Title September 2020

JE KUPOKEA CHANJO NI DHAMBI?

Kupokea chanjo ni dhambi kibiblia?

Chanjo ni “ugonjwa dhaifu” unaoingizwa ndani ya mwili wa mtu, ambao mwili una uwezo wa kuudhibiti, na hivyo kuuachia mwili kumbukumbu ya ugonjwa huo pindi utakapokuja tena katika ukamilifu wote siku za mbeleni.

Ili kuelewa zaidi tafakari mfano huu “Mfanya biashara mmoja aliyefanikiwa katika biashara zake, alikuwa akihifadhi fedha zake nyumbani, na nyumba yake hiyo haukuwa na uzio zaidi ya mlango wake mmoja tu wa kuingilia ndani. Siku moja wahalifu walimvamia usiku na kujaribu kuvunja mlango wake, lakini kutokana na kwamba mlango wake ule ulikuwa imara sana na wahalifu wale hawakuwa na zana za kutosha walishindwa kuuvunja mlango ule, wakaondoka…hivyo tukio lile lilimtafakarisha sana yule mfanya biashara, na hivyo akatafuta suluhisho ili tukio kama lile lisijirudie tena, kwamba wasije wahalifu wengine wenye nguvu kuliko wale wa kwanza na kufanikiwa kuvunja mlango na kumwibia na kumdhuru, hivyo kulizuia hilo, kulipopambazuka aliita mafundi wakatengeneza uzio mkubwa kuizunguka nyumba yake yote, na pamoja na hayo akaweka na mlinzi getini pamoja na mbwa”.

Sasa ukilitafakari tukio hilo utagundua kwamba…kwa lile tukio la kwanza lililomtokea la wezi wasio na nguvu za kutosha kujaribu kuvunja mlango wake ni kama limemfungua akili mfanya biashara yule na kugundua kuwa kumbe yupo katika hatari na hivyo anapaswa kujilinda zaidi.

Sasa katika ulimwengu wa sayansi ya tiba, hao wezi dhaifu ndio  wanafananishwa na “chanjo” wanapowekwa ndani ya mwili, lengo ni kuupa mwili taarifa za hatari iliyopo na hivyo kujitengenezea kinga madhubuti kwa hatari itakayokuja kutokea mbeleni iliyo mfano wa hiyo.

Kwahiyo matabibu (madaktari) wakati mtoto anapozaliwa, ili kumnusuru wanamweka mtoto chanjo hizo mbalimbali za magonjwa tofauti tofauti..lengo ni ili ule mwili wa mtoto upate taarifa na ujitengenezee kinga mapema kabla huo ugonjwa haujaja kwa nguvu siku za mbeleni. Sasa hilo ndio lengo la kwanza la Chanjo. Na kwa lengo hilo basi sio dhambi kumpa mtoto chanjo, au mtu kupokea chanjo.

Lakini pia sio lazima, kwasababu viwango vya Imani vinatofuatiana. Wapo wengine waliopewa neema ya kumwamini Mungu, na hivyo huweza kuishi bila hivyo vitu, na wasipatikane na madhara yoyote. Hao ni wachache, na wanafanya vizuri zaidi. Lakini pia sio wote wenye imani hiyo, kwahiyo nao pia sio dhambi wakipokea chanjo.

Warumi 14: 1  “Yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, walakini msimhukumu mawazo yake.

2  Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula mboga.

3  Yeye alaye asimdharau huyo asiyekula, wala yeye asiyekula asimhukumu huyo alaye; kwa maana Mungu amemkubali”.

Hivyo sio dhambi kupokea chanjo!.Na hata kama unayo Imani ya kutokupokea hiyo, hupaswi kuwafanyia hivyo watoto wako, wala kuwahukumu wale wanaopokea…Ni vizuri ukawapeleka watoto wako kwenye chanjo, wewe baki na imani yako..watakapokuwa watu wazima watachagua..

Pia kuna jambo la kuzingatia. Sio kila chanjo ni lazima kupokea au kumpa mwanao, Zipo chanjo za msingi kabisa, ambazo zinajulikana katika mahospitalini, ambazo ni chache sana. Chanjo chache ni vizuri zaidi kwasababu anayetupa afya ni Mungu, na si wanadamu, KİLA KİTU TUNAPASWA TUKİFANYE KWA KİASİ. Na si kuweka tegemeo letu huko asilimia 100, kwamba ndio uhai wetu na ulinzi wetu upo huko. Tukiweka mategemeo yetu huko asilimia 100, hiyo ni dalili tosha kwamba hatuna Imani kwa Mungu hata kidogo. Jambo ambalo ni dhambi na linamtia Mungu wetu wivu na huzuni kwasababu hizo ni sawa na ibada za sanamu.

Hivyo kwa hitimisho: Kupokea Chanjo sio dhambi, wala kumpa mwanao chanjo sio dhambi…Wala kuipa mifugo yako chanjo sio dhambi. Isipokuwa inapaswa itumike kwa kiasi, kwa mimi nionavyo chanjo 3 zinatosha zikizidi sana 4. Mengine tumwamini Mungu atupaye afya na uzima, na atuponyaye. (Zaburi 107:20).

Na chanjo tunayoizungumzia hapa ni ile ya HOSPITALINI na si ya kwa waganga wa kienyeji. Chanjo za waganga wa kienyeji ambazo zinahusisha “kuchanjwa chale” ni za kishirikina, ambazo ni machukizo makubwa kwa Mungu wetu, hizo zinahusiana na ibada za sanamu na Mungu kazikataza..(Soma Walawi 19:28)

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Je Kutoa Mimba ni dhambi?

Naomba kujua nini maana ya kuteguka uvungu wa paja?

Mkatale ni nini katika biblia? (Matendo 16:24)

NJIA MOJAWAPO YA KUPATA MSAADA KUTOKA KWA MUNGU.

NAYE HERI AWAYE YOTE ASIYECHUKIZWA NAMI.

Jabari ni nini, kama linavyotumika kwenye biblia?

Rudi Nyumbani:

Print this post

ULIMWENGU WA ROHO UPO NA UNA MADHARA KATIKA MAISHA YETU! 

Shalom, karibu tujifunze Biblia.

Katika kitabu cha Mwanzo tunasoma kuhusu uumbaji..Tunasoma Mungu alimwumba Mtu kutoka katika mavumbi ya nchi, lakini Zaidi ya hayo tunaona aliumba na vitu vingine vinavyoonekana kama miti, Wanyama, samaki n.k.

Sasa kama umekisoma vizuri kitabu hicho utagundua kuwa vimetajwa tu vitu na viumbe vinavyoonekana kwa macho, lakini vile visivyoonekana kwa macho havijatajwa. Kwamfano hutaona viumbe kama bakteria wametajwa hapo katika uumbaji..ingawa ni wengi kuliko idadi ya  viumbe vyote vinavyoonekana kwa macho, na tena kuna aina nyingi za bakteria na virusi, hutaona pia Mungu kazitaja chembe chembe hai za damu zilizopo ndani ya mwili wa Adamu zinazoishi ndani yake na kumlinda dhidi ya maadui wa mwili wake..hali kadhalika utaona Mungu kataja mavumbi katika kitabu cha mwanzo…lakini hajataja elementi nyingine zilizo ndogo sana na nyingi kuliko mavumbi yote ya dunia na mchanga zinazoitwa protoni na elektoni, zilizopo ndani ya huo mchanga na ndani ya kila kitu.

Kwahiyo hiyo ina maana kuwa Uumbaji wa Mungu sio tu huu wa vitu tunavyoviona kwa macho, bali pia kuna vitu na viumbe vingine vingi visivyoonekana kwa macho ambavyo Mungu kaviumba pia vinavyoishi katikati yetu..Hii tunayoiona ni kama tu “summary” ya vitu vilivyoumbwa.

Na kama umegundua matatizo mengi na mafanikio mengi yanatokana na hivi vitu tusivyoviona…Kwamfano matatizo ya magonjwa yote ni kutokana na hawa bakteria au virusi. Hawaonekani lakini wanaweza kusababisha madhara makubwa, hata kifo, virusi vya korona havionekani kwa macho lakini leo hii vinausumbua ulimwengu.

Vivyo hivyo mafanikio mengi  yanatokana na vitu visivyoonekana..kwamfano unaweza kushangaa inawezekanikaje kioo chenye waya waya tu kinaweza kuonyesha sura ya mtu na matukio yake..(kumbe ukifuatilia nyuma yake ni hivyo vitu vidogo sana visivyoonekana protoni na elecroni vinatumika), na umeme ni hivyo hivyo, unajiuliza ule waya mwembamba vile unawezaje kupitisha nguvu kubwa vile ya kuwezesha mashine kusukuma vyuma Na hata kusaga nafaka na kuzifanya unga, au unawezaje kupitisha moto mwingi kiasi kile cha kuchemsha maji kwa dakika tano na yakatokota kabisa. Kumbe nguvu ile inatokana na sayansi ya vitu visivyoonekana (protoni na electroni).

Kwa mantiki hiyo basi, hakuna sababu za kusema kwamba shetani hayupo kwasababu tu hatumwoni, au hakuna sababu ya kusema kwamba mapepo hayapo kwasababu hatuyaoni kwa macho, wala hatuna sababu za kusema kwamba Malaika hawapo..kwasababu tu hatuwaoni. 

Matukio mengi yanayoendelea sasa duniani, yanaanzia rohoni. Hata hii dunia tu yenyewe imeumbwa kutoka katika vitu visivyoonekana..kasome Waebrania 11:3.

Kwahiyo vitu vile visivyoonekana ndio vya kuvizingatia Zaidi kuliko vile vinavyoonekana. 

2Wakorintho 4:18  “tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele”.

Na pia vipo vitu vingine ambavyo hata kwa kutumia hizo hadubini havionekani lakini vipo..na tunaamini kuwa vipo..Kwamfano Ile “nguvu ya uvutano ya sumaki” haionekani kwa njia yoyote ile. Mpaka leo hakuna mtu wala mwanasayansi aliyegundua kifaa cha kuiona..Imebakia fumbo mpaka leo.

Vivyo hivyo ndugu, ulimwengu wa roho upo, huo hauonekani kwa macho, vipo viumbe vya rohoni pia navyo havionekani kwa macho, lakini madhara yake ni makubwa katika Maisha yetu.

Kama unakiogopa kirusi cha ukimwi usichokiona kisiingie mwilini mwako kwa kujitenga na uasherati.. Basi kuna viumbe vingine vibaya kuliko hivyo virusi ambavyo vinaweza kuingia mwilini mwako kwa njia hiyo hiyo ya uasherati,(mapepo) vitakavyokuletea madhara kwenye Maisha yako moja kwa moja. Pepo mmoja tu anayeweza kuingia katika Maisha yako kwa njia ya tendo moja tu la uasherati na ana uwezo wa kukuharibia Maisha yako moja kwa moja.

Kama unaogopa kupigwa shoti usiyoiona kwa kushika nyaya za umeme bila uangalifu, basi iogope dhambi kwasababu vipo vitu katika ulimwengu wa roho vibaya kuliko kuliko umeme.. ambavyo havionekani, vyenye uwezo wa kukusababishia hata kupoteza Maisha yako ghafla utakapovisogelea tu.

Biblia ndio “hadubini yetu”. Unaposoma Neno ni rahisi kuzigundua roho hizi na jinsi zinavyotenda kazi..na namna ya kujihadhari nazo. Kwamfano biblia inasema katika Mithali…

Mithali 6:32 “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake”

Hivyo mtu akilijua hili Neno na akaenda kinyume nalo, anakuwa amefungua mlango wa mapepo kuingia katika Maisha yake.. hataona kwa macho, lakini baada ya kipindi Fulani kupita ndipo atakapoona madhara yake. Madhara ya uasherati wengi wanafikiri ni yale ya kupata HIV tu basi!.. lakini hawajui kuwa mtu anaweza kutoka kufanya usherati leo na akaanguka ghafla tu na kupoteza Maisha, au akafa tu ghafla kifo kisichoeleweka, au akapata ajali au akapoteza tu ghafla kitu cha muhimu katika Maisha yake kama kazi, au heshima. 

Bwana atusaidie kuyajua Zaidi mambo ya rohoni kuliko ya mwilini, na kutupa Imani Zaidi.. Nasema hivyo kwasababu siku chache tu nyuma nimekutana na pepo, kwa macho haya ya mwilini barabarani, ndipo Mungu akanipa somo kuwa hizi roho zinazurura huku duniani kutafuta watu kwa nguvu  kuwaangamiza, na yanaongeza bidii siku hizi za mwisho kwasababu yanajua muda wao ni mchache, hivyo wanawinda watu kwa nguvu, ili kuwaangamiza.

Hivyo kuwa makini sana. Mambo rohoni sio kama unavyoyasikia. Ingia ndani ya Kristo uwe salama.

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

KITABU CHA UZIMA

MAFUNDISHO YA MASHETANI

MIHURI SABA

MTUMAINIE YESU ASIYEISHA MATUKIO.

UFUNUO: Mlango wa 6

Rudi Nyumbani:

Print this post

Mavyaa ni nani kibiblia?(Mika 7:6)

Mavyaa ni nani?


Neno hilo tunalipata katika mstari huu kwenye biblia;.

Mika 7:6 “Kwa maana mwana humwaibisha babaye, na binti huondoka ashindane na mamaye; na mwanamke aliyeolewa hushindana na MAVYAAYE; adui za mtu ni watu wa nyumbani mwake mwenyewe.

7 Lakini mimi, nitamtazamia Bwana; nitamngojea Mungu wa wokovu wangu; Mungu wangu atanisikia”.

Mavyaa ni Neno la kiswahili linalomaanisha mama-mkwe, – Yaani mama wa mke/mume wako.

Na kwa upande wa Baba-mkwe ni hivyo hivyo linabadilika na kuwa Bavyaa– Yaani baba wa mke/mume wako.

Hivyo kwenye mstari huo, tunapewa picha ya jinsi audui unavyoanza…Kwamba hauanzii mbali, labda kwa watu wasiotujua hapana, bali uadui wa kwanza sikuzote huanzia kwa watu nyumbani mwetu wenyewe, Lakini uadui hauji hivi hivi bali ni lazima uwe na sababu yake. Na ndio maana mstari ambao Bwana Yesu aliurejea alipokuwa anazungumzia habari za mtu kujikana nafsi yake pale anapotaka  kumfuata yeye, ulikuwa ni huu, na alisema maneno haya:

Mathayo 10:34 “Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.

35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;

36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.

37 Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.

38 Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili.

39 Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona”.

Hivyo, katika wewe safari yako ya imani, (yaani umeokoka), ni lazima uweke akilini kuwa adui za kwanza kukupinga watakuwa ni watu wa nyumbani mwako, aidha watoto wako, au binti zako, au  mavyaako, au bavyaako, au kaka zako, au wajomba zako au binamu zako n.k. Usitazamie vita vikubwa kutokea mbali.

Kwasababu adui za mtu ni watu wa nyumbani mwake mwenyewe. Hivyo ukikutana nayo ushingae, songa mbele, ishinde vita, Na Bwana atakuwa pamoja na wewe.

Tazama tafsiri ya maneno mengine ya biblia chini.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Mkatale ni nini katika biblia? (Matendo 16:24)

Daawa ni nini kama tunavyosoma katika biblia?

Jabari ni nini, kama linavyotumika kwenye biblia?

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

UTAWALA WA MIAKA 1000.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Mkatale ni nini katika biblia? (Matendo 16:24)

Mkatale ni nini?


Mkatale ni pingu ya kufungia mtu, inaweza ikawa ya chuma, au mbao nene. Na huwa inafungwa sana sana miguuni, lakini pia shingoni au mikononi,.. Tazama picha juu.

Vifungu vinavyolitaja Neno hilo katika biblia ni kama vifuatavyo;

Matendo 16:24 “Naye akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga MIGUU KWA MKATALE.

25 Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.

26 Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa”.

 

Ayubu 13:25 “Je! Utalitaabisha jani lipeperushwalo? Au, je! Utayafuatia hayo mabua makavu?

26 Kwani umeandika maneno ya uchungu juu yangu, Na kunirithisha maovu ya ujana wangu;

27 Waitia MIGUU YANGU KATIKA MKATALE, na kuyaaua mapito yangu yote; Wajiandikia alama kuzizunguka nyayo za miguu yangu”;

 

Yeremia 20:2 “Ndipo Pashuri akampiga Yeremia, nabii, AKAMTIA KATIKA MKATALE, uliokuwa pale penye lango la juu la Benyamini, lililokuwa katika nyumba ya Bwana. 3 Hata ikawa, asubuhi, Pashuri huyo akamtoa Yeremia katika MKATALE. Ndipo Yeremia akamwambia, Bwana hakukuita jina lako Pashuri, bali Magor-misabibu”.

Soma pia  Ayubu 33:11, 2Nyakati 16:10, Yeremia 29:26.


 

mkatale ni nini

Hata sasa shetani anawatia watu katika mikatale yake ya mauti. Lakini Yesu Kristo peke yake ndiye anayeweza kuwatoa humo.  Swali ni Je! Mimi na wewe Yesu ameshatuweka huru?.  Kumbuka hakuna uhuru wowote nje ya Kristo, haijalishi unajiona upo salama kiasi gani, wewe bado upo kwenye mikatale mibaya ya shetani. Na lengo lake ni ufe katika hali hiyo uishie kuzimu.

Hivyo kama hujaokoka, mgeukie Kristo mapema ayaokoe maisha yako, ndani ya hichi kipindi kifupi tulichobakiwa nacho hapa duniani.

Zaburi 107:13 “Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao.

14 Aliwatoa katika giza na uvuli wa mauti, Akayavunja mafungo yao.

15 Na wamshukuru Bwana kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu.

16 Maana AMEIVUNJA MILANGO YA SHABA, AMEYAKATA MAPINGO YA CHUMA”.

Bwana akubariki.

Tazama ufananuzi wa maneno mengine chini.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Jabari ni nini, kama linavyotumika kwenye biblia?

KAMA MMOJA TU NDIO HIVI! SI ZAIDI 153?

KILA MMOJA WENU AJUE KUUWEZA MWILI WAKE.

Nyamafu ni nini?

MKUU WA UZIMA AKUWEKE HURU.

 

Rudi Nyumbani:

Print this post

KWANINI LEO HII KUNA KUNDI KUBWA LA WAKRISTO WALIORUDI NYUMA?

Shalom. Karibu tujifunze Neno la Mungu, maadamu ule mwisho unakaribia..

Kila siku tunapaswa tukumbuke kuwa wokovu ni tunu ya thamani ambayo tunapaswa tuishikilie kwa gharama zozote, wokovu kuupata ni rahisi sana, lakini kuushikilia mpaka mwisho si kitu kirahisi, kwasababu kuna ufalme mwingine (wa giza) hapa duniani ambao upo mahususi kwa kazi hiyo moja tu ya kuhakikisha watu wanaupoteza wokovu hata kama walikuwa wameshaupata.

Na ndio hapa wahubiri tunapaswa tusisitize kwa watu, Kwasababu ndivyo walivyofanya hata na mitume (baba zetu wa imani), ukiangalia utaona mafundisho yao yote yalikuwa ni ya kutilia msisitizo  suala la kuishindiania imani, wakatuambia TUISHINDANIE imani ambayo tumekabidhiwa sisi watakatifu mara moja tu.

Yuda 1:3 “Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu”.

Sio kwamba walikuwa hawaoni fursa za kibiashara zilizokuwa zimewazunguka mitaani mwao, walikuwa wanaziona, pengine hata zaidi ya sisi, lakini hawakuona sababu ya kutuandikia kwenye hichi kitabu kinachoitwa biblia, kwasababu walijua  vita hasaa vipo wapi, mapambano hasa ya mwanadamu duniani yapo wapi..

Tukumbuke kuwa tukibadilishwa maisha yetu, na kufanywa kuwa viumbe vipya, mambo hayatabakia kuwa vilevile kama yalivyokuwa mwanzoni.. Shetani ni lazima aamke na kuanza kuuwinda wokovu wako kwa gharama zozote zile.. atakuchukia kwa ukomo wa chuzi pale tu atakapokuona unaanza kupiga hatua katika wokovu wako, na sio katika mafanikio ya biashara yako, shida yake kubwa ni Imani yako.

Na katika kipindi ambacho unapaswa ujiandae kukutana naye uso kwa uso basi ni wakati ambapo umeanza maisha mapya ya wokovu.

Lakini kama usipoliweka hilo akilini, ukaambiwa ukiokoka basi, wewe ni wa mbinguni moja kwa moja, njoo sasa tukufundishe mambo mengine ya kidunia..Nataka nikuambie maisha yako ya rohoni yapo hatarini sana kugeuka.(Ndio maana kuna kundi kubwa la wakristo waliorudi nyuma leo hii).

Kwasababu shetani ni lazima atahakikisha analeta mambo mawili kwako, la kwanza ni DHIKI, na la pili ni UDHIA.

Mathayo 13:20 “Naye aliyepandwa penye miamba, huyo ndiye alisikiaye lile neno, akalipokea mara kwa furaha;

21 lakini hana mizizi ndani yake, bali hudumu kwa muda; ikitukia dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara huchukizwa”.

Dhiki, ni mateso unayoyapata kutokana na kile ulichokiamini; Na udhia ni maudhi utakayoyapata kutoka kwa watu, kwa kile unachokiamini, huu ndio wakati ambapo pengine hata ndugu/familia hawatakuelewa au watakutenga, ni wakati ambapo pengine utajikuta unapingwa na viongozi wako wa dini, au wanakupiga na kukufunga kisa tu umemfuata Yesu, au umekuwa na msimamo Fulani wa Neno la Mungu, ni wakati ambapo mambo yako yanaweza yasiende sawa, utapitia kuvunjwa moyo mara kadhaa, lakini Mungu atakuwa pamoja na wewe,  kumbuka yote hayo yanasababishwa na shetani, ili tu kukutikisha urudi ulipotoka. Yanatokea kwa ruhusa maalumu kutoka kwa Mungu.

Lakini ni ya muda tu, hayawezi kudumu milele, Mungu hawezi kuruhusu yadumu milele. Kuna kipindi kitafika yataisha. Lakini ni wachache sana wanaoweza kuvumilia hata hicho kipindi kiishe..

Na hapa ndipo watu wengi wanaporudi nyuma. Na kuuacha wokovu. Kwasababu hawakujiandaa kwa huo wakati.

Kumbuka kuwa tutaufikia mwisho mzuri wa imani, kwa kuishindania kwa gharama zozote na  kwa kuvumilia..hilo tu.

Luka 8:15 “Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia”.

Bwana atusaidie tuweze kuyashinda hayo yote.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Je kupiga miayo ni ishara ya mapepo?

MUNGU HANA MBARAKA MMOJA TU!..MWAMINI.

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1

Daawa ni nini kama tunavyosoma katika biblia?

FUNGUO ZA UZIMA, MAUTI NA KUZIMU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Kamsa ni nini kwenye biblia? (Sefania 1:16, Wimbo 3:8)

Kamsa ni nini?


Kamsa ni Ukelele wa habari ya moto au vita (kwa lugha ya kiingereza-Battle cries)

Vifungu hivyo vinaeleza Neno hilo;

Wimbo 3:8 “Wote wameshika upanga, Wamehitimu kupigana; Kila mtu anao upanga wake pajani Kwa hofu ya KAMSA ZA USIKU”.

 

Sefania 1:15 “Siku ile ni siku ya ghadhabu, Siku ya fadhaa na dhiki, Siku ya uharibifu na ukiwa, Siku ya giza na utusitusi, Siku ya mawingu na giza kuu,

16 Siku ya tarumbeta NA YA KAMSA, Juu ya miji yenye maboma, Juu ya buruji zilizo ndefu sana.

17 Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda Bwana dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi.

18 Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya Bwana; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha”.

Unaona? Ile siku kuu ya Bwana imefananishwa na ya kama kelele za vita..ambazo huwa zinatokea ghafla..Mfano tu wa Wana wa Israeli walivyozizunguka zile kuta za Yeriko kwa muda wa siku 7 na siku hiyo hiyo ya saba, wakapiga kelele kubwa sana (Kamsa) kuashiria kuwa vita vimeanza..

Na baada ya kilele kutoka, zile kuta za Yeriko zilizama chini saa ile ile, na biblia inatuambia mioyo ya watu wa Yeriko ikayeyuka (Yoshua 5:1) wakaishiwa nguvu kabisa.

Yoshua 6:20 “Basi watu wakapiga kelele, na makuhani wakazipiga tarumbeta; hata ikawa, hapo watu waliposikia sauti ya tarumbeta hao watu wakapiga kelele kwa sauti kuu sana, na ule ukuta wa mji ukaanguka nchi kabisa, hata watu wakapanda juu, wakaingia katika mji, kila mtu akiendelea kukabili mbele; wakautwaa huo mji.

21 Basi wakaangamiza kabisa vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mji, wanaume na wanawake, watoto na wazee, na ng’ombe, na kondoo, na punda, kwa makali ya upanga”.


Ndivyo itakavyokuwa katika siku ule ya Mwisho Kristo atakapotokea mawinguni na malaika zake watakatifu.. Tarumbeta na Kamsa italia kutoka mbinguni, kuashiria kuwa mwisho wa kila mwenyewe dhambi umefika..

Siku hiyo kila jicho litamwona, na mataifa yote wataomboleza kwa kilio kisichoweza kuelezeka, lakini hiyo  haitasaidia, waovu wote watakuwa kama mizoga juu ya dunia nzima. Ndugu tusitamani tuwepo katika hicho kipindi kibaya sana.

Soma Ufunuo sura ya 19 na 20 yote uone jinsi waovu watakavyoangamizwa na Bwana mwenyewe siku hiyo ikifika.

Swali ni Je! Na wewe unataka uwepo huo wakati? Mimi sitaki, Kumbuka mpaka hayo yote yatokee unyakuo utakuwa umeshapita. Watakaoshuhudia hayo ni wale wote ambao hawakwenda katika unyakuo, watakaopokea chapa ya mnyama.

Ili kufahamu kwa marefu juu ya kalenda  ya matukio yote ya siku za mwisho, angalia vichwa vya masomo mengine chini.

Hivyo tubu dhambi zako kama bado wewe ni mwenye dhambi, hizi ni siku za mwisho kweli kweli , siku za Kamsa za Mungu  mwenyezi.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

SIKU YA HASIRA YA BWANA.

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Rudi Nyumbani:

Print this post

Juya ni nini kwenye biblia? (Mathayo 13:47)

Juya maana yake ni jarife, au wavu wa kuvulia samaki.

Habari hiyo inapatikana kwenye vifungu hivi vya maandiko;

Habakuki 1:13 “Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama ukaidi, mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu ammezapo mtu aliye mwenye haki kuliko yeye;

14 na kufanya wanadamu kuwa kama samaki wa baharini, kama vitu vitambaavyo, ambavyo havina mtawala?

15 Yeye huwatoa wote kwa ndoana yake, huwakamata katika wavu wake, na kuwakusanya katika JUYA lake; ndiyo sababu afurahi na kupendezwa.

16 Kwa sababu hiyo huutolea wavu wake sadaka, na kulifukizia uvumba JUYA lake; kwa sababu kwa vitu vile fungu lake limenona, na chakula chake kimekuwa tele.

17 Je! Atawatoa walio katika wavu wake, asiache kuwaua watu wa mataifa daima”?

Na katika agano jipya Bwana Yesu aliutumia pia mfano wa Juya la mvuvi kufananisha na jinsi mwisho wa dunia utakavyokuwa.

Mathayo 13:47 “Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna;

48 hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa.

49 Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki,

50 na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.

Lakini ni ujumbe gani mkubwa tunaupata kwenye mfano wa  Juya?

Hapo katika mfano wa Yesu tunaona walivuliwa samaki wa aina zote na kupelekwa nje kabisa ya pwani, ikiashiria kuwa wanadamu wote watavunwa ile siku ya mwisho, wawe ni watakatifu wawe ni waovu wote watavunwa, maana yake ni kuwa kila mmoja wetu atahusika, tutatolewa kwenye huu ulimwengu wa sasa, na hapo ndipo walio wema wataenda mbinguni kwa Mungu na wale walio waovu watatupwa katika ziwa la moto.

Na kibaya zaidi siku zenyewe ndio hizi tuishizo. Wakati wowote paraparanda italia, na mwisho utafika, Je bado upo vuguvugu, bado unautumaini ulimwenguni usiodumu milele?.

Kama wewe ni mwenyewe dhambi na unataka leo Yesu ayaokoe maisha yako. Ili ikitokea hata mwisho umefika leo, uwekwe kapuni mwa Bwana, basi uamuzi huo ni mzuri sana. Kumbuka biblia inasema saa ya wokovu ni sasa, Na wakati uliokubalika ni huu.

Kama ni hivyo fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba na Mungu akubariki  >>>> SALA YA TOBA

Tazama pia maneno mengine ya biblia chini.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

LAKINI USIKU WA MANANE, PAKAWA NA KELELE.

UMEFUMBULIWA MACHO YAKO YA KIROHO?

UNYAKUO.

https://wingulamashahidi.org/ikabodi-maana-yake-ni-nini/

Biblia inamaanisha nini inaposema “Tusitweze unabii”?

Rudi Nyumbani:

Print this post

SIKU ZA WATUMISHI WA MUNGU.

Luka 17:26  “Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu. 

27  Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote.

28  Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga; 

29  lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote”.

Jina la Bwana wetu Yesu libarikiwe. 

Unabii huo ulitolewa na Bwana wetu Yesu mwenyewe kupitia kinywa chake, haukutolewa kwa kutumia kinywa cha  Mtume Paulo, au Yohana, au Petro au hata Luka mwenyewe aliyekiandika hichi kitabu, bali ni Bwana mwenyewe ndiye aliyeutoa…akilelezea jinsi ujio wake unavyofananishwa.

Katika unabii huo aliufananisha na siku za Nuhu pamoja na za Lutu. Sasa pamoja na mengi aliyoyafananisha kwamba watu watakuwa wakioa na kuolewa (ndoa za jinsia moja), watu watakuwa wakila na kunywa (karamu za ulafi pamoja na ulevi)kama nyakati za Nuhu, pia katika siku za ujio wake watu watakuwa wakiuza na kununua (biashara haramu na za magendo) kama ilivyokuwa nyakati za Lutu

Lakini pamoja na hayo yote ambayo mengi ya hayo yameshatimia..kuna vipengele viwili ningependa tuvione katika mistari hiyo, ambavyo ukiisoma kwa haraka haraka ni rahisi kuvipita tu. Na vipengele hivyo ni 1) KAMA ZILIVYOKUWA SIKU ZA NUHU na 2) KAMA ZILIVYOKUWA SIKU ZA LUTU

Katika vipengele hivyo hakusema “kama zilivyokuwa siku za gharika, au kama zilivyokuwa siku za maangamizi ya moto ya Sodoma na Gomora”..Bali utaona anatumia siku za Nuhu na siku za Lutu…

Sasa Nuhu na Lutu walikuwa ni watumishi wa Mungu.. Kwasababu walionywa na Mungu juu ya maangamizi yanayokuja mbeleni na pia wakapewa nafasi ya kwenda kuwahubiria wengine.

Lutu kabla ya kutolewa Sodoma, alihubiriwa na wale malaika wawili mambo yatakayokwenda kutokea kipindi kifupi mbele na akapewa nafasi ya kwenda kuwahubiria wakwe zake, na ndugu zake pia, ikiwemo mke wake, wanawe wawili na ndugu zake.. Waliokubali ni mke wake pamoja na wanawe wawili, wengine walimwona kama kikaragosi tu kinacholeta habari za mababu.

Mwanzo 19:12 “Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je! Unaye mtu hapa zaidi? Mkwe, wanao, na binti zako, na wo wote ulio nao katika mji, uwatoe katika mahali hapa; 

 13 maana tutapaharibu sisi mahali hapa, kwa kuwa kilio chake kimezidi mbele za Bwana; naye Bwana ametupeleka tupaharibu. 

 14 Lutu akatoka akasema na wakweze, waliowaposa binti zake, akasema, Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu Bwana atauharibu mji huu. Lakini akawa kama achezaye machoni pa wakweze”

Vivyo hivyo Nuhu kabla ya kuingia safinani alihubiriwa na Mungu juu ya hukumu itakayokwenda kutokea kipindi kifupi mbele, na pia akapewa nafasi ya kwenda kuwahubiria ndugu zake, lakini waliokubali kuambatana naye ni mke wake na wanawe watatu, pamoja na wake za wanawe, jumla watu 8 tu..wengine wote walimwona kama fundi mbao aliyerukwa na akili.

Hivyo utaona hapa Bwana Yesu anazitaja kama siku ni ZAO.. Na anazifananisha na siku za ujio wake.. Maana yake ni kwamba siku za ujio wake, atawanyanyua watumishi wake mfano wa Nuhu na Lutu kuonya ulimwengu juu ya hukumu ijayo.

Ndugu..hukumu ipo!.. Wakina Nuhu wapo wengi leo, katika kila Taifa na mkoa..(Watumishi wote wanaouonya ulimwengu juu ya siku za mwisho ni wakina Nuhu na Lutu), na hizi ndizo siku zao… “zinaitwa Siku za Hao watumishi” na sio “siku za kuangamizwa dunia”..Lutu alionekana anacheza mbele za wakwe zake.

Kibaya zaidi ni kwamba, watu wengi watakaokuwa wanasikia habari hizo wataoana kama wanacheza tu nao pia, wanapiga ngonjera, wamekosa kazi ya kufanya,.Lakini mwisho utakapowakuta kwa ghafla ndipo watakajuta majuto yasiyoelezeka…

Ukiona unasikia habari za mwisho wa dunia kwa nguvu, jua ndio injili ya kumalizia hiyo, baada ya hapo ni hukumu. Hizi ni siku za mwisho, siku za Watumishi wa Mungu..Na zitaisha!

Je umempokea Kristo? Kwa kutubu na kubatizwa?.. kama bado unasubiri nini?.. Yesu yu karibu kurudi, hivi karibuni hutasikia tena ukiombwa uingie ndani ya safina, hutasikia tena sauti ya Roho Mtakatifu ikikushawishi kutubu..kutakuwa na ukimya nje na ndani, mlango wa Neema utakuwa umeshafungwa, kitakachobakia ni hukumu..

Watu wa kipindi cha Nuhu walisubiri Mungu azungumze nao pengine kwa kutumia jua ndipo waamini, hivyo wakaishia kumdharau Nuhu, vivyo hivyo wa kipindi cha Lutu. Wakati huu ambao watu wanaidharau injili ya kurudi kwa Kristo, hatupaswi kufanana na  wao hata kidogo.

Hivyo ndugu mpokee Kristo leo kama hujafanya hivyo, kisha nenda katafute ubatizo sahihi wa maji mengi (Yohana 3:23) na kwa Jina la YESU, ambalo ndio jina la Baba, mwana na Roho Mtakatifu (Matendo 2:38, Mathayo 28:19), na kuanzia wakati huo Roho Mtakatifu ataingia ndani yako na kukuongoza na kukutia katika kweli yote ya maandiko.. Na utaiepuka hukumu ambayo ipo karibuni kuujilia ulimwengu wote.

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

WANA WA MUNGU, NA BINTI ZA WANADAMU.

SIKU ZA MWISHO WA DUNIA.

Naomba kujua watakaoenda mbinguni je! ni wengi au wachache?

KUTAKUWA NA MATETEMEKO YA NCHI, NJAA NA TAUNI.

JINSI DHAMBI INAVYOMGHARIMU MTU SANA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Daawa ni nini kama tunavyosoma katika biblia?

Daawa ni madai, au mashitaka, malalamiko, au hukumu.

Kwamfano pale mwenzako anapokukosea, au amekudhulumu, au amekutukana au amekufanyia jambo baya, na unataka kwenda kumshitaki , sasa hilo shitaka au madai ndio kwa jina lingine linaitwa  Daawa.

1Wakorintho 6:1 “Je! Mtu wa kwenu akiwa ana daawa juu ya mwenzake athubutu kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya watakatifu?

2 Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo?

3 Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya”?

Unaona, biblia inatushauri sisi kama watakatifu tukiwa na daawa/shitaka juu ya ndugu zetu wa kikristo, hatupaswi kuyapeleka kwa watu wasioamini watusaidie kuamua, badala yake tunapaswa tuyawasilishe mbele ya kanisa, sisi kwa sisi wenyewe tuyaamue, Kwasababu Mungu mwenyewe ametupa jukumu hilo la kuhukumu mambo ya mwili kwa haki, kwasababu hata huko tutakapokwenda tutawahukumu malaika pia biblia inatuambia ..Hivyo basi, hakuna sababu ya kupelekana mahakamani, ili watu waioamini watusaidie kutoa hukumu, wakati sisi wenyewe tupo na tunayo hukumu ya haki zaidi ya wale wengine kule. Hivyo daawa zetu zote, zinapaswa ziamuliwe na kanisa.

Mistari mingine inayoeleza juu ya Neno hili, ni kama ifuatayo:

Ayubu 31:13 “Kama nimeidharau daawa ya mtumishi wangu, au ya kijakazi changu, Waliposhindana nami;

14 Basi Mungu atakapoinuka nitafanya nini? Naye atakapozuru, nitamjibuje?

15 Je! Huyo aliyenifanya mimi ndani ya tumbo, siye aliyemfanya na yeye? Si yeye mmoja aliyetufinyanga tumboni”?

 

Kumbukumbu 16:19 “Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza daawa ya wenye haki”.

 

Kumbukumbuku 17:8 “Ikiwa limezuka neno lililo zito kukupita wewe, katika maamuzi kati ya damu na damu, na kati ya daawa na daawa, na kati ya pigo na pigo, nayo yashindaniwa katika malango yako; ndipo nawe uondoke, ukwee uende mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako”;

Mengine ni hii: (2Samweli 15, Ayubu 5:8, 23:4,29:16,35:14)

Hiyo ndio tafsiri ya Neno hilo, pia angalia tafsiri ya maneno mengine chini..

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Jabari ni nini, kama linavyotumika kwenye biblia?

Areopago ni nini? Kwanini mtume Paulo walimpeleka huko?

MAMBO MENGINE HAYATOKI ISIPOKUWA KWA KUFUNGA.

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 8 (Kitabu cha Ezekieli)

 

TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

Rudi Nyumbani:

Print this post

Neno beramu lina maana gani katika biblia?

Beramu ni nini?


Beramu ni jina lingine la neno BENDERA. Hivyo mahali popote kwenye biblia unapolisoma neno hili basi fahamu kuwa linamaanisha bendera.

Hesabu 1:52 “Na wana wa Israeli watazipanga hema zao, kila mtu katika marago yake mwenyewe, kila mtu hapo ilipo beramu yake mwenyewe, kama majeshi yao yalivyo”.,

Vipo vifungu vingi katika biblia, vinavyolitaja neno hili hatuwezi kuvihorodhesha hapa vyote, kwahiyo kama unahitaji kuvijua baadhi yao, basi soma kitabu cha Hesabu sura ile ya pili yote utakutana na Neno hili sehemu kadha wa kadha.

Lakini beramu/bendera sikuzote inasimama badala ya nini?

Tunafahamu kuwa kila bendera tunayoiona mahali fulani imesimamishwa, aidha kwenye mji, au chama, au jamii n.k. huwa  ina maana yake.

Nyingine zimebeba historia ya jamii husika/taifa, nyingine zimebeba tunu, nyingine zinaeleza tabia ya nchi, au vitu vya asili vya nchi n.k.

Hivyo hata rohoni napo, kila mmoja wetu kwa namna moja au nyingi ni lazima atakuwa ameshikilia bendera mojawapo inayomwakilisha yeye.

Na ndio maana leo hii ukienda kwenye mabalozi yote, ni lazima uone bendera ya nchi yake inayoiwakilisha imesimamishwa pale. Hiyo ni kukutambulisha kuwa umefika katika makao ya muda ya nchi ile.

Hivyo mambo yote yahusuyo nchi hiyo huko ugegenini utasaidiwa ukifika pale, huduma zote utapewa sawasawa tu na kama ungekuwa katika nchi yako.

Vivyo hivyo na hapa duniani, kila mmoja wetu ni balozi wa mahali Fulani. Na tunatambuliwa kwa beramu/bendera zetu rohoni.

Ikiwa wewe ni mwenye dhambi, moja kwa moja unapeperusha bendera ya kuzimu, kwa matendo yako maovu, ambayo asili yake ni kuzimu na mkuu wake ni ibilisi.

Lakini kama wewe ni mtakatifu, nawe pia ni lazima upeperushe bendera ya ufalme wa mbinguni kwa matendo yako, ambayo ni lazima yawe ya kumpendeza Mungu, na pili uwe unaihubiri injili(kuwashuhudia wengine habari njema).

Kama hayo mawili huyafanyiki ndani yako na unasema umeokoka, hakuna beramu/bendera yoyote unayoipeperusha ya ufalme wa mbinguni duniani.

Hivyo jitathimini maisha yako ni beramu gani unaipeperusha, katika hichi kipindi kifupi tuliobakiwa nacho hapa duniani. Je, ni ya mbinguni au kuzimu?

Lakini ikiwa leo hii unasema mimi na dhambi basi, nataka Yesu anibadilishe maisha yangu kuanzia leo , nataka anifanye kiumbe kipya nianze na mimi kuipeperusha beramu ya Yesu maishani mwangu. Basi uamuzi huo ni wa busara sana kwako, ambao utaufurahia maisha yako yote. Bwana anasema:

Na uzuri ni kuwa yeye mwenyewe anasema “yeye ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe” (Yohana 6:37)..

Hivyo kama upo tayari na umemaanisha  kufanya hivyo leo, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba.>>>KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

https://wingulamashahidi.org/ikabodi-maana-yake-ni-nini/

Jabari ni nini, kama linavyotumika kwenye biblia?

Neno Korbani linamaanisha nini? (Marko 7:11)

Mahuru ndio nini?

UNYAKUO.

Areopago ni nini? Kwanini mtume Paulo walimpeleka huko?

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

Rudi Nyumbani:

Print this post