Nini maana ya Kuota unatembea juu ya maji ?.
Kama tunavyojua stori ya mtu mmoja katika biblia ambaye alirekodiwa kutembea juu ya maji, ni Bwana wetu Yesu Kristo peke yake.
Lakini swali la kujiuliza, ni kwanini aamue kufanya vile? Kulikuwa na umuhiimu gani wa yeye usiku ule kutembea juu ya maji? Je, ni kwasababu alikuwa anawahi mahali fulani, au alikuwa anawaonyesha tu wanafunzi wake ukuu wake..
Tunafahamu kuwa kila jambo alilolifanya Bwana Yesu, lilikuwa na somo la kutufundisha sisi, na wala sio kutuburudisha..Hata kitendo cha kupaa kwake tu, kilibeba ujumbe mzito kwetu sisi.
Ukifahamu hilo utajua pia sababu ya kwanini wewe unaota ndoto za mara kwa mara unatembea juu ya maji.
Sasa kabla Bwana Yesu usiku ule kutembea juu ya maji utaona alitumia masaa mengi sana kule mlimani katika kusali, hakutembea kwanza bila kuwepo uweponi mwa Bwana muda mrefu..ndipo baadaye sana, akaondoka kuwafuata wanafunzi wake mle baharini, na alipoikaribia boti walimwona kwa mbali wakaogopa lakini Petro akajitia ujasiri akaomba amfuate kule alipo. Bwana hakumkatalia, akamwambia Njoo, ndipo Petro akaanza kutembea, akapiga hatua kadhaa, akadhani ni rahisi kama anavyofikiria, Lakini wimbi lilipomjia akaogopa akaanza kuzama..
Lakini Bwana Yesu alimwambiaje?, Embu Tusome..
Mathayo 14:25 “Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari. 26 Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu. 27 Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope. 28 Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. 29 Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu. 30 Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe. 31 Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka”?
Mathayo 14:25 “Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari.
26 Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu.
27 Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope.
28 Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.
29 Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu.
30 Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe.
31 Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka”?
Sasa kama ukiitafakari hiyo Habari kwa karibu utagundua somo Kristo alilokuwa anawafundisha wanafunzi wake, ni kuwa YOTE YAWEZEKANA KWA MTU ASIYEKUWA NA SHAKA..
Lakini sasa hayo mashaka mtu anayaondoaje..ndipo baadaye alikuja kuwaambia wanafunzi wake.. jinsi ya kuondoa shaka rohoni..
Mathayo17:21 [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.
Na ndio maana kabla ya tukio lile Bwana alikuwa katika sala muda mrefu..
Hivyo uotapo ndoto za wewe unatembea juu ya maji, au unakimbia juu ya maji au unapaa wakati mwingine.. Ujue ni Mungu anakukumbusha Habari ile ya Kristo kuwa yote yanawezekana..Lakini haiwezekani kirahisi rahisi tu bali kwa kufunga na kuomba (yaani kwa kujiweka karibu na Mungu kwa wakati mwingi uwezavyo.)
Sasa ikiwa wewe ni mwenye dhambi, hakuna lolote litakalowezekana kwako lile ambalo haliwezekani kibinadamu..Ikiwa Kristo yupo mbali na wewe (yaani hujamkabidhi Maisha yako)..Huwezi kufanya kila kitu..
Vilevile ikiwa umeokoka, na huna muda Mungu, yaani hata huwezi kujitengea muda kusali hata lisaa limoja kwa siku, husomi Neno, huna bidii ya kuishi maishi yampendezayo Mungu,..kamwe huwezi kutenda yale yasiyowezekana kwa macho ya kibinadamu.
Hivyo kama hujaokoka, ujumbe huu ni wako, mkaribishe Yesu maishani mwako leo..Hapo ulipo dhamiria kwanza kuacha mienendo yako yote ya dhambi, kisha ndio uje uombe rehema Mungu akusamehe, kama hujadhamiria basi ni heri usimwombe Mungu msamaha, kwasababu utakuwa unamdhihaki..Geuka kivitendo, ndipo umwomba Mungu rehema na yeye atakusamehe,..
Uthibitisho kuwa amekusamehe, ni ile amani atakayoileta ndani yako..Na kuanzia hapo anza kuishi maisha ya kikristo..nenda kabatizwe ikiwa hujafanya hivyo, na Roho Mtakatifu atakuja juu yako kukusaidia kutimiliza yale ambayo yatakuwa yamesalia.
Vilevile ikiwa wewe ulikuwa tayari ndani ya Kristo lakini ulizembea zembea wakati wako ndio huu wa kuyatengeneza upya, ukizingatia hizi ni nyakati za mwisho..ongeza viwango vyako vya maombi, funga, jifunze biblia sana, kuliko kitu kingine uwezacho kujifunza, pia ongeza viwango vyako vya Maisha ya utakatifu..Na wewe mwenyewe utaona jinsi utakavyoweza kufanya visivyowezekanika kirahisi sana.
Mambo ambayo kwa namna ya kawaida yaliyonekana hayawezaniki kwa mtu kama wewe kuyafanya lakini ukiitii hiyo kanuni ya Kristo hapo ndipo watu watakaposhanga kukuona ukifanya..ndio tafsiri ya ndoto yako..lakini kumbuka tena neno hili..
[Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga. (Mathayo17:21) shalom.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Mada Nyinginezo:
KUOTA AJALI, KUNAMAANISHA NINI?
KUOTA MAFURIKO,KUOTA MAJI MENGI,KUOTA MAWIMBI.
KUOTA UNAOLEWA/UNAOA.
KUOTA UNAKOJOA KITANDANI.
TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Fuatilia kisa hii,
Binti mmoja akiwa bado mdogo wa miaka 9 aliwauliza wazazi wake, Je! Wazazi wangu Niishi maisha gani ili nifanikiwe,
Wazazi wake wakamwambia, mwenetu, wewe huihtaji kwenda shule kupata elimu, wala huna haja ya kujua jambo lingine lolote kwa wakati huu wewe tafuta pesa kwa namna yoyote ile utakayoona ni rahisi, ukishazipata basi maisha yako yatakuwa sawa..
Ndipo Yule msichana akalizingatia hilo akaendelea kukua, hakujali elimu yoyote ya maisha mpaka alipofikisha umri wa miaka 12 akajiingiza mtaani, Na kule mtaani alikutana na makahaba wakamshawishi ajiingize katika shughuli kama za kwao za kujiuza, atapata fedha kirahisi..Ndipo Yule msichana kwasababu alishauriwa hivyo hivyo pia na wazazi wake, akaona ni ushauri mzuri na yeye pia akajiingiza kwenye biashara hiyo na kweli akaanza kupata fedha, na alipowaletea wazazi wake fedha zile, na kuwaeleza jinsi alivyozipata, basi wale wazazi wake, hawakumuonya kwa lolote japo walijua madhara ya vitendo vile, wakamwacha aendelee, ili awe anawaletea fedha nyingine nyumbani..
Na Yule binti aliendelea kuifanya ile kazi kwa bidii kwasababu aliwaonea huruma pia wazazi wake wasije wakaishi maisha ya shida,..aliendelea hivyo kwa miaka, mpaka akabobea katika hiyo kazi, Na kila mwisho wa mwezi anawapelekea wazazi wake fedha nyingi sana..
Lakini siku moja alianza kuumwa ghafla , hali yake ikabadilika sana, wazazi wake walivyoona vile walijua kabisa mwanao kwa dalili zile lazima atakuwa amesha athirika, lakini kwa hofu hawakumshauri akapime afya yake, bali walimfariji tu, wakimwambia hiyo itakuwa ni hali ya magonjwa ya kawaida tu, uwe unakunywa pain-killer hali itakuwa sawa…endelea tu kutafuta fedha mwenetu..(wakisema hivyo kuogopwa binti asije kujua akaacha hiyo kazi ya kuwaletea fedha).
Lakini Yule binti hali yake ilipozidi kuwa mbaya, mpaka akawa hawezi hata kutembea, ikabidi yeye mwenyewe siku moja, ajiamulie kwenda hospitali kupima, na alipopima afya yake,akagundulika kuwa ana virusi vya ukimwi..
Baada ya hapo akaanza kulia sana, akajutia maisha yake,akitazama na umri wake, ingawa mwenyewe mwenyewe tu alishasikia sikia kuhusu gonjwa hilo lakini hakulitilia maanani sana, kama angelisikia kutoka kwa wazazi wake waliomzaa…akaenda kuwaeleza wazazi wake, akiwahadithia sababu zilizomfanya apate ugonjwa ule, alizoelezwa na daktari, ndipo Akawauliza wazazi wake, kama je walijua kazi ile ingeweza kumletea madhara makubwa kama yale huko mbeleni.. ndio walikiri waziwazi ndio tulijua kuwa utaathirika, lakini tuliogopa kukwambia..Mtoto akasema nyie kama wazazi ulikuwa ni wajibu wenu kunionya mimi kama mtoto madhara yake kwani mimi nilikuwa ni bado sijajitambua, mmesubiri mpaka mimi mwenyewe nimejigundua mpaka dakika hii hali imekuwa mbaya,..Je! ni kweli mlikuwa mnanipenda au mlikuwa mnanitumia tu?
Habari hiyo inatufundisha nini?
Tukiona mpaka leo hii, Mkuu wa nchi anatangaza watu WATUBU DHAMBI ZAO, kwasababu wamemkosea Mungu, na wananchi pia wanafanya hivyo..Halafu sisi tunaojiita ni manabii na mitume, na watumishi, na waalimu hatukuwahi kuwaonya watu kabla ya mambo haya, kuwa ni sababu ya dhambi zetu, mpaka wamegundua wao wenyewe..basi tujue tuna dhambi kubwa mbele za Mungu..
Watu wasiomjua Mungu leo hii wanagundua tatizo, ni nini?.. kuwa ni DHAMBI lakini sisi, miaka nenda rudi, tunawahubiria tu injili za mafanikio, na huku tunajua dhambi bado ipo mioyoni mwao, tunawahubiria amani tu, hatuwaonyi dhambi zao, kisa tunaogopa hawataleta zaka, hawataleta sadaka…Ni nani aliyekuambia utumishi wa Mungu ni zaka tu na sadaka?.
Tujue kuwa watu wanapokwenda kumtafuta Mungu, wanamaanisha kweli kutafuta uzima wa nafsi zao, lakini wewe unapowaelekeza kwenye biashara, na mafanikio, na mwisho wa siku wanagundua kuwa hayawezi kutatua matatizo yao..Wanakuonaje wewe nabii, au mtume au mwalimu?
Hutaki kuwaonya watu kuwa hii dunia inakwenda kuisha na siku si nyingi unyakuo utapita na mpinga-Kristo atanyanyuka, na ataleta dhiki kubwa duniani ambayo hajiwahi kutokea kwa watu ambao watakuwa wameachwa,..kinyume chake sisi tunawahubiria mwaka huu watakwenda China kufanya biashara, na watashusha makontena, watabarikiwa..Hayo makontena wanayokwenda kushusha China mwaka huu yako wapi?.
Hatuwahubirii kuwa yapo mapigo ya vitasa saba, ambayo Mungu atayaleta juu ya dunia nzima kipindi sio kirefu kwa wale wote wasiomcha Mungu, kiasi kwamba magonjwa haya tunayoyaona leo hii, yatakuwa si kitu kulinganisha na hayo yanayokuja huko mbeleni..Ili watu watu watubu leo waache dhambi,tupone!..lakini sisi Tupo busy kuwatabiria tu majumba na magari. Ni nani aliyekuambia mioyo yao ipo kwenye magari na majumba?
Hutaki kujua hali za watu rohoni kuwa mtu akifa leo kama hajaokoka, atakwenda kuzimu, matokeo yake tuwasisitize watengeneze mambo yao na Mungu hata ikitokea wamekufa ghafla, basi wanakuwa upande salama, upo bize, kuanzia mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka, kuwatabiria mema, angali wapo bado katika dhambi. (Mbaya zaidi ni kwamba tunaujua ukweli lakini hatutaki kuwaambia watu). Tafakari ingekuwa ni dada yako wa damu, au ndugu yako..
Na wewe pia unayehubiriwa jiulize, Kristo akirudi leo, utakuwa katika upande upi? Usiridhishwe tu na mahubiri ya vichekesho, na burudani, ndugu ijali roho yako, siku hizi ni za mwisho. Haya tuyaonayo sasa ni mwanzo wa utungu tu…Yanakuja mengine makubwa zaidi na ya kutisha kuliko haya biblia imeshatabiri.
Lakini wakati unafika, ambao Mungu ataleta hukumu juu ya manabii wote wa Uongo, na Watumishi wote, wanaolitumia jina la Mungu isivyopasa..wakati huo unafika, nao upo karibu sana..
Yeremia 23:14 “Katika manabii wa Yerusalemu nimeona neno linalochukiza sana; hufanya zinaa; huenenda katika maneno ya uongo, HUTIA NGUVU MIKONO YA WATENDAO MAOVU, HATA IKAWA HAPANA MTU AREJEAYE NA KUUACHA UOVU WAKE; wote pia wamekuwa kama Sodoma kwangu, na wenyeji wake kama Gomora. 15 Basi Bwana wa majeshi asema hivi, katika habari ya manabii, TAZAMA, NITAWALISHA PAKANGA, nitawanywesha maji ya uchungu; kwa kuwa kutoka kwa manabii hao wa Yerusalemu kukufuru kumeingia katika nchi yote”.
Yeremia 23:14 “Katika manabii wa Yerusalemu nimeona neno linalochukiza sana; hufanya zinaa; huenenda katika maneno ya uongo, HUTIA NGUVU MIKONO YA WATENDAO MAOVU, HATA IKAWA HAPANA MTU AREJEAYE NA KUUACHA UOVU WAKE; wote pia wamekuwa kama Sodoma kwangu, na wenyeji wake kama Gomora.
15 Basi Bwana wa majeshi asema hivi, katika habari ya manabii, TAZAMA, NITAWALISHA PAKANGA, nitawanywesha maji ya uchungu; kwa kuwa kutoka kwa manabii hao wa Yerusalemu kukufuru kumeingia katika nchi yote”.
Siku zote tujifunze kuiogopa ghadhabu ya Mungu na tujiepushe nayo na wengine pia.
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
WAKAMTUKANA MUNGU, WALA HAWAKUTUBU.
JINSI NEEMA YA MUNGU ILIVYOKUWA KUBWA KWA MKE WA LUTU.
Chapa zake Yesu ni zipi hizo?
EWE MKE! HESHIMA YAKO IPO KWA WAKWE ZAKO.
ANGALIA UZURI WAKO, USIGEUKE KUWA KITANZI CHAKO.
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
Kwanini yule mtu afe kwa kuliwa na simba?
Shalom karibu tujifunze Biblia, kwasababu Neno la Mungu ndio mwanga wa njia zetu na taa iongozayo miguu yetu.
Ni wapi mahali sahihi pa kulipa zaka je ni kanisani, au kwa mayatima au kwa wajane?..Hili ni swali linaloulizwa na wengi..Leo kwa neema za Bwana tutajifunza..
Andiko linalofahamika na wengi wetu lihusulo mahali sahihi pa kulipa zaka ni hili..
Kumbukumbu 26:12 “Utakapokwisha kutoa zaka, katika zaka zote za maongeo yako mwaka wa tatu, ambao ndio mwaka wa kutolea zaka, umpe zile zaka Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, wapate kula ndani ya malango yako na kushiba;”
Sasa kabla ya kuingia kwa undani kulielezea andiko hili..ni muhimu kwanza kufahamu mambo machache yafuatayo..
Kwa mtu aliyeokoka na kuitambua Neema ya Yesu kikweli kweli, Zaka ni jambo la lazima ingawa sio la sheria.(Mathayo 23:23)
Ipo michango mingine tofauti na Zaka..ambayo ni ya muhimu pia kwa kila aliyebadilishwa na kuwa mkristo kuitoa…na michango hiyo ni CHANGIZO, na SADAKA…Hii miwili ni tofauti na Zaka…Zaka ni sehemu ya Kumi ya Mapato…Changizo ni chochote ambacho mtu anaweza kumtolea Mungu kama mchango, (hakina sheria, wala kiwango maalumu)..na sadaka ni dhabihu mtu anayomtolea Mungu wake, inaweza kuwa sadaka ya shukrani, ya malimbuko, au ya ombi ya kutimiziwa hitaji fulani.(Warumi 15:26, 1Wakorintho 16:1 )
Jambo la tatu la kufahamu ni kwamba..Zaka/fungu la 10…Ndiyo sadaka inayopaswa ichukuliwe kuwa ya kiwango cha chini kuliko hizo nyingine zote… haipaswi kuchukuliwa kama ni adhabu wala kitu kikubwa kuliko vingine…(maana yake changizo na sadaka zinaweza kuzidi mara nyingi sana Zaidi ya zaka).
Sasa tukirudi kwenye swali letu..Je! zaka inapaswa itolewe wapi..JIBU NI RAHISI INAPASWA ITOLEWE KANISANI TU!!…Na si penginepo!..Michango mingine inaweza kwenda kwa masikini, kwa wasio jiweza ambayo hiyo inaweza ikawa hata ni nyingi sana kuliko zaka..Kwa mfano mtu aliyepata mapato ya laki moja, maana yake hapo zaka ni elfu 10..kilichosalia ana uhuru nacho kusaidia kiwango chochote kwa wasiojiweza na masikini wa mitaani, kama atawapa elfu 50 au Zaidi ya hapo ni mapenzi yake mwenyewe..na tena ni vizuri Zaidi…Kwasababu ndivyo atakavyojiwekea daraja zuri Zaidi la kubarikiwa kama maandiko yanavyosema heri kutoa kuliko kupokea, lakini ZAKA ni kanisani tu!.
Sasa swali linakuja..kwanini hapo juu kwenye Kumbukumbu la Torati, maandiko yanasema zaka iliwe na maskini, mjane, yatima na Mlawi?.
Jibu rahisi ni kwamba katika Agano la kale…Kanisa la Mungu lilikuwa ni jamii nzima ya wana wa Israeli…Wote waliovuka bahari ya shamu hilo ndilo lililokuwa kanisa la kwanza yaani uzao wa Ibrahimu…Hivyo Zaka zililihusu kanisa hilo lote kwa ujumla…ambapo ilikuwa inawekwa kwa utaratibu maalumu kwamba walio wajane kweli kweli ambao hawana watu wa kuwasaidia, Pamoja na walawi(yaani makuhani na uzao wao) ambao hawa hawakuwa na shughuli yoyote Zaidi ya kuhudumu katika nyumba ya Mungu…pamoja na mayatima wasio na ndugu wala wazazi na wageni walio wayahudi..Kwa utaratibu maalumu Zaka waligawanyiwa wao.
Hivyo kwa ujumla hilo ndilo lililokuwa kanisa la Mungu la kwanza…Utauliza ni wapi wana wa Israeli walijulikana kama ni kanisa…Soma, Matendo 7:37-38. Hivyo zaka ziliwahusu wana wa Israeli tu.. yaani maskini, walawi, wajane, na mayatima na wa Israeli tu..hazikuwahusu maskini waliokuwepo Babeli, wala wajane wa Ashuru.
Na katika Agano jipya…Zaka zinalihusu kanisa la Kristo peke yake…na si penginepo…Yaani maana yake ni kwamba (wajane,yatima, maskini, na walawi ambao kwasasa wanawakilisha wachungaji, waalimu,manabii, mitume na wote wanaohudumu madhahabuni, au wanaoifanya kazi ya Mungu kwa ujumla wake)..Hao ndio wanaopaswa kunufaika na zaka zitolewazo…na si wajane wa mitaani, au maskini tunaopishana nao barabarani…hao wanaweza kupewa michango ambayo mtu anaweza kutoa kama apendavyo..na pia inaweza ikazidi hata kiwango cha zaka..sio dhambi….lakini zaka ni kwa KANISA TU!. Maana yake kwa wajane ambao ni wakristo waliopo pale kanisani ambao ni wajane kweli kweli, wamedumu katika utakatifu na kuosha watakatifu miguu kama maandiko yanavyosema katika…1Timotheo 5:9-16,..Na mayatima ni hivyo hivyo…wale ambao ni wakristo au wazazi wao walikuwa ni wakristo walioshuhudiwa na kanisa.
Sasa swali linakuja..je nikipata zaka nimtafute Yatima fulani au mjane fulani pale kanisani nimpe, au nimtafute mchungaji pale kanisani au nabii nimpe kwa siri, nitakuwa tayari nimeshalipa Zaka??…Jibu ni hapana!..hupaswi kwenda kumpa mchungaji binafsi zaka yako, wala yatima binafsi, wala mjane..Kama unataka kufanya hivyo basi unaweza kufanya kama mchango tu kwao, yaani ukawatafuta wao binafsi kwa fedha yako ukawapa lakini zaka usifanye hivyo…
Tayari tumeshapewa utaratibu katika biblia wa namna ya kulipa zaka..
Tusome…
Matendo 4: 32 “ Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika. 33 Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote. 34 Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa, 35 wakaiweka miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya alivyohitaji”.
Matendo 4: 32 “ Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika.
33 Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote.
34 Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa,
35 wakaiweka miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya alivyohitaji”.
Umeona hapo?..wote walipeleka sadaka zao na zaka zao miguuni mwa mitume…Na ndipo Mitume wakawa wanawagawia kila mtu kama alivyohitaji (maana yake kila mkristo mwenye mahitaji, na sio maskini wa barabarani), Hivyo wenye mahitaji walikuwa wanachunguzwa kwanza wenye vigezo vya kimaandiko vya kupewa ndipo wanapewa sio tu kila mtu ambaye anashida anapewa tu hapana!..palikuwa na utaratibu…Na kama wewe ni msomaji mzuri wa biblia utakuja kuona kuwa hata bado huo mfumo ulikuwa ni ngumu kuusimamia mitume..mpaka wakaweka watu wengine 7 wenye hekima Zaidi, ambao wataweza kujua na kusimamia ni nani anastahili Zaidi na nani hastahili, na ni nani anapaswa apate Zaidi na nani asipate, Ndio wakapatikana wakina Stefano huko huko ambao ndio walikuwa mashemasi…Sasa Mashemasi kazi yao ndio hiyo kusimamia bajeti ya kanisa na kuigawanya kwa watu kulingana na katiba ya kimaandiko.
Kwahiyo kwa hitimisho katika Agano la kale na agano jipya…hakuna mahali popote zaka walipelekewa watu wa nje ya kanisa…na kulikuwa na utaratibu maalumu. Hivyo kama kuna mtu umemwona ana uhitaji labda umekutana naye barabarani, au mtaani au popote pale nje ya kanisa mpe kwa kadiri uwezavyo lakini si zaka..zaka yako peleka katika kanisa lako unaloshiriki(hiyo inawahusu watakatifu)…Huko kama ni kanisa la kweli la Kristo wanaujua utaratibu wa kimaandiko wa namna ya kuigawanya.
Bwana akubariki..
UFANYE NINI KAMA MKRISTO WAKATI HUU WA JANGA LA CORONA?
UFUNUO:Mlango wa 6-( Maelezo ya Muhuri saba)
NAO WAKADHANI YA KUWA YUMO KATIKA MSAFARA;
Biblia inamaanisha nini inaposema “Tusitweze unabii”?
Kutubu sio kuomba rehema kwa Mungu!.
Jina la Bwana libarikiwe.
Ipo tofauti kati ya kutubu na kuomba rehema…Wengi tunaomba rehema lakini hatutubu…Ndugu, Rehema bila Toba ni bure!.
Kuomba rehema hakuna tofauti na kuomba msamaha…Unapomwomba Mtu msamaha hapo ni umemwomba rehema…(akurehemu), Lakini Toba haiombwi, toba ni inafanywa na wewe.
Sasa Toba/kutubu ni nini?
Toba maana yake ni KUGEUKA NA KUCHA KILE ULICHOKUWA UNAKIFANYA. Ulikuwa unakwenda mbele ghafla ukaghairi ile njia uliyokuwa unaiendea na kugeuka nyuma na kurudi ulikotoka au kuiendea njia nyingine kutokana labda na sababu fulani ambazo unazijua wewe….sasa hicho kitendo cha kugeuka na kughairi ndicho kinachoitwa Toba. Lakini kuomba msamaha sio kutubu.
Ili kuelewa tofauti Zaidi tofauti ya vitu hivi viwili..tafakari mfano ufuatao.
Mzazi kamwita mwanawe ili amtume mahali, lakini yule mtoto akamfanyie jeuri mzazi wake yule na kumtusi na akaenda kuendelea na michezo…Wakati yupo njiani anaelekea kwenye michezo njiani, dhamiri ikamchoma akagundua amefanya kosa…Hivyo akaghairi safari yake ya kwenda kwenye michezo, akarudi kwa mzazi wake..akampigia magoti akamwambia nisamehe Mama kwa jeuri yangu nimekosa, nipo tayari kwenda kule ulikonituma.
Sasa mtoto huyo pale alipokuwa njiani na kughairi njia yake na kugeuka na kurudi kwa Mama, Hapo ndipo alipotubu…Na hatua ya pili kwenda kumwomba mama yake msamaha kwa jeuri yake ile pale ndipo alipoomba Rehema. Hivyo umeona tofauti ya mambo hayo mawili?…Hauwezi ukasema umeomba rehema na huku hujatubu…Toba inaanza ndipo ndipo kuomba rehema kunafuata.
Ndio mfano ambao Bwana Yesu aliutoa juu ya wale wana wawili..Tusome
Mathayo 21:28 “Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo nenda kafanye kazi katika shamba la mizabibu. 29 Akajibu akasema, Naenda, Bwana; asiende. 30 Akamwendea yule wa pili, akasema vile vile. Naye akajibu akasema, Sitaki; baadaye akatubu, akaenda. 31 Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa pili…”
Mathayo 21:28 “Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo nenda kafanye kazi katika shamba la mizabibu.
29 Akajibu akasema, Naenda, Bwana; asiende.
30 Akamwendea yule wa pili, akasema vile vile. Naye akajibu akasema, Sitaki; baadaye akatubu, akaenda.
31 Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa pili…”
Wakati huu wa matatizo haya yaliyoikumba dunia..sio wakati wa kuomba rehema…ni wakati wa kutubu, maana yake ni wakati wa kuacha dhambi…kughairi mabaya tunayoyafanya…kughairi rushwa tulizokuwa tunakula na tunazoendelea kuzila sasa, ni wakati wa kuacha uasherati kabla ya kumkaribia Mungu wetu kumwomba rehema…ni wakati wa kutupa na kuchoma vimini…niwakati wa kutupa mahereni, mabangili, na kuondoa make-up na kutuacha kuwa asili kama Mungu alivyotuumba, na baada ya hapo ndipo tunamwambia Baba tumeacha sanamu zote hizi tunaomba uturehemu..Ni wakati wa kuwarudishia watu vitu tulivyowarusha au kuwatapeli, ni wakati wa kuwasamehe waliotukosea, ni wakati wa kupatana na ndugu zetu ambao tulikuwa tumewachukia mpaka tukawawekea vinyongo, Ni wakati wa kuacha kutukana kabisa, ni wakati wa kuacha kuwaseng’enya jirani zetu na kuwatakia shari, Ni wakati wa kuacha ULEVI, na kwenda Disko, ni wakati wa kuacha starehe za kidunia na kumgeukia Mungu..
Tukiyafanya hayo, mbele za Mungu wetu ndio tutakuwa tumetubu..kwasababu tutakuwa tumegeuka na kuziacha njia zetu mbaya..na hivyo akiona Toba yetu hiyo ndipo hata pasipo kutumia nguvu nyingi kuomba rehema..yeye mwenyewe ataturehemu kwasababu ni mwingi wa rehema…Lakini tukienda na lipstick zetu midomoni, mbele zake kumwomba rehema, tukienda na zinaa zetu mbele yake kumwomba aturehemu, tukienda na nguo zetu za nusu uchi mbele zake na kumwomba msamaha…Ni sawa na kijana anayekwenda huku amelewa pombe na huku ana sigara mdomoni mbele za Baba yake na kumwambia Baba naomba unisamehe kwa ulevi wangu. Hapo atakuwa anamdhihaki mzazi wake. Na ndivyo tunavyoonekana mbele za Mungu wetu tunapokwenda kumwomba rehema huku bado hatujadhamiria kuacha dhambi zetu tunazozifanya kwa siri au kwa wazi.
Wakati huu tunayo nafasi ya kuomba rehema kwaajili ya nchi Pamoja na nafsi zetu na ndugu zetu…Ni wakati wa kutanguliza TOBA kwanza kabla ya REHEMA. Na hilo linatosha kabisa kupata rehema bila hata ya sisi kutumia nguvu nyingi…Kama Habari ile ya mwanampotevu..alipoghairi Maisha yake yale na kugeuka kuamua kurudi kwa Baba..hata alipokuwa mbali Baba yake alimwona na kumpokea..hakutumia nguvu nyingi sana Kupata rehema kutoka kwa Baba yake.
Bwana akubariki, kama hujampa Yesu Kristo Maisha yako..unangoja nini?..Wewe ni shahidi wa nyakati hizi tunazoishi na majira haya..bado makubwa zaidi ya haya unayoyaona yanakuja huko mbeleni kwa wote ambao wapo nje ya Kristo. Hivyo tubu leo na Bwana atakurehemu na kukupa Roho wake Mtakatifu kwasababu anatupenda sana.
Maran atha!
USIISHIE KUTAZAMA JUU, ENDELEA MBELE.
MTINI, WENYE MAJANI.
JE MOYO WAKO NI MNYOFU MBELE ZA MUNGU
JE UNAMTHAMINI BWANA?
Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?
KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA.
WhatsApp
SWALI: Hujambo ndugu.Nina ulizo kuhusu kabila 12 ya Yakobo (Israeli) katika mwanzo 49 tunaona kabila la DANI lipo, lakini katika ufunuo 7 kabila la Dani halipo badala yake lipo manase. Kwanini?
JIBU: Katika kitabu cha Ufunuo sura ya 7, kabila la Dani halionekani miongoni wa watu wale watakaoitiwa muhuri siku ya mwisho ili kuiamini Injili itakayokuja kuhubiriwa pale Israeli..Sasa Mungu hakulisahau kabila hilo, hapana bali aliliondoa kwa makusudi kabisa pale na kuliweka hilo la manasae.
Lakini ni kwanini Mungu afanye vile?.. Tukijua jambo hilo jinsi laana za Mungu zilizo kali basi na sisi hatutauchezea wokovu wetu tuliopewa sasa na Mungu wetu.. Kwasababu neema ikishaondoka imeondoka kweli kweli.
Sasa tukisoma kwenye biblia Mungu alishatoa angalizo hili tangu zamani…
Kutoka 20:2 “Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. 3 Usiwe na miungu mingine ila mimi. 4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. 5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,”
Kutoka 20:2 “Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
3 Usiwe na miungu mingine ila mimi.
4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,”
Unaona Mungu alisema kabisa katika amri zake, kuwa yeye ni Mungu mwenye wivu, na pia anapatiliza maovu yao hata kizazi cha tatu na cha nne..ikiwa na maana kuwa ukifanya dhambi ya makusudi baada ya kuujua ukweli mapatilizo yake yanaweza kuendelea hata kwa vizazi vya wanao huko mbele.
Na tena alisema katika kitabu cha Mambo ya walawi..
Walawi 18:27 “(kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;) 28 ili kwamba hiyo nchi isiwatapike na ninyi pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu. 29 Kwani mtu awaye yote atakayefanya machukizo hayo mojawapo, NAFSI HIZO ZITAKAZOYAFANYA ZITAKATILIWA MBALI NA WATU WAO”.
Walawi 18:27 “(kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;)
28 ili kwamba hiyo nchi isiwatapike na ninyi pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu.
29 Kwani mtu awaye yote atakayefanya machukizo hayo mojawapo, NAFSI HIZO ZITAKAZOYAFANYA ZITAKATILIWA MBALI NA WATU WAO”.
Sasa kabila la DANI lilikuwa ni kabila mojawapo la makabila ya Israeli, na kwamba kabila hili lingetakiwa lionyeshe kielelezo kwa watu wa Mataifa kuwa Mungu wa Israeli ndio Mungu na ndiye pekee anayepaswa kuabudiwa,..Lakini lilifika wakati hilo kabila lenyewe likaamua kumuacha Mungu na kwenda kusimamisha SANAMU katika mji wake, na kuiabudu na kuitolea kafara..Ni kabila pekee katika biblia nzima liliokuwa na ujasiri wa kufanya jambo kama hilo..Habari yote hiyo unaweza kuisoma mwenyewe katika kitabu cha Waamuzi sura ya 17 na 18
Sasa jambo hilo lilimfanya Mungu, alifute katika mpango wake wa wokovu..(sawasawa na Neno lake alilolisema) na ndio maana hapo tunaona katika kitabu cha ufunuo ambacho kinazungumzia habari za siku za mwisho, wakati ambapo wana wa Israeli watarejeshewa tena neema hii ya wokovu tuliyonayo sisi, kabila hilo la Dani halitakuwepo katika hesabu hiyo.
Hiyo inatukumbusha na sisi, tusipoizingatia neema hii ya wokovu, tukawa tunaifanyia mzaha, tunajiweka hatarini kwa Mungu kutuacha na kwenda kwa wengine.
Ubarikiwe.
Kwanini kabila la Dani na Efraimu hayaonekani yakiorodheshwa miongoni mwa yale makabila 12 ya Israeli katika Ufunuo 7?
MISTARI SHETANI ANAYOITUMIA KUWAANGUSHA WATU
KITABU CHA UZIMA
JE KUNA UISLAMU KATIKA BIBLIA?
MIHURI SABA
SWALI: Mahuru ndio nini? Kama Bwana alivyosema katika Mathayo 17:26, Na ni jambo gani tunajifunza pale?
JIBU: Tusome;
Mathayo 17:25 “Naye alipoingia nyumbani, Yesu alitangulia kumwuliza, akisema, Waonaje, Simoni? Wafalme wa dunia hutwaa kodi ama ushuru kwa watu gani? Kwa wana wao au kwa wageni? 26 Naye aliposema, Kwa wageni, Yesu alimwambia, Basi, kama ni hivyo, WANA NI MAHURU. 27 Lakini tusije tukawakwaza, enenda baharini ukatupe ndoana, ukatwae samaki yule azukaye kwanza; na ukifumbua mdomo wake utaona shekeli ichukue hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako”.
Mathayo 17:25 “Naye alipoingia nyumbani, Yesu alitangulia kumwuliza, akisema, Waonaje, Simoni? Wafalme wa dunia hutwaa kodi ama ushuru kwa watu gani? Kwa wana wao au kwa wageni?
26 Naye aliposema, Kwa wageni, Yesu alimwambia, Basi, kama ni hivyo, WANA NI MAHURU.
27 Lakini tusije tukawakwaza, enenda baharini ukatupe ndoana, ukatwae samaki yule azukaye kwanza; na ukifumbua mdomo wake utaona shekeli ichukue hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako”.
Ukisoma mstari huo..Bwana alikuwa anazungumzia juu ya wale wanaostahili kulipishwa kodi kulingana na tamaduni za wakati huo…Kwamba kwa wakati huo watu wanaotoka mji mmoja kuingia mwingine ambao si wa kwao walikuwa wanatozwa ushuru…lakini wale wenyeji walipokuwa wanarudi kuingia kwao hawatozwi ushuru kwasababu wao ni wenyeji au wana wa huo mji…
Hivyo hapa Bwana alikuwa ametoka na wanafunzi wake kutoka mji mmoja kwenda mwingine ndani ya Mkoa wake mwenyewe ulioitwa Galilaya…lakini wakataka kumtoza nusu shekeli na ilihali yeye ni mwenyeji wa Mkoa ule na wala si mgeni (Galilaya ilikuwa inajumuisha majimbo ya Nazareti, Korazini, Kapernaumu, Tiberia, Naini, Magdala na mengine machache madogo madogo), na Galilaya yote ilikuwa chini ya Mfalme Herode wa kirumi. Hivyo yoyote aliyekuwa mzawa wa majimbo hayo alikuwa huru kwenda popote katikati ya hayo majimbo pasipo kutozwa ushuru wowote…
Ni sawa na sisi tulivyo na uhuru wa kusafiri mkoa wowote bila vizuizi.
Lakini hawa walipomwona Yesu waliingiwa na tamaa ingawa walijua kabisa ni mzawa, lakini waliingiwa na tamaa labda pengine walimwona anafuatwa na watu wengi wakadhani atakuwa na pesa nyingi hivyo wakawa wanatafuta sababu za kupata fedha kutoka kwake..
Sasa Bwana ndio anamwuliza Petro je wanaotozwa ushuru ni wageni au WANA ?(neno wana ni sawa na wenyeji)…Ndio Petro anamjibu kwamba ni Wageni ndio wanaopaswa kutozwa ushuru na si wenyeji…Ndipo Bwana akamwambia basi kama ni hivyo Wana au kwa lugha nyingine wenyeji ni MAHURU..yaani maana yake wazawa WAPO HURU…Hawapaswi kutozwa chochote kulingana na sheria ya nchi.
Lakini kwasababu Bwana ana hekima nyingi na siku zote anampendeza Mungu na wanadamu hakutaka kuwakwaza kwa vyovyote vile..ndio akamwambia Petro akavue na samaki atakayezuka wa kwanza mdomoni atakuta fedha aje kuilipa kwaajili yake na ya Petro.
Tunajifunza hapo na sisi…sio kila vita vya kupambana nayo…vingine mwachie Bwana akupiganie..Hebu jiulize hapa Petro angeanza kugoma..oo hapana hiyo sio haki, mnatuonea, mnatunyanyasa..sisi ni wenyeji n.k Bila shaka asingeuona ule muujiza Bwana alioufanya…Na kama ukichunguza pale hawakuwa hata na senti..ndio maana Bwana akamwambia Petro akavue…Sasa kwa utulivu wa Petro faida aliyoipata ya kuwa mtulivu na kumtii Bwana na kumwamini alipoenda kuvua ili aje kulipa ushuru ambao si halali yake kuulipa.. alipata faida mara mbili..
Faida ya kwanza aliyoipata ni kwenda kulilipa lile deni alilokuwa anadaiwa ambalo halikuwa halili kwake kulilipa…na faida ya pili na ya muhimu ni Yule samaki…pengine alikwenda kumuuza au kumtumia kwa kitoweo baada ya kumtoa ile sarafu mdomoni…
Vivyo hivyo wakati mwingine tunaweza kusingiziwa kesi au madeni ambayo si halali kwetu kuyalipa…usining’unike katika hali kama hiyo..umejaribu kuonyesha kwamba sio halali lakini hueleweki usianze kunung’unika na kulalamika mpaka kuonekana sasa huna imani na maana..mpaka watu wakaanza kushangaa kama kweli wewe ni mkristo au la!..kwa matusi hayo na manung’uniko hayo..
Wewe unachopaswa kukifanya nenda katafute namna ya kulipa deni lile au kuikabili kesi ile, hata kulipa kile chote wanachokushitaki..na huko huko njiani Mungu atakufanyia muujiza wa kuilipa ile na utapata cha ziada.
Hizo zilikuwa ni kanuni za Bwana wakati wote, nasi tupate kitu kidogo cha kujifunza hapo..
Luka 6: 29 “Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang’anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu. 30 Mpe kila akuombaye, na akunyang’anyaye vitu vyako, usitake akurudishie”.
Luka 6: 29 “Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang’anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu.
30 Mpe kila akuombaye, na akunyang’anyaye vitu vyako, usitake akurudishie”.
TAHADHARI YA NEEMA YA MUNGU.
MOJA YA HIZI SIKU TUTAONA MABADILIKO MAKUBWA SANA.
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
Je kupiga miayo ni ishara ya mapepo?
NIMEOKOKA, ILA MUNGU NDIYE ANAYEJUA NITAKWENDA WAPI.
KARAMU YA MWANA-KONDOO.
Ni jambo la kawaida, kuona tabia za watu zinabadilika hususani pale wanapoona wanakaribia kwenda kuangamizwa wote,..Utaona wengi wao wanajigeuza na kujifanya kama vile wao ni kama wale wengine, ili wafanikiwe kijipenyeza kisirisiri katikati yao wasalimishe roho zao..
Hiyo ilitokea wakati wa kipindi cha Esta, pale ambapo maadui wa Wayahudi walipokusudia kuwaua wayahudi wote kwa kibali cha mfalme Ahasuero, lakini kibao kilipowageukia na kuona mfalme ndio amewapa heshima mara dufu,na ziadi ya yote amewapa mamlaka ya kuwatafuta wale maadui zao wawaue, biblia inatuambia jamii kubwa ya watu wakajigeuza na wenyewe kujifanya ni wayahudi ..
Esta 8:16 “Ikawa nuru na furaha na shangwe na heshima kwa Wayahudi. 17 Na katika kila jimbo, na kila mji, po pote palipowasili amri ya mfalme na mbiu yake, Wayahudi wakapata furaha na shangwe, karamu na sikukuu. Hata wengi wa watu wa nchi wakajifanya Wayahudi, kwa kuwa hofu ya Wayahudi imewaangukia”.
Esta 8:16 “Ikawa nuru na furaha na shangwe na heshima kwa Wayahudi.
17 Na katika kila jimbo, na kila mji, po pote palipowasili amri ya mfalme na mbiu yake, Wayahudi wakapata furaha na shangwe, karamu na sikukuu. Hata wengi wa watu wa nchi wakajifanya Wayahudi, kwa kuwa hofu ya Wayahudi imewaangukia”.
Unaona hapo?..
Tunasoma tena habari nyingine, kuna wakati jamii mbili za wana wa Israeli zilipigana, ambazo ni Ni jamii ya watu wa Efraimu, na watu wa Gileadi… Sababu ya vita yenyewe ilikuwa ni wale watu wa Gileadi walikwenda kupigana na maadui zao, bila kuwashirikisha watu wa Efraimu kwenda kuwasaidia, hivyo watu wa Efraimu wakakasirika kuona uamuzi ule waliouchukua ndugu zao hivyo wakapanga vita wawapige na Wagileadi, Lakini mambo yalikuwa ni tofuati, kinyume chake wao ndio waliopigwa..
Sasa baada ya kuona wanazidiwa na hali ndio inakuwa mbaya, ikawabidi, watoroke watu wengi, wajaribu kuvuka kujichanganya na jamii ya wagileadi. Sasa ilikuwa ili kufika ng’ambo ni sharti uvuke mto wa Yordani..Lakini wao walidhani ni rahisi rahisi tu kama siku zote, unavuka tu na kuingia bila kuulizwa chochote..wengine wakadhani hata wakiulizwa wewe ni nani, je ni mwenyeji wa huku watasema tu ndio, halafu basi wataruhusiwa kuvuka..
Hawakujua kuwa wale wagileadi walipata taarifa juu ya njama zao, Hivyo walichokifanya ni kwenda kusimama pale kwenye vivuko vya Yordani, pale mpakani, na watu wote, waliochanganyikana nao walipofika wavuke wasijue kuwa huyu ni nani na huyu ni nani, walitumia njama moja ya kuwakamata waefraimu katikati ya wagileadi, waliwaambia watamke Neno “shibolethi” tusome..
Waamuzi 12:5 “Nao Wagileadi wakavishika vivuko vya Yordani kinyume cha hao Waefraimu; kisha ilikuwa, hapo watoro waliotoroka Efraimu mmojawapo aliposema Niache nivuke, hao watu wa Gileadi wakamwambia, Je! Wewe u Mwefraimu? Kwamba alisema, La; 6 ndipo wakamwambia, Haya, tamka sasa neno hili, Shibolethi; naye akasema, Sibolethi; kwa maana hakuweza kufanya midomo yake kutamka neno hilo sawasawa; ndipo wakamshika, na kumwua hapo penye vivuko vya Yordani; basi wakaanguka wakati huo watu arobaini na mbili elfu wa Efraimu”.
Waamuzi 12:5 “Nao Wagileadi wakavishika vivuko vya Yordani kinyume cha hao Waefraimu; kisha ilikuwa, hapo watoro waliotoroka Efraimu mmojawapo aliposema Niache nivuke, hao watu wa Gileadi wakamwambia, Je! Wewe u Mwefraimu? Kwamba alisema, La;
6 ndipo wakamwambia, Haya, tamka sasa neno hili, Shibolethi; naye akasema, Sibolethi; kwa maana hakuweza kufanya midomo yake kutamka neno hilo sawasawa; ndipo wakamshika, na kumwua hapo penye vivuko vya Yordani; basi wakaanguka wakati huo watu arobaini na mbili elfu wa Efraimu”.
Unaona, walitumia kigezo cha Lugha, kuwashika, vinginevyo wasingewatambua kwa namna yoyote, kwasababu walijua lugha ya asili ni kitu kinachoshikamana na mtu kuliko kitu kingine chochote, walijua lugha ya asili inaweza kweli kuigwa lakini haiwezi kuigwa kwa ufasaha wake wote, haijalishi mgeni atajifunza kwa miaka mingapi, ile lugha ambayo hajazaliwa nayo hawezi kuiiga kwa ufasaha wote..Hata leo hii mzungu aishi uswahilini hata miaka 50 na akakijua Kiswahili chote, bado kuna vimelea vya lugha hatoweza kuvitamka ipasavyo kama Yule mzawa..
Sasa Biblia inatuambia agano la kale ni kivule cha mambo yatakayotokea katika kipindi cha agano jipya..Na habari hizo hazijaandikwa ili kutusisimua tu, hapana bali zina ujumbe mkubwa sana kwetu katika roho.
Inamaana kuwa utafika wakati mambo ya wokovu hayatakuwa kama yalivyo leo hii, kuna wakati wale waovu watatamani sana kwa nguvu kujiingiza katika ufalme, watajigueza kwa kila namna ili tu wapate nafasi, lakini safari hii, haitakuwa ni kwa njia rahisi kwa wanavyodhani, bali watakuwa na mtihani mkubwa wa kufanya..
Luka 16:16 “Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu”.
Utapimwa wokovu wako, sio kwa kusema tu mimi nimeokoka, mimi nilibatizwa, mimi ninakwenda kanisani bali vitazingatiwa vigezo vya ndani zaidi, utaulizwa je! Huo wokovu unauzoefu nao kiasi gani, Je, ni wa kujifunza tu, au ulikuwa ni sehemu ya maisha yako tangu zamani..
Hili ndio lile kundi ambalo Bwana alilitolea mfano wake, wa mtu Yule aliyekutwa ndani ya harusi lakini hana vazi la harusi mpaka watu wakawa wanashangaa ameingiaje ingiaje mule ndani na wakati hana vazi la harusi..Kumbuka wakati huu kule nje kulikuwa kunaendelea machinjo.. Akatoroka akaingia ndani, lakini alionekana kwasababu hakuwa na vazi (hakuwa na kadi ya mwaliko tangu zamani) Kilichofuata ni kwamba alikamatwa na kufungwa na kwenda kutupwa nje..
Ndipo Bwana akamalizia kwa kusema maneno haya.. “Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache”. Soma (Mathayo 22:1-14)
Hivyo ndugu anza kuujenga uhusiano wako na Mungu kuanzia sasa, usisubiri wakati Fulani, kubali kuzaliwa mara ya pili leo uikulie wokovu ujifunze lugha ya kimbinguni, kama bado hujaokoka.. kwasababu unafika wakati hapo mbele hakutakuwa tena na mlango wa neema ya yule atakayetaka kuingia.. kwa maana hizi ni nyakati za mwisho jambo ambalo hakuna mtu asiyelijua hilo.
Ubarikiwe sana.
MUNGU WETU, JINSI LILIVYO TUKUFU JINA LAKO DUNIANI MWOTE!
BASI TUENDELEE KUMJUA MUNGU,NAYE ATATUJILIA KAMA MVUA YA VULI.
Mitume wote waliopita walikuwa ni watu weupe hata manabii wote waliopita hadi Ma-papa ni ngozi nyeupe. ni kweli ngozi nyeusi ililaaniwa ?
Yeshuruni ni nani katika biblia?
Watu baadhi kutoka nchi mbalimbali wamenitumia ujumbe wanasema, mtumishi huku kwetu hali sio nzuri hatuwezi kwenda kanisani kama tulivyozoea, hatuwezi kufanya chochote isipokuwa tu ni kukaa nyumbani, na wala hakuna dalali ya jambo hilo kuisha hivi karibuni…Tufanye nini?
Shalom, ndugu,
Ipo Habari moja katika biblia tunapaswa tujue na tujifunze kama wakristo katika wakati huu ambao dunia ipo katika taharuki kubwa, Tukisoma kitabu cha matendo ya Mitume, kuna wakati ambapo mitume wa Bwana walipitia kipindi fulani cha ukimya mkubwa sana, jambo ambalo liliwapasa wasifanye kitu kingine Zaidi ya kwenda kujifungia gorofani. Kwanini walilazimika kuwa vile, ni kwasababu ni kipindi ambacho, Sio YESU tu peke yake ambaye walizoea kumwona na kutembea naye kila siku hakuwa nao, bali pia Roho Mtakatifu ambaye walisikia habari zake alikuwa bado hajashuka juu yao.. walikuwa katikati ya pengo, kama vile mayatima fulani..
Kitu pekee kilichowafanya wawezi kukivuka hicho kipindi kifupi cha ukimya, ilikuwa ni ile AHADI TU, waliopewa na Bwana Yesu siku ile aliyokuwa anapaa..
Hiyo ndio iliyokuwa salama yao kwa wakati huo waliokuwa wanapitia..Kumbuka hawakujua ahadi hiyo itatimia lini, lakini maaadamu wana Neno la Ahadi, basi hiyo iliwafanya wapate nguvu siku baada ya siku, wavumilie hicho kipindi cha mpito mbele yao wakitumai kuwa siku si nyingi itatimia, na AHADI yenyewe ilikuwa ni kungojea YERUSALEMU, mpaka wakatakapopokea kipawa cha Roho Mtakatifu..Basi.
Matendo 1:3 “wale aliowadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, akiwatokea muda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu. 4 Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu; 5 ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache”.
Matendo 1:3 “wale aliowadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, akiwatokea muda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu.
4 Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu;
5 ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache”.
Hivyo baada ya ile siku ya 40, hawakumwona, wala hawakusikia chochote, wala hawakuoona uwepo wowote, wala hawakuwa na shughuli nyingine yoyote ya kuhubiri, au kushuhudia kama pale mwanzo, au kuzunguka huku na huko kuhubiri..Bali iliwagharimu kwenda kukaa tu sehemu moja..na zaidi ya yote biblia inasema nje kulikuwa na hofu ya wayahudi.
Lakini biblia inatuonyesha ahadi hiyo haikuchelewa, bali ndani ya siku 10 mbeleni ilitimia, ambayo ndio iliyokuwa siku ya Pentekoste, Roho Mtakatifu aliwashukia mitume wake kwa nguvu ya ajabu, na hapo ndipo Mungu akaleta uamsho mwingine tena ambao uliitikisa dunia nzima katika historia..
Sasa swali ni Je ndani ya kipindi kile cha mpito ambacho hakukuwa na sapoti yoyote ya kimbinguni mitume walikuwa wanafanya nini ndani, Je! walikuwa wamelala tu au wameacha wakovu wao sasa wafikirie mambo yao ya kale, au walikuwa wamekaa wanapiga tu story na kuzungumzia Maisha ya wengine, au wanaangalia movie, au wanachat whatasapp kila wakati au wanacheza magemu, au wanafanya nini??
Embu Tusome..
Matendo 1:10 “Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, 11 wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni. 12 Kisha wakarudi kwenda Yerusalemu kutoka mlima ulioitwa wa Mizeituni, ulio karibu na Yerusalemu, wapata mwendo wa sabato. 13 Hata walipoingia, wakapanda orofani, walipokuwa wakikaa; Petro, na Yohana, na Yakobo, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo wa Alfayo, na Simoni Zelote, na Yuda wa Yakobo. 14 Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja KATIKA KUSALI, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake”.
Matendo 1:10 “Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe,
11 wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.
12 Kisha wakarudi kwenda Yerusalemu kutoka mlima ulioitwa wa Mizeituni, ulio karibu na Yerusalemu, wapata mwendo wa sabato.
13 Hata walipoingia, wakapanda orofani, walipokuwa wakikaa; Petro, na Yohana, na Yakobo, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo wa Alfayo, na Simoni Zelote, na Yuda wa Yakobo.
14 Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja KATIKA KUSALI, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake”.
Unaona, biblia inasema hapo walikuwa WAKIDUMU KWA MOYO MMOJA KATIKA KUSALI,..
Ndugu, wakati huu wa LOCKDOWN, na kuwa karantini kutokana na janga la Corona, nchi yoyote uliyopo. Wakati huu Wa kuzuiwa kufanya ibada, au kuzunguka huku na huko, wa kuzuiwa kwenda mtaani kuhubiri kama ulivyokuwa unafanya hapo mwanzoni, wa kuzuiwa kuitishi mikutano ya injili, wa kuzuiwa kwenda kumwabudu Mungu kanisani, kwenda kwenye masomo ya biblia, kila baada ya siku mbili, sio wakati wako wa wewe kuwa na kisingizio cha kuacha kumtafuta Mungu, na kurudi nyuma kwenye ulimwengu ulipokuwepo, wa kurudi kuanza sasa kutokusoma biblia yako,..bali huu ndio unapaswa uufanye muda wakati wako wa kudumu katika KUSALI kwa bidii ukiingalia ahadi ya Mungu iliyo mbele yako, kwamba hivi karibuni atakwenda tena kutuachilia, lakini hatatuachilia hivi hivi, bali atatuachilia na UAMSHO MKUBWA WA ROHO ambao haujawahi kutokea..kama ilivyokuwa katika kipindi cha Pentekoste.
Hivyo huu sio wakati wa kuzimia mioyo, wala sio wakati wa kuogopa maadamu tupo ndani ya Kristo, badala yake ndio tuongeze kutazama juu, tukiziangalia Ahadi za Bwana ndani ya kipindi hichi cha mpito, tukiongeza viwango vyetu vya kujisomea biblia nyumbani, na kusali sana tena Zaidi ya pale tulipokuwa mwanzoni, ikiwezekana kufunga, na kila wakati kumtafakari Mungu kweli kweli..
Sisi hatujapitia kipindi cha kuachwa na mbinguni kwa Muda kwa ilivyokuwa kwa mitume, lakini wao hawakuiacha Imani, badala yake walidumu katika kusali tena walipanda OROFANI, juu kabisa mahali ambapo hapana usumbufu wa watu kuingia na kutoka, ili wamtuafakari Mungu vizuri na kusali..
Vivyo hivyo huu ni wakati wa wewe, kupanda OROFANI (mahali penye utulivu), Umtafute Mungu peke yako, kwasababu UAMSHO MKUU SANA, Unakwenda kuzuka duniani kote hivi karibuni. Kipindi cha nyuma pengine ulikuwa na visingizio vya kutokusali, kwamba upo bize kutafuta riziki na shughuli leo hii mazingira yanakulazimisha kukaa nyumbani, na tena kuna agizo limetolewa la kuomba, hivyo isiwe sababu ya wewe kuhukumiwa siku ile kwa kutokuomba sasahivi…Unayo sababu inayoeleweka kidunia ya wewe kutozurura zurura mtaani, basi kaa nyumbani kuomba…utajitetea vipi siku ile??..Utasema ulikosa muda? Utasema serikali ilikuzuia kuomba? Leo hii imekutangazia wewe kuomba?.. Utasema sikuomba kwasababu mazingira yalikuwa hayaruhusu?..jibu unalo.
Hivyo nakutia moyo wewe mkristo ambaye umeathiriwa na hali hii ya sasa duniani, Fahamu kuwa ni kipindi kifupi tu cha Siku 10 rohoni kinapita ambacho ni Mungu mwenyewe kakiruhusu..hivyo kuwa na akili, kujua nyakati na majira, ongeza viwango vyako vya utakatifu kama vile hukuwahi kuishi hivyo hapo kabla, ni wakati wa kutubu (kutubu maana yake ni kuacha yale uliyokuwa unayafanya yasiyo mpendeza Mungu) ili hiyo PENTEKOSTE itakapokuja kwa watu wa Mungu duniani, uwe na wewe ni mmojawapo..
Bwana akubariki.
JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOWAFUNULIA WATU MAANDIKO.
KWARESMA IPO KIMAANDIKO?
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
YA KALE YAMEPITA, TAZAMA YAMEKUWA MAPYA
NAO WALIOKUWA WAMEKUSUDIWA UZIMA WA MILELE WAKAAMINI.
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe.
Karibu tujifunze biblia na kujikumbusha mambo yale yale ambayo tumekwisha kujifunza huko nyuma kupitia sehemu mbalimbali..
Wengi wanajiuliza je ubatizo ni wa muhimu?..Jibu ni NDIO ni wa muhimu sana na si kidogo. Shetani hapendi wengi wajue siri iliyopo katika ubatizo sahihi kwasababu anajua madhara yake.
Wakati wana wa Israeli wanatoka Misri, Farao bado alikuwa anawafuatilia fuatilia..lakini walipovuka tu bahari ya shamu na majeshi ya Farao yote kuzama kwenye ile bahari ya shamu ndio ikawa mwisho wa Farao na majeshi yake kuwafuatilia wana wa Israeli.
Kutoka 14:26 “Bwana akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi tena juu ya Wamisri, juu ya magari yao, na juu ya farasi zao. 27 Musa akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakakimbia mbele yake; na Bwana akawakukutia mbali hao Wamisri kati ya bahari. 28 Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja. 29 Lakini wana wa Israeli wakaenda katika nchi kavu katikati ya bahari; na hayo maji yalikuwa ni kuta upande wao wa kuume, na upande wao wa kushoto. 30 Ndivyo Bwana alivyowaokoa Israeli siku ile mikononi mwa Wamisri; Waisraeli wakawaona Wamisri ufuoni kwa bahari, wamekufa”.
Kutoka 14:26 “Bwana akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi tena juu ya Wamisri, juu ya magari yao, na juu ya farasi zao.
27 Musa akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakakimbia mbele yake; na Bwana akawakukutia mbali hao Wamisri kati ya bahari.
28 Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja.
29 Lakini wana wa Israeli wakaenda katika nchi kavu katikati ya bahari; na hayo maji yalikuwa ni kuta upande wao wa kuume, na upande wao wa kushoto.
30 Ndivyo Bwana alivyowaokoa Israeli siku ile mikononi mwa Wamisri; Waisraeli wakawaona Wamisri ufuoni kwa bahari, wamekufa”.
Sasa siri ilikuwa ni nini mpaka Mwisho wa Farao ukawa kwenye hiyo bahari ya Shamu?..Jibu ni rahisi: Ni huo ubatizo wana wa Israeli waliobatizwa kwa kupita katikati ya bahari hiyo.
Utauliza je!..ina maana wana wa Israeli walibatizwa katika bahari ya Shamu?..Jibu ni ndio!..
1Wakorintho 10:1 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; 2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;”
1Wakorintho 10:1 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;
2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;”
Unaona hapo?..kitendo cha Wana wa Israeli kupitishwa katika yale maji ya Shamu, pasipo kupatikana na madhara ndiko kunakofananishwa na ubatizo. Hivyo ule ubatizo ndio uliohitimisha kazi ya shetani na majeshi yake kuwafuatilia, haijalishi kuwa tayari walishapewa ruhusu huko nyuma ya kuondoka.
Hali kadhalika, ubatizo sahihi wa maji mengi sasa unafanya kazi hiyo hiyo. Unapoingia katika yale maji na kubatizwa katika jina la Yesu na kutoka katika yale maji…wewe utatoka salama ukiwa na furaha, na amani lakini nyuma yako yale majeshi ya mapepo wabaya yaliyokuwa yanakufuatia yanakufa na maji huko nyuma.
Hivyo maji ni ishara ya wokovu kwako na maangamizi kwa shetani na majeshi yake. Ndio maana Bwana Yesu alisema katika Roho kwamba pepo amtokapo mtu hupitia mahali pasipo maji(maana yake mahali ambapo hapana maji) ili apumzike na akirudi na kukuta nyumba yake imefagiliwa anakwenda kuwachukua pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye, na hali ya mwisho ya Yule mtu inakuwa mbaya kuliko ya kwanza.
Maana yake ni kwamba pepo likimtoka mtu na Yule mtu kama hatachukua uamuzi wa kuukamilisha wokovu wake ikiwemo kubatizwa ubatizo sahihi wa kuzama mwili mzima kulingana na maandiko na kudumu katika usafi..Mtu huyo yupo hatarini kurudiwa na zile zile nguvu za giza zilizomwacha hapo kwanza. Hivyo ubatizo sahihi ni wa muhimu sana…Na ubatizo sio dini mpya bali ni maagizo ya Bwana wetu Yesu…na kwa faida yetu kama ilivyokuwa kwa faida kwa wana wa Israeli wakati wanatoka Misri, kama sio yale maji Farao angeendelea kuwafuatilia daima.
Shetani na mapepo yake yataendelea kumfuata Yule mtu ambaye hajakamilisha wokovu wake…Na Bwana alishatuambia katika Neno lake, kwamba “aaminiye na kubatizwa ataokoka”..maana yake mambo hayo mawili yanakwenda pamoja, hayaachani, vinginevyo ni ngumu sana kuokoka na mkono wa Adui.
Kama unakumbuka kile kisa cha Yule mtu aliyekuwa na mapepo yaliyojitambulisha kama JESHI. Mtu Yule aliingiwa na mapepo, na mapepo yale yalipomtoka yaliwaingia nguruwe…Jinsi wale Nguruwe walivyokwenda kuangamia majini ni mfano wa Farao na majeshi yake yalivyozama majini…Kwahiyo unaweza kuona kuna uhusiano mkubwa sana wa maji na majeshi ya Adui. Hivyo ubatizo ni wa muhimu sana. Pale tu mtu anapoamini na kutubu anapaswa akabatizwe bila kuchelewa…
Itakuwa ni jambo la kushangaza, mtu utasema umeokoka, halafu miezi inapita, miaka inapita, bado hujabatizwa, unaishi kwa kanuni ipi ya wokovu?
Bwana akubariki sana.
MUNGU KUSEMA NA WEWE PEKEE, HAITOSHI KUKUPA USHINDI.
JINA LA MUNGU NI LIPI?
KUTAKUWA NA MATETEMEKO YA NCHI, NJAA NA TAUNI.
USITUPE LULU ZAKO MBELE YA NGURUWE.
HISTORIA YA WILLIAM BRANHAM
Kabla Mungu hajaleta maangamizi katika dunia, huwa anawatuma kwanza malaika zake wapelelezi kwenda kuhakiki hicho kilichomfikia kuwa ni kweli au La, na ikithibitika kuwa ni kweli basi hatua inayofuata saa hiyo hiyo ni wale malaika kutekeleza hukumu ya Mungu juu ya watu hao au Mji huo. Kwananini anawaagiza malaika hawa kwanza kupeleleza, je ni kwasababu yeye mwenyewe hajui kiwango cha maasi na haki yaliyomo ulimwenguni?..jibu ni hapana!..anajua kila kitu pasipo hata kutegemea malaika zake, wala mwanadamu..lakini anafanya hivyo ili pawepo na mashahidi ya kile kinachoendelea…Kama biblia inavyosema “Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa.(2Wakorintho 13:1)”
Ndicho kilichotokea kipindi kifupi kabla ya miji ya Sodoma na Gomora kuangamizwa. Mungu aliwatuma malaika zake wawili, kwenda kuipeleleza miji ile, na kama tunavyoifahamu habari, malaika wale walipofika jioni ile, wakakutana na Lutu, Lutu naye akawalazimisha kuingia nyumbani kwake, mwanzoni walikataa, lakini baadaye wakafika, na walipofika tu kumbe huku nyuma, walikuwepo pia wapelelezi wengine wanawafuatilia malaika wale, na hao si wengine zaidi ya watu wa miji ile..
Hivyo sio malaika tu waliokuwa wanapeleleza, na wao pia walikuwa wanapelelezwa, jambo ambalo linaendelea sasa katika roho..
Sasa walipoona hatma yao ni wapi, kuwa ni ile nyumba ya Lutu, hawakufanya chochote, bali walisubiri mpaka usiku ulipoingia ndipo wakakusanyika wote wakaizingira ile nyumba ya Lutu na kumwambia Lutu, awatoe hao watu ili wapate kulala nao..Embu fikiria hali yao ilivyokuwa mbaya..Sasa kama ukichunguza pale utaona, wale malaika hawakuchukua hatua yoyote kwanza, ni kama walikuwa wanawasikiliza walichokuwa wanamueleza Lutu pale nje, na mashindano yao pale mlangoni..Na baadaye ilipoonekana Lutu anashindwa, wakawa wanakaribia kuuvunja mlango, ndipo wakanyanyuka wakamvuta Lutu ndani, kisha wakawapiga upofu wale watu waliokuwepo pale mlangoni..
Hiyo ilisababisha ripoti yao ya upelelezi iwe imekamilika, kwamba Sodoma kumeoza na wao ni mashahidi, kilichobakia kwao ni kumuhimiza Lutu kwa haraka aondoke Sodoma kwa sababu miji ile wanakwenda kuiteketeza. (Soma Mwanzo 19 yote)
Ndugu yangu, dalili kubwa inayotutambulisha kuwa tunaishi katika wakati wa upelelezi wa malaika hawa, Sio kuzuka kwa vitendo vya Ushoga na usagaji tu peke yake, hapana, kwani hivyo vilikuwepo tangu zamani..lakini ni kuzuka kwa vitendo vya Ushoga na Usagaji katika nyumba ya Mungu…Tunavyoona leo hii ushoga unafungishwa katika nyumba ya Mungu, basi tujue hiyo ni dalili mbaya, ni sawa na kutaka kuzini na malaika wa Mungu walio katika kanisa lake..
Malaika hao wameshapita na wameshaona kile ambacho kilitokea wakati wa sodoma na Gomora ndicho kinachotokea na sasa hivi, hivyo wanachokifanya sasa ni kuwapiga watu upofu kwa kasi sana, ili wasione mlango wa neema tena ambao wenyewe wanauvunjia heshima, na kinachobakia kwa watu hao ni maangamizi tu..
Unapojiona wewe ni mtazamaji wa Pornography, ujue kuwa wewe ni kundi moja na hawa wanaoufanya ushoga nyumbani mwa Mungu, isipokuwa wewe tu ni mfuasi wa nyuma, lakini adhabu yenu ni moja,,..na hivi sasa unapigwa upofu, ambao hutakaa uuone mlango wa neema kamwe kama hutatubu. Ukiona unazini, na kwako wewe zinaa ni kama kitu cha kawaida na huku unajiita ni mkristo bado, ujue upofu unaendelea sasahivi duniani, ukiona unajihusisha na mambo yote ya kizinzi (iwe ni kujichua, au ulawiti) ujue upo katika kundi hilo la kupigwa upofu na malaika hawa wapelelezi wa Bwana.
Wanapopita na kuangalia makundi mengi ya watu, leo hii yapo kwenye simu zao mikononi, kutwa kuchwa ku-download video za pornography na kutazama video hizo, na miziki ya kidunia..ujue kuwa hao watu wanapigwa upofu, na malaika hao waliotumwa na Mungu kuipepeleza dunia, kabla ya kwenda kuangamizwa dunia hii kwa moto siku hizi za mwisho.
Wakati huu ni wakati wa hatari nyingi, ikimbie dhambi, unaweza kuona inavutia leo machoni pako, na ndivyo ilivyo dhambi siku zote ni ya kuvutia lakini mwisho wake ni majuto ya milele. Mungu tayari ameshakikasirikia kizazi hiki, kinachoichezea madhabahu yake mpaka kufikia hatua ya kufanya mambo ya ajabu kama hayo madhabahuni pake..Utasema ni hao sio mimi, kumbuka kile kikundi kichache kilichokuwa kinacheza mlangoni mwa Lutu ndicho kilichouwashia moto mji mzima wa Sodoma na Gomora..ikasababisha hata wengine walio mbali wasiojua chochote ambao wanafanya mambo kama hayo mwisho wao kufika. Kwahiyo uovu unapoendelea katika nyumba ya Mungu ni jambo la kuomboleza kwa wote.
Hivyo na sisi Bwana atusaidie tusiwe wamoja wapo, bali tuchukue hatua ya kutubu dhambi zetu kwa kumaanisha kabisa kumgeukia yeye, katika huu wakati mfupi wa kumalizia kabla ya unyakuo kupita. Kwasababu tusidhani kuwa yaliyowakuta wale, hawayawezi kutukuta na sisi.
USINIPITE MWOKOZI
JINSI SODOMA NA GOMORA ILIVYOKUWA INAVUTIA SANA..
UWEPO WA BWANA HATA KATIKATI YA MATESO.
JIRANI YANGU NI NANI?
Je! Hamna nyumba za kulia na KUNYWEA?.Mstari huu unahalalisha unywaji wa pombe?
DANIELI: Mlango wa 8