).

Hema ya kukutania ni nini, na ilikuwaje?

UBATIZO NI NINI NA ULIO SAHIHI NI UPI?

NA TAA YA MUNGU ILIKUWA BADO HAIJAZIMIKA

Je! dhambi zote ni sawa Kuna dhambi kubwa na ndogo?

Kisiwa cha Patmo kipo nchi gani?.

Rudi Nyumbani:

Print this post

BWANA SI MWEPESI WA HASIRA, LAKINI BWANA NI MWINGI WA HASIRA.

Kuna wakati ulifika Nabii Nahumu alifunuliwa juu ya hatma ya mji mmoja ulioitwa Ninawi, Mji huu ndio uliokuwa mji mkuu waTaifa la Ashuru, ulikuwa mji wa kwanza kwa ukubwa kuliko mji yote iliyokuwa ulimwengu kwa wakati ule. Baadaye ndio ikaja kutokea miji mwingine ulioitwa Babeli ..Sasa katika mambo aliyoongozwa Nabii Nahumu kuandika ni pamoja na uvumilivu wa hasira ya Mungu, pamoja na ukali wa hasira ya Mungu. Maneno hayo utayaona mwanzoni kabisa mwa kitabu cha Nahumu..

Nahumu 1:1 “Ufunuo juu ya Ninawi. Kitabu cha maono aliyoyaona Nahumu….

2 Bwana ni Mungu mwenye wivu, naye hujilipiza kisasi; Bwana hujilipiza kisasi, NAYE NI MWINGI WA HASIRA; Bwana hujilipiza kisasi juu ya adui zake, huwawekea adui zake akiba ya hasira.

3 BWANA SI MWEPESI WA HASIRA, ana uweza mwingi….”

Unaona, sasa unaweza ukajiuliza ni kwanini Mungu azungumze maneno hayo mawili kwa wakati mmoja?

Utakumbuka kuwa mji huu wa Ninawi ndio ule mji ambao Nabii Yona alitumwa kwenda kuwahubiria juu ya dhambi zao kwamba watubu..Kama tunavyoijua ile habari, watu wale walisikia injili ya Yona, na walipotubu Mungu aliwarehemu japokuwa walikuwa sio wakamilifu ipasavyo.. hiyo ilimfanya mpaka Yona amkasirikie Mungu kwanini hajawaangamiza wale watu waovu..Ndipo Mungu akamwambia Yona maneno yafuatayo;

Yona 4:11 “na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi ya mia na ishirini elfu, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?”

Unaona huruma za Mungu jinsi zilivyokuwa nyingi?.. Japokuwa walikuwa ni waabudu miungu, wapagani, lakini Mungu aliwahurumia tu pale walipotubu dhambi zao na kugeuka…Lakini tunavyozidi kusoma biblia tunaona, mambo hayakuwa hivyo siku zote ulifika wakati mji huo wa Ninawi ulirudia mambo yale yale ya kale, uovu ukaendelea kama ulivyokuwa pale mwanzo kipindi Yona anatumwa, wakasahau kuwa walinusurika kuwa jivu mfano wa Sodoma na Gomora.

Matokeo yake ndio tunakuja kuona Nabii Nahumu akitokea na kutoa unabii juu ya mwisho wa Taifa hilo..Pengine wakati Nahumu anatoa unabii huu waliona kama ni utani tu, kwamba watatubu tu kama kipindi kile cha Yona?..Wakawa wanasema tunajua Mungu siku zote si mwepesi wa hasira, Mungu ni wa rehema, anaghahiri mabaya..Hata hivyo hawezi kuliangamiza Taifa kubwa kama hili duniani (Ashuru) na mji wetu huu Ninawi ulio msaada wa mataifa mengi ulimwenguni.

Ndivyo walivyodhania, wakapumbazwa, wakajisahau kabisa, tena na jinsi walivyoona wamefanikiwa kuwachukua wayahudi utumwani, (yale makabila 10), ndio wakadhani kuwa Mungu amewapendelea..

Lakini Nabii Nahumu akatoa unabii juu ya mji huo..akisema.

Nahumu 3:7 “Hata itakuwa, wote wakutazamao watakukimbia, wakisema, Ninawi umeharibika; ni nani atakayeuhurumia? Nikutafutie wapi wafariji”?

Hayo maneno aliyoyasema nabii Nahumu yalikuja kutimia kama yalivyo, ni kwa vile tu, biblia haiwezi kuandika kila kitu, na kila historia, kama ingekuwa ni hivyo vitabu visingetosha duniani vya biblia. Lakini historia ipo wazi kabisa inaonyesha, ulipofika mwaka wa 612 KK, Wababiloni pamoja na wamedi waliunganisha nguvu, na kuizunguka Ninawi mji mkuu wa Ashuru, na kuuteka na kuungamiza, na hapo ndipo ikawa mwisho wa Taifa linaloitwa ashuru na mji wa Ninawi mpaka leo hii tunavyozungumza ni miaka zaidi ya 2,500, ni vipande vya mawe tu vimesimama pale kaskazini mwa Iraq. Na taifa la Babeli ndipo lilipopatia nguvu hapo, ambalo nalo baadaye lilikuja kuangamizwa hivyo hivyo.

Nahumu 3:19 “Jeraha yako haipunguziki; jeraha yako ni nzito sana; wote wasikiao habari zako wapiga makofi juu yako; kwa maana ni nani ambaye uovu wako haukupita juu yake daima”?

Biblia inasema Ninawi ni mji uliokuwa umekaa pasipo kufiri, upo upo tu, ukidhani wenyewe ndio wenyewe, ulipokuwa unashinda vita vingi, na unafanikiwa kuchukua mateka mataifa mengi, lakini siku yao ilipofika, yalikuwa ni majuto yasiyoelezeka..

Sefania 2:13 “Naye atanyosha mkono wake juu ya upande wa kaskazini, na kuiangamiza Ashuru; naye ataufanya Ninawi kuwa ukiwa, kuwa mahali pakavu kama jangwa…..

15 HUU NDIO MJI ULE WA FURAHA, ULIOKAA PASIPO KUFIKIRI, ULIOSEMA MOYONI MWAKE, MIMI NIKO, Wala hapana mwingine ila mimi. Jinsi ulivyokuwa ukiwa, Mahali pa kulala pa wanyama wa bara! Kila mtu apitaye atazomea, Na kutikisa mkono wake”.

Ezekieli 32:22 “Ashuru yuko huko, na watu wake wote jamii; makaburi yake yamzunguka; wote pia wameuawa, wameanguka kwa upanga”

Ni nini Bwana anataka tujue?

Hiyo ni kuonyesha kuwa japokuwa Mungu si mwepesi wa Hasira, lakini hasira yake inapofika kilele basi ni MWINGI WA HASIRA..yaani haipoi kwa haraka, inadumu milele kama sio kwa kipindi kirefu sana..

Na ndio maana leo hii watu wengi wanaposoma yale mapigo yaliyoandikwa kwenye kitabu cha ufunuo wanaona kama hayafikirikiki kwa akili za kibinadamu, ni kweli unaweza kudhani hivyo lakini ndugu yale mapigo unavyoyaona pale ndivyo yatakavyokuwa.. Ziwa la moto unavyolisikia ndivyo lilivyo. Ukienda kule, hutatamani hata adui yako afike huko kwa mateso yaliyo kule yasiyoelezeka.. “Mungu si mwepesi wa hasira, lakini ni mwingi wa hasira”

Kama leo unalikataa Neno lake, na unaona hakuna chochote kinachotokea au kitakachoweza kutokea juu yako, pengine Mungu amekuambia utubu mara nyingi, lakini unafanya hivyo leo, kesho unarudia mambo yale yale ya kidunia.. Upo wakati utafananishwa na Ninawi..Utakatwa na kupotea moja kwa moja, wakati huo ukifika hata uombeje, hata ulieje, hakuna rehema tena juu yako.

Mambo haya sio uongo!..yaliwatokea watu wa Ninawi kama yalivyo..kasome katika Historia baada ya kukataa maonyo, na pia yaliwatokea wana wa Israeli vile vile kwa kukataa maonyo, na hata kusababisha Mungu kukataa kuwasamehe. Soma mistari ifuatayo utathibitisha..

2Nyakati 36: 15 “Naye Bwana, Mungu wa baba zao, akatuma kwao kwa mikono ya wajumbe wake, akiondoka mapema, na kutuma; kwa sababu aliwahurumia watu wake, na makao yake;

16 lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, hata ilipozidi ghadhabu ya Bwana juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya.

17 Kwa hiyo akaleta juu yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao kwa upanga nyumbani mwa patakatifu pao, asiwahurumie kijana wala mwanamwali, mzee wala mkongwe; akawatia wote mkononi mwake”.

Mathayo 3:10 “Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni”.

Kama hujampokea Yesu, fanya hivyo sasa..

Bwana akubariki.

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

AMELAANIWA AANGIKWAYE MSALABANI.

YONA: Mlango wa 4

JE KUVAA PETE NI DHAMBI?

JE! KUBET NI DHAMBI?

HAPANA HATA MMOJA ATAKAYEIONJA KARAMU YANGU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Uwanda wa dura ni nini?

Ni vizuri kufahamu kwanza maana ya uwanda, Uwanda ni sehemu iliyowazi iliyonyooka. Hivyo uwanda wa Dura ni sawa na kusema eneo la Dura lililo wazi.

Eneo hilo lilikuwepo Babeli na ndilo Nebukadneza mfalme alilichagua kuwa sehemu ya sanamu yake ya dhahabu aliyoitengeneza kwa ajili ya watu wa ulimwengu mzima kuisujudia. Eneo hilo la uwanda wa dura lilikuwa zuri kwa sanamu kuonekana vizuri na watu wengi kukusanyika.

Danieli 3:1 “Nebukadreza, mfalme, alifanya sanamu ya dhahabu, ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita; akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli.

2 Ndipo Nebukadreza akatuma watu kuwakusanya maamiri, na manaibu, na maliwali, na makadhi, na watunza hazina, na mawaziri, na mawakili, na wakuu wa wilaya zote, ili wahudhurie wakati wa kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha”.

Je! unafahamu ile sanamu inafunua nini siku hizi za mwisho?

Je! unajua chapa ya mnyama ndio itakuja kwa namna hiyo? Ili kufahamu hayo kwa upana fungua vichwa vya masomo tulivyoviorodhesha chini.

Mada Nyinginezo:

DANIELI: Mlango wa 3

UFUNUO: Mlango wa 13

CHUKIZO LA UHARIBIFU

WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.

JE UDHAIFU WANGU UNAWEZA KUZUIA INJILI?

Rudi Nyumbani:

Print this post

SHUSHANI NGOMENI NI WAPI KWA SASA?

Shushani ngomeni ni sehemu gani kwasasa?


Mji wa shushani/Susa kwasasa upo eneo linaloitwa Shush katika  nchi ya Iran.

kabla wamedi na waajemi kuiangusha Babaeli, Shushani ulikuwa ni mji mkuu wa Elamu, ambao tunaona Danieli akiuzungumzia katika.

Danieli 8:1 “Katika mwaka wa tatu wa kumiliki kwake mfalme Belshaza maono yalinitokea mimi, naam, mimi Danieli, baada ya hayo yaliyonitokea hapo kwanza.

2 Nami naliona katika maono; ilitukia, nilipoona, nalikuwako huko Shushani ngomeni, katika wilaya ya Elamu; nikaona katika maono, nami nalikuwa karibu na mto Ulai”.

Lakini baada ya wamedi na waajemi kuuchukua ufalme, mji huu ulikuja kugeuzwa kuwa mji wa kifalme wa wafalme wa Uajemi na Umedi.

Katika biblia tunaona Esta aliishi sehemu kubwa ya umalkia wake katika mji huu wa kifalme Shushani.

Esta 1:1 Zamani za Ahasuero; naye huyu Ahasuero alimiliki toka Bara Hindi mpaka Kushi, juu ya majimbo mia na ishirini na saba;

2 siku zile mfalme Ahasuero alipoketi katika kiti cha enzi cha ufalme wake, huko Shushani ngomeni;

Unaweza kusoma pia, (Esta 2:3,5,8  Esta 3:15, Esta 4:8,16, Esta 8:14, Esta 9:6,11,12,13.)

Vilevile Nehemia naye alipokuwa mnyweshaji wa mfalme wa kiajemi alikuwa katika mji huu, huu wa Shushani..

Nehemia 1:1 “Habari za Nehemia, mwana wa Hakalia. Ikawa katika mwezi wa Kisleu, mwaka wa ishirini, nilipokuwapo Shushani ngomeni,

2 Hanani, mmoja wa ndugu zangu, akanijia, yeye na watu wengine waliotoka Yuda; nami nikawauliza habari za Wayahudi waliopona, hao watu wa uhamisho waliosalia; na habari za Yerusalemu”.

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia masomo ya biblia ya mara kwa mara kwa njia ya whatsapp au email yako, basi tutumie ujumbe kwa kupitia namba hii: +255 789001312

Mada Nyinginezo:

MTO YORDANI UKO NCHI GANI KWA SASA?

Mto Frati upo nchi gani, Umuhimu wake katika biblia ni upi?

Israeli ipo bara gani?

UNYAKUO.

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Safari ya mbinguni.

Safari ya kwenda mbinguni ni safari isiyo na siku ya kupumzika. Kama vile moyo unavyodunda bila kusimama kwa miaka na miaka…Ndivyo safari ya Mbinguni ilivyo.. Ni mwendelezo kila kukicha, tukilala, tukiamka tupo safarini.

Hivyo ni lazima kulikumbuka hilo. Na safari ya kwenda mbinguni ni ngumu kuliko ya kwenda kuzimu.  Hata katika hali ya kawaida, kupanda juu ni kugumu kuliko kushuka… Ukitaka kushuka kilima unaweza kujiachia tu ukaserereka mpaka ukafika chini, pasipo kutumia nguvu yoyote. 

Lakini upandapo kilima huwezi kujiachia, ni lazima kupambana na kutumia nguvu nyingi ili kufika juu. Na safari ya kwenda mbinguni ipo hivyo hivyo. Kila hatua ni ya kujishika usianguke.  Kwasababu ipo nguvu itakayotuvuta chini  tusipojishika vizuri.

1Wakorintho 10:12 “Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke”.

Hivyo ni lazima tujiangalia sana! kwasababu kubomoa ni rahisi kuliko kujenga, mahali tunapoishi, mahali tunapofanyia kazi, mazingira tunayoishi n.k Ni lazima kuhakikisha hayaharibu imani yetu na wala hayakwamishi safari yetu ya kwenda mbinguni.

Mbingu ipo! na Kristo Mwana wa Mungu anarudi!. 

Bwana akubariki.


Mada Nyinginezo:

IPELEKE SADAKA YAKO MAHALI SAHIHI,ILI UBARIKIWE.

Je! Shetani alitolea wapi uovu?

UNATAKA KUBARIKIWA? BASI USIKWEPE GHARAMA ZAKE.

FUNGUO ZA UZIMA, MAUTI NA KUZIMU.

NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA!

Rudi Nyumbani:

Print this post

JIOKOE WEWE NA NYUMBA YAKO.

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze Neno la Mungu ambalo ndio taa ya miguu yetu na mwana uiongozayo njia yetu (Zab.119:105).

Katika safari ya Imani usisahau kamwe kuifanya kazi ya Mungu kwa bidii, kuhakikisha Habari ya ufalme inamfikia kila mtu. Lakini lililo kubwa Zaidi ni kuhakikisha wewe Pamoja na nyumba yako mnaokolewa, wewe Pamoja na Watoto wako, mume wako, mke wako na Watoto wako na wote unaoishi nao wanaokolewa. Utasema hiyo inawezekana hata kama hawataki kabisa kusikia Habari za Mungu?..Jibu ni ndio inawezekana.

Kama umewahi kusoma Habari za Rahabu, utakuwa unaelewa…alipopewa nafasi ya kuokoka yeye peke yake binafsi, hakuona ni vyema kuokoka mwenyewe bali aliiokoa na familia yake yote..

Yoshua 2:12 “Basi sasa, nawasihi, niapieni kwa Bwana, kwa kuwa nimewatendea ihisani, ya kwamba ninyi nanyi mtaitendea ihisani NYUMBA YA BABA YANGU; tena nipeni alama ya uaminifu

13 ya kwamba mtawaponya hai baba yangu na mama yangu, na ndugu zangu wanaume na wanawake, na vitu vyote walivyo navyo, na kutuokoa roho zetu na kufa.

14 Wale wanaume wakamwambia, Uhai wetu badala ya uhai wenu, ikiwa hamwitangazi habari ya shughuli yetu hii; kisha itakuwa, wakati Bwana atakapotupa nchi hii, tutakutendea kwa ihisani na uaminifu”

Kama umewahi kusoma pia Habari za Lutu utakuwa unajua kuwa kabla ya maangamizi kushuka, aliondoka na mke wake na Watoto wake wawili, na baadhi ya ndugu zake pia aliwahubiria.

Na hata wakati wa Gharika..Nuhu hakuona vyema kuokoka yeye peke yake lakini biblia inasema Safina ile aliyoitengeneza ilikuwa pia ni kwaajili ya Watoto wake.

Waebrania 11:6 “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

7 Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, ALIUNDA SAFINA, APATE KUOKOA NYUMBA YAKE. Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa Imani”.

Umeona hapo? Anasema aliiunda ili apate kuiokoa familia yake, kwahiyo lengo la Safina halikuwa kumwokoa Nuhu tu, Mungu angeweza kumwokoa Nuhu kwa njia nyingine bila hata hiyo Safina, lakini kwasababu Nuhu alikuwa na familia na pia kulikuwa na Wanyama, Ndipo Mungu akatengeneza njia hiyo ya wokovu kwa kupita Safina.

Na kama umegundua kitu ni kwamba Mungu hakuitengeneza yeye ile Safina bali alimwambia Nuhu aitengeneze, kwasababu aliyekuwa ameonekana mwenye haki mbele za Mungu ni Nuhu peke yake, (Mwanzo 6:8) hao mwengine hawakustahili, hawakumpendeza Mungu kabisa katika njia zao, ndio maana utaona Hamu kipindi kifupi tu baada ya kutoka kwenye Safina aliutazama uchi wa Baba yake kwa makusudi, na wala hata hakusikia kitu kikimhukumu ndani yake kwa alichokifanya. (Sasa unaweza kujiuliza imekuwaje mtu kama huyo hakuangamia kwenye gharika Pamoja na waovu wengine). Jibu ni kwasababu ya Baba yao…hivyo gharama za kuwaokoa watoto wake na mke wake zilikuwa ni za Nuhu..

Hivyo Nuhu ilimbidi afanye kazi kubwa ya kutengeneza Safina ile kwa miaka mingi sana, ili tu familia yake ipone na baadhi ya wanyama.

Kadhalika utasoma pia Musa, alikuwa ni mtu wa namna hiyo hiyo, kwani ulipofika wakati wana wa Israeli jangwani walipomkasirisha Mungu kiasi cha Mungu kutaka kuwaangamiza wote, Musa alisimama kuwatetea mbele za Mungu kwa bidii.

Kutoka 22:7 “Bwana akamwambia Musa, Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao,

8 wamepotoka upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu, wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.

9 Tena Bwana akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu.

10 basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.

11 Musa akamsihi sana Bwana, Mungu wake, na kusema, Bwana, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu?

12 Kwa nini Wamisri kunena, wakisema, Amewatoa kwa kuwatenda uovu, ili apate kuwaua milimani, na kuwaondoa watoke juu ya uso wa nchi? Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako.

13 Mkumbuke Ibrahimu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele.

14 Na Bwana akaughairi ule uovu aliosema ya kwamba atawatenda watu wake”

Mifano ipo mingi sana, hatuwezi kuandika yote hapa, lakini kwa hiyo michache unaweza kuelewa kuwa sisi tuliobahatika neema ya wokovu, tunalo jukumu la kusimama kwaajili ya nyumba zetu. Bwana amekupa neema wewe mmoja, ili wengine wote katika nyumba yako waokolewe. Ni jukumu lako na si la Mungu, kupambana kwa bidii ili waingie ndani ya mlango huu wa Neema, kama Musa alivyopambana, kama Nuhu alivyopambana, kama Lutu alivyopamba na kama Rahabu alivyopambana. Na hiyo inakuja kwa kuwaombea kwa bidii na si kuwahukumu, inakuja kwa kuhubiria wanao kwa bidii sana Habari za wokovu, kwa kumhubiria mkeo au mumeo na kumwombea..huku wewe mwenyewe ukionyesha kumpendeza Mungu na kutokuiga wala kufanya matendo kama yao.

Kwa kufanya hivyo ipo neema ya wokovu ambayo itamwagika kwa watu wa nyumbani kwako pia, nao pia mwishoni wataokolewa kama wewe. Hivyo hupaswi/hatupaswi kufurahia wokovu ukiwa kwetu tu!.. tunapaswa tufurahie ukiwa kwa wengine pia.

Mwisho kabisa. Bwana anakaribia kurudi, mambo yote ya ulimwengu yatabatilishwa, na mlango wa neema utafungwa Bwana Yesu alisema wengi watatamani kuingia siku hiyo wasiweze. Hivyo kama hujampokea Yesu na unasoma jumbe hizi kila siku, au jumbe nyingine zinazofanana na hizi, basi siku ile hutasema hukusikia, nakushauri yakabadhi Maisha yako kwa Yesu, yeye ndiye Njia, kweli na Uzima..hakuna namna utaweza kuiona mbingu kama unakataa Habari za uzima sasa.

Bwana atubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

HATUTAACHA KUJIFUNZA NENO KILA INAPOITWA LEO.

Je ni kweli huwezi kuijua karama yako mpaka uwekewe mikono na wazee?

USHAURI KWA MWANAMKE WA KIKRISTO.

Yesu ni Mungu?, Na Kama ni Mungu kwanini alikufa?

HUYU SI YULE SEREMALA, MWANA WA MARIAMU?

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 2

Rudi Nyumbani:

Print this post

IKABODI MAANA YAKE NI NINI?

Ikabodi maana yake ni “Utukufu umeondoka”

Hili ni jina ambalo alipewa mtoto wa Finehasi na mke wake siku alipokuwa anajifungua, na hiyo ni baada ya kusikia  Mume wake amekufa katika vita, pamoja sanduku la agano kuchukuliwa na wafilisti na  yeye vilevile anakaribia kufa ndipo akaona jina sahihi linalompasa huyo mtoto ni IKABODI, akiwa na maana kuwa utukufu wa Mungu umeondoka katika Israeli.

1Samweli 4:19 “Tena mkwewe, mkewe huyo Finehasi, alikuwa mja-mzito, karibu na kuzaa; basi, aliposikia habari ya kutwaliwa sanduku la Mungu, na ya kwamba mkwewe na mumewe wamekufa, akajiinamisha, akazaa; maana utungu wake ulimfikilia.

20 Hata alipokuwa katika kufa, wale wanawake waliohudhuria karibu naye wakamwambia, Usiogope; kwa maana umezaa mtoto mwanamume. Walakini hakujibu, wala hakumtazama.

21 Akamwita mtoto, IKABODI, akisema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; kwa sababu sanduku la Mungu lilikuwa limetwaliwa, na kwa sababu ya mkwewe na mumewe.

22 Naam, akasema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; maana sanduku la Mungu limetwaliwa”.

Lakini hiyo yote ni kwasababu ya Makosa ya Eli kuhani mkuu kutowazuia watoto wake (Hofni na Finehasi) kuinajisi madhabahu ya Mungu, kwa kulala na wale wanawake waliokuwa wanahudumu mbele ya hema ya Bwana. Japokuwa walionywa sana lakini hawakusikia, ndipo Mungu akamwambia Eli kwa kinywa cha Samweli kuwa atafanya jambo ambalo wakisikia, masikio yao wote yatawasha..Na jambo lenyewe ndio hilo la Sanduku la Mungu kuibwa na maadui jambo ambalo halijawahi kutokea katika historia ya taifa la Israeli.

Hata sasa, utukufu wa Mungu unaweza kuondoka katika kanisa Fulani(Ikabodi), ikiwa wahudumu au watumishi wa madhabahuni hiyo ya Mungu watainajisi nyumba ya Mungu kwa kufanya dhambi za makusudi, mfano wa hawa watoto wa Eli.

Vilevile utukufu wa Mungu unaweza kuondoka(Ikabodi), kwa mtu binafsi, ikiwa ataonywa mara nyingi asisikie. Ikiwa na wewe unaonywa mara nyingi auche dhambi, uache uzinzi, uache anasa, utubu umgeukie Kristo lakini husikii, upo wakati huo utukufu wa Mungu utaondoka ndani yako moja kwa moja, na siku ukiondoka basi habari yako imeishia hapo hapo kamwe hutakaa uiamini injili tena.

Hivyo ikiwa upo bado nje ya Kristo tubu dhambi zako ukabatizwe. Na Bwana atakuponya.

Kama upo tayari kufanya hivyo, fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Ubarikiwe.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo ya biblia kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye  namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?

USISUBIRI MPAKA MUNGU AKUAMBIE, NDIO UFANYE!

 

CHA KUTUMAINI SINA lyrics

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

EPUKA MUHURI WA SHETANI

Rudi Nyumbani:

Print this post

AKAMSHIKA MKONO YULE KIPOFU, AKAMCHUKUA NJE YA KIJIJI.

Shalom.

Marko 8:23-26 Inatuambia Yesu alipokutana na Yule kipofu kule Bethsaida, Hakumponya palepale kama ilivyokuwa desturi yake ya kuponya watu wote wanaomfuata, bali biblia inatuambia alimchukua kwa kumshika mkono na kuanza kumtoa kwanza nje ya kijiji.

“22 Wakafika Bethsaida, wakamletea kipofu, wakamsihi amguse.

23 Akamshika mkono yule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu?

24 Akatazama juu, akasema, Naona watu kama miti, inakwenda.

25 Ndipo akaweka tena mikono yake juu ya macho yake, naye akatazama sana; akawa mzima, akaona vyote waziwazi.

26 Akampeleka nyumbani kwake, akisema, Hata kijijini usiingie”.

Jaribu kutengeneza picha, wewe ni kipofu, unapelekwa kwa daktari kwa ajili ya kupewa dawa uondoke, badala ya kukutibu anakuchukua anaondoka na wewe, bila maelekezo yoyote, na kibaya zaidi afadhali angekuwa anakupeleka hospitali nyingine badala yake anakupeleka mahali ambapo hata husikii tena sauti za watu, nje kabisa ya mji, ni rahisi kudhani huyu mtu hana nia nzuri na mimi.. Lakini tunaona huyu kipofu alitii, japokuwa hajui ni wapi anapelekwa, pengine alitembezwa na Yesu kilometa kadhaa, mpaka wanafikia mahali ambapo hamna makazi ya watu, ni mashamba tu, hata wale watu waliompeleka kwake walishamwacha, amebaki yeye tu na Yesu, na pengine na wanafunzi wake tu.

Akiwa sasa hana tumaini lolote, haelewi ni kitu gani kinaendelea hapo ndipo Yesu anamwekea mikono yake, na kumponya..Lakini utajiuliza tena, ni kwanini biblia inatuaeleza aliponywa mara ya kwanza na ya pili?..Ni kwasababu kuna jambo Yesu alitaka tujue kuhusu upofu wa Yule mtu..Ukiyatafakari vizuri maneno yake utagundua kuwa mtu Yule hakuwa kipofu tangu alipozaliwa, bali aliupata upofu wake wakati Fulani katika maisha yake. Kwasababu kama angekuwa ni kipofu wa kuzaliwa asingesema naona watu kama miti inakwenda..Mtu aliyezaliwa kipofu hawezi kutofautisha mti na mtu.

Hivyo upofu wake hakuzaliwa nao, aliupata sehemu Fulani, na huko si kwingine zaidi ya kule kijijini alipokuwepo. Na ndio maana utaona Bwana Yesu alimpomaliza kumponya akamwambia..Hata kijijini usiingie.

Hichi ndicho kinachoendelea sasahivi rohoni, ulimwengu huu umewapofusha watu wengi rohoni, masumbufu ya ulimwengu huu, anasa, mambo ya kidunia, hawaoni tena kuwa hizi ni siku za mwisho, hawaoni tena kuwa unyakuo upo karibu, hawaoni tena kuwa dunia hii imeshaoza, haijalishi watasikia injili ngumu kiasi gani bado wataona ni kawaida tu..

2Wakorintho 4:3 “Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea;

4 AMBAO NDANI YAO MUNGU WA DUNIA HII AMEPOFUSHA FIKIRA ZAO WASIOAMINI, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu”.

Lakini kama tunavyosoma hapo, mtu akitaka Yesu amfumbue macho, hakuna njia ya mkato vigezo ni sharti Yesu akuchukue nje ya kijiji..Ni lazima kwanza katika upofu wako ukubali Yesu akutoe katika ulimwengu, ni sharti ukubali kujitenga na anasa, lazima ukubali kuacha fashion na kuvaa mavazi ya kikahaba, ni lazima ukubali kuachana na marafiki wabaya, na mambo yote yasiyompendeza Mungu, yaani kwa ufupi ukubali kuipoteza nafsi yako kwenye mambo ya kidunia, na hapo ndipo Bwana YESU atakapokufumbua macho yako, na kuona mambo yote ya rohoni WAZI WAZI,

Kumwona shetani jinsi anavyofanya kazi katikati ya watu wa ulimwengu huu, kuona jinsi unyakuo ulivyo karibu, kuona jinsi ulivyokuwa hatarini kuelekea kuzimu.. Hapo ndipo utajijua kweli ulikuwa kipofu, lakini sasa hivi upo kwenye ulimwengu huwezi kujiona kwasababu tayari umepofushwa macho.

Ndugu pengine hii ni mara yako ya elfu kulisikia hili Neno kuwa hizi ni siku za mwisho, Hata kama Unyakuo hautakukuta, basi ujue hata siku zako za kuishi hapa duniani si nyingi, hujui kesho utaamkia wapi? Wanaokufa na kushuka kuzimu idadi yao haihesabiki, ukifa leo katika upofu ulio nao, hakuna tumaini tena la uzima baada ya hapo.

Kama wewe ni mkristo na unajua kuwa hili ndio kanisa la mwisho la 7 lijulikanalo kama Laodikia (Ufu.3:14) na kwamba hakutakuwa na kanisa lingine baada ya hili (Ufu.10:7), halafu bado huyathamini maisha yako ya rohoni, hiyo ni dalili kubwa kuwa umepofushwa macho na ulimwengu huu.

Huu ni wakati ambao tayari magugu na ngano vimeshajitenga, wale walio hapo katikati (yaani vuguvugu), upande wao ni wa shetani, kwasababu Bwana Yesu alishasema atawatapika..Ni heri utemwe, kuliko kutapikwa, matapishi hata kuyaangalia huwezi, sembuse kuliwa tena?.Usisibiri utapikwe, Tubu mtafute Bwana Yesu hichi kipindi cha kumalizia.

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

SABATO TATU NI NINI?

Wanaowachukua wanawake wajinga mateka ni akina nani?

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 8 (Kitabu cha Ezekieli)

JE TATIZO LA KULA KUCHA NI ISHARA YA KUWA NA MAPEPO?

MAMBO YATAKAYOTOKEA ISRAELI SIKU ZA HIVI KARIBUNI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

JE UDHAIFU WANGU UNAWEZA KUZUIA INJILI?

Je udhaifu au ulemavu wangu unaweza kuzuia watu kumwamini Yesu?


Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia.

Lipo swali moja muhimu sana linaloulizwa na wengi?..Je kama mimi nina tatizo fulani labla la kuona, au kusikia, au nina ulemavu fulani ambao unaonekana kabisa…Je hali kama hiyo nikienda kuhubiri/kushuhudia watu wataokoka kweli?..Si wataniuliza mbona huyo Mungu hajakuponya wewe kwanza atawezaje kutuponya sisi?.

Hii ni mojawapo ya silaha ya shetani anayoitumia kuhakikisha injili haihubiriwi!…Na silaha nyingine anayoitumia ni sauti inayosema “umemkufuru Roho Mtakatifu”..ukisikia sauti yoyote unakuambia hayo maneno mawili kwamba “huwezi kuhubiri kutokana na udhaifu wako” au “umeshamkufuru Roho Mtakatifu”.. Basi jua moja kwa moja hizo ni sauti za Adui shetani, hivyo zipuuzie!.

Sasa kabla ya kuendelea mbele ni vizuri tukafahamu mambo machache yafuatayo.

Kwanza Aliyepewa jukumu la kuhubiria wanadamu injili, ni Mwanadamu huyo huyo na si malaika. Hakuna mahali popote Mungu amewahi kumtuma malaika akahubiri injili. Na hakuna mwanadamu aliyeumbwa na Mungu asiye na kasoro kabisa!..Hata yule mhubiri maarufu na mashuhuri unayemfahamu na kumsikia anayo mapungufu yasiyohesabika. Kwahiyo Mungu anajua kabisa wanadamu wote wanayo mapungufu lakini akawapa hivyo hivyo jukumu la kubeba maneno yake na kuwasambazia wengine wasiyo nayo. Hivyo angekuwa anaangalia udhaifu kama ndio kigezo cha mtu kwenda kulihubiri neno lake, hakuna mwanadamu angestahili kuwa mhubiri…pengine Mungu angewatumia malaika wake walio watakatifu huko mbinguni na wala si wanadamu. 

Kwahiyo kumbe kasoro zetu hazihusiani na sisi kukidhi vigezo vya kuhubiri Neno la Mungu!..maana yake ni kwamba uwe mrefu, uwe mfupi, uwe unajua kuongea au hujui kuongea vizuri, uwe na kigugumizi,  uwe mzungu, uwe mwafrika, uwe albino, uwe kiziwi, uwe kipofu, uwe huna miguu, uwe huna mikono, uwe maskini, uwe tajiri, uwe hujui kusoma, uwe mtu mdogo kabisa katika jamii, uwe mtu mkubwa.. uwe yoyote yule uwazaye kuwa, maadamu unaitwa MWANADAMU!. Basi umeshafuzu kuwa na uwezo wa kulibeba Neno la Mungu na kuwapelekea wengine. 

Kigezo cha kwanza cha wewe kuweza kuwapelekea wengine NENO la Mungu ni wewe kwanza uwe na hilo Neno la Mungu ndani yako. Hicho ndio kigezo cha kwanza na cha Muhimu, kwasababu hata katika hali ya kawaida, hakuna mwalimu anaweza kumfundisha mwanafunzi maarifa ambayo yeye mwenyewe hana!. Hivyo ni lazima Neno la Kristo likae ndani yako, na hiyo inakuja kwa kumpokea Mwokozi Yesu Kristo na kulisoma Neno lake na KULIISHI HILO NENO!.

Baada ya hapo! Unaweza kuhubiri Injili kwa mtu yeyote yule.. Usisubiri Uone maono, au utokewe na Yesu au Malaika.. Wengi wanaisubiri hii hatua na hawaifikii..Wanatamani wasikie sauti KWANZA ikiwaambia nenda kahubiri!.. “Ndugu usiisubirie hiyo sauti “ hutakaa uisikie milele..Ni kwanini hutakaa uisikie?..Ni kwasababu tayari alishasema katika neno lake… “ENENDENI MKAWAFANYE MATAIFA YOTE KUWA WANAFUNZI..(Mathayo 28:28)”. Usisubiri sauti nyingine..hutaisikia!!

Sasa Swali lingine…Ni nini kinachomgeuza Mtu kama sio Ukamilifu wetu wa kuongea na kusikia vizuri?

Tusome mstari ufuatao kisha tutajua..

Waebrania  4:12  “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. 

13  Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu”

Hapo anasema “NENO LA MUNGU” Sio maneno yaliyopangiliwa vizuri, wala sio midomo yetu inayoweza kuumba maneno mwanana, wala sio rangi za nyuso zetu, wala sio masikio yetu yanayosikia vizuri maneno tunayoulizwa na wale tunaowahubiria, wala macho yetu yanayotazama vyema watu tunaowahubiria wala ufupi wetu, wala urefu wetu, wala elimu yetu…Bali NENO LA MUNGU!..Hilo ndio lenye nguvu…linapotajwa na mwanadamu yeyote ambaye kalishika…basi linapenya mpaka ndani ya ule moyo wa anayelisikia..linamchana chana na kumgawanya moyo wake…linapenya na kumfunulia yule anayelisikia mambo yake ya siri anayoyafanya atoke katika hali yake ya kawaida. Wakati wewe unafikiri anasikiliza kigugumizi chako, au anazitafakari kasoro zako… kumbe mwenzio Roho Mtakatifu anateta naye huko, anaugulia ndani kwa ndani..

2Wakoritho 10:4  “(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) 

5  tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo”

Kwahiyo usikubali kusikiliza uongo wa shetani ambao unakukatisha tamaa kwenda kuhubiri injili..Kama husikii vizuri, wewe hubiri hivyo hivyo, yule unayemhubiria akikuuliza swali sogea karibu msikilize tena na tena, ukiona bado humsikiI, wewe endelea mbele..usianze kuutafakari udhaifu wako…kwasababu hata yeye wakati huo atakuwa hautafakari udhaifu wako!… na pia hatakuchukia ila lile Neno utakalomwambia hata kama ni moja tayari ni Nguvu ya Mungu..na ni mbegu..

Tatizo kubwa la wengi ni kufikiri kwamba Injili ni maneno mengi… jambo ambalo sio kweli!…Mtu anayehubiri maneno mengi basi ni kaongozwa na Roho kufanya hivyo…Lakini Neno moja tu la MUNGU!..Linatosha kubadilisha moyo mgumu wa jiwe na kuwa mlaini.. Kwa neno moja tu la Mungu na iwe Nuru!..ndio iliumba jua hili ambalo mpaka leo tunalo vizazi na vizazi.. Hivyo usitafute sana ujuzi wala utaalamu katika kwenda kulitangaza Neno la Mungu…Wewe Tafuta Roho Mtakatifu. Kisha itumie karama yako Mungu aliyokupa.

Mwanamke mmoja mashuhuri anayeitwa Fanny Crosby alizaliwa akiwa mzima lakini baada ya wiki mbili akawa kipofu, aliishi duniani katika hali hiyo hiyo ya upofu kwa muda wa miaka 95, lakini hakuacha kutafuta mahali ambapo angemtumikia Mungu licha ya kuwa alikuwa kipofu, alifanikiwa kuandika nyimbo zaidi ya 8,000, katika kipindi hicho cha karne ya 19, akajulikana kwa jina la malkia wa nyimbo za injili, na mwimbaji kipofu, moja ya tenzi mbili muhimu ambazo mpaka leo hii unazijua na kuziimba “Usinipite Mwokozi” na “Ndio dhamana Yesu wangu”  pengine ulikuwa hujui ziliimbwa na huyu mama kipofu, na kwa kupitia uimbaji wake, na kuwahubiria wengine alifanikiwa kuwavuta watu wengi kwa Kristo.

Hivyo na sisi, kila mmoja wetu amesimame na kile Mungu alichokiweka ndani yake kuhakikisha injili inawafikia wengi.

Bwana akubariki.

www wingulamshahidi org

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

USINIPITE MWOKOZI Lyrics

REKEBISHA YAFUATAYO ILI MAMBO YAENDE SAWA.

MAPAMBANO DHIDI YA SHETANI.

Mti wa MLOZI alioonyeshwa nabii Yeremia 1:12 tafsiri yake ni nini?

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU

Rudi Nyumbani:

Print this post

WE HAVE A RESPONSIBILITY TO LEAD CAPTIVITY CAPTIVE.

2 Corinthians 10:3-4 Kjv

For though we walk in the flesh, we do not war after the flesh:

(For the weapons of our warfare are not carnal, but mighty through God to the pulling down of strong holds;)

Christian mission to go into all nations and make disciples is likened to the activities of soldiers on a battlefield. The soldiers launch an ambush to attack the Enemy’s camp by surprise; without their knowledge. Having destroyed the whole camp and taken some captive,the soldiers plunder the Enemy’s goods.

Likewise, as we go out to win souls,we are not supposed to make any treaty or agreement with the enemy nor seek counsel with him.All we have to do is to attack the enemy’s camp and lead captivity captive.

Wherever we are,and whatever we are doing ,it is our responsibility to tell others about Jesus.With great courage and intrepidity of mind,get to work.We can’t leave it to chance that someone else will do it for us.For amid the Enemy’s camp are many who are captive.Though sure enough that he will be defeated,the enemy will try to fight back,but we as the soldiers of Christ should stand in the hottest place of the battle and sustain the whole fire of the enemy.

Utilize every available chance in preaching the Good news. If you meet a sick person,pray for them that they may get well.In the same way,when you encounter a demon-possessed person, use the opportunity to rebuke and drive the demons out of them so they may be free.Thereafter,tell them about Jesus.

Let not anything deter you from teaching and preaching the gospel.Factors like age,education,status,fame,way of dressing,among others should not scare you. Don’t compromise on anything, whether the person is your leader,or your teacher, or you’ve just met for first time,preach to them fearlessly. You have been furnished with “weapons mighty through God to pulling down of strongholds.” Remember, there are many whose lives were changed through people who have never been to school. All you need to do is to put on God’s amour and get to work.

The very power by which you were changed is the same that will change others.Until you came to believe and obey the gospel, God used his servant to lead you to liberty,and so you became a slave to righteousness through Christ. He then gave you the grace to serve him in the newness of life.The gift given unto you is a weapon by which you are to win more souls for him.

Ephesians 4: 7-8 Kjv

7 But unto every one of us is given grace according to the measure of the gift of Christ.

8 Wherefore he saith, When he ascended up on high, he led captivity captive, and gave gifts unto men.

All who have accepted Jesus are indebted to him in everything. It is our responsibility to share the gospel with others so they may be changed.We are to actively take the gospel to all people,whether in the villages,schools, hospitals, prisons,within the country or in foreign countries. Don’t hesitate in fulfilling your purpose to make disciples. God has promised to be with you:

Matthew 28:18-20 Kjv

18 And Jesus came and spake unto them, saying, All power is given unto me in heaven and in earth.

19 Go ye therefore, and teach all nations, baptizing them in the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Ghost:

20 Teaching them to observe all things whatsoever I have commanded you: and, lo, I am with you always, even unto the end of the world. Amen.

God is faithful and as he has promised in his Word,so it shall be.He will be with you until the end of times.But this will only be if we will go into all nations and make them disciples of the Lord.May the Lord of all power and grace help us to trust him.

Our motive should not be on gaining fame or getting money,but to pass along to others the kindnesses shown to us.We are to be faithful in our mission,knowing that we have a reward kept for us in heaven. Seek God’s erring children lone and lost,and help lead them to the place of safety.Christ is coming soon(quickly).

Revelation 22:12-13 Kjv

12 And, behold, I come quickly; and my reward is with me, to give every man according as his work shall be.

13 I am Alpha and Omega, the beginning and the end, the first and the last.

God bless you.

Related articles:

STRIVE TO BE AT PEACE WITH ALL MEN.

JACHIN AND BOAZ

What does it mean “in the abundance of wisdom there is the abundance of sorrows”.

LEARN GOD’S COMMITMENT AND HOSPITALITY.

Home:

Print this post