Wimbo Ulio Bora 5:2-6
[2]Nalikuwa nimelala, lakini moyo wangu u macho, Sikiliza! Mpendwa wangu anabisha!Â
Nifungulie, umbu langu, mpenzi wangu, Hua wangu, mkamilifu wangu,Â
Kwa maana kichwa changu kimelowa umande, Nywele zangu zina manyunyu ya usiku.Â
[3]Nimeivua kanzu yangu; niivaeje? Nimeitawadha miguu; niichafueje?Â
[4]Mpendwa wangu aliutia mkono wake tunduni, Na moyo wangu ukachomeka kwa ajili yake.Â
[5]Nikaondoka nimfungulie mpendwa wangu; Mikono yangu ilidondoza manemane, Na vidole vyangu matone ya manemane, Penye vipini vya komeo.Â
[6]Nalimfungulia mpendwa wangu, Lakini mpendwa wangu amegeuka amepita;Â
(Nimezimia nafsi yangu aliponena),Â
Nikamtafuta, nisimpate, Nikamwita, asiniitikie.Â
Habari hii inaeleza kisa cha mtu na mpenzi wake, ambayo inafunua mahusiano ya mtu na Kristo, na jinsi mwitikio Wake unavyopaswa uwe.
Â
Hapa anaonyesha mwanamke mmoja akiwa ndani usiku amelala peke yake na mara akasikia mpenzi wake anabisha Mlango amfungulie,Â
Lakini alijawa na uzito, akaanza kukawia-kawia, pengine huwenda kwasababu ya starehe ya kitanda, au kuna mambo yake mengine ya siri alikuwa anayafanya
Lakini bado mpenzi wake aliendelea kugonga, bila mfanikio ya kufunguliwa…na safari hii akatoa mpaka maneno ya upendo yamkini yatamshawishi ili aje kufungua kwa haraka. Lakini bado hakufua dafu.
Nifungulie, umbu langu, mpenzi wangu, Hua wangu, mkamilifu wangu,Â
Mpaka dakika ya mwisho, alipogonga, na mbisho ule kuingia moyoni mwa yule mwanamke, ukamchoma ndipo akatoka haraka na kwenda kumfungulia..
Lakini kwa bahati mbaya hakumkuta, kumbe tayari alishaondoka…akaanza kutoka kumtafuta bila mafanikio..na matokeo yake huko nje kukutana na madhara mengine.
Hili ni jambo ambalo watu wengi humfanyia Kristo rohoni sasa…Anasema..anasema..
Ufunuo wa Yohana 3:20
[20]Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.Â
Lakini watu hukawia-kawia kwasababu ya udanganyifu wa mambo Ya duniani, mwingine atasema ngoja kwanza nimalize ujana, ndio nitaokoka, mwingine ngoja nipate kazi mwingine ngoja niolewe, mwingine ngoja ifike mwakani, mwingine ngoja nikimaliza masomo ndio nitampokea Yesu..n.k
Ndugu Saa ya wokovu ni sasa Kristo anakuita, wakati ndio huu, usipoufungua moyo wako sasa, utafika Wakati utamtafuta Kristo na hutampata…
Luka 13:24
[24]Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.Â
Luka 12:36-40
[36]nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.Â
[37]Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.Â
[38]Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao.Â
[39]Lakini fahamuni neno hili, Kwamba mwenye nyumba angalijua saa atakayokuja mwivi, angalikesha, wala asingaliacha nyumba yake kuvunjwa.Â
[40]Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.Â
Okoka leo ndugu, neema ya wokovu ipo sasa lakini haitadumu milele..hiyo sauti inayoita moyoni mwako itii, haraka, starehe za duniani zinapita, maisha yanapita, ikiwa upo tayari kumkabidhi Bwana maisha yako, basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii bure kwa msaada huo..
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Mshulami ni msichana gani?
Yahu ni nani? (Wimbo 8:6).
Kimiami ni nini? (Wimbo ulio bora 2:9).
Â
About the author