Ikabodi maana yake ni “Utukufu umeondoka”
Hili ni jina ambalo alipewa mtoto wa Finehasi na mke wake siku alipokuwa anajifungua, na hiyo ni baada ya kusikia Mume wake amekufa katika vita, pamoja sanduku la agano kuchukuliwa na wafilisti na yeye vilevile anakaribia kufa ndipo akaona jina sahihi linalompasa huyo mtoto ni IKABODI, akiwa na maana kuwa utukufu wa Mungu umeondoka katika Israeli.
1Samweli 4:19 “Tena mkwewe, mkewe huyo Finehasi, alikuwa mja-mzito, karibu na kuzaa; basi, aliposikia habari ya kutwaliwa sanduku la Mungu, na ya kwamba mkwewe na mumewe wamekufa, akajiinamisha, akazaa; maana utungu wake ulimfikilia. 20 Hata alipokuwa katika kufa, wale wanawake waliohudhuria karibu naye wakamwambia, Usiogope; kwa maana umezaa mtoto mwanamume. Walakini hakujibu, wala hakumtazama. 21 Akamwita mtoto, IKABODI, akisema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; kwa sababu sanduku la Mungu lilikuwa limetwaliwa, na kwa sababu ya mkwewe na mumewe. 22 Naam, akasema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; maana sanduku la Mungu limetwaliwa”.
1Samweli 4:19 “Tena mkwewe, mkewe huyo Finehasi, alikuwa mja-mzito, karibu na kuzaa; basi, aliposikia habari ya kutwaliwa sanduku la Mungu, na ya kwamba mkwewe na mumewe wamekufa, akajiinamisha, akazaa; maana utungu wake ulimfikilia.
20 Hata alipokuwa katika kufa, wale wanawake waliohudhuria karibu naye wakamwambia, Usiogope; kwa maana umezaa mtoto mwanamume. Walakini hakujibu, wala hakumtazama.
21 Akamwita mtoto, IKABODI, akisema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; kwa sababu sanduku la Mungu lilikuwa limetwaliwa, na kwa sababu ya mkwewe na mumewe.
22 Naam, akasema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; maana sanduku la Mungu limetwaliwa”.
Lakini hiyo yote ni kwasababu ya Makosa ya Eli kuhani mkuu kutowazuia watoto wake (Hofni na Finehasi) kuinajisi madhabahu ya Mungu, kwa kulala na wale wanawake waliokuwa wanahudumu mbele ya hema ya Bwana. Japokuwa walionywa sana lakini hawakusikia, ndipo Mungu akamwambia Eli kwa kinywa cha Samweli kuwa atafanya jambo ambalo wakisikia, masikio yao wote yatawasha..Na jambo lenyewe ndio hilo la Sanduku la Mungu kuibwa na maadui jambo ambalo halijawahi kutokea katika historia ya taifa la Israeli.
Hata sasa, utukufu wa Mungu unaweza kuondoka katika kanisa Fulani(Ikabodi), ikiwa wahudumu au watumishi wa madhabahuni hiyo ya Mungu watainajisi nyumba ya Mungu kwa kufanya dhambi za makusudi, mfano wa hawa watoto wa Eli.
Vilevile utukufu wa Mungu unaweza kuondoka(Ikabodi), kwa mtu binafsi, ikiwa ataonywa mara nyingi asisikie. Ikiwa na wewe unaonywa mara nyingi auche dhambi, uache uzinzi, uache anasa, utubu umgeukie Kristo lakini husikii, upo wakati huo utukufu wa Mungu utaondoka ndani yako moja kwa moja, na siku ukiondoka basi habari yako imeishia hapo hapo kamwe hutakaa uiamini injili tena.
Hivyo ikiwa upo bado nje ya Kristo tubu dhambi zako ukabatizwe. Na Bwana atakuponya.
Kama upo tayari kufanya hivyo, fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Ubarikiwe.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo ya biblia kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?
USISUBIRI MPAKA MUNGU AKUAMBIE, NDIO UFANYE!
CHA KUTUMAINI SINA lyrics
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
EPUKA MUHURI WA SHETANI
Rudi Nyumbani:
Print this post
Mto Yordani uko nchi gani kwa sasa duniani?
Mto Yordani upo katika eneo la Mashariki ya kati, ni mto ambao unasimama kama mpaka wa mataifa mbalimbali, Ikiwemo Lebanoni, Syria, Israeli, na Yordani.
Ni kama vile ziwa Tanganyika lilivyo simama kama mpaka wa nchi 4, Congo, Burundi, Tanzania, na Zambia ndivyo ilivyo hata na kwa mto Yordani,
Nchi ya Yordani, unayoisikia leo hii pale mashariki ya kati, imechukua jina lake kutoka katika mto huu.
Mto huu chanzo chake ni kwenye chemchemi kadhaa zinazotiririka kutoka katika mlima Hermoni ulio mpakani mwa Lebanoni na Syria.Kisha kutoka hapo unateremsha maji yake mpaka Israeli kwenye bahari ya Galilaya/Tiberia/Genesareti. Na kutoka hapo unaibukia upande wa pili na kuendelea na safari yake moja kwa moja mpaka bahari ya Chumvi.
Tazama picha chini.
Mto huu, umekuwa kitovu katika historia ya Israeli kuanzia agano la kale mpaka agano jipya. Yoshua aliusimamisha mto huu na wana wa Israeli wakavuka kuelekea Yeriko.
Vilevile mto huu huu katika agano jipya ndio makutano mengi yalikuwa yanavuka kumwendea Yesu ili waponywe.(Mathayo 19:1-2), Na ni mto ambao Yesu mwenyewe alibatiziwa.
Kuonyesha kuwa ili nawe upate wokovu na ushindi dhidi ya maadui zako,na ili uponywe nafsi yako, ni lazima Uvuke Yordani yako ya Rohoni..Ili ukakutane na Yesu ng’ambo ya pili huna budi kuvuka Yordani, Na Unavukaje Yordani? Ni kwa kubatizwa, kama Yesu alivyobatizwa kwenye mto ule.
Hivyo na wewe sharti ukishamwamini Yesu moja kwa moja ukabatizwe, mahali popote penye maji tele kama ishara ya kuwa umeokoka kweli kweli. Na kuwa unakwenda kuwashinda maadui zako.
Marko 16:16 “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.
Wengi wanapuuzia maagizo haya ya msingi, wanadhani kuamini tu inatosha, Ndugu kubatizwa ni tendo lenye maana kubwa sana kwako rohoni, aliyetupa maagizo hayo hakuwa amekosa cha kutuagiza bali alijua umuhimu wake.
Swali Nji wewe umebatizwa ipasavyo? Kama sivyo basi kafanye hivyo.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda masomo yetu yawe yanakufikia njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Israeli ipo bara gani?
Wafilisti ni watu gani.
MJUMBE WA AGANO.
Zile mbao mbili za mawe Musa alizoambiwa achonge zilikuwaje?
Mlima sinai upo nchi gani? Na Je unaijua Sinai yako ya rohoni?
CHUKIZO LA UHARIBIFU
UNYAKUO.
Mlima sinai upo nchi gani? Na Je unaijua Sinai yako rohoni?
Mlima Sinai, au kwa jina lingine unajulikana kama Mlima Horebu, upo katika Rasi ya Sinai, Nchi ya Misri..Tazama katika picha.
Mlima huu, ni mlima ambao Mungu aliutumia kuwapa wana wa Israeli Torati na zile Amri 10. Ni mlima ambao wana wa Israeli waliutazama kwa muda mrefu kama mlima ambao unamtambulisha Mungu yupoje pale anapotaka kuzungumza na watu wake. Kufuatana na mstari huu;
Kutoka 19:16 “Ikawa siku ya tatu, wakati wa asubuhi, palikuwa na ngurumo na umeme, na wingu zito juu ya mlima, na sauti ya baragumu iliyolia sana. Watu wote waliokuwa kituoni wakatetemeka. 17 Musa akawatoa hao watu katika kituo, akawaleta ili waonane na Mungu; wakasimama pande za chini za kile kilima. 18 Mlima wa Sinai wote pia ukatoa moshi, kwa sababu Bwana alishuka katika moto; na ule moshi wake ukapanda juu kama moshi wa tanuu, mlima wote ukatetemeka sana. 19 Na hapo sauti ya baragumu ilipozidi kulia sana, Musa akanena, naye Mungu akamwitikia kwa sauti. 20 Bwana akaushukia mlima, juu ya kilele cha mlima; Bwana akamwita Musa aende hata kilele cha mlima; Musa akapanda juu”.
Kutoka 19:16 “Ikawa siku ya tatu, wakati wa asubuhi, palikuwa na ngurumo na umeme, na wingu zito juu ya mlima, na sauti ya baragumu iliyolia sana. Watu wote waliokuwa kituoni wakatetemeka.
17 Musa akawatoa hao watu katika kituo, akawaleta ili waonane na Mungu; wakasimama pande za chini za kile kilima. 18 Mlima wa Sinai wote pia ukatoa moshi, kwa sababu Bwana alishuka katika moto; na ule moshi wake ukapanda juu kama moshi wa tanuu, mlima wote ukatetemeka sana.
19 Na hapo sauti ya baragumu ilipozidi kulia sana, Musa akanena, naye Mungu akamwitikia kwa sauti.
20 Bwana akaushukia mlima, juu ya kilele cha mlima; Bwana akamwita Musa aende hata kilele cha mlima; Musa akapanda juu”.
Unaona, wana wa Israeli walijiundia picha kuwa siku zote Mungu akishuka mahali kuzungumza na mtu/watu ni lazima kuwe na moto, na matetemeko, na upepo mkali n.k. .
Eliya naye alidhani vivyo hivyo, wakati mmoja alipokuwa anamkimbia Yezebeli, alienda kwenye mlima huu wa Musa, mlima Sinai (Horebu) kwa ajili ya kukutana na Mungu, Na yeye akidhani kuwa ili Mungu ashuke mahali Fulani ni lazima uwepo moto, na matetemeko ya ardhi. Lakini siku hiyo alipokwenda kwenye mlima huo ndio alijua ukweli wote wa Mungu.
Ni kweli kama ilivyo ada, Mungu alijifunua kwake kama alivyojifunua kwa Musa na Wana wa Israeli kwa radi, mingurumo n.k. Lakini Eliya aligundua mbona bado simwona MUNGU?
1Wafalme 19:8 “Akainuka, akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu. 9 Akafika kunako pango, akalala ndani yake. Na tazama, neno la Bwana likamjia, naye akamwambia, Unafanya nini hapa, Eliya? 10 Akasema, Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia, mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu, waiondoe. 11 Akasema, Toka, usimame mlimani mbele za Bwana. Na tazama, Bwana akapita; upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima, ukaivunja-vunja miamba mbele za Bwana; lakini Bwana hakuwamo katika upepo ule; na baada ya upepo, tetemeko la nchi; lakini Bwana hakuwamo katika lile tetemeko la nchi; 12 na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; lakini Bwana hakuwamo katika moto ule; na baada ya moto sauti ndogo, ya utulivu. 13 Ikawa, Eliya alipoisikia, alijifunika uso wake katika mavazi yake, akatoka, akasimama mlangoni mwa pango. Na tazama, sauti ikamjia, kusema, Unafanya nini hapa, Eliya”?
1Wafalme 19:8 “Akainuka, akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu.
9 Akafika kunako pango, akalala ndani yake. Na tazama, neno la Bwana likamjia, naye akamwambia, Unafanya nini hapa, Eliya?
10 Akasema, Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia, mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu, waiondoe.
11 Akasema, Toka, usimame mlimani mbele za Bwana. Na tazama, Bwana akapita; upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima, ukaivunja-vunja miamba mbele za Bwana; lakini Bwana hakuwamo katika upepo ule; na baada ya upepo, tetemeko la nchi; lakini Bwana hakuwamo katika lile tetemeko la nchi;
12 na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; lakini Bwana hakuwamo katika moto ule; na baada ya moto sauti ndogo, ya utulivu.
13 Ikawa, Eliya alipoisikia, alijifunika uso wake katika mavazi yake, akatoka, akasimama mlangoni mwa pango. Na tazama, sauti ikamjia, kusema, Unafanya nini hapa, Eliya”?
Unaona Eliya alipoisia tu ile sauti ya utulivu na upole. Hapo ndipo alipousikia uwepo wa Mungu ukibubujika ndani yake akajua sasa Mungu ameshuka kuzungumza na mimi.. Hapo ndipo alipofahamu kuwa Mungu hakai katika milima, hakai katika tufani, hakai katika upepo wa kisulisuli, bali katika utulivu na upole.
Vivyo hivyo na wewe leo hii unahitaji kumwona Mungu, unahitaji kukutana na Mungu katika Sinai, yako..Basi jifunze kujinyenyekeza mbele zake, kaa katika utulivu mkubwa wa Roho, huku ukijifunza kanuni za Mungu katika maandiko, na hakika atajifunua kwako zaidi hata ya alivyojifunua kwa wana wa Israeli. Mungu ni mnyenyekevu na hivyo anajifunua kwa wanyenyekevu kwake, wanaolitii Neno lake.
Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; 30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.
Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au kwenye namba hii +255 789001312
Neno Korbani linamaanisha nini? (Marko 7:11)
SAYUNI ni nini?
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
Nitaitofautishaje sauti ya Malaika na ya Roho Mtakatifu?
Neno Kristo, na Masihi ni kitu kimoja, isipokuwa kwa lugha ya Kiebrania linatamkwa kama Masihi, lakini kwa lugha ya kigiriki linatamkwa kama Kristo.
Yohana 1:41 “Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo)”.
Hivyo Neno hili Kristo/Masihi linamaanisha mtiwa mafuta.
Mtiwa mafuta ni mtu yeyote aliyechaguliwa au aliyetengwa na Mungu kuwa wakfu kwa ajili ya kutimiza kusudi lake Fulani..Aidha na kuokoa, au kutawala, au kuchunga.
> Hivyo manabii wote unaowasoma katika biblia walikuwa ni masihi au Kristo kwa Mungu, kwa lengo la kuitabiria Israeli, na kuwaelekeza maagizo yatokayo kwa Mungu.
1Nyakati 16:22 “Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu”.
> Makuhani wote tunaowasoma katika biblia walikuwa ni masihi au maKristo wa Bwana wakifanya kazi ya upatanisho wa dhambi za watu na makosa yao.
> Waamuzi wote unaowasoma katika biblia walikuwa ni masihi wa Bwana waliotiwa mafuta kwa lengo la kuwakomboa wanadamu.Wakina Gideoni, Samsoni, Yeftha wote hao walikuwa ni masihi wa Bwana.
> Vilevile wafalme wote iwe ni wa wale waliotoka Israeli, au hawajatoka Israeli tunaowasoma katika biblia walikuwa ni masihi wa Bwana kwa ajili ya kuwaongoza watu wake.
1Samweli 24:5 “Lakini halafu, moyo wake Daudi ukamchoma, kwa sababu amekata upindo wa vazi lake Sauli. 6 Akawaambia watu wake, Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA,neno hili,kuunyosha mkono wangu juu yake,kwa maana yeye ni masihi wa BWANA”.
1Samweli 24:5 “Lakini halafu, moyo wake Daudi ukamchoma, kwa sababu amekata upindo wa vazi lake Sauli.
6 Akawaambia watu wake, Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA,neno hili,kuunyosha mkono wangu juu yake,kwa maana yeye ni masihi wa BWANA”.
Isaya 45:1 “Haya ndiyo Bwana amwambiayo Koreshi, masihi wake,ambaye nimemshika mkono wake wa kuume,ili kutiisha mataifa mbele yake,name nitalegeza viuno vya wafalme;ili kufungua milango mbele yake,hata malango hayatafungwa. 2 Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma”;
Isaya 45:1 “Haya ndiyo Bwana amwambiayo Koreshi, masihi wake,ambaye nimemshika mkono wake wa kuume,ili kutiisha mataifa mbele yake,name nitalegeza viuno vya wafalme;ili kufungua milango mbele yake,hata malango hayatafungwa.
2 Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma”;
Lakini hao wote walikuwa ni kivuli cha MASIHI/KRISTO MKUU NA HALISI atakayekuja, ambaye alitiwa mafuta mengi sana yasiyoelezeka kuliko wote, biblia inasema hivyo, na huyo si mwingine zaidi ya YESU.
Waebrania 1:8 “Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi,Mungu,ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili. 9 Umependa haki, umechukia maasi; KWA HIYO MUNGU, MUNGU WAKO, AMEKUTIA MAFUTA, MAFUTA YA SHANGWE KUPITA WENZIO”.
Waebrania 1:8 “Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi,Mungu,ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.
9 Umependa haki, umechukia maasi; KWA HIYO MUNGU, MUNGU WAKO, AMEKUTIA MAFUTA, MAFUTA YA SHANGWE KUPITA WENZIO”.
Na ndio maana haitwi tu Yesu peke yake, bali anaitwa YESU KRISTO.
Yesu Kristo ametiwa mafuta ya mengi sana ya kuwakomboa wanadamu. Yeye anayo mafuta yote ya kikuhani ndani yake, anayo mafuta ya kifalme ndani yake, anayo mafuta ya kinabii ndani yake, anayo mafuta ya kichungaji ndani yake.. Yaani kwa ufupi mafuta yote ya karama za Mungu yapo ndani yake.
Hivyo mtu akimwamini Yesu, basi amepata kila kitu, ikiwemo ukombozi wa roho yake.
Lakini tahadhari ni kuwa biblia imetabiri kuwa siku za mwisho kutatokea makristo wengi wa uongo ili kuwadanganya watu wengi.
Mathayo 24:24 “Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. 25 Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele”.
Mathayo 24:24 “Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.
25 Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele”.
Kumbuka anasema watatokea makristo, hasemi ma-yesu, ikiwa na maana kuwa watakuwa ni watiwa mafuta lakini ni watiwa mafuta ya uongo, watakuwa wanaweza kweli wakawaombea watu kwa jina la Yesu na wakapona lakini injili yao ni injili potofu isiyoweza kumwokoa yeye, wala hao anaowaongoza.
Na ndio maana Bwana Yesu alisema..
Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.
Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.
Hivyo je! Swali na wewe umechukuliwa na hili wimbi la makristo wa uongo?
Tunaishi katika wakati mgumu na wa hatari kuliko yote katika historia, hivyo kama maisha yako yapo mbali na Kristo basi ujue upo hatarini sana kupotezwa.
Kwanini usimpe Kristo leo maisha yako ayabadilishe, kisha yeye mwenyewe akupe Roho wake Mtakatifu atakayekusaidia kuijua kweli yote ya kimaandiko, ambaye atakaa ndani yako kukulinda mitego yote ya ibilisi?. Kama leo upo tayari kufanya hivyo, na unasema sitaki tena maisha ya dhambi nataka Yesu aniokoe awe peke yake masihi ndani yangu. Basi fungua link hii kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
UPAKO NI NINI?
KUWA MWAMINIFU KWA MANENO YAKO MWENYEWE,
AMELAANIWA AANGIKWAYE MSALABANI.
Yakobo alikuwa na watoto wangapi?
REKEBISHA YAFUATAYO ILI MAMBO YAENDE SAWA.
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU UPENDO.
NAMWANDAMA BWANA Lyrics~ Swahili?| Trust and Obey
Nyimbo hii iliandwa mwaka 1887, na Mchungaji mmoja aliyeitwa John H Sammis, (Mmarekani), ambaye alifanikiwa pia kuandika nyimbo nyingine Zaidi ya 100 zenye maudhi ya tenzi.
Historia ya wimbo huu ilianza siku moja, katika mkutano wa injili uliofanyika huko Massachusetts Marekani mwaka 1886, katika mkutano huo alisimama kijana mmoja ambaye alitoa ushuhuda wa wokovu wake, Kijana huyu alikuwa hajui mambo mengi kuhusu Mungu, ni mchanga katika wokovu, Lakini katika maneno yake machache alisema..
“Sina uhakika sana, lakini nitakwenda kuamini na kutii”
Maneno hayo yalimgusa sana mwendesha mziki aliyekuwa katika mkutano huo aliyeitwa Danieli Towner, mpaka akaamua kuyaandika maneno yale kwenye kikaratasi, na kisha baadaye akamtumia Rafiki yake ambaye alikuwa mchungaji aliyeitwa John H Sammis, huyo ndiye akauandika wimbo huo, “Namwandama Bwana”. Ambao ndani yake una vina vya maneno ya huyo kijana, nitaamini nitii.
Alipokuwa anauandika, alizingatia vipengele tofauti tofauti ya Maisha yetu tunayopaswa kutii.
NAMWANDAMA BWANA lyrics.
*****
******
Ni nini tunaweza kujifunza katika historia ya wimbo huu Namwandama Bwana ?
Ushuhuda wako, hata kama utakuwa ni mdogo vipi, unaweza ukawa chanzo cha baraka cha watu wengine wengi duniani na kuwaokoa. Kama kijana huyu angeudharau ushuhuda wake, leo hii tusingekuwa na tenzi yenye faraja ya kipekee kama hii maishani mwetu.
Hivyo nawe pia usigope kushuhudia mambo makuu ya Mungu maishani mwako.
Shalom.
TENZI ZA ROHONI
USINIPITE MWOKOZI Lyrics
BWANA MUNGU NASHANGAA KABISA lyrics
NI SALAMA ROHONI MWANGU Lyrics
KUMTEGEMEA MWOKOZI Lyrics/Swahili.
UFUNUO: Mlango wa 1
NI KITU GANI PETRO NA YOHANA WALIKIGUNDUA KABURINI?
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tuyatafakari maandiko pamoja.
Katika maisha, hakikisha unarekebisha vitu vinne. 1) Kazi unayoifanya 2) Kabila unalotoka 3) Nchi unayotoka 4) Mahali unapotoka.
Haya ni mambo makuu manne ambayo ni nguzo katika kuyajenga au kuyaharibu maisha. Na kimojawapo kisipokaa sawa mbele za Mungu, basi kitakuletea tufani kubwa katika maisha.
Hebu tuisome kidogo habari ifuatayo..
Yona 1:7 “Wakasemezana kila mtu na mwenzake, Haya, na mpige kura, mpate kujua mabaya haya yametupata kwa sababu ya nani. Basi wakapiga kura, nayo kura ikamwangukia Yona. 8 Ndipo wakamwambia, Tafadhali utuambie, wewe ambaye mabaya haya yametupata kwa sababu yako; kazi yako ni kazi gani? Nawe umetoka wapi? Nchi yako ni nchi ipi? Nawe u mtu wa kabila gani? 9 Akawaambia, Mimi ni Mwebrania; nami namcha Bwana, Mungu wa mbingu, aliyeziumba bahari na nchi kavu. 10 Ndipo watu wale wakaogopa mno, wakamwambia, Ni jambo gani hili ulilolitenda! Kwa maana watu wale walijua ya kuwa amekimbia, ajiepushe na uso wa Bwana, kwa sababu alikuwa amewajulisha. 11 Basi wakamwambia, Tukutende nini, ili bahari itulie? Kwa maana bahari ilikuwa inazidi kuchafuka“
Yona 1:7 “Wakasemezana kila mtu na mwenzake, Haya, na mpige kura, mpate kujua mabaya haya yametupata kwa sababu ya nani. Basi wakapiga kura, nayo kura ikamwangukia Yona.
8 Ndipo wakamwambia, Tafadhali utuambie, wewe ambaye mabaya haya yametupata kwa sababu yako; kazi yako ni kazi gani? Nawe umetoka wapi? Nchi yako ni nchi ipi? Nawe u mtu wa kabila gani?
9 Akawaambia, Mimi ni Mwebrania; nami namcha Bwana, Mungu wa mbingu, aliyeziumba bahari na nchi kavu.
10 Ndipo watu wale wakaogopa mno, wakamwambia, Ni jambo gani hili ulilolitenda! Kwa maana watu wale walijua ya kuwa amekimbia, ajiepushe na uso wa Bwana, kwa sababu alikuwa amewajulisha.
11 Basi wakamwambia, Tukutende nini, ili bahari itulie? Kwa maana bahari ilikuwa inazidi kuchafuka“
Walipoanza kwenye nchi, aliwaambia yeye ni Mwebrania..hivyo wakajua moja kwa moja ni mtu wa Taifa la Israeli,ametokea katika mojawapo ya miji ya kule, alipoendelea mbele kidogo, kwenye shughuli anayoifanya akasema yeye anamcha Mungu (yaani maana yake ni mtumishi wa Mungu), anayehudumu katika shamba la Mungu, na kwamba ameikimbia kazi ya Mungu, ndipo walipoelewa tatizo lipo hapo, wakaogopa na kutafuta suluhisho kabla mambo hayajazidi kuharibika.
Sasa endapo Yona ingekuwa hajaikimbia kazi ya Mungu na baharini imewachafukia vile, basi tatizo ni lazima lingekuwa aidha kwenye kabila analotokea, na kama sio kwenye kabila basi kungekuwa na tatizo kwenye nchi anayotokea..au mahali anapotokea.
Hivyo Nataka uone leo kwamba kazi yako unayoifanya inaweza kuwa chanzo cha Tufani na misukosuko, hakikisha kazi unayoifanya yoyote ile aidha ya mikono, iwe inampendeza Mungu kwa viwango vyote, uwe mwaminifu katika kazi yako na pia jiepushe na hila na wizi. Vilevile kama unafanya kazi ya Mungu hakikisha hukwepi majukumu yako kama mtumishi, wala huifanyi kwa ulegevu vinginevyo utakumbana na tufani kama iliyokuta Yona.. Na mkristo yoyote ni lazima awe na jukumu katika kazi ya Mungu. Hivyo jihakiki sana.
Yeremia 48:10 “Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya Bwana kwa ulegevu”
Vile vile kabila unalotoka linaweza kuwa chanzo cha matatizo. Makabila mengi yana mila na desturi zilizo kinyume na Neno la Mungu, makabila mengi yana matambiko na ushirikina, jiepushe na hayo yote baada ya kuokoka. Zipo mila nyingine ambazo ni aibu hata kuzisema hapa..Hizo zote ni rahisi kukusababisha tufani katika maisha yako, na hasira ya Mungu kuwaka juu yako. Jiepushe na hizo mila…Sisemi kwamba ujiepushe na ndugu zako au wazazi wako wanaofanya hizo mila!, na uwachukie na kuwasema Hapana!..endelea kubaki na ndugu zako, waheshimu,wapende, watunze, waombee, na ishi nao kwa furaha zote na kushirikiana nao kwa mambo mengine yote mazuri wanayoyafanya lakini usishiriki mila hizo zilizo kinyume na neno la Mungu.
Pia nchi unayotokea au mahali ulipo panaweza kuwa chanzo cha tufani katika maisha yako..Hivyo ni wajibu wa kushiriki mambo mazuri yanayoendelea katika nchi yako, na kuyakataa yale mabaya yote, Nchi inaweza kuhalalisha ndoa za jinsia moja kisheria kabisa!, nchi inaweza kuhalalisha uvutaji wa bangi, nchi inaweza kuhalalisha utoaji mimba, nchi inaweza kuhalalisha ndoa za wanadamu na wanyama n.k.
Nchi ya namna hiyo tayari ipo chini ya laana na hasira ya Mungu na watu wake ni hivyo hivyo..Hivyo ni wajibu wa wewe uliyeokoka unayeishi ndani ya nchi kama hiyo, kujitenga kwa kutofanya hayo mambo au kukubaliana nayo, ili usiwe miongoni mwa wanaomwudhi Bwana Mungu. Na kujitenga sio kutoongea nao, au kutofanya nao kazi kwenye kampuni moja!..hapana..bali kujiepusha na njia zao, mfano wa Danieli, Meshaki, Shedraka na Abednego jinsi walivyoishi katikati ya taifa la Babeli lakini hawakushiriki matendo ya watu wa Babeli, na walifanikiwa sana katikati ya Taifa lile ovu.
Bwana atusaidie na Bwana atubariki
Na mwisho kabisa kama umejaliwa kupata watoto, au unampango wa kuwa na watoto..kumbuka kuwalea katika njia inayowapasa, angali wakiwa wadogo, kwasababu wakiwa wakubwa hawataiacha biblia inasema hivyo, Na pia wewe mwenyewe kama hujaokoka!. Mlango wa Neema upo wazi, usiidharau injili hata kidogo inayohubiriwa kwako bure! Bila kutozwa chochote… Hata vitu vingi vinavyoishiaga kutolewa bure mara nyingi huwa ni vya gharama sana na vya muhimu sana, kwasababu kama vingeuzwa basi hakuna mtu angeweza kununua..
Hata madawa yanayotolewa bure! Mengi ni ya gharama ya juu sana, yananunuliwa ghali sana aidha na serikali au mashirika binafsi lakini yanakuja kutolewa bure tu kwa watu ili kuokoa maisha!. Na wokovu ni wa gharama sana na wa muhimu kwa kila mtu, ndio maana tunapewa bure!, hivyo usiudharau, Laiti tungetozwa fedha ili kuupata, basi hakuna ambaye angeweza kuununua, hata dunia nzima tungekusanya nguvu zetu zote, tusingeweza kununua wokovu wa mtu mmoja tu! Licha ya watu wa dunia nzima. Mpokee Yesu leo kama hujampokea, na ukabatizwe na kupokea Roho Mtakatifu. Kwa usalama wa maisha yako.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
YONA: Mlango 1
YONA: Mlango wa 2
JINA LA MUNGU NI LIPI?
USIPOKUWA MWAMINIFU, NAFASI YAKO ITACHUKULIWA.
KUMCHA MUNGU NI NINI? NA MTU ANAMCHAJE MUNGU?
JE NI LAZIMA MKRISTO AOE/AOLEWE?
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..
KAMA ZILIVYOKUWA SIKU ZA NUHU NA ZA LUTU.
Yakobo, mjukuu wa Ibrahimu, alipewa neema na Mungu ya kuwa na Watoto 13, Kati ya hao 12 ni wa kiume na 1 wa kike aliyejulikana kama Dina.
Yakobo alikuwa na wake wawili, Na hao wake zake kila mmoja alikuwa na kijakazi wake mmoja, ambao baadaye walikuja kufanyikiwa kuwa masuria wa Yakobo.
Mke wa kwanza aliitwa Lea, Na mke wa pili aliitwa Raheli. Kijakazi wa Lea aliitwa Zilpa Na kijakazi wa Raheli aliitwa, Bilha.
Habari yote ya uzao wao utaipata katika kitabu cha Mwanzo, kuanzia sura ya 29 na kuendelea.
Mwanzo 29:31 “Bwana akaona ya kwamba Lea hakupendwa, naye akafungua tumbo lake; bali Raheli alikuwa hazai. 32 Lea akapata mimba akazaa mwana, akampa jina lake, Reubeni, maana alisema, Kwa kuwa Bwana ameona teso langu; sasa mume wangu atanipenda. 33 Akapata mimba tena akazaa mwana, akasema, Kwa kuwa Bwana amesikia ya kwamba mimi sikupendwa, amenipa na huyu; akamwita jina lake Simeoni. 34 Akapata mimba tena, akazaa mwana, akasema, Basi wakati huu mume wangu ataungana nami, kwa sababu nimemzalia wana watatu. Kwa hiyo akamwita jina lake Lawi. 35 Akapata mimba tena, akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu Bwana; kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; akaacha kuzaa…………..”
Mwanzo 29:31 “Bwana akaona ya kwamba Lea hakupendwa, naye akafungua tumbo lake; bali Raheli alikuwa hazai.
32 Lea akapata mimba akazaa mwana, akampa jina lake, Reubeni, maana alisema, Kwa kuwa Bwana ameona teso langu; sasa mume wangu atanipenda.
33 Akapata mimba tena akazaa mwana, akasema, Kwa kuwa Bwana amesikia ya kwamba mimi sikupendwa, amenipa na huyu; akamwita jina lake Simeoni.
34 Akapata mimba tena, akazaa mwana, akasema, Basi wakati huu mume wangu ataungana nami, kwa sababu nimemzalia wana watatu. Kwa hiyo akamwita jina lake Lawi.
35 Akapata mimba tena, akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu Bwana; kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; akaacha kuzaa…………..”
Angalia Habari za watakatifu wengine wa kale chini.
Pia kama utapenda mafundisho ya biblia yawe yanakufikia kila mara kwa njia ya whatsapp basi utatumie ujumbe kwa namba hii : +255 789001312
Nuhu alikuwa na watoto wangapi?
Mariamu Magdalene ni nani. Na hilo jina amelitolea wapi?
Bwana aliposema kuwa yeye ni “Mungu wa miungu” alikuwa na maana gani?..je! yeye ni Mungu wa sanamu?
VIFO VYA MITUME WA YESU/ JINSI MITUME WALIVYOKUFA.
Nimrodi ni nani?
Yeshuruni ni nani katika biblia?
Kuota unaolewa/ unaoa kunamaanisha nini?
Zipo ndoto zenye maana katika Maisha yetu, na pia zipo ndoto zisizo na maana yoyote katika Maisha yetu,.
Hizi zisizo na maana ni ndoto ambazo, ubongo wetu unajiundia wakati tunapokuwa tumelala kutoka katika mazingira yetu yanayotuzunguka, au mambo ambayo tulikuwa tunayawaza au tunayafanya mara kwa mara, Na ndio maana biblia inasema;
Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi..”
Hivyo asilimia kubwa ya ndoto tunazoziota kila siku, zinaangukia katika hili kundi. Kama wewe ni mshonaji, basi tarajia asilimia kubwa ya ndoto utakazokuwa unaota mara kwa mara zitakuwa ni za namna hiyo,..Vilevile ndoto kama Kuota unaolewa/unaoa, wazo hilo pengine si geni katika kichwa chako,kwamba siku moja umekuwa ukifikiria kuwa utakuja kuoa au utaolewa, Hususani pale unapokuwa umefikia umri huo, lakini bado haijawa hivyo kwako.
Au inakuja kutokana na kuwa umekuwa ukihudhuria mazingira ya harusi mara kwa mara, Hivyo ubongo wako ukayachukua hayo matukio na kuyarudia hivyo hivyo au kwa namna nyingine unapokuwa umelala.
Lakini pia ndoto za namna hii zinaweza kuwa ni za rohoni, hivyo kubeba maana Fulani,
Kwa mfano ikiwa ulikuwa katika kumwomba Mungu, akupe mume/mke, ukiota upo katika ndoa, basi ujue jambo hilo lipo mlangoni kwako.
Lakini unachopaswa kufanya ili Mungu akupe sawasawa na chaguo lake.
Lakini ukiwa ni mzinifu, unatanga tanga na kila mwanaume, au mwanamke, au unaishi mtu ambaye hamjaona, sahau Mungu kulitekeleza hilo, na kama likifanikiwa basi ujue huyo utakayempata hujachaguliwa na Mungu.
Ili kufahamu njia sahihi ya kumpa mweza wa Maisha fungua hapa;
>>> NJIA SAHIHI YA KUMPATA MWENZA WA MAISHA KIBIBLIA.
Lakini hayo yote ni lazima uwe katika wokovu, ukimpata Kristo, umepata vyote, Ukimkosa yeye, umepoteza vyote mpaka uzima wako. Hivyo kama leo hii unahitaji kumkaribisha Bwana Yesu maishani mwako, basi uamuzi huo ni mzuri kwako..Ikiwa upo tayari kufanya hivyo sasa, basi fungua link hii, kwa ajili ya kuongozwa sala ya toba. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Pia kama utahitaji kujiunga katika magroup yetu ya Whatsapp unaweza ukabofya hapa chini>>
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Bahari mbalimbali zilizoorodheshwa kwenye biblia.
UNAMCHUKULIA YESU KWAKO KAMA NANI?
KUOTA UNA MIMBA.
KUOTA UPO UCHI.
KUOTA NYOKA.
Je! Unazijua faida za kufunga na kuomba?
Embu isome Habari ifuatayo kwa makini;
Mathayo 17:18 “Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile. 19 Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa? 20 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. 21 [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga”.
Mathayo 17:18 “Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile.
19 Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa?
20 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.
21 [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga”.
Mstari wa 21 unasema.. “Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga”
Hii ikiwa na maana kuwa yapo mambo ambayo mtu atashindwa kuyafanya, haijalishi yeye ni mkristo au la, haijalishi yeye ni mtakatifu au la! kama hafungi na kuomba, basi atashindwa kufanya mambo mengi sana.
Embu tuzitazame faida za kufunga na kuomba..
1) Pale mtu unapofunga, ina maana kuwa hali chakula, au hanywi maji, kwa wakati Fulani, Na hiyo inampelekea mtu kuwa katika uhitaji mkubwa, Sasa uhitaji huo ndio unaoutesa mwili na kufanya mates ohayo yapenye mpaka kwenye nafsi ya mtu. Nafsi ya mtu ikishapokea mabadiliko hayo inaifanya roho ya mtu kuwa na mwitikio wa tofauti sana katika mambo ya rohoni. Tofauti na mtu ambaye hajafunga kabisa.
Kufungu kunakwenda sambamba na magonjwa, kwamfano mtu aliye katika hali nzito ya kuumwa au kuugua mwilini, mateso yale huwa yanashuka mpaka kwenye nafsi ya mtu, na ndio hapo utaona wagonjwa wengi wapo karibu na Mungu kuliko watu walio na afya zao,
Sasa turudi katika kufunga, pale unapofunga hata maombi yako yanakuwa na uzito wa tofauti ukilinganisha na siku nyingine ambazo ulikuwa hufungi, (jaribu hilo utalithibitisha) kama ulikuwa katika kuyatafakari maandiko, uelewa wako unakuwa wa ndani Zaidi tofauti na siku nyingine ambazo ulikuwa hufanyi hivyo .
Na kwa jinsi atakavyozidi kuenendelea kufunga kwa siku nyingi, ndivyo utakavyozidi kuwa mwepesi katika mambo ya rohoni.
Musa alifanikiwa kufunga siku 40 asiku na mchana bila kula, na sote tunajua ni nini alipata kule mlimani..Mungu alizungumza naye uso kwa uso, na kumpa zile Amri 10, Vivyo hivyo hata kwa Eliya naye alipofunga siku 40, Mungu alisema naye kwenye ule ule mlima wa Musa..
Halikadhalika na kwa Bwana wetu Yesu Kristo, yeye pia alifunga siku 40 usiku na mchana bila kula chochote, mpaka ibilisi akatokea kumjaribu na kushindwa na aliposhuka kule mlimani alishuka na nguvu nyingi za Roho Mtakatifu ndipo akaanza kuhubiri injili na kuponya wangojwa katika Israeli yote.
Hivyo mifungo ya muda mrefu inafaa sana.
2) Faida nyingine ya kufunga inakusaidia kushusha chini matamanio ya mwili. Kwa kuwa chakula kinakuwa hakina sehemu kubwa katika mwili kwa wakati huo, hivyo hata kazi za uzalishaji wa homoni, zinapungua na hivyo inamfanya yule mfungaji awe katika hali ya utulivu Zaidi katika kumtafuta Mungu.
Biblia inatuambia pia, ukifunga, Mungu anakupa thawabu, Hiyo ni kuonyesha kuwa Mungu anathamini kujitesa kwetu kwa ajili yake.
Mathayo 6:16 “Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. 17 Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; 18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.
Mathayo 6:16 “Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.
17 Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;
18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.
Lakini pia unapaswa kujua kuwa kufunga kokote ni lazima kuambatane na kuomba..hivi ni vitu viwili vinavyokwenda sambamba, ni sawa na chai na sukari, unapobandika chai jikoni, inamaanisha kuwa sukari ni lazima iwepo chini pale inaongojea chai iepuliwe, vinginevyo haitaitwa chai.
Vivyo hivyo na Katika kufunga, hupaswi kufunga tu, unaamka asubuhi, unarudi jioni, halafu hufanyi lolote, unarudia tena hivyo kesho, na kesho kutwa,..hapo ni sawa na kufanya “diet” tu , Lakini unapofunga ni lazima uwe na malengo ya rohoni kwanini unafanya hivyo.
Hapo ndipo hapo sasa suala la kuomba lazima lijitokeze; Danieli alipofunga alikuwa mwombaji, vivyo hivyo na watu wote katika biblia..
Danieli 9:3 “Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu. 4 Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake; 5 tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako”;
Danieli 9:3 “Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.
4 Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake;
5 tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako”;
Ukizingatia vigezo hivyo basi faida za kuomba ni kama zifuatazo;
Mathayo 26:40 “ Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja? 41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu”
Mathayo 26:40 “ Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja?
41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu”
Mathayo 6:5 “Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao 6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.
Mathayo 6:5 “Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao
6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi”.
Kama tulivyoona katika mistari ya mwanzoni juu, Bwana aliwaambia wanafunzi wake, pale waliposhindwa kutoa mapepo, kuwa namna ile haitoki isipokuwa kwa kufunga na kusali. Hata wewe unapojijengea ustaarabu wa kuwa mwombaji mzuri, basi unapokea mamlaka kubwa Zaidi ya kuamrisha nguvu za giza ziwatoke watu.
Siri nyingine ya maombi ni kuwa, kwa jinsi unavyodumu kwenye kuomba ndivyo unavyoukaribisha uwepo wa Mungu ndani yako..Na matokeo yake ni kuwa ile furaha ya wokovu inajengeka ndani yako.
Usipokuwa mwombaji, ni ngumu sana kuufurahia wokovu wako, utaona kama Mungu yupo mbali na wewe kila siku, utakosa ujasiri wa Imani yako, lakini ukiwa mwombaji amani Fulani utaipata na ujasiri.
Hivyo kama wewe, ulikuwa unalega lega, au ulikuwa hujua faida za kufunga, basi anza leo kufanya hivyo, pia hakikisha unajijengea utaratibu wa kuomba, saa moja kila siku, hicho ndio kiwango cha chini tulichopewa na Bwana Yesu.Kama ukifanya hivyo hakika utaona matokeo makubwa katika Maisha yako..
Utaona tofauti yako ya leo na jana.
Ikiwa utatamani kujua Zaidi juu ya faida za kufunga, basi tazama masomo mengine yaliyoorodheshwa chini hapa.
Lakini Kama hujaokoka, na unatamani kuokoka leo, Basi uamuzi huo ni mzuri sana, hivyo fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >>>>>
KUONGOZWA SALA YA TOBA
NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.
Namna ya kuomba
KAMA UNAPENDA MAISHA, NA KUTAKA SIKU YAKO IWE NJEMA.
KIAMA KINATISHA.
NA NENO LA BWANA LILIKUWA ADIMU SIKU ZILE.
SABATO TATU NI NINI?
Kuota unalia kwa uchungu/Ukiota unalia maana yake ni nini kibiblia?.
Zipo ndoto zenye maana, na pia zipo ndoto zisizo na maana yoyote katika maisha ya mtu, hizi za pili ni ndoto ambazo zinatengenezwa na ubongo wako tu wenyewe, kwa kuchukua matukio ambayo aidha ulishawahi kuyafanya au kuyapitia huko nyuma, au mazingira unayoishi sasa, au mambo unayoyafanya mara kwa mara.
Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi…;”
Kwamfano kama wiki iliyopitia ulikuwa unahudhuria sana kwenye sherehe, tarajia moja ya ndoto unazoziota kila siku kuwa za namna hiyo.. Vivyo hivyo na ndoto hii ya kuota unalia/ukiota unalia kwa uchungu, inaweza kuja kutokana na mazingira yako ya nyuma, Wengine walifiwa na jamaa zao wa karibu kipindi sio kirefu, wengine walikuwa misibani.n.k..Hivyo ubongo unachukua matukio hayo na kuyarudia rudia kwenye ndoto zetu za kila siku.
Lakini pia ndoto ya namna hii inaweza kuja kwa namna ya kitofauti sana, pengine hujafiwa siku za hivi karibu, au hujapitia matatizo yoyote mazito ya kukufanya uwe katika huzuni kubwa..Lakini unashangaa usiku umeota unalia kwa uchungu mwingi, bila kujua sababu ya kulia kwako ni nini. Unalia tu, unalia tu,
Ukiona hivyo basi lipo jambo unapaswa ulijue rohoni..
Ndugu unayesoma ujumbe huu, fahamu kuwa hizi ni siku za mwisho, na Yesu anakaribia kuja kulinyakua kanisa lake. Mwisho wa dunia upo karibu sana.
Kuota unalia kwa uchungu, Ni Mungu anakuonyesha kuwa jinsi hali itakavyokuja kuwa huko mbeleni ikiwa utaachwa katika unyakuo, na watu wote watakavyokuwa..Haijalishi wewe ni muislamu, ujumbe huu unakuhusu pia wewe, kiama kipo karibu, watu wataomboleza, kwa kilio na uchungu usioeleza, kwa hayo mambo ya kutisha ambayo Mungu atayaleta katika hii dunia,
Biblia inasema hivi;
Sefania 1:14 “Hiyo siku ya Bwana iliyo kuu i karibu; I karibu, nayo inafanya haraka sana; Naam, sauti ya siku ya Bwana; SHUJAA HULIA KWA UCHUNGU MWINGI HUKO! 15 Siku ile ni siku ya ghadhabu, Siku ya fadhaa na dhiki, Siku ya uharibifu na ukiwa, Siku ya giza na utusitusi, Siku ya mawingu na giza kuu, 16 Siku ya tarumbeta na ya kamsa, Juu ya miji yenye maboma, Juu ya buruji zilizo ndefu sana. 17 Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda Bwana dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi. 18 Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya Bwana; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha”.
Sefania 1:14 “Hiyo siku ya Bwana iliyo kuu i karibu; I karibu, nayo inafanya haraka sana; Naam, sauti ya siku ya Bwana; SHUJAA HULIA KWA UCHUNGU MWINGI HUKO!
15 Siku ile ni siku ya ghadhabu, Siku ya fadhaa na dhiki, Siku ya uharibifu na ukiwa, Siku ya giza na utusitusi, Siku ya mawingu na giza kuu,
16 Siku ya tarumbeta na ya kamsa, Juu ya miji yenye maboma, Juu ya buruji zilizo ndefu sana.
17 Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda Bwana dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi.
18 Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya Bwana; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha”.
Unaona, hali itakavyokuwa kwa watu hata wale wanaojiona mashujaa leo, watalia kwa uchungu mwingi..
Isaya 33:7 “ANGALIA, MASHUJAA WAO WANALIA NJE, WAJUMBE WA AMANI WANALIA KWA UCHUNGU. 8 Njia kuu zimeachwa, msafiri amekoma; ameyavunja maagano, ameidharau miji, hamjali mtu. 9 Nchi inaomboleza, na kulegea; Lebanoni imetahayarika na kunyauka; Sharoni imekuwa kama jangwa; Bashani na Karmeli zimepukutika majani”.
Isaya 33:7 “ANGALIA, MASHUJAA WAO WANALIA NJE, WAJUMBE WA AMANI WANALIA KWA UCHUNGU.
8 Njia kuu zimeachwa, msafiri amekoma; ameyavunja maagano, ameidharau miji, hamjali mtu.
9 Nchi inaomboleza, na kulegea; Lebanoni imetahayarika na kunyauka; Sharoni imekuwa kama jangwa; Bashani na Karmeli zimepukutika majani”.
Ni mambo ya kutisha sana, ikiwa leo Yesu amerudi, na umeachwa, kitakachokuwa kinaendelea kwako, ni zaidi ya ulichokiona katika ndoto..
Yeremia 4:8 “Kwa sababu hiyo jifungeni nguo za magunia; ombolezeni na kulia kwa uchungu; kwa maana hasira kali ya Bwana haikugeuka na kutuacha. 9 Na katika siku hiyo itakuwa, asema Bwana, moyo wa mfalme utapotea, na moyo wa wakuu wake; na makuhani watastaajabu, na manabii watashangaa”.
Yeremia 4:8 “Kwa sababu hiyo jifungeni nguo za magunia; ombolezeni na kulia kwa uchungu; kwa maana hasira kali ya Bwana haikugeuka na kutuacha.
9 Na katika siku hiyo itakuwa, asema Bwana, moyo wa mfalme utapotea, na moyo wa wakuu wake; na makuhani watastaajabu, na manabii watashangaa”.
Mathayo 13:41 “Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi, 42 na kuwatupa katika tanuru ya moto, NDIKO KUTAKUWAKO KILIO NA KUSAGA MENO”.
Mathayo 13:41 “Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi,
42 na kuwatupa katika tanuru ya moto, NDIKO KUTAKUWAKO KILIO NA KUSAGA MENO”.
Yapo maandiko mengi yanayoelezea maombolezo yatakayokuwa yanaendelea katika kipindi hicho lakini hatuwezi kuiorodhesha yote hapa, Kama utapenda kufahamu kwa marefu juu ya siku hiyo ya mwisho itakavyokuwa basi fungua hapa usome.>>> MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
Hivyo Kama wewe hujaokoka, na unajijua kabisa unaishi katika maisha ya dhambi, basi ni vema ukamgeukia Kristo leo, ayaokoe maisha yako, Kukutana na ujumbe huu sio bure, Umeoteshwa ndoto hiyo ni kwasababu Mungu ana mpango na wewe. Hivyo usifanye moyo wako mgumu, mkabidhi Yesu maisha yako leo aanze kutembea na wewe na hakika utamwona kwa namna ambayo hukuwahi kumtazamia, na atahakikisha kuwa mabaya hayo yote hayatakukuta ikiwa atarudi leo..
Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki sana.
Pia angalia vichwa vya masomo mengine chini, fungua upitie naamini vitakutoa sehemu moja kiroho hadi nyingine.
Ikiwa utapenda kupata mafundisho ya Neno la Mungu ya kila siku kwa njia ya whatsapp basi tutumie ujumbe kwa namna hii: +255 789001312
Au jiunge kwa kubofya hapa chini;
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
NA YEYE ALIYEKETI JUU YA WINGU AKAUTUPA MUNDU WAKE JUU YA NCHI, NCHI IKAVUNWA.
SIKU ILE NA SAA ILE.
MAONO YA NABII AMOSI.
FAHAMU MAJIRA ULIYOPO NA NINI UNAPASWA UWE NACHO.