Kiwango cha uelewa kuhusu wokovu au Mungu waliokuwa nacho Kiwango cha uelewa, hutupaswi tuwe nacho sisi kwa wakati huu, tunapaswa tuende zaidi ya pale, Hata mambo ya kidunia yanatufundisha, elimu ya kidato cha 4 aliyokuwa nayo mtu wa mwaka 1960, Si sawa na elimu ya kidato cha 4 aliyonayo mtu wa sasa hivi.
Wakati ule, elimu hiyo ilimtosha mtu kupata kazi hata ngazi za juu katika mashirika makubwa, lakini kwa sasahivi elimu hiyo haina thamani yoyote japokuwa ni elimu ile ile.
Ndivyo ilivyo hata katika ukristo, wakati mwingine unajiuliza ni kwanini hauisikii nguvu ya wokovu ndani yako, japokuwa utasema umeokoka, na umefuata vigezo vyote vya kuokoka kama tu watu wa kale walivyofanya, lakini bado huoni ndani yako moto kama waliokuwa nao wale, Ni kwasababu tunataka tuishi kama watu wa zamani, kama kipindi cha mitume, kama kipindi cha Martin Luther, kwamba ukimkiri Yesu kwa kinywa ya kuwa ni Bwana na tena ukaamini kwamba alikufa akafufuka utaokoka (Warumi 10:9)..Hilo tu basi!..
Kwa kudhani kwamba hilo tu linatosha kutufanya tuimalize hii safari salama. Ndugu hilo lilitosha kwa wakati wao, ambao kwanza hawakupata neema ya kuwa na mikusanyiko ya vitabu vyote vya maandiko kama tulivyonavyo sisi, Au kama walikuwa navyo basi hawakuruhusiwa kuvisoma (Fuatilia historia utaona), hiyo ni moja, pili, shetani alikuwa hafanyi kazi kwa nguvu kama anavyofanya sasa hivi.
Ikiwa hutaki kuongeza maarifa yako kuhusu Mungu katika nyakati hizi, na umeng’ang’ana tu kusema mimi nilishaokoka basi, nataka nikuambie kuwa ukristo wa namna hiyo safari hii hautakufikisha popote. Hilo pekee halitoshi kukufikisha popote, wala kutufikisha popote!.
Hili ndio kanisa pekee linaloonekana lina makundi mawili ya wakristo (yaani Wanawali werevu na Wanawali wapumbavu. Math.25). Ikiwa na maana kutakuwa na wakristo wenye bidii ya kupata maarifa, na wakristo ambao hawatakuwa na ujuzi wowote mioyoni mwao, na biblia inaonyesha wale werevu tu ndio watakaoenda kwenye unyakuo. Jambo hilo halikuwahi kuonekana katika vipindi vyote vya kanisa huko nyuma..
Na katika wakati ambao ni mgumu kuliko wakati wote uliowahi kutokea katika historia ya dunia basi ni huu!, kwasababu hili ndio kanisa la mwisho lijulikanalo kama Laodikia, “ndio tonge la mwisho linalokomba mboga yote” na shetani analijua hilo, huu ndio wakati wake wa kufanya kazi kwa nguvu zaidi ili kuwaangusha wengi, Hivyo wewe na mimi tunaojiita mkristo tusipojua ni nini tunapaswa tuwe nacho kwa majira haya, ndugu basi tumekwisha!.
Ukisoma kitabu cha Ufunuo, utaona wapo wale wenye uhai 4, wanaosimama mbele ya kiti enzi cha Mungu, mmoja akiwa na uso kama wa Simba, mwingine wa Ndama, mwingine kama wa mwanadamu na Mwingine kama wa Tai (Ufu 4:7).
Sasa hizo nyuso zao na mionekanayo yao sio urembo tu, hapana bali zilikuwa zinafunua nguvu za Roho Mtakatifu katika nyakati tofauti tofauti za kanisa..Sasa mwenye uhai wa kwanza hadi yule wa Tatu, walifanya kazi kwa vipindi vya makanisa 6 ya mwanzo, kwa urefu wa Habari hiyo fungua hapa >> UFUNUO: Mlango wa 4
Lakini yule mwenye uhai wa 4 ambaye ndiye mwenye uso wa Tai, alianza kutenda kazi katika kanisa la 7 na la mwisho lijulikanalo kama Laodikia, ambalo ndio tunaishi mimi na wewe, na kanisa hili lilianza mwaka 1906, (hilo linajulikana na wanazuoni wote na wana theolojia wote duniani, sio jambo la kutengeneza)..
Sasa kama tulivyosema, Sio kwamba huyo mwenye uhai wa 4 ndio anayetenda kazi hapana, bali Ni Roho ya Mungu yenye tabia ya Tai ndio iliyoachiwa kwa kanisa la Mungu tangu huo wakati na kuendelea (Mwaka 1906- Pentekoste ya mwisho ilipoanza)
Hivyo mimi na wewe tunaishi katika Upako huo wa Roho ya Tai.
Sasa ni kwanini iwe ni Tai na sio wale wengine, labda simba, au ndama, au mwanadamu?.
Ni kwasababu kanisa la sasa hivi linahitaji wakristo wenye jicho la TAI,..Kumbuka tai ni ndege anayeona tokea mbali kuliko kiumbe kingine chotechote duniani, Tai anaona kwa umbali ambao wewe mwenyewe huwezi kumwona angani. Anaweza kuona vitu vya mbali sana, vidogo sana,..tofauti na ndege wengine kama kuku, kuku yeye anaona hapa chini tu, lakini kile kinachotokea maili mbili mbele hawezi kukiona.
Hivyo jicho hilo la Tai ni jicho la kinabii, Kwamba wakristo wote waliopo duniani leo hii Roho hii inapaswa iwepo juu yao, ili wawezi kuushinda ulimwengu huu wa sasa, vinginevyo watakachukuliwa tu maji..Na ndio maana kusema tu Umeokoka, hilo halitoshi kwa majira haya..Ni lazima uwe na jicho la kinabii.. Na jicho la kinabii sio kuona maono usiku, wala wachawi, wala kutabiri…Bali ni utashi wa kujua wakati tuliopo, na kuona mambo yajayo, ambayo bado hayajafika yatakayoupata ulimwengu, na hivyo kuchukua tahadhari mapema.
Mungu alijua kabisa wakati huu udanganyifu utakuwa mkubwa duniani, na watu watamsahau Mungu kupindukia kama alivyosema watu watakuwa wa kupenda anasa kuliko kumpenda Mungu (2Timotheo 3:4), alijua kabisa kutatokea mapinduzi makubwa ya kiteknolojia, alijua kabisa kutakuwa na mwingiliano mkubwa wa watu na wa-kiutamaduni katikati ya mataifa, alijua kabisa dini nyingi zitaongezeka duniani, kiasi kwamba mpaka sasa duniani zipo dini Zaidi ya 4,300, ukristo ni mmojawapo na madhehebu yasiyoweza kuhesabika.
Alijua kabisa lile wimbi kubwa la makristo wa uongo, na manabii wa uongo, alilolitabiri zamani halitatokea wakati mwingine wowote, bali katika wakati wetu huu wa siku za mwisho.
Alijua kabisa wale watu wa kudhahaki, wale wanatakaosema yupo wapi huyo Yesu mnayemngojea mbona harudi, watazaliwa katika wakati wetu, (2Petro 3:3-4) mambo ambayo hapo nyuma hayakuwepo.
Alijua kabisa ile siri ya kuasi itakuwa inatenda kazi kwa nguvu, katikati ya ukristo, kiasi kwamba watu wengi watazombwa na nguvu hiyo..
Na ndio maana katika kizazi hichi chetu aliiachilia Roho ya Tai, Ili kukabiliana na udanganyifu uliopo sasa hivi. Na ni lazima kila mtu awe nayo, kwasababu ni kwaajili yetu.
Sasa dalili za mtu ambaye hana Roho hiyo ni ipi?
Ukiona hupendi kuongeza maarifa na kutaka kujifunza kitabu cha Ufunuo kinachozungumzia mambo yajayo, na vitabu vingine vya manabii, basi ujue Roho huyo bado hajaanza kutenda kazi ndani yako. Watu wengi tunadhani Mungu hana agenda yake ya kutimiza mambo, tunadhani tupo tu tunangojea siku Fulani ya unyakuo ifike halafu tuondoke kana kwamba hapa katikati Mungu hafanyi kazi yoyote.
Kama ulikuwa hufahamu Bwana Yesu alisema, kabla ya kurudi kwake atamtuma Eliya, ili kuigeuza mioyo ya wana iwaelekee baba zako, kwa kanisa letu Mungu alishaanza kutimiza hiyo agenda, na bado ataendelea kuitimiza,..Zipo ngurumo saba, ambazo zimezungumziwa katika Ufunuo 10:4. Ambazo hazijaandikwa kabisa katika maandiko, na hizo ni sharti zije zifunuliwe katika siku za mwisho kabla Kristo hajarudi, hapo ndipo Mungu atakapoitimiza siri yake yote (Ufu 10:7), kwasasa hivi siri ya Mungu bado haijatimizwa yote.
Hatujui sauti za ngurumo hizo 7 zitakuwa ni nini, Lakini siku zitakaposemwa duniani, wale wanawali wapumbavu hawataelewa chochote. Hata leo hii Mungu anasema, lakini usipokuwa na jicho la Tai huwezi kuona..Huwezi kuona hizi ni siku zenyewe, kwasababu macho yako yanaona tu ya ulimwengu huu, wapo ambao hata Ugonjwa wa Corona wanaona kama ni ugonjwa wa kibailojia tu, umetengenezwa na watu!. Huwajui kuwa hizi ndizo tauni Yesu alizozizungumzia zitatokea siku za mwisho (Luka 21:11).
Yapo mambo mengi, ya kujifunza wakati huu, Hivyo usiridhike na dini yako tu, au dhehebu lako tu, Chukua biblia yako, itafakari, na huko huko Roho Mtakatifu atakufundisha siri zake nyingi, na mipango yake, ukiwa msomaji wa biblia mzuri, itakuwa ni rahisi kuzijua hila za ibilisi kwa haraka, na kutokupotezwa na udanganyifu wa shetani wa siku hizi za mwisho.
Na zaidi sana kumwomba Mungu azidi kutuongezea jicho hilo la Tai ndani yetu kila siku. Kwasababu pasipo kuwa nalo hilo, hakuna Unyakuo.
Bwana akubariki sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
KWANINI UKATE TAMAA?
Ulokole ni nini? Na kwanini wakristo waliookoka wanaitwa walokole?
UTAWALA WA MIAKA 1000.
FAIDA ZA MAOMBI.
SHUKURU KWA KILA JAMBO.
HAPO NDIPO WATU WALIPOANZA KULIITIA JINA LA BWANA.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Jina la Bwana Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze Biblia. Huu ni mwendelezo wa vitabu vya biblia ambao tumeshatazama vitabu 17 vya mwanzo..Ikiwemo kitabu cha Ezra na Yeremia. Hivyo leo kwa Neema za Bwana tutaendelea na kitabu kimoja mbele ambacho ni kitabu cha Ezekieli. Kama hujapitia vitabu vya nyuma nakushauri ukavipitia kwanza wewe binafsi taratibu na kwa utulivu, ili hapa iwe ni sehemu ya kujiongezea vitu vichache juu ya vile ambavyo unavifahamu.
Kitabu cha Ezekieli ni kitabu cha 26 katika orodha ya vitabu vya Biblia na kina sura 48. Mwandishi wa kitabu hichi ni Ezekieli mwenyewe…na tafsiri ya jina Ezekieli ni “Mungu atatia nguvu”. Kitabu hichi kinakadiriwa kuandikwa kati ya mwaka 593-570 KK. Kiliandikwa kwa miaka isiyopungua 20. Na kilianzwa kuandikwa wakati wa lile kundi la pili la wayahudi kupelekwa Babeli.
Kumbuka hatuna za kupelekwa Babeli kwa wana wa Israeli ziligawanyika katika makundi matatu.
Sasa ukisoma vitabu vya nyuma vya Mambo ya nyakati na Wafalme, na kitabu cha Yeremia utaona ni jinsi gani Nabii Yeremia alivyowalilia wana wa Israeli juu ya kuamishwa kwao, lakini hawakusikia mpaka walipotolewa wote kwenye nchi ya ahadi na kupelekwa Babeli.
Sasa wakina Danieli, Shedraka, Meshaki na Abednego walichukuliwa wakiwa vijana wadogo sana katika kundi la kwanza na kutangulia Babeli..Tutakuja kuona Habari zao vizuri katika mfululizo wetu baada ya kitabu hichi. Lakini kipindi kifupi tu baada ya wao kufika Babeli likatolewa kundi lingine la pili ambalo ndilo Ezekieli alikuwepo ndani yake. Wakiwa njiani kuelekea Babeli kijana mdogo Ezekieli alianza kuona maono. Hatuwezi kuyaandika haya maono yote aliyoyaona hapa (unaweza kuyasoma binafsi katika kitabu hicho cha Ezekieli 1 na 2).
Lakini kwa ufupi tu ni kwamba aliona Mbingu zimefunguka kama Nabii Isaya na Mtume Yohana walivyoona, na akaona makerubi na kiti cha enzi cha Mungu.
Ezekieli 1:1“Ikawa katika mwaka wa thelathini, mwezi wa nne, siku ya tano ya mwezi, nilipokuwa pamoja na watu waliohamishwa, karibu na mto Kebari, mbingu zilifunuka, nikaona maono ya Mungu”.
Akiwa katika maono hayo Mungu alimpa “gombo” alile (Ezekieli 2:9).. Na gombo lile lilikuwa limeandikwa nje na ndani. Sasa tafsiri ya gombo hapo sio kitu Fulani mfano wa chakula, hapana bali ni aina Fulani ya vitabu vya kale ambavyo vinaandikwa kwa kuviringishwa. Hivyo ni kitabu ndicho alichopewa akile, na sio chakula..Sasa utauliza alikulaje kulaje kitabu?..Hatujui!..kama kiligeuka na kuwa mkate hilo hatujui..lakini mwisho ni kwamba tunajua alikula kile kitabu alichopewa.
Na kile kitabu kilikuwa kimendikwa maneno nje na ndani.. Na maneno yalioandikwa humo yalikuwa yanahusiana na MAOMBOLEZO, VILIO NA OLE.
Sasa Huduma/ kusudi la Mungu kumwita Ezekieli lilikuwa ni lipi?
Tusome kidogo mistari ifuatayo ndipo tutajua Zaidi..
Ezekieli 3:1 “Akaniambia, Mwanadamu, kula uonacho; kula gombo hili, kisha enenda ukaseme na wana wa Israeli. 2 Basi nikafunua kinywa changu, naye akanilisha lile gombo. 3 Akaniambia, Mwanadamu, lisha tumbo lako, ulijaze tumbo lako kwa hili gombo nikupalo. Ndipo nikalila, nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu, kama utamu wa asali. 4 Akaniambia, Mwanadamu, haya! Waendee wana wa Israeli ukawaambie maneno yangu. 5 Maana wewe hukutumwa kwa watu wa maneno mageni, ama wa lugha ngumu, bali kwa nyumba ya Israeli; 6 si kwa watu wa kabila nyingi wenye maneno mageni, na lugha ngumu, ambao huwezi kufahamu maneno yao. Bila shaka, kama ningekutuma kwa watu hao, wangekusikiliza”
Ezekieli 3:1 “Akaniambia, Mwanadamu, kula uonacho; kula gombo hili, kisha enenda ukaseme na wana wa Israeli.
2 Basi nikafunua kinywa changu, naye akanilisha lile gombo.
3 Akaniambia, Mwanadamu, lisha tumbo lako, ulijaze tumbo lako kwa hili gombo nikupalo. Ndipo nikalila, nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu, kama utamu wa asali.
4 Akaniambia, Mwanadamu, haya! Waendee wana wa Israeli ukawaambie maneno yangu.
5 Maana wewe hukutumwa kwa watu wa maneno mageni, ama wa lugha ngumu, bali kwa nyumba ya Israeli;
6 si kwa watu wa kabila nyingi wenye maneno mageni, na lugha ngumu, ambao huwezi kufahamu maneno yao. Bila shaka, kama ningekutuma kwa watu hao, wangekusikiliza”
Umeona hapo? Ezekieli alitumwa kwa watu wa Israeli…Hususani kwa lile kundi la mwisho..ambalo bado limebaki nyuma, halijafika bado Babeli..Kile kitabu alicholishwa ni lugha ya rohoni inayofunua KULISHWA MANENO YA MUNGU, Na maneno hayo ni Kuwaonya (yaani OLE), kuwaombolezea kwa yatakayowapata wasipotubu, na kuwatabiria vilio vitakavyowakuta kipindi kifupi kama hawatatubu.
Baada tu ya kula hicho kitabu katika maono…Roho ya Mungu ilimshukia kwa nguvu na kuanza kuwatabiria wana wa Israeli yatakayowakuta. Wakati huo Sedekia akiwa mfalme wa waisraeli, alikuwa ni mbishi na mwenye kiburi, hakutaka kuamini kwamba atachukuliwa utumwani kwenda Babeli, Nabii Yeremia alikuwa bado yupo hai kipindi hicho na alikuwa anamwonya aache njia zake mbaya na ajinyenyekeze, lakini hakusikia…Ikiwa bado imesalia miaka michache Mji wote uchomwe moto Ezekieli naye huko anaona maono na maneno kama yale yale ya Yeremia ya kuwaonya juu ya hukumu ile ile. Kwa hiyo huko Israeli yupo Yeremia na huku njiani kuelekea Babeli yupo Ezekieli..Wote wanazungumza kitu kimoja!.
Hivyo kuanzia Sura ya 1 hadi ya 24 ya kitabu cha Ezekieli.. Inaelezea Unabii juu ya kuangamizwa kwa Yerusalemu, kwa lile kundi lililobakia. Na maono hayo yalikuja kutimia vile vile kama alivyosema.
Baada ya Yerusalemu kuteketezwa na hilo kundi la tatu kufikishwa utumwani, Bwana alianza kumpa Ezekieli maono mengine..juu ya mataifa mengine yaliyobaki kama Misri na mengine yaliyo kando kando, kwamba nayo pia yatachukuliwa utumwani kwenda Babeli. Jambo ambalo Nabii Yeremia pia alilitabiri.
Hivyo kuanzia Sura ya 25-32. Bwana anampa Ezekieli maono juu ya kuangamizwa kwa mataifa mengine yaliyosalia, kwani nayo pia yalikuwa yamemwasi Mungu.
Na baada ya mataifa hayo yote kupitia kile yalichokipitia Israeli (yaani yote kuangamizwa na watu wao kupelekwa utumwani Babeli). Bwana akaanza kumpa Ezekieli tena maono mengine ya kuwaonya Wana wa Israeli watubu sana.. kwasababu anawazia kuwafanyia mema mwishoni. Katika Sura ya 33 utaona wito huo Mungu anaowaita wana wa Israeli.
Na mwisho kabisa baada ya wito huo kuanzia Sura ya 34-48. Bwana anampa Ezekieli maono mengine ya mwisho kabisa…Maono ni juu ya kujengwa upya Yerusalemu katika siku za mwisho..Na baadhi ya maono hayo bado hayajatimia mpaka sasa…kwani kuna Hekalu la Tatu la mwisho ambalo limezungumziwa humo kwamba litatengenezwa siku za mwisho bado halijatimia…Ingawa mpaka sasa vifaa vyote vya ujenzi vipo tayari, vinasubiriwa nyakati na majira tu yaliyoamriwa na mbingu…ambapo siku moja isiyokuwa na jina Hekalu litaanza kujengwa kwa haraka sana na kwa kipindi kifupi kutimiza huo unabii wa Ezekieli.
Hivyo huo ndio ufupisho wa kitabu cha Ezekieli ..(katika Sura hizo zote zimejaa, maonyo mengi sana, na tabiri nyingi sana zihusuzo siku za mwisho, na ole nyingi na maombolezo), na ole nyingine zinatuhusu hata sisi!..Ndani yake Bwana aliwaonya manabii wote wa Uongo vikali, na kuwalaani….kwamfano hebu soma ole hii..
Ezekieli 13:1 “Kisha neno la Bwana likanijia, kusema, 2 Mwanadamu, tabiri juu ya manabii wa Israeli wanaotabiri, uwaambie wanaotabiri kwa mioyo yao wenyewe, Lisikieni neno la Bwana; 3 Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao manabii wajinga, wanaoifuata roho yao wenyewe, wala hawakuona neno lo lote!”
Ezekieli 13:1 “Kisha neno la Bwana likanijia, kusema,
2 Mwanadamu, tabiri juu ya manabii wa Israeli wanaotabiri, uwaambie wanaotabiri kwa mioyo yao wenyewe, Lisikieni neno la Bwana;
3 Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao manabii wajinga, wanaoifuata roho yao wenyewe, wala hawakuona neno lo lote!”
Unaona, yapo mafunzo mengi na maonyo, ambayo Roho Mtakatifu anatamani kumfunulia kila mtu atakayekisoma kitabu hiki. (Ndani ya kitabu cha Ezekieli utajifunza ni jinsi gani Mungu hapendi ibada za sanamu, utajifunza ni jinsi gani Mungu hapendezwi na maovu, na kusema kila nafsi itendayo dhambi itakufa! Kasome Eze.18:4,18:20). Pia ndani ya kitabu hichi utajifunza madhara ya kutokuifanya kazi ya Mungu, maana yake ni kwamba Mungu anapokuambia kitu ili ukawaonye watu na wewe hutaki kwenda kuwaonya basi wakifa katika dhambi zao bila wewe kuwaonya, damu yao itakuwa juu yako.
Ezekieli 33:7 “Basi wewe, mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli; basi ulisikie neno hili kinywani mwangu, ukawape maonyo yangu. 8 Nimwambiapo mtu mbaya, Ewe mtu mbaya, hakika utakufa, nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo, aiache njia yake, mtu mbaya huyo atakufa katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. 9 Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi aiache; wala yeye asiiache; atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa roho yako”.
Ezekieli 33:7 “Basi wewe, mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli; basi ulisikie neno hili kinywani mwangu, ukawape maonyo yangu.
8 Nimwambiapo mtu mbaya, Ewe mtu mbaya, hakika utakufa, nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo, aiache njia yake, mtu mbaya huyo atakufa katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.
9 Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi aiache; wala yeye asiiache; atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa roho yako”.
Hivyo sio kufurahia kusikia tu…bali tunaposikia injili au maonyo ya Mungu yanageuka kuwa deni kwetu kwenda kuwaonya wengine. Ndio maana Ezekieli baada ya kula lile gombo, kinywa aliliona litamu lakini tumboni lichungu..
Ndani ya kitabu hichi, utajifunza juu ya vita kubwa ambayo itakuja kupigwana pale Israeli, ambapo mataifa yanayoizunguka nchi ile yataongozwa na nchi ya magogu (Urusi kwa sasa),ili kupigana nao, Vita hiyo Israeli itashinda, pengine mimi na wewe tunaweza kuishuhudia vita hiyo katika kizazi chetu.
Hivyo tenga muda wa kukisoma chote wewe binafsi, usiridhike na haya yaliyoandikwa hapa, na kujitumainisha kwamba tayari umeshakielewa! Huu ni muhtasari tu wa kukupa dira!,..kila kitu kipo kule!..
Biblia haijaeleza kifo cha Ezekieli, lakini ni wazi kuwa alifia huko huko Babeli..Na sehemu kubwa ya maono yake inafanana na maono aliyoyaona Mtume Yohana katika kisiwa cha Patmo..tutakapofika kitabu cha Ufunuo wa Yohana, tutaelewa Zaidi.
Mwisho kabisa…Kumbuka hizi ni siku za mwisho!..tunaishi katika kanisa la Mwisho lijulikanalo kama kanisa la Laodikia…Kanisa la Laodikia sio dhehebu linaloitwa Laodikia, au shirika Fulani la dini hapana!…Bali ni hali ya kanisa ya dunia nzima inavyoonekana mbele za Mungu, kwamba inafananishwa na kanisa la saba kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Ufunuo 3:14. Ni kanisa vuguvugu, ambalo Kristo alisema atalitapika. Na hakutakuwa na kanisa lingine Zaidi ya hili. Hivyo Kristo anatuita kwasababu ule mwisho umekaribia, na hataki hata mmoja wetu apotee.
Hivyo kama hujaokoka kikamilifu, kama hujaacha ya ulimwengu..kama ni mwasherati bado, kama ni mzinzi, kama ni mtazamaji wa pornography kama ni mtukanaji, tubu leo..kwasababu wokovu ni bure, na atakusamehe na kukutengeneza upya. Na kusudia kuacha yote mabaya unayoyafanya na Bwana atakupa Roho wake Mtakatifu atakayekusaidia kushinda dhambi na kukuongoza katika kuijua kweli yote.
Bwana akubariki.
Kama utahitaji uchambuzi wa vitabu vya nyuma basi utatumia ujumbe inbox. Kitabu kitakachofuata kitakuwa ni kitabu cha Danieli hivyo usikose mwendelezo.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
NENO LA MUNGU NI DAWA ILIYO TOFAUTI NA DAWA NYINGINE.
DANIELI: Mlango wa 1
Je! Ni ipi tarehe sahihi Evil-merodaki alimtoa Yekonia gerezani?
UFUFUO TUNAOUSUBIRIA UTAHITIMISHA YOTE.
KUTAKUWA NA MATETEMEKO YA NCHI, NJAA NA TAUNI.
Wafilisti ni watu gani.
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
Ili kujua vizuri ni kwanini tunaomba kwa jina la Yesu. Tafakari kidogo mfano huu.
Jaribu kuwaza, mfano wewe ni mwekezaji halafu umeona shamba zuri mahali Fulani na unataka kwenda kuekeza kwa ukulima wa kisasa, Ukaanza kufuata taratibu zote za kupata eneo hilo, kuanzia ngazi ya kijiji mpaka almashauri, lakini ‘process’ imekuwa ngumu, mara unaambiwa kinahitajika hiki, mara kinahitajika kile, mara bado hujakidhi vigezo, n.k. Na umeendelea kusubiria hivyo kwa miaka 2 sasa lakini bado hujapewa eneo hilo.
Lakini kwa bahati nzuri siku moja raisi, akiwa anapita, kuzungumza na wajasirimali, ukapata fursa, ya kumweleza shida zako, na raisi akatoa agizo saa hiyo hiyo na kusema ‘Mimi ninaagiza mtu huyu apewe shamba hilo’ Unadhani, itakuwa ni ngumu kama ulivyokuwa unahangaika wewe mwenyewe?
Kwa agizo tu hilo la raisi unakuwa na mamlaka hata ya kuwaharakisha wale wahusika wafanye haraka, nao watatii na kutimizi ndani ya ule wakati walioambiwa.
Ndivyo ilivyo kwa Yesu, utauliza ni kwanini tunaomba kwa jina la Yesu,. Ni kwasababu jina hili ndilo jina lililo kuu kuliko majina yote hapa Duniani, ni zaidi ya jina la raisi yeyote unayemjua, au mfalme yeyote, au Sultani yeyote aliyewahi kuishi hapa duniani. Hivyo unapolitumia jina hili agizo halitoki kama ombi, bali kama amri..
Biblia inasema..
Wafilipi 2:9 “Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; 10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; 11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba”.
Wafilipi 2:9 “Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba”.
Hivyo popote pale unapopeleka maombi yako mbele za Mungu, ni lazima uende wa jina hilo la YESU KRISTO..Vinginevyo huwezi kukubaliwa na mbingu, kwa lolote lile unaloliaomba.
Unaposhindana na nguvu za giza, ni lazima uziamrishe kwa jina hili la YESU KRISTO, Vinginevyo, utaumia wewe mwenyewe..
Na ndio maana biblia imetuambia jambo lolote liwe tulifanyalo kwa Neno au kwa tendo tufanye katika jina hili, kwa faida yetu wenyewe na kwa usalama wetu.
Wakolosai 3:17 “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye”.
Vilevile unapookoka, ni sharti ulikiri hili jina kuwa ndio jina pekee linalookoa, Maana ndio tafsiri ya jina lake (YESU-YEHOVA ANAOKOA)
Vivyo hivyo tunapokwenda kubatizwa baada ya kumpokea kwetu Kristo, ni lazima tubatizwe kwa jina hili na sio lingine.
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.
Soma tena (Matendo 8:16, 10:48, 19:5)
Ukizingatia yote hayo, basi rohoni unaonekana umepigwa chapa zake, kiasi kwamba laana yoyote haiwezi kukupata, wala nguvu za giza kukushinda….
Wagalatia 6:17 “Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu”.
Na wewe je! jina hili lina nguvu yoyote ndani yako?. Usidhani ni kulitamka tu, halafu basi, shetani ndio atakuogopa, hilo wazo liondoe, wapo watu waliojaribu kufanya hivyo katika biblia na huku maisha yao yapo mbali na wokovu, kilichowakuta hadi leo habari yao tunaisoma..
Matendo 19:13 “Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. 14 Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. 15 Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? 16 Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa. 17 Habari hii ikajulikana na Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, hofu ikawaingia wote, na jina la Bwana Yesu likatukuzwa”.
Matendo 19:13 “Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo.
14 Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo.
15 Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani?
16 Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa.
17 Habari hii ikajulikana na Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, hofu ikawaingia wote, na jina la Bwana Yesu likatukuzwa”.
Unaona hapo ili jina la YESU liwe na nguvu ni sharti umpokee yeye kwanza, na ukishampokea ndipo unapokuwa na mamlaka ya kulitumia jina hilo kuwasilisha mahitaji yako kwa Mungu, vilevile kuziamrisha nguvu za giza, na kufungua kifungo vyote vya laana vilivyokufunga katika maisha yako.
Hivyo kama upo tayari leo kumruhusu Yesu Kristo aingie maishani wako, basi, fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya toba.>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa imani, basi kuanzia sasa ni vizuri ukaanza kujifunza mafundisho mengine ya rohoni kukusaidia kukua kiroho..Pakua tovuti hii, kwani yapo masomo zaidi ya 1000, na majibu ya maswali mengi yaliyojibiwa, ambayo ukiyasoma maisha yako ya rohoni hayatabaki kama yalivyokuwa.
Au yakufikie kwa njia ya Whatasapp: +255789001312
Lakini kwasasa anzana na haya tuliyoyaorodhesha chini hapa..
BASI MUNGU AKAMUADHIMISHA SANA..
JINA LA MUNGU NI LIPI?
WEWE U MWALIMU WA ISRAELI,NA MAMBO HAYA HUYAFAHAMU?
UMUHIMU WA KUZALIWA MARA YA PILI.
KWA KUPIGWA KWAKE SISI TUMEPONA.
JINSI MUNGU ANAVYOIPIGA NA KUIPONYA AFRIKA.
Je kuvaa pete ni dhambi kwa mkristo?
Awali ya yote kabla hatujafahamu kama kuvaa pete ni dhambi au sio dhambi ni vizuri kwanza tukajua jambo hili kuwa biblia imekataza wanawake wacha Mungu(Wakristo), kujipamba kwa mfano wa wanawake wa kidunia. Biblia ililijua hilo tangu zamani kuwa wanawake wengi watatamani kufanya hivyo, na ndio maana vifungu hivyo vya zuio la kujipamba viliwalenga moja kwa moja wao na sio wanaume..
Tusome,
1Timotheo 2:9 “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; 10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu”.
1Timotheo 2:9 “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu”.
Sasa huyo ni Paulo aliandika hivyo, lakini mtume Petro naye pia alilirudia Neno hilo kuonyesha msisitizo wa maagizo wa maagizo hayo ya Mungu kwa wanawake wote..tusome..
1Petro 3:3 “Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; 4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. 5 Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao”.
1Petro 3:3 “Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;
4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.
5 Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao”.
Unaona wakina Sara hawakujipamba, wakina Mariamu hawakujipamba, na wanawake wengine wote mashujaa tunaowasoma kwenye biblia hawakufanya hivyo ni mwanamke mmoja tu katika biblia aliyeitwa Yezebeli ndiye tunamwona alikuwa akijimbana na kujipaka ma-wanja, na sisi sote tunajua tabia zake alikuwa ni mwanamke wa namna gani hakuna haja ya kuzisimulia..
Hivyo kama wewe ni mwanamke uliyeokoka, unamcha Mungu, na umekuwa ukijipamba, kwa mawigi, mikufu, mahereni, make-ups, kucha za bandia, n.k…Ni vizuri kuacha mara moja..Ukristo ni mabadiliko ya rohoni na mwilini, ukishindwa maagizo madogo kama hayo, utawazaje yale mengine?
Sasa tukishapata huo msingi turudi kwenye swali letu lililoulizwa je kuvaa pete ni dhambi?
Jibu ni kuwa; inategemea, zipo pete za mapambo kwa lengo la kujipamba tu, na zipo pete zinazotambulisha ndoa..
Ikiwa pete unazovaa ni kwa ajili ya mapambo, hapo unaingia katika hilo kundi la mapambo ambayo hayamstahili mkristo yeyote, unakuwa huna tofauti na anayevaa vikuku, na mahereni,..fungu lenu ni moja.
Lakini ikiwa pete unayovaa ni kwa ajili ya kuitambulisha Ndoa, Hilo haliwi tena pambo bali inakuwa ni kiashirio cha kitu Fulani, kama tu vile mtu anayevaa saa mkononi, ipo kwa lengo la kutambulisha majira.
Hivyo ikiwa unakwenda kuoa/ kuolewa, na unahofu labda ukivaa pete ya ndoa itakuwa ni dhambi, hilo sio kweli, biblia imeorodhesha baadhi ya waaminio waliovaa pete katika kanisa la Kristo. Soma.
Yakobo 2:1 “Ndugu zangu, imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendelea watu. 2.2 Maana akiingia katika sinagogi lenu MTU MWENYE PETE YA DHAHABU na mavazi mazuri; kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu; 2.3 nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu, 2.4 je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu”?
Yakobo 2:1 “Ndugu zangu, imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendelea watu.
2.2 Maana akiingia katika sinagogi lenu MTU MWENYE PETE YA DHAHABU na mavazi mazuri; kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu;
2.3 nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu,
2.4 je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu”?
Umeona hapo?. Kwahiyo hakuna dhambi yoyote kuvaa pete ikiwa tu ni kwa lengo la kuitambulisha ndoa, tena zipo faida nyingi katika kufanya hivyo, na mojawapo ni kuzuia usumbufu usiokuwa wa lazima, jaribu kufikiria mwanamke ambaye pengine kaolewa bila pete, halafu anatembea barabarani, ni rahisi kusumbuliwa na baadhi ya wanaume ambao hawajaoa wakidhani kuwa hajaolewa, lakini kama angekuwa na pete mkononi mwake, wale watu wangeiona, na ingekuwa ni rahisi kumwacha apitie wakijua kuwa ameshaolewa mtu Yule.
Kwahiyo ina faida nyingi zaidi ya hasara,
Lakini jambo la kuzingatia ni kuwa, kuvaa pete pia sio lazima kwa wana-ndoa, inawezekana kanisani kwenu hamna huo utaratibu, au kwenye jamii yenu, au nyie wenyewe hampendelei kufanya hivyo, hiyo bado ni ndoa takatifu iliyopokelewa na Mungu..Hilo nalo ni sawa tu kwasababu katika biblia hakuna masharti yoyote yaliyomkataza/kumruhusu mtu avae au asivae pete.
Wakolosai 3:14 “Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu. 15 Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja…;”.
Wakolosai 3:14 “Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.
15 Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja…;”.
Hivyo amani ya Kristo iamue ndani yako.
Je! Mwanamke anapaswa afunikwe kichwa anapokuwa ibadani?
MAJONZI YA MTUME PAULO KWA NDUGU ZAKE.
YATAMBUE MAJIRA YA KUJILIWA KWAKO.
NI SALAMA ROHONI MWANGU Lyrics
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
UNYAKUO.
KIAMA KINATISHA.
SWALI: Biblia inaposema “Na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto” Ina maana gani? (Yuda 1:22).
JIBU: Ukisoma kitabu chote cha Yuda kwa utulivu ambacho ni sura 1 tu, utaona maudhui kubwa iliyoandikwa pale ilikuwa ni kulionya kanisa juu ya kuishindania Imani ambayo walikabidhiwa mara moja tu, (soma binafsi kwa utaratibu utaliona hilo), Na hiyo ni kutokana na kuwa tangu ule wakati kulizukua wimbi kubwa la manabii wa uongo, ambao walifananishwa na Kora na Balaamu, Pamoja wa watu waovu, mfano wa Sodoma na Gomora na watu wasio na imani (aliowaitwa makafiri), waliojiingiza kwa siri katikati ya kanisa la Mungu, ambao kazi yao ilikuwa ni kuleta matengano ndani ya kanisa.
Hivyo mtume Yuda alilionya sana kanisa kuhusu watu hawa, na ndipo mwishoni kabisa katika waraka wake akalisihi kanisa, kila mmoja kwa nafasi yake, afanye kazi ya kuwarejesha wengine katika Imani kwa bidii, na ndio hapo akasema..
Yuda 1:22 “Wahurumieni wengine walio na shaka, 23 na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili”.
Yuda 1:22 “Wahurumieni wengine walio na shaka,
23 na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili”.
Unaona jambo la kwanza aliwaambia wawahurumie walio katika shaka: Maana yake ni kwamba kuna wapo watu ambao walishaathiriwa na mafundisho ya watu hao waongo, mpaka wakawa na mashaka na Imani, Hivyo watu kama hao aliwasihi, wawahubirie kwa kuwajengea misingi ya Imani tena, ili wasimame, na wasiyumbishwe na uongo unaozagaa huko.
Lakini pia akawaambia..
“na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto”. Hii ikiwa na maana kuwa wapo wengine ambao walikuwa tayari wameshazama kabisa katika udanganyifu wao wa mauti, ni kama vile unamuona mtu ambaye yupo motoni, wewe unadhani njia rahisi kumtoa pale itakuwa ni ipi? Ni wazi kuwa haitakuwa ya kumsihi, au kumwomba, hapana, utatumia maneno ya nguvu na vitendo, kwa kumnyakua kutoka kule motoni ili tu apone kwanza,
Ndivyo ilivyo katika kuwahubiria watu wengine ambao wameshakuwa sugu wa Habari za wokovu (Shetani ameshawapofusha macho), Inapofikia wakati kama huo, injili za upendo na huruma za Kristo hazitawafaa, bali injili za hukumu na ziwa la moto, na mateso ya milele, na dhiki kuu, zinazowangoja watu waovu, ndizo zitakazowatafakarisha Zaidi na kuwageuza.
Kuna watu wanasema, hatupaswi kuhubiri Habari za dhiki kuu, na jehanum ya moto kufanya hivyo ni kuwatisha watu, hivyo inawafanya wawe waoga, wampokee Yesu kwa sababu wanaogopa kwenda kuzimu na sio kwasababu wanampenda.
Ndugu, Ni heri aokoke kwa hofu ya Jehanum, kuliko, upotelee huko milele. Na huko ndiko kuwaokoa wengine kwa kuwanyakua kutoka moto, sio kwa kuwahubiria maneno ya kuwapendezesha, bali kuwaonya na hatari watakayoikuta mbeleni..Na hata hivyo sio uongo, bali ni kweli ndivyo ilivyo kwa watu wote ambao hawatatubu.
Kama biblia inavyosema.
2Wakorintho 5:10 “ Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya. 11 BASI TUKIIJUA HOFU YA BWANA, TWAWAVUTA WANADAMU; lakini tumedhihirishwa mbele za Mungu. Nami natumaini ya kuwa tumedhihirishwa katika dhamiri zenu pia”
2Wakorintho 5:10 “ Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.
11 BASI TUKIIJUA HOFU YA BWANA, TWAWAVUTA WANADAMU; lakini tumedhihirishwa mbele za Mungu. Nami natumaini ya kuwa tumedhihirishwa katika dhamiri zenu pia”
Ni kweli kabisa yapo makundi yanayostahili kufundishwa sana juu ya Upendo wa Kristo, kwa mfano watu waliokata tamaa ya Maisha, au mtu aliye katika dhiki na mateso na vifungo vya shetani, au mtu ambaye hamjui Mungu kabisa, au mwenye shauku ya kumjua Mungu, lakini hajui ni wapi pa kuanzia,..Hawa wanastahili injili za Upendo wa Mungu..Ndizo zitakazowafungua na kuwapeleka viwango vingine..
Mathayo 11.28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; 30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.
Mathayo 11.28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.
Lakini lipo kundi lingine ambalo, limeshahubiriwa, na linafahamu kila kitu, lakini bado lipo katika dhambi, pengine ili kuliokoa (kulinyakua kutoka huko liliko) injili inayolifaa ni ile ya Ziwa la Moto wa milele, Na bado tutaendelea kuzihitaji kwa wakati huu wa siku za mwisho.
Ubarikiwe.
JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?
HATARI YA KUHUBIRI INJILI TOFAUTI NA ILIYOANDIKWA KWENYE BIBLIA.
JE KIFO NI NINI? NA JE KUNA AINA NGAPI ZA VIFO?
JE NI LAZIMA MKRISTO AOE/AOLEWE?
KUTUBU SIO KUOMBA REHEMA.
WhatsApp
Hili ni moja ya swali lenye mtafaruku mkubwa sana miongoni mwa wakristo, na wengi hata wameishia mpaka kugombana kabisa!..Wapo wanaoamini kanisa litapitia dhiki kuu ndipo linyakuliwe na wapo wanaoamini kanisa halitapita dhiki kuu, yaani utaanza kwanza unyakuo ndipo dhiki kuu ifuate.
Kuna kitu kimoja cha kimaandiko ambacho hakijulikani na wengi..nacho ni Mgawanyiko wa ujio wa Kristo;
Ujio huu umegawanyika katika vipengele vikuu 3, mtu akishindwa kuvielewa vipengele hivi basi biblia itamchanganya. Na vipengele hivyo ni kama ifuatavyo.
Huu ni ule wakati Kristo alipozaliwa na Bikira Mariamu, na kuishi kwa miaka 33 na nusu na kisha kufa, na kufufuka na kupaa mbinguni alikotoka.
Huu utahusisha Kristo kuwapokea wateule wake mawinguni katika tendo maarufu lijulikanalo kama unyakuo. Wakati huo, wafu waliopo makaburini watafufuka wataungana na watakatifu walio hai na kwa pamoja watakwenda mawinguni kumlaki Bwana. Katika Ujio huu Kristo hatashuka duniani, atabaki mawinguni, watakaonyakuliwa ndio watakaokwenda mawinguni kumfuata na kwenda naye mbinguni kwenye makao waliyoandaliwa.
Katika hatua hii ndio litatimia lile neno.. la kwenye Luka 17:34
“Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. 35 Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. 36 Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa”.
“Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
35 Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
36 Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa”.
Vilevile lile Neno “atakuja kama mwivi usiku”, ndio litatimia katika hatua hii..Pengine utakuwa umelala na mume wako/mke wako aliyeokoka na ghafla! utapoamka asubuhi hutamkuta kitandani. n.k.
Huu hautakuwa ujio wa kila jicho kumwona Yesu, kwasababu hatakuja kwa hukumu bali kwa ajili ya kuwachukua wateule wake na kwenda nao mbinguni kwenye karamu aliyowaandalia, ili kuwaepusha na dhiki ambayo itakwenda kuanza duniani muda sio mrefu. Dhiki ambayo inajulikana kwa jina lingine kama saa ya kuharibiwa ulimwengu!.
Ufunuo 3:10 “Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi”.
Sasa huo sio wakati wa kila jicho kumwona Yesu mawinguni, wakati wa kila jicho kumwona utakuwa ni wakati wa ujio wa tatu, ambao tutauona mbele kidogo.
Sasa kabla ya kwenda hatua ya mwisho ya Ujio wa tatu, hebu tujiulize maswali machache juu ya huu ujio wa pili.
Na wakati wa kila jicho kumwona Kristo, biblia inasema Mataifa yote wataomboleza..na milima itahama na visiwa, kutakuwa na tetemeko kubwa la nchi, na jua litazima na mwezi utakuwa mwekundu kama damu. Kwa ufupi mwisho wa dunia utakuwa umefika..Sasa kama mambo hayo yote yatatokea katika siku ile ya unyakuo, ni nani atakuwa amelala kitandani, au yupo shambani analima, katikati ya dhiki kubwa namna hiyo, huyo mpinga-Kristo atatokea wapi na atawapa watu chapa muda gani?..
Kwahiyo ni wazi kuwa siku ya unyakuo ni nyingine na siku ya Ujio wa Kristo ambao kila jicho litamwona nayo ni nyingine. Haiwezekani siku ya unyakuo ndio iwe siku hiyo hiyo ya kila jicho kumwona, na visiwa na milima kuhama.
Sasa twende hatua ya mwisho ya tatu.
UJIO WA TATU:
Baada ya unyakuo kupita katika ujio wa pili, baadhi ya watu watatoweka, na dunia haitaelewa chochote, wengi watahisi watu wamepotea tu, kama ilivyo kawaida ya watu kupotea potea na kupatikana, na wengine wengi watajua ni habari za kuzusha tu!..taarifa chache zitafika vituoni, lakini mwisho zitaishia kupuuziwa… Kama baadhi ya taarifa za watu kupotea zinavyopuuzwa leo. Pasipo kujua kuwa Kristo tayari kashalinyakua kanisa lake (kundi dogo). Na siku hiyo hakutakuwa na ishara yoyote angani, wala jua halitazima..kutakuwa na ukimya tu kama wa siku zote.
Sasa katikati ya hicho kipindi, ndio utakuwa wakati wa mpinga-kristo kunyanyuka…Ndani ya miaka mitatu na nusu ya kwanza (yaani miezi 42), utakuwa ni wakati wa mpinga-kristo kuwadanganya watu waipokee chapa yake..wengi wataipokea chapa pasipo kujua, wakidhani ni mfumo mpya tu! Wa kimaendeleo umezuka, ambao utasaidia watu kutambulika kirahisi..Utakubalika duniani kwa muda mfupi sana, kiasi kwamba mtu atakayeukataa atakuwa anaenda kinyume na serikali, hivyo atatafutwa na kusingiziwa mambo yasiyofaa.
Wachache sana wataipokea kwa kujua, kwa kujua kabisa kwamba hii ni chapa, lakini wengi hawatajua..kwasababu mpinga-kristo hatakuwa mtu mwenye mapembe kama watu wanavyofikiri, bali atakuwa ni mtu mwenye ushawishi mkubwa sana wa kisiasa, kidini, kiuchumi na kijeshi, na anatakua ni mtu anayeshika biblia!. Hivyo hatajulikana na wengi kuwa ndiye mpinga-kristo mwenyewe, kwasababu ataheshimika kama kiongozi wa dini, atakayeleta amani..hivyo atapewa nguvu na dunia nzima.
Baada ya miaka mitatu na nusu ya kwanza kuisha, wale wachache ambao wataikataa chapa yake hiyo ndio watakaoanza kuipitia DHIKI KUU, wengine hawataguswa!..wataendelea na shughuli zao za KUUZA NA KUNUNUA bila usumbufu!…Lakini walioikataa watajaribu kujificha lakini watakamatwa na kupewa shutuma za uongo na hivyo kukusanywa katika magereza maalumu ya mateso…wakiwa humo watateswa mateso ambayo hayajawahi kutokea tangu dunia kuumbwa…na watamani kufa lakini wale waliowafunga hawatawaua mapema!!…
Lakini mwisho wa siku watakufa wote….na karibia na mwisho ya hiyo miaka mitatu na nusu ya mwisho, wataisha wote…Ndipo Mungu ataanza kuwapiga wanadamu wote waliopokea hiyo chapa ya mnyama kwa yale mapigo ya VITASA SABA, tunayoyasoma katika ufunuo 16. Kwahiyo DHIKI KUU, itaongezewa juu yake vitasa saba..Na Mwisho kabisa, miaka hiyo ya dhiki na vitasa itakapoisha, biblia inasema Jua litatiwa giza, na mwezi utakuwa mwekundu kama damu, Ishara ya mwana wa Adamu itaanza kuonekana mbinguni..
Bwana Yesu mwenyewe Mfalme wa wafalme atatokea mawinguni pamoja na jeshi kubwa na watakatifu walionyakuliwa…Atashuka kwa ajili ya vita vya Harmagedoni, na kwaajili ya utawala wa miaka elfu duniani.
Sasa siku hii kwa wale wachache ambao watakuwa wamesalia duniani, ambao waliipokea chapa lakini hawakufa katika mapigo ya vitasa saba..Wataona umeme ukimulika kutoka mashariki hata magharibi!..na dunia yote itakuwa giza ghafla (jua litazimwa)!…Na watamwona Kristo mawinguni, uso wake uking’aa kuliko jua…Hofu kuu itawaangukia wataomboleza kwa hofu, biblia inasema watatamani milima iwaangukie..
Mathayo 24:29 “Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; 30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi 31 Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.”.
Mathayo 24:29 “Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika;
30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi
31 Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.”.
Soma tena…
Ufunuo 6:12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; JUA LIKAWA JEUSI KAMA GUNIA LA SINGA, MWEZI WOTE UKAWA KAMA DAMU, 13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi. 14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. 15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, 16 WAKIIAMBIA MILIMA NA MIAMBA, TUANGUKIENI, TUSITIRINI, MBELE ZA USO WAKE YEYE AKETIYE JUU YA KITI CHA ENZI, NA HASIRA YA MWANA-KONDOO. 17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?.
Ufunuo 6:12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; JUA LIKAWA JEUSI KAMA GUNIA LA SINGA, MWEZI WOTE UKAWA KAMA DAMU,
13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.
14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.
15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
16 WAKIIAMBIA MILIMA NA MIAMBA, TUANGUKIENI, TUSITIRINI, MBELE ZA USO WAKE YEYE AKETIYE JUU YA KITI CHA ENZI, NA HASIRA YA MWANA-KONDOO.
17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?.
Sasa utauliza hao wateule ambao Bwana atawakusanya wakati wa kutokea mawinguni kwa utukufu mwingi ni wakina nani?
Hao watakuwa ni Wayahudi 144,000, waliotiwa muhuri wa Mungu baada ya kuisikia ile injili ya manabii wawili wa kwenye Ufunuo 11, hivyo walifichwa mbali na mpinga-kristo na dhiki ya vitasa (Ufunuo 12:14-15). Kundi hili la wayahudi 144,000 ambao walifichwa mbali na yule joka…Ndio wanaoitwa wateule..
Hawa wakati Kristo atakaokuja ndio watakaokusanywa kutoka pepo nne, na kuletwa juu ya mlima Sayuni uliopo pale Israeli..(Ufunuo 14:1 “ Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao”).
Kwahiyo sio kanisa ambalo litakusanywa kutoka pembe nne, bali ni wayahudi hao 144,000, ambao waliisikia ile injili iliyohubiriwa na wale manabii wawili katika Ufunuo 11, na kutiwa muhuri wa Mungu juu ya vipaji vya nyuso zao…Kanisa tayari lilikuwa utukufuni, na ndio linalorudi na Kristo hapa!.
Sasa upo utata mmoja maarufu katika Ufunuo 7:9-16..Tusome
“ 9 Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao; 10 wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo………………………… 13 Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Na wametoka wapi? . 14 Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo. 15 Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao. 16 Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote”
“ 9 Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;
10 wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo…………………………
13 Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Na wametoka wapi? .
14 Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.
15 Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao.
16 Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote”
Mstari huu ndio unaowafanya wengi wahitimishe kwamba dhiki kuu itaanza ndipo tuende mbinguni…Lakini hebu soma vizuri mstari huo wa 9 unasema “nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi”.
Hapa ni mbinguni baada ya unyakuo…na sio kundi moja la watu Fulani tu! Bali ni la watu wote (sio tu walio hai) bali hata waliokufa katika Kristo katika vizazi vyote vya nyuma, wakina Petro waliokatwa vichwa, wakina Stephano waliopigwa mawe, wakina Perpetua waliopitia dhiki za kuwekwa kwenye maarena na kufunguliwa Wanyama wakali, wakina Polikapi waliochomwa moto, wakina Antipa na wengine wengi na hata wakristo wote wanaopitia dhiki za kiimani hata sasa ambao watakuwa hai mpaka ile siku ya kunyakuliwa….
Sasa wote hawa kwa pamoja ndio wanaolijenga hilo jeshi kubwa hapo juu la Ufunuo 7…Kwahiyo hilo sio kundi moja tu la watu Fulani tu wachache!..bali ni la watu wa vizazi vyote waliokufa katika Kristo(Na mbele za Mungu, ni washindi wa dhiki za ulimwengu, kama Bwana Yesu alivyosema “ulimwenguni mnayo dhiki”). Mbinguni hakutakuwa na makundi mawili; ya waliopitia dhiki na ambao hawajapitia dhiki, ndio maana unaona hapo hakuna makundi mawili, bali kundi moja tu!.
Huo ni ufupisho tu kwa yatakayotokea siku za mwisho…Hivyo kwa hitimisho ni kwamba kanisa halitapitia Dhiki kuu ya mpinga-kristo… “litaepushwa na saa ya kuharibiwa”..watakaopitia dhiki kuu ya mpinga-kristo ni wale watakaoachwa kwenye unyakuo..na watauawa na mpinga-kristo (na hawatakuwa miongoni mwa watakaokwenda mbinguni), wataikosa karamu ya Mungu mbinguni ingawa wakati wa Kristo kurudi na watakatifu, watafufuliwa na kuingia katika utawala wa miaka elfu hapa duniani.
Na siku ya unyakuo sio siku ya kila jicho kumwona Yesu mawinguni, sio siku ya mataifa yote kuomboleza.
Sasa ni kitu gani kinachowafanya watu wachanganyikiwe?
Ni kwasababu ya kutoelewa kalenda ya Neno la Mungu…Ni wachache sana wanalijua na kulielewa andiko la kwenye Warumi 11, linalozungumzia Upofu waliopigwa Wayahudi (yaani waisraeli). Upofu huo walipigwa wasimwamini Masihi, Yesu Kristo ili sisi watu wa mataifa tupate Neema (hebu tenga muda binafsi soma taratibu Warumi 11 yote).
Kutokana na upofu waliopigwa iliwafanya wasimwamini kabisa Yesu, na kujikuta wakimtazamia Masihi mwingine. Na sisi watu wa Mataifa ikawa ni nafasi kwetu kumwamini, kwani wale mitume ambao walipaswa watumwe kwa wayahudi walikuja kwetu na sisi tukamwamini Yesu, macho yetu yakafunguliwa..tukaipokea hiyo neema. Na tumekaa na hiyo neema sasa kwa Zaidi ya miaka 2,000, ndio maana huoni ugumu leo kuhubiri injili ya Yesu na watu wakamwamini kirahisi tu!..Neema hii haipo kwa Waisraeli unaowaona leo!..Ukienda Israeli ukiwaeleza Habari za Yesu, wanakuona ni mwendawazimu…wanakupinga kabisa!..ni wachache sana wanaomwamini, lakini Zaidi ya asilimia 90 ya waisraeli wanamkataa Yesu. Na hiyo ni kutokana na upofu waliopigwa..yaani neema waliyopokonywa ili tupewe sisi.
Lakini biblia inasema katika hiyo hiyo warumi 11…kwamba hawatakuwa katika hiyo hali ya kutomwamini Yesu milele. Itafika siku ambapo macho yao yatafumbuliwa..Siku hiyo itakuwa ni zamu ya watu wa mataifa kupitia ukame wa rohoni kama wanayoipitia sasa waisraeli.
Siku hiyo itakuwa ni siku ya Neema ya wokovu kuondoka kwa watu wa Mataifa milele na kuhamia Israeli. Sasa Neema hiyo itahitimishwa na tukio la unyakuo. Kristo atakapolinyakua tu kanisa lake, na Mlango wa Neema siku hiyo hiyo utakuwa umefungwa kwa watu wa Mataifa na kubakia kwa waisraeli peke yao. Huku hata mtu aombe vipi, hakuna rehema. Roho Mtakatifu atahamia kwa Waisraeli, watahuzunika sana na kujilaumu ilikuwaje kuwaje mpaka wakamkataa Masihi kwa miaka yote hiyo…
Kwa kupitia injili ya wale manabii wawili, ndio watapatikana idadi ile 144,000 (Haijulikani kama ndio namba kamili, au ni ya kuwakilishi tu, kwamba idadi inaweza kuwa kubwa Zaidi ya hiyo). Lakini hao tu ndio watakaosalimika, ndio wateule, na watakusanywa katika Mlima Sayuni.
Warumi 11:25 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili. 26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake. 27 Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao”.
Warumi 11:25 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.
26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.
27 Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao”.
Sasa hapa kwenye WAKATI WA MATAIFA na WAKATI WA WAYAHUDI, ndiko kunakowafanya watu washindwe kuuelewa ujio wa Bwana. Asilimia kubwa ya watu hawajui kuwa kuna wakati wa Wayahudi kurudiwa na kumwamini mwokozi…wengi wanajua tu! Kuna unyakuo basi!…kwamba baada ya unyakuo hakuna chochote kitakachoendelea, na wanaamini kuwa mbinguni tutakaa huko milele, wala hakuna wakati tutarudi tena huko..Hawajui kwamba kuna utawala wa miaka elfu wa kutawala na Kristo duniani unatungoja. N.k
Tukiyajua hayo..huu sio wakati wa kucheza na Neema tuliyopewa sisi watu wa mataifa hata kidogo…Sasahivi unaweza kusikia injili, ukaikataa kwa mdomo lakini moyoni mwako ukashuhudiwa kwamba ni kweli yanayozungumzwa…Hicho kinachokushuhudia ndani yako ni sauti ya wito wa Mungu (Ni neema ya Mungu bado inatuita)..Itafika kipindi itaondoka kabisa…itahamia Israeli.. na hiyo sauti ya Roho Mtakatifu itakapoondoka..Ndipo mpinga-kristo atafunuliwa.
2Wathesalonike 2:7 “Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa. 8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake”
2Wathesalonike 2:7 “Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.
8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake”
Bwana atubariki.
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
YONA: Mlango wa 3
NA YEYE ALIYEKETI JUU YA WINGU AKAUTUPA MUNDU WAKE JUU YA NCHI, NCHI IKAVUNWA.
Kile kinara cha Taa ndani ya Hekalu la Sulemani kilikuwa kinawakilisha nini?
YAKINI NA BOAZI.
NEEMA YA MZALIWA WA PILI.
JINSI SODOMA NA GOMORA ILIVYOKUWA INAVUTIA SANA..
Zaburi 91, Ni Zaburi iliyo ya kipekee sana yenye nguvu, Na shetani analijua hilo, ukitaka kuamini jiulize, ni kwanini Shetani aliitumia Zaburi hii kumjaribu Bwana,? Kiasi kwamba mtego wake ungekubali basi Zaburi hii ndio ingekuwa silaha ya kumwangushia Bwana.
Ni kwanini ainukuu Zaburi 91? Shetani aliijua nguvu na ulinzi Mungu aliouweka juu ya wampendao..Lakini wengi wetu hatuifahamu…Alimwambia hivi Bwana..
Mathayo 4:6 “akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako”.
Mathayo 4:6 “akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako”.
Unaona, alijua kuwa mtu yeyote aliyempendeza Mungu, huwa anaachiliwa ulinzi wa kipekee, Mungu anamuagizia mpaka malaika zake, wamlinde, asijikwae,..
Hivyo kama wewe umeokoka na umesimama vizuri basi fahamu Zaburi 91, Ni salaha yako madhubuti ya kummaliza shetani na vitisho vyake, na majeshi yake..Isipokuwa tu usiitumie hiyo kwa lengo la kumjaribu Mungu, vinginevyo utampa shetani nafasi ya kukuangusha kama alivyojaribu kufanya kwa Bwana Yesu.
Embu tuisome,
ZABURI 91 1 Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi. 2 Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini. 3 Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.
ZABURI 91
1 Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
2 Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.
3 Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.
Bwana anasema, atakuepusha na mitego ya mwindaji(Shetani), na tauni iharibuyo..akiwa na maana atakulinda na magonjwa hatari mfano wa Tauni kama Corona..Unaona ikiwa wewe ni mtakatifu, huna haja ya kuwa na hofu.
Anaendelea kusema…
Zaburi 91:4 Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao. 5 Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana, 6 Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri,
Zaburi 91:4 Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.
5 Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana,
6 Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri,
Ndugu uliyeokoka, Bwana atakulinda tu, huna haja ya kuogopa, iwe ni mchana au usiku atakuwa na wewe kukulinda na mikono ya magonjwa na maadui.
Zaburi 91:7 Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe. 8 Ila kwa macho yako utatazama, Na kuyaona malipo ya wasio haki. 9 Kwa kuwa Wewe Bwana ndiwe kimbilio langu; Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako. 10 Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.
Zaburi 91:7 Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe.
8 Ila kwa macho yako utatazama, Na kuyaona malipo ya wasio haki.
9 Kwa kuwa Wewe Bwana ndiwe kimbilio langu; Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako.
10 Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.
Haijalishi utaona ni wangapi, wanadondoka, au wanashindwa pembeni yako, wameanguka, lakini wewe Bwana atakuwa na wewe wakati wote kuhakikisha hushindwi wala hupatwi na mabaya hayo yote, hata kama utaonekana kama unashindwa,lakini mwisho wa siku ushindi utakuwa ni wako tu,
Zaburi 91:11 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote. 12 Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 13 Utawakanyaga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.
Zaburi 91:11 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote.
12 Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
13 Utawakanyaga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.
Unaona zaidi ya hiyo, Malaika wa Bwana watakuwa na wewe kukulinda kila wakati, usijikwae, na mabaya..Na hiyo yote ni kwasababu gani? Ni kwasababu, umempenda Mungu na umemtafuta kwa bidii, umemfanya yeye kuwa tegemeo lako, na ndio maaana anasema..
Chapisho hili limefadhiliwa na https://www.swisswatch.is/ washirika wetu.
Zaburi 91:14 Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu. 15 Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza; 16 Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.
Zaburi 91:14 Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.
15 Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;
16 Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.
Maneno ya faraja sana na yanayotia nguvu, lakini mpaka Mungu kukutamkia hivyo ujue ni lazima kwanza uwe ni mwana wake mpendwa, vinginevyo, hakuna ulinzi wowote, utaokao kwake utakufikia..
Ili Mungu akulinde na tauni (Corona) isikuue, au magonjwa mengine ya kutisha yaliyozuka duniani leo hii, ni lazima uwe mwana wake mpendwa, ili Mungu akulinde na maadui (mapepo na wachawi), Ili Mungu akuagizie malaika zake watembee na wewe kila wakati kama alivyofanya kwa Elisha..basi ni lazima kwanza ufanyike mwana wake.
Ndipo hapo nawe utakapoitamka Zaburi 91 kwa ujasiri wote, na iwe kweli na maana kwako. Kumbuka Zaburi hii ilimwingia sana shetani kichwani, na ndio maandiko pekee aliyoyatamka kwa kinywa katika biblia nzima, hiyo ni kuonyesha kuwa ni jinsi gani anaona wivu, kuona watoto wa Mungu wanapokea ulinzi wa kipekee kutoka kwa Mungu.
Maana yake ni kuwa ukimkosa leo Kristo, basi huwezi mshinda shetani, kwasababu ulinzi wa Mungu haupo juu yako.. Hivyo kama upo tayari leo kumpa Yesu maisha yako, basi uamuzi utakaofanya ni mzuri na wa busara sana..Kama ni hivyo fungua hapa kwa ajili ya maelekezo juu ya sala ya Toba.>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Tafadhali Share na wengine,
Whatsapp: +255789001312
TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.
AGANO LAKO LINABEBWA NA NANI?.
WEWE NI BWANA UNIPONYAYE.
JIFUNZE KUJITOA KWA MUNGU NA KUWA MKARIBISHAJI.
Shalom, jina la Bwana wetu libarikiwe daima.
Neno linatuambia..
“Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi.
Ni mpya kila siku asubuhi..” (Maombolezo 3:22-23).
Na wewe usomaye ujumbe huu rehema za Bwana zisikome juu yako daima.
Leo tutajifunza kwa ufupi, mambo machache ya kuzingatia tunapokwenda nyumbani kwa Bwana aidha kuzungumza naye, au kumwabudu, inaweza ikawa ni kanisani, au kwenye semina, au popote pale unapoweza kumfanyia Mungu ibada.
Kama tunavyosoma katika agano la kale tunaona kuna wakati ulifika wa Sulemani kumjengea Mungu Nyumba (Hekalu) ambalo lingekuwa ni kitovu cha waisraeli wote, na mataifa yote ulimwenguni kumwabudia Mungu , na kufanyiwa upatanisho wa makosa yao kwa wakati ule.. Kama tunavyojua hekalu lile lilijengwa kwa kipindi cha Miaka 7, na katika ujenzi ule, kulikuwa na vigezo vingi sana vya kuzingatia, pamoja na vipimo. Na kila kitu kilichotengenezwa kule kilikuwa kilikuwa kinafunua jambo kubwa sana rohoni kwa kanisa la Sasa, wale makerudi waliowekwa kule walikuwa wanafunua jambo Fulani rohoni, vile vinara 7 vya taa, vilivyokuwa na maana yake pia, halikadhalika zile madhabahu za dhahabu na za shaba , zote zilikuwa na maana, na lile sanduku la agano, mpaka yale mapambo yaliyokuwa kule ndani.
Sasa, karibu na mwisho kabisa wa ujenzi ule, Sulemani aliongozwa kujenga vitu vingine viwili muhimu katika hekalu, navyo si vingine Zaidi ya nguzo kubwa mbili zilizosimama katika maingilio ya Hekalu. Nguzo hizo zilikuwa ni ndefu na pana..
Nguzo ya kwanza iliwekwa upande wa kulia mwa kuingilia hekaluni, Na nguzo pili iliwekwa upande wa kushoto.
Ile iliyokuwa upande wa Kulia iliitwa YAKINI.. Na ile iliyowekwa upande wa kushoto iliitwa BOAZI.
2Nyakati 3:17 “Akazisimamisha nguzo hizo mbele ya hekalu, moja upande wa kuume, na ya pili upande wa kushoto; akaliita jina la ile ya kuume Yakini, na jina la ile ya kushoto Boazi”
Sasa maana ya maneno hayo ni hii:
Yakini ni: IMEDHANIWA KUWA ATATHIBITISHA.
Na Boazi: IMEDHANIWA KUWA IMO NGUVU.
Kulikuwa hakuna namna yoyote kuhani aingie hekaluni, apitilize mpaka patakatifu pa patakatifu, kwenda kufanya mambo ya ibada asipite katikati ya hizo nguzo mbili. Zilikuwa kama mihimili ya hekalu.
Ikifunua kuwa yeyote atakayeingia kule avukapo nguzo hizo ni lazima jambo hilo liwe kichwani mwake, kuwa Mungu atathibitisha(Yakini), Na humo humo ndani pia ipo nguvu ya Mungu (Boazi).
Hivyo kuhani akiingia mule, kwa shughuli yoyote ile aidha ya upatanisho au ya kuwasilisha maombi ya watakatifu, kichwani mwake anauhakika kuwa ni lazima Mungu ajibu maombi yao yaani alithibitishe agano lake alioingia nao kwa kupitia Ibrahimu, Na vilevile anajua kuwa nguvu ya Mungu ipo mule, kwahiyo ni lazima awe makini kwa atayayafanya vinginevyo atakuwa anajitafutia kifo mwenyewe au hata matatizo kwa wana wa Israeli wote.
Nguzo hizo zilisimama kwa wakati wote hekalu lilipokuwepo.
Lakini Ni ujumbe gani tunapewa kwa agano jipya?
Biblia inafananisha kanisa la Kristo kama hekalu la Mungu, tunapotoka na kwenda nyumbani mwake au uweponi mwake, Sisi wote tunaenda kuwa kama makuhani wa Mungu, hivyo Bwana anataka kila mmoja wetu, ajue kuwa nguzo hizo mbili (yaani Yakini na Boazi) zimesimama mbele ya hekalu lake takatifu.
Anataka tujue kuwa tunapokwenda nyumbani mwake tufahamu kuwa Mungu yupo pale, ili kulithibitisha agano lake aliloingia na watakatifu kupitia Yesu Kristo.. Na kwamba unapokwenda kusali, au kumwabudu au kumwomba chochote, yupo pale kukusikia na kukujibu maombi yako, sawasawa na maneno ya Kristo (Yohana 14:13) Huo ni uhakika, Hivyo uingie ukijua jambo hilo kichwani kuwa Mungu ni Mungu mshika maagano.
Vilevile anataka ujue kuwa ipo nguvu yake kule ndani, Hivyo uwe makini pia usiende kidunia/kimazoea.. Wapo watu wanajiamulia tu kuingia kanisani wanavyotaka na mavazi yao kizinzi, wanaingia kanisani na vimini, na suruali, wakidhani kule wanaenda kukutana na miungu isivyoweza kufanya jambo lolote. Hawajua jengo likishaitwa kanisa, Au nyumba ya Mungu, tayari nguzo mojawapo itwayo Boazi imesimama pale nje!, yaani ndani imo nguvu kubwa sana ya Mungu, inayoua na kuhuisha.
Kwahiyo pale mtu anapoingia bila heshima, anakuwa anajitafutia mwenyewe laana..Hilo unapaswa ulijue hili binti wa Mungu, hilo unapaswa ujue kijana,.Unapokwenda kanisani, halafu unajua jana umetoka kuzini, na wakati huo huo unakwenda kushiriki meza ya Bwana,..Unajitafutia matatizo yako mwenyewe..(Soma hapa uone laana iliyowapata watu wa dizaini hiyo katika kanisa la Kristo IWakorintho 11:27-34)
Nyumba ya Mungu, si ya kuifanyia mzaha hata kidogo..
Marko 11:17 “Akafundisha, akasema, Je! Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi”.
Hivyo ndugu kama wewe ni mkristo, zingatia hayo mambo mawili, yaweke kichwani mwako daima Nyumbani mwake Mungu anathibitisha, na nyumbani mwake imo nguvu. (Yakini na Boazi)
Ikiwa hujaokoka, kumbuka leo tena tumepiga hatua nyingine ya kuukaribia ule mwisho, pengine itakuwa leo, au kesho asubuhi, au wiki hii au vyovyote vile, hatuhitaji kuishi maisha ya kubahatisha, hivyo tukiyajua hayo, ni wakati wa kuamka usingizini, na kuzisafisha taa zetu.. Mpe leo Kristo maisha yako ayaokoe. Ufanyike kuwa mwana wake.
MAWE YALIYOKWISHA KUCHONGWA MACHIMBONI.
KUOTA UMEFUNGA NDOA.
USIINGIE MKATABA NA DHAMBI.
IFANYE KAZI YA MUNGU PASIPO HOFU!
AHADI ZA MUNGU.
POPOBAWA NI KWELI YUPO?
Je Kifo ni nini? Na kuna aina ngapi za vifo?
Kifo ni pale uhai unapoondoka ndani ya kiumbe hai chenyewe. Kwa ufupi kifo ni Mwisho wa Maisha ya mwilini.
Lakini katika Biblia vipo vifo vikuu vya aina tatu.
Kifo cha Mwilini:
Hichi ni pale mwili na roho vinapotengana. Kifo hichi kinamkuta kila mmoja wetu, pale anapomaliza safari yake ya Maisha ya duniani ikiwa unyakuo utakuwa haujakukuta basi utakufa na kuzikwa.
Mwanzo 3:19 “…. kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi”.
Kifo cha namna hii haikuhusishi roho ya mtu..Roho inakuwa bado inaendelea kuishi sehemu nyingine..Bwana Yesu alisema..
Mathayo 10:28 “Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.”
Kifo cha Rohoni:
Hichi ni kifo ambacho kinamkumba mtu kwa ndani, lakini kwa nje bado anakuwa anaendelea kuishi kana kwamba hakuna chochote kinachoendelea.. Na kifo cha namna hii, kila mmoja wetu anacho aidha kwa kujua au kwa kutokujua..Leo hii ikiwa Maisha yako yapo mbali na dhambi (yaani umeokoka), tayari wewe rohoni unaonekana kuna mauti imetokea ndani yako, yaani unaonekana tayari umeshakufa kwa Habari ya dhambi, biblia inasema hivyo..
Warumi 6:1 “Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? 2 Hasha! SISI TULIOIFIA DHAMBI tutaishije tena katika dhambi.. 6:11 “Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu”.
Warumi 6:1 “Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? 2 Hasha! SISI TULIOIFIA DHAMBI tutaishije tena katika dhambi..
6:11 “Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu”.
Vilevile ikiwa injili inahubiriwa kwako halafu hubadiliki, fahamu kuwa katika ulimwengu wa roho umekufa kwa Habari ya haki hata kama utakuwa unaishii..
1Timotheo 5:6 “Bali, yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai”.
Kifo cha Roho:
Kifo hichi ndio kibaya Zaidi, Na ndio kifo cha mwisho kinachojulikana kama Mauti ya pili. Kifo hichi ni pale, unapotenganishwa moja kwa moja na uso wa Mungu milele, katika lile ziwa la moto.. Ambapo utatetezwa huko na roho yako itaangamia milele.
Ufunuo 20:13 “Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.
Ufunuo 20:13 “Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.
Lakini Pamoja na hayo sisi tulio ndani ya Kristo tunalo tumaini la uzima wa milele ikiwa tutakufa leo. Kwasababu Yesu Kristo ambaye alishinda mauti, atakuja kutufufua tena, katika hii hii miili yetu, kisha atatuvika miili mingine mipya ya utukufu ya kimbinguni isiyo kufa wala kuugua, wala isiyo na madhaifu, na hiyo ndiyo tutakayoishi nayo milele.
Lakini ikiwa wewe ni mwenye dhambi bado hujamkabidhi Kristo Maisha yako ayaokoe, ukifa leo hii, huna tumaini lingine lolote Zaidi ya kungojea ile mauti ya pili ambalo ni ziwa la moto..
Lakini kwanini hayo yote yatukute angali tunayo nafasi bado?..Ikiwa wewe ni mmojawapo ambaye yupo bado katika dhambi, Na leo hii unataka Bwana Yesu akuokoe, hutaki neema ya wokovu ikupitie, basi popote pale ulipo anaweza kukusamehe dhambi zako ikiwa tu utamaanisha kufanya hivyo.
Kama upo tayari kutubu sasa dhambi zako, basi fungua hapa kwa ajili ya maelekezo ya sala ya Toba. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Ikiwa umemfuata maelekezo hayo ya kuokoka, sasa, upo tayari kujifunza na masomo mengine ya rohoni.Tafadhali tazama chini vichwa vya masomo kisha bofya lolote upendalo uzidi kujifunza zaidi.
MAUTI YA PILI NI NINI?
NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?
MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.
RABI, UNAKAA WAPI?
KAMA MMOJA TU NDIO HIVI! SI ZAIDI 153?
Kwanini Mungu awachome watu kwenye ziwa la moto na hali yeye ndiye aliyewaumba?
KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?
PENGINE MUNGU ALISHASEMA NAWE KWA NJIA HII.
Ni watu gani hao ambao mahali pao hapakuonekana? (Ufunuo 20:11)
JIBU: Tusome..
Ufunuo 20:11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana”.
Hao wanaozungumziwa hapo kwamba “mahali pao hapakuonekana” sio binadamu!..bali ni “MBINGU NA NCHI”. Tafsiri za lugha nyingine zinaelezea vizuri.
Na kwanini zikimbie uso wake?..ni kwasababu ya utukufu wake…kwasababu hakuna kitu chochote kinachoweza kusimama mbele ya uso wa Mungu kwa kuwa yeye mkuu sana na mtakatifu!. Maserafi tu waliopo mbinguni ambao ni watakatifu, bado wanafunika nyuso zao na miguu yao mbele yake..si Zaidi viumbe vilivyopo katika mbingu na nchi tulizopo sisi?.
Ayubu 41:10 “….BALI NI NANI AWEZAYE KUSIMAMA MBELE YANGU MIMI?
Hivyo hakuna kiumbe chochote ambacho kinaweza kumkaribia Mungu kwa ukamilifu wake. Lakini ashukuriwe Mungu kwa sababu yupo mmoja ALIYESTAHILI KUMKARIBIA YEYE, na huyo si mwingine Zaidi ya mwanawe wa pekee aliyemtoa ambaye yeye alishinda na kustahili kumkaribia Mungu, na kuketi Pamoja naye katika kiti chake..Huyo pekee ndiye aliyestahili kumkaribia Mungu…na kwa kupitia yeye sisi tuliompokea tumepata nafasi ya kumkaribia Mungu..
Ufunuo 3:21 “Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi”.
Ufunuo 5:11 “Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu, 12 wakisema kwa sauti kuu, ASTAHILI MWANA-KONDOO ALIYECHINJWA, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka. 13 Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele”.
Ufunuo 5:11 “Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,
12 wakisema kwa sauti kuu, ASTAHILI MWANA-KONDOO ALIYECHINJWA, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.
13 Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele”.
Hivyo tukimwamini na kuingia ndani yake tunapata ujasiri wa kumkaribia Mungu sana, jambo ambalo katika hali ya kawaida lisingekaa liwezekane kabisa, lakini limewezekana kwa kupitia Yesu, lakini tukimkataa huyu Yesu, basi hatuna ujasiri wowote na hatuwezi kumkaribia Mungu kamwe…Tutaukimbia uso wake na kutengwa naye milele katika ziwa la moto.
Waebrania 10:19 “Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, 20 njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake; 21 na kuwa na kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu; 22 na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi”.
Waebrania 10:19 “Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu,
20 njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake;
21 na kuwa na kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu;
22 na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi”.
Shalom.
UFUNUO: Mlango wa 20
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
Kitabu cha YASHARI kinachozungumziwa katika 2Samweli 1:17-18, ni kitabu gani?
URIMU NA THUMIMU NI NINI KATIKA BIBLIA?
ALIYOKUTANA NAYO YESU, YERIKO.
ZIKIMBIE TAMAA ZA UJANANI! NA MTU YEYOTE ASIUDHARAU UJANA WAKO.