Title December 2019

NDOA NI NINI?

Ndoa ni nini? Je ndoa za kibinadamu ni zipi na ndoa ya kimbinguni ni ipi?


karibu tujifunze masomo ya ndoa na elimu ya ndoa na mafunzo ya ndoa kwa mapana.

Ndoa ni muunganiko wa kimwili kwa namna ya roho kati ya watu wawili wa jinsia mbili tofauti.  Kuna aina mbili za Ndoa. Zipo ndoa za kibinadamu na ndoa ya kimbinguni.

Ndoa za kibinadamu zinahusisha Mume mmoja na mke mmoja…Lakini Ndoa ya kimbinguni inahusisha Mume mmoja (Aitwaye Yesu Kristo) na mke wake mmoja aitwaye Kanisa.

Ndoa za kibinadamu.

Kama tulivyotangulia kusema hapo juu..Ndoa hii ni muunganiko wa kimwili baina ya watu wawili wa jinsia mbili tofauti. Ndoa ya kwanza ilifungishwa na Mungu mwenyewe pale Edeni…baada ya Adamu kukabidhiwa Hawa aliyetoka ubavuni mwake. Na ilihusisha Mume mmoja na mke mmoja…Hakuumbwa Adamu mmoja na wakina Hawa wengi…au Hawa mmoja na wakina Adamu wengi. Kama ingekuwa ni hivyo basi Ndoa ya mume mmoja na wake wengi ingekuwa halali..au ya mke mmoja waume wengi.

Mathayo 19:3 “Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?

4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,

5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?

6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe”.

Na kuna tofauti kati ya ndoa na harusi..Ndoa ndio kama tulivyoizungumza hapo juu kwamba ni muunganiko wa kimwili watu wawili wa jinsia mbili tofauti.  Lakini harusi ni sherehe au karamu inayofanywa baada ya ndoa kufungwa.

Sasa kuna maswali machache yafuatayo ya kujiuliza: Maswali haya yanalenga kwa urefu juu  ya masomo ya ndoa na mafunzo ya ndoa/Elimu ya ndoa

  • Je ni lazima kuoa au kuolewa?

Biblia haijaweka sharti la kwamba kila mtu ni lazima aoe au aolewe. Zaidi ya yote ni vizuri mtu kutokuoa kabisa au kutokuolewa kwa ajili ya kuifanya kazi ya Mungu. Biblia inasema hivyo katika..

1 Wakorintho 7:32 “Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;

33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe.

34 Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.

35 Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine”

Kuna faida kubwa ya kutokuoa au kutokuolewa kwaajili ya kuifanya kazi ya Mungu..lakini kama sio kwasababu hiyo ni heri kuoa au kuolewa. Kwasababu Ndoa ina faida kubwa sana, na ina baraka na heshima.  Mtu aliyefunga ndoa takatifu. Kuna Baraka za kipekee na Neema kutoka kwa Mungu anazipokea zaidi ya yule ambaye hajaoa au hajaolewa. Hivyo ni vizuri kuoa au kuolewa..(hususani Unapozidi kuelewa upana juu ya ndoa ni nini na majukumu yako baada ya ndoa hiyo utabarikiwa sana kuliko kawaida )

lakini pia ni vizuri kutooa au kutokuolewa kwaajili ya ufalme wa mbinguni.

Maswali mengine ya muhimu ya kujiuliza kuhusu elimu ya ndoa/mafunzo ya ndoa ni kama yafuatayo.

  • Nitampataje Mwenza wa Maisha?: Jibu la Swali hili utalipata mwisho kabisa wa somo hili. au bofya hapa >> Mwenza wa Maisha
  • Je ni ruhusa kutoa Talaka baada ya kufunga ndoa?: Jibu la Swali hili pia utalipata mwishoni mwa somo hili au bofya link hii >> Talaka
  • Je ni Lazima kutoa mahari kabla ya kufunga ndoa?, Na je pia ndoa ni lazima ifungiwe kanisani?: Jibu la swali hili pia utalipata mwishoni kabisa mwa somo hili kwenye link za mapendekezo au bofya hapa kujua >> Mahari
  • Je Ndoa ya Yesu Kristo ikoje? Kwa mapana zaidi?: Jibu la Swali hili pia unaweza kulipata katika link za mapendekezo mwishoni mwa somo hili, Au bofya hapa kusoma >> Ndoa ya Kristo

Kama utakuwa umeyafuatilia hayo masomo ya ndoa hapo juu na kuzifungua link hizo kwa umakini utakuwa umeelewa kwa sehemu kubwa ndoa ni nini?.  Hivyo kama umedhamiria kuoa au kuolewa..Basi kumbuka jambo moja na la muhimu kuwa “Ndoa inapaswa iheshimiwe na watu wote.”. Sio iheshimiwe na wewe tu na mpenzi wako peke yenu!.. Hapana bali watu wote..Ikiwa na maana kuwa ukifanya jambo lolote litakaloifanya ndoa yenu isiwe na heshima, watu wakaidharau…Hiyo tayari ni dhambi! mbele za Mungu.

Waebrania 13:4 “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu”.

Ukishaoa au kuolewa huo sio wakati wa kutanga tanga huku na huko kuzungumza zungumza habari za ndoa yenu..huko ni kuiondolea heshima ndoa yenu! na ni dhambi..Ukishaoa sio wakati wa kuudhiana mpaka kutupiana maneno au kupigana hadi watu wa nje wanawaona..huko ni kuivunjia heshima ndoa…ambapo ni dhambi! n.k

Ukishaoa sio wakati wa kukaa kwenye vibaraza vya mizaha, na vijiweni kuzungumza kama mtu ambaye hajaoa au hajaolewa, na wala si wakati wa kuvaa kama kahaba, au mhuni huko ni kuivunjia heshima ndoa ambako ni dhambi na kujitafutia laana. Ni lazima ufahamu ndoa ni nini!

Kama hujafahamu Agano lililopo katika ndoa ni heri ukasubiri kwanza, kuliko kukurupuka na kuoa au kuolewa na kisha kuiharibu ndoa na kuangukia Hukumu.

Yapo mengi ya kuzungumzia juu ya ndoa ni nini, lakini hapa hatuwezi kuyaandika yote, naomba ufungua link hizo nilizokupatia hapo juu au hizi hapa chini, yapo maelezo marefu na ya kutosha kuhusu ELIMU YA NDOA.

Bwana akubariki sana.

Na kama hujampa Yesu Kristo maisha yako.. Nakushauri ufanye hivyo sasa. Mahusiano ya kwanza ya kutafuta kabla ya kuoa au kuolewa ni mahusiano yetu sisi binafsi na Yesu Kristo. Huyo ndiye tumaini la wokovu wetu na mwokozi wa kila mwenye mwili. Na biblia inasema pia itatufaidia nini tuupate ulimwengu mzima na tupate hasara ya nafsi zetu..

Hivyo kila kitu kitapita…hata baada ya kifo hakutakuwa na kuoa wala kuolewa..Ni mambo mengine yatafuata. Hivyo ni muhimu sana kwanza kutafuta uhusiano binafsi na Yesu Kristo kabla ya mambo yote..Na huo tunaupata kwa kumwamini, na kutubu dhambi zetu zote kwa kukudhamiria kutozifanya tena..Na kubatizwa..na Roho Mtakatifu atatuongoza katika kweli yote.

Maran atha!


Mada Nyinginezo:

NJIA SAHIHI YA KUMPATA MWENZA WA MAISHA KIBIBLIA.

JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI AU KUTOA TALAKA?

Je Mahari ina ulazima wowote?

NDOA NA HARUSI TAKATIFU.

Je! Ni sahihi kwa mkristo kuoa/kuolewa na mtu wa imani nyingine?

Rudi Nyumbani:

Print this post

MADHABAHU NI NINI?

Jiunge na group la Whatsapp, ujifunze biblia na upate Neno la siku kila asubuhi. Pamoja na maswali mengi ya biblia yaliyojibiwa..kwa link hii >>> https://chat.whatsapp.com/FAyJLXo8guQ0iZ0JzQKbXg

Madhabahu ni nini?..Je madhabahu ya kuvukiza uvumba ni nini?..je hata sasa watu wanatengeneza madhabahu za kutolea dhabihu?…madhabahu ya kwanza kutengenezwa ni ipi?

Madhabahu ni mahali ambapo sadaka zinatolewa.. Katika Agano la Kale, Bwana Mungu aliwaagiza wana wa Israeli wamtolee sadaka…Zilikuwepo sadaka za aina mbali mbali kama vile sadaka za dhambi, sadaka za shukrani na nyinginezo.

Lakini sadaka yoyote iliyokuwa inatolewa kama ni sadaka kuteketezwa, Ilikuwa ni lazima madhabahu itengenezwe. Kwa lugha rahisi na ambayo inaweza kueleweka ni kwamba baada ya mnyama yule aliyewekwa tayari kwaajili ya sadaka kuchinjwa..aliwekwa juu ya kuni zilizopangwa vizuri zilizo juu ya mawe…hivyo madhabahu ilitengenezwa kwa mawe na kuni..Ni sehemu maalumu ya kumchomea yule mnyama mpaka eteketee kabisa..

Madhabahu ya kwanza ilitengenezwa na Habili ambaye alimtolea Bwana sadaka ya kuteketezwa juu yake. Na Mungu aliiitakabali zaidi ya Kaini ndugu yake.

Katika Biblia tunasoma pia Nuhu alimjengea Bwana madhabahu baada ya kutoka kwenye safina.(Soma Mwanzo 8:20)

Na pia Ibrahimu alimtengenezea Mungu madhabahu mara kadha wa kadha alipotaka kumtolea Mungu sadaka…Ndio maana tunaona hata wakati ule alipojaribiwa na Mungu amtoe Isaka mwanawe..tunaona alitengeneza madhabahu.

This image has an empty alt attribute; its file name is Abraham-to-Sacrifice-Isaac-2.jpg

Na wengine wote kama akina Yakobo, Eliya, na Musa walipotaka kumtolea Mungu sadaka walitengeneza madhabahu..Na kulikuwa na maagizo maalumu ya namna ya kutengeneza madhabahu kama Mungu anavyotaka…ilikuwa sio ruhusa kutengeneza madhabahu kama za wapagani..kulikuwa na maagizo maalumu ya namna ya kuitengeneza ambapo hatuwezi kuyaangalia yote lakini mojawapo ilikuwa ni hili…

Kumbukumbu  27:5 “Na huko umjengee madhabahu Bwana, Mungu wako, madhabahu ya mawe, usitumie chombo cha chuma juu yake.

6 Jenga hiyo madhabahu ya Bwana, Mungu wako, kwa mawe yasiyochongwa; ukamtolee Bwana, Mungu wako, sadaka za kuteketezwa juu yake;”

Kulikuwepo pia kuna aina nyingine ya madhabahu iliyojulikana kama madhabau ya kuvukizia uvumba (Soma kutoka 30:27). Hii ilitumika kwaajili ya kuchomea uvumba mtakatifu ndani hema ya Mungu au Nyumba ya Mungu ..Madhabahu hii haikutengenezwa kwa mawe na kuni kama ile madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa..Hii ilikuwa ndogo na ilikuwa ni kama jiko hivi…Tazama picha chini.

madhabahu ya kuvukizia uvumba

Lakini katika Agano jipya hatuna tena hizo Madhabahu zenye mfano huo..

Madhabahu yetu kwa sasa ni mioyo yetu…Tunapomkubali Yesu Kristo na kuingia moyoni mwetu…Na anapotusafisha na kutupa Roho wake mtakatifu hapo ndipo madhabahu yetu inapokamilika katika viwango Mungu anavyovitaka..Na kuanzia huo wakati shughuli zotezote za kiibada, ikiwemo sadaka, maombi, dua, sala, utukufu, shukrani ndipo vinakubalika mbele za Mungu.

Zaburi 51:16 “Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa, Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa.

17 Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau”

Lakini kama mtu hajasafishwa maisha yake kwa damu ya Yesu basi madhabahu ya moyo wake inakuwa ni chafu na hivyo hawezi kumpendeza Mungu kwa chochote kile.

Mbali na hilo, upo pia utaratibu wa kuiita mimbari ya kanisa kuwa ni madhabahu..Kiuhalisia ile sio madhabahu..Lakini pia si dhambi kuiita madhabahu na kuiheshimu. Kwasababu ni mahali ambapo Neno la Mungu (chakula cha Roho zetu linahubiriwa na tunapeleka matoleo yetu pale)..Na pia chochote kitakachofanyika pale kinyume na Neno la Mungu au kisichokuwa na utukufu wa Mungu, Ni dhambi na hivyo ni kujitafutia laana badala ya baraka..Na kumbuka pia sehemu ya mimbari ya kanisa (ambayo inajulikana kama madhabahu)..haipaswi kupambwa pambwa na mishumaa, au sanamu mpaka kufikia hatua watu wanakwenda kuvisujudia na kuviangukia na kuviogopa…Hiyo ni ibada za sanamu na ni machukizo makubwa mbele za Mungu. Mimbari inapaswa iwe ni sehemu ya kawaida tu…

Lakini madhabahu halisi ni mioyo yetu..Na hatupaswi kuweka msisitizo mkubwa wa kuiheshimu madhabahu ya kanisa na huku madhabahu halisi ya mioyo yetu imechafuka. Biblia inasema..

Mithali 4:23 “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima”

Utakuta mtu anaiogopa madhabahu ya kanisa na kuiheshimu..Lakini kuiheshimu madhabahu halisi ya moyo wake ambapo ndipo mahali Mungu yupo karibu sana na yeye haiheshimu..Atamwabudu Mungu huku moyoni mwake ni muuaji, mwasherati, mwenye chuki na kinyongo na kutokusamehe.

Bwana atusaidie kufanya madhabahu za mioyo yetu kuwa safi..ili maombi yetu, sala zetu, dua zetu pamoja na sadaka zetu zipate kibali mbele za Mungu wetu.

Ubarikiwe sana.

+255693036618/ +255789001312


Mada Nyinginezo:

Rudi Nyumbani:

Print this post

USILALE USINGIZI WAKATI WA KUMNGOJEA BWANA.

Usilale usingizi wakati wa kumngojea Bwana.


 

Luka 12: 35  “Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka; 

36  nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara. 

37  Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia. 

38  Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao. 

39  Lakini fahamuni neno hili, Kwamba mwenye nyumba angalijua saa atakayokuja mwivi, angalikesha, wala asingaliacha nyumba yake kuvunjwa. 

40  Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.”

Tusome mstari mwingine tena unaofanana na huo…

Marko 13:35 “Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi; 

36  asije akawasili ghafula akawakuta mmelala. 

37  Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni”.

Hapa tunaona tukio la Mtu mmoja ambaye tajiri…ambaye ana nyumba yake yenye wafanyakazi wengi..na kila mfanyakazi ana majukumu yake kama tunavyojua…wapo wa wakutengeneza chakula, wakufanya usafi, wapo wa kulisha mifugo, wapo wakuhakikisha usalama, n.k Kila mmoja ana majukumu yake.

Lakini tunaona alitoka siku moja na kwenda arusini..akawaambia watumwa wake wakeshe!..hakuwaambia kwamba atarudi siku hiyo hiyo…lakini aliwaaambia tu atarudi siku yoyote…Hivyo akawaambia muda wowote wawe tayari..siku atakayokuja kama ni jioni, au asubuhi au usiku wa manane awakute wakiwa katika shughuli zao kama kawaida..waohusika na usalama basi wawe wa kwanza kumfungulia mlango atakapofika n.k

Akawasisitiza sana wawe macho muda wote kwasababu hawajui siku wala saa atakapokuja. Sasa endapo angekuja baada ya siku mbili mida ya saa 8 usiku akawakuta wamelala unadhani angejisikiaje?..Ni wazi kuwa angeudhika sana na kuwafukuza kazi wote..

Mfano huo huo unalinganishwa na kurudi kwake Bwana Yesu mara ya pili. Kumbuka mtu yoyote aliyeokoka kwa dhati ni mtumishi wa Yesu Kristo..Ni lazima kuna kitu Fulani ambacho amepewa na Kristo kwaajili ya kuundeleza ufalme…Na kitu hicho ni karama aliyopewa…Na karama hiyo Bwana Yesu anataka iendelee kufanya kazi muda wote mpaka siku atakayokuja.. Lakini akija na kukuta Karama aliyokupa imekufa haifanyi kazi…Na sio tu haifanyi kazi bali pia wewe mwenyewe umelala usingizi (yaani umechukuliwa na ulimwengu)..Basi kuna hatari ya kutupwa katika ziwa la moto.

Hivyo tukumbuke kila siku kwamba tupo kazini..na hivyo tuwe waaminifu na majukumu yetu tuliyokabidhiwa na Bwana.

usilale usingizi..Kwasababu Biblia inasema katika;

Waebrani 10:37  “Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia”.

Bwana akubariki.

Mada nyinginezo;

BIRIKA LA SILOAMU.

TUUTAZAME PIA MWISHO WA UJENZI WETU.

VIUNO VYENU VIWE VIMEFUNGWA NA TAA ZENU ZIWE ZINAWAKA

MAUTI YA PILI NI NINI?

BONDE LA KUKATA MANENO.

LITANIA YA BIKIRA MARIA JE! NI SALA YA KIMAANDIKO?

USISIKILIZE DHIHAKA ZA SHETANI, ZITAKUKWAMISHA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

HAPANA HATA MMOJA ATAKAYEIONJA KARAMU YANGU.

“Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu”


Tukisoma Luka 14 kuanzia mstari wa 16-24. Tunaona Bwana Yesu akitoa mfano wa mtu mmoja aliyefanya karamu kubwa sana. Na siku ilipofika ya sherehe muda wa chakula akatuma mtumwa wake kwenda kuwaita wale waliolikwa waje karamuni lakini mwitikio wao siku hiyo ulikuwa ni tofauti, badala ya kuja kila mmoja akaanza kutoa udhuru mmoja akasema mimi nimenunua shamba ni sharti niende kulitazama nisije nikawa nimeuziwa bonde, hivyo nisamehe, mwingine akasema nimenunua ng’ombe hivyo ni sharti niende kiwajaribu nisije nikawa nimeuziwa vilema na wagonjwa, mwingine akasema nimeoa nitakwenda honey-moon siwezi kuja nisamehe..

Lakini yule mtu alikasirika sana..Ukisoma pale kwa makini utagundua kuwa hakukasirika kwa waliokuwa wamepanga kuyafanya, hapana lakini alikasirika kwa wao kupuuzia mwaliko wake. Kwasababu udhuru zao hawakuzitoa mwanzoni kabisa walipoalikwa kabla hata sherehe kuanza, Bali walisubiria wazitoe siku ambayo kila kitu kipo tayari,.. mahali ambapo mwenye kualika hawezi kuahirisha na kufanya wakati mwingine ambapo wote watakuwa free. Hiyo ni kuonyesha kuwa walikuwa hawataki kabisa kuhudhuria sherehe ya yule aliyewaalika tangu mwanzo, na ndio maana wakazihifadhi sababu zao wasizitoe tangu siku nyingi na kuzitoa siku ile ya sherehe yenyewe, walijifanya kama wamepatwa na emergency hivi kumbe mambo hayo walikuwa wanayatambua tangu mwanzo..

Lakini sasa tunaona mwisho wa mfano ule, Bwana YESU anasema maneno haya:

Luka 14:24 “Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu”.

Hapa ndipo kiini cha somo kilipo..

Kwanini aseme tena hivyo “wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu.”

Kulikuwa kuna maana gani ya kusema hivyo wakati tayari walishaikataa tangu mwanzo?..Embu jaribu kufikiria mtu amekualika unakataa halafu anakuapia hutaonja sherehe yake…Si unaweza kumwona kama ni Mwenda wazimu?. Lakini ukiwa na akili utajiuliza maswali Fulani kichwani kwako kwanini aniambie vile??

Kipindi Fulani nyuma, kuna Rafiki yangu ambaye alipomaliza masomo yake alikwenda katika mafunzo ya jeshi kwa matumaini kuwa akimaliza aajiriwe kule, lakini kwa bahati mbaya walikaa kule muda mrefu, sana, wakisubiria ajira kwa muda mrefu lakini hazikutoka..Mpaka wakati wa mafunzo ulipoisha sasa wanalazimika kila mmoja arudi nyumbani kwao, ni kama vile alikata tamaa akiangalia ameshapoteza miaka kadhaa kule jeshini na leo hii anaambiwa arudi nyumbani!!..

Lakini wakiwa huko nyumbani, tamko linatolewa na raisi kuwa kuna mgodi mahali Fulani unahitaji ujenzi wa kuzungushwa ukuta mgodi wote, na wanaohitajika kwa shughuli hiyo ni walewale vijana waliokuwa katika mafunzo ya jeshi, lakini kwa sharti kuwa hakuna malipo, wala posho bali ni kitendo tu cha kujitolea..hivyo anayetaka kwenda na aende, na asiyetaka vilevile ni sawa.

Wengi wao waliposikia hivyo hawakutaka hata kufuatilia habari hizo, wengine walidhihaki, wakagoma, wakaona kama ni mambo yaleyale, kwenda kupoteza muda halafu mwisho wa siku hautazamwi unarudishwa nyumbani kukaa.Lakini huyu Rafiki yangu na wenzake wachache sana, wakaamua tu kwenda kujitolea kufanya kazi hiyo, wakitumaini pengine labda wataangaliwa wakishamaliza ujenzi huo, lakini walifanya kazi ile kwa shida ananiadithia, kwasababu ilikuwa ni ngumu na walipewa kipindi kifupi sana cha kuimaliza..

Wakafanikiwa kuimaliza, kisha wakapewa kila mmoja cheti, wakitumaini wataitwa walau jeshini, lakini wakaambiwa asanteni kwa msaada wenu rudini nyumbani..Basi wakarudi nyumbani, muda ukapita wale wengine wakaanza kuwacheka, na kuwakejeli, lakini sasa baada ya ujenzi ule kukamilika na serikali kuona imefanikiwa kukusanya mapato mengi kwa kipindi kifupi kwasababu ya ujenzi wa ukuta ule,.kukomweshwa kwa vya utoroshaji madini. Ndipo raisi akakumbuka Je! Wale watu waliojengwa ule ukuta wamefanyiwa fadhila gani?..Akatoa tamko la siku 2 wale vijana wote waliojenga ukuta ule wafike makao makuu ya polisi wakiwa na vyeti vyao mkononi wapokee ajira zao za kujiunga na Jeshi.

Sasa wale wengine ambao walikataa kujitolea waliposikia hivyo, matumbo yalijaa moto, wakaanza kuhangaika huku na huko wengine wanatafuta namna ya kufoji vyeti vile, wengine wakatafuta namna ya kutoa rushwa, wengine siku ile ile na wao pia walifunga safari wakiungana na wale wenzao kwa ajili ya udahili, wakitumainia kuwa na wao pia watapata rehema ya kuruhusiwa kujiunga na wenzao..Lakini pamoja na kwamba safari zao kuwa ndefu, kutoka kila mkoa nchini.. waliishia kufukuzwa tu getini pale..wengine wakaanza kulia na kulaumu, wakiona wale ambao walikuwa wanawacheka sasa sio wenzao tena..Wenzano wanapata ajira wao wanarudi nyumbani..Wengine wakawa wanajuta ni kwanini walikataa mwaliko ule wa kuujenga ukuta wa mgodi..waliokuwa wanawaambia nyimbo za mizaha leo hii wao ndio wanalia..

 

Na ndivyo itakavyokuwa katika karamu ya mwana-kondoo. Leo hii wengi wanaalikwa mamilioni kwa mamilioni takribani karibu kila mtu duniani anaalikwa ili tu kuingia katika karamu ile ya mwana-kondoo, lakini wanaouitikia mwaliko huo ni wachache sana, tena sana, pengine hao ambao hawaitikii wana sababu zao za msingi sana za kusimamia..wengine wanasema wokovu hauna faida, wengine wanasema unanifanya niwe maskini, wengine wanasema, nilichonacho sasa kinanipa faida kuliko hicho ninachokitazamia kuja huko mbeleni..Wengine wanasema siwezi kuacha biashara yangu hii haramu, ni sharti nitafute fedha kwanza kisha Mungu uzeeni, nikishastaafu…Wengine wanasema nimeujaribu wokovu huo kwa muda mrefu na sijaona faida yake hivyo sitaki kuusikia…Wote hawa wanaosababu zao, na pengine ni sababu za msingi sana..

Lakini nataka nikuambie, leo hii hutaki, lakini siku moja kibao kitakugeukia wewe.. utatamani hicho ulichokikataa lakini utakuwa tayari umeshachelewa?. Ni kwasababu gani utamani kukipata tena hicho ulichokikataa? Ni kwasababu utaona mambo yaliyo kinyume na matarajio yako.

Wale waliopewa mwaliko na kuanza kutoa udhuru wa kununua ng’ombe wengine shamba wengine wameoa..waliidharau ile karamu na Zaidi ya yote walijua hata wakienda kwenye ile karamu watagharimika gharama nyingine za kutoa zawadi..Lakini kinyume chake pengine yule Bwana arusi aliwaalika kwenye karamu yake aliwaalika kwenda kuwapa zawadi waalikwa wake na si kupokea zawadi..Utajisikiaje unaikataa harusi ambayo ulidhani unakwenda kutoa zawadi kumbe ndio unakwenda kupewa zawadi?..Unaona wenzako waliokwenda wanapewa majumba, mashamba, magari, mang’ombe n.k … utatatami kwenda kujiunga lakini utashindwa..?

Ndivyo itakavyokuwa siku watakatifu watakapokwenda mbinguni…Wewe uliyeudharau mwaliko leo..Utaona kwa mbali uzuri ambao Mungu amewaandalia watu wake, milele, utaona hiyo miili mipya waliyoandaliwa wateule wa Mungu milele jinsi ilivyo mizuri yenye utukufu mwingi, na wewe huna, utaona hiyo miji mizuri na majumba mazuri walioandaliwa watakatifu na wewe utakuwa huna chochote, utaona mambo ambayo hata wale walioitikia mwaliko, hawajawahi kuyaona, wala kuyasikia, wala kuyategemea..Siku hiyo utajuta utasema ni kwanini sikuitikia mwito ule wa karamu ya mwanakondoo..

 

Utafanya bidii kweli uingie lakini hutaweza..Ndio hili Neno litakapotimia juu yako..

Luka 14:24 “Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu: yangu”.

Ndugu Parapanda ipo karibuni kulia, UNYAKUO ni tendo tunalolitazamia sasahivi mbele yetu,..Ukiendelea kuutazama huu ulimwengu ambao haukuahidii kitu chochote baada ya kufa, utapata hasara ya nafsi yako mwenyewe. Ushauri wangu ni kuwa Chukua hatua tubu dhambi zako mgeukie Kristo, maadamu wakati wa kuitikia wito mwaliko unao, kabla siku za hatari hazijakukuta..

Ufunuo 19:9 “Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu”.

 

Maran Atha!

Mada Nyinginezo:

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

NGUVU ILIYOPO KATIKA MAAMUZI.

WAZAZI WA YOHANA NA YAKOBO.

HALI ZETU JINSI ZINAVYOWEZA KUATHIRI UTOAJI WETU.

WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.

USIWE NA HAKI KUPITA KIASI.

Rudi Nyumbani:

 

Print this post

NJIA SAHIHI YA KUMPATA MWENZA WA MAISHA KIBIBLIA.

Kuchagua mwenza wa Maisha si jambo la kulichukulia kiwepesi wepesi tu kama vile kuchagua Rafiki, ambaye hata mkigombana mnaweza mkaachana na kurudiana muda wowote.

Tena ikiwa wewe ni mtu uliyeokoka ndio unapaswa uwe makini mara dufu, kwasababu ukifanya maamuzi yasiyosahihi utajikuta sio tu kuupoteza wokovu wako bali pia kufanyika chombo cha kuwapoteza na wengine.

Ipo mifano mingi katika biblia ya watu ambao waliingia katika mikono ya wenza ambao sio sahihi. Kwamfano tunamwona mtu mmoja aliyeitwa Ahabu yeye alimwoa Yezebeli, hakuna asiyejua mke wake huyu jinsi alivyokuwa mwiba kwake na kwa Israeli nzima.. Na hiyo yote ni kwasababu alifanya uamuzi usiosahihi katika kuchagua mwenza wa maisha wa kuoa.

1Wafalme 21:25 “(Lakini hapakuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza atende maovu machoni pa Bwana ambaye Yezebeli mkewe alimchochea. 

26 Akachukiza mno, kwa kuzifuata sanamu sawasawa na yote waliyoyafanya Waamori, Bwana aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.)”

Tunamwona tena mtu mwingine aliyeitwa Samsoni, jinsi alivyoanguka katika mikono ya mwanamke Delila, binti wa kifilisti, Tunamwona tena Sulemani alivyoanguka kwa wanawake wa mataifa mengine jinsi walivyomgeuza moyo na kumfanya aabudu miungu mingine ikiwa kikwazo kwake kwa Mungu hadi ikafikia hatua ya Mungu kumuundokeshea maadui ….

Vilevile tunaomwona mwanamke Abigaili jinsi alivyoanguka mikononi kwa mume  mpumbavu  mlevi aliyeitwa Nabali..Ambaye ilikuwa ni nusura tu amsababishie mauti yeye pamoja na familia yake yote na wafanyakazi wake wote (soma 1Samweli 25).

Tunaomwona Herode naye, ambaye alijiingiza katika uuaji wa damu isiyokuwa na hatia ya Yohana Mbatizaji  kwa wivu tu wa mke wake, ambaye kiuhalisia hata hakuwa mke wake bali mke wa kaka yake alimuua Yohana kwa shinikizo la mke wake katili.

Matatizo kama hayo vilevile yanaweza kumpata mtu yeyote kama asipojua njia ipasayo ya kumpata mwenza wa maisha sahihi.

Leo hii tutajifunza kanuni chache za kibiblia ambazo ukizifuata utakuwa na uhakika wa kuwa huyu uliyempata asilimia mia ni mwenza Mungu aliyekupangia.

Sasa kabla hatujaenda mbali hapa natazamia kuwa naongea na mtu ambaye ameshaokoka. Kama hujaokoka basi mwisho wa somo hili fanya hivyo, ndio ujumbe huu utakuwa na manufaa kwako.

HATUA YA KWANZA:

Usiwe na haraka ya kuoa au kuolewa: Biblia inatuambia wazi kuwa mapenzi huwa yanachochewa na huwa yanaamshwa..na kama yanaamshwa inamaanisha kuwa kumbe huwa yanapoa  pia soma:

Wimbo uliobora 2:7 “Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe”.

Hizi ni hekimu tunafundishwa.. mambo ya kuingia katika ndoa si ya kuyakurupukia. Kisa umemwona Fulani ameolewa au Fulani kaolewa, au umempenda binti yule au kijana yule hivyo na wewe ukaamua moja kwa moja ukaanze mahusiano naye ili mfunge ndoa..Biblia inatuasa tusiyachochee mapenzi kabla ya wakati wake..Mapenzi yana wakati wake..

Ikiwa wewe bado ni binti/kijana mdogo unatafuta mpenzi wa nini wakati unajua kabisa hamna mpango wa kuoana?. Hali kama hiyo ikikujia au vishawishi kama hivyo vikikujia vikatae, kwasababu wakati wake haujafika….Au wewe ni mwanafunzi hujamaliza masomo yako, unataka kuingia katika mahusiano ambayo lengo lake linapaswa liwe ni ndoa, Je utamwoa huyo au yule na huku ukiwa bado masomoni? Huoni kama huo sio wakati wake?..Hivyo ukijikuta unataka kufanya hivyo kataa hiyo hali, toa mawazo yako huko, fanya mambo yako kama vile mtoto mchanga, mpaka wakati wake huko mbeleni utakapofika..

Vilevile wewe bado upo chini ya wazazi wako, au unajijua bado hali yako kiuchumi bado haijaimarika vizuri, unakimbilia wapi kufikiria mambo kama hayo..Simaanishi kuwa mpaka uwe Tajiri ndio uoe, lakini unapaswa ujiandae kisaikolojia, je! Nikifanya hivi, huyo mke wangu nitaweza kumuhudumia hata kwa yale mahitaji ya msingi tu,?  Mambo kama hayo unatakiwa uyafikirie kabla hujaanza kutafuta mwenza wa maisha.

Wimbo uliobora 2:7 “Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe”.

Usiogope labda umri umeenda au vipi, Isaka na Yakobo walipata wake zao wakiwa katika umri mkubwa tu, lakini tunaona wake waliowapata walikuwa ni bora Zaidi ya wake wa watu wengine..Vivyo hivyo usikimbilie tu kuoa au kuoelewa kwasababu Fulani Fulani bali uvumilivu pia ni muhimu katika kupata mwenza sahihi na ndoa iliyo bora.

Lakini sawa ikiwe umeyazingatia hayo vizuri na sasa upo tayari kuwa mwenza, basi zingatia mambo yafuatayo:

  1. NI LAZIMA AWE NI MKRISTO.

Nikisema ni lazima awe ni mkristo simaanishi awe amezaliwa katika dini ya ki-kristo, anaweza akawa amezaliwa lakini matendo yake yapo mbali na ukristo, bali namaanisha ni lazima awe ameokoka, na yupo katika mstari ulionyooka wa wokovu wake, Maisha yake yakimshuhudia kuwa ameokoka, kama wewe ulivyo.

Ukiangalia watu wote tulioona kwenye biblia kuanzia Ahabu mpaka Sulemani wote hao waliingia katika matatizo makubwa kwasababu waliyakaidi maagizo ya Mungu..Pale walipoambiwa wasioe wala wasioelewe na watu walio nje ya taifa la Israeli.

Soma

Kumbukumbu 7:3 “binti yako usimpe mwanawe mume, wala usimtwalie mwanao mume binti yake. 

4 Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya Bwana juu yenu, naye atakuangamiza upesi”.

Mungu alikuwa na sababu kuwaambia vile, kwasababu alijua watawageuza moyo na kuandamana nao na miungu yao.

Nehemia 13:25 “Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang’oa nywele zao; nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe. 

26 Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; walakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye”.

Hivyo jambo la kwanza kabisa la kumtambua kuwa huyu ni mwenza wa maisha sahihi au sio sahihi usikimbilie kumtazama sura, au maumbile yake, au upendo wake kwako..Hilo jambo liondoe akilini kabisa..Usiangalie elimu yake au fedha zake, au ukarimu wake..wala usikimbilie kusema nimeoteshwa kwenye ndoto au nimeonyeshwa kwenye maono kuwa huyu ndio mpenzi wangu…Nataka nikumbie Neno la Mungu ni Zaidi ya ndoto au maono yoyote..Ndoto yoyote  au unabii unaokinzana  na Neno la Mungu unapaswa uukatae hata kama utaonekana unao uhalisia kiasi gani, Neno ndio linatuambia hivyo soma Kumbukumbu 13 utalithibitisha hilo.

Hivyo mwanamke yeyote au mvulana yeyote, anayekujia anataka kukuoa au unataka  kumuoa, mwangalie kwanza Je! yeye ni mkristo aliyesimama katika Imani?…Na kama sio mkristo Je! Yupo tayari kuamini na kumfuata YESU..Ikiwa yupo tayari aanze kwa  kugeuka kwanza ndipo hatua nyingine za kumtathimini sifuate.

2.USIWE NA HARAKA KUFUNGA NAYE NDOA:

Jambo lingine watu wasilolijua ni hili, pindi imetokea tu amemwona kuwa huyu ni mzuri, au anafaa, au ni mtakatifu, anaenda kanisani, bila kutuliza akili zao, moja kwa moja wanakimbilia kwenda kuoa au kuolewa naye..Na baadaye akishagundua kumbe yupo hivi au vile  hiki anaishia kujuta..

Sikuzote tendo la haraka haraka mara nyingi huwa halitokani na Mungu. Ukiona mtu Fulani anakushurutisha haraka haraka ufanye kitu Fulani, au mfanye biashara Fulani bila hata kuwa na nafasi ya kuitafakari vizuri basi ikatae moja kwa moja, ukiona mtu anakulazimisha ununue hiki au kile harakaraka bila hata ya kukiangalia vizuri basi usikinunue kwanza hata kama kwa macho kinaonekana ni kizuri.. Shetani naye huwa ndio anawashurutisha watu hivyo kuingia katika dhambi, atakuambia fanya hichi chapchap hakina shida, lakini baadaye ndio utakuja kujutia milele kwanini ulifanya vile.

Hivyo ukishamthibitisha kuwa huyu au yule ni mkristo, mtakatifu anampenda Mungu, chukua nafasi kumtathimini, pata muda wa kutosha hata miezi kadhaa, ikiwezekana hata mwaka kumwangalia Maisha yake, ..hiyo itakusaidia kuondoa kule kukurupuka ndani yako, na utapata nafasi ya kujua vile ambavyo mwanzoni alikuwa huvijui kuhusu yeye au vile ambavyo amevificha mbele yako. Yusufu hakuwa na haraka ya kumfanya Mariamu kuwa mke wake, bali alingoja kwa kipindi Fulani na ndio maana alipogundua kuwa ana mimba, kumbuka mpaka mimba ionekane labda ni kuanzia miezi 3 na kuendelea, hivyo wakati huo wote hakuwahi kumkaribia wala kumjua, isipokuwa alikuwa amemposa tu, na baadaye alipogundua kuwa ana mimba, akawa radhi kumuacha..Ndipo Mungu akasema usimuache.. Hivyo na wewe chukua nafasi ya kumtathimini huyo anayetaka kuwa mpenzi wako.

Kisha ukiwa katika hali hiyo ya kumtazama sasa ndipo umwombe Mungu..Hapo unajinyenyekeza mbele za Mungu unamwambia nimemwona dada huyu au kaka huyu, ikiwa ni sawasawa na mapenzi yako Ee Mungu naomba unifanikishe na ikiwa sio sawa na mapenzi yako uniepushe naye..

Ukishamaliza kuomba hivyo kwa muda wa kutosha, ikiwezekana kufunga kwa kipindi Fulani..Basi anza harakati za kwenda kutoa mahari kama wewe ni mume, na kama wewe ni mwanamke himiza tendo hilo kwa huyo mwanaume, kwasababu Mungu yupo pamoja na wewe katika kila hatua, kama huyo siye yeye Mungu mwenyewe atamwondoa kwako, au atakuepusha naye, hivyo uwe na amani kuanzia huo wakati kwasababu ulishazitanguliza kwanza kanuni zake, hivyo ni wajibu wa Mungu kukulinda baada ya hapo..

Hakikisha unakwenda kujitambulisha kwao, na yeye kwenu, unatoa mahari, mnafuata hatua zote za ndoa ya kikristo.Kisha baada ya hapo mnafungishwa ndoa kanisani…Hapo ndipo huyu anakuwa mwenza Mungu aliyemkusudia kwa ajili yako.

Ikiwa utazingatia kufuata hatua hizo zote, ondoa wasiwasi kuwa ndoa yako itakuwa na miiba ndani yake, kinyume chake ndio utaimarika hata katika Imani yako kwasababu mke atakuwa msaidizi kwa mume, na mume atakuwa ulinzi kwa mke..Wote wawili wakisimama katika imani mafanikio tele ya rohoni na mwilini yataambatana  nao, na Watoto wao pia watabarikiwa.

IKIWA HAUJAOKOKA:

Lakini kama wewe hujaokoka. Fahamu kuwa upo katika hatari kubwa sana, kwanza kwa kuukosa uzima wa milele, Na pili kwa kutokuwa na ndoa yenye baraka za Mungu..Kwasababu unataka kuoa au kuolewa lakini hujui kuwa anayeifungisha ndoa yenye heri na baraka ni Mungu..Sasa ikiwa umekosana na Mungu wako unatazamia vipi uwe heri katika ndoa yako unayoitazamia..Au upate wapi mwenza wa maisha aliye sahihi..Kwasababu wewe hapo ulipo tayari sio sahihi..utaishia kuoa asiyesahihi mwenzako na mwisho wake ni mlipuko.

Ni vizuri ukafanya uamuzi sahihi leo. Hizi ni siku za mwisho. Yesu yupo mlangoni kurudi..Dalili zote zinaonyesha kuwa unyakuo ni wakati wowote, Parapanda itakapolia wewe utakuwa wapi, wakati wenzako wapo mbinguni wewe utakuwa hapa chini katika dhiki kuu ya mpinga-kristo. Na baada ya hapo unaishia katika ziwa lile la moto. Kama ulikuwa hujui hili ndio kanisa la mwisho, lijulikanalo kama Laodikia, soma Ufunuo 3, Na kwanza hakutakuwa na kanisa lingine Zaidi ya hili,.Na kanisa hili ndio lililokemewa sana na Bwana Yesu kuliko makanisa mengine yaliyotangulia nyuma,.kwamba lipo vuguvugu,..Ni heri tungekuwa baridi au moto, kwasababu hiyo tumeambiwa tutatapikwa.Na tunajua matapishi huwa hayarudiwi tena. Hivyo ikifikia hatua ya wewe ndugu yangu kutapikwa, basi ujue hutakaa urudiwe tena, sehemu yako itakuwa ni katika lile ziwa la moto.

Unasubiri nini kwanini usimpe Yesu Kristo Maisha yako leo ayaokoe, Kesho inaweza ikawa isiwe yako. Nazungumza na wewe unayejiita mkristo, lakini huishi kama KRISTO, ndio maana Bwana anasema wewe ni vuguvugu…

Kama upo tayari kufanya hivyo kumpa Bwana Maisha yako…

Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU  MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Na Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Zingatia hayo na Bwana atakuwa pamoja nawe. Vilevile Usiacha kutembelea Website hii  https://wingulamashahidi.org mara kwa mara ili ujifunze maneno ya uzima..

Ubarikiwe sana.

Mada Nyinginezo:

NDOA NA HARUSI TAKATIFU.

Je! ni halali kutoa cheti kwa wakristo wanaooa?

Je! Ni halali kuoa/kuolewa na mtu ambaye tayari anao watoto?

Je! Ni sahihi kuoa/kuolewa na mtu uliyemzidi umri?

JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI AU KUTOA TALAKA?

ANTIPA SHAHIDI WANGU, MWAMINIFU WANGU.

JE ADAMU ALIKUWA NA KITOVU?

Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?

Rudi Nyumbani:

Print this post

IMANI NI NINI?

Jiunge na group la Whatsapp, ujifunze biblia na upate Neno la siku kila asubuhi. Pamoja na maswali mengi ya biblia yaliyojibiwa..kwa link hii >>>> https://chat.whatsapp.com/F1fZHcuNCB69aZsaGFpe3E

Imani ni nini? ..Je tunaweza kufikia imani ya kuhamisha milima?..Nini maaha ya mstari huu?..Warumi 10:17 “Basi imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo”.

Biblia imesema wazi nini maana ya Imani katika kitabu cha Waebrania..

Waebrania 11:1 “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana”.

Unakuwa na uhakika kwamba jambo fulani litatokea ambalo halipo sasa..Hiyo ni Imani. Na imani sio tumaini wala ujasiri..Unaweza ukawa na matumaini ya kutokea jambo fulani lakini bado usiwe na uhakika. Imani maana yake ni kuwa na uhakika…Kwamba asilimia 100 unaamini jambo fulani litatokea…Na kwamba jambo hilo ni lazima litokee..

Na Imani mtu hujiamulii kuamini tu!..Bali lazima kiwepo kitu cha kuishikilia hiyo Imani.

Kwamfano mwanafunzi ambaye amesoma kwa bidii na ameshafanya mazoezi ya kutosha huko nyuma na kuufahamu uwezo wake hivyo ujapo mtihani wa mwisho mbele yake anaamini kwamba ni lazima afaulu!..Kwanini anaamini hivyo?..Ni kwasababu ameshajiandaa vya kutosha. Hawezi tu kusema nitafaulu mtihani huu wakati hata kushika kalamu hajawahi kuiona. (Sasa huo ni mfano tu).

Tukirudi katika Ukristo ni hivyo hivyo..Mtu ili awe na Imani..Ni sharti kiwepo kitu cha kuisupport au kuishikilia hiyo Imani yake..Vinginevyo hiyo haitakuwa Imani bali tumaini.

Kadhalika katika Ukristo Mtu ili awe na Imani labda ya kuponywa ugonjwa wake na Yesu Kristo, Ni lazima awe ameshawahi kusoma au kusikia mahali kwamba Yesu anaponya..au ameshawahi kushuhudia mtu mwingine akiponywa na Yesu..au ameshawahi kuthibitisha uponyaji wa Yesu kwa kusikia ushuhuda mahali fulani….Nguvu ya Ushuhuda ule ndio unaoelezea Nguvu ya Imani mtu aliyonayo…Haiwezekani mtu ambaye hajawahi kusikia kabisa habari za Yesu kwamba ni mponyaji akawa na Imani ya kuponywa..Hiyo haiwezekani ni lazima awe amesikia kwanza..

Ndio maana Biblia inasema..

Warumi 10:17 “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo”.

Ndio maana ili kuikuza imani..Mtu anatakiwa alijue sana Neno la Mungu..Na Kulijua Neno la Mungu sio kukariri mistari ya Biblia…hapana bali kumwelewa Yesu Kristo kwa mapana na marefu na kuzifahamu shuhuda zake.

Unaposoma Neno na kukutana na Mstari ambao Yesu Kristo alimponya kipofu Batimayo katika Marko

Marko 10:46 “Wakafika Yeriko; hata alipokuwa akishika njia kutoka Yeriko, pamoja na wanafunzi wake, na mkutano mkubwa, mwana wa Timayo, Bartimayo, yule mwombaji kipofu, alikuwa ameketi kando ya njia.

47 Naye aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, alianza kupaza sauti yake, na kusema, Mwana wa Daudi, Yesu, unirehemu.

48 Na wengi wakamkemea ili anyamaze, lakini alizidi kupaza sauti, Mwana wa Daudi, unirehemu.

49 Yesu akasimama akasema, Mwiteni. Wakamwita yule kipofu, wakamwambia, Jipe moyo; inuka, anakuita.

50 Akatupa vazi lake, akaruka, akamwendea Yesu.

51 Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu wangu, nataka nipate kuona.

52 Yesu akamwambia, Enenda zako, imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani”.

Imani ni nini? Unaposoma habari hiyo na kulihifadhi tukio hilo moyoni mwako badala ya kuikariri mistari hiyo..Hapo tayari Neno la Mungu umeliweka moyoni…hata kama hujaikariri mistari hiyo…Sasa tukio hilo tayari ni Neno la Mungu na tayari ni chanzo cha Imani…Sasa unapopitia wakati wa majaribu labda umeugua kifua…Ukamwomba na ukawa hatiani kufa..Ukalikumbuka hilo tukio…na kusema moyoni kama Bwana alimponya kipofu Batimayo hata mimi nitapona tu!..Hiyo tayari ni Imani yenye chanzo sahihi cha Neno la Mungu..Hivyo italeta majibu tu! haijalishi itachukua muda gani.

Na wakati ukifika kifua hicho kikapona kulingana na Imani hiyo…Imani yako kwa Mungu itakuwa zaidi.. Hivyo hata Lijapo jaribu lingine kubwa kuliko hilo..Unatumia ushuhuda wa Bartimayo na ushuhuda wa kwako kupona kifua unazijumlisha shuhuda hizo kuangusha tatizo hilo kubwa lililokuja mbele zako hata kufikia imani ya kuhamisha milima….Lakini huwezi kuangusha tatizo lolote kubwa mbele yako au huwezi kuamini jambo kubwa kama litatoke kama huna ushuhuda wowote au Neno la Mungu kukushikilia nyuma.

Unaweza kujiuliza Daudi alitolea wapi Imani kubwa kama ile ya kumwangusha Goliathi…Hakikuwa ni kitu cha kuamka tu na kupata ujasiri! hapana..Ile Imani ilitengenezwa tangu siku nyingi…Ukisoma Biblia utaona Mungu alikuwa anamwokoa Daudi na makucha ya simba na dubu wakati anachunga…sasa mkusanyiko wa shuhuda zile ziliipandisha Imani yake na hata kufikia kusema kama Bwana ameniokoa mikononi mwa simba basi hakuna mwanadamu yoyote ambaye Bwana hawezi kuniokoa mikononi mwake. Na alipokutana na Goliathi alimwona ni mdogo kuliko simba na dubu aliokoka nao.

1Samweli 17:33 “Sauli akamwambia Daudi, Huwezi wewe kumwendea Mfilisti huyu upigane naye; maana wewe u kijana tu; na huyu ni mtu wa vita tangu ujana wake.

34 Daudi akamwambia Sauli, Mtumishi wako alikuwa akichunga kondoo za baba yake, na alipokuwa akija simba, au dubu, akamkamata mwana-kondoo wa lile kundi,

35 mimi hutoka nikamfuata, nikampiga, nikampokonya kinywani mwake; na akinirukia, humshika ndevu zake, nikampiga, nikamwua.

36 Mtumishi wako alimwua simba na dubu pia; na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu aliye hai.

37 Daudi akasema, Bwana aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Enenda, na Bwana atakuwa pamoja nawe”.

Lakini Huwezi kuwa na imani hii kabla ya kuliamini Neno la Mungu..Usipoamini kwamba Bwana Yesu ni kweli alimponya Bartimayo huwezi kuwa na Imani ya kuponywa…Usipoamini kwamba ni kweli Yesu Kristo alikuja duniani miaka 2000 iliyopita na alikuja kufa kwaajili ya dhambi zetu, na alifufuka huwezi kuwa na Imani ya kitu chochote.

Hivyo inatangulia kwanza imani ya kumwamini Yesu Kristo na maneno yake..Ukimwamini huyo ndipo Imani kwa vitu vingine itafuata na utaona mambo makubwa na ya ajabu katika maisha yako ambayo yanaonekana kama hayawezekaniki..lakini yatawezekanika kwa kumwamini Yesu Kristo.

Hivyo kama hujamwamini Yesu Kristo ni wakati wako leo… Tambua kwamba yupo, na hapo ulipo anakutazama na anakutamani uwe wake na anakuita hivyo usishupaze shingo yako..Mkubali kwa kutubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kutozifanya tena…kama ulikuwa mwasherati unaacha uasherati wako kuanzia sasahivi..kama ulikuwa ni mshabiki wa mambo ya ulimwengu huu kama miziki leo hii unaiacha yote na kama ipo kwenye simu yako ya mkononi..ifute sasahivi yote usiache hata mmoja..kama ulikuwa ni mlevi acha leo, na kama unazo pombe kwenye friji yako kazimwage sasahivi..na mkubali huyu Yesu aingie moyoni mwako.

Na ukishamwamini kwa vitendo namna hiyo..tafuta mahali ambapo unaweza kujifunze Neno la Mungu kwa ufasaha zaidi..Roho Mtakatifu atakayeingia ndani yako atakuongoza katika kweli yote..Pia hakikisha unabatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo sawasawa na Matendo 2:38. Na kwa kufuata hatua hizo utakuwa umeokoka kwa kuzaliwa mara ya pili.. Hivyo usitende dhambi tena, na Roho Mtakatifu atakupa uwezo wa ajabu wa kushinda dhambi…Na hapo utakavyozidi kudumu katika kuyasoma maneno ya Yesu Kristo Imani yako itakuwa mpaka kufikia Imani ya kuhamisha milima.

Hivyo kwa hitimisho Imani ni nini?..Ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo..na chanzo chake ni kuyaamiini maneno ya Yesu Kristo. Na maneno ya Yesu Kristo ni Yesu mwenyewe (Yohana 1:1). Ukimpokea Yesu umeyaamini maneno yake, hivyo tayari una Imani.

Bwana akubariki sana.

Tafadhali share na wengine.

+255693036618/ +255789001312


Mada Nyinginezo:

Rudi Nyumbani:

Print this post

USIWE NA HAKI KUPITA KIASI.

Shalom mtu wa Mungu karibu tujifunze Biblia…Neno la Mungu linatuambia katika kitabu cha.. Mhubiri 7:16 “Usiwe na haki kupita kiasi; Wala usijiongezee hekima mno; Kwani kujiangamiza mwenyewe?”.  Maana yake ni nini?

Hapo kuna maswali machache tunayoweza kujiuliza….Je ni kwanini inasema hivyo?..Kwani kuna ubaya gani kuwa mwenye haki kupita kiasi…Mbona ndio vizuri Zaidi kuwa mwenye haki kupita kiasi kuliko kuwa mwovu au kuwa mwenye haki kidogo?.

Ni kweli tukiusoma mstari huo kwa mantiki hiyo tunaweza kuchanganyikiwa na kuona kama biblia inajichanganya kuona sehemu moja inatuasa tuwe wenye haki na hapa inatuambia tusiwe wenye haki kupita kiasi….Lakini ukweli ni kwamba Biblia ni kitabu kilichohakikiwa na Roho wa Mungu aliye mmoja tu asiyeweza kukosea wala kufanya masahihisho..Na huyo sio mwingine zaidi ya Mungu aliyeziumba Mbingu na nchi, aliyefunuliwa ndani ya YESU KRISTO (Waebrania 1;1-2, 2Wakorintho 5:19).

Huyo hawezi kukosea embu jaribu kifiria tangu hii dunia iumbwe jua halijawahi kukosea majira yake, kwamba siku moja lichelewe lisionekane upande mmoja, au siku siku nyingine liwahi kupambazuka, miaka nenda rudi, majira yake hayabadiliki, hiyo ni kuthibitisha kuwa kazi ya Mungu haijawahi kuwa na mapungufu hata kidogo, siku zote sisi ndio tunaotazama mzunguko wa jua ili kurekebisha majira yetu, na sio jua kututegemea sisi…miungu mingine iliyotengenezwa kwa mchanga na ngano, na chokaa na vipande vya kuni hiyo ndiyo inaweza kukosea lakini si Mungu wetu Yehova tunayemwabudu kupitia Yesu Kristo kwake hakuna mapungufu..

Biblia iliposema tusiwe na haki kupita kiasi ilimaanisha…

“Tusiwe watu wa kujihesabia haki mno!”..Mtu anayejihesabia haki mno anakuwa na kiburi na kuishia kudharau wengine wote na kujiona yeye ni bora kuliko wengine..

Bwana Yesu aliwaona mafarisayo na masadukayo kwamba ni watu wenye kujihesabia haki mno.

Luka 18:9 “ Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote.

10  Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru.

11  Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.

12  Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote.

13  Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.

14  Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa”.

Umeona?..Haki yetu haipaswi kuzidi mipaka hiyo hadi kufikia hatua ya kujikweza na kuwa na kiburi na kuwadharau wengine wote…Elimu yetu ya dini isitufanye tujione tu wenye haki kuliko wengine wote…karama zetu zisitufanye tujione sisi ni bora mbele za Mungu kuliko wengine wote…hata usafi na utakatifu tulio nao usizidi mipaka ya kujiona tu wenye haki saana!..tukifanya hivyo tutakuwa tu wenye haki kupita kiasi. Kadhalika kama tuna hekima ya ki-Mungu basi tusijione ni wenye hekima sana ya Neno la Mungu kiasi kwamba hakuna kama sisi, wala hakuna mtu yeyote anayeweza kutuongezea  kitu…tukifanya hivyo tutakuwa tumejiongezea hekima kupita kiasi!..na hivyo tutajiangamiza wenyewe.

Mhubiri 7:16 “Usiwe na haki kupita kiasi; Wala usijiongezee hekima mno; Kwani kujiangamiza mwenyewe?”.

Mafarisayo na Masadukayo walijiangamiza wenyewe kwa haki yao iliyozidi na kujiona kwao wanajua maandiko kuliko wengine wote..Mwishowe wakajikuta badala ya kumwamini Mwokozi wa ulimwengu wakajikuta wanampinga na hata kwenda kumwua.

Kadhalika wewe ni Mchungaji, au Nabii au Mhubiri au Mwalimu au Una Neno la Hekima na Maarifa, au una karama ya uponyaji, au Imani au miujiza au ni Muumini ambaye kuna Neema ya kipekee ambayo Mungu kakukirimia ambayo inaweza kukutofautisha wewe na wengine kwa sehemu Fulani au popote pale ulipo…Neno hili usilisahau…“USIWE MWENYE HAKI KUPITA KIASI”. Kila siku jione wewe si kitu mbele za Mungu..ni kwa Neema tu za Mungu upo kama ulivyo na si kwa haki yako..wala kwa nguvu zako binafsi,. Haki yako isizidi mipaka na kujiona ni kwa jitihada zako umestahili kuwa hivyo ulivyo..Hakuna anayestahili hata mmoja wote ni makapi tu! tumechaguliwa na kuokolewa kwa Neema..hivyo hakuna cha kujisifia..

Waefeso 2:8  “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; 9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu”

Bwana akubariki.

Kama bado hujaokoka!..Dunia  hii inakwenda kuisha..Kipindi sio kirefu sana Dunia itakwenda kushuhudia mabadiliko makubwa ya ghafla!..Ghadhabu ya Mungu itamwagwa duniani kote na wale wote waliomkataa Mwana wa Mungu Yesu Kristo, wataangamizwa kwa maangamizo makubwa yasiyoelezeka kasome Ufunuo 16. Hivyo unyakuo upo karibuni sana kutokea ambapo watakatifu (Yaani wale wote waliompokea Yesu Kristo na kuishi maisha ya utakatifu) watanyakuliwa na kwenda mbinguni kwa Bwana kuipisha ghadhabu hiyo kupita. Je wewe utakuwa wapi?..kama leo hii bado unamkataa Kristo?..kama leo hii bado ni mlevi, ni mwasherati, mtazamaji wa picha chafu, mchatiji wa mambo machafu mitandaoni, mfanyaji masturbation, mtukanaji, mtoaji mimba, mvaaji nusu uchi, mpakaji malipstick, mvaaji mawigi, masuruali n.k?..Siku hiyo utakuwa wapi?

Leo isikupite kabla hujageuka, biblia inasema saa ya wokovu ni sasa..Unachopaswa kufanya hapo ulipo ni kujitenga peke yako, na kupiga magoti na kuomba toba mbele za Mungu..Mwombe Mungu akusamehe dhambi zako leo..na yeye ni mwaminifu atakusamehe..Baad a ya Toba hiyo anza leo kubeba msalaba wako na kumfuata Kristo..Futa leo miziki yote ya kidunia iliyopo kwenye simu yako na picha zote za uchafu pamoja na namba za wanaume/wanawake uliokuwa unachat nao..kadhalika kachome nguo zote fupi ulizonazo pamoja na vipodozi vyote na suruali..baki kama ulivyo katika uhalisia wako. Na mambo mengine yote yasiyompenda Mungu uliyokuwa unayafanya.

Ukishafanya hivyo..basi utakuwa umemwonyesha Kristo kwamba umeamua kweli kumfuata yeye kwa matendo yako..Na yeye akishaona hivyo..Neno lake linasema “Yoyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe Yohana 6:37”. Hivyo atakuwa na wewe na utasikia Amani ya ajabu ambayo hujawahi kuisikia hapo kabla..

Na baada ya kumgeukia Yesu kwa vitendo namna hiyo..haraka sana katafute mahali ambapo unaweza kuukulia wokovu..na pia kubatizwa kama hukubatizwa..Kumbuka Ubatizo sahihi ni muhimu na ni ule wa maji mengi (Yohana 3:23) na wa Jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38). Na Roho Mtakatifu ndani yako atakusaidia kupembua mema na mabaya baada ya hapo na kuendelea..atakuongoza mpaka kufikia utimilifu na Zaidi ya yote atakuwezesha kushinda dhambi na vishawishi vyote vya huu ulimwengu, na yale mambo maovu yaliyosalia ndani yako ambayo kwa nguvu zako ulishindwa kuyaondoa, yeye atayashughulikia yote..

Ukifanya hivyo kwa dhati kabisa utakuwa umezaliwa mara ya pili..na kuwa miongoni mwa wateule wapendwao na Bwana..Na hata unyakuo ukipita leo, nawe utakuwa miongoni mwa wale watakokwenda kuishuhudia karama ya mwana-kondoo ambayo Kristo alikuwa amekwenda kutuandalia kwa miaka elfu mbili sasa.

Maran atha.

Tafadhali share na kwa wengine


Mada Nyinginezo:

CHACHU YA MAFARISAYO NA CHACHU YA HERODE.

NGUVU ILIYOPO KATIKA MAAMUZI.

NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.

DUNIANI MNAYO DHIKI.

kanisa la kwanza duniani ni lipi?

IELEWE SAUTI YA MUNGU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

MARIAMU AKUTANA NA ELISABETI.

Njia za Mungu hazichunguziki, Mariamu akutana na Elisabeti..Elisabeti katika uzee wake aliambiwa atapata mimba, wakati ambao kizazi kimeshanyauka. Je! Ni nini tunaweza kujifunza hapo?.

Nakusalimu katika jina kuu la Emanueli, Bwana wetu YESU KRISTO.

Wakati tukiwa katika kipindi hichi cha Krisimasi na kufunga mwaka. Napenda tufunge kwa kuwatazama wanawake hawa wawili Mariamu na Elisabeti. Wanawake hawa wanawakilisha makundi mawili ya Watoto wa Mungu ambao wapo tayari kupokea baraka zao hivi karibuni.

Kama tunavyojua walikuwa ni wanawake waliokuwa wanamcha Mungu, mmoja alikuwa ni mzee sana, na mwingine alikuwa bado ni kijana mdogo. Lakini cha ajabu ni kuwa kila mmoja alipokea ripoti ambayo ilikuwa ni kinyume na matarajio yake.

Elisabeti katika uzee wake aliambiwa atapata mimba, wakati ambao kizazi kimeshanyauka, na mayai ya uzazi hayapo, wakati ambapo mawazo ya kuwa na mtoto kichwani yameshafutika, Anachosubiri ni kifo tu, lakini ghafla anapokea ripoti kutoka kwa malaika Gabrieli kuwa atazaa mtoto mwanamume, na sio tu mtoto ilimradi mtoto bali mtoto ambaye atakuwa mkuu sana Luka 1:15).

Tukirudi upande wa pili wa Mariamu, yeye naya akiwa bado binti mdogo tu, ndio kwanza amechumbiwa..Akiwa bado hata hajamkaribia mwanamume, hata mawazo ya kuwa na mtoto hayajaingia kichwani mwake. Lakini tunaona hapa yeye naye anapokea ripoti ya ghafla kutoka kwa malaika yule yule Gabrieli kuwa atapata mimba. Naye atazaa mtoto, naye si mtoto ilimradi mtoto tu, bali atakuwa mfalme mkuu, ambaye ufalme wake utakuwa hauna mwisho.

Mariamu apolisikia hivyo hakukawia, alifunga safari kwenda kwa Elisabeti kuusikiliza ushuhuda wake, huku naye pia akiwa na ushuhuda wa kumweleza wa kwake.. shauku ilimjaa sana..

Jaribu kufikiria walipokutana walianza kuzungumza maneno gani..Mmoja atasema, nilidhani mpaka nitakapokutana na mwanamume ndio nitapata ujauzito, mwingine atasema, nilidhani wakati nilipokuwa na mwanamume, wakati ambao mayai yangu yakiwa tumboni ndio ningepata ujauzito..Lakini sasa wakati ambapo hatukutegemea hapo ndipo Mungu alipotuonekania..

Hata wewe leo ambaye umeokoka, unaweza ukajiona bado ni mchanga, bado ni mdogo Mungu kukutimizia malengo yako, unaweza ukadhani mpaka Bwana anitumie katika kazi yake ni lazima ufikie umri wa makamo, Au mpaka ufanikiwe ni lazima uwe umemaliza shule kwanza, au umefanya kazi miaka kadhaa, au umefikisha umri fulani.. Nataka nikuambie ondoa mawazo hayo kichwani kwako ikiwa wewe ni mtoto wa Mungu…

Njia za Mungu hazichunguziki, Mariamu hakuwahi kufikiria kuwa angewahi kubeba ujauzito kabla ya kukutana na mwanamume..Lakini iliwezekana kwasababu Gabrieli alimwambia hakuna linaloshindikana kwa Mungu..(Luka 1:37)

Vivyo hivyo na wewe. Neema hiyo Bwana anaweza akaishusha juu yako, ni nani ajuaye itakuwa katika huu mwaka unaonza 2020, atakuwa tayari ameshakupigisha hatua kubwa katika utumishi wako?, katika huduma yako?..ukawa msaada kwa wengi.. Kama ulikuwa nawe ni Tasa, Bwana akakupatia mtoto kama Elizabeth…Na Katika Maisha yako pia?, ukawa na nyumba yako mwenyewe, ukawa na biashara zako mwenyewe? Angali bado ni mdogo, angali hujasoma, angali bado hujaoa au hujaolewa? ..Lakini hiyo yote ni kama utakuwa katika mstari wa kutembea katika mapenzi ya Mungu..

Vilevile mwingine unaweza ukajiona, muda umeshakwenda sana, umri umesogea, ukiangalia kile ulichokuwa unakiongojea kwa muda mrefu hakijakufikia kwa wakati, mpaka sasa hujapiga hatua inayoonekana kwa macho, bado huna kwako, bado kula ni kwa shida..Ukiangalia hata useme ukaanze kutafuta bado utakuwa umechelewa, ni kama vile umeshajikatia tamaa kila kitu..Nataka nikuambie hata Elisabeti alidhani hivyo katika uzee wake, lakini wakati ulipofika wa yeye kupata mimba ya shujaa wa Imani aliyeitwa Yohana Mbatizaji ambaye Bwana Yesu alimshuhudia kuwa katika uzao wa wanawake hakuwahi kutokea aliye mkuu kama yeye, yaani kwa namna nyingine hata akina Musa, na Eliya na manabii wote hakuna hata mmoja aliyemzidi kwa ukuu Yohana Mbatizaji kule mbinguni..

Vivyo hivyo na wewe uliyeokoka ambaye kwa muda mrefu unaona kuna utasa katika huduma yako au biashara yako, au kazi yako..Ni nani ajuaye kipindi hichi ndicho Mungu anatungisha mimba hiyo ya mafanikio yako. Na mpaka mwaka kesho unaisha unakuwa umeyafikia malengo na kuvuka hata Zaidi ya matarajio yako?

Wagalatia 4:27 “Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na mume”.

Lakini hiyo yote inakuja ikiwa upo katika mstari ulionyooka wa kuyatenda mapenzi ya Mungu kama alivyokuwa Elisabeti biblia inavyosema alikuwa mtu wa Haki, akienenda katika amri zote za Mungu bila lawama (Luka 1:6).

Lakini kama upo nje ya Kristo. Usitegemee miujiza ya Mungu kama hii kuja katika Maisha yako..Ni vizuri ndugu uumalize mwaka wako na Bwana, Ili ukifungua mwaka mpya, Bwana naye aanze na wewe.. Na akishaanzana na wewe, anaanzana na wewe kweli kweli Kama vile tulivyoona hapo juu, njia za Mungu hazichunguzi, unaweza kusema bado sana, kumbe ni wakati wenyewe..Unaweza kusema nimechelewa kumbe ndio wakati wa kufarijiwa

Unachopaswa kufanya ni kuyasalimisha Maisha yako kwa Bwana..Na hiyo inakuja kwa kutubu kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi zako zote bila kubakisha hata moja, kama ulikuwa ni mlevi leo hii unasema basi, kama ulikuwa ni mzinzi leo hii unasema inatosha, kama ulikuwa unaishi na mke au mume ambaye si wako leo hii unaaacha, kama ulikuwa unatapeli watu unasema sitaki tena mambo hayo nataka nianze mwaka wangu upya na Bwana..Na hutubu kwasababu unataka uwe na gari au nyumba..unatubu kwasababu umeona maisha yako yanamhitaji Yesu Kristo, na hayatoshi bila yeye.

Sasa ikiwa utakuwa umefanya hivyo kwa moyo wako wote, na umemaanisha kumgeukia Kristo kikweli kweli fahamu kuwa Mungu atauona moyo wako, na akishauona umegeuka basi yeye mwenyewe atakuwa ameshakusamehe na atakuwa na jukumu la kukuvuta kwake Zaidi kwa nguvu ya ajabu sana..Atakuvika uwezo wa kipekee wa kufanyika mwana wa Mungu ,(Yohana 1:12) Na uwezo huo ndio utakaokufanya uweze kuyashinda yale yaliyosalia yaliyokuwa magumu kuyashinda na kudumu katika wokovu.

Vilevile ukishafanya hivyo ili kuukamilisha wokovu wako, tafuta kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamwishwa katika maji mengi (Yohana 3:23) na kwa jina la YESU KRISTO sawasawa na Matendo 2:38, Na baada ya hapo Roho Mtakatifu atakuwa na wewe daima, Mpaka siku ya kufa kwako, ikiwa unyakuo utakuwa bado haujapita. Na baraka zote hizo ambazo Mungu anazileta nje ya matarajio yetu kwa Watoto wake wote wampendao zitaachiliwa na juu yako wewe uliyeokoka.

Bwana akubariki sana. Tafadhali “Share” na wengine ujumbe huu.

Shalom.


Mada Nyinginezo:

MWAKA WA BWANA ULIOKUBALIWA.

YOHANA MBATIZAJI

Mungu anasema hatagharikisha dunia na maji tena,.Kwanini watu wanasema dunia itaangamizwa?

FREEMASONS NI NINI? NA MTU ATATOKAJE HUKO?

UMEFUNULIWA AKILI?

Sanduku la Agano lilikuwa linawakilisha nini katika Agano jipya?

Rudi Nyumbani:

Print this post

UWEPO WA BWANA HATA KATIKATI YA MATESO.

Shalom…Jina la Bwana, libarikiwe..Karibu tuzidi kujifunza Neno la Mungu…Ambalo ni Taa iongozayo miguu yetu na mwanga wa njia zetu. (Zaburi 119:105).

Leo tutajikumbusha namna Mungu anavyotenda kazi ili tusijikute tunaingia kwenye manung’uniko pale tunapojikuta tunapitia hali fulani tofauti na vile tulivyoitegemea…Kama wengi wetu tujuavyo Maisha ya Yusufu kwenye Biblia yamebeba funzo kubwa sana ya jinsi gani Mungu anaweza kumtoa mtu aliyekata tamaa katika mateso na kumnyanyua juu tena.

Lakini pamoja na hayo kuna jambo la Muhimu la kujifunza juu ya Yusufu…Ukitazama katika hatua zote Yusufu alizopitia utagundua kuwa Mungu alikuwa naye hakumwacha…

Utaona wakati yupo nyumbani kwa Potifa..japokuwa alikuwa ni mtumwa ndani ya ile nyumba lakini Mungu alimfanikisha kila alilolifanya lilifanikiwa….Akiwa ndani ya nyumba ile pengine mifugo aliyopewa aisimamie na Bwana wake ilizaliana na kuwa na afya Zaidi kuliko ya wafanyakazi wengine…Pengine shamba alilopewa alisimamie lilikuwa linazaa Zaidi ya watumwa wengine…pengine kila alilotumwa na Bwana wake Potifa lilikuwa linafanikiwa..tofauti na wanapotumwa watumwa wengine n.k…Hivyo Potifa Bwana wake aliliona hilo ndipo akaamua kumweka juu ya kila kitu chake kwasababu aliona kijana ana Neema ya mafanikio.

Mwanzo 39:2 “Bwana akawa pamoja na Yusufu, naye akasitawi; naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule Mmisri.

3 Bwana wake akaona ya kwamba Bwana yu pamoja naye, na ya kuwa Bwana anafanikisha mambo yote mkononi mwake.

4 Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake.

5 Ikawa tokea wakati alipomweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na vyote vilivyomo, Bwana akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Mbaraka wa Bwana ukawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba.

6 Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa Yusufu; wala hakujua habari za kitu cho chote chake, ila hicho chakula alichokula tu”.

Vivyo hivyo…hata baada ya Yusufu kupachikiwa kesi ya jaribio la ubakaji…alipokuwa mule gerezani Mungu aliendelea kuwa naye…Na yale yale aliyoyaona Potifa kwa Yusufu..Mkuu wa gereza naye akayaona kwa Yusufu..akaona mbona tangu huyu kijana amekuja humu gerezani utaratibu wa gereza umebadilika…mambo yanakwenda vizuri…Na alipojaribu kumweka kuwa kiongozi wa wafungwa ndio mambo yalivyozidi kunyooka Zaidi, usumbufu wa wafungwa ulipungua…pengine alitamani hata Yusufu angeendelea kuwa mfungwa siku zote jinsi mambo yanavyokuwa yanakwenda vizuri mule gerezani.

Lakini ni nini tunaweza kujifunza hapo?…Hata katika hali ya utumwa na vifungo Mungu yupo na watu wake… Wengi hawalijui hilo?..wanadhani kama ni mkristo ukishapitia kwenye matatizo basi huo ni uthibitisho tayari Mungu kashakuacha…. Kitendo tu cha wewe kuwa mtumwa wa mwingine basi Mungu hayupo na wewe hivyo unahitaji maombi ya kufunguliwa…kitendo tu cha kufanya kazi ya kusafisha barabara basi upo chini ya laana na vifungo…Kuuza genge basi wewe ndio huna roho ya mafanikio Huo ni uongo wa shetani.

Hufanyi kazi wizarani lakini unafanya kazi katika nyumba ya mtu kama kijakazi…Kazi hiyo siyo uthibitisho kwamba Mungu hayupo na wewe…yupo na wewe huko huko kama alivyokuwa na Yusufu katika nyumba ya Potifa maadamu unajua umeokoka na unaishi kulingana na Maneno ya Yesu Kristo basi uwe na amani uwepo wa Bwana upo na wewe…Yusufu hakuwa na laana ya ukoo yeye kuuzwa utumwani…Alikuwa ni mwana wa Ibrahimu aliyebarikiwa….

Hivyo Kuwa tu mnyenyekevu usinung’unike ni suala la muda tu…utafika wakati utapelekwa hatua nyingine…lakini wewe tazama tu..kama kiongozi wako anapenda kuwa na wewe…na anaona anapata raha kuwa na wewe..na anafanikiwa sana anapokuwa na wewe kuliko alivyokuwa na wengine huko nyuma na hataki uondoke huo ni uthibitisho kwamba Mungu anafanikisha mambo yake kwaajili yako wewe…kama ilivyokuwa kwa Yusufu…Hivyo kuwa mnyenyekevu bado uwepo wa Bwana upo na wewe ni suala la muda tu…Usianze kusema anakutesa au anakutumia wewe kupata faida zake mwenyewe, wewe kuwa mtulivu endelea kuwa mwaminifu kama Yusufu.

Mungu hakushindwa kumtoa Yusufu nyumbani kwa Potifa na kwenda kumpa kwake binafsi na ambariki lakini alimbakisha pale pale kwa Potifa kwa kusudi maalumu.…Na Mungu hakuvifanikisha vitu vya Yusufu bali alivifanikisha vitu vya Potifa kwaajili ya Yusufu…Alifanikisha mifugo ya potifa na si ya Yusufu..ingawa chanzo cha baraka hizo ilikuwa ni Yusufu…Kadhalika aliistawisha kazi ya mkuu wa Gereza na si Yusufu..

Lakini ulipofika wakati, siku, tarehe, mwezi na Mwaka katika kalenda za kimbinguni…Njaa ilikuwa imekusudiwa duniani kote…na kwamba kwa kupitia mtu mmoja Yusufu dunia yote ilipaswa ipate Neema…Ndipo wakati wa Yusufu ulifika….Sasa hebu jaribu kufikiri endapo Mungu angemfungua Yusufu awe huru wakati wa Potifa na Mungu na kwenda kukaa kwake na kujenga nyumba nzuri na kumstawisha na kumbariki…je! huo wakati wa njaa ungefika na Yusufu na utajiri wake wote angekuwa wapi?..si na yeye angekufa na njaa tu kama wengine au angeuza kila kitu chake anunue chakula kama wengine?…manyumba yake yangekuwa wapi saahiyo?..mifugo yake ingekuwa wapi saahiyo?..Baba yake huko alikokuwa amemwacha Mungu alimbarikia katika mifugo na mali nyingi lakini pamoja na baraka zote hizo kutoka kwa Mungu walifunga safari kwenda Misri kutafuta chakula…unadhani endapo na Yusufu asingepitia hatua hizo angesalimika vipi na hiyo njaa ambayo imeikumbwa dunia?.

Kwahiyo wakati wa Mungu ni bora kuliko wakati mwingine wowote!..Na huo si mwanadamu anauamua..bali ni Mungu mwenyewe anaupanga mbinguni…tunachopaswa sisi kufanya ni kujinyenyekeza kila siku chini ya kusudi lake na kuishi Maisha yasiyo ya manungu’uniko tukijua kuwa uwepo wa Bwana bado upo na sisi…Usiseme mimi sasa nauza hiki au kile ningepaswa niwe kule au kama yule…Usiseme hivyo, jiangalie je! Unakwenda sawa na Mungu katika unachokifanya kama Yusufu?.. huku ukifahamu kuwa hata katikati ya dhiki, au katikati ya shida, au katikati ya misiba, au katikati ya utumwa mgumu, au katika ya kukandamizwa…Mungu yupo pamoja na sisi na anatuwazia yaliyo mema…

Endao tukiwa waaminifu kuishi katika Neno lake Kila mahali Mkono wa Mungu upo na sisi kutuongoza..hakuna tutakapopitia yeye asiwe pamoja na sisi biblia inasema hivyo…

Zaburi 139:5 “Umenizingira nyuma na mbele, Ukaniwekea mkono wako.…….7 Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako?

8 Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.

9 Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari;

10 HUKO NAKO MKONO WAKO UTANIONGOZA, Na mkono wako wa kuume utanishika.

11 Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku;

12 Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa.”.

Hivyo nakutia moyo wewe uliyeamua kujikana nafsi na kuukataa ulimwengu na kumfuata Yesu Kristo kwa gharama zozote, amesema yupo na wewe ni kweli yupo na wewe Neno lake si uongo Uwepo wa Bwana utakuwa nawe siku zote….Zidi kumtegemea, zidi kumwamini, ishi Maisha ya furaha, usijifananishe na wengine..Bali mtazame Mungu katika mambo yako yote. Na mambo yote Mungu atayafanikisha mbele zako kwa wakati wake.

Bwana akubariki.

Mada Nyinginezo:

TWEKA MPAKA VILINDINI.

KAMA MUNGU ANABORESHA KAZI ZAKE, KWANINI WEWE USIBORESHE ZA KWAKO?.

UTHABITI WA AGANO LA MUNGU KWA MKRISTO.

UPAKO NI NINI?

Nini maana ya maneno haya ya Bwana? “Nami nikiinuliwa juu ya nchi,NITAWAVUTA WOTE KWANGU”(Yohana12:32).

Rudi Nyumbani:

Print this post

ANTIPA SHAHIDI WANGU, MWAMINIFU WANGU.

Vitabu vilivyothibitika vya historia vinavyoeleza maisha na vifo vya watakaifu wengi wa kwanza vinaeleza kuwa Antipa alikuwa ni kasisi aliyeteuliwa na mtume Yohana, kuwa mwangalizi wa kanisa lililokuwa Pergamo. Kama vile Timotheo alivyowekwa na Mtume Paulo kuwa mwangalizi wa makanisa yote baada yake.

Ikumbukwe kuwa kipindi hicho ndio wakati ambao kanisa la kwanza la Kristo lilikuwa katika kilele cha dhiki ambacho kiliasisiwa na mtawala katili wa kirumi aliyeitwa Nero (54 W.W -68 W.W)..

Nero ndiye aliyehusika kwa kumwagika kwa damu ya mashahidi wengi wa Kristo katika kanisa la kwanza. Na hiyo ilisababishwa na tukio la moto usiojulikana chanzo chake ni nini kuzuka huko Rumi mjini, na kusingiziwa wakristo ndio waliousababisha moto huo..Hivyo marufuku ikapigwa kwa mtu yeyote kujihusisha na imani ya kikristo.

Kipindi hicho mtu yeyote ambaye alionekana anaishikilia imani ya kikristo adhabu yake ilikuwa ni kifo na kama hutakufa basi utafungwa na kupelekwa uamishoni. Mtume Yohana baada ya kukwepa majaribio mengi ya kifo kimiujiza walimshika na kwenda kumfunga katika kisiwa cha Patmo. Huko ndipo Mungu alipompa ufunuo wa kitabu cha Ufunuo.

Na katika moja ya barua alizopewa azirudishe kwa yale makanisa 7, ndani yake Kristo alimkumbusha juu ya mtu aliyemfahamu anayeitwa Antipa..

Tusome:

Ufunuo 2:12 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili.

13 Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani”.

Unaona Antipa alikuwa ni mtu aliyethibitika katika imani, japo alikuwa katikati ya vita vikali vya imani kama vile vya kuuawa na kuteswa, lakini hakuacha kuihubiri injili kwa nguvu. Katika utumishi wake alifanikiwa kuwageuza watu wengi wa mji ule kuacha kutoa sadaka kwa miungu , na masanamu. Lakini makuhani wa kipagani wa Rumi, walipomwona anawavuna watu wao wengi, na kuiacha Imani yao. walimfuata na kumkataza asiwafundishe watu imani za miungu migeni katika jamii yao. Na asiingilie miungu yao. Kama tu ilivyokuwa kwa Mtume Paulo alipofika kule Efeso, na kuwahubiria watu habari ya Kristo, wale wachonga vinyago walipoona biashara yao inakaribia kufa, walizusha vurugu katika mji.(Matendo 19:24)

Lakini Antipa hakusita kuwaambia bila kuogopa.. Alisikika akiwaambia

“mimi siyatumikii mapepo ambayo yanaweza kunikimbia, yasiyo na maisha ya milele, mimi ninamwabudu Mungu muweza yote, Na nitaendelea kumwabudu Mungu muumba wa vyote, katika Kristo Yesu na Roho Mtakatifu siku zote za maisha yangu”.

Wale makuhani wakamjibu, na kumwambia mungu wetu sisi alikuwepo tangu zamani, lakini nyie mnamuabudu Yesu ambaye aliuliwa na Pontio Pilato kama uhalifu.

Lakini Antipa naye hakuacha kuwajibu..

“miungu yenu ya kipagani ni kazi ya mikono ya watu ambayo ndani yake kinachozaliwa si kingine zaidi ya maovu na machafuko”.

Antipa aliendelea kwa ushujaa huo huo kuikiri imani yake katika YESU KRISTO bila woga mbele zao daima. Wale makuhani wa kipagani walipoona mtu huyu hana dalili ya kuacha kumuhubiri Kristo, na kuwafundisha watu wasiabudu sanamu, uzalendo ukawashinda wakamkamata na kumpeleka mbele Ya hekalu la mungu wao Artemi. Wakamtupa ndani ya tanuru la moto jekundu la shaba ambalo walikuwa wameliandaa kwa ajili ya kutengeneza ng’ombe wao kwa shaba ile.wakamtupa ndani mule.

Wakati akiwa ndani ya moto ule mkali alisikika akiomba, akisema Mungu ipokee roho yangu. Na pia ziimarishe imani za wakristo wote. Kisha akalala katika usingizi wa amani kama ule wa Stefano.

Usiku ulipofika, ndugu zake wa imani wakaja kumchukua na kwenda kumzika  pembezoni mwa mji huo wa Pergamo.

Siku zikapita siku zinakaenda, pengine akasahaulika na wengi lakini siku moja baada ya miaka kadhaa mbele, Mtume Yohana akiwa katika kisiwa cha Patmo.. alimsikia Yesu Kristo akimtaja kwa maneno haya:..

Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu”..

Hadi sisi leo hii tunazisoma na kuziandika habari zake.

Mtume Paulo aliandika hivi juu ya watu hawa:

Waebrania 11:36 “wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani;

37 walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya;

38 (watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi.

39 Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi;

40 kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi”.

Kisha akamalizia na kusema..

Waebrania 12:1 “Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na WINGU KUBWA LA MASHAHIDI namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu”.

Tunapokuwa wakristo halafu bado tunashikilia mizigo ya vimini, mizigo ya makeup, mizigo ya nguo za kikahaba, mizigo ya uchawi, ushirikina, uzinzi na hasira… tutawezaje kupiga mbio kwa spidi kama hawa watu waliojikana nafsi siku ile?. Ikiwa leo hii mizigo ya uzinzi bado tunaishikilia, mizigo ya mustabation, mizigo ya betting, mizigo ya usengenyaji, mizigo ya rushwa, mizigo ya shughuli za ulimwengu huu zisizotupa hata nafasi ya kumfanyia Mungu ibada..Tutaweza siku ile kufananishwa na kundi hili la watu?.

Bwana hana upendeleo, kile apandacho mtu ndicho atakachovuna.. Mungu atusaidie sana tupande kilichochema, ili siku ile tuvune kilichochema. Tuitumie mizigo yetu. Tumtazame Kristo.

Ikiwa hujampa Kristo Maisha yako!..Nataka nikuambie haijalishi utakufa kifo cha heshima kiasi gani na kuzikwa na watu wengi kiasi gani…Kumbukumbu lako litakuwa limeishia hapo hapo hakuna mtu atakukumbuka wala Mbingu haitakukumbuka…lakini Ukitubu na kumwishia Kristo leo, ukasema kuanzia leo mimi ni anasa basii,..mimi na ulevi basii mimi na uasherati basii..ukaonyesha kwa vitendo kabisa kwamba umeachana na hivyo vitu…

Basi Yesu Kristo atakusamehe kama alivyosema katika Neno lake..na hata ukifa leo hii kumbukumbu lako halitasahauliwa kama Antipa..na Bwana atakupa kipawa cha Roho wake mtakatifu atakayekusaidia kushinda dhambi ulizokuwa unashindwa kuzishinda..na atakuongoza na kuijua kweli yote ya maandiko..Ikiwa upo tayari kufanya hivyo..hapo ulipo tubu na Bwana atakusamehe.

Ubarikiwe sana..

Mada Nyinginezo:

VIFO VYA MITUME WA YESU/ JINSI MITUME WALIVYOKUFA.

TUMEPEWA, SI KUMWAMINI TU KRISTO, ILA NA KUTESWA KWA AJILI YAKE;

ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.

SIKU ILE NA SAA ILE.

WAMNGOJEAO BWANA WATAPATA NGUVU MPYA.

 

Rudi Nyumbani:

Print this post