Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu libarikiwe.
Karibu tujifunze biblia Neno la Mungu wetu lililo taa ya miguu yetu na mwanga wa njia yetu.
Kuna mambo makuu mawili ambayo yanaweza KUMUUNGANISHA MTU MOJA KWA MOJA NA USHIRIKA WA MAPEPO.
Na mambo hayo ni SADAKA NA UASHERATI. Haya mambo mawili yanaenda pamoja, ndio maana wanaoenda kwa waganga utaona wanaambiwa watoe sadaka, au wafanye zinaa, lengo la zile sadaka si kuimairisha maisha ya wale wanaozitaka (waganga), wala lengo la ile zinaa si kuwafurahisha hao waganga bali ni kumuunganisha yule mtu na madhabahu ile!.
Sasa nataka tuangalie mfano mmoja wa kwenye biblia wa watu waliojiunganisha na madhabahu za mashetani kwa njia hizo mbili; (MATOLEO PAMOJA NA UASHETANI). Na hao si wengine Zaidi ya Wana wa Israeli walipokuwa katika safari yao ya kwenda Kaanani.
Tusome,
Hesabu 25:1 ”Basi Israeli akakaa Shitimu, KISHA WATU WAKAANZA KUZINI PAMOJA NA WANAWAKE WA MOABU; 2 kwa kuwa waliwaalika hao watu WAENDE SADAKANI, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao. 3 IKAWA ISRAELI KUJIUNGAMANISHA NA BAAL-PEORI; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israeli. 4 Kisha Bwana akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa hao watu, ukamtungikie Bwana watu hao mbele ya jua, ili kwamba hizo hasira kali za Bwana ziwaondokee Israeli. 5 Basi Musa akawaambia waamuzi wa Israeli, Waueni kila mtu watu wake waliojiungamanisha na Baalpeori”
Hesabu 25:1 ”Basi Israeli akakaa Shitimu, KISHA WATU WAKAANZA KUZINI PAMOJA NA WANAWAKE WA MOABU;
2 kwa kuwa waliwaalika hao watu WAENDE SADAKANI, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao.
3 IKAWA ISRAELI KUJIUNGAMANISHA NA BAAL-PEORI; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israeli.
4 Kisha Bwana akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa hao watu, ukamtungikie Bwana watu hao mbele ya jua, ili kwamba hizo hasira kali za Bwana ziwaondokee Israeli.
5 Basi Musa akawaambia waamuzi wa Israeli, Waueni kila mtu watu wake waliojiungamanisha na Baalpeori”
Mstari wa 3 hapo unasema hao watu kajiunganisha na “Baali-peori” ambaye ni mungu wa wamoabi, na njia waliojiunganisha nayo ni UASHERATI na SADAKA!
Na adui njama aliyoitumia ni KUALIKA!.. walioalikwa tu! Lakini kumbe walikuwa wameshaandaliwa “wanawake wa kuzini nao” na kwa tamaa zao wakaingia kwa wanawake hao na kuzini, pasipo kujua kuwa kwa kitendo hiko tayari walikuwa wameshajiungamanisha na miungu yao, na hivyo hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli na Mungu akapigo kwa pigo kuu.
Ndugu, (kaka, dada,mama, baba) jihadhari na uasherati, jihadhari na Mialiko isiyo rasmi inayohusisha jinsia mbili tofauti.. Mtego wa shetani si wewe ufanye tu dhambi ya uzinzi, bali lengo lake ni wewe kukuunganisha na miungu na madhabahu ya huyo unayekwenda kuzini naye.
Na madhara ya kuunganishwa na mtu huyo ni kwamba zile “laana” na “hukumu” anazozibeba na wewe unazibeba..Ndicho kilichowatokea wana wa Israeli walipozini na wanawake wa Moabu, Taifa la Moabu lililaaniwa na wote waliozini na wale wanawake walibeba zile laana.
Ndivyo maandiko yanavyosema katika 1Wakorintho 6:15…
1Wakorintho 6:15 “Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!
16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja”.
Sasa inawezekana ulifanya hayo pasipo kujua, na hivyo ulijiungamanisha na madhabahu za kuzimu. Suluhisho la kwanza si kwenda kuombewa!… bali ni wewe kutubu! Kwa kumaanisha kutofanya machukizo hayo tena. Na baada ya kutubu, hatua inayofuata ni ubatizo sahihi na kisha kudumu katika Imani huku ukijitenga na uovu na vichocheo vyake vyote.
1Wakorintho 6:18 “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe”.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mada Nyinginezo:
Bwana aliposema “sikuja kutangua torati bali kuitimiliza” alikuwa anamaanisha nini?
Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?
Sadaka ya Amani ilikuwaje?
MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.
Chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu ndio kipi? (Matendo 21:25).
Rudi nyumbani
Print this post