Category Archive Home

BABA YANGU ANATENDA KAZI HATA SASA!.

Shalom! Mwana wa Mungu, Karibu tujifunze Neno la Mungu…ambapo leo tutajifunza mambo machache yahusuyo utendaji kazi wa Mungu. Tutajifunza ni wakati gani Mungu anatenda kazi kwa watu wake.

Swali ambalo limekuwa ni changamoto kueleweka, na linaloulizwa na wengi ni kuhusu siku gani inayopasa iwe ni ya kuabudia au ya kukutana na Mungu, je! ni jumapili, jumamosi au lini?…miongoni wa wanaosema jumamosi ndio siku ya kuabudu mstari mama wanaousimamia ndio huu:

Mwanzo 2: 3 “Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya”

Hali kadhalika pia miongoni mwa wanaosimamia kuwa jumapili ndio siku ya kuabudu, mstari huu ndio msingi wao.

Marko 16: 9 “Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambaye kwamba alimtoa pepo saba”..

Kulingana na mstari huo siku ya kwanza ya juma ni jumapili, Hivyo hiyo ndio siku ya kupumzika na kuabudia kulingana na wao kwasababu ni siku ambayo walipata ushindi wao kwa kufufuka kwa Bwana Yesu.

Kumekuwa na kushindana kusikoisha kati ya makundi haya mawili, kila moja likitetea hoja zake..Lakini Biblia inasema Mungu ni Roho nao wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

Kwahiyo Mungu aliruhusu watu waishike sabato katika agano la kale, kufunua sabato halisi itakayokuja huko mbeleni (yaani pumziko la roho), kadhalika aliruhusu wana wa Israeli katika agano la kale wakati wanatoka Misri waishike pasaka (ile siku waliyotoka Misri), kufunua pasaka wetu halisi atakayekuja huko mbeleni yaani (Bwana wetu Yesu Kristo), ambaye kwa yeye tunapata ondoleo la dhambi na kutolewa kutoka katika utumwa wa dhambi. 1 Wakorintho 5: 7 “Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;”

Kwahiyo katika agano jipya hatuna sheria yoyote ya lazima ya kushika sabato wala pasaka, wala sikukuu yoyote ile..Kwasababu tumepata ufunuo kamili wa mambo hayo yalikuwa yanamaana gani.

Wakolosai 2:15 “akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.

16 Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au SABATO; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo”

Pia jambo lingine la muhimu la kujua ni kuwa, Mungu hana siku maalumu ya kupumzika, kwa sababu yeye hachoki, Neno linaposema “katika siku ya saba aliacha kufanya kazi zake zote akapumzika” haimaanishi kuwa katika siku ya saba..shughuli zake zote alizisimamisha au zilisimama hapana!! bali alimaanisha kuwa katika siku hiyo “aliacha kufanya kazi ya kuumba vitu vipya”..

Kwasababu kama katika siku ya saba shughuli zake zote zilisimama basi mwanadamu pia angeacha kupumua kwasababu na yeye ni kazi ya Mungu, wanyama pia wangesimama kupumua, na kila kitu kingesimama, hata jua lingesimama..lisingekuchwa,na mito nayo ingesimama, kwasababu vyote hivyo ni kazi ya Mungu, unaona! lakini tunaona vitu vyote viliendelea kama kawaida hata katika hiyo siku ya saba, maji yaliendelea na mizunguko yake, jua liliendelea kusogea, miti iliendelea kuota n.k..kwahiyo kazi ya Mungu ilikuwa inaendelea…na inaendelea mpaka leo, yeye hapumziki anaendelea kutenda kazi.

Ndio maana wakati Fulani mafarisayo walitaka kumkamata Bwana Yesu kwa habari hiyo hiyo ya kuishika sabato, wakitaka kumwonyesha kuwa katika siku ya saba hapaswi mtu yoyote kufanya kazi kwasababu hata Mungu mwenyewe alistarehe katika siku hiyo akaacha kufanya kila kitu alichokuwa anakifanya..Lakini Bwana alikuwa na ufunuo mkubwa zaidi ya huo na kuwaambia…

Yohana 5:14 “Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.

15 Yule mtu akaenda zake, akawapasha habari Wayahudi ya kwamba ni Yesu aliyemfanya kuwa mzima.

16 Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwudhi Yesu, kwa kuwa alitenda hayo siku ya sabato.

17 Akawajibu, BABA YANGU ANATENDA KAZI HATA SASA, NAMI NINATENDA KAZI”.

Umeona hapo?..Bwana anawaambia wale waliokuja kumshitaki kuwa siku ya saba hapaswi kufanya kazi…lakini Bwana akawaambia, BABA YAKE ANATENDA KAZI HATA SIKU HIYO, NA YEYE ANATENDA KAZI. Umeona hana siku ambayo anapumzika. Wao walitaka kumwambia siku ya saba Mungu alipumzika, lakini yeye akawaambia Baba yake anatenda kazi hata sasa. Kazi zake bado zinaendelea.

Bado anaendelea kuumba kimiujiza, bado anaendelea kutengeneza wanadamu kwenye matumbo ya wanawake, bado anaendelea kulitembeza jua kwa amri yake, bado anaendelea kutushushia mvua, bado anaendelea kuiumba miti na mimea, ndio maana ukiukata mti leo baada ya muda Fulani utaukuta umekua tena, hiyo ni kazi ya Mungu iliyo katika mwendelezo wake, haina pumziko, kama Bwana Yesu alivyosema “Baba yangu anafanya kazi hata sasa nami ninatenda kazi” kadhalika na sisi pia tunatakiwa tuseme maneno hayo Kama Baba yetu wa mbinguni anavyotenda kazi nasi pia TUNAZITENDA.

Na kazi hizo ni zipi?..Si nyingine zaidi ya zile zile Bwana Yesu alizozifanya.

Yohana 14 : 12 “Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, KAZI NIZIFANYAZO MIMI, YEYE NAYE ATAZIFANYA; NAAM, NA KUBWA KULIKO HIZO ATAFANYA, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.

13 Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.

14 Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya”

Sasa Bwana Yesu alifanya kazi gani?; aliponya wagonjwa wa kila aina (wa mwilini na wa rohoni). Kama Baba naye anavyojishughulisha kuiponya dunia kila siku, hapumziki, Bwana Yesu alirudisha uhai wa mtu aliyekufa, aliumba macho ya mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa kwake n.k, aliwahubiriwa watu injiii, na sisi Bwana katuambia kazi hizo tunaweza kuzifanya kwa jina lake.

Kwahiyo nataka nikuambie wewe unayesoma ujumbe huu, hakuna UGONJWA, WALA SHIDA, WALA KIFUNGO CHOCHOTE CHA SHETANI Kitakavyoweza kusimama mbele yako kuanzia leo hii kama umeuelewa ujumbe huu, kama umemwamini Yesu Kristo kwa dhati kabisa kutaka moyoni mwako.

Kama ni ugonjwa Kristo anao uwezo wa kukuponya sasa hivi, sio kesho, na ametupa uwezo wa kuombeana sisi kwa sisi na kupokea uponyaji wetu. Kwahiyo kama una ugonjwa wowote sasahivi hapo ulipo, Weka mkono wako mahali penye tatizo na uambie huo ugonjwa maneno haya kwa sauti na kwa Imani  

“EWE UGONJWA!!, BABA YANGU WA MBINGUNI ANATENDA KAZI HATA SASA, NAMI NATENDA KAZI KAMA YEYE, ONDOKA KWANGU NA USIRUDI TENA KWA JINA LA YESU”

 Baada ya kusema hivyo AMINI! Na uhai wa huo ugonjwa utakuwa umeishia hapo hapo.

Utasema mbona sijawahi kumuona Baba akiniponya leo iweje aniponye kwa dakika moja? Nataka nikuambia ulishawahi kumwona akikuponya isipokuwa ulikuwa hujui tu kama ameshawahi kukuponya mara nyingi! Chukua mfano siku ile ulipojikata na kisu mkononi na baada ya wiki mbili ile ngozi ikajirudia tena vile vile, kama ilivyokuwa mwanzo huoni huo tayari ulikuwa ni uponyaji?..Hapo ni Baba yako anafanya kazi yake ya kukuponya kila siku, unapokata nywele na baada ya wiki mbili zinaota tena huoni huo ni uumbaji tayari… sasa kwanini na wewe usifanye kazi ya kutamka uponyaji juu yako na kwa watu wengine, hiyo ndio sababu iliyomfanya Kristo akafanye miujiza kila mahali pasipo kizuizi chochote sio cha sabato wala cha sikukuu yoyote, kwasababu aliona Baba hana mipaka kila siku anafanya kazi zake.

Kila siku katika maisha yako, likumbuke hilo neno, Mungu hapumziki katika kazi zake na wala hachoki,anafanya kazi kila dakika na kila sekunde…na hivyo nasi pia hatupaswi kupumzika katika kuzifanya kazi zake..Kila siku tunapaswa tuumbe jambo jipya moyoni mwetu na maishani mwetu, kama yeye anavyoumba watu wapya kila siku kwenye matumbo ya wanawake. Kwasababu huo uwezo tumepewa..Tukitamka tu! Kwa IMANI TUSIPOKUWA NA MASHAKA, Hilo tulilolisema ni lazima litokee..

Ndugu nakuambia hilo kwasababu mimi binafsi Bwana kanitendea katika maisha yangu, watu kadha wa kadha nimewaombea nao wamepona! Na mimi mwenyewe Bwana ameniponya mara nyingi kwa njia hiyo. Hivyo mwamini Mungu.

Bwana akubariki sana..

Tafadhali “share” ujumbe huu na wengine.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

UPONYAJI WA YESU.

SABATO HALISI NI LINI, JE! NI JUMAPILI AU JUMAMOSI?, NI SIKU GANI ITUPASAYO KUABUDU?

JE! “MAJIRA NA SHERIA” MPINGA-KRISTO ATAKAYOKUJA KUBALISHA NI KUPINDUA SIKU YA SABATO NA KUWA JUMAPILI?


Rudi Nyumbani

Print this post

MLIMA WA BWANA.

Mara nyingi tunaposoma biblia katika agano la kale Mungu alipokuwa akitaka kukutana au kusema na watu wake, aliwaita milimani, hilo tunaliona tokea mbali kabisa jinsi Mungu alivyomwita baba yetu Ibrahimu katika ule mlima Moria amtolee sadaka na kumfanyia ibada, Tunakuja kuona tena baadaye Musa akiitwa na Mungu katika milima Sinai kupewa amri zote na hukumu na sheria kwa ajili ya wana wa Israeli, tunaona tena manabii wengi jinsi Mungu alivyokuwa akisema nao katika milima, mfano nabii Eliya Mungu alizungumza naye katika mlima Karmeli, na wengine wengi mfano wa Elisha ambao ukisoma habari zao mara nyingi utakuta walikuwa wakikutana na Mungu katika milima, 

Hivyo hiyo ilikuwa ni kama desturi yao kupanda milimani na kukutana na Mungu..Kwasababu iliaminika hivyo na ndivyo hata alivyofanya Mungu mara nyingi alipotaka kuzungumza na watumishi wake, alifanya kuwatenga kwanza kisha kuwapandisha milimani na baadaye kuzungumza nao. (Isaya 18:7). Na kama ukichunguza vizuri utaona kuwa wote waliokuwa wanaitwa kusema na Mungu milimani waliteuliwa na Mungu mwenyewe, sio kila mtu tu alikwenda, utakuta pengine wataanza safari wengi lakini mwisho wa siku wanaofikia kule juu mlimani ni wachache, ndivyo ilivyokuwa kwa Ibrahimu, Musa na manabii.

Tunaona hata kipindi cha Bwana wetu Yesu Kristo, mara nyingi alipokusudia kusali au kwenda kuzungumza na Baba yake alikuwa na desturi ya kupanda katika mlima wa Mizeituni, na tunaona pia wakati fulani alipotaka kuonyesha utukufu wake zaidi aliwatenga kwa kuwachagua baadhi ya mitume wake,(yaani watatu tu kati ya 12) kisha akawapandisha katika mlima MREFU sio mfupi, bali mrefu na huko huko ndiko alikowabadilikia sura..tunasoma..

Mathayo 17:1 “Na baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani;

2 akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang’aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru.

3 Na tazama, wakatokewa na Musa na Eliya, wakizungumza naye”.

Sasa tukirudi kwenye kiini cha somo letu kinachosema “mlima wa Bwana”. Tunapaswa tujiulize ni kwanini Mungu alikuwa anawaita watu milimani na sio mahali pengine popote…kwanini asiwe anawaita katika mabonde azungumze nao, lakini badala yake aliwaita milimani?. Je! milima ina upako zaidi ya visiwa, au nyika?. Je! milima inakibali cha kipekee sana mbele za Mungu zaidi ya mahali pengine popote?. Kama sivyo basi ilifunua nini?

Ni wazi kuwa kila mmoja wetu alishawahi kupanda mlima na kama sio mlima basi angalau kajilima na kujionea jinsi hali ilivyo katika kuupanda..si kazi rahisi wala si kazi nyepesi, kama ilivyo katika kushuka mabondeni, au kutembea katika nchi tambarare, tunajua kabisa kupandisha mlima inachukua nguvu nyingi hivyo kama wewe ni mlegevu hutafika kileleni..Kupanda mlima ni lazima utoke jasho la kutosha, sio kama kushuka mabondeni.Wanaoweza kupanda milima mrefu sikuzote ni wachache sana na tena unapaswa uwe mtu wa mazoezi lakini kuteremka bondeni, kila mtu anaweza kufanya hivyo, tena ni raha iwe unazo nguvu au hauna hakuna asiyeweza kushuka bondeni..

Mambo hayo yanafunua nini katika Roho?

Sasa tukirudi katika agano jipya mambo ya mwilini yanafunua mambo yanayoendelea rohoni, Na ndio maana ukisoma mahali popote palipo na bonde utaona kuwa ni mauti inapatikana huko, BONDE LA UVULI WA MAUTI, bonde LINAFUA SHIMO LA KUZIMA, mahali makao ya shetani yalipo Na siku zote kushuka huko ni rahisi sana..Mahali Fulani Bwana alipowatoa pepo, walimsihi asiwaamuru waende shimoni, ikifunua kuwa ni sehemu ya hatari…Lakini katika vilele vya milima Mungu anapatikana, kwasababu Mungu anaketi Juu siku zote, sehemu za juu zilizoinuka.

Hivyo ndugu tukitaka leo hii kukutana na Mungu, ukitaka kuuona uso wa Mungu kwa namna nyingine na ile uliyoizoea, ukitaka Mungu aseme na wewe katika viwango vya juu sana ukitaka Mungu akufunulie njia zake kwa namna ambayo hujawahi kuona huna budi kupanda mlimani katika roho, huna budi kugharimika kuupanda mlima wa Bwana. Tena na kwa jinsi unavyopanda zaidi ndivyo utakavyofunuliwa uso wa Mungu katika viwango vya juu zaidi.

SASA TUNAPANDAJE PANDAJE MLIMA HUO, NA NI NANI ASTAHILIYE KUUPANDA MLIMA WA BWANA?

Biblia imetoa majibu yote tunaposoma kitabu cha Zaburi..

Zaburi 24:3-6 “Ni nani atakayepanda katika MLIMA WA BWANA? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake?

4 Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila.

5 Atapokea baraka kwa Bwana, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake.

6 Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.

Inasisitiza tena na kusema:

Zaburi 15:1 “Bwana, ni nani atakayekaa Katika hema yako? Ni nani atakayefanya maskani yake Katika KILIMA CHAKO KITAKATIFU?.

2 Ni mtu aendaye kwa ukamilifu, Na kutenda haki. Asemaye kweli kwa moyo wake,

3 Asiyesingizia kwa ulimi wake. Wala hakumtenda mwenziwe mabaya, Wala hakumsengenya jirani yake.

4 Machoni pake mtu asiyefaa hudharauliwa, Bali huwaheshimu wamchao Bwana Ingawa ameapa kwa hasara yake, Hayabadili maneno yake.

5 Hakutoa fedha yake apate kula riba, Hakutwaa rushwa amwangamize asiye na hatia. Mtu atendaye mambo hayo Hataondoshwa milele”.

Unaona hapo?, vigezo vya kuuendea mlima huo?

1) Kwanza Ni mtu yule aendaye kwa ukamilifu, na kutenda haki, watu wengi wanaona shida kuishi maisha matakatifu, wanaona yatawasaidia nini? watapata faida gani, kujitaabisha kujizuia na tamaa, kutokunywa pombe, kutokufanya uasherati, kutokuvaa nguo za kizinzi, watapata faida gani?..wanaona ni ngumu sana mtu kuishi kwa namna hiyo, wanaona mtu kutenda haki, kutokula rushwa ni jambo ambalo ni gumu kutolifanya, lakini hawajui hizo ndizo gharama za kuupanda mlima wa Mungu, ambapo yeye yupo huko, mahali anapopatikana.

2) Biblia inasema pia mtu asemaye kweli kwa moyo wake, utakuta mtu kuwa muwazi wakati wote kwake ni shida, na bado anajiita mkristo, biblia inaendelea kusema Asiyesingizia kwa ulimi wake. Wala hakumtenda mwenziwe mabaya, Wala HAKUMSENGENYA JIRANI YAKE.

Unaona hapo?, utakuta mtu anajiita ni mkristo, na anahudhuria ibadani, na anasali, na anafanya kazi yote ya Mungu, lakini anaona ni vigumu kuuzia ulimi wake kutokuwazungumzia wengine vibaya, kusengenya watu kwake ni kama chakula chake,. Sasa mtu kama huyu asitazamie kumkaribia Mungu kwa namna yoyote ile hata kama atakuwa anafunga kiasi gani, hata kama atakauwa anatoa sadaka kiasi gani, hata kama atakuwa anahubiri kiasi gani..Hatoweza kupanda mlima wa Bwana..

3) Biblia inasema tena mtu ambaye macho yake huwaheshimu wamchao Bwana,

Mtu ambaye macho yake yanamfarahia yule tu anayejitaabisha kwa Bwana, na sio watu wengine,. Sasa Hapa utakuwa mtu ni Mkristo lakini hamu na Mungu hana hata kidogo, yupo tayari kuwa mshabiki wa mipira, kuwa mfuasi wa siasa, kuwa mshabiki wa watu maarufu wa kidunia hii, muda wote anapoteza kufuatilia mambo yao, lakini tukirudi katika upande wa Mungu, ukimuuliza hata historia ya kanisa la Kristo ilianzia wapi hajui, ukimuuliza nitajie ziara za mtume Paulo zilianzia wapi na kuishia wapi? Hajui, lakini ukimuuliza ziara za maraisi wote duniani na wasanii, atakutajia na yanayokuja na kitu gani kinaendelea sasahivi katika ulimwengu wa siasa atakutajia..Sasa hiyo ni roho ya kumkinai Mungu na watu kama hao biblia inasema hawataweza kufanya maskani yao katika mlima mtakatifu wa Mungu..Watu kama hao hata waseme wao ni wakristo kiasi gani, ndani ya maisha yao wanajijua kabisa kuwa wapo mbali na ufalme wa mbinguni.

4) Biblia inandelea kusema mtu ambaye hali rushwa.

Katika shughuli mkisto anazozifanya, je! Anakaa mbali na vitu kama rushwa na ukwepaji kodi?. Leo utashangaa ni mkristo lakini naye pia anatafuta njia za mkato za kukwepa kodi, mwingine anakuwa tayari kutoa rushwa ili afanyiwe jambo fulani..Sasa mambo kama hayo mtu akiwa nayo kadhalika asitarajie kumwona Mungu maishani mwake au Mungu kujifunua katika maisha yake, hata kama alibatizwa nakunena kwa lugha hiyo haijalishi, hatakaa amjue Mungu.

Hivyo Mungu kachagua sehemu ya juu iliyoinuka ili akutane na watu wake huko, sio rahisi kufika, inahitaji juhudi na bidii, kuacha usengenyaji sio rahisi kuliondoa kwa kuomba tu kama unavyodhani, inahitaji kuonyesha bidii yako binafsi kwa vitendo, mazungumzo yoyote unayoona yanakupelekea kumzunguzia mwingine kwa ubaya, ni kuyakwepa kwa namna zote, ukiudhiwa ni kuvumilia sio lazima uanze kutoa habari za mtu mwingine hadharani, unajizuia kwa nguvu, kila siku uendelee hivyo hivyo mpaka mwisho wa siku unajikuta inaumbika na kuwa ni tabia yako kutokuwazunguzia wengine vibaya..Hata na wale watu wanaokuletea hizo habari wakishakuona hauvutiwi na habari hizo, wao wenyewe watakuacha na kwenda kutafuta wanaoendana nao..Na kwa kufanya hivyo ndivyo unavyopiga hatua moja zaidi kuelekea mlima mtakatifu wa Bwana, Mungu alipo ili kusema na wale wote wamchao.

Kadhalika kutokufanya mambo ya ubatili, yaani uasherati, kampani mbovu zisizo na maana, kutokukaa wakati wote mitandaoni kuchati mambo yasiyo na maana, kutokwenda disco, kutofuata anasa za dunia hii, bali kinyume chake kujishughulisha na mambo ya Mungu, ni jinsi gani umpendeze yeye..Kumbuka Bwana anasema nikaribieni mimi nami nitawakaribia..Hivyo ukiwa unafanya bidii kukaa mbali na mambo maovu na kutafauta kujua habari zake, kwa kujifunza Neno, ndivyo unavyozidi kupanda kidogo kidogo mpaka kileleni alipo yeye..

Hizi ni siku za mwisho, na ndio kile kipindi ambacho Bwana Yesu alisema saa yaja ambayo waabuduo halisi watamwabudu Mungu katika roho na kweli.

Yohana 4.19 “Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii!

20 Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia.

21 Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu…

23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu”.

Ndugu unaona hiyo saa ni sasa Kristo aliyokuwa anaizungumzia, wakati huo ndio huu, Mungu anakutafuta wewe na mimi tupande tukamwabudu yeye katika MLIMA WA ROHO, huko ndiko tutakapomwabudu katika roho na kweli. Hivyo tuanze kupanda mlima huo sasa, kwa kuacha mambo hayo mabaya tuliyoyaona hapo juu bila kuchoka, bila kukata tamaa, ni kweli jasho litakutoka kidogo, lakini ili uonekane kuwa umestahili kukutana na Mungu wako uso kwa uso zaidi ya wale wengine, huna budi kupanda mlima huo wa roho kwa ukakamavu.

Tazama Neno la Mungu linavyosema..

Isaya 2:2 “Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi.

3 Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu.

4 Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.

5 Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika NURU YA BWANA.

Unaona siku hizi ndizo siku hizo za mwisho.

Ni maombi yangu kuwa mimi na wewe tutaanza kwenda katika nuru hii ya Neno la Mungu ili kutuongoza katika mlima huo wa Bwana.

Zaburi 43:3 “Niletewe nuru yako na kweli yako ziniongoze, Zinifikishe kwenye mlima wako mtakatifu na hata maskani yako.

4 Hivyo nitakwenda madhabahuni kwa Mungu, kwa Mungu aliye furaha yangu na shangwe yangu; Nitakusifu kwa kinubi, Ee MUNGU, Mungu wangu”.

Zaburi 123:1 “Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele.

2 Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele.”

Ubarikiwe sana.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

SAYUNI NI NINI?

NYOTA YA ASUBUHI.

USIONDOE ALAMA YA MPAKA ILIYOWEKWA NA MABABA.

UTAMBUE UJUMBE WA SAA UNAYOISHI.


Rudi Nyumbani

Print this post

MJI WENYE MISINGI.

Ibrahimu tunamwita ni Baba wa Imani, kutokana na Imani tunayoiona aliyokuwa nayo kwa Mungu wake licha ya kukaa kwa muda mrefu bila kupata mwana Mungu aliyekuwa amemuahidia akizingatia na huku umri umeshakwenda yeye na mke wake, hakukata tamaa kumwamini Mungu badala yake aliendelea kusubiria mpaka Mungu alipotimiza alichomuahidia na hata alipopata mwana, zaidi ya yote tunasoma katika uzee ule Mungu alimjaribu tena amtoe mwanawe kuwa sadaka ya kuteketezwa, Nalo hilo Ibrahimu halikumtikisa bali alidhubutu kumtoa, ndipo Mungu akavutiwa sana na Imani ya Ibrahimu..

Lakini hilo pekee tu pekee lingetosha Mungu kumfanya Ibrahimu kuwa baba wa imani na mtu wa kuigwa kwa vizazi vyote? Watu watakaokuja kumwamini yeye baadaye?..Lipo jambo lingine la ndani zaidi tunapaswa tulijue ambalo ndilo tutaligusia siku ya leo.

Tukisoma kitabu cha Waebrania tunapata kuona tabia nyingine tofauti ambayo Ibrahimu aliionyesha kwa Mungu wake. Tunasoma:

Waebrani 11:8 “Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.

9 KWA IMANI ALIKAA UGENINI KATIKA ILE NCHI YA AHADI, KAMA KATIKA NCHI ISIYO YAKE, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.

10 Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu”.

Sasa ukiyachunguza hayo maandiko kwa makini utaona kuwa Ibrahimu alikuwa na jicho lingine la mbele zaidi hata ya lile alilokuwa ameahidiwa na Mungu katika mwili..Na ndio maana siku zake zote maisha yake yote hakusumbuliwa na mambo yanayopita, hukusumbuliwa na kukawia kwake kupata mtoto,hakusumbuliwa na hata kutoa mwanawe Isaka kuwa sadaka kwa Mungu wake…

Embu Soma tena hapo anasema. 9 KWA IMANI ALIKAA UGENINI KATIKA ILE NCHI YA AHADI, KAMA KATIKA NCHI ISIYO YAKE,..

Kumbuka Mungu alimtoa Ibrahimu nchi ya mbali sana huko Uru ya Ulkadayo na kumleta Kaanani, mahali ambapo Mungu alimwahidia kumpa kila kitu ambacho ni chema, alimwahidia kuwa atamfanya kuwa taifa kubwa sana, atamfanya kuwa uzao hodari, uzao ambao utamiliki malango yote ya adui zake wote..Atamfanya kuwa taifa tajiri, na lenye nguvu sana..

Sasa embu jaribu kutengeneza picha ingekuwa hiyo nafasi umepewa wewe, Mungu anakuambia utakuwa na uzao hodari katika nchi fulani na kwa kupitia wewe mataifa yote duniani yatabarikiwa, hivi utajisikiaje?…Ni wazi kuwa utajiona kuwa ni mtu wa kipekee mbele za Mungu kuliko wengine wote, utatanua mbawa kidogo, utajiona kuwa wewe ni mtu muhimu sana mbele za Mungu kuliko wengine..Hata ukifika katika hiyo nchi Mungu aliyokuahidia utaimiliki pengine kwa kiburi fulani, utaishi kama mfalme fulani au chifu fulani hivi kwani Mungu tayari ameshakuridhia na kukupa wewe..hata watu wote wa huo mji wakitaka kupigana na wewe hutaogopa, kwasababu Mungu alishakupa wewe milki hiyo.

Lakini kwa Ibrahimu haikuwa hivyo, alikuwa na jicho la mbali zaidi, hakutazama Baraka hizo Mungu alizomwahidia za kitambo tu, hakutazama wingi wa uzao atakaokuwa nao duniani, hakutazama ukuu wa taifa atakalolizaa duniani, hakutazama utajiri wa kimwilini, kwa hili jicho la kimwilini, bali aliyatafakari maisha yake kwa utulivu sana, akiangalia jinsi Mungu alivyomtoa Nchi ya Ulkadayo na kumleta pale Kaanani, na jinsi Mungu alivyomwepusha katika taabu zote zile, za kungojea nchi ambayo Mungu amemwahidia, akajiuliza kama Mungu anao uwezo wa kunifanya taifa kubwa ndani ya dakika moja, kwanini anakawia hivi kunipa mwana? Sababu nini?..Ibrahimu alitaka kujua kusudi la maisha, nyuma ya haya yote kuna nini?.. Na ndipo akafahamu kuwa maisha yake ni picha ya mambo yatarajiwayo mbeleni yajayo baada ya ulimwengu huu kupita. Alifahamu kuwa maisha yake ni somo, maisha yake ni sauti Mungu anayozungumza naye juu ya mambo ya mbeleni sana..ng’ambo ya pazia..

Na ndio maana tunasoma Ibrahimu licha ya kupewa utajiri wote ule wa kimwilini, bado aliendelea kuishi katika nchi ile ambayo ni kweli ilikuwa ni haki yake kustarehe na kujifurahisha lakini biblia inatuambia aliishi mule kama vile siyo nchi yake, aliishi katika milki yake kama vile sio milki yake, kama vile mgeni nyumbani kwake mwenyewe..aliisha na mke wake Sara kwenye mahema, fikiria Ibrahimu alikuwa ni mtu tajiri sana mwenye mali nyingi alizopewa na Mungu lakini hakuishi kwenye makasri,..hiyo inafunua nini?..Inaonyesha ni jinsi alivyoishi kama mpitaji hapa duniani?.

Unadhani alikuwa hajipendi?. Hapana..Biblia inatuambia ni kwasababu alikuwa anautazama mji ulio bora, alikuwa anautazamia mji wenye misingi, sio ule wa Kaanani aliopewa ambao Mungu kweli alimpa kuwa milki yake, lakini huo ingempasa aweke misingi yeye iliyodhaifu, ingempasa aubuni yeye..Lakini badala yake Ibrahimu hakufanya hivyo bali aliutazamia mji wenye misingi ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu mwenyewe.. Na mji huo si mwingine zaidi ya YERUSALEMU MPYA ya mbinguni HALELUYA!!.

Jambo hilo ndilo lililomfanya Mungu apendezwe na Ibrahimu na kumfanya awe kielelezo cha kuigwa kwa watu wote, ikiwemo mimi na wewe.

Ndugu leo hii, umekuwa ukimsubiria Mungu aje kukufanikisha katika jambo fulani ambalo alikuahidia atakufanyia zamani, au tayari ameshakufanyia, pengine alikuahidia kukupa mtoto kwa muda mrefu na sasa amekupa, pengine alikuahidi utakapa mali amekupa, ulisubiria nyumba amekupa, ulingojea hiki au kile kwa muda mrefu sasa amekupa, Je! unadhani hayo ndio mapenzi ya Mungu kwako?.

Usipokuwa makini utakuwa unaona kila siku pale Mungu anapokufanikisha katika mambo yako ndio anapendezwa na wewe, ndio mrithi wake, utaona kila unalomwomba anakupa na wakati mwingine hata umetolewa unabii utakuja kuwa raisi, au mtoto wako atakuja kuwa bilionea wa kwanza duniani, Mungu kakuotesha utakuja kuwa kichwa cha ukoo wako mzima, wote wasiokupenda watakuja kukuinamia, ukadhani kuwa hayo ndio mapenzi ya Mungu kwako!!.

Ni kweli Mungu atatimiza Neno lake kwa alichokuahidia,lakini usipokuwa naUFAHAMU kama wa IBRAHIMU, Jua tu siku ile ikifika, hutaingia katika mji ule YERUSALEMU MPYA BIBI-ARUSI WA KRISTO. Siku ile kama Bwana Yesu alivyosema watatoka watu kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni; 12 bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. ( Mathayo 8:11)..Unaona hapo, wataketi na Ibrahimu, na Bwana hawezi kuwaketisha pamoja na Ibrahimu watu wasiofanana na Ibrahimu katika mienendo.

Hiyo Yerusalemu mpya, kwa tafsiri nyingine ni BIBI-ARUSI wa Kristo, yaani watakatifu wa Kristo, sasa sio kila mtu anayejiita ni mkristo atakuwa bibi-arusi wa Kristo, hapana, kama vile biblia inavyosema hawawi wote waisraeli walio wana wa Israeli, Vivyo hawawi wote wakristo, walio wa-kristo. Kuna tofauti kati ya suria na mke, wanawali wenye busara na wanawali wapumbavu, magugu na ngano. kadhalika mbele za Mungu, si kila mkristo ni bibi-arusi wa Kristo, si kila mtu ataujenga YERUSALEMU WA MBINGUNI. Bali ni wale tu waliokamilishwa katika wokovu.

Biblia inatumbia mji huo hakitaingia kilicho kinyonge, wala kidhaifu, ndugu ukiona umekosa tu unyakuo basi ufahamu kuwa wewe si miongoni mwa mji mtakatifu wa Mungu. Ukiona umekosa tu karamu ya mwanakondoo siku ile ya unyakuo basi hali yako ni itakuwa mbaya sana.

Ukisoma kitabu cha ufunuo sura ya 21 utaona ni jinsi gani hawa watu walivyo wa tofauti sana, wenye imani hii ya Ibrahimu, kundi hili dogo sana wanavyofananishwa na uzuri wa mji ule , ulipambwa ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu mwenyewe..Watu ambao Mungu amewajenga katika misingi iliyo imara..Na tunasoma misingi yenyewe ni mitume na manabii,(Biblia takatifu) na sio misingi ya pesa na mafanikio..sio misingi ya utajiri na ufahari, sio misingi ya urembo na umaarufu, sio misingi ya elimu ya dunia hii kama wengine wanavyodhani.

Mji huo unaonekana ukiwa na vipimo sahihi kabisa, urefu wake, na mapana yake, na kwenda juu kwake ni sawa sawa, kuonyesha uimara wake na umakini wa ujenzi wake, kuonyesha jinsi ulivyo FITI, kwa vifaa vilivyotumika kuujengea mji huo..jinsi watakatifu hao walivyostahili kwa utakatifu wao kujengwa juu ya misingi ya mitume na manabii (yaani BIBLIA) na sio katika mapokeo ya kibinadamu na madhehebu.

Mji huo unaonekana ukiwa umejaa dhahabu kote, ikiashiria utakatifu wa wateule..Unaonekana ukiwa umepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna, ikiwakilisha wito na utumishi tofauti tofauti wa wateule wa Mungu.

Embu tusome kidogo tabia za mji huu..

Ufunuo 21:9 “Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, NJOO HUKU, NAMI NITAKUONYESHA YULE BIBI-ARUSI, MKE WA MWANA-KONDOO.

10 AKANICHUKUA KATIKA ROHO MPAKA MLIMA MKUBWA, MREFU, AKANIONYESHA ULE MJI MTAKATIFU, YERUSALEMU, UKISHUKA KUTOKA MBINGUNI KWA MWENYEZI MUNGU;

11 wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri;

12 ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli.

13 Upande wa mashariki milango mitatu; na upande wa kaskazini milango mitatu; na upande wa kusini milango mitatu; na upande wa magharibi milango mitatu.

14 Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.

15 Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake.

16 Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa.

17 Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika.

18 Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi.

19 Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi;

20 wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto.

21 Na ile milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.

22 Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake.

23 Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo.

24 Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.

25 Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku.

26 Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake.

27 Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.”

Unaona hapo Yohana anaonyeshwa MKE WA MWANAKONDOO ambaye ndiye YERUSALEMU MPYA, na hapo mwisho kabisa anakuambia 21.24 “Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake”.

Sasa mwisho kabisa Mungu akishamaliza kuujenga huu mji ambao mpaka sasa anaujenga katikati ya watu wake na unakaribia kuisha, hapo ndipo maskani ya Mungu itakapokuwa na wanadamu, Hapo ndipo Mungu atakaposhuka na kukaa katikati ya wanadamu kwenye maskani yake..Na maskani yake ndio huu mji Yerusalemu mpya, ambayo inamwakilisha bibi-arusi kwa Kristo tu peke yake. Hivyo Mungu atakaa ndani ya hawa watu… Hawa watakuwa ni watu wa-kipekee sana mbele za Mungu, kama vile sisi tuwaonavyo malaika, ndivyo itakavyokuwa watu watakaopewa neema ya kuingia kule watakavyowaona hawa bibi-arusi wa Kristo..

Huo ndio mji ambao Ibrahimu alikuwa anautazamia.. licha ya kuahidiwa kuwa taifa hodari duniani hakujisumbua kulitazama hilo kama alivyolingojea hili kwa saburi zote..Swali ni je! Wewe nawe ni miongoni mwa mji mtakatifu wa Mungu ambao Mungu anauandaa sasa?..Yerusalemu mpya, bibi-arusi wa Kristo?..Je! Kristo akirudi leo unao uhakika wa kwenda naye?. Je! unaishi maisha ya kutazama mbinguni, au mambo tu ya duniani?.

 Je! umeoshwa dhambi zako, na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi, kama Neno lenyewe “ubatizo” linavyomaanisha, na kwa jina la YESU KRISTO?. na ikiwa umefanya hivyo vyote je! maisha yako yanauhakisi utakatifu? (Waebrania 12:14), maana biblia inasema hakuna mtu atakayemwona Mungu asipokuwa nao huo.

Ikiwa hayo hayapo ndani yako.. unao muda, sasa mji ule unakaribia kuisha ujenzi wake, fanya bidii uingie kabla mlango wa neema haujafungwa. Ulimwengu huu na mali zisiwe kisingizio siku ile. Kwasababu wapo waliokuwa na mali zaidi yangu na yako na waliokuwa na mafanikio kupita ya Ibrahimu lakini waliishi kama wapitaji tu hapa dunia.

Isaya 35: 8 “Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; WASAFIRIO, WAJAPOKUWA WAJINGA, HAWATAPOTEA KATIKA NJIA HIYO.

Ni matumaini yangu utatubu leo na Bwana akujalie kuishi katika utakatifu na usafi.

Ubarikiwe sana.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.

UFUNUO: Mlango wa 21

ALIPO NA ATAKAPOKUWEPO BIBI-ARUSI WA YESU KRISTO.


Rudi Nyumbani

Print this post

HUDUMA YA UPATANISHO.

2 Wakorintho 5: .17 “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.

18 Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, ALIYETUPATANISHA sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho;

19 yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.

20 Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.

Kuna sababu kadha wa kadha kwanini Yesu Kristo Bwana wetu, anajulikana kama Mwana wa Mungu, hiyo ni moja ya sifa yake kuu..Ingawa yeye alikuwa ni MUNGU katika mwili, lakini hilo halikuwa na umuhimu mkubwa sana kwetu kulifahamu , kuliko kumfahamu yeye kama mwana wa Mungu, ndio maana huoni mahali popote akitafuta kujionyesha yeye kuwa ni MUNGU. Hakutaka hilo, kwasababu hiyo sio sababu kubwa iliyomleta duniani, hakuja kutafuta kuabudiwa duniani…bali kutafuta kilichopotea. Kama ingekuwa amekuja kutafuta kuabudiwa kama Mungu, basi angekaa huko huko mbinguni kwenye utukufu wake angekuwa hana sababu ya kushuka huku duniani kwenye mavumbi..

Raisi anapokutana na familia yake cheo chake kinabadilika na kuwa Baba na MWANA-FAMILIA na sio raisi tena, hatamwadhibu mwanawe kwa kutumia vyombo vya dola, bali atatumia fimbo kama ikiwezekana, na Yesu Kristo alivyokuja duniani cheo chake cha kimungu kilibadilika na kuwa MWANA. Kwahiyo ilimpasa awe kama mwanadamu, ndio maana watu wasiomwelewa Bwana YESU wanapinga vikali kuwa yeye sio Mungu, Mungu gani anakufa? Analia? Anakula na kunywa?…Ni kweli kwa kumchunguza tu pasipo kuwa na ufunuo wa utendaji wake kazi hutaweza kuona uungu wowote ndani yake. Lakini akikujalia kupata ufunuo utamwelewa vizuri yeye ni nani. ukisoma Wafilipi 2:5-8, pamoja na 1Wakorintho 2:6-8, na Tito 2:13 na Timotheo 3:16, Utapata  picha halisi ya kuwa yeye ni nani. Na kwamba alikuja katika SIRI KUU SANA, ijulikanayo kama Siri ya utauwa..Na biblia inasema siri hiyo haijulikani kwa kila mtu bali kwa wakamilifu tu peke yao ya kwamba Kristo YESU ni MUNGU.

Lakini Bwana Yesu alipokuja duniani alitamani sana sisi tumjue yeye kama Mwana wa Mungu kuliko kumjua yeye kama Mungu, ndio maana aliwauliza wakati Fulani wanafunzi wake..”watu husema ya kuwa mimi ni nani?” wakasema wengine Eliya, wengine Yohana mbatizaji, wengine Yeremia n.k akawauliza na wanafunzi wake, na ninyi mnasema ya kuwa mimi ni nani? “PETRO AKAJIBU WEWE NDIWE KRISTO, MWANA WA MUNGU ALIYE HAI.

Unaona?  Bwana Yesu alimsifia Petro kwa ule ufunuo alioupata wa kumtambua Kristo kama mwana wa Mungu..

“Yesu akajibu, akamwambia, HERI wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni” (Mathayo 16:16-19)

Zingatia hilo neno “HERI” Ikiwa na maana kuwa amebarikiwa yeye alifahamuye hilo, unaweza ukajiuliza kwanini Bwana hakumrekebisha Petro na kumwambia hapana! Mimi si mwana wa Mungu, bali ni Mungu mwenyewe niliyekuja katika mwili. Unaona jambo ni lile lile, Yeye anataka tumwelewe ni kitu gani kilichomleta Duniani zaidi ya kuelewa ni kitu gani alichokiacha mbinguni.

Alifanyika kuwa MWANA WA MUNGU, ili kutuonyesha sisi NJIA ya jinsi mwana wa Mungu anavyotakiwa awe, ili siku atakapoondoka duniani, sisi tuliosalia kwa kuyaangalia maisha yake, tujifunze kwake, alikuja kutengeneza njia iliyoharibika..ili kwa kumtazama yeye tuyarekebishe maisha yetu. Ili yafanane na ya kwake ili nasi tuwe WANA WA MUNGU kweli kweli. Kama yeye alivyomtegemea Baba nasi tumtegemee Baba asilimia 100, kama yeye alivyokuwa mtakatifu hata akashuhudiwa mbinguni nasi tuwe hivyo hivyo, kama yeye alivyovumilia nasi tuvumilie majaribu, kama yeye alivyokuwa na upendo nasi tuwe na upendo.n.k Hizo ndio tabia za kuwa MWANA WA MUNGU. Sio kusema sisi ni wana wa Mungu lakini maisha yetu hata kidogo hayafanani na ya kwake, yeye ametupa kielelezo, kama yeye alivyofanya na kuishi na sisi pia tufanye na kuishi vilevile kama yeye..

Ni sawa na mwalimu aliyeona wanafunzi wake hawamwelewi akaamua kuvua cheo chake cha ualimu na kuvaa uniform za kiuanafunzi na kwenda kuketi pamoja na wanafunzi, na kujifanya yeye ni mwanafunzi na kusoma nao na kujiweka chini ya changamoto zote za kiuanafunzi ili tu kuwaonyesha njia bora ya kusoma inavyopaswa na kumwelewa mwalimu anapofundisha. Ndivyo na Bwana Yesu alivyofanya kuacha enzi na mamlaka kuja duniani. Ni kutuonyesha tu sisi njia!

Lakini tukiachana na hayo, tunaweza kujifunza pia sifa nyingine kuu ya KUWA MWANA WA MUNGU, Na sifa hiyo si nyingine zaidi ya UPATANISHO, Sifa hii ndio iliyobeba kiini cha somo letu leo…

Sasa sababu nyingine kubwa iliyomfanya Bwana Yesu kuwa mwana wa Mungu na si malaika ni KUTUPATANISHA SISI NA MUNGU. Kumbuka sisi tulikuwa tumepotea dhambini, na tulikuwa tayari wote ni wa kwenda kuzimu, hakuna hata mmoja wetu angepona hata Musa, hata Eliya, hata Yohana Mbatizaji hata Adamu mwenyewe wote walikuwa ni wakupotea…Lakini kwa kupitia damu ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu tumepatanishwa na Mungu. Tunakwenda mbinguni bure endapo tukimwamini yeye na kuyaishi maneno yake.

Hivyo basi ili na sisi tuwe wana wa Mungu ni lazima tuwe wapatanishi kama yeye. Utauliza? Na sisi kwahiyo inatupasa tumwage damu kama yeye?? Jibu! Damu ya Yesu inatosha!

ilishamwagika mara moja, lakini alitupa kielelezo kama yeye alivyotufanyia sisi na sisi tuyafanye kwa wengine, kwahiyo ndio wakati mwingine kama inabidi inatupasa na sisi kumwaga damu au kutoa uhai wetu kwaaajili ya wengine..maandiko yanasema hivyo katika kitabu cha 1 Yohana 3:16” Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu” HUO NDIO UPATANISHO, Na kwa kufanya hivyo tutaonekana tumekuwa WANA WA MUNGU,kwa macho yakimbinguni, tutafananishwa na MWANA WA MUNGU,Yesu Kristo aliyetoa uhai wake kwa ajili yetu. Biblia inasema katika kitabu cha Mathayo..

Mathayo 5:9 “HERI WAPATANISHI; Maana hao WATAITWA WANA WA MUNGU”

Upatanishi unaozungumziwa hapo juu, sio kuwapatanisha watu wanaogombana au watu waliokosana hapana! Bali kujitoa kwa hali na mali kwa ajili ya kuwapatanisha watu na Mungu wao, KWA KUWAPELEKEA HABARI NJEMA za wokovu na hata kugharimika kufa, ilimradi tu umpatanishe mtu na Muumba wake, kama Bwana Yesu alivyofanya. Maandiko yanasema..

2 Wakorintho 5: 17 “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.

18 Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, NAYE ALITUPA HUDUMA YA UPATANISHO;

19 yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; NAYE AMETIA NDANI YETU NENO LA UPATANISHO.

20 Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, KANA KWAMBA MUNGU ANASIHI KWA VINYWA VYETU; twawaomba ninyi kwa ajili ya KRISTO MPATANISHWE NA MUNGU.

Umeona hapo? Ndugu…Kristo,Mwana wa Mungu alitupatanisha sisi na Mungu ndio maana akaitwa Mwana wa Mungu, kwasababu heri walio wapatanishi hao wataitwa wana wa Mungu, na sisi Bwana ametupa huduma ya upatanisho..Ndiyo haya maneno yanayosema nawe sasa,…kama maandiko yanavyosema hapo katika mstari wa 20 “KANA KWAMBA MUNGU ANASIHI KWA VINYWA VYETU; twawaomba ninyi kwa ajili ya KRISTO MPATANISHWE NA MUNGU.”

Biblia inakusihi ndugu unayesoma ujumbe huu ambaye hujawa kiumbe kipya bado, ambaye ni vuguvugu katika imani, ambaye bado unaupenda ulimwengu, ambaye bado hujaacha anasa, wala usengenyaji, wala ulevi, wala tamaa mbaya…inakuomba upatanishwe leo na Mungu.

Mgeukie yeye leo ukanywe maji ya uzima, kama Bwana mwenyewe alivyosema katika Ufunuo 22:17 “Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.”..Ni bure kabisa yanapatikana…Utafika wakati haya maji hutayapata bure wala kwa fedha, yatakuwa hayapo…Na unajua madhara ya kukosa maji ya uzima baada ya kifo??..ni mabaya sana usitamani uyakose huko.

Kama hujatubu dhambi zako, bado hujachelewa, mwambie Bwana akusamehe, mahali popote ulipo, jitenge peke yako kwa muda kisha tubu! Mwambie Bwana kuanzia leo unahitaji kuwa kiumbe kipya, unahitaji kupatanishwa naye, wewe mwenye dhambi na kama umemaanisha kufanya hivyo yeye “anakubali wakosa” atakusamehe na atakupa amani ya ajabu moyoni mwako, hiyo amani ndio uthibitisho wa kusamehewa dhambi zako, na bila kupoteza muda haraka sana nenda katafute ubatizo sahihi wa kimaandiko, wa maji mengi na kwa JINA LA YESU KRISTO (kulingana na Matendo 2:38) ili dhambi zako ziondoke kabisa kabisa, Baada ya kufanya hivyo Bwana Yesu Mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu atakayekusaidia kushinda dhambi na kuilewa biblia vizuri..

Kwa kukamilisha hatua hizo utakuwa umezaliwa mara ya pili na kuwa kiumbe kipya…kama maandiko yalivyosema hapo juu..” MTU AKIWA NDANI YA KRISTO YA KALE YOTE YAMEPITA TAZAMA YAMEKUWA MAPYA”..Bwana mwenyewe atayafanya mapya maisha yako kwa kila NYANJA!

Mungu akubariki sana…Na kama tayari ulishakuwa ndani ya Kristo, yaani umeshazaliwa mara ya pili, Neno linasema TUMEPEWA HUDUMA YA UPATANISHO, hivyo ni wajibu wako pia kwenda KUWAPATANISHA WENGINE NA MUNGU WAO, yaani kwenda kuwaambia habari za Neema zilizopo ndani ya Yesu Kristo na Raha na Tumaini, na toba!. Huo ndio uthibitisho wa kuwa kweli umefanyika kuwa mwana wa Mungu, kumbuka Neno hili “heri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu”.

Ubarikiwe sana.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO

MWANA WA MUNGU.

UHURU WA ROHO.


Rudi Nyumbani

Print this post

USIMWABUDU SHETANI!

Mungu alipomtuma Musa, kwa Farao, tunasoma habari alimpa maagizo ya nini cha kufanya atakapofika kwa Farao, na mojawapo ya maagizo hayo alimwambia akifika aitupe chini ile fimbo aliyokuwa nayo mkononi mbele ya Farao nayo itageuka na kuwa nyoka, na kisha aitwae tena mkononi mwake nayo itageuka kuwa fimbo kama mwanzo. Na pia tunaona Bwana alimfanyisha mazoezi kabisa akiwa kule kule mlimani kabla hata ya kwenda Misri kwa Farao, maana Mungu alimwambia palepale aitupe chini ile fimbo na alipoitupa ikageuka kuwa nyoka na Musa alipoona fimbo imegeuka kuwa nyoka alitaka kukimbia..

Bwana akamwambia akamshike Yule nyoka Mkia, kwa kusitasita na kutetemeka alikwenda na kumshika, na mara saa hiyo hiyo Yule nyoka akageuka na kuwa fimbo tena..Zoezi hilo lilimsadia kupata ujasiri, pindi atakapofika kwa Farao na kuitupa chini ile fimbo itakapogeuka na kuwa nyoka, asiigope kuishika na kuitwaa tena iwe fimbo.

Sasa swali la kujiuliza ni kwanini Mungu aitumie ile fimbo kuigeuza kuwa nyoka na wala si kitu kingine, kwanini hakutaka igeuke na kuwa chuma, au igeuke na kuwa sungura, au kiumbe chochote kile tofauti na NYOKA!.

Ili tuelewe hilo vizuri, turudi kidogo kujifunza histori ya Taifa la Misri, Misri ni Taifa lililopo kwasasa katika Bara la Afrika, kaskazini mashariki mwa Afrika, na asili ya Taifa hilo ilikuwa ni wana wa HAMU, aliyekuwa mwana wa Nuhu, Yule aliyeuona uchi wa Baba yake na asiusitiri, na hivyo akalaaniwa. Kwahivyo wana wa Hamu wakasafiri pande za kusini wakajenga miji huko, na Taifa mojawapo la wana hao wa Hamu ndio Misri. Mambo mengi yaliendelea hapo katikati hatuna muda wa kutosha wa kuyazungumzia yote lakini historia inasema ndio Taifa lililokuja kuwa na nguvu kuliko mengine yote kwa wakati huo.

Utamaduni wa Taifa hilo haikuwa kumwabudu Mungu wa Israeli, kwasababu walikuwa hawamjui Mungu wa Israeli bado, hivyo walikuwa wana miungu yao mingine mingi mingi tu!, waliabudu jua, mwezi na mambo mengine mengi…lakini moja ya miungu waliyokuwa wanaiabudu na kuipa heshima ya juu zaidi, ilikuwa ni NYOKA. Na aina ya nyoka hao waliokuwa wanawaabudu anajulikana kama COBRA. Walikuwa wanaamini kuwa nyoka aina ya Cobra ni mungu mkuu ambaye ana uwezo mkubwa sana katika kulilinda taifa lote la Misri dhidi ya Maadui zao, walitumia sanamu yake kama ishara kila mahali katika nyumba zao za kawaida na katika makasri yao makubwa ya kifalme. Hata katika kofia za kifalme za wafalme kulikuwa ni kijisanamu kidogo cha cobra kwenye kipaji cha uso kinachoangalia mbele, hicho kilikuwa kinavaliwa daima waliamini kuwa kama vile nyoka aina ya Cobra anavyotema mate ya sumu dhidi ya maadui zake usoni, vivyo hivyo cobra wanayemwabudu huyo huyo atawatemea moto maadui wa Farao wote wanaokuja mbele yao.

Kwahiyo ilikuwa ni imani iliyoheshimika sana, na ilikuwa inawapa matunda, kwasababu nyuma yake alikuwa ni shetani, na kama unavyojua shetani naye anawapa anaowapenda kama anavyotaka. Kwahiyo huyo mungu wao nyoka alikuwa anawapa ushindi mara nyingi ndio maana, Taifa hilo la Misri likainuka kuwa na nguvu kila mahali.

Wengi tunafikiri kuwa miungu hiyo ya Misri haikuwa na nguvu yoyote! Usidanganyike! Ilikuwa ina nguvu kama kawaida, na wamisri walikuwa wanaona inavyowasaidia, na endapo wakiwa hawaiabudu inavyopaswa ilikuwa inawaletea madhara, kwahiyo sio kwamba wamisri walikuwa wanaabudu kitu kisicho dhahiri!.. Ukitaka kujua walikuwa wanaabudu kitu kilicho dhahiri au la! Tazama yale mapigo, Musa aligeuza fimbo kuwa nyoka nao pia wakafanya hivyo hivyo, na baadhi ya mapigo pia waliweza kuiga, sasa kama hiyo miungu yao haikuwa dhahiri kwanini iliweza kufanya ile miujiza?? Jiulize hilo, na kama hiyo miungu yao ilikuwa na nguvu ya mpaka kuweza kubadilisha fimbo kuwa nyoka unadhani ingeshindwa vipi kutemea moto kwa maadui zao wakiwa vitani??..

Hata Israeli wakati Fulani walipokengeuka na kuanza kuabudu mabaali, sio kwamba walikuwa wanaabudu kitu kisichokuwepo, hapana! Walikuwa wanaabudu kitu kilicho dhahiri kabisa (ambacho ni shetani mwenyewe pasipo wao kujijua)..Na hata wakati ule walipojaribu kushusha moto mbele ya Eliya juu ya ile dhabihu usidhani ni kwamba walikuwa wanafanya kitu cha kujaribisha au kubahatisha, hapana! hiyo miungu yao kushusha moto sio jambo kubwa, Na ilishawahi kushusha hapo kabla, ndio maana unaona walipata ujasiri mbele ya Eliya kulileta lile shindano, lakini kilichowashtusha ni kama tu hicho kilichomshtusha Farao kuona nyoka wake wanamezwa mbele ya macho yake, na makuhani wa mabaali vivyo hivyo walishtuka kuona mbona moto haushuki kama siku zote!..

Kwahiyo Musa wakati anamwendea Farao, Mungu alitumia ishara ya nyoka, ili kuwaonyesha wa Misri kuwa mungu wanayemwabudu sio wa kweli, ingawa anawatendea miujiza , na kwamba nguvu zake zina mipaka, yupo mwenye nguvu kuliko mungu wao cobra wanayemwabudu, ndio maana alitumia ishara ya nyoka awali kabisa ili wamisri wamwelewe vizuri, kwasababu laiti angetumia ishara ya kugeuza fimbo kuwa sungura wamisri wasingeiamini kwasababu wao wanajua miungu ni mfano wa viumbe wakali kama nyoka, na ndio maana unaona nyoka wa Musa aliwameza wale nyoka wa Farao. 

Kwa ufupi ishara ile, ilitosha kabisa kumwaminisha Farao kuwa Mungu wa Israeli ni Mungu mkuu kuliko mungu wao. Hata wamisri wote baada ya kuiona ile ishara waliamini, kulikuwa hakuna haja ya kuendelea na ishara nyingine mbele…kwasababu mbele ya macho yao wameshuhudia mungu wao cobra wanayemweshimu na anayewasaidia siku zote katika vita, amemezwa na Mungu mwingine, ni ishara madhubuti kuwa endapo wakiendelea kushindana na huyo Mungu watamezwa vile vile, kama mungu wao alivyomezwa…Lakini kwasababu Mungu alitaka kuonyesha utukufu wake wote, ndiyo akaufanya moyo wa Farao usiamini, uwe mgumu. Lakini katika hali ya kawaida, Farao tayari alishaamini.

Ndugu kama uliwahi kuomba rozari na ikakupa majibu uliyoyaomba, uliiomba fedha ikakupa, uliiomba rozari ushindi ikakupa, na ukaiamini kiasi kwamba unatembea nayo kila siku shingoni, kwasababu haikuangushi……napenda nikwambie ndugu yangu mpendwa huyo sio Mungu ni shetani nyuma ya hiyo rozari, haijalishi hiyo rozari imekufanikisha kiasi gani, nataka nikuambie yupo Mungu aliye mkuu kuliko hiyo rozari atakayeimeza hiyo rozari unayoivaa na kuiomba kila siku, Hata Farao alitumia nyoka kuamini hakuna mungu zaidi ya huyo, na nguvu za Cobra zilimfanikisha kuliko mataifa yote duniani, lakini alipokuja Mungu wa miungu na kumkataa huyo. Misri iligeuka kuwa kama jalala la dunia.

Kama umekuwa ikiisujudia sanamu kanisani kwako pasipo kujua kuwa unamwabudu shetani na imekujibu maombi na kukupa kila unachokihitaji… Mungu hakuweza kukuhukumu kwasababu ulikuwa huujui ukweli, lakini leo umeujua ukweli, umgeukie yeye mwenye nguvu kuliko hiyo sanamu, itupe leo ivunje vunje leo, acha kuiabudu kwasababu yupo Mungu juu mwenye nguvu kuliko hiyo sanamu ya BIKIRA MARIA unayoiabudu na anataka kukubariki kuliko hata hapo ulipo. Anataka kukupa mafanikio kuliko hata hayo uliyonayo. Ambayo shetani amekupiga upofu kukudanganya kwamba ni mafanikio, kumbe ni mafanikio feki,…hiyo sanamu haiwezi kukupa raha nafsini mwako, hiyo sanamu haiwezi kukusamehe dhambi, hiyo sanamu haiwezi kukufanya uwe mtakatifu, hiyo sanamu haikupi kibali cha kuingia ufalme wa mbinguni, hiyo sanamu haiwezi kuondoa ulevi ulionao! Haiondoi uasherati ndani yako!! Hiyo sanamu sio Mungu wa kweli! Kwasababu ndivyo ilivyokuwa hata kwa Farao, wale nyoka aliokuwa anawaabudu walimpa utajiri lakini walikuwa hawamhukumu kuhusu tabia yake mbaya ya kuonea watu wasiokuwa na hatia! Mungu gani huyo!

Utasema huyo Mungu mbona watu wake ni maskini, nataka nikuambie hata Farao aliwaona wana wa Israeli ni maskini na kuwatesa kule kwenye mashimo ya matope! Lakini Misri yote ilishtuka kuona kuwa wale wanaowadharau kumbe ndio wanaomwabudu Mungu mwenye nguvu kuliko Mungu wao…..siku ile walipoona Misri yote imeteketea,…na wewe usiangalie hali ya watu wanaomwabudu Mungu wa Kweli ipoje, wapo vile kwasababu fulani tu, lakini hawatakuwa vile siku zote, ipo siku watang’aa kama jua, isikilize hii sauti ya Mungu inayozungumza nawe sasa…Mungu wa kweli sio nyoka, wala ekaristi, wala sanamu ya kiumbe chochote kile, wala sanamu ya mwanadamu yoyote Yule, wala Mungu wa kweli haabudiwi kwa kupitia sanamu ya Bikira Maria, wala chochote kile, Mungu wa kweli anaabudiwa juu mbinguni KATIKA ROHO NA KWELI.

Pengine umekwenda kwa waganga wa kienyeji na kwa kupitia wao umepata mafanikio, na wamekwambia wakristo hawamwabudu Mungu wa kweli, nataka nikuambia ndugu yangu, wamekudanganya na wamekupoteza..Wale nyoka walimpa Farao mafanikio makubwa sana kuliko uliyonayo wewe, lakini hao hao hawakuweza kumwokoa na hukumu ya Mungu iliposhuka juu ya Misri.

Na wewe siku hizi usiweke moyo wako mgumu, achana na hao waganga, kwasababu utaelekea kwenye ziwa la Moto, tupa leo hirizi zote walizokupa, choma moto, mvue mwanao hirizi zote ulizomvalisha kiunoni na shingoni na mikononi, tupa na wewe kila kitendea kazi ulichopewa na mganga wa kienyeji eti upate amani, fedha au utajiri, au vikulinde…hivyo vitendea kazi vitakulinda dhidi ya wachawi wenzako tu tena wenye nguvu kidogo kuliko mganga wako lakini wakija wachawi wengine wenye nguvu kuliko wewe na mganga wako watakuua na kukushinda tu!, na zaidi ya yote ni heri ingekuwa hivyo tu!! Ghadhabu ya Mungu bado inakungojea endapo ukikataa kutubu ndiyo itakayokuharibu kabisa kama ilivyomuharibu Farao, alipoteza fahari yake yote na kufiwa na mwanawe wa pekee.

Ukiyafahamu hayo ni wakati wa kugeuka, Bwana anakupenda na kukuhitaji, kama hujampa Bwana maisha yako, mlango wa Neema bado upo, ila hautakuwepo siku zote, biblia inasema utafika wakati mlango utafungwa, na watu watalia na kuomboleza wakiomba Bwana awafungulie, na Bwana hatawafungulia, Hivyo tubu leo kwa kumaanisha kuacha kabisa maisha ya dhambi uliyokuwa unayaishi huko nyuma, maisha ya usengenyaji, maisha ya rushwa, maisha ya uasherati, maisha ya utazamaji pornography, maisha ya usagaji, maisha ya ulawiti, maisha ya ushirikina, na uhudhuriaji wa waganga wa kienyeji,maisha ya aubuduji sanamu, maisha ya ulevi na sigara.n.k n.K

Na baada ya kufanya hivyo kama hujabatizwa nenda katafute ubatizo sahihi mahali popote pale kulingana na maandiko, na ubatizo sahihi ni wa maji mengi na kwa JINA LA YESU kulingana na Matendo 2:38, na baada ya hapo Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu atakayekusaidia kushinda dhambi, maana kwa nguvu zetu hatuwezi kamwe kushinda dhambi, na Roho huyo huyo atakusaidia kuielewa biblia na kukuongoza katika kweli yote usipotee kwa kuchukuliwa na upepo wa shetani. Na ukizingatia kufanya hivyo utakuwa umezaliwa mara ya pili, na kuwa na uhakika wa kuiona mbingu.

Bwana akubariki sana.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine, na utakuwa umeshiriki katika kuisambaza injili ya Kristo.

Maran atha!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

NEHUSHTANI (NYOKA WA SHABA)

UZAO WA NYOKA.

WANA WA MAJOKA.

BWANA YESU ALIMAANISHA NINI ALIPOSEMA TUWE NA BUSARA KAMA NYOKA?


Rudi Nyumbani

Print this post

SIRI YA KUASI KATIKA KANISA LA MUNGU.

Yapo mambo umeshawahi kujiuliza ni kwanini, hayaishi kutokea kila kukicha katikati ya kanisa la Mungu hususani kwa watu wanaosema wao ni watumishi wa Mungu. Utaona leo kunatokea vituko hivi kesho vile, leo mmoja ananaswa kwenye jambo hili baya, kesho lile, sasa mambo kama hayo ukiyaona usianze kuunyooshea ukristo wote kidole au watumishi wote vidole, badala yake uogope kwasababu mlengwa ni wewe na usipojua sababu ya hayo mambo kuzidi kukithiri sana hususani katika kipindi hichi cha mwisho , utajikuta umetumbukia katika shimo ambalo hutajua ni lini umeingia humo..

Embu fuatilia mazungumzo haya dada huyu aliyonitumia kisha tutaendelea..

“mimi (…..) napenda kuuliza Hivi ni sahihi kwa mtumishi unayetumiwa na Mungu kufanya vituko kwa makusudi kwa kujinadi kwamba utatubu? Hii inanipa shida nafsini maana sielewi

Kwani kuna jambo kwa huyu mtumishi ambaye ndo aliyekua akinifundisha mambo ya kumjua Mungu kwa aliyoyafanya nilikata tamaa nikawa naenda tu kanisani lakini sina imani hata na wachungaji tena. nahisi nao watakua hivyo hivyo japokua natamani sana nikae kwenye mstari lakini nikikumbuka matukio mabaya nasikilizia tu neno ibadani lakini hayakai kabisa, nahitaji msaada zaidi kimaombi peke yangu siwezi mtumishi.

Kwanza huyu mtumishi ni mchafu kwenye mitandao pia ni mzinzi sana yani mno sasa kwa mimi ambaye ni mchanga kiroho nashindwa kuelewa ukimuonya ndio hayo anakujibu usimnyoshee kidole mtumishi wa Mungu utapata ukoma kamuulize Miriamu kilimpata nini.

nilimuuliza inakuaje unajua kabisa uzinzi ni dhambi au matusi ni dhambi alafu unafanya kwa makusudi?

akajibu hakuna mchungaji ambaye hajawai kuanguka na bado wanaendelea kuanguka, ndo nikamwambia kwahiyo wewe unawaiga hao? Mungu sio mjomba wako akasema Mungu ni wa rehema kila wakati, mtu anafanya dhambi anatubu anaendelea mbele nikasema naenda kumwambia mchungaji wako na askofu wako akasema ole wangu nikamharibie kule maana wana mwamini sana na hawajui mwenendo wake upoje na yupo kanisa moja la TAG mahali fulani hivi kule (……..).

natamani sana wachungaji wake wamjue tabia zake asiendelee kuchafua kanisa ndio sielewi nifanyeje.

Yananipa shida moyoni.” Naomba msaada.

***mwisho***

Watu wengi wanashindwa kuendelea mbele na Mungu wao kwa kuwatazama watu wa namna hii, Na hicho ndicho shetani anachotafuta kwako hata wewe usomaye ujumbe huu. ni kweli wanakatisha tamaa, na sio tu kukatisha tamaa bali pia wanawakosesha watu wengi waliowachanga kiimani jambo ambalo Bwana YESU anasema “Ingewafaa zaidi kwa watu wa namna hiyo jiwe la kusagiwa lifungiwe shingoni mwao, wakatupwe baharini kuliko kuwakosesha wadogo hao”.. wadogo wanaozungumziwa hapo ni watu wadogo katika imani (wachanga)/ wanyenyekevu…

Lakini je suluhisho ni nini?..Ni kuwanyoshea watumishi wote wahubirio injili vidole?..Hapana tukifanya hivyo tutajikuta tunapoteza hata vile vizuri Mungu alivyokusudia tuvipate katika Mwili wake [ambalo ndio kanisa lake]. Lakini uzuri ni kwamba Jambo kama hilo Bwana alishakwisha kuliona na kulitolea ufafanuzi uliobora zaidi embu tusome hapa kwa pamoja:

Mathayo 13:24 “Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake;

25 lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.

26 Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu.

27 Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu?

28 Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye?

29 Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing’oa ngano pamoja nayo.

30 Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.”

Tukizidi kusoma tunaona Bwana akitoa tafsiri yake kama ifuatavyo: 

“Azipandaye zile mbegu njema ni Mwana wa Adamu;

38 lile konde ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu;

39 yule adui aliyeyapanda ni Ibilisi; mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika.

40 Basi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia.

41 Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi,

42 na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

 

Ndugu fahamu tu jambo moja Mungu ameruhusu kwa makusudi kabisa, watu wote waovu na wema wote wamee kwa wakati mmoja katika kanisa lake kwa kila kizazi, haijalishi ni wazinzi, au walevi, au washirikina wote, au waabudu sanamu, n.k. wote wameruhusiwa wawepo katikati ya watakatifu, wote waabudu pamoja kana kwamba wote wamekubaliwa na Mungu, karuhusu wote wapokee vipawa vya roho, wote watoe unabii, wote wahubiri, wote wafundishe, wote waponye magonjwa, wote watoe mapepo,. Na wala kusiwe na chochote cha kuwadhuru..Hiyo ni SIRI KUU..Biblia inaiita SIRI YA KUASI. Wote Wameruhusiwa pia kusimama madhahabuni kufundisha, hivyo hilo pia lisikupe shida,..

Magugu na ngano vyote vipokee mbolea ya ardhi na mvua kutoka kwa Mungu..Hivyo si ajabu hata kuwaona wanaombea hata wafu wanafufuka lakini Mungu hawatumbui. 

Kwanini Bwana hataki kuwang’oa sasa?. Tukirudi kwenye ule mfano wa magugu na ngano tunaweza kuendelea kujifunza kitu, 

kwa mfano mbegu zozote wakati zikiwa changa ni ngumu sana kuzitofautisha zipi ni ngano na yapi ni magugu mpaka zitakapokomaa ndio utajua kiwepesi, kadhalika pia unaweza ukang’oa magugu yote kumbe hujui kuwa zipo mbegu nyingine za magugu zilikuwa zimefukiwa chini hazijamea vizuri, na ukajikuta umeziacha zile..Hivyo ili zote uzipate kiwepesi bila kubakisha hata moja itakupasa uwe mvumilivu kidogo ungoje kwanza kipindi fulani kipite zote zichipue, kubwa na ndogo. Ili sasa uzitoe zote kiwepesi na mara moja, kwasababu utakuwa una uwezo wa kuzitofautisha.

Na vivyo hivyo waovu na wema katika hatua za awali huwezi kuwatofautisha katika kanisa la Mungu, lakini kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda mwisho wao utawaweka wazi wote..Ndipo hapo watakapokuja kukusanywa wote na kutupwa katika lile ziwa la moto. Siku ile ndio lile kundi la Bwana! Bwana! Hatukutoa unabii kwa jina lako?, hatukufufua wafu? Hatukufanya miujiza mikubwa n.k??..Litakapomfuata Bwana. Lakini Bwana atawakana dhahiri..na kuwaambia siwajui nyinyi tokeni kwangu nyinyi mtendao maovu.

Watu wa namna hiyo ni mahususi kabisa wamepandwa na shetani kuliharibu shamba la Mungu. Ni ule UZAO WA NYOKA wenyewe. Na wanajua kabisa mtu yeyote aliye muhubiri atapata hukumu iliyokubwa zaidi kuliko wengine endapo atayahalifu mapenzi ya Mungu lakini wao hata hawaogopi kufanya, wanaendelea tu!..Huo ni uzao wa nyoka. Wanageuza kazi ya Mungu kuwa biashara, huku hofu yoyote ndani yao kuwalipisha watu pesa ili wapate huduma ya kiroho. Ni washirika kanisani lakini bado wanakwenda kwa waganga wa kienyeji, na wengine ni wachawi.. Wanafanya mambo ya ajabu kwa siri huwezi kuwagundua, lakini siku ile watajulikana.

Wanafahamu kabisa hakuna mlevi yoyote atakaye urithi ufalme wa mbinguni lakini wanakunywa pombe, na wakati huo huo bado utawakuta katika vikundi vya maombi, utawakuta wanahubiri, utawakuta wana imba kwaya, utawakuta wanahudumu kanisani, utakuwa ni manabii, ni waalimu na ni wachungaji, lakini bado matusi wanazidi kutukana.. Wanafanya jina la Mungu linatukanwa, si ajabu kwasababu ndio utumishi shetani aliowaitia huo.

Ni UZAO WA NYOKA..kama Bwana alivyosema.. “Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum? Mathayo 23.33”……Ni Wana wa shetani waliopandwa mahususi na ibilisi kuliharibu shamba la Mungu.

Hivyo wewe unayesoma, usiache unyofu wako na usafi wako uliokuwa umeuanza kwa kuutazama tu uzao wa nyoka katika kanisa la Mungu na kutetereka . Usitishwe na wao kwasababu uzao huo haukuanzia siku za mitume tu hapana, bali chimbuko lake lilitokea tangu Edeni, pale tu Hawa alipokubali kudanganywa na nyoka na kula tunda, kisha baadaye akaenda kula na mume wake. na ndio maana ndani ya tumbo la Hawa kulionekana watoto wawili Kaini na Habili…Mmoja uzao wa Nyoka na mwingine Uzao wa Adamu, tunafahamu habari ilivyokuwa jinsi Kaini alivyokuwa mwovu kwa tabia zake, na ndivyo ilivyo katika kanisa la Kristo

Mtume Paulo aliandika haya kwa uweza wa Roho..

2Wakorintho 11: 2 “Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.

3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo”.

Unaona, Sisi tuliposwa kwa Kristo [mfano dhahiri wa Adamu ]kama bikira safi lakini lile JOKA ibilisi akapanda mbegu zake chafu katika kanisa la Kristo ambalo linafananishwa na Hawa,. Na hivyo mpaka sasa kumetokea watoto wawili KAINI na HABILI..kwenye kanisa…Kaini ndio hawa wakristo-wa-uwongo.

Lakini mtume Paulo anatushauri tusiuache unyofu na usafi wa Kristo. Hivyo huu si wakati wa kulelemaa tu, kwa kufuata kila wimbi la mafundisho yanayokuja mbele yako. Bali ni wakati wa wewe binafsi kujitathimini, je! umesimama katika IMANI,? Je! Kristo akirudi leo utakwenda naye? Je! wewe binafsi upo katika utakatifu? Ambao biblia inasema pasipo huo hakuna mtu atakayemwona Mungu?(Waebrania 12:14) Je! unayashika maagizo yake?…Usisimame kwa niaba ya mwingine! Simama wewe kama wewe Kama ukijifunza kuenenda kwa utaratibu huo basi shetani hataweza kukunasa hata akija na wimbi kubwa kiasi gani la watumishi wake wa uongo, au mafundisho yake ya uongo, hata kupata kwasababu umejengwa juu ya mwamba imara YESU KRISTO.

Ubarikiwe sana.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Print this post

ROHO ZILIZO CHINI YA MADHABAHU:

Ufunuo 6:9 “Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.

10 Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?

11 Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vilevile kama wao.”

Shalom! Mpendwa wa Bwana. Leo ni siku nyingine Bwana ametupa, hivyo usikubali siku ya leo ipite bila kupata maarifa mapya yahusuyo maandiko hususani katika siku hizi za hatari tunazoishi.

Na leo tutatazama juu ya hizi roho zinazoonekana hapo zikiwa chini ya madhabahu zikilia kwa nguvu na kuugua kutaka zilipiziwe kisasi juu ya hao wakaao juu ya nchi, Leo tutaona hizi roho ni wakina nani.

Kama hufahamu bado juu ya ufunuo wa Mihuri saba ambayo habari yake inaanzia kutokea ule mstari wa kwanza, basi ni vizuri ukatenga muda wako kupitia maelezo yake hapa >> Ufunuo wa Mihuri saba  ili ukifika hapa ikusaidie pia kupata picha kamili ya kitu kinachoendelea katika huu muhuri wa tano tunaokwenda kuutazama.

Watu hao wanaoonekana hapo si wengine zaidi ya wayahudi ambao waliuawa katika kipindi cha Holocaust, kilichotokea kati ya kipindi cha mwaka 1941-1945, Ambapo wayahudi wengi zaidi ya milioni 6 waliuawa kikatili chini ya utawala wa kidicteta wa NAZI Ujerumani..Historia inarekodi Mbili ya tatu ya wahayudi wote waliokuwa wanaishi bara la ulaya waliuliwa. Na Leo tutatazama kwa ufupi baadhi ya mateso waliyokuwa wanayapitia mpaka kupelekea kuwaona hapa chini ya madhabahu wakilia na kuuga kuomba kisasi kisikawie kulipizwa juu ya adui zao.

1) CHEMBA ZA GESI:

Wakati huo waayahudi wengi walikusanywa kutoka katika vijiji na miji mingi katika majimbo yote yaliyokuwa yanatawailiwa na Nazi, na kuahidiwa kuwa wanapelekwa mahali pa kutunzwa mbali na vita penye nyumba nzuri na utulivu.. Lakini badala yake walichukuliwa na kuwekwa katika treni, na kusafirishwa umbali mrefu kwa siku kadhaa bila hata maji wala chakula mbali na makazi ya watu, na kumbe huko kulikuwa tayari wameandaa kambi za mateso na kazi tu kwa ajili ya wayahudi. Sasa Walipokuwa wanawasili kwenye kambi, wanaume na wanawake na watoto walikuwa wanatengwa tofauti,.

Wale wanaume wenye nguvu walichukuliwa na kupelekwa kufanyishwa kazi ngumu za ujenzi wa reli na kukata magogo, lakini wale wanawake na watoto pamoja na wazee wote, walikuwa wanadanganywa kuwa kabla ya kwenda kupangiwa majukumu yao ya kazi inawapasa kwanza waende kuogeshwa kwa pamoja katika mabafu ya moto ili kuzuia magonjwa ambayo yamekuwa yakilipuka mara kwa mara katika kambi nyingi za ki-NAZI.

Hivyo bila kujua chochote wale wanawake na watoto wanakubali kuvua nguo zao, pamoja na kukatwa nywele zao. Kisha wanawachukulia kwa upole na kuwapelekwa kwenye vyumba maalumu vinavyoonekana kama mabafu yenye mabomba ya mvua.

Wakishawaingiza wote huko, kuhakikisha kuwa hakuna nafasi hata kuzunguka huku na kule kwa mtu yeyote kutokana na kubanana kwao, ghafla mlango wa chumba hicho kisichokuwa hata na sehemu ya kupitisha hewa kinafungwa kwa nyuma..Na taa zote kuzima eneo lote linakuwa giza kwa muda fulani.

Wakati wale watu kule ndani wanashangaa ni jambo gani linaendelea, ghafla tundu la chumba hicho kwa juu linafunguliwa kuruhusu mwanga wa jua kupita kwa muda mfupi, wakidhania kuwa wanafunguliwa maji kwa juu kumbe hapo juu anakuwa amesimama mtu ameshika makopo maalumu ya gesi mbaya ijulikanayo kama “ZYKLON B”, kitu anachofanya ni anaitaupa hiyo gesi chini kwa haraka kwenye hicho chumba cha shimo walichomo hao watu kisha anafunga mlango wa tundu.

Baada ya muda mfupi, kinachosikika huko nje ni kilio na mahangaiko ya watu, gesi ile ni mbaya kwasababu inaua oxgen yote, halafu inachoma mapafu mtu akiivuta anasikia kama moto unawaka kwenye kifua chake, damu zinaanza kutoka puani na midomoni, sasa kwa kuwa hakuna sehemu ya kutokea, basi watu kwa kujaribu kuokoa maisha yao wanarukiana huku na kule kama vile kuku aliyechinjwa wakijaribu kutafuta walau hata sehemu ya kuokoa maisha yao. Lakini kwa kuwa gesi ile ni kali sana mtu hafi kifo cha raha bali cha mateso makali na mahangaiko yasiyoelezeka, wengi wao wanakutwa wamekufa huku wametokwa na haja zote mbili. Na ndani ya muda wa dakika chache tu, kila mmoja anakuwa ameshakufa, kisha baadaye kidogo kama baada ya dakika ishirini hivi, askari wa ki-NAZI anakuja kufungua mlango wa ile chemba, na kuvuta miili yote nje. Na wakitoka hao wanaingizwa wengine.

Sasa kwa kuwa kambi hizi zipo mbali na makao ya watu, wale askari wanakuwa tayari wameshachimba mashimo makubwa na marefu, kwa ajili ya kuichomea miili ile, na kwa jinsi gesi ile ilivyo mbaya miili ikitoka pale hata kuitambua tena ni ngumu kwa jinsi ilivyoaribiwa na gesi ile. Moshi ule hauishi kwasababu kila siku idadi ya watu wasiopungua watu “ELFU SITA” walikuwa wanaingizwa katika chemba za gesi. Na hiyo ni takwimu ya kambi moja, na kulikuwa na kambi kama hizi nyingi tu za mateso.

Jaribu kufikiria ni unyama kiasi gani huo anafanyiwa mwanadamu mwenzako. Kumbuka wayahudi hawakufanya kosa lolote listahilio mateso hayo makali, walichukiwa kwasababu wao ni WAYAHUDI tu! Uzao wa Mungu basi!..wala hakuna sababu nyingine yoyote, iliyowafanya watende mambo ya kinyama kama hayo. Mamilioni ya wayahudi waliuawa kwa namna hii ya kuwekwa katika chemba za gesi.

Huo ni mfano wa mambo madogo sana yatakayokuja kutokea huko mbeleni kwa watu wale watakaoukosa unyakuo.

2) UCHUNGUZI WA KIMAABARA:

Sasa wale ambao watanusurika kwenda kwenye chemba za gesi, baadhi yao wanachukuliwa na kwenda kufanywa “SAMPULI” kwa majaribio katika mahabara. Wengine wanachukuliwa na kwenda kufungiwa katika vyumba maalumu, na ndani ya vyumba hivyo hawapewi maji wala chakula. Bali maji ya chumvi tu tena yale ya baharini, ili kutafiti ni jinsi gani wanadamu anaweza kuishi kwa muda mrefu kwa kutegemea tu maji ya bahari.

Hivyo kama wewe umesoma unaelewa ni jinsi gani chumvi inavyofonyonza maji mwilini, unakaukiwa maji kabisa, kiasi kwamba hata mate yanaisha mdomoni.. Jaribu kufikiria watu hao wanawekwa katika hali hiyo ya maji tu ya chumvi mpaka kufa kwao. Mfanyakazi mmoja wa kambi hizo anasema alishuhudia watu wale wakilamba sakafu kwa ajili ya maji yanayochuruzika wakati wa usafi katika sakafu. Lakini walikufa wote baada ya kipindi Fulani.

Wengine walichukuliwa na kuwekwa katika vyumba vya baridi vyenye barafu, uchi, kama majaribio wakifanyiwa utafiti kuona ni jinsi gani mtu anaweza kutibiwa kwa haraka kutoka katika ugonjwa wa Hypothermia, huu ni ugonjwa utokanao na mtu kupigwa na baridi sana na kupoteza fahamu kuwa kama kichaa..Lakini wengi wao hawakuweza kustahimili walikufa baada ya kipindi Fulani na wengine wale waliostahimili waliishia kupata mtindio wa ubongo wa kudumu.

Wengine walichukuliwa na kutolewa misuli yao mwilini wakishuhudia kwa macho yao na kuong’olewa mifupa yao bila hata ya ganzi yoyote, na kujaribu kuupandikizwa kwa mwengine ili wajaribu kuona kama kuna uwezekano wa kuamisha viungo kutoka kwa mwanadamu mmoja hadi kwa mwanadamu mwengine kwa muda mfupi na kuendelea kufanya kazi..Wengi wao kutokana na maumivu makali walikufa na baadhi ya walipata ulemavu wa kudumu na wale waliokuwa dhaifu waliuliwa au walipelekwa katika chemba za gesi.

Walikuwa wanawachukua vijana wadogo umri katika ya miaka 11-12 na kuwafunga mahali wasipoweza kuhangaika kisha wanafungiwa nyundo juu ya vichwa vyao na ile nyundo inaachiwa ishuke juu ya vichwa vyao kila baada ya dakika kadhaa, kupima kiwango cha ustahimiliji wa mtu anapojeruhiwa maeneo ya vichwani..wengi wa hao kama wasipokufa basi wanaishia kuwa vichaa.

Wanawachukua mapacha katika pea. Na kumfanyia utafiti aidha mmoja wao, huku mwingine akimtazama, wanaweka “dai” kwenye macho ya mmoja, kupima mabadiliko ya vina saba kwa mwingine..baadaye Yule akishamaliza kufanyiwa utafiti na kuonekana kuwa hafai tena ni kufa tu, basi wanamalizia kumuua na yule mwenzake, kwasababu hana kazi tena hapo.

Waliwahasi wayahudi wengi kwa njia tofauti tofauti wengine kwa x-ray, au upasuaji au kwa madawa makali n.k. kuona ni ipi iliyonyepesi ya kuwahasia watu kwa haraka bila kupoteza muda na gharama za matibabu. Wayahudi waligeuzwa kuwa wanyama.,.Na HITLER alikuwa na kauli mbiu yake inayosema “ hawa watu wasife tu kifo cha kawaida, bali wahakikishe wanakufa vifo vya mateso”. Mambo haya unaweza ukadhani ni hadhithi au yalitokea zamani sana lakini ni mambo yaliyotekea miaka 76 tu iliyopita!. Wapo watu baadhi ambao bado hawajafa walioshuhudia hizo kambi za mateso..

Wengine walichukuliwa juu kwenye  helikopta za jeshi na kupelekwa juu sana na kisha kutupwa chini, pasipo parachuti na wanajeshi wale waliruka na maparachuti kujaribu kujijaribu uwezo wao wa kuokoa watu endapo wataanguka kutoka kwenye helikopta au ndege, wengi wa wayahudi hao waliishia kuanguka chini na kufa papo kwa hapo, na wale wanajeshi wakitua chini na parachuti wakiwa salama.

Wengine walichukuliwa na kufungiwa kwenye mabehewa, na magari ya mizigo, na huko ndani inapitishwa mirija yenye gesi ya carbon-monoxide..ile ya mkaa ambayo inamuua mtu kwa haraka sana. Kisha baadaye wanafunguliwa na kutupwa kwenye mashimo huko misituni.

Na Wale wanaosalia kufanya kazi ngumu, maisha yao ni ya viboko viboko na kazi, chakula ni supu tupu mchana, na kipande cha mkate kidogo usiku..hayo ndio maisha yao ya kila siku huku ukiwa kwenye kazi ngumu..ukionyesha udhaifu wowote kule kambini uliuliwa au ulinyongwa. Ndivyo ilivyokuwa katika kambi zote.

Kaka/dada hayo ni baadhi tu mateso ndugu zetu hawa wayahudi waliyoyapitia, katika kile kipindi cha vita ya pili ya dunia, na ndio hao wanaoonekana hapo chini ya madhabahu wakisema

“Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi? Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vilevile kama wao.”

Unaona? Biblia inasema “WAKAAMBIWA WASTAREHE BADO MUDA MCHACHE”.

Mpaka itimie idadi ya wajoli wao watakaouawa vile vile kama wao. Na hiyo ndugu itakuwa si wakati mwingine zaidi ya wakati wa DHIKI KUU ambayo ipo karibuni kutokea..bado muda mfupi sana. Ni dhiki ambayo Bwana Yesu anasema haijawahi kutokea wala haitakaa itokee tena kama hiyo baada ya hapo,.Yaliyowakuta wayahudi kipindi cha Hitler ni mfano mdogo sana kulinganisha na yatakayokuja kuwakuta tena wakati wa ile dhiki kuu mpinga-Kristo atakaponyanyuka kupambana na uzao wote wa Mungu .

Mpinga-Kristo atawaua watu wote ambao watakataa kuipokea ile chapa ya mnyama, lakini wale wote ambao watakubali kuipokea hatawaua,na watakuwa ni wengi sana watakaoikubali chapa ile, kwasababu haitakuja kwa wazi kama wengi wanavyodhani, na kwa pamoja wataingoja ile siku ya Bwana inayotisha ambayo itatokea kipindi kifupi tu baada ya dhiki kuu kuisha.

Na safari hiyo haitakuwa kwa wayahudi tu peke yao, bali pia kwa wale wakristo watakaochwa kwenye unyakuo. Na hawa hawatauliwa ovyo ovyo tu barabarani kama wengi wadhanivyo, bali watapelekwa pia katika makambi ya siri ya mateso, huko ndio kutakuwa na kilio na kusaga meno. Usitamani uwepo ndugu!

Bwana ameshatuonya, Dalili zote zinaonyesha Kristo yupo mlangoni kurudi, unyakuo ukipita leo je! Utakuwenda na Bwana katika karamu ya arusi ya mwanakondoo? Au utabakia hapa? Jibu unalo ndugu. Ni maombi yangu kwamba utaanza kuyatengeneza maisha yako tena upya.

Tubu dhambi zako sasa, ili usamehewe. Kisha ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO, upate ondoleo la dhambi zako, na baada ya hapo uendelee kuishi maisha ya kumtazama Bwana na utakatifu mpaka siku unyakuo utakapokukuta.

Maran Atha!

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine na Bwana atakubariki, kwani utakuwa umeshiriki kuifanya kazi ya Mungu.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

UNYAKUO

KATI YA UNYAKUO WA KANISA, DHIKI KUU, VITA VYA HAR-MAGEDONI, UTAWALA WA MIAKA 1000, VITA YA GOGU NA MAGOGU, HUKUMU YA KITI CHA ENZI CHEUPE. JE, NI NINI KINAANZA NA KINGINE KUFUATA KWA MPANGILIO WA MATUKIO HAYO?

UFUNUO:Mlango wa 6


Rudi Nyumbani

Print this post

MWANZI ULIOPONDEKA.

Mathayo 12:20 “Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala utambi utokao moshi hatauzima, Hata ailetapo hukumu ikashinda.

21 Na jina lake Mataifa watalitumainia.”

Wakati nautafakari huu mstari nikakumbua tukio lilotokea mahali nilipokuwa ninaishi kipindi cha nyuma, Nakumbuka wakati fulani tulipanda migomba. Na kila siku jioni na asubuhi nilikuwa na desturi ya kwenda kuimwagilia,.mpaka ikakua kiasi cha kuanza kuzaa ndizi,.Lakini siku moja usiku upepo ulivuma, usiokuwa wa kawaida, na tulipoamka asubuhi tulikuta migomba mingi kati ya ile imelala chini, na kibaya zaidi yote iliyovunjika ilikuwa ni ile iliyokuwa imeanza kutoa Ndizi, nadhani kutokana na kulemewa na uzito wa ile mikungu ndio maana ikashindwa kustahimili upepo na kuanguka, ilibaki michache tu ambayo haikuanguka na hiyo ilikuwa ni ile ambayo haijazaa..Haikuwa migomba ya hapo tu, bali mpaka ya majirani pia ilianguka..

Sasa Kitu tulichokifanya ni kujaribu kuinyanyua ili kuisapoti na mirunda ya miti, lakini mingi ilivunjia vibaya kiasi kwamba hata ukiunyanyua upande huu, unaangukia upenda ule, hata mfano uweke mirunda 6 kuusapoti mgomba mmoja bado hauwezi kusimama, na kuikata hatuwezi, tutakosa ndizi na ndizi bado ni changa. Hivyo ilitubidi kupambana nayo hivyo hivyo kujaribu kuisimamisha au kuigemeza kwa namna ambayo haitaweza kukauka mpaka hapo ndizi zitakapokomaa.Tulipitia changamoto Fulani mfano Leo utaisimamisha hivi, kesho utakuta umeanguka tena, leo utauweka hivi kesho utaikuta ipo vile. Lakini japo iliendelea kuwa katika hali mbaya ya kusua sua, lakini hatukukosa kabisa kupata ndizi, tulivuna ndizi zilizokomaa kabisa zisizo na matatizo.

Sasa ndio najiuliza kama sisi hatukuweza kuikatia tamaa migomba ile, ambayo sio kwamba ilikuwa ndio chakula pekee tulichonacho, hapana lakini hatukupenda tu kuiona katika hali ile ya kuanguka,..lakini hatukuikatia tamaa kabisa mpaka ilipofika wakati wa kutoa matunda mazuri kabisa yaliyokomaa,..UNADHANI MUNGU ATATUKATIAJE TAMAA SISI ?. Embu yatafakari tena haya maneno yaliyonenwa juu ya Bwana Yesu.

“Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala utambi utokao moshi hatauzima, Hata ailetapo hukumu ikashinda.

21 Na jina lake Mataifa watalitumainia.”

Mwanzi, ni shina lolote la mmea, inaweza ikawa ni mti, mchicha, mgonga n.k. Lakini anasema ukipondeka huo, hata kufikia hatua ya kukosa matumaini kabisa yeye anasema hatamalizia kuuvunja..Utambi utoao moshi ni kama umeshazima, yaani utambi ukishafikia hatua ya kutoa moshi tu, ni wazi kuwa huo tayari umeshazima huo, lakini yeye anasema hataumalizia kuuzima, moyo ambao wewe huwezi kuwa nao, huwezi kuwa na tumaini na utambi ambao unatoa moshi tu, tena kikubwa utakachofanya hapo ni kuuzima haraka usiendelee kukotelea moshi. Lakini kwa YESU haikuwa hivyo, yeye bado aliutazama, na kuuhangaikia..Na utambi huo ni sisi, mwanzi huo ni mimi na wewe!

Inawezekana maisha yako ni sawa na mwanzi uliopondeka, umefika hatua, unaona kabisa tayari ulishakosea njia, na hakuna matumaini tena ya kumrudia Mungu, umekuwa mlevi wa kupindukia, unatumia madawa ya kulevya mpaka yamesha kauthiri huwezi tena kuacha.,Umekuwa mwasherati mpaka imefikia hatua umepata UKIMWI, na wewe bado ni kijana mdogo tu na hivyo umekata tamaa ya kuishi, unaona kama jamii haiwezi kuwa na wewe tena, wala Mungu kukupokea kwa mambo uliyoyafanya. Umekuwa katika magonjwa yasiyoponyeka, huna tumaini tena. Nataka nikuambie, YESU yupo, sio marehemu, kutaka kukusimamisha tena, na kukunyanyua tena uwe mwana Mungu BUREEE!!.

Yeye ndiye aliyetabiriwa maneno haya

Isaya 61: 1 “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA AMENITIA MAFUTA niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao”.

Unaona? Unaweza ukawa ni mdhaifu wa Imani, imefikia wakati unataka kusema Mungu hayupo umekuwa utambi unaotoa moshi, ni hatua moja tu imebaki ya wewe na kukata tamaa ya maisha, umekuwa katika vifungo vya giza, umeingia katika ushirikina, na uchawi, maisha yako unaona kabisa yapo hatarini kutoweka, hujui kama hata kesho utaishi kwa jinsi ulivyo katika vifungo vya hofu, wewe ni utambi unaotoa moshi, pengine unaweza ukawa ulianza vizuri na Kristo huko nyuma ulikuwa moto kweli kweli utambi wako ulikuwa unawaka vizuri huna shida yoyote , lakini wakati ukafika shughuli za dunia na udanganyifu wa mali na anasa vikakusonga, sasa umepoa huna tofauti na watenda dhambi wengine..Yesu ni wa rehema bado anatamani kukuwasha tena uangaze upya. Ametiwa mafuta kwa kazi hiyo.

Ulimwengu utakukatia tamaa, lakini Kristo anakutazama haijalishi umedondoka mara ngapi, Upo katika masononeko ya roho, upo katika tabu na maumivu mbali mbali, Njoo kwa Yesu. Leo hii sema ni mwisho naanza tena na Bwana naye atakupokea,..

Ukisoma pale mbele kidogo utaona anaendelea kusema Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala utambi utokao moshi hatauzima, HATA AILETAPO HUKUMU IKASHINDA..Unaona? Hukumu inayozungumziwa hapo, ni kusudi la Mungu, au mapenzi ya Mungu juu ya mtu huyo…Ikiwa na maana kuwa Yesu atahakikisha mtu Yule ampokee yeye..japo atakuwa ameharibika kiasi cha kutokuweza kutengenezwa tena, yeye mwenyewe atahakikisha anamfanya upya maisha yake na kuhakikisha mapenzi yote ya Baba yake aliyokusudia juu ya huyo mtu yanatimia. Na ndio maana anasema:

Mathayo 11: 28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”

Ndugu ni nani awezaye kukuahidi mambo mema kama haya kama sio YESU peke yake.?Kwanini kila siku unasikia YESU ni rafiki wa wengine, Na asiwe rafiki yako? Hata sisi tulipokuwa walevi, na wazinzi, na watukanaji, wa endaji disco, watazamaji pornography, tulikuwa katika hofu, japo mbele za watu tulijifanya wenye furaha siku zote, na wenye ujasiri..Lakini siku YESU alipotupa raha nafsini mwetu ndipo tulipojua hakika raha halisi ipo wapi?..Kwahiyo tunafahamu vizuri hali unayopitia wewe uliye katika dhambi, kwasababu na sisi tulikuwa huko, lakini tumeonja huku, na tumejua hakika Bwana ni mwema.

Njoo! Kwa mwokozi wako ambaye ni mwokozi wetu pia, muda unazidi kwenda, moja ya siku hizi UNYAKUO utapita, au kama hautapita basi KIFO kitakukuta, sasa huko uendako ni nani atakuwa mtetezi wako? Kama umemkataa mtetezi wako angani u hai?..Ukimpokea leo atakuwa ni rafiki mwema kwako.

Bwana akuangazie rehema zake.

Ubarikiwe na Bwana.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoenda:

UPONYAJI WA YESU.

NAMNA GANI NITAPOKEA NGUVU ZA BWANA YESU?

JIPE MOYO.


Rudi Nyumbani

Print this post

MWINUE YESU KRISTO KATIKA MAISHA YAKO.

Shalom! Mtu wa Mungu, karibu tujifunze Neno la Mungu, kwa Neema zake, leo tutajifunza kuhusu umuhimu wa kumwinua Yesu Kristo katika maisha yetu, Tunaweza tukajifunza katika safari ya wana wa Israeli wakati wametoka Misri, ambapo tunaona wakati Bwana amewatoa katika utawala mgumu wa Farao, wakiwa njiani kuelekea nchi yao ya ahadi, walikutana na jeshi la shetani kuwapinga safarini. Na hawa hawakuwa wengine zaidi ya WAAMALEKI. Waamaleki walikuwa ni watu kutoka katika uzao wa Esau ndugu yake Yakobo..

Kama unakumbuka Isaka wakati anawabariki wanawe Esau na Yakobo, Yakobo alimnyang’anya ndugu yake mbaraka wake, kwasababu ya yeye kutokuujali ukubwa Mungu aliompa. Hivyo ikatengeneza aina fulani ya chuki kati ya hao ndugu wawili, yaani Esau na Yakobo, na Baba yao tunasoma baada ya kumbariki Yakobo alimwambia Esau maneno haya…

Mwanzo 27: 38 “Esau akamwambia babaye, Una mbaraka mmoja tu, babangu? Unibariki mimi, mimi nami, Ee babangu. Esau akapaza sauti yake, akalia.

39 Isaka, baba yake, akajibu, akamwambia,Angalia, penye manono ya nchi patakuwa makao yako,Na penye umande wa mbingu unaotoka juu.

40 Kwa upanga wako wewe utaishi, nawe utamtumikia nduguyo; NA ITAKUWA UTAKAPOPONYOKA, UTALIVUNJA KONGWA LAKE KATIKA SHINGO YAKO.

41 Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ule mbaraka babaye aliombarikia. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo”.

Kwahiyo unaweza kuona hapo hizo Baraka, hazikuwa kwa Esau na Yakobo tu peke yao, bali ni kwa vizazi vyote vya Esau na vizazi vyote vya Yakobo,.Kwamba Israeli atakuwa akimshinda Esau lakini endapo Israeli atalemaa katika roho basi Esau atampiga na kulivunja kongwa lake katika shingo yake.

Sasa hapa baada ya miaka mingi sana zaidi ya miaka 400 Kupita..tunaona uzao wa Yakobo ambao ndio wana wa Israeli unakutana tena katika mapambano na uzao wa Esau ambao ndio hao Waamaleki. Hivyo Israeli walijua kabisa endapo tusipokuwa makini, na hawa wakiwa na bidii basi unabii unaosema hatutamshinda Esau utatimia juu yetu..Hivyo ile vita haikuwa ya kawaida palikuwa na changamoto kubwa sana katika, Israeli hawakuwa na namna nyingine zaidi ya kumgeukia Mungu na kumtegemea yeye…

Ndipo tunasoma Musa baada ya kupata hizo habari kuwa waamaleki wamewazunguka alikwenda kumwomba Mungu wa Israeli na Bwana akampa maagizo ya kufanya kama tunavyosoma katika…

Kutoka 17: 8 “Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu.

9 Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu.

10 Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima.

11 Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda.

12 Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa.

13 Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga”.

Hapa tunaona mkono wa Musa ndio uliowapa ushindi waisraeli, alipounyanyua juu, ndivyo waisraeli walivyokuwa wanapata nguvu vitani, na alipoushusha waamaleki waliwapiga waisraeli..Lakini kama tunavyosoma mwisho wa siku Israeli walishinda kutokana na Mikono ya Musa kusimama juu muda wote.

Ni nini tunachoweza kujifunza katika habari hii ??

Wakristo sisi ni uzao wa Mungu, ambapo tumefanyika kuwa uzao wa Mungu kweli kweli, kupitia Yesu Kristo Bwana Wetu, Mkuu wa Uzima, sisi tunafananishwa na Uzao wa YAKOBO ambao umebarikiwa…Lakini pia upo uzao wa yule Adui, huo unafanana na uzao wa ESAU, na huo kazi yake ni kupambana na sisi kila siku kutupinga katika safari yetu ya kwenda mbinguni,..Na Bwana alitoa unabii kama alivyotoa kwa Yakobo na Ndugu yake kwamba Yakobo atampiga Esau lakini pia Esau akiponyoka atamvunja kongwa Yakobo katika shingo yake {Kwa tafsiri iliyo nyepesi ni hii: Esau akijitahidi na kupata nguvu, basi ataweza kuondoa utawala wa ndugu yake juu yake}..Na pia Bwana alizungumza juu yetu, na kusema.

“nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino. Mwanzo 3:15”

Wengi tunaishia hapo kwamba, uzao wako utamponda kichwa, lakini tunasahau kuwa pia uzao wa nyoka umepewa mamlaka ya kutuponda sisi kisigino, tusipokuwa makini”

Kwahiyo katika ulimwengu wa Roho ni vita vikali vinaendelea, hivyo inahitajika umakini mkubwa sana, na msaada ya Mungu.

Sasa Biblia inasema… “kama vile Musa alivyomwinua nyoka wa shaba jangwani” ili kila amtazamaye yule nyoka wa shaba apone, ndivyo hivyo hivyo Mwana wa Adamu alipaswa ainuliwe msalabani ili kila mtu amtazamaye aokolewe..

Kadhalika kama Musa alivyounyanyua mkono wake juu ili kila Mwisraeli aliyeko vitani apate kupona na kuteka na kupata ushindi dhidi ya Maadui zake..NA WAKRISTO VIVYO HIVYO HATUNA BUDI KUMWINUA YESU KRISTO KATIKA MAISHA YETU ili tuweze kupata ushindi dhidi ya maadui zetu (yaani roho ya uadui inayotenda kazi ndani ya watu na majeshi ya mapepo wabaya).

 Na kumbuka kumwinua Kristo katika maisha yetu sio kumwimbia mapambio na nyimbo za kuabudu, hiyo ni sehemu mojawapo, Lakini sehemu kubwa ya kumwinua Mungu katika maisha yetu ni kumaanisha kumwamini kwa kuzitubia dhambi na kuzicha, na kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu na kuishi maisha ya utakatifu yanayoonekana mbele za watu kuanzia huo wakati na kuendelea, huko ndiko kumwinua Kristo kunakozungumziwa.

Kumbuka pia hakuna ushindi pasipo Yesu Kristo kuinuliwa juu ya maisha yetu. Musa alipoishiwa nguvu watu walikuja kumsaidia kuitegemeza mikono yake ili isishuke…Na sisi katika maisha yetu ya kikristo ya vita, tunapoishiwa nguvu…tunapaswa tufanye juu chini tusiiangushe imani yetu kwa Kristo tuishikilie kwelikweli kwa bidii zote maana hiyo tumekabidhiwa mara moja tu!…Biblia inasema “Mpende Bwana Mungu wako kwa nguvu zako zote, kwa akili zako zote, na kwa moyo wako wote”.

Vinginevyo tukisema tuiache Imani, shetani yupo na amepewa amri ya kutuponda visigino. Amri hiyo kapokea kutoka kwa Mungu.

Ndugu unayesoma ujumbe huu, Yesu Kristo ni muhimu sana katika maisha haya…kama ulimsikia kwa juu juu tu!! kanisani, au mahali popote pale, kama umehubiriwa ni wa-mafanikio-ya-kibiashara Yesu ni zaidi ya hapo!…. jaribu tena kutenga muda umtafakari, hakuna tumaini, wokovu, hakuna maisha, hakuna mafanikio yoyote nje ya Yesu Kristo!…Waliomwamini ndio wanaoitwa wabarikiwa. Huwezi kumpendeza Mungu wala kumwelewa Mungu, wala kumshinda shetani nje ya Yesu Kristo!…Kama ule mkono haujanyanyuliwa juu (Yesu Kristo) hata kama unajiona unatenda wema kiasi gani kama hujamnyanyua juu ni kazi bure! Ni sawa na mtu anayefanya kazi katika shirika ambalo hajaajiriwa, wala hawamjua akitumai kupata mshahara mwisho wa mwezi kutoka huko.. mipango yako ni mizuri lakini nje! Ya Yesu Kristo ni bure!..

Suluhisho ni kumtamani aje aingie katika maisha na kuanza maisha mapya katika yeye..

Bwana akubariki sana.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.

USIMWABUDU SHETANI!

NEHUSHTANI (NYOKA WA SHABA)

JAWABU LA MAISHA YA MTU.


Rudi Nyumbani

Print this post

WATU WASIOJIZUIA.

Kutokujizuia ni kitendo cha kukosa uwezo wa kutawala kitu fulani kisitokee kisichopaswa kufanyika kwa wakati huo. Kwa mfano mtu anapokuwa mlevi wakati mwingine anajikuta amejisaidia pale pale, au kinywa chake kinaanza kuzungumza maneno yasiyokuwa na maana, pengine ataanza kutukana au kufoka..Huko ni kutojizuia..mambo ambayo mfano angekuwa na akili timamu, asingeweza kuyafanya hadharani.

Biblia inasema moja ya dalili kubwa itakayotuonyesha kuwa tunaishi katika siku za mwisho ni kuwepo kwa wimbi kubwa la watu wasioweza KUJIZUIA. Na kutojizuia kunakozungumziwa hapo sio kujizuia kutokutokwa na haja, hapana bali kutojizuia kutenda maovu hadharani mbele za watu, hivyo si watu wema wanaozungumziwa hapa bali wanazungumziwa wale walio waovu, ili kutofautisha uovu ule wa nyuma na huu wa siku za mwisho, kumbuka waovu wa zamani walikuwa na kitu kinachoitwa Kujizuia, lakini waovu wa siku za mwisho biblia inaweka wazi kuwa hicho kitu hakitaonekana ndani yao kabisa.

2 Timotheo 3:1-17

1 Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.

2 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,

3 wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, WASIOJIZUIA, wakali, wasiopenda mema,

4 wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;

5 wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.

Ilikuwa zamani, mwanamke kahaba ni mtu wa kujificha, anafanya ukahaba wake kwa siri hata ni ngumu kumtambua, mavazi yake ya kikahaba alikuwa anayavaa usiku tu tena katika eneo la shughuli zake, nje ya hapo huwezi kumkuta, ilikuwa huwezi kumwona hadharani ovyo ovyo eti anazunguka na uwazi wake barabarani, haikuwahi kutokea hivyo wakati wowote. lakini angalia sasa, makahaba wanashindwa kujiuzia kufanya mambo yao, wanakosa ule uwezo wa kutawala tamaa zao, ile hofu ya watu kuwaona na kuwachukulia hivi au vile haipo tena ndani yao, wapo tayari kupiga picha za uchi, na kutengeneza video za zisizofaa ambazo hazistahili kabisa kuwepo, na kwa ujasiri kabisa wana zi-post katika mitandao, ili watu wote wawaone, na kibaya zaidi wanaofanya hivyo wengi wao ni watu wanaojulikana, ili kusudi kwamba uchafu wao uweze kuwafikia watu wengi zaidi kwa muda mfupi, hizi ndizo ishara madhubuti za siku za mwisho.

Sio kana kwamba hayo mambo yalikuwa hayafanyiki zamani, hapana yalifanyika kwani biblia inatuambia hakuna jambo jipya chini ya mbingu, lakini kwanini unaona kama siku hizi maovu yameongezeka zaidi ya zamani,? Jibu ni kwamba hayajaongezeka kwa kiwango kile unachofikiri bali kinachoendelea sasa ni kwamba wafanyao maovu wa sasa wamepoteza kile kitu kinachoitwa kujizuia ndani yao..Roho ya kutokujali lolote imewavaa, roho ya “fuata mambo yako”, roho ya “ishi maisha yako”..roho ya “kutokujali” ndio inayotawala maisha yao. Na ndio maana hushangai hata kuona watu wa karne hizi watu waki-tengeneza video wanazini na wanyama n.k..Si ajabu tena kwao, kudhihirisha aibu zao wazi. Inasikitisha sana!

Kutukana hadharani hakukuwepo zamani, lakini sasa viwango vya matusi vimekithiri, mabarabarani, kwenye nyimbo za kidunia, kwenye mitandao, si watu wazima si watoto wadogo, maneno yanayozungumzwa huwezi kuamini kama marika kama hayo yanaweza kutoa maneno magumu kama hayo katika vinywa vyao.

Mashoga na wasagaji, wanajitangaza hadharani, hawajali tena hata vyombo vya dola na huku wanajua kabisa kwamba Sheria za nchi haziruhusu vitendo hivyo na kwamba mtu anayefanya hivyo adhabu yake ni kali, wao hilo wanaliona kabisa hawalijali sembuse Mungu wasiyemwona?. KUTOJIZUIA.

Washirikina waendao kutafuta mali kwa waganga wa kienyeji, zamani walikuwa hawadhubutu kuiathiri jamii hadharani kama wafanyavyo sasa hivi, lakini angalia leo, mtu anafikia hatua hata ya kwenda kukata viungo vya watu wasio na hatia (ma-albino, na mtatiti ya mabinti wadogo) kwa tamaa tu za mali.

Kutokujizui, Biblia inasema pia hapo juu siku za mwisho watatokea watu WAKALI, Wasiopenda mema, ile dhambi inapata nguvu mpaka sasa hawezi kutulia ndani, inajidhihirisha nje bila kujali kitu chochote wala mtu yoyote..

Dalili nyingine inayozungumziwa hapo juu ni “KUSINGIZIA”..Tafsiri halisi iliyotumika hapo, kusingizia maana yake, ni “kumzunguzia mwingine vibaya”, au “kumsengenya mtu” kwa lugha nyepesi iliyozoelewa sasa Ni ‘’Umbea”. Kusengenya ni KIU mtu anakuwa nayo ya kutaka kupakua habari za maisha ya mtu mwingine kwa nia ya udadisi ili kupata huko mambo ya kumzungumzia yasiyopendeza mbele za Mungu..

Haya mambo zamani yalikuwepo lakini sio kwa kiwango cha uwazi kilichopo sasa, utakuta mtu anashindwa kujizuia kabisa, Anashindwa kufanya mambo yake mwenyewe, anashindwa kuwazungumzia watu kwa wema, anajikuta kutwa kuchwa ni kudadisi maisha ya watu wengine kwa ubaya. Sasa ukiona wimbi la watu wa namna hii linaongezeka basi fahamu kuwa tunaishi katika majira ya mwisho wa Dunia.

Ndugu yangu. Kama vile hilo andiko linavyosema “siku za mwisho kutakuwako na nyakati za HATARI ”. Fahamu kuwa nyakati zenyewe ndio hizi tunazoishi..Ikiwa utashindwa kujizuia mwenyewe na kuona kila kitu kufanya ni SAWA TU!…Zamani ulikuwa unaona aibu kuvaa vimini na kutembea navyo barabarani lakini sasa unaona hakuna shida yoyote! Ujue kuwa upo katika hatari kubwa sana..roho ya kutokujali imekuingia.

Ukiona zamani ulikuwa ukitukana unajisikia vibaya lakini sasa matusi yamekuwa ni sehemu ya maisha yako. Ujue kuwa ile roho ya kutokujali imekuvaa..Kama vile wale watu wa sodoma na gomora, jinsi walivyokuwa na tabia ya kutokujizuia hata kufikia hatua ya kutaka kulala na wageni wale (malaika wa Mungu) waliokuja yamkini kusitiri uovu wao,lakini wao wakashindwa kujizuia. Jambo gani lilitokea muda mfupi baada ya pale?. Kwanza kabla hata maangamizi hayajawafikia walipigwa upofu. Na upofu ule ni wa daima..Vivyo hivyo na kwa watu wasiojizuia sasa, Upofu unakuja, na upofu huo ni wa daima, ukishamkuta tu mtu, basi huyo mtu hata afanyeje ni wa kuangamizwa tu! hawezi kutubu tena, neema inakuwa haipo tena juu yake, hata ahubiriweje injili.

Zamani ulikuwa unajisikia vibaya kula rushwa, na kufanya utapeli lakini sasa yote yamekuwa sawa kwako, zamani uliogopa hata kusogelea msonge wa waganga wa kienyeji lakini siku hizi pamekuwa kama nyumbani kwako, namba za waganga na watabiri wa nyota zimejaa kwenye simu yako ya mkononi. Upo katika hatari kubwa sana.

Hujizuii mwili wako, unatembea nusu-uchi barabarani na ku-post picha chafu mitandaoni, humwogopi tena Mungu kama hapo zamani, unakuwa ni sababu ya watu wengi kumkosea Mungu, kwa kutazama vitu unavyovipost na mavazi unayoyavaa..Dada upo katika HATARI kubwa sana. Hukumu yako haitakuwa sawa na wale wengine..siku ile fahamu tu utapigwa sana, kama usipotubu, kwasababu uliijua kweli na bado ukaendelea kufanya kwa makusudi. Kuzimu ipo ni kitu halisi kabisa, mtu yeyote asikudanganye kuwa hakuna kuzimu, ipo kabisa.

Tukiyajua hayo, basi ni wajibu wetu kumrudia muumba wetu, kabla ya huu uharibifu mkubwa ambao utaikumba dunia nzima haujatukuta sisi.. Tubu dhambi zako sasa, ukabatizwe upate ondoleo la dhambi zako.

Mwenye sikio asikie Neno hili, ambalo Roho wa Mungu anatuonya watu wa kizazi hiki. Kwamba tujihadhari nacho.

Ubarikiwe.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

Print this post