Maseyidi 12 wa Ishmaeli, ni wakina nani?.2)Taa ya Mungu ambayo ilikuwa haijazima wakati wa Eli ni ipi?

Maseyidi 12 wa Ishmaeli, ni wakina nani?.2)Taa ya Mungu ambayo ilikuwa haijazima wakati wa Eli ni ipi?

SWALI: Naomba kuuliza watumishi wa Mungu katika Mwanzo 17:20 anaposema kwa habari ya Ishmaeli atazaa maseyidi 12, hao ndio akina nani kwa Sasa?

2) Pia katika 1samweli 3:3 anasema kipindi Samweli anaitwa na Mungu taa ilikua haijazimika bado Nia taa gani hiyo? Asante Sana Ni hayo.


JIBU: 

  1. Tusome..

Mwanzo 17:18 “Ibrahimu akamwambia Mungu, Lau kwamba Ishmaeli angeishi mbele yako.

19 Mungu akasema, Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake.

20 Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu”.

Neno Seyidi linamaanisha  mtawala, hivyo hapo biblia ilimaanisha kuwa Ishmaeli atazaa watawala 12.. ambao  utaona wakitajwa kwa majina  katika Mwanzo 25:13

Mwanzo 25:13 “Na haya ndiyo majina ya wana wa Ishmaeli, kwa majina yao, na kwa vizazi vyao. Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, ni Nebayothi, na Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu,

14 na Mishma, na Duma, na Masa,

15 na Hadadi, na Tema, na Yeturi, na Nafishi, na Kedema.

16 Hao ndio wana wa Ishmaeli, na hayo ni majina yao, katika miji yao, na katika vituo vyao, maseyidi kumi na wawili kwa kufuata jamaa zao.

Katika historia  wana hawa wa Ishmaeli walikuwa watu wakuu sana, na ndio chimbuko la mataifa ya kiharabu tunayoyaona sasahivi  kule mashariki ya kati.

2) Je ni Taa ipi hiyo inayozungumizwa katika 1Samweli 3:1?,

Tusome.

1 Samweli 3:1 “Basi, mtoto Samweli akamtumikia Bwana mbele ya Eli. Na neno la Bwana lilikuwa adimu siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri.

2 Ikawa wakati huo, Eli alipokuwa amelala mahali pake (tena macho yake yalikuwa yameanza kupofuka, hata asiweze kuona),

3 na taa ya Mungu ilikuwa haijazimika bado, na Samweli alikuwa amelala katika hekalu la Bwana, palipokuwa na sanduku la Mungu;

Inadhaniwa kuwa hiyo ni ile taa ya hekaluni, lakini ukitafakari kwa ukaribu, utaona kuwa biblia haikumaanisha ile taa ya hekaluni au ile ya kwenye hema ya kukutania, bali ilimaanisha pumzi au uhai wa Eli, ukikumbuka kuwa habari iliyokuwa inazungumziwa hapo juu ni kuhusu uzee wa Eli, ambapo inasema umri wake ulikuwa umeshaenda sana mpaka macho yake yalikuwa yameshaanza kupofuka.

Biblia inasema..

Mithali 20:27 “Pumzi ya mwanadamu ni taa ya Bwana; Hupeleleza yote yaliyomo ndani yake”.

Unaona? Hivyo hapo ilimaanisha kuwa Pumzi ya uhai wa Eli ilikuwa bado haijamuacha.

Hiyo ni kutukumbusha pia, kuwa upo wakati na sisi Taa ya Mungu itazima ndani yetu. Na kama tunavyojua taa ikizimika huwa kunakuwa na giza na sikuzote gizani hakuna shughuli yoyote inayoendelea. Vivyo hivyo na siku ambayo kila mmoja wetu atakufa, huko atakapoenda hakuna jambo lolote la kimaendeleo atakalolifanya, Hatakuwa na nafasi ya pili ya kutubu ikiwa alikufa katika dhambi, hatakuwa na nafasi ya pili ya kufanya marekebisho ikiwa alizembea zembea katika masuala ya wokovu wake akiwa hapa duniani. Atakachokuwa anasubiria huko ni hukumu tu.

Mhubiri 9:5 “kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa”.

Hivyo tunapaswa tujithamini maisha yetu tunamalizaje mwendo tukiwa hapa duniani? . Kwasababu huko ng’ambo hakuna nafasi ya pili.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

Wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa.

SWALI: Biblia inamaanisha nini iliposema “wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa;?

JIBU: Tusome vifungu vyenyewe..

2Petro 2:12 “Lakini hao kama wanyama wasio na akili, ambao walizaliwa kama wanyama tu wa kukamatwa na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao;

13 Wakipatikana na madhara, ambayo ni ujira wa udhalimu wao, WAKIDHANIA KUWA ULEVI WAKATI WA MCHANA NI ANASA; wamekuwa ni mawaa na aibu wakifuata anasa zisizo kiasi katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi”;

Hapa Mtume Petro, alikuwa anaeleza jinsi watu waovu wanavyoenenda katika tamaa za mwili, ukisoma tokea juu utaona akiwafananisha na watu wa Sodoma na Gomora..Na moja ya tabia zao ndio hiyo aliyosema “Wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa” akiwa na maana kuwa, wamefikia hatua ambayo kwao anasa zao kama ulevi hawazifanyi tena usiku, bali hata mchana.

Ikumbukwe kuwa anasa zote huwa zinajulikana kuwa zinafanyika usiku.. Na ndio maana wakati ule wa Pentekoste, Roho aliposhuka, wale watu waliwashutumu mitume kuwa wamelewa kwa mvinyo, Lakini Petro aliwaaambia, hakuna aliyelewa, kwasababu sasa hivi ni saa tatu ya mchana (akiwa na maana ni saa 9 alasiri), hakuna mtu anayelewa muda huo.

Matendo 2:13 “Wengine walidhihaki, wakisema, wamelewa kwa mvinyo mpya.

14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu.

15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana”;

Soma pia..

1Wathesalonike 5:7 “Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku”.

Umeona, hivyo mpaka mtu imetokea anafanya anasa kama ulevi wakati wa mchana,. Ni mtu aliyevuka mipaka, haoni tena shida kufanya mambo yake maovu hadharani amewazidi hata  wenye dhambi wengine wafanyao mambo kama hayo.Ndivyo walivyofanya watu wa Sodoma na Gomora, walivuka mipaka waliuanika ushoga wao hadharani, bila aibu yoyote.

Ni kama vile tu leo hii, hakuna staha tena duniani, mambo ya giza yanafanyika wazi kwenye matamasha, kwenye TV, yanatumwa Whatsapp, yanaonekana Youtube na kwenye mitaa yetu.

Hii ni kuonyesha kuwa tunaishi katika majira ya kurudi kwa pili kwake Yesu Kristo. Wakati huu ni wa kuilinda mioyo yetu isilemewe na mambo ya kidunia, kama alivyofanya Lutu alivyokuwa Sodoma. Kwasababu ulimwengu huu utakwenda kuangamizwa kwa moto muda si mrefu, kama mtume Petro alivyomalizia kusoma katika waraka huo.

2Petro 3:10 “Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.

11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,

12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?”

Je umeokoka? Je parapanda ikilia leo unaouhakika wa kwenda mbinguni?. Majibu sote tunayo.

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

KURUDI ISRAELI KWASASA NI KUGUMU, SIO KAMA KULE MWANZONI.

Isaya 10:22 “Maana watu wako, Ee Israeli, wajapokuwa wengi kama mchanga wa pwani, ni mabaki tu watakaorudi; kuangamiza kumekusudiwa, kunakofurika kwa haki”.

Wana wa Israeli walidhani, kuchukuliwa tena utumwani na kurudishwa (Babeli na Misri)  kungekuwa ni kurahisi kama ilivyokuwa wakati ule walipotolewa Misri. Walidhani Mungu atakuja kuwatoa tena kama taifa kwa mkono hodari wa nabii kama Musa, na wote watarudi nchi yao.

Lakini mambo hayakuwa hivyo, Mungu aliwaonya mapema akiwaambia hilo jambo halitakuwepo, na ndio maana alitumia muda mrefu sana kuwasihi, watubu waache njia zao mbaya, lakini hawakusikia badala yake wakawa wanawapiga manabii wake na wengine kuwaua,

Lakini siku ya siku ilipofika, yale mataifa 10 yalichukuliwa utumwani Ashuru,  na biblia inatuonyesha hakuna hata mmoja aliyerudi hadi wakati huu wa sasa.. watu wote waliendelea kubaki kule kule,  hata na lile taifa moja la Yuda, ambalo lilikuja kuchukuliwa nalo baadaye Babeli na Nebukadreza, japokuwa nalo lilikuwa na watu wengi sana, lakini ni kikundi kidogo sana, yaani watu wachache sana ndio Mungu aliwarudisha, na hiyo ilikuwa tu ni kuwatunzia uzao vinginevyo wangefananishwa na Sodoma na Gomora, kwa jinsi ambavyo wangepotea wote.

Warumi 9:27 “Isaya naye atoa sauti yake juu ya Israeli, kusema, Hesabu ya wana wa Israeli,ijapokuwa ni kama mchanga wa bahari,ni mabaki yao tu watakaookolewa.

28 Kwa maana Bwana atalitekeleza neno lake juu ya nchi, akilimaliza na kulikata.

29 Tena kama Isaya alivyotangulia kunena, Kama Bwana wa majeshi asingalituachia uzao, Tungalikuwa kama Sodoma, tungalifananishwa na Gomora”.

Sasa biblia inasema mambo hayo yaliandikwa kwa mifano ili kututahadharisha na sisi tulio katika nyakati hizi za hatari (1Wakorintho 10:11). Kwasababu kanisa la Israeli la mwilini lilikuwa linawakilisha kanisa la Kristo la rohoni sasa hivi. Kumbuka mara baada ya Israeli kuingiliwa na ukengeufu,  pale walipoanza kuabudu miungu mingine, hapo ndipo Mungu alipokusudia kuwaangamiza wote, mikononi mwa maadui zao.

Vivyo hivyo na katika Kanisa la Kristo leo hii, Bwana alishatabiri kuwa kuwa kuna majira litaingiliwa na ukengeufu..ndio yale magugu yaliyopandwa na ibilisi ndani ya kanisa (Mathayo 13:24-30).. Sasa ukengeufu huu, ndio unaowafanya wakristo wengi wawe vuguvugu kupita kiasi, Hatushangai kuona idadi ya watu wanaojiita wakristo duniani ikizidi kuongezeka, sasa hivi ni Zaidi ya bilioni tatu.. Ni kama mchanga wa bahari tu, hata zaidi ya walivyokuwa Israeli.

Lakini hiyo sio tija kwamba wote tutaokolewa siku ile.  Ni mabaki tu ndio yatakayookoka, ambayo Yesu aliyafananisha na ‘kundi dogo’

Luka 12:32 “Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme”.

Na ndio maana Bwana Yesu alisema. Walioitwa ni wengi lakini wateule ni wachache. Hichi ni kipindi cha kurekebisha mienendo yetu kama wakristo, kwasababu kurudi Yerusalemu kwa sasa ni kugumu sio kama kule kwa kwanza. Nguvu ya kukuvuta umgeukie Mungu sasa sio kama ile ya kwanza ulipoanza kuamini.

Ni wachache tu ndio watakaorejea, na sisi tuwe miongoni mwa hao. Mungu anatuita kuache dhambi, tumgeukie yeye, tusiungalie ulimwengu, kwani unapoteza sana.. Kwasababu hizi ni nyakati za mwisho na Kristo yupo mlangoni, wakati huu ni ule wa kumalizia, siku yoyote, wakati wowote, tunaweza kushuhudia tendo hilo kuu la unyakuo. Ambapo kwa upande mmoja utakuwa ni furaha na shangwe, lakini kwa upande mwingine kilio na kusaga meno na majuto makubwa.

Bwana atusaidie.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Ni nani aliyesema “Nitume mimi”? katika (Isaya 6:8)

PINDO LA VAZI LAKE SASA LIMEREFUSHWA.

JE UPENDO WAKO UMEPOA?

Fuawe ni nini? Kama tunavyosoma katika Isaya 41:7

EPUKA KUUNDA MATARAJIO YAKO, KWENYE AHADI ZA MUNGU.

Rudi nyumbani

Print this post

Amri zilizo ndogo alizozizungumzia Yesu ni zipi?

SWALI: Tukisoma  Mathayo 5:19 Inasema..

“Basi mtu ye yote atakayevunja AMRI MOJA katika hizi ZILIZO NDOGO, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu ATAKAYEZITENDA na KUZIFUNDISHA, huyo ataitwa MKUBWA katika ufalme wa mbinguni”.

Swali langu 👆Amri ndogo zinazozungumziwa hapo ni zipi? Ningependa kuzijua!

Kama kuna Amri ndogo ,bila shaka na Amri kubwa au kuu zitakuwepo pia ningependa kufahamu hilo.

Asante na Mungu awabariki kwa majibu yenu.


JIBU: Ukisoma maneno ya juu yake yaliyotangulia utaona anasema.. sikuja kuitangua torati bali kuitimiliza, Hii ikiwa na maana kuwa vipo vipengele vya torati ambavyo havikukamilika, au havikueleweka kwa wengi ndio sasa yeye akaja kuviweka sawa, na kuvimalizia..

Sasa kwa wayahudi (Yaani mafarisayo  na waandishi) waliona kama ni sheria mpya Yesu anawaletea watu, sheria ambazo Musa hakuziandika, visheria vidogo vidogo ambavyo si lazima mtu kuvishika, japo vinaelezea uhalisia.

Kwa mfano Musa aliwaagiza wasizini, lakini jambo lingine lolote linalohusiana na uzinzi, kama vile kutazama pornography, au kufanya masturbation ni sawa, lakini Yesu alipokuja na sheria mpya kwamba kila amtazamaye mwanamke kwa kumtamani ameshakwisha kuzini naye.. Waliona kama ni jambo la ziada  (kama sheria ndogo tu), lakini hawajui kuwa mtu ambaye atazishika hizo ndizo zitakazomfanya awe mkubwa sana katika ufalme wa mbinguni.

Vilevile Musa alisema usiue, lakini Bwana Yesu akasema mtu atakayemwonea ndugu yake hasira tayari ni muuaji. Hivyo hatupaswi kuwekeana  vinyongo sisi kama ndugu, haijalishi tumeudhiana sana kiasi gani. Sasa ikitokea unapuuzia maneno haya, ujue kuwa katika ufalme wa mbinguni unaonekana ni mdogo sana, haijalishi kuwa hujawahi kufikiria hata kuua.

Musa alisema Jicho kwa jicho, na jino kwa jino, lakini Yesu alisema, tusishindane na watu waovu, mtu akupigaye shavu la kuume mgeuzie na la kushoto.

Musa alisema, usiape uongo, lakini Yesu alisema usiape kabisa kwa kiapo chochote.

Alisema tena mpende jirani yako, mchukie adui yako, lakini Yesu alisema wapendeni adui zenu waombeeni wanaowaudhi..n.k n.k.

Sasa amri kama hizo za Yesu  zilionekana ni ndogo hivyo zikadharauliwa, wengi wakawa hawazishiki, ni sawa na leo hii tu, mtu akuambie umuombee adui yako, ni jambo ambalo unaweza ukalidharau, na ndio maana huwezi kulisikia kwenye vinywa vya watumishi, vilevile ni ngumu kuviona watu wakiviishi, zinapuuziwa lakini ndizo zinazotupa ukubwa mbinguni.

Ndio maana Yesu alisema pale juu.. “Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni”(Mathayo 5:20).

Akiwa na maana tukiyatenda tu yale ambayo watu wa dini wanayatenda kwa desturi na mazoea, hatuna cha ziada ndani yetu, tujue kuwa mbinguni hatutaingia.

Nasi tunafundishwa, tuyashike kwa kuyaishi na kuyafundisha, sana hayo maagizo ya Yesu, ambayo ndio yanayokamilisha torati nzima. Soma  kitabu Mathayo sura ya 5 mpaka ya 7 utapata maagizo hayo yote kwa urefu.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

TUTAMKARIBIA MUNGU KWA IDADI YA MVI ZETU ROHONI.

Shalom, nakukaribisha katika kuyatafakari maneno ya uzima, biblia inatuambia..

Mithali 16:31 “KICHWA CHENYE MVI NI TAJI YA UTUKUFU, Kama kikionekana katika njia ya haki”.

Wengi wetu tunatafuta wokovu ili tu tuende mbinguni,  tunadhani wokovu ni kumkiri tu Yesu na kubatizwa, basi imeishia hapo, tunachosubiria tu ni  kufa na kwenda mbinguni.. Ndugu Mawazo kama hayo ndiyo yanatufanya kila siku tuwe watu wa kulegea legea watu wa kusubiri subiri, tukisema siku moja wataokoka, siku tunayokaribia kufa, siku ambayo tukishatimiza malengo yetu ndio tutakayomtumikia Mungu, hatujui kuwa kuchelewa kwetu kunatupotezea nafasi nyingi na kubwa sana mbinguni.

Ndugu yangu, maisha ya mwilini ni kivuli tosha cha maisha ya rohoni. Kama vile katika mwili kuna hatua, ya utoto, utu uzima na uzee, na kwamba ili mtu afikie ile ya mwisho ni lazima azipitie hizi za kwanza zote, vivyo hivyo na rohoni..

Kumbuka Uzee siku zote una kibali, una heshima,  na una utukufu,

Biblia inasema..

Walawi 19:32 “Mwondokeeni mtu mwenye mvi; heshimuni uso wa mtu mzee; nawe mche Mungu wako, Mimi ndimi Bwana”.

 Unaona na utukufu wake unadhihirishwa kwa zile mvi zinazotokea juu ya kichwa chake. Hali kadhalika rohoni, kwa jinsi mtu anavyokua kiroho, anavyodumu katika wokovu, anavyomtumikia sana Bwana, ndivyo mvi zake zinavyoongezeka kidogo kidogo, na kwa jinsi atakavyoendelea kung’ang’ana na Bwana atafikia  hatua kichwa chake chote kinajaa mvi, kinakuwa cheupe pe chote.

Ukishafikia hatua hiyo rohoni, ujue wewe ni mtu ambaye utakuwa karibu sana na Mungu utakapofika mbinguni.

Ukisoma kitabu cha Ufunuo, utawaona kuna wazee 24 mbinguni, Wale ni malaika wa Mungu, ambao wanafanana na wanadamu wazee, utajiuliza ni kwanini Mungu kawaweka pale kama wazee  na si vijana au watoto ili wakizunguke kiti chake cha enzi, tena wakiwa katika idadi yao hiyo ndogo ya 24?. Hiyo ni kuonyesha kuwa watu wa namna hiyo, ndio watakaokuwa karibu sana na Mungu hata wakati ule ukifika.

Ufunuo 4:3 “na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi.

4 Na viti ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wanne, wameketi, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu”.

Na kama tunavyojua ili kumtambua mzee  utaona mvi nyeupe katika kichwa chake. Katika biblia tunamwona Bwana wetu Yesu Kristo akiwa kama mzee wetu wa kwanza rohoni mwenye nywele hizo nyeupe..

Ufunuo 1:14 “Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto”;

Sasa kama tulivyosema, mpaka mtu afikie hatua ya uzee, ni sharti kwanza apitie utoto na ujana,..Vivyo hivyo rohoni ili tufikie ukomavu Mungu anaoutarajia kwetu hatuna budi kuukulia wokovu vya kutosha angali tukiwa hapa hapa duniani.

Inashangaza kuona mtu anayachukulia maisha yake ya rohoni, kirahisi rahisi tu, leo inapita bado yupo katika dhambi, kesho nayo hivyo hivyo, mwezi unapita, miaka inapita, anasikia tu injili anapuuzia, bado hajali maisha yake ya milele yatakuja kuwaje huko atakapokwenda, yeye anajitaabisha tu na haya maisha ya kitambo ya miaka 80, lakini yale ya mabilioni ya miaka hayaangalii. Anadhani kule ni kufa na kuingia tu, hajui kuwa zipo nafasi na vyeo, ambavyo si watu wote watapewa na Mungu.

Mwingine atasema ameokoka, lakini miaka nenda rudi, bado ni mchanga kiroho, hakui yupo pale pale, maisha yake hayana ushuhuda, ukimuuliza ni nini umefanya kwa Mungu wako, hana, yeye ni kusikiliza tu, basi, akidhani ndicho Mungu alichotuitia hapa duniani.

Tunapaswa tukifika kule tutambuliwe kwa mvi zetu rohoni, tumemtumikia Mungu wetu kweli kweli, sio tunatambuliwa kama vitoto vichanga tena.

Unapoyasikia maneno haya, usiyapuuzie, kumbuka unapaswa uwe ndani ya Kristo ukimtumikia kwa muda wa kutosha ukiwa hapa duniani, ili ujijengee daraja zuri kule unapokwenda, usidhani wokovu ni kuamini tu basi..wokovu ni maisha, kila siku unajenga maisha yako ya baadaye, kama vile unavyojijengea maisha yako ya mwilini.

Hivyo mimi na wewe kuanzia sasa, tutamani kuwa karibu na Mungu, kwasababu tukifa kule tutatambuliwa kwa idadi ya mvi zetu rohoni.

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

Bwana Yesu alimaanisha nini kusema “yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari?”

SWALI : Shalom .. Tukisoma Mathayo 5:43-45 Inazungumzia juu ya mtu ili awe mkamilifu hana budi kumjali mwingine hata kama Anatukosea,kwamba sisi tumeambiwa tuwaombee tuwapende N.K..Sasa tukisoma tena Mathayo 18:6..Inasema Hivi..

“Bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari.”..Sasa Hapa mtumishi Sjaelewa kwenye Haya maneno aliyoyazungumzia Bwana katika huu mstari, Kwasababu Mathayo 5:43-45 inasema tuwaombee ila hapa Mathayo 18:6 inasema afadhali Afungiwe jiwe ikiwa na maana Aangamizwe..Naona pananitatiza kidogo


JIBU: Bwana Yesu alisema hivi katika Mathayo 5:43-44

“43 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;

44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,”

Bwana alimaanisha kweli kusema hivyo, kwa namna ya kawaida ukishakuwa  mwanadamu tu, mwenye kitu Fulani kipekee ndani yako, ni lazima utakuwa tu na maadui, wengine watakuwa maadui zao kutokana na wivu, aidha  wa utumishi wako, au ndoa yako, au mafanikio yako, au cheo chako, au kipawa chako, au mwonekano wako, n.k.  Na wivu huo unaweza kufikia hatua hata ya hao watu kutaka kukuua.

Lakini ukijikuta katika hali kama hiyo  wewe kama mkristo unapaswa ufanyaje? Je na wewe uwalipizie kisasi, jibu ni la hapo unapaswa tuwe kama Bwana Yesu alivyokuwa, pale ambapo walimtundika msalabani aliwaombea msamaha, pale ambapo Stefano anauliwa kwa kupigwa mawe mbele ya Paulo aliwaombea na kusema Bwana asiwahesabie kosa lile.

Umeona ni jukumu letu kuwaombea rehema.

Lakini pamoja na hayo kuna wakati mtu anafanya makosa kinyume na Mungu mwenyewe, na hiyo ni hatari zaidi, kwasababu japo Mungu  kasema yeye ni mwingi wa rehema lakini pia ni mwingi wa hasira,  Na ndio maana utasoma hapo, Bwana Yesu akisema..

Mathayo 18:6 “bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari”

Unapaswa uwe makini sana na Watu waliomwamini Bwana Yesu, hususani wale ambao ni wachanga kiroho, watu waliotubu dhambi zao na kumwelekea Bwana, kwa mioyo yao yote, halafu wewe unakwenda kuwaondoa katika mstari wa wokovu kwa namna moja au nyingine, ukifanya hivyo ujue hukumu yako ni kubwa sana.

Katika biblia utamwona mtu mmoja anaitwa Balaamu, huyu alijua kabisa wana wa Israeli wanaenda sawa na Mungu wao, sasa akatafuta njia ya kuwakosesha kwa makusudi ili wafarakane na Mungu ili waadhibiwe.. Hivyo akabuni njia ya kuwakosesha, kwa kuwaletea wanawake wa kimataifa ili wazini nao, (jambo ambalo Mungu aliwakataza wana wa Israeli)  kisha baada ya hapo Mungu awaadhibu na kuwaacha..Na kweli adhma yake ilifanikiwa, na matatizo yakawakumba kweli wana wa Israeli (Ufunuo 2:14).

Leo hii wapo watumishi wanaozini na washirika wao, mpaka imepelekea, wale wengine ambao walikuwa wameanza kuamini wameuacha wokovu, kutokana na matendo mabaya ya viongozi wao. Sasa watu kama hawa wanamudhi sana Mungu, hawajui tu. Mpaka kufikia hatua kama hiyo ya Mungu kusema..ingemfaa zaidi mtu kama huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake akatupwe baharini… Ni Kuonyesha kuwa hukumu yake ni kubwa sana…Hata akifungiwa jiwe kubwa na kwenda kutupwa kwenye vilindi vya bahari kwa tendo hilo bado Mungu anaona ni sawa tu, amestahili.

Lakini swali ni je! Kwa ruhusu hiyo, tukawafungue watu mawe shingoni? Jiulize Wewe unaweza kufanya hivyo? Unaweza kudhubutu kumtupa mwanadamu mwenzako baharini? Au ulishawahi kufanya hivyo?. Kuna wakati Mungu alikuwa anamwambia Musa kwa hasira kwamba ajitenge na wana wa  Israeli ili awaangamize kwasababu wamemwacha upesi na kugeukia kuabudu masanamu. Na yeye atamfanya kuwa taifa kubwa.

Lakini Musa alizituliza hasira za Bwana, akawaombea rehema, Sio kwamba angekubali Mungu asingetimiziwa aliyoahidiwa, angetimiza kweli, Mungu angeenda kumfanya kuwa taifa kubwa, na yeye angekuwa mfalme juu yao, lakini bado asingekuwa mkamilifu mbele za Mungu. Na ndio maana mtu kama Musa alipata kibali cha kipekee sana mbele za Mungu.

Kumbukumbu 9:12 “Bwana akaniambia, Ondoka huko, shuka upesi; kwa kuwa watu wako uliowatoa Misri wamejiharibu; wamekengeuka mara katika njia niliyowaamuru; wamejifanyia sanamu ya kusubu.

13 Tena Bwana akasema nami zaidi, akaniambia, Nimeliona taifa hili; na tazama, ni taifa lenye shingo ngumu;

14 niache, nipate kuwaangamiza, na kulifuta jina lao chini ya mbingu; nami nitakufanya wewe uwe taifa kubwa lenye nguvu kuwapita wao”.

Nasi pia, Tunapaswa tuitulize hasira ya Mungu, kwa kuwaombea rehema, na Sio kwa kuitekeleza.

Maombi ya kuwaangamiza maadui zetu, tunapaswa tujue kwa mkristo, hayana nafasi.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

NITAFANYA YERUSALEMU KUWA JIWE LA KUWALEMEA .

Kongwa ni nini kwenye biblia?(Wagalatia 5:1)

Kwanini wale dubu waliowauwa vijana wa Elisha walikuwa wa kike?

Kwanini Yesu aliwakataza mitume wake kumdhihirisha?

KWASABABU MUDA TULIOBAKIWA NAO SI MWINGI.

NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.

Rudi nyumbani

Print this post

Nini maana ya kuruzuku katika biblia?

Maana ya Neno “kuruzuku” ni “kutoa Riziki”. Unapompa mtu mwingine riziki hapo umemruzuku. Katika biblia tunaona neno hilo limetokea mara kadhaa Mungu akiwaruzuku watu.

Katika kitabu cha Nehemia tunaona Neno hilo likitajwa..

Nehemia 9: 21 “Naam, muda wa miaka arobaini uliwaruzuku jangwani, wasihitaji kitu; nguo zao hazikuchakaa, wala miguu yao haikuvimba”.

Na pia tunaliona neno hilo katika kitabu cha Zaburi.

Zaburi 65:9 “Umeijilia nchi na kuisitawisha, Umeitajirisha sana; Mto wa Mungu umejaa maji; Wawaruzuku watu nafaka Maana ndiwe uitengenezaye ardhi”.

Na mwisho tunaona neno hilo katika kitabu hicho hicho cha Zabur 68,

Zaburi 68:10 “Kabila yako ilifanya kao lake huko; Ee Mungu, kwa wema wako uliwaruzuku walioonewa”.

Kama Bwana alivyowaruzuku wana wa Israeli Jangwani, mahali ambapo hapakuwa na kilimo wala maji, lakini Mungu wa mbingu na nchi akawapa MANA kutoka mbinguni na maji kutoka mwambani, na nyama kimiujiza, akakupe na wewe mtu wa Mungu uliyempokea na kumwamini Yesu Kristo, riziki zote za mwilini na rohoni. Akakuruzuku kwa riziki nyingi katika jina la Yesu.

Amen

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji zilikuwaje?

NAWAAMBIA MAPEMA!

NAWE UTAGEUZWA KUWA MTU MWINGINE.

 Nini maana ya “Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati”

Rudi nyumbani

Print this post

Maziwa yasiyoghoshiwa ni nini? Kwanini biblia inatumia mfano huo?

1Petro 2:1 “Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote. 2 Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu”;

Kughoshi ni kugeuza, au kutia dosari, lengo likuwa ni kukifanya kionekane kama kile cha kwanza, leo hii utasikia maneno kama ‘vyeti vimeghoshiwa’, maana yake ni kuwa wametengeza vyetu bandia ili waonekane kama na wao ni wahitimu kumbe ni uongo. Utasikia tena watu pia ‘wanaghoshi fedha’, maana yake ni kuwa wanatengeneza fedha bandia ili zionekane kama zile halisi, zifae kwa manunuzi.

Sasa mtume Petro aliposema yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, alitumia mfano wa maziwa yanyonywao na watoto wachanga kufananisha na Neno la Mungu. Kwamba maziwa yale kwa asili huwa hayagoshiwi, hayatiwi kitu kingine chochote, wala hayaingiliwi na uchafu wowote, kwani mtoto hujafyonza moja kwa moja kutoka kwa mama yake.

Lakini kama vile leo hii utaona mambo yamebadilika watoto wachanga hawapewi tena maziwa  yanayotoka moja kwa moja katika matiti ya mama zao, badala yake wanakwenda kuletewa maziwa mengine ya kwenye makopo, ya ng’ombe, ambayo kwa kutazama unaweza kuona yanafanana sana na yale ya mama,  lakini kumbe yapo mbali sana kiubora na kiafya kwa mtoto mchanga.  Utakuta hayo ya kwenye makopo yamechanganywa na vitu vingine wanavyoviita virutubisho, na kemikali baadhi za kuyafanya yasiharibike mapema..Sasa maziwa hayo ni maziwa yaliyoghoshiwa. Mtoto ananyweshwa kama mbadala wa maziwa halisi ya mama yake, na kamwe hayawezi kuwa na ubora ule ule kama wa yale ya mama.

Vivyo hivyo na sisi kama wakristo, tunapaswa tuyafyonze maziwa yanayotoka moja kwa moja kwa Mungu wetu mwenyezi, yanayotoka katika maandiko matakatifu (yaani BIBLIA), hayo ndio matiti yetu. Ili tuukulie wokovu katika afya njema za rohoni Mungu anazozihitaji.  Lakini kama tutataka tuikulie injili nyingine ambayo si ile tunayoisoma katika maandiko tufahamu, tunajidhohofisha wenyewe.

Na ndio hapo, utashangaa kwanini mkristo anashindwa kusimama vema katika Imani, leo yupo sawa kesho kaanguka katika dhambi, utakuta mwingine yupo katika kanisa kwa miaka mingi, lakini ukitafuta matunda yoyote kwa Mungu wake hana, ukitafuta ni wangapi alishawahi waleta kwa Kristo, hupati, hayo yote ni matokeo ya kunywa maziwa ya aina nyingine yasiyomtia mtu nguvu rohoni.

Ukiona unakaa mahali na kuhubiriwa injili ya mafanikio tu wakati wote,  auhubiriwi utakatifu, au mambo ya ufalme wa mbinguni na siku za mwisho, ujue kuwa hayo ni maziwa ya kughoshiwa, yanayofanana na yale halisi, hayatakusaidia chochote katika kuushinda ulimwengu.

Lakini mtume Paulo anasisitiza kwa kusema..‘Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu’

Unaona ni wajibu wetu kuitamani injili ya kweli, injili ile iliyoandikwa na mitume kwenye biblia, ili kwamba tuweze kuukulia wokovu wetu vema inavyostahili, tusishindwe na shetani kivyepesi, pia ili tuwe watu wa kumzalia Mungu matunda katika ukristo wetu.

Kumbuka hizi ni siku za mwisho, mafundisho mengi ya uongo yameenea sasa ulimwengu mzima, na ndio maana Bwana Yesu alituonya na kusema .ANGALIE JINSI MSIKIAVYO (Luka 8:18)..Akiwa na maana tuwe makini na yale tunayohubiriwa kwasababu si yote yanajenga roho zetu.Mengi ya hayo ni feki, yanatia ubovu roho zetu.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA PILI WA YOHANA.

MAMA UNALILIA NINI?

Bwana Yesu alimaanisha nini kusema “Saa yangu haijawadia?”

Je! Daudi hakuwa mtoto wa ndoa wa Yese? (Zab 51:5)

MAPEPO YANATAFUTA HIFADHI NDANI YAKO KWA BIDII SANA.

Je ni kweli imani ya mtu ndiyo itakayomuokoa, na si kitu kingine?

Rudi nyumbani

Print this post

Je ni kweli imani ya mtu ndiyo itakayomuokoa, na si kitu kingine?

JIBU: Kama ulishawahi kuwahubiria watu kadha wa kadha habari za wokovu, naamini ulishawahi  kukutana na watu baadhi wakikueleza, maneno haya, kwamba haijalishi wewe ni dini gani, au unaamini nini, imani yako ndiyo itakayokuokoa, ukiwa na imani kuwa  Mungu  yupo, hilo tu, linakutosha, hayo mengine si ya muhimu sana.

Atakuambia hata anayeabudu kupitia mti, au anayeabudu kupitia ng’ombe Mungu anamsikia hata, anayeabudu kupitia Rozari Mungu anamsikia kinachojalisha ni imani yake tu wala si kingine.

Ni kweli kabisa mawazo yao ni sahihi, kwamba imani ni daraja la kumfikia Mungu, kama vile maandiko yanavyosema katika..

Waebrania 11:6 “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”.

Lakini hawajui kuwa Imani ambayo haijakamilishwa haikufikishi popote, nikiwa na maana imani ambayo haijulikana msingi wake ni upi, imejengwa katika nini  haikupeleki popote.. Kitendo cha kuamini tu Mungu yupo, hata wachawi wanaamini hivyo, na ukiwauliza watakuambia ndio namwamini Mungu na pia ananisaidia, mapepo nayo yatakuambia sisi nasi tunamwamini Mungu na pia tunatetemeka tunapolisikia jina lake..

Utalithibitisha hilo katika..

Yakobo 2:19 “Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka”.

Sasa kama unasema mimi naamini Mungu, na namwogopa, ujue kuwa huna tofauti na mashetani. Kama unadhani utakwenda mbinguni kwa imani ya namna hiyo, basi ujue mashetani watakutangulia kwanza mbinguni kisha wewe utayafuata baadaye.

Bwana Yesu alisema wazi kabisa katika Yohana 14:6..”mimi ndio njia na kweli na uzima, mtu hafiki kwa Baba isipokuwa kwa njia yangu mimi.” Akiwa na maana hakuna imani yoyote itayokufikisha mbinguni isipokuwa ile ya kumwamini yeye (Yesu Kristo).

Ni sawa na leo useme unayo simu, yenye line nzuri, yenye salio la kutosha, hivyo unaweza sasa kuwasiliana na mimi wakati wowote.. Jibu ni la! kama hutakuwa na namba yangu ya simu, kamwe hutakaa  uwasiliane na mimi.. Haijalishi utakuwa na simu nzuri, au salio la kutosha au namba za watu wengine elfu kwenye kitabu chako cha kumbukumbu, kama huna namba yangu mimi binafsi, kamwe huwezi kuwasiliana na mimi.

Leo hii watu wanataka kuwasiliana na Mungu, kwa njia zao wenyewe walizojitungia, wanajaribu kupiga kila namba wanayoibuni tu vichwani mwao, wengine wanamtafuta Mungu kupitia dini zao, wengine wadhehebu yao, wengine wanyama, wengine miti,sanamu, jua, mwezi, n.k. wakidai kuwa wanamtafuta Mungu Yule Yule mmoja, ukiwaeleza dini au dhehebu halikufikishi popote, watakuambia usitupotoshe, imani yako ndio itakayokuokoa..

Ndugu, usipomuamini Yesu, hutafika popote. Na kumwamini Yesu sio kusema mimi ni mkristo, au mimi namwamini Yesu, hapana, bali kunakuja kwa kutubu kwanza dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha, pili kwa kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji tele katika jina lake sawasawa na Matendo 2:38, Kisha kupokea Roho Mtakatifu. Na kuanzia hapo kuishi maisha matakatifu yanayoendana na Neno lake,(yaani BIBLIA). Sasa Kwa kufanya hivyo imani yako itakuwa imekamilishwa mahali sahihi. Hapo ndipo utakuwa na uhakika unamwabudu Mungu kweli, kupitia mwana wake Yesu Kristo.

Lakini kwa kusema tu mimi namwamini Mungu, imani yangu itaniokoa na huku hujui Mungu kakuagiza nini katika Neno lake, au anakutaka ufanye nini..Ujue kuwa umepotea, na ukifa leo utakwenda kuzimu. Vilevile ukijivunua dhehebu lako, na hutaki kumtafuta Kristo Yesu aliye njia, ujue kuwa kuzimu itakuwa pia ni sehemu yako. Hakuna njia za kubuni buni katika kumfikia Mungu.. Ni sharti umwamini Yesu, na kuoshwa dhambi zako na yeye.

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

CHANGIA SASA.

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1

NITAUPATAJE UPENDO WA KI-MUNGU NDANI YANGU?

Nini maana ya “kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi?”

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Rudi nyumbani

Print this post

Nini maana ya “wanawake saba watamshika mtu mume mmoja”

SWALI: Isaya 4:1 na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, tutakula chakula chetu na kuvaa nguo zetu wenyewe lakini tuitwe  tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu. Je; andiko hili linamaanisha nini?


Kwanini wanawake? Kwanini wawe saba? Kwanini chakula chao na nguo zao na sio za mume wao? maana yake mume akioa moja ya majukumu ya kwake kufanya kwa mkewe ni kumlisha na kumvika sasa hawa wanakula na kuvaa vya kwao ni kitu gani hawa wanawake?

JIBU: ufunuo wa mstari huo ni huu..wanawake saba ni makanisa saba (katika vipindi saba vya kanisa kama inavyooneka katika ufunuo 2 & 3)..

Mtu mume mmoja ni Yesu Kristo,.Lakini hao wanawake wote 7 wanasema watakula chakula chao wenyewe na kuvaa nguo zao wenyewe bali waitwe tu kwa jina la yule mtu mume mmoja ambaye ni Yesu Kristo.Jambo hili la kusema tutakula chakula chetu na kuvaa nguo zetu wenyewe ni tabia za hayo makanisa yote 7 yalivyokuwa, kila kanisa lilikuwa na tabia yake pekee, na yote yanatafuta kumpendeza Yesu Kristo lakini kwa njia zao wenyewe,

kwahiyo hicho “chakula” kinachozungumziwa hapo ni mapenzi yao wenyewe, na mienendo yao wenyewe hawataki chakula cha Bwana wao,(ambalo ni neno la Kristo lisiloghoshiwa), wala hawataki “mavazi” ya Bwana wao (Ambao ni utakatifu na matendo mema soma ufunuo 19:8,) bali waitwe tu kwa Jina la Bwana Yesu aibu yao iwaondoke hii aibu ina maana waiepuke hukumu itakayokuja na ndio maana yale makanisa yote hayakuweza kuoana na Kristo kikamilifu yalikuwa na mapungufu yake, na sisi pia tupo katika kanisa la mwisho la saba la LAODIKIA ni kanisa vuguvugu, na ndilo lililomkinai Bwana wake kuliko mengine yote yaliyotangulia soma..

ufunuo 3:14-22,”14 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.

15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.

22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.”

Lakini tunapaswa wote tushinde ili tuvuke kutoka kuwa masuria na kuwa bibi-arusi safi wa Yesu Kristo waliokubaliwa tayari kwenda kwenye arusi ya mwanakondoo itakayofanyika mbinguni kwa Baba. Kumbuka bibi-arusi sio sawa na suria. Kwahiyo ndugu watakaoshiriki karamu ya mwanakondoo ni bibi-arusi tu, je! wewe ni bibiarusi? umepokea Roho Mtakatifu? umejiweka tayari kumpokea Bwana wako atakaporudi? matendo yako yanastahili wokovu? jibu lipo moyoni mwako. Tubu sasa umgeukie Bwana kumbuka tunaishi kizazi ambacho kitashuhudia kuja kwa pili kwa Kristo.

ufunuo 19: Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.

Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

KWANINI UNAPASWA UWE BIBI ARUSI NYAKATI HIZI ZA MAJERUHI?

NAMNA YA KUMTAMBUA BIBI ARUSI WA KWELI WA KRISTO.

Rudi Nyumbani:

Print this post