Biblia haijaweka bayana safina ilijengwa kwa muda gani, Wapo wanaosema ilijengwa kwa muda wa miaka 120 kufuatia mstari wa kitabu cha Mwanzo 6:3 ” Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.”
Lakini bado hiyo haileti maana kamili..Lakini pia biblia inasema Nuhu aliwazaa watoto wake akiwa na miaka 500,(Mwanzo 5:32) Na inasema aliingia katika safina akiwa na miaka 600, hivyo kufanya tofauti ya miaka 100 hapo, ambayo ndani ya hiyo pengine ndiyo aliyotumia kuijenga safina, lakini pia hoja hiyo ina mapungufu kidogo.
Kwa ufupi ni kwamba biblia haijaeleza ilijengwa kwa muda gani, hivyo pengine ni jambo ambalo halina umuhimu sana kwetu kulijua.
Jambo la Muhimu kujua ni kwamba, Kama dunia ya kwanza iligharikishwa na maji kwa ajili ya maovu ya watu, basi na dunia hii ya pili tunayoishi mimi na wewe nayo pia itagharikishwa vile vile kutokana na maovu ya wanadamu.. Na Biblia inasema haitagharikishwa kwa maji tena bali kwa moto.
Biblia inasema hivyo katika
2Petro 3:6 ” kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.
7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.”
Dhambi kama uzinzi, rushwa, chuki, fitina, kutokusamehe, ulevi, ushoga, ulawiti, usagaji, utukanaji, tamaa mbaya, utoaji mimba, wizi na nyingine zote ndio iliyoizamisha dunia ya kwanza kwenye maji. Na ndizo zitakazoizamisha dunia hii tunayoishi sasa katika moto. Kama Mungu alipozungumza alitenda kwa Nuhu, kadhalika alivyozungumza sasa katika Neno lake atatenda.
Je! na wewe bado upo ulimwenguni? bado hujampa Kristo maisha yako, na kuacha dhambi? Unyakuo upo karibu sana kutokea.
Bwana akubariki
Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya kila siku, kwa njia ya email, au whatsapp, basi tutumie ujumbe kwenye namba hii : +255789001312
Mada Nyinginezo:
NUHU ALIKUWA NA WATOTO WANGAPI?
NUHU ALIWALETAJE LETAJE WANYAMA KWENYE SAFINA?
Nuhu aliishi jumla ya miaka 950, hiyo ndio jumla ya miaka yake…Aliishi miaka 600 kabla ya Gharika, na aliishi miaka mingine 350 baada ya gharika.
Mwanzo 9:28 “Na Nuhu akaishi baada ya ile gharika miaka mia tatu na hamsini.
29 Siku zote za Nuhu zilikuwa miaka mia kenda na hamsini, akafa”.
Nuhu na wanawe ndio walikuwa watu wamwisho kuishi umri mrefu, kwani baada ya gharika Bwana Mungu alisema miaka ya Mwanadamu itakuwa 120 tu!
Tunajifunza kuwa si lishe bora ndiyo inayompa mtu maisha marefu, wala si kuzingatia mazoezi la hapana! Kinachompa mtu maisha marefu ni KUMCHA BWANA, Laiti kama wanadamu wa wakati ule wasingefanya maovu kiasi kile cha kuleta gharika juu ya nchi…mpaka leo wanadamu tungekuwa tunaishi mamia ya miaka, lakini kutokana na maovu yetu miaka yetu imeshusha namna hii.
Hivyo tukitaka tuishi maisha marefu katika haya maisha tuliyopewa hatuna budi kumcha Mungu, lakini tukivunja amri zake na kuishi maisha ya dhambi ndio tunakivuta kifo chetu karibu nasi.
Bwana atusaidie sana kwa hilo.
Mada Nyinginezo:
NUHU ALIKUWA NA WATOTO WANGAPI?
NUHU ALIJENGA SAFINA KWA MIAKA MINGAPI?
NUHU ALIWALETAJE LETAJE WANYAMA KWENYE SAFINA?
Biblia inasema Nuhu alikuwa na watoto watatu tu! SHEMU, HAMU na YAFETI, ambao wote walikuwa wakiume.
Mwanzo 5:32 “Nuhu alikuwa mwenye miaka mia tano, Nuhu akawazaa Shemu, na Hamu, na Yafethi”
Mwanzo 10:1 “Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika”.
Na Hao ndio walioingia kwenye safina pamoja na wake zao.
Mwanzo 7:7 “Nuhu akaingia katika safina, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye; kwa sababu ya maji ya gharika”.
Hivyo ndani ya safina kulikuwa na watu 8 tu!
Inasikitisha kiasi gani? watu 8 tu ndio waliopona kati ya mabilioni waliokuwa wanaishi duniani?..Mlango wa safina ulipofungwa watu walitamani kuingia lakini wakashindwa.
Na sisi je tutapataje kupona tusipouthamini wokovu mkuu namna hii? (Waebrania 2:3). Na dunia hii ya mwisho biblia inasema watakaopona ni wachache sana, watakaonyakuliwa ni wachache sana..Ni wale tu watakaojitahidi kuingia kwa kupitia mlango mwembamba
Luka 13.24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.
27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu”.
Tujitahidi tuwe mimi na wewe
Maran atha!
Mada Nyinginezo:
NUHU ALIJENGA SAFINA KWA MIAKA MINGAPI?
NUHU ALIWALETAJE LETAJE WANYAMA KWENYE SAFINA?
Kuzimu ni mahali, ambapo roho za watu waliokufa zinakwenda..Ni sehemu ya rohoni ambayo haionekani kwa macho ya kibinadamu..
JE! WANAOENDA KUZIMU NI WATU GANI?
Wanaoenda kuzimu ni watu ambao wameasi Neema ya Yesu Kristo, wale wote ambao waliikataa Neema ya Msalaba iliyoletwa na Mwana wa Mungu Yesu Kristo, watahesabika kuwa na hatia ya kuingia kuzimu…Kwasababu biblia inasema tunahesabiwa haki kwa Neema, ambayo hiyo inatokana na Imani ya kumwamini Yesu Kristo.
Kwahiyo mtu anapokufa, katika dhambi (Yaani nje ya Neema ya Yesu Kristo) anashuka moja kwa moja kuzimu, ambako huko kuna mateso makali, na roho yake inakuwa imefungwa. Atakaa huko mpaka wakati wa mwisho wa KITI CHEUPE CHA HUKUMU, Ambapo biblia inasema wafu wote watafufuliwa na kisha kuhukumiwa kulingana na matendo yao, hivyo mtu aliyekufa katika dhambi atasimama siku ile mbele ya kiti kile cheupe cha Hukumu na kisha kuhukumiwa sawasawa na matendo yake. Na baada ya kuhukumiwa atahamishwa kutoka kuzimu alipokuwepo na kuhamishiwa katika ZIWA LA MOTO, Ambako kuna matezo mengi zaidi..
Kinyume chake wanaokufa katika haki sasa, wanakwenda mahali panapoitwa Paradiso, mahali pa raha, wakingojea ufufuo wa Unyakuo ambapo watafufuliwa na kuvaa miili ya Utukufu na kisha kwenda Mbinguni kwa Bwana.
Je Umempa Bwana Yesu maisha yako? Upo ndani ya Neema ya Yesu Kristo, au unasubiria ufe na kwenda kuzimu? Kumbuka hakuna nafasi ya Pili ya kutubu baada ya kushuka kuzimu..Kila atakayeingia kuzimu atasubiria adhabu ya ziwa la moto.
Bwana akubariki!
Mada Nyinginezo:
KUMWAMBIA MTU MWENYE DHAMBI KUWA ATAKWENDA KUZIMU ASIPOTUBU JE! NI KUHUKUMU?
NITAAMINI VIPI KAMA KUNA MBINGU AU KUZIMU?
JIHADHARI NA ROHO ZIDANGANYAZO.
UTHABITI WA AGANO LA MUNGU KWA MKRISTO.
Jambo ambalo watu wengi hawafahamu ni kuwa ndani ya mtu kuna kitu kinachoitwa DHAMIRI.. Hichi ndicho kinachomshuhudia mtu kuwa alichokifanya ni sahihi au sio sahihi hata kama jambo hilo litaonekana mbele za watu ni jema, ikiwa ni baya, basi ndani ya moyo wake mtu huyo dhamira yake yenyewe tu itamshuhudia kuwa alichofanya sio sahihi, au kama kitendo alichokifanya ni sahihi, basi dhamira yake vilevile itamshuhudia hivyo hata kama ulimwengu mzima utasema alichokifanya ni kibaya.
Sasa mtu anapofanya kosa, labda tuseme labda kamtukana ndugu yake, au katoka nje ya ndoa kisirisiri, au kaiba, au kamsengenya mwenzake, au kamsababishia mwenzake jambo baya pengine kamwambukiza ugonjwa wa ukimwi kwa makusudi, moja kwa moja ndani ya moyo wake mtu huyo, Dhamiri yake inamshuhudia kafanya kitendo baya…
Hivyo siku ile ya mwisho Mungu ataihukumu dhamira yake.
1Timotheo4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, WAKICHOMWA MOTO DHAMIRI ZAO WENYEWE;”
Dhamiri yako inakushuhudia kabisa umefanya makosa.
Wengi wetu tunaogopa tuomba msamaha, bali tunatafuta njia mbadala ya kujisafisha..
Mimi sio mfuatiliaji wa mambo ya siasa lakini linikutana na jambo moja nikajifunza, kama wewe ni mfuatiliaji wa Siasa utakumbuka kuna kipindi baadhi ya wabunge na mawaziri walimzungumzia vibaya Mheshimiwa Raisi, na sauti zao zikarekodiwa na kusikiwa karibu kila mahali nchi nzima..
Lakini baadhi yao, walipoona kuwa walichokifanya sio sahihi, walijisalimisha wenyewe na kwenda kumfuata Raisi ikulu kumwomba msamaha..Na mmojawapo akakiri mwenyewe na kusema tangu ule wakati mambo hayo yalipojulikana hakuwa na Amani kabisa, hata usiku usingizi alikuwa hapati, lakini sasa anasema baada ya kumwona Raisi na kumwomba msamaha, ile amani yake yote imemrudia tena..
Unaona hapo? Kilichokuwa kinamtesa ndani ya nafsi yake ndio hiyo dhamiri ambayo pengine hata wewe inakusumbua leo hii, Dhamiri yake ilikuwa inamshuhudia kuwa alichokifanya kweli sio sahihi, hivyo moja kwa moja hakwenda kutafuta njia mbadala ya kujisafisha, kwa namna yoyote ile, kama angefanya vile basi ile hali ya kuhukumiwa bado ingeendelea kubaki ndani yake, haijalishi watu nchi nzima itamwona ameonewa..Hivyo njia pekee ilikuwa ni kwenda kuomba msamaha.
Vivyo hivyo na wewe pengine umefanya jambo unajua kabisa sio sahihi,..na dhamiri yako inakushuhudia, nataka nikuambie usikawie kuomba msamaha, ikiwa ulimkosea mzazi wako basi mfuate na kumwomba msamaha, ikiwa ulimkosea rafiki,au bosi, au jirani, mke wako, mume wako au Mungu mwenyewe kwa kufanya dhambi za makusudi mbele zake basi usikawie kuomba msamaha,..
Kwasababu faida ya kwanza utakayoipata kwa kuomba msamahani ni kuwa utakuwa HURU na kujihisi AMANI nyingi. Ipo sauti inaweza kukwambia ndani yako Aaah! Yule hatakusamehe, au aah! Yule atakuona wewe ni mnyonge!!..Nataka nikuambie hakuna mtu ambaye akiona mtu amejishusha mbele zake na kumwomba masamaha asimuhurumie Yule mtu, hakuna…Hata kama ni wewe ukiona mtu ambaye siku moja alikusema vibaya akaja kwa upole na kukiri kuwa alikukosea, akaomba msamaha kwa dhati kabisa, ukamchukia mtu huyo haiwezekani..Kwanza ndivyo utakavyompenda zaidi..Sasa na wewe usiogope kwenda kuomba msamaha..fanya haraka kabla hujafa katika hali hiyo.
Pia Mungu anataka kitendo cha kuomba msamaha kiwe sehemu ya maisha yetu mbele zake,..Na ndio maana hata katika ile sala ya Baba yetu..utaona tunasema Utusamehe dhambi zetu, kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea.
Mathayo 6:9 “Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,
10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
11 Utupe leo riziki yetu.
12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]”
Hivyo usiogope kuomba msamaha.
Ubarikiwe.
Mada nyinginezo:
SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
Bwana Yesu alikuja, akaondoka naye atarudi tena?
Swali ni je! atarudi kufanya nini?
Jibu: Atarudi kuitawala hii dunia pamoja na watakatifu wake, Biblia inasema dunia hii, enzi na Mamlaka amepewa Yesu na Mungu Baba…Mamlaka hayo, hapo mwanzo yalitoka kwa Mungu…akampa Adamu…Adamu akayapoteza, na shetani kuyachukua…Na alipokuja Yesu Kristo, shetani alinyanganywa mamlaka hayo na na kukabidhiwa Yesu Kristo. Hivyo ni lazima Kristo aje kutawala dunia..Kwasababu hakuna mamlaka yoyote isiyokuwa na Utawala.
Mathayo 28:18 “Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani”.
Na kama atakuja kutawala, wapo watu waovu wasioupenda utawala wake, hivyo hao atawaondoa..na wale wanaoupenda atawapa thawabu na nafasi za kutawala naye.
Ufunuo 2:20 “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi”
Kwa urefu jinsi utawala huo utakavyokuwa fungua somo hapa chini lenye kichwa kinachosema UTAMBUE UTAWALA WA MIAKA 1000
Bwana akubariki.
Mada Nyinginezo:
BWANA ALIPOSEMA KUWA YEYE NI “MUNGU WA MIUNGU” ALIKUWA NA MAANA GANI?..JE! YEYE NI MUNGU WA SANAMU?
JE! WATAKAOENDA MBINGUNI NI WENGI?
SWALI: Katika Biblia tunamsoma Mwanamke mmoja aliyeitwa Mshunami, ambaye alimsaidia Nabii Elisha sehemu ya malazi wakati wa huduma yake..Mwanamke huyu aliitwa Mshunami
2 Wafalme 4:12 “Akamwambia Gehazi mtumishi wake, Mwite yule Mshunami. Naye alipokwisha kuitwa, akasimama mbele yake. 13 Akamwambia, Sema naye sasa, Tazama, wewe umetutunza sana namna hii; utendewe nini basi? …”
Sasa Swali Mshunami maana yake nini?
JIBU: Ukisoma Mlango huo kuanzia juu kidogo, utaona kuwa Mshunami sio jina la mtu bali ni jina la sehemu..
2 Wafalme 4:8 “Hata ikawa siku moja, Elisha alikwenda Shunemu; na huko kulikuwa na mwanamke mmoja mwenye cheo; naye akamshurutisha aje ale chakula. Ikawa kila alipopita njia ile, huingia kula chakula”.
Kwahiyo Mshunami sio jina la Mtu, bali ni jina la mahali…Katika Israeli kulikuwa na mahali panapoitwa “SHENEMU” Kwahiyo mtu yeyote awe mwanamke au mwanamume kama ametokea sehemu hiyo basi aliitwa Mshunami…Ni sawa na nchi Tanzania, yeyote aliyetokea huko ataitwa Mtanzania.
Hivyo SHUNEMU ilikuwa ni Eneo la Israeli, lililokuwa urithi wa kabila la Isakari…Tunalithibitisha hilo katika kitabu cha…
Yoshua 19:17 “Kisha kura ya nne ilitokea kwa ajili ya Isakari, maana, ni kwa ajili ya wana wa Isakari kwa kuandama jamaa zao.
18 Na mpaka wao ulifikilia Yezreeli, na Kesulothi, na Shunemu“
Na sio tu huyu mwanamke aliyemsaidia Nabii Elisha alitokea huko shunemu, kuna wanawake wengine pia biblia imerekodi walitokea huko huko shunemu…Mmoja wapo na Abishagi aliyeletwa kwa Mfalme Daudi
1 Wafalme 1:3 “Basi wakatafuta kijana mzuri mipakani mwote mwa Israeli, wakamwona Abishagi, Mshunami, wakamleta kwa mfalme.
4 Naye kijana huyo alikuwa mzuri sana; akamtunza mfalme, akamtumikia; walakini mfalme hakumjua”
Mungu akubariki
Mada Nyinginezo:
TUSIFUNGWE NIRA PAMOJA NA WASIOAMINI.
KWANINI TUWE WENYE BUSARA KAMA NYOKA?
TUMEAMBIWA TUNAPOSALI TUSIPAYUKE-PAYUKE, JE! HUKO KUPAYUKA PAYAUKA NDIO KUPI?
Mpaka mtu au kitu kiweze kupaa ni wazi kuwa kimefanikiwa kushinda hali inayoweza kukivuta chini. Na ndio maana kinachopaa kama ndege huwa kina kasi zaidi na kinaona mbali sana tofauti na kitu kinachotembea. Hata mtu akijiona kwenye ndoto anapaa kutoka sehemu moja hadi nyingine huwa anajiona ni mwepesi sana, na anayokasi tofauti na anavyoota ndoto nyingine.
Sasa ndoto hizi zinaweza kutoka katika vyanzo viwili, chanzo cha kwanza ni kwa Yule mwovu. ili kujua ndoto uliyoota inatoka kwa Yule mwovu, utaona pengine unapaa na watu usiowajua na wanakupeleka usipojua, au unaenda sehemu za kutisha, na unapoamka unakuwa huna amani umejawa na hofu na wasiwasi mwingi, ukiona hivyo fahamu kuwa ndoto hiyo ni ya kutoka kwa Yule mwovu, hivyo kama wewe ni mkristo, unapaswa uikemee saa hiyo hiyo kwa jina la YESU na mambo kama hayo hayatakutokea tena..
Lakini ikiwa unaota unapaa tu katika mazingira ya kawaida labda tuseme nyumbani, au hata kama ni maeneo usiyoyajua lakini ni ya asili na unajiona unaowezo wa kuruka mbali sana kama vile upo mwezini, na ndoto hiyo inajirudia rudia na ukiamka huoni chochote,kawaida tu, basi unapaswa uzingatie kwasababu ni Mungu anakupitishia ujumbe wake hapo na hivyo umefanya vema kutafuta kujua tafsiri yake.
Sasa kama bado upo nje ya YESU KRISTO, Mungu anakuonya furaha yako, au mafanikio yako, ni ya muda tu, Kwasasa unaweza ukawa katika hali ambayo huwezi ukajifananisha na wengi, pengine umefanikiwa, au umesoma zaidi, au umepiga hatua Fulani, lakini mwisho wako utakuwa ni mbaya sana, kama hutamrudia muumba wako. Unapojiona unapaa ni ishara ya kufanikiwa Fulani.
Ayubu 20:4 “Je! Hujui neno hili tangu zamani za kale, Tangu wanadamu kuwekwa juu ya nchi,
5 Ya kuwa shangwe ya waovu ni kwa muda kidogo, Na furaha ya wapotovu ni ya dakika moja tu?
6 Ujapopanda ukuu wake mpaka mbinguni, Na kichwa chake kufikilia mawinguni;
7 Hata hivyo ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe; Hao waliomwona watasema, Yuko wapi?
8 ATARUKA MFANO WA NDOTO, asionekane; Naam, atafukuzwa kama maono ya usiku,”
Hivyo tubu umgeukie Mungu, kama ulikuwa unafanya mambo maovu, Tubu, uishi kama mkristo, kama ulikuwa unafanikiwa kutoka katika biashara haramu kama uuzaji pombe, au madawa ya kulevya, au rushwa au ushirikina acha mara moja mgeukie yeye…Bwana YESU anasema itakufaidia nini kuupata ulimwengu mzima halafu upate hasara ya nafsi yako.?..Unafanikiwa sasa lakini mafanikio yako yatakupoteza hivyo mgeukie Mungu..Bwana anakupenda na ndio maana anakuotesha ndoto za namna hiyo.
Lakini kama upo ndani ya Kristo, basi fahamu kuwa Mungu anakusisiza uzidi kumtazama yeye zaidi kwasababu anaompango wa kukushushia vipawa vya kimbinguni zaidi, kwasababu sikuzote mbinguni ndipo vipawa vilipo..
Zaburi 68:18 “Wewe umepaa juu, umeteka mateka, Umepewa vipawa katikati ya wanadamu; Naam, hata na wakaidi, Bwana Mungu akae nao”.
Hivyo songa mbele, kama ulikuwa unalegalega ungeza nguvu zaidi Bwana yupo karibu na wewe usiangalie mazingira yanayokuzunguka, zidi kumtafuta Mungu kwa bidii.ili kupaa kwako kusiishie tu hapa duniani bali mpaka mbinguni..Kama vile Kristo, alimpendeza Mungu akapaa hadi mbinguni kwa Baba, na sisi pia tumewekewa siku moja ya kupaa moja kwa moja na siku hiyo ndio ile siku ya UNYAKUO ambayo tutwenda kumlaki Bwana Yesu mawinguni. Maran Atha!
Ubarikiwe!
Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi
Mada Nyinginezo:
FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUZA KITU.
Zaburi 34:19 “Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote”.
Wengi wanauliza inawezekana mwenye haki akapitia mateso?..Jibu ni ndio! Mwenye haki anapitia mateso..
Tunaweza kuchukua mifano kadhaa katika Maandiko, Yusufu alikuwa mwenye haki, alimheshimu Baba yake kuliko kaka zake 11, hakusema uongo kwa Baba yake, na zaidi ya yote alipendwa na Baba yake kutokana na haki yako..Lakini tunasoma alipitia mateso makali…Alinusurika kuuawa na ndugu zake, aliuzwa Utumwani, akawa mtumwa, zaidi akafungwa gerezani akakaa huko sehemu ya mateso kwa miaka mitatu. Lakini kama maandiko yanavyosema Mateso ya mwenye haki ni Mengi lakini Bwana atamponya nayo yote. Hataacha hata moja!!
Tangu akiwa na kijana wa miaka 16 mateso yake ndio yalianza, na yalikuja kupungua akiwa na miaka 30 na kuisha kabisa akiwa na miaka 37…Bwana alimponya nayo yote…
Kadhalika Ayubu, alipotelewa na mali zake zote ndani siku moja, kondoo, Mbuzi, punda, ngamia, Wafanyakazi na zaidi ya yote akafiwa na Wanawe wote na akakaa vile kwa muda mrefu mpaka mkewe akamshauri amkufuru huyo Mungu wake akafe…Lakini Biblia inasema Mateso ya mwenye haki ni mengi, lakini Bwana atamponya nayo yote..
Ulipofika wakati wa kuponywa alivipata vyote alivyovipoteza kwa wakati mmoja na mara mbili zaidi.
Ipo mifano Mingi, unaweza ukaenda kuisoma mwenyewe, mifano kama ya akina Hana, Yefta, Daudi, Ruthu, Bathsheba, n.k
Wa mwisho mwenye haki kuliko wote na aliyepitia Mateso makuu kuliko wote ni BWANA WETU YESU KRISTO, Huyo alitemewa mate wazi wazi bila kosa lolote je wewe ambaye una dhambi ulishawahi kuchukiwa kiasi hicho cha kutemewa mate wazi wazi?!..yeye alisulibiwa akiwa tupu, je wewe ulishawahi kuchukiwa kiasi cha watu kufikiria kukuua kikatili kiasi hicho?
Kwahiyo kama unapitia mateso kwa ajili ya Imani yako nataka nikupe Moyo, Bwana atakuponya nayo yote, haijalishi ni siku ngapi, wiki, miezi au miaka mingapi itapita lakini siku moja utauona wokovu wa Bwana. Kama Bwana Yesu alivyouona wa Mungu kumfufua na kumweka juu sana zaidi hata ya Malaika.
Hivyo ukipitia mateso mtafakari Yesu, yeye aliponywa nawe utaponywa!
Waebrania 12:2 “tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.
3 Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu”.
Ubarikiwe sana, Kama Hujampa Yesu Maisha yako, Ni vyema ukafanya hivyo kabla siku ya Unyakuo haijafika.
Mada Nyinginezo:
IKO NJIA IONEKANAYO KUWA SAWA MACHONI PA MTU.
JE! MUNGU ANAUPENDELEO KWA WANAUME ZAIDI YA WANAWAKE?
JE! KUFANYA MASTURBATION (PUNYETO) NI DHAMBI?
Ufunuo 16:15 “(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)”
Kipindi Fulani nyuma kabla sijampa Bwana maisha yangu, niliota ndoto moja ambayo hadi leo sitaisahau, niliota nimejikuta nipo uchi, halafu nakatiza barabarani mjini maeneo ya posta Dar es salaam, sasa nilipojiona nipo vile nikawa ninatafuta namna ya kujificha..
Nikawa ninajibanza banza kwenye vikona vya majengo, nikivizia watu wapungue kisha nikimbilie upande mwingine, hivyo hivyo hadi kigiza kingie nikimbilie nyumbani, na kweli nilifanikiwa kujificha ficha hivyo hivyo nisionekane na watu au marafiki zangu mpaka nilipofanikiwa kufika nyumbani nikafurahi sana kwasababu nilijiona kama sijaoenekana na watu wengi, hususani na wanaonijua, lakini muda kidogo nikashangaa marafiki zangu wa chuo, tena wa kike wananijia kwa mshangao, wakiniambia mbona tumeona picha zako na video zako zimezagaa mtandaoni ukiwa uchi unakatiza barabarani, kwa kweli wakati nikiwa huko huko kwenye ndoto niliishiwa nguvu, nilijiona nipo katika aibu na fedheha ya milele isiyoweza kufutika, nikawa nawaza ni heri nisingezaliwa, kwasababu jambo kama lile halina tofauti na wale wanaoigiza mikanda ya video za zinaa, ambalo litaendelea kuwepo mitandaoni daima..
Sasa wakati nikiwa katika hali mbaya sana huko huko kwenye ndoto neno moja la kiingereza likaja mbele yangu, ambalo sikuwahi hata kulijua wala kulisoma mahali popote na hilo ndilo lililonifanya mpaka leo hii ninaikumbuka ndoto hiyo na neno lenyewe ni hili “NUDE”.. Muda huo huo nikashutuka, nikafurahi kwa kuwa kwa kuwa ilikuwa ni ndoto lakini nikasema ngoja nilitazame kwenye kamusi ya kiingereza lile neno lina maana gani ndipo nikakuta lina maana ile ile ya UCHI kama nilivyokuwa katika ndoto.
Kwa kweli nilikaa muda mrefu sana bila kuelewa ndoto ile ilikuwa na maana gani. Lakini siku nilipokuja kumpa Kristo maisha yangu, ndipo Bwana aliponifundisha maana ya ile ndoto niliyoita.. Nataka nikuambie ukiota ndoto yoyote upo uchi, halafu upo katikati ya kadamnasi, au mahali popote pale iwe shuleni, au kazini, au stendi ya mabasi, au sokoni, basi fahamu kuwa ndivyo hali yako ya kiroho ilivyo kwa sasa.
Sikuzote UCHI unazaa ni Aibu, na Aibu inakupelekea mtu kwenda kujificha..Adamu na Hawa walipoasi pale Edeni, walijiona kuwa wapo uchi, ndipo aibu ikawaingia na hapo hakuna kingine zaidi ya kwenda kutafuta namna ya kujisitiri..
Mwanzo 3:8 “Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone.
9 Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?
10 Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha”.
Hivyo unapoota ndoto hii moja kwa moja ujue kuwa utukufu wa Mungu umeondoka juu yako, au upo mbioni kuondoka kabisa juu yako kama hutataka kutubu dhambi zako, Na ndio maana Mungu anakuonyesha kwa jinsi hiyo hiyo unavyoweza kuona aibu ndivyo itakavyokuwa siku ile siri zako zote na dhambi zako zote unazofanya kwa siri zitakapowekwa wazi mbele ya malaika wake wote wa mbinguni
Warumi 2:16 katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.
Danieli 12:2 “Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele”.
Jiulize siku hiyo utakuwa katika aibu ya namna gani, utakuwa katika hali ya kudharauliwa kwa namna gani…ubaya zaidi aibu hiyo itakuwa ni ya milele..Mimi nilipokuwa katika dhambi Mungu aliniotesha hilo na haikuwa mara moja, ziliendelea kuja hivyo hivyo mara kwa mara mpaka nilipompokea Bwana Yesu.
Vilevile ndoto hii haimuhusu aliye nje ya Kristo tu peke yake hapana hata Yule ambaye yupo ndani ya Kristo lakini bado ni vuguvugu, Kristo anamtaka na yeye ayatengeneze mambo yake sawa kabla ya siku za aibu ya milele hazijamfikia..
Ufunuo 3:14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, NA UCHI.
18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, NA MAVAZI MEUPE UPATE KUVAA, AIBU YA UCHI WAKO ISIONEKANE, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”.
Unaona? Mungu anakupenda na anahitaji siku ile uweze kuketi pamoja naye katika kiti chake cha enzi, lakini kama tu leo hii utakuwa tayari kununua kwake mavazi meupe ili aibu ya uchi wako isionekane ambayo hiyo inakuja kwa KUTUBU, yaani kuufungua tu mlango wa moyo wako aingie ndani yako..Fungua tu mlango naye ataingia, anakupenda ndio maana anakuonyesha ndoto kama hizo.
Ubarikiwe.
Jiunge na Group letu ya whatsapp, la masomo ya kila siku kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUZA KITU.
TOFAUTI KATI YA NDOTO NA MAONO NI IPI?