Swali: Kuna tofauti gani ya “kutakabari” na “kutakabali”, sawasawa Warumi 1:30 na Mwanzo 4:4-5?
Jibu: Tuanze na 1) kutakabari..
Warumi 1:30 “wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao”.
“Kutakabari” maana yake ni “kuwa na kiburi” kinachokuja kutokana na kuwa na kitu Fulani, au kujiamini sana..
Matokeo ya kutakabari ni kuanguka..
Mithali 16:18 “Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko. 19 Afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu pamoja na maskini, Kuliko kugawanya nyara pamoja na wenye kiburi”.
Mithali 16:18 “Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.
19 Afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu pamoja na maskini, Kuliko kugawanya nyara pamoja na wenye kiburi”.
Mfano wa mtu kwenye biblia aliyetakabari na akaanguka ni Mfalme wa Ashuru aliyeitwa Senakeribu.. Huyu alijiinua mbele za Mungu kwa kiburi kikuu na anguko lake likawa kubwa. (Soma 2Wafalme 19:28-37).
Unaweza kujifunza Zaidi juu ya kutakabari kwa kufungua hapa >>Kutakabari ni nini katika biblia?.
Mistari mingine inayozungumzia juu ya kutakabari ni pamoja na 1Samweli 2:3, Nehemia 9:10, Isaya 13:3, na 1Wakorintho 13:4.
2. KUTAKABALI.
“KUTAKABALI” ni tofauti na “kutakabari”…. Kutakabali ni “kukubali kitu”.. Utaona sadaka ya Habili Mungu aliitakabali (maana yake aliikubali na kuiheshimu zaidi ya ile ya Kaini).
Mwanzo 4:4 “Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana AKAMTAKABALI Habili na sadaka yake; 5 bali Kaini HAKUMTAKABALI, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana”
Mwanzo 4:4 “Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana AKAMTAKABALI Habili na sadaka yake;
5 bali Kaini HAKUMTAKABALI, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana”
Na sisi tunapomtolea Mungu sawasawa na Neno lake, Sadaka zetu atazitakabali, lakini tukitoa nje na neno lake hatazitakabali kama vile sadaka ya Kaini alivyoikataa..
Yeremia 14:12 “Wafungapo, mimi sitasikia kilio chao; na watoapo sadaka za kuteketezwa na sadaka ya unga, sitazitakabali; bali nitawaangamiza kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni”
Vile vile tukimwomba Mungu sawasawa Neno lake basi Maombi yetu atayatakabali na kutujibu, lakini tusipoomba kulingana na Neno basi hata maombi yetu hayatajibiwa..
Zaburi 6:9 “Bwana ameisikia dua yangu; Bwana atayatakabali maombi yangu”.
Kujua kuomba kulingana na Neno la Mungu fungua hapa >>>>KWANINI MUNGU HAJIBU MAOMBI?
Mistari mingine inayohusu KUTAKABALI ni pamoja na Zaburi 20:3, Mhubiri 5:20, Ezekieli 20:41, Hosea 14:2 na Malaki 2:13.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
DHAMBI ILIYOMKOSESHA SHETANI:
Kiburi cha Uzima ni nini? (1Yohana 2:16)
UDHAIFU WA SADAKA!
Mtu wa kwanza kufa alikuwa nani?
MUNGU HUWAPINGA WENYE KIBURI.
Rudi nyumbani
Print this post