Katika biblia Neno “Mshenzi” linatajwa.Kwanini liwekwe?

Katika biblia Neno “Mshenzi” linatajwa.Kwanini liwekwe?

SWALI: Katika Wakolosai 3:11 tunaona neno “Mshenzi” likitajwa.Kwanini Neno hili liwekwe pale?


JIBU: Tusome..

Wakolosai 3:11 “Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mgeni wala MSHENZI, mtumwa wala mwungwana, bali Kristo ni yote, na katika yote”.

Mshenzi kulingana na kamusi ni mtu asiyejali mambo ya Ki-Mungu, asiyekuwa na staha, au adabu ni rahisi kujiamulia tu mambo yake mwenyewe, hata kuua yeye hajali, na mara nyingi anakuwa ni mkatili na mnyama.

Sasa enzi hizo za kanisa la kwanza kulikuwa na kundi maalumu lililojulikana kama washenzi, jamii ya watu hao walikuwa wanaishi kando kando mwa bahari ya Nyeusi(Black sea) ambao kwasasa ni maeneo ya Urusi, Ni watu ambao walikuwa hawana elimu na walikuwa ni wafugaji wanaohama hama, pia walikuwa ni wakatili na wanyama sana, walikuwa mara nyingi wanafananishwa na wanyama wa mwituni kwa ukatili wao.

Hivyo watu wa namna hiyo, waliitwa washenzi.. Lakini cha ajabu ni kwamba na wao pia walihesabiwa kustahili neema ya Yesu Kristo.

Hata sasa zipo jamii nyingi za watu ulimwenguni wa namna hizi au zaidi hata huku Afrika, ambazo zinaweza kuonekana kama hazistahili kupokea neema ya injili kwa staili yao ya maisha, kwa kuwa nyuma kimaendeleo, watu wake kuwa ni wajinga, ma-bushmen, wanaotembea uchi, wanakula nyama za watu, hawana imani na kitu chochote kile n.k.(Ambao kwa namna nyingine wangeitwa washenzi ) Lakini kumbe hao nao Mungu anawatazama na neema yake ya wokovu inapaswa iwafikie kama wengine..

Hiyo ni kutufundisha kuwa hatupaswi kuchagua mtu bali ni sharti injili ihubiriwe kwa kila kiumbe.(Mungu hana ubaguzi kwa mtu yoyote yule, katika suala la wokovu hatatazami rangi, wala ukabila wala utaifa, wote ni watu wake wanaostahili wokovu sawa kupitia mwanawe mpendwa Yesu Kristo, ambaye ni Bwana wetu)

Bwana atubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

TUWATAFAKARI NZIGE WA JANGWANI.

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 2

TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?

Je! Ni kweli ubatizo wa maji hatuuhitaji tena?

 

Je ni sahihi kumtenga mtu anapofanya dhambi kanisani?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments