SWALI: Kwanini Mtume Paulo, alimkataza Timotheo asiwaandike wajane vijana? Je wajane vijana hawapaswi kusaidiwa au?
Jibu: Kabla ya kwenda kwenye jibu la swali letu, kuna mambo muhimu ya kufahamu kwanza ya utangulizi.
Katika kanisa la kwanza kulikuwa na utaratibu wa kuwasaidia wazee, hususani wale wenye umri mkubwa sana. Ambao hawawezi kufanya kazi wala hawana mtu wa kuwasaidia, kama Watoto au wajukuu.
Sasa haikuwa kila mzee tu, anayejiunga na kanisa alikuwa anasaidiwa la! Haikuwa hivyo, Kulikuwa na vigezo au sifa za wazee waliokuwa wanastahili kusaidiwa. Na sifa hizo tunazisoma katika kitabu cha Timotheo..
1Timotheo 5:9 “Mjane asiandikwe isipokuwa umri wake amepata miaka sitini; naye amekuwa mke wa mume mmoja;
10 naye ameshuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata kwa bidii kila tendo jema”.
Maana yake ni kwamba kama sio mjane, anaye mume..basi huyo tayari anaweza kuhudumiwa na Mume wake, kwa mahitaji yake, hivyo asiandikwe kwenye orodha ya wanaostahili kusaidiwa na kanisa ili kanisa lisije likalemewa.
Maana yake ni kwamba akiwa chini ya umri huo, bado anayo nguvu za kufanya kazi za kujipatia kipato, hivyo anaweza kuendelea kufanya kazi zake za mikono huku akiendelea na kazi ya kuhudumu katika kanisa..Ili kanisa lisije likalemewa.
Maana yake ni kwamba kabla ya mume wake kufa, awe na rekodi ya kuwa na huyo huyo mume mmoja, na sio awe na rekodi ya kuwa na wanaume wengi. Mwanamke yeyote mwenye hiyo rekodi ya kuwa na wanaume wengi, hana sifa ya kuandikwa kwenye orodha ya wanaohitaji kusaidiwa.
Maana yake ni kwamba sio tu mtu, kazeeka hivyo anaona sehemu ya kwenda kumalizia pensheni ya uzeeni ni kanisani, hivyo anakwenda kujiunga ili tu awe ana hudumiwa. Biblia imesema watu wa namna hiyo wasiandikwe..Watu wanaopaswa kuandikwa ni lazima wawe na rekodi ya kuifanya kazi ya Mungu katika kanisa Pamoja na matendo mema, na utakatifu.
Sasa hapo biblia imeruhusu watu wenye sifa hizo kusaidiwa, lakini haikusema kila mwanamke anayefikia umri wa miaka 60 au Zaidi na ni mjane, ni lazima aandikwe kwenye orodha ya watakaosaidiwa. Hapana!!.. Kama mjane ana miaka Zaidi ya 60, na una uwezo mzuri wa kiuchumi, hapaswi kuandikwa, vile vile kama anao Watoto, au ndugu ambao wanaweza kumtunza vizuri, ni mume tu ndio hana, vile vile hapaswi kuandikwa. Wanaondikwa ni wale wajane kweli kweli ambao hawana mtu yeyote waliyebakiwa naye wa kuwasaidia, wamebaki wenyewe. Na tumaini lao lote lipo kwa Bwana, hao ndio wanaopaswa kuwekwa kwenye orodha ili kanisa lisilemewe.
1Timotheo 5:3 “Uwaheshimu wajane walio wajane kweli kweli.
4 Lakini mjane akiwa ana watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kuyatenda yaliyo wajibu wao kwa jamaa zao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Kwa kuwa hili lakubalika mbele za Mungu.
5 Basi yeye aliye mjane kweli kweli, ameachwa peke yake, huyo amemwekea Mungu tumaini lake, naye hudumu katika maombi na sala mchana na usiku”
1Timotheo 5: 16 “Mwanamke aaminiye, akiwa ana wajane, na awasaidie mwenyewe, Kanisa lisilemewe; ili liwasaidie wale walio wajane kweli kweli”.
Sasa tukirudi kwenye swali, ni kwanini wajane vijana hawapaswi kuandikwa?.
Sababu ya kwanza tumeshaiona hapo juu, ni ili kanisa lisilemewe, kwasababu wanao nguvu na uwezo wa kufanya kazi, hivyo fungu hilo la posho, ni heri likawasaidie wale ambao hawana uwezo kabisa wa kufanya kazi, wenye umri mkubwa, ambao hawana tumaini kabisa.
Sababu ya pili ndiyo hiyo tunayoisoma katika 1Timotheo 5:11-15.
Tusome..
1Timotheo 5:11 “Bali wajane walio vijana ukatae kuwaandika hao, maana, wakizidiwa na tamaa kinyume cha Kristo, wataka kuolewa;
12 nao wana hukumu kwa kuwa wameiacha imani yao ya kwanza.
13 Tena, pamoja na hayo, hujifunza kuwa wavivu, wakizunguka-zunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi na wadadisi, wakinena maneno yasiyowapasa.
14 Basi napenda wajane, ambao si wazee, waolewe, wazae watoto, wawe na madaraka ya nyumbani; ili wasimpe adui nafasi ya kulaumu.
15 Kwa maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani”
Ni ukweli usiopingika kuwa asilimia kubwa ya wanawake ni “watu wa kupenda udadi, au umbea, kutafuta tafuta kujua mambo ya watu wengine”.. Na wengi wa hao ni wale ambao hawana shughuli maalumu za kufanya, na wenye umri kati ya miaka 20-45 na wengine hadi 50. Mwanamke wa rika hili, akishakosa shughuli ya kufanya, na Zaidi akiwa hajaolewa, ni rahisi sana kuchukuliwa na hiyo roho ya udadisi dadisi. Na wivu wivu, tofauti na mwanamke ambaye ameolewa au mwenye shughuli maalumu ya kufanya. Kwasababu mwanamke aliyeolewa atakuwa akili yake yote ipo katika kuiendesha familia yake na kuitunza na kuangalia Watoto wake.
Sasa katika kanisa pia wapo wanawake, ambao ni wa rika hilo, Ambao baada ya waume zao kufa wamekuwa wajane, hivyo na wenyewe wanajiweka kwenye kundi hilo la wanawake wajane ambao kazi yao ni kudumu katika sala na maombi na kuhudumu kanisani siku zote (tumaini lao lote lipo kwa Bwana 1Timotheo. 5:5)… Hivyo na wao wanajiweka katika kundi la watu wanaohitaji kusaidiwa na kanisa.
Lakini tatizo lilionekana kwamba wengi wa wanawake hawa ambao ni vijana, wanakuja kugeuka tabia siku za mbeleni na kuanza kujiingiza kwenye mahusiano yasiyo rasmi, na tabia hizo za udadisi. Na hivyo hivyo wanakuwa wameiacha Imani ambayo walikuwa nayo hapo kwanza. Na hivyo kujiingia kwenye hukumu, kwasababu wameiacha Imani.
Kuacha Imani ya kwanza, maana yake kuacha njia ya haki waliyokuwa wanaiendea hapo kwanza.
Kwahiyo wanawake hawa, biblia imesema wasiandikwe, badala yake ni vizuri wakaolewa tena, ili wazae Watoto, wawe na majukumu, kwasababu watakapokuwa na majukumu na watakapokuwa na Watoto, watakuwa busy na familia zao, hivyo si rahisi kushawishika kuwaka tamaa na kuwa wadadisi, tofauti na wakitanga tanga bila kuwa na majukumu, ni rahisi kuchukuliwa na tamaa za kila namna.
Lakini pia kumbuka si wanawake wote ambao ni wajane na ni vijana, wana tabia hizo…Hapana!..Hapo biblia imemaanisha ni wengi wao, lakini si wote. Wapo ambao ni wajane vijana, au hawajaolewa lakini wanaishikilia Imani, Ingawa wapo wachache sana. Katika biblia alikuwepo mwanamke aliyeitwa Ana, ambaye aliishikilia Imani bila kuiacha tangu mume wake alipokufa angali akiwa bado binti mdogo, na mpaka akiwa na miaka 80, hakuiacha Imani. Na Mungu akampa neema ya kumjua mtoto Yesu kuwa ndiye Masihi katika uchanga ule. Wakati wengine hata Yesu alipokuwa mtu mzima bado hawakumwamini.
Luka 2:36 “Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake.
37 Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.
38 Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake”.
Bwana atubariki
Maran atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618.
Jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
CHUKI ULIZO NAZO KWA MAADUI ZAKO, SIZO ALIZONAZO MUNGU JUU YAO.
Nguo za magunia( au mavazi ya magunia) ndiyo mavazi ya namna gani ?
Magunia kama biblia inavyotafsiri ni tofauti na inavyotafsiriwa sasa, Leo hii ukizungumzia magunia unamaanisha labda mifuko aina ya Salfeti (Sulphate) ambayo yanatumika sana sana katika kuhifadhia nafaka, au utakuwa unazungumiza magunia yaliyoshonwa kwa nyuzi za katani.
Lakini mavazi ya magunia, biblia haiyatafsiri kama mavazi yaliyotengenezwa kwa mojawapo ya malighafi hizo (salfeti au nyuzi za katani). Bali mavazi ya magunia yaliyozungumziwa kwenye biblia ni mavazi yaliyotengenezwa kwa MANYOYA YA MBUZI.
Nguo hizo zilitengenezwa mahususi, kuashiria aidha vitu hivi viwili Maombolezo au Toba
1. Maombolezo.
Watu zamani za biblia waliopitia misiba, au majanga walikuwa wanavaa nguo hizo za magunia kuonyesha hali ya maombolezo, kuonyeshwa kuguswa na tatizo hilo, na kwamba wapo katika huzuni na si furaha..
Mfano wa hao ni Rispa aliyeomboleza baada ya kufiwa na wanawe.
2Wafalme 21:10 “Naye Rispa, binti Aya, akatwaa nguo ya magunia akajitandikia mwambani, tangu mwanzo wa mavuno hata waliponyeshewa mvua toka mbinguni; wala hakuacha ndege wa angani kukaa juu yao mchana, wala wanyama wa mwitu usiku”
Tunaona mfano mwingine ni wana wa Israeli, baada ya kupata msiba wa kupelekwa utumwani..biblia inasema iliwapasa wavae mavazi ya magunia kwa maombolezo..
Yeremia 4: 8 “Kwa sababu hiyo jifungeni NGUO ZA MAGUNIA; ombolezeni na kulia kwa uchungu; kwa maana hasira kali ya Bwana haikugeuka na kutuacha”
Yeremia 6:26 “Ee binti wa watu wangu, ujivike NGUO YA MAGUNIA, na kugaagaa katika majivu; fanya maombolezo, kama maombolezo kwa ajili ya mwana wa pekee, maombolezo ya uchungu mwingi; maana mwenye kuteka nyara atakuja juu yetu ghafula”.
Mifano mingine watu waliovaa mavazi ya magunia, kuashiria maombolezo unaweza kuisoma katika mistari ifuatayo (2Wafalme 6:30, 2Wafalme 19:1)
2. Toba
Watu pia walipotaka kujisongeza mbele za Mungu, kwa toba..walivaa nguo za magunia, kuashiria hali ya unyenyekevu, na kujishusha, kwamba wao si kitu mbele ya Mungu mkuu, na hivyo kutaka rehema kutoka kwake. Mfano wa watu hao ni nabii Danieli.
Danieli 9:3 “Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na KUVAA NGUO ZA MAGUNIA na majivu.
4 Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake”
Na mfano mwingine ni watu wa Ninawi..
Yona 3: 5 “Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, WAKAJIVIKA NGUO ZA MAGUNIA, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo.
6 Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, AKAVUA VAZI LAKE, AKAJIVIKA NGUO ZA MAGUNIA, na kuketi katika majivu”
Na wengine mfano wa hao, unaweza kuwasoma katika mistari ifuatayo (2Wafalme 19:1, Nehemia 9:1).
Je wakristo sasa Nasi pia tunapaswa kuvaa mavazi ya magunia pindi tunapotubu kwa Mungu wetu au tunapomboleza pindi tunapopitia na misiba?.
Huo ni uchaguzi wa mtu avae au asivae. Lakini biblia haijatoa amri kwamba lazima mtu avae magunia anapotubu.. Ilichotia msisitizo ni hichi..
Yoeli 2:12 “Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea;
13 RARUENI MIOYO YENU, WALA SI MAVAZI YENU, MKAMRUDIE BWANA, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya”
Hapo inasema turarue mioyo yetu na si mavazi yetu…Kumbuka mavazi yanayozungumziwa hapo ndio hayo ya magunia, na si vile vimini, au mavazi yasiyo ya heshima yanayovaliwa na wadada. Hayo mtu anapookoka hapaswi kabisa kuendelea kuyavaa.
Je umeurarua moyo wako kwa Bwana? Kama bado Ni vyema ukafanya hivyo mapema
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618.
Jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Jina la Bwana wetu Yesu libarikiwe. Unapomkiri Yesu kwa Kinywa, au unapojisalimisha kwa Yesu, kwa kudhamiria kabisa, dakika hiyo hiyo..Shetani anaangushwa juu yako, kama umeme…Na anawekwa chini ya miguu yako na unakabidhiwa mamlaka, juu yake.
Luka 10: 18 “Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni KAMA UMEME.
19 Tazama, NIMEWAPA AMRI YA KUKANYAGA NYOKA NA NGE, NA NGUVU ZOTE ZA YULE ADUI, wala hakuna kitu kitakachowadhuru”
Hapo kuna vitu vitatu ambavyo unapewa amri juu ya hivyo.
Amri ya kukanyaga NYOKA. 2). amri ya kukanyaga NGE na 3). amri ya kukanyaga NGUVU ZOTE ZA YULE ADUI.
Nyoka ni kiumbe anayeuma (au anayeng’ata kwa kutumia mdomo)..Silaha yake kubwa ni mdomo na mate yake, hana silaha nyingine kiasi kwamba ukikibana kile kichwa hakuna atakachoweza kufanya ili kukudhuru. Nyoka ni mfano wa Watu wanaotumika na shetani, kwa kujua au kwa kutokujua kukudhuru wewe kupitia maneno wanayoyazungumza…Yaani kwaufupi silaha yao ni maneno..
Zaburi 143:1 “Ee Bwana, uniokoe na mtu mbaya, Unihifadhi na mtu wa jeuri.
2 Waliowaza mabaya mioyoni mwao, Kila siku huondokesha vita.
3 Wamenoa ndimi zao kama nyoka, Sumu ya fira i chini ya midomo yao”
Fira ni nyoka aina ya KOBRA, Sasa hao Biblia imesema tumepewa amri juu yao..”kuwakanyaga”…Sasa hatuwakanyagi na sisi kwa kuwarudishia maneno.. Hapana, tukifanya hivyo na sisi tutakuwa ni nyoka kama hao. Lakini tunakanyaga vichwa kwa kuyapuuza maneno yale, na kuyazuia yasiingie moyoni mwetu..
Kwasababu ukiyaruhusu yaingie moyoni mwako, yatakuwa sumu kwako na yatakudhuru.. Hivyo unayapuuzia yale maneno na kuyapiga mateke, hiyo ni silaha kubwa sana..Ambayo kwa hiyo utaweza kuwakanyaga nyoka wote.. (Kumbuka nyoka hapo ni lugha ya rohoni, usimwite kamwe ndugu yako nyoka hata kama ni mbaya kiasi gani kwako).
Nge ni mdudu anayeuma kwa kutumia MKIA, na si Mdomo kama nyoka. Hawa ni jamii ya watu ambao wanatumika na shetani pasipo kujua au kwa kujua. Ambao kwa mbele ni wazuri lakini kwa nyuma wanatumia mkia kukudhuru, na kama unavyojua mkia wa nge, umepanga juu ukazunguka lengo lake ni kukuchoma wewe kwa nyuma, pasipo kujua ni nani kakudhuru.
Hivyo shetani anaweza kutumia watu wanaoonekana ni wazuri kwa nje lakini kumbe ni wenye madhara juu yako, watu wa namna hiyo tumepewa amri ya kuwakanyaga..Hatuwakanyagi kwa kuwachukia wala kufanya nao vita bila wao kujijua, tukifanya hivyo na sisi tutakuwa nge, ambao hatungati kwa mdomo lakini tunang’ata kwa mkia..Hivyo na hawa tumepewa silaha ya kushughulika nao, na hiyo si nyingine Zaidi ya MIGUU YETU, Maana yake kutotafuta tafuta wanachokiwaza juu yetu wala kukifikiri juu yako wanatuwazia nini, maana yake wewe unasonga mbele, hufuatilii wewe unaendelea mbele na mambo yako unayoyafanya.
Kama vile watu wanavyolikanyaga neno la Mungu chini, maana yake ni kwamba wanalipuuzia, wanaendelea na mambo yao, vivyo hivyo na wewe unakanyaga maneno yao, au hila zao…kwa kuzipuuzia, na kwajinsi unavyozidi kuzipuuza ndivyo zinavyozidi kuishiwa nguvu, kwasababu utakuwa umempa Mungu nafasi kubwa ya kukupigania, na mwisho wa siku watatubu na kushawishika kumwamini Mungu wako, na utakuwa umeokoa roho zao.
Kipengele hicho ndio cha mwisho na cha Muhimu sana..Ambacho shetani hataki watu wakijue wala wakielewe, kwasababu kinamhusu yeye mwenyewe na mapepo yake, na wala hakiwahusu watu anaowatumia..
Shetani anapenda kuwaaminisha watu kuwa yeye ana nguvu sana, na hivyo akishika mahali ni ngumu yeye kutolewa..Hivyo watu wengi wamefungwa na nguvu za Ibilisi kwa muda mrefu kwasababu tu ya Imani hiyo ndani yao. Utakuta mtu anaumwa, au anapitia tatizo Fulani, na lile tatizo ndani yake kashalikuza na kuwa kubwa mno, na kuamini kuwa inahitajika nguvu nyingi sana za rohoni kuliondoa, au upako mwingi kuliondoa..Wengine wanatokewa kabisa na mapepo wazi, wangine yanawajia katika ndoto, wengine wananyanyaswa na mashetani usiku, kiasi kwamba hata wanaogopa kulala wenyewe. Wengine wanatishiwa na kusumbuliwa na shetani kwa namna ambayo hata wanashindwa kusimulia, mwisho wa siku wanakata tamaa hata ya kuishi. Na kundi hili lipo kubwa sana.
Sasa watu kama hawa, shetani amewashika kwa kutumia Imani yao kupata nafasi ya kuwatesa.
Biblia inasema hapo, tumepewa Amri ya KUKANYAGA… Unaelewa maana ya kukanyaga???…Kukanyaga maana yake ni KULIPOTEZEA JAMBO!!..Kulishusha hadhi, kulipunguza nguvu, kuliabisha, kulidhalilisha, kulidharau. Hiyo ndio maana ya kukanyaga, wala kukanyaga sio kuingia kwenye maombi ya mifungo ya masafa, hapana hiyo sio maana yake.. Maana yake ni kuliweka chini yako jambo. Kama tu vile watu wanavyolikanyaga chini neno la Mungu, wanafanya hivyo kwa kulidharau…Kitendo cha kukidharau kitu tayari umekikanyaga chini.
Waebrania 10.28 “Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.
29 Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?”
Umeona hapo?. Watu wote wanaoihesabia damu ya agano la Yesu kuwa ni kitu ovyo, na kumdharau (au kwa lugha ya sasa, ni kuipotezea), watu hao ndio wanahesabika kama wamemkanyaga Mwana wa Adamu.
Ni hivyo hivyo, mtu anayehesabia kazi za shetani kuwa ni kitu ovyo, hapo anakuwa amemkanyaga chini, ya miguu yake.
Hivyo kwa silaha ile ile tunayotumia kukanyaga nyoka na nge, ndiyo hiyo hiyo tunayotumia KUZIKANYAGA NGUVU ZOTE ZA YULE ADUI. Wala hakuna silaha nyingine, shetani asikuogopeshe ikiwa upo tayari ndani ya Kristo..
Maana yake ni hii.
Baada ya kumkiri Yesu, kama ulikuwa unaumwa na kuamini kwamba ni ngumu kupona ugonjwa ulio nao, HILO wazo unaanza kulidharau ndani yako, kuanzia sasa (unalikanyaga!)..
> Shetani alikuwa amekutishia kwamba dhambi yako haisameheki, unalidharau hilo wazo, na kulipoteza kwenye akili yako..
> Mapepo yalikuwa yanakuhubiria kwamba utakufa kila siku kwenye mawazo yako, unayapotezea hayo mawazo na kuyadharau, na kusema hilo halipo..kwa jinsi unavyozidi kuyashusha hadhi hayo mawazo ya shetani, na uongo wake huo…ndivyo na yenyewe yanavyozidi kukosa nguvu juu yako na hatimaye kupotea kabisa.
> Maroho yalikuwa yanakukaba usiku, Hizo sauti zinazokuambia kwamba yatarudi tena huzitilii maanani..acha kabisa kuyapa hayo mapepo heshima kubwa kiasi hicho!, yashushe hadhi..
> Mandoto ya ajabu ajabu shetani alikuwa anakutumia, anza kuyapotezea wala usiyatafakari tafakari, wala usitafute kujua maana zake, yaache yapite…yakanyage chini!.. usiyakuze, kwenye kichwa chako kana kwamba ni kitu cha muhimu sana.
> Mawazo shetani anayokuletea kwamba mapepo yatakudhuru, hayo mawaza anza kuacha kuyawaza, yakanyage chini, badala yake huo muda tumia kutafakari mambo mengine, tumia kutafakari Maneno ya Mungu, hapo utakuwa unammaliza nguvu shetani kwa kasi sana..Maana shetani kazi yake ni kukutisha wewe ili uanze kumfikiria yeye na kumkuza kwenye akili yako, ndipo apate nguvu juu yako..sasa wewe nenda kinyume naye.
>Shetani alikuwa amekuaminisha kwamba ni lazima kila siku aje akutese, yakatae hayo mawazo, wala usiyatafakari, tena yasahau kabisa kwenye kichwa chako, na wala usipate ratiba ya kufikiri jinsi anavyokutesaga..kwa jinsi unavyozidi kumpotezea, naye anapotea..
Kwasababu Miguu yetu ni silaha kubwa na ina nguvu kuliko vichwa vya nyoka, ina nguvu kuliko mikia ya nge, na ina nguvu kuliko nguvu za adui shetani.
Likumbuke hili neno..Luka 10: 18 “Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni KAMA UMEME. 19 Tazama, NIMEWAPA AMRI YA KUKANYAGA NYOKA NA NGE, NA NGUVU ZOTE ZA YULE ADUI, wala hakuna kitu kitakachowadhuru”
Bwana akubariki.
Kama hujaokoka kumbuka hizi ni siku za mwisho na Yesu anakaribia kurudi, biblia inasema itatufaidia nini tukiupata ulimwengu mzima na kupata hasara za nafsi zetu?..Tafakari neno hilo kwa makini, hivyo kama utaamua leo kumpa Kristo Maisha yako, utakuwa umefanya jambo la busara sana, ambalo hutakaa ujutia katika maisha yako, hivyo kwa msaada Zaidi na maombezi fungua hapa >> SALA YA TOBA.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618.
Jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Shalom, leo tutajifunza madhara ambayo tunaweza kuyapata pale tunapoukataa ule upendo wa mwisho kabisa wa Yesu Kristo.
Yuda alikuwa ni mtume wa Yesu, lakini kama tunavyojua habari yake, alikuwa mwizi, na pia hakuwa na upendo wa dhati kwa Bwana.. Tunaona katika biblia hali hiyo ya uasi aliendelea nayo kwa muda mrefu sana, lakini katika kipindi hicho chote haikuleta madhara yoyote katika maisha yake, aliendelea kutembea na Yesu, aliendelea kushiriki baraka zote za Yesu kama mmojawapo wa mitume wengine..
Mpaka anafikia hatua ya kwenda kupatana na wakuu wa makuhani ili kumsaliti Yesu bado, nafasi alikuwa nayo ya kuahirisha mawazo yake, uwezo huo alikuwa nao, isitoshe alikuwa anaona Yesu akimpa viashiria vingi kuwa anavyovifanya anaweza kuviahirisha, lakini hilo halikumwingia moyoni mwake. Mpaka siku ile walipokuwa wameketi chakulani jioni na Yesu akaanza kuwatawadha miguu, kuonyesha upendo wake kwao, akamtawadha na Yuda miguu yake, huku Yuda akiyatazama macho ya Emanueli yenye upole, yasiyo na kosa lolote, akisikia kabisa rohoni anashuhudiwa kuwa anachojaribu kukifanya sicho sawa..aghahiri mawazo yake, haoni mpaka Bwana wake amekuja kumuosha miguu yake, kumthibitishia kuwa miguu yake haitakiwi kuwa myepesi kukimbilia maovu.. Lakini hilo halikuwa kitu kwa Yuda.
Mpaka dakika ya mwisho kabisa tuona Kristo anaonyesha Upendo wake wa mwisho, wa kuchukua chakula chake cha heshima na kumgawia Yuda peke yake, kama heshima ya kipekee, tusome;
Yohana 13:21 “Naye alipokwisha kusema hayo, Yesu alifadhaika rohoni, akashuhudia akisema, Amin, amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti.
22 Wanafunzi wakatazamana, huku wakiona shaka ni nani amtajaye.
23 Na palikuwapo mmoja wa wanafunzi wake, ameegama kifuani pa Yesu, ambaye Yesu alimpenda.
24 Basi Simoni Petro akampungia mkono, akamwambia, Uliza, ni nani amtajaye?
25 Basi yeye, hali akimwelekea Yesu kifua chake, akamwambia, Bwana, ni nani?
26 Basi Yesu akajibu, Ndiye mtu yule nitakayemtowelea tonge na kumpa. Akatowelea tonge, akalitwaa akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskariote.
27 NA BAADA YA HILO TONGE SHETANI ALIMWINGIA. Basi Yesu akamwambia, Uyatendayo yatende upesi.
28 Wala hakuna mtu katika wale walioketi chakulani aliyeijua sababu ya kumwambia hivyo.
29 Kwa maana wengine walidhania, kwa kuwa Yuda huchukua mfuko, ya kwamba Yesu alimwambia kama, Nunua mnavyovihitaji kwa sikukuu; au kwamba awape maskini kitu.
30 Basi huyo, akiisha kulipokea lile tonge, akatoka mara hiyo. Nako kulikuwa ni usiku”.
Sasa Tonge sio ule mkate wa Pasaka, au sio ule mkate aliowapa wanafunzi wake kama mwili wake waule siku ile, hapana, Tonge ni chakula cha heshima kilichokuwa kinaandaliwa na wayahudi zamani, ambacho kinaweza kikawa na mkate au kitu kingine, lakini sana sana kilitumika mkate, ambacho hicho mtu alikuwa anampa Yule mtu anayemuheshimu sana, au wa muhimu kwake, ili kuinyesha thamani yake. Hivyo aliyeuandaa aliuchua mkate huo na kuuchovya katika mboga iliyoandaliwa pamoja na huyo mtu aliyemwandalia.
Utaliona Hilo katika kipindi cha Ruthu, alivyoitwa na Boazi kwake..
Ruthu 2:14 “Tena wakati wa chakula huyo Boazi akamwambia, Karibu kwetu, ule katika mkate wetu, na ulichovye tonge lako katika siki yetu. Basi akaketi pamoja na wavunaji, nao wakampitishia bisi, naye akala akashiba, hata akasaza”.
Soma pia Ayubu 31:16, na Mithali 23:6, utaliona neno hilo.
Sasa alichokifanya Bwana ndicho hichi, kumpa Yuda heshima ya kipekee, wa kuchovya donge lake pamoja naye,. Kuonyesha upendo wake wa kipekee kwake.
Lakini mara baada ya kula tu, angali moyo wake bado hujaiacha nia ya kumsaliti biblia inatuambia shetani akamwingia saa hiyo hiyo …Akawa amefikia “point of no return”. Hii Ikiwa na maana kuwa sasa shetani anayo nafasi ya kumchukua huyu mtu asilimia 100, anaweza kumwendesha kwa jinsi anavyotaka, (amepata hati miliki maalumu) na ndio hapo utaona akawaendea wale makuhani na kuwapa mikakati yote ya kumkamata Yesu. Na Mwisho wa siku yeye mwenyewe akajiua, kwasababu tayari alikuwa ameshavaliwa na pepo mkuu mwenyewe ibilisi.
Na sisi vivyo hivyo, Kristo anapotuonyesha upendo wake kwetu, na hatuoni jambo lolote baya likitokea kwenye maisha yetu pale tunapofanya dhambi kwa makusudi, pengine unazini na upo kanisani, na huoni jambo lolote baya likikutokea, na saa nyingine unamwomba Yesu akutendee jambo Fulani na anakutendea, na wewe unadhani itaendelea hivyo hivyo kila siku..
Upo wakati atakuonyesha upendo mkubwa zaidi ya huo, (atakumegea Tonge lake) na kama usipojua nini maana ya Upendo huo kwamba anakutaka wewe utubu, wewe ukadhani anafurahishwa na unachokifanya, na ndio maana kukubariki, ujue tayari mwisho wako umefika. Ibilisi anakuingia na hapo ndipo unapokuwa mwisho wako.
Hivyo tusipumbazwe na rehema za Kristo. Tukiona hatuadhibiwi kwa makosa yetu, tuogope kwasababu utafika wakati tutakabidhiwa shetani moja kwa moja.
Bwana akubariki.
Hizi ni nyakati za mwisho Je! Umeokoka? Je! Umepokea Roho Mtakatifu. Kumbuka Yesu ndio mwokozi wa ulimwengu. NA HUO NDIO UKWELI PEKEE ULIODUMU DUNIANI KWA WAKATI WOTE.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618.
Jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Bwana Yesu aliposema pesa za bindoni alimaanisha pesa za mfukoni.. mfuko unaozungumziwa ni ule wa kuvaa kiunononi ambayo ndio ilitumika zamani. tazama picha.
Marko 6:7 “Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu;
8 akawakataza wasichukue kitu cha njiani isipokuwa fimbo tu; wala mkate, wala mkoba, wala pesa za bindoni”;
Ni kwanini Bwana Yesu alisema hivyo?
Ieleweke kuwa Bwana Yesu hakumaanisha kuwa injili haihitaji fedha, wala mahitaji hapana, injili inahitaji fedha, tena sana ili isonge mbele.…Lakini hapo alikuwa halengi kazi ya injili bali aliwalenga wale wapeleka injili. Kwamba hao ndio wanapaswa wasifikiri kuwa inahitajika maandalizi mengi au makubwa ili wao wamtumikie Mungu.
Bwana aliwatuma wao kama wao, na mambo mengine yote aliwapa huko mbele ya safari. Na ndio maana sehemu nyingine aliwauliza hapo nilipowatuma hamna kitu Je! Mlipungukiwa na chochote? Wakasema hapana.
Luka 22:35 “Akawauliza, Je! Hapo nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? Wakasema, La!
Hiyo ni kuonyesha kuwa mahitaji ya muhimu aliwapatia. Huko walipoenda. Hata na sisi, tunapaswa tujue kuwa tunapotaka kumtumikia Mungu tusifikirie sana hali zetu, labda tutaanzia wapi,au tuna nini, au hatuna nini, hilo wazi tuliondoe, Ni kweli wazo hilo ni gumu kulipokea lakini ndio maagizo ya Bwana.. tunapaswa tuyaamini, na kwamba yeye mwenyewe atatupatia.
Shalom.
Jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Kwanini wale dubu waliowauwa vijana wa Elisha walikuwa wa kike?
Fitina ni nini?
Katika biblia Fitina maana yake ni “kufanya mageuzi au mapinduzi”. Mtu ambaye anataka kufanya mapinduzi labda ya kimamlaka, kutokana na kwamba labda hakubaliani na serikali yake, au mamlaka yake, na hivyo akakusanya watu kadhaa na kutafuta kuiangusha serikali, kwa lugha ya kibiblia mtu huyo anafanya fitina.
Katika biblia (Agano la kale) tunaona mifano ya watu kadhaa waliofanya fitina katika biblia..
Huyu Shalumu, alimng’oa Mfalme Zekaria kwenye kiti chake kwa hila, na yeye akatawala mahali pake
2Wafalme 15: 10 “Na Shalumu mwana wa Yabeshi akafanya fitina juu yake, akampiga mbele ya watu, akamwua, akatawala mahali pake……
15 Basi mambo yote ya Shalumu yaliyosalia, na fitina aliyoifanya, tazama, yameandikwa katika kitabu-chatarehe cha wafalme wa Israeli.”.
Huyu naye alimng’oa madarakani mfalme Peka wa Israeli kwa kumuua na kutawala mahali pake.
2Wafalme 15:30 “Na Hoshea mwana wa Ela akafanya fitina juu ya Peka mwana wa Remalia, akampiga, akamwua, akatawala mahali pake, katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia.”
Na wengine wengi ambao unaweza kuwasoma katika mistari hii..(2Wafalme 17:4, 2Wafalme 21:23, 2Nyakati 13:6)
Katika agano jipya pia tunaona mifano ya baadhi ya watu waliofanya fitina.
Huyu Baraba, alipanga kunyanyuka kinyume na mamlaka iliyokuwa inatawala, akataka kufanya mapinduzi…Na pia aliua watu kadhaa katika harakati zake hizo za mapinduzi..
Luka 23: 18 “Wakapiga kelele wote pamoja, wakisema, Mwondoe huyu, utufungulie Baraba.
19 Naye ni mtu aliyetupwa gerezani kwa ajili ya FITINA iliyotokea mjini, na kwa uuaji”
Na katika kanisa la Kristo pia kuna fitina za shetani.
Fitina ndani ya kanisa la Kristo ipoje?..Ni pale mtu anapotaka KULIPINDUA NENO LA MUNGU, na kulisimamisha lake.
Warumi 16:17 “Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale WAFANYAO FITINA na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao.
18 Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu”.
Asilimia kubwa ya watu WANAOLIPINDUA NENO LA MUNGU, na kulisimamisha lao, ni ili tu wapate faida Fulani, labda fedha, ndio biblia inasema hapo, watu wa namna hiyo hawamtumikii Kristo bali matumbo yao. Hawa wanaweza kuupindua Uponyaji wa Yesu uliopo katika JINA LAKE, na kulazimisha uwe katika Maji, au mafuta..lengo lao wala si kwasababu wana huruma sana, lengo lao ni ili wauze hayo maji na mafuta mengi wapate pesa, ndio maana yanawekwa kwa kiwango kidogo lakini bei kubwa.
Tumeonywa tujihadhari nao.. tusichukuliwe na fitina zao.
Hali kadhalika wapo wahubiri wanaomfitini Kristo, na kutafuta kuchukua nafasi yake, ili waabudiwe au waonekane ni miungu-watu, hawa nao pia tumeonywa tujiepushe nao.
Je umeokoka?. Kama bado unasubiri nini tubu leo na kumpokea Kristo, unyakuo upo karibu
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu katika uchambuzi wa vitabu vya biblia, tumekwisha jifunza vitabu kadhaa vya mwanzo, kama utakuwa hujavipitia na ungependa kufanya hivyo, basi unaweza kufungua hapa>> VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
Na leo tutazidi kusonga mbele, kwa kutazama kitabu kimoja Zaidi ambacho ni kitabu cha Ayubu.
KITABU CHA AYUBU.
Kitabu cha Ayubu ndio kitabu kikongwe kuliko vitabu vyote vya biblia, Kitabu hichi kiliandikwa kabla ya kuandikwa kitabu cha Mwanzo. Kitabu cha Mwanzo kiliandikwa na Nabii Musa, kadhalika na kitabu hichi cha Ayubu, ni nabii Musa huyo huyo ndiye aliyekiandika.
Nabii Musa alikiandika kwanza kitabu hichi kisha ndio vikafuata vitabu vingine vingine vya torati kama kitabu cha Mwanzo, kutoka n.k.. Sasa sio kwamba Musa alikuwepo wakati Ayubu anaishi duniani na akawa ananakili Maisha aliyokuwa anayapitia hapana!.. Ayubu aliishi miaka mingi sana kabla ya Nabii Musa kutokea, na mambo yote Ayubu aliyoyapitia yalinakiliwa na Ayubu mwenyewe Pamoja na watu waliomzunguka Ayubu (maana yake marafiki zake na ndugu zake). Hivyo hata baada ya kufa Ayubu, historia ya Maisha yake iliendelea kuwepo, lakini haikuwepo katika mpangilio bora, Sasa Musa alipokuja kutokea miaka mingi baadaye, kwa uongozo wa kiMungu alikusanya Pamoja taarifa zote za Ayubu kwa usahihi na kuziweka kwenye mfumo wa kitabu, ndio kikatokea hicho kitabu cha Ayubu tunachokisoma leo katika biblia.
Kitabu cha Ayubu kinaanza na Historia ya Ayubu mwenyewe mahali alipozaliwa na uelekevu wake kwa Mungu. Ayubu alizaliwa katika nchi ya “Usi”. Nchi ya Usi kwasasa ni maeneo ya kusini mwa nchi ya YORDANI. (kufahamu nchi ya Yordani ilipo, unaweza kutazama ramani).
Ayubu aliishi kabla ya Ibrahimu, hivyo hakuwa Mwisraeli. Lakini alimjua Mungu wa kweli wa mbingu na nchi na alimcha yeye, kutoka kwa mababu zake (akina Nuhu)
Kitabu cha Ayubu kimegawanyika katika Sehemu kuu 4.
Tukianza na sehemu ya kwanza:
Sehemu hii ni ile milango miwili ya mwanzo, na ndio milango iliyo mirahisi kuieleweka kuliko milango mingine yote inayofuata. Hapa inaelezea Ayubu jinsi alivyokuwa Mkamilifu na mwelekevu mbele za Mungu, kwamba alikuwa ni mcha Mungu na ni mtu aliyejiepusha sana na uovu.
Lakini pia katika Sura hizi mbili za Mwanzo ndizo Sura pekee katika biblia nzima zilizotupa, taswira kamili ya kinachoendelea katika katika mamlaka yaliyopo juu yetu sisi wanadamu. Sura hizi ndizo zimetufumbua macho na kuelewa kuwa kumbe wakati sisi tunaendelea na Maisha yetu, kuna mmoja anatushitaki mbele za Mungu, na ndiye sababu ya majaribu yetu yote tunayoyapitia. Ni ukurasa mmoja tu katika biblia lakini umekuwa muhimu sana kwetu. Inaeleza jinsi sababu ya mwenye haki wakati mwingine kupitia majaribu. Sasa ili kujua kwa urefu ni kwa namna gani mashitaka hayo yanaendelea juu mbinguni dhidi yetu, unaweza kufungua hapa na kusoma upatapo nafasi >>> JINSI SHETANI ANAVYOZUIA MAJIBU YA MAOMBI YETU. Kwasasa hatutaingia sana huko.
Sehemu ya Pili:
Sehemu hii ni kuanzia ule mlango wa 3 hadi wa 38, Sehemu hii ni imeelezea majibizano kati ya Ayubu na Rafiki zake watatu, walioitwa ELIFAZI, BILDADI, na SOFARI.
Marafiki hawa walikuwa ni marafiki wa Ayubu wa kitambo kirefu, na walikuwa wamejaa hekima ya ki-Mungu ndani yao. Na waliposikia Rafiki yao kapatwa na majanga yale, na misiba ile walitoka huko walipokuwepo kuja kumliwaza na kumshauri.
Rafiki zake hawa walikuja na Mashauri yao, lakini hawakujua kuwa Mashauri yao hayakuwa yaliyonyooka mbele za Mungu. Wenyewe katika akili zao waliamini asilimia mia moja kwamba Ayubu kuna mahali atakuwa alimkosea Mungu ndio maana akapatwa na majanga yale, walitumia mitazamo yao tu, hawakujua kuhusu vita vilivyokuwa vinaendelea mbinguni. Hivyo walikuja kwa nia moja tu, KUMWAMBIA AYUBU ATUBU!!, Atubie dhambi zake zote alizozifanya kwa siri, zilizompelekea apate majanga yote yale. Kwasababu walimwambia hakuna mtu anayeweza kukutwa na majanga yale, kama hajamkosea Mungu.
Na Ayubu alipowaambia kwamba hajafanya chochote kilicho kibaya cha siri, bado hawakumwamini Ayubu..waliendelea kumwambia kwamba amemkosea Mungu. Hivyo ikawa mlolongo mrefu wa mashauriano, kila mmoja akitumia hekima yake kutoa Mashauri yake dhidi ya Ayubu. Ayubu naye akitumia hekima zake kuwajibu kuwa hajafanya kosa lolote..mazungumzo yakawa marefu mno, mwishoni wakachoka kumshauri Ayubu, kwasababu alionekana anajihesabia haki machoni pake mwenyewe. Akatokea kijana mmoja aliyeitwa Elihu, naye pia akajaribu kutoa Mashauri yake kwa Ayubu na Rafiki zake watatu.
Na katika mazungumzo yao wote wanne (yaani Ayubu na Rafiki zake watatu, yalikuwa yamfikia Mungu juu pasipo wao kujua, na Mungu alikuwa anawasikiliza. Sasa kwa urefu pia kuhusu huduma za hawa Rafiki zake Ayubu, Na kufahamu jinsi, shetani anavyoweza kuwatumia watu wanaoitwa watumishi wa Mungu kuwamaliza watumishi wengine wakamilifu, fungua hapa kwa ajili ya somo hilo kwa urefu >> HUDUMA YA ELIFAZI, BILDADI NA SOFARI,
Sehemu ya Tatu:
Baada ya mazungumzo yao yote, Mungu anamjibu Ayubu kwa upepo wa kisulisuli, maana yake kwa Tufani, jambo ambalo Ayubu hakuwahi kuliona hapo kabla, na anaanza kwa kumuuliza.
Ayubu 38:1 “Ndipo Bwana akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,
2 Ni nani huyu atiaye mashauri giza Kwa maneno yasiyo na maarifa?”
Maana yake ni “Ni nani huyo anayehoji kazi zangu kwa maneno ya upumbavu”…Swali hilo Mungu alimwuliza Ayubu, akimlenga Ayubu na marafiki zake watatu.. Kutokana na maneno waliyokuwa wanazungumza, juu ya Mungu alichomfanyia Ayubu.
Na ukiendelea kusoma mpaka huo Mlango wa 41, utaona Bwana anaendelea kumuuliza maswali Ayubu, kuhusu utukufu wake, ambayo maswali hayo hayana majibu mpaka sasa..(Ili Ayubu ajue kuwa hakuna mtu yeyote anayeweza kuzihoji kazi zake wala kuzipatia majibu)…Mfano wa swali moja Mungu alilomuuliza Ayubu ni ili..
Ayubu 38:4 “Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu.
5 Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua? Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake?”
Hili swali hakuna mtu anaweza kutoa jibu lake. Na maswali mengine mengi aliyoulizwa unaweza kuyasoma mpaka mlango ule wa 41.
Sehemu ya Nne:
Na baada ya Mungu kumuuliza Ayubu hayo maswali. Ayubu alikosa majibu, na akajinyenyekeza akatubu, naye akajiona alikosea sana katika kunyanyua mdomo wake kuzihoji hoji kazi za Mungu, Pamoja na marafiki zake, ijapokuwa hakuzihoji kwa ubaya, lakini kitendo cha kushindana tu, tayari alitambua lilikuwa ni kosa. Hivyo akatubu mbele za Mungu kwa kuvaa nguo za magunia, na kufunga mdomo wake. Utasoma habari hiyo katika ule mlango wa 42.
Ayubu 42:1 “Ndipo Ayubu akamjibu Bwana, na kusema.
2 Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika.
3 Ni nani huyu afichaye mashauri bila maarifa? KWA MAANA, NIMESEMA MANENO NISIYOYAFAHAMU, MAMBO YA AJABU YA KUNISHINDA MIMI, NISIYOYAJUA.
4 Sikiliza, nakusihi, nami nitanena; Nitakuuliza neno, nawe niambie.
5 Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio; Bali sasa jicho langu linakuona.
6 Kwa sababu hiyo NAJICHUKIA NAFSI YANGU, NA KUTUBU KATIKA MAVUMBI NA MAJIVU”.
Na baada ya Ayubu kujinyenyekeza na kujua kosa lake, Bwana aliwageukia wale Rafiki zake watatu, Elifazi, Bildadi na Sofari, ambao ndio waliomfanya Ayubu, azungumze maneno mengi, na zaidi ya yote, maneno yao ndio yaliyozihoji vibaya kazi za Mungu kuliko hata Ayubu. Hivyo Mungu akawakasirikia na kutaka kuwaadhibu.
Ayubu 42:7 “Basi ikawa, baada ya Bwana kumwambia Ayubu maneno hayo, Bwana akamwambia huyo Elifazi Mtemani, Hasira zangu zinawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili; kwa kuwa ninyi hamkunena yaliyo sawa katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu.
8 Basi sasa, jitwalieni ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba, mkamwendee mtumishi wangu Ayubu, mjisongezee sadaka ya kuteketezwa; na huyo mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi; kwa kuwa nitamridhia yeye, nisiwatende sawasawa na upumbavu wenu; kwani ninyi hamkunena maneno yaliyonyoka katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu.
9 Basi Elifazi, Mtemani, na Bildadi, Mshuhi, na Sofari, Mnaamathi, wakaenda, wakafanya kama vile Bwana alivyowaamuru; naye Bwana akamridhia Ayubu”.
Na mwisho, katika kitabu hichi tunaona, tunaona Mungu akimuhurumia Ayubu na kumbariki tena na kumpa mara dufu ya vile alivyokuwa navyo.
Kuonyesha jinsi mwisho wa Mungu ulivyo mwema.
Kwa hitimisho katika kitabu hichi tunajifunza mambo yafuatayo:
1 . Kumcha Bwana na kuepukana na uovu kama Ayubu:
2. Uvumilivu wakati wa majaribu: (Yakobo 5: 11 Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.)
3. Kuishi Maisha ya usafi: kwasababu mshitaki wetu ibilisi, anapeleka mashitaka kuhusu sisi kila siku. Kama alimshitaki Ayubu kwa uzuri wake, unadhani tukiwa wabaya atakuwa anapeleka nini mbele za Mungu kama si kutuchongea tuangamizwe.
4. Kutokuwa na mashindano ya dini (hata kama unajua kitu, sio busara kulumbana na mtu asiyetaka kuamini unachokiamini) Ayubu alijua yupo sahihi, na marafiki zake hawapo sahihi, lakini kitendo cha kujibizana vile, ikawa tayari ni jambo lisilompendeza Mungu. Hivyo na sisi hatupaswi kuwa hivyo (Tito 3:9, 2Timotheo 2:14).
5. Mwenye haki kupitia mateso, haimaanishi Mungu hayupo naye; Tofauti na mitazamo ya watu wengi leo hii, wakishaonekana tu mtu aliyeokoka, anapitia hali Fulani mbaya labda ni hali ngumu ya kifedha, au ni magonjwa, basi moja kwa moja wanahitimisha kuwa Mungu amemwacha, au Mungu hayupo pamoja naye.
6. Kuwaombea Rafiki zetu na maadui zetu. (Hapo tunaona japokuwa Ayubu aliudhiwa na kukoseshwa na marafiki zake hao, lakini mwishoni aliwaombea rehema kwa Mungu, na wala hakuwalaani, na kwa kufanya vile {yaani baada ya kuwaombea tu}ndio ikafungua mlango wa baraka zake za mwisho).
Ayubu 42:10 “Kisha Bwana akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; Bwana naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza”.
Hivyo na sisi tukitaka kufungua milango ya baraka hatuna budi kuwapenda adui zetu, na kuwaombea wale wanaotuudhi sawasawa na maneno ya Bwana wetu Yesu aliyotuasa katika..
Luka 6:27 “Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi,
28 wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi”
Je umeokoka? Kama bado unasubiri nini ndugu?..Kristo anarudi, je akirudi leo kulichukua kanisa utakuwa wapi?..hayo Maisha ya uasherati, ulevi na anasa yanakusaidia nini sasa? Zaidi ya kukuharibu tu?.
Kama leo utaamua kuokoka utakuwa umefanya uamuzi bora ambao hautaujutia, ni vizuri ukafanya hivyo sasa, na wala usingoje kesho…kwamaana hujui yatakayozaliwa ndani ya siku moja.. Hivyo kama upo tayari kutubu leo na kumpokea Kristo fungua hapa kwa msaada Zaidi >>> SALA YA TOBA.
Usikose mwendelezo wa vitabu vinavyofuata.
Bwana akubariki.
Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Kijicho ni nini kibiblia?
Kijicho ni kitendo kilichoaminika na jamii nyingi za zamani, kwamba mtu anaweza kukusababishia madhara au kukuletea laana, kwa kukutazama tu kwa macho yake, na hiyo inaweza ikawa amekusudia au hajakusudia kufanya hivyo. Na hiyo huwa inasababishwa na wivu.
Imani hii hata sasa ipo kwa watu wengi, wanaamini kuwa jicho la mtu linaweza kukuloga, au kukuletea mikosi, gundu, magonjwa. N.k. Hivyo wanatumia vitu kama hirizi, na matambiko kujilinda na madhara ya watu hao.
Lakini Je katika Marko 7:22 Yesu alimaanisha hicho?
Tusome;
Marko 7:21 “Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,
22 wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, KIJICHO, matukano, kiburi, upumbavu.
23 Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi”.
Ni wazi kuwa Yesu hakumaanisha kijicho hicho kinachoaminiwa na wengi, hapana, bali hapa alimaanisha, JICHO OVU, jicho la uchoyo, jicho la wivu, na husuda.
Kuna mahali alisema..
Mathayo 20:15 “Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema”?
Maneno hayo aliyasema alipokuwa anatoa ule mfano wa Yule mtu aliyewaajiri wafanyakazi wake shambani, na mwisho wa siku akawalipa wote sawa, bila kujali huyu alifanya sana, na huyu kidogo,.Vivyo hivyo na sisi macho yetu yanaweza yakawa maovu kwasababu ya mtu mwingine kuwepwa upendeleo kama wetu, pengine mfanyakazi mpya amekuja na analipwa mshahara sawa au zaidi ya sisi tuliokuwepo kwa muda wa miaka 20 hapo kazini. Sasa kule kuona wivu, kutaka apewe kidogo kuliko wewe, hicho ndicho kijicho chenyewe ambacho Kristo anachokizungumzia kwamba kinamtia mtu unajisi.
Sehemu nyingine kwenye biblia inasema;
Kumbukumbu 15:9 “Jitunze, msiwe na neno lisilofaa moyoni mwako, kusema, Umekaribia mwaka wa saba, mwaka wa maachilio; JICHO LAKO LIKAWA OVU juu ya nduguyo usimpe kitu; naye akamlilia Bwana juu yako, ikawa ni dhambi kwako”.
Unaona, aina nyingine ya kijicho ndio hiyo, kumdhulumu mtu haki yake kwa lengo la kumfanya aendelee kukutumikia, au pengine kwa wivu tu ili asifaidike akaweza kujitegemea. Hivyo wewe unadhamiria kumdhulumu haki yake ya utumishi kwako. Inaweza ikawa ni housegirl wako au houseboy wako au mlinzi wako, unapomnyima maslahi yake, hicho ni kijicho ambacho kitakutia unajisi na kukufanya usikubaliwe na Mungu.
Na ndio maana Bwana Yesu alisema;
Mathayo 6:22 “Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru”.
Tunapaswa tuliondoe “jicho ovu” ndani yetu, Na hiyo inatokana na jambo moja tu, nalo ni kuushinda wivu. Wivu ukiondoka ndani ya mtu hataona uchungu kwa mwenzake kufanikiwa, hataona sababu ya kumdhulumu mfanyakazi wake, hataona sababu ya kumuundia visa jirani yake. Na matokeo yake Kijicho hufa ndani yake. Bwana atusaidie tuyatendee kazi na hayo. Ili nafsi zetu zisinajisike.
Shalom.
Tazama tafsiri za maneno mengine ya biblia chini.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Kuna pepo moja lililowasumbua sana mitume wa Yesu, hilo halikuwa sawa na pepo mengine waliyokutana nayo, walihangaika nalo mchana kutwa lakini hawakufua dafu mpaka alipokuja Bwana Yesu mwenyewe kulikemea na kulitoa.
Lakini leo hatutazungumzia juu ya pepo hilo kwasababu habari yenyewe tunaijua, ila katika habari hiyo lipo jambo ambalo ni vizuri sisi tukajifunza, husasani kwa wazazi au walezi, wanaoishi na watoto wadogo. embu tusome tena alichokifanya Yesu kisha, tuende kwenye ujumbe wenyewe..
Marko 9:20 “Wakamleta kwake; hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye akaanguka chini, akagaa-gaa, akitokwa na povu.
21 Akamwuliza babaye, AMEPATWA NA HAYA TANGU LINI? Akasema, TANGU UTOTO.
22 Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia”.
Sasa katika habari hiyo, usidhani Yesu alikuwa hajui matatizo ya huyo mtoto ndio maana akamwuliza vile, Kumbuka Yesu alikuwa anajua kila kitu wala alikuwa hana haja ya mtu kumuadhithia chochote, biblia inatuambia hivyo katika Yohana 16:30, Lakini aliuliza vile kwa lengo la kutaka watu wote wajue matatizo ya Yule mtoto yalianzia wapi, na ndio maana akamuuliza vile yule mzazi “Amepatwa na haya tangu lini?”.
Ndipo yule mzee akamjibu na kusema, “amepatwa na haya tangu utotoni”. Ulishawahi kuutafakari vizuri huu mstari, tangu utotoni? ..Hiyo ni kutuonyesha kuwa kuna mapepo ambayo, agenda yao kuu, ni watoto. Kwasababu yanajua yakianzia katika msingi, baadaye yatakuwa ni magumu kutoka.
Inashangaza leo hii kuona wazazi hawajali maisha ya kiroho ya watoto wao, wanaona kama wao ni watoto tu, shetani hawezi kuwashambulia, hawajui kuwa wanapaswa kulindwa kwasababu shetani huwa hatambui cha mtoto au cha mzee, lengo lake ni kuharibu. Kama alimuingia Nyoka ambaye ni mnyama tu, ataachaje kumwingine mtoto ambaye ni mwanadamu? ndio target yake kubwa?
Mzazi, anamruhusu mtoto wako mdogo atezame tv masaa 24 wakati wote hata zile programu ambazo haziendani na umri wake anamwacha azitazame, anamwacha asikilize miziki ya kidunia, tena Zaidi ya yote unafurahi anapocheza, lakini nyimbo za tenzi hata moja haujui, Mzazi mwingine hata hampeleki mtoto wake Sunday school ili afundishwe njia ya kikristo angali akiwa mdogo, yeye anachojua ni kumnunulia mtoto wake nguo nzuri tu, kumtafutia nursery nzuri ya kusoma, anajali vya mwilini vya mwanawe anapuuzia na vile vya rohoni. Hata kumwombea mtoto wake anashindwa.
Nachotaka nikuambie ni kuwa tusipowawekea msingi mzuri watoto wetu, shetani atatusaidia kuwawekea wake, kama alivyofanya kwa mtoto wa huyu mzee tunayesoma habari zake. Lile pepo lina haki ya kuwa gumu kutoka kwasababu tayari lilikuwa na msingi tangu utotoni. Na ukiangalia lengo la hilo pepo si lingine zaidi ya kumwangamiza tu, mara litake kumtupa kwenye maji, kwa bahati nzuri pengine watu wanamuona wanamuokoa, mara litake kumtupa kwenye moto, lakini Mungu anafungua rehema zake anaepukika.
Leo hii utaona kumenyanyuka kundi kubwa la watoto ambao wanaonyesha tabia ambazo hazieleweki chanzo chake ni nini, na wewe unaweza ukadhani ni yeye anafanya kumbe ni pepo ambalo tayari lilishamvaa tangu utotoni ndio linaonyesha tabia hizo ndani yake.
Wazazi ndio wanapaswa waanze kubadilika, ndio watoto wabadilike. Wewe kama mzazi, kama hutaonyesha kujali maisha ya kiroho ya mtoto wako, usidhani mtoto atabadilika mwenyewe au atakuwa na tabia njema huko mbeleni.
Mithali 22:6 “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee”
SASA UTAYAZUIAJE MAPEPO YA UHARIBIFU KAMA HAYO YASIMWINGIE MWANAO?
Kwanza ni kwa kutumia kiboko: Biblia inasema hivyo, …Pale unapoona kuna tabia Fulani ambayo sio nzuri, mfano kiburi, anatukana, hana nidhamu, hapo hapo hupaswi kuiacha hiyo tabia imee, mpaka hilo pepo liumbike ndani yake.. Utalitoa hilo kwa kiboko.
Mithali 23:13 “Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
14 Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu”.
Pili Ni kwa kumfundisha kanuni za imani: Unamfundisha biblia, unamfundisha nyimbo za kikristo, unamfundisha kusali, unamfundisha hata kukariri vifungu vya biblia, hata kama hataelewa sasahivi lakini vitabaki moyoni mwake kama hazina itakayokuja kumsaidia baadaye. Na hakikisha pia unampelekea kwenye mafundisho ya watoto kanisani.
Tatu Unamwombea; Mara kwa mara unahakikisha unamfunika mwanao, kwa damu ya Yesu Kristo, unatenga muda mrefu wa kumuombea.
Na Nne unamzuia kufanya/kutazama mambo ambayo hayapasi: Si lazima kila unachokitazama wewe, mtoto naye akitazame, magemu anayoyacheza mtoto si yote yanamaudhui mazuri, vilevile nguo unazomvisha mtoto si zote ni njema. Hivyo jifunze kumchagulia mtoto vinavyomfaa.
Ukizingatia hayo, basi mapepo kama hayo ambayo ni hatari na sugu, hayatamkuta mwanao. Kumbuka biblia inasema shetani ni kama simba angurumaye, akitafuta mtu ammeze, hivyo usipuuzie haya maagizo, mjenge mwanao, mjenge mdogo wako, mjenge mtoto yoyote auishiye naye.
Na Bwana atakubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618.
Jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
Jina la Bwana wetu Yesu, libarikiwe. Karibu tujifunze biblia.
Katika biblia Mungu hakuwabadilisha watu majina kutokana na tafsiri za hayo majina. Ni muhimu kufahamu sana hili, vinginevyo shetani anaweza kukutesa na tafsiri ya jina lako. Kwasababu usipomwelewa Mungu jinsi anavyotenda kazi, utachukuliwa na kila aina ya upepo wa elimu, na mafundisho ya mashetani, ambayo kazi ya hizo elimu ni kuwafunga watu wala sio kuwafungua, Kuwatwisha watu mizigo mizito na wala si kuwatua.
Yohana 8:36 “Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli”
Sasa hebu tuangalie watu wachache waliobadilishwa majina katika biblia, na tafsiri za majina yao kabla na baada ya kubadilishwa, ndipo tutajua tabia ya Mungu.
Huyu mara ya kwanza alikuwa anaitwa “Abramu”. Tafsiri ya jina Abramu ni “Baba aliyeinuliwa” na Ibrahimu tafsiri yake ni “Baba wa mataifa mengi”.
Sasa kulingana na tafsiri hizo, sio kwamba Mungu aliona tafsiri ya jina lake la kwanza ilikuwa ni mbaya, na hivyo akataka kumpa jina jipya lenye tafsiri zuri, hapana!..ilikuwa ni nzuri tu… kuitwa “Baba aliyeinuliwa” sio jina baya, lakini ilipofika wakati wa Mungu kumpa agano kwamba atakuwa Baba wa mataifa mengi, ndipo jina lake likabadilishwa na kuwa Ibrahimu. (Hivyo lilibadilishwa kwasababu ya huduma iliyopo mbele yake).
Huyu alikuwa ni mke wa Ibrahimu, ambaye hapo kwanza alikuwa anaitwa “Sarai” maana yake ni “binti wa mfalme” lakini jina lake lilibadilishwa na kuwa “Sara” ambalo maana yake ni “mama wa wana wa wafalme”. Hivyo halikubadilishwa kwasababu lilikuwa na maana mbaya, bali kwasababu ya Ahadi ya Mungu, ya mumewe Ibrahimu kuwa Baba wa mataifa mengi, hivyo hana budi na yeye kuwa mama wa mataifa na wafalme wengi, Ni sawa wewe ubadilike sasa kutoka kuitwa mtoto, na kuitwa Baba wa watoto wengi…au kutoka kuitwa binti mpaka kuitwa mama wa mabinti wengi..(Ni kutokana na kubadilika majukumu, umetoka kwenye utoto sasa umeingia kuwa mama/baba)
Mtu wa tatu ni Yakobo, mwana wa Isaka, jina lake lilibadilishwa kutoka kuitwa Yakobo hadi kuitwa Israeli.. Tafisiri ya jina “Yakobo” ni “mshika kisigino”..Jina hilo aliitwa kutokana na jinsi alivyozaliwa, kwani alipozaliwa alizaliwa huku kamshika ndugu yake kisigino.(Mwanzo 25:26)..na Tafsiri ya jina Israeli ni “Kushindana na Mungu”. Sasa Yakobo jina hilo halikubadilishwa kutokana na tafsiri yake ni mbaya..Hapana bali ni kutoka na ahadi mpya Mungu aliyokwenda kumpa baada ya kushindana na yule malaika na kumshinda..Kwasababu kama tafisiri ya Jina Yakobo lingekuwa ndio sababu ya Mungu kumbadilisha jina, basi Mtume wa Yesu aliyeitwa Yakobo, angepaswa naye pia abadilishwe jina. Na aliyeandika kitabu cha Yakobo, naye pia angepaswa abadilishwe.. Lakini tunaona hawajabadilishwa, lakini bado waliendelea kuwa Mitume wa Yesu, waaminifu mpaka mwisho.
Petro hapo kwanza alikuwa anaitwa Simoni.. Yohana 1:42 “Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe)”. Sasa tafsiri ya jina Simoni ni “Amesikia”.. Na tafisiri ya Kefa/Pertro ni “jiwe dogo la kurusha” na sio “mwamba”. Hivyo kwa hali ya kawaida, Simoni ndio lenye tafsiri bora kuliko Petro..
Sasa utaona Bwana Yesu hakumbadilisha jina Simoni kwasababu lina maana mbaya, hapana bali ni kwasababu ya huduma yake inayokwenda kuanza, kwamba Bwana atamtumia kama jiwe lake, kwa kazi yake. Sasa jina “Simoni” lingekuwa na tafsiri mbaya inayomchukiza Mungu au yenye madhara kiroho kwa Petro, basi angembadilisha pia mtume wake mwingine miongoni mwa wale 12, ambaye naye pia alikuwa anaitwa Simoni mkananayo (Mathayo 10:4). Kwasababu Bwana asingeweza kumbadilisha mtume mmoja na kumwacha mwingine mwenye jina kama hilo hilo. (Kwahiyo Petro naye alibadilishwa kutokana na huduma iliyopo mbele yake)
Na wa mwisho tunayeweza kumwona ni Mtume Paulo ambaye hapo kwanza alikuwa anaitwa “Sauli” ambapo tafsiri ya jina hilo ni “Ombea” (mf. Kuombea kitu fulani kwa Mungu), hiyo ndiyo tafisiri ya jina Sauli, lakini jina hilo lilikuja kubadilishwa na kuwa “Paulo” ambalo maana yake ni “Mdogo”.
Hivyo unaona hapo, jina lake halikubadilishwa kwasababu lilikuwa na tafsiri mbaya, hata wewe katika hali ya kawaida ungeambiwa uchague uitwe jina lenye tafsiri ya “mdogo” au uitwe jina lenye tafsiri ya “Ombea”..Bila shaka ungechagua lenye tafsiri ya “ombea”. Lakini Mungu alimbadilisha Sauli na kumpa hilo lenye tafisiri ya mdogo.
Na kwanini Mungu alimpa jina hilo Paulo?. Ni kwasababu ya huduma yake, ambayo anakwenda kuifanya hapo mbeleni (ambayo itampasa awe mdogo sana na mnyenyekevu).
Waefeso 3:7 “Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake.
8 MIMI, NILIYE MDOGO KULIKO YEYE ALIYE MDOGO WA WATAKATİFU WOTE, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;
9 na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote”.
Kwahiyo jambo kubwa la kujifunza ni kwamba… tafsiri za majina yetu, hazina maana sana mbele za Mungu wetu. Ndio ni vizuri kuwa na jina lenye tafsiri nzuri, lakini hilo halikusogezi mbele za Mungu. Kwasababu majina yaliyoandikwa kwenye kitabu cha uzima, hayajaandikwa kulingana na maana za majina hayo, bali kulingana na matendo ya mtu.
Watakuwepo wengi mbinguni ambao majina yao hayana tafsiri nzuri, na vile vile watakuwepo wengi kuzimu wenye majina mazuri, watakuwepo wakina Ibrahimu wengi kuzimu, watakuwepo wakina Paulo wengi kuzimu, watakuwepo wakina Petro wengi kuzimu, na watakuwepo wakina Yohana wengi kuzimu. Vile vile watakuwepo wakina Sauli wengi mbinguni, watakuwepo wakina Yakobo wengi mbinguni, watakuwepo wakina matatizo wengi mbinguni, watakuwepo wakina Majuto wengi mbinguni, watakuwepo wakina masumbuko wengi n.k
Kwahiyo baada ya kuokoka, Tafsiri ya jina lako isikusumbue sana. Kama umependa kulibadilisha kwa mapenzi yako mwenyewe (kwamba hupendwi kuitwa hilo jina katikati ya jamii yako)ni sawa hutendi dhambi, na Kama Bwana amekuongoza kubadilisha jina lako pia ni sawa fanya hivyo!!, lakini kama Bwana hajakuongoza wala usiwe na hofu, wala usitishwe na elimu zilizozagaa kwamba utapata mikosi kwa jina hilo, au jina hilo ni kikwazo kwako na mafanikio yako.
Kuwa tu kama Simoni Mkananayo mwanafunzi wa Yesu, ambaye jina lake lilibakia kuwa lile lile, lakini bado aliendelea kuwa mwanafunzi wa Yesu..ijapokuwa mwenzake alibadilishwa na kuwa Petro, yeye aliendelea kuwa vile vile Simoni. Kwasababu Mungu hatembei na wewe kwasababu ya tafsiri bora ya jina lako, bali kwasababu ya uaminifu wako kwake katika kuyafanya mapenzi yake. Kama vile asivyobagua rangi, vivyo hivyo habagui watu kutokana na tafsiri za majina yao.
Katika Biblia kuna mtu anaitwa Tabitha au Dorkasi, tafisiri ya jina hilo ni “Paa” kasome Matendo 9:36, sasa “paa” kwa lugha inayoeleweka ni “mnyama Swala”..Lakini pamoja na jina lake hilo lenye tafisiri isiyo na maana, tunasoma Tabitha alimpendeza Mungu sana..
Matendo 9:36 “ Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa”.
Kadhalika katika biblia kuna mtu aliyeitwa Yabesi (1Nyakati 4:9-10), huyu alipewa jina lenye tafsiri mbaya ya HUZUNI, lakini alimpendeza Mungu sana.(Kwa habari zake ndefu unaweza kututumia ujumbe inbox). Na ipo mifano mingine mingi kwenye biblia ambayo hatuwezi kuitaja hapa yote. Lakini kwa hiyo michache itoshe tu kusema kwamba, Kama ulikuwa na hofu na tafsiri ya jina lako, badilisha mtazamo sasa..Anza kuwa na hofu na mwenendo wa maisha yako katika hatima ya maisha yako, zaidi ya tafisir ya jina lako.
Ufunuo 20:12 “Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, SAWASAWA NA MATENDO YAO”.
Hivyo utazame mwenendo wako, je umesimama katika Imani sawasawa?..Je matendo yako yanampendeza Mungu?..kama bado basi rekebisha leo kabla hujafikia mwisho wa siku zako za kuishi hapa duniani.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
JINA LAKE KWA KIEBRANIA NI ABADONI, NA KWA KIYUNANI NI APOLIONI.