Mithali 17: 1 Afadhali mego kavu pamoja na utulivu, Kuliko nyumba yenye karamu nyingi pamoja na magomvi.
JIBU: Mego ni neno linalotokana na kitenzi “mega”,(kumega) kitu kilichomegwa, ni kama kimenyofolewa sehemu Fulani kwa sana. Kwa lugha rahisi tunaweza kusema ni kitu kidogo sana.
Sasa hapo anaposema Afadhali mego kavu, anamaanisha afadhali chakula kidogo sana (Mfano wa mkate mkavu), pamoja na utulivu, au amani, au furaha, kuliko nyumba yenye karamu nyingi pamoja na magomvi, hasira, wivu, fitna, yaani, nyumba ambayo, utapata kila kitu, utakula chakula chenye mboga saba mezani, utakunywa kila aina ya kinywaji, lakini nyuma yake kuna vikwazo, na mafarakano.
Hiyo inatufundisha pia katika mambo ya Maisha, ni heri ufanye kazi mahali utalipwa mshahara mdogo lakini, utapata nafasi ya kutulia na Mungu wako, au utafanya kazi halali itakayokupa amani, kuliko kukimbilia kazi zenye mishara mikubwa, lakini nyuma yake inakukosesha, au haikupi muda wa kutosha kumtafakari Mungu wako.
Na ndio maana sehemu nyingine biblia inatumia neno “konzi” ikiwa na maana kipimo cha mkono tu, uridhike nacho kuliko vipimo vingi lakini unataabika rohoni na mwilini.
Mhubiri 4:6 “Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kujilisha upepo”.
Kabla hatujaamua jambo lolote tunapaswa tujihakikishie kwanza usalama wa roho zetu, si kila aina ya fursa inayokuja mbele yetu ni ya kuikimbilia kisa tu inatupa donge nono, au inatupa Maisha mazuri. Wengi wamerudi nyuma kiimani, kama sio kuupoteza wokovu wao kabisa kisa tu tamaa ya “VINGI” au Tamaa ya mali.
Yupo mtu mmoja aliacha kazi ya uchungaji alioitiwa na Mungu, kisa tu haimlipi vizuri, akaingia katika biashara, akaanza kufanikiwa na kuzidi, mpaka akawa anaenda China kuleta mzigo, sikumoja akiwa njiani anaelekea katika miradi yake Daresalaam, akapata ajali mbaya sana, akafa.
Jiulize huko anatapokwenda atakuwa mgeni wa nani?
Hivyo na wewe ridhika na kile unachokipata hata kama ni mego kavu, maadamu kinakupa amani, na Muda kwa Mungu wako. Ridhika tu na hicho, hapa duniani tunapita.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho
Mada Nyinginezo:
Wibari ni nani?(Mithali 30:26)
Pomboo ni nini katika biblia?(Kutoka 25:5, Ezekieli 16:10)
Mkatale ni nini katika biblia? (Matendo 16:24)
Mpumbavu ni nani katika biblia? (Zaburi 14:1, Mithali 10:14)
Je ni wanyang’anyi wawili waliomtukana Bwana Yesu au mmoja?
Shalom jina Kuu la Mwokozi wa Ulimwengu, Yesu Kristo libarikiwe.
Karibu tujifunze biblia, Neno la Mungu wetu lililo hai.
Katika biblia tunasoma kisa cha Nabii Mmoja aliyetumwa na Mungu kwa mfalme Yerobohamu, amtolee unabii juu ya maovu anayoyafanya, ambayo kwa hayo anawakosesha Israeli yote. Na nabii Yule alipomaliza kutoa unabii ule, kama tunavyosoma, Mungu alimwonya asirudi kupitia njia ile aliyoijia, wala asile kitu njiani, wala asiingie kwenye nyumba ya mtu yeyote. Na alipomaliza kutoa unabii ule kwa Mfalme Yeroboamu aliondoka mbele zake na kwenda kama Bwana alivyomwagiza.
Lakini tunasoma wakati yupo njiani alitokea Nabii mwingine, akamwambia kuwa “Mungu kamwonyesha kwamba arudi aingie nyumbani kwake ale”. Lakini Nabii Yule alidanganya, Mungu hakumwambia chochote. Alitaka tu Yule nabii arudi, apumzike kwake..Na Yule nabii aliyetumwa na Mungu kutoa unabii, bila kufikiri mara mbili, alijikuta anarudi na kuungana na huyu nabii wa uongo, na hatimaye kufanya dhambi.
Tusome.
1Wafalme 13:7 “Mfalme akamwambia mtu wa Mungu, Karibu nyumbani kwangu ujiburudishe, nami nitakupa thawabu.
8 Mtu wa Mungu akamwambia mfalme, Ujaponipa nusu ya nyumba yako, sitaingia pamoja nawe, wala sitakula chakula, wala sitakunywa maji mahali hapa;
9 maana ndivyo nilivyoagizwa kwa neno la Bwana, kusema, Usile chakula cho chote wala usinywe maji, wala usirudi kwa njia ile uliyoijia.
10 Basi akaenda zake kwa njia nyingine, wala hakurudi kwa njia ile aliyoijia Betheli.
11 Basi nabii mmoja mzee alikuwa akikaa katika Betheli; na wanawe wakamwendea wakamwambia kila neno alilolitenda yule mtu wa Mungu siku ile katika Betheli; na maneno aliyomwambia mfalme, hayo nayo walimwambia baba yao.
12 Baba yao akawaambia, Amekwenda zake kwa njia ipi? Kwa maana wanawe walikuwa wameiona njia ile aliyoiendea yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda.
13 Akawaambia wanawe, Nitandikieni punda. Wakamtandikia punda, naye akampanda.
14 Akamfuata mtu wa Mungu, akamkuta ameketi chini ya mwaloni, akamwambia, Je! Wewe ndiwe yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda? Akamwambia, Mimi ndiye.
15 Akamwambia, Karibu kwangu nyumbani, ule chakula.
16 Naye akamwambia, Siwezi kurudi pamoja nawe, wala kuingia pamoja nawe; wala sili chakula wala sinywi maji pamoja nawe hapa;
17 kwani nimeambiwa kwa neno la Bwana, Usile chakula wala usinywe maji huko, wala usirudi kwa njia ile uliyoijia
18 AKAMWAMBIA, MIMI NAMI NI NABII KAMA WEWE, NA MALAIKA AKANIAMBIA KWA NENO LA BWANA, KUSEMA, MRUDISHE PAMOJA NAWE NYUMBANI KWAKO, ALE CHAKULA, AKANYWE MAJI. LAKINI ALISEMA UONGO.
19 Basi mtu yule akarudi pamoja naye, akala chakula, akanywa maji nyumbani mwake.
20 Hata ikawa, walipokuwa wameketi mezani, neno la Bwana likamjia nabii yule aliyemrudisha;
21 akamlilia yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda, akinena, Bwana asema hivi, KWA SABABU UMEIASI KAULI YA BWANA, WALA HUKUISHIKA AMRI ILE ALIYOKUAMURU BWANA, MUNGU WAKO,
22 bali umerudi, ukala chakula ukanywa maji, hapo alipokuambia, Usile chakula, wala usinywe maji; maiti yako haitaliingia kaburi la baba zako.
23 Basi ikawa, alipokwisha kula chakula na kunywa maji, yule nabii aliyemrudisha akamtandikia punda. 24 Na alipokuwa amekwenda zake, simba alimkuta njiani, akamwua. Maiti yake ikatupwa njiani, na yule punda akasimama karibu naye; na yule simba naye akasimama karibu na maiti.
25 Na tazama, watu wakapita, wakauona mzoga umetupwa njiani, na yule simba akisimama karibu na mzoga, wakaenda, wakatoa habari katika mji ule alimokaa yule nabii mzee.
26 Na yule nabii aliyemrudisha njiani alipopata habari, akasema; Ndiye yule mtu wa Mungu, aliyeiasi kauli ya Bwana; kwa hiyo Bwana amempambanisha na simba, simba akamrarua, akamwua, sawasawa na neno la Bwana alilomwambia.”
Kumbuka tunaishi katika siku za mwisho, yaliyomtokea huyu mtu wa Mungu wa kweli, ndio yanayoendelea kuwatokea wengi katika siku hizi za Mwisho. Wengi wanarudishwa nyuma na kuangushwa na watu wanaojiita watumishi wa Mungu, ambao pengine hapo kwanza waliowaona wakitoa unabii wa kweli, na ukatimia, ambao hapo kwanza waliwaona wakifanya miujiza mingi, watu hawa wanajitambulisha mbele za watu kuwa ni watumishi wa Mungu, na Mungu anazungumza nao, lakini wanadanganya n.k.
Lakini jambo la kuogopesha na kustaajabisha ni kwamba, japokuwa ni waongo, ni wazinzi, ni walevi wengine..lakini upako wa Mungu haujawaacha…wataendelea kusikia sauti ya Mungu ikiwapa unabii wa kweli, wataendelea kufanya miujiza mingi..LAKINI NI WAONGO!!!, mfano wa huyu Nabii mzee, alimdanganya mwenzake tena kwa jina la Bwana, lakini tunaona bado Mungu aliendelea kuzungumza naye…anaendelea kumpa unabii tena wa kweli kabisa na si wa uongo!!. Hilo ni jambo la kuogopesha sana kwa kweli, ikifunua kuwa sio tu kutoa unabii ndio tiketi ya kuwa mtumishi wa Mungu wa ukweli. Hapana!!..
Leo hii manabii na watumishi kama hawa wapo wengi, wanakuja na “BWANA ANASEMA HIVI, yeye hatazami mavazi anatazama roho, na wanalithibitisha neno hilo kwa kutoa ishara Fulani, ya kiungu” Lakini kumbe ni waongo, wanajua kabisa “Mwili wa mtu ni hekalu la Mungu, lakini wanadanganya makusudi ili kupata faida Fulani kutoka kwa Yule mtu”…na wengi pasipo kusimama katika Neno la Mungu wanachukuliwa na uongo wao.
Kwamfano Neno la Mungu limetuambia…
Luka 9:23 “Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate”.
Na tena inasema..
Luka 17:32 “Mkumbukeni mkewe Lutu.
33 Mtu ye yote atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza; na ye yote atakayeiangamiza ataiponya”.
Lakini anatokea Mtu anayejiita (mtumishi wa Mungu), anakuambia.. Kumfuata Yesu hakuna haja ya kujikana, huna haja ya kubeba msalaba wako, huna haja ya kuacha kuvaa nguo za kikahaba, huna haja ya kuacha kupaka wanja na lipstick, huna haja ya kumwacha mtu unayeishi naye ambaye si mke wako/mume wako, huna haja ya kuuacha ulimwengu!!…. Nataka nikuambie, unarudishwa Betheli na huyo Nabii bila wewe kujijua!. Jiokoe nafsi yako, rudi katika agizo la awali la Mungu katika Neno lake.
Biblia ndio kitabu pekee kinachotupa maelekezo sahihi jinsi ya kuishi kulingana na mapenzi ya Mungu, na si unabii wa mtu yeyote, akitokea mtu yeyote akitoa unabii, na ule unabii unakinzana na Neno la Mungu, biblia imetuonya tusimsikilize huyo nabii haijalishi katoa ishara kubwa kiasi gani, hata kama atashusha moto kama Eliya, lakini kama atatuambia ni ruksa kuishi maisha ya uzinzi, huyo nabii tumeambia tujihadhari naye.
Kumbukumbu 13: 1 “Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu,
2 ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo;
3 wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote.
4 Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye”
Dada Mhubiri wako anayekuambia kuwa kuvaa vimini na suruali si dhambi!..anakudanganya, usipumbazike na unabii anaotoa,au ishara anazozifanya..wewe litazame Neno la Mungu…linalosema.
1Timotheo 2:9 “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe KWA MAVAZI YA KUJISITIRI, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu. 2.11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna”.
Mhubiri anayekuambia kuwa Ulevi si dhambi, na mtu unaweza kuoa mke zaidi ya mmoja, Usimsikilize, bali lisikilize Neno la Mungu linalosema…
Waefeso 5:17 “Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.
18 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho”.
Mhubiri anayekuambia kwamba Bado sana Kristo arudi, na kwamba endelea kuponda mali, na kujitumainisha na ulimwengu…Usimsikilize, bali lisikilize Neno la Mungu linalosema..
Mathayo 24:43 “Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.
44 Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja”.
Na mambo mengine yote, yanayozungumzwa na yeyote anayejulikana kama mtumishi wa Mungu, ni muhimu kuyaweka katika mizani ya Neno la Mungu, kuyapima..kama yanakubaliana na Neno au la!..Kama hayakubaliani basi tunayaweka chini na kulifuata Neno la Mungu, kwasababu tumeshaonywa tuwe watu wa kuzipima roho.
Bwana atubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho
Mada Nyinginezo:
BASI TUENDELEE KUMJUA MUNGU,NAYE ATATUJILIA KAMA MVUA YA VULI.
Rudi nyumbani > jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Baada ya Kaini kumuua ndugu yake, na Mungu, kumlaani kwa laana ile ya kwamba atakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani, utaona alimwomba Bwana ampunguzie adhabu yake, na baada ya kupunguziwa kwa kutiwa alama, haikuishia hapo, bado Mungu alimuhakikishia usalama mwingine wa juu Zaidi. Tusome;
Mwanzo 4:14 “Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.
15 Bwana akamwambia, KWA SABABU HIYO YE YOTE ATAKAYEMWUA KAINI ATALIPIZWA KISASI MARA SABA. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga”.
Unaona hapo kwenye mstari wa 15, Bwana akimuhakikishia ulinzi wa kipekee sana. Jambo ambalo si rahisi mtu mwovu kufanyiwa na mtu yeyote, kwasababu hakuna tendo lolote la kishujaa alilotenda Kaini mpaka alipiziwe kisasi mara saba, kwa yeyote atakayemuua,ni heri ingekuwa ni mara moja, lakini mara saba, hiyo angepaswa afanyiwe mtu mwenye haki.
Tengeneza picha diktekta, ambaye ameshutumiwa kwa mauaji wa maelfu ya watu, kama vile HITLER wa ujerumani, leo hii, unasikia Mungu anasema mtu yeyote atakayemuua Hitler atalipizwa kisasi mara saba, unaweza kudhani Mungu anafurahishwa na maovu. Ndivyo ilivyokuwa kwa Kaini, Mungu haoni shida kumuhakikishia mwovu ulinzi na mafanikio. Hilo tunapaswa tulijue.
Lakini afadhali ingeishia kwa Kaini tu, Tabia yake ya uuaji iliendelea mpaka kwa uzao wake. Utaona yupo mmoja aliitwa, Lameki, yeye alikuwa muuaji kuliko hata baba yake, anasema alimuua mtu kwa kumtia jeraha tu, alimuua mtu kwa kumchubua tu, akiwa na maana mtu aliyemkosea kwa jambo dogo sana alikuwa radhi kumuua, bila kujali chochote.
Huku akitumia kivuli kile kile cha baba yake, cha usalama aliohakikishiwa na Mungu, tena na Zaidi, anasema kama ikitokea mtu atataka kumlipizia kisasi kwa uuaji wake, basi akumbuke kuwa Mungu atamlipizia sio tu mara saba, bali mara saba sabini.
Mwanzo 4:23 “Lameki akawaambia wake zake, Sikieni sauti yangu, Ada na Sila; Enyi wake za Lameki, sikilizeni usemi wangu; Maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha; Kijana kwa kunichubua;
24 Kama Kaini akilipiwa kisasi mara saba, Hakika Lameki atalipiwa mara sabini na saba”.
Unaona? Walikuwa wanajiamulia kufanya mauaji tu kama vile kuchinja kuku, kwasababu walijua hakuna laana yoyote itakayowapata,. Hiyo ndio sababu ulimwengu wa kipindi kile ulizidi kuwa mwovu kupitiliza, mpaka ikafikia hatua ya Mungu kusema, mwisho wa kila mwanadamu umefika.
Mwanzo 6:5 “Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote.
6 Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.
7 Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya…….
11 Dunia ikaharibika mbele za Mungu, dunia ikajaa dhuluma.
12 Mungu akaiona dunia, na tazama, imeharibika; maana kila mwenye mwili amejiharibia njia yake duniani.
13 Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia.
Lakini siku moja ilipofika Gharika kubwa ilishuka ikauangamiza ulimwengu wote, wakapona tu watu 8, yaani Nuhu pamoja na familia yake. Na adhabu yao haikuishia tu, pale, bado huko kuzimu walipo sasa hivi, wanaendelea na mateso makali yasiyokuwa ya kawaida.
Ndugu yangu, fahamu kuwa Mungu anaweza kukuahidia ulinzi, na usalama, na afya na amani, na furaha, angali bado upo katika dhambi zako, hilo sio jambo gumu kwake kukupa, liweke tu akilini, angali ukiwa unafanya uchawi wako bado Mungu anaweza kukuhakikishia Maisha ya heri hapa duniani, angali unaua watu, unauza madawa ya kulevya unauza pombe, unazini nje ya ndoa.. Bado Mungu atakuhakikishia ustawi wa mambo yako.
Hivyo usishangae kwanini waovu hawakumbwi na madhara yoyote, tena Zaidi ndio wanafanikiwa na kustarehe kama ulivyokuwa uzao wa Kaini, jinsi ulivyokuwa na mafanikio makubwa duniani, kuliko hata ule uzao wa Sethi lakini mwisho wao ulikuwa ni gharika.
Huu si wakati wa kustarehe katika dhambi, kisa tu hatuoni dhara lolote mbele yetu, tujue kuwa sisi watu wa kizazi hichi ndio tupo katika hatari kubwa ya kukumbana na ghadhabu kali ya Mungu, inayokaribia kuja duniani hivi karibuni, kuliko hata vizazi vingine vya nyuma vilivyotangulia.
Kwasababu maovu tunayoyafanya sasa hivi, yamezidi hata yale ya wakati wa Nuhu, licha ya kwamba sisi tumeshaufahamu ukweli wote na kuiona njia..
Bwana Yesu alisema.
Mathayo 11:23 “Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo.
24 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe”.
Ndugu, Tubu dhambi zako, usipumbazwe na ulinzi wa Mungu, angali upo bado katika dhambi, hizi ni siku za mwisho, mwisho wa dunia upo karibu sana, dalili zote zimeshatimia, Jiulize UNYAKUO ukipita leo, utakuwa wapi ndugu yangu? Utamweleza nini Kristo siku ile ya hukumu, utamwambia mimi sikusikia injili? Na wale wa Sodoma na Gomora ambao sasahivi wapo kuzimu waseme nini?
Tafakari Maisha yako, duniani hapa tunapita, na vitu vyote vinapita,. Mgeukia Kristo ayabadilishe Maisha yako leo ili akufanye kuwa kiumbe kipya, kisha uishi Maisha ya kama mtu anayemsubiria Kristo kweli kweli, na sio kama mtu wa kidunia, acha kudhani kuwa Mungu haioni maovu unayotenda.
Bwana atusaidie sote.
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho
Mada Nyinginezo:
USIOMBE MAOMBI YASIYOKUWA NA MAJIBU NA WALA USIMTUKANE MUNGU.
Ni muhimu kufahamu kuwa kila kitu kilichopo sasa au kitakachokuja tayari kilishatabiriwa. Watu wanaomtafuta Mungu walishatabiriwa na vile vile watu watakaomkataa Mungu tayari wameshatabiriwa.
Kadhalika upo unabii wa watakaokolewa siku za mwisho, na upo unabii wa watakaotupwa katika lile ziwa la moto.
Unabii wa watakaokolewa siku ya mwisho, ni kama huu ufuatao…
Mathayo 8:11 “Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;”
Na unabii wa watakaopotea siku za mwisho ni kama huu ufuatao…
Mathayo 7:22 “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.
Sasa nabii hizo mbili ni lazima zitimie kama zilivyotabiriwa, maana yake watakuwepo watu watakaokolewa na watakaopotea, hakuna namna yeyote jambo hilo litaepukika, wala kubadilishwa, hata tufunge na kuomba Nabii hizo mbili lazima zitimie.. watakuwepo watakaokwenda jehanamu!..na watakuwepo watakaoenda mbinguni.
Sasa kitu cha kipekee katika Nabii zote Mungu anazozitoa huwa HATAJAGI MAJINA, Kwamba Fulani na Fulani ndio wataokolewa, na Fulani na Fulani ndio watakaopotea. Hapana! Kamwe hatoi majina, ikiwa na maana kuwa nafasi ya kwenda mbinguni ipo kwa kila mtu, vile vile nafasi ya kwenda motoni ipo kwa kila mtu. Hivyo nijukumu la kila mtu kuhakikisha anapambana kuwepo miongoni mwa watakaokolewa, na si miongoni mwa wanaopotea. Na kama akishinda maana yake atakuwa katika lile kundi la waliotabiriwa uzima wa milele. Lakini akishindwa atakuwa miongoni mwa waliotabiriwa kuingia kwenye adhabu ya milele.
Hivyo hata utabiri wa Yuda kumsaliti Bwana Yesu haukumtaja jina kwamba atatokea Mtu Fulani anayeitwa Yuda, huyo atamsaliti Bwana. Hapana! Hakuna utabiri wowote unaosema hivyo.. bali ulitaja tu tabia.
Zaburi 41:9 “Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake”
Maana yake ni kwamba miongoni mwa wale mitume 12, kila mmoja alikuwa anayo nafasi ya kumsaliti Bwana na kutimiza unabii huo!, na vile vile kila mmoja alikuwa na nafasi ya kutomsaliti Bwana. Sasa inapotokea mmoja anayeendekeza hiyo tabia ya kutokujali, zaidi ya wengine wote, pamoja na kwamba anaonywa na anaujua ukweli, lakini hataki kubadilika na kuufuata ukweli, basi huyo ndio anachukua nafasi ya kutimiza huo unabii. Na miongoni mwa wanafunzi wa Bwana wote, ni Yuda pekee ndiye aliyekuwa anaonyesha tabia za kutokujali, alikuwa ni mtu wa kupenda fedha, hata alikuwa anafikia hatua ya kuiba katika mfuko wa Bwana. Ingawa Bwana alishawambia mapema kwamba mmoja wao atamsaliti, lakini Yuda kwa kulijua hilo wala hakujali, wakati wengine walitilia maanani, na kujizuia kwa hali zote ili wasimsaliti Bwana, lakini Yuda hakujali, na mwishowe..akawa yeye ndiye aliyetimiza huo unabii… “Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake”
Hivyo kwa hitimisho ni kwamba, Yuda alikuwa na hatia kuisaliti damu ya Bwana Yesu, na alifanya dhambi.
Lakini ya Yuda yamepita, Na unabii wake kashautimiza, tumebaki sisi, tunaoishi sasa…je na sisi unabii wetu ni upi?
Tusome 2Timotheo 3….
2Timotheo 3:1 “Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.
2 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,
3 wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,
4 WASALITI, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;
5 wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao”.
Hapo Mstari wa 4 hapo unasema, watatokea watu WASALITI, na sio wasaliti tu!, bali pia watakuwa wakaidi, wenye kujivuna, wakali, wasiopenda mema n.k.. Yuda alikuwa ni MSALITI tu!, lakini hakuwa na hizo tabia nyingine. Lakini hawa wa siku za mwisho wametabiriwa kuwa na usaliti pamoja na tabia nyingine mbaya nyingi juu yake.
Jiulizae kama wewe ni miongoni mwa hao?.. kama una tabia moja wapo ya hizo au baadhi ya hizo, basi fahamu kuwa unautimiza huo unabii bila ya wewe kujua, hivyo huna sababu ya kumshangaa, wala kumlaumu Yuda kwa kumsaliti Bwana, kwasababu wewe ni zaidi ya Yuda.
Bwana atusaidie, tusiwe miongoni mwa watakaotimiza unabii wa watu waovu wa siku za mwisho, bali tutimize unabii wa watu wema watakaotokea siku za mwisho,ambao wataurithi uzima wa milele.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho
Mada Nyinginezo:
Nini maana ya “Siku moja nyuani mwa Bwana ni bora kuliko siku elfu”?
Moja ya mambo muhimu kuyafahamu pia ni kuhusu Roho Mtakatifu. Kwasababu Roho Mtakatifu ndio ukamilifu wa sauti ya Mungu kwetu..
Sasa kabla ya kwenda kuzitazama kazi kuu tatu za Roho Mtakatifu, hebu tuweke msingi kidogo wa kuufahamu utendaji kazi wa Mungu, katika ofisi zake tatu.
Wakati wa agano la kale, Mungu alizungumza na watu kutoka mbinguni, mwanzo wa agano hili jipya Mungu akazungumza na sisi ndani ya mwili wa Bwana Yesu.(Waebrania 1:2), na baadaye akazungumza na sisi kupitia Roho Mtakatifu. Ni sawa na kusema.. Mungu alizungumza nasi akiwa juu yetu(Kama Baba), kisha akazungumza nasi akiwa pamoja nasi katika mwili wa kibinadamu (Imanueli) na mwisho Mungu anazungumza ndani yetu kama(Roho Mtakatifu).
Katika hatua hizi tatu, hatua hiyo ya mwisho ndio hatua kamilifu kuliko nyingine zote, kwasababu Ni sauti ya Mungu iliyo karibu sana na sisi kuliko ilivyokuwa juu yetu (kama Baba), au ilivyokuwa pamoja nasi (kama mwana).
Ni sawa mtu azungumze na wewe kwa sauti kuu akiwa juu kabisa kwenye gorofa, kiasi kwamba humuoni ila unachoweza kusikia ni sauti yake tu na wewe upo chini ya hilo ghorofa, bila shaka kuna maneno ambayo unaweza usiyasikie vizuri kwasababu yupo mbali, hivyo maneno mengine unaweza kuyaelewa kinyume na alivyosema.. Lakini huyo mtu atakapotoka huko aliko na kushuka chini ukamwona, akawa kama mita 5 kutoka mahali ulipo, akizungumza na wewe ni rahisi kumsikia vizuri kuliko alivyokuwa kule juu, ambapo ulikuwa unasikia sauti tu na sasa unamsikia na kumwona, lakini pia bila shaka wakati anazungumza kuna maneno unaweza usiyasikie vizuri, hata wewe unapozungumza na mtu aliye karibu na wewe ni lazima utapitia vipindi vichache vichache vya kuomba arudie alichosema…
Lakini hebu tafakari tena endapo huyo huyo mtu akikukaribia sana kiasi kwamba mdomo wake unafika katika sikio lako, bila shaka hapo utakuwa unamsikia vizuri zaidi kuliko alivyokuwa mita mbili mbele yako..hapo huwezi kumwambia arudie rudie yale anayoyasema.. Hivyo utamsikia vizuri kuliko kawaida, na utamwelewa, kwasababu amesogea karibu sana na wewe.
Na utendaji kazi wa Mungu ni hivyo hivyo, Roho Mtakatifu ni sauti ya Mungu iliyo karibu sana na sisi, haijaishia kusikika masikioni tu, bali inasikika hadi mioyoni mwetu. Ni sauti isiyo na chenga chenga. Sauti ya Bwana Yesu ilikuwa ni kamilifu, lakini ilikuwa na chenga chenga kwetu, hatukuweza kumwelewa vizuri kwasababu alikuwa anazungumza nje ya miili yetu. Ndio maana ilimpasa Bwana aondoke ili Yule Roho aje juu yetu.
Yohana 16:7 “ Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu”.
Umeona hapo? Bwana hana budi kuondoka ili Roho Mtakatifu aje…(Na kumbuka Roho Mtakatifu ndiye Yule Yule Bwana Yesu mwenyewe, isipokuwa anakuja katika roho (soma 2Wakorintho 3:17),
Sasa baada ya kuelewa hayo, twende kwa pamoja tukazitazame kazi kuu tatu za Roho Mtakatifu kwa ulimwengu.
1) Kazi ya kwanza ni kuuhakikisha ulimwengu kwa habari ya DHAMBI 2) Atauhakikisha kwa habari ya HAKI 3) Atauhakikisha kwa habari ya HUKUMU.
Hizi ndio kazi kuu tatu za Roho Mtakatifu kwa Ulimwengu, tutaziangalia moja baada ya nyingine.
1. Kwa habari ya dhambi:
Yohana 16:8 “Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.
9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi”
Kuhakikisha maana yake ni “kuweka sawa jambo”. Kitu ambacho hakikukaa vizuri sasa kimewekwa vizuri maana yake kitu hicho“kimehakikiwa”. Kadhalika Hapo Bwana Yesu anasema huyo Roho atakapokuja atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, maana yake hapo kwanza yeye alizungumza kuhusu dhambi lakini hakueleweka vizuri, lakini atakapokuja huyo Roho ataizungumzia vizuri dhambi kwa sauti ya ukaribu zaidi, na atafanya wengi kuelewa dhambi ni nini, kuliko jinsi wangemwelewa Bwana.
Ndio maana Bwana Yesu anasema hapo… “Kwa habari ya dhambi, KWA SABABU HAWANIAMINI MIMI ”… maana yake yeye aliihubiri sana kuhusu dhambi, lakini watu hawakumwamini. Hivyo Roho Mtakatifu atakuja kuielezea vizuri na wengi wataamini. Na kumbuka dhambi ni “kutomwamini Mwana wa Mungu, kwamba yeye ndiye mkombozi wa ulimwengu”. Hiyo ndiyo dhambi…hayo mengine kama uasherati, wizi, uchawi, uuaji n.k ni matokeo ya dhambi. Kwahiyo Bwana Yesu alihubiri sana kwamba “kila amwaminiye atapata uzima wa milele lakini Yule asiyemwamini atahukumiwa, maana yake atakuwa na dhambi”. Lakini pamoja na kuyasema hayo sana kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu, si wengi waliomwamini, ndio maana injili haikufika duniani kote, kipindi Bwana Yesu yupo duniani anahubiri. Ni wachache tu ndio waliokuwa wanaisikia sauti yake, wengine walikuwa hawamwelewi.
Lakini baada ya Roho Mtakatifu kushuka siku ile ya Pentekoste, Petro alivyosimama siku ile kuhubiri habari ya dhambi, biblia inasema watu zaidi ya elfu tatu waliokoka ndani ya siku moja.(Matendo 2:41). Na wakati miezi miwili tu nyuma, Bwana Yesu alizungumza maneno hayo hayo, tena mji ule ule Yerusalemu, lakini waliishia kumsulubisha, kwasababu hawakumwelewa.
Yohana 12:37 “Walakini ajapokuwa amefanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, hawakumwamini;
38 ili litimie lile neno la nabii Isaya alilolisema, Bwana, ni nani aliyezisadiki habari zetu; Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?”
Lakini miezi miwili tu baadaye kama tunavyosoma katika kitabu cha Matendo 2, Roho Mtakatifu alipozungumza kwa kinywa cha Petro, wale ambao hawakumwamini Bwana Yesu Yerusalemu, walianza kumwamini kwa kasi sana.
2. Kwa habari ya HAKI.
Yohana 16:10 “kwa habari ya haki, kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena”
Katika kipengele ambacho Bwana hakukigusia kabisa wakati yupo hapa duniani, ni kipengele cha HAKI. Na haki inayozungumziwa hapo, ni haki ile ipatikanayo kwa njia ya IMANI. Hii Bwana hakuigusia kabisa, na lengo la kutoielezea hii ni kwasababu ya ugumu wa mioyo ya watu, Ndio maana aliwaambia “yapo mambo ya kuwaambia lakini kwa wakati huo wasingeweza kustahimili,mpaka huyo Roho atakapokuja”
Yohana 16:12 “Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, LAKINI HAMWEZI KUYASTAHIMILI HIVI SASA.
13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake”.
Umeona jambo mojawapo ambalo wasingeweza kustahimili endapo wangeambiwa ni hilo la “HAKI”. Laiti Bwana angewafunulia siri Mitume kwamba, sisi watu wa mataifa nasi ni warithi wa ahadi za Mungu, kwamba kwa NEEMA tunahesabiwa HAKI kwa Kumwamini Yesu, kwamba na sisi ni warithi wa ahadi za Mungu, ni dhahiri kuwa wangerudi nyuma. Wangesema Bwana Yesu kachanganyikiwa. Yule aliyemwita Yule mwanamke wa kimataifa “Mbwa” halafu leo anamwita “mrithi”?.. Yule ambaye aliwatuma na kuwaambia “msifike miji ya mataifa kuhubiri (Mathayo 10:5)” ghafla anawaita tena mataifa ni warithi!!… Yule aliyesema “sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli (Mathayo 15:24)”. Leo hii yeye ndio atutume sisi huko kwao kuhubiri??.. Hakika amechanganyikiwa.
Hivyo Bwana aliliacha hilo hakuwaambia mitume, pamoja na mengine mengi ili yaje kufunuliwa na Roho Mtakatifu baada ya kuondoka kwake. Kwasababu kwa uchanga waliokuwa nao Mitume, wangeambiwa hizo siri, wangemwacha Bwana na kurudi nyuma (wasingeweza kustahimili)
Na siku ya kuifunua hiyo siri ya HAKI YA MUNGU ilipofika, Roho Mtakatifu alimfunulia kwanza Mtume Petro, kipindi kile cha lile ono la Kornelio, na baada ya hapo alikuja kumfunulia tena Mtume Paulo hiyo siri..
Hebu soma hichi kisa taratibu..
Matendo 11:1 “Basi mitume na ndugu waliokuwako katika Uyahudi wakapata habari ya kwamba watu wa Mataifa nao wamelipokea neno la Mungu.
2 Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemu, wale walio wa tohara wakashindana naye,
3 wakisema, Uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao.
4 Petro akaanza kuwaeleza kwa taratibu, akasema,
5 Nalikuwa katika mji wa Yafa, nikiomba, roho yangu ikazimia, nikaona maono; chombo kinashuka, kama nguo kubwa inatelemshwa kutoka mbinguni kwa pembe zake nne, kikanifikilia.
6 Nikakitazama sana, nikifikiri, nikaona wanyama wa nchi wenye miguu minne, na wanyama wa mwituni, nao watambaao, na ndege wa angani.
7 Nikasikia na sauti ikiniambia, Ondoka, Petro, ukachinje ule.
8 Nikasema, Hasha, Bwana, kwa maana kitu kilicho kichafu au kilicho najisi hakijaingia kabisa kinywani mwangu.
9 Sauti ikanijibu mara ya pili kutoka mbinguni, Alivyovitakasa Mungu, usivinene wewe najisi.
10 Jambo hili likatendeka mara tatu, kisha vitu vyote vikavutwa tena juu mbinguni.
11 Na tazama, mara hiyo watu watatu wakasimama mbele ya nyumba tuliyokuwamo, waliotumwa kwangu kutoka Kaisaria.
12 Roho akaniambia nifuatane nao, nisione tashwishi. Ndugu hawa sita nao wakaenda pamoja nami, tukaingia katika nyumba ya mtu yule;
13 akatueleza jinsi alivyomwona malaika aliyesimama nyumbani mwake na kumwambia, Tuma watu kwenda Yafa ukamwite Simoni aitwaye Petro,
14 atakayekuambia maneno ambayo yatakuokoa, wewe na nyumba yako yote.
15 Ikawa nilipoanza kunena, Roho Mtakatifu akawashukia kama alivyotushukia sisi mwanzo.
16 Nikalikumbuka neno lile la Bwana, jinsi alivyosema, Yohana alibatiza kwa maji kweli, bali ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.
17 BASI IKIWA MWENYEZI MUNGU AMEWAPA WAO KARAMA ILE ILE ALIYOTUPA SISI TULIOMWAMINI BWANA YESU KRISTO, MIMI NI NANI NIWEZE KUMPINGA MUNGU?”
Umeona hapo? Kornelio ambaye ni mtu wa Mataifa anapokea Roho Mtakatifu baada ya kuamini, tena Roho Yule Yule waliyepokea wakina Petro walio waisraeli, bila shaka Petro alijua ni kwanini Bwana Yesu hakuwaambia hiyo siri wakati wapo duniani, alijua ingekuwa ni ngumu wao kumeza!… Maana unaona hapo juu tu kama tulivyosoma, mitume wengine walipopata habari ya kwamba Petro kaingia kwa watu wa mataifa, walishindana naye vikali..Mpaka Petro alipowaelezea kwa utaratibu..
Hiyo ndiyo siri ya Mungu ambayo ilisitirika tangu zamani, kwamba sisi watu wa MATAIFA, ni warithi wa ahadi za Mungu, kwamba tunahesabiwa HAKI YA KUURITHI UZIMA WA MILELE bure kwa njia ya IMANI YA KUMWAMINI YESU, Mitume hapo kabla walidhani wokovu ni kwaajili yao tu! (Wayahudi), lakini kumbe sivyo!.. hata watu wa mataifa pia..
Mtume Paulo naye aliielezea siri hii katika Wakolosai 1:26-27, na katika Waefeso 3:6, unaweza kuisoma mistari hiyo binafsi.
Hiyo ndio maana Bwana Yesu akasema kwamba…. “kwa habari ya haki, kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena”…..Maana yake alipaswa aelezee hiyo Haki, lakini anaondoka anakwenda kwa Baba na wala hawatamwona tena, na wala hataielezea hiyo siri, lakini Roho atakuja kuliweka hilo sawa!..maana yake atalifunulia kanisa.
3. Kwa habari ya HUKUMU.
Yohana 16:11 “kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa”.
Hapo mkuu wa Ulimwengu anayezungumziwa ni “shetani”. Na Bwana Yesu anasema…Mfalme wa ulimwengu amekwishahukumiwa.. Sasa hukumu inayozungumziwa hapo si ile ya ziwa la moto, (Hiyo ni kweli ilishapitishwa kitambo), lakini hukumu inayozungumziwa hapa si hiyo, bali ni hukumu ya kunywang’anywa mamlaka ya ulimwengu!!. Na kwamba mamlaka yote ya Duniani amekabidhiwa Yesu.
Na mamlaka hayo shetani aliyapoteza wakati Bwana Yesu akiwa hapa duniani!. Kwajinsi alivyoutoa uhai wake kwaajili ya wengi, akakabidhiwa mamlaka yote ya mbinguni na duniani.
Mathayo 28:18 “Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, NIMEPEWA MAMLAKA YOTE MBINGUNI NA DUNIANI”.
Sasa atakapokuja Roho Mtakatifu, ataliweka hilo sawa katika mioyo ya watu wengi, Watu wataelewa kwa undani ni kwa jinsi gani sasa hivi YESU NDIYE ANAYETAWALA MBINGUNI NA DUNIANI, NA HAKUNA MFALME MWINGINE KAMA YEYE. Mitume hawakumwelewa Bwana Yesu vizuri wakati wakiwa naye!!. Walikuja kumwelewa vizuri baada ya kuondoka kwake!. Kwamba alikuwa ni nani?.. Yule Yohana ambaye alikuwa anaegemea kifuani pa Yesu, ambaye alikuwa anamwona Bwana Yesu kama kaka yake tu! (Yohana 13:23)… Huyo huyo anakuja kumwona Bwana Yesu katika kisiwa cha Patmo kama miale ya moto, na anaanguka chini ya miguu yake kama mtu aliyekufa!! (Kasome Ufunuo 1). Roho Mtakatifu anamfunulia Yule Yule Yesu kama Mfalme wa wafalme, ambaye enzi na mamlaka yote ni zake.
Waefeso 1:20 “aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;
21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;
22 AKAVITIA VITU VYOTE CHINI YA MIGUU YAKE, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo
23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote”
Hivyo Roho Mtakatifu, atakapokuja atauonyesha ulimwengu kuwa YULE mkuu wa ulimwengu, shetani…hata kitu! Mbele za Bwana, kashashindwa…
Yohana 14:30 “ Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu”
Hana mamlaka yoyote juu ya wote waliomwamini Yesu..kashahukumiwa na kunyang’anywa mamlaka ya duniani na kuzimu. Wafu wote wanamilikiwa na Bwana Yesu (Warumi 14:9), maana yake ni kwamba mfano wa jambo lililotokea kwa Samweli, kuletwa juu na yule mchawi, kwasasa haliwezekani tena, kwasababu mkuu wa ulimwengu kashahukumiwa (kashanyang’anywa hayo mamlaka), anayewamiliki wafu wote kwasasa ni Mkuu wa Uzima, YESU!. Huyo pekee yake ndiye mwenye mamlaka ya kuileta roho ya mtu juu na kuishusha chini, yeye peke yake ndiye mwenye mamlaka na uwezo wa kufufua au kuua!.
Kwahiyo kwa kazi hizo tatu ambazo Bwana Yesu alizozitaja, ndizo zinazokamilisha ushuhuda kamili wa Roho Mtakatifu kwa ulimwengu!!..
Na Roho huyo ndiye anayeshuhudia hata sasa…Na anashuhudia kwa vinywa vya watumishi wake waliojazwa na Roho Mtakatifu, Kwamba Kristo ni kweli!, na Watu wote kutoka mataifa yote na makabila yote anawapokea na kuwakubali na kuwahesabia Haki ya kupata uzima wa milele endapo watamjia, Kadhalika Bwana YESU ndiye mmiliki wa mbingu na nchi na shetani hana kitu mbele zake. Hivyo yeye ndio tumaini pekee la kulikimbilia na kulitegemea.
Je umezitii ushuhuda hizo za Roho Mtakatifu???.. kwa Kumpokea Yesu maishani mwako na kutubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha kabisa???, kumbuka yeye anapokea watu wote haijalishi ni kutoka Taifa gani, wala kabila gani.
Kama bado hujamwamini, basi fahamu kuwa umeukataa ushuhuda wa Roho Mtakatifu maishani mwako.. Na hivyo utakuwa na HATIA kubwa, kwasababu Roho Mtakatifu amezungumza na wewe kwa sauti ya kueleweka kabisa, hivyo umeukataa ushuhuda ulio mkamilifu kabisa.
Hivyo mpokee leo Yesu maishani mwako, Ukubali ushuhuda wa Roho Mtakatifu, ili ufanikiwe katika roho yako, biblia inasema yeye Roho Mtakatifu anatutamani kiasi cha kutuonea wivu, anatamani aingie ndani yako kuliko wewe unavyotamani aingie ndani yako, hivyo ulichobakisha tu ni kutii!.. kwa kutubu dhambi zako na kwenda kubatizwa ubatizo sahihi, kama bado hujabatizwa. Kumbuka ubatizo sahihi ni ule wa maji mengi (Yohana 3:23), na kwa jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38).
Na baada ya hapo, Neema ya kipekee ya Bwana itakuwa nawe daima.
Bwana atubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho
Mada Nyinginezo:
Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?
Jibu: Tusome.
Marko 6.7 “Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu;
8 akawakataza wasichukue kitu cha njiani ISIPOKUWA FIMBO TU; wala mkate, wala mkoba, wala pesa za bindoni;
9 lakini wajifungie viatu; akasema, Msivae kanzu mbili.
10 Akawaambia, Mahali po pote mtakapoingia katika nyumba, kaeni humo hata mtakapotoka mahali pale”
Hapo Bwana aliwakataza wasichukue chochote katika safari yao, maana yake huko wanakokwenda watavipata vyote, wasitie wasiwasi, kwamaana endapo wakianza kutia wasiwasi na kuvisumbukia vitu hivyo kwamba huko wanakokwenda watakula nini, watalala wapi, watavaa nini..itawasababisha kupoteza umakini wa hiyo kazi wanayoiendea, itawagharimu kuanza kwanza kutafuta fedha za kutosha, itakayowawezesha kwenda kukaa siku hizo zote na kurudi.. Hivyo Bwana kwa kulijua hilo akawaambia wasibebe chochote hata chakula kwasababu Mungu atawapatia huko waendako.
Lakini pamoja na kwamba aliwaambia wasibebe chochote, mwisho aliwaambia “isipokuwa fimbo tu”
Sasa kwanini fimbo?
Fimbo si chakula, wala si fedha..bali ni kifaa ambacho kilikuwa kinawasaidia watu katika kutembea.. Kwa nyakati zetu hizi, mara nyingi ni wazee ndio wanaotumia fimbo, lakini zamani marika yote walikuwa wanatembea na fimbo, kwasababu kuna nyakati za kutembea umbali mrefu, na kupanda milima na kushuka, hivyo fimbo ilikuwa ni kifaa cha msaada sana, katika hayo mazingira..hususani katika kupandia milima.
Hivyo wanafunzi katika kwenda kuhubiri kwao, hapana shaka watapanda milima mingi na mabonde mengi ili kuwafikia kondoo wa Mungu waliotapakaa huko na kule, hivyo kifaa hicho ni cha muhimu kwao, ndio maana Bwana akawaambia wakibebe.
Hata sasa, agizo la Bwana ni hilo hilo, popote tuendapo, atuagizapo kwenda kuhubiri, tusiangalie hali tulizonazo…kwasababu huko tuendapo atatufungulia mlango wa kupata riziki, sisi tufikiri tu kusudi lake, mengine tumuachie yeye..Ndio maana baadaye tunaona wanafunzi waliporudi walitoa ushuhuda kuwa hawakupungukiwa..
Luka 22:35 “Akawauliza, Je! Hapo nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? WAKASEMA, LA!”
Bwana ni Yule Yule, hajabadilika kama aliwatuma wanafunzi wake bila chochote lakini hawakupungukiwa katika safari zao, hata sisi atakapotutuma hatutapungukiwa. Tunachopaswa kufanya ni kumwamini tu na kujinyenyekeza chini yake na kuukubali utumishi wake kwa moyo wote. Hayo mengine tumwachie yeye, atahakikisha anatuhudumia.
Bwana atubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho
Mada Nyinginezo:
Shalom! karibu tujifunze biblia, Neno la Mungu wetu, taa iongozayo miguu yetu na Mwanga wa njia yetu, iendayo mbinguni.
Katika biblia tunaona yapo maagizo mengi ambayo Mungu wetu ametupatia Moja kwa moja, Kwamfano agizo la Upendo!. Hili ni agizo ya kwamba ni lazima tupendane!
1Yohana 3:10 “Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.
11 Maana, hii ndiyo habari mliyoisikia tangu mwanzo, KWAMBA TUPENDANE SISI KWA SISI”
Maana yake tusipokuwa na upendo! Hata tufanye nini hatuwezi kuiona mbingu, haijalishi tutanena kwa lugha kiasi gani, haijalishi tutatoa unabii, na kufanya miujiza mikubwa kiasi gani…
1Wakorintho 13: 1 “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
2 TENA NIJAPOKUWA NA UNABII, NA KUJUA SIRI ZOTE NA MAARIFA YOTE, NIJAPOKUWA NA IMANI TIMILIFU KIASI CHA KUWEZA KUHAMISHA MILIMA, KAMA SINA UPENDO, SI KITU MIMI.
3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu”.
Hayo ni maagizo ya moja kwa moja ambayo tumepewa. Lakini pia yapo maagizo ambayo hatujapewa moja kwa moja, lakini tusipoyafanya tutahukumiwa kwayo.
Leo tutajifunza Agizo moja la msingi, ambalo hatujaagizwa, lakini ni wajibu wetu kulitenda….(Tafadhali naomba usome kwa makini huku ufahamu wako ukiupeleka katika kupata kitu kipya na si kutafuta kasoro, akili yako ukiipeleka katika kutafuta kasoro, shetani atakusaidia kuipata, lakini ukiipeleka katika kujifunza basi utapata kitu kipya).
Sasa agizo hilo si linguine zaidi ya “UTOAJI”.
Suala la utoaji limekuwa lango la watu wengi kuingia katika wokovu na kutokea. Wapo ambao wakisikia kuhusu utoaji wanalipokea Neno hilo kwa furaha na kuwasogeza zaidi kwa Mungu na wapo ambao wakilisikia, ndio linawatoa zaidi kwa Mungu..Na ndio linakuwa tiketi/sababu ya kuuacha wokovu kabisa kabisa, kwasababu ndani ya fahamu zao shetani kashawapandikizia mbegu ya kwamba wanataka kunyonywa vya kwao. Hivyo shetani analichukua wazo hilo na kuwahubiria waiache njia ya wokovu au waidharau. Lakini leo nataka tupate akili mpya kuhusu Utoaji, ili itusaidie tusije tukakosa kuingia katika ufalme wa mbinguni.
Kabla ya kuendelea mbele hebu tusome mistari michache, tuilinganishe na mingine kisha tutapata kuelewa kiini cha somo letu la leo. (Katika mistari hiyo zingatia vipengele vilivyoanishwa kwa herufi kubwa)
Mathayo 10:7 “Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.
8 Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; MMEPATA BURE, TOENI BURE.
9 Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu;
10 wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; MAANA MTENDA KAZI ASTAHILI POSHO LAKE.
11 Na mji wo wote au kijiji cho chote mtakachoingia, tafuteni ni nani humo aliye mtu mwaminifu; mkae kwake hata mtakapotoka.
12 Nanyi mkiingia katika nyumba isalimuni.
13 Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikilie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi. 14 NA MTU ASIPOWAKARIBISHA wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung’uteni mavumbi ya miguuni mwenu.
15 Amin, NAWAAMBIA, ITAKUWA RAHISI NCHI YA SODOMA NA GOMORA KUSTAHIMILI ADHABU YA SIKU YA HUKUMU, KULIKO MJI ULE”.
Maagizo hayo ni Bwana Yesu aliwapa wanafunzi wake, wakati anawatuma kwenda kuhubiri, akawaambia wanapotoka wasibebe chochote, (fedha au chakula) kwasababu huko wanakokwenda, Mungu atawafungulia mlango wa kuvipata hivyo, maana yake wapo watu watakaoguswa moyo na kuwakaribisha na kuwapa mahitaji yao,kama chakula, fedha, nguo n.k kwasababu sio wote watakuwa na moyo mgumu wa kutoa. Lakini Mwisho wa maagizo hayo anawaambia.. “mtu yeyote asiyewakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung’uteni mavumbi ya miguuni mwenu”. Halafu anamalizia kwa kusema… “Amin, NAWAAMBIA, ITAKUWA RAHISI NCHI YA SODOMA NA GOMORA KUSTAHIMILI ADHABU YA SIKU YA HUKUMU, KULIKO MJI ULE”.
Maana yake ni kwamba kitendo cha wale watu kutowakaribisha (maana yake wasipowafadhili) wala kusikia maneno yao, watapata adhabu kubwa kuliko watu wa Sodoma.
Sasa hebu twende pamoja tena katika Mathayo 25
Mathayo 25:31 “ Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;
32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;
33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto….
41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, ONDOKENI KWANGU, MLIOLAANIWA, MWENDE KATIKA MOTO WA MILELE, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
42 KWA MAANA NALIKUWA NA NJAA, MSINIPE CHAKULA; NALIKUWA NA KIU, MSININYWESHE;
43 NALIKUWA MGENI, MSINIKARIBISHE; NALIKUWA UCHI, MSINIVIKE; NALIKUWA MGONJWA, NA KIFUNGONI, MSIJE KUNITAZAMA.
44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?
45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.
46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele”.
Umeona hapo?. Bwana alipowatuma wakina Petro bila kubeba chakula cha safari, lengo lake ni wale wapate riziki kupitia wale watakaowahubiria, ndio maana akamalizia pale juu kwa kusema “MAANA MTENDA KAZI ASTAHILI POSHO LAKE.” Wakina Petro ni watenda kazi, (yaani wanafanya kazi ya kuhubiri), hivyo wanastahili posho zao, yaani riziki zao huko wanakokwenda kuhubiri, ndio maana akawaambia hata wasihangaike kutoka na akiba ya chakula, wala mavazi, kwasababu watavipata huko wanakokwenda.
Lakini chaajabu ni kwamba Bwana Yesu, hajatoa sheria wala hajatoa Agizo kwa wale watakaohubiriwa kwamba ni lazima watoe!!.. Kwamba ni lazima au ni amri kuwafadhili wakina Petro na Mitume wanapohubiri,.. Angeweza kuwaambia wakina Petro kwamba wawaambie watu wanaowahubiria kwamba “Kila mkutano wanaofanya wachangie, au kila mtaa wanaofika, Bwana kasema wapewe chochote”.. Lakini Bwana aliwaambia wasiseme lolote..wao kazi yao ni kutoa bure!, wasipopewa chochote wasonge mbele, wala wasionyeshe kama ni wahitaji!, wala wasiombe ombe!… Lakini mwisho tunaona Bwana anatangaza hukumu kwa wale wote ambao hawakuwakaribisha watumishi hao wa Mungu. Kwamba atawabagua kama mbuzi!
Ni nini tunajifunza hapo?
Yapo maagizo ambayo hayajaagizwa. Unaweza leo ukakwepa kumtolea Mungu, ni kweli hajakulazimisha, wala hajakuwekea kiasi, wala hajakuagiza kwamba ni lazima umtolee, amekaa kimya kuhusu hilo eneo, lakini huna budi kufahamu na kuwa na hekima kwamba ni wajibu wako kumtolea Mungu. Kama huamini kuwa kitendo cha kutomtolea Mungu ni dhambi soma tena hiyo Mathayo 25:31-43. Jiulize ni kwanini Bwana hajawafananisha wale mbuzi na watu wanaomkufuru, au wanaomtukana, au manabii wa uongo, lakini badala yake kawafananisha na watu ambao walikuwa hawamjali kimatoleo.
Ndio siku hiyo utasema.. “Bwana hukusema watumishi wako watoe bure?”… ni kweli alisema hivyo “lakini na wewe hukupaswa kukaa tu bila kuwa na hekima”. Hata mgeni anapokuja nyumbani kwako hatakuja kama anauhitaji, atakuja kama kashiba, au kama hana kiu..Lakini pengine ana njaa, na kiu..na anaweza kuondoka hivyo hivyo, kama wewe hutatumia hekima, angalau kumletea hata glasi ya maji… sio lazima akuambie naomba chakula!..kamwe hutasikia hilo likitoka kinywani mwake kama huyo mgeni ni mstaarabu.. Na Bwana Yesu ni hivyo hivyo, yeye ni mstaarabu wa wastaarabu, na watumishi wake wa kweli ni hivyo hivyo…kamwe hatakuja kwako na kukwambia nina haja na hichi au kile. Ni wajibu wako wewe kulijua hilo. Na kama hutakuwa na hekima ya kutosha ya kuweza kupambanua mambo, basi ni rahisi kuangukia katika hukumu siku ile ya mwisho.
Hilo ni jambo ambalo leo ningependa tulitafakari, leo ndugu. Popote pale ulipo mjali Bwana, pasipo kuambiwa, yapo maagizo ambayo Bwana atatuambia moja kwa moja bila kupinda panda, lakini yapo maagizo ambayo Bwana katuachia sisi wenyewe tuyapambanue, na tuyatekeleze…
Hebu tafakari hapo kanisani kwako, ni nini umefanya tangu umefika!.. kumbuka matendo yako yanatangulia hukumuni. Lakini usipokuwa na hekima kwa kudhani kuwa hakuna haja ya kumjali Bwana kwa matoleo yako, basi siku ile atakuweka katika kundi la mbuzi. Ni heri tukalijua hili mapema, ili siku ile ya mwisho tusije tukazuiliwa.
Hegai 1:4 “Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika”
Bwana atubariki na kutusaidia.

Nini maana ya siku moja kwa Bwana ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja? (2Petro 3:8)

Yeremia 48:11 “MOABU AMESTAREHE TANGU UJANA WAKE, NAYE AMETULIA JUU YA SIRA ZAKE, WALA HAKUMIMINWA KUTOKA CHOMBO KIMOJA KUTIWA CHOMBO KINGINE, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika.
12 Basi, tazama, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo nitampelekea wamiminao, nao watammimina, nao watamwaga vyote vilivyomo vyomboni mwake, na kuzivunja chupa zake vipande vipande.
Unajua sira ni nini?
Sira ni yale makapi yanayosalia baada ya pombe kuchachushwa, ni mchanganyiko wa maganda ya mbegu na wadudu waliokuwa wanaichachusha pombe hiyo. Kwa kawaida pombe kama divai inapomalizika kuchachushwa, wanachofanya ni kuimimina kwenye vyombo vingine kwa ajili ya matumizi na kuiacha Sira chini.. kwasababu yenyewe inakuwa kama topetope au urojo urojo fulani hivi.
Lakini makapi haya huwa yanathamani kubwa sana kwa wachachushaji, kwasababu pombe inayokaa muda mrefu juu ya Sira, huwa inaubora tofauti na ile ambayo, imekaa kwa muda mfupi. Kwa jinsi itakavyokaa sana juu ya sira basi ladha ya divai ndivyo inavyokuwa nzuri sana, vilevile mwonekano wake na harufu yake inakuja Zaidi, Lakini ile ambayo imechachushwa tu na saa hiyo hiyo au baada ya kipindi kifupi ikaondolewa na kupelekwa katika vyombo vingine huwa haina uzuri saa kama ile iliyodumu muda mrefu juu ya sira.
Wanaotengeneza divai, za ghali kama vile zinazoitwa champagne, huwa zinaachwa muda mrefu juu ya sira, hata miezi 4 na Zaidi, hivyo ubora wake unakuwa wa juu Zaidi kulinganisha na divai nyingine za kawaida. (Soma pia Isaya 25:6)
Sasa tukirudi katika mstari huo tuliousoma hapo juu, biblia inasema..
“Moabu amestarehe tangu ujana wake, naye ametulia juu ya sira zake, wala hakumiminwa kutoka chombo kimoja kutiwa chombo kingine…”
Moabu katika historia ni taifa ambalo, tangu lilipozaliwa halikupitia migogoro kabisa, au kama lilipitia basi ni midogo midogo sana ambayo haikulisababishia taifa hilo madhara makubwa, ukilinganisha na mataifa mengine, Moabu haikuwa na majanga, wala vita, wala njaa wala shida shida, lakini pamoja na kwamba ilijaliwa hivyo haikujua ni kwanini Mungu aliwaacha wawe vile, kinyume chake yenyewe iliendelea tu kufanya maovu na matendo yasiyompendeza Mungu kwa muda mrefu.
Na ndio maana hapo inafananishwa na divai ambayo imekaa juu ya sira yake kwa muda mrefu, divai ambayo haikuharakishwa kumiminwa miminwa kwenye vyombo vingine, ikiwa na maana kuwa haikuchukuliwa utumwani, haikupitishwa katika matatizo, iliendelea kubakia katika ustawi wake kwa muda mrefu..
Ikawa inadhani kuwa kamwe haitakaa ikumbane na mabaya, yenyewe imebarikiwa tu, ikafikiria hao wengine wanaoadhibiwa kama Israeli wana laaana na mikosi kutoka kwa Mungu.
Lakini tukisoma mistari inayofuata inasema hivi..
Moabu amestarehe tangu ujana wake, naye ametulia juu ya sira zake, wala hakumiminwa kutoka chombo kimoja kutiwa chombo kingine, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika.
12 Basi, tazama, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo nitampelekea wamiminao, nao watammimina, nao watamwaga vyote vilivyomo vyomboni mwake, na kuzivunja chupa zake vipande vipande.
Umeona, kuna wakati ulifika, wakaldayo walikuja na kuwaangamiza na kuwachukua utumwani na kuwaharibu kabisa, na uzuri wao ukapotea ghafla, jambo ambalo hawakutazamia kama lingekaa liwapate, kama wengine.
Ndugu yangu, leo hii unatenda dhambi lakini huoni chochote, unazini Bwana hakuadhibu kwa lolote, unafanya mambo yako machafu kwa muda mrefu sasa, unakwenda kwa waganga, hauumwi, kinyume chake unazidi kustawi, unaendelea kufanya anasa na ulevu, unasema mbona hakuna dhara lolote linalonipata, hujiulizi ni kwa nini? Unachodhani ni kuwa wewe ni spesheli sana kwake sio? embu soma mstari huu tena ujifunze jambo..
Sefania 1:12 “Kisha itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; nami NITAWAADHIBU WATU WALIOGANDA JUU YA SIRA ZAO; wasemao katika mioyo yao, Bwana hatatenda mema, wala hatatenda mabaya”.
Umeona, Mungu utafika wakati atakuchunguza kwa taa, wewe ambaye umetulia juu ya Sira yako, huangaishwi angaishwi, unafanikiwa angali upo katika dhambi, unayesema, Mungu hawezi fanya jambo lolote hata nikiwa mwovu kiasi gani.
Jiangalie, hukumu ipo, utakufa ghafla, na moja kwa moja utajikuta upo jehanamu kama yule Tajiri wa Lazaro, ambaye hapa duniani alikuwa akijitumaisha katika Maisha yake ya anasa tu, hajali kama kuna kuzimu, au hukumu, hajali kama kuna kiama chake mbeleni.. Na wewe ndipo utakapojikuta huko kama hutatubu, ukilia na kuomboleza, ukisema laiti ningelijua, laiti ningelijua..
Wakati huo utakuwa umeshachelewa ndugu. Leo hii ukiona Mungu hafanyi chochote juu ya dhambi zako, sio kwamba anayafurahia hayo Maisha unayoishi, anakutazama tu, yamkini siku moja utatubu, lakini ikifikia wakati haoni badiliko lolote la wewe kumgeukia yeye, atakujia na kukuondoa duniani kama alivyofanya kwa Wamoabu.
Biblia inasema saa ya wokovu ni sasa, na wakati uliokubali ni leo, usingojee siku Fulani ukasema hiyo ndio itakuwa siku yako ya wokovu, haitakaa ije kamwe. Mpe Yesu Kristo Maisha yako leo ayaokoe, Tubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha, kisha tafuta mahali ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO ili upate ondoleo la dhambi zako, na Kisha mwenyewe Mungu atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu ili akae na wewe siku zote za Maisha yako.
Hata kama ikitokea Maisha yako yamefikia ukingo leo, basi unaouhakika wa kuurithi uzima wa milele.
Ikiwa utapenda kuokoka, na unahitaji msaada huo basi unaweza, kutafuta kanisa la kiroho lililokaribu na wewe, wakusaidie au ukawasiliana na sisi kwa namba zetu hizi +255693036618 /+255789001312 kwa ajili ya Sala ya Toba na maagizo mengine.
Bwana akubariki sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho
Mada Nyinginezo:
Shalom, karibu tujifunze Neno la Mungu. Biblia inatuambia..
“Ondoa takataka katika fedha, Na chombo kitatokea kwa mtakasaji; (Mithali 25:4)
Tunapoiona dhahabu au madini mengine yote, yanang’aa sana, mpaka kufikia kiwango cha kuuzwa kwa thamani kubwa sana, hatupaswi kudhani, huko chini yanapochimbwa yanatoka kama yalivyo. Hapana, mengi ya hayo yanakuwa yamechanganyikana na mawe mengine au uchafu mwingi tofauti tofauti, kiasi kwamba unaweza kukutana na mwamba mkubwa sana, na ndani yake kukawa na kiwango kidogo sana cha dhahabu au fedha.
Hivyo, ili kuitapata dhahabu yenyewe safi, inawagharimu wafuaji wafanye kazi ya ziada, na kazi yenyewe ndio hiyo ya kutenganisha madini hayo kutoka katika hizo takataka nyingine, Zipo takataka ambazo unaweza kuziondoka kwa kuzichuja tu au kupepeta, lakini zipo ambazo itakuhijitaji utumie moto ili kuzitenganisha, kwasababu inakuwa zimechanganyikana na dini lenyewe hadi ndani.
Hivyo wanachokifanya ni kwenda kuyachoma mawe hayo, kwa joto kali sana mpaka yayeyuke, na yakishayeyuka na kuwa kama uji uji, ndipo sasa uchafu unajitenga na dhahabu yenyewe. Kwa kupanda juu, hapo ndipo yule mfuaji anapoondoa uchafu ule, na atarudia tena hizo hizo hatua kwa jinsi atakavyoweza, na kwa jinsi atakavyozidi kuondoa takatakata hizo zote hata zile ndogo, ndivyo, mnga’o wa fedha hiyo unavyozidi kuja.. hatimaye, inatokea ikiwa nzuri sana yenye kunapendeza, tayari kwa matumizi yenye thamani.
Mithali 25:4 “Ondoa takataka katika fedha, Na chombo kitatokea kwa mtakasaji;”.
Hivyo na sisi pia kama wakristo, tunapookoka tunakuwa hatuna tofauti na fedha/dhahabu iliyochimbwa katikati ya miamba, tumetolewa huko tukiwa na mambo mengi ya kidunia ambayo yameshikamana sana na sisi,
Sasa tunapookoka, kanuni ni ile ile inatugharimu tuingizwe katika moto, ili tuwe safi kabisa, Na moto huo anayetuingiza Mungu, na pia tunajiingiza sisi wenyewe.
Hapo ndipo utaona pale tunapokuwa wakristo tu, Mungu anaruhusu tupitishwe katika majaribu mbali mbali ya moto ili tuwekwe safi. Ndio maana biblia inasema;
1Petro 1:6 “Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali;
7 ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo”.
Yakobo 1:2 “Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;
3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi”.
Unaona, ni jambo la kawaida Mungu, kuwapitisha watoto wake katika majaribu ya namna mbalimbali, lengo sio kuwaangamiza, bali kuwaimarisha Zaidi.
Pia Neno la Mungu linatuambia na sisi wenyewe, tunapaswa tuondoe takataka katikati ya kila kitu tunachokifanya katika maisha yetu ya ukristo ili Mungu aweze kutufanya kama vile anavyotaka, iwe ni katika huduma zetu, au shughuli zetu n.k..
Tukitaka tumwone Mungu katikati ya Maisha yetu, tuondoe mambo ambayo hayampendezi, tuondoke uzinzi, tuondoe usengenyaji, tuondoke kuchat chati kusikokuwa na maana mitandaoni, na kutazama muvi muvi zisizotujenga, tuondoe mizaha, tuondoe unafki, tuondoe rushwa, tuondoe uvaaji mbovu, n.k. Mambo kama haya tukiyazingatia basi Mungu, atatuletea ule mng’ao tunaostahili kuwa nao sisi kama wakristo, na tutakuwa wa thamani nyingi mbele zake na mbele za ulimwengu.
2Wakorintho 7:1 “Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu”.
Kumbuka mambo kama haya kuyaondoa, haihitaji kuwa mlegevu legevu, inahitaji kujiingiza wewe mwenyewe katika moto wako, (kujinyima, kukataa na kuepuka) kila kitu ambacho unaona hakimpendezi Mungu. Hata kama nafsi yako inakitamani vipi, unakipinga. Unakubali kuonekana wa ajabu, lakini moyo wako uwe salama, na faida yake utaiona baadaye.
Vilevile hata katika Maisha yetu ya huduma, ili Kristo atende kazi vema, na ukuu wake uthibitike tunapaswa tuondoe mambo yote maovu katikati ya kanisa, tusiwe radhi na wazinzi na wapotoshaji katikati yetu, na Mungu atajifunua miongoni mwetu.
Mithali 25:4 “Ondoa takataka katika fedha, Na chombo kitatokea kwa mtakasaji;
5 Mwondoe asiye haki mbele ya mfalme, Na kiti chake cha enzi kitathibitika katika haki”.
Bwana atusaidie sote, Na atubariki.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho
Mada Nyinginezo:
Jibu: Hakuna mstari wowote katika biblia takatifu unaosema kwamba dunia siku moja itakunjwa kama karatasi na kutupwa motoni. Mstari ambao unawachanganya wengi ni ule wa Isaya 34:4 unaosema..
Isaya 34:4 “Na jeshi lote la mbinguni litafumuliwa, NA MBINGU ZITAKUNJWA KAMA KARATASI, na jeshi lao lote litanyauka kama vile jani la mzabibu linyaukavyo na kupukutika, na kama jani la mtini linyaukavyo na kupukutika.”
Ukiisoma hiyo Isaya 34, utaona ni unabii wa Siku ya mwisho. Na katika huo mstari wa 4, unabii unasema kuwa siku hiyo “mbingu zitakunjwa kama karatasi”. Hapo anasema “mbingu” na si “nchi” au “ardhi” au “dunia” bali mbingu!!. Hizo ndizo zitakazokunjwa kama karatasi… Na mbingu inayozungumziwa hapo sio ile Malaika watakatifu waliyopo, La!.. bali ni hii tunayoiona yenye nyota, mwezi na jua, na sayari.
Na hazitakunjwa kama karatasi na kisha kutupwa motoni!.. La! Maandiko hayajasema hivyo, yameishia tu hapo kusema kuwa zitakunjwa kama karatasi. Na kukunjwa kunakozungumziwa hapo sio kukunjwa kwa kusokotwa sokotwa kama uchafu, hapana! Bali kukunjwa kama vile mtu anayekunja ngozi.
Sasa ili tuelewe vizuri zitakunjwaje kunjwaje siku hiyo kama karatasi, twende pamoja kwenye kitabu cha Ufunuo.
Ufunuo 6: 12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,
13 NA NYOTA ZIKAANGUKA JUU YA NCHI KAMA VILE MTINI UPUKUTISHAVYO MAPOOZA YAKE, UTIKISWAPO NA UPEPO MWINGI.
14 MBINGU ZIKAONDOLEWA KAMA UKURASA ULIVYOKUNJWA, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.
15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.
17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?”
Umeona hapo?.. Katika siku ile ya mwisho, muhuri wa 7 utakapofunguliwa, wakati Yesu atakaporudi na watakatifu wake aliowanyakua. Siku hiyo, nyota zitaanguka, (maana yake zitaondolewa). Ghafla tu, watu watashangaa jua limezama wakati wa adhuhuri, na mwezi umekuwa mwekundu kama damu.. na juu nyota zinaanza kujikusanya pamoja na kuanguka..kama vile ukurasa (Yaani karatasi) linavyofunguliwa..
Tunaweza kulisoma tena jambo hilo vizuri katika kitabu cha Mathayo..
Mathayo 24:27 “Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
28 Kwa kuwa po pote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.
29 Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, NA NYOTA ZITAANGUKA MBINGUNI, NA NGUVU ZA MBINGUNI ZITATIKISIKA;
30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi”
Unaweza kusoma pia unabii huo katika Isaya 13:9-11.
Kwahiyo dunia haitakunjwa kunjwa na kutupwa motoni, bali ni mbingu, na mbingu hizo hazitakunjwa na kutupwa motoni, bali zitaanguka (maana yake zitaondolewa!!). Na tendo hilo litatokea baada ya unyakuo wa kanisa kupita na dhiki kuu kupita, wakati ambapo Kristo atarudi kwa mara nyingine pamoja na watakatifu wake wale walionyakuliwa, sasa wale ambao watakuwa wamesalia duniani, waliopokea chapa, na kunusurika katika mapigo ya vitasa saba, watalishuhudia hilo tendo la mbingu kuondolewa kama ukurasa, siku hiyo jua litazima ghafla na mwezi utakuwa kama damu, na wataona nyota zinashuka kama vile vimondo vinavyoonekana usiku… Na kutokana na hilo tendo, itasababisha dunia iwe katika giza nene sana, kwasababu hakuna jua, mwezi unaoangaza wala nyota..
Na wakiwa katikati ya hilo giza nene watamshuhudia Kristo akitokea mawinguni kwa utukufu mwingi kama umeme, pamoja na wale watakatifu wake aliowanyakua, na chini ya ardhi visiwa vitahama, na kutatokea na tetemeko ambalo halijawahi kutokea mfano wake, watu wote watakufa, isipokuwa kundi dogo, ambalo lilihifadhiwa kuingia katika ule utawala wa miaka elfu, Kristo atakapotawala na bibi arusi wake hapa duniani.
Bwana atusaidie tusiukose unyakuo, ili siku moja tutawale naye tukiwa kama makuhani na wafalme. Ni heri tukose kila kitu katika huu ulimwengu lakini tusiikose mbingu.