Haiwezekani kuwafanya tena upya hata wakatubu

Haiwezekani kuwafanya tena upya hata wakatubu

Nini maana ya huu mstari.“Haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu” (Waebrania 6:6)

Tusome,

Waebrania 6:4 “Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,

5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo,

6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri”.

Kipengele cha muhimu cha kuzingatia hapo ni hicho.. “Hata wakatubu”.

Maana ya andiko hilo kwa lugha rahisi ni kwamba “watu waliopewa Nuru (Maana yake walioipokea Neema ya Wokovu) na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, kama ikitokea wakaiacha Imani, kwa makusudi, na kurudia tena mambo machafu ya ulimwengu haitawezekana kuwafanya tena WATUBU”.

Sio kwamba wataomba msamaha na Mungu hatawasamehe, hapana!…bali haitawezekana tena kuwa na huo moyo wa kutubu!..Kwasababu nguvu ya kutubu inaletwa na Roho Mtakatifu, hakuna mtu yeyote amewahi kutubu na kumgeuka kwa nguvu zake.

Yohana 6:44 “Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho”.

Na pia maandiko yanazidi kusema..

Yohana 15:16 “Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda…”

Maana yake ni kwamba, tunatubu kwasababu ni Mungu katuwekea moyo wa toba, lakini kama tumemfedhehesha Roho Mtakatifu anayetupa moyo wa toba, na akaondoka kwetu?..Je! Tutafanyaje ili tutubu?..tutabaki tu kuendelea na maisha ya dhambi.

Hiyo ni tahadhari kwetu tuliomwamini Bwana Yesu na kusimama katika Imani, na kuvionja vipawa vya Roho, na kuona kwamba Bwana ni mwema ni lazima tuchukue tahadhari, tuangalie tusiurudie ulimwengu na kuishi tena maisha ya dhambi kama zamani.

1 Wakorintho 10:12 “Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke”.

Mtume Petro ameliweka tena hilo vizuri kwa kusema.

2 Petro 2:20 “Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.

21 Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa

22 Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.”.

Pengine wewe unayesoma ujumbe huu ulikuwa umeshaanza kurudi nyuma, ingawa ulishavionja vipawa vya Mungu, Na sasa umesikia huu ujumbe na umekuogopesha na kukushtua.

Hiyo hofu iliyoingia ndani yako ni kuonesha kuwa bado Neema haijaondoka juu yako, lakini ipo mbioni kuondoka kwako kama hautageuza njia zako (Hiyo ni kulingana na maandiko).

Siku itakapoondoka hutashtushwa tena na habari kama hizi, wala hutamwona tena Yesu ni wa maana katika maisha yako, utaishia kuwa mtu wa kudhihaki na kutokujali, Toba itakuwa mbali sana nawe.

Lakini sasa bado neema ipo nawe, ndio maana sasa hivi una hofu usikiapo habari za kiMungu.

Sasa Nini cha kufanya?

Ule ulevi ambao tayari ulikuwa umeuacha usiurudie tena, ule uzinzi, uasherati, uuaji, wizi n.k ambao ulikuwa umeshauacha, usiufanye tena, kwasababu kuna hatari kubwa kuyarudia mambo tuliyokuwa tumeyaacha.

Bwana atubariki.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Ni kwa namna gani Bwana amekuja kuwafanya wanaoona wawe vipofu?

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3

ULIMWENGU WA ROHO UPO NA UNA MADHARA KATIKA MAISHA YETU! 

ULIMWENGU WA ROHO UPO NA UNA MADHARA KATIKA MAISHA YETU! 

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Magdalena
Magdalena
2 years ago

Mbarikiwe Watumishi wa Bwana