Yearly Archive 2020

MTU ASIYE PAMOJA NAMI YU KINYUME CHANGU.

Jina kuu la Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe…Karibu tena tujifunze maandiko…kwa kuwa jukumu kuu tulilonalo kila siku ni kumjua sana Yesu Kristo mwana wa Mungu na kuhakiki kila siku ni nini kimpendezacho sawasawa na Waefeso 4:13 na 5:10.

Leo tutayatafakari maneno ya Bwana Yesu Kristo aliyoyasema katika kitabu cha Mathayo.

Mathayo 12:30 “Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya”.

Ukianzia mstari wa juu kidogo utaona kuna tukio Fulani lilifanyika ambapo likamsababisha aseme hayo maneno..Lakini tukiyatafakari maneno hayo kwa undani tunaweza tabia mojawapo ya Mungu na hivyo kuchukua tahadhari kwa kila tunachokifanya..

Sasa mstari huo Bwana Yesu anasema… “Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu”…na… “Mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya”..Hizo ni sentensi mbili zinazozungumzia kitu kimoja.

Nimewahi kukutana na mtu anasema mimi simwamini Bwana Yesu lakini natenda haki, nasaidia maskini, sinywi pombe, siibi, situkani n.k..Je Mungu atanihukumu kwa sababu tu simwamini Yesu Kristo?..Mwingine atakuambia mimi simwamini Yesu lakini nampenda na namuheshimu na simpingi…..Nataka nikuambie ndugu yangu..kitendo tu cha wewe kutokuwa upande wa Yesu Kristo hata kama unatenda mema kiasi gani..mbele zake tayari upo kinyume chake..haijalishi unafanya mema mengi kiasi gani..kitendo tu cha wewe kujiepusha na yeye tayari upo kinyume chake..roho ya mpinga-kristo ipo ndani yako. Tayari unahesabika kama mtu unayempinga Kristo ..kwasababu anasema.. “Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu”

Kadhalika kama huifanyi kazi ya Mungu na umepewa hiyo neema…na unasema “aa mimi sifanyi kazi ya Mungu lakini siipingi kazi ya Mungu”…Nataka nikuambie kitendo tu cha wewe kutoifanya kazi ya Mungu na huku umepewa hiyo Neema…mbele zake unaonekana unaitapanya kazi yake…kwasababu anasema “Mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya”..Na wewe hukusanyi pamoja na Mungu, hivyo ni wazi kuwa unakusanya sehemu nyingine ambayo inakinzana na Mungu..Kitendo cha wewe kukataa kuifanya kazi ya Mungu na kuendelea kufanya mambo yako mengine, tayari unaiharibu kazi ya Mungu…Kwahiyo kuna madhara makubwa ya kukaa kutokuifanya kazi ya Mungu..kwasababu mbele zake tunaonekana kama tunaitapanya.

Ndio maana kuna mfano mmoja Bwana aliutoa na kusema..

Luka 13:6 “Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate.

7 Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, MBONA HATA NCHI UNAIHARIBU?

8 Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi;

9 nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate”.

Nataka uuone huo mstari unaosema ..“Mbona hata nchi unaiharibu”..Maana yake ule mti ambao hauzai matunda kitendo tu cha kuendelea kuwepo pale tayari unaiharibu nchi/ardhi. Unaweza kusema si ubaki tu kwani usipozaa unaathari gani? …Biblia inasema “kwa kuendelea kuwepo pale unaiharibu nchi”.

Vivyo hivyo kuwepo kwako kama hufanyi kazi ya Mungu basi fahamu kuwa Unaiharibu kazi ya Mungu bila kujua…Kuwepo kwako kama hufanyi mapenzi ya Mungu basi unaiharibu kazi ya Mungu…kadhalika unaishi maisha ya kuvaa nusu uchi,kuvaa suruali na nguo zinazobana na fupi, na kupaka lipstick, wanja, kuvaa mawigi na hereni ni kweli una moyo mzuri unasaidia watu, una huruma na wakati mwingine unakwenda kanisani, na wala hutukani, wala huibi, …ni kweli unafanya mambo mazuri mengi lakini kwa mavazi yako unaiharibu kazi ya Mungu..kwasababu wakati Roho wa Mungu anafanya kazi kwa nguvu kuwahubiria watu waepukane na mavazi hayo ya kikahaba na mambo ya kidunia..wewe unafanya kazi ya kuwahubiria waendelee kuvaa kwa jinsi wanavyokuona wewe unavyoyavaa,…

Wakati Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa nguvu kuwaonya watu waache kupaka hivyo vitu usoni na kichwani na wajiepushe na hukumu inayokuja…wewe unawahubiria mambo hayo ni sahihi kufanya kwa jinsi unavyoendelea kuyafanya….Hivyo unakwenda kinyume na kazi ya Mungu (unaiharibu kazi ya Mungu…) “Unakuwa hukusanyi pamoja na Kristo bali unatapanya”.. na hivyo unahesabika kwamba upo kinyume na Kristo (yaani mpinga-kristo)…haijalishi unafanya mema mengi kiasi gani.

Bwana akubariki.

Kama hujaokoka, mlango wa Neema upo wazi fanya hivyo leo..Tunaishi katika siku za mwisho, na Siku yoyote parapanda inalia, na watakatifu watanyakuliwa kwenda mbinguni..Na biblia inasema “ufalme wa Mungu unapatikana kwa nguvu”..Nao wenye nguvu ndio watakaouteka…Hivyo si wakati wa kujivuta vuta tena, Si wakati wa kuhubiriwa injili ya kubembelezwa..ni wakati wa kujitwika msalaba wako na kumfuata Kristo pasipo kuangalia nyuma au kuangalia ndugu au Rafiki anasemaje.

Hivyo unachopaswa kufanya sasa ni kutubu kwa kumaanisha kabisa…maana yake unaacha maisha yote ya dhambi uliyokuwa unaishi ambayo yalikuwa yanaifanya kazi ya Mungu iharibike..Unaacha ulevi, usengenyaji, wizi, rushwa, utukanaji, unaacha kujichua, unaacha visasi, wivu, uvaaji mbaya, unakwenda kuchoma vimini vyote na suruali na vipodozi vyote ulivyokuwa unatumia na mambo mengine yote yasiyofaa.

Na baada ya kufanya tendo hilo la Imani, utakuwa umemtii Kristo, na hivyo Neema ya kipekee itaachiliwa juu yako ambayo hiyo itakusaidia kushinda dhambi bila kutumia nguvu nyingi..utajikuta tu ile hamu na nia ya kufanya dhambi inakufa yenyewe…lakini sharti kwanza uamua kuacha wewe mwenyewe kwa vitendo ili Bwana aione Imani yako.

Na mwisho, tafuta kanisa la kiroho ambalo linamhubiri Yesu Kristo wa kwenye biblia jiunge hapo na pia ulizia ubatizo, ili ukabatizwe kama hujabatizwa,..kumbuka ubatizo sahihi ni ule wa kuzamishwa mwili wote kwenye maji mengi..na kwa Jina la Yesu Kristo sawasawa na (Matendo 2:38)..zingatia hilo sana..Na Bwana atakuongoza kufanya mengine yaliyosalia ikiwemo kukuuongoza na kukutia katika kweli yote ya maandiko.

Bwana akubariki sana.

Mada Nyinginezo:

Mbona Mungu anaruhusu watu wapate shida, ilhali ana uwezo wa kutuepusha?

Ulinzi wa daima (eternal security) Je! ni neno la kimaandiko?

Je! mtu aliyeokoka anaruhusiwa kumiliki Lodge ambayo ina Bar ndani yake?

Je kuzalishwa na mkunga wa kiume ni dhambi?

HAJANENA KAMWE MTU YE YOTE KAMA HUYU ANAVYONENA.

UFUNUO: Mlango wa 1

NENO NI LILE LILE, LAKINI UJUMBE NI TOFAUTI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Ukweli dhidi ya uongo.

JIHADHARI NA UONGO WA SHETANI.

Print this post

Kwanini kila nikitaka kusali naingiwa na uvivu?

 SWALI: Kwanini kila nikitaka kusali naingiwa na uvivu, au nikitaka kusoma Neno ninapatwa na usingizi je! hizi ni nguvu za giza zinazisonga au ni nini?.

JIBU: Mtu yeyote aliyeokoka mbele yake, wapo maadui wawili wakubwa, adui wa kwanza ni shetani, na adui wa pili ni Mwili.

Shetani anachofanya ni kuhakikisha kuwa unakaa mbali na Mungu..Atafanya hivyo kwa kuhakikisha analeta kila namna ya presha za nje ili tu kukufanya uchukie maombi au ukose muda wa kusoma Neno la Mungu kwa ujumla..Anaweza kutumia ndugu, au mke au mume, kukukataza kusali, anaweza kunyanyua mazingira Fulani ili kukufanya ukose muda kwenda maombi, au kusikiliza maneno ya Mungu.

Kwamfano muda ambao ungepaswa uwe unasali, shetani anakuletea vipindi vya tamthilia kwenye televisheni, anakuletea magroup ya kuchati, anakuletea party za kuhudhuria, kazi Fulani ya kufanya n.k. Na kama mtu usipokuwa na msimamo katika imani yako , kuhakikisha kuwa Mungu anapewa nafasi ya kwanza, basi utachukuliwa na ulimwengu na kujikuta umesharudi nyuma,.baadaye ndio unakuja kushtuka ukiangalia mara ya mwisho kuomba ilikuwa ni miezi miwili iliyopita, mara ya mwisho kusoma biblia ni miezi mitatu iliyopita…Na ukijaribu kufanya tena hivyo huwezi…Hali kama hiyo ikishakukuta basi ujue shetani amekuweza.

Lakini Adui wa pili ambay ni mwili: Tofauti na watu wengi wanavyofikiri, kwamba Ukiwa ibadani halafu ukasinzia basi huyo ni shetani aliyekufanya usinzie, au ukiwa anasoma Neno nyumbani ukasinzia basi huyo ni shetani aliyekufanya ulale,..Nataka nikuambie huyo sio shetani bali ni mwili wako mwenyewe. Ukishaokoka shetani hana mamlaka na mwili wako.

Wale ambayo hawajaokoka labda shetani ndio anaweza kuwaletea nguvu nyingine za mapepo kwenye miili yao ili wasimkaribie Mungu, lakini kwa mtu aliyeokoka, shetani hawezi kufanya hivyo.

Yesu alipowachukua wanafunzi wake watatu na kwenda kusali nao saa chache kabla ya kwenda kuteswa, alirudi na kuwakuta wamelala..akawaamsha wasali, akaenda kusali akarudi tena akakuta wamelala ,..Lakini Bwana Yesu hakukimbilia kuwaambia mna mapepo ndani yenu kemeeni hizo roho, hapana alijua tatizo ni nini ndipo akawaambia maneno haya:

Marko 14:37 “Akaja akawakuta wamelala usingizi, akamwambia Petro, Je! Simoni, umelala? Hukuweza kukesha saa moja?

38 Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni, roho i radhi ila mwili ni dhaifu.

39 Akaenda zake tena, akaomba, akisema neno lilo hilo”.

Unaona? Aliwaambia Roho I radhi, lakini mwili ni dhaifu..Mwili sikuzote unashindana na roho, haupendi mambo ya rohoni, wakati unasema nataka kusali, mwili unasema lala, wakati unasema nataka nisome Neno la Mungu, mwili unakuambia umechoka sana pumzika, kesho utafanya hivyo.

Hivyo njia pekee ya kuushinda mwili wako ni kuulazimisha uitii Nia ya Kristo. Usiubembeleze, hakikisha ukitaka kusali unakaa mahali ambapo hapana vichocheo vya usingizi, hudhuria ibada za maombi, jumuika na watakatifu wengine katika kusali, hiyo inasaidia sana, biblia inasema kamba ya nyuzi tatu haikatiki haraka..Ukisali na mwenzako utapata motishi na nguvu ya kuzidi kusali kuliko unavyoweza kusali mwenyewe. Ukitaka kila siku kwenda mwenyewe mwenyewe kuna mahali utakwama tu.

Vilevile hakikisha unajijengea utaratibu wa kuongeza kiwango chako cha kusali kila siku..Kama uwezo wako ulikuwa ni dakika 15 kesho ongeza nyingine 5, kesho kutwa 5, hivyo hivyo hadi mwezi unapoisha unakuta uwezo wako wa kwenda masafa marefu umeongezeka, unaenda hata masaa kadhaa katika maombi bila kusimama.. Na ukawa bado hujachoka, siku umesali nusu saa unajiona hujasali kitu.

Vile vile ongeza bidii binafsi katika kujifunza Biblia kila siku, hakikisha siku haipiti bila kusoma NENO,.. sio kusoma mstari Fulani na kwenda kulala, hapana, bali kusoma na kulitafakari Neno, na kujifunza, kwa muda mrefu kwa jinsi uwezavyo..kila jambo linahitaji bidii..

2Petro 1:10 “Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe”.

Ukizingatia hayo, hutaona ugumu wowote katika kutimiza nguzo zote za Imani.

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

Je Mahari ina ulazima wowote?

JE! MTUMISHI KUTOKUWA NA FEDHA NI ISHARA KUWA KUNA TATIZO KATIKA IMANI YAKE?

JIEPUSHE NA MASHINDANO YA DINI.

NENO LA MUNGU NI TAA

KUOTA UNAENDESHA GARI.

Je! Ni dhambi kwa kijana aliyeokoka kuvaa suruali za kubana (model), kunyoa mitindo (mfano kiduku), ?

KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?

Rudi Nyumbani:

Print this post

MTUMWA SI MKUU KULIKO BWANA WAKE.

Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe.


Yohana 13:13 ‘Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo.

14 Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi.

15 Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.

16 Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka.

17 Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda’.

Bwana Yesu alisema..Mtu akitaka kuwa mkubwa kuliko wote ni sharti awe mtumishi wa wote..

Mathayo 20: 26 “Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu;

27 na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu;

28 kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi”.

Maana yake ni kwamba mbele za Mungu..yule anayewatumikia wengine huyo ndio mkubwa kuliko wote anaowatumikia mbele za Mungu…Na thawabu yake mbinguni ni kubwa kuliko wote…

Wengi wetu huwa hatupendi kusikika hivyo…lakini huo ndio utaratibu Mungu aliouweka…sisi wanadamu, aliye mtumishi wetu ndiye mdogo kuliko wote.

Na Yesu Kristo Bwana wetu kuonyesha kielelezo yeye alikuwa mdogo kuliko wote…hata kufikia hatua ya kutoka kwenye kiti na kuwakalisha wanafunzi wake, na yeye ambaye asili yake ni mbinguni alishuka chini, akashika miguu ya wanafunzi 12 kwa usiku mmoja…Jumla ya miguu 24, yenye mavumbi na isiyovutia ya wavuvi..aliishika na kuiosha, na kuifuta kwa kitambaa…Huyo ni Mkuu wa Uzima ambaye sisi leo tunamwita Bwana. Kashika miguu ya watu waliomkana na kumsaliti. Inatupasaje mimi na wewe?.

Ndugu siku zote Mungu anajifunua katika udogo sana mambo yaliyodharaulika katika ulimwengu huu Mungu ndiyo anayoyaangalia…Wengi wetu leo hii ni ngumu hata kuwapa mikono wakristo wenzetu, tutawezaje kuwaosha miguu?. Nimewahi kumsikia Mtu anasema… “kuoshana miguu kwa sasa hakupo”..Pale Bwana alikuwa anaonyesha mfano tu!!.

Tutaficha wapi nyuso zetu, siku ile tutakapokutana na Bwana uso kwa uso?…Yeye mkuu wa Uzima aliosha miguu watumwa wake sisi hatujawahi hata siku moja?..Si atatuambia tutoke mbele zake?. Maana anasema ….

“14 Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi.

15 Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.

16 Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka. ”

Mtumwa si mkuu kuliko Bwana wake, sasa wewe ni mkuu kuliko Yesu?..Tukikataa kuoshana miguu maana yake wewe ni mkuu kuliko Yesu, agizo hili ni la msingi na la lazima kwa kila mwamini, haijalishi ni mchungaji, nabii, mwalimu, askofu, mtume au mtu yoyote yule… Hakuna urembo wala utanashati katika kunyenyekeana…Na siku ile wengi watatupwa nje kwa kukosa tu hichi kitu…Kwasababu mbinguni hataingia yoyote ambaye anajiona ni mkuu kuliko Yesu. Na anasema “yeyote ajikwezaye atashushwa, naye ajishushaye atakwezwa.”

Hivyo ndugu kama ulikuwa huna desturi hiyo tunazidi kukumbushana..anza leo, kama mahali unapoabudu hawafanyi hivyo…mwulize mchungaji wako kwanini hafanyi hivyo?…Mwulize pia kama na yeye anafanya hivyo?. Kama hafanyi hivyo basi fahamu kuwa “mchungaji wako kajiweka kuwa mkuu kuliko Bwana wako Yesu”…Sasa utapenda kukaa mahali ambapo Bwana wako Yesu Kristo anashika nafasi ya pili?.

Tendo la kuoshana miguu ,licha ya kumtii tu Kristo lakini pia linafaida kubwa sana kiroho..kama ulikuwa hupatani na watu kitendo cha kujishusha na kuosha miguu ya mwamini mwenzako, roho Fulani ya maelewano na ya mapatano inakuvaa…na roho zote za magomvi na kutokuelewana zinakuondoka..kwa kufanya tu hicho kitendo cha kuoshana miguu..(Maroho ya Adui yanakukimbia kwa hicho kitendo tu..watu wengi hawajui hilo).

Kuna siri kubwa sana katika kuoshana miguu, hivyo hakikisha mahali unapokusanyika jambo hilo linafanyika…Miguu yako inapooshwa na mwamini mwenzako, na yeye anapoosha ya kwako..Kuna Neema Fulani kubwa sana ya kiroho inaachiliwa …

Neema ya umoja na ushirikiano..Sio tu kanisani, lakini hata mnapokusanyika wawili au watatu, mnaweza kufanya tendo hilo.

Sasa shetani analijua hilo, na hataki watu wafanye hivyo…au anataka watu wafanye isivyopaswa ili aharibu mambo juu ya maisha ya huyo mtu…Na moja ya njia shetani anayoitumia isiyofaa ni…kuoshana miguu kwa jinsia mbili tofauti…(Miguu inapaswa waoshane wanaume kwa wanaume katika kanisa na wanawake kwa wanawake..na sio kuchanganya)

Vivyo hivyo njia nyingine shetani anayoitumia kuharibu tendo la kuoshana miguu ni “wanawake kuoshwa miguu kwenye saluni za kike”..Wanawake wengi wanaoshwa miguu na wanaume katika masaluni na katika vibaraza…Kuna hatari kubwa sana ya kiroho kufanya hivyo (Tutakuja kuona madhara ya kufanya kitu hicho siku ya kesho kutwa Bwana akitupa Neema).

Lakini zidi kukumbuka Neno hili “Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka”..Jishushe na Bwana atakukweza kwa wakati wake.

Maran atha.

Mada Nyinginezo:

MEZA YA BWANA, NA KUTAWADHANA MIGUU.

JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.

HERI YULE ATAKAYEKULA MKATE KATIKA UFALME WA MUNGU.

TUMTOLEE MUNGU VILE VINAVYOTUGHARIMU ZAIDI.

URIMU NA THUMIMU NI NINI KATIKA BIBLIA?

ALIKUWAKO NAYE HAYUKO, NAYE YU TAYARI KUPANDA KUTOKA KUZIMU.

MZEITUNI HALISI UTAKAPOPACHIKWA.

WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA; NAO WATAMWOMBOLEZEA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

LOLOTE ATAKALOWAAMBIA FANYENI.

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, libarikiwe daima. Nakukaribisha katika kuyatafakari maneno mazuri ya Bwana wetu.

Kama tukisoma kitabu cha Yohana, sura ile ya pili tunaona, habari ile ya Yesu kualikwa katika harusi huko kana ya Galilaya, Na mamaye Yesu alikuwa ni mmoja wa wanakamati wa harusi ile..Lakini kwa bahati mbaya kama tunavyosoma habari divai iliwaishia katikati kabla hata ya sherehe kuishi.

Pengine lile lingekuwa ni aibu kwa wana-kamati, kwanini hawakulifikiria hilo kuwa divai inaweza kuwa chache na hivyo wangepaswa wanunue nyingi Zaidi kwa dharura kama hizo, lakini Mariamu, alikumbuka kuwa yupo mtenda miujiza katikati ya watu..Ndipo akamfuata na kumweleza tatizo hilo, lakini Yesu aliposikia akamwambia mama yake ‘wakati wake haujafika’, Mamaye hakukata tamaa kuambiwa vile Zaidi ya yote aliwapa maagizo wale watenda kazi wa kwenye sherehe na kuwaambia…

Yohana 2:5 “…Lolote atakalowaambia, fanyeni…”

Tujiulize ni kwanini aliwaambia vile “Lolote atakalowaambia, fanyeni” au kwa lugha nyepesi alimaanisha kuwaambia “chochote atakachowaelekeza kufanya mtiini bila kushuku shuku”..

Kumbuka Mariamu alikuwa na Bwana Yesu tangu akiwa mtoto, na hivyo alikuwa anajua tabia yake vizuri ni mtu wa namna gani. Pengine wakati fulani huko nyuma kulishawahi kutokea matatizo fulani yanayofanana na haya, Na Yesu akawashauri wafanye kitu fulani wakakipuuzia, na baadaye wanalipopata hasara na kugundua kuwa uamuzi wa YESU wa mwanzoni ndio ulikuwa bora, wakajuta kwanini hawakumskiliza.

Au pengine walitaka kufanya jambo fulani la kimaaendeleo, labda tuchukulie mfano tu, walikuwa wanataka kutanua biashara yao ya useremala, hivyo wakaamua kwenda kutafuta eneo zuri Zaidi la mjini ambapo pana watu wengi na wanunuzi wengi..

lakini Yesu akawashauri na kuwaambia msiende mjini bali rudini nendeni katika kijiji fulani mkanunue shamba kule, na muifanye kazi hiyo pale..Pengine mawazo yake yalionekana kuwa hafifu ya mtu asiyekuwa na tageti, mtu aende kijijini atapata wapi wateja wazuri wa kununua fanicha zao..Lakini pengine baada ya miezi mitatu wakasikia serikali ya Pilato, imeteua makazi mapya, na Kijiji hicho ndicho kimeonekana kuwa ni kizuri kwa makao hayo ya watu na uwekezaji, hivyo amri imetolewa Rumi na kaisari kwamba wale wajenzi wanaoishi maeneo yale yale ndio wapewe tenda ya muda mrefu ya ku-sambazavifaa vyote vya ujenzi pamoja na fanicha za ndani..

Lakini wao sasa wameshakwenda mjini, hawawezi kurudi tena kule,.Na baadaye wanagudua kuwa mawazo ya YESU yalikuwa bora Zaidi kuliko ya kwao, wangemsikiliza tu, japo mwanzoni yalioonekana kama ya kipuuzi.. (Sasa Huo ni mfano tu!).

Sasa matukio kama hayo, au tofauti na hayo lakini yenye maudhui hayo hayo walikutana nayo sana wakina Mariamu mpaka ikafikia wakati wakaamua sasa wawe wanamsikiliza yeye tu ushauri wake na kuufanya hata kama utaonekana unaenda kinyume na hali halisi ya mazingira.. walikuwa wanatii tu. kwasababu walikuwa wanajua Kristo alijaa hekimu ya ki-Mungu ndani yake, na kila alilolifanya lilifanikiwa..

Sasa tukirudi kwenye sherehe hii tunaona matatizo kama yaleyale ya nyuma yanajitokeza tena, Kama kawaida Mariamu anamfuata tena Yesu na kumwambia Divai imetuishia tufanye nini?…Lakini Yesu anamwambia Mariamu wakati wangu haujafika..akimaanisha wakati wake wa kuanza kutenda miujiza haujafika..Lakini Mariamu akawaambia wale watumishi..

“watumishi, Lolote atakalowaambia, fanyeni..”

Msipuuzie atakalowaambia, mnaweza kuliona halina maana machoni penu, lakini anajua kitu gani anachokisema…Anaweza akawapa maagizo ya ajabu ajabu tu lakini mtiini fanyeni atakachowaambia ili mfanikiwe..Na kweli walipokwenda kwa Yesu, wakakutana na jambo kama vile la kipuuzi kweli…

waliambiwa wachukue mabalasi wakayajaze maji na kisha wampelekee mkuu wa meza..Kumbuka hayo mabalasi biblia inatuambia yalikuwa yanatumika kwa kutawadhia..Embu fikiria pipa la kutawadhia unaambiwa ukalijaze maji halafu uyachote upeleke mezani kwenye harusi…ni kama uendawazimu hivi..

Yohana 2:6 “Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu.

7 Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu.

8 Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka”

Basi wale watu wakafanya hivyo, si rahisi kuyatii maagizo kama hayo, ikiwa hujamjua vizuri mtu anayekuambia ufanye hivyo..

Yohana 2:9 “Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi,

10 akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa”.

Unaona mwisho wa siku walipata divai iliyo bora kuliko hata ile ya kwao. Lakini kwa kutii tu maagizo ya Yesu.

Desturi hiyo hiyo Kristo aliendelea kuwa nayo..utakumbuka wakati fulani aliwaambia wayahudi na wale wanafunzi wake waliokuwa wanafuatana naye, kwamba mtu yeyote asipoula mwili wake na kuinywa damu yake hana uzima wowote ndani yake..

Yohana 6:53 “Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.

54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

55 Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.

56 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake”.

Lakini wengi waliposikia maneno yale, jinsi tu yasivyo eleweka-eleweka wengine wakayapuuzia, na wengine kuanzia siku hiyo hiyo wakaacha kufuatana naye, wakamwona kama huyu ni mchawi fulani hivi..anataka kuleta elimu yake ya uchawi..Lakini hawakujua kuwa alikuwa anazungumzia habari za uzima wao.

Hata sisi pamoja na maagizo mengi aliyotuachia ya namna ya kupokea Baraka Fulani.. Bwana alituachia Agizo moja la MUHIMU SANA la kufuata mara tu tunapoamini na kuchukua misalaba yetu na kumfuata. Alisema mtu yeyote akishaamini, hatua inayofuata ni lazima akabatizwe.

Luka 16:16 “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa..”

Lakini wengi wanayapuuzia maagizo haya, na kusema aah! Hakuna jambo kama hilo ubatizo sio muhimu, kinachookoa ni damu ya Yesu na sio maji..Lakini nataka nikuambia ubatizo unaweza usiwe na maana sana kwako lakini unamaana sana kwa Yesu aliyekuagiza ufanye hivyo.

“Lolote atakalowaambia, fanyeni..” Maji ndani ya vyombo vya kutawadhia, yaligeuka divai juu ya meza za harusi…Maji unayoyakataa leo kwa ubatizo wako ndio Bwana anayoyaagiza kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Unayakiuka maagizo ya Mungu, halafu bado unatazamia dhambi zako ziondolewe, utakuwa unajidanganya!..Hata daktari akikupa dawa halafu ukaacha kuzitumia hadi mwisho kwa kisingizio kuwa umeshaanza kujisikia nafuu, siku itafika ugonjwa utakurudia na hali yako itakuwa ni mbaya ziadi kuliko ilivyokuwa pale mwanzo…Vivyo hivyo ubatizo kwa mtu anayeamini ni jambo lisiloweza kuepukika, Na ubatizo Yesu aliouagiza ni ule wa kuzamishwa katika maji tele (Yohana 3:23) kwa jina la YESU KRISTO. Sawasawa na (Matendo 2:38)..Ubatizo mwingine tofauti na huo ni batili!.

Vilevile Bwana aliagiza tushiri meza yake. Hivyo Kama wakristo ni muhimu kufanya hivyo, tusipofanya hivyo kama yeye alivyosema “hatuna uzima ndani yetu”..Ni kweli tutakuwa hatuna uzima ndani yetu..Kwani kitendo kile cha kushiriki divai na mkate, tunakuwa tunaitangaza mauti yake mpaka ajapo.

Vilevile alitoa maagizo mengine ya mwisho ambayo ni muhimu sana..Nayo ni kutawadhani miguu watakatifu..Hili linapuuziwa lakini ukweli usiopingika watakatifu ni sharti tulitimize agizo hili nalo..Alisema..

Yohana 13:12 “Basi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Je! Mmeelewa na hayo niliyowatendea?

13 Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo.

14 Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi.

15 Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.

16 Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka.

17 Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda”.

Hivyo kama ulikuwa hujafanya mojawapo ya hayo matatu yaani (KUBATIZWA, KUSHIRIKI MEZA YA BWANA, na KUTAWAZANA MIGUU )..ni vizuri ukaanza kufanya hivyo sasa.

Wengi waliyapuuzia maagizo ya Yesu lakini baadaye walikuja kuona umuhimu wake, wakati ambao wameshachelewa. Na wewe usije ukaukosa uzima kwa kuzembea maagizo ya Bwana wetu YESU KRISTO, mshauri wa ajabu.

“Lolote atakalowaambia, fanyeni..”

Ubarikiwe sana.

Mada Nyinginezo:

MTUMAINIE YESU ASIYEISHA MATUKIO.

BASI MUNGU AKAMUADHIMISHA SANA..

UMUHIMU WA YESU KWETU.

KAMA MHUBIRI NI WOKOVU UPI UNAUPELEKA KWA WATU?

KRISIMASI (CHRISTMAS) NI NINI? JE IPO KATIKA BIBLIA?

JIEPUSHE NA MASHINDANO YA DINI.

KWANINI YESU ALIMUITA BABA YAKE “ABA”?

Rudi Nyumbani:

Print this post

TOA SADAKA ISIYO NA KASORO KWA BWANA.

Toa sadaka isiyo na kasoro kwa bwana.


Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo, libarikiwe!. Karibu tena tujifunze biblia..Hatuna budi kufanya hivyo kila siku..maadamu tumepewa uhai.

Leo tutaendelea kujifunza umuhimu wa kumtolea Mungu kitu kilicho bora..kama hujapita somo lililotangulia lenye kichwa kinachosema “TUPENDE KUMTOLEA MUNGU VILE VINAVYOTUGHARIMU ZAIDI.”..Naomba ulipitie kwanza ili tuweze kwenda pamoja katika masomo haya yanayofuata.

Kuna umuhimu mkubwa sana kumtolea Mungu vitu vinavyotugharimu. Tusipende kutoa tu ilimradi tumetoa, kwasababu Mungu wetu ana hekima kuliko sisi na anaitazama mioyo yetu kwa undani sana. Mtu akija na kukupa wewe zawadi..na ile zawadi aliyokupa ukaja kugundua haikuwa imekusudiwa uipokee wewe..Ilikuwa ni ya mtu mwingine lakini kwasababu mtu huyo hakuwepo, na hakuna wa kumpa ukapewa wewe, hutaichukulia kwa moyo wa furaha sana kama kama ingekuwa imelengwa kwako moja kwa moja, Sasa ni kweli umepewa zawadi..jambo jema na la kushukuru, hata hicho umekipata, lakini zawadi ile ingekuwa na nguvu kwako kama ingekuwa wewe ndio mlengwa wa kwanza. Kama sisi wanadamu tuna hisia kama hizo..basi Mungu naye hapendezwi na sadaka za masalia.

Anapenda tumtolee kitu ambacho tulikuwa tumekipanga kumtolea yeye na si makombo, hapendi kuwekwa wa pili…Kumweka wa pili ni kumdharau…Haangalii wingi bali anaangalia ubora wa ile sadaka. Sadaka unayomtolea ina ubora kiasi gani..inaugusa moyo wake kiasi gani, umeigharimikia kiasi gani, hata kama ni sh.100 lakini haikuwa chenji ya kiatu ulichokwenda kununua..

Katika Agano la kale ambapo utoaji wa sadaka ulihusisha kafara za Wanyama…Wanyama ambao walitumika kwa kafara hizo kama ng’ombe, mbuzi, kondoo, njiwa n.k Mungu alitoa amri kwamba kamwe wasitolewe wakiwa na kilema, udhaifu, ugonjwa wala wenye lawama yoyote..

Ilikuwa kumtolea Mungu ng’ombe aliye na chongo ni dhambi, kumtolea mwanakondoo aliye mlemavu ni dhambi…kadhalika kumtolea ng’ombe mwenye kumbukumbu yoyote mbaya huko nyuma kama kuua mtu, au kuua ng’ombe mwenzake au kufanya jambo lolote baya ilikuwa ni dhambi kumtoa kama sadaka ya kuteketezwa kwa Mungu. Ng’ombe wa sadaka alikuwa ni lazima asiwe na hatia.

Walawi 22: 20 “Lakini mnyama ye yote aliye na kilema msimtoe; kwa kuwa hatakubaliwa kwa ajili yenu”

 

Kumbukumbu 17:1“Usimchinjie Bwana, Mungu wako, ng’ombe wala kondoo aliye na kilema, wala neno ovu lo lote; kwa kuwa hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako”

 

Malaki 1:13 “Tena mwasema, Tazama, jambo hili linatuchokesha namna gani! Nanyi mmelidharau, asema Bwana wa majeshi; nanyi mmeleta kitu kilichopatikana kwa udhalimu, na kilema, na kilicho kigonjwa; ndivyo mnavyoleta sadaka; je! Niikubali hii mikononi mwenu? Asema Bwana.

14 Lakini na alaaniwe mtu mwenye kudanganya, ambaye katika kundi lake ana mume, akaweka nadhiri, ila amtolea Bwana kitu kilicho na kilema; kwa maana mimi ni Mfalme mkuu, asema Bwana wa majeshi, na jina langu latisha katika Mataifa”.

Katika agano la kale ilikuwa hairuhusiwi hata kwenda kununua ng’ombe wa mtu usiyemjua..kwasababu hujui huyo ng’ombe au kondoo alikuwa na kasoro gani huko nyuma..labda alishaua mtu utajuaje!..au alishapigana na mwenzake na kumuua utajuaje?..kwahiyo ilikuwa ni lazima mnyama aidha atoke kwenye zizi lako mwenyewe au kwa mtu unayemjua ambaye ni mwaminifu sana au anayeaminika na watu..Ili kuepuka kumtolea Mungu kitu chenye kasoro.

Umewahi kujiuliza ni kwanini siku ile Bwana Yesu alipoingia hekaluni alikuta watu wanauza njiwa, ng’ombe na mbuzi na hakukuta wanauza mashati, nguo, viatu au vyakula?.

Yohana 2:13 “Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu.

14 Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng’ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi”

Unajua ni kwanini?..Ni kwasababu watu walikuwa wanatoka mbali..wengine mataifa ya mbali na hivyo wengi wanaona uvivu kutenga muda kwenda kutafuta ng’ombe asiye na lawama wala kilema wala kasoro yoyote…walikuwa wanaona ni jambo linalochukua muda sana na linalogharimu fedha nyingi mpaka umpate huyo mnyama wa viwango hivyo…na bado ni gharama kumsafirisha yule mnyama kutoka huko waliko mpaka hekaluni kwa makuhani ili atolewe kama sadaka ya kuteketezwa..

Sasa ili kulikwepa hilo wakawa wanatafuta njia mbadala ya kuwapata wale Wanyama mahali karibu na hekalu lilipo..sasa watu wa mataifa wakaona hiyo ni fursa..wakaanza kupeleka ng’ombe zao zilizonona kwenda kuziuza karibu na hekalu, wengine wakawa wanauza ng’ombe waliowaiba, wengine wanauza ng’ombe ambao wanamagonjwa ambayo hayajaanza kujidhihirisha bado…lengo lao wapate fedha..wengine mbuzi wanaowauza wamelala na wanadamu huko nyuma…nani anajali ilimradi tu wapate fedha..wapo radhi hata kudanganya kwamba mbuzi yule au kondoo huyu hana hatia kabisa alikuwa msafi na mpole tangu anazaliwa ili wamuuze tu wapate fedha na Kesho walete wengine..wetengeneze pesa nyingi..wakaikoleza biashara mpaka pakageuka kuwa soko na vibaka wakawemo humo humo ndani pengine hata na kamari zilichezeshwa humo.

Na kwasababu wayahudi wanaokuja pale wanaotoka mbali huko na huko hawapendi kujisumbua kutafuta kilicho bora mbele za Mungu…wanauziwa pale pale hakaluni Wanyama ambao ni machakizo kuwatoa mbele za Mungu, ambao hawajui hata wametoka wapi..…Wanatoka nyumbani bila chochote..wanafika hekaluni wananua mbuzi, wanawapa makuhani wanatolewa sadaka mbele za Mungu, wanarudi nyumbani..na kuamini kwamba wametoka kubarikiwa…kumbe wametoka KULAANIWA!..Wakidhani kwamba wametoka kumheshimu Mungu kumbe wametoka kumdharau..Ndio maana Bwana aliwafukuza wote wanaouza hao wanyama mule hekaluni..kwasababu yalikuwa ni machukizo yanayoendela mule..

Je na unaithamini sadaka yako unayomtolea Mungu kila siku?..je ina kasoro yoyote?..Kama umeipata kwa njia ya wizi usiende kumtolea Mungu hiyo tayari ina dosari kadhalika kama sadaka uliyoipata umeipata kwa njia ya ukahaba usimtolee,.. kama umeipata kwa njia ya kuuza bar, au sigara, au madawa ya kulevya au kamari, au ufisadi, au rushwa au wizi ni heri usimtolee Mungu…kama ni vimasalia salia ndio umepanga umtolee Mungu..usivitoe…Kwasababu Biblia inasema..

Mithali 15: 8 “Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana..”

Ni masuala ya sadaka haya haya ndio yaliyoutoa uhai wa Anania na mkewe Safira…Anania kauza kiwanja kapanga kumtolea Mungu fedha yote aliyouzia kiwanja..lakini yeye akawa anakwenda kumtolea Mungu chenji huku fedha nyingine kaizuia..matokeo yake akafa yeye na mkewe..na hiyo ni agano jipya sio agano la kale.

Kwahiyo ukitaka kumtolea Mungu tafuta donge nono..ambalo huwezi kumwambia hata mtu kwasababu atakushangaa na kukuona wa ajabu..Unapomtolea Mungu mtolee kwa fedha iliyopatikana kihalali na kiwango cha juu ili sadaka yako isiwe na kasoro..Na njia nyingine bora ambayo Mungu atakuongoza umtolee yeye ambayo haitakuwa ni ya kumdharau..mtolee yeye ili ubarikiwe.

Bwana akubariki sana.

Kama hujaokoka..Okoka sasahivi na kama hujabatizwa katafute ubatizo sahihi haraka sana..kwasababu mambo hayo mawili yanakwenda pamoja..

Mada Nyinginezo:

USILETE UJIRA WA KAHABA, NYUMBANI KWA MUNGU.

Tofauti katika ya zaka na sadaka ni ipi?

TUMTOLEE MUNGU VILE VINAVYOTUGHARIMU ZAIDI.

KIJITO CHA UTAKASO.

UWEPO WA BWANA HATA KATIKATI YA MATESO.

TUMAINI NI NINI?

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

JE WAJUA?

 • Je Wajua kuwa Yesu ni Mungu bofya hapa kujua zaidi >> Yesu
 • Je Wajua kwamba dunia itateketezwa kwa moto na si kwa maji tena? >> Dunia
 • Je Wajua kuwa tunaishi katika kanisa la mwisho lijulikanalo kama Laodikia >> Laodikia
 • Je Wajua mtu ambaye hajaokoka hawezi kuingia mbinguni?
 • Je Wajua kuwa watu watakaonyakuliwa ni wachache? >> Wachache
 • Je Wajua roho ya mwenye haki ikifa inakwenda paradiso na si mbinguni? >> Roho ya mtakatifu.
 • Je Wajua kuwa Unyakuo utakuwa ni siri na ni wachache ndio watakaojua na hakutakuwa na maajali mabarabarani >> Unyakuo
 • Je Wajua kuwa Nusu ya kitabu cha Ufuno kimeshatimia?>> Ufunuo
 • Je Wajua kwamba mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyeko mbinguni zaidi ya Yesu? >> Mbinguni
 • Je Wajua kwamba mpinga-Kristo atakuwa ni mtu anayeshika biblia? >> Mpinga Kristo
 • Je Wajua kumlaani Adui yako ni dhambi? >> Adui
 • Je Wajua hakuna kiwanda chochote cha fedha kuzimu? >>Fedha kuzimu
 • Je Wajua kucheza karata ni dhambi? >> Kucheza karata
 • Je Wajua kipaimara si jambo la kimaandiko >> Kipaimara
 • Je Wajua kuwa Mwanamke hapaswi kuwa Mchungaji wala Shemasi >> Nafasi ya Mwanamke
 • Je Wajua kuwa kuna utawala wa miaka 1000 unaokuja huko mbele?>> Miaka 1000
 • Je Wajua kuwa Mariamu si malkia wa mbinguni >> Malkia

Mada Nyinginezo:

Je! mtu aliyeokoka anaruhusiwa kumiliki Lodge ambayo ina Bar ndani yake?

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

DHAMBI ILIYOMKOSESHA SHETANI:

JE KUJIUA NI DHAMBI?

Je! Ni sahihi kwa mkristo kuoa/kuolewa na mtu wa imani nyingine?

Kwanini Mungu awachome watu kwenye ziwa la moto na hali yeye ndiye aliyewaumba?

KUOTA UMECHELEWA MAHALI FULANI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

JE! WATOTO WACHANGA WANAWEZA KUHUKUMIWA NA KUTUPWA MOTONI.

Je! watoto wachanga wanaweza kuhukumiwa na kutupwa motoni.


Biblia inatuonyesha kuwa watoto wachanga wanaweza kushiriki adhabu za watu wengine waovu wakiwa hapa hapa duniani kama tu vile wanavyoweza kushiriki baraka za watu wema wakiwa hapa hapa duniani ..Lakini baada ya kifo biblia haisemi kama watoto wachanga watatupwa motoni au watakwenda mbinguni..

Ipo mifano kadha wa kadha katika biblia ya watoto kuadhibiwa kwa makosa ya wengine, kwa mfano tukisoma habari za Nuhu, Tunaweza kuona Nuhu aliambiwa aingie katika Safina yeye na familia yake tu ( jumla, watu 8)..Jiulize huko nje kulikuwa na Watoto wangapi wachanga, au wanawake wangapi waliotoka tu kujifungua muda mfupi kabla ya gharika kuanza,..Lakini ulipofika wakati wa Mungu kuuondoa uovu ulimwenguni kote, waliarithiwa na Watoto nao ambao kwa jicho letu la kibinadamu tunaweza kusema walikuwa hawana hatia yoyote..

Vivyo hivyo katika Sodoma na Gomora, walipona watu watatu (3) tu kati ya maelfu kama sio mamilioni ya Watu (ikiwemo na Watoto wadogo) waliokuwepo katika miji ile.

Utaona sehemu nyingi katika biblia, Mungu akitoa laana kwa mtu mwovu ambayo wakati mwingine  haiishii kwake tu, bali inakwenda kuwaarithi mpaka wazao wake wote. Soma (2Samweli 21:1-10, Yoshua 7:1-26,)

Daudi alipomwasi Mungu na kwenda kuzini na mke wa Uria, kilichotokea, ni Mungu kumpiga yule mtoto aliyemzaa kwa maradhi hadi mwisho wa siku akafa, hiyo yote ilikuwa ni kwasababu ya kosa la Daudi kuimwaga damu isiyo na hatia na kulala na mwanamke ambaye hakuwa mke wake.

Vilevile hata katika kipindi cha Yona kutumwa Ninawi, alipoambiwa awahubirie watu wale kuwa  zimebakia siku 40  tu mji ule uteketezwe wote…Bila shaka jambo lingejirudia lile lile, kisingesalia kitu, sio tu Watoto, bali pia mifugo ambayo haina hatia yoyote, lakini walipotubu Mungu akaurehemu mji ule..Na sikia Mungu alichomwambia Yona..

Yona 4:11 “na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi ya mia na ishirini elfu, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana”?

Unaona hao wasioweza kupambanua mkono wao wa kulia kutoka katika mkono wao wa kushoto wengi wao ni Watoto.

Hivyo dhambi ni mbaya sana, Na inatabia ya kuambukiza,,Na ndivyo itakavyokuja kuwa hata katika mwisho wa dunia..Siku Mungu atakapokuja kuteketeza kila kitu, Adhabu itawakuta wote…

Lakini kuhusu hukumu ya Watoto kwenda kutupwa katika ziwa la moto. Hilo hatulijui, lakini tunachojua ni  kuwa Mungu ni Mungu wa haki. Hawezi kumuhukumu mtu kwa kosa ambalo halijui. Watoto wachanga hawawezi kutofautisha kati ya jema na baya, kama ni hivyo basi hapo  tunaweza kusema hakuna hukumu ya adhabu juu yao..

Mithali 8:20 “Natembea katika njia ya haki, Katikati ya mapito ya hukumu”.

Zaidi ya yote biblia inawachukulia Watoto wachanga kama mfano mzuri wa kuigwa kwa wale watakourithi ufalme wa mbinguni..

Mathayo 19:14  “Lakini Yesu akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu; wala msiwazuie; kwa maana walio mfano wa hao, ufalme wa mbinguni ni wao”

Unaona anasema tena. …

Mathayo 18:2  Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao,

3  akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

Unaona, tabia za Watoto  ni tabia zenye sifa njema mbinguni kwahiyo hapo tunaweza kupata picha kuwa Watoto ambao bado hawajajitambua, wanaweza kuwepo mbinguni wote, lakini pale wanapojitambua tu, kwamba wanaweza kutofautisha kati ya mabaya na mema haijalishi watakuwa katika umri gani iwe ni miaka 6 au 10, hao moja kwa moja watapanda hukumuni. Na kama wamestahili kuzimu watakwenda kuzimu,  kama wamestahili uzima watakwenda uzimani.

Kwasababu biblia inasema, siku ile ya hukumu watakuwepo wakubwa kwa wadogo ili wahukumiwe..

Ufunuo 20:12  “Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao”

Hivyo kwa kuhitimisha. Upo wezekano mkubwa  kwa Watoto wote wachanga wanaokufa kuwepo mbinguni. Japo suala la hukumu tunamwachia Mungu mwenyewe..hivyo Kikubwa tu tuwalee Watoto wetu katika njia iwapasayo, ili  atakapofikia umri ule wa kuweza kupambanua mema na mabaya basi wawe katika mstari mzuri wa kumtii Mungu ili hata ikitokea kwa bahati mbaya amefariki hapo katikati basi tuwe na uhakika wapo katika mikono ya Mungu.

Ubarikiwe sana.

Mada Nyinginezo:

Mbona Mungu anaruhusu watu wapate shida, ilhali ana uwezo wa kutuepusha?

KILEMBA CHA NEEMA, JE! UMEMVIKA MWANAO?

LENGO LA SHETANI KWA WATOTO WA KIZAZI HIKI.

JE! UNAYO NAFASI MBINGUNI?

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?

USIWE NA HAKI KUPITA KIASI.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Rudi Nyumbani:

Print this post

HERI YULE ATAKAYEKULA MKATE KATIKA UFALME WA MUNGU.

Luka 14:15 “Basi aliposikia hayo mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye alimwambia, Heri yule atakayekula mkate katika ufalme wa Mungu”.

Enzi za biblia chakula kilichokuwa kinapewa heshima kubwa zaidi katika sherehe kilikuwa ni mkate uliookwa vizuri kwa upishi makini..Ni sawa na tuseme leo hii KEKI..Tunajua sherehe isiyokuwa na keki haijakamilika..miongoni mwa vyakula vyote vya kwenye sherehe keki huwa ndio inayopewa heshima kubwa kuliko zote na huwa inawekwa pale mbele kabisa, ili kuliwa na watu mahususi, Na sio na kila mtu tu aliyealikwa tu karamuni..bali wale walengwa tu..wengine wote watakula vyakula vingine vilivyoandaliwa kwa ajali yao..

Hivyo Keki huwa ndio inayofunua vyeo vya watu pale karamuni..Wale wanaopewa kipaumbele cha kwanza kuila ndio wanatambulika kuwa wale ni walengwa wa juu, au wenye kuheshimiwa ziadi, vivyo hivyo na wanao fuata na wanaofuata..

Sasa tukirudi katika mstari ule, tunapaswa tujiulize yule mtu aliona tukio gani mpaka ikamsukumwa kusema maneno kama yale “Heri yule atakayekula mkate katika ufalme wa Mungu”??..Tukisoma mistari ya juu kidogo tunaona alizungumza maneno yale baada ya kuona mfumo mzima wa karamu aliyokuwa amealikwa siku hiyo..Biblia inatuambia, Farisayo mmoja mkuu sana, aliyekuwa na cheo kikubwa, aliamua afanye karamu yake siku ya sabato, na alipofanya akawaalika ndugu zake tu, na watu wakubwa wakubwa tu, pengine mawaziri wa nchi, au wabunge wa nchi, na marafiki zake walio mtajiri na majirani zake wale wenye vyeo na fedha n.k. Na huko huko akamwalika huyu mtu na Bwana YESU pia..

Sherehe ile bila shaka ilikuwa ni ya kifahari sana, pengine walikuwa katika ukumbu uliopambwa sana. Sasa wakiwa huko baadhi ya watu walioalikwa wengine wakawa wanakimbilia viti vya mbeleni ili wawe wa kwanza kutambuliwa na kulishwa mkate au tuiite keki ya wakati huo..Utasema hilo tumelijuaje kuwa walikuwa wanakimbilia viti vya mbele?..Tumelijua hilo kwa maneno ya Bwana Yesu mwenyewe pale alipowaambia wale waliolikwa..

Luka 14:7 “Akawaambia mfano wale walioalikwa, alipoona jinsi walivyochagua viti vya mbele; akisema,

8 Ukialikwa na mtu arusini, usiketi katika kiti cha mbele; isiwe kwamba amealikwa mtu mwenye kustahiwa kuliko wewe,

9 akaja yule aliyewaalika wewe na yeye, na kukuambia, Mpishe huyu! Ndipo utakapoanza kwa haya kushika mahali pa nyuma.

10 Bali ukialikwa, nenda ukaketi mahali pa nyuma, ili ajapo yule aliyekualika akuambie, Rafiki yangu, njoo huku mbele zaidi; ndipo utakapokuwa na utukufu mbele ya wote walioketi pamoja nawe.

11 Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa”.

Unaona Vile vile utasema tumejuaje sherehe ile ilikuwa ni ya watu wakubwa tu..Tumelijua hilo kutoka katika kinywa chwa Bwana Yesu mwenyewe….

Luka 14:12 “Akamwambia na yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo.

13 Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu,

14 nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki”.

Sasa, kutokana na hali nzima ya mazingira yaliyokuwa yanaendelea pale, kila mtu anatamani angepewa heshima ya mbele, aketi katika viti vya mbeleni, awe wa kwanza kulishwa keki, kutambuliwa..Ndio sasa tunaona huyu mtu mmoja aliyealikwa anatokea na kumwambia Bwana ama! kweli! HERI HERI YULE ATAKAYEKULA MKATE KATIKA UFALME WA MUNGU..

Alipiga hesabu akasema kama duniani mambo ndio hivi, itakuwaje mbinguni mtu kupewa heshima ya juu zaidi katika karamu ile ya mwana-kondoo?.. Kuwa wa kwanza kulishwa MKATE wa mbinguni..Kupewa heshima ya viti vya mbele..Kuketi karibu kabisa na Kristo, kuzungumza naye kama mgeni rasmi mwalikwa..Utajisikiaje siku hiyo, kwenye meza moja na Ibrahimu, na manabii na mitume wa Kristo, mnacheka na kufurahi na Kristo akiwa katikati yenu…Ukiangalia wengi mmealikwa lakini si wote mpo katika meza moja na Bwana..

Mathayo 8:11 “Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;

12 bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.

Leo hii yeye akiwa hapa duniani ataachaje kusema.. Heri yule atakayekula mkate katika ufalme wa Mungu?..Hata mtu yeyote anayejua thamani ya sherehe, anaelewa ni raha gani unajisikia unapopewa heshima ya juu zaidi katikati ya waalikwa.

Ndugu yangu karamu ya mwana-kondoo ipo karibu sana.. SIku ile ambayo parapanda italia, na wafu kufufuka, wakiungana na wale ambao watakuwa hai wakati huo, wote kwa pamoja wataisikia sauti ya Bwana Yesu ikiwaita hapo juu..Siku hiyo ndipo watakapoacha ardhi, na moja kwa moja safari ya kuelekea katika malango ya mbinguni itaanza..Siku hiyo wale walionyakuliwa hawataamini kwa macho yao kama kweli ndio siku hiyo imefika..Lakini ndivyo ilivyo wataanza safari mpaka mbinguni huku mabilioni kwa mabilioni ya malaika yakiwalaki..

Na moja kwa moja watapelekwa katika ukumbi wa kimbinguni usioelezeka kwa uzuri wake, miili yao wakati huo itakuwa imebadilishwa, watakuwa kama malaika..wana mavazi mazuri meupe yanayong’aa kama jua, wataketishwa katika sehemu waliyoandaliwa karamuni..Watayaona yale makao waliokuwa wamekwenda kuandaliwa kwa zaidi ya miaka 2000, na YESU.. Watazimia mioyo kwa furaha, wataketi watakula na kunywa na Bwana divai mpya..Watamwona Mungu,..watafurahi milele na milele.

Mathayo 26:29 “Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu’’.

Lakini wakati huo huku chini, mambo yatakuwa tofauti wengine watakuwa wakilia na kusaga meno. Wakihangaika katika dhiki ya mpinga-kristo,.Wengine watakuwa wanajuta..

Ndugu dalili zote zimeshatimia, pengine sisi sote tutashuhudia tukio hili la kunyakuliwa kwa kanisa siku za hivi karibuni..Lakini swali linakuja Je! na wewe ni mmojawapo wa watakaonyakuliwa? Je! unaouhakika hata ukifa leo utakuwepo katikati ufufuo wa kwanza? Kama hujui basi ni ishara kuwa utabaki hapa duniani, ndugu umgeukie Mungu angali muda unao, Tubu dhambi zako kuwa maanisha kumuishia Mungu katika kipindi hichi kifupi cha kumalizia ili kama akirudi hapa katikati nawe uwe mmojawapo wa wale watakaokwenda naye.

Ufunuo 19:6 “Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki.

7 Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.

8 Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.

9 Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu”.

Bwana akubariki.Tafadhali Share ujumbe huu na kwa wengine. Pia usiache kutembelea website yetu hii (www wingulamashahidi org) kwa mafundisho zaidi.

Maran Atha.

Mada Nyinginezo:

JE! UNAYO NAFASI MBINGUNI?

UFALME WA MUNGU HAUPATIKANI KIRAHISI.

Yeshuruni ni nani katika biblia?

JIEPUSHE NA MASHINDANO YA DINI.

MKUU WA ANGA.

ANTIPA SHAHIDI WANGU, MWAMINIFU WANGU.

Tofuati kati ya Myahudi, Mwisraeli na Muebrania ni ipi?

Rudi Nyumbani:

Print this post

NAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA!

Shalom. Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe…

Ni kwa Neema za Bwana tumeuona tena mwaka huu mpya wa 2020. Si wote waliovuka lakini sisi tumevuka..Utukufu na heshima na shukrani zina yeye. Amina.

Nakutakia mafanikio katika huu mwaka ulioanza. Mafanikio ya roho yako..ambayo hayo yatazaa mafanikio mengine yote yaliyosalia..kama maandiko yanavyosema katika..

3Yohana 1:2 “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo”.

Katika Mwanzo wa mwaka wana wa Israeli waliachiliwa kutoka katika nyumba ya utumwa, wakawa huru, Hivyo Bwana akuachilie nawe pia kutoka katika nyumba ya utumwa wa Ibilisi katika jina la Yesu Kristo. Kila aina ya mikakati na vifungo vya Ibilisi Bwana akaviweke mbali nawe katika mwaka huu wa 2020. Ulioanza. Kila kilichokuwa kigumu Bwana akakifanye kuwa kilaini.

Pale ulipokuwa huwezi kusonga mbele katika Imani kutokana na majaribu mazito ya Adui..Bwana akayazuie katika mwaka huu katika jina la Yesu Kristo.

Mwaka huu ukawe mwaka wa Bwana, na kila ufanyalo kwa ajili ya Bwana, na kwa ajili yako binafsi likafanikiwe na kustawi.

Nakumbuka mwaka Fulani nyuma..tulikuwa tunafanya kila siku jioni ibada ndogo nyumbani..Tulikusudia kupitia vitabu vyote vya biblia sura baada ya sura, kila siku sura moja..Sasa miezi michache kama miwili na nusu hivi nyuma kabla ya mwaka huo kuisha tulianza kujifunza kitabu cha Zaburi..ikawa kila siku tunasoma mlango mmoja…hivyo hivyo, kama kawaida kesho tunafuata mwingine..maana yake baada ya siku 30 tulikuwa tumeshasoma Sura 30 za kitabu hicho…

Hatukuacha hata siku moja..Wakati tunaendelea kila siku kukichambua kitabu hicho, hapo ni baada ya kumaliza baadhi ya vitabu vingine vya nyuma, sasa ilipofika tarehe 31 Disemba usiku tulikuwa tumefika sura ya 65 ya kitabu hicho cha Zaburi..Siku hiyo hatukusoma tukatenga siku hiyo iwe maalumu kwa kumsifu Mungu na kumshukuru na kumwimbia..Hivyo tukasema tutaisoma hiyo sura ya 65 kesho yake yaani tarehe 1.. Tulimwimbia Mungu na kumsifu kwa namna isiyo ya kawaida, Ilipofika terehe moja jioni, tukakusanyika tena tuendelee na kitabu chetu hicho ambacho siku hiyo tulikuwa tumefika mlango wa 65. Je! Unajua katika mlango huo ndani yake tulikutana na nini?

Tusome..

Zaburi 65:9 “Umeijilia nchi na kuisitawisha, Umeitajirisha sana; Mto wa Mungu umejaa maji; Wawaruzuku watu nafaka Maana ndiwe uitengenezaye ardhi.

10 Matuta yake wayajaza maji; Wapasawazisha palipoinuka, Wailainisha nchi kwa manyunyu; Waibariki mimea yake.

11 UMEUVIKA MWAKA TAJI YA WEMA WAKO; Mapito yako yadondoza unono”

Mstari huo wa 11 unaosema “Umeuvika mwaka taji ya wema wako”.. ndio ukawa neno la Mwaka wetu..

Ilitufariji sana…hatukujua kuwa sura hiyo ya 65, inazungumzia habari ya mwaka mpya…hivyo ukawa ndio uthibitisho Mungu kazungumza na sisi, na kutupa Neno la Mwaka….Tukafahamu kumbe, ibada zetu zote zilikuwa zinahesabiwa!..Kumbe kila sura ilikuwa inahesabiwa..na hivyo Mungu ameilengesha ile siku ya tarehe moja katika mlango ule.

Na mwaka huo ulikuwa ni mwaka wa wema kweli wa Mungu kwa wote tuliokuwepo pale..Bwana alitufanyia wema mwingi sana sana kupita kiasi..kulitimiza Neno lake hilo alilotuambia.

Hivyo leo hii neno hili pia liwe lako. Bwana akauvike mwaka wako “taji ya wema wake”. Ukaone maajabu ambayo hujawahi kuyaona katika Maisha yako. Bwana akaufanye mwaka wako huu uwe mwaka wa Pentekoste, mwaka wa kumzalia matunda, mwaka ya kuishi maisha yampendezayo mwaka wa furaha na mafanikio. Akakubariki kila unapoingia na kila unapotoka.

Lakini Pamoja na Baraka hizo zote, pia nakukumbusha mwaka huu walee wanao katika njia iliyobora Zaidi ya kumcha Mungu kuliko mwaka jana. Usimnyime mwanao mapigo pale panapostahili kwasababu biblia inasema hatakufa!. Na pia mwaka huu fanya bidii kupiga hatua moja mbele, usiwe mvivu wa kufunga, pale ikupasapo kufunga na kuomba.. Usikubali kiwango kile kile cha rohoni ulichokuwa nacho mwaka jana, uwe nacho tena mwaka huu..Zidisha kiwango chako cha usafi na utakatifu..Anza mwaka wako na Bwana, Mwaka huu hesabu matunda utakayomletea Bwana yawe ni mara 10 zaidi ya mwaka jana..Yaani kwa ufupi kila kitu ulichokizembea mwaka jana usikiruhusu kivuke mwaka huu..

Na kwa kufanya hivyo Mungu kama alivyosema katika Neno lake, atakujilia na kukustawisha na kukutajirisha sana, na kisha ATAUVIKA MWAKA WAKO TAJI YA WEMA WAKE.(Zaburi 65)..Ndivyo itakavyokuwa kwako kwa jina la YESU KRISTO.

Amen.

Heri ya mwaka mpya 2020.

Mada Nyinginezo:

NI NINI KINAKUPATA UNAPOIPUUZIA INJILI?

TUMTOLEE MUNGU VILE VINAVYOTUGHARIMU ZAIDI.

OKOA BADALA YA KUANGAMIZA!

SAA YA KIAMA.

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

Rudi Nyumbani:

Print this post