Ayala ni mnyama jamii ya swala, ambaye anapatikana sana maeneo ya nchi za barini, wana pembe ndefu zilizotawanyika kama mashina ya miti (Tazama picha juu).
Paa ni jamii ya swala wenye mistari meupe, (Maarufu kama Gazelle kwa lugha ya kiingereza). Paa wanapatikana zaidi maeneo ya ukanda wa joto, kama Afrika. (Tazama picha chini). Na pia kwenye biblia kuna watu waliitwa Paa.
Matendo 9:36 “Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa”.
Na Kulungu pia ni jamii ya swala, ambao nao pia wanapatikana nchi za ukanda wa baridi kama Ulaya. (Tazama picha chini).
Wanyama hawa kwa pamoja tunawasoma wametajwa katika biblia katika kitabu cha Isaya..
1Wafalme 4: 22 “Na vyakula vya Sulemani vya siku moja vilikuwa kori therathini za unga wa mzuri, na kori sitini za ngano. 23 na ng’ombe kumi walionona, na ng’ombe ishirini za malisho, na kondoo mia, pamoja na ayala, na paa, na kulungu, na kuku walionona”.
1Wafalme 4: 22 “Na vyakula vya Sulemani vya siku moja vilikuwa kori therathini za unga wa mzuri, na kori sitini za ngano.
23 na ng’ombe kumi walionona, na ng’ombe ishirini za malisho, na kondoo mia, pamoja na ayala, na paa, na kulungu, na kuku walionona”.
Sasa kwanini biblia iwataje wanyama hawa?
Kwanza ni wanyama ambao kimwonekano ni wazuri, na wepesi, na pia wana-mbio sana, (soma Habakuki 3:19, Isaya 35:6, Zaburi 18:33, 2Samweli 22:34, na 2Samweli 2:18). simba ni rahisi kumkamata punda milia lakini si swala… Sasa katika roho vijana wanafananishwa jamii ya hawa wanyama wa swala. Vijana wana nguvu na pia kimwonekano ni wazuri kuliko wazee, na pia ni wepesi wa kufanya mambo..
Na ndio maana biblia inatoa maonyo haya..
Wimbo 2: 7 “Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe”.
Maana yake usiwe mwepesi kuruka huko na huko kama kulungu kuzichochea tamaa za mwili, waasherati wote biblia imesema hawataurithi uzima wa milele.
2Timotheo 2:22 “Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi”.
Maran atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Hayawani ni nini katika biblia?
Katika biblia Neno “Mshenzi” linatajwa.Kwanini liwekwe?
Wibari ni nani?(Mithali 30:26)
Nyinyoro ni nini?
Ni kwanini mifugo ya Yakobo iliongezeka kwa wingi kiasi kile?
Rudi nyumbani
Print this post
Tusome..
Wimbo 2:1 “Mimi ni ua la uwandani, Ni nyinyoro ya mabondeni. ”
Hapo kuna vitu viwili, 1) Ua la uwandani, na 2) Nyinyoro ya mabondeni.
Sasa kwa urefu juu ya Ua hili la uwandani unaweza kufungua hapa ili tuende pamoja >> Ua la Uwandani
Lakini tutaiangalia sehemu ya pili inayozungumiza Nyinyoro ya mabondeni...
Sasa Nyinyoro ni jamii ya maua ijulikanayo kama “Lil” kwa lugha ya kiingereza.. (Tazama picha juu). Ua la uwandani au kwa lugha nyingine “Ua la Sharon, lenyewe linaota sehemu tambarare”. Lakini jamii ya haya maua ya Nyinyoro (au Lily) yanasitawi sehemu za mabonde na miteremko. Ni maua mazuri sana kwa mwonekano kama hayo ya maua mengine ya Sharon.
Sasa hilo ua ni nani?
Si mwingine zaidi ya Mwokozi wa Ulimwengu, yeye ndiye Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho…Yeye ndiye Ua la Sharon linalostawi sehemu tambarare na ndiye Ua la Nyinyoro linalostawi mabondeni, ndio Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho..
Kama vile maua yavutiavyo na yatoavyo harufu nzuri, ndivyo Yesu alivyo mzuri naye, hakuna aliyemtumainia akajuta, wala kumkinai, amejaa Mema, na raha. Wana raha na heri wote wanaomkimbilia. Je wewe ni mmoja wao?
Kama bado hujampokea basi umekosa kitu cha muhimu sana katika maisha yako, hivyo fanya hima leo, mpokee na utapata raha nafsini mwako..
Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha”.
Maran atha!
Sharoni ni nini au ni wapi kibiblia?(1Nyakati 5:16)
Areopago ni nini? Kwanini mtume Paulo walimpeleka huko?
Bwana Yesu alimaanisha nini kusema “Saa yangu haijawadia?”
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
Jibu: Pambaja ni neno linalo maanisha “upendo” (ule wa mwanaume na mwanamke). Upo upendo wa ndugu kwa ndugu, mfano upendo wa Mzazi na mtoto, dada na kaka wa familia moja na pia upo upendo wa mwanamke na mwanamke. Sasa upendo huu wa mwanaume na mwanamke kwa lugha nyingine ndio unaoitwa PAMBAJA. Neno hili linaweza kutumika kama wingi, lakini linamaanisha vile vile upendo.
Wimbo ulio Bora 1: 2 “Kubusu na anibusu kwa kinywa chake. Maana pambaja zako zapita divai”
Wimbo ulio Bora 4: 10 “Jinsi zilivyo nzuri pambaja zako, umbu langu, Bibi arusi, ni nzuri kupita divai; Na harufu ya marhamu yako Yapita manukato ya kila namna”
Pia unaweza kulipata neno hilo kwenye mistari hii; Wimbo 1:4, Wimbo 7:12.
Sasa ni kwanini upendo huu umetajwa hapo?, je una umuhimu wowote kwetu sisi wakristo?. Ndio una umuhimu mkubwa, kwanza kwa wana-ndoa na Pili kwa Kristo na Kanisa lake.
Kumbuka Sisi wakristo katika roho tunafananisha na bibi-arusi na Kristo ndiye Bwana Arusi. Hivyo jinsi Kristo anavyolipenda kanisa upendo wake ni kama wa mke na mume (yaani Pambaja). Na kama unavyojua wivu ni mbaya kuliko ghadhabu..Na ndivyo Kristo anavyotuonea wivu, tunapoiacha njia ya haki na kuufuata ulimwengu.. Tunamtia wivu.
Wimbo 8: 6 “Nitie kama muhuri moyoni mwako, Kama muhuri juu ya mkono wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu”
Hivyo sisi tuliookoka ni watu wa thamani mbele ya Kristo, ni bibi-arusi wake, anayetupenda na kutujali na katuandalia mambo mengi mazuri mbinguni katika karamu yake aliyotuandalia..
Ufunuo 21: 9 “Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo. 10 Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu”
Ufunuo 21: 9 “Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo.
10 Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu”
Je utaikosa hiyo Yerusalemu mpya iliyoandaliwa mahususi kwa bibi-arusi?. Kama hujampokea Kristo hutaurithi uzima huo wa milele. Hivyo mpokee leo, kwa kutubu na kwenda kubatizwa na yeye atakupokea.
UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?
SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.
JE! UKIMWI UNATIBIKA?
JIKANE NAFSI MTEULE WA MUNGU.
BWANA SI MWEPESI WA HASIRA, LAKINI BWANA NI MWINGI WA HASIRA.
Kwamfano tukisoma katika injili ya Mathayo, tunaona, mwandishi anaanza kueleza ukoo wa Yesu tangu Ibrahimu Mpaka Yusufu, lakini alipofika kwa Daudi, aliendelea na kusema Daudi akamzaa Sulemani, (Mathayo 1:6)..Lakini tukirudi tena kwenye Luka hapo hapo tunaona Daudi alimzaa Nadhani (Luka 3:31), Hiyo ni kuonyesha kuwa Yesu alipitia uzao wa Nathani na sio wa Sulemani, kulingana na Luka. Lakini Mathayo anasema alipitia kwenye uzao wa Sulemani, kwanini iwe hivyo?
Pia ukisoma tena mwishoni utaona kulingana na Injili ya Mathayo, baba yake Yusufu alikuwa ni Yakobo, lakini Luka anatuambia baba yake Yusufu alikuwa ni Eli (Luka 3:23).. Naomba ufafanuzi juu ya hili.
JIBU: Ni wazi kuwa ukisoma kitabu cha Mathayo na kile cha Luka utaona kuna tofauti kubwa kwenye vizazi vya ukoo wa Yesu. Luka anatuambia baba wa Yusufu alikuwa ni Eli, na Mathayo inasema babaye alikuwa ni Yakobo. Lakini je! Hilo linamaanisha biblia inajipinga?
Jibu ni la! Ikumbukwe kuwa zamani katika taifa la Israeli walikuwa na desturi ya mtu kumnyanyulia ndugu yake uzao, na mtoto huyo kuitwa kwa jina la marehemu ikiwa mtu huyo atakufa kabla hajapata mtoto.. Soma. Kumbukumbu 25:5-6,
Kwamfano, kama wewe ni mwanaume umezaliwa katika familia, na ukaoa, lakini kwa bahati mbaya ukafa bila kupata mtoto, basi anatafutwa ndugu yako wa karibu aidha katika familia au katika ukoo, Yule aliye karibu zaidi na wewe, kisha anakwenda kumuoa huyo mke wako uliyemwacha, kisha anamzalia mtoto, lakini huyo mtoto hataitwa kwa jina lake, bali ataitwa kwa jina lako wewe marehemu, haijalishi kuwa watoto huyo watakuwa wametoka katika viungo vya mtu mwingine. Na Wanafanya hivyo ili kulitunza jina lako lisipotee.
Na ndicho walichokifanya Israeli wakati ule, ndicho alichokifanya Boazi kwa Ruthu, (ukisoma Ruthu 4:6-9)
Sasa tukirudi katika Injili. Mathayo aliandika Uzao wa Yusufu (Babaye Yesu), akifuata ubaba wa kibaolojia, na Luka aliandika uzao wa Yusufu akifuata ubaba wa kijina.
Ikiwa na maana kuwa Eli pengine alikufa kabla ya kupata mtoto, hivyo Yakobo akamchukua mke wake, na kuzaa naye ili kumtunzia jina, ndipo akamzaa Yusufu. Hivyo kibaolojia Yusufu alikuwa ni mtoto wa Yakobo lakini kisheria alikuwa ni mtoto wa Eli.
Na ndio maana Yakobo hatajwi katika injili ya Luka, bali ni Eli.. Lakini Mathayo anamtaja Yakobo Kama baba wa Yusufu lakini kibaolojia. Hivyo maandiko yapo sawa.
Kwafaida ya asiyekuwa na biblia anaweza kuvipitia, vifungu hivyo vya biblia hapa chini:
Mathayo 1:1-16 1 Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu. 2 Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake; 3 Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu; 4 Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni; 5 Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese; 6 Yese akamzaa mfalme Daudi. 7 Sulemani akamzaa Rehoboamu; Rehoboamu akamzaa Abiya; Abiya akamzaa Asa; 8 Asa akamzaa Yehoshafati; Yehoshafati akamzaa Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia; 9 Uzia akamzaa Yothamu; Yothamu akamzaa Ahazi; Ahazi akamzaa Hezekia; 10 Hezekia akamzaa Manase; Manase akamzaa Amoni; Amoni akamzaa Yosia; 11 Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli. 12 Na baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli; 13 Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori; 14 Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa Eliudi; 15 Eliudi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa Yakobo; 16 Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.
Mathayo 1:1-16
1 Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.
2 Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake;
3 Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu;
4 Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni;
5 Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese;
6 Yese akamzaa mfalme Daudi.
7 Sulemani akamzaa Rehoboamu; Rehoboamu akamzaa Abiya; Abiya akamzaa Asa;
8 Asa akamzaa Yehoshafati; Yehoshafati akamzaa Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia;
9 Uzia akamzaa Yothamu; Yothamu akamzaa Ahazi; Ahazi akamzaa Hezekia;
10 Hezekia akamzaa Manase; Manase akamzaa Amoni; Amoni akamzaa Yosia;
11 Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli.
12 Na baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli;
13 Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori;
14 Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa Eliudi;
15 Eliudi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa Yakobo;
16 Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.
Na..
Luka 3:23-38 23 Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri wake kama miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli, 24 wa Mathati, wa Lawi, wa Melki, wa Yana, wa Yusufu, 25 wa Matathia, wa Amosi, wa Nahumu, wa Esli, wa Nagai, 26 wa Maathi, wa Matathia, wa Semei, wa Yusufu, wa Yuda, 27 wa Yoana, wa Resa, wa Zerubabeli, wa Shealtieli, wa Neri, 28 wa Melki, wa Adi, wa Kosamu, wa Elmadamu, wa Eri, 29 wa Yoshua, wa Eliezeri, wa Yorimu, wa Mathati, wa Lawi, 30 wa Simeoni, wa Yuda, wa Yusufu, wa Yonamu, wa Eliakimu, 31 wa Melea, wa Mena, wa Matatha, wa Nathani, wa Daudi, 32 wa Yese, wa Obedi, wa Boazi, wa Salmoni, wa Nashoni, 33 wa Aminadabu, wa Aramu, wa Hesroni, wa Peresi, wa Yuda, 34 wa Yakobo, wa Isaka, wa Ibrahimu, wa Tera, wa Nahori, 35 wa Serugi, wa Ragau, wa Pelegi, wa Eberi, wa Sala, 36 wa Kenani, wa Arfaksadi, wa Shemu, wa Nuhu, wa Lameki, 37 wa Methusela, wa Henoko, wa Yaredi, wa Mahalaleli, wa Kenani, 38 wa Enoshi, wa Sethi, wa Adamu, wa Mungu.
Luka 3:23-38
23 Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri wake kama miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli,
24 wa Mathati, wa Lawi, wa Melki, wa Yana, wa Yusufu,
25 wa Matathia, wa Amosi, wa Nahumu, wa Esli, wa Nagai,
26 wa Maathi, wa Matathia, wa Semei, wa Yusufu, wa Yuda,
27 wa Yoana, wa Resa, wa Zerubabeli, wa Shealtieli, wa Neri,
28 wa Melki, wa Adi, wa Kosamu, wa Elmadamu, wa Eri,
29 wa Yoshua, wa Eliezeri, wa Yorimu, wa Mathati, wa Lawi,
30 wa Simeoni, wa Yuda, wa Yusufu, wa Yonamu, wa Eliakimu,
31 wa Melea, wa Mena, wa Matatha, wa Nathani, wa Daudi,
32 wa Yese, wa Obedi, wa Boazi, wa Salmoni, wa Nashoni,
33 wa Aminadabu, wa Aramu, wa Hesroni, wa Peresi, wa Yuda,
34 wa Yakobo, wa Isaka, wa Ibrahimu, wa Tera, wa Nahori,
35 wa Serugi, wa Ragau, wa Pelegi, wa Eberi, wa Sala,
36 wa Kenani, wa Arfaksadi, wa Shemu, wa Nuhu, wa Lameki,
37 wa Methusela, wa Henoko, wa Yaredi, wa Mahalaleli, wa Kenani,
38 wa Enoshi, wa Sethi, wa Adamu, wa Mungu.
Shalom.
MWANZO WA INJILI YA YESU KRISTO.
JE BWANA WETU YESU ALIKUWA NI MZUNGU?
Je! Bwana Yesu alitumwa kwa Waisraeli tu peke yao?
JE! SISI KAMA WAKRISTO NI DHAMBI KUSHEHEREKEA KRISMASI?.
Biblia haijatoa idadi kamili ya malaika Mungu aliowaumba, inatumia neno “MAJESHI” ambayo majeshi yenyewe hayo yapo maelfu kwa maelfu.
Waebrania 12:22 “Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na MAJESHI ya malaika ELFU NYINGI”,
Umeona ni wengi sana kiasi kwamba hata mwandishi ameshindwa kutoa idadi kamili ya majeshi hayo, anaishia kusema tu elfu NYINGI..maana yake hayahesabiki.
Sehemu nyingine, inasema idadi yake ni elfu mara elfu na elfu kumi mara elfu kumi..utaona hapo mwandishi bado anapata shida kuelezea idadi hiyo kamili ya malaika hao, jinsi walivyo wengi, Ni malfu mengi yanayojizidisha, na kujizidisha na kujizidisha..
Ufunuo 5:11 “Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,”
Katika biblia Malaika wapo wa aina tofauti tofauti,
Wapo malaika wa Sifa: Hawa wapo mbele za Mungu usiku na mchana kuilinda enzi yake, ndio wale Maserafi na makerubi; ambao tunawasoma kwenye biblia. Ezekieli 1:4-28, Isaya 6:2-6
Wapo malaika wa vita: Mfano wa hawa ni Mikaeli na malaika zake: 2Wafalme 6:17, Ufunuo 12:7, Yeremia 5:14, 38:17, Hosea 12:5
Wapo malaika wajumbe: Mfano wake ni Gabrieli. Danieli 8:16, 9:21, Luka 1:19,26.
Wapo malaika wa vitu vya asili tu: kama vile moto, maji n.k. Ufunuo 16:5, 14:18
Wapo malaika wa ulinzi, (Mji, na mataifa): Danieli 4:13
Wapo malaika wa ulinzi (wanadamu): Mathayo 18:10, Zaburi 34:7
Wapo malaika wa Huduma (watumishi): Matendo 5:19, 7:30, 8:26, 12:15, 27:23,Waebrania 1:14,
Wapo malaika wa mapigo: Zaburi 78:49, Ufunuo 16
Wapo malaika wa uponyaji: Yohana 5:4, Isaya 6:7
Pamoja na hayo wapo pia malaika walioasi. Ambao biblia inatuambia walikuwa ni theluthi tu ya malaika wote waliokuwa mbinguni. Na hao idadi yao haihesabiki, katikati yao kuna ambao wapo vifungoni saa hii wanasubiria hukumu ya mwisho, (Yuda 1:6)
Wengine wapo vifungoni lakini watakuja kuachiliwa kwa muda kidogo wafanye kazi duniani kwa muda mfupi kisha wataondolewa(Ufunuo 9:1-11),
na wengine wapo bado hapa hapa duniani wakizurura zurura tu kuwaharibu watu, na kusababisha maovu duniani..
Jaribu tu kutengeneza picha tu yale mapepo yaliyomwingia Yule kichaa, kule makaburini, Yesu alipowauliza jina lako nani, yakasema LEGIONI, yaani jeshi, yakimaanisha hatuhesabiki..Sasa Kama ndani ya mtu mmoja yanaweza kukaa mapepo yasiyohesabika, jiulize mapepo yaliyopo ndani ya watu wote ambao hawajampa Kristo maisha yao leo hii yapo mangapi?
Hivyo hiyo inafanya idadi ya malaika ambao Mungu aliwaumba kuwa nyingi sana isiyoweza kuhesabika, hata zaidi ya idadi ya wanadamu wote walioishi na wanaoishi duniani tangu dunia iumbwe.
Hiyo ni kutuonyesha jinsi Mungu alivyojawa na uweza na nguvu na utukufu.
Zaburi 139:17 “Mungu, fikira zako zina thamani nyingi kwangu; Jinsi ilivyo kubwa jumla yake! 18 KAMA NINGEZIHESABU NI NYINGI KULIKO MCHANGA; NIAMKAPO NIKALI PAMOJA NAWE”.
Zaburi 139:17 “Mungu, fikira zako zina thamani nyingi kwangu; Jinsi ilivyo kubwa jumla yake!
18 KAMA NINGEZIHESABU NI NYINGI KULIKO MCHANGA; NIAMKAPO NIKALI PAMOJA NAWE”.
JINA LA BWANA LIHIMIDIWE DAIMA.
Nitaitofautishaje sauti ya Malaika na ya Roho Mtakatifu?
Kwanini Mungu anasema “Afanyaye malaika zake kuwa pepo”?
MALAIKA WAPELELEZI WA HUKUMU WANAPITA SASA.
KUWAHUDUMIA MALAIKA PASIPO KUJUA.
UTAWALA WA MIAKA 1000.
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tulitafakari Neno la Mungu pamoja, kwani ndicho chakula pekee kinachoweza kuziponya roho zetu kabisa kabisa.
Lipo swali tunaweza kujiuliza ni kwanini kuna wasaa ilimgharimu Bwana wetu kulia sana na kutoa machozi ? Tunajua alikuwa ni mkamilifu , alikuwa hana hofu na chochote, na lolote alilomwomba Mungu, dakika hiyo hiyo alipewa, lakini ni kwanini wakati mwingine ilimpasa atoe machozi mengi, na kulia ili apoke?
Kitabu cha Waebrania kinatuambia hivyo;
Waebrania 5:7 “Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja NA KULIA SANA NA MACHOZI, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu”;
Wakati mwingine Bwana wetu Yesu alilia sana kama katoto kadogo, mbele za Mungu wake, alitoa machozi mengi, Yesu huyo ambaye leo hii tunamwita Bwana wa Mabwana na Mfalme wa Wafalme, na kama hilo halitoshi tunamwita mwanaume wa wanaume.
Lakini mwanaume huyu alilia, alitoa machozi katika kumwomba Mungu wake, na kwasababu hiyo Mungu akamsikia, japokuwa hata asingefanya hivyo angesikiwa tu, lakini hisia zake zilizidi uwezo wake, na mamlaka yake, na nguvu zake..alipokuwa mbele za Baba yake machozi yalimtoka mwenyewe tu, pale alipoutafakari uwezo wake jinsi ulivyo mkuu, yalimtoka mwenyewe alipoona Upendo wa Baba yake unavyozidi upeo, yalimtoka mwenyewe pale alipowahurumia watu aliopewa na Baba yake.
Jambo hilo halikuishia tu kwake, tunaona pia aliwaambukiza mpaka na mitume wake waliomtumikia baadaye..Kwa mfano utamwona Paulo wakati mwingi sio tu alilia katika kuomba bali hata alipokuwa anawahubiria watu alitoa machozi, kwa vile alivyokuwa anawahurumia roho zao.
Matendo 20:31 “Kwa hiyo kesheni, mkikumbuka ya kwamba miaka mitatu, usiku na mchana, sikuacha kumwonya kila mtu kwa machozi”.
Soma tena..
2Wakoritho 2:4 “Maana katika dhiki nyingi na taabu ya moyo niliwaandikia na machozi mengi; si kwamba mhuzunishwe, bali mpate kujua upendo wangu nilio nao kwenu jinsi ulivyo mwingi”.
Na…
Wafilipi 3:18 “Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo”;
Unaona hisia hizo nyingi za Paulo ndizo zilizochangia pia hata huduma yake duniani kuwa na mafanikio makubwa. Kwasababu aliyachukulia mambo ya Mungu kwa uzito mkubwa, aliithamini neema katika hisia za hali ya juu sana, ambazo zilimpelekea hata kutoa machozi wakati mwingi alipokuwa anafanya kazi ya Mungu.
Na sisi pia, tuziamshe hisia zetu kwake. Mwingine anaweza kusema mimi siwezi! Ndio huwezi kulia kwasababu hujakaa chini na kuutafakari kwa makini uweza wake wote kwako, aliokufanyia tangu umekuja hapa duniani.
Ungetafakari kwa undani ni kwanini Mungu amekupa uhai mpaka leo hii, na hujampa chochote, ni kwanini unavuta hewa yake bure, na hajawahi kukuchaji hata senti, ni kwanini umekuchagua wewe na kukupa wokovu na muda huo huo kuna wengine hawataki hata kusikia habari za mUNGU, ukidhani kwamba wewe kichwa chako ni chepesi sana kuelewa kuliko wale?, Hilo ondoa akilini, ni kwamba Mungu kachagua tu kukuvuta wewe kwake, hilo tu, huna cha ziada ulichomfanyia. Ukikumbuka siku ile ulikuwa katika jaribu fulani akakuvusha, kama sio yeye ungekuwa ni marehemu sana.. Ukikumbuka hayo yote, hutabaki kama ulivyo,
Ukikumbuka ni kwanini mwaka huu unakwisha, wewe hujafa na KORONA, wakati mamilioni ya watu wamekufa na bado wanaendelea kufa duniani leo hii.. nakwambia utabaki kama ulivyo.. utalia tu, na kutoa machozi kwa kumpa Mungu shukrani, kwa kulibariki jina lake.
Unapoumaliza huu mwaka, usizizuie hisia zako kwa Mungu. Huu ni mwaka ambao sote tunahitaji kumshukuru Mungu, kwa nguvu zaidi kuliko hata miaka mingine yote iliyowahi kututangulia.
“Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele”. (1Nyakati 16:34)
Mungu atujalie kulijua hilo, ayagange macho yetu.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Fadhili ni nini? Nini maana ya “fadhili zake ni za milele” kibiblia?
KUMCHA MUNGU NI NINI? NA MTU ANAMCHAJE MUNGU?
MUNGU HANA MBARAKA MMOJA TU!..MWAMINI.
TUMEPEWA AMRI YA KUKANYAGA NGE NA NYOKA.
USITAFUTE KUKANWA NA BWANA SIKU ILE.
Biblia inapozungumza juu ya fadhili za Mungu, ni zaidi ya zile fadhili ambazo tunazojua ambazo mtu anaweza kuzifanya kwa mtu mwingine, yaani kumuonyesha ukarimu na wema..
Kibiblia Fadhili za Mungu ni Neno pana sana, kwa kiebrania linatamkwa “Hesed”, ambalo tafsiri yake huwezi kuelezea kwa neno moja, au kwa maneno machache.
Fadhili za Mungu sio tu wema na ukarimu Mungu anaotufanyia sisi, bali linamaanisha pia Upendo wa Mungu usioelezeka, upendo wa kusaidia, upendo wa kuvumilia, Upendo wa kuokoa upendo wa kutoa,..
Ni wema usio na masharti, kwamba hatutendei fadhili zake kisa sisi tumemfanyia kitu kwanza, au tumekuwa marafiki zake, Hapana. Anatenda kama vile ni wajibu wake kufanya, Wema huo hauwezi kuelezeka, kwasababu unagusa kila Nyanja, ambazo haziwezi kufikiwa na mwanadamu yoyote Yule, au kiumbe chochote kile mbinguni au duniani., umeingia ndani kabisa.
Na ndio maana Neno hili utalisoma sehemu nyingi sana katika biblia, Na pia utaona Daudi kila alichokiona au alichokitaja alihitimisha na neno “kwa maana fadhili zake ni za milele”..
ZABURI 136
1 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 2 Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 3 Mshukuruni Bwana wa mabwana; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 4 Yeye peke yake afanya maajabu makuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 5 Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 6 Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 7 Yeye aliyefanya mianga mikubwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 8 Jua litawale mchana; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 9 Mwezi na nyota zitawale usiku; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 10 Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 11 Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 12 Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 13 Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 14 Akawavusha Israeli katikati yake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 15 Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 16 Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
1 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2 Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
3 Mshukuruni Bwana wa mabwana; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
4 Yeye peke yake afanya maajabu makuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
5 Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
6 Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
7 Yeye aliyefanya mianga mikubwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
8 Jua litawale mchana; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
9 Mwezi na nyota zitawale usiku; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 10 Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
11 Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
12 Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
13 Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
14 Akawavusha Israeli katikati yake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
15 Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
16 Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Vipo vifungu vingi sana Soma pia.. 1Nyakati 16:34, Zaburi 106:1 n.k.
Utaona pia Musa alipofumbuliwa macho yake na kumwona Mungu kwa sehemu, alipokuwa kule mlima alitangaza na kusema;
Kutoka 34:6 “Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, MWENYE FADHILI, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;
Vivyo hivyo kilichomchea Mungu kumtuma mwanawe duniani kuja kutuokoa, hakikuwa kingine zaidi ya Fadhili zake za milele zinazodumu kwetu daima..
Alikuwa tayari kumtoa mwanawe wa pekee kafara ili sisi tupate wokovu, Jiulize wewe unaweza kumtoa mwanao, tena yule unayempenda kuliko wote awe sadaka ili jirani yako ambaye hakusaidii chochote apone au afaidike? Unaweza kufanya hilo? Huwezi kwasababu hujafikia kiwango hicho cha fadhili za Yehova.
Hivyo kama tukiyajua hayo ni wajibu wetu kumwimbia usiku na mchana, kumshukuru juu ya wema wake aliotuonyesha na anaotufanyia kila siku. Na Tunampa Mungu sifa za vinywa vyetu, pamoja na kwa MATOLEO YETU.
Jina la Yesu Kristo libarikiwe daima.
Haleluya.
ZIKUMBUKE FADHILI ZA MUNGU
NI NANI ATAKAYETUTENGA NA UPENDO WA KRISTO?
KWA KUWA NGUVU ZA MBINGUNI ZITATIKISIKA.
NJIA YA KUPATA WOKOVU.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
WhatsApp
Vikuku ni vitu mfano wa bangili ambavyo vinavaliwa aidha mikononi au miguuni, kwa lengo la urembo. Tazama picha juu. Katika enzi za zamani vikuku vilivaliwa na jinsia zote, yaani wanaume na wanawake.
Katika biblia tunaona neno hilo likitokea mara kadhaa..
2 Samweli 1:10 “Basi, nikasimama karibu naye, nikamwua, kwa sababu nalijua hakika ya kuwa hawezi kupona baada ya kuanguka; kisha nikaitwaa ile taji iliyokuwa kichwani mwake, na kikuku kilichokuwa mkononi mwake, nami nimevileta hapa kwa bwana wangu”.
Na pia unaweza kusoma mistari ifuatayo binafsi iliyozungumzia juu ya vikuku Mwanzo 24:47, Isaya 3:19, Ezekieli 16:11 na Ezekieli 23:42.
Lakini sio hilo tu, vikuku pia vilitumika katika kutengenezea mishikio ya masanduku. Kwa mfano utaona sanduku la Agano lilitengenezwa kwa vikuku katika pande zake za chini ili kuwezesha upitishaji wa zile fimbo zake, na kufanya ubebaji wake uwe mrahisi… Tazama picha chini.
Kutoka 25: 14 “Nawe tia hiyo miti katika vile vikuku vilivyo katika pande mbili za sanduku ili kulichukua hilo sanduku. 15 Hiyo miti itakaa katika vile vikuku vya sanduku; haitaondolewa. 16 Kisha tia ndani ya sanduku huo ushuhuda nitakaokupa”.
Kutoka 25: 14 “Nawe tia hiyo miti katika vile vikuku vilivyo katika pande mbili za sanduku ili kulichukua hilo sanduku.
15 Hiyo miti itakaa katika vile vikuku vya sanduku; haitaondolewa.
16 Kisha tia ndani ya sanduku huo ushuhuda nitakaokupa”.
Lakini je! Katika agano tunaruhusiwa kuvaa vikuku?
Jibu ni la!. Mwanaume au mwanamke wa kikristo hapaswi kutoboa pua na kuweka hazama, hapaswi kujiharibu ngozi kwa kujichubua, hapaswi kuvaa vikuku katika mikono yake au miguu yake..Kwasababu miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu.
1Petro 3:3 “Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; 4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. 5 Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao”
1Petro 3:3 “Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;
4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.
5 Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao”
Mwanamke anayevaa kikuku mguuni, anakuwa hana tofauti na kahaba. Matumizi ya vikuku yabaki katika kutengenezea masanduku na bidhaa nyingine lakini si kuivalisha miili yetu.
Hazama ni nini katika biblia?(Ezekieli 16:12, Kutoka 24:47)
KUJIPAMBA NI DHAMBI?
UUMBAJI BORA WA MUNGU, UPO NDANI YA MWANADAMU.
UFUNUO NI NINI, NA NITAPOKEAJE UFUNUO KUTOKA KWA MUNGU?
UFUNUO: Mlango wa 3 part 3
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, Ni neema tumeiona tena siku ya leo, hivyo nakukaribisha katika kuyatafakari Maneno ya uzima wa roho zetu.
Leo tutajifunza jinsi wokovu unavyopatikana.. Tunapozungumzia wokovu maana yake ni tunazungumzia Uponyaji wa Roho zetu. Upo uponyaji wa mwili na uponyaji wa roho. Sasa njia ya uponyaji wa mwili ni tofauti na ile ya roho.
Sasa kama utakumbuka katika hatua za mwanzo kabisa za wana wa Israeli kutolewa Misri, utaona Farao alikuwa akipigwa kwa mapigo kadha wa kadha…Utaona alikuwa analetewa makundi ya nzige, mara nzi, mara Vyura na chawa n.k. Na kila walipomlilia Bwana awaondolee hayo mapigo Mungu alikuwa anayaondoa katikati yao..
Kutoka 8: 8 “Ndipo Farao akawaita Musa na Haruni na kuwaambia, Mwombeni Bwana, ili awaondoe vyura hawa kwangu mimi na kwa watu wangu; nami nitawapa watu ruhusa waende zao, ili wamtolee Bwana dhabihu. 9 Musa akamwambia Farao, Haya, ujitukuze juu yangu katika jambo hili; sema ni lini unapotaka nikuombee wewe, na watumishi wako, na watu wako, ili hao vyura waangamizwe watoke kwako wewe na nyumba zako, wakae ndani ya mto tu. 10 Akamwambia, Kesho, Akasema, Na yawe kama neno lako; ili upate kujua ya kwamba hapana mwingine mfano wa Bwana, Mungu wetu. 11 Hao vyura wataondoka kutoka kwako wewe na nyumba zako, na watumishi wako, na watu wako; watasalia mtoni tu. 12 Basi Musa na Haruni wakatoka kwa Farao; Musa akamlilia Bwana katika jambo la hao vyura aliokuwa amewaleta juu ya Farao. 13 Bwana akafanya sawasawa na neno la Musa; na hao vyura wakafa kutoka katika zile nyumba, na katika viwanja, na katika mashamba”
Kutoka 8: 8 “Ndipo Farao akawaita Musa na Haruni na kuwaambia, Mwombeni Bwana, ili awaondoe vyura hawa kwangu mimi na kwa watu wangu; nami nitawapa watu ruhusa waende zao, ili wamtolee Bwana dhabihu.
9 Musa akamwambia Farao, Haya, ujitukuze juu yangu katika jambo hili; sema ni lini unapotaka nikuombee wewe, na watumishi wako, na watu wako, ili hao vyura waangamizwe watoke kwako wewe na nyumba zako, wakae ndani ya mto tu.
10 Akamwambia, Kesho, Akasema, Na yawe kama neno lako; ili upate kujua ya kwamba hapana mwingine mfano wa Bwana, Mungu wetu.
11 Hao vyura wataondoka kutoka kwako wewe na nyumba zako, na watumishi wako, na watu wako; watasalia mtoni tu.
12 Basi Musa na Haruni wakatoka kwa Farao; Musa akamlilia Bwana katika jambo la hao vyura aliokuwa amewaleta juu ya Farao.
13 Bwana akafanya sawasawa na neno la Musa; na hao vyura wakafa kutoka katika zile nyumba, na katika viwanja, na katika mashamba”
Na Mainzi ni hivyo hivyo na mapigo mengine yote… Wamisri walipomwomba Mungu awaondolee, Mungu aliwasikia na kuliondoa lile tatizo…soma Kutoka 8:29-30.
Lakini tunakuja kuona mbele kidogo tu, wakati wana wa Israeli tayari wameshavuka bahari ya Shamu, walipomuudhi Mungu, na Mungu alipowaletea zile nyoka za moto…Walimlilia Mungu aziondoe lakini hakuziondoa…badala yake aliwatafutia dawa ili kila aliyeumwa, wanapoitazama ile nyoka ya shaba wapate kupona.
Hesabu 21: 5 “Watu wakamnung’unikia Mungu, na Musa, Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu. 6 Bwana akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa. 7 Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung’unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa Bwana, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu. 8 Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. 9 Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi”.
Hesabu 21: 5 “Watu wakamnung’unikia Mungu, na Musa, Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu.
6 Bwana akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa.
7 Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung’unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa Bwana, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu.
8 Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi.
9 Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi”.
Hapo Bwana hakuwaondoa hao nyoka, kama alivyoondoa wale vyura, au nzige, au chawa wakati wa Farao. Badala yake aliwaacha nyoka waendelee kuwepo (maana yake waendelee kuuma watu)..Na mtu mwenyewe achague aidha UZIMA au MAUTI. Kama atachagua uzima basi atajinyenyekeza na kwenda kuitazama ile nyoka wa shaba, lakini kama hatataka na kuamua kutafuta njia zake yeye mwenyewe anazozijua za kujitibu, basi atakufa.
Sasa Jambo hilo ufunuo wake ni upi?
Bwana Yesu mwenyewe alitufumbua macho na kutupa ufunuo wa tukio hilo katika kitabu cha Yohana. Anasema;
Yohana 3:14 “Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; 15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye”
Yohana 3:14 “Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;
15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye”
Umeona?.. Yule nyoka wa shaba ni mfano wa Yesu Kristo pale msalabani, na wale nyoka ni dhambi iletayo mauti. Hivyo kila mtu anayetumikishwa na dhambi ambayo mshahara wake ni mauti, Akitaka tiba ya hiyo dhambi ni kumtazama Kristo tu.
Kristo kazi yake hakuja kuiondoa dhambi katikati ya jamii yetu, hapana, dhambi ipo ndio maana unaona mpaka leo watu wanaitenda. Alichokuja kukileta ni dawa ya hiyo dhambi. Na sio lazima mtu kupokea uponyaji, ni uchaguzi wa mtu, kuchagua uzima au kifo. Kwa namna ile ile, jinsi wale nyoka walivyoendelea kuachwa katikati ya wana wa Israeli, hawakuondolewa..ili kila mtu ajue kifo kipo na hivyo achague uzima au kifo.
Ndugu usomaye ujumbe huu. Kama hujayakabidhi maisha yako kwa Yesu, biblia inasema..
Kumbukumbu 30:15 “Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya”
Wokovu sio wa kuchaguliwa na mtu, au kuletewa na mtu, ni jukumu la wewe binafsi kuchagua.. Mungu hawezi kulazimisha wokovu uingie ndani yako kama wewe hutaki. Hivyo ni jukumu lako aidha kuchagua kuishi katika dhambi siku zote ambapo mshahara wake ni mauti ya mwilini na rohoni, au umtazame Kristo pale msalabani upate uzima wa milele. Uchaguzi ni wako.
Bwana akubariki.
KWANINI YESU KRISTO NI WA MUHIMU KWETU SASA?
WAPE WATU WANGU RUHUSA ILI WAPATE KUNITUMIKIA.
UMUHIMU WA KUZALIWA MARA YA PILI.
Bwana Yesu alikuwa anamaanisha nini kusema Marko 2:19″walioalikwa harusini wawezaje kufunga maadamu bwana-arusi yupo pamoja nao?”
JE UPENDO WAKO UMEPOA?
Ashera au kwa jina lingine anajulikana kama Ashtorethi, Ni mungu-mke wa kipagani ambaye alikuwa anabudiwa katika nchi ya wakaanani, Waashuru na mataifa mengine ya kando kando pale mashariki ya kati..
Ashera pamoja na Baali ni moja ya miungu ambayo ilikuwa ni maarufu sana duniani kwa wakati huo.
Katika nchi ya Kaanani walikuwa wanamwabudu katika mfumo wa mti, ambao ulipandwa chini, na kuchongwa katika maumbile ya mwanamke, kumwakilisha yeye. Wakimwona kama ndiye mti wa uzima.
Sasa tunaona katika maandiko, Wana wa Israeli wakiwa bado jangwani Mungu aliwaonya sana, juu ya miungu ya nchi hiyo ya Kaanani wanayoiendea, kwamba wasijichanganye nayo, badala yake wakifika huko waivunje vunje, na kuiondoa, kwasababu yeye ni Mungu mwenye wivu;
Kutoka 34:12 “Ujihadhari nafsi yako, usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea, lisiwe mtego katikati yako. 13 Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunja-vunja nguzo zao, na kuyakata-kata maashera yao. 14 Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa kuwa Bwana, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni Mungu mwenye wivu”.
Kutoka 34:12 “Ujihadhari nafsi yako, usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea, lisiwe mtego katikati yako.
13 Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunja-vunja nguzo zao, na kuyakata-kata maashera yao.
14 Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa kuwa Bwana, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni Mungu mwenye wivu”.
Lakini tunaona walipofika nchi ya ahadi hilo hawakulizingatia badala yake, nao wao pia wakaanza kuiga desturi za wale wafiisti ambao hawakuwamaliza wote, wakaanza na wao kuabudu Maashera..
2Wafalme 17:9 “Tena, wana wa Israeli wakafanya kwa siri mambo yasiyokuwa mema juu ya Bwana, Mungu wao, wakajijengea mahali pa juu katika miji yao yote, kutoka mnara wa walinzi hata katika miji yenye boma. 10 Wakajisimamishia nguzo na maashera juu ya kila mlima mrefu, na chini ya kila mti wenye majani mabichi”;
2Wafalme 17:9 “Tena, wana wa Israeli wakafanya kwa siri mambo yasiyokuwa mema juu ya Bwana, Mungu wao, wakajijengea mahali pa juu katika miji yao yote, kutoka mnara wa walinzi hata katika miji yenye boma.
10 Wakajisimamishia nguzo na maashera juu ya kila mlima mrefu, na chini ya kila mti wenye majani mabichi”;
Ikafikia hatua mpaka wafalme wengine wakawa sio tu wanaibudia nje kwa siri, bali waliichukua kabisa nguzo zake na kuipeleka katika hekalu la Mungu, mahali ambapo Mungu ameliweka jina lake, watu wamwabudu na kumfanyia dua, wao wanaingiza miungu migeni, Matokeo yake wakamtia Mungu wivu mkubwa zaidi, wakapewa adhabu ambayo isiyosameheka, na adhabu yenyewe ilikuwa kuuliwa, mji kuteketezwa na kuchukuliwa utumwani Babeli.
Mfalme ambaye alifanya kitendo hicho aliitwa Manase;
2Wafalme 21:7 “Akaiweka sanamu ya kuchongwa ya Ashera aliyoifanya ndani ya nyumba, ambayo Bwana alimwambia Daudi, na Sulemani mwanawe, Katika nyumba hii, na katika Yerusalemu, niliouchagua miongoni mwa kabila zote za Israeli, nitaliweka jina langu milele”;
Utasoma habari za maashera katika vifungu hivi;
2Nyakati 14:2,17:6, 19:3, 24:18, 23:14
Je hadi leo kuna maashera yanayoabudiwa?
Hata sasa Mambo hayo yanatendeka katika Kanisa la Kristo hata leo, na cha kusikitisha zaidi ni kuwa wanajua kabisa Mungu amekataza lakini wao wanafanya.
Unapoliweka sanamu la mtakatifu fulani (tuseme bikira Mariamu), na kuanza kulihusianisha na ibada, unaomba kwa kupitia hilo, unaeleza shida zao kwa kutazama sanamu hilo, ujue kuwa unamwabudu Ashera moja kwa moja.
Na tendo hilo linamtia wivu Mungu sana, wivu ambao unaweza kukusababishia mauti. Ni heri ukutane na hasira ya Mungu kuliko Wivu wake..Kwasababu wivu unakula na hivyo mapigo yake ni makali zaidi.
Wimbo 8:6b..Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera.
Biblia inasema tena…
Mithali 27:4 “Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika; Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu”.
Unaona?, shida inakuja ni pale mtu anapoelezwa ukweli kama huu, anadhani dini yake inashutumiwa..Nakwambia ni heri dini ishutumiwe roho yako ipone, kuliko roho iangamie dini yako iendelee kumtia Mungu wivu, faida yake itakuwa ni nini sasa? Tubu mgeukie Kristo, uokoke. Hizi ni nyakati za mwisho.
HISIA YA MUNGU ILIYO MBAYA KULIKO ZOTE.
USIIGEUZE NYUMBA YA MUNGU KUWA PANGO LA WANYANG’ANYI.
KUABUDU SANAMU/IBADA ZA SANAMU.
JIEPUSHE NA MANENO YA MANABII WA UONGO.
Nini maana ya uvuvio?.