Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi;
Mithali 20:13 “Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo.
Mithali 20:19 “Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Basi, usishirikiane naye afunuaye midomo yake sana”.
Mtu mwenye kitango kwa lugha ya sasa ambayo ni rahisi kueleweka na watu wengi ni mtu “MMBEA”. Yaani mtu ambaye hawezi kusitiri jambo, yupo tayari kukizungumza kila kitu anachokisikia au kukiona kwa watu wengine.
Kwamfano utakuta mtu labda kakaribishwa nyumbani kwa jirani yake au ndugu yake wa mbali, ili akae au aishi tu pale kwa muda, sasa katika kuishi kwake akaona mapungufu fulani fulani ndani ya nyumba ile, ambayo hata wenye nyumba wenyewe hawakuona vema, kuyatangaza, lakini utakuta yeye anatoka pale na kuanza kufichua siri za nyumba hiyo kwa watu wengine, bila hata kujali utu, wale wapo hivi, wapo vile, yule mwanaume kumbe yupo hivi au vile n.k… Sasa mtu kama huyo ni mtu mwenye kitango ambaye biblia imetuonya, tusishirikane naye.
Mwingine ataelezwa jambo la siri na rafiki yake pengine labda ugonjwa fulani usiotibika, na akaombwa sana asimwambie mtu yeyote iwe siri yake, lakini yeye anatoka pale, anaanza kutangaza mtaa mzima yule fulani ana hiki au kile, mpaka habari inamrudia yule mwenyewe muhusika. Sasa watu wa namna hiyo ni hatari sana, hatupaswi kushirikiana nao, kwasababu hata kwa namna ya kawaida ikiwa anaweza kufichua siri za watu wengine kwako, ni wazi kuwa hata za kwako ameshawahi kuzifichua kwa watu wengine. Hivyo ukishakutana na watu kama hawa usijaribu kuwaeleza mambo yako ya siri, wala usikubali kusikiliza wanachokuambia.
Mara nyingi tunaziharibu siku zetu mapema kabisa kunapopambazuka, kwa midomo yetu wenyewe, biblia inasema;
1Petro 3:10 “Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, NA KUONA SIKU NJEMA, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila”.
Ukitaka ufurahie maisha, jifunze,kuudhibiti ulimi wako, ukitaka siku yako ibarikiwe tangu asubuhi mpaka jioni, jifunze kuutawala mdomo wako, sio kila jambo unaloliona au unalolisikia ni la kutangaza kwa watu , jifunze kutunza siri za watu wengine, kwani kwa kufanya hivyo sio tu siku yako itakuwa ni nzuri, lakini pia utakuwa unampendeza Mungu, Kwasababu Mungu naye hachukui mambo yetu ya siri na kwenda kuyatangaza kwa watu ovyo ovyo, japokuwa anajua mambo yetu wote ya siri tunayoyafanya.
Mathayo 5:48 “Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu”.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
SWALI: Shalom mpendwa katika Bwana , swali langu lipo katika kutoka 33:5 BWANA alipomwambia Musa vueni “vyombo vyenu vya uzuri” ili nipate kujua nitakalowatenda . Nataka kujua aliposema hivyo alikuwa na maana gani?
JIBU: Tusome habari yenyewe tokea mstari wa kwanza, lipo jambo zaidi ya hilo la kujifunza;
Kutoka 33:1 “Bwana akanena na Musa, Haya, ondokeni, katokeni hapo, wewe na hao watu uliowaleta wakwee kutoka nchi ya Misri, waende nchi hiyo niliyomwapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, niliposema, Nitakipa kizazi chako nchi hii;
2 nami nitamtuma malaika aende mbele yako; nami nitawafukuza Mkanaani, na Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi;
3 waifikilie nchi imiminikayo maziwa na asali; kwa maana mimi sitakwenda kati yenu; kwa sababu ninyi ni watu wenye shingo ngumu; nisiwaangamize ninyi katika njia.
4 Watu waliposikia habari hizo mbaya wakaomboleza WALA HAPANA MTU ALIYEVAA VYOMBO VYAKE VYA UZURI.
5 Bwana akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli, Ninyi ni watu wenye shingo ngumu; kama mimi nikiingia kati yenu dakika moja, nitawaangamiza; basi sasa VUENI VYOMBO VYENU VYA UZURI ili nipate kujua nitakalowatenda.
6 Basi wana wa Israeli wakavua vyombo vyao vyote vya uzuri, tangu mlima wa Horebu na mbele”.
Vyombo vya uzuri,ni mapambo ya aina yote, ikiwemo mikufu, pete, hereni, vikuu, nguo za thamani n.k.. Wana wa Israeli baada ya kumkosea sana Mungu, kwa kutengeneza ndama wa dhahabu, Mungu alikusudia kuanzia huo wakati kuwaacha moja kwa moja asitembee nao tena, kinyume chake awape malaika wake wawe wanaenda badala yake, lakini sio yeye tena. Lakini wana wa Israeli waliposikia hivyo wakamlilia sana Mungu wasiachwe, ndipo watu wote wakavua vyombo vyao vya uzuri, yaani vitu vyao vya thamani, wakavaa nguo za maombolezo, wakamlilia sana Mungu na kutubu kwa uchungu mwingi ili tu wasiachwe.
Hiyo ilikuwa ni desturi ya Israeli tangu zamani, na hata mataifa mengine, inapofikia wakati wa kuomba toba, au kuomboleza, ni sharti uweke kando mavazi ya thamani, na mapambo yako, uvae nguo za magunia uomboleze.
Lakini ni nini, tunaweza kujifunza katika habari hiyo?
Wana wa Israeli walitamani waangukie mikononi mwa Mungu kuliko mikononi mwa malaika zake, Kwasababu walimjua Mungu ndio uzima wao, licha ya kuwa ni mwenye ghadhabu nyingi, lakini pia bado ni mwenye rehema nyingi. Ni sawa na kilichomtokea Daudi kipindi kile, alipoambiwa na Mungu achague adhabu mojawapo kati ya zile tatu, yaani njaa miaka mitatu, au akimbizwe na adui zake miezi mitatu, au Tauni iletwe siku tatu juu ya nchi,. Daudi akachagua kuangukia mikononi mwa Mungu, kwa ile Tauni siku ya tatu, kwasababu alijua, mioyo ya wanadamu sio kama wa Mungu, kuliko kukimbizwa na maadui zake, ni heri aadhibiwe na Mungu..Na kweli japokuwa Mungu aliwaua maelfu ya watu, lakini baadaye aliuzuia mkono wake, akarehemu.
Je! Na wewe umechagua kuangukia mikononi mwa nani? Mungu, au mwanadamu?.
Daudi alisema..
Zaburi 118:18 “Bwana ameniadhibu sana, Lakini hakuniacha nife”.
Inasikitisha kuona kwamba watu wanakataa kuongozwa na Mungu, wanataka waongozwe na wanadamu, wanachukia kuadhibiwa na Mungu, wanataka wakaadhibiwe na wanadamu. Wana wa Israeli waliomboleza kusikia tu wanakwenda kuongozwa na malaika,ambao hata hawana shida yoyote, lakini waliona bado hakuna kiongozi mzuri na bora zaidi ya Bwana.
Ndugu yangu huna kimbilio lingine lililo salama kwako, zaidi ya Mungu.. Si hata malaika wake, si mwanadamu, au kiumbe kingine chochote, au kitu kingine chochote. Mkimbilie Bwana leo hii akuokoe, na ayasafishe maisha yako. Usizifiche dhambi zako mbele za Mungu, kwa hofu ya kwamba atayakemea matendo yako, ni kweli lazima ayakemee, na wakati mwingine akuadhibu, lakini adhabu zake ni dawa, na sio mauti. Hivyo chagua kuangukia mikononi mwake, uwe salama.
Ufunuo 3:19 “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu”.
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Karibu tujifunze maneno matukufu ya uzima, maadamu tumeiona leo.
Wakristo wameganyika katika makundi makuu matatu, makundi hayo yanafananishwa na miti ya matunda.
Na Miti ya matunda ipo ya aina tatu;
Hii Ndio ile miti ambayo Bwana Yesu aliizungumzia katika mfano ule mfano wa mpanzi, akasema mbegu zake ndio zile zilizopandwa katika udongo mzuri ambazo nyingine zilizaa 30 nyingine 60 nyingine 100 (Mathayo 13:8). Akasema hao ni wakristo ambao, walistahimili vishindo vyote vya ibilisi, kwa kuvumilia ndipo wakaweza kumzalia Mungu matunda.
Luka 8:15 “Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda KWA KUVUMILIA”.
Walivumilia nini?
Walivumilia dhiki na udhia shetani alizowaletea kutokana na ukristo wao, waliweza kulitunza Neno la Mungu mioyoni mwao, kwa kutoruhusu masumbufu ya maisha haya kuwaingilia sana, mpaka kuwafanya wasilitendee kazi Neno., Na kundi hili lipo dogo sana. Na Kristo ameahidi kulipalilia, na kulisafisha ili liendelee kumzalia zaidi. (Yohana 15:2)
Mfano wa miti huu, ndio ile ambayo Bwana Yesu aliutolea mfano huu;
Luka 13:6 “Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate.
7 Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu?
8 Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi;
9 nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate”.
Hawa ni wakristo, ambao mara baada ya kuokoka, wana-relax, wanadhani wokovu ni kukiri tu kwa kinywa na kuamini, basi, na baada ya hapo unaendelea na mambo yako mwenyewe. Hawataki kujishughulisha kutafuta mambo ya rohoni baada ya kuamini na kubatizwa, licha ya kwamba, Mungu anawatia samadi kila siku kwa kuwafundisha na kuwahubiria njia zake, lakini wao hawaonyesha badiliko lolote, Hawapo kwenye maovu, wala hawapo kwenye mema. Lakini wakati wote, wanasikiliza Neno la Mungu na kulipokea, kundi hilo lipo kubwa sana.
Kristo ameahidi kutochukuliana nalo muda mrefu sana, utafika wakati litakatwa, na ukishakatwa, ndio habari yako imeishia hapo, unakuwa umekufa kiroho, haijalishi utasema niliokoka zamani. Bwana Yesu anatazamia, tunapookoka, tuonyeshe matendo yanayotendana na wokovu wetu, kuanzia huo wakati, tuwe waombaji, wafungaji, tuwaambie na wengine habari njema za wokovu, tuchangie kwa mapato yetu kazi ya Mungu isonge mbele, n.k. Lakini tukiwa sisi ni wa kupokea tu vya Mungu, lakini hatumtolei na yeye, tujue kuwa safari yetu haitakuwa ndefu.
Mfano wa miti hii, ndio kama huu Ambao Mungu aliizungumza katika Isaya sura ya 5.
Isaya 5:1 “Na nimwimbie mpenzi wangu wimbo wa mpenzi wangu katika habari za shamba lake la mizabibu. Mpenzi wangu alikuwa na shamba la mizabibu, Kilimani penye kuzaa sana;
2 Akafanya handaki kulizunguka pande zote, Akatoa mawe yake, Akapanda ndani yake mzabibu ulio mzuri, Akajenga mnara katikati yake, Akachimba shinikizo ndani yake; Akatumaini ya kuwa utazaa zabibu, Nao ukazaa zabibu-mwitu.
3 Na sasa, enyi wenyeji wa Yerusalemu, nanyi watu wa Yuda, amueni, nawasihi, kati ya mimi na shamba langu la mizabibu.
4 Je! Ni kazi gani iliyoweza kutendeka ndani ya shamba langu la mizabibu nisiyoitenda? Basi, nilipotumaini ya kuwa litazaa zabibu, mbona lilizaa zabibu-mwitu?
5 Haya basi, sasa nitawaambieni nitakalolitenda shamba langu la mizabibu; nitaondoa kitalu chake, nalo litaliwa; nitabomoa ukuta wake, nalo litakanyagwa;
6 nami nitaliharibu; wala halitapogolewa wala kulimwa, bali litamea mbigili na miiba; nami nitayaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.
7 Kwa maana shamba la mizabibu la Bwana wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni mche wake wa kupendeza; akatumaini kuona hukumu ya haki, na kumbe! Aliona dhuluma; alitumaini kuona haki, na kumbe! Alisikia kilio”.
Kundi hili ndilo baya zaidi, kwasababu, ni kundi ambalo linazaa matunda ya upande mwingine,. Hawa ni wakristo ambao mara baada ya kuokoka, mara baada ya kukaa kanisani kwa muda mrefu, mambo wanayoyaonyesha kwa matendo yao ni kinyume kabisa na ukristo unavyopaswa uwe.. Utakuta mtu ni mzinzi wa muda mrefu, mwingine ni mtukanaji, mwingine ni mwizi, mwingine ni tapeli n.k. na bado anasema nimeokoka, nimebatizwa, nimepokea Roho Mtakatifu, Yaani kwa ufupi yale mambo ambayo wanayafanya watu wa kidunia na yeye anayafanya, vivyo hivyo, hakuna tofauti yoyote.
Kundi hili nalo ni kubwa sana na Mungu ameahidi kuliondolea kitalu chake (Kuliua)..
Tukiyajua hayo ni wajibu wako wewe kama mkristo kujichunguza ni kundi lipi unaloangukia, na matokeo yake mbeleni yatakuwaje, , Fahamu tu upo wakati mwenye shamba atakuja kukupeleleza, Kwahiyo ni wajibu wako wewe kujua kuwa upo hapa duniani kwa malengo, na Mungu anatarajia kuona badiliko katika maisha yako katika kipindi alichokuweka hapa duniani. Kama upo miaka mingi katika wokovu na huoni kama kuna chochote unakifanya kinampendeza Mungu, au kinaisaidia injili yake isonge mbele, jiulize unaekea wapi? Je, ni wa Kukatwa au kupaliliwa. Jibu unalo, jibu ninalo.
Hivyo tubu ugeuke, umpokee Kristo kwa kumaanisha, na kuonyesha bidii katika kusoma Neno lake, kuomba, na kumfanyia ibada, ndipo utakapopata nguvu ya kumzalia yeye Matunda.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Jibu: Kwanza ni muhimu kufahamu kuwa makosa yote yanastahili msamaha. Hata kama tumetendewa makosa makubwa kiasi gani, mwisho wa siku ni lazima tusamehe, hiyo ndio sheria ya Imani. Hakuna ukristo bila msamaha, kwasababu kila mwanadamu katenda dhambi, na wote tunapata msamaha wa dhambi bure kupitia damu ya Yesu, tunapomwamini. Hivyo na sisi hatuna budi kusamehe kama Bwana alivyotusamehe sisi.
Lakini kuna jambo moja ambalo Bwana Yesu alilizungumza ambalo tukijifunza hilo vizuri tutapata kuelewa vizuri muktakabadhi wa msahama
Tusome..
Luka 12:58 “Maana, unapofuatana na mshitaki wako kwenda kwa mwamuzi, hapo njiani fanya bidii kupatanishwa naye, asije akakuburuta mpaka mbele ya kadhi; yule kadhi akakutia mikononi mwake mwenye kulipiza, na yule mwenye kulipiza akakutupa gerezani.
59 Nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho”
Hayo maneno yalizungumzwa na Bwana Yesu mwenyewe. Na kama ukiyatafakari kwa makini utagundua kuwa Bwana anaonyesha hatua za mtu ambaye ni Mdhulumuji, na hataki kukiri dhuluma zake, na kuzidi kujihesabia haki (au kwa lugha nyepesi yule mtu ambaye hataki kuacha njia zake mbaya), kama ni mwizi au tapeli, anatapeli leo na kesho anarudia inakuwa kama ni tabia yake, yeye kazi yake ni kusababisha wengine walie tu na kuhuzunika kila siku.
Sasa Bwana Yesu anasema mtu wa namna hiyo akiri makosa yake mapema, aachane na hiyo kazi ya utapeli aiache(maana yake apatane na jamii yake, mapema) kabla hajashikwa na kupandishwa mahakamani na kuhukumiwa… Hapo Bwana Yesu anamalizia kwa kusema “NAKUAMBİA, HUTOKİ HUMO KAMWE HATA UİSHE KULİPA SENTİ YA MWİSHO” Ukisoma Mathayo 5:26 inasema … “ Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.”…. Neno Amin amini, maana yake ni Hakika!!… hakika!!
Sasa unaweza kujiuliza kwanini Bwana aseme maneno hayo?..Hakika hakika!! Hutoki huko.
Ni kwasababu anataka kuonyesha kuwa Mahakama na Vyombo vya dola vimepewa mamlaka makubwa ya kutawala kutoka mbinguni.. Ukitiwa mikononi mwa polisi kwa kosa lolote ambalo ni halali umelitenda ni sawa kabisa na umetiwa mikononi mwa Mungu mwenyewe kwaajili ya adhabu..
Hivyo kwa lugha rahisi kabisa tunaweza kusema polisi ni kiboko cha Mungu..
Warumi 13: 1 “Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.
2 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu.
3 Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake;
4 kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu.
5 Kwa hiyo ni lazima kutii, si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri”
Kwahiyo basi kama umemwona mtu ni tapeli na anatapeli watu, na kuwafanya waumie..mwitie Polisi, hufanyi dhambi, atakwenda polisi na hatatoka huko!! Mpaka ameiva vizuri!!..Lakini kama akikiri njia yake mapema na kuiacha, hapo amepatana na wewe na jamii yote, hivyo umwache usifanye lolote, wala usimpeleke polisi. Na pia kama ni kibaka kakuibia, hapo hapo na ukamshika na akatubu mbele yako kwa kuomba radhi kabisa msamehe, usimripoti..
Lakini kama mtu ni muuaji, au jambazi.. mripoti polisi (hufanyi dhambi)...Lakini kama alikuwa ni muuaji miaka ya zamani na sasa kashabadilika ni mtu mwema na hata pengine kashaokoka, huna haja ya kuchimbua makosa yake ya zamani na kuyapeleka polisi.
Vivyo hivyo kama ni mbakaji, au ni mtu wa dhuluma, au ni mtu asiyefaa kitabia katika jamii, anayefanya mambo maovu kwa makusudi na huku anajua kabisa anayoyafanya sio sawa na anandelea kuyafanya, pamoja na kuonywa mara nyingi..Mtu huyo mripoti polisi utakuwa hujafanya dhambi na zaidi ya yote utakuwa umefanya jambo jema.
Vivyo hivyo kama umedhulumiwa mali zako na yule mdhulumuji unaona ni mtu aliyejizoeza kuyafanya hayo, na ameshawafanyia wengi, na anazidi kuwafanyia wengine..maana yake huyo kashaonywa mara nyingi lakini kashupaza shingo, mtu wa namna hiyo mpeleke mahakamani, utakuwa umesaidia asiendelee kufanya hivyo kwa watu wengine, na kusababisha huzuni na majonzi kwa watu wengine. Utakuwa hujafanya dhambi. Lakini kumbuka hatuzungumzii suala la kujichukulia sheria mkononi, kwamba ameiba sasa unampiga, au ameua sasa na wewe unatafuta kumuua.. Hapana! Ukifanya hivyo utakuwa unatenda dhambi…Kwasababu biblia hapo juu inasema Mamlaka ndio zimepewa ruhusa za kutoa hukumu, na Mungu mwenyewe, na si wewe wala mimi.
Na mambo mengine yoyote ambayo unaona kuna mtu au watu wanayafanya ambayo yanaleta au yataleta madhara makubwa sana katika jamii, na kuifanya jamii iharibike, au watu kupoteza maisha..Ripoti polisi, kwasababu vyombo hivyo pia vinatimiza kusudi la Mungu duniani.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Jibu: Si kweli kwamba mtu anayeua anakuwa anazibeba dhambi zote za yule aliyemuua, na kwamba yule aliyeuawa yupo huru, (anakuwa hana dhambi tena huko anakokwenda).
Kama mtu atamkataa Mungu na ghafla akafa katika dhambi zake, kwa kifo cha aina yeyote ile, iwe kwa kuuawa, au labda kwa kugongwa na gari, au kupewa sumu, au kupigwa mpaka kufa.. Mtu huyo dhambi zake anazibeba mwenyewe, na anakwenda nazo huko anakokwenda, hakuna yeyote atakayezuchukua. Yule aliyemuua atabeba dhambi ya mauaji, kwa alilolifanya lakini si dhambi za yule aliyemuua.
Wagalatia 6: 5 “Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe”.
Ni kitu kimoja tu ambacho Mungu atamdai mtu yule ambaye hatamwonya mwingine aiache njia yake mbaya. Na hicho si kingine zaidi ya Damu ya huyo mtu.
Ezekieli 3:18 “Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako”.
Sasa nini maana ya kuwa hatia na damu ya mtu?.
Kuwa na hatia ya damu ya mtu, si kuzichukua dhambi zake na kuzibeba.. La!..Bali maana yake ni kuwa na kila sababu za kuwajibishwa kwa kumsababishia mwingine madhara. Maana yake ni kwamba kama hujamwonya mtu aache njia mbaya, na ilihali ulikuwa na nafasi ya kufanya hivyo, na yule mtu akafa bila kusikia maonyo yoyote, basi wewe ambaye ulipaswa umwonye, kuna adhabu itakayokuja juu yako. Na adhabu hiyo inaweza kuwa laana au wakati mwingine hata kifo.
Ili tuelewe vizuri tafakari tu, mtu aliyemuua mwenzako…katika sheria za nchi, yule aliyeua hachukui madeni ya yule aliyemuua.. Maana yake ni kwamba, kama yule aliyeuawa alikuwa na madeni ya benki, au madeni mengine yoyote, madeni hayo hatayarithi yule aliyemuua. Yule aliyemuua atahukumiwa kwa kosa la mauaji (ambayo adhabu yake ndio hiyo ambayo inaweza kuwa hata kifo), lakini hatatwikwa madeni yote ya yule aliyemuua kwamba benki imfuate imwambie alipe deni la marehemu . Ndio hivyo hivyo pia kwa mtu aliyemuua mwingine, hatabeba dhambi za aliyekufa.
Hivyo tunachojifunza ni kwamba tuwe makini, hususani kama umeshaokolewa, ni wajibu wako kuwapelekea wengine injili, ili damu yao isiwe juu yako, kama Mtume Paulo alivyosema mahali fulani..
Matendo 20:25 “Na sasa, tazameni, mimi najua ya kuwa ninyi nyote niliowahubiria ufalme wa Mungu, nikienda huko na huko, hamtaniona uso tena.
26 Kwa hiyo nawashuhudia wote siku hii ya leo, ya kuwa mimi sina hatia kwa damu ya mtu awaye yote.
27 Kwa maana sikujiepusha na kuwahubiria habari ya kusudi lote la Mungu”
Na kuipeleka injili sio tu kwenda kuhubiri, bali kuchangia hata kuichangia kazi ya Mungu, pia ni kuipeleka injili.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Yeremia 4:22 “Kwa maana watu wangu ni wapumbavu, hawanijui; ni watoto waliopungukiwa na akili, wala hawana ufahamu; ni wenye akili katika kutenda mabaya, bali katika kutenda mema hawana maarifa”.
Shalom, Mungu anatazamia kila mmoja wetu siku anapofanyika kuwa kiumbe kipya, bidii mpya iumbike ndani yake na hari mpya ya kutafuta kumpendeza yeye kwa namna yoyote ile ionekane.
Kama vile tunavyojua mtu aliyekatika dhambi huwa hakai hivi hivi tu, bali anafanya juu chini kuhakikisha kuwa kile anachokitamani anakipata katika ubora wote.. Kwamfano ukimtazama mlevi, utajiuliza huyu ni kwanini mwaka mzima anakunywa tu?. Unaweza kusema ana pesa nyingi, Sio kwamba ana pesa nyingi sana kwenye akaunti yake zaidi ya wewe, hapana, bali ukimchunguza utagundua kuwa ili aweze kunywa kwa kadiri awezavyo, na kutoshelezeka itamgharimu mchana kutwa akifanyie kazi, ili apate pesa jioni au wikiend akanywe makreti ya bia. Unaona hapo ametumia akili katika mambo yake, ilimpasa akakifanyie kazi, ili afurahie ulevi wake, na ndio maana Bwana Yesu alisema,
Luka 16: 8b “…wana wa ulimwengu huu katika kizazi chao wenyewe huwa na busara kuliko wana wa nuru”.
Lakini mkristo, anayejua kuwa jumapili anahitajika kwenda kanisani, mahali ambapo analishwa chakula cha kiroho, mahali ambapo anapata baraka za kimbinguni, hawezi kudunduliza chochote na kukipeleka nyumbani kwa Bwana atakwenda mikono mitupu. Na mtu kama huyo, bado anatazamia viwango vyake vya kiroho viwe kama anavyotarajia.. Kumtolea Bwana sio kumnufaisha mchungaji wako, kumtolea Bwana ni kuonyesha upendo wako kwake, na kuwa unathamini wokovu wake aliokupatia bure bila malipo.
Lakini mwingine wakati huo huo akisikia, kuna shughuli ya jirani yake, pengine harusi na kunahitaji michango mikubwa, ataanza kulihangaikia hilo, hata miezi miwili au mitatu kabla, ili huo wakati utakapofika atoe kiwango kile kile alichopangiwa, asiabike. Sasa mkristo kama huyu kibiblia ni mjinga katika kutenda mema, bali mwenye maarifa katika kutenda mambo mengine.
Vivyo hivyo katika kusali,
Mtu wa mwilini labda tuseme mwanafunzi, anajua kabisa ili afaulu katika masomo yake itamgharimu, kusoma kwa bidii, kila siku na wakati mwingine kukesha usiku,..lakini kwa mkristo, haipo hivyo, atataka akue kiroho katika mazingira ya kusubiria ahubiriwe kanisani jumapili, au aombewe, na hata kama akiomba mwenyewe basi ataomba dakika mbili, tatu,., Hapo ni sawa na tunakuwa wajinga katika kutenda mema, tumepungukiwa akili katika mambo ya rohoni. Tukitaka tupate matokeo mazuri rohoni, ni sharti tutumie akili zilezile tulizokuwa nazo katika dhambi, isipokuwa tu tunazihamishia kwa Mungu,. Hapo tutaufurahia wokovu wetu sana.
Biblia inatuonyesha zipo faida za kuyatafuta mambo mema hususani pale tunapotumia bidii, na faida kuu ni kuwa Mungu atamshusha mara moja shetani chini ya miguu yetu, Anakuwa hana nguvu yoyote ya kutushinda sisi. Soma.
Warumi 16.19 “….lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya.
20 Naye Mungu wa amani ATAMSETA SHETANI CHINI YA MIGUU YENU UPESI. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. [Amina.]
Je! Unataka shetani na kwako awe ni kitu kirahisi sana, kitu kinyonge?, jibu ni moja tu, kuwa mjinga katika kutenda mabaya, na kinyume chake tumia akili zako nyingi katika kumtumikia Mungu. Fanya zaidi ya pale ulipozoelea kufanya siku zote. Kila siku hakikisha unaiga hatua moja kiroho, hatua katika kumtolea yeye, katika kuomba, katika kusali, katika kufunga, n.k. Na matokeo utayaona. Utaishi maisha kama vile shetani hakujui wewe. Kumbe ni siku nyingi sana Mungu alishamshusha chini ya miguu yako.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Zaburi 32:9 :Msiwe kama farasi wala nyumbu, Walio hawana akili. KWA MATANDIKO YA LIJAMU NA HATAMU Sharti kuwazuia hao, au hawatakukaribia:.
Hatamu ni kifaa, kinachotumika kumwongozea farasi, ikijumuisha ule mkanda unaoshikilia kichwa, na ile kamba inayokwenda moja kwa moja kwa mwongozaji farasi. Kazi ya hatamu ni kumwongoza farasi, na kumpa balansi wakati wa kumwendesha, Tazama picha chini
Lijamu ni kifaa kidogo, ambacho huwa kinapitishwa katikati ya midomo wa farasi, hichi kinashikiliwa na Hatamu yenyewe, kazi yake ni kuongeza Presha kwa mnyama, ikivutwa sana mwendo wa farasi unaongeza, ikivutwa kidogo mwendo unapungua..lijamu ndio inayoeleza mwendo wa farasi. Tazama picha chini;
Hivyo Hatamu na lijamu vyote vinafanya kazi pamoja, kumwendesha na kumwongoza farasi.
Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi baadhi,
Yakobo 3:3 “Angalieni, twatia lijamu katika vinywa vya farasi, ili wamtii, hivi twageuza mwili wao wote.
4 Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote anakoazimia kwenda nahodha.
5 Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana”.
Zaburi 39: 1 “Nalisema, Nitazitunza njia zangu Nisije nikakosa kwa ulimi wangu; Nitajitia lijamu kinywani, Maadamu mtu mbaya yupo mbele yangu”.
Soma pia Mithali 26:3, Isaya 37:29
Hivyo kulingana na vifungu hivyo unaweza kuona tunaonywa tuvichunge vinywa vyetu, tuviweze, tuvitawale, na sio vitutawale sisi. Tutie lijamu, ikiwa na maana kuwa si kila habari ya usengenyaji na sisi tuwepo, si kila maneno yasiyo na maana na sisi tuyachangie, si kila maneno ya laana na sisi tuyatamke. Tunapaswa tujifunze chagua ni kipi cha kuchangia na kipi cha kukaa kimya. Kwasababu ulimi ni kama moto.
Lakini pia tukirudi katika kitabu cha Ufunuo tunaona, siku ile, Kristo atakapokuja kuitekeleza ghadhabu ya Mungu duniani, biblia inatuambia, kwa maangamizi yatakayotokea, damu itakayomwagika itakuwa ni nyingi sana, kiasi cha kufikia urefu wa hatamu ya farasi, (ambayo hiyo ni sawa na futi 5 au 6 karibia kimo cha mwanadamu wa kawaida)..Na itaenda kwa umbali wa maili 200 ambayo ni sawa na km 321. Hilo ni ziwa la damu.
Ufunuo 14:19 “Malaika yule akautupa mundu wake hata nchi, akauchuma mzabibu wa nchi, akazitupa zabibu katika shinikizo hilo kubwa la ghadhabu ya Mungu.
14:20 Shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, damu ikatoka katika shinikizo mpaka kwenye hatamu za farasi, kama mwendo wa maili mia mbili”.
Haijalishi itakuwa ni lugha ya picha au halisi, lakini hiyo inatupa kujua hali halisi jinsi kutakavyokuwa huku duniani wakati huo kwa wale watakaobaki, wanadamu wataadimika kama dhahabu..
Hivyo sisi hatupaswi kuchukulia, kirahisi rahisi haya maisha, ni kujihakiki je! Tupo ndani ya wokovu au la, kama hatupo basi, huu ndio wakati wa kuyatengeneza mambo yetu sawa, kwasababu kipindi hicho hakipo mbali.
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
JINA LAKE KWA KIEBRANIA NI ABADONI, NA KWA KIYUNANI NI APOLIONI.
Mfalme wa kwanza wa Israeli alikuwa anaitwa Sauli. Mungu alivyomchagua mtu huyu, ilikuwa ni nje ya matarijio ya waisraeli wengi sana. Kwasababu ikumbukwe hapo kabla walikuwa hawana mfalme, hivyo baada ya kuona mataifa mengine yaliyokuwa yanawazunguka yana wafalme hodari na mashujaa na wao pia wakaingiwa na tamaa wakamwomba Mungu awapatie mfalme. Jambo ambalo halikuwa mapenzi ya Mungu, lakini Mungu aliwapa tu hivyo hivyo haja ya moyo wao. Ndipo akawapa huyu Sauli
Sasa, Sauli, alikuwa ni mtu mlaini laini tu, mtu ambaye sio machachari, mtu ambaye, huwezi kumwita shujaa hata kwa sura yake tu, kwa lugha ya kisasa wengine watamuita mtoto wa mama tu. Hiyo ni kweli kwasababu biblia inatuambia hata yeye mwenyewe alijiona ni dhaifu machoni pake mwenyewe Soma 1Samweli 15: 17
Hata siku aliyopokea unabii kutoka kwa Samweli kuwa atakuwa mfalme alishangaa mwenyewe..Jaribu kutengeneza picha, wewe hujui mambo ya siasi, wala hujawahi kuwa na ujuzi wowote wa uongozi, halafu siku moja Mungu anakuambia mwezi ujao utakuwa raisi.. Unaweza kusema Mungu kakosea kunichagua mimi.. amchague mwingine!! Ndicho alichokifanya hata Musa wakati ule alipoitwa na Mungu, alikuwa dhaifu machoni pake mwenyewe, na ni kweli ndivyo ilivyokuwa, lakini uchaguzi wa Mungu ulikuwa juu yake, haijalishi hali ya udhaifu aliyokuwa nayo.
Ndivyo ilivyokuwa kwa Sauli wakati ule alipokuwa anakwenda kutafuta punda wa baba yake waliopotea, ndipo katika kutembea tembea kwake akafika kwa Nabii Samweli ndipo akamtolea unabii huo.. Sasa moja ya maneno aliyoambiwa na Samweli yalikuwa ni haya..
1Samweli 10:6 “na roho ya Bwana itakujilia kwa nguvu, NAWE UTATABIRI PAMOJA NAO, NAWE UTAGEUZWA KUWA MTU MWINGINE.
7 Basi, hapo ishara hizi zitakapokutukia, fanya kama uonavyo vema; kwa kuwa Mungu yu pamoja nawe”.
Unaona aliambiwa asiogope, pindi tu Roho ya Mungu itakaposhuka juu yake, atageuzwa moyo na kuwa mtu mwingine kabisa..hatakuwa Sauli Yule wa kwanza tena.
Jambo hilo Israeli hawakulielewa bali waliendelea tu kumdharau Soma (1Samweli 10:27), mpaka siku moja ambayo maadui zao wamesimama wanataka kuwachukua mateka na hawajui cha kufanya, wanalia tu, bila matumaini yoyote ndipo wakamwona Sauli Yule mtoto wa mama anasimama kwa ujasiri wa ajabu ambao hawakuwahi kuuona kwake hapo kabla, halafu anatoa amri kuwa watu wote watakwenda vitani na mtu asipokwenda naye mifugo yake yote itauliwa. Soma 1Samweli 11 yote.
Na kweli walienda vitani na ushindi wakaupata, ndipo kuanzia huo wakati watu wakamwogopa na kumuheshimu Sauli. Biblia inatueleza ushujaa wa Sauli ulikuwa mkubwa sana, mpaka siku anayokaribia kufa..
Ni nini ninataka ukione siku ya leo?
Ilihitaji Roho wa Mungu kumfanya Sauli kuwa mtu mwingine, ilihitaji Roho Mtakatifu kumfanya Sauli kuwa Mfalme atakayeweza kuichunga Israeli. Vivyo hivyo na leo hii, itamuhitaji Roho Mtakatifu ndani ya mtu ili aweze kufanywa kiumbe kipya, aweze kufanya mtu mwingine, aweze kushinda ya ulimwengu huu, aweze kuushinda uzinzi, na ulevi, na anasa. Vilevile aweze kuyashinda majaribu yote ya shetani, yeye peke yake kwa nguvu zake, hataweza hata afanyaje, anahitaji msaada wa Roho nyingine itakayo juu.
Zekaria 4: 6b “..Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi”.
Na ndio maana kuna umuhimu wa kuzaliwa mara ya pili. Pale mtu anapozaliwa mara ya pili, hapo hapo Roho wa Mungu anashuka ndani yake. Na uwezo huo anaupokea.
Je! Mtu anazaliwaje mara ya pili?
Ni kwa kutubu dhambi zake, kisha kubatizwa, na kuanza kuishi maisha yanayoendana na toba yake. Na anapokuwa katika hali hiyo , Roho wa Mungu anashuka juu yake, na hapo anakuwa tayari amezaliwa mara ya pili.
Matendo ya Mitume 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”.
Je! Na wewe unataka kupokea uwezo huu wa kufanywa mtu mwingine, uwezo wa kuishinda dhambi kirahisi? Uwezo wa kuyavuka majaribu ya adui?.. Basi tubu,dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha, kisha ukabatizwe katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO, ikiwa jambo hilo halijawahi kufanyika kwako ipasavyo. Na baada ya hapo Mungu atakumwagia kipawa chake cha Roho Mtakatifu. Na wewe mwenyewe utaanza kuona badiliko lingine ndani ya maisha yako. Kiu ya mambo mengi utaona imekata, n.k. ukiona hivyo ujue hapo tayari Roho kashaanza kukuunda upya.
Fanya hivyo na Bwana akubariki.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
SWALI:Kwanini biblia inaitaja mara kwa mara dhahabu ya Ofiri? Umuhimu wake ni upi?
Ofiri ni eneo, lililokuwa maarufu zamani enzi za biblia kwa biashara ya madini na vito, eneo hili lilikuwa maeneo ya huko Arabia. Kwamfano dhahabu zote Sulemani alizotumia kujengea hekalu alikwenda kuzichukulia huko Ofiri kwa merikebu zake (Wafalme 10:22)
Ni sawa na leo useme dhahabu ya Geita, Au Tanzanite ya mererani,. Ndivyo ilivyokuwa zamani dhahabu au mawe ya thamani yalikuwa yapatikana eneo hilo la Ofiri.
Hivi ni baadhi ya vifungu ambavyo utaweza kukutana na Neno hilo;
1Wafalme 9:28 “Wakafika Ofiri, wakachukua toka huko dhahabu, talanta mia nne na ishirini, wakamletea mfalme Sulemani”.
1Wafalme 10: 11 “Tena merikebu za Hiramu, zilizochukua dhahabu kutoka Ofiri, zikaleta kutoka Ofiri miti ya msandali mingi sana, na vito vya thamani”.
1Wafalme 22: 48 “Yehoshafati akafanya merikebu za Tarshishi ziende Ofiri kuchukua dhahabu; walakini hazikuenda; kwa maana merikebu zilivunjika huko Esion-geberi”.
Ayubu 22: 24 “Nawe hazina zako ziweke mchangani, Na dhahabu ya Ofiri iweke kati ya mawe ya vijito”;
Soma pia, Ayubu 28:16,
Sasa tukilijua hilo, upo unabii ambao Isaya aliuzungumza kuhusu siku ile ya Bwana inayotisha, akasema jinsi Mungu atakavyoleta maangamizi, watu wataadimika sana, kama dhahabu, tena akaeleza kwa mifano kabisa akasema, wataadimika kama ile dhahabu ya Ofiri, watu wanaoifahamu sana, ili watu wapate picha yenyewe jinsi mambo yatakavyokuwa mabaya, ni sawa na leo tuseme, watu watakuwa adimu kama Tanzanite, ile Tanzanite ya mererani..
Tusome;
Isaya 13:9 “Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.
10 Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.
11 Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali;
12 nitafanya wanadamu kuadimika KULIKO DHAHABU SAFI, na WATU KULIKO DHAHABU YA OFIRI.
13 Kwa hiyo nitazitetemesha mbingu, na dunia itatikiswa itoke katika mahali pake, kwa sababu ya ghadhabu ya Bwana wa majeshi, na kwa sababu ya siku ya hasira yake kali”.
Siku hiyo watu wengi sana watakufa,idadi isiyohesabika, watauliwa na Mungu mwenyewe, kiasi kwamba kumwona mwanadamu mwenzako ulimwenguni itakuwa ni kama vile kuona dhahabu..Kwa jinsi watakavyoadimika.
Leo hii duniani kuna watu si chini ya bilioni saba, hatushangai wakati huo wakabaki watu elfu moja tu, au hata chini ya hapo. Ni kama ilivyokuwa kipindi cha Nuhu kati ya mabilioni ya watu waliokuwepo duniani, walibaki watu nane tu, vivyo hivyo siku ile ya Bwana itakuwa kwa namna hiyo.
Siku hizo zipo karibu sana, kwasababu biblia inasema, uharibifu utakuja wa ghafla wakati ambao watu hawautarajii kabisa, wakati ambao wanasema kuna amani. (1Wathesalonike 5:3)
Lakini habari njema ni kwamba mpaka hiyo siku ya Bwana ije duniani, unyakuo utakuwa tayari umeshapita, na watakatifu wameshanyakuliwa.
Vivyo hivyo na sisi wakati huu ni wa kujiweka tayari, kumtazama Bwana. Na kuhakikisha kuwa wokovu upo ndani yetu. Ili hata kama unyakuo utapita leo usiku basi, tuwe na uhakika hatubaki hapa duniani, kwenye ghadhabu na hasira ya Mungu.
Shalom
Ili kufahamu kwa undani siku hiyo itakavyokuwa tazama vichwa cha masomo mengine chini;
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
SWALI: Kwanini Mungu aliwaagiza wana wa Israeli siku ile ya kuondoka wasikisaze chakula hata asubuhi?
JIBU: Kusaza chakula maana yake ni kukibakisha ili ukimalizie kukila baadaye au kesho yake…Na hiyo inaweza kutokana na mtu kushiba sana wakati huo, hivyo badala ya kukimwaga anakuwa anakihifadhi hicho chakula ili akimalizie kukila tena wakati mwingine.
Kama tunavyojua siku ile wana wa Israeli walipokuwa wanatoka Misri, Mungu aliwapa maagizo kuwa usiku ule kabla ya kuondoka wamchinje mwanakondoo, na damu yake waipake kwenye miimo ya milango, na kisha wamle yule mwanakondoo waliomchinja, (na maagizo hayo yaliihusu kila familia), hivyo kila familia ilichinja mwanakondoo na damu yake kuipaka milangoni, na kumla yule mwanakondoo..Na yalikuwepo pia maagizo ya namna ya kumpika, utaona waliambiwa wasimtokose majini, yaani wasichemshe(wasile mchemsho), bali wamuoke motoni..vilevile wamle pamoja na mboga chungu, na kwa haraka sana maana yake wasijivutevute wakajikuta kumepambazuka na bado hawajamaliza kula ikawa dhambi.
Sasa pamoja na maagizo yote hayo walipewa agizo lingine tena la msingi, kwamba Huyo mwanakondoo watakayemla, kila familia ihakikishe haisazi nyama yake mpaka asubuhi, maana yake ni kwamba aidha wamle wote amalizike, au wamle mpaka pale watakapoona wameshiba na kama bado nyama ipo, basi waitwae ile nyama na waiteketeze kwa moto, kisisalie chochote kabla hakujapambazuka..Maana yake ni kwamba kama kuna familia haitafanya hivyo, itakuwa imetenda dhambi kwa Bwana Mungu. Unaweza kuyasoma maagizo hayo vizuri katika kitabu cha (Kutoka 12:1-13).
Sasa ni kwanini Mungu alitoa hayo maagizo?
Sababu ni kwamba Bwana alikuwa ameanza kuwafundisha wana wa Israeli wamtegemee yeye kwa asilimia mia moja. Kwamba wasiwe na hofu ya kesho, watakula nini, watavaa nini.. bali akili zao zote zianze kumfikiria yeye. Kwasababu asingefanya hivyo, watu usiku ule ule wangekula kidogo na kusema tuache kingine kwaajili ya kesho asubuhi kunywea chai, hivyo wangeanza kufikiri matumbo zaidi ya kumfikiria Mungu.
Na pia utazidi kuona Mungu hata ile MANA ambayo walikuwa wanalishwa iliyotoka mbinguni, Bwana Mungu aliwakataza wasiweke akiba, wala wasiisaze, aliwaambia wakusanye chakula cha siku moja, wakile wakimalize chote wasikisaze wakile tena kesho, kwasababu hiyo kesho Mungu atawapa kingine..hivyo wasiwe na hofu ya kesho kwamba watakula nini?..Lakini baadhi yao hawakuitii sauti ya Mungu, wakawa wanakisaza matokeo yake vikatoa uvundo..
Kutoka 16:19 “Musa akawaambia, Mtu awaye yote asikisaze hata asubuhi.
20 Lakini hawakumsikiza Musa; wengine miongoni mwao wakakisaza hata asubuhi, nacho kikaingia mabuu na kutoa uvundo; Musa akawakasirikia sana.
21 Basi wakaokota asubuhi baada ya asubuhi, kila mtu kama ulaji wake ulivyokuwa; na hapo jua lilipokuwa ni kali, kikayeyuka”
Jambo hilo hilo ni somo kwetu, kwamba Tusiwe na hofu sana kuhusu maisha yetu, baada ya kuokoka.. Hatupaswi kuwa na hofu ya kupitiliza kuhusu kesho zetu, kwamba tutakula nini, au tutavaa nini, hata kama leo tunaona hakuna dalili ya kuiona hiyo kesho.Bado tunapaswa kufahamu kuwa ya kesho itajisumbukia, na Mungu atafungua mlango tu. Kama Bwana Yesu alivyosema mahali fulani..
Mathayo 6:31 “Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake”.
Baba yetu anajua tuna haja na hayo yote, hawezi kutuokoa na kutuacha yatima kabisa..yupo pamoja na sisi kuhakikisha anatuhudumia kwa mahitaji yetu ya kila siku.
Sasa kama umeona ni wakati wa kuweka akiba sasa iweke, hufanyi dhambi, lakini jiangalie jinsi unavyojiwekea hiyo akiba, kwasababu kama utajiwekea akiba na huku moyoni mwako Mungu umemwacha, na huku tumaini lako lote lipo katika hiyo akiba yako uliyojiwekea, utapotea kama yule Tajiri wa kwenye Luka 16:19.
Lakini kama utajiwekea akiba kulingana na mapenzi ya Mungu, basi utafanikiwa…
Sasa swali utajiwekeaje akiba sawasawa na mapenzi ya Mungu ?
Turudi kwenye huo mfano wa Mana. Ukiendelea kusoma mbele kidogo utaona akiba iliyompendeza Mungu ilikuwa ni ipi..Tusome.
Kutoka 16: 21 “Basi wakaokota asubuhi baada ya asubuhi, kila mtu kama ulaji wake ulivyokuwa; na hapo jua lilipokuwa ni kali, kikayeyuka.
22 Basi ikawa siku ya sita wakaokota kile chakula sehemu maradufu, kila mtu pishi mbili; na wazee wote wa mkutano wakaenda na kumwambia Musa.
23 Akawaambia, Ndilo neno alilonena Bwana KESHO NI STAREHE TAKATIFU, SABATO TAKATIFU KWA BWANA; OKENI MTAKACHOOKA, NA KUTOKOSA MTAKACHOTOKOSA; NA HİCHO KITAKACHOWASALIA JİWEKEENI KILINDWE HATA ASUBUHI.
24 Basi wakakiweka hata asubuhi, kama Musa alivyowaagiza; NACHO HAKİKUTOA UVUNDO WALA KUINGIA MABUU.
25 Musa akasema, Haya, kuleni hiki leo; kwa kuwa leo ni Sabato ya Bwana; leo hamtakiona nje barani”.
Umeona hapo?.. Walipojiwekea akiba ili kwamba kesho yake (ambayo ni siku ya sabato), wasiwe bize kutafuta hicho chakula,ILA WAWE BIZE KUMTAFUTA MUNGU..Hapo ndipo akiba yako haikuoza, Na ndiyo akiba iliyompendeza Mungu, ndio maana hicho walichokiweka akiba hakikutoa uvundo kesho yake. Lakini pale walipojiwekea akiba kwa lengo la kujikusanyia hazina ya kesho, ili wastarehe tu ndani, kesho yake wasitoke kwenda kutafuta, wakafanye anasa, walale, wacheze, waruke, wafurahi, wacheze cheze kidogo, hapo ndipo akiba yao ilipoingia mabuu..
Hivyo na sisi akiba zinazompendeza Mungu, ni zile tutakazosema…Leo nitafanya kazi sana, au wiki hii yote nitatumia muda mwingi kufanya kazi sana, na kukusanya akiba ya wiki mbili…kwasababu wiki inayokuja yote nitakuwa bize kuomba, au nitakuwa bize kuhubiri, sitapata muda wa kushughulika…Ukiweka akiba kwa malengo hayo, hapo ndipo akiba hiyo inakuwa haiozi, na zaidi ya yote Mungu anafungua milango ya baraka mara mbili zaidi sasa.. Lakini akiba ya kujiwekea mali nyingi, na huku huna malengo yoyote na Mungu, akiba hiyo inaoza, unaweka akiba ili wiki ijayo upate muda wa kulala, upate nafasi ya kwenda disko, ili utakapokuwa mzee upumzike, utakapokuwa, uwe tajiri sana wa kuheshimika, hata mpaka jumapili huendi kanisani, … Kesho utaamka haipo, imepukutika yote, hiyo miaka itafika utaikuta hiyo akiba imeingia mabuu na inatoa uvundo.
Luka 12: 16 “Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana;
17 akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu.
18 Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.
19 Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.
20 Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?
21 NDIVYO ALIVYO MTU AJIWEKEAYE NAFSI YAKE AKIBA, ASIJITAJIRISHE KWA MUNGU”.
Bwana atusaidie na kutubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo: