Title December 2019

KWANINI NAYAWEZA MAMBO YOTE KATIKA YEYE ANITIAYE NGUVU?

Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu..


Wafilipi 4:12 “Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.

13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”.

Huu ni mstari unaohamasisha sana, hususani  tunapopitia katika hali Fulani ngumu, pale tunapoona hatuwezi kuvuka au kuendelea mbele katika kitu fulani, pale tunapoona bado hatua moja tu ya sisi kukata tamaa.. Lakini tunapousoma mstari huu unatupa nguvu ya kuendelea mbele.. Na kubakia kusema..

Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu..

Lakini kama ukisoma vizuri mistari ya juu yake utaona mtume Paulo anazungumzia mambo aliyoyapitia huko nyuma, kuna wakati alipitia kufanikiwa sana, vilevile kuna wakati alipitia kuishiwa sana, akawa hana hata shilingi mfukoni mwake, au kama anayo basi ni kidogo sana ukilinganisha na mahitaji aliyokuwa nayo.Tunalithibitisha hilo, wakati Fulani Paulo akiwa   Rumi alimwagiza Timotheo na kumwambia siku atakapokwenda aende la lile joho lake aliloliacha kwa Karpo kabla ya wakati wa baridi kuanza.

2Timotheo 4:13 “Lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa, ujapo ulilete, na vile vitabu, hasa vile vya ngozi”.

Kulikuwa hakuna sababu ya Paulo kumwambia Timotheo ambebee joho lake asafiri nalo mamia kama sio maelfu kwa maelfu  ya kilometa na mzigo wa koti, Mtume Paulo angeweza tu kununua joho(koti) lingine kule kule kama angekuwa na fedha ya kutosha, lakini hiyo yote ni kwasababu wakati wa kupungukiwa ulimpitia, lakini hakuiacha imani na maneno yake yalikuwa ni haya.. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Paulo anasema tena nimefundishwa kushiba na kuona njaa.. Katika ziara zake za kuhubiri injili alipitia vipindi vigumu sana mahali ambapo hakukuwa na namna yoyote ya kupata chakula, tunaweza kuliona pia hilo wakati ule alipokuwa anasafirishwa pamoja na wafungwa wengine kuelekea Rumi..Wakiwa kule kilindi kwa muda mrefu waliishiwa na chakula, mpaka watu waakanza kuishiwa na nguvu..Lakini Mungu alimuuokoa yeye pamoja na wafungwa wale katika hali ile, wala hakutetereka katika imani yake..

Matendo 27:20 “Jua wala nyota hazikuonekana kwa muda wa siku nyingi, na tufani kuu ikatushika, basi tukakata tamaa ya kuokoka.

21 Na walipokuwa wamekaa wakati mwingi bila kula chakula, Paulo akasimama katikati yao, akasema, Wanaume, iliwapasa kunisikiliza mimi na kutokung’oa nanga huko Krete, na kupata madhara haya na hasara hii.”

Na ndio maana hata huku mbele anaoujasiri wa kusema..

Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu..

Anasema tena, nimefundishwa kuwa na vingi na kupungukiwa. Kuna wakati alifika hakuwa na haja ya kitu chochote, mpaka akawa na kitu cha kuwagawia wengine, lakini pia kuna wakati ulifika wa kupungukiwa lakini katika hayo yote kimiujiza ujiza katika vipindi hivyo vyote, baridi , joto, mvua na mafuriko hakutikisika hata kidogo katika imani yake..Anasema:

2Wakorintho 11:26 katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang’anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo;

27 katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi.

28 Baghairi ya mambo ya nje, yako yanijiayo kila siku, ndiyo maangalizi ya makanisa yote.

 Unaona, mtu kama huyu pamoja na kupitia taabu zote hizi, na bado hajaiacha imani ataachaje kusema..

“Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”?

Lakini nataka nikuambie mpaka mtu apokee uweza huu wa kuweza mambo yote..Si suala la kujiamulia tu mtu mwenyewe kwa bidii zake, au kujitamkia tu kwa kinywa chake..Unaweza ukajitamkia kuanzia januari mpaka Disemba kwamba “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”. Lakini ikija tufani kidogo tu  unaweza kwenda na maji.

 Kama wewe sio mkristo, ukweli ni kwamba huyawezi mambo yote..Kama unajiita mkristo halafu hujaokoka,  bado huyawezi mambo yote..Wala usijidanganye kusema hivyo,…Hutakaa uweze kushinda majaribu yote ya huu ulimwengu na bado ukadumu kwa Kristo kwa moto ule ule, hutakaa uweze kustahimili taabu zote na bado usifanye dhambi..Kwamwe hutakaa uweze..

Kumbuka mtume Paulo hasemi “Nayaweza mambo yote katika mimi au katika nguvu zangu”.. anasema, Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu..”Yeye anitiaye nguvu”..Hivyo ni lazima huyu akutiaye nguvu awe ndani yako ndio uwezo huo wa kuweza mambo yote ukujie.

Unajiuliza saa nyingine ni kwanini unajaribiwa na vishawishi vya uzinzi, halafu unazidiwa na tamaa unakwenda kufanya uzinzi, ni kwasababu huyo akutiaye nguvu za kuweza kushinda vishawishi hivyo hayupo ndani yako, kama angekuwepo usingekaa utamani kufanya jambo hilo..

Au ulitamani usitazame pornography, au usifanye punyeto lakini ukajitahidi siku mbili,tatu mbele. Mwezi ulipopita  ukazidiwa na tamaa ukaenda kurudia yale yale uliyokuwa unayafanya…Ni kwasababu gani? Ni kwasababu Yule ambaye angepaswa kukutia nguvu ya kuweza kushinda majaribu hayo milele hakuwepo ndani yako.

Au ulikuwa unaonyesha dalili ya kumpenda Mungu kweli, lakini ulipokutana na vita kutoka kwa ndugu au wazazi wako, au marafiki wako, wakakuzidi nguvu, ukayarudia yaleyale uliyokuwa unayafanya mwanzoni kwa kuogopa tu utatengwa au utachukiwa..Ni kwasababu gani ulishindwa kustahimili? Ni kwasababu Yule akutiaye nguvu hakuwa ndani yako.

Au ulikuwa ni mkristo mzuri tu, unashuhudia hata wengine habari njema..lakini labda ulipitia hali Fulani ngumu ya kiuchumi, ukayumba kidogo na hiyo ikakufanya uamue kuacha wokovu wako na kwenda kujichanganya na dunia..Ni kwanini ulishindwa kuendelea mbele na imani? ni kwasababu Yule akutiaye nguvu ulishamwacha zamani.

Au sio tu katika shida, bali pia hata katika mafanikio,..Pengine Mungu alipokufanikisha katika kitu Fulani, labda pengine alikupa kazi nzuri yenye mshahara mkubwa, au alikupa nyumba nzuri, au alikupeleka nchi za nje kuishi, au alikuponya ugonjwa wako, na matokeo yake umemsahau Mungu wako umeyarudia yale yale ya zamani..Na leo hii unajiuliza imekuwaje kuwaje nimechukuliwa kirahisi na fahari za ulimwengu huu.. Jibu ni kwamba Yule akutiaye nguvu amekuacha na ndio maana huyawezi mambo yote.. Katika hayo bado huwezi kudumu katika njia wa wokovu..Umepimwa katika mizani nawe umepunguka.

Lakini leo hii ukasema ninataka kuanza upya na Bwana, ninataka atembee na mimi, anipe uwezo wa kuyaweza mambo yote, katika milima awe na mimi kunitia nguvu, katika mabonde awe na mimi kunifariji, katikati ya maadui awe na mimi kama mchungaji wangu, katikati ya vilindi awe nahodha wangu, katikati ya raha awe furaha yangu nisimuache..katikati ya mafanikio awe tajiri wangu, katikati ya afya awe sifa yangu..katika chochote kile kiwe ni chema au kibaya, bado awe ni Bwana na mwokozi wa maisha yangu..

Nami niwe na ujasiri wa kusema.. “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu” Shetani haniwezi kwa wimbi lolote atakalolita mbele yangu.. Unahitaji uwezo huo sasa ukujie??

Kumbuka ili uweze kupokea nguvu hizo kutoka kwa Bwana, yeye anachotaka kwako tu ni MOYO wa TOBA unaotamani tu kugeuka na kuacha..Moyo uliomaanisha kweli kweli kuacha hivyo vitu..Watu wengi hawaoni matokeo yoyote au badiliko lolote katika maisha yao kwasababu tu, hawamaanishi kuviacha vitu walivyokuwa wanavifanya nyuma.

Mwingine ni mlevi, anataka Mungu ampe nguvu ya kuacha ulevi, lakini hayupo tayari kuacha ulevi wenyewe, mwingine anakula ugoro, mwingine anavuta sigara, mwingine madawa ya kulevya, mwingine punyeto, mwingine ukahaba, wote hawa wanataka Mungu awepe nguvu ya kuacha lakini wao wenyewe bado wanatamani kuendelea kufanya hivyo vitu..

Ukisema nataka niache, unatakiwa umuonyeshe Mungu unakichukia hicho kitu kweli kweli, na kwamba ndio sababu ya kukupeleka kuzimu..Mungu anataka watu wanaomaanisha na sio watu wanaojaribu..Na Mungu akishaona moyo wako kama huo ambao unaambata na vitendo basi moja kwa moja anakushushia nguvu ya ajabu ambayo hiyo itakufanya wewe uone yale uliyokuwa unayafanya nyuma ni takataka na uozo,..

Sisi tulikuwa ni wazinzi wa kupindukia, tulikuwa ni watazamaji wa pornography, tulikuwa ni walevi, tulikuwa ni watukanaji lakini uwezo huo uliposhushwa juu yetu KIU ya hayo mambo yote yalikatwa ghafla. Na muda  wote tulikuwa tunatamani tu kumjua Mungu..Na hadi sasa ni miaka mingi imepita hata chembe ya mambo kama hayo haipo ndani yetu.. haijalishi ni vishawishi vingapi vinakuja mbele yetu ..tunaoujasiri wa kusema..

“Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”

Tumejengwa juu mwamba imara usioweza kutikiswa kwa kitu chochote.

Hivyo kama Mungu alikuwa mwaminifu katika Neno lake kutufanyia sisi hivyo..Anao uwezo huo pia wa kukuanyia na wewe leo hii kama utakubali..

Kama upo tayari kufanya hivyo kumpa Bwana Maisha yako…

Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU  MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo. Ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Na Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako sawasasawa na Matendo 2:38. Kumbuka ubatizo sahihi ni muhimu sana kwa mtu aliyeokoka hivyo usipuuzie agizo hilo la Bwana.

Zingatia hayo na Bwana atakuwa pamoja nawe. Vilevile Usiacha kutembelea Website hii  https://wingulamashahidi.org mara kwa mara ili ujifunze maneno ya uzima..

Ubarikiwe sana.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:

Mada Nyinginezo:

SIRI YA KUFANIKIWA KWA MTUME PAULO.

ANTIPA SHAHIDI WANGU, MWAMINIFU WANGU.

KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?

NAMNA YA KUMTAMBUA BIBI ARUSI WA KWELI WA KRISTO.

Kwanini Musa alipewa mbao mbili za mawe na sio moja au zaidi

UNYAKUO.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Rudi Nyumbani:

Print this post

Mungu anaweza kuongea wakati yeye ni Roho?

Swali 1: Mungu anaweza kuongea wakati yeye ni Roho?..Roho inaweza kuelewa, kutambua, kuona bila ubongo?.. Swali 2: Adamu na Hawa walimwona Mungu?.. Swali 3: Na je! Mungu anazidi kujificha kwetu au kujidhihirisha kadiri muda unavyozidi kwenda?.


Swali 1: Mungu anaweza kuongea wakati yeye ni Roho?..

Jibu: Kabla ya kwenda kwa Mungu, tuanze kwanza kwa mtu.  Mtu anapozungumza, kuzungumza kwake kunaanzia rohoni..katika roho yake ndio anazungumza..Mwili ni kama kipazia sauti cha roho katika mazingira ya kidunia… Ili kuelewa vizuri tafakari mfano ufuatao.

Umechukua simu yako na ukampigia ndugu yako (video-call) ambaye yupo mkoa mwingine au nchi nyingine..mkawa mnazungumza huku mnaonana kabisa kupitia simu…ukawa unamwona yule ndugu yako kupitia simu ile na kuisikia sauti yake…Sasa yule ndugu yako aliyeko mkoa mwingine, je anaweza kusema pasipo simu wewe huwezi kuzungumza naye?..Jibu ni hapana…unaweza kuzungumza naye hata pasipo simu, endapo akisafiri akakufuata mahali ulipo au ukimfuata mahali alipo bado mnaweza kuzungumza tu tena vizuri sana Zaidi hata ya kutumia simu…

Sasa simu ni kiunganishi tu, ambacho ili kiweze kutuunganisha na watu walioko mbali nasi kinahitaji kiwe na chaji, kiwe na betri, kiwe na network, kiwe na spika, na kiwe na jicho la kamera ili kiweze kumrekodi yule aliyeko mbali.

Na miili yetu ndio hivyo hivyo, ni kama simu tu! Ili iweze kuziunganisha roho zetu na mazingira ya kimwili Inahitaji ubongo, inahitaji moyo unaosukuma damu, inahitaji, macho mawili kurekodi matukio ya nje na kuyatuma katika roho zetu, inahitaji pua kuchukua taarifa za mwili kuzipeleka rohoni, n.k

Lakini pia pasipo hii miili tunaweza kuongea, kutazama, kuzungumza tena vizuri sana pasipo hata kuwa na miili.. Kama vile ilivyomubashara Zaidi mtu kuzungumza uso kwa uso na mwenzake Zaidi kuliko kuzungumza naye kwenye simu. Tukitoka katika huu mwili bado tunauwezo wa kuona, kusikia, kuzungumza n.k Mwili si kitu cha lazima sana kama vile simu isivyokuwa ya lazima.

Kwahiyo mwili ni njia tu, lakini mambo yote yanaanzia katika utu wa ndani. Na kama sisi tupo hivyo basi Mungu uwezo wake ni mkubwa Zaidi na mpana sana..upeo wake ni mkuu Zaidi ya huo na anaweza kufanya zaidi ya hayo. Ndio maana utaona mara kadhaa sauti ilisikika kutoka mbinguni ikisema huyu ni mwanangu mpendwa wangu.

Swali 2: Adamu na Hawa walimwona Mungu?

Jibu: Biblia haijasema moja kwa moja walikuwa wanamwona kwa namna gani, lakini kulingana na habari ile ni wazi kuwa walikuwa wanamwona kabisa wazi.

Swali 3: Kadiri muda unavyozidi kwenda, Mungu anazidi kujificha kwetu au kujidhihirisha?

Jibu: Mungu yupo karibu na sisi siku zote…hana wakati ambao alishawahi kuwa karibu nasi sana kuliko wakati mwingine wowote, wala hana wana wakati ambao alijitenga nasi. kamwe yeye yupo pale pale.  Kinachotufanya sisi tumwona yupo mbali nasi au karibu nasi ni kiwango cha maovu yetu na utakatifu wetu.

Isaya 59: 1 “Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;

2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia”.

Yakobo 4: 8  “Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili”.

Anatushauri haya..

Kumbukumbu 30: 11 “Kwa maana maagizo haya nikuagizayo leo, si mazito mno kwako, wala si mbali.

12 Si mbinguni, hata useme, Ni nani atakayetupandia mbinguni akatuletee, aje atuambie tusikie, tupate kuyafanya?

13 Wala si ng’ambo ya pili ya bahari, hata useme, Ni nani atakayetuvukia bahari, akatuletee, aje atuambie, tusikie, tupate kuyafanya?

14 Lakini neno li karibu nawe sana, li katika kinywa chako na moyo wako, upate kulifanya.

15 Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya”

Ubarikiwe.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:

Tafadhali share na wengine.


Mada Nyinginezo:

WEWE SI MALI YAKO MWENYEWE!

HISTORIA YA ISRAELI.

UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?

ALIJARIBIWA SAWASAWA NA SISI KATIKA MAMBO YOTE.

SAUTI NI SAUTI YA YAKOBO, LAKINI MIKONO NI YA ESAU.

JINSI YA KUJIWEKA KARIBU NA MUNGU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

UMUHIMU WA YESU KWETU.

Umuhimu wa Yesu kwetu, ni mkubwa sana kama tunavyousoma katika kitabu cha .Waefeso 4:13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na KUMFAHAMU SANA MWANA WA MUNGU, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;”

Shalom jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tena tujifunze Neno la Mungu, ambalo ndio taa ingozayo miguu yetu na mwanga wa njia zetu.(Zab 119:105).

Kama tulivyotangulia kujifunza, na kama wengi wetu tunavyojua kwamba mtu wa rohoni sio mtu mwenye uwezo wa kuwaona wachawi..kama inavyoaminika na wengi.. Wale watu wawili waliokuwa wanakwenda Emau, macho yao ya rohoni yalipofumbuliwa hawakuona wachawi, au majini yaliyokuwa yanawazunguka..Bali walimwona Yesu.(kasome Luka 24:13-33,)

Hivyo mtu wa rohoni ni Yule mwenye uwezo wa kumwona na kumtambua Yesu Kristo katika maandiko na katika maisha yake. Mtu aliyefunuliwa macho ya rohoni atamjua sana Mwana wa Mungu, Yesu Kristo Zaidi ya kitu kingine chochote,atajua dhumuni la yeye kuja duniani ni lipi, mamlaka aliyonayo nayo ni yapi, nafasi aliyonayo sasahivi ni ipi, na ni wapi kaandikwa katika maandiko, na umuhimu wa Yesu katikati ya wanadamu…Na mtu wa namna hiyo ataishia kumheshimu na kuwa mwangalifu na Maisha yake kuwa ya kipekee sana.

Ukishindwa kumwelewa Yesu Kristo, basi haijalishi unaona maono kiasi gani, au una elimu  ya dini kubwa kiasi gani, au unaelimu nyingine kubwa kiasi gani, au unaona wachawi kiasi gani, bado wewe ni mfu kiroho na macho yako ya rohoni yamefumbwa… Kiini cha kumwona na kumjua Mungu ni Yesu Kristo.

Wakolosai 2:9  “Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili”

Na ndio maana Biblia inatuambia tena katika ”..

Waefeso 4:13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na KUMFAHAMU SANA MWANA WA MUNGU, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;”

Hivyo tunahitaji kumahamu sana huyu MWANA WA MUNGU, mafundisho yetu, mawazo yetu, shule yetu wakati wote inapaswa ilenge katika huyu mtu mmoja Yesu Kristo..Ili tuwe watu wa rohoni. Na leo kwa neema za Mungu tutajifunza kidogo juu ya huyu mwana wa Mungu (Yesu Kristo).

Tofauti na wengi tudhaniavyo kwamba Yesu Kristo anahitaji sana sifa kutoka kwetu..pasipo kumjua yeye ni nani?..Lakini ukweli ni kwamba Yesu Kristo anahitaji kwanza tumjue ndipo sifa zetu ziwe na maana kwake.  Hata katika hali ya kawaida, huwezi kuzithamini pongezi au sifa za mtu ambaye hakujui, ametokea tu huko ghafla na amesikia tu jina lako mitaani..halafu anakuja na kuanza kukupongeza na kukusifia kidogo utakuwa na mashaka..jambo la kwanza utamwuliza..je unanijua?…Tofauti na kama ingekuwa ni ndugu yako, ni wazi kuwa pongezi hizo utazithamini kwasababu anakujua sana,  anajua ulipotoka, uliyopitia, ulipo sasa na unapokwenda…

Hivyo pongezi zake zitakuwa na maana sana kwako kuliko za hao wengine ambao hawakujui wala hamjuani..Utafahamu ni za kinafki tu.

Kwahiyo hata sifa zetu tunazomsifia Bwana kama hazijachanganyikana na maarifa yakutosha ya kumjua yeye kiundani..basi sifa zetu ni za kishabiki tu ambazo hazina nguvu yoyote kwa Mungu.

Sasa hebu kwa ufupi tumwangalie kdogo huyu mwana wa Mungu (yaani umuhimu wa Yesu kwetu wanadamu).

Mungu alipomwumba Adamu alimpa mamlaka yote ya duniani..ikiwemo kutawala kila kiumbe pamoja na kuitiisha nchi..Adamu na uzao wake akafanywa kuwa mtawala wa vitu vyote..Hata shetani alikuwa chini yake,..hakuna kiumbe chochote kingekuwa na mamlaka ya  kusogeza hata jani moja isipokuwa kwa mamlaka ya Adamu, mamlaka hiyo Adamu aliendelea kuwa nayo mpaka  siku Hawa alipodanganywa na nyoka na kula tuna na kumpa mumewe..na wote wawili walipoasi hiyo mamlaka yote waliyopewa wakamwuzia shetani. Hivyo shetani akawa mtawala wa ulimwengu..akitaka kumtupia mwanadamu ugonjwa anweza, hata akitaka kumwua anao uwezo huo. Akitaka kuleta tufani anaweza na mwanadamu yoyote asimzuie.

Na hata funguo za kuzimu pia alizichukuwa shetani. Habari yetu sisi wanadamu ikawa imeishia pale, tukawa tumejiharibia wenyewe..Tukawa kundi moja na malaika walioasi, ambao wanasubiriwa kutupwa katika lile ziwa la moto…Kukawa hakuna tena nafasi ya kusamehewa, njia ya uzima ikafungwa kama ilivyofungwa kwa malaika walioasi mbinguni..shetani hakuwa na nafasi ya kutubu wala kuokolewa…Na sisi tukawa ndio hivyo hivyo..Hivyo likawa limesalia jambo moja tu mbele yetu, kufutwa sisi sote…

Lakini kwa huruma za Mungu..akatengeneza njia ya wokovu kwa mwanadamu….kwamba mwanadamu aokolewe..yaani ni kama bahati tu!..shetani na mapepo yake hawakupata hiyo bahati ya nafasi ya pili kama tuliyopata sisi. Na kwasababu ni mwanadamu ndiye aliyejiharibia hamna budi kwa njia ya mwanadamu huyo huyo ukombozi utokee.

Hivyo Mungu akaanza uumbaji mwingine wa mtu mwingine, ambaye huyo atakuwa kama Adamu..ambaye atapewa mamlaka yote ya duniani, atawale kila kitu na kila kiumbe,na vitu vyote viwe chini yake, kama Adamu, mtu huyo Ataumbwa akiwa mkamilifu na bila dhambi kama alivyoumbwa Adamu. Na huyo si mwingine zaidi ya YESU KRISTO..Huyu Yesu ni Adamu wa Pili….Ameumbwa kwa viganja vya Mungu kwa uweza wa Roho katika tumbo la Bikira. Huyu alikuwa ni mwanadamu kabisa, lakini kuna SIRI kubwa iliyokuwepo ndani yake…japokuwa alionekana kama mwanadamu lakini alikuwa ni Mungu mwenyewe aliyeuvaa mwili..(kasome 1Timotheo 3:16). Lakini hilo halikuwa la muhimu sana sisi kulijua ndio maana biblia ikaliita ni siri..

Hivyo wakati wa Yesu Kristo kama Adamu wa pili kuzaliwa, kulikuwepo na kizazi pia cha Adamu ambacho kilishaasi na hivyo kinapaswa kiondolewe kibaki kizazi cha Yesu Kristo tu!.. Sasa Yesu Kristo hakuwa na mke wa kimwili kama Adamu wa kwanza..wala hakuwa na watoto wa kimwili…Kwasababu hiyo basi ili sisi tusiangamie na hiyo ghadhabu ya Mungu itakayomwangwa juu ya uzao wote wa Adamu ulioasi akatutwaa sisi na kutufanya kuwa kama uzao wake, na ndugu zake wakike na wakiume..(akatu-adopt).

Ulishawahi kuona mtu ambaye ni tajiri sana hana watoto, anakwenda nchi ya mbali  kutafuta mayatima ambao maisha yao yapo hatarini na kuwaleta kwake na kuwafanya kuwa wanawe? (anawaa-adopt)..Ndio hicho hicho, Bwana Yesu alichokifanya kwetu…alitutwaa sisi ambao tayari tulikuwa tumeshatamkiwa hukumu na kutufanya kuwa wake..Hivyo kwa yeyote ambaye atatii na kumkubali na kujiunga naye atahesabiwa kuwa ni uzao wa Yesu Kristo,  naye pia atashiriki pamoja naye katika ufalme aliopewa na Mungu kwamba akatawale viumbe vyote, na kila kitu kilichopo duniani, na vitu vyote.

Mathayo 28:18 “Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani”.

Sasa kabla ya wakati wa kuondolewa uzao wote wa Adamu ulioasi haujafika,Bwana Yesu  anatuma kwanza mwaliko, kwamba popote pale wanadamu wote walipo walio wa uzao wa Adamu wa kwanza walioasi ambao wanapenda maisha, waje kwake naye atawapokea…kwamba wamwendee huyu Yesu Kristo aliyekabidhiwa mamlaka yote ya mbinguni na duniani wapate uzima.

Na huyu Yesu alianza kutuma mwaliko huo tangu vizazi vyuma na hata sasa anatuma..kwamba ufalme wake kuanza kutawala dunia umekaribia..kwamba muda ni mchache tu tuliobakiwa nao wa sisi kuitikia wito wa kuingia ndani ya hiyo neema..Utafika wakati wa utawala wake kuanza ambapo kutakuwa hakuna tena nafasi ya mtu yoyote kuingia..Mlango wa neema utafungwa.

Luka 13:23 “Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,

24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.

25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;

26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.

27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu”.

Wakati huo huyu Yesu Kristo tunayemwona sasa ambaye anatusihi sasa hatakuwa hivi tunavyomwona leo..Atageuka na kuwa miale ya moto,na  Mungu atakihukumu kizazi chote cha Adamu kilichoasi na kumkataa mwanawe mpendwa…na kuwanusuru wale wote waliomkimbilia Mwanawe pekee Yesu Kristo.

Unaweza kuona jinsi hiyo neema ilivyo ya ajabu..Sisi kupata nafasi ya kufanyika Uzao wa Yesu Kristo?…Watu ambao tulikuwa tumewekwa kundi moja na malaika walioasi?..

1Petro 2:9 “Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;

10 ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema”.

Ndugu Bwana Yesu ndiye aliyekabidhiwa kila kitu sasa…Hajaanza kutawala kwa utukufu wake sasa wala kuushusha  ufalme wake, kwasabababu bado anataka watu watubu ili wasiangamia…lakini fahamu kuwa ufalme wake umekaribia sana…na siku atakapokuja mataifa yote waliomkataa wataomboleza na kulia….Kama ulikuwa unamfahamu tu Yesu Kristo kama “mwanadamu wa kawaida ambaye hana umuhimu sana”..leo futa hayo mawazo…Yule sio wa kawaida kabisa…kashakabidhiwa mambo yote na sasa hivi yupo mbinguni,  angekuwa ni wa kawaida angekuwa duniani sasahivi au kaburini…lakini yupo mbingu ya juu sasa, ambako hakuna aliyewahi kufika hata sasa,  anasubiri mtu wa mwisho kuingia ndani, mlango ufungwe ashuke kuja kutawala…

Mathayo 28.16 “Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu.

17 Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka.

18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, NIMEPEWA MAMLAKA YOTE MBINGUNI NA DUNIANI”.

Je bado unamchukulia kama ulivyokuwa unamchukulia?..Je bado unaichezea neema yake hiyo?..na kuendelea kuupenda ulimwengu?..bado unaendelea kuwa mzinzi, mtukanaji, mlevi, washerati, mvaaji nusu uchi, muwekaji make-up, mvaaji suruali,mpakaji wanja, lipstick, mvaaji mawigi na maherini? bado mtazamaji picha chafu mitandaoni, mfanyaji masturbation na mhudhuriaji disko,mtoaji mimba, bado unaendelea kuishi na mwanamke/mwanamume ambaye hamjaoana n.k?..

Itakuwa ni vizuri kama utamgeukia leo..Yeye atakupokea, na wokovu ni leo na si kesho kwasababu hujui mwisho wako ni lini..Hivyo kama umeamua kuingia na kufanyika mwanawe..unachopaswa kufanya hapo ulipo ni kijitenga binafsi kwa dakika chache peke yako..Kisha piga magoti na nyosha mikono yako juu kuonyesha kuwa umejishusha na umejitambua wewe ni mkosaji..

Halafu anza kutubu kwa kuyakiri makosa yako yote, na yeye atakusamehe..na ukishatubu kwa namna hiyo hakikisha unaacha yale mambo uliyokuwa unayafanya..unaacha uzinzi, unatupa makeup zote, unachoma nguo zote za kikahaba ulizokuwa unavaa, unaacha kwenda bar, unaacha pia kuvuta sigara na kujitenga na makundi yote yanayochochoe hivyo vitu.

Na ukishaacha vyote kwa namna hiyo, toba yako itakuwa thabiti..Hatua inayofuata katafute ubatizo kama hujabatizwa, ubatizo sahihi ni ule wa maji tele (Yohana 3:23), na kwa jina la Yesu Kristo (Matendo 2:3)Na Mungu atakupa uwezo wa ajabu wa kushinda hizo dhambi..haitakuwa ngumu kwako kuishi bila kuzifanya. Na Roho Mtakatifu atakuongoza kufanya yaliyosalia..Na kuzidi kukufundisha umuhimu wa Yesu katika maisha yako na ya watu wengine.

Kumbuka ufalme wake umekaribia..na yeye ajaye aja upesi na wala hatakawia.

Bwana akubariki.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:


Mada Nyinginezo:

MWANA WA MUNGU.

SIRI YA MUNGU.

KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?

KWANINI MUNGU ALITUUMBA WANADAMU.

JE ADAMU ALIKUWA NA KITOVU?

JE ! BWANA YESU ALIKUJA DUNIANI KUAMUA NINI?

Rudi Nyumbani

Print this post

TUMTOLEE MUNGU VILE VINAVYOTUGHARIMU ZAIDI.

Tumtolee Mungu vitu vinavyotugharimu hata kuhatarisha maisha…2Samweli 23:15 Daudi akatamani, akasema, Laiti mtu angeninywesha maji ya kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango!

Shalom, Jina la Bwana Yesu libarikiwe. Ni siku nyingine tumepewa neema ya kuiona, hivyo nakukaribisha tushiriki pamoja kujifunza maneno matakatifu ya Mungu.

Leo kwa ufupi tutaichunguza habari moja inayotoka katika  kitabu kile cha Samweli wa pili, sura ile ya 13, tunaona kuna wakati Daudi alipokuwa katikati ya vita vikali na wafilisti, wakati akiwa kule mafichoni katika pango moja lijulikanalo kama pango la Adulamu, alitamani maji ya Kisima kilichokuwa Bethlehemu Lakini wakati huo  mji wa Bethlehemu ambao ndio ulikuwa mji wa Daudi ulikuwa umezungukwa na wafilisti (Maadui zao), na ndipo walipokuwa wameweka kambi zao hapo.. Hivyo Daudi akiwa kule mabondeni biblia inatuambia alitamani sana maji ya kisima cha Bethelehemu kule maadui zake walipo, Hivyo watatu kati ya wale mashujaa wake 300 aliokuwa nayo waliposikia maneno yale ya Daudi, wao wenyewe kwa sirisiri  wakapanga mikakati ya kwenda kumletea Daudi maji ya kisima kile bila hata ya kumwambia..

Ndipo wakaanza safari kutoka katikati ya kambi ya Daudi, wakaondoka hivyo hivyo bila kujali wanakwenda kuingia katika kambi ya maadui zao, kwasababu ilikuwa ili kufikia Kisima hicho ni lazima upenye katikati ya wafilisti, lakini wao waliondoka hivyo hivyo, hatujui walitumia njama gani, lakini walidhubutu kuhatarisha Maisha yao, kwa hali na mali ili tu wafikie azimio lao, la kuchota maji yale ya Kisima kile na kumletea Daudi..

Halikuwa jambo rahisi ni sawasawa na wewe leo uone umewekewa simba 100 mbele yako, halafu nyuma yao kuna lulu unayopaswa ukaichukue, si jambo rahisi kibinadamu lakini hawa mashujaa watatu wa juu wa Daudi hawakujali hilo, walifanikiwa kweli kupenya katikati ya wale watu kisirisiri, na kuyachota maji yale ya Kisima cha Bethlehemu na kumletea Daudi…Lakini Daudi alipoona Maji yale, tunaona mwitikio wake ulikuwa ni kinyume na matazamio yao..tusome..

2 Samweli 23:13 “Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka, wakamwendea Daudi wakati wa mavuno mpaka pango la Adulamu, na kikosi cha Wafilisti walikuwa wamefanya kambi katika bonde la Warefai.

14 Naye Daudi wakati ule alikuwako ngomeni, na jeshi la Wafilisti wakati ule walikuwako Bethlehemu.

15 Daudi akatamani, akasema, Laiti mtu angeninywesha maji ya kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango!

16 Basi hao mashujaa watatu wakapenya jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi; walakini yeye hakukubali kuyanywa, akayamimina mbele za Bwana.

17 Akasema, Hasha, Bwana, nisifanye hivi; je! Si damu hii ya watu hao waliohatirisha nafsi zao? Kwa hiyo hakukubali kuyanywa”.

“Hayo ndiyo waliyoyafanya wale mashujaa watatu”

Kama tunavyoona hapo, Daudi hakudhubutu kuyanywa maji yake.Kwa nje yalikuwa yanaonekana ni maji lakini kwa ndani Daudi aliyaona ni damu.. Na damu sikuzote huwa hainywewi, kwasababu damu inabeba uhai..Na uhai unazungumza..

Daudi aliona maji yale ni dhabihu tosha ambayo haistahili kutolewa kwake ili kwa Mungu tu peke yake. Na ndio maana alichokifanya ni kuyachukua yale maji na kwenda kuyamwaga mbele za Bwana.. kama vile damu imwagikayo kwa ajili ya dhabihu.

Hivyo tunaona badala maji yale kuenda tumboni mwa Daudi, yalikwenda moja kwa moja hadi katika madhabahu ya Mungu mbinguni..Na hivyo bila shaka kwa tendo lile si tu Mungu kuwarehemu wale watu kwa jicho la tofauti bali pia kuwapa ushindi dhidi ya maadui zao.

Habari hiyo inafunua nini katika agano  jipya tulilopo?

Daudi anamfunua Bwana wetu Yesu Kristo, kumbuka wale mashujaa wa Daudi walikithamini kiu cha Daudi hawakujali kuwa hata pale kulikuwa na maji mengi tu si angekunywa ya pale  kwanini atafute ya mbali, lakini wao hawakujali hilo..na hivyo wakawa tayari kuhatarisha Maisha yao kwa ajili tu ya kuishibisha kiu yake, Hivyo kwa tendo lile ikamfanya Daudi asiyanywe maji yale, bali kwenda kuyamwanga mbele za BWANA.

Kristo naye alipokuwa msalabani alisema ninaona KIU..Lakini wale askari hawakuithamini kiu yake..Vilevile hadi sasa Kristo anasema ninaona kiu, lakini wengi wetu tunaidharau kiu yake tunaona kama anataka kutuau huyu, kutufilisi, yeye si ana kila kitu iweje tena atuombe sisi maji, utasema ni wapi kwenye maandiko Yesu anasema nina kiu..ukisoma Mathayo 25 utaona  anawaambia wale watu aliowafananisha na mbuzi kuwa alikuwa na kiu lakini hawakumnyeshwa, vilevile na wale wengine ambao aliwafananisha na kondoo akiwaambia  nilikuwa nina kiu na mlininywesha..

Ni kweli tunamnywesha kila siku maji kwa matoleo yetu, lakini Je! Maji hayo tunaweza kuyageuza kuwa Damu?. Kiasi kwamba ashindwe kuyanywa na kuyamwaga mbele za Mungu mbinguni kama dhabihu?

Kristo anatazamia, tumtolee kilicho bora, bila kujali inatugharimu kiasi gani..bila kujali tutapoteza nini, au tunapata hasara kiasi gani baada ya hiki, na hiyo yote ni kwa faida yetu sisi wenyewe (anataka tumtolee Mungu vile vinavyotugharimu)….Na kwa kufanya hivyo..haitamfikia tena kama maji yakatayo kiu,.. bali sadaka yako itamfikia kama DAMU..kama uhai wako mwenyewe..

Ukiingia  gharama kubwa kumpa Kristo kitu Fulani  jambo ambalo mtu wa kawaida hawezi kufanya, ..mbinguni unahesabika ni kama umemwaga damu yako kwa ajili yake..Haijalishi hicho kitu ni kidogo kiasi gani, kinachojalisha ni gharama uliyoingia. Je ni kubwa kiasi gani..mbele za Mungu, Yule mwanamke aliyekuwa mjane, aliingia gharama kubwa kutoa kila alichonacho ingawa kwa nje ilikuwa ni senti mbili tu.

Mtu anayefanya hivyo  anapata thawabu kama tu aliyechinjwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu. Hivyo tumtolee Mungu vile vinavyotugharimu Zaidi. Ili tuvuke hata kiwango vya baraka tu za kimwilini bali mpaka zile za mashahidi wa Yesu.

Tumtolee Mungu wetu kwa wingi, naye atatujaza kwa vingi.

Shalom.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengin

Mafundisho mengine:

Tafadhali Share ujumbe huu na kwa wengine.


Mada Nyinginezo:

https://wingulamashahidi.org/2019/09/01/tofauti-katika-ya-zaka-na-sadaka-ni-ipi/

SADAKA YA MALIMBUKO.

HALI ZETU JINSI ZINAVYOWEZA KUATHIRI UTOAJI WETU.

INJILI YA KRISTO HAITANGAZWI KWA HATI MILIKI.

UWEPO WA BWANA HATA KATIKATI YA MATESO.

Biblia inamaana gani kusema;aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi?

Rudi Nyumbani:

Print this post

URIMU NA THUMIMU NI NINI KATIKA BIBLIA?

Urimu na thumimu ni nini?


Katika Agano la kale Mungu alikuwa akitumia njia kuu tatu aidha kuwasilisha  ujumbe au leta majibu au kuthibitisha jambo..Njia ya kwanza ni manabii, njia ya pili ni ndoto, na njia ya tatu ni Urimu na thumimu.

Tunalithibitisha hilo katika kitabu cha 1Samweli 28:4  pale ambapo Mfalme Sauli alipokwenda kuuliza kwa Bwana kuhusu vita iliyokuwa inamkabili mbele yake dhidi ya wafilisti, Kama watashinda au La, lakini Bwana hakumjibu kwa njia yoyote kati ya hizo tatu..

1Samweli 28:4 “Nao Wafilisti wakakusanyika, wakaenda kufanya kambi huko Shunemu; naye Sauli akawakusanya Waisraeli wote, nao wakapiga hema katika Gilboa. 

5 Basi alipowaona hao majeshi ya Wafilisti, huyo Sauli akaogopa, na moyo wake ukatetemeka sana. 

6 Lakini Sauli alipouliza kwa Bwana, Bwana hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii”.

URIMU NA THUMIMU maana yake nini nini?

Urimu maana yake ni “Mianga” Na Thumimu “mikamilifu”..Haya Ni mawe 12 ya aina tofauti tofauti yaliyokuwa yamegundishwa katika ki-mfuko kidogo kilichokuwa kinakaa katika kifua cha kuhani mkuu. Hivyo ikiwa kuna jambo watu wanahitaji kupata uhakika kutoka kwa Bwana basi Mawe haya yalikuwa yanatoa mwanga Fulani unaoakisiana, kuthibitisha jambo hilo, Na hivyo kama jambo hilo sio sawa basi hayakutoa mwanga wowote. Urimu na Thimumu ilikuwa inatoa jibu la mwisho japo si mara zote ilikuwa inatumika.

Kwa mara ya kwanza urimu na thumimu inaonekana katika kitabu cha Kutoka 28:29-30

29 Na Haruni atayachukua majina ya wana wa Israeli katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu juu ya moyo wake, hapo atakapoingia ndani ya mahali patakatifu, kuwa ukumbusho mbele ya Bwana daima. 

30 Nawe utie hizo Urimu na Thumimu katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu; nazo zitakuwa juu ya moyo wa Haruni, hapo atakapoingia ndani mbele ya Bwana; na Haruni atachukua hukumu ya hao wana wa Israeli juu ya moyo wake mbele ya Bwana daima.

Soma tena..

Walawi 8:6 Basi Musa akawaleta Haruni na wanawe, akawaosha kwa maji. 

7 Kisha akamvika Haruni ile kanzu, na kumfunga mshipi, na kumvika joho, na kumvika naivera, na kumfunga huo mshipi wa kazi ya mstadi wa naivera na kumfunga naivera kwa huo mshipi. 

8 Kisha akamtia kile kifuko cha kifuani; akatia hizo Urimu na Thumimu katika hicho kifuko cha kifuani. 

9 Akamvika na kile kilemba kichwani mwake; na juu ya kilemba, upande wa mbele, akakitia kile kipande cha dhahabu, hiyo taji takatifu; kama Bwana alivyomwagiza Musa.

Ukipata tena nafasi Soma  Kumbukumbu 33:8, Hesabu 27:21..

Tunaona tena, wakati mfalme Sauli alipopishana na mwanawe kuhusu kuvunjwa viapo ambavyo alivyoweka, alitaka Mungu ahukumu katikati yao ni nani mwenye makosa, Hivyo alitumia Urimu na Thumimu kuomba uthibitisho huo.

1Samweli 14:41 “Kwa hiyo Sauli akamwambia Bwana, Mungu wa Israeli, [Kwani usimjibu mtumishi wako leo? Ikiwa dhambi i ndani yangu, au ndani yake Yonathani mwanangu, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, utoe Urimu; bali ukisema hivi, Dhambi i katika watu wako Israeli,] utoe Thumimu ,Basi Yonathani na Sauli wakatwaliwa,lakini watu wakapona”.

JE! URIMU NA THUMIMU iliendelea kudumu muda wote?

Wakati wana wa Israeli wanachukuliwa tena utumwani Babeli, na hekalu la Mungu kubomolewa, ndio ilikuwa mwisho wa kutumika kwa urimu na thumimu. Hata waliporudi na kujenga upya nyumba ya Bwana, kitendo hicho hakikuonekana kikitendekea tena katikati ya makuhani.

KATIKA AGANO JIPYA URIMU NA THUMUMI NI NINI?

Kama vile ilivyokuwa katika agano la kale, ili kuthitisha jambo ilikuwa ni lazima mawe yale yatoe mwangaza Fulani wa tofuati, vivyo hivyo katika agano jipya Urimu na thumimu yetu ni BIBLIA TAKATIFU. Kila Neno, kila ndoto au kila unabii, kabla haujapokelewa au kuaminiwa ni lazima kwanza uletwe kwenye biblia ambayo ndio Urimu na Thumimu yetu..Na unabii huo au ndoto hiyo kama haipatani na maandiko basi tunapaswa tuukate ufunuo huo haijalishi utaonekana unao uhalisia mkubwa kiasi gani.

Katika nyakati hizi za mwisho shetani anabuni njama mpya za kuwadanganya watu kila siku kwa kivuli cha Neno Ufunuo..Kila mmoja anasema nimefunuliwa..hata jambo ambalo linaonekana linakiuka misingi ya Imani ya kikristo mtu anasema amefunuliwa.. Ni kweli tunayahitaji mafunuo ili tuyaelewe maandiko, lakini kila ufunuo  ili ukubalike ni lazima upatane na Urimu na Thumimu yetu ambayo ni biblia.

Upotashaji uliopo.

Lakini utajiuliza mbona, nabii yule alipokutabiria hivi au vile ni kweli vilitokea kama vilivyo na leo  hii kakupa tena maagizo mengine uachane na mume wako au mke wako ukaoane na mwingine..Nataka nikuambie kama Neno la Mungu likiwa halijakaa vizuri ndani yako unaweza kumsikiliza ukadhani kuwa ni maagizo ya Mungu, ukamwacha mke wako ukaenda kuoa mwingine au kuoelewa na mwingine, kisa tu nabii kasema, na kisa tu alishakutabiria kipindi cha nyuma na jambo Fulani likawa ni kweli..

Lakini wewe kwa kukosa ufahamu wa kimaandiko, hujui kuwa unakwenda kuishi katika uzinzi, umeshachukuliwa na maji, kwasababu biblia inasema mtu amwachae mke wake na kwenda kuoelewa na mwingine azini..

Marko 10:11  “Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake;

12  na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini”.

Ndugu yangu embu soma maandiko haya upate picha halisi ya kitu  ninachokuambia..

KUMBU: MLANGO 13

1 Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, 

2 ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; 

3 wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. 

4 Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye. 

5 Na yule nabii, au yule mwotaji wa ndoto, na auawe, kwa kuwa amesema yaliyopotoka juu ya Bwana, Mungu wenu, aliyewatoa katika nchi ya Misri, akakukomboa katika nyumba ya utumwa, apate yule mtu kukupotoa katika njia aliyokuamuru Bwana, Mungu wako, uiendee. Ndivyo utakavyouondoa uovu utoke katikati yako. 

Unaona? Tunapaswa kabla ya kupokea Neno lolote au unabii wowote, tuutazame je unakubaliwa na Urimu na thumimu yetu (yaani biblia) au La. Tukizingatia hayo tutakuwa tumejiweka katika nafasi nzuri ya kuzishinda kirahisi hila za shetani katika nyakati hizi za mwisho ambazo anazileta kupitia   manabii wake na walimu wake wa uongo, katika siku hizi za mwisho. Mfano tena mtu anaweza akaja akakwambia kata mti huu au ule, unasababisha vifo vya wababa katika familia au ngo’a ua hili au lile, linatunza majini, au usifuge paka, au njiwa wanatumiwa na wachawi n.k. .

Mafundisho ya uongo.

Yote hayo ni mafundisho au mafunuo yaliyotoka kuzimu ambayo hayana msingi wowote wa kimaandiko, Zaidi tu yanawafanya watu waishi Maisha ya woga na wasiwasi wakidhani kuwa vitu vya nje vinaweza kuathiri Maisha yao rohoni, na kusahau kuwa asili ya laana zote zipo rohoni pale mtu anapokuwa mbali na muumba wake, anapotenda dhambi ndipo anapokumbana na laana. Na mafunuo mengine mengi ya namna hiyo..

Leo hii umeshaijua urimu na thumimu yako(BIBLIA), Hivyo jambo lolote linapokujia lipime kwanza na maandiko.

Je! Umeokoka? Je unafahamu kuwa tunaishi katika kizazi ambacho dalili zote zinaonyesha kuwa tutashuhudia tukio la kurudi kwa pili kwa YESU KRISTO?. Je! Una habari kuwa hili ndio kanisa la saba na la  mwisho lijulikanalo kama LAODIKIA tunaloishi(Ufunuo 3), na baada ya hili hakutakuwa na kanisa lingine mbeleni. Je! Unataarifa kuwa Israeli imeshachipuka, na hii neema siku si nyingine itarudi kwao na ikisharudi kule, upande wetu mlango wa neema utakuwa umeshafungwa?

Unaona tupo katika hatari kubwa kiasi gani..Unasubiri nini usiokoke..Usimpe Kristo Maisha yako.. Huu ulimwengu umekupa faida gani tangu uanze kutaabika nao, Lakini Kristo anakuahidi amani idumuyo isitoshe anakupa na uzima wa milele juu.. Hakuna mwanadamu yoyote anaweza kukuahidia mambo mazuri kama hayo.

Yeye mwenyewe anasema..

Mathayo 11:28  “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29  Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30  kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”

Unaona? Amekuahidi mizigo yako yote ataitua, yeye hasemi uongo, ukiwa utakuwa tayari tu kumpokea muda huo huo anaanza kufanya kazi ndani yako ya kukugeuza..Hivyo usifanya moyo wako kuwa mgumu, chukua uamuzi huo sasa..

Kama upo tayari kufanya hivyo kumpa Bwana Maisha yako…

Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU  MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Na Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Zingatia hayo na Bwana atakuwa pamoja nawe. Vilevile Usiacha kutembelea Website hii  https://wingulamashahidi.org mara kwa mara ili ujifunze maneno ya uzima..

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:

Mada Nyinginezo:

KUFUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE?

Zile tunu (Dhahabu, uvumba na manemane) Mamajusi walizozitoa kwa Bwana (Mathayo 2) . ziliwakilisha nini?

Je! sisi ni wafalme na makuhani kwa namna gani?

USIPOKUWA MWAMINIFU, NAFASI YAKO ITACHUKULIWA.

UNAMALIZAJE MWAKA WAKO, JE NA MUNGU AU SHETANI?

USIWE NA HAKI KUPITA KIASI.

UNYAKUO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

USIPOKUWA MWAMINIFU, NAFASI YAKO ITACHUKULIWA.

Usipokuwa mwaminifu sasa, nafasi yako itachukuliwa na mtu mwingine.


Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, Mkuu wa Uzima libarikiwe. Karibu tujifunze Biblia Neno la Mungu..Taa iongozayo miguu yetu na mwanga wa njia zetu.

Leo tutajifunza madhara ya kutokuwa mwaminifu katika kazi ya Mungu… Kuna tofauti ya utendaji kazi kati ya mtu na mtu…Mtu anatenda kazi ya Mungu kulingana na karama aliyopewa. Hivyo kama mtu kapewa karama Fulani halafu karama ile haitumii au anaitumia isivyopaswa basi kuna madhara makubwa sana…Na moja ya dhara hilo ni nafasi yake kunyang’anywa na kupewa mwingine.

Na kitu cha kuogopesha ambacho watu wengi hawakifahamu ni kwamba Mungu kamwe hamnyang’anyi mtu karama…bali anamnyang’anya ile huduma…Yaani ile Neema ambayo Mungu angetembea naye kwa karama aliyompa..Neema hiyo anapewa mwingine ambaye atazaa Zaidi lakini yule mtu ataendelea kukaa na karama yake ile ile lakini hatatumika katika viwango ambavyo Mungu alikuwa amemkusudia atumike. Kama alikuwa na karama ya kinabii..ataendelea kuona maono..Lakini lile kusudi kuu ambalo Mungu alilikusudia kumtumia kwa karama ile linahamishiwa kwa mtu mwingine.

Katika Biblia tunamwona mtu mmoja aliyeitwa SAULI ambaye alipakwa mafuta na Mungu mwenyewe, na Roho wa Mungu akamshukia juu yake kwa nguvu ile awe mtawala juu ya Israeli. Lakini pamoja na kuwa alitiwa mafuta na Mungu mwenyewe na Mungu alimnyanyua kutoka chini, na kupewa uweza na nguvu nyingi..lakini mtu yule hakuitumia vyema nafasi yake, aliacha kumheshimu Mungu na kumtii…Mungu akimwambia afanye hivi..yeye anafanya vile..na kile asichopaswa kukifanya ndicho alichokuwa anakifanya, na alikuwa anafanya vile kwa makusudi. Jambo ambalo lilimhuzunisha Mungu na kufikia hatua ya kuondoa nafasi yake na kumpa mtu mwingine.

1Samweli 15:24 “Ndipo Sauli akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi; maana nimeihalifu amri ya Bwana, pia na maneno yako; kwa sababu naliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao.

25 Basi sasa, nakuomba, unisamehe dhambi yangu; rudi pamoja nami, nipate kumwabudu Bwana.

26 Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la Bwana, Bwana naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli.

27 Naye Samweli alipogeuka, aende zake, Sauli akaushika upindo wa vazi lake, nalo likararuka.

28 Basi Samweli akamwambia, Leo Bwana amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko wewe.

29 Tena Yeye aliye Nguvu za Israeli hatanena uongo, wala hataona majuto; maana siye mwanadamu, hata ajute”.

Wakati Sauli anaidharau hiyo nafasi aliyowekwa..Tayari Mungu alikuwa ameshamwandaa Daudi kuichukua nafasi yake.

Sulemani naye baada ya kutumika kwa muda mrefu..ilifika kipindi akakengeuka na kuitumikia miungu migeni jambo ambalo ni kinyume na maagizo ya Mungu..Nafasi yake naye ikachukuliwa na mtumishi wake.

1Wafalme 11:11 “Kwa hiyo Bwana akamwambia Sulemani, Kwa kuwa umefanya hayo, wala hukuyashika maagano yangu, na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme usiwe wako, nami nitampa mtumishi wako”.

Na ipo mifano mingine mingi katika biblia..lakini wa mwisho tunausoma ni wa Yuda aliyekuwa mwanafunzi wa Yesu. Huyu naye alipewa nafasi katika huduma ya Kristo..lakini aliichezea na kuidharau nafasi ile..na mwishowe kufungua mlango wa roho ya shetani kumwingia ili kumsaliti Bwana..Na siku zote kazi ya Mungu haipwayi..

Wala hakuna mtu maalum kwa Mungu..ukikataa kumtumikia Mungu sasa..basi Mungu anao watu wengi, nafasi yako inachukuliwa na mtu mwingine…Yeye hana mtu mmoja tu au watu Fulani kadhaa anaowategemea kwamba wakikosekana hao basi kazi yake haiendi mbele. Nataka nikuambie hata Paulo angeukataa wito wa Mungu angenyanyuka mtu mwingine kuifanya kazi kama ile ile ya Paulo kwa wakati ule ule..Lakini Paulo na wengine wamekuwa vile walivyo kwasababu waliutii utumishi wa Mungu na kuuheshimu.

Matendo 1:15 “Siku zile akasimama Petro kati ya hao ndugu (jumla ya majina ilipata mia na ishirini), akasema,

16 Ndugu, ilipasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daudi, katika habari za Yuda aliyewaongoza wao waliomkamata Yesu;

17 kwa sababu alikuwa amehesabiwa pamoja na sisi, akapata sehemu ya huduma hii.

18 (Basi mtu huyu alinunua konde kwa ijara ya udhalimu; akaanguka kwa kasi akapasuka matumbo yake yote yakatoka………20 Kwa maana imeandikwa katika chuo cha Zaburi, Kikao chake na kiwe ukiwa, Wala asiwepo mtu mwenye kukaa humo;

21 Basi katika watu waliofuatana nasi wakati wote Bwana Yesu alipokuwa akiingia na kutoka kwetu,

22 kuanza tangu ubatizo wa Yohana, hata siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu, inapasa mmoja wao awe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi.

23 Wakaweka wawili, Yusufu, aitwaye Barsaba aliyekuwa na jina la pili Yusto, na Mathiya.

24 Kisha wakaomba, wakasema, Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili,

25 ashike mahali katika huduma hii na utume huu, alioukosa Yuda, aende zake mahali pake mwenyewe. 26 Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja.”

Umeona?..Mungu hakufanya kazi ya hasara…kumbe wakati Yuda anaanza kufikiria kumsaliti Bwana..Tayari Mungu alikuwa ameshaandaa mtu wa kuichukua nafasi yake tangu wakati ule ule…Huyu Mathiya alikuwa na Yesu tangu ubatizo wa Yohana mpaka kupaa kwake…alikuwa ameshawekwa tayari kuichukua nafasi ya Yuda.

Hata sisi leo hii, wapo watu waliowekwa tayari kuzichukua nafasi zetu, tangu siku ile tulipookoka..Tunapozichezea hizi nafasi tulizopewa sasa katika kumtumikia Mungu, katika kuhubiri injili, katika kuihudumia Injili..Siku inafika kinara kitaondolewa na kupewa mwingine ambaye tayari alikuwa ameshaandaliwa.

Mifano hiyo tuliyojifunza ni ya kwenye biblia..lakini tunaweza kujifunza mfano mwingine katika mtu wa nyakati zetu..Na huyu si mwingine ya Mhubiri wa Mungu mashuhuri Reinhard Bonnke…ambaye wengi wetu tunamfahamu, ambaye wiki kadhaa nyuma tulisikia habari za kufariki kwake. Huyu mwanzoni mwa huduma yake kabla hajaingia kwenye kazi ya kuwavuna mamilioni ya watu kwa Kristo, alikuwa anasua sua kidogo. Mungu anamwita kufanya kazi ya kupeleka injili kwa mataifa ya Afrika ili mamilioni waokolewe..lakini yeye akawa anakawia kawia na kujishauri shauri kana kwamba yeye ni mtu maalumu sana.

Wakati bado yupo anajifikiria fikiria, siku moja alisikia sauti inamwambia “nafasi hiyo nimekupa kwasababu kuna mwingine alipewa akaikataa, na wewe ukiikataa atapewa mtu mwingine”. Baada ya kusikia hivyo aliogopa sana..Ndipo akaamua kwa gharama zote kuifanya kazi ya Mungu ili nafasi yake isichukuliwe na mwingine..Na matokeo ya kutii kwake ndiyo tunayoyaona leo,..Mungu alimtumia kuvuna mamilioni ya watu Afrika waliokuwa wanakwenda kuzimu.

Hivyo na sisi tunajifunza..Kamwe tusijione ni watu maalum mbele za Mungu. Kamwe tusijidhanie ni sisi tu ndio Mungu anao..Mungu anao watu wake wengi, ambao wapo tayari kwa utumishi wake..Eliya Mtishbi kuna kipindi alikwenda kusimama mbele za Mungu na kumwambia.. “Ni mimi tu peke yangu nimebaki nabii wako” ..lakini Mungu alimwambiaje?

Warumi 11: 3 “Bwana, wamewaua manabii wako, wamezibomoa madhabahu zako, nami nimesalia peke yangu, nao wananitafuta roho yangu.

4 Lakini ile jawabu ya Mungu yamwambiaje? Nimejisazia watu elfu saba wasiopiga goti mbele ya Baali”.

Leo hii unajiona una kipawa cha kuimba..Wewe ukiimba watu wanatubu, lakini unavaa vimini, unapiga make-up, unavaa nusu uchi, ni mwasherati kwa sirisiri..umeonywa mara kadhaa lakini hutaki kusikia…Nataka nikuambie kamwe usijifikirie upo peke yako..Nafasi yako atapewa mtu mwingine.

Wewe ni Mchungaji, au Mwalimu, au Nabii au Mtume au Mhubiri…lakini chini kwa chini ni mwasherati, chini kwa chini ni unalivuruga kundi, chini kwa chini ni mtu wa kupenda anasa na mapato ya udhalimu, chini kwa chini ni mzinzi..unadhani Mungu hakuoni..Utamficha mwanadamu lakini si Mungu…Nafasi yako itachukuliwa na mwingine na pengine hata imeshachukuliwa hujui tu!..Unaweza ukawa bado unaendelea kuota ndoto, unaendelea kuona maono, unaendelea kuimba vizuri hiyo siyo hoja!…

Hata Sulemani aliponyang’anywa ufalme wake hakuondolewa kila kitu alibakishiwa hekima yake…hata Sauli aliponyang’anywa ufalme wake hakupokonywa siku hiyo hiyo alikufa akiwa mfalme, lakini kumbe tayari utukufu wa Mungu ulikuwa umeshamwondokea…Hata Yuda nia ya kumsaliti ilipoingia ndani yake Bwana hakumfukuza aliendelea kutembea naye lakini, utukufu ulikuwa tayari umeshamwondoka na siku ya mwisho alipasuka matumbo.

Hivyo sikia maonyo ya Mungu leo mtu wa Mungu, na Bwana azidi kutusaidia tudumu katika Neema yake kithabiti. Tukikumbuka kuwa muda tuliona nao ni mchache..Kristo yu malangoni kurudi.

Bwana akubariki.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:

Mada Nyinginezo:

TUZO UTAPEWA KULINGANA NA NAFASI YAKO.

UNAMALIZAJE MWAKA WAKO, JE NA MUNGU AU SHETANI?

NI KIPI MUNGU ANACHOKITAZAMA ZAIDI, MOYO AU MWILI?

JUMA LA SABINI (70) LA DANIELI

MPINGA-KRISTO

UNYAKUO.

JE! UNA MASIKIO YANAYOSIKIA?

Rudi Nyumbani:

Print this post

UNAMALIZAJE MWAKA WAKO, JE NA MUNGU AU SHETANI?

Unamalizaje mwaka wako?.Unamtukazaje Mungu katika sikukuu hizi na mwisho wa mwaka wako?


Ilikuwa ni Disemba 24, 1964, jaribio la kwanza la wanasayansi la kusafiri kutoka katika obiti (muhimili) wa dunia na kuelekea katika obiti ya mwezi..Ni jaribio ambalo lilikuwa ni la kwanza na la hatari sana, kiasi kwamba ingetokea tu injini moja ya chombo cha wana anga hao kufeli basi watu hao ndio wangepotea milele katika anga za mbali..

Tukio hilo la kuondoka kwao lilishuhudiwa na dunia nzima siku hiyo, watu wakiwa na shauku ya kuona ni nini kitatokea, katika ziara hiyo ya masafa ya mbali ya anga, vyombo vyote vya habari vilikuwa wazi na televisheni zote wakizungumzia safari hiyo ambayo ilichukua takribani siku tatu kuifikia orbit ya mwezi,..Sasa wana anga hao wakiwa tayari wameshaingia katika obiti ya mwezi wakijiandaa kuizunguka mara 10 Wakiwa kule angani kuchukua picha za matukio kitendo cha kuishuhudia “Dunia kunyanyuka”..Sio “Mwezi kunyanyuka” kama tulivyozea huku kuona mwezi ukinyanyuka kutoka mashariki mpaka kufika angani..Wao walifika hatua hiyo ya kushuhudia na kuchukua video ambayo ipo mitandaoni hadi leo jinsi dunia inavyoonekana kwa mbali ikinyanyuka kutoka katika pembe za mwezi hadi juu kama vile mwezi unavyonyanyuka kutoka katika pembe za dunia..

Lakini sasa wana anga wale 3, wakiwa wanajiandaa kutoa ripoti hiyo..Walikatisha matangazo yao..wakiwa sasa kule kule angani wakaiambia Dunia maneno haya..

Nukuu.

“Wakati tunakaribia kushuhudia tukio hili kuu, timu yetu ya Apollo 8 tunao ujumbe tunataka tuwaambie watu wote mlio katika dunia.. Na ujumbe wenyewe ndio huu..

1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.

2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.

4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza.

5 Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.

6 Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji.

7 Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo. 8 Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili.

9 Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo.

10 Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.”

Walipomaliza kuisoma mistari hiyo ya kitabu cha Mwanzo 1:1-10 wote watatu, walifunga biblia zao kwa kusema maneno haya:

“Sisi kama timu ya Apollo 8, tunamalizia kwa kuwaambia muwe na usiku mwema, wenye amani, na Heri ya krisimasi, Mungu awabariki wote, wote mlio katika dunia nzuri.”

Mwisho wa Nukuu.

Ikiwa utapenda kusikia audio hiyo basi bofya link hii.>>

Maneno hayo yaliugusa moyo wa ulimwengu mzima kwa wakati ule.. Na kuwafanya watu wengi, wajifikirie mara mbili juu ya Maisha yao ya rohoni, ikiwa wanasayansi wanaukiri utukufu wa Mungu wakiwa maelfu ya kilometa mbali na dunia..Inatupasaje sisi?..

Watu wale waliporudi salama duniani, Habari zao zikavuma sana, ndio waliowekwa kuwa watu wa mwaka kipindi hicho..

Kama hiyo haitoshi mwaka mmoja baadaye..timu nyingine ya wanasayansi wa anga (Astronauts) iliyojulikana kama Apollo 11,nayo ya watu watatu, ilifunga safari nyingine tena, lakini awamu hii sio kama ile ya kwanza ya kuuzunguka mwezi, bali hii ilikuwa ni kutua kabisa mwezini kwa mara ya kwanza..

Safari ilianza July 20, 1969 na ilipofikia July 21 walikuwa wameshafika katika uso wa mwezi..muda mchache tu baada ya kutua, mmojawapo kati ya wale watatu aliitoa divai yake na mkate wake, aliyoichua kutoka kanisani mwao..akamwomba kamanda wake wasitishe matangazo yote kwa muda, jambo lisilo la kawaida aliashiriki meza ya Bwana akiwa kule mwezini..Na alipomaliza aliomba wasikilizaji wake wote duniani wasikilize anachowaambia..

Akausoma mstari huu kwa nguvu dunia nzima ikiwa inasikia..

Yohana 15:5 “Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote”.

Akafunga biblia yake..wakaendelea na shughuli za kule mwenzi Na Walipomaliza shughuli zao baada ya masaa kadhaa, wakawasha chombo chao, wakaondoka..Sasa akiwa wanauacha mwezi, huku wakiangalia magimba ya ajabu Mungu aliyoyaumba angani..huyu mwanaanga aliyeitwa Buzz Aldrin.

Akaifungua tena biblia yake, akasema ninao ujumbe bado kwa dunia yote…huku mamilioni ya watu duniani wakiwasikiliza akasoma tena mstari huu..

Zaburi 8:3 “Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha;

4 Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie”

Haleluya!!..Kama ilivyo ada maneno hayo yaliigusa mioyo ya watu wengi duniani..wakisema ikiwa watu hawa wanafanikiwa katika mambo makubwa kama haya, Lakini bado hawaachi kuitangaza mauti ya Kristo, na utukufu wa Mungu..Inatupasaje sisi ambao hatujafika popote?

Kama ulikuwa hujui hawa ndio waliokuwa wanadamu wa kwanza na wa mwisho kutua mwezini..Lakini katika mafanikio yao hawakuacha kumtukuza Mungu..hawakuacha kuyatimiza maagizo Kristo aliyowapa kama wakristo pasipo kujali hali na mazingira..

Embu tujiulize Watu kama hawa Mungu ataachaje kuwafikisha mbali ikiwa wanaiadhimisha Krisimasi yao kwa kuutangaza utukufu wa Mungu, wanafunga mwaka kwa kuubariki uumbaji wa Mungu..

Hata wakiwa mwezini mahali ambapo hapana oxyjeni, kusikoweza kuishi kiumbe chochote mkristo huyu haachi kuishiriki meza ya Bwana, wanaithamini damu ya Emanueli iliyomwagika pale Kalvari kwa ajili yao miaka 2000 iliyopita..Na sisi Je tutapate kupona tusipouthamini wokovu mkuu namna hii..

Wewe na mimi hatujawahi kufika mwezini, hatujawahi kuona hata mambo makubwa na ya kustaajabisha, wala hatuna elimu ya juu na utajiri wa kuwafikia watu hawa na taifa lao, ambao kimsingi ndio wangepaswa wawe wakwanza kusema hakuna Mungu lakini kinyume chake katika mafanikio yao ndio wanaokuwa wa kwanza kumuhubiri Kristo..

biblia inatuambia…

Waebrania 12:1 “Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,

2 tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu..”

Na wewe Je! Bado unafikiria kuumaliza mwaka wako bar, au guest? Au Disko? Au Casino? Au kwenye kumbi za starehe?…Kumbuka hawa ndio watakaotuhukumu siku ile.. Ni heri ukaufunga mwaka wako kwa Bwana na kusema kuanzia leo nimeamua kumfuata Kristo kwa moyo wangu wote.

Ukifanya hivyo kwa kumaanisha kabisa, atakupokea, ameahidi hivyo katika Neno lake kuwa yeyote aendaye kwake hatamtupa nje kamwe..(Yohana 6:37).Na yeye si mwongo mwongo kama sisi.

Unasubiri Nini tubu leo dhambi zako kabla ya kuingia mwaka huu mpya..Ukabatizwe katika ubatizo wa kimaandiko wa kuzamishwa katika maji mengi kwa jina la YESU KRISTO upate ondoleo la dhambi zako, kisha Bwana akupe kipawa cha Roho wake Mtakatifu kukulinda na kukuongoza hadi siku ile ya mwisho wa Maisha yako kama unyakuo utakuwa haujapita..Usisieme mimi ni wa dini hii, au ile hivyo siwezi kuwa mkristo, wala usiseme mimi dhehebu langu ni hili, hivyo siwezi kuokoka..Wokovu ni mlango wa wazi kwa watu wote..na wokovu ni wa lazima! Kama tunapenda maisha.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:

Shalom.

Mada Nyinginezo:

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

SAA YA KIAMA.

CHAPA YA MNYAMA

SIKU YA TAABU YA YAKOBO.

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.

ZIFAHAMU NAMBA KATIKA BIBLIA NA MAANA ZAKE.

Rudi Nyumbani:

Print this post

JIEPUSHE NA MASHINDANO YA DINI.

Shalom.Karibu tujifunze Biblia..Neno la Mungu linasema katika 1Timotheo 6:20 “ Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na maneno yasiyo ya dini, yasiyo na maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa uongo”.

Moja ya vitu vinavyobomoa Imani au vinavyomharibu mtu au vinavyoharibu huduma ni mashindano ya dini. Aina yoyote ya mashindano ya dini yanaasisiwa na shetani mwenyewe.

Na chanzo kikubwa cha mashindano ya dini ni Ujuzi wa mambo Fulani. Inapotokea mtu anafahamu kitu Fulani ambacho anahisi mwingine hajakifahamu au anahisi mwingine hafanyi kama inavyostahili….Mtu huyu Ule ujuzi unaweza kumletea kiburi na ni rahisi kuzaa majivuno na mwishowe mashindano..

Biblia inasema hivyo katika 1Wakorintho 8:1 “… Twajua ya kuwa sisi sote tuna ujuzi. Ujuzi huleta majivuno, bali upendo hujenga”.

Baadhi ya mashindano hayo ambayo yametengenezwa na shetani mwenyewe katika hizi siku za mwisho ni haya.

  • Mashindano kati ya uislamu na ukristo.
  • Mashindano ya Yesu ni Mungu au si Mungu
  • Mashindano ya kushindania siku ya kuabudu kama ni jumapili, au jumamosi
  • Mashindano ya kula nyama ya nguruwe n.k
  • Mashindano ya dhehebu la kweli la kuabudu.

Yapo mengi lakini hayo ndiyo yanayoshika nafasi za juu..Utakuta watu wanabishana tangu asubuhi mpaka jioni kila mmoja akitaka kumthibitishia mwenzake kwamba yupo sahihi na kwamba yeye anajua Zaidi.

Sasa kama ukichunguza mwisho wa mabishano hayo ni magombano au kutukanana au kudhihakiana au kuwekeana vinyongo au kupigana au Kuumizana au kuaibishana… Na mabishano hayo huwa hayaishagi..utaona yametulia tu kidogo baada ya masaa kadhaa au hata siku kadhaa yanaanza tena..kila mmoja kaenda kukusanya point zake mpya huko alikokwenda..na anarudi kwenye uwanja wa mapambano upya!..na mashindano yanaanza tena.

Kamwe hutaona katika hayo mazungumzo pamoja na point zao zote wanazozitoa na kukosoana..hutaona hata mtu akitubu, hutaona mtu akigeuka na kusema asante Bwana kwa kunifumbua macho!..hutaona mtu akitoka na moyo wa furaha na upendo na uchangamfu!.. Sasa ikiwa kama matunda ya Roho hayapatikani katikati ya hayo mazungumzo unategemea vipi yawe mazungumzo ya ki-Mungu?..Ni wazi kuwa ni mazungumzo ya kishetani…kwasababu mazungumzo ya kishetani ndiyo yanayozaa hasira, vinyongo, chuki, wivu, matusi, dhihaka, kuaibishana n.k

Biblia imetuonya sehemu kadha wa kadha juu ya mashindano ya dini..kwamba tuyaepuke..

2Timotheo 2:14 “Uwakumbushe mambo hayo, ukiwaonya machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya maneno, ambayo hayana faida, bali huwaharibu wasikiao”.

Sasa swali linakuja… kama je! Unafahamu jambo ambalo unaamini ni sahihi na unataka kumshirikisha mtu asiyelijua na unapoanza tu kumshirikisha anaanza kushindana na wewe..katika hali hiyo unafanyaje?.

Jibu: Unapokutana na mtu ambaye unapomweleza ukweli hataki kusikia, jambo la kwanza yeye ni kupinga na kutaka kuleta mashindano..katika hali kama hiyo wewe unayemhubiria unahitaji kuwa na hekima..Hapo unapaswa ujishushe uwe mpole…Hakuna mtu asiyempenda mtu mpole au anayejishusha!..Unaanza kumweleza kwa upole na kwa utaratibu…Yule mtu akiona upole wako na utaratibu wako, akiona amekutupia tusi umenyamaza hujamrudishia..amekulaani umetulia kimya…hawezi kuendelea kukutukana wala kukupazia sauti, anapoona hakuna muitikio upande wa pili..hivyo atatulia na kukusikiliza..na moyoni atajua kuwa wewe hujaja kushindana naye bali umekuja kumfundisha..hivyo atakuheshimu, hata kama hatakubaliana na wewe katika baadhi ya points lakini hatashindana na wewe!…

Sasa taratibu ataanza kukusikiliza na Roho wa Mungu atamshuhudia ndani yake kwamba unayoyasema ni kweli…hata kama hatayakiri hapo mbele yako lakini baadaye atakapokwenda kutafakari atagundua kuwa ni kweli.

Lakini pale tu unapokutana naye na kuanza kujionyesha kwamba wewe unajua Zaidi yake, na anapotoa maneno ya kutukana unachokiamini na wewe unatukana anachokiamini, anapokurushia mshale na wewe unajibu mapigo kwa kutumia mistari..hapo tayari utakuwa umeshawasha moto wa mashindano na kamwe hamtafikia suluhu..ataishia kusema wewe ni mbishi na hujui lolote, hata kama unachozungumza kina ukweli kiasi gani.

1Petro 3:15 “Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu”.

Mungu hawezi kamwe kuwepo mahali penye machafuko kama Neno lake linavyosema katika..1 Wakorintho 14: 33 “Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu”. Hivyo katika kuhubiri au kushuhudia au kumshirikisha mtu jambo Fulani ni lazima pawepo na hali ya utulivu ndipo Roho Mtakatifu aweze kuwepo katikati yetu kutuhudumia.

Na Zaidi ya hayo, wapo watu ambao wamepandikizwa na shetani mwenyewe katika kumharibu mtu wa Mungu ambaye amesimama katika Imani ili aonekane ni mwovu..Na watu hao ni watu wa kuanzisha ubishi, ambao kazi yao kubwa ni kwenda kumchochea mtu aliyesimama abishane au agombane ili watu wengine wanaomzunguka wamwone kuwa si kitu, ni mtakatifu feki!..na waishie kutomsikiliza tena…Watu wa namna hiyo watakuja tu na kuanzisha mada na kukutaja wakitaka mchango wako..lakini lengo lao ukiwasoma si kutaka kujifunza bali kubishana na wewe…Watu kama hao wameanzisha mada na umejaribu kuwajibu kwa upole na hawaonyeshi kuelewa hao biblia imeturuhusu tuwakatae…Tusizungumze nao, wakituhoji ni ruksa kutowajibu….Wengi wa hao wametumwa na shetani kabisa kufanya hiyo kazi.

Tito 3:9 “Lakini maswali ya upuuzi ujiepushe nayo, na nasaba, na magomvi, na mashindano ya sheria. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana”

Hivyo mijadala ya mashindano tujiepushe nayo, mijadala ya kushindania mistari ya biblia tujiepushe nayo na mijadala ya kila aina ambayo mwisho wake ni ugomvi na makelele tujiepushe nayo vilevile…

2Timotheo 2:23 “Walakini uyakatae maswali ya upumbavu yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi.

24 Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu;

25 akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na kuijua kweli;

26 wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambao hao wametegwa naye, hata kuyafanya mapenzi yake”

Bwana atusaidie katika kulitimiza na hilo pia..

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii 0789001312.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:

Mada Nyinginezo:

NGUVU ILIYOPO KATIKA MAAMUZI.

USILALE USINGIZI WAKATI WA KUMNGOJEA BWANA.

UNATAKA KUBARIKIWA? BASI USIKWEPE GHARAMA ZAKE.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

UFUNUO: Mlango wa 1

DANIELI: Mlango wa 1

ESTA: Mlango wa 1 & 2

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1

Rudi Nyumbani:

Print this post

Kwanini biblia inasema mtu wa rohoni huyatambua yote?

SWALI: Mstari huu una maana gani? 1Wakorintho 2:15 “Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu”?


JIBU: Ukianza kusoma kuanzia ile mstari wa kwanza utaona mtume Paulo, akieleza vizuri maana halisi ya kuwa mtu wa rohoni.. mtu wa rohoni sio mtu anayeona wachawi, au anayeota ndoto, au anayeona maono, mtu anaweza akawa na vipawa hivyo vyote lakini bado asiwe ni mtu wa rohoni.

Kulingana na mistari hiyo mtu wa rohoni ni mtu aliye na ufahamu wa kuzitambua siri za Mungu kwa Roho Mtakatifu. Na siri kuu ya Mungu ipo katika kumjua Yesu Kristo, ambayo biblia inasema kama watawala wa dunia hii wangeijua , wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu;(1Wakorintho 2:8)..

Unaona, wangejua kuwa suluhisho la mambo yote lipo kwa Yule, maarifa yote na siri zote walizokuwa wanazitafuta kwa miaka na miaka zipo kwa Yule, wasingemsulibisha…biblia inaeleza kabisa..Lakini walifumbwa macho yasione, hivyo wakabakia kuyatambua mambo ya mwilini tu.

Yohana 12:37 “Walakini ajapokuwa amefanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, hawakumwamini;

38 ili litimie lile neno la nabii Isaya alilolisema, Bwana, ni nani aliyezisadiki habari zetu; Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?

39 Ndiyo sababu wao hawakuweza kusadiki; kwa maana Isaya alisema tena,

40 Amewapofusha macho, Ameifanya mizito mioyo yao; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakafahamu kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.

41 Maneno hayo aliyasema Isaya, kwa kuwa aliuona utukufu wake, akataja habari zake”.

Hivyo ukiona wewe kila siku unamjua Kristo katika viwango vingine, basi ujue kuwa wewe ni mtu wa rohoni mwenye viwango vya hali ya juu..Ukiona kila usomapo Biblia unaziona habari za Yesu, kila ukitazama vitu vya asili unaiona injili ya Yesu, kila Ukitazama Maisha ni kama unayasikia maneno ya Yesu yanazungumza na wewe masikioni yanakuonya kila unalotaka kulifanya unatamani liwe linalompendeza Yesu… hapo wewe ni mtu wa rohoni…Na sio ukisoma biblia unaona wachawi, au ukisali unaona wachawi hapo bado hujawa mtu wa rohoni.

Na ndipo hapo biblia inasema.. mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu.. Utakuwa na uwezo wa kuyatambua mambo yote, na siri zote za Mungu wanadamu wasizozijua…hakuna jambo lolote litakuwa ni jipya machoni pako na zaidi ya yote bado utakuwa hautambuliwi na yeyote.. Yaana maana yake, hakuna mwanadamu yeyote mwenye tabia ya asili atakayeweza kukutambua, akikuangalia ataishia tu kuona vya nje, watasema umerukwa na akili kama vile Paulo alivyoambiwa, wengine watasema una mapepo, kama vile Yohana Mbatizaji alivyoambiwa..Wengine watakauambia umelogwa..

Ni kwasababu ufahamu wao umeishia hapo kwenye mambo ya nje, hawawezi kuona zaidi ya hapo..furaha na tumaini lililopo ndani yako..Hawajui kuwa ndani yako ni Roho Mtakatifu anakufundisha, lakini wewe utakuwa na ufahamu wa kuelewa yao yote. Utagundua kuwa wanavyokufikiria wewe sivyo ulivyo.

Hivyo upo umuhimu wa kumpa Kristo maisha yako, kama hujampa au kama ulishampa hapo kabla na ukapoa ni wakati wa kuweka mambo yako sawa..Ili Roho wa Mungu awe na nafasi ya kukufunulia yale usiyoyajua kuhusu Bwana Yesu Kristo.

Ubarikiwe.

Kwa mawasiliano/mafundisho zaidi kwa njia ya whatsapp, tutumie ujumbe kwenye namba hizi: +255789001312/ +255693036618

  

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:

Mada Nyinginezo

Je! dhambi zote ni sawa Kuna dhambi kubwa na ndogo?

YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI

Tofauti kati ya uchafu wa mwilini na rohoni ni  ipi?

Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?

Nini maana ya “wazimu” katika biblia?

Je ni viatu gani Musa aliambiwa avivue?  Vya mwilini au vya rohoni? (Kutoka 3:5).

TUTAMKARIBIA MUNGU KWA IDADI YA MVI ZETU ROHONI.

Rudi Nyumbani

Print this post

KUOTA UNAFANYA TENDO LA NDOA.

Kuota unafanya tendo la ndoa au kuota unafanya mapenzi na mtu usiyemjua maana yake ni nini?


Awali ya yote tunapaswa kufahamu kuwa Ndoto yoyote ya zinaa, haitokani na Mungu..Ni aidha inatokana na mtu mwenyewe au shetani. Leo tutaangazia makundi mawili ya watu wanaoota ndoto za namna hii:

Kundi la kwanza ni: Kwa mtu ambaye hajaokoka:

Biblia inasema..

Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi;…”

Hii ikiwa na maana kuwa, yale mambo au vile vitu tulivyokuwa tunavifanya au kuvifikiria mchana kutwa mara nyingi huwa ndio hivyo hivyo tunaviota tukiwa tumelala..

Hata kama hatutaviota vilevile kama vilivyo lakini tutaota mambo yanayoendana na matukio tuliyokuwa tunayafanya katika mazingira yanayotuzunguka..Kwamfano kama wewe wiki nzima ulikuwa unashinda mashambani tu kulima na kupalilia shamba lako..Uwezekano wa wewe kuota upo shambani unafanya shughuli kama hizo ni mkubwa sana..Kama wewe ulikuwa shuleni mwaka mzima bwenini uwezekano wa kuendelea kuota ndoto upo shuleni ni mkubwa..

Vivyo hivyo kama wewe ni mlevi unayeshinda bar kila siku usiku uwezekano wa kuota ndoto za upo bar unakunywa pombe na marafiki zako ni mkubwa..Haiwezekani mtu ambaye hajawahi kuenda bar au kunywa pombe Maisha yake yote akaota anakunywa pombe bar na akalewa. Vivyo hivyo hata katika zinaa, kama Maisha yako yote, na wakati wako wote unawaza uzinzi kichwani, unatazama picha chafu mitandaoni, na video za pornography, unafanya mustarbation, unaangalia muvi za mapenzi, unasiliza nyimbo za kidunia za kizinzi, maneno unayozungumza kila mara ni ya usherati tu, jinsi ya kumpata binti yule au kaka yule..Nataka nikuambie kila siku usiku kuota unafanya tendo la ndoa au unafanya mapenzi na mtu usiyemjua au unayemjua itakuwa ni jambo la kawaida kwako.

Kwasababu Maisha yako yote yapo katika uzinzi..Shughuli kubwa iliyo katika ubongo wako ni zinaa..

Vilevile yapo mapepo ya namna hii mahususi kutoka kuzimu yanawavaa watu ambao hawajaokoka ili kuchochea hii hali ndani yao. Ndio hapo utamwona mtu ndoto kama hizi zinakuwa ni sehemu ya Maisha yake, anajikuta mara kwa mara anafanya mapenzi na mtu asiyemjua, leo,Kesho, anapumzika wiki moja hali ile ile inajirudia tena na tena, ukiona hivyo ujue lipo pepo limeshakuvaa.

Unahitaji kugeuzwa Maisha yako.

Kundi la Pili: Kwa mtu aliyeokoka.

Lakini kama wewe upo ndani ya Kristo.

Mambo mawili yanaweza yakawa yanahusika.

La Kwanza. Ni ishara ya kuwa kuna mahali unapoa,.Umepunguza kiwango chako cha nguvu za rohoni, kuna mahali unapadokoa au baadhi ya mambo kidunia yanakuchukua..Hivyo hapo unapaswa uongeze bidii yako kwa Mungu, ongoza kiwango chako cha maombi, tumia muda mrefu kusoma biblia kuliko kufuatilia mambo yasiyokuwa na maana. Simama imara katika Imani yako. Kabla hujalala jijengee utaratibu kwa kuomba. Na hiyo hali haitajirudia tena.

Lakini kama wewe umeokoka na bado unauhakika umesimama imara katika Imani, na ndoto kama hiyo imekujia bila kutazamia, na ishara kuwa ulikuwa hufurahii ni kwamba hata katika hiyo ndoto ulikuwa unaonyesha upinzani,kukataa hicho kitendo, au kujiuliza inakuaje kuaje nipo katika hali hii na mimi nimeokoka.. basi hali kama hiyo ikikujia Ikimee mara moja kwa jina la YESU, kisha mwambie shetani huwezi kunijaribu kwa kishawishi chochote..Na ndoto kama hizo hutaziota tena..

Jambo ambalo watu wengi hawafahamu ni kuwa zinaa, kuiondoa ndani ya mtu inahitaji muujiza, na anayeweza kuikata kiu hiyo ni YESU KRISTO peke yake, haijalishi wewe ni mkristo au wewe ni muislamu au hauna dini ..Ni Yesu pekee ndio anayeweza kukubadilisha na kukufanya uishi Maisha yaliyo  mbali na zinaa.

Dhambi hii, inawashinda wengi, na ndio dhambi inayoongoza kuwapeleka watu kuzimu.  Isitoshe biblia inasema, Kama vile ilivyokuwa katika siku za Sodoma na Gomora ndivyo itakavyokuwa siku za kuja kwake mwana wa Adamu. Kumbuka siku za Sodoma na Gomora, kulikuwa na uzinzi wa kiwango vya hali ya juu kama vilivyopo sasa, kulikuwa kuna mashoga na wasagaji waliokuwa wanajidhirisha waziwazi kama ilivyo sasa.. Na hiyo ndio ikiwa sababu ya miji ile kuteketezwa..Lakini cha kuogopesha Zaidi ni kwamba, kati ya maelfu kama sio mamilioni ya watu waliokuwa katika miji ile, ni watu watatu tu ndio walionusurika..wengine wote waliteketea kwa moto..

Luka 17:28  “Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga;

29  lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote.

30  Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu”

Soma tena kwa makini mstari huu:

Yuda1:7  “Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.

8  Kadhalika na hawa, katika kuota kwao, huutia mwili uchafu, hukataa kutawaliwa, na kuyatukana matukufu”.

Unaona? Vivyo hivyo na jambo kubwa Zaidi litakalofanya ulimwengu huu uteketezwe siku ambazo si nyingi, ni dhambi ya zinaa, vilevile watakaonusurika watakuwa ni wachache sana. Mungu huwa hana wengi wape,.Leo hii unaweza kusema mbona kila mtu yupo hivi au yupo vile..Lakini nataka nikuambie  hata kama dunia nzima imeamua kuasi Mungu akimuona mtu mmoja tu, inatosha yeye kuangamiza..

Hivyo ikiwa wewe ni mwenye dhambi, haijalishi dini yako, au dhehebu lako.Yesu anawaokoa watu wote, na bado anaendelea kuokoa ikiwa mtu atakuwa tayari kutaka kuokolewa naye, kwasababu neema yake kaiachia kwa watu wote. Ikiwa leo hii unataka kusema Maisha ya uzinzi basi, nataka YESU anasaidie niishinde dhambi hii na nyingine zote…Ukiwa unamaanisha kweli kufanya hivyo..Basi leo hii hapo ulipo anaweza kukuokoa na kukugeuza na kukufanya kuwa mtoto wake.

Ikiwa upo tayari kubadilishwa leo Maisha yako na Yesu..Basi fahamu kuwa yeye yupo hapo pembeni yako kukusaidia, unachopaswa kufanya ni kufungua tu moyo wako..Uhitaji unione mimi, au usikie sauti yangu..Suala la wokovu ni Zaidi ya upeo wa fikra za kibinadamu. Leo hii YESU atayageuza Maisha yako, na atafanya muujiza mkubwa ndani yako kwa namna ambayo hujawahi kuidhania.

Hata na yale mengine mbali na uzinzi, labda ulevi, matusi, wizi yote atayaua ndani yako ikiwa tu utakuwa tayari kumpokea Leo. Yesu yupo hai, yupo tayari kwa mtu yeyote kumsaidia wakati wowote bure.. hivyo bila kukawia kawia hapo ulipo chukua muda jitenge eneo la utulivu. Kama upo ndani tafuta chumba ujitenge peke yako, kisha piga magoti..Ukiwa hapo chini umepiga magoti sema sala hii kwa sauti..

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU  MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU WA KUSHINDA DHAMBI, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA, NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KWA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani Mungu amekusikia ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa matendo, hapo ulipo ikiwa ulikuwa na picha chafu katika siku yako, anza kwa kuzifuta, ikiwa ulikuwa unayafanya  mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Kuanzia leo hii utaanza kuona badiliko kubwa ndani yako. Jambo lingine unalohitaji kufanya ni kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na katika kujifunza biblia ili uukulie wokovu.

Hata kama wewe ulikuwa ni muislamu, tafuta kanisa lililokaribu na wewe la kiroho, waeleze uamuzi wako uliouchukua, kisha wao watakuelekeza hatua inayofuata au kama utahitaji msaada wa kanisa kwa eneo lako basi wasiliana nasi kwa namba hizi 0789001312.. Ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Yazingatie hayo. Na Bwana atakuwa pamoja na wewe katika kila hatua ya Maisha yako. Na ndoto zote hizo za Kuota unafanya tendo la ndoa au kuota unafanya mapenzi na mtu usiyemjua, zitaisha.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:


Bwana akubariki.

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Pia zidi kutembelea website yetu hii, kwa mafundisho mengine

Mada Nyinginezo:

Nitajuaje kama ndoto ni ya Mungu au ya Shetani?

KUOTA UPO UCHI.

KUOTA UNAKULA CHAKULA.

Kuota unafanya Mtihani.

Kuota unakimbizwa.

MKUU WA ANGA.

UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?

Rudi Nyumbani:

Print this post