Jina tukufu la Bwana YESU KRISTO libarikiwe.
Je umewahi kutafakari kwanini mapigo yote tisa (9) aliyopigwa Farao bado moyo wake ulikuwa mgumu? Na kwanini lile pigo moja la mwisho la kufa wazaliwa wa kwanza ndipo akawaruhusu wana wa Israeli?.
Sasa hakuna mahali popote maandiko yanasema kuwa “Mungu aliufanya moyo wa Farao kuwa mlaini”.
Maana yake Farao aliendelea kuwa na moyo mgumu mpaka alipoingia kwenye ile bahari ya Shamu, na hapo ndio ikawa mwisho wake.
Sasa ni nini kilitokea mpaka Farao akawaachia wana wa Israeli?… Si kingine bali ni ule msiba alioupata,
Na huku bado moyo wake ukiendelea kuwa mgumu, alivunja sheria ya moyo wake na kuwafukuza wana wa Israeli kwa muda. (Lakini moyo wake bado ulikuwa mgumu tu).
Kutoka 11:1 “BWANA akamwambia Musa, Liko pigo moja bado, nitakaloleta juu ya Farao na juu ya Misri; baadaye atawapa ninyi ruhusa mtoke huku; naye hapo atakapowapa ruhusa, atawafukuza mtoke huku kabisa kabisa”
Sasa ni siri gani iliyokuwepo ndani ya wazaliwa wa kwanza wa Misri hata kumfanya Farao awafukuze wana wa Israeli?…Kwani ni wazi kuwa hata Farao angepigwa kwa mapigo gani ya asili asingewaachia wana wa Israeli.
Ila ni nini kilikuwa kwa wazaliwa wa kwanza wa kiMisri?
Kilichokuwa ndani ya wazaliwa wa kwanza wa Misri, ikiwemo mwana wa Farao si kingine zaidi ya “miungu ya kimisri”..
Hivyo kifo cha wazaliwa wa kwanza ilikuwa ni hukumu kubwa kwa miungu yao pamoja kudhalilika kwa miungu yao ambao waliamini ina nguvu nyingi.
Ndio maana MUNGU aliposhuka kuwaharibu wazaliwa wa kwanza pia alisema ataiharibu na miungu yao (ambayo kiuhalisia ilikuwa inaishi ndani ya hao wazaliwa wa kwanza).
Kutoka 12:12 “Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, namij nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA.”
Zamani katika nchi ya Misri na hata katika mataifa mengine ya dunia, wazaliwa wa kwanza wa kiume waliaminika kama miungu ya familia na ya nchi.
Na wanyama wa kwanza kuzaliwa, ndio waliotumika kwa kafara za miungu yao.
Hivyo watoto wote wa kwanza wa kiume walikuwa wanabeba ukuhani wa miungu, na roho zote za miungu zilikuwa zinakaa ndani yao.
Kwahiyo kilichomwumiza zaidi Farao si msiba wa mtoto, bali ni kuhukumiwa kwa miungu yao iliyokuwepo ndani ya wale watoto!!..
Kwaufupi Farao alichanganyikiwa kidogo, hakuelewa ni nini kimetokea katika eneo lake la imani.
Na hata waMisri wote walichanganyikiwa vivyo hivyo, hakuna ambaye hakulia..wote walilia na kuhofu na kutoelewa ni nini cha kufanya, waliyeyuka mpaka kufikia hatua ya wana wa Israeli kuwateka nyara.
Kutoka 12:33 “Wamisri nao wakawahimiza watu, kuwatoa katika nchi kwa haraka, maana walisema, Tumekwisha kufa sote.
34 Watu wakauchukua unga wa mikate yao kabla haijatiwa chachu, na vyombo vyao vya kukandia wakavitia ndani ya nguo zao mabegani.
35 Wana wa Israeli wakafanya kama neno lile la Musa; wakataka kwa Wamisri vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu, na mavazi.
36 BWANA akawajalia kupendelewa na Wamisri hata wakawapa kila walichokitaka. Nao wakawateka Wamisri nyara”
Ni ujumbe gani tunapata hapo?..au ni kitu gani kilichokuwa kimewafunga wana wa Israeli?
Si utajiri wala hazina zilizoko Misri kwamaana Bwana aliuharibu utajiri wake wote kwa zile mvua za mawe na nzige, vile vile si uzuri wa Misri, kwasababu Bwana aliharibu uzuri wake kwa zile mvua za mawe lakini bado wana wa Israeli walikuwa kifungoni.
Wala si ushujaa wa waMisri kwasababu Bwana aliwapiga kwa chawa, na majipu na aliwanyima maji ya kunywa kwa siku saba, hivyo walikuwa dhaifu..lakini bado wana wa Israeli walikuwa kifungoni.
Ni nini kilichokuwa kimewashikilia wana wa Israeli???…..jibu ni “miungu ya kimisri” iliyokuwa inaabudiwa ndani ya watu.
Hiyo ilipopigwa pamoja na makuhani wake (ambao ndio wazaliwa wa kwanza)..vifungo vikalegea, wana wa Israeli wakaachiwa.
Laiti Bwana Mungu angelileta hilo pigo mwanzoni kabla ya yote, Farao angeshaawaachia Israeli kitambo sana pamoja na moyo wake kuwa mgumu, lakini Mungu aliliruhusu liwe mwisho wa kusudi lake maalumu.
Na ukiendelea kusoma mbele utaona Bwana anawapa amri wana wa Israeli wawatakase wazaliwa wa kwanza na kwamba kila mzaliwa wa kwanza atakuwa ni wa Bwana, maana yake atakuwa kuhani wa Bwana kwa lazima (kwasababu kulikuwa na kitu katika wazaliwa wa kwanza).
Maana yake kila mzaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli alipaswa kutolewa kwa Bwana kama Hana alivyomtoa Samweli kwa Bwana (hiyo ilikuwa ni amri).
Lakini sheria hiyo ilikuja kubadilika, na ukuhani wa wazaliwa wa kwanza likapewa kabila la Lawi.
Hesabu 3:12 “Mimi, tazama, nimewatwaa Walawi na kuwatoa kati ya wana wa Israeli badala ya wazaliwa wa kwanza wote wafunguao tumbo katika wana wa Israeli; na hao Walawi watakuwa wangu;
13 kwa kuwa hao wazaliwa wa kwanza wote ni wangu; katika siku ile niliyowapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri nikajiwekea wakfu wazaliwa wa kwanza wote wa Israeli, wa wanadamu na wa wanyama; watakuwa wangu; mimi ndimi BWANA”.
Hivyo wazaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli wanaozaliwa ilikuwa ni sharti wakombolewe kwa sadaka ili watokane na kiapo hiko cha Bwana cha kuwa makuhani.
Na maana ya kukombolewa si kutolewa katika vifungo vya laana, kama mafundisho ya siku hizi za mwisho yanavyofundisha.
Bali ukombozi ilikiwa ni ile hali ya mtoto kutolewa katika nafasi ya kikuhani ambayo angepaswa kuitumikia maisha yake yote.
Hivyo anapokombolewa anakuwa huru kama watu wengine wasio na utumishi wa kikuhani (kwa ufupi anafunguliwa kutoka katika vifungo vya ukuhani)
Na mtoto wa kwanza asipokombolewa anabaki katika kifungo cha dhambi ya nafasi ya kikuhani.
Sasa swali je hata sasa katika agano jipya tunasheria hizo za kukomboa mzaliwa wa kwanza?.
Jibu ni la!..katika agano jipya hatuna sheria za kumkomboa mzaliwa wa kwanza au wa mwisho, kwasababu sote tuliomwamini Bwana YESU na kutakaswa kwa damu yake tunafanyika kuwa makuhani wa Bwana.
Ufunuo wa Yohana 1:6 “na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina”.
Hivyo sote tunayo huduma ya kikuhani na mbele za Mungu, na ukishakuwa tu kuhani tayari ni mzaliwa wa kwanza pasipo kujali rika…Hivyo kanisa la Kristo ni wazaliwa wa kwanza.
Waebrania 12:23 “mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika”.
Kwahiyo hakuna sadaka yoyote ya ukombozi kwa wazaliwa wa kwanza kwa jinsi ya mwili.
Mafundisho na maombi ya kukombolewa kwa wazaliwa wa kwanza si ya kiMungu, bali ni ya ibilisi.
Ndio tunaweza kuwaombea wazaliwa wetu wa kwanza na kuwaweka wakfu kwa Bwana, dhidi ya roho zinazofuatilia, lakini si kuwakomboa….uwakomboe na nini?…je uwakomboe uwatoe katika ukuhani?…maana ndio lengo la ukombozi hilo kibiblia lililokuwepo juu ya wana wa Israeli juu ya wazaliwa wa kwanza.
Zaidi sana watoto wetu wa kwanza wanapaswa wawe wazaliwa wa kwanza kiroho kwa kumwamini YESU na kutakaswa ndipo wanapofanyika makuhani kama wengine wote waliomwamini YESU.
Mwisho, fahamu kuwa kilichowafuga wana wa Israeli ni miungu ya misri, iliyokuwa inaabimudiwa ndani ya kila kiumbe kilichokuwa cha kwanza.
Hali kadhalika vile vitu vinavyojiinua katika maisha yetu vilivyo vya kwanza ndivyo ni lazima tuwe navyo makini kwani hivyo ibilisi anaweza kuvitumia kama mlango wa kutufunga.
Je cha kwanza kwako ni nini?…je ni kazi uliyonayo?…au ni cheo ulicho nacho?..au ni uzuri au ni Bwana YESU?..
Ni heri BWANA YESU akawa wa kwanza kwako, kwani yeye ndiye njia, kweli na Uzima.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Waliouawa Shitimu kwa pigo walikuwa ni watu Elfu 23 au elfu 24?.
SWALI: Je! tunalisoma wapi kwenye maandiko panasema ndoa inapaswa ifungwe kanisani. Utaratibu huo upoje?
JIBU: Ili kujibu swali hili tuanzie mbali kidogo.
kufahamu ndoa ni nini? aina za ndoa, kisha mahali sahihi pa kufungia ndoa ni wapi?.
Ndoa ni muunganiko kati ya watu wawili(mwanaume na mwanamke ) unaotambulika na kuheshika kijamii, au kisheria.
Pale mwanaume anapomwona mwanamke na kupatana naye waishi pamoja kama mume na mke, kwa kufuata taratibu husika za kijamii, labda kukutanishwa kwanza wazazi, au walezi, wazee wa ukoo, kupokea mahari, kisha kuidhinisha jambo hilo, au serikali kuidhinisha, hiyo tayari inaitwa ndoa.
Aina mbili za ndoa.
Ndoa za wapagani. Hizi ni ndoa lakini hazijadhibitiwa na kanuni timilifu za Mungu. Mfano wa hizi, ndio hizo kama za kijamii, na kiserikali, au za dini nyingine zote mfano wa ki-hindu, kiislamu, ki-budha n.k. zote hizi ni ndoa za wapagani.
Zingatia: (Hapa hatumaanishi zile za mashetani, kama za jinsia moja, au za wanadamu na wanyama hapana kwasababu hizo sio ndoa, bali tunazungumzia hizi za kawaida kabisa za asili).
Kiuhalisia mtu anaweza akawa katika mojawapo ya ndoa hizi, na asihesabike kuwa ni mkosaji kwasababu ndoa hasa ni jambo la kiutamaduni, ambalo huusisha wanadamu wote, bila kuchagua dini, rangi, au kabila.
Hivyo si sawa kudhani kuwa kwasababu watu fulani hawajafungishwa ndoa kikristo(kanisani) basi, zote hizo sio ndoa kwamba ni sawa tu hata kwenda kuoa tena hapo, au kuivuruga, wasiishi pamoja. Ukifanya hivyo Mungu atakuwajibisha kwa kuzivuruga ndoa za watu wengine.
Aina ya pili ya ndoa ni ndoa ya kikristo.
Hii ni ndoa inayofungwa katika kanuni timilifu za Mungu alizozikusudia tangu mwanzo.
Kanuni zenyewe ni hizi
i) Wote wawe waamini.
(1Wakorintho 7:39, 1Wakorintho 9:5, 2Wakorintho 6:14 – 16)
Kuamini si lazima muwe katika viwango sawa kiroho, lakini wote muwe upande mmoja wa Kristo, (Kwasababu hayo mengine yanaweza rekebika). Lakini mmoja ni mganga wa kienyeji, mwingine mkristo,.au mmoja ni muislamu mwingine mkristo. Hilo si sawa ni sharti wote wawe wakristo. Kwasababu hakuna ushirika wowote kati ya nuru na giza.
Kwasababu Ndoa ya kikristo ni lazima iwe katika jina la Bwana, vinginevyo, itaangukia katika lile kundi lingine.
ii) Mume mmoja, mke mmoja.
Tofauti na ndoa za wapagani. Ambazo kwao unaweza kuwa na mke zaidi ya mmoja, lakini mtu anayetaka ndoa yake itimilike mbele za Kristo, basi mume/mke atambue kuwa hana ruhusa ya kuongoza mwenza mwingine.
Mathayo 19:4-5
[4]Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
[5]akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? a
iii) Malazi yawe safi:
Waebrania 13:4
[4]Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.
Malazi kuwa safi maana yake ni nidhamu ya kiasi, katika kukutana kimwili. Mkristo hapaswi kuwa mtu wa hulka ambaye wakati wote anawaza zinaa, mpaka anakosa muda wa kujishughulisha na mambo ya rohoni.
1 Wakorintho 7:5
[5]Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.
Vilevile viitendo kama kuingiliana kinyume na maumbile haviruhusiwi ndani ya ndoa (1Wakorintho 6:9).
iv) Hakuna talaka.
Tofauti na ndoa za wapagani, mtu anaweza kuacha/kuachwa kwa sababu yoyote, labda mfano wamechokana, au wameudhiana, lakini katika ukristo hilo jambo halipo mtaendelea kuishi pamoja mpaka kifo kitakapowatenganisha.
Bwana alitoa ruhusa hiyo katika eneo la uasherati tu lakini ukumbuke, alisema pia ‘samehe mara saba sabini’. Hivyo kwa kauli hiyo hakuna popote tunaona wigo wa wanandoa kuachana kwa sababu yoyote ile.(1Wakorintho 7:39-40)
V) Mume ni sharti ampende mkewe.
Mume kumpenda mkewe ni amri ya kindoa, anawajibu wa kumtunza na kumuhudumia na kujitoa kwa ajili yake, kama Kristo alivyolipenda kanisa.(Waefeso 5:25-31)
Vi) Mke ni sharti amtii mumewe.
Ni amri mke amtii mumewe kwa agizo atakaloambiwa/ elekezwa. Tofauti na ndoa za wapagani ambazo hili linaweza lisiwe la muhimu. Kwenye ukristo, ni lazima utii wa mwanamke uonekane kwa mumewe.
Waefeso 5:22
[22]Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.
Sasa vigezo hivi wakivikidhi hawa wakristo ambao wameokoka na wanatarajia kuishi kama mke na mume. Basi hiyo huitwa ndoa ya Kikristo iliyokidhi vigezo vitimilifu vya Mungu,.haijalishi imefungwa kanisani au kwenye familia, .
Swali ni je? kwanini watu wafungie kanisani? Na Je ni takwa?
Mkristo ambaye anathamini ukamilifu wote wa ki-Mungu, katika maeneo yake yote ya kiroho na kimwili, kufungia ndoa yake kanisani itakuwa ndio chaguo lake bora. Kwanini iwe hivyo?
Hizi ndio faida za ndoa kufungiwa kanisani
Biblia inatueleza mashtaka yetu, hayapaswi kutatuliwa na watu wa ulimwengu, bali ndani ya kanisa. Kwasababu kanisa ni zaidi ya mahakama yoyote, ambayo Mungu ameiheshimu mpaka akaamua malaika zake wahukumiwe katika hiyo.
Hivyo endapo kuna migogoro, au kutoelewana, au kupatiwa misaada, au mashauri, au maonyo, au maongozi, basi kanisa, limewekwa na Mungu kwa ajili yako kukusaidia katika hayo yote.
Lakini ikiwa hukuifungia ndoa yako kanisani. Fahamu kuna mambo kama hayo yatakupita, au yatakuwa magumu kwetu kutatulika.
1 Wakorintho 6:1-3
[1]Je! Mtu wa kwenu akiwa ana daawa juu ya mwenzake athubutu kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya watakatifu?
[2]Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo?
[3]Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?
2) Ushuhuda mwema.
Mungu anapenda mambo mema atufanyiayo tumtukuze mbele ya kusanyiko la watakatifu. Tunajua Ndoa ni kitu chema, hivyo tunapoweka wazi mbele za Bwana, na mbele ya kanisa lake, yeye hutukuzwa lakini pia tunapokea baraka za kanisa, Ikiwa tunapoumwa na kuponywa hatuoni sawa kukaa na shuhuda zetu ndani, tunakwenda kushuhudia mbele ya kanisa, si zaidi ndoa zetu?, ni ushuhuda mkubwa, ambao utawafariji wengine, lakini pia utaihubiri injili ya Kristo.
Zaburi 35:18
[18]Nitakushukuru katika kusanyiko kubwa;
Nitakusifu kati ya watu wengi.
Hivyo, kwa maelezo hayo tunaweza kusema hakuna sababu ya Mkristo yoyote kuifungia ndoa yake, mbali na kanisa.
Lakini hiyo haimaanishi kuwa usipofungia kanisani, ndoa yake haitambuliwi na Mungu. Maadamu umekidhi vigezo “mama”, tulivyoviorodhesha juu. Hiyo ni ndoa.
Bwana akubariki
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Rudi Nyumbani
Swali: Je Bwana YESU alikuwa amemfunga shetani wakati wa kuzaliwa kwake Kulingana na Mathayo 12:29?
Jibu: Turejee.
Mathayo 12:29 “Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, ASIPOMFUNGA KWANZA yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake”.
Jibu ni kwamba shetani hakuwa amefungwa wakati wa kuzaliwa Bwana YESU, na hata sasa shetani hajafungwa!, kwani Ingekuwa shetani amefungwa wakati wa kuzaliwa Bwana, basi Herode asingetafuta kumwua mtoto..
Mathayo 2:13 “Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize”.
Tukio hilo linaeleweka vizuri katika Ufunuo 12:1-6.
Vile vile Ibilisi asingesimama kumjaribu Bwana kule jangwani..
Mathayo 4:1 “Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ILI AJARIBIWE NA IBILISI.
2 Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.
3 Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate”
Na ikiwa shetani amefungwa leo, maasi yasingeendelea kuwepo na maandiko yasingetuonya kuwa tusimpe nafasi..
Waefeso 4:28 “wala msimpe Ibilisi nafasi.
28 Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji”.
Maandiko yametabiri shetani kuja kufungwa katika ule utawala wa miaka elfu wa Bwana wetu YESU hapa duniani. Na utawala huo utaanza baada ya dhiki kuu kuisha, na hukumu ya Mungu kwa mataifa kupita (Ufunuo 16), hapo ndipo utawala wa miaka elfu moja utakapoanza na shetani (pamoja na majeshi yake) kufungwa kwa kipindi hiko.
Ufunuo 20:1 “Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake.
2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu;
3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache”.
Kwahiyo shetani kwasasa yupo na hakuwahi kufungwa wakati wowote huko nyuma, lakini atakuja kufungwa baada ya hukumu ya Mungu kwa mataifa inayotajwa katika Ufunuo 16.
Sasa swali kama ni hivyo je! Maandiko hayo katika Mathayo 12:29 yana maana gani?….
Turejee tena..
Mathayo 12:29 “Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, ASIPOMFUNGA KWANZA yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake”.
Haya ni maneno ambayo Bwana YESU aliyasema, akifundisha nguvu iliyo kuu/kubwa inapoingia mahali basi inateka au inafunga ile nguvu iliyo dhaifu.
Na ukisoma kuanzia juu kidogo utaona ni wakati ambapo Mafarisayo walimwona akitoa pepo kwa uweza wa Mungu, lakini wakasema yeye hatoi kwa uweza wa Mungu bali kwa uwezo wa Pepo mkuu aitwaye Beelzebuli, ambaye ni shetani mwenyewe.
Na Bwana akawahoji, akiwauliza yawezekanaje Shetani amtoe shetani mwenzake?..jambo ambalo haliwezekani!, vinginevyo ufalme wa giza hauwezi kusimama, lakini kama wakiona pepo katolewa maana yake katolewa kwa uweza wa Mungu, kwasababu kamwe shetani hawezi kumtoa shetani mwenzake.
Na ili kulifanya hilo lizidi kueleweka vizuri ndipo akatoa mfano mwingine kwamba… “Awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, ASIPOMFUNGA KWANZA yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake”
Ikifunua kuwa Bwana anapotoa pepo, kwanza anauteka ule ufalme wa giza (maana yake wote unakuwa chini ya amri yake) halafu ndipo anaamrisha pepo zitoke na kwenda atakako yeye soma Mathayo 8:28-32.
Sasa kitendo cha Bwana YESU kusimama na kuamrisha, maana yake mamlaka yake ni KUU inayoteka, na kufunga, na kuhamisha.. Na mamlaka hiyo hajabaki kwake tu pake yake, bali pia amewapa na wale wote wanaomwamini na kufanya mapenzi yake, kwamba kwa jina lake wanateka, na wanafunga na kuhamisha kila falme za giza.
2Wakorintho 10:4 “(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; NA TUKITEKA NYARA KILA FIKIRA IPATE KUMTII KRISTO;
6 tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia”.
Kwahiyo mantiki ya Bwana YESU hapo ya KUFUNGA, haikuwa ya kumfunga shetani asiwepo duniani, bali katika kuzifunga kazi za ibilisi na majeshi yake zisisimame mbele yetu. (lakini shetani yupo, na ataendelea kuwepo na kuwasumbua wale wote wasiomwamini na kumfuata Bwana YESU), lakini walio na Bwana shetani hana nguvu juu yao.
Mathayo 18:18 “Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni”.
Je umeokoka??..Hizi ni siku za hatari na BWANA anarudi. Na shetani anajua wakati wake uliobaki ni mchache sana, hivyo anafanya kazi kwa kasi sana kusudi asiende kwenye lile ziwa la moto peke yake.
Ufunuo 12:12 “Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu”
Je bado wewe ni rafiki wa dunia?, bado ni mshabiki wa mipira, bado unacheza Kamari, bado unavaa kidunia na kuupenda ulimwengu?
1Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Je YUDA alikuwa ni shetani kulingana na Yohana 6:70?
NIFANYE NINI NIMSHINDE SHETANI?
Je! Yesu aliwezaje kuchukuliwa na shetani juu ya kinara cha hekalu kujaribiwa?
Nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu.
Swali: Kitani ni nini, na Bafta ni nini? Kama tunavyosoma katika Isaya 19:9?
Jibu: Turejee.
Isaya 19:9 “Tena wao wafanyao kazi ya kuchana KITANI watafadhaika, na hao pia wafumao BAFTA”.
1.KITANI
“Kitani” ni aina ya mmea unaostawi kwa sana maeneo ya mashariki ya kati, mbegu za mmea huu hutumika kwa matibabu lakini pia nyuzi zake hutumika kati kutengenezea mavazi mbalimbali ikiwemo mavazi ya harusi.
Ufunuo 19:7 “Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.
8 Naye amepewa kuvikwa KITANI NZURI, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.
9 Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu”.
Lakini si tu mavazi ya harusi bali pia ilitumika katika kutengenezea sanda za maziko.
Yohana 19:40 “Basi wakautwaa mwili wake Yesu, wakaufunga sanda ya KITANI pamoja na yale manukato, kama ilivyo desturi ya Wayahudi katika kuzika”
Mistari mingine inayozungumziwa mavazi ya Kitani ni pamoja na Mithali 31:22, Ezekieli 44:17, Danieli 10:4-5,Marko 14:51 na Ufunuo 18:16.
Vazi la kitani kiroho linafunua “Matendo ya Mtu” ikiwa ni kitani safi bali ni matendo safi, (Sawasawa na Ufunuo 19:8) lakini ikiwa ni kitani iliyoharbika, basi maana yake ni matendo yaliyoharibika.
2. BAFTA.
“Bafta” ni Kiswahili kingine cha “Pamba”.. Zao la pamba mbali ni kutumika katika matibabu, linatumika sana pia katika utengenezaji wa mavazi. Nyuzi za kitani zilitumika kutengeneza mavazi magumu nay ale ya nakshi, lakini pamba hutumika kutengenezea mavazi au mapazia yenye nyuzi laini na zenye kuhifadhi joto.
Ezekieli 9:11 “Na tazama, mtu yule aliyevaa bafta, mwenye kidau cha wino kiunoni, akaleta habari, akisema, Nimefanya kama ulivyoniamuru”.
Mistari mingine inayotaja mavazi na mapazia ya Bafta ni pamoja na Esta 1:6, Ezekieli 9:2 na Ezekieli 10:7.
Je unaye YESU maishani mwako?.. ni vazi gani ulilonalo kiroho?.. je ni kitani nyeupe? Au iliyoharibika? Je unayatunza mavazi yako au umeyaacha yaharibike?.. Kwa maarifa Zaidi ya namna ya kutunza mavazi yako kiroho fungua hapa >>
Bwana akubariki.
+255789001312/ +255693036618
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
kwanini yule kijana aliitupa ile nguo ya kitani chini na kukimbia uchi?
TUNZA MAVAZI YAKO NA FUA NGUO ZAKO!