Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, Mkuu wa Uzima libarikiwe…Karibu tujifunze Neno la Mungu, na leo kwa Neema zake tutajifunza Maana ya kumheshimu Mungu ni ipi?, Tukijifunza kupitia maandiko matakatifu.
Maana ya kumpa mtu heshima…haina tofauti sana na “kumpandisha mtu hadhi”, Biblia inaposema “waheshimu Baba yako na Mama yako” haina tofauti sana na kusema fanya jambo lolote ambalo likawaletea wazazi wako heshima mbele za Mungu na mbele za jamii inayowazunguka…Kwa kufanya hivyo ni sawa na umewaheshimu wazazi wako.
Kwamfano mtoto anapokuwa ni msafi wa tabia na mwenendo, anasalimia wakubwa, mpole, mtulivu, msikivu, mwelekevu na watu wote wa nje wakamwona..jambo la kwanza watu watakwenda kuwatazama wazazi wake na kuwasifia wazazi kwamba wanajua kumlea mtoto katika maadili, hivyo wazazi wa yule mtoto wanapata heshima kwa kupitia mwanao.Kwahiyo hapo huyo mtoto tayari katimiza amri ya Mungu ya kuwaheshimu mzazi wake, hata kama wazazi wake nyumbani hawajamfundisha hayo maadili.
kadhalika kijana wa kike, anapovaa mavazi ya nusu uchi na anatembea mtaani au barabarani, hata kama kapewa ruhusu ya kuvaa hayo mavazi na wazazi wake mwenyewe lakini bado mbele za Mungu na wanadamu HAJAWAHESHIMU MZAZI WAKE..Ni kwasababu gani?..Ni kwasababu Kwa mavazi yale anasababisha kuwadhalilisha wazazi wake na ndugu zake mbele za watu walio nje na mbele za Mungu. Na hili ndio tatizo kubwa kwa vijana wengi wa kike wanadhani kwasababu tu wazazi wao wanavaa nguo fupi na zaidi ya yote wanapewa ruhusa na wao kuvaa nguo fupi kama za wazazi wao, basi wanadhani mbele za Mungu tayari wanawaheshimu wazazi wao.
Wanaona wazazi wao wanakunywa pombe, na pengine hata wazazi wao wanawaacha na wenyewe wanywe pombe, wanadhani kuwa ndio wanawaheshimu wazazi wao.
Binti usijidanganye kumheshimu mzazi wako sio kumtii tu! bali ni kumpa hadhi kama mzazi, hata kama mzazi wako anakuruhusu au anakuhimiza uvae nguo za nusu uchi, au vimini, au suruali wewe kataa..mwambie Mama/Baba sitaki kukuvunjia heshima kwa kuvaa hizo nguo,.
Na pia kwa kijana wa kiume hata kama mzazi wako anatoboa masikio, au anakuruhusu nawe utoboe masikio, au anafuga rasta au anakunywa pombe hivyo anataka na wewe uwe mlevi kama yeye…wewe usikubali kwani kinyume chake kwa kukataa kwako ndiko utakuwa umemheshimu…ukitii kwa kukubali kuwa mlevi kama yeye, utakuwa hujamheshimu, hivyo kama maandiko yanavyosema “wote wasiowaheshimu wazazi wao watakuwa na siku chache za kuishi duniani”..Na wewe utakuwa ni mmoja wao..Lakini endapo ukakataa na watu wakikuona wewe sio mlevi kama baba yako, hata kama watamdharau baba yako kwa ulevi wake lakini pia kwa sehemu fulani watampa heshima baba yako kwa kulea mtoto mwenye adabu mbele za watu.
Na hivyo wewe kijana utakuwa umempandisha hadhi mzazi wako(umempa heshima yake).N.k Na mambo mengine yote ambayo unaweza kufanya yakampandisha hadhi mzazi wako mbele za Mungu na mbele za wanadamu, ukiyafanya hayo ndio utakuwa umemheshimu mzazi wako na kwa Mungu wa Mbingu na nchi.
pia ni hivyo hivyo, hatumheshimu Mungu wetu kwa KUMPA SHIKAMOO hapana! Mungu haheshimiwi hivyo, Yapo mambo matatu tunayoweza kufanya yakampa Mungu HESHIMA kubwa sana, nayo ni 1) IMANI… 2)UTAKATIFU…….3)MWONEKANO
Hayo mambo matatu ndio yatakayomfanya Mungu apate heshima kutoka kwetu., Lakini leo hatutazungumzia hayo mawili ya kwanza, bali tutazungumzia hilo moja la mwisho, ambalo ni MWONEKANO, tutaliangalia ni kwa namna gani litampa Mungu heshima.
Mavazi yamekuwa ni tatizo kubwa sana, kwa watu wanaojiita ni watu wa Mungu, hasa hasa kwa wanawake..Utakuta mwanamke hata kwenye Ibada anakwenda na suruali, au kimini, au anakwenda kajipaka uso rangi na mdomoni kaweka kila rangi. Na anaujasiri wote wa kukaa kiti cha mbele kabisa na anapaza sauti yake kwa nguvu akiabudu na kusifu, na ni kila siku anafanya hivyo.
Binti unayesoma haya, nakwambia kwasababu pengine uliambiwa lakini hukuelewa au ulipuuzia…Kwa mwonekano huo HUMWESHIMU MUNGU HATA KIDOGO. Kama tu ni aibu kutembea na Baba yako mzazi njiani ukiwa umevaa hizo nguo, si zaidi KUSIMAMA MBELE YA MUNGU WA MBINGU NA NCHI ukiwa na hizo nguo?..Hebu chukua muda kutafakari hili jambo, usilichukulie kiwepesi tu! Usidhani pale unapokwenda kuabudu hakuna macho ya Mungu, yapo na anaangalia kama tunavyoangalia sisi wanadamu, kwasababu Mungu huyo huyo aliyeuimba roho ndio huyo huyo aliyoumba mwili. Kwahiyo acha kusikiliza Ubeti wa shetani uliotungiwa kuzimu kwamba MUNGU ANAANGALIA ROHO HAANGALII MWILI.
Hebu tujifunze kwenye maandiko kidogo watu waliomheshimu Mungu kwa mwonekano wao.
Yohana 21 : 1-25
“1 Baada ya hayo Yesu alijidhihirisha tena kwa wanafunzi wake, penye bahari ya Tiberia, naye alijidhihirisha hivi.
2 Simoni Petro, na Tomaso aitwaye Pacha, na Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, na wana wa Zebedayo, na wengine wawili wa wanafunzi wake, walikuwapo pamoja.
3 Simoni Petro aliwaambia, Naenda kuvua samaki. Nao wakamwambia, Sisi nasi tutakwenda nawe. Basi wakaondoka, wakapanda chomboni; ila usiku ule hawakupata kitu.
4 Hata asubuhi kulipokucha, Yesu alisimama ufuoni; walakini wanafunzi hawakujua ya kuwa ni Yesu.
5 Basi Yesu akawaambia, Wanangu, mna kitoweo? Wakamjibu, La.
6 Akawaambia, Litupeni jarife upande wa kuume wa chombo, nanyi mtapata. Basi wakatupa; wala sasa hawakuweza kulivuta tena kwa sababu ya wingi wa samaki.
7 Basi yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda akamwambia Petro, Ndiye Bwana. Naye Simoni Petro, aliposikia ya kwamba ni Bwana, akajifunga vazi lake, (maana alikuwa uchi), akajitupa baharini.
8 Na hao wanafunzi wengine wakaja katika mashua; maana hawakuwa mbali na nchi kavu; ila yapata dhiraa mia mbili; huku wakilikokota lile jarife lenye samaki.
9 Basi waliposhuka pwani, wakaona huko moto wa makaa, na juu yake pametiwa samaki, na mkate”.
Ukisoma habari hiyo kwa makini utaona kwamba Petro alikuwa anavua na wenzake akiwa uchi (sasa uchi unaozungumziwa hapo sio uchi kabisa wa kukosa nguo zote, hapana bali ni uchi ambao mtu anakuwa amebakiwa tu na nguo ya ndani). Kutokana na desturi za uvuvi, wavuvi wengi wanapunguza nguo zao wakati wa kuvua ili wawe wepesi wa kuogelea na wanakuwa vile kwasababu wanakuwa wanaenda mbali na makazi ya watu, kwahiyo kwa mwonekano wao hawawezi kuiharibu jamii..
Kwahiyo hapa Petro alikuwa yupo na nguo ya ndani tu, gafla akatokea Bwana ufukweni na hawakumtambua lakini walipomtambua tu! PETRO ALIVAA VAZI LAKE HARAKA NA KISHA AKAJITUPA BAHARINI!.
Hebu tafakari hilo tukio!! Petro huyo ni mwanaume, na akatokea Yesu ambaye pia ni mwanaume kama yeye lakini Petro kwa kumheshimu Bwana akavaa haraka vazi lake, na hata baada ya kuvaa akaona haitoshi, ili kujisitiri zaidi akajitupa kwenye maji. Kwasababu anajua aliyesimama mbele yake ni nani?…alijua kabisa ni zaidi ya mwanadamu ni Mungu, na hivyo mbele zake anapaswa ajisitiri.
Kwa tukio hilo unaweza ukaona kabisa kamwe wanafunzi wa Yesu walikuwa hawajiachii mbele zake, ikiwa na maana kuwa walikuwa wanajisitiri mbele zake kila wakati, walikuwa hata hawadhubutu kubaki kifua wazi mbele zake ingawa wote walikuwa ni wanaume kama yeye.
Sasa kama hawa wanafunzi wa Bwana Yesu walio wanaume walikuwa wanajisitiri hivyo mbele za Bwana, unadhani wale wanawake waliokuwa wanamfuata walikuwaje mbele zake??..unadhani wakina Mariamu Magdalena walikuwa wanavaaje mbele zake, unadhani wangeweza hata kuonyesha vifua vyao mbele yake? walikuwa wanajisitiri kuliko kawaida, pengine hata walikuwa wanaficha wakati mwingine hata nyuso zao mbele zake.
Lakini leo hii unamwambia binti wa Mungu, kwa kumhurumia na kwa upendo, jisitiri unapoingia mbele za Mungu, na sio tu mbele za Mungu bali kila mahali, uendako unamwonyesha na maandiko kuhusiana na yeye kujisitiri (1Timthotheo 2:9)…anakuambia Mungu haangalii mavazi anaangalia roho, Injili ambayo haijulikani ilitoka wapi.
Mwanaume hawezi kwenda kwenye ibada na kaptura, au malapa lazima kuna kitu ndani yake kitamhukumu, na ukiona kaenda na malapa basi ni kweli huyo mtu hana viatu au anamajeraha..Lakini mwanamke ataingia kapaka wanja, lipstick, kapaka uso rangi, kapuliza pafyumu mita 5 mbele watu wanasikia, mgongo wote uko wazi, kavaa sketi fupi ambayo ni aibu kuelezea mfano wake, na ndani hakuna kitu kinamchoma!! Lazima kuna tatizo ndani ya huyo mtu.
1 Samweli 2: 30 “Kwa sababu hiyo, Bwana, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; LAKINI SASA BWANA ASEMA, JAMBO HILI NA LIWE MBALI NAMI; KWA MAANA WAO WANAONIHESHIMU NITAWAHESHIMU, NA WAO WANAONIDHARAU WATAHESABIWA KUWA SI KITU”.
Mwanamke unapokwenda kwenye ibada na mwonekano usio wa heshima, jua unakwenda kukutana na Bwana Yesu mwenyewe, unamshushia Yesu Kristo heshima yake, na hivyo na yeye hawezi kukuheshimu ndivyo Neno lake linavyosema, Watu wasio wakristo wanasema dini yenu ni ya namna gani? watu wanamwabudu Mungu uchi. Jina la Mungu linatukanwa kwa ajili yako. Utajikuta unakwenda kujitafutia laana badala ya Baraka..Hata kama hilo kanisa unalokwenda mchungaji wake anawaruhusu wanawake kuvaa hivyo au haongei chochote…wewe usiende kujitafutia laana mbele za Mungu, vaa kwa kujisitiri, vaa nguo za heshima jisitiri mbele za Mfalme Mkuu Yesu Kristo, na mbele za wanadamu Kama Petro aliyeteuliwa na Bwana alijisitiri mbele zake, na alikuwa ni mwanamume alifanya hivyo wewe mwanamke ni nani usifanye hivyo. Vaa nguo yako ndefu, funika kichwa chako, hata watu wasione kifua chako ndivyo utakavyokuwa UMEMHESHIMU MUNGU, na HIVYO MUNGU ATAKUHESHIMU.
Ni matumaini yangu kuwa Bwana atakupa macho ya kuyaona hayo ewe mwanaume/mwanamke..kwamba utamheshimu Mungu kwa mwonekano wako ili naye akuheshimu.
Mungu akubariki sana.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
Tukiachilia mbali ule waraka wa kwanza ambao Mtume Yohana aliuandika kwa watu wote, zile nyaraka mbili za mwisho zilizosalia hakuzielekezwa kwa watu wote, bali kwa watu husika, na tunaona ndio zimekuwa nyaraka fupi kuliko zote katika biblia nzima, lakini zimebeba ujumbe wa msingi sana, kwa makundi ya watu waliozungumziwa huko..Kwa mfano kama tukiutazama ule waraka wa tatu, tunasoma mtume Yohana aliuelekeza kwa ndugu mmoja anayeitwa GAYO.
Sasa wengi wanaupenda mstari mmoja maarufu sana unaotoka katika kitabu kile unaosema..”MPENZI NAOMBA UFANIKIWE KATIKA MAMBO YOTE NA KUWA NA AFYA YAKO, KAMA VILE ROHO YAKO IFANIKIWAVYO.(3YOHANA 1:2)”..Ni mstari unaopendwa na kila mmoja kwasababu ni mstari unatoa Baraka na mafanikio..Lakini tunashindwa kuelewa kuwa waraka ule haukuandikwa kwa watu wote bali kwa mtu anayeitwa GAYO peke yake ndio aliyeambiwa maneno yale ya baraka, na ni lazima ujue ni kwanini Baraka zile alizistahili yeye na si mwingine kutoka kwa Mungu, na kwa kujifunza kupitia yeye na sisi ndio tunaweza kustahili kupata Baraka kama zile, kwa ufupi kama ukisoma pale utagundua kuwa mtu huyu alikuwa na moyo wa kipekee sana, aliwakaribisha wageni waliokuwa wanasafiri kwa ajili ya kazi ya Mungu, alijitoa kwa ajili ya Bwana kweli kweli, aliwahudumia watumishi wa Mungu waliokwenda kuhubiri nchi za ugenini, kwa hali na mali kiasi cha kwamba hata watumishi hao waliosafirishwa na yeye wakawa hawana mahitaji yoyote kutoka kwa watu wasioamini, Hivyo sifa zake zikavuma katikati ya makanisa yote mpaka kuwafikia mitume..Na ndipo ukija kusoma utaona maneno hayo ya Baraka yanatamkwa mbele yake..
Sasa leo utamwona mtu ni mkristo lakini hata kutoa kitu kidogo kwa Mungu wake anaona shida, na huyo huyo bado ndio wa kwanza kumwambia Mungu, ulisema nifanikiwe katika mambo yote..Hajui kuwa ili Mungu akubariki kwa Baraka kama hizo kuu na nono sio hivi hivi tu..BALI KWA WATU WENYE TABIA KAMA ZA GAYO. Watu ambao hawapo tayari kuona kazi ya Mungu haikwamishwi na kitu chochote.
Vile vile na leo tutaona kwa ufupi juu ya ujumbe ulio katika huu Waraka wa PILI wa Yohana, je! Unamhuhusu nani?. Ni vema ukapata muda wa kuusoma wote peke yako. kwanza ni mfupi na pia itakusaidia tuende pamoja katika uchambuzi huu tunaokwenda kuuangalia..
Tunasoma…
3Yohana 1:1 “Mzee, kwa MAMA MTEULE, na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na wote waijuao ile kweli;
Awali ya yote tunaona Hapa mtume Yohana anajitambulisha kama MZEE, na sio kama mtume, au mtumwa wa Kristo, kufikisha ujumbe kama mkomavu, mtu aliyekula chumvi nyingi, anafahamu mambo mengi yahusuyo kanisa na shamba la Mungu kwa ujumla, anayejua jinsi ya kupambanua mitego ya Yule mwovu aliyowahi kuiona katika maisha yake ya kikristo, na jinsi mitego hiyo inavyoweza kunasa makundi mbali mbali ya watu na namna yake, “kijana kwa wazee”, watoto kwa wakubwa, waume kwa wake, n.k.
Hivyo hapa waraka huu tunaona moja kwa moja anaulekeza kwa MAMA MTEULE..Na sio mama tu wa kawaida, Bali anasema mama MTEULE tena pamoja na watoto wake..Hivyo ni wazi kuwa ujumbe huu unawahusu WANAWAKE WOTE, WALE WALIO WATEULE WA KRISTO, ambao wameshaokolewa, ambao walishaoshwa dhambi zao kwa damu ya Yesu Kristo, ambao neema ya Mungu tayari ipo juu yao siku zote, ambao ni watakatifu tena wenye watoto,.
Sasa yapo mambo 3 makuu yalipaswa yazingatiwe au yaonekane katikati wanawake watuelu wa Mungu wa namna hiyo..Na ndio hayo tutayatazama leo katika vipengele vyake. Jambo la kwanza ni..
1) KUWAONGOZA WATOTO KATIKA KWELI:
Kama ukisoma hapo utaona mzee huyu alianza kwanza kwa kuchunguza hali ya watoto wa mama Yule mkristo, katika nyumba yake, na kutamani sana kuona jinsi alivyoweza kuwajali watoto wake au watu wa nyumbani kwake kwa kuhakikisha kuwa wanamcha Mungu, wanadumu katika utakatifu, alitamani kumwona mama huyu jinsi ambavyo angejitoa katika kuangalia hali ya kiroho ya watoto wake kuliko kitu kingine chochote wakifanyacho.. na kama tunavyosoma ni kweli mwanamke huyu mteule alikuwa nacho Tunasoma.
1:1 “Mzee, kwa mama mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na wote waijuao ile kweli;
2 kwa ajili ya hiyo kweli ikaayo ndani yetu, nayo itakuwa pamoja nasi hata milele.
3 Neema, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo Mwana wa Baba, zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.
4 Nalifurahi mno kwa kuwa nimewaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba”.
Unaona hapo mstari wa 4 anasema.
“4 Nalifurahi mno kwa kuwa nimewaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba.”
Hivyo ikiwa wewe ni mama, na unataka kuitwa MTEULE wa Kristo, Swali ni je!.unahakikisha watoto wako wanaenenda katika misingi ya kumjua Mungu?, Unawakemea wanapotenda dhambi au unawaangalia tu, je! Unafuatia hali zao za kiroho, au kila wakati upo buzy kufuatilia tu mahudhurio yao ya shuleni na huku mahusiano yao na Mungu yanadorora kila siku. Watoto wako mstari mingapi ya biblia wanaifahamu mpaka sasa, lakini nyimbo za kidunia kila siku unawasikia wakiimba lakini huwasemeshi? Na bado unajiita MAMA MTEULE wa Kristo unayempenda Mungu….Huo sio uteule mama, siku ile hautakuwepo katikati ya wanawake wateule wa Kristo kama wakina SARA na HANA, na wengineo ikiwa utawaona watoto wako wanapotea na wewe huwasemeshi kitu, ikiwa utawaona hawamjui Mungu na wewe hutaki kuwafundisha, unawanunulia kila siku vitabu vipya vya shuleni lakini biblia huwanunulii, unawalipia tution kila siku lakini fellowship na bible study huwapeleki…Huo sio uteule mama…Hali kadhalika na wewe ambaye bado hujawa na watoto, je! Hayo malengo yapo kwenye kichwa chako?
2) KUWA NA UPENDO:
Jambo la pili Mzee huyu alilotamani kuliona katikati ya mwanamke huyu mteule wa Kristo ni UPENDO.
Tunasoma.
“5 Na sasa mama, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane.
6 Na huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. Hii ndiyo ile amri, kama mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo”.
Unaona hapo? Anasema Hii ndiyo ile amri, kama mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo. Sasa Amri hiyo aliyokuwepo tangu mwanzo ni ipi?
Marko 12:29 “Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;
30 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.
31 Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.”
Umeona hizo mbili zote alitazamia kuziona kwa mwanamke huyu, ahakikishe kuwa kumpenda Mungu kupo ndani yake siku zote, juu ya kulea watoto katika kweli lakini pia kumcha Mungu kuwepo ndani yake, awe na amani kuwepo uweponi mwa Bwana, awe mwombaji, au msomaji wa Neno.
Na pia awapende ndugu, kwa furaha kabisa kama vile biblia isemavyo upendo huvumilia, upendo hauhusudu, upendo haujivuni, upendo hauhesabu mabaya,.
Lakini mwanamke anayesema ameokoka, lakini hana habari na Mungu, hataki kujifunza maneno ya Mungu, hata kusali kwake ni shida, huruma hana, ni msengenyaji wakati wote, hana uvumilivu ndani yake, akiudhiwa kidogo tu, yeye naye anaanza kusengenya. Na suala hili limekuwa hafifu kwa wanawake wengi, na hivyo kimekuwa kikwazo kikubwa sana cha UTEULE WAO pasipo wao kujijua, Hivyo kama wewe ni mwanamke na unajiita mteule fanyia kazi hilo kwa bidii, shindana na usengenyaji huo mpaka uushinde.
3) KUJILINDA NA WADANGANYIFU.
Hili ndio jambo la tatu na la mwisho mzee huyu mwenye hekima alimwomba mama huyu mteule alizingatie. Hapa anaendelea kusema..
“7 KWA MAANA WADANGANYIFU WENGI WAMETOKEA DUNIANI, wasiokiri ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo.
8 Jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda, BALI MPOKEE THAWABU TIMILIFU.
9 Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu. Yeyeadumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba na Mwana pia.
10 Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu.
11 Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu”.
Tazama hapo anasema “KWA MAANA WADANGANYIFU WENGI WAMETOKEA DUNIANI”,…Sasa kumbuka kama wadanganyifu hawa walitokea wakati ule, watatokea na sasa, na pia zingatia jambo hili ili usichanganyikiwe roho ya mpinga-kristo ni ile ile, lakini utendaji wake kazi unabadilika kulingana na nyakati na majira. Wadanganyifu waliokuwepo wakati ule wa mitume walikuwa na kazi moja tu, yaani Kumkana Kristo kuwa hakufufuka..Kwasababu habari ya ukristo ndio kwanza zilikuwa zinaanza kuhubiriwa, Hivyo shetani ili kuuuwa ukristo usiaminiwe na wengi kwa wakati ule, alitumia udanganyifu wa kuwa Kristo hajafufuka, na pia hawezi kurudi katika mwili..Hao ndio walioitwa wapinga-kristo wa wakati ule, na ndio hao Mzee huyu alikuwa anamwonya mama huyu MTEULE ajitenge nao pamoja na mafundisho yao…Kwasababu kwa uzoefu wake wa rohoni Mungu aliompa aliona kuwa wanawake wengi wateule ndio wanaokuwa rahisi kuchuliwa na wimbi hili na wapinga-kristo zaidi ya wanaume wateule,.(sisemi kuwa wanaume hawadanganyiki), hapana bali wengi ni wanawake.
Lakini roho ile ile ya udanganyifu, inatenda kazi hata sasa isipokuwa kwa namna ya ujanja mkubwa zaidi, mpaka kufikia hatua Bwana Yesu kusema wakati huo watawadanganya yamkini hata walio WATEULE…Hivyo roho hii ya udanganyifu haiji tena kwa kusema Yesu hakufufuka, au haikuambii Yesu hatarudi, kwani mpaka sasa shetani anafahamu kuwa hakuna mkristo asiyejua kuwa Kristo alifufuka, na Yesu siku moja atarudi..kila mtu analijua hilo, lakini badala yake anakuja na udanganyifu mwingine nao ndio huu “Kushusha thamani ya wokovu na injili ya YESU KRISTO.”
Kuwafanya watu wasichukulie tena kwa uzito na umakini habari za wokovu, watu wajue kuwa ni kweli Yesu anaokoa lakini maisha yao yasiathiriwe na wokovu huo, anahakikisha kuwa mtu anakuwa vuguvugu, nusu kwa Mungu nusu kwa dunia, injili ya kisasa, injili ya I don’t care, injili ya “haijalishi!”..injili ya kutabiriwa tu mafanikio basi, lakini mambo ya toba yasigusiwe kabisa..Na hali hiyo inawalewesha hata wale ambao walikuwa wamesimama waanze kuwa vuguvugu.
Na roho hii inawakamata sana sana wakina mama, tena hata wale wateule, na ndio maana hapo Mtume Yohana anamwambia. “9 Kila apitaye cheo, wala asidumu katika MAFUNDISHO YA KRISTO, yeye hana Mungu”.
Umeona, njia pekee ya kuwatumbua hao ni kudumu katika mafundisho ya Kristo (Yaani Neno la Mungu)…
Webrania 12: 14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
Hivyo ikiwa wewe ni mwanamke mteule unayetaka kupokea THAWABU TIMILIFU kama huyu mama, hakikisha unaufanya imara uteule wako kama maandiko yanavyosema, kwa kuzingatia hayo mambo matatu kuwa yapo ndani yako.
2 Petro 10 “Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na UTEULE WENU; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe”.
Mungu akubariki. Tafadhali “Share” ujumbe huu kwa wengine. Na Bwana atakubariki zaidi.
Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA TATU WA YOHANA.
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU
Ni nani aliyeidharau siku ya mambo madogo?…Ni swali Bwana alilouliza.
Jina la Bwana Yesu Kristo, libarikiwe, karibu katika kujifunza Neno la Mungu, Leo kwa Neema za Mungu, tutajifunza namna ya kusimama imara siku ya mambo madogo?.
Najua unajiuliza SIKU YA MAMBO MADOGO NDIO NINI?...Lakini kabla ya kufikia huko kuelezea siku ya mambo madogo, hebu tujikumbushe kidogo historia fupi ya Taifa la Israeli, ambapo kwa kupitia hiyo tutaelewa kwa undani nini maana ya “siku ya mambo madogo”.
Kama wengi wetu tunavyojua Mungu aliwatoa wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri, na kuwaingiza katika nchi ya ahadi, ambapo ndani ya nchi ile aliwaahidia kula mema yote endapo wataishi kwa kuzishika amri zake, na kama ni msomaji mzuri wa biblia utagundua kuwa vipo vizazi vilivyofanya vizuri kwa kwenda katika sheria za Mungu, ambavyo viliishi kwa raha na kwa amani, na vipo pia vizazi vya wana wa Israeli ambavyo havikufanya vizuri, vilikengeuka na kuacha kuyashika maagizo ya Mungu waliyopewa na badala yake vikapitia vipindi vya tabu sana.
Na utaona pia baada tu ya Israeli kugawanyika na kuwa sehemu mbili yaani YUDA NA ISRAELI …ndio kipindi ambacho wana wa Israeli walipozidi kukengengeuka kwa viwango vya hali ya juu. Kuanzia kipindi cha Mfalme Yeroboamu mpaka kipindi cha mfalme Hosea wa Israeli kulikuwa hakuna unafuu kabisa, watu waliabudu mabaali na sanamu wazi wazi na kuvukiza uvumba katika sehemu za juu. Na kwasababu ya maasi kuwa mengi, Bwana alituma idadi kubwa sana ya manabii wake katika kipindi hichi kuliko vipindi vyote vilivyotangulia ili kuwaonya wana wa Israeli wageuke na kuacha njia zao mbovu, hivyo kuanzia huo wakati manabii wengi sana walitokea kama wakina Eliya, Elisha, Nathani, Yona, Habakuki,Sefania, Hosea, Mika, Yeremia,Isaya, Obadia, Amosi,Nahumu,Ezekieli,Yoeli,Mika, Zekaria n.k Wote hawa walitokea ndani ya kipindi cha wafalme wa Israeli..Lakini hawakusikia, kinyume chake waliwaua wengine na kuwapiga kwa mawe.
Hivyo maovu yalipozidi hata kufikia kikombe cha ghadhabu ya Mungu kujaa, kukawa hakuna tena kusamehe, Mungu akaahidi kuwa watakwenda utumwani, na Miji yao yote itachomwa moto, na watu wengi sana watauawa kwa upanga, na wengine watakufa kwa njaa, na wengine kwa Tauni. Na lile hekalu ambalo mfalme Sulemani alilitengeneza kwa gharama nyingi litavunjwa na kuteketezwa kabisa..Na kweli wakati ulipowadia Neno la Bwana lilitimia, Israeli ilichukuliwa utumwani Ashuru na wale waliosalia wa Yusa ,Wakaldayo(yaani watu wa Babeli)..walifika Yerusalemu wakauteketeza mji wao kwa moto, wakalivunja lile hekalu kama Ilivyotabiriwa wakawaua watu wengi kwa upanga; wanawake, kwa watoto na wachache waliobakia waliwachukua utumwani kwenda nao Babeli. Israeli Mji ambao ulipata sifa na kuogopeka na mataifa yote ulimwenguni ukageuka kuwa kama jalala.
Lakini Mungu ni wa rehema aliwaahidi kuwa hawatakaa huko utumwani milele, bali watakaa huko wakimtumikia Mfalme wa Babeli kwa miaka 70 tu! na baada ya hiyo miaka 70 kuisha watarejeshwa tena kwao.
Sasa ndio tunaelekea kwenye kiini cha somo letu, baada tu ya wana wa Israeli kutimiza ile miaka 70, wakiwa Babeli Mungu aliwafungulia mlango wa kurudi tena nchini mwao, lakini waliporudi kule walikuta tayari kuna watu wengine ambao walikuwa wanakaa pale, ambao sio waisraeli, ambao mfalme wa Uajemi aliwaweka wakae kule…Lakini Hao watu walipoona wana wa Israeli wamerudi tena nchini mwao wakaanza kuwapiga vita.
Wakati wana wa Israeli wanapanga kumjengea tena Mungu Hekalu lingine jipya baada ya lile la kwanza kuharibiwa na Mfalme wa Babeli miaka 70 iliyopita, wanakutana tena na changamoto nyingine ya kusumbuliwa…hivyo kwasababu ya hao watu iliwafanya waishiwe nguvu kabisa ya kuijenga tena nyumba ya Mungu, kwasababu pia kwa idadi yao waliorudi Israeli walikuwa ni wachache sana.
Lakini ulipofika wakati Mungu aliwanyanyua manabii wake wawili HAGAI na ZEKARIA kuwatabiria wana wa Israeli kwamba wasimame imara waijenge nyumba ya Mungu wasiogope changamoto zilizopo mbele yao, ijapokuwa hawana fedha wala utajiri lakini Bwana atakuwa nao katika UDOGO WAO. Bwana akamwambia Hagai maneno haya awaambie wana wa Israeli.
Hegai 2: 1 “Katika mwezi wa saba, siku ya ishirini na moja ya mwezi, neno la Bwana lilikuja kwa kinywa cha Hagai nabii, kusema,
2 Sema sasa na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, liwali wa Yuda, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na hayo mabaki ya watu, ukisema,
3 Miongoni mwenu amebaki nani aliyeiona nyumba hii katika utukufu wake wa kwanza? Nanyi mnaionaje sasa? Je! Mbele ya macho yenu, siyo kama si kitu?
4 Lakini sasa uwe hodari, Ee Zerubabeli, asema Bwana; nawe uwe hodari, Ee Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, nanyi iweni hodari, enyi watu wote wa nchi hii, asema Bwana; MKAFANYE KAZI, kwa kuwa mimi ni pamoja nanyi, asema Bwana wa majeshi;
5 KAMA NENO LILE NILILOAGANA NANYI MLIPOTOKA KATIKA NCHI YA MISRI; NA ROHO YANGU INAKAA KATI YENU; MSIOGOPE.
6 Kwa maana Bwana wa majeshi asema hivi, Mara moja tena, ni kitambo kidogo tu, nami nitazitikisa hizo mbingu, na hii nchi, na bahari, na nchi kavu;
7 nami nitatikisa mataifa yote, na vitu vinavyotamaniwa na mataifa yote vitakuja; nami nitaijaza nyumba hii utukufu, asema Bwana wa majeshi.
8 FEDHA NI MALI YANGU, NA DHAHABU NI MALI YANGU, asema Bwana wa majeshi.
9 Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema Bwana wa majeshi; na katika mahali hapa nitawapa amani, asema Bwana wa majeshi”.
Unaona maneno hayo?..Bwana anawatia moyo wana wa Israeli kuwa WASIOGOPE! Utukufu wa hekalu la pili utakuwa mkubwa kuliko utukufu wa lile Hekalu la Kwanza. Hivyo wasonge mbele, wakafanye kazi, wasiangalie umaskini walio nao, wala shida waliyo nayo wasonge mbele kwasababu utukufu wa nyumba ya pili utakuwa ni mkubwa kuliko utukufu wa nyumba ya kwanza, na FEDHA NA DHAHABU NI MALI ya Bwana.. haleluya!! Haleluya!!.
Zaidi ya hayo wakati wana waisraeli wakiongozwa na kiongozi wao aliyeitwa ZERUBABELI wanatazama kuwa kujenga nyumba na uchache wao, na umaskini wao, pamoja na wingi wa maadui uliowazunguka ni jambo lisilowezekana, ni kama mlima mkubwa umewekwa mbele yao halafu uusawazishe kwa beleshi..Lakini jicho la Mungu lilikuwa linaona tofauti..Na ndio Bwana akampa nabii Zekaria maono mengine miezi miwili baada ya yale maono ya Hagai na kusema..
Zekaria 4: 5 “Ndipo malaika aliyesema nami akajibu, akaniambia, Hujui vitu hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu.
6 Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, SI KWA UWEZO, WALA SI KWA NGUVU, BALI NI KWA ROHO YANGU, ASEMA BWANA WA MAJESHI.
7 NANI WEWE, EE MLIMA MKUBWA? MBELE YA ZERUBABELI UTAKUWA NCHI TAMBARARE; NAYE ATALILETA LILE JIWE LA KUWEKWA JUU KABISA PAMOJA NA VIGELEGELE VYA, NEEMA, NEEMA, ILIKALIE.
8 Tena neno la Bwana likanijia, kusema,
9 Mikono yake Zerubabeli imeiweka misingi ya nyumba hii, na mikono yake ndiyo itakayoimaliza; nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwenu
10 MAANA NI NANI ALIYEIDHARAU SIKU YA MAMBO MADOGO? Kwa kuwa watafurahi, nao wataiona timazi katika mkono wa Zerubabeli…..”
Unaona hapo anasema NANI WEWE, EE MLIMA MKUBWA? MBELE YA ZERUBABELI UTAKUWA NCHI TAMBARARE, Mbele ya changamoto zote zinazoonekana kama ni milima, mbele za masihi wa Bwana zitakuwa ni nchi tambarare…na sio kwa uwezo wa Zerubabeli wala kwa nguvu zao bali kwa roho yake Bwana ndio watausawazisha huo mlima.
Na zaidi ya yote Bwana anamwambia Zerubabeli.. “MAANA NI NANI ALIYEIDHARAU SIKU YA MAMBO MADOGO”…
Sasa siku ya mambo madogo ndio ipi?..Ndio hiyo siku ambayo walikuwa hawana chochote, siku ambayo walikuwa wanaona hakuna chochote kinachoweza kufanyika, siku ambayo walikuwa wanaona ndio kwanza mambo bado hata hayajaanza, siku ambazo nguvu zao ni chache, hizo ndio siku za mambo madogo?..Na Bwana anawauliza ni nani anayezidharau siku hizo??…Ni nani anayesema kwamba jambo hilo la kuisimamisha nyumba yenye utukufu mwingi halitafanikiwa?..Ni nani anayesema kuwa katika udhaifu huo hakuna chochote kinachoweza kufanyika?!…sentensi hiyo huwa inamuhuzunisha Mungu sana.
Ndugu somo hili ni la kukutia moyo tu! wewe ambaye upo katika safari ya kwenda mbinguni, kuwa USIIDHARAU SIKU YA MAMBO MADOGO.
Kama ndio kwanza unaanza kumtafuta Mungu, usizidharau siku hizi ambazo unajiona huwezi kuitenda kazi ya Mungu, siku inafika utakayoleta matunda mengi kwa Kristo, endapo hutazimia unachopaswa kufanya ni kuendelea kusonga mbele kwa bidii zote bila kukata tamaa,…Mtaji ulionao moyoni mwako uzalishe, kwasababu ni kama mbegu ndogo, na itakapokuwa itakuletea faida nyingi sana mbeleni. Mwingine aliniambia jana siwezi kumgeukia Mungu kwasasa sina kazi,..ndugu hata ukipata bilioni 100 leo bado utajiona tu hujafika, anza leo na Bwana.
Na pia katika maisha ya kawaida ya kujitafutia riziki, ikiwa wewe ni mkristo na kwanza ndio shughuli uzifanyazo zinaanza kuchipuka, upo kama fukara tu! au una mtaji kidogo, au kazi yako ni ya hadhi ya chini sana, na ukiangalia mbele unaona milima mikubwa, hiyo milima isikuogopeshe, ITAKUWA NCHI TAMBARARE…. Usidharau siku ya mambo madogo nenda kakifanyie kazi hicho kidogo, kakizalishe!! Usimvunjie Mungu heshima kwa kutomwamini endelea kutenda haki katika utakatifu wote kwa sababu fedha na dhahabu ni mali yake, mwisho wa siku atakunyanyua tu! kama alivyomnyanyua Zerubabeli na haitakuwa kwa nguvu zako wala kwa uwezo wako bali kwa ROHO WA MUNGU,…NI NANI WEWE UNAYEIDHARAU SIKU YA MAMBO MADOGO! Mungu mwenyewe haidharau wewe ni nani uidharau na mtu mwingine yoyote yeye ni nani hata aidharau siku ya mambo yako madogo!!..Hata kama unauza mchicha usizidharau hizo siku.
Na mwisho kabisa tunaona baada ya Zerubabeli kupata unabii ule kutoka kwa Bwana, kwa vinywa vya Hagai na Zekaria Manabii wa Bwana, alipata nguvu mpya yeye pamoja na Yoshua na wana wa Israeli wote na kwenda kuijenga nyumba ya Mungu, na baada tu ya kutia nia ya kwenda kuijenga nyumba, wakati huo huo vibali vikaanza kufunguka, mara mfalme anatoa amri wapewe ruhusa ya kujenga pasipo kusumbuliwa, mara mfalme anasema wapewe fedha na wasilipishwe kodi yoyote na fursa nyingi na upendeleo mwingi waliupata kutoka kwa watu na mfalme, nyumba ya Mungu ilipatikana na dhahabu nyingi na fedha nyingi, na ikamalizika chini ya mikono ya Zerubabeli salama sawasawa na unabii Bwana alioutoa.
Hivyo ndugu, Bwana ndiye anayenyanyua na ndiye anayeshusha, kama alikushusha chini wakati mwingine ni kwasababu ya maovu yako (ingawa sio kila kushushwa chini ni kwasababu ya maovu, nyingine ni kwa utukufu wa Mungu kama Ayubu), kama ilivyo tu kufanikiwa, sio mafanikio yanatoka kwa Mungu…lakini kama maisha yako yalikuwa hayampendezi Mungu huko nyuma na akakushusha ni kwasababu anakupenda anataka akupe tumaini tena, kama alivyowashusha wana wa Israeli kukaa Babeli miaka 70, na walipotubu aliwarudisha tena katika nchi yao na kuwapa faraja kubwa kama hiyo, na kuwanyanyua tena! Kwanini na wewe asikufanyie hivyo endapo utatubu kabisa kwa kumaanisha kuziacha dhambi zako na kumgeukia yeye. Na kumbuka USITUBU! Kwasababu tu unataka KUPATA UTAJIRI WA ULIMWENGU HUU, tubu kwasababu unataka kwanza kupata UTAJIRI WA ULIMWENGU UNAOKUJA!…..Huo ukiupata hata huu wa ulimwengu hauhitaji kuuhangaikia, Bwana alisema TUTAZIDISHIWA, kuzidishiwa sio kusumbukia, kitu cha kutafuta ni Ufalme wa Mungu, huo ndio tumeambiwa tuutafute kwa bidii zote …“ Mathayo 6:33..utafute kwanza ufalme wake na haki yake, na hayo mengine mtazidishiwa”.
Hivyo Kama hujampa Bwana maisha yako, huu ndio wakati wako wa kufanya hivyo, kabla mlango wa Neema haujafungwa, Roho wa Mungu anataka utii thabiti kutoka ndani ya moyo wako na sio kulazimishwa, anataka utubu kabisa kwa kudhamiria KUACHA, sio KUPUMZIKA, hapana bali kuacha dhambi, unakusudia kuacha kwa vitendo usengenyaji, uasherati, rushwa, utukanaji, ulevi, uvaaji usio na heshima(vimini na suruali kwa wanawake), unakusudia kuacha anasa zote za ulimwengu, na ukisha tubu hatua inayofuata ni ubatizo sahihi, na ubatizo sahihi ni wa maji Mengi na kwa Jina la Yesu Kristo, kulingana na Matendo 2:38, na kisha baada ya ubatizo Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu atakayekusaidia kushinda dhambi. Na hapo utakuwa umezaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho.
Mungu akubariki sana.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
SHETANI ANATOLEA WAPI FEDHA, ANGALI TUNAJUA FEDHA NA DHAHABU NI MALI YA BWANA?.
Moja ya somo pana sana katika biblia ni somo lihusulo IMANI. Imani ni kama Elimu, kama vile watu wasemavyo Elimu haina mwisho hali kadhalika Elimu ya IMANI nayo haina mwisho.
Watu wawili wanaweza wakasema ni wasomi, wamehitimu pamoja, wamepokea shahada kwa pamoja wakajulikana na serikali kama ni watu wasomi wazuri wenye manufaa makubwa katika nchi lakini unajua kuwa mmoja anaweza akawa ni mjinga kwa mwingine sawasawa tu na mtu Yule ambaye hajakwenda shule kabisa, Unauliza ni kivipi?.
Jaribu kufikiria mmoja alipomaliza elimu ya msingi alikwenda kusomea masomo ya urubani, na yule mwingine akaenda kusomea udaktari..sasa na elimu zao embu jaribu kumchukua Yule daktari umpe ndege aendeshe abiria, au umpeleke Yule rubani kwenye chumba cha upasuaji kwa vichwa vya wanadamu awatibu wagonjwa..wewe Unadhani ni jambo gani hapo litatokea?..Ni maafa makubwa sana..Sasa tukiwahukumu hawa wote kwa kutazama maafa yaliyotokea na kusema kuwa ni wajinga, tutakuwa hatujatathmini uhalisia wa mambo….Ukweli ni kwamba Yule daktari ni msomi lakini ni msomi aliyebobea katika mambo ya udaktari hivyo masuala ya Jeografia kwake ni kama maruweruwe, hali kadhalika na yule Rubani.
Na ndivyo ilivyo hata katika mambo ya Imani.. Imani haina mchipuko mmoja kama wengi wadhanivyo, Sio kila imani mtu aliyonayo ndani yake itatenda miujiza, sio kila imani mtu aliyonayo itamwokoa hali kadhalika si imani yoyote tu mtu aliyonayo ITAMPENDEZA MUNGU, vile vile sio kila imani itakuja kwa kulisikia Neno la Mungu, ukiyafahamu hayo vizuri itakujengea ufahamu mzuri wa kupima kiwango chako cha Imani kilipo…. Leo kwa neema za Bwana tutatazama kwa ufupi baadhi ya vipengele hivi vya imani, na kisha tutaangalia ni IMANI ya aina gani, ambayo Mungu anaiona kama ni kiini cha mkristo anapaswa awe nayo.
Embu tuchambue mojawapo ambayo tuliiona ikijitokeza kwa mtu fulani kipindi kile cha Bwana Yesu..Tunasoma:
Luka 7:1 Alipokwisha kuyamaliza maneno yake yote masikioni mwa watu, aliingia Kapernaumu.
2 Na mtumwa wake akida mmoja alikuwa hawezi, karibu na kufa; naye ni mtu aliyempenda sana.
3 Aliposikia habari za Yesu, alituma wazee wa Wayahudi kwake kumwomba aje amponye mtumwa wake.
4 Nao walipofika kwa Yesu, walimsihi sana wakisema, Amestahili huyu umtendee neno hili;
5 maana, analipenda taifa letu, naye alitujengea sinagogi.
6 Basi Yesu akaenda pamoja nao. Hata alipokuwa si mbali na nyumba yake, yule akida alituma rafiki kwake, akamwambia, Bwana, usijisumbue, maana mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu;
7 kwa hiyo nilijiona sistahili mwenyewe kuja kwako; lakini, sema neno tu, na mtumwa wangu atapona.
8 Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.
9 Yesu aliposikia hayo alimstaajabia, akaugeukia mkutano uliokuwa ukimfuata, akasema, Nawaambia, hata katika Israeli sijaona imani kubwa namna hii.
10 Na wale waliotumwa waliporudi nyumbani, wakamkuta yule mtumwa ni mzima”.
Sasa huyu Akida kumbuka hakuwa myahudi, wala hakuijua torati kama wayahudi wenyewe walivyokuwa, kwanza kwa wakati ule ilikuwa ni mwiko wayahudi kuchangamana na watu wa mataifa. Mtu huyu alikuwa ni akida wa kirumi, aliye chini ya utawala wa Kaisari, lakini alikuwa ni mkarimu sana tofauti na maakida wengine waliowekwa kuilinda Israeli,, aliwapenda wayahudi na kuwatendea mema, mpaka kufikia hatua ya kuwajengea Sinagogi, Lakini ikatokea siku moja mtumwa wake aliyempenda sana akaugua karibu na kufa, hivyo akahitaji uponyaji kutoka kwa Yesu, na wayahudi waposikia wakaenda kumwombea kwa Yesu ili aende kumponya. kama tunavyosoma habari ile Bwana akiwa njiani tu yule akida alipata taarifa kuwa YESU anakuja kwake, hivyo akatuma haraka haraka watu kwake na kumwambia atamke Neno tu, na mtumwa wake naye atapona…
Sasa jambo la kutazama hapo, si kawaida mtu kuwa na imani kubwa kiasi kile kama hajaipata kutoka mahali fulani..Imani haiwezi kuja kama haina chanzo..Lakini kumbuka biblia inatuambia Imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa Neno la Kristo.. Lakini huyu mtu hakuwa mkristo, wala hakuwa myahudi, bali mrumi..basi imani kubwa kama ile mpaka YESU kusema hajaiona hata kwa wayahudi, hata kwa kwa makuhani, hata kwa mitume, hata kwa marabi, yeye aliitolea wapi?.
Siri ipo pale pale kwenye maandiko tukisoma mbele kidogo utaona anamwambia Bwana “Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.”
Unaona hapo?, Yeye alitumia experience (au Uzoefu) wa maisha yake kumwesabia Mungu kuwa ni muweza..Yeye mwenyewe alijiona katika hali aliyopo, anao wakuu wengi juu yake ambao wakati wowote wakimwambia fanya hivi hufanya, tenda hili hutenda, hali kadhalika anao watumwa wengi chini yake akiwaamrisha fanya hivi hufanya tenda lile hutenda pasipo hata yeye kuwepo mahali husika na jambo lile hutendeka vile vile kama alivyotoa yale maagizo pasipo kuongezwa wala kupunguza..
Kwahiyo akasema huyu ni YESU naye ni MKUU kuliko sisi wote, mambo yale yale niliyoonyesha kwa watumwa wangu, au niliyoonyeshwa kwa wakuu wangu waliyafanyika bila kasoro yoyote pasipo sisi kuwepo, atashindwaje huyu kutoa tu maagizo na uponyaji kutokea, Kuliko kuja kujitaabisha huku?..Na ndio hapo akawambia Bwana aseme Neno tu!…Hapo hapo Akapokea alichokuwa anakitafuta!!.Haleluya.
Ndugu Imani yoyote ya kupokea chochote kwa Mungu, iwe ni uponyaji, au mahitaji, au mafanikio, au kutendewa miujiza, au kutenda miujiza, hiyo haitegemei Ile IMANI inayozungumziwa katika Warumi 10:17 “(Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.”)..hapana hii Inategemea ni jinsi gani wewe unavyomwelewa Mungu na kumchukulia hata katika hatua ya maisha inayopitia sasa, kwa kutazama tu mazingira yanayokuzunguka, au unayoyaishi unaweza ukaumba mambo makubwa mpaka dunia ikashangaa.
Itafakari tena ile habari ya Yule mwanamke aliyemwendea Yesu ambaye hakuwa myahudi kabisa, alitokea huko Tiro ambapo kwa sasa ni Nchi ya Lebanoni, lakini alipomwendea Yesu ili amponywe binti yake, Bwana alimwambia si vema kutwaa chakula cha watoto na kuwapa mbwa, lakini Yule mwanamke akamwambia Bwana hata mbwa hula makombo yanayondoka mezani pa watoto,.Ndipo Bwana akamwambia mama imani yako ni kubwa na iwe kwako kama utakavyo..(Marko 7:27)
Unaona huyu naye hakusoma mahali popote kwenye maandiko mpaka, awe na imani kubwa kama ile, kiasi cha Bwana kumwambia, Wote hawa wanatumia (uzoefu wao) wa maisha na kumuhesabia Mungu kuwa anaweza pia , na hivyo wanapata majibu ya maombi yao kwa Mungu.
Hata na wewe unaweza kupata lolote kwa Imani ya namna hiyo, uponyaji, kutoa pepo, na vitu vingine kama, gari, nyumba, mafanikio, kuamrisha vitu navyo vikatokea, n.k. na kwa jinsi utakavyoamini sana kwa kumchukulia Mungu kuwa anaweza ndivyo utakavyopokea zaidi. lakini fahamu kuwa Imani ya dizaini hiyo hata kama itafikia hatua ya kuweza kuhamisha milima bado uwezekano wa kwenda Jehanum ya moto ukawa ni mkubwa kwako kama hutafahamu shabaha ya Imani ambayo Mungu anataka kuiona kwa mtu.
Imani hii haiwezi ikakupa faraja, imani hii haiwezi ikakupa tumaini, imani hii haiwezi ikakupa uzima wa milele imani hii haiwezi ikakupa tumaini, Imani hii haiwezi ikakupa MAFUNUO kutoka kwa Mungu…Wengi leo wanaikimbilia hii ambayo kimsingi ni nzuri lakini wanasahau kiini cha imani mama impasayo kila mtu awe nayo kwa mambo yote.
IMANI MAMA NI IPI?
Warumi 10:17 “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa NENO LA KRISTO”.
Sasa nataka ufahamu kuwa ipo imani inajengeka ndani ya mtu si kwa uzoefu fulani hapana, kama alioupata yule akida aliyeponyewa mtumwa wake au aliyoipata yule mama wa Tiro aliyeponyewa binti wake, bali ni kwa kulisikia Neno la Kristo tu, Kumfahamu Kristo tu kwa mapana yake na marefu yake basi, hii ni Imani timilifu katika Neno la Kristo. Si wengi wanayo, na hii haifikiwi hivi hivi labda kwa kusali sana, au kwa kufunga sana, hapana bali inafikiwa kwa kumjua sana Kristo tu katika Neno lake..Tunaposema kufahamu Neno la Mungu hatumaanishi kukariri vifungu vya biblia tu hapana, bali ni kupata ufunuo wa Yesu Kristo ni nani katika maisha yako, na hiyo inakuja kwa kumtafakari sana Bwana Yesu, na kumjua yeye kwa upana wake na urefu wake kwa maana biblia inasema katika “Wakolosai 1:19.. Kwa kuwa katika yeye ilipendeza UTIMILIFU wote ukae;
Sehemu nyingine biblia inasema katika Waefeso 4:13 “hata na sisi sote tutakapoufikia UMOJA WA “IMANI” NA KUMFAHAMU SANA MWANA WA MUNGU, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu”.
Shetani hapendi kabisa watu watafute IMANI ya NAMNA HII,..Hapendi kabisa watu wapoteze muda mwingi kufundishwa habari za YESU, bali za mafanikio na uponyaji tu kila wakati..Kwani anajua watu imani yako ikishajengwa katika ufunuo wa kumjua YESU KRISTO ni nani kwao? Basi watamsumbua sana yeye na kuleta madhara makubwa katika ulimwengu kwa roho. Kwahiyo hapendi watu wamjue sana Yesu Kristo, hababaiki watu wawe hata na imani ya kuhamisha mlima, hiyo haimbabaishi inaogopa sana mtu mwenye Imani iliyojengwa katika kumjua Yesu Kristo, nguvu za kufufuka kwake.
Jiulize ni kwanini utakuta mtu ameshakuwa ni mkristo kwa muda mrefu lakini leo hii hana hata Amani katika maisha yake, jiulize ni kwanini hana furaha, ni kwanini anaona kama vile Mungu hamsikii, ni kwanini anayo hofu ya kufa, kwanini anayumbishwa na mafundisho ya uongo, kwanini kila siku ni mchanga kiroho, kwanini hapokei mafunuo yoyote kutoka kwa Mungu, kwanini anawaogopa wachawi? Ni kwanini hata ujasiri kwa Mungu wake hana, na bado ni mkristo wa muda mrefu…
Hajui kuwa tatizo lipo hapo, Imani yake haijajengwa katika misingi ya kumjua YESU KRISTO bali katika misingi mingine..Amekuwa hataki kufundishwa habari za msalaba, yeye anataka tu, atabiriwe ndoa yake, atakata tu aombewe juu ya uponyaji wake, anataka tu aombewe biashara yake, anataka tu afundishe mafundisho laini laini, ya kubembeleza, ya faraja, mafupi, na ya kuchekesha,..Sasa ile Imani inayozungumziwa na Mungu mtu wa dizaini hii asitazamie kama ataipata.
Ndugu tafuta kumjua Yesu na uweza wake, weka uhusiano wako sawa na YESU maishani mwako, jishughulishe sana kumtafuta kwa kumchunguza, na kwa kusoma habari zake zote, na kwa kumtafiti sana, huko huko ndiko utakapopata ufunuo wa kumjua YEYE ni nani kwako. Zipo faida nyingi, na mojawapo ni kuwa wewe utayapata yote utakayotaka, ya mwilini na ya rohoni, ukimwomba Baba vya mwilini atakupa kwasababu tayari utakuwa ameshakuonyesha njia ya kuvipata, halikadhalika rohoni utakuwa ni amani, furaha, utulivu, tumaini, ujasiri,faraja na maji ya mito ya uzima kuyatakuwa yanatiririka moyoni mwako. Kwasababu Imani yako imejengwa katika misingi ya kumjua YESU KRISTO. Umeshapata ufunuo wa Yesu Kristo ni nani kwako, Hivyo shetani hawezi kukusumbua tena. Yesu Kristo ndio siri ya Mungu iliyotabiriwa itafunuliwa katika siku za mwisho, Unabii wote wa biblia unamuhusu yeye, na ushuhuda wake ndio roho ya Unabii (Ufunuo 19:10).
Ndugu ikiwa bado unasua sua katika imani, huu ni wakati wa kuweka mambo yako sawa, Tubu, anza mwanzo mpya na Bwana, badili mfumo wako wa maisha kwa ujumla na wa kumwendea Mungu, angalia Imani yako unaijenga katika Nyanja ipi? Kumbuka hilo eneo la IMANI ni pana kama ilivyo Elimu…Hivyo chaguo ni lako Ni matumaini yangu kuwa sote tutachagua kujenga katika misingi ya Neno lake ili tupate vyote.
Ubarikiwe sana. Tafadhali “Share” ujumbe huu na wengine, na Bwana atakubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
JE! NI SAHIHI KWA MKRISTO KUOA/KUOLEWA NA MTU WA IMANI NYINGINE?
JE! NI LAZIMA WATU WOTE WANENE KWA LUGHA?
NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?
Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, natumai u mzima, karibu tushiriki pamoja maneno ya uzima, leo tutazungumzia juu ya ujio wa mpinga-kristo.
Mpaka sasa dunia inatazamia ujio wa watu wawili huko mbeleni kabla ya mambo yote kuisha, wa kwanza ni KRISTO na wa pili ni MPINGA-KRISTO. Na kila mmoja amekuwa akitazamiwa na watu na bado anaendelea kutazamiwa. Lakini kuna mahali ambapo watu wengi wanakosa shabaha hususani katika namna ya kumtambua mpinga-kristo na utendaji kazi wake. Tambua kuwa njia pekee ya kumjua shetani ni kumfahamu Mungu tu, hakuna njia ya mkato, huwezi kusema unamjua vizuri shetani na huku hata mahusiano yako na Mungu ni mabovu, Neno la Mungu halipo ndani yako Roho wa Mungu yupo mbali na wewe, hapo ni sawa na unajidanganya tu hata kama utasema wewe unamjua shetani namna gani, na ndio hapo utamwona mtu anaishia kudhani shetani ni freemason aliyekaa kuzimu anawatajirisha watu na kuwaambia watoe kafara za watu ili awape utajiri, na kusababisha ajali, na mambo mabaya hilo tu,.na utakuta mtu huyo anapoteza muda wake mwingi kuchunguza ishara na alama kila mahali, na kwenye vibao, vya kichawi ili kujiepusha navyo, utakuta anafahamu alama zote wazitumiazo wachawi. Na kwa hilo anajisifu kuwa anamfahamu shetani, lakini hafahamu kuwa hivyo ndivyo shetani anavyotaka afikirie siku zote, apoteze muda mwingi kuwafahamu wachawi na vikundi vyao, lakini asidhubutu hata kidogo kumfahamu Kristo na Neno lake.
Ndugu usipoifahamu noti original utawezaje kuitambua noti feki, watu wengi wanafikiria kuwa Mpinga-kristo atakuja kuwa ni mtu wa ajabu na wa tofauti, mtu katili sana, mtu ambaye ulimwengu mzima utakwenda mbele yake na kumsujudia na mtu yeyote asipomsujudia atauawa kama kuku, mtu ambaye atawalazimisha watu kwa nguvu wapokee chapa na endapo mtu asipopokea atachinjwa hadharani bila huruma yoyote, atakuwa mtu mkali kupindukia, atakuwa anakunywa damu za watu hadharani n.k..Hivyo hiyo inawafanya watu wastarehe wadhani kuwa bado muda mrefu sana, mpaka atokee mtu wa namna hiyo, bado hajaanza kutenda kazi na siku atakapoanza tutajua…
Lakini turudi katika upande wa pili..watu vivyo hivyo wanadhani YESU yupo mbinguni ametulia , na yeye ipo siku moja atakuja, na siku atakayokuja makaburi yatafunguka na watu wote watawaona wafu wakifufuka, atasimama mawinguni, parapanda italia, malaika wataonekana kila pande, hivyo kwasasa bado unyakuo haujaanza siku utakapotekea siku ndiyo tutakapojua.
Kitu ambacho hatukifahamu mpaka sasa ni kwamba Kristo anakuja katika roho na anawanyakua watu wake mbali na watu waovu, Bwana Yesu hajakaa katika kiti fulani huko mbinguni mpaka sasa miaka elfu mbili imepita akisubiria tu siku moja ifike aje kuwachukua wateule wake, hapana badala yake tangu kuondoka kwake amekuwa na AGENDA, na bado anatenda kazi, na agenda hiyo imekuwa akifanyia kazi kizazi baada ya kizazi, amekuwa akizungumza na watu wake katika kipindi kimoja cha kanisa hadi kingine, vipindi hivyo tunaviona katika kitabu cha ufunuo 2&3. Kila nyakati amekuwa akilinyakua kanisa lake na kulihadhi mahali fulani, hata sasa bado anaendelea kuwanyakua watu wake na kuwahifadhi, na kama utakufa na ule mwisho bado haujakukuta unahifadhiwa mahali fulani ukingojea siku ya kujumuika na wengine watakao kuwa hai na kwenda nao mbinguni.
1Wathesalonike 4.13 “Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.
14 Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.
15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele”.
Unaona hapo siku ile unyakuo haimuhusu tu yule atakayekutwa hai hapana bali inawahusu na wale wengine ambao walishakufa wakiwa wanatembea katika mstari wa Kristo kabla ya hapo.
Lakini vigezo vya kunyakuliwa vipo wazi, ni hicho si kingine zaidi ya alama utakayotiwa, au Chapa au Muhuri uliojuu yako..Na muhuri wenyewe si mwingine zaidi ya ROHO MTAKATIFU. Pasipo huo muhuri huwezi Kunyakuliwa ndugu..aidha iwe hai au uwe umekufa..
Waefeso 4.30 “Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; AMBAYE KWA YEYE MLITIWA MUHURI HATA SIKU YA UKOMBOZI”.
Hali kadhalika na kwa mpinga-kristo, hangojewi eti mpaka kipindi fulani kitakapofika ndio adhihirishe kazi zake, ni kweli kwasasa hajatokea lakini biblia ipo wazi kabisa kuwa utendaji kazi wake upo tangu zamani na ile roho inazidi kuendelea kufanya kazi hata sasa,..na kama vile Bwana alivyokuwa na Muhuri au chapa yake, Halikadhalika ibilisi naye anayo chapa yake au Muhuri wake,.Na chapa hiyo ni KU-MPINGA-KRISTO, na mtu anampingaje Kristo? Ni kwa kumkataa Roho Mtakatifu ndani yake..Kuupinga wokovu ndani ya moyo wako..Kuzipinga-kazi za Mungu ndani ya moyo wako…Kwenda kinyume na njia za Bwana, kukaidi maagizo ya Mungu kama shetani mwenyewe alivyo. Kuutua msalaba, kulikosoa Neno la Mungu, kuipuuzia injili na kuona kama ni hadithi za kizee, kuwatukana watu wote wanaoutumainia msalaba. N.k. sasa mtu ukishajiona upo katika hali hiyo basi ujue tayari ulishapokea chapa ya mnyama..Hivyo mtu yeyote atakayekufa leo katika hali hiyo yeye naye atahifadhiwa mahali pa mateso panapoitwa, akisubiria siku ya kukamilishwa kwa wapinga-Kristo wenzake, na kwa pamoja wote wataungana na kwenda kuhukumiwa kwa kupokea chapa ya mnyama, na wote kwa pamoja watatupwa katika lile ziwa la moto.
1Yohana 2: 18 “Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo YUAJA, HATA SASA WAPINGA KRISTO WENGI WAMEKWISHA KUWAPO. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.
2Wathesalonike 2:5 “Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?
6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.
7 MAANA ILE SIRI YA KUASI HIVI SASA INATENDA KAZI; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.
8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;
9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;
10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa”.
Hivyo usidanganyike kuwa ukifa sasa bila kuufika wakati wa mpinga-kristo umeotea, kwamba umeikwepa chapa yake..fahamu kuwa chapa inapigwa hata sasa, na jua kuwa chapa ile ipo katika roho na si mwili kama vile biblia inavyosema wale watakaokutwa hai wakati wa Bwana hawatawatangulia wale waliokufa siku ile ya unyakuo..Hali kadhalika wale watakaopokea chapa ya mnyama wakati ule wa dhiki kuu, hawatawatangulia wale waliokwisha kuipokea zamani kabla ya dhiki kufika;..Watakaosalia katika ile siku ya dhiki kuu, kwa kupitia kitambulisho cha dini na udhehebu wataithibitisha chapa ya mnyama ambayo tayari imo katika roho zao.
Pia biblia inatueleza kuwa Bwana alikuja, akaondoka, na atarudi tena, halikadhalika na yule mnyama biblia inasema, alikuwako, naye hayuko naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu..Hii inatuweka wazi kuwa kazi zilishaanza zamani sambamba na za Bwana wetu Yesu Kristo.
Ufunuo 17:8 “Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako”.
Unaona?, Sasa ni vizuri kufahamu pia Mpinga-Kristo mwenyewe atatokea wapi..Biblia inatueleza atatokea RUMI, katika ule utawala wa mwisho kabisa wa chuma..VATICAN ndiyo yatakayokuwa makao yake makuu, katika kiti cha KI-PAPA…Mpinga-Kristo hatashika bunduki, wala visu, anashika biblia, na anahubiri..lakini injili yake ni ya uongo.
Kwanini usifanye uamuzi sasa wa kumgeukia muumba wako?, hatari uliyonayo ni kubwa kama hutageuka sasa, mambo yote yanakaribia kuisha, ukifa leo katika dhambi huko utaenda kuwa mgeni wa nani. Tafakari hilo, usiishi tu ilimradi siku zinapita, Neema inapatikana bure, uamuzi ni wako, Ni matumaini yangu utatubu leo na kumgeukia muumba wako angali muda upo, saa zaja utakazotamani huu wakati wa sasa lakini utaukosa.
Mungu akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO
Mtu ambaye ni mwepesi kuudhiwa, au mwepesi kulia, au mwepesi kukasirishwa basi mtu huyo mara nyingi anakuwa pia ni mwepesi kusahau makosa, au mwepesi kufurahi au mwepesi kucheka..Lakini mtu ambaye ni mzito kuudhika pale anapoudhiwa, au kukasirika au kulia au kuwaka hasira, basi mtu huyo vile vile mpaka afikie hatua ya kukasirishwa na baadhi ya mambo basi ujue kuwa itachukua muda sana kuituliza ghadhabu yake au hasira yake.
Tuchukulie tu mfano mtoto mdogo, kama ukimtazama kwa siku anaweza kulia hata mara tano au sita, utakuta kinachomliza ni vitu vidogo vidogo tu visivyo na maana, lakini mtu huyo huyo dakika chake mbeleni utakuta ameshasahau anacheza na wewe kana kwamba hujawahi kumuudhi kabisa..Lakini tuje kwa mtu mzima, anaweza asidondoshe chozi kwa hata kwa mamiaka, lakini siku ukimkuta analia basi ujue kuna jambo zito, tena zito sana tena sio jepesi hata kidogo, pengine utakuta ni msiba au kaumizwa sana,au kajeruhiwa sana, na hivyo mpaka hali hiyo imetokea ndani yake, basi haiwezi kuwa ni kitendo cha dakika chache kuondoka, pengine itamgharimu miezi au miaka ndipo iishe kabisa.
Hali kadhalika biblia imetuweka wazi kabisa, kuhusu hali ya Mungu wetu wa mbinguni tunaye mwabudu siku zote, yeye ni Mungu mvumilivu sana, ni mwingi wa rehema, ni mnyenyekevu, ni mwenye neema, ni mwingi wa huruma, haoni hasira haraka,..Na ni kweli ndivyo alivyo hata sisi wenyewe tunalishuhudia leo hilo pale tunapoona watu tunaona wanatembea barabarani uchi, watu wanamtukana Mungu hadharani lakini hasemi chochote, watu wanawachinja wenzao kama wanyama bila huruma na Mungu hafanyi lolote, watu wanawakata viungo watoto wadogo wasio na hatia wakiwa hai, na kuchukua viungo vya maalbino, wengine wanawachuna ngozi ili kwenda kuuza kwa waganga, mpaka tunajiuliza hivi Mungu hayaoni haya yote? Mbona hachukui hatua yoyote kali..Ingekuwa ni wewe au mimi ni Mungu ni wazi kuwa hakuna hata mmoja angesalia tungeshawateketeza wote.Lakini kwa Mungu haipo hivyo yeye alisema “..
Bwana si mwepesi wa hasira, (Nahumu 3:1)…Ni mpole wa Hasira, mwingi wa rehema (Hesabu 14:8)
Pia
Kutoka 34: 6 “….,Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;
7 mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi;..”
Na pia Daudi anashuhudia hilo na kusema “Bwana ana fadhili, ni mwingi wa huruma, Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, Zaburi 145:8” Na ukisoma pia Yona 4:2 na Nehemia 9:17..utathibitisha jambo hilo hilo.
Unaona hiyo ndio sifa yake kuu.. Lakini yeye kuonyesha rehema zake hata kwa waovu sio kwamba anapenda kuendelea kuwaona wanafanya mambo yao maovu, bali kinyume chake anataka wote wafikie toba, na ndio maana kila siku anawahubiria watubu, Lakini wasipotaka kutubu, kama tulivyoona kuwa mtu Yule ambaye si mwepesi kuudhika, ikifika siku ameudhika basi jua kuwa ghadhabu yake haiishi leo wala kesho, ndivyo ilivyo kwa Mungu ukali wa hasira yake hakuna atakayeweza kuuzima, si kwa toba wala kwa kulia siku ile itakapofika..
Watu wa kipindi cha Nuhu walipuuzia sana uvumilivu wa Mungu kwao, walihuburiwa injili kwa miaka mingi, lakini waliona mbona hakuna dalili yoyote ya kuadhibiwa, kama vile Mungu hayupo, Mungu hawezi kuangamiza dunia yote na watoto ndani yake,ndivyo walivyokuwa wanajifariji, Nuhu alionekana kama kichaa anacheza lakini siku ile walipoingia kwenye safina, ndipo waovu walipojua kweli hasira ya Mungu ni kali…watu 8 tu kati ya mabilioni ya watu waliokuwa wanaishi duniani ndio waliopona…Vivyo hivyo ilikuwa katika siku za Lutu, na ndivyo itakavyokuwa katika SIKU ILE YA HASIRA YA BWANA kama Bwana alivyoifananisha siku ile na hizo, ambayo hiyo ipo karibuni sana kutokea. Kutakuwa na kulia lakini Mungu hatasikia, kutakuwa na maombolezo lakini Mungu hataokoa, utasema ni wapi tena jambo hilo lilishawahi kutokea kwenye Maandiko,? Wakati wana wa Israeli walipoonywa kwa mamia ya miaka waache maovu na wamgeukie Mungu, lakini hawakutaka, Bwana aliwaonya waache maovu wasije wakapelekwa utumwani hawakusikia, wakatenda maovu mpaka ikafikia hatua ya Mungu kutokusamehe tena..kikombe cha ghadhabu ya Mungu kilikuwa kimejaa juu yao, ulinzi wa kiMungu ukaondoka juu yao, Nebukadneza akaja akawachinja watu mbele ya macho kama kuku, na waliosalia akawapeleka utumwani Babeli.. Tunasoma hayo katika.
2 Nyakati 36: 11 “Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja, alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na mmoja;
12 akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, Mungu wake; wala hakujinyenyekesha mbele ya Yeremia nabii aliponena kwa kinywa cha Bwana.
13 Tena akamwasi mfalme Nebukadreza, aliyemwapisha kwa Mungu; lakini akajifanyia shingo ngumu, akajitia moyo nguvu asimgeukie Bwana, Mungu wa Israeli.
14 Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno sawasawa na machukizo yote ya mataifa; wakainajisi nyumba ya Bwana aliyoitakasa katika Yerusalemu.
15 Naye Bwana, Mungu wa baba zao, akatuma kwao kwa mikono ya wajumbe wake, akiondoka mapema, na kutuma; kwa sababu aliwahurumia watu wake, na makao yake;
16 lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, hata ilipozidi ghadhabu ya Bwana juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya.
17 Kwa hiyo akaleta juu yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao kwa upanga nyumbani mwa patakatifu pao, asiwahurumie kijana wala mwanamwali, mzee wala mkongwe; akawatia wote mkononi mwake”.
Soma tena mstari wa 15 na wa 16…inasema.. “Bwana aliwatumia wajumbe wake, kwasababu aliwahurumia lakini wakawacheka na kuwadhihaki, hata ilipozidi ghadhabu HATA KUSIWE NA KUPONYA”..Unaona kuna hatua inafika kutakawa HAKUNA KUPONYWA TENA!! Yaliyotokea yametokea, hayawezi kubadilika tena wala kubadilishwa.
Ndugu usidhani ukiachwa sasa kwenye UNYAKUO utakuwa na nafasi ya pili mbele za Mungu, kwamba utatubu na Mungu atakuhurumia, Fahamu nafasi ni moja tu nayo ni kwa Njia ya YESU KRISTO peke yake na sio kwa njia yako, ingekuwepo ipo nafasi nyingine, Yesu asingesema mtu haji kwa Baba isipokuwa kwa njia yangu mimi, badala yake angesema mtu haji kwa Baba isipokuwa kwa njia yangu au yako..Hautafika mbinguni ndugu kama chujio la UNYAKUO litakupita.. Na wote watakaobaki hakuta kuwa na lingine lililosalia kwao isipokuwa kukutana na ghadhabu ya hasira ya Mungu, na hiyo haina lengo lingine zaidi ya kuwaharibu watu wote waovu ambao, walikataa neema, walikataa kuishi maisha ambayo Mungu alikusudia kila mwanadamu ayaishi, ni mapigo ambayo hata mtu aombolezaje hawezi kusikiwa.
Kumbuka hiyo ni tofauti na dhiki ya mpinga-kristo, siku ya Bwana ni tofauti kabisa, ni wakati Mungu aliojitengea kujilipizia kisasi cha hasira yake. Usitamani uwepo huo wakati ukadhani kuwa utastahimili, au utaokoka..
Yoeli 2: kwa kuwa siku ya Bwana ni kuu, yenye kitisho sana; naye ni nani awezaye KUISTAHIMILI.
Bwana anasema tena Siku hiyo watu duniani wataadimika kuliko DHAHABU, kumbuka sio kama dhahabu, hapana! bali kuliko dhahabu…Tafakari hilo neno tunajua dhahabu ni jamii ya mawe, lakini upatikanaji wake sio wa kwenda tu nje na kuikota kama kokoto, ndivyo itakavyokuwa siku hiyo watu watakuwa wachache sana kama vile dhahabu ilivyoadimu, si ajabu hili taifa lote la Tanzania watasalia watu 2 au 3 tu au asisalie mtu kabisa…wakati wa gharika watu waliadimika kama dhahabu, alisalia Nuhu tu wanawe watatu na wake zao.
Isaya 13: 6 “Pigeni kelele za hofu; maana siku ya Bwana i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu.
7 Kwa sababu hiyo mikono yote italegea, na moyo wa kila mtu utayeyuka.
8 Nao watafadhaika; watashikwa na utungu na maumivu; watakuwa na utungu kama mwanamke aliye karibu na kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto.
9 Tazama, siku ya Bwana inakuja, SIKU KALI, YA HASIRA NA GHADHABU KUU, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.
10 Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.
11 Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali;
12 NITAFANYA WANADAMU KUADIMIKA KULIKO DHAHABU SAFI, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri.
13 Kwa hiyo nitazitetemesha mbingu, na dunia itatikiswa itoke katika mahali pake, kwa sababu ya ghadhabu ya Bwana wa majeshi, na kwa sababu ya siku ya hasira yake kali.
Adhabu hiyo itakuwa ndani ya yale mapigo ya vitasa 7. (Ufunuo 16 :1-21). Embu tazama kwa ufupi yatakayo tokea.
Ufunuo 16:1 “Nikasikia sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Enendeni, mkavimimine vile vitasa saba vya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi.
2 Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na jipu baya, bovu, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake.
3 Na huyo wa pili akakimimina kitasa chake juu ya bahari, ikawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa.
4 Na huyo wa tatu akakimimina kitasa chake juu ya mito na chemchemi za maji; zikawa damu.
5 Nami nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako, Mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi;
6 kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; nao wamestahili.
7 Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, ni za kweli, na za haki, hukumu zako.
8 Na huyo wa nne akakimimina kitasa chake juu ya jua, nalo likapewa kuwaunguza wanadamu kwa moto.
9 Wanadamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, nao wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu yamapigo hayo; wala hawakutubu wala kumpa utukufu.1
10 Na huyo wa tano akakimimina kitasa chake juu ya kiti cha enzi cha yule mnyama; ufalme wake ukatiwa giza; wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu,
11 wakamtukana Mungu wa mbingu kwa sababu ya maumivu yao, na kwa sababu ya majipu yao; wala hawakuyatubia matendo yao.
12 Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.
13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.
14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.
15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)
16 Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.1
17 Na huyo wa saba akakimimina kitasa chake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu, katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa.
18 Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo.
19 Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.
20 Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena.
21 Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.
(Ikiwa utahitaji kufahamu kwa urefu juu ya vitasa 7 nitumie ujumbe inbox, nitukutumie uchambuzi wake wote.)…Sasa baada ya hayo mapigo kuisha kitakachofuata ni Hukumu kisha ziwa la moto.
Lakini hayo ni machache kati ya mengi yatakaowakuta wale wote ambao watakosa UNYAKUO sasa ambapo dalili zote zinaonyesha kuwa kizazi chetu hichi ndio kile Yesu alichokizungumzia kuwa hayo yote yatatimia..Ni saa gani hii tunaishi?..Kwanini huyathamini maisha yako ya milele?..Kwanini unaipuuzia hiyo neema iliyo juu yako? Unazini lakini Mungu hakusemeshi chochote, unatazama pornography kwa siri, lakini Mungu hakuadhibu kwa lolote, unafanya mambo machafu lakini Mungu kama vile hakuoni..sio kwamba anapendezwa na wewe au kwamba wewe ni mtu pekee sana kwake, na ndio maana hayakukuti mabaya sasa..
Lakini fahamu si mwepesi wa hasira ni Mwingi wa huruma..uvumilivu wake ndio unaokuvuta utubu..
2Petro 3:8 “Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.
9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, BALI HUVUMILIA KWENU, MAANA HAPENDI MTU YE YOTE APOTEE, BALI WOTE WAFIKILIE TOBA.
10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,”
Usipotubu leo upo wakati mbaya unakusubiria mbeleni usiokuwa na msamaha. Leo hii ukiwa tayari kuyakabidhi maisha yako kwa Bwana kwa kumaanisha kabisa, na sio nusu nusu, mguu mmoja huku na mwingine kule atakusamehe kabisa na kuyafuta makosa yako yote, kwasababu hicho ndicho anachokitafuta kwako.
Na ndio maana anasema:
Sefania 2: 3 “Mtafuteni Bwana, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; HUENDA MTAFICHWA KATIKA SIKU YA HASIRA YA BWANA”.
Uamuzi ni wako, lakini maombi yangu leo utubu ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.Kisha baada ya hapo utakuwa umezaliwa mara ya pili, kwa Roho Mtakatifu atakayeingia ndani yako”
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo
Mada Zinazoendana:
SIKU YA BWANA INAYOTISHA YAJA!
KIKOMBE CHA GHADHABU YA MUNGU KINAJAA…NI WAKATI WA KUTUBU NA KUMGEUKIA MUNGU
MUNGU ANASEMA HATAGHARIKISHA DUNIA NA MAJI TENA,.KWANINI WATU WANASEMA DUNIA ITAANGAMIZWA?
Shalom Mwana wa Mungu, karibu tujifunze biblia, chakula cha uzima, kitupacho afya rohoni, leo kwa Neema za Bwana tutajifunza kwa ufupi, juu ya SIRI YA MUNGU.
Biblia imetaja sehemu kadha wa kadha juu ya Siri ya Mungu, na leo tutajifunza hii siri ya Mungu ni ipi.
Warumi 16: 25 “Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara, sawasawa na injili yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile SIRI iliyositirika tangu zamani za milele”.
Unaona hapo, biblia imetaja kuwa ipo SIRI iliyokuwa imesitirika tangu zamani za milele.
Sasa kabla ya kwenda kujifunza hiyo siri ni ipi, ni vizuri kwanza tukaelewa neno SIRI lina maana gani kama lilivyotafsiriwa katika biblia yetu hii ya Kiswahili, Kumbuka lugha yetu ya Kiswahili haijajitosheleza kwa maneno mengi, kwamfano yapo maneno katika lugha ya kiingereza au kigiriki ambayo ukiyaleta katika lugha yetu ya Kiswahili yanakosa tafsiri. Na pia yapo maneno yetu ya lugha ya Kiswahili ambayo ukiyapeleka katika lugha ya kiingereza yanakosa tafsiri, kwa mfano neno “shikamoo” halina tafsiri kwa kiingereza. Lakini pia yapo maneno ya kiingereza yenye tafsiri zinazokaribiana sana hivyo yakiletwa katika lugha yetu ya Kiswahili yanatumia tafsiri moja, kwamfano neno la kingereza “mouse” na “rat” tafsiri yake kwa kiswahili ni moja tu ambayo ni panya, hali kadhalika maneno mengine kama “rabbit” na “hare” yote kwa Kiswahili tafsiri yake ni “sungura”
Lakini pia kuna maneno mawili ya kiingereza yenye maana zinazokaribiana sana lakini hayafanani..na maneno hayo ni “Secret” na “mystery”…yote tukiyaleta katika lugha yetu ya Kiswahili yana tafsiri moja yaani “SIRI” lakini yana maana mbili tofauti.
“Secret” ni neno la kiingereza lenye maana ya “kipande cha taarifa ambacho kinajulikana na mtu mmoja au zaidi ya mmoja, na kimehifadhiwa kisijulikane na watu wengine zaidi ya hao wanaokijua”…kwamfano wahalifu wawili wanapopanga njama ya kuvamia mahali fulani hiyo njama ni “siri”, au vikundi fulani vya upelelezi huwa vinafanya kazi zao katika siri, ikiwa na maana vina baadhi ya taarifa ambazo ni wao tu wanaozijua na hawampi mtu mwingine yeyote taarifa hizo, (wanafanya kazi zao katika siri).
Lakini tukirudi kwenye neno la pili la kiingereza linaloitwa “mystery” ambalo kwa Kiswahili limetafsiriwa hivyo hivyo “siri” lenyewe lina maana tofauti kidogo, neno hili mystery tafsiri yake halisi ni hii “ni taarifa ambazo hazijulikani na mtu hata mmoja, hazijulikani chanzo chake, wala sababu ya jambo hilo”..kwamfano mtu anapowasha taa na giza kuondoka, ulishawahi kujiuliza lile giza linakwenda wapi? Hakuna mtu anayejua, wala huwezi kupata jibu la hilo swali kwa mtu yeyote Yule, kwahiyo hiyo inajulikana kama mistery “Mystery”, ambapo kwa Kiswahili tunaweza kusema ni siri ya ndani sana isiyoweza kueleweka wala kuchunguzika.
Biblia inasema katika:
Ayubu 38: 19“Iko wapi njia ya kuyafikia makao ya nuru? Na giza pia, mahali pake ni wapi?
20 Upate kuipeleka hata mpaka wake, Upate kuelewa na mapito ya kuiendea nyumba yake?
Ayubu 38: 24 “Je! Nuru hutengwa kwa njia gani, Au upepo wa mashariki hutawanywaje juu ya nchi?”
Hizo zote ni mystery au siri za ndani zisizoelezeka. Hali kadhalika jinsi mtoto anavyoumbika katika tumbo la mwanamke, hakuna ajuaye ni nani alipeleka mifupa migumu kule, ni nani aliingiza nywele, n.k. vyote hivyo vinabakia katika siri kuu sana (Mysteries), zisizojulikana na kushangaza watu.
Sasa baada ya kuelewa hayo, tukirudi kwenye biblia kuna kitu kinachoitwa SIRI YA MUNGU, kama tulivyotangulia kusema…sasa hiyo siri inayozungumziwa hapo sio siri yenye tafsiri ile ya kwanza “secret” bali ni siri yenye tafsiri ile ya pili “mystery”, Kwahiyo siri ya Mungu haikuwa ni kipande cha taarifa fulani kilichojificha kilichojulikana na baadhi ya watu wachache tu, na kwamba kisingepaswa kijulikane na watu wengine, hapana badala yake bali siri ya Mungu ilikuwa ni taarifa au jambo ambalo lililokuwa halijulikani na mtu awaye yeyote Yule hata MALAIKA wa mbinguni, walikuwa hawalijui wala hawalielewi, hakuna taarifa zozote kuhusiana na hilo jambo, mtu anaweza akakisia tu lakini asiwe na taarifa zozote sahihi kuhusiana na hilo jambo, kama tu vile tusivyoelewa giza huwa linakwenda wapi pindi mwanga unapokuja, na linatokea wapi pindi mwanga unapoondoka..wala hakuna mtu yeyote anaweza kutupa majibu ya hayo maswali, kadhalika na siri ya Mungu ndio ilikuwa hivyo hivyo(ilikuwa ni mystery na sio secret).
Sasa hii SIRI ya ajabu ya Mungu ilikuwa ni ipi?
Mtume Paulo alitoa majibu ya swali hilo kwa uwezo wa Roho.
Wakolosai 1:26 “SIRI ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake;
27 ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa SIRI HII KATIKA MATAIFA, nao ni KRISTO NDANI YENU, TUMAINI LA UTUKUFU
28 ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo”.
Unaona hapo, biblia inasema siri ambayo ilikuwa imefichwa tangu vizazi vyote, ikiwa na maana hakuna mtu aliyekuwa anaijua, lakini ilifunuliwa zamani za mitume, na siri hiyo haikuwa nyingine zaidi ya KRISTO YESU KUINGIA ndani yetu sisi watu wa MATAIFA. Haleluyaa!!
Tangu zamani yote, hakuna mtu angeweza kudhania kuwa sisi watu wa mataifa tungekuja siku moja kuwa wana wa Mungu, sisi tuliokuwa tunaitwa najisi, watu tuliokuwa mbali na Mungu, hakuna mtu angetegemea siku moja Wana wa Farao waliowatesa wana wa Israeli kwamba wangekuja kuitwa wana wa Mungu aliye juu, hakuna mtu angedhania kuwa wafilisti watu waliokuwa wanaitwa wasiotahiriwa kwamba siku moja watakuja kuitwa wana wa Mungu aliye juu, hakuna mtu angekuja kujua kuwa wamoabi waliowalaani wana wa Israeli wakati wanaelekea nchi ya ahadi, siku moja watakuja kuitwa wabarikiwa wateule wa Mungu aliye juu kwa kupitia Yesu Kristo, Ingekuwaje kuwaje kwanza ni sawasawa na sasahivi mtu akwambie kuna wakati utafika wachina wote wataitwa wamasai tena wamasai wa damu kabisa, ni jambo lisilosadikika. hakika hiyo ilikuwa ni siri ya ajabu ambayo isingeweza kudhaniwa na mtu yeyote, ni siri ambayo hata malaika walikuwa hawaijui. Lakini ilikuja kufunuliwa siku za mwisho.
Hakuna mtu angeweza kudhania kuwa MASIHI ambaye ametabiriwa kuja kuwaokoa wana wa Israeli peke yao, angekuja kwanza kuanza wokovu kwa watu wa mataifa, wanaoabudu sanamu, hakuna mtu au malaika angeweza kudhania kuwa siku moja Roho mwenyewe wa Mungu atakaa ndani ya watu wa mataifa. Hata malaika wa mbinguni hawakujua hiyo neema imetoka wapi, kama vile tusivyojua giza chanzo chake ni wapi, hiyo ni mystery.
Kwahiyo YESU KRISTO, kuja kutuokoa sisi watu wa MATAIFA hiyo ndiyo ilikuwa SIRI YA MUNGU, iliyofichika tangu zamani za milele, hata Musa alikuwa hajui kwamba siku moja Uzao wa Farao utamwabudu Mungu wa Israeli kupitia Masihi, hata Eliya alikuwa hajui kwamba siku moja wale alioomba moto ushuke juu yao watoto wao watakuja kumjua Mungu wa kweli na kupata kibali mbele za Mungu, Hata Daudi hakujua kwamba wale aliokuwa anawaimbia maadui maadui siku moja watakuja kuwa marafiki wa karibu wa Mungu kupitia BWANA WA UTUKUFU YESU KRISTO.
Waefeso 3:1 “Kwa sababu hiyo mimi Paulo ni mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa;
2 ikiwa mmesikia habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu;
3 ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa SIRI HIYO, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache
4 Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika SIRI YAKE KRISTO.
5 SIRI HIYO HAWAKUJULISHWA WANADAMU KATIKA VIZAZI VINGINE; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho;
6 YA KWAMBA MATAIFA NI WARITHI PAMOJA NASI WA URITHI MMOJA, na wa mwili mmoja, NA WASHIRIKI PAMOJA NASI WA AHADI YAKE ILIYO KATIKA KRISTO YESU KWA NJIA YA INJILI”
7 Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake.
8 Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;
9 NA KUWAANGAZA WATU WOTE WAJUE HABARI ZA MADARAKA YA SIRI HIYO, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote;
10 ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho;
11 kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu”.
Mstari wa 9 unasema “NA KUWAANGAZA WATU WOTE WAJUE HABARI ZA MADARAKA YA SIRI HIYO”.
Ndugu unayesoma ujumbe huu, ukimjua Yesu Kristo, kwa mapana haya au zaidi ya haya, utaogopa!! Utajua ni jinsi gani hatukustahili lakini tumefanywa tustahili, utajua ni jinsi gani Neema ya Mungu inatisha,..kwasababu kama linafanyika jambo ambalo kwa namna ya kawaida haliwezekani, wala halielezeki, hiyo inatisha!! Hakuna mtu yeyote anayeweza kuelezea hii neema imetoka wapi? Kila mtu anashangaa hata malaika…iweje hawa watu wasiofaa wapokee kipawa cha neema kubwa namna hii? Manabii wa zamani na wenyewe walionjeshwa kidogo tu! Lakini bado hawakuielewa. Waliona tu lakini wasielewe chochote, pengine walidhani watu wa mataifa watakujua kumweshimu masihi tu, lakini sio kufanywa na wao warithi wa ahadi za Mungu.
Ndugu, usiudharau msalaba, Kristo amehubiriwa kwako mara ngapi?..utapataje kupona usipouthamini wokovu MKUU namna hii?? Waebrania 2:3…kumbuka maisha yako ni kitabu na matendo yako ni kalamu yenye wino, yanaandika matendo yako kila siku, kila mwezi na kila mwaka,. siku inapopita ni unaanza aya mpya, kila mwezi ni unafungua ukurasa mpya, na kila mwaka ni unaanza sura mpya ya kitabu chako,. Na kitabu chako unaanza kukiandika siku unapozaliwa…na kinaanza na JINA LAKO kwa nje, ndio maana baada ya kuzaliwa tu unapewa jina, na pengine umeshaandika nusu ya kitabu chako mpaka kufikia sasa, jitathamini katika hiyo nusu uliyoiandika umeandika ipasavyo?, siku ile ya mwisho kitabu chako kitafunguliwa tena maandiko yanasema hivyo na kitalinganishwa na kile kitabu cha uzima kama matendo yaliyoandikwa kwenye kitabu chako hayafanani na matendo ya kile kitabu cha Uzima, sehemu yako itakuwa ni katika lile ziwa la moto. Huko ndiko kukosekana jina lako katika kitabu cha uzima. Na kumbuka mbinguni hakuna makaratasi, hivyo kitabu cha uzima sio makaratasi yaliyoandikwa majina kama nakala za ankra, hapana bali na chenyewe ni maisha yaliyoandikwa, na cha kuogopesha ni kwamba hayo maisha sio mengine zaidi ya maisha ya watu yaliyoandikwa kwenye biblia, maisha ya mitume, maisha ya Yesu Kristo, maisha ya watakatifu wote, na Maneno yao waliyoyahubiri katika Roho, Ndio maana unaona biblia ni kitabu kilichojaa habari za maisha ya watakatifu, watu siku ya mwisho ndio watahukumiwa kulingana na hayo. Paulo anasema katika kitabu cha Warumi 2:16 “katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu”
Ufunuo 20: 11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.
12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; NA VITABU VIKAFUNGULIWA; na kitabu kingine kikafunguliwa, AMBACHO NI CHA UZIMA; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao………
15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”
Kwahiyo usiidharau sauti ya Mungu inapozungumza nawe moyoni, Bwana anataka kukupa uzima wa milele na kukuepusha na hukumu inayokuja, tumefunuliwa hii siri ya Mungu, ambayo wakina Musa walitamani kuijua lakini hawakuijua, na manabii wengine wote vivyo hivyo, kwahiyo saa ya wokovu ni sasa, sio baadaye wala kesho, kama hujayakabidhi maisha yako kwa Bwana fanya hivyo leo, hata kama wewe ni muislamu au mbudha unasoma ujumbe huu, siku ile hutasema hukusikia, na kumpa Bwana maisha sio kumpa lisaa, au masaa au siku, hapana unampa maisha yako yote yaani kuanzia leo na kuendelea mpaka siku utakapoondoka duniani, unakusudia kuishi kwa kumfuata yeye, katika njia zake zote, unakusudia kuacha dhambi zote ulizokuwa unafanya kama uasherati, ulevi, anasa, usengenyaji, chuki, kutokusamehe, usagaji, utoaji mimba, ushoga, utazamaji pornography, masturbation, disco, uvaaji wa vimini na suruali, na upakaji wa makeup mpaka unatoka kwenye asili yako ya ubinadamu n.k .
Yeye anakubali wakosa na atakupa uwezo wa kushinda dhambi, , kwasababu kwa nguvu zako hutaweza kushinda dhambi hata kidogo….yeye ndiye atakuwezesha kwa namna ya ajabu utajikuta unashinda mambo hayo endapo utakubali kumfuata, wengine tulikuwa wabaya kuliko wewe lakini Bwana alitutengeneza, tulikuwa tunadhani ilikuwa haiwezekani kuishi bila kufanya hayo mambo, lakini tumeahakikisha maneno ya Mungu ni kweli kuwa ni rahisi na ni raha sana kuishi bila hayo mambo, na hatuna tena mizigo wa dhambi,na hakuna kiu tena hata kidogo ya hayo mambo, kama aliyafanya kwetu, atayafanya na kwako pia, isipokuwa Bwana anataka watu wanaomaanisha sio watu wanaositasita katika mawazo mawili, ukishakusudia kwa matendo kuacha hayo mambo haraka sana bila kupoteza muda nenda kabatizwe katika ubatizo sahihi kulingana na maandiko ambao ni wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa Jina la Yesu Kristo kulingana na (Matendo 2:38), ili upate ondoleo la dhambi zako. Na baada ya hapo utakuwa milki halali ya Roho wa Mungu, utafanyika kuwa hekalu la Mungu kwa Roho atakayeingia ndani yako.
Na kama ulirudi nyuma, shetani anataka urudi zaidi ya hapo, nia yake ni akupeleke kwenye ziwa la Moto, hiyo ndiyo ndoto yake kubwa, sasa usikubali ndoto ya shetani itimie juu ya maisha yako, ziwa la moto aliandaliwa yeye na malaika zake..lakini anataka na wewe uende huko, hivyo mpinge na Bwana atakuwa upande wako.
Mungu akubariki sana.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
INARUHUSIWA KULA NYAMA YA NGURUWE KWA MKRISTO WA KWELI?
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, libarikiwe sana. Karibu tujifunze Biblia, leo kwa Neema za Bwana tutajifuza juu ya Namna ya kutoka katika uvuguvugu wa kidunia.
Katika kitabu cha ufunuo sura ya pili na ya tatu tunasoma juu ya ufunuo wa yale makanisa saba, na kama tunavyojua makanisa yale yalikuwa ni makanisa halisi kabisa, yaliyozaliwa kutokana na Injili za Mitume hususani mtume Paulo aliyokuwa anaihubiri nyakati hizo, hata hivyo yalikuwa ni zaidi ya saba, lakini Roho aliyachagua hayo saba kwa kusudi maalum kuyafundisha makanisa ya siku za mwisho ambayo tunayoishi, utaona kulikuwa na makanisa mengine yaliyokuwa Korintho, Galatia, thesalonike, filipi nk. lakini hayajatokea katika kitabu cha ufunuo isipokuwa yale saba tu..
Hivyo kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa vipindi vya kanisa utakuwa unajua kuwa, tayari kuna vipindi sita vimeshapita vya kanisa tangu Bwana Yesu Kristo aondoke, na sasa tupo katika kipindi cha kanisa la saba, na kanisa tulilopo ndilo la saba na la mwisho linalojulikana kama LAODIKIA. Kama hujafahamu kabisa jambo hili au ndio mara ya kwanza unalisikia basi katafute kujua kwasababu ni jambo linalojulikana na wasomaji wengi wa biblia, au nitumie ujumbe inbox nikutumie uchambuzi wa nyakati hizi saba za kanisa na wajumbe wake.
Sasa tabia ya hili kanisa la LAODIKIA ni kanisa vuguvugu, kama tunavyosoma katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana mlango wa tatu.
Ufunuo 3: 14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
16 Basi, kwa sababu UNA UVUGUVUGU, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja name”.
Kanisa hili la Laodikia lilianza mwaka 1906, na litaisha siku unyakuo utakapofika, sasa hili kanisa ndilo lililoonyesha tabia ya hatari kuliko makanisa mengine yote ya nyuma, kwasababu mbele za Bwana limepimwa na kuonekana kuwa ni vuguvugu, nusu Mungu, nusu shetani, ni kanisa Nafki, na ndio inayopelekea kuonekana kuwa ni kanisa lililoharibika kuliko makanisa yote.
Sasa huu uvuguvugu unatoka wapi?..Huu uvuguvugu ni Pepo maalumu lililotoka kuzimu, na kutumwa duniani ili kufanya kazi maalumu ya ushawishi, na hili pepo halijatumwa kwa mtu mmoja hapana bali limetumwa kwa kizazi…Ni pepo lenye nguvu mara saba zaidi ya mapepo mengine yote..Ni pepo linalotenda kazi katika viwango vya juu kabisa vya utendaji kazi wa shetani, ambalo kazi yake hasa ni kuwakosesha wanadamu wa kizazi cha siku za mwisho wamkosee Mungu wao, ili Mungu awakatae kabisa kabisa na kuwakana.
Sasa tujifunze kwa ufupi hili pepo linatendaje kazi, kabla ya kuja kuona madhara atakayoyapata mtu yule endapo hatalishinda..
Biblia inasema katika Waefeso 6: 11
“Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, JUU YA WAKUU WA GIZA hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho”.
Sasa Hawa wakuu wa giza wanaozungumziwa hapa wapo SABA, katika kila kanisa kulikuwa na mkuu mmoja, na katika hili kanisa la Laodikia yupo mmoja na ndiye mwenye nguvu kuliko wote. Na kama jina lake lilivyo “mkuu wa giza” anahakikisha kunakuwa na giza katika ulimwengu wa roho, anahakikisha hakuna nuru, na anahakikisha Nuru ya haki haiwazukii watu.
Na kauli mbiu yake aliyoipokea kutoka kwa shetani mkuu wake ni “KUHAKIKISHA WATU WOTE WANAKUWA VUGUVUGU DUNIANI”…kwahiyo anayo mapepo chini yake anayofanya nayo kazi kuhakikisha anatimiza lengo hilo. Kumbuka huyu mkuu wa anga, hatumshindi kwa kumkemea, hapana! Tutakuja kuona mbeleni namna ya kulishinda hili pepo.
Sasa anachokifanya ni kutumia nguvu za giza, na mapepo yake kuwafanya watu wawe vuguvugu, sio wanakuwa baridi wala moto! Hapana bali wanakuwa vuguvugu, hilo ndio lengo lake kubwa…Anahakikisha watu wamfahamu Mungu kidogo, na waufahamu uovu kidogo!..hataki kabisa mtu awe baridi hilo halitaki, anataka mtu awe hapo katikati..kwasababu anajua Mungu anamchukia mtu vuguvugu kuliko hata mtu yule aliye baridi..yaani kwa Mungu ni heri mtu awe mlevi na mwasherati moja kwa moja, kuliko mtu ambaye ni mwasherati kwa siri na bado anaenda kanisani au bado anasali..Huyo kwa Mungu anafananishwa na MATAPISHI!! Ni Bwana mwenyewe ndio alisema hivyo “ni heri ungekuwa moto au baridi kuliko kuwa vuguvugu”. Hivyo kule kuzimu katika vikao vyao ndio wameona wakifanikiwa kumfanya tu mtu awe vuguvugu, basi watakuwa wamemlaza kwa kila kitu.
Sasa hili pepo lenye nguvu mara saba kuliko mengine ndio lengo lake kubwa hilo!… wengi wanajua kuwa shetani mwanzoni alikuwa ni malaika mbinguni, lakini hawajui kuwa baada ya kulaaniwa hakunyanganywa nguvu zake na akili zake bali aliendelea kuwa nazo..Hivyo ni muhimu kujua kuwa yeye naye anatenda kazi kwa akili sana kiasi kwamba pasipo Roho wa Mungu, ni rahisi kuwadanganya hata yamkini walio wateule. Atahikikisha anatumia ushawishi mkubwa kumfanya mtu ajione yupo sawa na Mungu wakati bado ni mwasherati, mlevi, mla rushwa, anaishi na mwanamume au mwanamke ambaye hawajafunga ndoa, na bado mtu huyo ajione yupo sawa na Mungu n.k.
Huwa inauma sana unapokutana na mtu na unamwuliza umempa Bwana maisha yako na anakujibu NDIO, na unaendelea kumwuliza je! Bwana akija leo una uhakika wa kwenda naye mawinguni anakujibu NDIO nina uhakika kabisa, lakini ukija kumwangalia maisha yake utahuzunika kiasi cha kufa..
Kwamfano kuna mtu mmoja alinitumia ujumbe akaniambia mtumishi naomba uniombee kwasababu ni miaka mingi sasa sijapandishwa kazi, mimi ni kibarua tu,kazi yangu ni ya udereva, na bado ninafamilia, kwakweli alivyokuwa anaeleza alitilisha huruma sana huyu ndugu, nikamwuliza umempa Bwana maisha yako? akanijibu NDIO, nikazidi kumwuliza je! unauhakika Bwana leo akija utakwenda naye? Akajibu Ndio ninauhakika..Nikazidi kumwuliza tena je! una uhakika uovu wote haupo ndani ya maisha yako?.. namaanisha sio mlevi, sio mwasherati, hauna mwanamke unayetembea naye ambaye hamjaoana, sio mtukanaji, sio mla rushwa, sio mtazamaji wa pornography, sio mfanyaji masturbation n.k. akaniambia ndio hafanyi hayo yote!…na zaidi ya yote ameoa na ana mtoto, sasa lengo la kumwuliza vile sio kumweka kwenye mtego hapana! Bali kujua chanzo cha tatizo lake ili nijue namna ya kumsaidia kulingana na maandiko.
Baada ya kuniambia vile basi nikamwambia huna haja ya kuwa na hofu, wala usiogope! Maadamu upo katika mstari wa Bwana, Bwana hawezi kukutupa, Zidi kudumu katika haki subiri wakati wa Bwana, Bwana atakupatia kazi nzuri tu! mwamini yeye, akajibu amina!..Najua alitegemea nimwombee lakini sikufanya vile..
Baada ya siku kadhaa, nikaingia kwenye mitandao, nikakutana na post yake mahali.. “nguvu ziliniishia”…mambo anayo ya-post hata wasiomjua Mungu kabisa wanaona aibu kushiriki na wengine post hizo, ni picha chafu zisizoelezeka!!..Nilijihisi vibaya sana.
Nimekutana na watu wengi sana wa namna hiyo..wanahitaji Bwana awafanyie kitu fulani katika maisha yao, wanatamani wafanikiwe katika maisha, wawe matajiri, lakini hawajijui kuwa wao ni maskini wa roho, wanajiona kuwa ni matajiri wa roho kumbe ni maskini, wanajiona wapo sawa na Mungu kumbe hawamjui Mungu kabisa, ni lile lile pepo la Laodikia ndio lipo juu yao na ndilo linalowapusha wengi macho! Wasitambue ni hali gani mbaya ya kiroho waliyopo.
Nikakutana na dada mwingine nikamwuliza umempa Bwana maisha yako, akajibu ndio nampenda sana, nikamwuliza unamfahamu mtu fulani (nilimtaja tu mhubiri fulani maarufu wa zamani)..akajibu ndio namjua, nikamwuliza ulimsikia wapi..akanitajia nilimsoma kwenye agano la kale!..nikamwambia mbona huyo hayupo kwenye agano la kale,..akaniambiaa aah samahani nilimsoma kwenye agano jipya! Nikwambia hayupo hata kwenye agano jipya, akaniambia yupo wapi?, nikamwambi ni muhubiri tu aliyewahi kutokea miaka hamsini iliyopita nyuma..Huyu pia sikumwuliza kwa nia ya kumtega bali nilikuwa nataka nimfundishe kitu,…lakini tayari yeye alikuwa anajiona anajua kila kitu hana haja ya kitu kingine, baada ya muda mfupi nilijaribu kumpeleka kwenye maandiko nimfundishe, akakwazika akaondoka.
Nikakutana na mwingine tena, …nikamwuliza dada umempa Bwana Yesu maisha yako akanijibu ndio nimempa, ndio mwokozi wangu na ninampenda sana, nikamwambia akija leo una uhakika wa kwenda naye, akanijibu kabisa asilimia 100, nikamwuliza unamjua aliyeandika kitabu cha mhubiri? Akasema hamjui, nikamwuliza aliyendika kitabu cha wimbo uliobora je! akasema pia simjui, nikamwambia kama kweli unampenda Bwana ingekupasa kuyajua haya yote na zaidi ya haya, ila sikulaumu!..nikataka kujaribu kumfundisha msingi wa imani ya kikristo kwanza ndipo tuendelee mbele..hakutaka kuendelea kuongea akakatisha mazungumzo na kuondoka.
Hilo ndio tatizo la watu wengi katika kizazi chetu hichi cha Laodikia, Tunamwomba Mungu utajiri, na wakati ndani ya mioyo yetu ni Adui yetu, tangu lini mtu akaenda kumwomba adui yake gari, au mali au fedha?? Je! Atampa? Sharti apatane naye kwanza ndipo hayo yote apewe…Wengi leo wanapenda kwenda kumwomba Mungu mali wakati ndani ya mioyo yao wamekorofishana naye, ni matapishi mbele za Mungu, wapo mbali naye, ndani ya mioyo yao kuna kila aina ya uchafu..uasherati, ulevi, rushwa, anasa, mizaha, usengenyaji, pornography, punyeto n.k Biblia inasema ..”
Mathayo 23:25 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang’anyi na kutokuwa na kiasi.
26 Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi.”
Ni lile lile pepo la LAODIKIA linalotenda tenda kazi katika siku hizi za mwisho, kuwafanya watu wajione kuwa wana kila kitu katika roho, wakati ni maskini wa roho..
Bwana Yesu anasema maneno haya… “Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi”.
Ndugu unayesoma ujumbe huu, kamwe usiruhusu hii roho ya uvuguvugu, kila siku yachunguze maisha yako, shetani yupo kazini, kuhakikisha kuwa unakuwa hapo katikati, si moto wala si baridi…Na kama maandiko yalivyotangulia kusema, Ni heri uwe baridi kabisa…ni heri ukawe mwasherati na useme hujaokoka, ni heri uwe mvaaji vimini na mpakaji lipstick na wanja na useme hujaokoka, ni heri uwe unaenda disco kila siku au unaishi na mwanamke/mwanamume ambaye hamjaoana na useme sijaokoka na wala simjui Mungu, wewe adhabu yako siku ile haitakuwa kubwa, kuliko useme mimi nimeokoka na unampenda Bwana wakati bado unavaa vimini, tena bila aibu unauonyesha maungo yako wazi kwenye mitandao, bado unapaka wanja mfano wa Yezebeli na lipstick kiasi kwamba tofauti yako na mwanamziki maarufu wa kidunia hapa nchi hakuna. Unamdhihaki Mungu. Wewe mbele za Mbele za Mungu ni matapishi na kinyaa.
Ni heri ukatubu sasa, na kukusudia kuacha hayo mambo, usiruhusu fikra zako zipotoshwe na mkuu wa ulimwengu huu(shetani) kwa kupitia wakuu wake wa anga..
Waefeso 2: 1 “Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;
2 ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, NA KWA KUMFUATA MFALME WA UWEZO WA ANGA, ROHO YULE ATENDAYE KAZI SASA KATIKA WANA WA KUASI;
3 ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.
4 Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda;”
Unaona? Bwana anaweza kukugeuza ukikusudia kumfuata kweli kweli, unachopaswa kufanya ni kutubu kwa kudhamiria kabisa kuacha dhambi, na kufanya maamuzi ya kutokuwa vuguvugu tena!! Hiyo ndio njia pekee ya kulishinda hili PEPO(MKUU WA ANGA)wa Laodikia…Ni kufanya maamuzi thabiti kwamba kuanzia leo mimi na dhambi basiii….lipstick basi, vimini basi, ulevi basi, uasherati basi, rushwa basi, anasa basi, marafiki wabaya basi, pornography basi,..Huo ndio ushauri wa Bwana alioutoa kwa kanisa la Laodikia…anasimama mlangoni na kubisha, hataingia mpaka wewe umefungua mlango, hatavunja mlango wa moyo wako na kuingia kwa nguvu, anasubiri wewe ufanye maamuzi ya kuacha dhambi, ndipo aingie. Na baada ya hapo fanya hima ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo. Usishirikiane kabisa na MKUU WA GIZA HILI, na Bwana mwenyewe atachukua nafasi ya kuhakikisha haujikwai.
Mada Zinazoendana:
Waebrania 6:4 “Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,
5 na kulionja neno zuri la Mungu, NA NGUVU ZA ZAMANI ZIJAZO.
6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri”.
Neno hili linatuonyesha kuwa kumbe licha ya mtu kuangaziwa nuru ya Mungu, yaani kupewa neema ya kumjua na kumwamini Yesu Kristo ambaye ndio Nuru yenyewe (Yohana 1:4-5), bado anaweza kuonja kitu kingine ndani yake, licha ya kuonja vipawa vya kimbinguni na kufanywa mshirika wa Roho Mtakatifu yaani kwa kuvuviwa karama za Roho kama vile Lugha, unabii, miujiza, utume, uchungaji, ualimu, uinjilisti n.k. mambo ambayo hapo kabla hayakuonekana kati ya watakatifu au kama yalionekana basi ni kwa sehemu ndogo sana, bado anaweza kuonja kitu kingine cha tofauti kabisa,.licha pia ya mtu kuliona Neno zuri la Mungu kama andiko hilo linavyotuambia, yaani Injili ya Yesu Kristo Bwana wetu ambayo kwa hiyo manabii wengi na wenye haki walitamani kuisikia lakini hawakupata neema kama sisi tunavyojua sasa, lakini bado lipo jambo lingine ambalo tunaambiwa mtu anaweza kulionja kwa wakati huu …Na jambo lenyewe KUONJA NGUVU ZA ZAMANI ZIJAZO..
Zamani zijazo ni nini?, Na nguvu zenyewe ndio zipi?
Biblia inapotumia Neno ZAMANI mara nyingi inamaanisha “nyakati fulani” au “kizazi fulani”..Na au kwa lugha rahisi ni “wakati wa Ulimwengu husika”..Hivyo inavyotumia Neno “Zamani hizi” inamaanisha kuwa wakati wa ulimwengu huu…Kwamfano pale Bwana Yesu alipowaambia wanafunzi wake.
“..Hakika nawaambia, hakuna mtu aliyeacha nyumba, au mke, au ndugu, au wazazi, au wana, kwa ajili ya ufalme wa Mungu,
30 asiyepokea zaidi mara nyingi katika ZAMANI HIZI, na katika ulimwengu ujao uzima wa milele. (Luka 18:29).”
Unaona, Hapo alimaanisha asiyepokea zaidi mara nyingi katika ulimwengu huu wa sasa, na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.
Vivyo hivyo inavyosema ZAMANI ZIJAZO..inamaanisha kuwa “nyakati za ulimwengu ujao”..Yaani ulimwengu baada ya huu mbovu tunaoishi kupita.
Sasa tukitazama mifano michache kwenye biblia itatusaidia kufahamu nini maana ya kuonja nguvu za zamani zijazo, embu tutazame ile habari moja ya yule mwanamke mkananayo ambaye Bwana Yesu alimfananisha na Mbwa.Tunasoma:
Mathayo 15: 21 “Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni.
22 Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.
23 Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.
24 Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
25 Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie.
26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.
27 Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao.
28 Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile”.
Sasa katika habari hii sio kwamba Bwana alikuwa anamtukana kumfananisha na mbwa, au labda alikuwa anajaribu kumkatisha tamaa ili amwache, hapana bali kinyume chake alikuwa anamweleza uhalisia wa mambo jinsi yeye alivyo katika ulimwengu wa roho, na si yeye tu peke yake, bali pia watu wote ambao hawakuwa wayahudi kwa kuzaliwa. Na ndio maana hata ukisoma habari utaona japo yule mwanamke alitaka kuzungumza na Bwana lakini Bwana hakumjibu chochote, mpaka alipokuwa anasisitiza sana, ndipo Bwana akalazimika kufungua kinywa na kumkumbusha nafasi yake ni ipi katika majira aliyokuwa anaishi…
Sasa kumbuka hakukuwa na wakati wowote ambao watu wa mataifa walimtazamia Kristo aje kuwaokoa isipokuwa wayahudi tu peke yao. Japo unabii ulishatangulia zamani kwa vinywa vya manabii kuwa utafika wakati ambao mataifa nao watamtumainia huyo masihi, lakini sharti kwanza akataliwe na watu wake, na kuuawa ndipo damu ipatikane ya kuwasafisha watu wote mataifa ili nao wapokee kipawa cha neema kwa namna ile ile moja kama wayahudi, ni lazima kwanza dhabihu itolewe ili iondoe kile kiambazi cha kati kinachowatenga watu wa mataifa na wayahudi, hivyo wakati huo usingekuja kwanza kabla ya watu wake wenyewe kumkataa..
Lakini tunaona huyu mwanamke wa huko Tiro nchi ya mataifa ya kipagani, kwa sasa ni nchi ya LEBANONI kaskazini mwa Israeli, anakuja na kumfuata Bwana kabla ya majira yake na kumwomba ampe neema amponye mwanae ambaye alikuwa amepagawa na mapepo, lakini Bwana akamwambia asubiri kwanza watoto washibe (yaani wayahudi waipate hiyo neema kwanza),Bwana alimwambia sikutumwa ila kwa kondoo wa Israeli waliopotea, lakini yule mwanamke hakusikia badala yake aliendelea kung’ang’ania kana kwamba ni haki yake, mpaka mwisho wa siku baada ya Bwana kuiona imani yake jinsi ilivyokuwa kubwa akampatia alichokuwa anakitafuta kinyume na mipango iliyokuwa imewekwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, tunaona mtoto wake alipona saa ile ile na ule haukuwa tu uponyaji wa mwili wake bali pia hata wa roho yake… mbwa hajasubiria makombo
Sasa Jambo lililofanyika pale katika ulimwengu wa roho, ni kuwa imani ya yule mwanamke ilikwenda mpaka kipindi cha mbeleni kabisa Kalvari siku ambayo Bwana anasulibiwa, Imani ile ikaichukua ile damu iliyokuwa inamwagika katika mishipa ya Emanueli pale Kalvari, ikairudisha sasa mpaka wakati wa nyuma waliokuwepo pale Tiro katika mazungumzo, ikadai haki yake ya ukombozi ambayo ilishapata huko mbeleni kwa mateso yake..Na matokeo yake ikapokea sawasawa na ilivyotaka…
Ni sawa na mtu leo analazimisa alipwe sasa hivi mshahara ambao anapaswa aje kulipwa baada ya miaka 10 , na anang’ang’ania alipwe sasa mpaka analipwa.
Sasa kwa tukio hilo huyu mwanamke tunaweza kusema “Ameonja nguvu za zamani zijazo”..Nguvu za Wakati ambao bado haujafika lakini tayari kashaanza kuyafurahia matunda yake.
Na ndivyo ilivyo hata kwa wakati huu wa kipindi hichi cha mwisho tunachoishi, biblia inaweka wazi kabisa kuwa mtu anaweza kuonja nguvu za zamani zijazo au nguvu za ulimwengu ujao..
Sasa Nguvu za ulimwengu ujao ndio zipi?
Biblia inatueleza huko katika ulimwengu mpya, katika utawala wa amani wa miaka 1000 na Kristo hakutakuwa na magonjwa,wala shida, wala tabu wala vifo.
Isaya 33: 24 “Wala hapana mwenyeji atakayesema, MIMI MGONJWA; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao.
Malaki 4: 2 Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawazukia, LENYE KUPONYA KATIKA MBAWA zake; nanyi mtatoka nje, na kucheza-cheza kama ndama wa mazizini”.
Unaona?, leo hii unapoumwa ugonjwa ambao hautibiki na Yesu anakuponya, hujui kuwa unaonja nguvu za zamani zijazo ambazo udhihirisho wake wote utaonekana katika ulimwengu ujao. Furaha na amani unayoipata sasa katika wokovu, hiyo ni kidokezo kidogo sana, kitakuja kujidhihirisha katika utimilifu wote kwenye huo ulimwengu ujao, Huna hofu ya mauti tena kama zamani kwasababu maisha yako yapo mikononi mwa Bwana, unatumaini sasa la uzima wa milele baada ya kifo, hapo umeonja uzima ambao unakuja huko mbeleni ambapo huko kutakuwa hakuna kufa.
Lakini kwa jinsi tunavyoukaribia mwisho basi fahamu kuwa ndivyo zile nguvu za ulimwengu ujao zitakavyozidi kuongezeka, na kuwa dhahiri katikati ya watu, unapoona wafu wanafufuliwa unadhani ni picha gani hapo Mungu anakuonyesha?,
Yapo mambo ambayo Mungu atakwenda kuyaachia siku hizi za mwisho yahusianayo na nguvu hizi za ulimwengu ujao ili kutimiza ule unabii wa Yoeli 2:28. Na jambo ambalo tutamalizia nalo ni kubadilishwa kwa miili yetu na kuvaa kutokuharibika yaani miili ya milele
1Wakorintho 15.53 “Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.
54 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda”.
Hivyo Bwana anatazamia kuiona Imani thabiti ndani ya watu wake, Imani ya kumwamini Yeye mpaka kufika hatua ya mauti kumezwa na uzima, hayo ni mambo ya ulimwengu ujao lakini ni sharti yaonekane sasahivi,ni sharti yaanzie hapa kwanza..Na ndio maana Bwana Yesu alisema….Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;
26 naye KILA AISHIYE na kuniamini HATAKUFA KABISA hata milele. Je! Unayasadiki hayo? (Yohana 11:25).
Unaona hapo?, yeye aishiye, na sio yeye aliyekufa..Hivyo tunapaswa tufikie kimo cha kumwamini huyu Bwana wa uzima, sisi tunaoishi sasa mimi na wewe, mpaka tuvionje vipawa hivi vya kutokuonja mauti kabisa, Henoko alivifikia kabla ya wakati, Eliya alivifikia kabla ya watu, lakini sisi tulio karibu kabisa na zamani zijazo, ndio tunapaswa tuvifikie, na watakaofikia Imani hiyo ndio wale watakaokwenda na Bwana kwenye UNYAKUO.. Itafika wakati kanisa litafikia hicho kiwango cha mauti kutokuwa na nguvu, litakapofikia hicho kiwango ndio unyakuo utakuwa umefika.
Je! mimi na wewe tumejiandaje?. Tunasema tunangojea Bwana, je! imani yetu kwake ina nguvu ya kuvuta mambo yajayo?..je! na wewe utakuwa miongoni wa watakaokuwa na imani ya kunyakuliwa?
Luka 18: …walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?
Mungu atusaidie sote.
Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine. Na Bwana atakubariki.
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze neno la Mungu, ambalo litatutoa sehemu moja hadi nyingine kiroho..Kama Daudi anavyosema..“Neno lako limesafika sana, Kwa hiyo mtumishi wako amelipenda. (Zaburi 119:140)”..Neno la Mungu ndio chakula chetu, ndio silaha yetu na ndio ngao yetu. Biblia inasema Neno la Mungu ni kama upanga wenye makali pande zote mbili, sio upande mmoja kama haya mapanga tunayoyajua sisi, bali una makali pande zote mbili mfano wa SIME, linakata kuwili.
Waebrania 4: 12 “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote UKATAO KUWILI, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
13 Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu”.
Mtu akichomwa na kisu cha kawaida tumboni au kifuani kitaishia kwenye utumbo tu au mapafu, lakini Neno la Mungu ambalo ni kama upanga, biblia inasema linachoma na kuingia mpaka kwenye viungo vyote vya mwili…na mafuta yaliyo ndani yake, mafuta yaliyozungumziwa hapo ni mafuta yanayotengenezwa ndani ya mifupa (bone marrows), katikati kabisa ya mifupa mikubwa panapotengenezwa chembechembe hai za damu nyeupe, ndipo mafuta hayo yanapotengenezwa, Neno la Mungu kote huko linapita..Na aliishii kupenya huko tu…biblia inazidi kutuambia linapenya hata kizifikia nafsi na roho mahali siri za moyo zinapositirika, na linakata kata na tenganisha na kuharibu kabisa.
Kwahiyo unaweza ukaona Neno la Mungu ni silaha kubwa kiasi gani kama tukiweza kulitumia…
Lakini leo hatutaingia sana huko, bali tutajifunza somo la JINSI YA KUITUMIA VYEMA NEEMA YA MUNGU ILIYO JUU YAKO.
Kwanza ni muhimu kufahamu nini maana ya Neema, NEEMA ni kitu mtu anachopewa ambacho hakustahili kuwa nacho..tafsiri yake inakaribia sana kufanana na ZAWADI lakini sio zawadi..Neema tafsiri yake ni ya ndani kabisa..kwasababu zawadi mtu anapewa kwasababu kafanya kitu fulani kizuri…lakini Neema haiko hivyo, neema ni kitu mtu anapewa pasipo kustahili…kwamfano mtu anaweza kupewa nafasi ya kusomeshwa bure na serikali au mtu binafsi kwasababu pengine huyo mtu hana uwezo wa kujisomesha, au pengine amefaulu sana hivyo anapewa kama offer fulani ya kusomeshwa bure…Lakini Neema haipo hivyo, neema ni pale mtu anapewa nafasi ya kusomeshwa bure pasipo kuangaliwa yeye ni tajiri au ni maskini, au ana uwezo fulani au hana uwezo, amekidhi vigezo au hajakidhi. Hiyo ndiyo tunaweza kusema ni NEEMA.
Na kipawa cha Neema sisi wanadamu hatuwezi kuvitoa, ni ngumu sana kuvitoa kwasababu mara nyingi tunaangalia hali ya mtu ndipo tunamsaidia…Ni nani leo anaweza kwenda kutoa shamba lake na kumpa bure tajiri namba moja duniani? Kwa nia ya dhati kabisa na sio ya kujipendekeza?.. na baada ya kumpa anasahau?..utagundua hakuna au ni wachache sana wanaoweza kufanya hivyo wengi watakwambia..aa kama ni wema si afadhali ningeenda kumpa hilo shamba maskini fulani, kuliko kumpa huyu mtu ambaye tayari ana mamilioni ya fedha, ndivyo mioyo yetu ilivyo sisi wanadamu. Lakini kwa Mungu haipo hivyo, NEEMA yake haina mipaka…haiangalii huyu ni tajiri au ni maskini, haiangalii huyu ni anacho au hana, anastahili kuwa nacho au hastahili.
Ndio maana wokovu na wenyewe ni NEEMA. Ingekuwa Mungu anaangalia hali fulani mtu aliyonayo ndio ampe wokovu, watu wengi wangeukosa..Tunaokolewa kwa NEEMA. Hakuna hali fulani tuliyonayo iliyomshawishi Mungu kutuokoa sisi zaidi ya NEEMA YAKE, …Ni buree kabisa tumeokolewa pasipo sababu. Sio kwa matendo yetu mema tumeokolewa, si kwa kusali kwetu sana tumeokolewa. Hapana.
Waefeso 2:8 “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu”.
Kwahiyo kama NEEMA ipo hivyo basi sio kitu cha kujisifia, kwasababu hakuna mtu kwa ajili ya sababu ndio amestahili au hakustahili kupewa.
Sasa Neema ya wokovu tumepewa wote, lakini pia kuna neema ya VIPAWA AU KARAMA, hii nayo ni vile vile, mtu hapewi kwasababu fulani fulani hivi..kwamba ni mtakatifu sana au kwamba si mtakatifu sana hapana! hii Mungu anampa mtu kama anavyotaka bila sababu yoyote na kama ni hivyo basi haipaswi kuwa ni ya kujisifia kwa namna yoyote, ukiona mtu anajisifia karama au kipawa, ujue huyo mtu bado hajauelewa UKRISTO hata kidogo, au ni mchanga sana kiroho.
Ukiona mtu anajisifia mimi ni mtu wa kusali sana, au mtakatifu sana, au nilimfanyia kitu fulani Mungu ndio maana naweza kufundisha, au ndio maana naona maono, au ndio maana ninaweza kunena kwa lugha, au ndio maana nina upako, nikimwekea tu mtu mikono anapona, tambua huyo mtu bado hajaelewa nini maana ya NEEMA, pengine atakuja kuelewa baadaye lakini kwa wakati huo anaojisifia bado hajaelewa maana ya neema.
Kwa ufupi Vipawa vya Mungu havitokani na juhudi zetu, baada ya kuamini tu na kubatizwa mtu unajikuta tu unapata uwezo wa kipekee katika kufanya jambo fulani la kimungu ndio hapo alikuwa hajui kama ana karama ya uponyaji, hivyo anapomwekea tu mtu mikono anapokea uponyaji n.k lakini sio jambo la kusema ni kwasababu fulani ndio maana ninao huu uwezo sasa..karama za Mungu sio zawadi kwamba tumefanya jambo fulani ndipo Mungu anatuzawadia kama pongezi, haiko hivyo karama za Mungu ni NEEMA unapewa pasipo sababu yoyote. Na Mungu anatoa jinsi anavyotaka yeye, huyu hivi yule vile.
Ukishindwa kuelewa hili, utajikuta unatamani kuwa kama mtu fulani ukidhani kuwa alifanya kajuhudi fulani mpaka kuwa vile, na unajikuta unashindwa kukaa katika nafasi yako, na kuanza kusifia watu, badala ya Mungu.
Sasa tukirudi kwenye kiini cha somo letu linalosema NAMNA YA KUITUMIA VYEMA NEEMA YA MUNGU ILIYO JUU YANGU, tutajifunza namna ya kuitumia vyema neema tulizopewa na kutuletea matokeo makubwa katika viwango vya kimbinguni.
Hebu tusome kwanza mistari ifuatayo na kisha tuendelee..
Luka 21 : 1-4
“1 Akainua macho yake akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina.
2 Akamwona mjane mmoja maskini akitia mle senti mbili.
3 Akasema, Hakika nawaambia, huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote;
4 maana, hao wote walitia sadakani katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo”.
Katika habari hiyo Bwana aliona makundi mawili ya watu: la kwanza ni yule mwanamke mmoja MASKINI, ambaye kwa NEEMA, Mungu aliyompa hakuwa na kingi, lakini alitoa vyote Na kundi la pili aliloliona ni MATAJIRI ambao walitoa sadaka katika sehemu iliyowazidia.
Katika mfano huu, tunaweza tukamfananisha yule mwanamke mjane na wale watu ambao Bwana amewapa vipawa vinavyoonekana kama ni vya chini kabisa katika kazi ya Mungu, ambapo kiuhalisia hakuna kipawa chochote kisichokuwa na umuhimu katika mwili wa Kristo kwamfano kuna wengine hawana kitu lakini utakuta siku zote kanisa lipo katika hali ya usafi, wanahakikisha usafi wa kanisa katika viwango vyote, wanajitoa katika viwango vyote…wengine kazi yao ni kusambaza nakala tu za Neno la Mungu ingawa hawana kitu, lakini kwa bidii zote wanajitahidi..Sasa hawa wanafananishwa na huyu mwanamke ambaye alitoa vyote alivyo navyo kwa Mungu.
Lakini kundi lingine linalojiona lenyewe ndilo la muhimu sana, pengine mchungaji, au nabii au mwalimu ambaye kila siku anaonekana pale madhabahuni akifundisha lakini haitumii karama yake inavyopaswa anaangukia katika hili kundi la pili la matajiri waliotoa katika sehemu ya mali iliyowazidi, kwasababu wao wanadhani kukaa kuonekana na kusifiwa na watu ndio hivyo hivyo ilivyo hata mbele za Mungu.
Sasa siku ya mwisho wale wa mwisho watakuwa wakwanza na wa kwanza watakuwa wa mwisho. Kwasababu katika utajiri wao hawakutoa vyote.
Na mimi leo nakwambia wewe unayesoma ujumbe huu USINIE MAKUU bali jishughulishe na mambo madogo, usitamani yaliyo makubwa wakati haya madogo huyafanyi yanavyopasa…katika haya haya madogo, fanya kwa bidii, toa vyote ulivyonavyo kwa ajili ya Bwana, toa muda wako wote kuhakikisha injili inakwenda mbele hata kama huna fedha, hiyo ndio thawabu yenyewe, usijilinganishe na wale wengine kwasababu Macho ya Mungu sio kama ya kwetu sisi wanadamu.
Usidanganyike na INJILI Kutoka kuzimu zinazosema, utafute kwanza mali ndipo umtumikie Mungu, ndugu yangu Mungu hakuhurumii umaskini wa mwili wako!! Ana uhurumia kwanza umaskini wa roho yako….Ingekuwa anauhurumia kwanza umaskini wa miili yetu, yule mwanamke mjane aliyetoa senti mbili pale pale angeanza kumuhurumia na kusemaa ooo maskini yule mwanamke asitoe chochote maana ni mjane na ni kile tu alichobakiwa nacho…lakini badala yake unaona Bwana alimwacha atoe vyote alivyo navyo kwa ajili ya roho yake, pingine hata chakula cha mchana bibi yule hakupata, ilimradi tu ahakikishe nyumba ya Mungu ipo katika hali nzuri…Bwana hakuuangalia umaskini wake wa pale…Bali aliuangalia UTAJIRI WAKE KATIKA MBINGU MPYA NA NCHI MPYA…Si ajabu tunaweza kwenda kumkuta kule mbinguni ameketi na Bwana katika kiti chake cha enzi.
Kwahiyo hiyo achana na INJILI ZA MAFANIKIO YA KUZIMU!!... injili za kuonyeshwa milki zote za dunia ndani ya dakika moja, Zile shetani alizomuhubiria Bwana Yesu na kumwambia NITAKUPA VITU VYOTE UKIANGUKA KUNISUJUDIA!!. Biblia inasema Bwana hatatupungukia kabisa,
Waebrania 13: 5 “Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.
6 Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?”
Bwana atatupa utajiri kwa wakati wake na kwa kuchuma kidogo kidogo, sio za leo na kesho! Mithali 13:11.
Ni matumaini yangu kuwa NEEMA iliyo juu yako utaitumia inavyopaswa, utaitumia yote..pasipo kuangalia mazingira yoyote ya nje, kwasababu Bwana pia alikupa pasipo kuangalia hali yako. Na Mungu akubariki.
Kama hujampa Bwana maisha yako ayatawale, usipoteze muda, mlango wa Neema upo wazi, ila hautakuwa hivi siku zote, ni vyema ukafanya hivyo sasa, kwasababu saa ya wokovu ni sasa…usidanganyike kuwa watu hawaokoki leo, wokovu unaanzia hapa hapa duniani..hivyo kama Roho anakuhimiza kufanya hivyo sasa usikawie, unachopaswa kufanya ni kutubu dhambi zako zote kwa kudhamiria kuziacha, na baada ya kutubu kwako, basi haraka sana nenda katafute mahali utakapoweza kubatizwa ubatizo sahihi wa kimaandiko, yaani wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO, na Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu atakayekusaidia kushinda dhambi na kuielewa biblia, na hapo utakuwa umezaliwa mara ya pili.
Mungu akubariki sana.
Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine, print ikiwezekana na Bwana akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
USIMFANYIE JEURI ROHO WA NEEMA.
UMEIZALIA MATUNDA MIAKA 4 YA NEEMA ULIYOPEWA?