Kuota umeachwa na gari, Maana yake ni nini?
Hii ni ndoto inayowapata watu wengi sana.Hususani wale ambao walishaokoka, lakini mambo mengine ya kidunia yanawasonga sasa hivi..Au walisharudi nyuma kabisa na kuacha wokovu
Ndogo hii inakuja katika maumbile tofuati tofauti wengine wanaota wameachwa na ndege, wengine wanaota wameachwa na wenzao ambao walikuwa wanakwenda pamoja, lakini wengi wao wanaota wameachwa na gari walilokuwa wanasafiria.
Kwa mfano mtu mmoja alinihadhithia ndoto hii, ambayo rafiki yake aliiota ikawa inamsumbua sana..
Aliota alikuwa kwenye basi anasafiri, sasa lile basi likafika mahali kwenye foleni, na yeye baada ya kuona vile limesimama pale, akaamua kushuka kidogo, na aliposhuka tu lile gari likaanza safari, anasema akaanza kulikimbilia, kumbe wakati analikimbilia kulikuwa na watu wengi nao wanalikimbilia lile gari, mchanganyiko wamama, watoto, na watu wengine n.k. Lakini baadaye yeye akajitahidi kwa nguvu sana kuliwahi akafanikiwa kuingia lakini kwa shida sana, na alipofika ndani akakuta siti yake imeshakaliwa na mtu mwingine..Ikimbidi ajikalie tu mwenyewe pale pembeni, lakini baada ya muda mfupi mzee mmoja akatokea akamsukuma atoke hata pale alipokuwa amekaa, akiwa hana sehemu ya kukaa kwa bahati nzuri akaona siti moja ipo wazi pembeni yake akaenda kuikalia na muda huo huo akashtuka..
Nilipo hoji nikagundua kuwa mtu huyo alikuwa ameokoka lakini baadaye alirudi nyuma, amesongwa na mambo ya ulimwengu huu..Na pale Mungu alikuwa anamwonyesha mwenendo wake jinsi ulivyo alipoona anakawia kukipata kile alichokuwa anakitafuta katika njia yake ya wokovu akaamua kwenda kukitafuta katika mambo ya ulimwenguni..Na hiyo itamgharimu kwasababu upo wakati atatamani kurudi lakini itakuwa ngumu sana kwake kwasababu wokovu sio safari ya kujaribu jaribu kama yule mke wa Lutu alivyofanya, aligeuka mara moja tu, na saa hiyo hiyo akageuka kuwa jiwe la chumvi.
Ikiwa na wewe ni mfano wa mtu kama huyu umeota ndoto ya namna hii umeachwa na basi ujue huo ni ujumbe kamili kutoka kwa Mungu, kuwa unaupoteza wokovu wako, na kuwa ukiendelea katika hali hiyo inayoendelea sasahivi ya kujitenga na wokovu, au kusongwa na mambo ya ulimwengu basi hautaupata tena daima na nafasi yako atapewa mwingine..
Lakini kama wewe hujaokoka kabisa yaani Bwana YESU hajayabadilisha maisha yako, wala huna habari na Mungu.. wewe umekuwa mkristo jina tu, au Muislamu, au huna dini kabisa..Hapo ni Mungu anakuonyesha jinsi gani inavyoogopesha na inavyosikitisha mtu unapoachwa safarini..Sasa jiulize, kwa mtu ambaye haujaanza kabisa safari, yeye atakuwa katika hofu nyingi kiasi gani?..Ndivyo ilivyo hali yako wee Upo katika dhambi, upo mautini, mbingu ipo mbali na wewe.
Sikia sauti ya Kristo, inayokuambia njoo kwangu leo.. Uanze naye safari njema ya kuelekea ufalme wa mbinguni. Kukutana na ujumbe kama huu si bure, Ni Mungu anazungumza na wewe.
Yesu anasema..
Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.(Yohana 14:6)..
Ikiwa unataka na wewe kwenda mbinguni basi YESU ndiye njia..wala hakuna mwingine.
Vile vile biblia inasema..
Isaya 35:8 “Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo”.
Dunia hii inapita na mambo yake..Utauhangaikia huu ulimwengu mpaka lini, Ukifa leo, ni nani atakuwa mgeni wako huko uendako?. Ni nani atakayekupokea, utaulizwa safari yako ilikuwa ya kuelekea wapi, utajibu nini..Kwanini leo usichukue tiketi yako mkononi, uanze maisha mapya na Bwana Yesu..Kwasababu ni kweli atayabadilisha maisha yako na wewe mwenyewe utaona ni jinsi gani umeianza safari njema, ya uhakika na yenye matumaini..Ulevi, uzinzi, starehe, sema leo ni mwisho ninaamua kumgeukia Kristo.
Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.
EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.
ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.
AMEN.
Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.
Ubarikiwe sana
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUZA KITU.
PENGINE MUNGU ALISHASEMA NAWE KWA NJIA HII.
KUOTA UPO UCHI.
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
USHUHUDA WA RICKY:
Swali: Bwana Yesu alikuwa na maana gani kusema.. “sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje”? Ni kwa namna gani atatupwa nje? Na ni kwanini atupwe nje na sio chini?
JIBU: Tusome huo mstari…
Yohana 12:31 “Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo; sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje.
32 Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu. ”
Kama ukichunguza vizuri hapo utaona anatumia neno “ATA” na si “ALI”.. yaani atatupwa na sio alitupwa au anatupwa..Ikionyesha kuwa ni kitendo kijacho ambacho bado hakijatokea..
Kumbuka tena hapo anasema atatupwa NJE, na sio atatupwa CHINI.. Shetani alishatupwa chini zamani sana, Kile kitendo cha yeye kuasi kule mbinguni biblia inasema kilimsababishia atupwe chini yeye pamoja na malaika zake (soma Ufunuo 12:7-10), Hivyo akawa ameganda tu hapa duniani kwenye giza nene, bila shughuli yoyote, wala tumaini lolote, akisubiria siku yake ya maangamizo ifike,apotee.. Mpaka sisi tunakuja kuumbwa, yeye alikuwa bado yupo hapa hapa anatazama tu, mwanadamu akimilikishwa kila kitu..
Lakini Adamu alipoasi, ndipo shetani akapata nafasi ya kuingia ndani ya ufalme ambao ulikuwa ni milki ya mwanadamu tu, Adamu akaiuza ile hati yake ya umiliki kwa shetani..Na tangu huo wakati shetani akapata nguvu akawa na mamlaka juu ya mambo mengi sana katika huu ulimwengu, akawa na uwezo hata wa kuwaendea wafu waliokufa(ikiwemo watakatifu) na kuzungumza nao kama alivyofanya kwa Samweli, akawa na uwezo hata wa kuzuia maombi ya watakatifu, yasimfikie Mungu …Yaani kwa ufupi japo watakatifu walikuwa wanalindwa na Mungu..lakini bado shetani alikuwa na uwezo fulani juu yao..
Sasa wakati ulipofika wa Mungu kuirudisha ile hati ya umiliki kwake, Ndipo akamletea mwanadamu aliyefanana na Adamu, ndiye Bwana wetu YESU KRISTO.. yeye alikuja kufanya kazi moja, na kazi yenyewe ilikuwa ni KUMFUKUZA SHETANI atoke ndani ya milki ya wanadamu..
Lakini si kwa wanadamu wote, bali wale tu watakaomwamini na kumpokea..
Na ndio maana sasa utaona Bwana Yesu anasema hapo.. sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje”? Ikiwa na maana bado kitambo kifupi tu atakwenda kutupwa nje ya milki ya utawala wa watakatifu..Na tukio hilo lilikuja kutimia siku ile, pale KALVARI Bwana Yesu alipokufa na kuchukua funguo zote za uzima, pia na za kuzimu na mauti (Ufunuo 1:18).
Sasa tangu huo wakati hali yake shetani ikarudia kama mwanzoni alipokuwa pale Edeni kabla ya Adamu kuasi, akawa hana nguvu yoyote kwa wale watu waliomwamini Yesu na kuoshwa kwa damu yake, akawa hawezi kujiamulia tena kitu chochote juu yao, hawezi kuwaendea wafu na kuzungumza nao tena, hawezi kumdhuru mtu yoyote wa Mungu, ikiwa Mungu hajaruhusu.
Hivyo leo hii mtu aliyeokoka, hahitaji kuogopa wachawi, hahitaji kuogopa mapepo au majini, hahitaji kuwa na wasiwasi labda shetani atamuua, hahitaji kuwa na hofu labda maombi yake yamezuiliwa sehemu fulani hapo juu ya wakuu wa anga kama Danieli.. Sasa hivi shetani hawezi kufanya hivyo kwa mtu aliyeokoka kweli kweli.
Lakini kama upo nje ya Kristo..basi Maisha yako yapo hatarini..Wewe unapaswa uwe na hofu ya kila kitu, hukosei kuwaogopa wachawi, au majini, au wanadamu..kwasababu huna ulinzi wowote wa Mungu na shetani bado yupo ndani ya maisha yako, kila siku akikupangia njama za kukuangamiza..hivyo upo sahihi kabisa kuwaogopa kikweli kweli.
Ni neema za Mungu tu zinakushikilia ili utubu ndio maana upo hai.. Mpe Kristo Maisha yako kama hujampa, Uwe salama.
Ubarikiwe.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789 001312.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo: