Luka 21:34 “Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo; 35 kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima”
Luka 21:34 “Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo;
35 kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima”
Shalom, Jina kuu la mwokozi wetu Yesu libarikiwe daima.
Wengi tunayafahamu maneno hayo ya Bwana, lakini hatujui ni ulevi na ulafi wa namna gani unaozungumziwa katika Habari hiyo mpaka siku hiyo iwajilie ghafla, kama mtego unasavyo..
Ili kupata picha embu tutazame mfano mmoja halisi kabisa wa kwenye biblia na jinsi walivyolemewa na ulafi na ulevi wa kipekee mpaka, mwisho wao ulipowakuta kwa ghafla..
Sasa kama tukisoma kile kitabu cha Danieli sura ya 5, tunamwona mfalme mmoja aliyejulikana kwa jina la Belshaza, huyu alikuwa ni mtoto wa Nebukadreza, kama wengi tunavyoifahamu Habari, ni mtu ambaye alibahatika kuona mambo yote ambayo Baba yake aliyoyapita na jinsi alivyoadhibiwa kutokana kiburi chake na ukatili wa kutesa watu wasiokuwa na hatia na wengine kuwatupa katika matanuru ya moto, kama sio kuwachinja, lakini baadaye Mungu alikikomesha kiburi chake, kwa kumng’oa katika ufalme wake, akawa anaishi misituni kama sokwe Fulani tu, mpaka miaka 7 ilipoisha, na pale alipogundua kuwa Mungu ndiye anayetawala dunia nzima, na kwamba yeye ndio anatakiwa aogopwe ndipo akatubu na kumgeukia Mungu na Mungu akamrehemu na akamrejeshea enzi yake kupita kiasi hata kuliko pale alipokuwepo mwanzo.
Sasa huyu mtoto wake aliyeitwa Belshaza, alikuwa anayaona hayo yote, na alikuwa ameshapata somo kamili ambalo haikumpasa yeye tena alipitie kwasababu babayake tayari ameshafanyika mfano..Kama tu vile sisi, watu wa kizazi hiki, tayari mifano mingi ilishatangulia mbele yetu huko nyuma, mfano ile ya watu wa Nuhu, na Watu wa sodoma na Gomora, jinsi walivyoangamizwa kwa maovu yao, lakini sasa tunaona na kuzipuuzia, na kuzichukulia tu kama Habari zilizopitwa na wakati kama tu huyu mtoto wa Nebukadreza.
Yeye alipuuzia yale yote ambayo Baba yake aliyotendewa na Mungu.. Na kibaya Zaidi akaamua kuchukua hatua nyingine mbaya kuliko zote, ambayo ndiyo iliyompelekea hata Mungu kumwangamiza kwa ghafla na kwa haraka sana..Na hicho ndicho wote tunachopaswa tujifunze leo hii.
Alichofanya ni kuchukua vile vyombo vya hekaluni, ambavyo baba yake alivichukua kutoka Yerusalemu, alipouteketeza mji na hekalu, na kuvihifadhi asivitumie kwa kitu chochote kwasababu vilikuwa ni vitakatifu, lakini yeye (huyu Belshaza), akawa mlevi, na mlafi wa kupindukia, akawa anafanya karamu, akaona kuwa haitoshi kunywea vyombo vyake mwenyewe, chupa zake za vilabu vyake, na kutumia visu vyake vya kifalme kuchinjia nyama zake, na hata sahani zake akaona hazitoshi kuzitumia kuwekea vyakula vyake haramu…
hivyo akaenda kwenye hazina ya baba yake, na kupekua pekua na kuvikuta vile vyombo vya hekaluni ambavyo vilikuwa vimefunga na kuhifadhiwa visitumike, yeye akavichukua vile vyombo vitakatifu vya Mungu, akaanza kuvinywea na kuvilia yeye Pamoja na wakuu wake, na makahaba wake..Unaweza kuona Ni uvunjifu wa heshima kiasi gani.?? Hayo ndio mambo yanayoendelea katika roho sasa hivi..
Na alipomaliza kufanya vile tu, saa hiyo hiyo kiganja cha mkono kikatokea, kikasogea mpaka ukutani mahali ambapo mwanga ulikuwa unapiga, akaona kikiandika maneno yale, MENE, MENE, TEKELI NA PERESI.. Kama tunavyoijua habari maneno yale yalikuwa ni Hukumu, kwamba mwisho wake umeshafika, ufalme wake ndio umeishia pale..
Sasa huyu Belshaza, utaona tena aliposikia vile badala atubu, ndio kwanza anafikiria kumpandisha Danieli cheo, na kumfanya awe mkuu, unajua ni kwanini?.. Ni kwasababu alidhani, jambo hilo haliwezekani kutokea kwake, na hata kama likiwezekana basi litakuwa ni jambo la baadaye sana, kwasababu mji wake wote ameshauzungushiwa kuta kubwa sana pande zote, ambazo juu yake wapo walinzi wamekaa wakiangalia malango yake usiku na mchana yenye askari waliobebea wenye sifa dunia nzima, (kwasababu kipindi hicho Babeli ndio iliyokuwa inatawala dunia nzima)..
Hivyo Habari hizo za Danieli hazikumwogopesha hata kidogo, akiangalia kuwa hayo mataifa ambayo ameambiwa yatakuja kuuchukua ufalme wake, yaani umedi na uajemi ni vitaifa vidogo, visivyokuwa na nguvu, hivyo akawa hana hofu tena..
Lakini ndivyo alivyojidanganya..Biblia inasema usiku ule ule, alivamiwa na kuuliwa, na ufalme wake kuchukuliwa kirahisi na Wamedi na Waajemi, ni jambo la ghafla sana..utajiuliza wale watu walitokea wapi asipate Habari siku zote..
Ili kufahamu ukirudi katika historia inasema, ule mji wa Babeli ulikuwa na mto mkubwa ambao ulikuwa unaingiza maji katika mji, sasa kwa namna ya kawaida, maji yanayoingia katika mji hayawezi kuwekewa kuta, hivyo pale pale kwenye maingilio ya mto ule ndipo hapo hapo Wamedi walipokuja kuingilia usiku ule, walichokifanya ni kuupindisha ule mto mbali sana hivyo maji yakapungua ndipo walipopatia nafasi ya kuuingia mji, na kuwaua watu wale kwa ghafla sana na haraka usiku ule..wakati walinzi wa mji wanaendelea kulinda mageti makubwa kule..kumbe huku kwa njia ya chini ya watu wameshaingia mjini na kuanza kuangamiza watu.
Hata leo, Kanisa la sasa limeshalemewa na ulafi na ULEVI WA ROHONI, ni heri ungekuwa ni ulevi wa kawaida, lakini ni ulevi unaotumia vyombo vya hekaluni mwa Bwana na hiyo ndiyo inayoleta ghadhabu.. Yaani watu wanapomchanganya MUNGU NA DUNIA..leo wapo kanisani, kesho disko, leo wanamwimbia Mungu, kesho shetani, leo wanashiriki meza ya Bwana, kesho wanakwenda kuzini, yaani hayo yamekuwa mambo ya kawaida kabisa, mtu kusema ameokoka, na huku, anakunywa pombe kisirisiri, anazini nje ya ndoa, anajichua, anatazama picha za ngono ni mambo ya kawaida, anakula rushwa, ana honga..
Huo ndio ulevi na ulafi Bwana Yesu aliokuwa anauzungumzia pale..
Moja ya hizi siku, dunia nzima itaingia katika mtego huo, wakati watu wakiwa katika vilele vya amani, katika furaha, ndipo mambo yatakapobadilika kwa ghafla. Hivyo ndugu, huu ni wakati wa kutengeneza uhusiano binafsi na Mungu..Dunia hii imeshaandikiwa MENE, MENE, TEKELI na PERESI..Ukizidi kung’ang’ania kwenda nao, mwisho wa siku itakuchukua kama ilivyomchukua Belshaza, Leo hii tubu itii injili, uokolewa, Usafishwa Maisha yako, Na Bwana atakusaidia kwa yale yaliyobakia.
Ubarikiwe sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
VIUNO VYENU VIWE VIMEFUNGWA NA TAA ZENU ZIWE ZINAWAKA
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
RABI, UNAKAA WAPI?
KUSUDI LA MIMI KUWEPO DUNIANI NI LIPI?
ANGALIA USIJE UKANG’OA NGANO KATIKATI YA MAGUGU.
MUNGU AKIKUPITA LEO, HAIMAANISHI KUWA HAJAKUCHAGUA.
HATA NA BARNABA PIA AKACHUKULIWA NA UNAFIKI WAO!!
Rudi Nyumbani:
Print this post
Chukua tahadhari juu ya neema ya Mungu.
Hakuna ulinzi mkubwa ambao mwanadamu anaweza kuupata kama ulinzi wa kuwa ndani ya Yesu..Kama wengi wetu tunavyojua au tulivyosikia kwamba watu wote waliompokea Yesu Kristo uhai wao unakuwa umefichwa pamoja na Kristo.(Wakolosai 3:3). Kiasi kwamba tunalindwa dhidi ya nguvu za giza na mipango yote ya Ibilisi.
Wengi wetu tunaifurahia neema hii na kutamani kuingia ndani yake lakini hatujui kuwa ikichukiliwa isivyopaswa ina madhara makubwa kuliko kitu kingine chochote tunachoweza kukijua.
Neema ya Mungu inafananishwa na nyumba ya karamu, yenye mlango…Mathayo 7:13. Sasa kama tujuavyo nyumba yoyote ile ya muhimu kama Ikulu au ukumbi wa sherehe ya muhimu sana ina mlango na vile vile ina uzio…na mara nyingi kuta zake zinakuwa zimezungushiwa uzio mwingine ambao ni wa umeme..Na kama ni nyumba yenye umuhimu mkubwa zaidi ya hayo inakuwa na walinzi wanaotembea tembea wenye silaha kuizunguka, lengo ni kuzuia watu wa wasiruke ukuta na kuingia ndani…Na ikitokea mtu akijaribu kukiuka na kuusogelea ukuta kutaka kuruka aingie ndani ndipo anaweza akajikuta kapigwa risasi au kapigwa shoti ya umeme, na hivyo hata kuweza kujisababishia kifo…Lakini ulinzi huo haujawekwa kwaajili ya kuangamiza watu, bali kulinda usalama.
Na Neema ya Mungu ni hivyo hivyo…Ipo nguvu ya ziada iwalindao wale watu walioingia ndani ya Neema ya Kristo..Nguvu hiyo ndiyo inayotulinda dhidi ya nguvu zote za giza, dhidi ya shetani na majeshi yake (mapepo na wachawi) na kila mpango mwovu wa Ibilisi..Hivyo yoyote anayejaribu kuingia kutaka kuwaharibu watu wa Mungu walio chini ya neema ya Mungu basi atakuwa anajitafutia matatizo yeye mwenyewe..
Lakini jambo lingine la kuogopesha ni kwamba ikitokea mtu aliyeko ndani ambaye tayari kashaingia ndani ya jengo hilo, akatoka na kwenda kupanda ukuta na kurukia zile nyaya za umeme zilizouzunguka ukuta, yeye naye atajeruhiwa vile vile kama sio kufa kabisa. Maumivu yale yale atakayoyasikia Yule anayetaka kuruka ukuta na kuingia ndani ndio hayo hayo atayapata Yule anayetaka kuruka na kutoka nje.
Madhara atakayoyapata mchawi anayetaka kuwadhuru watu wa Mungu, ndio hayo hayo atakayoyapata mkristo anayeuacha wokovu na kuurudia ulimwengu. Mkristo ambaye ameshaonja kipawa cha Mungu na kuburudika na neema ya Mungu, na ghafla anarudia uasherati wake, anarudia wizi wake, anarudia matusi yake, anarudia mauaji yake, usagaji wake, utoaji mimba wake, mambo ambayo alikuwa ameshayaacha machafu anayarudia tena…akidhani kwamba mkono wa Mungu ni kinyume cha wale waliopo nje pasipo kujua hata waliopo ndani ambao wanataka kutoka vile vile mkono wa Mungu upo kinyume chao.
Wengi wetu hatupendi kusikia mambo kama haya kwasababu hatupendi kuumizwa mioyo, hatupendi kusikia habari mbaya, lakini fahamu kuwa tahadhari siku zote sio habari njema, lakini zina umuhimu sana katika maisha hususani katika siku za baadaye…hata vidonge tupewacho na wataalamu wa afya ambavyo vinatumika kwa tiba, bado vina tahadhari zake…lengo la tahadhari zile sio kuwatisha watumiaji wala kuwakatisha tamaa bali kuwanufaisha zaidi.
Vivyo hivyo Neema ya Kristo inayo tahadhari…Na ni lazima kila mtu aijue tahadhari hiyo, wahubiri wengi hawaifundishi kwasababu watakosa waumini, na wao bado wanatafuta waumini…Lakini sikia leo hii mtu wa Mungu tahadhari, ili baadaye tusije kujuta, na tahadhari hii haikuhusu wewe unayesoma tu, hapana hata mimi ninayeandika inanihusu. Biblia inasema.. Waebrania 10:26 “Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; 27 bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao. 28 Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu. 29 Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?”
Vivyo hivyo Neema ya Kristo inayo tahadhari…Na ni lazima kila mtu aijue tahadhari hiyo, wahubiri wengi hawaifundishi kwasababu watakosa waumini, na wao bado wanatafuta waumini…Lakini sikia leo hii mtu wa Mungu tahadhari, ili baadaye tusije kujuta, na tahadhari hii haikuhusu wewe unayesoma tu, hapana hata mimi ninayeandika inanihusu. Biblia inasema..
Waebrania 10:26 “Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;
27 bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.
28 Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.
29 Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?”
Kama umeamua kumfuata Yesu basi umfuate kweli kweli..usiusogelee kabisa ukuta wa Neema..uwe ndani au nje ni upanga ukatao kuwili..Neno la Mungu linasema usizini…hizo ni kuta!..neno linasema usiibe, usiue hizo ni kuta..ukipanda na kuzivuka nguvu ya Mungu utakumaliza..ambayo hiyo Mungu hakuiweka kwaajili ya kuua watu, bali kwaajili ya kuwalinda watu wake.
Bwana akubariki.
JE KUPONYWA NI UTHIBITISHO WA MUNGU KUWA NA WEWE?
USITUPE LULU ZAKO MBELE YA NGURUWE.
MWISHO WA DUNIA UTAKUJAJE?
NAO WALIOKUWA WAMEKUSUDIWA UZIMA WA MILELE WAKAAMINI.
Je kupiga miayo ni ishara ya mapepo?
SWALI: Shalom, nimekuwa na shida usiku nakuwa kama nimeganda siwezi kusogeza mkono au mguu au kuongea lakini akili nakuwa bado ninayo huwa nakemea inachukua muda kidogo naachiwa nashindwa kujua tatizo ni nini naomba nisaidie.
JIBU: Ndoto yoyote ambayo inakuja, na unajikuta katika mazingira ya kupambana na hali Fulani na huku unatumia jina la Yesu, ambapo mwanzoni inaonekana kuleta upinzani Fulani lakini baadaye inakuja kuachia kwa jinsi unavyozidi kuendelea kukemea ni ndoto yenye ujumbe kutoka kwa Mungu..
Wengine wanaota wanashindana na wachawi, na wale wachawi mwanzoni ni kama wanataka kumshinda lakini baadaye anawashinda kwa jina la YESU, wengine wanaota wamekutana na roho za mapepo, halafu kila alipolitaja jina la Yesu sauti, haitoki, lakini kwa jinsi alivyokuwa anaendelea kulitaja mwisho wa siku sauti inatoka na anayashinda.. Mwingine hata sio mapepo bali hali fulani ya udhaifu, kama hiyo ya kwako, unajikuta umeganda huwezi kusogeza kiungo chako hata kimoja, kila unapojaribu unashindwa, unajikuta unahitaji msaada kwa kulitaja jina la Yesu, na unapofanya hivyo mwanzoni ni kama inashindakana lakini baadaye inaachia hali hiyo inaisha ghafla..
Zote hizo ni ndoto zenye ujumbe mmoja,..Ambao ni Mungu tu anakuonyesha SILAHA pekee ambayo inayoweza kukupa ushindi dhidi ya adui yako shetani, na silaha hiyo tayari umeshaijua ambayo ni jina la YESU. Hivyo ni kuongeza bidii ili uwe na mamlaka kamili juu ya jina hilo kuu.. (Kumbuka mamlaka hayaji kwa kulitamka tu kama ulivyoona kwenye ndoto, bali yanakuja kwa kumwelewa Yesu Kristo katika Neno lake, ndipo kutamka kwako kuwe na nguvu).
Yohana 15:7 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa”.
Unaona hakuna lolote litakalokushinda, ikiwa maneno ya Mungu yatakuwa ndani yako kwasababu utakuwa umepewa mamlaka kamili na Kristo mwenyewe ya kushinda mambo yote..
Luka 10:19 “Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru’’.
Hivyo jitahidi kumjua Kristo zaidi, au ongeza bidii, ili upokee mamlaka hayo kamili..Ndio ujumbe mkuu unaopewa hapo.
Vile vile sababu nyingine ya pembeni, ambayo unapaswa ujue katika ndoto kama hizo za kujikuta umeganda kitandani na huwezi kufanya chochote, ambapo wengine zinakuja katika uhalisia kabisa kana kwamba sio ndoto, bali ni kitu halisi na wanajiona hawawezi kusogeza kiungo chao chochote kitandani, na anatamani hata mtu amsaidie kusogeza mkono wake lakini hawezi kumwambia, na wengine wanasema amekufa lakini yeye anajiona bado ..Ni kwamba hapo Mungu anakuonyesha, hali halisi ya jinsi watu wanavyokufa, na Kwamba yapo maisha baada ya kufa, sio kama wengine wanavyodhani, ukifa huelewi chochote, La, ukifa roho yako inaendelea kuishi inaondolewa katika mwili wako na kupelekwa mahali pengine..(Mhubiri 12)..
Hivyo siku ya kufa, kila mtu atajiona jinsi anavyotoka katika mwili wake na kwenda sehemu nyingine, na ataona pia wanaomzunguka jinsi anavyowaacha!.
Hivyo tunapaswa tujiulize , je! tumejiandaaje huko tuendako? Jibu lipo katika maisha ya kila mmoja jinsi anavyoishi.
Ubarikiwe.
JINSI YA KUSOMA BIBLIA.
KUOTA NYOKA.
JINSI YA KUUHARIBU UJANA WAKO.
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)
WAKATI WA JIONI KUTAKUWAKO NA NURU.
WhatsApp
Kama watu wamefunga ndoa ya serikali na wakaachana, wanaweza kuoa au kuolewa tena na watu wengine?
JIBU: Shalom, Ndoa iliyofungwa kiserikali, au kwa namna yoyote ile…ambayo imehusisha makubaliano ya pande zote mbili na taratibu zote ikiwemo mahari na kutangazwa mbele ya jamii kuwa watu hao wawili wamekuwa mume na mke…kwa namna yoyote ndoa hiyo haipaswi kuvunjwa kwasababu imetangazwa tayari mbele ya mashahidi, hivyo hiyo tayari ni ndoa (ingawa sio ya kikristo)..
Na endapo ikitokea wawili hao wamefunga ndoa hiyo ya kiserikali na wakaachana, basi mbele za Mungu watakuwa na hatia…(Na kumbuka ndoa ya kiserikali hawafungi na wakristo, yaani maana yake mtu ambaye tayari ameshamjua Yesu Kristo na kumwamini, hawezi kwenda kufungishwa ndoa ya kiserikali, mkristo anayefunga ndoa ya kiserikali ni mwasherati), wanaofungishwa ndoa hizo za kiserikali ni wale ambao bado hawajamjua au kumwamini Yesu Kristo, au kwa namna nyingine wapagani, mfano wa ndoa hizo ni kama ile ya Herodia ambayo alimwacha mumewe aliyeitwa Filipo na kwenda kuolewa na ndugu ya mume wake, sasa ndoa hiyo ya Herodia na Filipo haikuwa ya kikristo, pengine ilikuwa ya kiserikali au ya kitamaduni za taifa lao au ya kidini yao lakini maadamu ilikuwa imeshahalalishwa na jamii yao au serikali yao basi ilikuwa ni dhambi kwa Herodia kumwacha mume wake huyo na kwenda kuolewa na ndugu ya mume wake (kasome kisa hicho katika Marko 6:17-18).
Lakini ikitokea mmoja wa waliofungishwa ndoa ya namna hiyo /kiserikali kaamini na kuwa mkristo na mwenzake hataki kuishi naye kwasababu tu kawa mkristo na akaamua kumuacha..hapo huyu aliyeachwa kwasababu ya Imani yake ya kikristo atakuwa huru kuolewa/kuoa na mtu mwingine ambaye ni mkristo mwenzake tu, lakini kama hata baada ya kuokoka kwake mwenziye ambaye anaishi naye hataki kuokoka lakini bado anataka kuendelea kuishi naye..huyu hana budi kuendelea kuishi naye hata kama hajaokoka..na endapo akimwacha kwasababu tu hataki kuokoka atakuwaa na hatia mbele za Mungu..Na akimwacha na kwenda kuoa/kuolewa na mwingine atakuwa anazini.
Sasa wapo watu huko nyuma kabla ya kuokoka walifunga ndoa ya kiserikali, na baada ya kuokoka wanapojaribu kuwashawishi wake zao/waume zao nao pia waokoke kama wao, wanapowaona wanakataa basi wanakusudia kuwaacha..ingawa bado wanapedwa na hao wenza wao na hawajaachwa..lakini wao kwasababu wameokoka hawataki tena kuishi na wale waume zao/wake zao ambao hawajaokoka..Ndugu usifanye hivyo ni dhambi kubwa sana!..Mume wako/mke wako uliyefunga naye ndoa hata kama ni mlevi lakini hataki kukuacha, basi hupaswi kumuacha…na hiyo ni kulingana na Biblia kasome..1Wakorintho 7:10-15.
Na pia ikitokea wote wawili hapo kwanza walikuwa wamefunga ndoa ya kiserikali na sasa wameokoka na kuifahamu neema ya Kristo, Hawa wote wawili wanapaswa kwenda kanisani kuifanya ndoa yao iwe ya kikristo. Kwasababu ilipofungwa kiserikali haikumhusisha Kristo wala maagizo yake, Wanapaswa kwenda kuahidiana upya mbele za Mungu na wanadamu kwamba wataishi kwa uaminifu pasipo kuachana, na kifo ndicho kitakachowatenganisha, na kwamba watakuwa kielelezo kwa watakatifu wengine wowote kwa kuishi katika ndoa ya kikristo ya mume mmoja na mke mmoja, na mambo mengine ambayo watayaahidi mbele ya kanisa la Mungu na mbele ya Kristo mwenyewe. Baada ya hapo ndoa yao itabarikiwa na Mungu, na kuwa ya kikristo na zile baraka zote za wanandoa zitafuatana nao.
Sasa kuna kundi lingine ambalo linajiita ni wanandoa…Hili ni lile ambalo walikutana tu na kuamua kuishi Pamoja, pasipo utaratibu wowote…ni ile watu wawili wamekutana tu kijana na binti na kuwekana ndani, hakuna cha mahari, hakuna imani. Hawa kibiblia wanafanya uasherati (NI WAASHERATI).
Na endapo ikitokea mmoja kaamini katika hali hiyo waliyopo ya kukaa Pamoja (maana yake katubu na kuwa Mkristo). Moja kwa moja yule aliyeamini anapaswa avunje hayo mahusiano, kwasababu ni uasherati ndio aliokuwa anaufanya..Anapaswa avunje hayo mahusiano hata kama wameshazaa Watoto, arudi kwa wazazi wake, au akaishi peke yake kwa kujitegemea na wanawe… mpaka huyo mwenzake naye atakapotubu kama yeye na kuwa mkristo na kwenda kufunga ndoa kanisani. Lakini endapo huyo mwingine kakataa kutubu katakata na kujisalimisha kwa Yesu Kristo, basi huyu aliyetubu yupo huru kuolewa/kuoa mtu mwingine lakini aliye mkristo kama yeye tu!…(hapaswi kwenda kuoa/kuolewa na mtu ambaye sio mkristo)
Kumbuka tena mtu ambaye ameshamjua Yesu Kristo, na kufahamu kuwa ndoa halali ni ile ya kikristo (mfano wa mimi na wewe ambao tumeshajua sasa) na ameshafahamu kuwa inapaswa ifungwe mbele ya kusanyiko la Kristo, akienda kufunga ndoa yoyote ile kinyume na hiyo, akaenda kufunga ndoa aidha ya kimila au ya kiserikali au akijichukulia tu mke/mume na kuishi naye ndani…pasipo kwenda kuifungisha ndoa yake kanisani BASI ANAFANYA UASHERATI!!…Na waasherati wote biblia inasema hawataurithi ufalme wa mbinguni (1Wakoritho 6:9).
Na pia maana halisi ya neno ndoa ni Muunganiko wa MUME na MKE na sio muunganiko wa mume na mume au mke na mke…Hivyo hicho kinachoitwa ndoa ya jinsia moja hakipaswi kiitwe hivyo…kinapaswa kiitwe “uasherati wa jinsia moja”…na sio “ndoa ya jinsia moja”..Hivyo serikali inayohalalisha “uasherati wa jinsia moja” Huo Mungu kaukataa na ni machukizo makubwa mbele za Mungu..kasome Walawi 20:13.
Je umemwamini Yesu Kristo?, kama bado unasubiri nini?, hizi ni siku za mwisho na Kristo yupo karibuni kulichukua kanisa lake, je utakuwa miongoni mwa watakaonyakuliwa, Unafahamu kuwa kanisa hili tunaloishi ndio kanisa la mwisho, hakutakuwa na kanisa lingine baada ya hapa?
Bwana atubariki.
JE NI DHAMBI KUWA NA MAHUSIANO KABLA YA NDOA?
Je! Ni sahihi kwa mkristo kuoa/kuolewa na mtu wa imani nyingine?
NDOA NA HARUSI TAKATIFU.
Je! ni halali kutoa cheti kwa wakristo wanaooa?
NJIA SAHIHI YA KUMPATA MWENZA WA MAISHA KIBIBLIA.
Kama kuna majira ambayo si ya kufanya mchezo na masuala ya wokovu wetu hata kidogo basi ni haya. Kwani moja ya hizi siku tutashuhudia mabadiliko makubwa sana na ya ghafla katika kanisa la Kristo,..wakati ambao Bwana Yesu anakwenda kuchukua hatua ambayo hakuwahi kuichukua tangu aondoke hapa duniani.. Na hatua yenyewe ni Kuingia na kuufunga mlango wa hekalu lake.
Hayo mambo pengine utayashuhudia kwa macho yako siku si nyingi,..Kumbuka biblia inalifananisha kanisa la Kristo na hekalu lake (Waefeso 2:19-22)..Sasa ukisoma kitabu cha Ezekieli utaona anaonyeshwa matukio yanayoambata na hakalu la Mungu, Na utaona akionyeshwa malango mengi ya hekalu yakiwa wazi, lakini ukisoma ile sura ya 44 utaona Ezekieli anaonyeshwa ghafla lango la mashariki likiwa limefungwa..Na anaambiwa halitafunguliwa tena, wala mtu awaye yote hataingia kwa kupitia lango hilo.
Ndipo Ezekieli akaambiwa sababu ya lango hilo kufungwa, na sababu yenyewe ilikuwa ni hii..tusome..
Ezekieli 44:1 “Kisha akanirudisha kwa njia ya lango lile la nje, la mahali patakatifu lililoelekea upande wa mashariki; nalo lilikuwa limefungwa. 2 Bwana akaniambia, Lango hili litafungwa, halitafunguliwa, wala mtu awaye yote hataingia kwa lango hili, kwa maana Bwana, Mungu wa Israeli, ameingia kwa hilo; basi kwa sababu hiyo litafungwa”.
Ezekieli 44:1 “Kisha akanirudisha kwa njia ya lango lile la nje, la mahali patakatifu lililoelekea upande wa mashariki; nalo lilikuwa limefungwa.
2 Bwana akaniambia, Lango hili litafungwa, halitafunguliwa, wala mtu awaye yote hataingia kwa lango hili, kwa maana Bwana, Mungu wa Israeli, ameingia kwa hilo; basi kwa sababu hiyo litafungwa”.
Unaona, sababu ni kuwa Bwana, Mungu wa Israeli (KRISTO), ameingia kwa lango hilo.. Hii ni kuonyesha kuwa mlango huo uliwekwa mahususi kwa ajili yake na si mwingine, yeye ndiye aliyekuwa amewekewa wazi mlango huo mpaka atakapofika,. Hivyo wale waliokuwa wanaingia kabla ya hapo ni neema tu, lakini haukuwekwa wazi kwa ajili yao..
Hivyo Habari hiyo jambo kwa sehemu limetimia lakini ni unabii wa siku za mwisho, wakati ambao Mlango wa Neema utafungwa.
Ndugu, huu mlango ambao tunauita wa neema tulio nao leo hii, Mungu kauacha wazi si kwasababu yetu, bali kwasababu ya Yesu Kristo, Ni mlango wa Kristo Yesu mwenyewe na sio wetu, na moja ya siku hizi, hivi karibuni atasimama, kisha ataupita, na akishaingia, basi utafungwa na ukishafungwa, Habari imeishia hapo hautafunguliwa tena milele..
Mambo yatakayokuwa yanaendelea humo ndani ni siri yake na wale watakaokuwa humo.. Kwahiyo usione unahubiriwa injili, usione unapigiwa kilele utubu dhambi ukadhani Mungu anakuangalia wewe sana, hilo jambo halipo! Mungu anamtazama Kristo tu!, achukue hatua yake, na akishaichukua, hapo ndipo kutakuwa na kilio na kusaga meno kama alivyosema, hakutania alimaanisha kweli wapo watu watalia kweli kweli wakitamani hata nusu saa nyuma lirudi watengeneze mambo yao lakini watakuwa wameshachelewa.
Luka 13:24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze. 25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako; 26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu. 27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu. 28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno…”
Luka 13:24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu. 27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.
28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno…”
Kumbuka hatua hiyo sio ya unyakuo, hapo unyakuo bado, mambo hayo yatatendeka hapa hapa duniani, kwasababu wakati huo utatamani umjue Kristo, lakini hutaweza tena, kwasababu anayewavuta watu kwa Kristo sasa ni Roho Mtakatifu na sio mtu mwenyewe..Hivyo Roho Mtakatifu akishaondoka juu yako huwezi tena kumfuata Mungu hata iweje..(Yohana 6:44)
Sasa muda mfupi baada ya huo wakati, Unyakuo ndio utapita, na wewe ambaye humtaki Kristo sasa…utaendelea kubaki hapa hapa duniani ambacho kitakachofuata ni dhiki kuu kabla hujafa na kuingia katika jehanamu ya moto. Kama tunavyoona mambo yalivyo sasa, ni tunaishi katika muda wa nyiongeza tu.., hii dunia ingepaswa iwe imeshaisha tangu zamani kulingana na unabii wa kibiblia, lakini dalili zote zinaonyesha sasa wakati wowote, mambo yatabadilika kwa ghafla sana. Na Mlango utafungwa na watu watatamani kuingia watashindwa..
Soma Habari hii kulithibitisha hilo tena..uone jinsi wanawali wale wapumbavu waliporudi na kukuta mlango umefungwa, ufananishe na hali itakavyokuwa wa wakristo wengi vuguvugu waliopo leo duniani..
Mathayo 25 : 1-13 “Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. 2 Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. 3 Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; 4 bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. 5 Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. 6 Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki. 7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao. 8 Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. 9 Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie. 10 Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa. 11 Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie. 12 Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi. 13 Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa”.
Mathayo 25 : 1-13 “Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi.
2 Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara.
3 Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; 4 bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.
5 Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi.
6 Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki.
7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao.
8 Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. 9 Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie.
10 Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.
11 Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie.
12 Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi.
13 Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa”.
Je! Na wewe bado nje ya mlango huo hujaingia tu ndani mpaka sasa?..Kumbuka tena jambo hili lango hilo likishafungwa mara moja, halitafunguliwa tena milele..(Na Yesu ndiye lango) Ni heri ukatubu dhambi zako leo ikiwa hujafanya hivyo..Ili Mungu atakusamehe na kukupa uzima wa milele bure.
Ufunuo 22:17 “Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.”
MAMBO 5 AMBAYO KILA MKRISTO ANAPASWA KUFAHAMU.
JE! WATOTO WACHANGA WANAWEZA KUHUKUMIWA NA KUTUPWA MOTONI.
Biblia inamaanisha nini inaposema “Tusitweze unabii”?
TUMAINI NI NINI?
Je! Adamu aliwasaliana na Mungu kwa lugha ipi pale bustanini?
JE ADAMU ALIKUWA NA KITOVU?
Katika maisha kila mwanadamu ambaye ameumbwa na Mungu mkuu, ni lazima ameumbiwa kitu kinachoitwa huzuni ndani yake. Maana yake ni kwamba ni lazima atapitia vipindi vya huzuni na vile vile atapitia vipindi vya furaha. Kila mwanadamu hata kama ni mtumishi wa Mungu ni lazima atapitia hivyo vipindi..Bwana wetu Yesu Kristo ambaye alikuwa ni mkamilifu asilimia zote alivipitia si zaidi sisi tusiokuwa wakamilifu?..Ni lazima tuvipitie. Na huzuni ni kama ugonjwa ukiwekwa katika mazingira Fulani inazidi na pia ikiwekwa katika mazingira Fulani unapungua.
Na huzuni inaweza kuja aidha kutokana na kupata taarifa mbaya, au umepatwa na jambo baya..au unakwenda kupatwa na jambo baya…au wakati mwingine inakuja pale linapotokea jambo ambalo hukulitegemea au hukulipanga, au hukutamani liwe hivyo lilivyo.
Mtu anapofikia hali kama hiyo anajikuta anazama katika dimbwi kubwa la mawazo, na kukosa hamu ya kufanya jambo lolote lile..hata hamu ya kula inatoweka, wakati mwingine hata hamu ya kuishi.
Siku ile ambayo Bwana ndio alikuwa anakwenda kusulibiwa, Huzuni kubwa iliwaingia wanafunzi wake, baada ya kuwaambia kwamba muda si mrefu atakwenda kusulibiwa, na ataondoka atakwenda zake kwa Baba..
Yohana 16:5 “Lakini sasa mimi naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka, wala hakuna mmoja wenu aniulizaye, Unakwendapi? 6 Ila kwa sababu nimewaambia HAYO HUZUNI IMEJAA MIOYONI MWENU. 7 Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu”.
Yohana 16:5 “Lakini sasa mimi naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka, wala hakuna mmoja wenu aniulizaye, Unakwendapi?
6 Ila kwa sababu nimewaambia HAYO HUZUNI IMEJAA MIOYONI MWENU.
7 Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu”.
Na zaidi ya yote walipoambiwa kwamba mmoja wao atamsaliti..Ndio kabisa moto wote ukakata ndani yao..Wakati wanadhani kwamba Kristo atazidi kuendelea kuwepo, yeye anawapa taarifa za msiba, kwamba anakwenda kusulibiwa..wakawa wanawaza kwanini hayo yote yampate Bwana wao, sasa maisha yatakuwaje baada ya yeye kuondoka.
Na hata Bwana alipowachukua usiku ule kwenda kusali naye hata nguvu zilikuwa zimewaisha kabisa, hawakusali sana wakalala kwasababu ya huzuni nyingi..Tusome..
Luka 22:45 “Alipoondoka katika kuomba kwake, akawajia wanafunzi wake, AKAWAKUTA WAMELALA USINGIZI KWA HUZUNI. 46 Akawaambia, Mbona mmelala usingizi? Ondokeni, mkaombe, msije mkaingia majaribuni”.
Luka 22:45 “Alipoondoka katika kuomba kwake, akawajia wanafunzi wake, AKAWAKUTA WAMELALA USINGIZI KWA HUZUNI.
46 Akawaambia, Mbona mmelala usingizi? Ondokeni, mkaombe, msije mkaingia majaribuni”.
Lakini katika hali kama hiyo, Bwana aliuona udhaifu wa mioyo yao kwamba wamechoka na wanahuzuni nyingi. Lakini aliwaambia waamke waombe..kwasababu roho i radhi lakini mwili ni dhaifu…Hivyo wanapaswa waishinde hali hiyo ya huzuni..kwasababu wana huzuni, lakini siku chache baadaye watakuwa na furaha. Hivyo alijaribu kuwaasa kwamba wajaribu kuishinda huzuni ambayo ilipelekea udhaifu wa mwili wasimame waombe kwasababu majaribu hayo ni ya siku chache tu..siku mbili baadaye watakuwa na furaha isiyo na kifani. Kwasababu aliwaambia bado kitambo kifupi hawamwoni (yaani atakufa na kuzikwa)..na tena bado kitambo kidogo watamwona tena (yaani siku atakapofufuka)..wataendelea kumwona mpaka Pentekoste na watakuwa na furaha kuu.(Soma Yohana 20:20).
Katika wakati huu unaoitwa wa pasaka miongoni mwa mambo mengi tunayojifunza basi ni muhimu kulijua hili pia…USIHUZUNIKE..Pengine umepitia shida Fulani, au umepata usumbufu Fulani, au huzuni Fulani, au tabu Fulani, au taarifa Fulani, au jambo lolote lile ambalo limekuletea huzuni kubwa moyoni hata umekata tamaa ya kila kitu na ya kuendelea mbele katika imani…Huo sio wakati wa kuzidi kuipalilia huzuni kwa kukata tamaa na kuiacha Imani, sio wakati wa kulala usingizi kwa huzuni..Bali ni wakati wa kusimama na KUOMBA kwa nguvu…ni wakati wa kuzidi kuendelea mbele kwasababu huzuni hiyo ni ya kitambo tu!. Baada ya siku chache itaondoka na furaha itakurudia kama mwanzo na utajuta kwanini siku chache nyuma ulikuwa unahuzunika…utajuta kwanini ule muda ambao ulikuwa na huzuni usingeutumia hata kuomba au kumsifu Mungu.
Hivyo simama sasa mtu wa Mungu, huu sio wakati wa kupalilia huzuni bali ni wakati wa kuomba..Mitume wa Yesu huzuni yao iligeuka furaha pale walipomwona Bwana kafufuka…nawe pale utakapoona kile kilichokuwa kimekufa kimefufuka, siku sio nyingi furaha yako itarudi. Hivyo usihuzunike..simama uombe, simama uendelee mbele kwasababu hatua zilizobakia mbele yako ni chache kuliko ulizoziacha nyuma. Hivyo sio wakati wa kunyongonyea ni wakati wa kuomba.
Bwana akubariki
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312.
USIKIMBILIE TARSHISHI.
USHAURI KWA MWANAMKE WA KIKRISTO.
JE SALA YA ROZARI TAKATIFU NI YA KIMAANDIKO?
JINSI EDENI ILIVYOKUWA.
Bwana wetu Yesu Kristo asifiwe ndugu yangu..
Nyakati hizi za mwisho tunazoishi sasa, ni nyakati ambazo zinakithiri kuwa na mseto wa watu wengi wanaojiita wakristo, leo hii ni rahisi kuona hata msanii wa kidunia anaimba nyimbo za Injili, ni rahisi kuona, mashoga wanatoa michango ya kujenga makanisa makubwa ulaya, wazinzi wanahudhuria kila jumapili ibadani, wengine mpaka wapo tayari kushiriki meza ya Bwana bila hofu nao wanaona ni kawaida tu. Ni kundi kubwa lenye mchanganyiko wa kila aina ya watu, wengine hawana hata mpango wa kufikiria maisha yao baada ya hapa, kinachowapeleka kwa Mungu tu, ni pengine waponywe waondoke, wengine wapate tu wachumba, wengine biashara zao ziende vizuri..basi hakuna cha zaidi baada ya hapo
Na wachache sana ndio wanaoutafuta wokovu wa kweli, ambao wapo tayari kumtii na kumfuata Yesu pale alipo yeye..
Embu leo kwa ufupi tuone habari moja ambayo, pengine unaijua sana, lakini tuiangalie kwa jicho lingine la ndani zaidi na naamini tutajifunza kitu kipya..
Na habari yenyewe ni ile ya Yesu akiwa bado kijana mdogo, alipokwenda na wazazi wake Yerusalemu kuila pasaka ya kila mwaka.. Lakini kama tunavyoijua habari baada ya sikukuu kuisha, ulipofika wakati wa kila mtu kurudi nyumbani kwake na katika taifa lake, wale waliotokea katika mikoa ya karibu kule Israeli walianza safari ya kurudi makwao, na wale waliotokea mataifa mengine ya mbali nao pia walianza kurejea makwao..
Lakini mambo yalikuwa tofauti kwa Bwana Yesu, yeye alibaki nyuma, wala hakuambata na makutano kurudi makwao, kama watu wengine walivyofanya, na kibaya zaidi hata wazazi wake hawakulijua hilo, wao wakakisia tu labda atakuwa katikati ya makutano wakirejea naye nyumbani…(Hilo ndio kosa linalofanywa na watoto wengi wa Mungu)
Luka 2:44 “Nao wakadhani ya kuwa yumo katika msafara; wakaenenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao; 45 na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta. 46 Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake. 48 Na walipomwona walishangaa, na mama yake akamwambia, Mwanangu, mbona umetutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni. 49 Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu”?
Luka 2:44 “Nao wakadhani ya kuwa yumo katika msafara; wakaenenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao;
45 na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta.
46 Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.
47 Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake.
48 Na walipomwona walishangaa, na mama yake akamwambia, Mwanangu, mbona umetutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni.
49 Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu”?
Kama tunavyoona hapo, ni wazazi wake tu pake yao, ndio waliokuwa walau wanamfikiria Yesu katikati ya ndugu zao wengi walioambatana nao, na walipoona Kristo hayupo katikati ya makutano, katikati ya wingi wa watu, katikati ya ndugu, katikati ya marafiki, katikati ya majirani, katikati ya wageni wa mataifa mengine, ndipo ikiwapasa wageuke wajaribu kwenda kuanza kumtafutia kule walipompotezea Yerusalemu.. ndipo wakamkuta yupo hekaluni katikati ya WAALIMU..
Na ni kama bahati tu walipita hekaluni, lakini kama wasingeingia kule, kamwe wasingemwona daima, wangehangaika Yerusalemu nzima wasingempata kwa muda mrefu sana..
NI KIPI MUNGU ANATAKA TUJIFUNZE?
Wakristo wachache wa leo hawajui kuwa, wapo katikati ya kundi kubwa la wakristo vuguvugu, linaloondoka mbali na mafundisho ya kweli ya Neno la Mungu.. na ndio maana wanapojaribu kumtafuta Kristo katikati yao ni kama vile hawamuoni, lakini wao bado wanataka kuendelea kutembea nao tu, hawajui kuwa kwa jinsi wanavyozidi kukaa nao ndivyo wanavyozidi kumpoteza YESU wasimpate kabisa..
Ndugu geuka kama ni wewe,..angalia ulipotoka, kule mlipotoka ndipo Kristo yupo,..Na! ulipotoka ni wapi?? Ni katikati ya waalimu, kule Kristo alipo, na waalimu makao yao huwa ni wapi?..Makao yao ni darasani sikuzote, wakiwafundisha wanafunzi, na hapo ndipo makao ya Kristo yalipo siku zote..
Hutampata sehemu nyingine yoyote, hutampata, kwenye michezo, maombezi, hutampata kwenye matamasha, hutampata kwenye taasisi za kidini, wala hutampata kwenye dhehebu lolote, wala katikati ya ndugu zako, au rafiki zao, au majirani zako, huko kote utapotea, Kristo hatembei katikati ya misafara ya watu wanaosafiri mbali na yeye bali Kristo utamwona PALE NENO LAKE LINAPOFUNDISHWA BASI..
Ukiona hupendi tena kujifunza Neno la Mungu basi ujue, upo mbali sana na Kristo kwa mujibu wa biblia, ukiona huna muda wa kusoma biblia, usijidanganye utakaa umwone Kristo akijifunua kwako, ukiendelea kudhani Kristo yupo katika msafara unaouona leo hii, wimbi la watu wengi wanaosema tumeokoka, lakini Neno la Mungu hawalifuati, ni wavivu katika kutamani kumjua Mungu, ukiwauliza habari ya unyakuo kwao ni kama habari mpya za kuchosha, ukiwauliza, habari za kwenda mbinguni kwao ni kama hadithi za kizee, muda wote ni kujionyesha tu, na kujisifia wameokoka, lakini biblia ni kama kitabu cha ziada tu kwao basi ujue wamempoteza Kristo katikati yao..
Bwana atusaidie nyakati hizi za hatari tusimpoteze yeye aliye mwamba wa wokovu wetu..
Maran Atha.
NI NANI ALIYEWALOGA?
NI NANI ALIYEWAONYA KUIKIMBIA HASIRA ITAKAYOKUJA?
https://wingulamashahidi.org/mafundisho-ya-ndoa/
JE YESU ATARUDI TENA?
Biblia inamaana gani kusema;aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi?
Katika 1Wafalme 20:35-37, Kwanini yule mtu afe kwa kuliwa na simba baada ya kukataa kumpiga yule nabii?..je Mungu anaruhusu watu kupigana?
JIBU:Tusome
1Wafalme 20:35-37 “Basi, mtu mmoja wa wana wa manabii akamwambia mwenzake kwa neno la Bwana, Nipige, nakusihi. Akakataa yule kumpiga. 36 Akamwambia, Kwa sababu hukuisikiliza sauti ya Bwana, angalia, mara ukitoka kwangu simba atakuua. Na mara alipotoka kwake, simba alimwona, akamwua. 37 Ndipo akaona mtu mwingine, akasema, Nipige, nakusihi. Yule mtu akampiga, hata kumpiga na kumtia jeraha”
1Wafalme 20:35-37 “Basi, mtu mmoja wa wana wa manabii akamwambia mwenzake kwa neno la Bwana, Nipige, nakusihi. Akakataa yule kumpiga.
36 Akamwambia, Kwa sababu hukuisikiliza sauti ya Bwana, angalia, mara ukitoka kwangu simba atakuua. Na mara alipotoka kwake, simba alimwona, akamwua.
37 Ndipo akaona mtu mwingine, akasema, Nipige, nakusihi. Yule mtu akampiga, hata kumpiga na kumtia jeraha”
Kuna wakati Mungu anatumia ishara za mwilini kuzungumza na watu wake au kufikisha ujumbe mahali..Kwamfano utaona Nabii Hosea aliambiwa aoe mwanamke wa kizinzi,
Hosea 1:2 “Hapo kwanza Bwana aliponena kwa kinywa cha Hosea, Bwana alimwambia Hosea, Enenda ukatwae mke wa uzinzi, na watoto wa uzinzi; kwa maana nchi hii inafanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha Bwana”.
Lengo la Mungu kumwambia Hosea akaoe mwanamke wa kizinzi sio kuhalalisha uzinzi kwa watu wake, hapana bali ni kuwaonyesha watu wake jinsi na wao wanavyofanya uzinzi mbele zake kinyume chake katika roho…Hosea hakuwa mzinzi lakini aliambiwa akamwoe mwanamke mzinifu, ambaye ni kahaba mwenye wanaume wengi, ambaye hatulii. Sasa nafasi ya Hosea ambaye hakuwa mzinifu ilimwakilisha Mungu na huyo mwanamke wa kizinzi ililiwakilisha taifa la Israeli, kwa jinsi yule mwanamke alivyokuwa ni kahaba baada hata ya kuolewa na Hosea ndivyo Taifa la Israeli lilivyofanya uzinzi katika roho na kumwacha Mungu wao ambaye ndiye mume wao kama Isaya 55:5 inavyosema “Kwa sababu Muumba wako ni MUME WAKO; Bwana wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote”
Sasa endapo Nabii Hosea angekataa maagizo yale Mungu aliyompa ya kwenda kumwoa mwanamke kahaba…na kusema hapana Bwana mimi sitaki kumuoa mwanamke yule ambaye ni mzinzi na kahaba hata nikimuoa bado ataendelea kuwapenda hao mabwana wake…Ni Dhahiri kuwa Hosea angetenda dhambi kwasababu amekataa shauri la Bwana la yeye kufanyika ishara kwa Israeli. Na hivyo angewafanya Israeli wasitubu, lakini ishara ile iliwafanya Israeli wengi watubu..Kwasababu walipokwenda kumuuliza wewe Nabii wa Mungu mbona unaoa mwanamke ambaye anamabwana wengi na zaidi ya yote tunamwona mkeo huyo yupo na mabwana wengine, unajisikiaje kwa hilo?..Ndipo Hosea atawajibu ni mfano wa nyinyi mlivyomwacha Mungu wenu ambaye ni mume wenu na kuigeukia miungu mingine kuiabudu..Hivyo mrudieni Mungu wenu ambaye ni Mume wenu kwasababu amewakasirikia sana.
Halikadhalika kuna wakati Mungu alimwambia nabii mwingine amwambie mwenzake kwamba ampige mpaka apate majeraha…ili kwa kupitia yale majeraha aonekane kama alikuwa katika vita vikali na aende kwa mfalme wa Israeli akiwa na yale majeraha…Ili mfalme adanganyike na kuamini kuwa ni kweli alikuwa kwenye mapambano kwasababu ana majeraha..na ndipo ampe fumbo ambalo litamtega…Na kweli mfalme alipomwona mtu anakuja mwenye majeraha akasema bila shaka mtu huyu atakuwa ametoka vitani kwa majeraha yale..na alipopewa lile fumbo na yule nabii kumbe lilikuwa linamhusu mfalme mwenyewe..kwasababu alimwacha huru Benhadadi ambaye alipaswa kumuua kabisa..
Hivyo akaambiwa sehemu yake ataichukua yeye. Unaweza kuisoma vizuri habari hiyo katika 1Wafalme 20:35-43.
Lakini yule mtu alikataa maagizo yale ya Mungu..ingawa aliambiwa ni maagizo kutoka kwa Mungu lakini akakataa kumpiga..hakujua kuwa kwa kukataa kule kungemfanya mfalme wa Israeli asiyaamini maneno yale ya Mungu…Na ikasababisha dhambi kwake, na ndio mbeleni akaenda kuliwa na simba..lakini yule mwingine hakulichukulia lile jambo la kumpiga nabii wa Mungu kwamba ni jambo la kumuumiza..bali aliona mbele kwamba kwa ishara ile ya majeraha ya yule nabii, mfalme ataamini ujumbe kutoka kwa yule nabii sawasawa na Neno la Mungu na hivyo atakuwa ameyatenda mapenzi ya Mungu Zaidi.
Hivyo ni jambo la kawaida kabisa Mungu kuzungumza kwa ishara za mwili, alifanya hivyo kwa Hosea, Kwa Ezekieli, na kwa manabii wengine wengi.
Bwana atubariki
YEZEBELI ALIKUWA NANI
Kuna haja gani ya kumwamini Yesu aliyezaliwa kama sisi?
MAMBO MANNE,YANAYODHOOFISHA UOMBAJI WAKO.
KWANINI YESU KRISTO NI WA MUHIMU KWETU SASA?
MKARIBIE BWANA ZAIDI ILI UFANYIKE NGUZO.
Shalom, Naomba kufahamu kitendo cha kupiga miayo mara kwa mara hususani wakati wa maombi, Je! Ishara ya kuwa na mapepo au nguvu za giza?.
JIBU: Kwa namna ya kawaida kupiga miayo ni ishara ya mambo mawili makuu katika mwili, 1) Ya kwanza ni njaa, 2) Ya pili ni usingizi.
Hivyo tukirudi katika masuala ya maombi mkristo hapaswi kufikiria kuwa kupiga miayo ni kitendo cha mapepo au nguvu za giza, hapana bali ni mwitikio wa mwili wake mwenyewe, ukimwambia kuwa huu sasa ni wakati wa kwenda kupumzika umechoka, sio wakati wa kusali..Na ndio maana utagundua ni wakati tu wa kusali, au wa kusikiliza Neno watu ndio wanasikia uchovu wa hali ya juu, lakini wakitoka hapo hiyo hali inapotea yenyewe, utajiuliza ni kwa nini?
Ni kwasababu Biblia inatufundisha kuwa mwili ni adui wa mambo ya rohoni sikuzote, wakati roho yako ipo tayari hata kuzama muda mrefu kwenye maombi mwili wako utaanza kutoa sababu nyingi, mara umechoka, unapaswa ukapumzike, utakuletea mpaka hivyo viashiria vya miayo mingi, ili tu kukuthibitishia, na tena kama utakuwa unafikiria chakula muda wa maombi ndio kabisa utakuletea mpaka miayo ya njaa, mpaka utatetemeka wakati ni muda mfupi tu nyuma hapo ulitoka kula.
Wagalatia 5:17 “Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka’’.
Hivyo, hali kama hiyo ikikujia, hupaswi kukemea mapepo, bali ni wakati kushindana na mwili wako mpaka ukutii wenyewe, na habari njema ni kuwa kwa jinsi utakavyozidi kuzama katika maombi, ndivyo hiyo hali itakavyokuwa inatoweka yenyewe ndani yako kidogo kidogo, mpaka mwishoni utajikuta unaweza kwenda muda mrefu mpaka utajiuliza ule usingizi mwanzoni ulitokea wapi.
Kwahiyo njia rahisi ni kuhakikisha wakati unaposali, peleka mawazo yako yote na fikra zako zote kwenye maombi na sio katika mambo mengine, ndivyo utakavyoweza kuushinda mwili kirahisi, na kama ni usiku unasali toka katika mazingira ya kitanda.
Mwisho, fahamu kuwa kama mkristo huwezi kuishi bila maombi.
Kwahiyo shindana na mwili wako mpaka uushinde, vinginevyo hutadumu muda mrefu katika imani au kama utaendelea kuwepo basi ujue maisha yako yatakuwa ni ya majaribu kila kukicha ambayo yangeweza kuepukika tu kwa maombi..
Mathayo 26:41 “ Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu”.
USIISHIE KUTAZAMA JUU, ENDELEA MBELE.
JE MOYO WAKO NI MNYOFU MBELE ZA MUNGU
JE WAKRISTO TUNARUHUSIWA KUSHEHEREKEA VALENTINE’S DAY?
PASAKA NI NINI? NA JE TUNARUHUSIWA KUSHEHEREKEA PASAKA?
Je! Ni dhambi kwa kijana aliyeokoka kuvaa suruali za kubana (model), kunyoa mitindo (mfano kiduku), ?
ROHO ZILIZO CHINI YA MADHABAHU:
Mathayo 7:6 “Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua”.
Maneno hayo yalizungumzwa na Bwana wetu Yesu. Akifunua kuwa sio kila neno/kitukinawafaa baadhi ya watu. Hivyo tuwe na hekima tunapotoa au tunaposema vitu vyetu vilivyo vya thamani mbele za watu, kwasababu unaweza ukasema kitu ukadhani kitakuwa na manufaa kwa yule unayemwambia badala yake kitu kile kikageuka kuwa matatizo kwako.
Tutajifunza mfano mmoja muhimu katika biblia kisha kupitia huo tutapata kuelewa Zaidi kiini cha somo letu.
Wakati Mungu anamtokea Musa na kuzungumza naye kwa mara ya kwanza katika kile kijiti kilichokuwa kinawaka moto lakini hakiteketei…Alimwambia maneno haya..
Kutoka 3:6 “Mimi ni Mungu wa baba yako Ibrahimu, Isaka na Yakobo…. 7 Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; 8 nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. 9 Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa. 10 Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri.”
Kutoka 3:6 “Mimi ni Mungu wa baba yako Ibrahimu, Isaka na Yakobo….
7 Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao;
8 nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.
9 Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa.
10 Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri.”
Baada ya Mungu kumwambia maneno haya ya ahadi na ya Faraja..alimwambia akawaambie habari hizo wana wa Israeli…Kwamba wamejiliwa na wanakwenda kutolewa katika nchi ya Misri ya utumwa na kupelekwa nchi ya Ahadi. Hivyo Musa akaenda kuwaambia wana wa Israeli habari hizo nao wakafurahi.
Lakini jambo la kipekee ni kwamba Mungu alipomwambia Musa aende kwa Farao…alimwambia amwambie Farao maneno mengine tofauti na hayo…Tusome..
Kutoka 3:16 “Enenda, ukawakusanye wazee wa Israeli pamoja, ukawaambie, Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea, akaniambia, Hakika nimewajilieni, tena nimeyaona mnayotendewa huko Misri; 17 Nami nimesema, Nitawapandisha kutoka katika mateso ya Misri na kuwaingiza katika nchi ya Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, nchi ijaayo maziwa na asali. 18 Nao watakusikia sauti yako; nawe utakwenda, wewe na wazee wa Israeli kwa mfalme wa Misri, na kumwambia, BWANA MUNGU WA WAEBRANIA, AMEKUTANA NASI; BASI SASA TWAKUOMBA, TUPE RUHUSA TWENDE MWENDO SIKU TATU JANGWANI, ILI TUMTOLEE DHABIHU BWANA MUNGU WETU. 19 Nami najua ya kuwa huyo mfalme wa Misri hatawapa ruhusa mwende zenu, la, hata kwa mkono wa nguvu”.
Kutoka 3:16 “Enenda, ukawakusanye wazee wa Israeli pamoja, ukawaambie, Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea, akaniambia, Hakika nimewajilieni, tena nimeyaona mnayotendewa huko Misri;
17 Nami nimesema, Nitawapandisha kutoka katika mateso ya Misri na kuwaingiza katika nchi ya Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, nchi ijaayo maziwa na asali.
18 Nao watakusikia sauti yako; nawe utakwenda, wewe na wazee wa Israeli kwa mfalme wa Misri, na kumwambia, BWANA MUNGU WA WAEBRANIA, AMEKUTANA NASI; BASI SASA TWAKUOMBA, TUPE RUHUSA TWENDE MWENDO SIKU TATU JANGWANI, ILI TUMTOLEE DHABIHU BWANA MUNGU WETU.
19 Nami najua ya kuwa huyo mfalme wa Misri hatawapa ruhusa mwende zenu, la, hata kwa mkono wa nguvu”.
Sasa unaweza kujiuliza kwanini Mungu hakumwambia Musa amwambie Farao kwamba “Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo nimeona mateso ya watu wangu jinsi gani unavyowatumikisha hivyo wape ruhusa waondoke waende nchi ya ahadi niliyowaahidia?”…Badala yake Mungu hakumruhusu Musa kumwambia Farao habari zozote kuhusu Ibrahimu, wala kuhusu mahali wanapokwenda..badala yake ni kama Mungu alimdanganya Farao kwamba wanakwenda tu kumtolea Mungu dhabihu jangwani kisha watarudi…kumbe ndio walikuwa wanakweda kutokomea huko.
Hivyo Farao akadanganyika akajua kuwa wana wa Israeli wanataka tu kwenda kumtolea Mungu wao dhabihu jangwani siku tatu na kisha watarudi kumbe nyuma yake kulikuwa na mpango mwingine wa wana wa Israeli kutokomea huko huko na kutokurudi tena…
Sasa japokuwa Farao alikuwa anajua ni kitendo tu cha kwenda na kurudi lakini alikuwa mgumu vile hebu tafakari laiti angejua kuwa wale watu ndio wamepanga wanaondoka kabisa kabisa hali ingekuwaje?..bila shaka vingeamka tena vita vingine visivyokuwa na maana.
Sasa Kwanini Mungu alifanya vile?, Ni kwasababu aliwazuilia wana wa Israeli wasitupe lulu zao mbele za nguruwe wasije wakazikanyaga mbele ya miguu yao na kugeuka na kuwararua.
Hivyo wana wa Israeli mpaka wanaondoka Misri…Farao alikuwa anajua kuwa ni wanakwenda tu na kurudi.. Hebu tusome mistari kadhaa kulithibitisha hilo..
Kutoka 5:2 “Farao akasema, Bwana ni nani, hata niisikilize sauti yake, na kuwapa Israeli ruhusa waende zao? Mimi simjui Bwana, wala sitawapa Israeli ruhusa waende zao. 3 Wakasema, Mungu wa Waebrania amekutana nasi; twakuomba, tupe ruhusa twende safari ya siku tatu jangwani, tumtolee dhabihu Bwana, Mungu wetu; asije akatupiga kwa tauni, au kwa upanga”.
Kutoka 5:2 “Farao akasema, Bwana ni nani, hata niisikilize sauti yake, na kuwapa Israeli ruhusa waende zao? Mimi simjui Bwana, wala sitawapa Israeli ruhusa waende zao.
3 Wakasema, Mungu wa Waebrania amekutana nasi; twakuomba, tupe ruhusa twende safari ya siku tatu jangwani, tumtolee dhabihu Bwana, Mungu wetu; asije akatupiga kwa tauni, au kwa upanga”.
Soma tena..
Kutoka 8:25 “Farao akawaita Musa na Haruni akawaambia, Endeni mkamtolee Mungu wenu dhabihu ndani ya nchi hii. 26 Musa akasema, Haitupasi kufanya hivyo; kwa kuwa tutamchinjia sadaka Bwana, Mungu wetu, na hayo machukizo ya Wamisri; je! Tutachinja sadaka ya hayo machukizo ya Wamisri mbele ya macho yao, wasitupige kwa mawe? 27 La, tutakwenda safari ya siku tatu jangwani, tumchinjie dhabihu Bwana, Mungu wetu, kama atakavyotuagiza. 28 Farao akasema, Mimi nitawapa ruhusa mwende, ili mmchinjie dhabihu Bwana, Mungu wenu, jangwani; lakini hamtakwenda mbali sana; haya niombeeni”.
Kutoka 8:25 “Farao akawaita Musa na Haruni akawaambia, Endeni mkamtolee Mungu wenu dhabihu ndani ya nchi hii.
26 Musa akasema, Haitupasi kufanya hivyo; kwa kuwa tutamchinjia sadaka Bwana, Mungu wetu, na hayo machukizo ya Wamisri; je! Tutachinja sadaka ya hayo machukizo ya Wamisri mbele ya macho yao, wasitupige kwa mawe?
27 La, tutakwenda safari ya siku tatu jangwani, tumchinjie dhabihu Bwana, Mungu wetu, kama atakavyotuagiza.
28 Farao akasema, Mimi nitawapa ruhusa mwende, ili mmchinjie dhabihu Bwana, Mungu wenu, jangwani; lakini hamtakwenda mbali sana; haya niombeeni”.
Umeona hapo Farao anawaambia “lakini hamtakwenda mbali sana”…maana yake alikuwa anafikiri kwamba watarudi baada ya kutoka kule…na sehemu nyingine utaona Farao anawaambia waende tu huko jangwani watu walio wazee lakini Watoto wabaki na mifugo (soma kutoka 10:24)…Hivyo ikabakia kuwa siri ya Musa na wana wa Israeli kwamba siku yao ya kutoka Misri kikabisa kabisa imefika…Farao na waMisri hawakuijua hiyo siri, walidhani wanakwenda tu jangwani watarudi baada ya siku chache watakapomaliza kutoa sadaka zao hizo, watarudi na kuendelea kuwatumikisha.
Farao alikuja kushtuka kuwa kalaghaiwa na wale watu, wamekimbia na hawana mpango wa kurudi tena siku alipokuja kupata taarifa kuwa wale watu hawaelekea ile njia ya jangwa bali waligeuka na kurudi kuikabili bahari…Ndipo alipoelewa kuwa wamefanya makosa makubwa kuwaachilia waondoke.. Tusome
Kutoka 14:5 “Mfalme wa Misri aliambiwa ya kuwa wale watu WAMEKWISHA KIMBIA; na moyo wa Farao, na mioyo ya watumishi wake, iligeuzwa iwe kinyume cha hao watu, nao wakasema, Ni nini jambo hili tulilotenda, kwa kuwaacha Waisraeli waende zao wasitutumikie tena?”
Ndugu katika safari ya wokovu… si kila kitu kizuri Bwana anachokuambia ni cha kwenda kuwaambia watu kama kilivyo…Bwana amekuahidia au amekupa ufunuo fulani wa jambo lako zuri linalokuja mbele usikurupuke na kwenda kusimulia simulia huku na huko…kwa kufanya hivyo utakuwa umempa adui nafasi na mlango mzuri wa kuyaharibu maono yako uliyopewa..
Hali kadhalika Bwana anapokutoa leo katika ulimwengu(yaani katika dhambi)…ambao inafananishwa na Misri yetu…sio kila kitu ambacho Mungu kakufunulia ni cha kukieleza mbele za watu wa kidunia…Unatakiwa uondoke katika dhambi kwa njama kama hizo za wana wa Israeli..
Kwamfano Ulikuwa unauza Bar…na majirani zako wanauza bar kama wewe, sasa umempokea Yesu na Roho Mtakatifu amekushuhudia ndani yako kwamba, biashara hiyo ni ya utumwa wa dhambi na itakupeleka kuzimu…sasa wewe anza kuifunga hiyo haraka sio lazima uwaambie wale wanaokuzunguka sababu ya kuifunga, wewe jiponye nafsi yako kwanza huo sio wakati wa kuanza kuwahubiria….baada ya kuifunga na kuhakikisha marago yako yote umeyatoa Misri, ndipo uwaambie mimi nimeokoka na hiyo kazi siirudii tena….lakini ukiwahi kuwaambia kwamba nimeokoka na Kesho au Kesho kutwa nitaifunga hiyo Bar, au nitaacha hii kazi ya kujiuza, au nitaacha haya madili haramu tunayoyafanya, au nitaacha uvaaji wa nguo hizi na vimini hivi, au nitaacha dansi..ukianza kumwambia huyo mpenzi wako unayefanya naye uasherati kwamba sasa umeokoka hivyo kuanzia Kesho nakuacha…nataka nikuambie kwamba utakuwa umejiweka kupitia vita visivyokuwa na lazima…mwache kwanza huyo unayefanya naye uzinzi, ikiwezekana mtoroke baadaye akikuuliza kwanini umeondoka bila kuniambia mwambie ni kwasababu nimeokoka na siwezi tena kuishi Maisha ya uasherati…lakini ukimwambia huku bado upo naye nyumba moja….nakwambia shetani atakupelekesha kweli kweli na unaweza kujikuta huwezi kumwacha wala kuuacha ulimwengu….Utapitia vita visivyokuwa na sababu..
Vita vinatakiwa vianze baada ya wewe kuondoka katika ulimwengu..Ulimwengu unatakiwa ujue kwamba wewe umeokoka baada ya kuondoa marago yako yote ulimwenguni na sio wakati ambao wewe bado upo katika ulimwengu…kama vile wana wa Israeli walivyoondoa majeshi yao ndipo Farao akabutuka na kujua kuwa wale watu hawakwenda safari ya kwenda na kurudi..bali walipanga kupotelea moja kwa moja..ndipo akapanga majeshi kumfuatilia.
Hivyo kama hujaokoka leo? Huu ndio wakati wako sasa..Tubu mpokee Yesu, kutubu maana yake ni kugeuka na kuacha yale uliyokuwa unafanya mwanzo…na njia ni hiyo hiyo, fungasha marago yako yote na kimbia kimya kimpya!…usitoe taarifa kamili kwanini utatoka mpaka utakapotoka Misri…Toka Misri leo kwa njama zozote zile uwezazo…Toka kwenye ulevi, toka kwenye ulimwengu wa starehe za kidunia,miziki, toka kwenye huo mtandao wa wala rushwa, wizi, , utapeli, usengenyaji, uasherati, ulawiti,ufisadi…
Kwa mwanzo igiza hata unaumwa ili wakupe ruhusa utoke katika kampuni yao hiyo ya bia..na baadaye wakikuuliza mbona hurudi waambie mimi nimeokoka na huko sirudi tena..Igiza hata unakwenda kusalimia nyumbani ili tu huyo mtu unayeishi naye ambaye mnafanya naye uasherati akupe ruhusa uondoke na huko akiona hurudi akikuuliza vipi mwambie nimeokoka huku huku na Maisha hayo siyaishi tena. Jiponye nafsi yako kwa gharama zozote…
Dunia inapita na mambo yake yote..Bwana Yesu alisema itakufaidia nini upate ulimwengu mzima na upate hasara ya nafsi yako?…Ikimaanisha kuwa nafsi ni kitu cha kulinda kuliko kitu kingine chochote…hivyo kwa gharama zozote na njama zozote jiokoe nafsi yako na huu ulimwengu.
Maran atha!
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 5
JINA LA MUNGU NI LIPI?
UJIO WA BWANA YESU.
JIHADHARI NA DHAMBI YA WIVU/HUSUDA.
UPEPO WA ROHO.