Mungu alipomtuma Musa, kwa Farao, tunasoma habari alimpa maagizo ya nini cha kufanya atakapofika kwa Farao, na mojawapo ya maagizo hayo alimwambia akifika aitupe chini ile fimbo aliyokuwa nayo mkononi mbele ya Farao nayo itageuka na kuwa nyoka, na kisha aitwae tena mkononi mwake nayo itageuka kuwa fimbo kama mwanzo. Na pia tunaona Bwana alimfanyisha mazoezi kabisa akiwa kule kule mlimani kabla hata ya kwenda Misri kwa Farao, maana Mungu alimwambia palepale aitupe chini ile fimbo na alipoitupa ikageuka kuwa nyoka na Musa alipoona fimbo imegeuka kuwa nyoka alitaka kukimbia..
Bwana akamwambia akamshike Yule nyoka Mkia, kwa kusitasita na kutetemeka alikwenda na kumshika, na mara saa hiyo hiyo Yule nyoka akageuka na kuwa fimbo tena..Zoezi hilo lilimsadia kupata ujasiri, pindi atakapofika kwa Farao na kuitupa chini ile fimbo itakapogeuka na kuwa nyoka, asiigope kuishika na kuitwaa tena iwe fimbo.
Sasa swali la kujiuliza ni kwanini Mungu aitumie ile fimbo kuigeuza kuwa nyoka na wala si kitu kingine, kwanini hakutaka igeuke na kuwa chuma, au igeuke na kuwa sungura, au kiumbe chochote kile tofauti na NYOKA!.
Ili tuelewe hilo vizuri, turudi kidogo kujifunza histori ya Taifa la Misri, Misri ni Taifa lililopo kwasasa katika Bara la Afrika, kaskazini mashariki mwa Afrika, na asili ya Taifa hilo ilikuwa ni wana wa HAMU, aliyekuwa mwana wa Nuhu, Yule aliyeuona uchi wa Baba yake na asiusitiri, na hivyo akalaaniwa. Kwahivyo wana wa Hamu wakasafiri pande za kusini wakajenga miji huko, na Taifa mojawapo la wana hao wa Hamu ndio Misri. Mambo mengi yaliendelea hapo katikati hatuna muda wa kutosha wa kuyazungumzia yote lakini historia inasema ndio Taifa lililokuja kuwa na nguvu kuliko mengine yote kwa wakati huo.
Utamaduni wa Taifa hilo haikuwa kumwabudu Mungu wa Israeli, kwasababu walikuwa hawamjui Mungu wa Israeli bado, hivyo walikuwa wana miungu yao mingine mingi mingi tu!, waliabudu jua, mwezi na mambo mengine mengi…lakini moja ya miungu waliyokuwa wanaiabudu na kuipa heshima ya juu zaidi, ilikuwa ni NYOKA. Na aina ya nyoka hao waliokuwa wanawaabudu anajulikana kama COBRA. Walikuwa wanaamini kuwa nyoka aina ya Cobra ni mungu mkuu ambaye ana uwezo mkubwa sana katika kulilinda taifa lote la Misri dhidi ya Maadui zao, walitumia sanamu yake kama ishara kila mahali katika nyumba zao za kawaida na katika makasri yao makubwa ya kifalme. Hata katika kofia za kifalme za wafalme kulikuwa ni kijisanamu kidogo cha cobra kwenye kipaji cha uso kinachoangalia mbele, hicho kilikuwa kinavaliwa daima waliamini kuwa kama vile nyoka aina ya Cobra anavyotema mate ya sumu dhidi ya maadui zake usoni, vivyo hivyo cobra wanayemwabudu huyo huyo atawatemea moto maadui wa Farao wote wanaokuja mbele yao.
Kwahiyo ilikuwa ni imani iliyoheshimika sana, na ilikuwa inawapa matunda, kwasababu nyuma yake alikuwa ni shetani, na kama unavyojua shetani naye anawapa anaowapenda kama anavyotaka. Kwahiyo huyo mungu wao nyoka alikuwa anawapa ushindi mara nyingi ndio maana, Taifa hilo la Misri likainuka kuwa na nguvu kila mahali.
Wengi tunafikiri kuwa miungu hiyo ya Misri haikuwa na nguvu yoyote! Usidanganyike! Ilikuwa ina nguvu kama kawaida, na wamisri walikuwa wanaona inavyowasaidia, na endapo wakiwa hawaiabudu inavyopaswa ilikuwa inawaletea madhara, kwahiyo sio kwamba wamisri walikuwa wanaabudu kitu kisicho dhahiri!.. Ukitaka kujua walikuwa wanaabudu kitu kilicho dhahiri au la! Tazama yale mapigo, Musa aligeuza fimbo kuwa nyoka nao pia wakafanya hivyo hivyo, na baadhi ya mapigo pia waliweza kuiga, sasa kama hiyo miungu yao haikuwa dhahiri kwanini iliweza kufanya ile miujiza?? Jiulize hilo, na kama hiyo miungu yao ilikuwa na nguvu ya mpaka kuweza kubadilisha fimbo kuwa nyoka unadhani ingeshindwa vipi kutemea moto kwa maadui zao wakiwa vitani??..
Hata Israeli wakati Fulani walipokengeuka na kuanza kuabudu mabaali, sio kwamba walikuwa wanaabudu kitu kisichokuwepo, hapana! Walikuwa wanaabudu kitu kilicho dhahiri kabisa (ambacho ni shetani mwenyewe pasipo wao kujijua)..Na hata wakati ule walipojaribu kushusha moto mbele ya Eliya juu ya ile dhabihu usidhani ni kwamba walikuwa wanafanya kitu cha kujaribisha au kubahatisha, hapana! hiyo miungu yao kushusha moto sio jambo kubwa, Na ilishawahi kushusha hapo kabla, ndio maana unaona walipata ujasiri mbele ya Eliya kulileta lile shindano, lakini kilichowashtusha ni kama tu hicho kilichomshtusha Farao kuona nyoka wake wanamezwa mbele ya macho yake, na makuhani wa mabaali vivyo hivyo walishtuka kuona mbona moto haushuki kama siku zote!..
Kwahiyo Musa wakati anamwendea Farao, Mungu alitumia ishara ya nyoka, ili kuwaonyesha wa Misri kuwa mungu wanayemwabudu sio wa kweli, ingawa anawatendea miujiza , na kwamba nguvu zake zina mipaka, yupo mwenye nguvu kuliko mungu wao cobra wanayemwabudu, ndio maana alitumia ishara ya nyoka awali kabisa ili wamisri wamwelewe vizuri, kwasababu laiti angetumia ishara ya kugeuza fimbo kuwa sungura wamisri wasingeiamini kwasababu wao wanajua miungu ni mfano wa viumbe wakali kama nyoka, na ndio maana unaona nyoka wa Musa aliwameza wale nyoka wa Farao.
Kwa ufupi ishara ile, ilitosha kabisa kumwaminisha Farao kuwa Mungu wa Israeli ni Mungu mkuu kuliko mungu wao. Hata wamisri wote baada ya kuiona ile ishara waliamini, kulikuwa hakuna haja ya kuendelea na ishara nyingine mbele…kwasababu mbele ya macho yao wameshuhudia mungu wao cobra wanayemweshimu na anayewasaidia siku zote katika vita, amemezwa na Mungu mwingine, ni ishara madhubuti kuwa endapo wakiendelea kushindana na huyo Mungu watamezwa vile vile, kama mungu wao alivyomezwa…Lakini kwasababu Mungu alitaka kuonyesha utukufu wake wote, ndiyo akaufanya moyo wa Farao usiamini, uwe mgumu. Lakini katika hali ya kawaida, Farao tayari alishaamini.
Ndugu kama uliwahi kuomba rozari na ikakupa majibu uliyoyaomba, uliiomba fedha ikakupa, uliiomba rozari ushindi ikakupa, na ukaiamini kiasi kwamba unatembea nayo kila siku shingoni, kwasababu haikuangushi……napenda nikwambie ndugu yangu mpendwa huyo sio Mungu ni shetani nyuma ya hiyo rozari, haijalishi hiyo rozari imekufanikisha kiasi gani, nataka nikuambie yupo Mungu aliye mkuu kuliko hiyo rozari atakayeimeza hiyo rozari unayoivaa na kuiomba kila siku, Hata Farao alitumia nyoka kuamini hakuna mungu zaidi ya huyo, na nguvu za Cobra zilimfanikisha kuliko mataifa yote duniani, lakini alipokuja Mungu wa miungu na kumkataa huyo. Misri iligeuka kuwa kama jalala la dunia.
Kama umekuwa ikiisujudia sanamu kanisani kwako pasipo kujua kuwa unamwabudu shetani na imekujibu maombi na kukupa kila unachokihitaji… Mungu hakuweza kukuhukumu kwasababu ulikuwa huujui ukweli, lakini leo umeujua ukweli, umgeukie yeye mwenye nguvu kuliko hiyo sanamu, itupe leo ivunje vunje leo, acha kuiabudu kwasababu yupo Mungu juu mwenye nguvu kuliko hiyo sanamu ya BIKIRA MARIA unayoiabudu na anataka kukubariki kuliko hata hapo ulipo. Anataka kukupa mafanikio kuliko hata hayo uliyonayo. Ambayo shetani amekupiga upofu kukudanganya kwamba ni mafanikio, kumbe ni mafanikio feki,…hiyo sanamu haiwezi kukupa raha nafsini mwako, hiyo sanamu haiwezi kukusamehe dhambi, hiyo sanamu haiwezi kukufanya uwe mtakatifu, hiyo sanamu haikupi kibali cha kuingia ufalme wa mbinguni, hiyo sanamu haiwezi kuondoa ulevi ulionao! Haiondoi uasherati ndani yako!! Hiyo sanamu sio Mungu wa kweli! Kwasababu ndivyo ilivyokuwa hata kwa Farao, wale nyoka aliokuwa anawaabudu walimpa utajiri lakini walikuwa hawamhukumu kuhusu tabia yake mbaya ya kuonea watu wasiokuwa na hatia! Mungu gani huyo!
Utasema huyo Mungu mbona watu wake ni maskini, nataka nikuambie hata Farao aliwaona wana wa Israeli ni maskini na kuwatesa kule kwenye mashimo ya matope! Lakini Misri yote ilishtuka kuona kuwa wale wanaowadharau kumbe ndio wanaomwabudu Mungu mwenye nguvu kuliko Mungu wao…..siku ile walipoona Misri yote imeteketea,…na wewe usiangalie hali ya watu wanaomwabudu Mungu wa Kweli ipoje, wapo vile kwasababu fulani tu, lakini hawatakuwa vile siku zote, ipo siku watang’aa kama jua, isikilize hii sauti ya Mungu inayozungumza nawe sasa…Mungu wa kweli sio nyoka, wala ekaristi, wala sanamu ya kiumbe chochote kile, wala sanamu ya mwanadamu yoyote Yule, wala Mungu wa kweli haabudiwi kwa kupitia sanamu ya Bikira Maria, wala chochote kile, Mungu wa kweli anaabudiwa juu mbinguni KATIKA ROHO NA KWELI.
Pengine umekwenda kwa waganga wa kienyeji na kwa kupitia wao umepata mafanikio, na wamekwambia wakristo hawamwabudu Mungu wa kweli, nataka nikuambia ndugu yangu, wamekudanganya na wamekupoteza..Wale nyoka walimpa Farao mafanikio makubwa sana kuliko uliyonayo wewe, lakini hao hao hawakuweza kumwokoa na hukumu ya Mungu iliposhuka juu ya Misri.
Na wewe siku hizi usiweke moyo wako mgumu, achana na hao waganga, kwasababu utaelekea kwenye ziwa la Moto, tupa leo hirizi zote walizokupa, choma moto, mvue mwanao hirizi zote ulizomvalisha kiunoni na shingoni na mikononi, tupa na wewe kila kitendea kazi ulichopewa na mganga wa kienyeji eti upate amani, fedha au utajiri, au vikulinde…hivyo vitendea kazi vitakulinda dhidi ya wachawi wenzako tu tena wenye nguvu kidogo kuliko mganga wako lakini wakija wachawi wengine wenye nguvu kuliko wewe na mganga wako watakuua na kukushinda tu!, na zaidi ya yote ni heri ingekuwa hivyo tu!! Ghadhabu ya Mungu bado inakungojea endapo ukikataa kutubu ndiyo itakayokuharibu kabisa kama ilivyomuharibu Farao, alipoteza fahari yake yote na kufiwa na mwanawe wa pekee.
Ukiyafahamu hayo ni wakati wa kugeuka, Bwana anakupenda na kukuhitaji, kama hujampa Bwana maisha yako, mlango wa Neema bado upo, ila hautakuwepo siku zote, biblia inasema utafika wakati mlango utafungwa, na watu watalia na kuomboleza wakiomba Bwana awafungulie, na Bwana hatawafungulia, Hivyo tubu leo kwa kumaanisha kuacha kabisa maisha ya dhambi uliyokuwa unayaishi huko nyuma, maisha ya usengenyaji, maisha ya rushwa, maisha ya uasherati, maisha ya utazamaji pornography, maisha ya usagaji, maisha ya ulawiti, maisha ya ushirikina, na uhudhuriaji wa waganga wa kienyeji,maisha ya aubuduji sanamu, maisha ya ulevi na sigara.n.k n.K
Na baada ya kufanya hivyo kama hujabatizwa nenda katafute ubatizo sahihi mahali popote pale kulingana na maandiko, na ubatizo sahihi ni wa maji mengi na kwa JINA LA YESU kulingana na Matendo 2:38, na baada ya hapo Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu atakayekusaidia kushinda dhambi, maana kwa nguvu zetu hatuwezi kamwe kushinda dhambi, na Roho huyo huyo atakusaidia kuielewa biblia na kukuongoza katika kweli yote usipotee kwa kuchukuliwa na upepo wa shetani. Na ukizingatia kufanya hivyo utakuwa umezaliwa mara ya pili, na kuwa na uhakika wa kuiona mbingu.
Bwana akubariki sana.
Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine, na utakuwa umeshiriki katika kuisambaza injili ya Kristo.
Maran atha!
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
BWANA YESU ALIMAANISHA NINI ALIPOSEMA TUWE NA BUSARA KAMA NYOKA?
Yapo mambo umeshawahi kujiuliza ni kwanini, hayaishi kutokea kila kukicha katikati ya kanisa la Mungu hususani kwa watu wanaosema wao ni watumishi wa Mungu. Utaona leo kunatokea vituko hivi kesho vile, leo mmoja ananaswa kwenye jambo hili baya, kesho lile, sasa mambo kama hayo ukiyaona usianze kuunyooshea ukristo wote kidole au watumishi wote vidole, badala yake uogope kwasababu mlengwa ni wewe na usipojua sababu ya hayo mambo kuzidi kukithiri sana hususani katika kipindi hichi cha mwisho , utajikuta umetumbukia katika shimo ambalo hutajua ni lini umeingia humo..
Embu fuatilia mazungumzo haya dada huyu aliyonitumia kisha tutaendelea..
Kwani kuna jambo kwa huyu mtumishi ambaye ndo aliyekua akinifundisha mambo ya kumjua Mungu kwa aliyoyafanya nilikata tamaa nikawa naenda tu kanisani lakini sina imani hata na wachungaji tena. nahisi nao watakua hivyo hivyo japokua natamani sana nikae kwenye mstari lakini nikikumbuka matukio mabaya nasikilizia tu neno ibadani lakini hayakai kabisa, nahitaji msaada zaidi kimaombi peke yangu siwezi mtumishi.
Kwanza huyu mtumishi ni mchafu kwenye mitandao pia ni mzinzi sana yani mno sasa kwa mimi ambaye ni mchanga kiroho nashindwa kuelewa ukimuonya ndio hayo anakujibu usimnyoshee kidole mtumishi wa Mungu utapata ukoma kamuulize Miriamu kilimpata nini.
nilimuuliza inakuaje unajua kabisa uzinzi ni dhambi au matusi ni dhambi alafu unafanya kwa makusudi?
akajibu hakuna mchungaji ambaye hajawai kuanguka na bado wanaendelea kuanguka, ndo nikamwambia kwahiyo wewe unawaiga hao? Mungu sio mjomba wako akasema Mungu ni wa rehema kila wakati, mtu anafanya dhambi anatubu anaendelea mbele nikasema naenda kumwambia mchungaji wako na askofu wako akasema ole wangu nikamharibie kule maana wana mwamini sana na hawajui mwenendo wake upoje na yupo kanisa moja la TAG mahali fulani hivi kule (……..).
natamani sana wachungaji wake wamjue tabia zake asiendelee kuchafua kanisa ndio sielewi nifanyeje.
Yananipa shida moyoni.” Naomba msaada.
***mwisho***
Watu wengi wanashindwa kuendelea mbele na Mungu wao kwa kuwatazama watu wa namna hii, Na hicho ndicho shetani anachotafuta kwako hata wewe usomaye ujumbe huu. ni kweli wanakatisha tamaa, na sio tu kukatisha tamaa bali pia wanawakosesha watu wengi waliowachanga kiimani jambo ambalo Bwana YESU anasema “Ingewafaa zaidi kwa watu wa namna hiyo jiwe la kusagiwa lifungiwe shingoni mwao, wakatupwe baharini kuliko kuwakosesha wadogo hao”.. wadogo wanaozungumziwa hapo ni watu wadogo katika imani (wachanga)/ wanyenyekevu…
Lakini je suluhisho ni nini?..Ni kuwanyoshea watumishi wote wahubirio injili vidole?..Hapana tukifanya hivyo tutajikuta tunapoteza hata vile vizuri Mungu alivyokusudia tuvipate katika Mwili wake [ambalo ndio kanisa lake]. Lakini uzuri ni kwamba Jambo kama hilo Bwana alishakwisha kuliona na kulitolea ufafanuzi uliobora zaidi embu tusome hapa kwa pamoja:
Mathayo 13:24 “Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake;
25 lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.
26 Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu.
27 Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu?
28 Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye?
29 Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing’oa ngano pamoja nayo.
30 Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.”
Tukizidi kusoma tunaona Bwana akitoa tafsiri yake kama ifuatavyo:
“Azipandaye zile mbegu njema ni Mwana wa Adamu;
38 lile konde ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu;
39 yule adui aliyeyapanda ni Ibilisi; mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika.
40 Basi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia.
41 Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi,
42 na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Ndugu fahamu tu jambo moja Mungu ameruhusu kwa makusudi kabisa, watu wote waovu na wema wote wamee kwa wakati mmoja katika kanisa lake kwa kila kizazi, haijalishi ni wazinzi, au walevi, au washirikina wote, au waabudu sanamu, n.k. wote wameruhusiwa wawepo katikati ya watakatifu, wote waabudu pamoja kana kwamba wote wamekubaliwa na Mungu, karuhusu wote wapokee vipawa vya roho, wote watoe unabii, wote wahubiri, wote wafundishe, wote waponye magonjwa, wote watoe mapepo,. Na wala kusiwe na chochote cha kuwadhuru..Hiyo ni SIRI KUU..Biblia inaiita SIRI YA KUASI. Wote Wameruhusiwa pia kusimama madhahabuni kufundisha, hivyo hilo pia lisikupe shida,..
Magugu na ngano vyote vipokee mbolea ya ardhi na mvua kutoka kwa Mungu..Hivyo si ajabu hata kuwaona wanaombea hata wafu wanafufuka lakini Mungu hawatumbui.
Kwanini Bwana hataki kuwang’oa sasa?. Tukirudi kwenye ule mfano wa magugu na ngano tunaweza kuendelea kujifunza kitu,
kwa mfano mbegu zozote wakati zikiwa changa ni ngumu sana kuzitofautisha zipi ni ngano na yapi ni magugu mpaka zitakapokomaa ndio utajua kiwepesi, kadhalika pia unaweza ukang’oa magugu yote kumbe hujui kuwa zipo mbegu nyingine za magugu zilikuwa zimefukiwa chini hazijamea vizuri, na ukajikuta umeziacha zile..Hivyo ili zote uzipate kiwepesi bila kubakisha hata moja itakupasa uwe mvumilivu kidogo ungoje kwanza kipindi fulani kipite zote zichipue, kubwa na ndogo. Ili sasa uzitoe zote kiwepesi na mara moja, kwasababu utakuwa una uwezo wa kuzitofautisha.
Na vivyo hivyo waovu na wema katika hatua za awali huwezi kuwatofautisha katika kanisa la Mungu, lakini kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda mwisho wao utawaweka wazi wote..Ndipo hapo watakapokuja kukusanywa wote na kutupwa katika lile ziwa la moto. Siku ile ndio lile kundi la Bwana! Bwana! Hatukutoa unabii kwa jina lako?, hatukufufua wafu? Hatukufanya miujiza mikubwa n.k??..Litakapomfuata Bwana. Lakini Bwana atawakana dhahiri..na kuwaambia siwajui nyinyi tokeni kwangu nyinyi mtendao maovu.
Watu wa namna hiyo ni mahususi kabisa wamepandwa na shetani kuliharibu shamba la Mungu. Ni ule UZAO WA NYOKA wenyewe. Na wanajua kabisa mtu yeyote aliye muhubiri atapata hukumu iliyokubwa zaidi kuliko wengine endapo atayahalifu mapenzi ya Mungu lakini wao hata hawaogopi kufanya, wanaendelea tu!..Huo ni uzao wa nyoka. Wanageuza kazi ya Mungu kuwa biashara, huku hofu yoyote ndani yao kuwalipisha watu pesa ili wapate huduma ya kiroho. Ni washirika kanisani lakini bado wanakwenda kwa waganga wa kienyeji, na wengine ni wachawi.. Wanafanya mambo ya ajabu kwa siri huwezi kuwagundua, lakini siku ile watajulikana.
Wanafahamu kabisa hakuna mlevi yoyote atakaye urithi ufalme wa mbinguni lakini wanakunywa pombe, na wakati huo huo bado utawakuta katika vikundi vya maombi, utawakuta wanahubiri, utawakuta wana imba kwaya, utawakuta wanahudumu kanisani, utakuwa ni manabii, ni waalimu na ni wachungaji, lakini bado matusi wanazidi kutukana.. Wanafanya jina la Mungu linatukanwa, si ajabu kwasababu ndio utumishi shetani aliowaitia huo.
Ni UZAO WA NYOKA..kama Bwana alivyosema.. “Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum? Mathayo 23.33”……Ni Wana wa shetani waliopandwa mahususi na ibilisi kuliharibu shamba la Mungu.
Hivyo wewe unayesoma, usiache unyofu wako na usafi wako uliokuwa umeuanza kwa kuutazama tu uzao wa nyoka katika kanisa la Mungu na kutetereka . Usitishwe na wao kwasababu uzao huo haukuanzia siku za mitume tu hapana, bali chimbuko lake lilitokea tangu Edeni, pale tu Hawa alipokubali kudanganywa na nyoka na kula tunda, kisha baadaye akaenda kula na mume wake. na ndio maana ndani ya tumbo la Hawa kulionekana watoto wawili Kaini na Habili…Mmoja uzao wa Nyoka na mwingine Uzao wa Adamu, tunafahamu habari ilivyokuwa jinsi Kaini alivyokuwa mwovu kwa tabia zake, na ndivyo ilivyo katika kanisa la Kristo
Mtume Paulo aliandika haya kwa uweza wa Roho..
2Wakorintho 11: 2 “Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.
3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo”.
Unaona, Sisi tuliposwa kwa Kristo [mfano dhahiri wa Adamu ]kama bikira safi lakini lile JOKA ibilisi akapanda mbegu zake chafu katika kanisa la Kristo ambalo linafananishwa na Hawa,. Na hivyo mpaka sasa kumetokea watoto wawili KAINI na HABILI..kwenye kanisa…Kaini ndio hawa wakristo-wa-uwongo.
Lakini mtume Paulo anatushauri tusiuache unyofu na usafi wa Kristo. Hivyo huu si wakati wa kulelemaa tu, kwa kufuata kila wimbi la mafundisho yanayokuja mbele yako. Bali ni wakati wa wewe binafsi kujitathimini, je! umesimama katika IMANI,? Je! Kristo akirudi leo utakwenda naye? Je! wewe binafsi upo katika utakatifu? Ambao biblia inasema pasipo huo hakuna mtu atakayemwona Mungu?(Waebrania 12:14) Je! unayashika maagizo yake?…Usisimame kwa niaba ya mwingine! Simama wewe kama wewe Kama ukijifunza kuenenda kwa utaratibu huo basi shetani hataweza kukunasa hata akija na wimbi kubwa kiasi gani la watumishi wake wa uongo, au mafundisho yake ya uongo, hata kupata kwasababu umejengwa juu ya mwamba imara YESU KRISTO.
Ubarikiwe sana.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Ufunuo 6:9 “Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.
10 Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?
11 Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vilevile kama wao.”
Shalom! Mpendwa wa Bwana. Leo ni siku nyingine Bwana ametupa, hivyo usikubali siku ya leo ipite bila kupata maarifa mapya yahusuyo maandiko hususani katika siku hizi za hatari tunazoishi.
Na leo tutatazama juu ya hizi roho zinazoonekana hapo zikiwa chini ya madhabahu zikilia kwa nguvu na kuugua kutaka zilipiziwe kisasi juu ya hao wakaao juu ya nchi, Leo tutaona hizi roho ni wakina nani.
Kama hufahamu bado juu ya ufunuo wa Mihuri saba ambayo habari yake inaanzia kutokea ule mstari wa kwanza, basi ni vizuri ukatenga muda wako kupitia maelezo yake hapa >> Ufunuo wa Mihuri saba ili ukifika hapa ikusaidie pia kupata picha kamili ya kitu kinachoendelea katika huu muhuri wa tano tunaokwenda kuutazama.
Watu hao wanaoonekana hapo si wengine zaidi ya wayahudi ambao waliuawa katika kipindi cha Holocaust, kilichotokea kati ya kipindi cha mwaka 1941-1945, Ambapo wayahudi wengi zaidi ya milioni 6 waliuawa kikatili chini ya utawala wa kidicteta wa NAZI Ujerumani..Historia inarekodi Mbili ya tatu ya wahayudi wote waliokuwa wanaishi bara la ulaya waliuliwa. Na Leo tutatazama kwa ufupi baadhi ya mateso waliyokuwa wanayapitia mpaka kupelekea kuwaona hapa chini ya madhabahu wakilia na kuuga kuomba kisasi kisikawie kulipizwa juu ya adui zao.
1) CHEMBA ZA GESI:
Wakati huo waayahudi wengi walikusanywa kutoka katika vijiji na miji mingi katika majimbo yote yaliyokuwa yanatawailiwa na Nazi, na kuahidiwa kuwa wanapelekwa mahali pa kutunzwa mbali na vita penye nyumba nzuri na utulivu.. Lakini badala yake walichukuliwa na kuwekwa katika treni, na kusafirishwa umbali mrefu kwa siku kadhaa bila hata maji wala chakula mbali na makazi ya watu, na kumbe huko kulikuwa tayari wameandaa kambi za mateso na kazi tu kwa ajili ya wayahudi. Sasa Walipokuwa wanawasili kwenye kambi, wanaume na wanawake na watoto walikuwa wanatengwa tofauti,.
Wale wanaume wenye nguvu walichukuliwa na kupelekwa kufanyishwa kazi ngumu za ujenzi wa reli na kukata magogo, lakini wale wanawake na watoto pamoja na wazee wote, walikuwa wanadanganywa kuwa kabla ya kwenda kupangiwa majukumu yao ya kazi inawapasa kwanza waende kuogeshwa kwa pamoja katika mabafu ya moto ili kuzuia magonjwa ambayo yamekuwa yakilipuka mara kwa mara katika kambi nyingi za ki-NAZI.
Hivyo bila kujua chochote wale wanawake na watoto wanakubali kuvua nguo zao, pamoja na kukatwa nywele zao. Kisha wanawachukulia kwa upole na kuwapelekwa kwenye vyumba maalumu vinavyoonekana kama mabafu yenye mabomba ya mvua.
Wakishawaingiza wote huko, kuhakikisha kuwa hakuna nafasi hata kuzunguka huku na kule kwa mtu yeyote kutokana na kubanana kwao, ghafla mlango wa chumba hicho kisichokuwa hata na sehemu ya kupitisha hewa kinafungwa kwa nyuma..Na taa zote kuzima eneo lote linakuwa giza kwa muda fulani.
Wakati wale watu kule ndani wanashangaa ni jambo gani linaendelea, ghafla tundu la chumba hicho kwa juu linafunguliwa kuruhusu mwanga wa jua kupita kwa muda mfupi, wakidhania kuwa wanafunguliwa maji kwa juu kumbe hapo juu anakuwa amesimama mtu ameshika makopo maalumu ya gesi mbaya ijulikanayo kama “ZYKLON B”, kitu anachofanya ni anaitaupa hiyo gesi chini kwa haraka kwenye hicho chumba cha shimo walichomo hao watu kisha anafunga mlango wa tundu.
Baada ya muda mfupi, kinachosikika huko nje ni kilio na mahangaiko ya watu, gesi ile ni mbaya kwasababu inaua oxgen yote, halafu inachoma mapafu mtu akiivuta anasikia kama moto unawaka kwenye kifua chake, damu zinaanza kutoka puani na midomoni, sasa kwa kuwa hakuna sehemu ya kutokea, basi watu kwa kujaribu kuokoa maisha yao wanarukiana huku na kule kama vile kuku aliyechinjwa wakijaribu kutafuta walau hata sehemu ya kuokoa maisha yao. Lakini kwa kuwa gesi ile ni kali sana mtu hafi kifo cha raha bali cha mateso makali na mahangaiko yasiyoelezeka, wengi wao wanakutwa wamekufa huku wametokwa na haja zote mbili. Na ndani ya muda wa dakika chache tu, kila mmoja anakuwa ameshakufa, kisha baadaye kidogo kama baada ya dakika ishirini hivi, askari wa ki-NAZI anakuja kufungua mlango wa ile chemba, na kuvuta miili yote nje. Na wakitoka hao wanaingizwa wengine.
Sasa kwa kuwa kambi hizi zipo mbali na makao ya watu, wale askari wanakuwa tayari wameshachimba mashimo makubwa na marefu, kwa ajili ya kuichomea miili ile, na kwa jinsi gesi ile ilivyo mbaya miili ikitoka pale hata kuitambua tena ni ngumu kwa jinsi ilivyoaribiwa na gesi ile. Moshi ule hauishi kwasababu kila siku idadi ya watu wasiopungua watu “ELFU SITA” walikuwa wanaingizwa katika chemba za gesi. Na hiyo ni takwimu ya kambi moja, na kulikuwa na kambi kama hizi nyingi tu za mateso.
Jaribu kufikiria ni unyama kiasi gani huo anafanyiwa mwanadamu mwenzako. Kumbuka wayahudi hawakufanya kosa lolote listahilio mateso hayo makali, walichukiwa kwasababu wao ni WAYAHUDI tu! Uzao wa Mungu basi!..wala hakuna sababu nyingine yoyote, iliyowafanya watende mambo ya kinyama kama hayo. Mamilioni ya wayahudi waliuawa kwa namna hii ya kuwekwa katika chemba za gesi.
Huo ni mfano wa mambo madogo sana yatakayokuja kutokea huko mbeleni kwa watu wale watakaoukosa unyakuo.
2) UCHUNGUZI WA KIMAABARA:
Sasa wale ambao watanusurika kwenda kwenye chemba za gesi, baadhi yao wanachukuliwa na kwenda kufanywa “SAMPULI” kwa majaribio katika mahabara. Wengine wanachukuliwa na kwenda kufungiwa katika vyumba maalumu, na ndani ya vyumba hivyo hawapewi maji wala chakula. Bali maji ya chumvi tu tena yale ya baharini, ili kutafiti ni jinsi gani wanadamu anaweza kuishi kwa muda mrefu kwa kutegemea tu maji ya bahari.
Hivyo kama wewe umesoma unaelewa ni jinsi gani chumvi inavyofonyonza maji mwilini, unakaukiwa maji kabisa, kiasi kwamba hata mate yanaisha mdomoni.. Jaribu kufikiria watu hao wanawekwa katika hali hiyo ya maji tu ya chumvi mpaka kufa kwao. Mfanyakazi mmoja wa kambi hizo anasema alishuhudia watu wale wakilamba sakafu kwa ajili ya maji yanayochuruzika wakati wa usafi katika sakafu. Lakini walikufa wote baada ya kipindi Fulani.
Wengine walichukuliwa na kuwekwa katika vyumba vya baridi vyenye barafu, uchi, kama majaribio wakifanyiwa utafiti kuona ni jinsi gani mtu anaweza kutibiwa kwa haraka kutoka katika ugonjwa wa Hypothermia, huu ni ugonjwa utokanao na mtu kupigwa na baridi sana na kupoteza fahamu kuwa kama kichaa..Lakini wengi wao hawakuweza kustahimili walikufa baada ya kipindi Fulani na wengine wale waliostahimili waliishia kupata mtindio wa ubongo wa kudumu.
Wengine walichukuliwa na kutolewa misuli yao mwilini wakishuhudia kwa macho yao na kuong’olewa mifupa yao bila hata ya ganzi yoyote, na kujaribu kuupandikizwa kwa mwengine ili wajaribu kuona kama kuna uwezekano wa kuamisha viungo kutoka kwa mwanadamu mmoja hadi kwa mwanadamu mwengine kwa muda mfupi na kuendelea kufanya kazi..Wengi wao kutokana na maumivu makali walikufa na baadhi ya walipata ulemavu wa kudumu na wale waliokuwa dhaifu waliuliwa au walipelekwa katika chemba za gesi.
Walikuwa wanawachukua vijana wadogo umri katika ya miaka 11-12 na kuwafunga mahali wasipoweza kuhangaika kisha wanafungiwa nyundo juu ya vichwa vyao na ile nyundo inaachiwa ishuke juu ya vichwa vyao kila baada ya dakika kadhaa, kupima kiwango cha ustahimiliji wa mtu anapojeruhiwa maeneo ya vichwani..wengi wa hao kama wasipokufa basi wanaishia kuwa vichaa.
Wanawachukua mapacha katika pea. Na kumfanyia utafiti aidha mmoja wao, huku mwingine akimtazama, wanaweka “dai” kwenye macho ya mmoja, kupima mabadiliko ya vina saba kwa mwingine..baadaye Yule akishamaliza kufanyiwa utafiti na kuonekana kuwa hafai tena ni kufa tu, basi wanamalizia kumuua na yule mwenzake, kwasababu hana kazi tena hapo.
Waliwahasi wayahudi wengi kwa njia tofauti tofauti wengine kwa x-ray, au upasuaji au kwa madawa makali n.k. kuona ni ipi iliyonyepesi ya kuwahasia watu kwa haraka bila kupoteza muda na gharama za matibabu. Wayahudi waligeuzwa kuwa wanyama.,.Na HITLER alikuwa na kauli mbiu yake inayosema “ hawa watu wasife tu kifo cha kawaida, bali wahakikishe wanakufa vifo vya mateso”. Mambo haya unaweza ukadhani ni hadhithi au yalitokea zamani sana lakini ni mambo yaliyotekea miaka 76 tu iliyopita!. Wapo watu baadhi ambao bado hawajafa walioshuhudia hizo kambi za mateso..
Wengine walichukuliwa juu kwenye helikopta za jeshi na kupelekwa juu sana na kisha kutupwa chini, pasipo parachuti na wanajeshi wale waliruka na maparachuti kujaribu kujijaribu uwezo wao wa kuokoa watu endapo wataanguka kutoka kwenye helikopta au ndege, wengi wa wayahudi hao waliishia kuanguka chini na kufa papo kwa hapo, na wale wanajeshi wakitua chini na parachuti wakiwa salama.
Wengine walichukuliwa na kufungiwa kwenye mabehewa, na magari ya mizigo, na huko ndani inapitishwa mirija yenye gesi ya carbon-monoxide..ile ya mkaa ambayo inamuua mtu kwa haraka sana. Kisha baadaye wanafunguliwa na kutupwa kwenye mashimo huko misituni.
Na Wale wanaosalia kufanya kazi ngumu, maisha yao ni ya viboko viboko na kazi, chakula ni supu tupu mchana, na kipande cha mkate kidogo usiku..hayo ndio maisha yao ya kila siku huku ukiwa kwenye kazi ngumu..ukionyesha udhaifu wowote kule kambini uliuliwa au ulinyongwa. Ndivyo ilivyokuwa katika kambi zote.
Kaka/dada hayo ni baadhi tu mateso ndugu zetu hawa wayahudi waliyoyapitia, katika kile kipindi cha vita ya pili ya dunia, na ndio hao wanaoonekana hapo chini ya madhabahu wakisema
“Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi? Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vilevile kama wao.”
Unaona? Biblia inasema “WAKAAMBIWA WASTAREHE BADO MUDA MCHACHE”.
Mpaka itimie idadi ya wajoli wao watakaouawa vile vile kama wao. Na hiyo ndugu itakuwa si wakati mwingine zaidi ya wakati wa DHIKI KUU ambayo ipo karibuni kutokea..bado muda mfupi sana. Ni dhiki ambayo Bwana Yesu anasema haijawahi kutokea wala haitakaa itokee tena kama hiyo baada ya hapo,.Yaliyowakuta wayahudi kipindi cha Hitler ni mfano mdogo sana kulinganisha na yatakayokuja kuwakuta tena wakati wa ile dhiki kuu mpinga-Kristo atakaponyanyuka kupambana na uzao wote wa Mungu .
Mpinga-Kristo atawaua watu wote ambao watakataa kuipokea ile chapa ya mnyama, lakini wale wote ambao watakubali kuipokea hatawaua,na watakuwa ni wengi sana watakaoikubali chapa ile, kwasababu haitakuja kwa wazi kama wengi wanavyodhani, na kwa pamoja wataingoja ile siku ya Bwana inayotisha ambayo itatokea kipindi kifupi tu baada ya dhiki kuu kuisha.
Na safari hiyo haitakuwa kwa wayahudi tu peke yao, bali pia kwa wale wakristo watakaochwa kwenye unyakuo. Na hawa hawatauliwa ovyo ovyo tu barabarani kama wengi wadhanivyo, bali watapelekwa pia katika makambi ya siri ya mateso, huko ndio kutakuwa na kilio na kusaga meno. Usitamani uwepo ndugu!
Bwana ameshatuonya, Dalili zote zinaonyesha Kristo yupo mlangoni kurudi, unyakuo ukipita leo je! Utakuwenda na Bwana katika karamu ya arusi ya mwanakondoo? Au utabakia hapa? Jibu unalo ndugu. Ni maombi yangu kwamba utaanza kuyatengeneza maisha yako tena upya.
Tubu dhambi zako sasa, ili usamehewe. Kisha ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO, upate ondoleo la dhambi zako, na baada ya hapo uendelee kuishi maisha ya kumtazama Bwana na utakatifu mpaka siku unyakuo utakapokukuta.
Maran Atha!
Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine na Bwana atakubariki, kwani utakuwa umeshiriki kuifanya kazi ya Mungu.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
Mathayo 12:20 “Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala utambi utokao moshi hatauzima, Hata ailetapo hukumu ikashinda.
21 Na jina lake Mataifa watalitumainia.”
Wakati nautafakari huu mstari nikakumbua tukio lilotokea mahali nilipokuwa ninaishi kipindi cha nyuma, Nakumbuka wakati fulani tulipanda migomba. Na kila siku jioni na asubuhi nilikuwa na desturi ya kwenda kuimwagilia,.mpaka ikakua kiasi cha kuanza kuzaa ndizi,.Lakini siku moja usiku upepo ulivuma, usiokuwa wa kawaida, na tulipoamka asubuhi tulikuta migomba mingi kati ya ile imelala chini, na kibaya zaidi yote iliyovunjika ilikuwa ni ile iliyokuwa imeanza kutoa Ndizi, nadhani kutokana na kulemewa na uzito wa ile mikungu ndio maana ikashindwa kustahimili upepo na kuanguka, ilibaki michache tu ambayo haikuanguka na hiyo ilikuwa ni ile ambayo haijazaa..Haikuwa migomba ya hapo tu, bali mpaka ya majirani pia ilianguka..
Sasa Kitu tulichokifanya ni kujaribu kuinyanyua ili kuisapoti na mirunda ya miti, lakini mingi ilivunjia vibaya kiasi kwamba hata ukiunyanyua upande huu, unaangukia upenda ule, hata mfano uweke mirunda 6 kuusapoti mgomba mmoja bado hauwezi kusimama, na kuikata hatuwezi, tutakosa ndizi na ndizi bado ni changa. Hivyo ilitubidi kupambana nayo hivyo hivyo kujaribu kuisimamisha au kuigemeza kwa namna ambayo haitaweza kukauka mpaka hapo ndizi zitakapokomaa.Tulipitia changamoto Fulani mfano Leo utaisimamisha hivi, kesho utakuta umeanguka tena, leo utauweka hivi kesho utaikuta ipo vile. Lakini japo iliendelea kuwa katika hali mbaya ya kusua sua, lakini hatukukosa kabisa kupata ndizi, tulivuna ndizi zilizokomaa kabisa zisizo na matatizo.
Sasa ndio najiuliza kama sisi hatukuweza kuikatia tamaa migomba ile, ambayo sio kwamba ilikuwa ndio chakula pekee tulichonacho, hapana lakini hatukupenda tu kuiona katika hali ile ya kuanguka,..lakini hatukuikatia tamaa kabisa mpaka ilipofika wakati wa kutoa matunda mazuri kabisa yaliyokomaa,..UNADHANI MUNGU ATATUKATIAJE TAMAA SISI ?. Embu yatafakari tena haya maneno yaliyonenwa juu ya Bwana Yesu.
“Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala utambi utokao moshi hatauzima, Hata ailetapo hukumu ikashinda.
21 Na jina lake Mataifa watalitumainia.”
Mwanzi, ni shina lolote la mmea, inaweza ikawa ni mti, mchicha, mgonga n.k. Lakini anasema ukipondeka huo, hata kufikia hatua ya kukosa matumaini kabisa yeye anasema hatamalizia kuuvunja..Utambi utoao moshi ni kama umeshazima, yaani utambi ukishafikia hatua ya kutoa moshi tu, ni wazi kuwa huo tayari umeshazima huo, lakini yeye anasema hataumalizia kuuzima, moyo ambao wewe huwezi kuwa nao, huwezi kuwa na tumaini na utambi ambao unatoa moshi tu, tena kikubwa utakachofanya hapo ni kuuzima haraka usiendelee kukotelea moshi. Lakini kwa YESU haikuwa hivyo, yeye bado aliutazama, na kuuhangaikia..Na utambi huo ni sisi, mwanzi huo ni mimi na wewe!
Inawezekana maisha yako ni sawa na mwanzi uliopondeka, umefika hatua, unaona kabisa tayari ulishakosea njia, na hakuna matumaini tena ya kumrudia Mungu, umekuwa mlevi wa kupindukia, unatumia madawa ya kulevya mpaka yamesha kauthiri huwezi tena kuacha.,Umekuwa mwasherati mpaka imefikia hatua umepata UKIMWI, na wewe bado ni kijana mdogo tu na hivyo umekata tamaa ya kuishi, unaona kama jamii haiwezi kuwa na wewe tena, wala Mungu kukupokea kwa mambo uliyoyafanya. Umekuwa katika magonjwa yasiyoponyeka, huna tumaini tena. Nataka nikuambie, YESU yupo, sio marehemu, kutaka kukusimamisha tena, na kukunyanyua tena uwe mwana Mungu BUREEE!!.
Yeye ndiye aliyetabiriwa maneno haya
Isaya 61: 1 “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA AMENITIA MAFUTA niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao”.
Unaona? Unaweza ukawa ni mdhaifu wa Imani, imefikia wakati unataka kusema Mungu hayupo umekuwa utambi unaotoa moshi, ni hatua moja tu imebaki ya wewe na kukata tamaa ya maisha, umekuwa katika vifungo vya giza, umeingia katika ushirikina, na uchawi, maisha yako unaona kabisa yapo hatarini kutoweka, hujui kama hata kesho utaishi kwa jinsi ulivyo katika vifungo vya hofu, wewe ni utambi unaotoa moshi, pengine unaweza ukawa ulianza vizuri na Kristo huko nyuma ulikuwa moto kweli kweli utambi wako ulikuwa unawaka vizuri huna shida yoyote , lakini wakati ukafika shughuli za dunia na udanganyifu wa mali na anasa vikakusonga, sasa umepoa huna tofauti na watenda dhambi wengine..Yesu ni wa rehema bado anatamani kukuwasha tena uangaze upya. Ametiwa mafuta kwa kazi hiyo.
Ulimwengu utakukatia tamaa, lakini Kristo anakutazama haijalishi umedondoka mara ngapi, Upo katika masononeko ya roho, upo katika tabu na maumivu mbali mbali, Njoo kwa Yesu. Leo hii sema ni mwisho naanza tena na Bwana naye atakupokea,..
Ukisoma pale mbele kidogo utaona anaendelea kusema Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala utambi utokao moshi hatauzima, HATA AILETAPO HUKUMU IKASHINDA..Unaona? Hukumu inayozungumziwa hapo, ni kusudi la Mungu, au mapenzi ya Mungu juu ya mtu huyo…Ikiwa na maana kuwa Yesu atahakikisha mtu Yule ampokee yeye..japo atakuwa ameharibika kiasi cha kutokuweza kutengenezwa tena, yeye mwenyewe atahakikisha anamfanya upya maisha yake na kuhakikisha mapenzi yote ya Baba yake aliyokusudia juu ya huyo mtu yanatimia. Na ndio maana anasema:
Mathayo 11: 28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”
Ndugu ni nani awezaye kukuahidi mambo mema kama haya kama sio YESU peke yake.?Kwanini kila siku unasikia YESU ni rafiki wa wengine, Na asiwe rafiki yako? Hata sisi tulipokuwa walevi, na wazinzi, na watukanaji, wa endaji disco, watazamaji pornography, tulikuwa katika hofu, japo mbele za watu tulijifanya wenye furaha siku zote, na wenye ujasiri..Lakini siku YESU alipotupa raha nafsini mwetu ndipo tulipojua hakika raha halisi ipo wapi?..Kwahiyo tunafahamu vizuri hali unayopitia wewe uliye katika dhambi, kwasababu na sisi tulikuwa huko, lakini tumeonja huku, na tumejua hakika Bwana ni mwema.
Njoo! Kwa mwokozi wako ambaye ni mwokozi wetu pia, muda unazidi kwenda, moja ya siku hizi UNYAKUO utapita, au kama hautapita basi KIFO kitakukuta, sasa huko uendako ni nani atakuwa mtetezi wako? Kama umemkataa mtetezi wako angani u hai?..Ukimpokea leo atakuwa ni rafiki mwema kwako.
Bwana akuangazie rehema zake.
Ubarikiwe na Bwana.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoenda:
NAMNA GANI NITAPOKEA NGUVU ZA BWANA YESU?
Shalom! Mtu wa Mungu, karibu tujifunze Neno la Mungu, kwa Neema zake, leo tutajifunza kuhusu umuhimu wa kumwinua Yesu Kristo katika maisha yetu, Tunaweza tukajifunza katika safari ya wana wa Israeli wakati wametoka Misri, ambapo tunaona wakati Bwana amewatoa katika utawala mgumu wa Farao, wakiwa njiani kuelekea nchi yao ya ahadi, walikutana na jeshi la shetani kuwapinga safarini. Na hawa hawakuwa wengine zaidi ya WAAMALEKI. Waamaleki walikuwa ni watu kutoka katika uzao wa Esau ndugu yake Yakobo..
Kama unakumbuka Isaka wakati anawabariki wanawe Esau na Yakobo, Yakobo alimnyang’anya ndugu yake mbaraka wake, kwasababu ya yeye kutokuujali ukubwa Mungu aliompa. Hivyo ikatengeneza aina fulani ya chuki kati ya hao ndugu wawili, yaani Esau na Yakobo, na Baba yao tunasoma baada ya kumbariki Yakobo alimwambia Esau maneno haya…
Mwanzo 27: 38 “Esau akamwambia babaye, Una mbaraka mmoja tu, babangu? Unibariki mimi, mimi nami, Ee babangu. Esau akapaza sauti yake, akalia.
39 Isaka, baba yake, akajibu, akamwambia,Angalia, penye manono ya nchi patakuwa makao yako,Na penye umande wa mbingu unaotoka juu.
40 Kwa upanga wako wewe utaishi, nawe utamtumikia nduguyo; NA ITAKUWA UTAKAPOPONYOKA, UTALIVUNJA KONGWA LAKE KATIKA SHINGO YAKO.
41 Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ule mbaraka babaye aliombarikia. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo”.
Kwahiyo unaweza kuona hapo hizo Baraka, hazikuwa kwa Esau na Yakobo tu peke yao, bali ni kwa vizazi vyote vya Esau na vizazi vyote vya Yakobo,.Kwamba Israeli atakuwa akimshinda Esau lakini endapo Israeli atalemaa katika roho basi Esau atampiga na kulivunja kongwa lake katika shingo yake.
Sasa hapa baada ya miaka mingi sana zaidi ya miaka 400 Kupita..tunaona uzao wa Yakobo ambao ndio wana wa Israeli unakutana tena katika mapambano na uzao wa Esau ambao ndio hao Waamaleki. Hivyo Israeli walijua kabisa endapo tusipokuwa makini, na hawa wakiwa na bidii basi unabii unaosema hatutamshinda Esau utatimia juu yetu..Hivyo ile vita haikuwa ya kawaida palikuwa na changamoto kubwa sana katika, Israeli hawakuwa na namna nyingine zaidi ya kumgeukia Mungu na kumtegemea yeye…
Ndipo tunasoma Musa baada ya kupata hizo habari kuwa waamaleki wamewazunguka alikwenda kumwomba Mungu wa Israeli na Bwana akampa maagizo ya kufanya kama tunavyosoma katika…
Kutoka 17: 8 “Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu.
9 Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu.
10 Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima.
11 Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda.
12 Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa.
13 Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga”.
Hapa tunaona mkono wa Musa ndio uliowapa ushindi waisraeli, alipounyanyua juu, ndivyo waisraeli walivyokuwa wanapata nguvu vitani, na alipoushusha waamaleki waliwapiga waisraeli..Lakini kama tunavyosoma mwisho wa siku Israeli walishinda kutokana na Mikono ya Musa kusimama juu muda wote.
Ni nini tunachoweza kujifunza katika habari hii ??
Wakristo sisi ni uzao wa Mungu, ambapo tumefanyika kuwa uzao wa Mungu kweli kweli, kupitia Yesu Kristo Bwana Wetu, Mkuu wa Uzima, sisi tunafananishwa na Uzao wa YAKOBO ambao umebarikiwa…Lakini pia upo uzao wa yule Adui, huo unafanana na uzao wa ESAU, na huo kazi yake ni kupambana na sisi kila siku kutupinga katika safari yetu ya kwenda mbinguni,..Na Bwana alitoa unabii kama alivyotoa kwa Yakobo na Ndugu yake kwamba Yakobo atampiga Esau lakini pia Esau akiponyoka atamvunja kongwa Yakobo katika shingo yake {Kwa tafsiri iliyo nyepesi ni hii: Esau akijitahidi na kupata nguvu, basi ataweza kuondoa utawala wa ndugu yake juu yake}..Na pia Bwana alizungumza juu yetu, na kusema.
“nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino. Mwanzo 3:15”
Wengi tunaishia hapo kwamba, uzao wako utamponda kichwa, lakini tunasahau kuwa pia uzao wa nyoka umepewa mamlaka ya kutuponda sisi kisigino, tusipokuwa makini”
Kwahiyo katika ulimwengu wa Roho ni vita vikali vinaendelea, hivyo inahitajika umakini mkubwa sana, na msaada ya Mungu.
Sasa Biblia inasema… “kama vile Musa alivyomwinua nyoka wa shaba jangwani” ili kila amtazamaye yule nyoka wa shaba apone, ndivyo hivyo hivyo Mwana wa Adamu alipaswa ainuliwe msalabani ili kila mtu amtazamaye aokolewe..
Kadhalika kama Musa alivyounyanyua mkono wake juu ili kila Mwisraeli aliyeko vitani apate kupona na kuteka na kupata ushindi dhidi ya Maadui zake..NA WAKRISTO VIVYO HIVYO HATUNA BUDI KUMWINUA YESU KRISTO KATIKA MAISHA YETU ili tuweze kupata ushindi dhidi ya maadui zetu (yaani roho ya uadui inayotenda kazi ndani ya watu na majeshi ya mapepo wabaya).
Na kumbuka kumwinua Kristo katika maisha yetu sio kumwimbia mapambio na nyimbo za kuabudu, hiyo ni sehemu mojawapo, Lakini sehemu kubwa ya kumwinua Mungu katika maisha yetu ni kumaanisha kumwamini kwa kuzitubia dhambi na kuzicha, na kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu na kuishi maisha ya utakatifu yanayoonekana mbele za watu kuanzia huo wakati na kuendelea, huko ndiko kumwinua Kristo kunakozungumziwa.
Kumbuka pia hakuna ushindi pasipo Yesu Kristo kuinuliwa juu ya maisha yetu. Musa alipoishiwa nguvu watu walikuja kumsaidia kuitegemeza mikono yake ili isishuke…Na sisi katika maisha yetu ya kikristo ya vita, tunapoishiwa nguvu…tunapaswa tufanye juu chini tusiiangushe imani yetu kwa Kristo tuishikilie kwelikweli kwa bidii zote maana hiyo tumekabidhiwa mara moja tu!…Biblia inasema “Mpende Bwana Mungu wako kwa nguvu zako zote, kwa akili zako zote, na kwa moyo wako wote”.
Vinginevyo tukisema tuiache Imani, shetani yupo na amepewa amri ya kutuponda visigino. Amri hiyo kapokea kutoka kwa Mungu.
Ndugu unayesoma ujumbe huu, Yesu Kristo ni muhimu sana katika maisha haya…kama ulimsikia kwa juu juu tu!! kanisani, au mahali popote pale, kama umehubiriwa ni wa-mafanikio-ya-kibiashara Yesu ni zaidi ya hapo!…. jaribu tena kutenga muda umtafakari, hakuna tumaini, wokovu, hakuna maisha, hakuna mafanikio yoyote nje ya Yesu Kristo!…Waliomwamini ndio wanaoitwa wabarikiwa. Huwezi kumpendeza Mungu wala kumwelewa Mungu, wala kumshinda shetani nje ya Yesu Kristo!…Kama ule mkono haujanyanyuliwa juu (Yesu Kristo) hata kama unajiona unatenda wema kiasi gani kama hujamnyanyua juu ni kazi bure! Ni sawa na mtu anayefanya kazi katika shirika ambalo hajaajiriwa, wala hawamjua akitumai kupata mshahara mwisho wa mwezi kutoka huko.. mipango yako ni mizuri lakini nje! Ya Yesu Kristo ni bure!..
Suluhisho ni kumtamani aje aingie katika maisha na kuanza maisha mapya katika yeye..
Bwana akubariki sana.
Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.
Kutokujizuia ni kitendo cha kukosa uwezo wa kutawala kitu fulani kisitokee kisichopaswa kufanyika kwa wakati huo. Kwa mfano mtu anapokuwa mlevi wakati mwingine anajikuta amejisaidia pale pale, au kinywa chake kinaanza kuzungumza maneno yasiyokuwa na maana, pengine ataanza kutukana au kufoka..Huko ni kutojizuia..mambo ambayo mfano angekuwa na akili timamu, asingeweza kuyafanya hadharani.
Biblia inasema moja ya dalili kubwa itakayotuonyesha kuwa tunaishi katika siku za mwisho ni kuwepo kwa wimbi kubwa la watu wasioweza KUJIZUIA. Na kutojizuia kunakozungumziwa hapo sio kujizuia kutokutokwa na haja, hapana bali kutojizuia kutenda maovu hadharani mbele za watu, hivyo si watu wema wanaozungumziwa hapa bali wanazungumziwa wale walio waovu, ili kutofautisha uovu ule wa nyuma na huu wa siku za mwisho, kumbuka waovu wa zamani walikuwa na kitu kinachoitwa Kujizuia, lakini waovu wa siku za mwisho biblia inaweka wazi kuwa hicho kitu hakitaonekana ndani yao kabisa.
2 Timotheo 3:1-17
1 Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.
2 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,
3 wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, WASIOJIZUIA, wakali, wasiopenda mema,
4 wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;
5 wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.
Ilikuwa zamani, mwanamke kahaba ni mtu wa kujificha, anafanya ukahaba wake kwa siri hata ni ngumu kumtambua, mavazi yake ya kikahaba alikuwa anayavaa usiku tu tena katika eneo la shughuli zake, nje ya hapo huwezi kumkuta, ilikuwa huwezi kumwona hadharani ovyo ovyo eti anazunguka na uwazi wake barabarani, haikuwahi kutokea hivyo wakati wowote. lakini angalia sasa, makahaba wanashindwa kujiuzia kufanya mambo yao, wanakosa ule uwezo wa kutawala tamaa zao, ile hofu ya watu kuwaona na kuwachukulia hivi au vile haipo tena ndani yao, wapo tayari kupiga picha za uchi, na kutengeneza video za zisizofaa ambazo hazistahili kabisa kuwepo, na kwa ujasiri kabisa wana zi-post katika mitandao, ili watu wote wawaone, na kibaya zaidi wanaofanya hivyo wengi wao ni watu wanaojulikana, ili kusudi kwamba uchafu wao uweze kuwafikia watu wengi zaidi kwa muda mfupi, hizi ndizo ishara madhubuti za siku za mwisho.
Sio kana kwamba hayo mambo yalikuwa hayafanyiki zamani, hapana yalifanyika kwani biblia inatuambia hakuna jambo jipya chini ya mbingu, lakini kwanini unaona kama siku hizi maovu yameongezeka zaidi ya zamani,? Jibu ni kwamba hayajaongezeka kwa kiwango kile unachofikiri bali kinachoendelea sasa ni kwamba wafanyao maovu wa sasa wamepoteza kile kitu kinachoitwa kujizuia ndani yao..Roho ya kutokujali lolote imewavaa, roho ya “fuata mambo yako”, roho ya “ishi maisha yako”..roho ya “kutokujali” ndio inayotawala maisha yao. Na ndio maana hushangai hata kuona watu wa karne hizi watu waki-tengeneza video wanazini na wanyama n.k..Si ajabu tena kwao, kudhihirisha aibu zao wazi. Inasikitisha sana!
Kutukana hadharani hakukuwepo zamani, lakini sasa viwango vya matusi vimekithiri, mabarabarani, kwenye nyimbo za kidunia, kwenye mitandao, si watu wazima si watoto wadogo, maneno yanayozungumzwa huwezi kuamini kama marika kama hayo yanaweza kutoa maneno magumu kama hayo katika vinywa vyao.
Mashoga na wasagaji, wanajitangaza hadharani, hawajali tena hata vyombo vya dola na huku wanajua kabisa kwamba Sheria za nchi haziruhusu vitendo hivyo na kwamba mtu anayefanya hivyo adhabu yake ni kali, wao hilo wanaliona kabisa hawalijali sembuse Mungu wasiyemwona?. KUTOJIZUIA.
Washirikina waendao kutafuta mali kwa waganga wa kienyeji, zamani walikuwa hawadhubutu kuiathiri jamii hadharani kama wafanyavyo sasa hivi, lakini angalia leo, mtu anafikia hatua hata ya kwenda kukata viungo vya watu wasio na hatia (ma-albino, na mtatiti ya mabinti wadogo) kwa tamaa tu za mali.
Kutokujizui, Biblia inasema pia hapo juu siku za mwisho watatokea watu WAKALI, Wasiopenda mema, ile dhambi inapata nguvu mpaka sasa hawezi kutulia ndani, inajidhihirisha nje bila kujali kitu chochote wala mtu yoyote..
Dalili nyingine inayozungumziwa hapo juu ni “KUSINGIZIA”..Tafsiri halisi iliyotumika hapo, kusingizia maana yake, ni “kumzunguzia mwingine vibaya”, au “kumsengenya mtu” kwa lugha nyepesi iliyozoelewa sasa Ni ‘’Umbea”. Kusengenya ni KIU mtu anakuwa nayo ya kutaka kupakua habari za maisha ya mtu mwingine kwa nia ya udadisi ili kupata huko mambo ya kumzungumzia yasiyopendeza mbele za Mungu..
Haya mambo zamani yalikuwepo lakini sio kwa kiwango cha uwazi kilichopo sasa, utakuta mtu anashindwa kujizuia kabisa, Anashindwa kufanya mambo yake mwenyewe, anashindwa kuwazungumzia watu kwa wema, anajikuta kutwa kuchwa ni kudadisi maisha ya watu wengine kwa ubaya. Sasa ukiona wimbi la watu wa namna hii linaongezeka basi fahamu kuwa tunaishi katika majira ya mwisho wa Dunia.
Ndugu yangu. Kama vile hilo andiko linavyosema “siku za mwisho kutakuwako na nyakati za HATARI ”. Fahamu kuwa nyakati zenyewe ndio hizi tunazoishi..Ikiwa utashindwa kujizuia mwenyewe na kuona kila kitu kufanya ni SAWA TU!…Zamani ulikuwa unaona aibu kuvaa vimini na kutembea navyo barabarani lakini sasa unaona hakuna shida yoyote! Ujue kuwa upo katika hatari kubwa sana..roho ya kutokujali imekuingia.
Ukiona zamani ulikuwa ukitukana unajisikia vibaya lakini sasa matusi yamekuwa ni sehemu ya maisha yako. Ujue kuwa ile roho ya kutokujali imekuvaa..Kama vile wale watu wa sodoma na gomora, jinsi walivyokuwa na tabia ya kutokujizuia hata kufikia hatua ya kutaka kulala na wageni wale (malaika wa Mungu) waliokuja yamkini kusitiri uovu wao,lakini wao wakashindwa kujizuia. Jambo gani lilitokea muda mfupi baada ya pale?. Kwanza kabla hata maangamizi hayajawafikia walipigwa upofu. Na upofu ule ni wa daima..Vivyo hivyo na kwa watu wasiojizuia sasa, Upofu unakuja, na upofu huo ni wa daima, ukishamkuta tu mtu, basi huyo mtu hata afanyeje ni wa kuangamizwa tu! hawezi kutubu tena, neema inakuwa haipo tena juu yake, hata ahubiriweje injili.
Zamani ulikuwa unajisikia vibaya kula rushwa, na kufanya utapeli lakini sasa yote yamekuwa sawa kwako, zamani uliogopa hata kusogelea msonge wa waganga wa kienyeji lakini siku hizi pamekuwa kama nyumbani kwako, namba za waganga na watabiri wa nyota zimejaa kwenye simu yako ya mkononi. Upo katika hatari kubwa sana.
Hujizuii mwili wako, unatembea nusu-uchi barabarani na ku-post picha chafu mitandaoni, humwogopi tena Mungu kama hapo zamani, unakuwa ni sababu ya watu wengi kumkosea Mungu, kwa kutazama vitu unavyovipost na mavazi unayoyavaa..Dada upo katika HATARI kubwa sana. Hukumu yako haitakuwa sawa na wale wengine..siku ile fahamu tu utapigwa sana, kama usipotubu, kwasababu uliijua kweli na bado ukaendelea kufanya kwa makusudi. Kuzimu ipo ni kitu halisi kabisa, mtu yeyote asikudanganye kuwa hakuna kuzimu, ipo kabisa.
Tukiyajua hayo, basi ni wajibu wetu kumrudia muumba wetu, kabla ya huu uharibifu mkubwa ambao utaikumba dunia nzima haujatukuta sisi.. Tubu dhambi zako sasa, ukabatizwe upate ondoleo la dhambi zako.
Mwenye sikio asikie Neno hili, ambalo Roho wa Mungu anatuonya watu wa kizazi hiki. Kwamba tujihadhari nacho.
Ubarikiwe.
Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
Shalom mtu wa Mungu, karibu tujifunze Maneno ya Mungu, kwa Neema zake, leo tutajifunza somo linalosema, Kuchaguliwa kabla ya kuwekwa misingi ya Ulimwengu.
Tunajua kuwa Mungu tunayemwabudu, yaani Yule aliyekuwa anaabudiwa na wana wa Israeli ambaye sasa tunamwabudu na sisi watu wa Mataifa, Mungu muumba wa Mbingu na nchi hana mwanzo wala hana mwisho, sentensi hiyo tu! Inatosha kutujulisha yeye ni Mkuu kiasi gani, yeye ni zaidi ya upeo wetu wa kufikiri. Kwasababu kitu kisichokuwa na mwanzo wala kisichokuwa na mwisho ni kitu cha namna gani hicho?.
Hivyo basi kama hana mwanzo wala hana mwisho ni dhahiri kuwa atakuwa na uwezo wa kufahamu mwanzo wa ulimwengu na mwisho wa Ulimwengu mzima, ndio maana katika Neno lake anatabiri yatakayotokea katika siku za mwisho maelfu ya miaka nyuma kabla hata ya hiyo siku kutokea…Anasema siku za mwisho kutatokea hiki na kile, anaendelea kusema, baada ya dunia kuisha kutakuja utawala wa miaka 1000, anaendelea kusema baada ya utawala wa miaka 1000 kuisha kiti cheupe cha hukumu kitawekwa, ambapo wafu wote watafufuliwa na kuhukumiwa n.k n.k..Mambo hayo yote Bwana tayari anayajua.
Na kama anajua mwisho wa dunia katika mtiririko wote, ni dhahiri kuwa atakuwa anajua pia mwanzo na mwisho wa kila mwanadamu katika mtiririko wote…ikiwa na maana kuwa anajua ni yupi ataokolewa na yupi hataokolewa, ni yupi ataingia mbinguni na ni yupi hataingia mbinguni siku ya mwisho…Na kama anayajua hayo ni dhahiri kuwa ni yeye huyo huyo ndiye anayechagua ni yupi ataokolewa na yupi hataokolewa..Kwasababu Bwana Yesu mwenyewe alisema “Hakuna awezaye kuja kwangu asipovutwa na Baba yangu aliyenipeleka (Yohana 6:44)”. Kwahiyo ni Roho Mtakatifu ndiye anayemvuta mtu kwa MUNGU na sio mtu mwenyewe anayejipeleka kwa Mungu.
Kama Mungu yupo hivyo pengine utasema, kwanini aumbe wengine hivi wengine vile? Huo ni kama vile udhalimu Fulani hivi…Jibu la swali hilo, Mtume Paulo alilitoa kwa uweza wa Roho akasema.. Tusome:
Warumi 9:13 “Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia.
14 Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha!
15 Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye.
16 Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu.
17 Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote.
18 Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu.
19 Basi, utaniambia, Mbona angali akilaumu? Kwa maana ni nani ashindanaye na kusudi lake?
20 La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi?.
21 Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?”.
Umeona hapo? Hakuna awezaye kushindana na kusudi la Mungu, anafanya yote kama atakavyo yeye… “HILO LINAOGOPESHA SANA.” Sisi wanadamu hatuwezi kumwuliza Mungu kwanini anafanya vile au kwanini anafanya hivi.. Ulishawahi kuaamka asubuhi na kuanza kumwuliza Mungu kwanini hakutuumba na mabawa, kama alivyowapa malaika? nasi tuwe tunaruka juu kama ndege?… Au kuku amwulize Mungu kwanini yeye kaumbwa kuku na wala si mtu? Ndivyo ilivyompendeza yeye tuwe hivi tulivyo…
Sasa swali linakuja nitajuaje kuwa mimi nimekusudiwa wokovu, na tena Nimechaguliwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu?.
Jibu la swali hilo hatuwezi kulipata kwa kufunga na kuomba Mungu atufunulie, wala hutuwezi kulipata kwa kukisia tu! Wala hatuwezi tukasema kwa kukisia tu Kwamba mimi nitakuwa ni miongoni wa waliochaguliwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Ili tujue kwamba sisi ni miongoni wa waliochaguliwa Jibu la swali hilo tutalipata katika BIBLIA TU!
Neno la Mungu linasema hivi katika kitabu cha.
Waefeso 1: 3 “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;
4 kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.
5 Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake”.
Ukitafakari kwa makini mstari huo wa nne utagundua vigezo vya kuchaguliwa tangu asili ni vipi?…hapo anasema “kama alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ILI TUWE WATAKATIFU, WATU WASIO NA HATIA MBELE ZAKE KATIKA PENDO”…Zingatia hili neno “ILI TUWE WATAKATIFU”…hii ikiwa na maana kuwa mtu aliyechaguliwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu..alama yake ni UTAKATIFU. Kama Yesu Kristo alivyokuwa mtakatifu tunapaswa tufanane naye ndio tuwe na uhakika kwamba na sisi ni miongoni mwa lile kundi lililochaguliwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu..
Na kama tunavyojua UTAKATIFU chanzo chake ni ROHO MTAKATIFU kama jina lenyewe lilivyo..roho chafu matunda yake ni uchafu, roho ya uzinzi matunda yake ni uzinzi, kadhalika na Roho takatifu matunda yake ni utakatifu. Kwahiyo kwa ufupi mtu yeyote ambaye maisha yake ni ya UTAKATIFU katika Kristo Yesu, huyo mtu asilimia 100 amechaguliwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Hakuna alama nyingine zaidi ya hiyo. Kwasababu anafanana na Yesu Kristo na kama maandiko yanavyosema pia katika kitabu cha waebrania.
Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, NA HUO UTAKATIFU, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao”
Unaona hapo? Tiketi ya kumwona Mungu ni UTAKATIFU. Kwahiyo kwa hitimisho namna ya kujichunguza kama umechaguliwa tangu asili ni kujichunguza maisha yako je! Ni ya utakatifu? Au sio ya utakatifu, hapo ndipo utakapojijua wewe upo kundi gani na ndipo utakapoijua roho iliyopo ndani yako? Je ni roho chafu au ni roho mtakatifu?..je! maisha yako yanafanana na maisha ya Yesu Kristo au Yuda eskariote, maana maandiko yanasema.
Warumi 8: 29 “Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.
30 Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita,hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza”.
Je! Na wewe ni mtakatifu kama mwana wa Mungu, Yesu alivyokuwa mtakatifu, umefananishwa na yeye?..au ni mla rushwa?, au ni msengenyaji?, au ni mzinzi, au Ni mwasherati? au ni mtazamaji wa pornography au mfanyaji masturbation? Au wewe ni msagaji? Na kahaba? Je! Ni mlawiti?, je! Ni mvaaji wa nguo fupi na suruali zinazokuonyesha maungo yako? je ni muuaji au mhudhuriaji kwa waganga na disko? Je! Ni mtukanaji. Kama hayo yote unayafanya na bado unakwenda kanisani na kujiita mkristo na kujifariji kwamba upo katika mstari wa watakaoenda mbinguni..napenda nikuambie ndugu yangu “ichunguze hiyo roho iliyopo ndani yako” sio roho mtakatifu bali ni roho nyingine ya Yule adui, inayokuongoza kwenda katika ziwa la moto. Roho wa Mungu aletaye utakatifu ndani ya mtu huyo ndio MUHURI AU ALAMA ya kukutambulisha kwamba wewe ni umechaguliwa tangu asili au la! Kwamba wewe umekusudiwa wokovu au la! Maandiko yanasema hivyo. (Waefeso 4: 30 “Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye MLITIWA MUHURI hata siku ya ukombozi”).
Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, KATIKA HAYO NAWAAMBIA MAPEMA, KAMA NILIVYOKWISHA KUWAAMBIA, YA KWAMBA WATU WATENDAO MAMBO YA JINSI HIYO HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU.”
Ndugu yangu, naamini na wewe ni mmoja wa waliochaguliwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ndio maana Roho Mtakatifu aletaye utakatifu hajakuacha kabisa yupo nje! Anagonga mlango wa moyo wako anataka kuingia ndani yako AKUTIE MUHURI WA UTAKATIFU, ili uwe na tiketi ya kumwona Mungu.
Lakini kama huisikii sauti yake wala kwako haina maana basi wewe sio miongoni mwa walio wake..kama biblia inavyosema katika Warumi 8:9 “Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. LAKINI MTU AWAYE YOTE ASIPOKUWA NA ROHO WA KRISTO, HUYO SI WAKE.”.
Swali linarudi lile lile..Je! wewe ni miongoni mwa walio wake au wasio wake??..je! wewe ni miongoni mwa watakaoenda mbinguni au watakaoenda katika lile ziwa la moto? Je! Unaisikia sasa sauti ya Roho mtakatifu anayekutaka utubu na uwe mtakatifu au huisikii?.. Jibu unalo wewe.
Ikiwa unataka leo hii Roho Mtakatifu aingie ndani yako, uwe miongoni mwa waliochaguliwa kabla ya msingi wa ulimwengu, unachopaswa kufanya hapo ulipo, tenga sio chini ya dakika 10 au zaidi hapo ulipo Tubu! mwambie Bwana akusamehe maovu yako yote, mweleze yote usifiche hata moja maana yeye anakujua kuingia kwako na kutoka kwako?..na kisha baada ya kufanya hivyo dhamiria kuacha hayo maisha ya dhambi uliyokuwa unaishi..usiende kulewa tena, usiende kufanya uasherati tena, achana na kampani mbovu n.k Kisha hatua ya pili inayofuata Nenda katafute ubatizo sahihi wa kweli wa kimaandiko nao ni wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo, ili kumbukumbu la dhambi zako zifutwe kabisa kabisa… na baada ya hapo Roho Mtakatifu ataingia ndani yako na kukupa wewe nguvu na uwezo wa kushinda dhambi na kuishi maisha ya utakatifu.
Uwezo huo au nguvu hiyo haiji isipokuwa kwanza umedhamiria kuacha njia zako mbaya za nyuma, wengi wanasema wametubu na kukoka lakini bado mioyo yao ipo Misri, na ndio maana wanashindwa kuishinda dhambi kwasababu hiyo.. Ile nguvu ya Roho Mtakatifu haijashushwa ndani yao kutokanana na mioyo yao kutokuwa thabiti kwa yeye waliyemtubia dhambi zako.
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja KWA JINA LAKE YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.”
Hivyo fanya hivyo leo na Bwana atakuangazia Nuru yake.Hapo ndipo utapata uhakika ya kuwa umechaguliwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu. Kesho si yako, hizi ni siku za mwisho.
Bwana akubariki sana.
Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine na Bwana azidi kukubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinaendana:
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
(Ndoto ya Ndugu Yusufu, kutoka Tabora, mwaminio wa ujumbe wa Malaki 4:5)
Mbarikiwe sana ndugu zangu, Ndugu zangu naomba nisaidieni kupata tafsiri ya hii hii njozi maana imenitatiza sana:
Niliota kwamba BWANA YESU KRISTO amekuja duniani .lakini alipokuja aliwakuta watu baadhi wakiendeleea na shughuli zao (hawakujua kuwa amekuja) .na alipo fika alichukua watu baadhi akatoka nao kidogo nje ya kijiji kile (lakini kuna mtu mwingine alisema kwamba kuna kitu amesahau sehemu basi akaamua kukirudia hicho kitu ;huku wale wengine ambao BWANA YESU kawatoa nje ya kijiji wakiambatana nae)_..
Sasa tulipofika mwisho wa kijiji kile (pembezoni mwa kijiji ) BWANA YESU akasema anaanza kubagua Kondoo na mbuzi kwenye lile kundi alilotoka nalo kwenye kile kijiji .. .tulipokuwa katika kujiandaa ghafla nikaona Kondoo na mbuzi mbele yetu ..basi watu wakaanza kwenda kwenye Kondoo na wengine kwenye mbuzi..
Bwana alipomaliza kuwabagua .akaenda tena kwenye kondoo ndicho kilicho nishangaza AKAANZA TENA KUWABAGUA HAO KONDOO TENA. alikuwa ananyosha kidole mkono wa kulia wanakuja kwake.. Lakini walikuwa kama wanataka kugombaniana kwenda kwa Bwana. Kati ya lile kundi walitoka watu wachache sana wa kwenda na Bwana. Sasa baada ya kuwachagua Bwana akaenda kama kwenye kitu cha usafiri hivi.(sikukifahamu ) na alipofika akaingia kwanza na sisi tukafuata nyuma lakini kabla ya kuanza kuingia akafika yule aliye omba ruhusa kule mwanzo afuate kitu sehemu akasema nae anasitahili awe na BWANA lakini Bwana hakumkubalia .. Yule ndugu alilia sana akisema nae anastahili kuingia kwenye ule usafiri.
Na nilipokuwa nawaangalia ndugu niliokuwa nao sikumwona hata mmoja ninaye fahamiana nae.( hata mama yangu sikumwona hata baba ,wadogo zangu,hata ndugu na dada zikumwona hata mmoja) .ndio nikaaanza kusikitika nikitaka kulia ghafla ikaja sauti ikiniambia kwamba (nilikuwa kama nafikiria ikisema HAKITAINGIA KILICHO KINYONGE .na tena ikasema kwamba WALIO CHAGULIWA KABLA YA KUWEKWA MISINGI YA ULIMWENGU.).
Ndipo nikasikia Bwana akisema akimwita ndugu fulani..nilisika akisema PETRO KUNA CHAKULA .NIKAMWONA BWANA KAMA ANAANDAA CHAKULA HIVI. (Lakini cha kushangaza haya yote yalikuwa yakifanyika chini duniani) Baada ya hapo nikaona Mwanga mkali mbinguni. Hapohapo nikaamka . Nini maana yake ya hii njozi MUNGU wa mbinguni awafunulie maana yake. Shalom.
Ni wazi kuwa Bwana amekuonyesha maono ya siku za mwisho..Na ndoto hiyo tutaichapisha ili na wengine pia wanufaike kwasababu ujumbe huo haukuhusu wewe mwenyewe bali pia unalihusu kanisa la Kristo kwa ujumla, ambao ni sisi sote humo humo kwa ujumla. Kwanza kuwa upande wako unapaswa uamini kuwa bibi-arusi wa Kristo ni tofauti na Kanisa la Kristo kwa ujumla, mke ni tofauti na suria japo wote wanaweza kuwa ni milki ya Bwana arusi .Maana yake ni kuwa wanaoitwa wakristo ni wengi lakini bibi-arusi wa Kristo ni wachache sana, na ndio hao peke yao watakaokwenda kwenye unyakuo, na kutokana na uchache wao dunia haitajua kitu kitakachokuwa kinaendelea.,
Tofauti na watu wengi wanavyodhani kuwa unyakuo ukifika duniani kote kutakotekea machafuko ya kila namna, kila mtu atajua, ajali zitatokea mabarabarani, mamilioni ya watu watapotea, kana kwamba njia ya mbinguni ni njia nyepesi kuiingia kama shetani anavyowadanganya watu, biblia inasema kule hakitaingia kilicho kinyonge, na kama ingekuwa wengi Bwana asingesema Kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, Embu kaa chini ufikirie siku za Nuhu walipona watu wangapi kama sio watu nane(8) tu kati ya mabilioni ya watu waliokuwa ulimwenguni?, Bwana asingesema tena kuja kwake kutafanana na kama zilivyokuwa siku za Lutu, siku zile walipona watu watatu (3) tu kati ya malaki ya watu waliokuwa katika miji ile…Ukisoma tena mahali pengine alisema “mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.(Mathayo 7:14)”..Yote hayo yanathibitisha kuwa mbinguni sio kurahisi kama watu wanavyokufikiri au wanavyofundishwa.. Unyakuo hautakuwa kwa mtu yeyote ambayo hajaonyesha nia ya kuuingia, sio kusema tu nimeokoka basi! Na kuendelea kuishi mtu anavyojisikia.
Na ndio maana hapo kwenye ndoto umeona kumbe hata katikati ya kondoo bado kulikuwa na mchujo..Hiyo inalingana na maandiko kabisa kama tukitazama mfano wa wale wanawali 10, (Katika Mathayo 25) ambao wote walikuwa ni wanawali (mabikira) safi, wote walikuwa wanamsubiria Bwana wao, isipokuwa katikati yao wengine walikuwa wenye busara na wengine wapumbavu. Wale wenye busara walichukua taa zao pamoja na mafuta ya ziada, lakini wale wapumbavu hawakubeba mafuta ya ziada katika vyombo vyao, na wakati ambao Bwana wao sasa anakuja ili awachukue taa zao zikawa zinaanza kuzima , Hivyo wale wapumbavu wakawaomba wenzao wawapunguzie kidogo, lakini wale wakasema hapana tukiwapa hayawezi kututosha sisi pamoja na nyie ni heri mshike njia mkanunue ya kwenu, na walipokwenda kununua, wakati wanarudi wakakuta tayari mlango umeshafungwa..Bwana akawaambia Amin, nawaambia, siwajui ninyi.
Unaona? Siku hizi ni siku za mwisho, na inasikitisha kuwa idadi kubwa ya watu wanaojiita ni wakristo sio wakristo kweli kweli, wanaitwa hivyo kwasababu tu wamezaliwa katika familia za kikristo, lakini ukiangalia mienendo yao, tabia zao, uvaaji wao, mazungumzo yao, yapo mbali kabisa na Ukristo, yaani ni wakristo-jina.
sasa hao ni ndio wale mbuzi uliowaona wakitengwa mbali na wale kondoo…Kadhalika wapo ambao kweli walianza vizuri na Bwana walisimama imara lakini ilifika wakati wakaanza kupoa mguu mmoja ukawa nje, mwingine ndani, mwanzoni macho yao yalikuwa yakielekea mbinguni, wamejitenga mbali na dhambi, wamethibitika katika imani lakini ikafikia wakati wakaanza kupoa mfano wa wale wanawali wapumbavu ambao hawakuwa na mafuta ya ziada katika taa zao. Na mafuta ya ziada ni UHAI WA ROHO WA MUNGU NDANI YA MTU. Sasa wakaanza kumzimisha Roho wa Mungu ndani yao, huko nyuma walianza vizuri lakini kidogo kidogo, wakaanza kupoa, mambo ya ulimwengu huu yakaanza kuwasonga, lakini ukiwatazama huwezi kujua kuwa wanamizigo ya kando inayowavuta, ibadani wanahudhuria, watavaa mavazi ya kujisitiri, hata katika maombi utawakuta, wanafanana kabisa na wale wakristo waaminifu waliosimama imara mbele za Mungu kwa uaminifu wote isipokuwa wao ni vuguvugu tu, sasa hao ndio wale kondoo uliowaona wakichambuliwa katikati ya kondoo…Walipaswa waende na wale wengine lakini kwa upumbavu wao wamebaki..
Ndugu hatupaswi kupoa kwa namna yoyote, hizi ni nyakati za mwisho, kanisa hili tunaloishi, ndilo kanisa la mwisho lijulikanalo kama Laodikia, Ndio lile la mwisho kati ya yale 7 yazungumziwayo katika kitabu cha Ufunuo 2&3, Israeli imeshakuwa taifa huru tena, Ni nini tunachokisubiria sasa kama sio UNYAKUO.
Na Bwana anasema Kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku za kuja kwake mwana wa Adamu,.Ikiwa utautazama upepo wa ulimwengu na kujifariji kwa mambo maovu yanayoendelea, ukidhani kuwa Bwana anatumia ile kauli ya “wengi wape”. Utajikuta unaingia katika gharika ya dhiki kuu, wakati wengi wapo mbinguni kwenye karamu ya mwanakondoo. Ndugu Unyakuo hautakuwa wa wazi kama watu wanavyodhani, unyakuo utakuwa ni SIRI, Na watakaofahamu ni wale wanawali werevu, wachache sana. Lakini dunia nzima itakuwa buzy wakati huo kumfurahia mpinga-Kristo na utawala wake.
Uamuzi ni wako ndugu unayesoma ujumbe huu, Kristo anarudi, na wala hatakawia, atakusanya ngano ghalani mwake na magugu atayatupa katika moto usiozimika…Tubu dhambi sasa, ukabatizwe, na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, kwasababu hatuna wakati mwingi katika kizazi hichi.
Ubarikiwe.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU
Luka 18:1 Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.
2 Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu.
3 Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu.
4 Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu,
5 lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima.
6 Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu.
7 Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao?.
8 Nawaambia, atawapatia haki upesi;
Shalom! Mwana/binti wa Mungu, karibu tuyachunguze maandiko, natumaini leo utajifunza jambo jipya litakalotusaidia katika maisha yako ya maombi..Embu jaribu kufikiria mfano huu watoto wawili mapacha wamemfuata baba yao tajiri kwa faragha na kumwomba awapatie kitu..mmoja kamwambia baba nimeona suruali nzuri dukani naomba uninunulie, na mwingine akasema baba nimeona ndege kubwa inapita angani, naomba uninunulie na mimi niwe na ya kwangu niendeshe..We unadhani maombi ya nani yatakuwa ya kwanza kujibiwa kwa haraka zaidi ya mwingine?..Ni wazi kuwa aliyeomba nguo inawezaka isipite hata siku awe ameshatimiziwa haja yake..Lakini huyo mwingine japo aliomba na mwenzake katika muda mmoja, japo walisikiwa wote katika muda mmoja, japo baba yao aliwahidi wote kuwapa walivyoviomba, lakini majibu ya huyu wa pili, yanaweza yasije kwa wakati alioutarajia, inaweza kumgharimu mambo mengi sana, ikiwemo muda, na maisha.
Na hiyo ni kwasababu gani?. Ni kwasababu jambo aliloliomba lina uzito mkubwa zaidi kuliko la Yule mwingine. Sasa japo baba yake alikuwa anao uwezo wa kumnunulia ndege hata wiki ile ile, lakini alijua kuwa kwa utoto wake hawezi bado kuendesha ndege, hana maarifa ya kutosha kwa alichokiomba, ni sharti kwanza aende shule, akasome masomo magumu ya sayansi, na Jeografia, kisha akajaribiwe katika vituo vingi vya ndege ndogo, na ndio baadaye sana pengine hata baada ya miaka 20 baada ya kufudhu madarasa hayo ndipo baba yake amnunulie ndege yake mwenyewe, aliyomwomba. Hivyo jambo atakalohakikisha baba kwa wakati huo ni kumwezesha kwa kumpeleka katika shule zenye mafunzo hayo, na kumkazania awe chini ya waalimu wazuri, na kusoma vitabu vingi, n.k. ili aweze kufikia malengo yake.
Vivyo hivyo na sisi, Bwana YESU alituambia imetupasa tumwombe Mungu sikuzote wala tusikate tamaa..Ukiona hujapata majibu ya maombi yako leo, haimaanishi kuwa Mungu hajayasikia, au Mungu anapenda kukuona una msumbua sumbua, kila siku kumpigia magoti hapana, jua kuwa majibu ya maombi yanatofautiana kulingana na hitaji lililopelekwa kwa Mungu.
Mungu huwa anamakusudi yake kufanya hivyo, na ndio wakati mwingine utaona unamwomba Mungu akufanyie kitu Fulani, utashangaa hata hujamaliza kuomba jambo hilo lilishatendeka zamani, na wakati huo huo pengine umekuwa ukimwomba Mungu hitaji fulani kwa muda mrefu lakini bado hujaona matokeo yoyote..Fahamu kuwa hilo uliloliomba lina uzito mkubwa mbele za Mungu kuliko lile la kwanza, na hivyo kabla hujalipokea linahitaji maandalizi kwanza.
Pengine wewe ni mgonjwa, na umeshamwomba Bwana kwa muda sasa pengine miaka akuponye ugonjwa wako lakini huoni dalili yoyote ya huo ugonjwa kuondoka, na wakati huo huo ukitazama unaona wengine wanakuja na matatizo makubwa hata zaidi ya ulionanayo na wanapokea miujiza yao saa ile ile, na wewe unajiuliza mimi nina makosa gani?..
Ndugu jambo hilo lisikufanye kujiona kuwa Mungu hakuoni, au anapenda uendelee kuteseka. Fahamu kuwa wote wawili alishawasikia wakati mmoja mlipo mwomba, na wote wawili alishaanza kuwajibu maombi yetu tangu wakati ule ule mlipomwomba…Isipokuwa Mungu anajua njia nzuri zaidi ya sisi kutupatia hitaji la ombi letu kuliko sisi tunavyofikiri, Hivyo ukiona hakuna matokeo yoyote leo wala kesho zidi kufurahi kwasababu ombi lako wewe limeonekana kuwa na faida kubwa zaidi mbeleni kuliko lile la mwingine, kwanza kwako mwenyewe, na pia katika ufalme wa Mungu.
Tunasoma kwenye biblia, wakati Fulani Lazaro, aliugua sana, pengine alikuwa na ugonjwa uliokuwa unamsumbua kwa muda mrefu, labda tuseme kwasasa kisukari na wakati huo huo biblia inatuambia alikuwa ni rafiki wa karibu sana na YESU, alitembea na Yesu sehemu nyingi, pamoja naye hata katika mikutano ya uponyaji alikuwa pamoja na Bwana, aliweza kushuhudia jinsi watu wengi walivyokuwa wanaponywa kimiujiza. Lakini yeye alikuwa bado na ugonjwa wake, mpaka ilipofikia wakati hali imekuwa mbaya sana sasa hawezi hata kutoka kitandani mwake,
Hivyo akapeleka watu kwa Bwana aje upesi kumwombea walau atoke kitandani..Lakini Bwana alipopata taarifa zile, hakwenda popote, jiulize ni kwanini Bwana hakuondoka haraka haraka na kwenda Huko kumwangalia rafiki yake kipenzi, badala yake akabaki pale pale siku nyingine mbili..
Tengeneza picha wale watu waliompelekea Yesu taarifa, wakati wanarudi njiani walikuwa wanawaza nini vichwani mwao?, pengine walisema, huyu alikuwa anampenda Lazaro kweli?, au alikuwa anaonyesha unafki tu!, haiwezekani rafiki yake yupo ICU mahutihuti, na yeye yupo buzy na watu wengine hata asiowajua, rafiki yake anaumwa tangu siku nyingi kwanini asimponye yeye kwanza.? Lakini Yesu alisubiri mpaka mauti ilipomkuta..Ndipo sasa akaondoka aende kumtembelea rafiki yake..Tunasoma.
Yohana 11.17 “Basi Yesu alipofika, alimkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne.
18 Na Bethania ilikuwa karibu na Yerusalemu, kadiri ya maili mbili hivi;
19 na watu wengi katika Wayahudi walikuwa wamekuja kwa Martha na Mariamu, ili kuwafariji kwa habari ya ndugu yao.
20 Basi Martha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alikwenda kumlaki; na Mariamu alikuwa akikaa nyumbani.
21 Basi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa.
22 Lakini hata sasa najua ya kuwa yo yote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa.
23 Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka.
24 Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho.
25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;
26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?
27 Akamwambia, Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni.
28 Naye alipokwisha kusema hayo, alikwenda zake; akamwita umbu lake Mariamu faraghani, akisema, Mwalimu yupo anakuita.
29 Naye aliposikia, aliondoka upesi, akamwendea.
30 Na Yesu alikuwa hajafika ndani ya kijiji; lakini alikuwa akalipo pale pale alipomlaki Martha.
31 Basi wale Wayahudi waliokuwapo na Mariamu nyumbani, wakimfariji, walipomwona jinsi alivyoondoka upesi na kutoka, walimfuata; huku wakidhania ya kuwa anakwenda kaburini ili alie huko.
32 Basi Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu, na kumwona, alianguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa.
33 Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake,
34 akasema, Mmemweka wapi?Wakamwambia, Bwana, njoo utazame.
35 Yesu akalia machozi.
36 Basi Wayahudi wakasema, Angalieni jinsi alivyompenda.
37 Bali wengine wao wakasema, Je! Huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife?
38 Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake.
39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne.
40 Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?
41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.
42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.
43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje.
44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake”.
Unaona hapo? Hata baadhi ya makutano waanza kudhihaki wakisema aliweza kuwaponya wengine kwanini alishindwa kumzuia huyu asife?..Lakini habari yote tunaijua, ule muujiza uliotokea pale, baada ya Lazaro kufufuliwa, Israeli yote Ilimtazama Kristo kwa jicho lingine, mpaka watoto wadogo wakawa wanamwimbia mabarabarani wakisema Hosana! na Mafarisayo na Masadukayo kuona vile sasa Israeli yote inakwenda kumgeukia ndipo walipopanga shauri la kumwua sio tu Yesu peke yake bali pia Lazaro kwasababu kwa ushuhuda wake aliwafanya watu wengi wamgeukie Mungu..Embu fikiria Lazaro alikufa na ugonjwa wake usiotibika, lakini sasa anafufuka bila ugonjwa wowote..alikufa pasipo umaarufu, lakini sasa anafufuka na umaarufu mkubwa.
Sasa angalia njia za Mungu zilivyo za ajabu, hata leo hii sikiliza shuhuda ambazo zinawajenga watu kuwafanya hata wakate shauri kumgeukia Mungu, utagundua kuwa shuhuda zao sio zile zilizokuja kwa majibu ya haraka, haraka mwingine atakwambia madaktari walithibitisha kuwa mapigo ya moyo yamesimama kabisa, lakini baadaye akaja kuamka, na kuwa mzima, n.k.
Hivyo ndugu Bwana anaposema imetupasa kumwomba Mungu bila kukata tamaa, haimaanishi kuwa Mungu anatupuuzia kama Yule kadhi dhalimu alivyokuwa anafanya hapana, Bali ni kwamba ametusikia na hivyo anatuandalia ushuhuda ulio bora zaidi kwetu sisi na kwa ajili ya ufalme wake. Unachopaswa kufanya ni kuzidi kumshukuru yeye kila wakati na kukaa katika uwepo wake bila kukata tamaa, haijalishi hali yako itakuwa enaendelea kuwa mbaya kiasi gani, jua tu hakuna dhara lolote litakalokutokea..Endelea tu kukaa uweponi mwake maombi yako yalishasikiwa tangu siku ya kwanza ulipoomba, Hivyo hiyo hali unayopitia sasa ni matokeo ya yale maombi.
Tukiyafahamu hayo, embu turudi sasa kwenye kiini cha somo letu kinachosema.. NI JAMBO GANI BWANA ANATAMANI SANA TUMWOMBE BILA KUKATA TAMAA?..
Kama tulivyoona kila hitaji tunalomwomba Mungu hatupaswi kulikatia tamaa, iwe ni afya, iwe ni mafanikio, au chochote kile chema..Lakini lipo jambo ambalo Mungu analitamani kila mmoja wetu aliombe hilo usiku na mchana, awe na haja ya hilo siku zote za maisha yake..Ni jambo ambalo Mungu analiona ni KUU kuliko hitaji lolote tunaloweza kumwomba Mungu, ni jambo ambalo mtu akilipata basi ni sawa na Yule mtoto aliyemwomba baba yake ndege zaidi ya aliyemwomba nguo.
Jambo hilo Yesu alilifunua katika maombi maneno yanayofanana na yale yale tuliyosoma hapo juu..tusome:
Luka 10: 5 Akawaambia, Ni nani kwenu aliye na rafiki, akamwendea usiku wa manane, na kumwambia, Rafiki yangu, nikopeshe mikate mitatu,
6 kwa sababu rafiki yangu amefika kwangu, atoka safarini, nami sina kitu cha kuweka mbele yake;
7 na yule wa ndani amjibu akisema, Usinitaabishe; mlango umekwisha fungwa, nasi tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kuondoka nikupe?
8 Nawaambia ya kwamba, ijapokuwa haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile asivyoacha kumwomba, ataondoka na kumpa kadiri ya haja yake.
9 Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.
10 Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
11 Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki, badala ya samaki atampa nyoka?
12 Au akimwomba yai, atampa nge?
13 Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni HATAZIDI SANA KUWAPA ROHO MTAKATIFU HAO WAMWOMBAO?.
Unaona hapo? HATAZIDI SANA KUWAPA ROHO MTAKATIFU HAO WAMWOMBAO?.Kwanini hakusema MALI, au AFYA, bali Roho Mtakatifu?..Ndugu kumbuka hii dunia isingekuwa hivi ilivyo kama Roho wa Mungu asingetua juu yake na kufanya uumbaji upya..Hata mtu yeyote anayesema amemwamini Yesu, hakumwamini hivi hivi kama hakuvutwa na Roho wa Mungu kwake (Yohana 6:44).. Hata leo hii anayesema amesimama, au anamtumikia Mungu, hafanyi hayo yote kama sio Roho wa Mungu amekufanya uwe hivyo. Roho wa Mungu ndio kila kitu kwenye maisha yetu..Ndio muhuri wa Mungu (waefeso 4:30), na ndio maana biblia inasema wale wote wasio na Roho wa Mungu hao sio wake (Warumi 8:9)..haijalishi utakuwa mwema kiasi gani…
Roho Mtakatifu ni karama ya bure kabisa, mtu anampokea pale tu anapoitii sauti yake na kumkaribisha ndani yake..Hii inakuja pale mtu anapokusudia kabisa kwa weupe wa moyo wake kutoka moyoni KUTUBU dhambi zake na kuacha maisha yake ya kale, kisha akaenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zake kulingana na (Matendo 2:38). Basi kuanzia hapo mtu wa namna hiyo anakuwa ametiwa muhuri na Mungu kwa Roho wake mtakatifu..Lakini hiyo peke yake haitoshi,.Kumwamini tu, bila ya kumtamani ROHO MTAKATIFU katika maisha yako, hutafika mahali popote…Wengi wameishia hapo na ndio mwisho wa siku Roho Mtakatifu amezimika ndani yao.
Pindi tu unapompokea BWANA kuanzia huo wakati na kuendelea ni jukumu lako kumtamani Roho Mtakatifu awe pamoja nawe. Na ndio hapo linakuja hilo ombi kuu la Bwana, Akupe Roho mtakatifu, au kwa lugha rahisi tunaweza kusema AKUJAZE Roho Mtakatifu…Ulikuwa katika kipimo cha chini lakini sasa unataka AKUJAZE mpaka kwenye kipimo cha juu kabisa. Kumbuka Roho Mtakatifu sio kunena kwa lugha, ni jambo lingine, Na kwa jinsi utakavyozidi kuendelea kuomba bila kukata tamaa, basi ujue ndivyo unavyojijengea daraja zuri la Mungu kuyatawala maisha yako yote, na kuruhusu madarasa Fulani upitie kwa kukuandaa kwa kazi yake teule ya utumishi mwema..Kama tunavyoona ilivyokuwa kwa Yohana mbatizaji, ilivyokuwa kwa Bwana Yesu na ilivyokuwa kwa mitume wake..Wote walipokea Ujazo wa Roho Mtakatifu,lakini hiyo ilikuja kwa jinsi walivyotamani kipawa hicho tunaona baadaye walikuja kuvipokea, Roho mtakatifu aliposhuka juu yao na kuwatia mafuta ya utumishi, ndipo hapo Mungu alitembea nao kwa namna ya kipekee sana.
Hivyo ni maombi yangu, mimi na wewe kila siku na sisi tusikate tamaa kuomba Roho Mtakatifu..Leo unaweza usione matokeo yoyote, lakini jua tu ombi lako limesikiwa, na kama hujakata tamaa juu ya hilo unaendelea kulishikilia basi jua maisha unayopitia sasa ni maandalizi ya kazi ya huyo Roho atakayekuja juu yako baadaye.
Waefeso 5:17 “Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.
18 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; BALI MJAZWE ROHO;”
Ubarikiwe sana.
“Share” ujumbe huu kwa wengine.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
RUDIA, TENA NA TENA KUMWOMBA MUNGU USIKATE TAMAA.
USIISHIE KUTAZAMA JUU, ENDELEA MBELE.
Wafilipi 1:29 “Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake; ”.
Ni mstari ambao wengi wetu hatuupendi, wala hautufurahishi… na mwingine ni
1 Wakorintho 14:34 unaosema “Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.
35 Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.”
Pamoja na..
1 Timotheo 2:11 “Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.
12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.
13 Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye.”,
Mistari hii kwa mtu ambaye hasomi kabisa biblia akisiisikia kwa mara ya kwanza anaweza akapinga kama vile haipo katika Biblia Takatifu. Ni mistari inayochokiwa na wengi, na huwa haihubiriwi mara kwa mara. Na hata ikihubiriwa inapindishwa pindishwa ikipakwa pakwa rangi, kuipotezea maana halisi ya mistari hiyo.
Lakini Mistari yote hii inapatikana katika Agano jipya na imevuviwa na Roho Mtakatifu, na kuthibitishwa na yeye mwenyewe kwa ajili ya afya ya Roho zetu, na kwa faida zetu. Ndio maana Roho Mtakatifu akaruhusu iwepo katika Biblia Takatifu katika vizazi vyote..Na kama Bwana Yesu anavyosema “Mbingu na Nchi zitapita lakini Maneno yangu hayatapita kamwe”…ndivyo maneno hayo yatakavyodumu siku zote. Na pia inasema maneno ya Mungu yamehakikiwa na ni safi kama fedha iliyosafishwa mara saba (Zaburi 12:6).
Leo kwa Neema za Bwana hatutajifunza hiyo Mistari miwili ya Mwisho bali tutajifunza huo wa Kwanza, unaozungumzia HABARI YA KUTESWA KWA AJILI YA KRISTO.
Ni muhimu kufahamu, chochote Mungu anachotaka tukifanye ni kwa faida yetu, ni kwasababu anatupenda na anataka tupate faida nyingi kwa kupitia hicho…Kwahiyo chochote kile kiwe kibaya au kizuri kitokacho kwa Mungu kinacholetwa juu yetu sisi tuliomwamini yeye, ni kwa ajili ya kutujenga sisi hana lengo la kututesa hata kidogo kwasababu yeye mwenyewe amesema hapendi kuwatesa wanadamu (Maombolezo 3:33.. Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha).
Hata mzazi mwenye upendo wa kweli kwa mwanawe, chochote kile akiletacho juu ya mtoto wake kiwe kizuri au kibaya..lengo lake sio kumharibu bali kumfundisha, na wala lengo lake sio kumhuzinisha, bali kumjenga..ndivyo ilivyo kwa Baba yetu wa mbinguni.
Hivyo Kwanini Bwana anataka tuendelee mbele hatua ya kuteswa kwa ajili yake?..ina maana hiyo ya kumwamini tu haitoshi?!!.. Jibu ni kwamba haitoshi ndio maana anataka tuendelee mbele.
Lengo la kufanya vile ni ili ATUFANANISHE NA YESU KRISTO, MWANA WAKE. Ili kwamba turithi kama Kristo alivyorithi, kwasababu yeye ili aweze kuzirithi mbingu za mbingu, kikombe cha mateso hakukiepuka…ingawa kuna wakati aliomba “Baba ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke”…Lakini Baba hakumwepushia lengo lilikuwa sio kumtesa bali ni kumpa sababu ya kupata zile mbingu za mbingu alizomwahidia kumpa sababu ya yeye kwanini awe juu ya malaika wote.
Na kama alimpitisha mwanawe mpendwa Yesu Kristo katika mateso yale, pia atawapitisha wanawe wengine wote katika njia ile ile, ili kwamba na sisi nasi tuwe tumestahili kuzirithi zile ahadi kubwa namna ile Yesu alizozirithi. Na yeye ni mwaminifu kama alivyokuwa na Bwana Yesu ndivyo atakavyokuwa na sisi wakati wa mateso..na atatupa ushindi kama alivyompa BWANA Yesu.
Ufunuo 3:21 “Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.”
Unaona nafasi ya kuketi na Bwana katika kiti cha enzi, ni lazima tushinde kama yeye alivyoshinda.
Yeye alipigwa pasipo sababu, na sisi hatuna budi kupitia wakati mwingine kupigwa pasipo sababu, yeye alichukiwa bure biblia inasema hivyo (Yohana 15:24-25), na sisi hatuna budi wakati mwingine kupitia kuchukiwa Bure kwasababu ya Imani yetu au mienendo yetu inayompendeza Mungu, yeye aliishinda hasira pale alipotemewa mate bila kosa lolote, na sisi hatuna budi kushinda hasira na ghadhabu tutakapozalilishwa pasipo sababu yoyote.
Yeye walimsimamishia mashahidi wa uongo lakini alishinda kwa kujinyenyekeza kama kondoo apelekwaye machinjoni wala hakupaza sauti yake kushindana na mtu, Isaya 53: 7 “Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, HAKUFUNUA KINYWA CHAKE”. Na sisi tunatakiwa tushinde vile vile, kwa kufumba vinywa vyetu tunapoonewa, na kusingiziwa mambo mabaya na kusimamishiwa mashahidi wa uongo.
Yeye alishinda kwa kuwaombea msamaha wale waliomsulibisha katika hatua yake ya mwisho ya uhai wake, na sisi tunapaswa tushinde kwa kuwasamehe wale wote wanaotutesa au kutuonea, au kutuumiza hata katika hatua ya mwisho ya uhai wetu.
Hiyo ndio maana ya kuteswa kwa ajili ya Kristo na kila mkristo wa kweli lazima apitie, kwasababu hatuwezi kusema tunafanana na Kristo, wakati historia za maisha yetu hazifanani na historia ya maisha yake. Ndio maana Bwana Yesu alituambia… “mtu yoyote akitaka kumfuata, sharti kwanza ajikane nafsi yake na ajitwike msalaba wake kisha amfuate”…Na zaidi ya yote apige gharama kwanza kabla ya kumfuata…Kwasababu njia ya Kristo ni njia ya Msalaba, ambayo mwisho wake ni KALVARI. Lakini mwisho wake una matunda makubwa sana.
Na tukishinda kama yeye basi tutarithi kama yeye alivyorithi…kama Mtume Paulo anavyosema mahali fulani..
2 Timotheo 2.9 “Nami katika hiyo nimeteswa hata kufungwa kama mtenda mabaya; lakini neno la Mungu halifungwi.
10 Kwa ajili ya hilo nastahimili mambo yote, kwa ajili ya wateule, ili wao nao waupate wokovu ule ulio katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele.
11 Ni neno la kuaminiwa. Kwa maana, Kama tukifa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia;
12 Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi;”
Lakini pia biblia imetuonya tusiteswe kwaajili ya matendo mabaya..hatupaswi kuteswa kwajili ni wezi, au watukanaji, au wasengenyaji, au wakorofi au waasherati, au wala rushwa au mafisadi, au wachokozi… na kusema tunateswa kwa ajili ya Kristo, Hapo tutakuwa hatuteswi kwa ajili ya Kristo bali kwa ajili ya shetani.
1 Petro 4:12 “Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho.
13 Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe.
14 Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia.
15 Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine.
16 Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.
17 Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje?
18 Na mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi?
19 Basi wao wateswao kwa mapenzi ya Mungu na wamwekee amana roho zao, katika kutenda mema, kama kwa Muumba mwaminifu”.
Bwana atujalie sote, kuyaelewa maandiko na kuyatendea kazi. Tutakapokutana na hayo basi tusizimie mioyo tukidhani kuwa Mungu hatupendi au tuna bahati mbaya..Kwani tukumbuke kuwa hata watakatifu waliotutangulia walipitia mambo kama hayo hayo, na hata sasa wengine wanaendelea kupitia.
Bwana akubariki sana.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA JIKANE MWENYEWE?(MATHAYO 6:24)
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA
SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.