Biblia inapozungumzia mioyo..haimaanishi hii mioyo iliyomo ndani ya vifua vyetu inayosukuma damu…hapana bali inazungumzia utu wa ndani ambao ni roho zetu.
Biblia inasema katika…
Waefeso 1:18 “macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo”
Umeona hapo inasema “macho ya mioyo”..sasa moyo wa nyama hauwezi kuwa na macho…maana yake ikimaanisha kuwa ni kitu kingine ndio kinachozungumziwa hapo…na hicho si kingine Zaidi ya ROHO ZETU.
Roho zetu ni mfano wa miili yetu, zina macho, zina masikio, zina miguu, zina mikono, zina kila kitu ambacho kinaweza kunaweza kuonekana kwenye hii miili ya damu na nyama…Roho zetu na zenyewe zinakula na zinaishi na zinaweza kufa pia endapo zikiwekwa katika mazingira fulani yasiyoruhusu uhai.
Mtu ambaye ni kipofu rohoni ni yule ambaye macho ya roho yake hayaoni…Na kumbuka sio yule ambaye haoni vitu vya ulimwengu wa roho kama wachawi, au malaika, au maono…Hapana bali ni yule ambaye halielewi Neno. Na mtu asiyelielewa neno kwake huyo haliwezi kumsaidia chochote, na ni rahisi kulipuuzia. Hata wewe ukisoma kitabu ambacho hukielewi ni rahisi kukipuuzia hata kama kitabu hicho kitakuwa kinasifiwa na wangapi..Na ndivyo hivyo biblia nayo, kama haieleweki kwa mtu inageuka na kuwa kitabu kisicho na maana yoyote kwa anayekisoma….Na kuelewa maana yake ni kutambua matumizi ya kile unachokisoma katika Maisha uliyopo sasa.
Sasa hebu turudi kwenye biblia tusome kisa kimoja tutajifunza Zaidi maana ya “kufumbuliwa macho ya kiroho”.
Kama wewe ni msomi mzuri wa biblia utakumbuka kisa kimoja cha vijana wawili waliokuwa wanaelekea Kijiji kimoja kilichoitwa Emau, siku ile Bwana Yesu alipofufuka, na njiani Yesu mwenyewe aliwatokea na kuungana nao na wao pasipo kujua kuwa ni Yesu walidhani kuwa ni mtu tu wa kawaida…Hebu tusome…
Luka 24: 13 “Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili.
14 Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia.
15 Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao.
16 Macho yao yakafumbwa wasimtambue.
17 Akawaambia, Ni maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao.
18 Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! Wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi?
19 Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote;
20 tena jinsi wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulibisha.
21 Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipotendeka mambo hayo;
22 tena, wanawake kadha wa kadha wa kwetu walitushitusha, waliokwenda kaburini asubuhi na mapema,
23 wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosema kwamba yu hai.
24 Na wengine waliokuwa pamoja nasi walikwenda kaburini wakaona vivyo hivyo kama wale wanawake walivyosema, ila yeye hawakumwona.
25 Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii!
26 JE! HAIKUMPASA KRISTO KUPATA MATESO HAYA NA KUINGIA KATIKA UTUKUFU WAKE?
27 AKAANZA KUTOKA MUSA NA MANABII WOTE, AKAWAELEZA KATIKA MAANDIKO YOTE MAMBO YALIYOMHUSU YEYE MWENYEWE.
28 Wakakikaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, naye alifanya kama anataka kuendelea mbele.
29 Wakamshawishi wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha. Akaingia ndani kukaa nao.
30 Ikawa alipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa.
31 Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua; kisha akatoweka mbele yao. 32 WAKAAMBIANA, JE! MIOYO YETU HAIKUWAKA NDANI YETU HAPO ALIPOKUWA AKISEMA NASI NJIANI, NA KUTUFUNULIA MAANDIKO?”
Sasa kama utagundua kitu…hawa hata wakati Yesu anazungumza nao kule barabarani na kuwafafanulia maandiko, bado walikuwa hata hawaelewi vizuri kile Bwana alichokua anakisema…Lakini baada tu ya kuula ule mkate…ghafla ufahamu ukawaingia wa yale maandiko Bwana aliyokuwa anazungumza nao kule njiani…uelewa wa ajabu wa kile Bwana alichokuwa anawaambia kule njiani ukawaingia, akili ya kuchambua maandiko ikawaingia, na mwisho wakaona mbona kama yale maandiko ndio yanayomhusu mtu fulani aliyekuwa na sauti kama ya huyu tunayezungumza naye hapa?…
Je huyu siye yule Yesu kweli ama ndugu yake??..hebu ngoja tumwangalie vizuri!..walipomtazama vizuri wakagundua ni yeye…kisha akatoweka mbele yao…lakini walianza kumgundua kwanza kwa andiko ndipo uso baadaye…Maana yake ni kwamba hata kama Yesu angewatokea kwa sura nyingine au hata kama angekuwa amejifunika uso wasimwone…kwa ufunuo wa maandiko bado wangemuhisi tu, …Hebu wasikie wanavyosema hapa katika ule mstari wa mwisho.. “WAKAAMBIANA, JE! MIOYO YETU HAIKUWAKA NDANI YETU HAPO ALIPOKUWA AKISEMA NASI NJIANI, NA KUTUFUNULIA MAANDIKO?”…Yaani maana yake ni kwamba imekuwaje kuwaje hatujamtambua tangu pale mwanzo alipoanza kutufunulia haya maandiko?..
Kwahiyo kilichofunuliwa cha kwanza ni macho ya mioyo yao (yaani uelewa wa maandiko) ndipo vitu vingine vikafuata… Kama wasingeyaelewa maandiko wasingemtambua Bwana kwa namna yoyote ile hata kama angejitambulisha wazi mbele yao kwamba yeye ndiye Kristo, bado wasingemwamini.
Kama sehemu fulani maandiko yanavyosema….
Yohana 12:37 “Walakini ajapokuwa amefanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, hawakumwamini;
38 ili litimie lile neno la nabii Isaya alilolisema, Bwana, ni nani aliyezisadiki habari zetu; Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?
39 Ndiyo sababu wao hawakuweza kusadiki; kwa maana Isaya alisema tena,
40 Amewapofusha macho, Ameifanya mizito mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakafahamu kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya”
Kwahiyo ni muhimu sana kutafuta kufumbuliwa macho ya rohoni, wengi wanatafuta kuona wachawi!, huko sio kufumbuliwa macho, wengine wanatafuta kuona maono..huko nako sio kufumbuliwa macho ya rohoni! Wala kuota ndoto za kimiujiza sio kufumbuliwa macho……kupata kuelewa Kwanini Yesu alikuja duniani, anataka nini sasa, na yupo wapi sasa, na kuyaelewa mapenzi yake na kuyafanya huko ndio kufumbuliwa macho ya rohoni…Na hapo utamwona Yesu kila siku katika Maisha yako..huhitaji macho ya damu na nyama kuhakiki, tayari macho yako ya ndani yanamwona kila siku katika Maisha yako.
Luka 24: 44 “Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi.
45 Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.
46 Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu”
Na mtu muuaji bado hajambuliwa macho, mtu anayevaa vimini hajafumbuliwa macho, mtu anayezini na anayefanya uasherati, na anayefanya mambo mengine ya kidunia bado ni kipofu wa rohoni, haijalishi anaona maono au anatabiri..bado ni kipofu! Kulingana na biblia.
Na tunafunguliwaje macho ya rohoni?..kwanza kwa kukubali kwamba sisi ni wakosaji, na kisha kwenda chini yake kwa unyenyekevu na kuomba rehema na toba…baada ya hapo kumtii maagizo yake ya kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi na kwa jina lake..kisha kupokea Roho wake mtakatifu..Huyo ndiye aliye na jukumu la kufumbua macho yetu ya rohoni na kutufanya kuyaelewa maandiko..lakini pasipo huyo kamwe hatuwezi kumwelewa Mungu wala kumjua…tutakuwa tu kama Wanyama ambao wana macho lakini hawaoni.
Bwana atubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
MAMBO MENGINE HAYATOKI ISIPOKUWA KWA KUFUNGA.
WAKAKAA KWAKE SIKU ILE. NAYO ILIKUWA YAPATA SAA KUMI.
WANA JUHUDI KWA AJILI YA MUNGU, LAKINI SI KATIKA MAARIFA.
WAKATI ULIOKUBALIKA NDIO SASA.
IKIMBIE DHAMBI KWA GHARAMA ZOZOTE ZILE!
USIMZIMISHE ROHO.
Yafahamu malezi ya mtoto mchanga kibiblia.
Ukitaka mtoto wako mchanga awe na afya na ukuaji bora, na baadaye aishi Maisha aliyokusudiwa na Mungu ya mafanikio rohoni..Basi ni vema ukatafuta ushauri wa kiblia, ili ujue ni jinsi gani unapaswa umlee mwanao tangu akiwa katika hatua za awali za uchanga wake.
Embu tukiangazie kisa kimoja katika biblia, naomba usome chote, na mwisho wa Habari hiyo utajifunza jambo kubwa sana ambalo pengine hata hukuwahi kulitafakari hapo kabla..Ni tukio linalomuhusu Sulemani na wanawake wale wawili makahaba.
Tusome..
1Wafalme 3:16 Ndipo wanawake wawili, makahaba, walimwendea mfalme, wakasimama mbele yake. 17 Na mwanamke mmoja akasema, Ee bwana wangu, mimi na mwanamke huyu tunakaa katika nyumba moja; nami nalizaa nilipokuwa pamoja naye nyumbani. 18 Kisha, siku ya tatu baada ya kuzaa kwangu, ikawa mwanamke huyu naye akazaa; na sisi tulikuwa pamoja; hapakuwa na mtu mwingine pamoja nasi nyumbani, isipokuwa sisi wawili tu. 19 Na mtoto wa mwanamke huyu akafa usiku, maana alimlalia. 20 Akaondoka kati ya usiku, akamwondoa mtoto wangu ubavuni pangu, mimi mjakazi wako nilipokuwa usingizini, akamweka kifuani pake, na mtoto wake mwenyewe, aliyekuwa amekufa, akamweka kifuani pangu. 21 Nilipoondoka asubuhi nimnyonyeshe mtoto wangu, kumbe? Amekufa. Hata asubuhi nilipomtazama sana, kumbe! Siye mtoto wangu niliyemzaa. 22 Ndipo yule mwanamke wa pili akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wangu ndiye aliye hai, na mtoto wako ndiye aliyekufa. Na mwenzake akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wako ndiye aliyekufa, na mtoto wangu ndiye aliye hai. Ndivyo walivyosema mbele ya mfalme. 23 Ndipo mfalme akasema, Huyu anasema, Mtoto wangu yu hai, na mtoto wako amekufa. Na huyu anasema, Sivyo hivyo; bali mtoto aliyekufa ni wako, na mtoto aliye hai ni wangu. 24 Mfalme akasema, Nileteeni upanga. Wakaleta upanga mbele ya mfalme. 25 Mfalme akasema, Mkate mtoto aliye hai vipande viwili, kampe huyu nusu, na huyu nusu. 26 Ndipo mwanamke yule, ambaye mtoto aliye hai ni wake, akamwambia mfalme kwa maana moyoni mwake alimwonea mtoto wake huruma, akasema, Ee bwana wangu, mpe huyu mtoto aliye hai, wala usimwue kamwe. Lakini yule mwingine akasema, Asiwe wangu wala wako; na akatwe. 27 Ndipo mfalme akajibu, akasema, Mpe huyu wa kwanza mtoto aliye hai, maana yeye ndiye mama yake. 28 Na Israeli wote wakapata habari za hukumu ile aliyoihukumu mfalme wakamwogopa mfalme; maana waliona ya kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake, ili afanye hukumu.
Tukianzana na hilo la kwanza: Utaona mwanamke yule mwerevu, alikuwa kila alipolala alikiweka kichanga chake Ubavuni. Ikiwa na maana alijitahidi kwa kadiri awezavyo kulala chali, ili mtoto apate nafasi ya kumwegemea yeye aidha ubavuni pake au kifuani pake, na sio yeye amwegemee mtoto,..Lakini yule mwingine hakulijali hilo, alimgeuza mtoto kuwa godoro, akamlalia..Na matokeo yake yakawa ni kifo.
Pili: Kama yule mwanamke angekuwa “hamchunguzi/hamdadisi” sana mtoto wake: Basi angeibiwa mwanawe bila habari. Lakini yeye tangu siku ya kwanza alikuwa anamkagua hadi kufikia siku ya tatu tayari alikuwa ameshamjua mwanawe ndani nje..,!, alijua umbile la mwanawe, na alama zake,..Hata pale alipojaribu tu kuchanganyiwa mtoto alilimtambua hilo mara moja.
Malalamiko mengi, ya wazazi, kuhusu Watoto wao kudhalilishwa kijinsia yanatokana na wazazi kutokuwa na tabia ya kuwachunguza Watoto wao, wanakuja kugundua hali imeshakuwa mbaya sana hairekebishiki. Anza kujijengea tabia hiyo ni kwa heri yako na kwa usalama wa kichanga chako.
Tatu: wanawake wale walikuwa ni wanyonyeshaji wa maziwa yao wenyewe ya asili kwa vichanga vyao na sio ya ng’ombe.
Sasa ili mtoto wako mchanga awe na ulinzi wa ki-Mungu maishani mwake..Mchukue ukamweke wakfu mbele za Mungu. Hakikisha pia huendi mikono mitupu, ambatanisha na sadaka yako ya shukurani kwa Mungu kwa kile alichokupa/alichowapa.
Ipo mifano mingi ya kimaandiko ya wanawake wenye akili walipeleka Watoto wao wapeleka mbele za Bwana wabarikiwe, na mpaka leo tunaona Watoto hao jinsi walivyokuwa nguzo muhimu katika Imani, Ukimsoma Samweli, yeye hakuwa vile hivi hivi tu, bali ni baada ya mama yake kumpeleka mbele za Bwana (Soma Samweli 1&2).
Ukimsoma Yohana Mbatizaji naye vivyo hivyo,. Ukimsoma pia Bwana wetu Yesu Kristo naye vivyo hivyo, wote walipelekwa mbele za Bwana. Vivyo hivyo mchukue mwanao, mpeleke nyumbani kwa Bwana awekwe wakfu kwa Bwana kwa kuwekewa mikono na wachungaji au wazee wa kanisa..Hiyo itakuwa ni salama ya Maisha ya baadaye ya mwanao.(Luka 2:22-24).
Huhitaji kusubiri mpaka awe mkubwa, siku za mwanzoni mwanzoni, au wiki za mwanzoni haraka bila kukawia mpeleke kwa Bwana..Kumbuka mtoto mchanga habatizwi kulingana na maandiko, Hivyo usifanye hivyo kwasababu haitasaidia chochote. Mpeleke akawekewe mikono tu awe wakfu kwa Bwana.
Na hili ndio jambo kuu kuliko yote ya kuzingatia. Unaweza ukaijali afya yake, lakini kama Mungu hamtambui ni kazi bure.Kwasababu shetani ndiye atakayemtambua.
Vilevile ni jukumu lako kumwombea mwanao kila wakati, Tenga muda maalimu wa kumwombea, walau lisaa 1 kila kipindi. Mwombee afya yake, mwombee ukuaji wake, mwombee kila pembe ambayo Mungu atakuongoza. Vilevile unapomwimbia Mungu imba Pamoja naye, Na hiyo ndio dalili nzuri upendo Mungu anaotaka mazazi aonyeshe kwa vichanga vyao.
Hivyo kwa kuhitimisha zingatia hayo mambo makuu 5.
Lakini kumbuka pia yote hayo ili yawe na maana ni lazima na wewe kama mzazi/wazazi, muwe mmemkabidhi Kristo Maisha yenu (yaani muwe mmeokoka). Hizi ni nyakati za mwisho na za hatari sana kama ulikuwa hujui, Pale Bwana Yesu aliposema..
Mathayo 24:19 “Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo! 20 Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato. 21 Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe”.
Jiulize ni kwanini alisema, ole kwa wanyonyeshao kama wewe?..Alisema hivyo kwasababu alijua mwisho ukiwakuta watu wa namna kama ya kwako, wakati huo utakuwa ni mgumu sana kwao..Embu jiweke katika mazingira kama hayo halafu usikie YESU karudi kulinyakua kanisa..Umebaki hapa duniani , halafu mpinga-Kristo anaanza kuchinja watu utakuwa katika hali gani na mwanao.
Angalia magonjwa yanayotokea duniani ya ajabu (covid-19), angalia, majanga, angalia matetemeko makubwa, mauaji ya ajabu na ya kinyama, angalia tetesi za vita vya ki-atomiki na kuibuka kwa manabii wa uongo..Hapo hatuwezi kusema tuna vizazi vingine mbele vya kuishi, pengine mimi na wewe tutashuhudia tukio zima la Unyakuo..Sasa utakuwa wapi ikiwa leo hii hujaokoka ndugu yangu..
Lakini ukitubu sasa, Kristo yupo tayari kukusamehe, unachopaswa kufanya ni kumaanisha tu, kutoka katika moyo wako, na kusema kuanzia leo mimi ninaacha dhambi ninamgeukia..Na wakati huu huu Kristo ataanza kufanya kazi ndani ya Maisha yako, Hivyo kama upo tayari kufanya hivyo leo.
Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.
Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.
Ubarikiwe sana
Mada Nyinginezo:
KILEMBA CHA NEEMA, JE! UMEMVIKA MWANAO?
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
Isaya 24:19 “Dunia kuvunjika, inavunjika sana; dunia kupasuka, imepasuka sana; dunia kutikisika, imetikisika sana.
20 Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela; na mzigo wa dhambi zake utailemea; nayo itaanguka, wala haitainuka tena”.
Shalom,
Hii dunia yetu imefananishwa na mlevi wa kupindukia.. Mlevi ni mtu ambaye ameshapoteza uwezo wake wa kuji-control, yaani akili yake na mwili wake havina uhuwiano tena, akisimama anajiona kama kaning’inizwa, na akianza tu kutembea anajiona kama anazungushwa kama tairi, hivyo mwendo wake unaishia kuwa ni kuyumba yumba tu safari nzima na mwisho wake unakuwa ni kuangukia mtaroni wakati huo akiwa hata tayari ameshajisaidia..
Na kibaya Zaidi akishaanguka pale, ndio haamki tena mpaka asubuhi..
Na hii dunia yetu ndio imekuwa hivyo, tumeinywesha pombe na maovu, na hivyo imelewa haiwezi kuji-control tena.. Leo hii utaona matetemeko makubwa na madogo ya ardhi kila mahali, utajiuliza ni kwanini hayo mambo yamekithiri sana wakati huu.. Ujue ni dhambi zetu zimeilewesha dunia na moja ya hizi siku itakwenda kuanguka.
Utaona, magonjwa makubwa ya mlipuko duniani kote (kama corona)..Utajiuliza tena ni kwanini?.. Ni kwasababu haiwezi kujidhibiti yenyewe, inawaya waya.
Utajiuliza ni kwanini vitendo viovu na mauaji ya kinyama yanaendelea duniani kote kila kukicha.. Ni kwasababu imeshalewa vya kutosha na hivyo itakwenda kupumzika tu muda sio mwingi.
Utajiuliza tena ni kwanini mafundisho mengi ya mashetani , na manabii wengi wa uongo wamezuka duniani kuliko vipindi vingine vyote vya nyuma..Jibu ni lile lile, haiwezi kustahimili tena, mzigo wa dhambi umekuwa mzito sana hivyo wakati wake wa kwenda kujipumzisha umekaribia sana.
Kwanini vitisho vya vita, vinavuma kila mahali, mabomu ya Atomic yanatengenezwa na mataifa kila pembe ya dunia..Utajiuliza ya nini yote hayo wakati kwa kizazi chetu, mbona tunaishi katika dunia inayosimamia masuala ya haki za kibinadamu.? Ni uthibitisho kwamba silaha hizo ni lazima zije kutumika tu wakati si mrefu.
Tumekuwa tukisikia habari za mwisho wa dunia, tunapuuzia, tunadhani, ni mambo ambayo yanahitaji maandalizi mengi sana, au yataanza taratibu taratibu, lakini biblia haituambii hivyo, inasema siku ambazo watu wanadhani kuna amani na salama ndipo uharibifu utakavyokuja kwa ghafla..
1Wathesalonike 5:1 “Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.
2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.
3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa”.
Unaona? Wakati wasemapo amani na salama..Lakini mtume Paulo anaendelea kwasisitiza watakatifu wote na kusema…
4 Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.
5 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.
6 Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.
7 Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku.
8 Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu”.
Je! Wewe bado upo usingizini?.. Bado upo gizani?..Je unatamani kuishuhudia hiyo siku ya kuanguka kwa dunia moja kwa moja jinsi itakavyokuwa?..Wakati huo ambao wenzako watakuwa wameshanyakuliwa wewe utakuwepo hapa chini kuyashuhudia yote..Na siku yenyewe biblia inasema itakuwa ya namna hii:
2Petro 3:10 “Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,
12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?
Kama tunavyosoma hiyo siku ya moto na Volkano duniani, sio ya kuitamani kabisa..Mimi siitamani, natumai na wewe pia..Hivyo Mgeukie Kristo sasa, kwa kutubu dhambi zako na kwa kumaanisha kumfuata Bwana, kama bado hujampokea.
Bwana akubariki sana.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
SWALI: Mtu astahiliye hofu ni mtu wa namna gani kama tunavyosoma katika Warumi 13:7?
JIBU: Tusome,
Warumi 13:7 “Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima”.
Hofu inayozungumziwa hapo ni tofauti ni ile tuliyozoea kuitafsiri…Tafsiri ya hofu inayojulikana na wengi “ni ile hali ya kuwa na woga”..na hivyo kukufanya ukose ujasiri au ukose nguvu ya kufanya kitu Fulani…Kwamfano Mtu anapokutana ghafla na simba au kitu cha kumdhuru hofu Fulani inamuingia au woga, ambao unamfanya ahisi kwamba anakwenda kupatwa na madhara mbele yake. Sasa hofu ya namna hiyo sio inayozungumziwa hapo katika Warumi 13:7.
Hofu inayozungumziwa hapo inafanana na ile ya kumhofu Mungu/kumwogopa Mungu. Biblia inaposema tumwogope Mungu haimaanishi tumwogope kama tunavyomwogopa simba anapotokea mbele yetu, hapana!…Bali inamaanisha tumpe heshima ya hali ya juu sana, kwa kiwango ambacho tunaelewa madhara ya kutomheshimu ni kujipatia hukumu…Na hali hiyo haitufanyi kuwa waoga mbele yake bali inatufanya tuwe makini.
Sasa mstari huo ndio ulikuwa unazungumzia hofu na ya namna hiyo…”ya kumheshimu mtu kwa kiwango ambacho, unajua madhara yake endapo hutampa heshima hiyo”…Na ukianzia juu kidogo utaona Mtume Paulo alivyokuwa anazungumzia juu ya kuwatii wenye mamlaka…na hapa ndio anasema mwenye kustahili kodi apewe kodi (maana yake bodi za mapato kama TRA), wanastahili kodi zao, wenye kustahili ushuru wapewe, wenye kustahili hofu kama MARAISI, na Viongozi wengine wa nchi,..ambao wasipopewa heshima inayostahili wanayo mamlaka hata ya kumfunga mtu, wapewe hadhi hiyo.
Ni dhambi kutowaheshimu wenye mamlaka, ni dhambi kuwadhalilisha, ni dhambi kuwajibu bila hekima, ni dhambi kuwafanyia kiburi…maadamu hawaingilii imani yako, si sahihi kutowatii kwa vyovyote vile. Na sio tu viongozi wa nchi bali hata viongozi wa mashule kama waalimu, wahadhiri pamoja na viongozi wa mahali tunapofanyia kazi(yaani waajiri, ma-meneja na wakurugenzi).
Waefeso 6:5 “Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, KWA HOFU NA KUTETEMEKA, KWA UNYOFU WA MOYO, KANA KWAMBA NI KUMTII KRISTO;
6 wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekazao kwa wanadamu bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo;
7 kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu;
8 mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru”
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
BASI TUENDELEE KUMJUA MUNGU,NAYE ATATUJILIA KAMA MVUA YA VULI.
Kuhutubu linatoka na neno “kuhutubia”… ambalo chanzo chake ni “HOTUBA”. Hotuba ni maneno yaliyoandaliwa ambayo mtu anaweza kuyazungumza mbele ya kadamnasi ya kuwafaa…yanaweza kuwa ya kimaendelea au ya kimikakati.
Tukirudi katika biblia….Kuhutubu ni tofauti na kuhutubu kwa watu wa kiulimwengu… Watu wa ulimwengu watahutubia mikakati ya kiulimwengu…lakini watu wa Mungu watahutubia maneno ya Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Sasa wachungaji na waalimu wanapolifundisha Neno la Mungu kwa uweza wa Roho Mtakatifu mbele ya mkutano hapo ni wanahutubu, yaani wanahutubia maneno ya Mungu ya uzima..
1Timotheo 5:17 “Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha”.
Matendo 20:7 “Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane”.
Lakini hali kadhalika watumishi wa Mungu, wenye karama ya kinabii wanaposimama mbele ya mkutano na kutoa maneno ya kinabii ya kuwajenga watu na kuwapa tumaini ya mambo yajayo hao pia ni WANAHUTUBU.
1Wakorintho 11:4 “Kila mwanamume, asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaaibisha kichwa chake.
5 Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa”.
Kuhutubu kunakozungumziwa hapo ni kutoa unabii au kwa lugha ya kiingereza “to-prophesy”..
Shalom
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
JE! MTUMISHI KUTOKUWA NA FEDHA NI ISHARA KUWA KUNA TATIZO KATIKA IMANI YAKE?
Biblia inatupa mwangaza wa jinsi shetani alivyomaanisha kweli kuwaangamiza wanadamu japokuwa sisi hatulijui hilo.. Unaweza ukadhani siku ukifa tu, ndio basi shetani anakuwa amemalizana na wewe. Huo mtazamo ni wakuuondoa kabisa kichwani..
Embu jaribu kifirikia kile kisa cha Musa, baada ya Kufa, ni nini kilitokea baadaye?..
Utasoma kwenye kitabu cha Yuda, Malaika Mikaeli alikuwa akihojiana naye sana na juu ya mwili wa Musa.. Tusome..
Yuda 1:9 “Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee.
Kumbuka hiyo ni baada ya Mungu kumuona Musa ni mwaminifu na amevipiga vita vyema, mwendo ameumaliza, na Imani ameilinda, Na sasa baada ya kufa Mungu anampa maagizo malaika Mikaeli amchue aende kumzika mahali pa siri pasipojulikana na watu (Soma Kumbukumbu 34:5-6).. Lakini shetani kwa kulijua hilo kuwa hawezi kumpata Musa tena, hawezi kumletea tena jaribu ili atende dhambi amshinde kwani roho yake tayari haipo pale ilishamtoka na kwenda sehemu nyingine siku nyingi..
Lakini yeye bado aliona fursa ya kuushitaki na mwili wa Musa pia, alitaka Mungu auache tu ardhini, alitaka usizikwe kipekee vile na Mungu, au alitaka aupate yeye kwa shughuli zake za kuwapotosha watu waabudu mahali alipozikwa, au mifupa yake….shetani japokuwa alijua ni muozo tu ule, na mavumbi, lakini hata hilo alililia apewe, bado anashughuli nao.
Alikuwa anahojiana na Mikaeli, pengine kwa kumwonyesha ubaya wake aliokuwa anaufanya duniani au madhaifu yake, kama alivyokuwa anamshitaki Ayubu ili tu Mungu aghahiri asizike mwili wake kipekee..Lakini tunasoma alishindwa kwasababu Musa alikuwa ni mtakatifu wa Mungu.
Sasa tujiulize, ikiwa maiti tu ya mtakatifu, ibilisi anaigombania, mfano tu wa wale askari walioligombani vazi la Yesu pale msalabani, ambalo walijua halikuwa na faida yoyote kwao,..Sisi je tutawezaje kumkwepa kirahisi huyu adui wa roho zetu ikiwa hatutakuwa milki ya YESU KRISTO?
Shetani haitaki tu roho yako, ingekuwa heri aishie hapo ..Lakini Akishaipata bado atataka na familia yako pia, atataka na afya yako, atataka na watoto wako, atataka na nyumba yako, na mali zako ulizozitaabia… pengine, atapelekea mashitaka mbinguni kuwa hata hizo nguo unazovaa ni mali yake.. Na siku ile ukifa hata huo mwili wako, pia atautaka kwa Mungu..Sasa jiulize ikiwa wewe ni mwenye dhambi ni nini kitamshawishi Mungu asimpe vyote hivyo?
Ndio hapo Kaburi lako badala lilindwe na Mungu, ndio shetani analifanya kuwa VILINGE VYA WACHAWI WAKE, mwili wako uliozikwa kwa heshima na wabunge wenzake, unafukuliwa na wachawi ili kuchukuliwa viungo ambavyo vitawasaidia katika shughuli zao za kiganga..Si ni kwasababu wewe ni mali yake?..shetani kashinda hoja mbinguni juu yako…anazo point za kutosha za kupewa mwili wako, na Mungu ni Mungu wa haki, anahojiana na shetani na vile vile pia anampa haki zake kama anastahili.
Hata sasa bado ukiwa hai, hivyo vyote ulivyonavyo shetani anavijengea hoja kwa Mungu, kwanini visiwe vyake?….Umetoka kuzini, na umeshajua Neno la Mungu linakataza kufanya hivyo, unatoka asubuhi unakwenda kazini..wakati upo njiani shetani kashafika mbele za Mungu na kusema…mwangalie Yule mtu ambaye unasema ni mtumishi wako ametoka kuzini..na masaa chache tu alitoka kulisoma neno lako linalomwambia usizini..hivyo huyu ni wangu, nataka nimtumie majeshi ya mapepo nimuue!…na malaika wa Mungu wanapojaribu kutafuta hoja mbili tatu za kukutetea wanapokosa..shetani anapewa haki yake, na wewe unakabidhiwa chini ya mikono yake..kwasababu ni wake yeye…
hivyo unajikuta unapata matatizo ambayo si ya kawaida..
Ndugu haya mambo sio hadithi za kutunga ni vitu vinavyoendelea katika roho kabisa…Je unajua tafsiri ya jina “shetani”?…Shetani maana yake ni “mchongezi/mshtaki” biblia imetoa tafsiri yake hiyo…Hivyo kazi yake ni kukuchongea mbele za Mungu..hata unapochukia tu, tayari kashafika mbele za Baba kupeleka mashtaka..Hivyo sio wa kujiungamanisha naye kabisa.
Unaweza kuona tupo hatari kubwa kiasi gani ndugu yangu.. Ulimwengu huu ni wa mashaka na hofu ikiwa tu Yesu Kristo sio kimbilio lako. Aliposema pale Yohana 17:15 “Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu” . Alimaanisha kweli wale wanaomkimbilia watalindwa na Yule mwovu shetani, mshitaki wao.
Hivyo yasalimishe maisha yako leo kwa Kristo, ndani ya hichi kipindi kifupi tulichobakiwa kabla Kristo hajarudi. Dalili zote zinathibitisha Unyakuo ni wakati wowote,..Na shetani hilo analijua na ndio maana na yeye anafanya kazi sana kwasababu anajua muda wake ni mchache..
Hivyo ingia zizini mwa Bwana kama bado upo nje. Tubu dhambi zako kwa kumaanisha kweli kuziacha, nenda kabatizwe kama ulikuwa hujafanya hivyo katika ubatizo sahihi wa maji tele na kwa jina la Yesu Kristo ambalo ndio jina la Baba, mwana na Roho Mtakatifu. Kisha utapokea Roho Mtakatifu ambaye ndiye atakayokusaidia na kukulinda hadi siku ile ya mwisho.
Ubarikiwe sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
MTU ASIYE PAMOJA NAMI YU KINYUME CHANGU.
NAO WAKADHANI YA KUWA YUMO KATIKA MSAFARA;
Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu ni wakina nani?
Je! Ni kweli ubatizo wa maji hatuuhitaji tena?
Kwanini Kristo hakuitwa Imanueli badala yake akaitwa Yesu?
JE NI DHAMBI KUWA NA MAHUSIANO KABLA YA NDOA?
Mathayo 17:21 [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]
Kuna mambo ambayo kamwe hayawezi kutokea bila kufunga…Neno “kufunga” maana yake ni “kutokuruhusu kitu kiingie wala kitoke sehemu fulani”…..kwamfano kuku ili aweze kuwa na Watoto hana budi kupitia kipindi cha mfungo wa siku 21, kutaga mayai sio kuwa na Watoto, bado kuna kazi nyingine ya ziada…itambidi, ajizuie kula, ajizuie kuzurura-zurura mitaani…ajizuie kucheza na wenzake..ili asilipoteze lile joto, vinginevyo akiwa mzembe mayai yatakuwa viza..na ndege wote wa angani ni hivyo hivyo, upo wakati itawabidi waliache anga kidogo, wajifungie ndani kutamia mayai yao.
Na sio tu mfungo wa kutokujizuia kula unahitajika ili kuumba jambo jipya…bali pia mfungo wa Maisha…kwamfano ili mwanafunzi aweze kufanya vizuri katika mitihani yake…hana budi kufunga milango fulani fulani…atakwenda shule ya bweni (huko tayari ni kifungoni)..atakaa huko miezi hata 6 bila kutoka hata nje ya uzio wa shule, mbali na wazazi wake na ndugu zake, na mafariki zake wa mtaani…ni kama tu kuku aliyeko bandani, sio hilo tu peke yake, itamlazimu aache matumizi ya simu, tv, aache kuangalia tamthilia hizi au zile, movie, aache kabisa kuzurura…itambidi kila siku za muda wake wa masomo aishi Maisha ya kuitumikia elimu..ataamka mapema asubuhi, atachelewa kulala…Sasa anafanya hayo ili asilipoteze lile joto…
Kwasababu anajua akishika mambo mawili au Zaidi kwa wakati mmoja…hatafaulu…kichwa hicho hicho kimoja akikijaza tamthilia, movie na miziki na wakati huo huo masomo…HATAFAULU!…Kwahiyo ni bora aache kimoja afuate kingine…Na Zaidi ya yote anakuwa radhi kuvumilia vyakula vibovu vya shuleni mpaka anahitimu ili tu apate anachokitafuta…
Vivyo hivyo…na katika Imani…hatuna budi kufunga baadhi ya mambo ili TUPATE YALIYO BORA!…Utasema mimi miaka yote nimeshindwa kuushinda uasherati…ni kwasababu haujaamua kuutoa maishani mwako…bado hujafunga baadhi ya milango!…Mbona wengine waliookoka wanaweza kwanini wewe ushindwe?..maana yake tatizo lipo kwako sio kwa Mungu wako!….Hujafunga hiyo milango ya uasherati…bado kuna vimelea vinavyokuchochea wewe kuendelea kuwa hivyo ulivyo…na hivyo si vingine Zaidi ya kampani ulizonazo, au picha unazoziangalia, au mazungumzo unayoyazungumza kila wakati yenye maudhui ya kizinzi, au mitandao unayoitembelea, au mtu unayeishi naye…Kama ukifunga kweli kweli na ukamaanisha kuutafuta uso wa Mungu…hayo mambo hayatakuendesha kamwe!!…
Kwanini hulielewi Neno la Mungu unapolisoma na huku umeshaokoka?… ni tabia tu uliyonayo!…na sababu zake ni zile zile za kwanini mwanafunzi haelewi anaposoma…Ni kwasababu hajaamua kuacha kila kitu na kuongeza umakini kwa kile anachokisoma….Utaona anafungua tu kitabu na kusoma Mada iliyopo katikati ya kitabu, halafu analalamika haelewi…sasa ataelewa vipi?..na wakati mada za kwanza zilipokuwa zinafundishwa darasani yeye alikuwa anacheza huko nje wakati wenzake wanasoma?…
Hali kadhalika utaelewa vipi kitabu cha Yeremia wakati madarasa ya biblia yanayofundishwa makanisani huudhurii??..Hujawahi hata kukisoma kitabu cha Mwanzo peke yako na kukimaliza…utakielewa vipi kitabu cha kutoka?…wakati wa asubuhi au jioni wa utulivu ambao ungetakiwa kukaa chini kwa bidii yako mwenyewe kusoma Biblia…wakati huo ndio unafungua whatsapp na facebook?, kusoma Habari za kidunia??…halafu unalalamika hulielewi neno?…Nakuambia ukweli biblia ni kitabu kirahisi sana kukielewa kuliko vitabu vyote endapo tu, tutaamua kumtii Mungu na kuzingatia kulisoma Neno lake kwa bidii…
kwasababu Roho Mtakatifu yupo kutusaidia kulielewa, kwahiyo kazi inakuwa rahisi sana…
Lakini kama Maisha yako hutajishughulisha kutenga muda kusoma Neno lako mwenyewe, angalau kuanzia kitabu cha Mwanzo, ukatulia, ukasoma hatua kwa hatua..bila kutegemea kufundishwa na mtu…utajikuta ufahamu wako unakuwa kwa haraka sana…na KUZALISHA KITU KIPYA KATIKA MAISHA. Lakini ukipalilia tabia ya kutolisoma kwa bidii Neno, hautazalisha chochote…
Hivyo funga leo vitu ambavyo ulikuwa umeviachia mlango wazi katika Maisha yako, ambavyo vinazuia wewe kutoivisha kitu chochote kipya!…matamthilia ya Kikorea, ya ki-Nigeria, ya-Kifilipino, ya Ki-hindi na mamovie yote pamoja na MIPIRA!…ni mambo yanayoondoa joto la Maisha yako ya kiroho, Jitenge achana nayo Jiondokee..…Wewe utaona unajifurahisha tu, lakini katika roho mayai uliokuwa unayatamia yanazidi kupoa na kuwa viza!…kwasababu tulivyoumbwa hatuwezi kushikilia mambo mawili kwa wakati mmoja.
Je Umewahi kuwasikia watu wanaosema “Ngoja nikatazame tamthilia fulani nipoteze mawazo au ngoja nikatazame movie au mpira nipoteze mawazo au kupunguza stress?”…. umewahi kujiuliza kwanini wanahusisha na neno “kuondoa stress au kupunguza mawazo”?….Ni kwasababu ni kweli wanapokwenda kutazama hayo mambo yanasababisha kile kitu ambacho kilikuwa kimeingia ndani ya mioyo yao kipotee, hivyo kama wakiendelea kujiburudisha hivyo kwa kipindi fulani hatimaye kile kitu ambacho kilikuwa kinawaumiza kichwa kinamezwa na zile burudani….Hali kadhalika kama mtu alikuwa ametoka kusoma Neno vizuri na kulielewa…ile ni mbegu inakuwa imepandwa ndani yake….Lakini sasa anapotoka na kwenda kutazama vichekesho, au mipira, au movie, au tamthilia wakati wote au kuhudhuria hudhuria party party zisizo za muhimu, kidogo kidogo kile kilichopandwa ndani yake kinaanza kujizika….hata kama hapendi! Kitapotea tu!..na baada ya kipindi kupita atajikuta kakisahau kabisa….
Hivyo tunajukumu zito la kulinda kile kilichowekwa ndani yetu na Mungu ili tupate kile tunachokitafuta kumbuka biblia tena hili Neno.
“namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga”.
Nyakati hizi ni za mwisho. Tukaze mwendo tuufikie mwisho mwema wenye mafanikio.
Kwani biblia inasema.. “Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako. (Ufunuo 3:11) ”…
Bwana atubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
JIEPUSHE NA MASHINDANO YA DINI.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 2
DUNIANI MNAYO DHIKI.
ALIYOKUTANA NAYO YESU, YERIKO.
WANA JUHUDI KWA AJILI YA MUNGU, LAKINI SI KATIKA MAARIFA.
MIJI YA MAKIMBILIO.
Ndoto ni eneo ambalo watu wengi wanadanganywa na kupotoshwa Na hiyo yote ni kutokana na kukosa maarifa ya kutosha. Wapo watu wengi mitandaoni, wanaowaeleza watu tafsiri za ndoto mbalimbali zao na mwisho wanaambatanisha na dawa zao za kibishara wakiwadanganya watu kuwa hizo zitaleta suluhisho la matatizo yao.
Wengi wa hao watu kama si wafanyabiashara basi ni waganga wa kienyeji na hawana lolote la kukusaidia zaidi ya kukuongezea matatizo. Kumbuka Ndoto si tatizo la kimwili hivyo hakuna tiba yoyote ya kimwili kama vile dawa ya kunywa au ya kumeza itakayoweza kuleta suluhisho la ndoto zako.
Kwa ufupi Zipo ndoto za aina tatu,
Ndoto zinazotokana na Mungu zinachukua sehemu ndogo sana ya ndoto zote mtu anazoota kila siku naweza kusema hata asilimia 5 tu ya ndoto zote ulizowahi kuota,..
Vivyo hivyo na za shetani nazo hazina asilimia kubwa ya ndoto unazoziota mara kwa mara.
Lakini ndoto zinazotokana na mtu mwenyewe hizi ndizo zinazochukua sehemu kubwa ya ulimwengu wa ndoto za wanadamu. Na hapa ndipo watu wengi wanapokosa shabaha, wakidhani kila ndoto tu wanayoita ni lazima iwe na tafsiri, au ni lazima iwe imebeba ujumbe maalum.
Sasa hizo aina mbili za kwanza, (yaani ndoto za Mungu, na za Shetani) huwa zinabeba maana kubwa sana rohoni, ili kufahamu jinsi ya kuweza kuzitambua aina hizi za ndoto fungua hapa..>>> Tofauti kati ya ndoto za Mungu na Shetani
Leo hii nitajikita kuorodheshea baadhi ya ndoto ambazo watu wengi wanaota na hawajui nyingi kati ya hizo zinatokana na mwili wenyewe..
Ukiota Hizi uzipuuzie, wala usihangaike kutafuta maana zake, kwasabu hizi huwa zinakuja aidha kutokana na shughuli nyingi..
Soma..
Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi;..”
Isaya 29: 8 “Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni”.
Hivyo watu wengi wanaota ndoto nyingi za namna hiyo, na nyingine ubongo unazitengeneza wenyewe. Kwamfano utakuta mtu anatafuta kufahamu Tafsiri za ndoto mbalimbali kama hizi:
Nakadhilika, Nakadhalika..zipo nyingi, nyingine unazijua wewe mwenyewe, hatuwezi kuziorodhesha zote hapa.. Lakini zote hizo hazina umuhimu wa kutafuta kujua maana zake. Kwasababu ukienda kwa mtindo huo utachanganyikiwa mwilini na rohoni.
Kikubwa ni kufahamu kuwa njia Kuu ambayo Mungu aliichagua kuzungumza na wanadamu ni kupitia Neno lake (Biblia tu)
Ikiwa wewe ni mwenye dhambi nataka nikuambie hizi ni nyakati za mwisho, Mafundisho mengi ya uongo, na ya mashetani yamezaa kila mahali, Usipotaka kusimama, shetani ni lazima akuzombe kwenye aina ya mafundisho hayo ya mashetani na kukupa tafsiri ya kila ndoto unayoita….
Tubu mgeukie Mungu wako, dalili zote zinathibitisha hilo kuwa tunaishi katika siku za mwisho. Maisha yako yapo hatarini sana, kwani hujui siku yako ya kuondoka ni lini, na hata kama hutaondoka leo au kesho, lakini UNYAKUO upo karibuni sana.. Yesu yupo mlangoni kuja kuwachukua wateule wake.
Angalia hali halisi ya ulimwengu ulivyo sasa halafu niambie ni dalili ipo Yesu aliyosema kuhusu siku za mwisho haijatimia, angalia magonjwa ya mlipuko, angalia tetesi za vita, angalia matetemeko, angalia kuongozeka kwa maasi duniani,..yote hayo yalitabiriwa.
Huu si wakati wa kuangalia mambo mengine Zaidi ya wokovu wako. Nani ajuaye leo hii Mungu kakupitisha kwenye ukurasa huu ni ili Akuokoe? Kwasababu anaompango mkubwa na wewe maishani mwako?
Hivyo kama wewe ni mwislamu usiogope kumkabidhi YESU Maisha yako leo, fungua tu moyo wako mruhusu atende kazi, nawe utaona badiliko la ajabu atakalolileta ndani yako.
Ikiwa upo tayari kufanya hivyo basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, . NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.
Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.
Ubarikiwe sana.
Bofya chini kwa kujiunga na magroup yetu ya Whatsapp, kwa mafundisho ya kila siku.
Mada nyinginezo:
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..
CHUKIZO LA UHARIBIFU
UNYAKUO.
MIJI YA MAKIMBILIO.
WAKATI ULIOKUBALIKA NDIO SASA.
MAHALI UNAPOPASWA USIMVUMILIE SHETANI HATA KIDOGO.
Hebu tuchukue muda kidogo kuisoma habari ifuatayo naamini tutajifunza kitu,
1Samweli 11: 1 “Ikawa, kama baada ya mwezi mmoja, Nahashi, Mwamoni ,akakwea na kupanga marago juu ya Yabesh-gileadi;na watu wote wa Yabeshi wakamwambia Nahashi, Fanya mapatano nasi,na sisi tutakutumikia.
2 Huyo Nahashi, Mwamoni, akawaambia, Kwa sharti hii mimi nitapatana nanyi, kila mtu ang’olewe jicho la kuume; na kwa jambo hilo nitawashutumu Waisraeli wote pia.
3 Basi wazee wa Yabeshi wakamjibu, Tuachie siku saba, ili tutume wajumbe waende mipakani mwote mwa Israeli; kisha, ikiwa hakuna atakayetuokoa, tutakutokea.
4 Hivyo wajumbe wakafika Gibea ya Sauli, wakasema maneno hayo masikioni mwa watu; na watu wote wakainua sauti zao wakalia.
5 Na tazama, Sauli akaja akifuata ng’ombe kutoka kondeni; naye Sauli akauliza, Watu hawa wana nini, hata wakalia? Wakamwambia maneno ya watu wale wa Yabeshi.
6 Na roho ya MUNGU IKAMJILIA SAULI KWA NGUVU, hapo alipoyasikia maneno yale, na hasira yake ikawaka sana.
7 Naye akatwaa jozi ya ng’ombe, akawakata-kata vipande, kisha akavipeleka vile vipande mipakani mwote mwa Israeli kwa mikono ya wajumbe, kusema, Ye yote asiyetoka nyuma ya Sauli na Samweli, ng’ombe zake watatendwa vivi hivi. Basi utisho wa Bwana ukawaangukia wale watu, wakatoka kama mtu mmoja.
8 Naye akawahesabu huko Bezeki; Waisraeli walikuwa mia tatu elfu, na Wayuda thelathini elfu.
9 Nao wakawaambia hao wajumbe waliokuja, Waambieni watu wa Yabesh-gileadi, Kesho, WAKATI WA JUA KALI, mtapata wokovu. Basi wale wajumbe wakaenda, wakawaarifu watu wa Yabeshi; nao walifurahiwa.
10 Kwa hiyo watu wa Yabeshi walisema, Kesho tutawatokea, nanyi mtatufanyia yote myaonayo kuwa ni mema.
11 Ikawa, kesho yake, Sauli akawapanga watu katika vikosi vitatu; nao wakaingia katikati ya marago kwenye zamu ya asubuhi, wakawapiga Waamoni hata WAKATI WA JUA KALI; kisha ikawa wale waliosalia wakatawanyika, hata wasiachwe wawili wao pamoja”.
Biblia inasema taa ya mwili ni jicho, maana yake mtu akitolewa macho anakuwa kipofu, giza linaingia katika mwili wake wote, hebu fanya utafiti wa kufunga macho yako uone utakachokiona…bila shaka ni giza tupu…
Mathayo 6:22 “Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru.
23 Lakini jicho lako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Basi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza hilo!”
Kwahiyo kwa tukio hilo hapo juu, kuna wakati Mfalme wa Moabu alitaka kuingia katika ardhi ya Israeli inayoitwa Yabeshi, na alipoingia kwasababu ya wingi wa majeshi yake akawatishia Israeli vikali, nao wakaogopa, wakanyenyekea chini yake wakamwambia fanya mapatano nasi (maana yake kama unataka kitu chochote kutoka kwetu hata kama ni kodi tutakupatia)..lakini Yule mfalme kwa kiburi akasema hatataka kitu chochote bali kumng’oa kila mtu wa mji huo wa Yabeshi jicho la kuume…Na lengo la kuwaambia hivyo ni ile awaaibishe na pia aliingize giza katika mji ule, kwasababu alijua jicho la mtu ndio mwangaza wake..mtu hakuna chochote anaweza kufanya.
Jambo hilo liliwahuzunisha watu wa Yabeshi, mpaka kufikia hatua ya kwenda kuomba msaada wa ndugu zao waisraeli walio kwenye majimbo mengine, na wakati huo Israeli walikuwa wameshajitakia mfalme, na walimteua Sauli…lakini kila mtu alikuwa anamdharau Sauli kwa kuwa walimwona kama ni kijana laini asiye na uwezo wa kutawala wala wa vita. Lakini biblia inasema ROHO YA MUNGU ilimjia Sauli kwa nguvu na kumpa moyo wa ujasiri na ushujaa, na kutoka kwenda kuwapiga wamoabu na kuwaangamiza wote kabisa…Lakini jambo pekee ni kwamba hawakuwapiga wakati wa jioni, au wakati wa asubuhi, bali waliwapiga wakati wa JUA KALI linaloangaza…Kuashiria kuwa wao sio WANA WA USIKU bali wa Mchana.. Na kamwe Nuru ya macho yao haiwezi kuzimwa…wala giza haliwezi kuingia kwao. Hivyo kwa imani waliwaua wakati wa jua kali..
Kama tujuavyo wakati wa jua kali, ndipo watu wanazimia nguvu, ndio wakati watu wanachoka haraka, ndio wakati ambao mwili unapungukiwa maji….Lakini kwa majeshi ya Bwana, hicho ni kinyume chake…wakati wa mchana ndio wakati wa kushinda na kupambana…
Wakati wa mchana(jua kali) ndio wakati wa kuingia vitani, wakati wa mchana ndio wakati wa kwenda kuyavamia majeshi ya adui, wakati wa mchana ndio wakati wa kwenda kuteka nyara, ndio wakati wa kumnyang’anya shetani mateka, wakati wa jua kali ndio wakati wa kuhubiri injili..
Bwana Yesu alisema…
Yohana 9:4 “Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi
5 Muda nilipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu.”.
Wakati huu wa jua kali ndio wakati adui yetu kukosa nguvu, ndio wakati anaoungua, ndio wakati ambao anakimbilia kivulini na mafichoni…hivyo ndio wakati wa kumfuata huko kwa vishindo kama Sauli alivyofanya, na kumwangusha na kumnyang’anya mateka sio wakati wa sisi kulitafuta giza au kivuli kama wao.. “Na Yesu ndio Nuru yetu, ndio jua letu..na sisi ni wana wa Nuru, jua lake halituchomi wala halituumizi wala halituchoshi, wala halitumalizi maji mwilini”..linawadhoofisha maadui zetu lakini si sisi.
Isaya 18:4 “Maanaa Bwana ameniambia hivi, Mimi nitatulia, na kuangalia katika makazi yangu, kama wakati wa mwangaza mweupe wa JUA KALI, mfano wa wingu la umande katika hari ya mavuno”.
Ifanye kazi ya Mungu wakati huu wa Neema, wakati huu wa jua kali…usiku unakuja ambao hutaweza…wakati adui atakuwa na nguvu…na wakati huo ni kipindi cha dhiki kuu…wakati ambao neema ya Yesu itafungwa…huo ndio wakati wa mamlaka ya nguvu za giza kutenda kazi..kutatokea dhiki isiyo ya kawaida!. Yule joka atakapopata nguvu…..Bwana atuepushe na hiyo dhiki, ili wakati huo utakapofika utukute tuwe tumeshanyakuliwa na watakatifu wengine kwenda mbinguni kwa baba na tumeshaimaliza kazi yake.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Nuhu alipataje ujuzi wa kuwatambua wanyama wale wote na kuwaweka ndani ya Safina?
Shalom,
Jina la mwokozi wetu, Mfalme wa Wafalme na Bwana wa mabwana, Yesu Kristo libarikiwe daima. Ni siku nyingine tena hivyo Nakukaribisha tuyatafakari pamoja maandiko.
Neno linasema..
Warumi 10:1 “Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe.
2 Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa”.
Kama tunavyoweza kuona hapo kuwa “Juhudi” tu peke yake hazitoshi, kama hatuna maarifa ya kutosha ya kumwabudu Mungu, tutakuwa tunafanya kazi bure.. Na hapa ndipo kundi kubwa la sisi wanadamu tunaposhindwa kumfikia Mungu, tunaishia kuona kama vile Mungu hayupo na sisi japokuwa tunajibidiisha kwake..
Leo tutayatazama makundi mawili ya watu wa namna hii katika biblia ambao kweli yana bidii kwa ajili ya Mungu lakini sio katika maarifa:
Kundi la kwanza ni lile la watu walio ndani ya Imani ya Kikristo.
Na Kundi la Pili ni lile lililo nje Ya Imani ya Kikristo, lakini linadai kuwa linamtafuta Mungu wa kweli na linampenda.
Tutayatazama yote mawili kibiblia, na ikiwa mimi au wewe, au sote tunaangukia kwenye mojawapo ya makundi hayo basi tujithamini mapema na kugeuka haraka sana kabla ya kupotea kwetu.
Tukianzana na hili kundi la kwanza ambalo ni la wale walio ndani ya Kristo…
Sasa Katika biblia Kuna mtu anaitwa Martha. Huyu Siku moja alimkaribisha Bwana Yesu kwake. Lakini yeye hakujua Kristo anataka nini, badala yake akawa anajitaabisha na mambo mengine yasiyo na maana sana machoni pa Bwana, mara anakwenda kuosha vyombo, mara anakwenda jikoni kuandaa chakula, mara anachota maji kwenye majagi kwa ajili ya wageni, mara anafanya hiki mara kile,..Na kibaya zaidi kilichokuwa kinamkasirisha ni pale anapomwona mdogo wake, Miriamu hajisumbui kwa lolote ameketi tu pale miguuni pake akimsikiliza Bwana..
Martha kuona vile akidhani ni utomvu wa nidhani, akamsemelea kwa Bwana ili aondoke pale..Lakini Bwana akasema..
Luka 10:41 “…. Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi;
42 lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa”.
Sasa huyu ni mfano wa watu ambao wanaobidii kweli kwa ajili ya Mungu lakini si katika maarifa..Wanadhani Mungu anapendezwa na taabu zao na masumbufu yao na huku maagizo ya msingi ya rohoni wanayaacha yawapite..
Leo hii lipo kundi la wakristo, ambao, hawana muda wa kuyatafakari maneno ya uzima ya Kristo, hawana muda wa kusali, hawana muda wa kumwomba Roho Mtakatifu awafundishe mapenzi ya YESU, hawana hata muda wa kuutafuta ubatizo sahihi, lakini kwenye kwaya wapo na wana bidii sana, kwenye ujenzi wa kanisa wapo, na wanajitoa kwa bidii, kwenye michango yote wapo haiwapiti, wako tayari kufanya hiki au kile kwa ajili tu ya Mungu hawaachi, wanajitoa kweli hata usafi wa kanisa ni wenye bidii sana, lakini tukirudi kwenye bible-study tu, huwaoni,..
Ni kweli wanachokifanya si kibaya, wanajuhudi kwa ajili ya Mungu lakini si katika maarifa kama vile Martha..Hivyo mbele za Mungu wanaonekana hawajafanya chochote haijalishi bidii yao ni kubwa kiasi gani. Kwasababu mambo ya msingi wameyaacha. Kwasababu ni heri usiwe unaimba kwaya, ni heri ukawa hufanyi mambo mengine lakini Neno la Mungu unalishika kwa bidii na unalisoma sana na kulichunguza, na umebatizwa, na umepokea Roho Mtakatifu, unaweza ukakosa kitu cha kuchangia lakini ukawa ni mtu wa kusali sana, ukawa ni mtu ambaye haiwezi kupita siku hujajifunza biblia na kuisoma peke yako pasipo kusubiria mtu fulani akuelezee, huku ukimtegemea Roho Mtakatifu akufundishe n.k.
Kundi la Pili: Ni la watu ambao si wakristo, lakini wapo ulimwenguni kote wanadai kuwa wanamuheshimu Mungu.. Na wengi wao ni kweli wanao nia nzuri, na wanaweza wakawa na juhudi kubwa kwa ajili ya Mungu kuliko hata wewe, lakini mwisho wake, watu wa namna hii, huwa ndio wanakwenda mbali kabisa na mpango wa Mungu, na wakati mwingine wanaiharibu kabisa kazi yake.. Na hiyo yote ni kutokana na kukosa maarifa ya kumwabudia Mungu.
Mfano wa watu hawa ni Mtume Paulo mwenyewe. Yeye kabla ya kumpokea Kristo alikuwa ni mtu mwenye bidii kwa Mungu kweli, lakini kwasababu alikosa maarifa matokeo yake akawa anawaua mpaka wakristo akidhani anamtolea Mungu sadaka (Wafilipi 3:6-7)..Na wayahudi wengine wote ndio walikuwa vivyo hivyo kama yeye.
Wengine walio katika kundi hili ni waislamu..Sio wote unaowaona wanawachinja watu kule Syria na Iraq na Somalia ukadhani hawampendi Mungu..hapana, wengine wanafanya vile kwasababu wanadhani ndio wanamuheshimu Mungu, kama mtume Paulo, kumbe juhudi zao si katika maarifa na hivyo inawafanya wazidi kupotea Zaidi na kwenda kinyume na Mungu, na hata kuwa adui wa Mungu kabisa..Kama vile Neno linavyosema..
Hosea 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa..”
Lakini maarifa sahihi yanapatikana wapi?
Ndugu, ni kwanini tunasisitiza sana YESU, YESU, YESU,? Nikwasababu maarifa yote na hekima yote zinapatikana kwake tu (Wakolosai 2:3). Huyo tu, ukimpata, au ukimjua katika usahihi wote, basi ujue kuwa utamwabudu Mungu katika maarifa na sio katika ujinga.
Waefeso 4:13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana MWANA WA MUNGU, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo”
Na Yesu yupo wapi? Jibu ni kuwa Yupo katika NENO lake(biblia)..Hivyo kama wewe ni muislamu au upo katika dini nyingine yoyote, mgeukie Yesu sasa, mwamini yeye, ayaongoze Maisha yako. umwabudu Mungu katika maarifa anayoyataka, ili akufurahie..kwasababu anasema..
Yohana 14:6 “…Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi”… Hakuna njia nyingine ya kumfikia Baba isipokuwa kwa kupitia Yesu.
Vilevile na wewe kama ni mkristo lakini bado unasua sua, unaishi kidini dini tu,..kwaya kwako ni muhimu kuliko kulisoma Neno, kutoa sadaka nyingi kwako ni muhimu kuliko kuutafuta ubatizo sahihi na Roho Mtakatifu, Huu ni wakati wako wa kujihurumia, na kugeuka na kuanza kumwabudu yeye katika Roho na Kweli, kwa kujifunza mapenzi yake katika Neno lake (biblia).
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo: