Kuna hatari kubwa sana kuidharau Neema ya Bwana YESU KRISTO, Katika agano la kale, kule jangwani Mungu alipokuwa anazungumza na wana wa Israeli katika mlima SINAI, Utukufu wa Mungu ulikuwa ni mkubwa kiasi kwamba hata watu wenyewe walikataa kuukaribia ule mlima kwa jinsi ulivyokuwa unatisha, kwa hofu na kwa kutetemeka walifikia hatua ya kumwambia Musa azungumze nao lakini sio Mungu. Mlima ule ulitisha sana hata kwa mnyama yoyote aliyeusogelea ilikuwa ni kifo.
Biblia inasema; katika Waebrania 12:18-25
“18 Maana hamkufikilia mlima uwezao kuguswa, uliowaka moto, wala wingu jeusi, na giza, na tufani,
19 na mlio wa baragumu na sauti ya maneno; ambayo wale walioisikia walisihi wasiambiwe neno lo lote lingine;
20 maana hawakuweza kustahimili neno lile lililoamriwa, Hata mnyama akiugusa huo mlima atapigwa kwa mawe.
21 Na hayo yaliyoonekana jinsi yalivyokuwa ya kutisha, hata Musa akasema, Nimeshikwa na hofu na kutetemeka.
22 Bali ninyi mmeufikilia MLIMA SAYUNI, NA MJI WA MUNGU ALIYE HAI, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,
23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,
24 na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.
25 Angalieni msimkatae yeye anenaye. Maana ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya nchi, ZAIDI SANA HATUTAOKOKA SISI TUKIJIEPUSHA NA YEYE ATUONYAYE KUTOKA MBINGUNI;”.
Kama biblia inavyosema sisi tulio kwenye AGANO lililo bora la DAMU YA YESU KRISTO, tunaukaribia mlima wa mbinguni(SAYUNI YA MBINGUNI) mbali na wana wa Israeli wao waliukaribia mlima wa duniani(SINAI),.. Ni dhahiri kuwa wale walioukaribia mlima wa mbinguni, ambao maelfu ya malaika wamekusanyika ndio walio karibu zaidi na Mungu kuliko hao wengine.Hivyo hawa wa mbinguni ndio wanapaswa wawe na hofu kubwa zaidi na wawe makini zaidi, kwasababu wapo karibu na Mungu, hivyo kosa moja linaweza likakugharimu mauti ya kiroho.
Na ndio maana biblia inasema
Wafilipi 2:12b-13 “ UTIMIZENI WOKOVU WENU WENYEWE KWA KUOGOPA NA KUTETEMEKA. 13 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.”
Hii tunayoiita NEEMA, ni kweli ni NEEMA lakini sio neema kwa wakati wote, Inapochezewa au kutupiliwa mbali inageuka kuwa laana mbaya kuliko zote. Biblia inasema hali ya mtu Yule aliyeidharau hali yake ya mwisho inakuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.
2Petro 2:20 “Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.
21 Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.
22 Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.”
Pale unapojiita mkristo halafu bado unakwenda kwa waganga ili upate kitu Fulani, ukijifariji kwamba utatubu tu siku moja, kwasababu neema bado ipo!! Usidanganyike NEEMA haifanya kazi kwa namna hiyo shetani anataka ufikirie hivyo ili ukumbane na mauti ya kiroho kutoka kwa Mungu mwenyewe.
Unapojiita mkristo halafu bado ni mwasherati, mlevi, mwabudu sanamu, na huku unafahamu kabisa hayo uyafanyayo sio sawa, ukijifariji utatubu, kwasababu tunaishi chini ya NEEMA, biblia inasema ingekuwa heri kwako kama usingeijua ile haki, Ndugu utaangukia hukumu ya kifo cha kiroho,na ukishafikia hiyo hatua, ndio pale injili kwako inageuka kuwa upuuzi tu masikioni mwako au hadithi za kutunga, ROHO MTAKATIFU anakuacha na kuondoka, na ile hali ya kuugua ndani juu dhambi inaondoka kwako, kutenda dhambi kunageuka kuwa ni kitu cha kawaida, hapo hata uhubiriweje injili huwezi kugeuka unasubiria moto wa jehanum.
Shetani ndiyo agenda yake sasa hivi, kuwapofusha watu na hili Neno “tunaishi chini ya neema” na kusema Mungu ataturehemu tu! Hata tuwe watenda dhambi.. Kumbuka Neema ina pande mbili, kwa Yule anayeikubali ndio italeta manufaa chanya kwake, lakini kwa Yule anayeidharau na kuitupilia mbali inageuka kuwa LAANI kubwa mno.
Waebrania 10:26-29 “Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, HAIBAKI TENA DHABIHU KWA AJILI YA DHAMBI;
27 BALI KUNA KUITAZAMIA HUKUMU YENYE KUTISHA, NA UKALI WA MOTO ULIO TAYARI KUWALA WAO WAPINGAO.
28 Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.
29 Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni KITU OVYO, NA KUMFANYIA JEURI ROHO WA NEEMA?”.
Unaona hapo usitende dhambi za makusudi ukidhani neema itaendelea kudumu siku zote maishani mwako, Ndugu huu ni wakati wa kujitazama tena maisha yako ni wapi haujakaa sawa, unalega lega au vuguvugu. Fanya bidii usimame imara angali bado Roho wa NEEMA analia ndani yako uache dhambi, fanya hima usimfanyie jeuri kabla haujachelewa, kwa maana wakati wa wokovu uliokubaliwa ni sasa.
Tubu mgeukie Kristo aliye mkuu wa uzima wako, naye ni mwaminifu atakuosha na kukupa uzima wa milele.
Mungu akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa mawasiliano, maombi/ushauri/ubatizo/ whatsapp: Namba zetu ni hizi: +255693036618/ +255789001312
Mada Nyinginezo:
JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOWAFUNULIA WATU MAANDIKO.
USIMFANYIE JEURI ROHO WA NEEMA.
Je Malaika Mikaeli ndiye Yesu mwenyewe?
Wakolosai 3:1 “Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, YATAFUTENI YALIYO JUU KRISTO ALIKO, ameketi mkono wa kuume wa Mungu.
2 YAFIKIRINI YALIYO JUU, SIYO YALIYO KATIKA NCHI.”
Kama wasafiri hapa duniani, kila siku shabaha yetu inapasa iwe ni kufika mbinguni kwa gharama yoyote ile, Biblia imetuambia “tuyatafute” na “kuyatafakari” yaliyo juu, ikiwa na maana kuwa kwa bidii zote na nguvu zetu zote, tutafute kanuni za kutufanya sisi kuingia mbinguni, tumeambiwa tuutafute kama vile tunavyotafuta fedha au kama hazina iliyositirika (Mithali 2:4),
> Mambo ya ulimwengu huu yasiwe kikwazo cha wewe kuikosa mbingu, unapaswa utumie hekima popote ulipo usiwe na kisingizio kwamba kitu fulani kimekusonga usimtafute Mungu, kumbuka wapo katika dunia hii hii matajiri wakubwa kuliko wewe na bado wanayafikiria yaliyo juu, na maisha yao ni kama wasafiri tu hapa duniani, kama mfano wa akina Sulemani katika biblia, japo alikuwa ni tajiri lakini aliyatafakari sana yaliyo juu ,
> Wapo wenye vyeo vikubwa kuliko wewe katika kizazi hiki hiki unachoishi lakini fikra zao na mawazo yao yapo mbinguni, usiku na mchana wanamwomba Bwana ufalme wake uje!, mfano ni kama Danieli alivyokuwa katika biblia,japo alikuwa mwenye cheo kikubwa lakini kutwa mara tatu alikuwa akimwomba Mungu kuhusu hatma yake na watu wake.
> Vivyo hivyo wapo maskini kuliko wewe, hawana chakula wala nguo wala mahitaji yoyote lakini mawazo yao na fikra zao si katika mambo ya ulimwengu huu bali mbinguni, japo wanapitia magumu, wanaishi kama wasafiri tu hapa duniani…Wanaishi kama Lazaro wa kwenye biblia, ingawa alikuwa anakula makombo lakini hakutupa wokovu wake chini.
> Wapo wenye shida nyingi kuliko zako; wagonjwa, walemavu, hawana watoto, mayatima, lakini kwao hayo yote si kitu, mawazo yao na fikra zao zimeelekea juu mbinguni, siku kwa siku wakijihakiki maisha yao wasianguke, wakijiepusha na maovu wasije wakaikosa mbingu.
Na wewe je! UNAYATAFUTA YALIYO JUU! Au FIKRA ZAKO ZIMEELEKEA JUU MBINGUNI? Katika hali yoyote uliyopo?..Kumbuka vya duniani vinapita, hivyo visiwe sababu ya wewe kukusonga na kuikosa mbingu. Anza sasa kutamani kwenda mbinguni.
Tunaishi katika muda wa nyongeza Bwana Yesu anakaribia kurudi.
Ubarikiwe.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.
MUNGU ALIKUWA ANAONGEA NA NANI ALIPOSEMA NA “TUMFANYE MTU KWA MFANO WETU”,(MWANZO 1:26)?
KATIKA BIBLIA KUNA UFUFUO WA AINA NGAPI?
Huu ni wakati wa kuwa makini sana juu ya hatma ya maisha yetu ya rohoni, kwasababu tusipokuwa makini katika nyakati hizi na kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda tunaweza tukajikuta tunaangukia katika vifungo vya shetani pasipo hata kujijua.
Kumbuka shetani sasa hivi anatenda kazi ndani ya KANISA la Mungu, hawezi kutilia mkazo sana kwa watu wa nje walio waovu kwasababu hao ameshawapata siku nyingi..anakutafuta wewe unayejiita mkristo unayejiona umesimama. Na unadhani atakupatia wapi zaidi ya kanisani.? Huko ndiko kiti chake cha enzi alipokiamishia.
Bwana Yesu alizungumza hivi;
Mathayo 13:24-30
24 Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake;
25 lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.
26 Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu.
27 Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu?
28 Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye?
29 Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing’oa ngano pamoja nayo.
30 Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.
Kumbuka magugu na ngano ni vitu vinavyofanana sana, kwa kuviangalia huwezi ukavitofautisha mpaka vitakapokuwa vikubwa na kutoa mazao, Katika mfano huo tunafahamu kuwa aliyepanda hizo mbegu njema ni BWANA YESU na shamba lake ni KANISA. Tunaweza tukaona jinsi kanisa la kwanza lilivyokuwa safi, takatifu lisilojichanganya na mafundisho yoyote ya uongo au mapokeo yeyote ya kibinadamu, ni kanisa lililokuwa halina dosari,
Lakini baada ya shetani kuona hilo alianza kuja na mbinu za kuliharibu, hivyo aliiga njia ile ile ya kupanda mbegu kama vile Bwana alivyofanya. Ndipo akaanza kwanza kwa kupenyeza mafundisho ya uongo katikati ya kanisa la Mungu, kisha ile mbegu ya uongo ilipomea baadaye ikageuka na kuwa dini, na kukaa katikati ya kanisa la Mungu. Kuanzia hapo hizi mbegu mbili zikawa zipo pamoja zikishindana katika kanisani la Kristo.(Magugu na Ngano)
Mungu kwa kulifahamu hilo aliruhusu vyote vimee kwa pamoja mpaka wakati wa mavuno utakapowadia kwasababu kama tulivyoona magugu yakiwa machanga ni ngumu kuyatofautisha na ngano, yanafanana sana kwa tabia zao. Na Mungu aliposema yaache yakue pamoja ni kiashiria kuwa yote yapate mvua kutoka kwa Mungu.(Mathayo 5:45). Ikiwa na maana kuwa Mungu aliyaruhusu yafanikiwe katika njia zao kama vile tu zile mbegu njema zifanikiwavyo mpaka wakati wa mavuno utakapowadia. Yote yananyeshewa mvua, kumbuka hata manabii wa uongo wanatabiri kwa jina la Bwana na inatokea, wanaponya na kutoa pepo kwa jina la Yesu na yanawatii, lakini siku ile Bwana atawaambia siwajui nyinyi mtendao maovu. Kwasababu hawa walinyeshewa mvua moja na ngano halisi lakini ndani yao walikuwa ni magugu.
Hivyo Kanisa katoliki lilianza kujitokeza katika kanisa la Mungu kama GUGU la kwanza, enzi zile za kanisa la kwanza, lilianza na mafundisho tu (MBEGU), baadaye likaota mizizi na kujiundia dini inayofanana na ukristo katika kanisa, likazidi kusambaa katika shamba la Mungu na kusonga zile mbegu halisi za Mungu na ndio maana tunaona hili kanisa lilianza kuharibu mafundisho ya NENO LA MUNGU na kupachika mafundisho ya uongo na kama tunavyofahamu tabia halisi ya gugu ni kuharibu kile kilicho halisi, na ndio maana baadaye tunavyosoma katika historia liliuawa watakatifu wa Mungu zaidi ya milioni 68 waliojaribu kwenda kinyume na mafundisho yake ya uongo.
Na lilipofikia kilele likazaa na magugu mengine mengi yanayofanana ni hilo, yakifanya kazi moja, kuiharibu mbegu halisi ya Mungu. Lakini biblia inasema wakati wa mwisho ambao ndio tuliopo sasa, yale magugu na ngano vitatenganishwa, yale magugu yataanza kwanza kwa kufungwa matita matita kwasababu yapo mengi,
JE! HAYA MATITA MATITA NI NINI?..Haya si mengine zaidi ya MADHEHEBU, na watakaoyafunga ni akina nani? Hawa Si wengine zaidi ya wanaojiita viongozi wa dini lakini ndani ni mitume wa uongo (2Wakoritho 11:13).
Mhubiri yoyote anayekupeleka kwenye dini yake zaidi ya kukupeleka kwa Kristo huyo ni mvunaji anayekufunga katika mojawapo ya tita la magugu. Kiongozi anayekufundisha mafundisho yasiyotokana na utakatifu, anakuambia tu! Mungu ni wa rehema, huku hana habari na mambo ya toba au kuhubiri utakatifu yeye anakazania mambo ya ulimwengu huu tu, ujue huyo ni mvunaji anayetaka kukufunga katika mojawapo ya tita la magugu lililoandaliwa kwa ajili ya kuchomwa moto.
Mhubiri anayekuhubira kutwa kuchwa mafanikio tu! Agusii hata siku moja hatma ya maisha yako ya rohoni, anayekuhubiria Kristo harudi leo wala kesho..mkimbie huyo ni mvunaji wa siku za mwisho kazi yake ni kuwafunga watu wa namna hiyo wasiotaka kujihusisha na mambo ya Mungu bali wajihusishao na mambo ya ulimwengu huu tu.
Ukiona kanisa linakuambia hakuna kuzimu na mateso yake, au halitaki kudumu katika NENO LA MUNGU peke yake,linakuongoza katika ibada za sanamu ambazo Mungu amezipinga vikali, kimbia haraka sana hilo ni TITA la kukusanya watu wa dizaini hiyo wasiotaka kudumu kutenda mapenzi ya Mungu..
2Wathesalonike 2:10 “na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; KWA SABABU HAWAKUKUBALI KUIPENDA ILE KWELI, WAPATE KUKOLEWA.
11 Kwa hiyo Mungu awaletea NGUVU YA UPOTEVU, WAUAMINI UONGO;
12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.”
Na Kumbuka kila siku hawa wavunaji(Manabii wa uongo) na haya matita ya magugu yanazidi kuongezeka kuonyesha kuwa huu ni wakati wa mavuno wa siku za mwisho.
LAKINI NGANO HALISI NI IPI
Ukisoma mfano huo kwa makini utaona kuwa NGANO HALISI haijakusanywa katika matita matita mengi kama magugu yalivyofanywa, bali Ngano imekusanywa pamoja mara moja tu na kupelekwa ghalani. Kuonyesha kuwa bibi-arusi wa Kristo hatakuwepo kati ya mojawapo ya hivyo vikundi, Bibi-arusi hana utambulisho wa kimadhehebu. Baada ya kukusanywa maramoja atapelekwa ghalani (mbinguni). Ndugu tunaishi katika wakati wa bibi-arusi wa Kristo kukusanywa kwa ajili ya unyakuo. Na anakusanyikia wapi?.
Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake katika
Mathayo 24: 23 “Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki.
24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.
25 Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele.
26 Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki.”
Hii Ikiwa na maana kuwa katika siku za mwisho watatokea mitume na manabii wengi wa uongo, na zitatokea dini nyingi na madhehebu mengi ya uongo, na kila moja likidai kuwa lenyewe lina Kristo, ili tu yapate kuwakufunga watu kwenye matita yao..lakini Bwana alisema yatakapowafuata na kuwaambia hivyo msisadiki?. Na ndipo wanafunzi wake wakamuuliza..kama hatutawasidiki hao basi tukusanyike wapi sasa? Jibu lake lilikuwa ni hili.
Luka 17: 37 “Wakajibu, wakamwuliza, WAPI, BWANA? Akawaambia, ULIPO MZOGA, NDIPO WATAKAPOKUTANIKA TAI.”
Mzoga ni NENO LA MUNGU, na TAI ni BIBI-ARUSI, Hivyo katika siku hizi za mwisho bibi-arusi safi wa Kristo hatakusanyika katika madhehebu na dini bali atakusanyika katika NENO LA MUNGU tu..yeye hatafungwa na dini bali atafungwa, ‘’na nini NENO linasema’’ Hicho tu. Hii ndio ndio nguvu Mungu aliyoiachia sasa hivi kwa bibi-arusi wake, kurudi katika imani ya Mitume, Biblia.
Hivyo ndugu jitathimini je! na wewe umefungwa kama magugu kwenye matita tayari kwa kuchomwa au unakusanywa ghalani mwa Mungu kwa NENO lake?. Kama umefungwa huko toka, sio kwa miguu bali kwa kugeuzwa moyo wako na kuligeukia NENO linachosema na sio mapokeo ya dhehebu. Kwasababu biblia inatuambia
1Petro 1:23 “Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; KWA NENO LA MUNGU LENYE UZIMA, lidumulo hata milele.”
Hivyo Umeona hapo? Bibi-arusi amezaliwa kwa mbegu isiyoharibika KWA NENO LA MUNGU tu, na sio kitu kingine.
Ni maombi yangu kuwa utazaliwa mara ya pili kwa NENO LA MUNGU na kumtazama Kristo peke yake aliyekufia msalabani ili ufanyike kuwa ngano na sio gugu.
Ubarikiwe.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
USIMFANYIE JEURI ROHO WA NEEMA.
WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU
“Moto hufa kwa kukosa kuni’’, na ndivyo ilivyo kwa uasherati
Mungu kamuumba kila mwanadamu na maamuzi yake binafsi yasiyoweza kuingiliwa na kitu kingine chochote, Mungu kayaheshimu maamuzi hayo kiasi kwamba hata yeye mwenyewe hajajipa mamlaka ya kuyaingilia japokuwa anao uwezo huo, si zaidi shetani? hawezi kumwamulia mtu mambo!!. Ukiamua kuwa mlevi hakuna kitu chochote kitakachoweza kukuzuia, ukiamua kuwa mchawi hakuna yeyote atakayeweza kukuzuia..Vivyo hivyo ukiamua kuwa mtakatifu hakuna chochote kitakachoweza kukuzuia.
Jambo analolifanya Roho Mtakatifu ni kumshawishi au kumpa mtu kila sababu ya yeye kutokufanya maamuzi ya jambo fulani ovu, na mtu anapoamua kutii ndipo Roho anapozidi kuwa msaada mkubwa kwake katika kuenenda katika mwenendo mtakatifu.
Vivyo hivyo na shetani naye anachofanya sio kumlazimisha mtu kufanya maamuzi fulani bali anamshawishi kwa kumjengea mazingira yote ya yeye kuchukua uamuzi wa kufanya uovu, na mtu anapomtii ndipo shetani anapapata nafasi zaidi ya kummiliki na kumuharibu. Mwisho wa siku unasikia mtu ana pepo la usherati, halikumwingia hivi hivi ni yeye mwenyewe alifungua mlango mahali fulani na kuliruhusu.
Mtu anaamua kuwa mzinzi mara baada tu ya kuyatii mahubiri ya shetani katika akili yake. Fahamu tu biblia inasema
1Wakoritho 6: 18 “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.”
Na pia inasema.. Mithali 6:32 “Mtu aziniye na mwanamke HANA AKILI KABISA; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.” . Unaona hapo?? mwasherati wa aina yoyote ile yupo katika HATARI kubwa sana kuliko mtu mwingine yeyote.
Kwanini wengi leo wanashindwa na dhambi ya uasherati?
Ni Kwasababu ile ile, wanachukuliana na mahubiri ya shetani katika maisha yao. na kuyatii. Na Mahubiri hayo ni yapi?.
Hii ni nyenzo kubwa sana shetani ameitumia kwa kizazi hiki kukiangamiza, Hii ni njia yenye ushawishi mkubwa kuliko zote, kiasi kwamba mtu akijiingiza huko uasherati hawezi akaukwepa kwa namna yoyote iwe ni ameshaingia kwenye ndoa au hajaingia, iwe ni kijana, au mzee haikwepeki, mtu huyo atabakia kuwa mwasherati au mzinzi daima. Na hapo shetani hajahusika kukufanya ukafanye uasherati hapana ni wewe mwenyewe kwa ufahamu wako kabisa na kwa miguu yako umeamua kuwa hivyo. Kama ingekuwa ni shetani kakuvaa ufanye hivyo, siku ile ya hukumu Mungu asingekuhukumu wewe angemuhukumu shetani.Lakini biblia inasema waasherati watahukumiwa… Na mtu anayetazama hivi vitu kama hatadondokea kwenye uasherati moja kwa moja basi ataishia kwenye masturbation ambayo nayo ni machukizo makubwa sana mbele za Mungu.
Biblia inasema 1Wakoritho 15: 33 Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema . “ Haya ni mahubiri ambayo utakuta shetani anamuhubiria mtu pasipo hata yeye mwenyewe kujua, utakuta vijana au wazee kutwa kuchwa wanazungumza habari za wanawake, na wanawake vivyo hivyo utawakuta wana jadili habari za wanaume muda wote, lakini muda wa kutafakari mambo ya muhimu ya Mungu hakuna, sasa hapo watu kama hao ni rahisi sana kutawaliwa na roho za tamaa, kwasababu vichwa vyao wakati wote vimejazwa hayo mafundisho ya zinaa. Biblia inasema “hata uasherati usitamkwe kati yenu.”Utakuta kijana muda wote anaumalizia mtandaoni..ukitazama ni kitu gani anafanya, utagundua kuwa anachati katika magroup ambayo misingi yake ni uasherati, sasa kwa tabia hiyo haiwezekani wewe kuushinda uasherati hata uombeweje ni wewe tu kuamua kuacha hivyo vitu na kuanza kutii mahubiri ya Roho Mtakatifu ndani yako.
Vimini, suruali, kaptura, nguo zinazobana na zinazoonyesha vifua na migongo wazi kwa wanawake n.k., hivi vyote ni vichecheo vya uasherati, mavazi hayo yalibuniwa kwa kazi hizo, kuwavuta wazinzi wasogee karibu na wewe, hivyo mtu anayejiita mkristo na kuanza kuzivaa moja kwa moja anakaribisha uwepo wa uzinzi ndani yake.
Kusikiliza miziki ya kidunia hii pamoja na filamu za kimapenzi ni kichecheo kikubwa cha kubebwa na roho hizi, asilimia 99 ya miziki yote ya kidunia zina mahudhui ya kiasherati ndani yake unategemea vipi uepukane na tabia hizo?. Na ndio maana utakuta mtu analalamika hawezi kuacha kuwa mzinzi/mwasherati wakati muda wote anaumalizia kwenye vitabu, filamu na tamthilia za kimapenzi. Viache hivi vitu kwanza na ndipo utakapoanza kuona wepesi.
Na mambo hayo yakishakaa ndani yako sana, sasa yanakuwa yakijirudia rudia yenyewe tu kwenye akili yako, mpaka inakuwa ngumu kuyakwepa kwasababu ndio yaliyoujaza moyo wako,
Hivyo ndugu ukitaka kuushinda uasherati usitafute kuombewa, dawa ipo ndani yako mwenyewe kwanza ni kuchukua uamuzi wa kukataa kutii mahubiri yote ya shetani, na kuanza kumtii Roho Mtakatifu anapougua ndani ya moyo wako, ukifahamu kuwa mtu atendaye mambo hayo mwisho wake ni kuzimu… kwa kufanya hivyo utampa Roho Wa Mungu nafasi ya kukutengeneza up mpaka mwisho wa siku unajikuta ile tamaa imezikwa kabisa, na kuweza kuishi maisha pasipo kutamani uasherati kabisa..Hivyo kataa hayo mahubiri yote ya shetani anayokuletea kupitia mtandao,(Pornography) na picha za uchafu, kwa kupitia kuchat katika mambo yasiyofaa, kwa kupitia mazungumzo mabovu, na kampani zisizo za ki-Mungu, kwa kupitia filamu, vitabu, tamthilia na miziki ya kidunia pamoja na mavazi ya kikahaba, Anza kukaa mbali kwanza na hivyo vitu vyote, na ndipo utakapoanza kuitawala mapenzi yako
Na pia mawazo machafu yanapokujia kichwani kwako ni kuyakataa kwa kutafakari NENO LA MUNGU badala yake, ukizingatia hayo kidogo kidogo Roho Mtakatifu anaanza kuyazika ndani yako, mpaka kufikia hatua ya kutoweka kabisa na kuwa na uwezo wa kujitawala. Kwasababu biblia inasema
(Mithali 26: 20a, “MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI”)….Hivyo uasherati pia hufa kwa kukosa vichochezi. Unapojitenga na vichocheo vyote hivyo hata ile tamaa ya kufanya uasherati inakuwa haipo. Roho Mtakatifu anaizika mpaka inafikia hatua watu watakushangaa unawezaje kuishi muda wote huo pasipo kuwa mwasherati?.
Lakini kama hutaki kuweka chini hivyo vitendea kazi vya uasherati kamwe hutaweza kumshinda shetani.Kwasababu biblia pia inasema WAASHERATI WOTE sehemu yao ni katika lile ziwa la Moto(Ufunuo 21:8)..Hivyo ndugu iogope hukumu ya Mungu, anza kubadilika sasa kimbia uasherati. Mwili wako ni Hekalu la Roho Mtakatifu, na mtu auharibuye Mungu kasema atamuharibu mtu huyo.
Ubarikiwe.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.
WALIO NA HEKIMA NDIO WATAKAOELEWA.
NINI TOFAUTI KATI YA UZINZI NA UASHERATI ?
TAZAMA KRISTO YUPO HAPA,AU YUKO KULE MSISADIKI.
Kitabu cha Ayubu sura ya 28, kinaeleza jinsi HEKIMA ilivyojificha mbali sana kiasi kwamba mwanadamu pamoja na ujuzi wake mwingi na maarifa yake mengi hajaipata, licha ya kwamba amefanikiwa kuchimba mahandaki makubwa ili kutafuta madini ndani yake lakini pia hajaipata, licha ya kwamba anayo teknolojia kubwa ya kuwa na vyombo maalumu vya kumfanya kutua mwezini, lakini alipofika na huko hakuikuta vile vile, biblia inasema wanyama nao hawajui inapatikana wapi, kadhalika na vitu vya asili kama bahari na milima havitambui ilipo,
Mstari wa 1-15
“1 Hakika kuna shimo wachimbako fedha, Na mahali wapatapo dhahabu waisafishayo.2 Chuma hufukuliwa katika ardhi, Na shaba huyeyushwa katika mawe.
3 Binadamu hukomesha giza; Huyatafuta-tafuta hata mpaka ulio mbali, Mawe ya giza kuu, giza tupu.
4 Hufukua shimo mbali na makao ya watu; Husahauliwa na nyayo zipitazo; Huning’inia mbali na watu, huyumba-yumba huko na huko.
5 Katika ardhi ndimo kitokeamo chakula; Na chini yake hupinduliwa kama kwa moto.
6 Mawe yake ni mahali zipatikanapo yakuti; Nayo ina mchanga wa dhahabu.
7 Njia ile hapana ndege mkali aijuaye, Wala jicho la tai halijaiona;
8 Wanyama wakali wajivunao hawajaikanyaga, Wala simba mkali hajaipita.
9 Huunyoshea mwamba wa gumegume mkono wake; Huipindua milima hata misingi yake.
10 Hukata mifereji kati ya majabali; Na jicho lake huona kila kito cha thamani
11 Hufunga vijito visichuruzike; Na kitu kilichostirika hukifunua.
12 BALI HEKIMA ITAPATIKANA WAPI? NA MAHALI PA UFAHAMU NI WAPI?
13 MWANADAMU HAJUI THAMANI YAKE, WALA HAIONEKANI KATIKA NCHI YA WALIO.
14 Vilindi vyasema, Haimo ndani yangu; Na bahari yasema, Haiko kwangu.
15 HAIPATIKANI KWA DHAHABU, WALA FEDHA HAITAPIMWA IWE THAMANI YAKE.”
Biblia inaendelea kueleza kama Hekima ingekuwa inapatikana kwa thamani ya dhahabu au fedha basi ingeshapatikana na watu siku nyingi, au ingekuwa inapatikana kwenye vilindi au baharini ingekuwa ni heri, lakini huko kote mwanadamu ameshafika na hakuikuta. Lakini je! Inapatikana wapi?.
Biblia inaendelea…
“16 Haiwezi kutiwa thamani kwa dhahabu ya Ofiri, Wala kwa shohamu ya thamani nyingi, wala kwa yakuti ya samawi.17 Dhahabu na vioo haviwezi kulinganishwa nayo; Wala kubadili kwake hakutakuwa kwa vyombo vya dhahabu safi.
18 Havitatajwa fedhaluka wala bilauri; Naam, kima cha hekima chapita marijani.
19 Yakuti ya rangi ya manjano ya Kushi haitasawazishwa nayo, Wala haitatiwa kima kwa dhahabu safi.
20 BASI HEKIMA YATOKA WAPI? NA MAHALI PA UFAHAMU NI WAPI?.
21 Kwa kuwa imefichwa mbali na macho ya wote walio hai, Na kusitirika na ndege wa angani.
22 Uharibifu na Mauti husema, Tumesikia habari zake kwa masikio yetu.
23 Mungu ndiye aijuaye njia yake, Naye anajua mahali pake.”
Viumbe vyote vya asili na visivyo vya asili na vyenyewe pia vinasema havijui makao yake, Ni Mungu pekee ndiye anayejua makao yake. Na tunasoma baada ya wote kushindwa kufikia makao ya HEKIMA na UFAHAMU, Ndipo Mungu naye akaazimu kuingilia kati na kuchunguza makao yao yako wapi?.. Naye pia kama mwanadamu aliingia katika uchunguzi wa kina na utafiti wa hali ya juu, akapanda milimani, akashuka vilindini, akashuka zaidi mpaka kuzimu, akarudi kwenye mbingu, akapitia sayari zote akazunguka kote kote kila mahali, akaingia mpaka kwenye mioyo ya wanadamu kuitafuta hekima, hakuna mahali ambapo hakufika. Ndipo mwishoni akaipata, na alipoipata akaihakiki na kuithibitisha, na ndipo akaja KUWAAMBIA WANADAMU.
Mstari wa 24-28 inaendelea kusema..
“24 Maana anatazama hata miisho ya nchi, Na kuona chini ya mbingu nzima.25 Apate kuufanyia upepo uzito wake; Naam, anayapima maji kwa kipimo.
26 Hapo alipoiwekea mvua amri, Na njia kwa umeme wa radi.
27 Ndipo alipoiona na kuitangaza; Aliithibitisha, naam, na kuichunguza.
28 Kisha akamwambia mwanadamu, TAZAMA, KUMCHA BWANA NDIYO HEKIMA, NA KUJITENGA NA UOVU NDIO UFAHAMU.”
Maneno hayo ndiyo aliyomalizia Bwana, baada ya utafiti na uchunguzi wa hali ya juu, Na sisi tunajua hakuna mwanadamu mwenye Akili zaidi ya Mungu, Utafiti wa Mungu ni bora mara nyingi zaidi kuliko utafiti wa wanasayansi au wanajimu, na wanafalsafa. Kama wanasema HEKIMA ni kusoma sana, au kuwa na akili nyingi za kimasomo au ujasiriamali, au kuwa tajiri sana, kama wao wanasema hekima ni kuwa maarufu, kama wao wanasema ufahamu ni kuwa na ujuzi wa kufanya jambo fulani, lakini sisi tunajua Bwana katuonyesha HEKIMA ni nini, na ufahamu unapatikana wapi?.. NI KUMCHA YEYE, NA KUEPUKANA NA UOVU. Hilo tu.! Tukizingatia hayo mbele za Mungu tutakuwa ni watu wenye hekima sana na Ufahamu mkubwa.
Sulemani ingawa alikuwa ni mtu mwenye maarifa mengi na ufahari mkubwa ambao hakuna mtu aliyekuwa mfano wake, tangu wakati ule hata sasa, Ni mtu aliyekuwa na elimu pamoja na ujuzi wa viumbe vyote, ikiwepo miti, samaki, wanyama, alikuwa na ujuzi wa hali ya juu kiasi cha kutunga nyimbo na mashairi kwa hekima nyingi sana, alikuwa na uwezo wa kutenganisha hukumu ambapo vitu kama hivyo vilihitaji watu wenye akili nyingi kama mahakimu. Ilifika wakati yeye mwenyewe alikiri kuwa hakukosa lolote, wala hakujinyima nafsi yake kwa chochote. Lakini pamoja ya kwamba aliipata hekima yote ya kidunia, aliisahau HEKIMA MOJA YA MUNGU.
Kwa Kupuuzia amri za Mungu, na kuanza kwenda kuoa wake wageni, na kuabudu miungu migeni, akalitangua lile NENO walilopewa wafalme kwa amri ya Musa kwamba mtu yeyote atakayekuja kuwa mfalme kati yao, asijiongezee wake, wala mali kupita kiasi, wala asiabudu miungu mingine, zaidi ya yote anapaswa aandike amri za Mungu katika chuo ajifunze huko siku zote za maisha yake namna ya kumcha Mungu katika ufalme wake.(Kumbukumbu 17:14-20). Lakini yeye hakufanya hivyo akakaidi.
Na alipogundua makosa yake kuwa aliiacha hekima hasaa inayopatikana katika kumcha Mungu, akaishia kusema UBATILI MTUPU, KILA KITU NI UBATILI.!
Sulemani alisema katika..
Mhubiri 2: 10 “Wala sikuyanyima macho yangu cho chote yalichokitamani; wala sikuuzuia moyo wangu katika furaha yo yote; maana moyo wangu ulifurahi kwa sababu ya kazi yangu yote, na hii ilikuwa sehemu yangu katika kazi yangu yote.
11 Kisha nikaziangalia kazi zote zilizofanywa kwa mikono yangu, na taabu yote niliyotaabika katika kuzitenda; na tazama, YOTE NI UBATILI na kujilisha upepo, wala faida hakuna chini ya jua.”
Na mwisho wa siku Sulemani alimalizia na kusema….”
Mhubiri 12:13-14
“13 HII NDIYO JUMLA YA MANENO; yote yamekwisha sikiwa; MCHE MUNGU, NAWE UZISHIKE AMRI ZAKE, MAANA KWA JUMLA NDIYO IMPASAYO MTU.
14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.”
Hivyo ndugu, kweli zipo hekima nyingi duniani na sio kwamba ni mbaya ni nzuri na nyingine zinahitajika sana katika jamii zetu lakini usisahau, Mungu mbele zake HEKIMA NI MOJA TU!. Anayoitambua yeye, nayo ni KUMCHA BWANA , NA KUEPUKANA NA UOVU. Ni heri ukakosa hizo nyingine lakini usiikose hiyo. Ichukie dhambi mpe Bwana maisha yako, mche yeye, Elimu yako, ujuzi wako, mali zako ni vizuri kuwa nazo lakini zisije zikakufikisha mahali ukasema ni ubatili mtupu kama alivyofanya Sulemani, kwa jambo moja tu, ya kupuuzia amri za Mungu sasa. Kwasababu Bwana alishasema mwenyewe..Hekima ya ulimwengu huu ni upuuzi mbele zake (1Wakoritho 3:19). Hivyo kuwa makini unavyoenenda katika ulimwengu huu. Kumbuka YESU KRISTO ndiye HEKIMA YA MUNGU.(1wakoritho 2:6-9)
Mungu akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
HUDUMA YA (ELIFAZI, BILDADI, NA SOFARI).
Bwana Yesu aliposema “UTAFUTENI kwanza ufalme wake na haki yake..”. Alikuwa na maana kubwa zaidi kuliko inavyodhaniwa,.kitu kama ni cha kutafuta inamaana kuwa kimesitirika na kinahitaji nguvu ya ziada kukipata. Kumbuka tunapompa Bwana maisha yetu leo haimaanishi kuwa tumeupata ufalme wa Mungu, hapana bali tumepiga hatua ya kwanza katika kuutafuta ufalme wake. Ni sawa na mtu anapokwenda kuandikishwa shuleni darasa la kwanza, haimaanishi kuwa tayari ameshakuwa msomi, hapana bali hiyo ni hatua ya kwanza tu ya yeye kupata elimu na ndivyo ilivyo katika ukristo. Unapompa Bwana maisha yako leo haimaanishi kwamba umeshaupata ufalme tayari.
Ndipo Bwana Yesu akawajibu alipoulizwa katika
Luka 17:20-21
“20 Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza;
21 wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.”
Wakati huo watu walidhani kuwa ipo siku ufalme wa Mungu utawajilia juu yao na kuutambua, lakini yeye alisema tazama ufalme wa Mungu tayari umo ndani yenu. Ikiwa na maana kuwa ni kitu kinachopatikana kwa mtu yoyote na mahali popote alipo atakapo. Sasa ni jukumu lake yeye kujua namna ya kuufanya uwe wake, kwasababu ni kweli unaweza ukawa upo ndani yako lakini usiwe wa kwako.
Mfano huo unalingana na utafutaji wa mali, kwamfano ukihitaji pesa huwezi ukasema unaenda kuzichukua benki kuu kwasababu tu benki kuna mkusanyiko mkubwa wa Fedha. Hutapata chochote, lakini badala yake ulitambua kuwa fedha hazipatikani kule bali zinapatikana hata hapo ulipo, zipo katikati ya jamii ya watu unaoishi nao. Ni wewe tu kufanya bidii kuzitoa kwao kwa njia halali na kuzifanya ziwe zako, sasa ili kwamba zoezi hilo lifanikiwe inakupasa ukafanye kazi kwa nguvu zako uzipate pengine ukafanye biashara, au ukauze duka, au ukalime shamba, n.k. ili uzipate, na ndipo kwa bidii zako utazipata baada ya kuzisumbukia.
Na ndio maana Bwana Yesu alisema ufalme wa Mungu hautashuka kwa kuusubiria bali upo katikati yetu, mioyoni mwetu, lakini haimaanishi kuwa kwasababu upo ndani yetu tumeshakwisha kuupata hapana bali inahitajika bidii ya ziada ili kuufanya uwe wa kwetu.Kama vile fedha ipo katikati yetu lakini si ya kwetu mpaka tuifanyie kazi. Zipo pia gharama za kuupata ufalme wa Mungu na kazi pia ipo.
Mahali pengine Bwana alisema Mathayo 11: 12 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.” Kama mkristo inahitajika bidii kumjua Mungu ili kuelewa kwa kina mapenzi yake ndani yako.
Tunaupataje ufalme wa Mungu?
Hii inakuja kwa kutaka kujifunza jambo jipya kila siku lihusulo Imani yako. Kwa kuyachunguza maandiko siku baada ya siku, kama vile fedha isivyotafutwa kwa chanzo kimoja, vivyo hivyo hata kwa ufalme wa mbinguni, unapaswa kutokugota katika ngazi moja ya kiroho siku zote, (Mathayo 13: 52 Akawaambia, Kwa sababu hiyo, kila mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale).
Bwana alisema heri walio na njaa na kiu ya haki maana watashibishwa, biblia inasema pia..Tuutafute ufalme wa Mungu kama tunavyotafuta fedha (Mithali 2:4). Haupaswi kuridhika katika hali moja hiyo hiyo ya kiroho bali kila siku unapaswa utafute chanzo bora zaidi cha kuongeza maarifa yako juu ya Mungu. Paulo alimwambia Timotheo “JITAHIDI KUJIONYESHA KUWA UMEKUBALIWA NA MUNGU, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.”
Hakuna mwanafunzi kila siku yupo kwenye ngazi moja tu, kila siku anavuka daraja. Tatizo kubwa lililopo katikati ya wakristo ni kuridhika na mapokeo ya madhehebu yao, na kupelekea kutokupiga hatua mbele, hawa biblia inawafananisha na wale wanawali wapumbavu, waliobeba taa zao bila kuwa na mafuta ya ziada pindi walipokuwa wanakwenda kumlaki Bwana wao (Mathayo 25). Lazima uwe na mafuta ya ziada ndugu, kwa kuutafuta ufalme wa Mungu maishani mwako kila siku.
FAIDA ZA KUUPATA UFALME WA MUNGU.
Unapoupata ufalme wa Mungu ndani yako, unakuwa sio mtu wa kutikiswa na kila upepo wa elimu, na mafundisho potofu ya uongo. Unakuwa na uwezo mkubwa wa kupambanua ukweli na uongo, na pia unaongeza uhusiano wa kipekee na Mungu wako, na mwisho unapokea ahadi za kipekee katika ule ufalme wa milele unaokuja kwenye mbingu mpya na nchi mpya.
Mitume wa Bwana Yesu pindi walipoingia gharama ya kuutafuta wakaahidiwa ahadi kubwa na za kipekee, Bwana aliwaambia katika ufalme ujao wataketi pamoja naye wakiyahukumu makabila 12 ya Israeli,
Vivyo hivyo na wote katika makanisa 7 walioshinda walipewa ahadi za kipekee vile vile, katika huo ulimwengu unaokuja, Kanisa letu la mwisho linalofananishwa na kanisa la LAODIKIA, Bwana aliahidi wale watakaoshinda atawapa nafasi ya kuketi pamoja naye katika kiti chake cha enzi kama yeye alivyoshinda.(Ufunuo 3:21). Kumbuka sio kila mkristo atakayeenda mbinguni atapokea hizo ahadi za kipekee, bali ni wale tu walioupata ufalme wa Mungu hapa duniani, na kushinda kama Bwana wao. Mambo yote yanakamilika hapa duniani mbinguni ni kuvikwa mataji tu. Hivyo kwa bidii shika sana ulichonacho asiye mwovu akalitwaa taji lako. asema BWANA.
Ufunuo 22: 12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.”
Jitahidi ndugu kuutafuta ufalme wa Mungu sasa angali muda tumepewa, kwa maana unapatikana kwa nguvu kama vile fedha inavyopatikana kwa nguvu kwasababu ni kitu cha thamani.
Uufanye imara wito wako na uteule wako kila siku na Bwana mwenyewe atakusaidia.
Ubarikiwe sana.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA JIKANE MWENYEWE?
Wana wa Israeli walipokuwa wanatoka Misri na kwenda katika nchi yao ya ahadi, walikuwa ni umati mkubwa sana wa kabila 12 za Israeli, Hivyo ili hayo makabila yote yaweze kukaa kila moja kivyake kwa amani iliwapasa waigawe ile nchi katika vipengele 12. Hivyo mipaka ikawekwa kama alama kwa kila kabila kwamba hiyo mipaka isivukwe na mtu yeyote yule kuingilia upande wa wenzake, Na atakaye jaribu kusogeza au kuondoa mpaka laana itamwangukia. Hivyo huo utaratibu uliendelea kujulikana kwa vizazi vyote vya wana wa Israeli kwamba mipaka iliyowekwa na wazee wa kale kwa kila kabila haitakiwi kuguswa kwa namna yeyote ile ibaki kama ilivyo.
Musa aliandika katika Kumbukumbu 19:14 “Usiiondoe alama ya mpaka wa jirani yako, waliouweka watu wa kale katika urithi wako, utakaorithi ndani ya nchi akupayo Bwana, Mungu wako, uimiliki.”
Na pia inasema..Kumbukumbu 27: 17 “NA ALAANIWE AONDOAYE MPAKA WA JIRANI YAKE. Na watu wote waseme, Amina.”
Hivyo hofu kubwa ilikuwepo kwa Israeli, kwa yeyote aliyejaribu kufanya tendo kama hilo.
Kadhalika hata katika Israeli ya Rohoni (KANISA) ambalo ndio sisi, nayo imewekewa mipaka na wazee wa zamani isivukwe wala isiondolewe, na kwa mtu yeyote atakayejaribu kufanya hivyo ataangukia laana nzito kutoka kwa Mungu mwenyezi. Mithali 22:28 inasisitiza… “ USIIONDOE ALAMA YA MPAKA WA ZAMANI, ULIOWEKWA NA BABA ZAKO.”
> MIPAKA YETU KWA SASA NI NINI?..Mipaka yetu ni NENO LA MUNGU.
> Na wazee wetu wa zamani ni wakina nani? . Ni MITUME NA MANABII.
Biblia inasema Waefeso 2:20 “Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.”. Sisi kama kanisa la Kristo tumejengwa juu ya mafundisho ya mitume na manabii, wale mitume wa Bwana Yesu Kristo na manabii wa agano la kale, hao ndio waliotuwekea mipaka ya IMANI yetu kwamba isivukwe zaidi ya hapo kwasababu maagizo waliyopokea yalikuwa ni moja kwa moja kutoka kwa Mungu mwenyewe na ndio maana Paulo kama mmoja wa mitume wa Kristo alisema..
Wagalatia 1: 8 “LAKINI IJAPOKUWA SISI AU MALAIKA WA MBINGUNI ATAWAHUBIRI NINYI INJILI YOYOTE ISIPOKUWA HIYO TULIYOWAHUBIRI, NA ALAANIWE.
9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.
10 Maana, sasa je! Ni wanadamu ninaowashawishi, au Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.
11 Kwa maana, ndugu zangu, injili hiyo niliyowahubiri, nawajulisha ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu.
12 Kwa kuwa sikuipokea kwa mwanadamu wala sikufundishwa na mwanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo.”
Unaona hapo hatari iliyopo katika kuvuka mipaka ya Injili iliyohubiriwa na mitume?. (Mipaka iliyowekwa na mababa?). Laana imekwisha tamkwa.
NA KUVUKA MIPAKA NI KUPI?.
1) Injili inasema katika matendo 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” Tunafahamu katika maandiko hakuna sehemu yoyote mtoto mchanga alibatizwa, na ubatizo sahihi ni katika jina la YESU KRISTO, sawasawa na (matendo 8:16, mdo 10:48, mdo 19:5), sehemu zote hizi watu wote walibatizwa kwa jina la YESU KRISTO. Hivyo mtu yeyote anayefanya kinyume na hicho ni sawa na kuvuka mipaka iliyowekwa na mababa, haijalishi umemaanisha kiasi gani, ni makosa.
2) Biblia inaposema. Kutoka 20:4 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 USIVISUJUDIE WALA KUVITUMIKIA; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,”….Na pale mtu anapochukua sanamu ya mtakatifu fulani aliyekufa siku nyingi na kuiabudu huko ni kuvuka mipaka iliyowekwa na manabii na mtu yeyote anayefanya au kwenda kinyume ataangukia laana iliyoandikwa hapo juu.
3) Kadhalika mitume kwa maagizo ya Bwana walionywa wasiwaruhusu wanawake wafundishe katika kanisa. Mtume Paulo alisema..
1Wakoritho 14:34 “Wanawake na WANYAMAZE katika kanisa, maana HAWANA RUHUSA YA KUNENA BALI WATII, kama vile inenavyo torati nayo.
35 Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.
36 Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu?
37 Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni MAAGIZO YA BWANA.
38 Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga.”……Na pia alisema.
1Timotheo 2: 8 Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano.
9 Vivyo hivyo wanawake na WAJIPAMBE KWA MAVAZI YA KUJISITIRI, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.
11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.
12 SIMPI MWANAMKE RUHUSA YA KUFUNDISHA,WALA KUMTAWALA MWANAMUME, bali awe katika utulivu.
13 Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye.
14 Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.” Hivyo kama tunavyosoma maandiko mwanamke kufundisha kanisani kwenye mchanganyiko wa wanaume na wanawake hairuhusiwi, kufanya hivyo kwa kisingizio cha haki sawa, au kisa wote ni watu wa Mungu, huko ni kuvuka mipaka iliyotangulia kuwekwa.
Kadhalika Kuvaa mavazi yoyote ya kutokujisitiri kwa wanawake, pia ni kuvuka mipaka.
4) Kuoa mke zaidi ya mmoja; angali Bwana Yesu alisema Hapo mwanzo Mungu alimuumba mtu mume na mtu mke, na hao wawili watakuwa mwili mmoja, na sio hao “wengi” watakuwa mwili mmoja(Mathayo 19:4-9). Hivyo mtu yeyote anayefanya hivyo ni kuvuka mipaka iliyowekwa na Mungu tangu zamani.
Biblia inasema katika Ayubu 24:2 “WAKO WAZIONDOAO ALAMA ZA MIPAKA; HUYACHUKUA MAKUNDI KWA JEURI NA KUYALISHA.”. Hawa ni wahubiri wanaondoa mipaka ya NENO LA MUNGU, na kuwafundisha watu mafundisho yasiyoendana na maagizo ya BIBLIA. Wapo wanaofundisha kuwa hakuna jehanamu ya moto, wapo wanaofundisha kuwa Dunia hii haiishi leo wala kesho tufurahie maisha, wapo wanaofundisha kuoa mke zaidi ya mmoja ni sawa, wapo wanaofundisha kusujudia sanamu katika ibada ni ishara ya unyenyekevu kwa Mungu hivyo hakuna shida. Wapo wanaofundisha Mungu huwa haangalii tena mambo ya mwilini tunaishi chini ya neema, hivyo kuvaa nguo za uchi ni sawa, ushoga ni sawa, Wapo wanaofundisha kuwa kunywa pombe ni sawa n.k. Na wengi wa hawa ni viongozi wakubwa wa dini wanaoheshimiwa na wengi.
Lakini Bwana anasema siku inafika atawamwagia ghadhabu yake kama maji. Hosea 5: 10 “WAKUU WA YUDA NI KAMA WATU WAONDOAO ALAMA YA MPAKA; nitawamwagia ghadhabu yangu kama maji.”
Hivyo ndugu kuwa makini na jinsi unavyoenenda katika ukristo wako, usije ukaangukia laana kwa kuyasikiliza mafundisho yaliyo nje ya NENO LA MUNGU, wanayoyafundisha manabii wa uongo. Dumu katika BIBLIA TU mipaka iliyowekwa na mababa wa kale(yaani Mitume na Manabii). Usiongeze wala usipunguze ili uwe na uhakika upo katika njia salama. Bwana alisema;
Ufunuo 22:
“18 Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
19 Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.”.
Mungu akubariki sana.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
usiiondoe alama ya mpaka iliyowekwa na mababa
Mada Nyinginezo:
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
JE! MUNGU ANAUPENDELEO KWA WANAUME ZAIDI YA WANAWAKE?
NINI TOFAUTI KATI YA KARAMA, UTENDAJI KAZI NA HUDUMA.
Katika ujenzi wa zamani majengo yote ili yasimame IMARA yalikuwa ni lazima lipatikane jiwe kubwa moja la mraba, na kuwekwa katika kona ya kuta mbili mahali zinapokutana, ili ujenzi uendelee katika mtiririko ulio sahihi, hivyo pasipo hilo jiwe kuwepo haiwezekani jengo kusimamishwa kwasababu ili matofali mengine yatakayokuja juu yake yaweze kusimama na kunyooka yalilitegemea sana hilo jiwe, ni sawasawa na pikipiki au baiskeli bila kuwa na ‘stand’ haiwezi kusimama.
Vivyo hivyo na jengo lolote lililojengwa zamani zile pasipo kuwa na hilo jiwe la pembeni jengo haliwezi kusimama. Na jiwe hilo lilikuwa linachongwa kwa vito tofauti vigumu na imara tofauti na mawe mengine, hivyo kupelekea jiwe hilo kuwa ghali zaidi ya mawe yote. (Tazama picha chini).
Kadhalika katika biblia Jiwe hili la pembeni limefananishwa na BWANA wetu YESU KRISTO.
Biblia inasema Waefeso 2: 20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, NAYE KRISTO YESU MWENYEWE NI JIWE KUU LA PEMBENI.
21 Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana.
22 Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu ikatika Roho.”
Hivyo sisi kama kanisa la Mungu (wakristo) tunafananishwa na mawe mengine madogo madogo tunaojengwa juu ya jiwe hilo kuu la pembeni, Kumbuka Bwana Yesu hajafananishwa tu na jiwe la pembeni bali ni kama JIWE ‘KUU’ LA PEMBENI. Ikiwa na maana kuwa ni jiwe la muhimu sana zaidi ya majiwe mengine yote ya pembeni. Kwamba pasipo hilo kazi inayofanyika ni sawa na bure. Ikiwa na maana pia sio kanisa tu peke yake linalohitaji jiwe kuu la pembeni, bali pia maisha ya mtu binafsi ni lazima yajengwe na jiwe kuu la pembeni.
Ndugu kumbuka kila mmoja hapa duniani ni ‘MUASHI’. Muashi maana yake ni ‘MJENZI’..Na je ni mjenzi wa nini?..Ni mjenzi wa MAISHA yake mwenyewe, kila mmoja anajenga maisha yake kwa namna yake mwenyewe, na kama ni mjenzi ni lazima uhitaji JIWE LA PEMBENI kutengeneza jengo lako. Swali Jiwe kuu lako la pembeni ni lipi?
Mawe ya pembeni yapo mengi sana. Shetani ni jiwe la pembeni; wapo wanadamu wanaotumainisha maisha yao yote katika nguvu za giza,uchawi na ushirikina, hivyo shetani ni jiwe kuu lao la pembeni.
Wapo watu ambao sababu ya maisha yao ili yawe na maana ni kuwa na MALI, hivyo mali ni jiwe kuu lao la pembeni.
Wengine wamefanya ELIMU kama tumaini la mwisho la maisha yao ya sasa na ya baadaye ni hapo tu, hawapo tayari kusikiliza habari nyingine zihusuzo Mungu au uzima wa milele uliopo katika Kristo Bwana, kwao wao ni kama upuuzi tu. N.k.
Hawa wote ni wajenzi na kila mmoja alichagua jiwe lake la pembeni kwa jinsi apendavyo. Lakini Biblia inasemaje?
1Petro 2: 4 “Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, LILILOKATALIWA NA WANADAMU, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.
5 Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.
6 Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.
7 Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, JIWE WALILOLIKATAA WAASHI [Wajenzi], LIMEKUWA JIWE KUU LA PEMBENI, .
8 Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha, Kwa maana hujikwaza kwa neno lile,wasiliamini,nao waliwekwa kusudi wapate hayo.”
Unaona hapo ndugu?. Hawa wajenzi wote walikuwa wanajiona wana hekima machoni pao wenyewe na kujichagulia MAWE wanayoyataka wao ili kuyafanya mawe yao makuu ya pembeni, lakini mwisho wao tunasoma walikuja KUJUTA baada ya jengo kukamilika, pale walipogundua kazi waliokuwa wanajitaabisha nayo ni BURE,japo ilikuwa inaonekana ina maana, jengo halifai Halina ubora wowote, baadaye walipopata akili kuwa kuna jiwe moja walilolidharau mwanzoni ndio lingepaswa kuwa jiwe kuu lao la kusimamishia jengo zima hata hivyo walikuwa wameshachelewa. JIWE limegeuka kuwa kwazo kwao (yaani HUKUMU).
Vivyo hivyo na wewe leo hii msingi wa maisha yako unaujenga wapi? je! ni ushirikina unazunguka kwa waganga, pale mambo yako yasipoenda sawa unakimbilia kwa waganga wa kienyeji kwasababu ndio jiwe kuu lako la pembeni, unaelezwa habari za Bwana Yesu kila siku, unazipuuzia kwasababu hazina umuhimu wowote katika maisha yako, lakini siku zinakuja utakapogundua kuwa Yule mwokozi uliyemkataa ndiye angepaswa awe msingi wa maisha yako, kumbuka wakati huo utakuwa umeshachelewa ni jehanamu ya moto itakuwa inakusubiria..
Wewe ambaye kutwa kuchwa ni elimu tu, habari za Yesu kwako ni hadithi za kutunga na zilizopitwa na wakati, lakini siku zinakuja utakapokugundua hukuchagua jiwe sahihi kuwa jiwe kuu la maisha yako…wakati huo utakuwa unalia na kuomboleza ukisema laiti ningejua. hata wale waashi walisema hivyo hivyo “laiti tusingelidharau jiwe lile!!”
Leo hii wewe ambaye pesa ndio kila kitu kwako, hata muda wa Kusikiliza habari za msalaba na neema ya YESU KRISTO hauna, unasema nipo buzy natengeneza maisha..Hakika unajenga kwa kutumia jiwe utakalokuja kulijutia maisha yako yote uliyoishi hapa duniani. Wapo waliotumaini mali kuliko wewe na kumweka Mungu nyuma, wanajuta leo hii katika mateso ya moto wa Jehanamu, soma habari ya tajiri wa Lazaro (Luka 16) utathibitisha jambo hilo.
Unayetumainia kipaji chako, uzuri wako,mitindo yako,afya yako na umaarufu wako kama jiwe kuu la pembeni kwa ajili ya mafanikio ya maisha yako na kuacha kumtazama aliye toa uhai wake kwa ajili ya wote wenye mwili (BWANA YESU KRISTO), nawe pia wakati utafika utakapoona kuwa kazi uliyokuwa unaifanya ni bure..Ndugu yangu usitamani ufikie hiyo hatua ya majuto makuu.
Nakushauri leo hii uchague jiwe lililo bora angali muda upo leo kumbuka hili biblia inasema limedharauliwa na waashi wengi, Lakini Mungu kasema kalifanya kuwa jiwe kuu kuliko yote,..Hayo mengine kwa muonekano yanaweza kuonekana ni mazuri lakini ni batili. Chagua jiwe bora YESU KRISTO, katika hatua uliyopo ya maisha yako sasa hivi JENGA KATIKA VIWANGO vitakavyokubaliwa na Mungu na kukupeleka mbinguni. Tubu mpe Bwana maisha yako ukabatizwe kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako, na Bwana atakupokea ikiwa umemaanisha. Na Umuushie Bwana.
Ubarikiwe sana.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
TUUTAZAME PIA MWISHO WA UJENZI WETU.
TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:
JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI AU KUTOA TALAKA?
Kama tukisoma biblia katika agano la kale, tunaona kuwa mambo yaliyokuwa yanamkasirisha sana Bwana Mungu na kumtia wivu, sio maovu yaliyokuwa yanatendeka katikati ya WATU WA MATAIFA, La! bali ni yale yaliyokuwa yanaendelea katikati ya watu wake (ISRAELI), watu alioingia nao agano. Na ndio maana zile amri 10 zilitolewa kwa wana wa Israeli tu! Na sio kwa watu wa mataifa yote ulimwenguni,.
Hivyo hao ndio watakaohusika na adhabu kwa Mungu endapo watakiuka mojawapo ya amri hizo. Kwa mfano mwanaume aliyemuoa mke wake kamwe hawezi kuona wivu kwa wanawake wengine wasiokuwa wake anapowaona wanafanya ukahaba, lakini akimwona mke wake aliyempenda na kumtolea mahari anafanya hivyo ni lazima aingiwe wivu na hasira na ghadhabu nyingi na ndivyo ilivyo hata kwa Mungu na Israeli.(Yeremia 3:14)
Kuna wakati ulifika maovu yalizidi sana katika nyumba ya Israeli ndipo Mungu akamuonyesha Ezekieli maono ya mambo yaliyokuwa yanaendelea kwa siri katikati ya watu wake. Alionyeshwa watu wakiabudu JUA katika ya nyumba yake, wengine walikuwa wanamlilia TAMUZI,(miungu ya wakaldayo), wengine wanaabudu vinyago kwa siri katika nyumba zao, na makuhani wanavukiza uvumba kwa miungu migeni,(Ezekieli 8:1-18), alionyeshwa dhuluma katika mji na umwagaji damu,na upotoshaji hukumu umejaa, na zaidi sana kulinyanyuka manabii wa uongo waliokuwa wanawatabiria watu amani wakati hamna amani. Yote haya yalimchukiza Mungu sana mpaka kuifikia kilele cha Mungu kuleta hukumu kwa watu wake wote.
Lakini kabla maangamizi hayajaja Mungu huwa anawatenga waovu na wema katikati ya watu wake kwa kuwatia ALAMA..kumbuka hawatengi hao watu katikati ya ulimwengu wote, hapana bali ni katikati ya watu wake(ISRAELI)..watu wa ulimwengu tayari Mungu alishawawekea hukumu yao katika siku ile. Na ndivyo alivyoonyeshwa Ezekieli katika habari hii..Tunasoma.
Ezekieli 9:1-11
“1 Kisha akalia kwa sauti kuu masikioni mwangu, akisema, Waamuru WALE WANAOUSIMAMI MJI wakaribie, kila mmoja na awe na kitu chake CHA KUANGAMIZA mkononi mwake.
2 Na tazama, watu SITA wakaja, wakitokea kwa njia ya lango la juu, lielekealo upande wa kaskazini, kila mmoja ana kitu chake cha kufisha mkononi mwake; na mtu mmoja kati yao amevaa bafta, naye ana kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. Wakaingia, wakasimama karibu na madhabahu ya shaba.
3 Na huo utukufu wa Bwana wa Israeli ulikuwa umepanda juu kutoka kwa kerubi, ambaye ulikuwa juu yake, mpaka kizingiti cha nyumba; akamwita mtu yule aliyekuwa amevaa bafta, mwenye kidau cha wino cha mwandishi kiunoni.
4 Bwana akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, UKATIE ALAMA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO VYA WATU WANAOUGUA NA KULIA KWASABABU YA MACHUKIZO YOTE YANAYOFANYIKA KATI YAKE.
5 Na hao wengine aliwaambia, nami nalisikia, Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma;
6 Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote MWENYE HIYO ALAMA; TENA ANZENI KATIKA PATAKATIFU PANGU. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.
7 Akawaambia, itieni nyumba unajisi, mkazijaze nyua mizoga ya hao waliouawa; haya, enendeni. Wakaenenda, wakapiga-piga katika mji.
8 Tena ikawa, walipokuwa wakipiga, nami nikiachwa, nalianguka kifudifudi, nikalia, nikasema, Ee Bwana MUNGU! Utaangamiza mabaki yote ya Israeli, wakati wa kumwaga ghadhabu yako juu ya Yerusalemu?
9 Ndipo akaniambia, Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda ni mwingi sana, nayo nchi imejaa damu, nao mji umejaa kupotosha hukumu; MAANA HUSEMA, BWANA AMEIACHA NCHI HII, NAYE BWANA HAONI.
10 Nami, jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma; lakini nitaleta njia yao juu ya vichwa vyao”.
11 Na tazama, mtu yule aliyevaa bafta, mwenye kidau cha wino kiunoni, akaleta habari, akisema, Nimefanya kama ulivyoniamuru.”
Hukumu hii iliyoletwa na hao malaika 6 ilikuja kutimia pale wa-babeli walipokuja kuuteketeza mji na kuwauwa wayahudi vijana, wazee na watoto, na kuiacha nyumba Israeli ukiwa isipokuwa kikundi kidogo sana kilichokuwa kinaugua na kulia juu ya maovu ya Israeli hao tu ndio waliosalimika(Ndio wale waliotiwa Alama katika roho) wengine wote walikufa na kuchukuliwa utumwani. Soma 2Wafalme 25:8-12, Sefania 3:11-13. utaona jambo.
Ndivyo ilivyo hata sasa hivi, Maovu makubwa yanayopelekea hasira ya Mungu kumwaga sio yatokanayo na watu wasiomjua Mungu.Hapana bali ni kwasababu ya maovu yanayoendelea katika nyumba ya Mungu (yaani kanisa), Katikati ya WAKRISTO aliowanunua kwa damu ya thamani nyingi wivu wake ndimo ulimo.
Kumbuka wana wa Israeli walidhani kuwa Mungu haoni waliyokuwa wanayafanya kwa siri, japo aliwapa muda mrefu wa kutubu lakini hawakugeuka mpaka kikombe cha ghadhabu kilipojaa hata kukawa hakuna kusamehewa tena, pale walipotengwa WEMA kati ya WAOVU.
Na katika kanisa la Kristo vivyo hivyo maovu yanayoendelea sasa hivi ni mengi mno vitu kama Siasa, ibada za sanamu ( sanamu za watakatifu waliokufa zamani mfano bikira Maria zikiabudiwa n.k.), kanisani kuna vichekesho na mizaha, mchungaji ni mlevi, mwasherati, na mpenda fedha, mtu anajiita mkristo lakini ni vuguvugu, leo yupo kwa Mungu kesho yupo kwa shetani, leo anaenda kanisani kesho disko, leo anavaa vizuri kesho kimini,.leo anamwimbia Mungu kesho anaimba nyimbo za kidunia, leo anasali kesho anasengenya. n.k.
Sasa mambo kama haya ndiyo yanayochochea ghadhabu ya Mungu, ni heri haya yangetendeka kwa mtu asiye mkristo kuliko mtu anayesema yeye ni mkristo na kakombolewa na damu ya Mungu na bado anatenda mambo kama hayo huko ni kumtia Mungu wivu mkubwa sana.
Lakini pamoja na hayo kabla Mungu hajashusha ghdhabu yake huwa anawatia ALAMA kwanza WATU WAKE waaminifu katikati ya wanaojiita wakristo, hawa anawatenga na kuwaepusha na mabaya yanayokuja mbeleni. Ndio kitu kinachoendelea sasahivi katika kanisa. Japo yanaonekana mambo ya ajabu na yasiyofaa katika Kanisa, Mungu anaendelea kuwatia muhuri wale waliojazwa Roho na waliowaaminifu na kuwaepusha na ile ghadhabu kwa KUWANYAKUA mbinguni kisha baadaye wale waliosalia wasiotiwa muhuri/alama wataangamizwa, katika siku ile kuu ya Bwana inayotisha.
Biblia inasema Nuhu na Luthu walikuwa ni watu wenye haki wakilia juu ya maovu yaliyokuwa yanaendelea katika nchi, hivyo Bwana akawaepusha na Hukumu iliyokuwa inakuja..Kadhalika Bwana YESU pia alisema kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu na Luthu ndivyo itakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adamu.
Hivyo ndugu, Kanisa tunaloishi sasa ndilo la mwisho linaloitwa LAODIKIA. Na ujumbe Bwana alioutoa kwetu sisi ni huu;
Ufunuo 3: 14-20
” Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. “
Wanaozungumziwa hapa ni wanaojiona kuwa ni wakristo, na sio watu wasiomjua Kristo, ule mfano wa magugu na ngano unawakilisha kundi lililopo kanisani..mfano wa wanawali 10, watano werevu na watano wapumbavu wote ni wanaojiona kuwa ni wakristo na sio watu wa wasiomjua Mungu. Hivyo Bwana alishatoa ONYO kwa wakristo wote wa kanisa hili tulilopo sasa wote walio vuguvugu kuwa ATAWATAPIKA, tena anasema ni HERI kuwa baridi kabisa au moto kuliko kuwa hapo katikati.
Huu ni wakati wa kufanya IMARA WITO wako na UTEULE wako. Kitu kinachoendelea sasahivi katika roho ni BWANA kuwatia alama wale wanaenenda katika ukamilifu na UTAKATIFU, wasiojitia unajisi na mambo ya ulimwengu huu, walioamua kumwishia Bwana tu na si kingine. Iogope ghadhabu ya Mungu inayokuja tubu sasa uyaweke mambo yako vizuri unyakuo usikupite.
Ubarikiwe.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
SABATO HALISI NI LINI, JE! NI JUMAPILI AU JUMAMOSI?, NI SIKU GANI ITUPASAYO KUABUDU?
Nini maana ya “Kandake” (Matendo 8:27)
MUNGU ALIKUWA ANAONGEA NA NANI ALIPOSEMA NA “TUMFANYE MTU KWA MFANO WETU”,(MWANZO 1:26)?
Wakati ule baada ya watu kumuudhi sana Mungu hata kufikia hatua ya BWANA kuleta GHARIKA juu ya dunia nzima, Na kama tunavyoijua habari ni Nuhu tu na familia yake ndio waliopona, lakini baada ya hapo BWANA akaweka UPINDE kama ishara ya agano aliloingia na Nuhu pamoja na uzao wake kwamba hataiteketeza tena dunia kwa maji..Tunasoma;
Mwanzo 9: 8 “Mungu akamwambia Nuhu, na wanawe pamoja naye, akisema,
9 Mimi, tazama, NALITHIBITISHA AGANO LANGU NANYI; tena na uzao wenu baada yenu;
10 tena na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, ndege, na mnyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu katika nchi pamoja nanyi; wote wanaotoka katika safina, hata kila kilicho hai katika nchi.
11 Na agano langu nitalithibitisha nanyi; wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika, baada ya hayo, kuiharibu nchi.
12 Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele;
13 MIMI NAUWEKA UPINDE WANGU WINGUNI, nao utakuwa ni ISHARA YA AGANO kati yangu na nchi.
14 Hata itakuwa NIKITANDA MAWINGU JUU YA NCHI, upinde utaonekana winguni,
15 nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili.
16 Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi.
17 Mungu akamwambia Nuhu, Hii ndiyo ishara ya agano nililoliweka kati yangu na wote wenye mwili walioko katika nchi.”
Ni rahisi kulichukulia agano hili kivyepesi vyepesi kwamba linafanya kazi pale tu tufani na gharika kubwa inapotaka kushuka juu ya nchi. Ni kweli kabisa Bwana alimwambia Nuhu ishara hii ya UPINDE wa RANGI SABA, Utaonakana mawinguni, lakini swali! je! ni kweli huu upinde unaonekana mawinguni tu peke yake??.
Kama ulishawahi kuona au kama hujawahi jaribu kufanya utafiti, utagundua kuwa huu upinde upo kila mahali palipo na asili au dalili ya maji. Mimi huwa nikinyeshea bustani kwa mpira nauona ukijiunda maji yanapochuruzika,,wakati mwingine nikiwa naoga na maji ya juu, unaonekana, ukiangali hata sehemu zenye maporomoko ya maji unaonekana, hata katika mito hususani pale jua linapopiga maji n.k. naamini nawe pia ulishawahi kuuona huo upinde mahali fulani tofauti na angani?. Lakini ulishawahi kujiuliza nikwanini unauona hata katika mambo madogo na sio tu mbinguni kwenye mawingu mengi ya mvua?, Hapo kuna jambo Mungu anatufundisha.
Biblia inasema Zaburi 12:6 “Maneno ya Bwana ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; ILIYOSAFISHWA MARA SABA”. Hii ikiwa na maana kuwa AGANO Mungu analoingia na watu wake alilolinena kutoka katika kinywa chake ni thabiti kama madini ya fedha yaliyohakikiwa mara 7, si ajabu hata tunauona UPINDE ukiwa na rangi SABA(7). Ikionyesha kwamba ni agano lililothibitishwa sana..Na ndio maana unaweza ukaliona katika mambo makubwa na madogo, unaweza ukaliona mbinguni na bado ukaliona kwenye ndoo ya maji.
Kumbuka upinde huu unafunua agano Mungu aliloingia na watu wake kwa kupitia damu ya YESU KRISTO mwana wake. Ni Agano lililo thabiti na kuhakikiwa sana, ni Imara kiasi kwamba kwa yeyote atakayeingia katika hilo, iwe ni katika MAMBO MAKUBWA AU MADOGO litakuwa naye kumwepusha na tufani shedtani atakayoileta. Mtu aliye ndani ya hilo agano, Iwe ni katika kushiba au njaa, iwe yupo katika raha au shida, iwe katika kupungukiwa au kuwa ni vingi litakuwa nawe, maadamu tu ameingizwa humo, HAKUNA GHARIKA yoyote ITAKAYOMGHARIKISHA. Na ndio maana biblia inasema;
Warumi 8: 33 “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.
34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? KRISTO YESU NDIYE ALIYEKUFA; NAAM, NA ZAIDI YA HAYO, AMEFUFUKA KATIKA WAFU, yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.
35 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! NI DHIKI au SHIDA, au ADHA, au NJAA, au UCHI, au HATARI, au UPANGA?
36 Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.
37 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.
38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,
39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu”.
Unaona hapo? Unapokuwa katika hilo agano ule upinde ambalo ni agano uliloingia na Bwana kwa kupitia damu ya Yesu Bwana utakupigania usijitenge na Mungu katika hali yoyote ile utakayokuwepo…
Ndugu unapokuwa mkristo fahamu kuwa upo safarini, na kama tunavyofahamu uthibitisho ya kwamba upo safarini ni kukatisha katika mazingira tofuati tofauti, kuna wakati utakutana na milima, kuna mahali utafika utakutana na mabonde, mahali pengine tambarare, kuna mahali utakuta mvua, sehemu nyingine joto n.k. lakini ukiona mazingira hayabadiliki nje basi ujue haupo safarini..upo pale pale…Hivyo usishangae kukutana na hizo hali ni jambo la kawaida.
Mkristo kupitia dhiki, shida, wakati mwingine magonjwa, au kupungukiwa, au njaa haimaanishi kuwa Mungu kakuacha kama wengi wadhanivyo, maadamu upo katika lile AGANO THABITI la Damu ya YESU KRISTO, fahamu kuwa wewe ni MBARIKIWA, japo utapitia hayo tena kwa kitambo tu, Mungu hataruhusu chochote kikugharikishe kabisa..ukumbuke ule upinde unaonekana katika mambo makubwa na madogo.
Wapo watu wanahubiri kipimo kwamba kipimo cha kwamba upo katika lile agano ni mafanikio ya kimwili tu wakati wote, kwahiyo mtu yeyote asiyefanikiwa kifedha amelaaniwa..ni safari gani hiyo isiyokuwa na mabonde na milima? biblia inasema;
Mhubiri 3:3……… kuna wakati wa Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;
4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;
5 Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;
6 Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;
Vile vile mambo mengine unaweza ukayaona ni madogo au usiyaone kabisa shetani aliyoyapanga dhidi yako, lakini Mungu anakuepusha nayo pasipo hata wewe kujua, kwa mfano wachawi kwa siri wamepanga kuidhuru familia yako, lakini Mungu anawaepushia mbali na Mungu hakwambii, wakati mwingine unakatisha njiani na nyoka anapita pembeni yako pasipo kukuuma, na wewe hujamwona, pengine utasema mimi sijawahi kukutana na nyoka maisha yangu yote, lakini fahamu umeshapishana nao wengi na kwamba wangekung’ata ungepata madhara makubwa mpaka leo..
Wakati mwingine umekula chakula chenye sumu pasipo hata wewe mwenyewe kujua, lakini Mungu anakiponya, utasema mimi mwaka mzima nina afya, ninazidi kunawiri lakini kumbuka mfano angeutoa ule UPINDE WAKE katika mambo madogo kama hayo ungekuwa umeshakufa siku nyingi. kila siku kwenye shughuli zako unakutana na mamilioni ya mapepo na majini pengine kukusababishia ajali, wakati mwingine kukuletea uchonganishi, ugomvi, visa, malumbano yasiyokuwa na maana, tamaa, uasherati n.k. vyote hivi Mungu anakuepusha navyo pasipo hata kukwambia. Kwako wewe siku inakuja siku inaenda upo salama…Hujui kuwa ni ule UPINDE wa Agano unatenda kazi ndani yako katika mambo madogo usiyoyajua wewe.
Kwahiyo ndugu ikiwa wewe ni Mkristo nikimaanisha kuwa umeokolewa kwa kumwamini BWANA YESU, na kubatizwa katika ubatizo sahihi kwa kuzamishwa kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi na kujazwa Roho mtakatifu na kuishia maisha matakatifu fahamu tu kuwa upo katika mahali salama kabisa kwasababu lile AGANO LA UPINDE linafanya kazi sehemu zote, halipo kwenye tufani kubwa tu, hata katika ndogo.
Ni thabiti katika hali zote katika utajiri na umaskini. Lakini kwa yeyote aliye nje ya hilo Agano la Damu ya Yesu hana ulinzi wowote iwe katika utajiri atagharikishwa tu, iwe katika umaskini atagharikishwa tu, iwe katika raha, shida, mafanikio, afya, magonjwa vyovyote vile gharika ikija hata ikiwa ndogo kiasi gani itampeleka tu …Kwa sababu hakuna UPINDE wa Agano katika maisha yake la kumfanya Mungu akumbuke agano aliloingia na yeye ili amrehemu.
Ndugu nje ya YESU KRISTO hakuna uzima. Yeye ndio njia kweli na uzima, na kumbuka kumwamini Bwana Yesu sio kuongozwa sala ya Toba tu, bali ni kuchukua uamuzi wa kutubu kwa kumaanisha kuziacha kabisa dhambi zako na maisha yako ya zamani, hapo utakuwa umezaliwa mara ya pili, na ndipo lile AGANO LA UPINDE litakapoanza kuonekana katika maisha yako, likitenda kazi katika nyakati za mambo makubwa na mambo madogo.
Ubarikiwe sana.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
FAHAMU KINACHOMGHARIMU MUNGU, KUTOA URITHI WAKE.
Kwanini Yakobo na Yohana waliitwa “Wana wa Ngurumo”?
BWANA ALIPOSEMA KUWA YEYE NI “MUNGU WA MIUNGU” ALIKUWA NA MAANA GANI?..JE! YEYE NI MUNGU WA SANAMU?