Mtume Paulo anamwambia Timotheo “Bali hadithi za kizee, ZISIZOKUWA ZA DINI, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa.”( 1Timotheo 4.7).
Hizi hadhithi za kizee ni zipi? (kwa kiingereza zinaitwa old wives’ tales). Ni Misemo na hadithi zilizotungwa na watu wa zamani, ambazo kwa kuzitazama kwa nje zinaonekana kama zina ukweli fulani ndani yake, lakini kimsingi hazina uhalisia wowote, ni hadithi za uongo. Karibu kila jamii zipo na naamini hata wewe ulishakutana nazo.
Kwa mfano embu jaribu kutafakari maneno haya ambayo pengine ulishawahi kuyasikia.
* Ukiwa unakojoa hakikisha unatema mate chini, vinginevyo mama yako atavimba matiti.
* Mtoto mchanga akiangalia kioo haoti meno,.
* Mtu akikuruka hutorefuka.
* Mtoto wa kike akikaa katikati ya mlango, hatoolewa
* Ukipita makaburini, ukanyoosha kidole chako kuelekea kule, king’ate mpaka kiume vinginevyo mama/baba yako atakufa.
* Binti akipika huku aimba, ataolewa mbali.
* Mwanaume asilie kwenye sufuria la sivyo siku ya ndoa yake mvua nzito itanyesha.
* Ukimuona albino usipojitemea mate kifuani mwako, basi wewe nawe utazaa albino. n.k N.K. zipo nyingi.
Sasa mambo haya, yameaminika kwa wengi, mpaka imefikia hatua licha tu ya kubakia kwenye jamii ya watu wasiomini (yaani watu wasio wakristo), sasa imefikia mpaka kwa watu wanaomfahamu Mungu, waliookoka . Siku moja nilisikia mtu mmoja anayejiita mtumishi wa Mungu kwenye Whatasapp, anaitwa Apostle Vincent Mkalla(samahani kwa kulitaja jina) akitoa ujumbe ambao umesambaa sana mitandaoni na unajulikana na wengi, katika ujumbe huo, alitoa habari ya mti mmoja ujulikanao kama mti MWAMVULI, akisema mti huu, ukiwa umepandwa nyumbani, basi fahamu kuwa utaleta mabalaa makubwa katika hiyo nyumba, anasema kwanza kabisa ukichunguza utaona kuwa baba ya nyumba hiyo lazima afe, pili, unaleta hali ngumu za kiuchumi katika familia, tatu unaleta magonjwa, na pia unasababisha familia kutawanyika, familia kuwa na madeni, pia watu wa nyumba hiyo wanajikuta wanapitia katika hali ya kulaumiwa pasipo kujua chanzo ni nini n.k.…na mambo mengine aliyoyasema pale kuhusiana na mti..
Lakini kilichonisikitisha zaidi wakati huo nilipokuwa ninasikiliza nilikuwa na mama mmoja, ambaye naye alikuwa anausikiliza kwa makini sana, kwa hofu akiamini kinachozungumzwa pengine ni kweli, na siku chache mbeleni nilikwenda nyumbani kwao, ambapo mti huo wenye kivuli ulikuwa umepandwa uwani, nikakutwa umekatwa, hali kadhalika niliporudi nyumbani kwetu kwa mama, nikakutwa umekatwa,maana hata nyumbani upo, na sehemu nyingine nyingi.. Kwa hofu kwamba madhara yatokanayo na mti huo waliosikia kutoka kwa mtumishi huyo wa Mungu yasiwakute.
Kaka/Dada hizi ni nyakati za mwisho na biblia inasema..
1 Timotheo4 : 1-2”Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wenginewatajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
Hizi ndizo siku hizo za mwisho, Na hizi ndio HADITHI ZA KIZEE ZISIZO ZA DINI Mtume Paulo anamwonya Timotheo ajiupushe nazo, ni mafundisho ya mashetani, hadithi ambazo zinafanya watu wapoteze shabaha ya kuujua uweza wa Mungu bila wao kujua wakidhani kuwa vitu vya asili vinaweza kuathiri hatma zao na sio mambo ya rohoni. Na hilo ndio linalowafanya wengi mpaka kufikia hatua ya kuabudu sanamu, kwasababu imani yao kidogo kidogo ilianza kuhamishwa kutoka kwa Mungu, na kuanza kuangalia mambo ya mwilini kama suluhisho la mambo yao na matatizo yao. Mwisho wa siku hata mtu akiwambiwa kaoteshe mkaratusi katikati ya shamba lako utapata hela atakwenda na kufanya hivyo kwasababu siku nyingi tayari alishahamishwa Imani yake kutoka katika Neno la Mungu na kuingizwa katika “Maashera” (ibada za masanamu), na pasipo yeye kufahamu hajui kuwa anamwabudu shetani mwenyewe..
Dada yangu tena sikumoja ananiambia ukiona mjusi au mende, kwenye nyumba hiyo ni ishara mbaya, ya kutokufanikiwa kiuchumi.
Siku nyingine nikakuta Ua moja ambalo sikujua maana yake, mpaka siku moja mama yangu mdogo ambaye amesema ameokoka aliponiambia ua lile, ni la Baraka linaeleza hali ya kiuchumi ya nyumba hiyo,likistawi basi uchumi unastawi, likisinyaa basi uchumi ni mdogo..Niliposikia vile nilisikitika sana rohoni.
Kumbukumbu 16:21 “Usipande mti uwao wote kuwa Ashera kwako kando ya madhabahu utakayofanya ya Bwana, Mungu wako”.
Sasa Yapo mambo mengi hatuwezi kuyasema yote hapa, yanafundishwa na baadhi ya watu wanaojiita ni watumishi wa Mungu na yanazidi kukithiri, na kusambaa, naamini hata na wewe ulishakutana yao.
Ndugu nataka nikuambie ukweli wa kibiblia hakuna ubaya wowote katika miti, ikiwa imepandwa kwa nia njema, hakuna ubaya wowote wa vyakula vya aina Fulani, ikiwa navyo vimepokelewa kwa shukrani kama biblia inavyosema, vyote vinatoka kwa Mungu, na vimeumbwa na Mungu..Kusema mti Fulani unasababisha kifo cha baba wa nyumba, jiulize ni nyumba ngapi duniani zimefiwa na wazazi wao,
Unaposema miti inasababisha hali mbaya kiuchumi ni familia ngapi duniani zinapitia matatizo ya kiuchumi?. Ndugu yangu, chanzo cha matatizo yote ni DHAMBI, na kutokumjua Kristo na uweza wake, lakini badala yake, wanafundisha chanzo cha mafarakano na magombano katika familia ni MITI, tangu lini mti ukimfarakanisha mtu na mtu?..Na mtu huyo anajiita ni mtumishi wa Mungu, na bado tena mkristo anamwamini mtu wa namna hiyo kisa tu katumia vipengele fulani vya maandiko kutibitisha uongo wake, na wengi wanamwamini, hujui kuwa hata shetani alitumia maandiko kuuthibitisha uongo wake kwa Yesu kule jangwani.
Hofu zimewakubwa watu wengi mpaka sasa, kila kitu wanachotokea hata kujikwaa kidogo tu anasema kalogwa, akipishana na paka, kuna mtu kamwendea kwa mganga, akipishana na mbwa mweusi usiku basi ni mchawi, sasa mbwa wa kweli atakuwa ni yupi? Kama kila mbwa ni mchawi, bundi wa kweli aliyeumbwa na Mungu atakuwa ni yupi kama wote ni wachawi, paka wa kweli aliye mweusi ambaye aliumbwa na Mungu atakuwa ni yupi kama kila paka mweusi ni mchawi,?…utasikia mwingine anakuambia jicho likicheza kidogo tu anasema kuna mtu anamsema, akipiga chafya kuna watu wanamtakia mabaya, huyo ni mkristo anazungumza maneno hayo. ..HADITHI ZA KIZEE zisizo na dini…
2 Timotheo 4.3 “Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;
4 nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.
5 Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako.”
Timotheo kama mwalimu alionywa ajiuepushe na injili za namna hiyo, hali kadhalika azikatae, azikemee zisifundishwe katika kanisa la Mungu, na sisi leo tunazikemea na tunazikataa zisifundishwe kwa watu..Leo watu wengi wanafahamu zaidi habari za uchawi na ushirikina kuliko hata kumjua Mungu, shuhuda zilizojaa kwenye kichwa vya watu ni uchawi tu, kana kwamba huo ndio msingi wa kuwa mtu wa rohoni. Na hiyo inapelekea watu kuwa WAOGA kwa shetani, kwasababu mioyo yao imejazwa shuhuda za shetani zaidi kuliko Mungu, Mtu anaogopa hata kusalimia, au kumsaidia mtu asiyemjua kwa hofu tu ya uchawi, lakini haogopi maneno ya Mungu yanayomkataza yeye kwenda kutenda dhambi za makusudi. Na siku zinavyozidi kwenda hofu hii inazidi kuongezeka katikati ya watu..(hususani wanaojiita wakristo).
Hivyo hata ukiwaeleza nguvu zilizokatika Neno la Mungu, haziwasaidii sana, kwasababu mioyo yao haijajazwa na Neno la Mungu bali Neno la Shetani. Kwasababu biblia inasema Hazina yako iliyo ndipo utakapokuwepo na moyo wako. Na hivyo kila elimu inayokuja inawachukua..leo hata wakiambiwa wasipange mchicha kwenye nyumba zao zinawaletea umaskini watafanya hivyo, kesho wakiambiwa wasitumie mafuta ya nazi ya roho za majini watatatii, kesho kutwa wakiambiwa wakate kidole gumba kinawaletea mikosi na wakithibitishiwa na maandiko mawili matatu, watafuata..kwasababu ndani yao kumjua Mungu hakupo..Biblia inasema Tumjue sana Mungu ili tuwe na AMANI sio tumjue sana shetani ndio tuwe na Amani…Elimu ya shetani haileti amani bali hofu.
Mtu akija kukuambia leo, kuna bundi nimemwona batini kwako jana usiku, na ni mchawi…kitakachofuata hapo ni hofu, na wala si kitu kingine, utaanza kuiogopa hata nyumba yako unayoishi…
Lakini leo hii utakaposikia elimu iliyopo katika uweza wa Mungu…Kwamba Kristo alitwaa madhaifu yetu na yeye anatupenda kiasi cha kutuhurumia, na tena anatuambia tuutafute kwanza ufalme wake na haki yake, Hakuna hata unywele wetu mmoja utakaopotea, na zaidi ya yote anatuambia sisi tuliomwamini kuwa Baba yetu wa mbinguni anatujali sisi kuliko baba zetu wa kimwili..Mambo hayo ukiyajua yanakupa amani na furaha katika wokovu…na hayakufanyi kuwa mateka zaidi yanakufanya kuwa huru, elimu ya mashetani ndio inayokufanya kuwa mateka, na matunda ya roho ya shetani ndio haya..uwoga, hofu, mashaka, kukosa raha, uchungu, wasiwasi,visasi, wivu, hasira, chuki n.k mambo haya yote yanazalishwa na roho za mashetani kupitia elimu zake. Na shetani ndio anataka mambo hayo yawepo ndani ya mtu, ili apate nafasi ya kumkandamiza kimawazo na kiakili, Lakini Roho Mtakatifu ndani ya mtu, hayupo hivyo na wala matunda yake hayapo hivyo ….matunda ya Roho wa Mungu ndio haya..
Wagalatia 5: 22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria”.
Hizi ni nyakati za hatari ndugu yangu, mafundisho kama hayo yatazidi kuongezeka, hayataishia kwenye miti, wanyama, na vyakula, yataendelea mpaka kwenye mwili wako, na maumbile yako..Hivyo usipokuwa makini kwa kutaka kukaa chini na kujifunza zaidi uweza wa Mungu katika Neno lake, KUMJUA SANA MWANA WA MUNGU (Waefeso 4:13)…badala yake unapenda kutafuta njia za mwilini kutatua matatizo yako nataka nikuambie ukweli wote, shetani atakutesa sana, utakosa raha ya kuishi hata kama unajiita umeokoka… na mwisho wa siku utachukuliwa na wimbi hilo na manabii, na waalimu wa uongo, ambao hao Injili ya kweli ya Kristo ipo mbali nao.
Sina muda wa kutosha ningekupa mifano kadha wa kadhaa ya hawa watumishi wa shetani ambao mimi binafsi nimewahi kukutana nao..ambao wengine wanatumia mifupa, na nywele, na biblia kuchukua watu mateka na sana sana wanawake kwasababu wao ndio sana sana wanahangaika huku na kule kutafuta mambo ya rohoni…Watumishi hawa ni ngumu sana kuwagundua kwasababu shetani kawanoa vya kutosha kama hujui maandiko wanakuchukua…na target yao kubwa ni wanawake…
1 Timetho 3:5 “…wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.
6 Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi;
7 wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.
8 Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani”.
2 Petro 1.16 “Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake”.
Kristo alipokuwa duniani hakutuelekeza katika miti, wala vyakula, wala wanyama, wala hakutuhubiria habari za washirikina na wachawi, badala yake alitumia muda mwingi kutufundisha jinsi ya kuwa na mahusiano ya karibu na Baba yetu wa mbinguni kama yeye alivyokuwa kwa baba yake..Na hilo ndio jambo la muhimu kwasababu ukishajua nafasi yako kwa Mungu wako basi hayo mambo mengine hayatakusumbua, hutakuwa na hofu, ya kifo, au matatizo, au shida, au chochote kile kwasababu baba yako atakuwa pamoja na wewe wakati wowote kukusaidia…hutakimbilia kwenda kuisingizia miti, na paka, na mbwa, na bundi, na mijusi, na popo, na fisi, kwa hali unayoipitia…Badala yake Mungu ndiye atakayekuwa jibu lako wakati wote.
Hivi unajua kwamba wapagani wasiomjua Mungu, hawakuanza hivi hivi kuabudu miti na mawe?..unalijua hilo?..walianza kidogo kidogo kufikiri tatizo Fulani linasababishwa na miti Fulani au mawe Fulani, na walipoisafisha ile miti na yale mawe waliona kama matatizo yameondoka lakini walipoona kuwa kuna mengine ni sugu..waliona njia pekee ni kwenda kwa unyenyekevu chini ya hiyo miti..kuiomba kwa upole na utaratibu iwaondolee hayo matatizo na endapo hayo matatizo yataondoka basi wanaahidi kuifanyia jambo Fulani labda kuipa heshima Fulani..na kwasababu ni shetani yupo nyuma ya ule mti..anaondoa lile tatizo lao kwa muda na wale wanadhani ni mti umesikia maombi yao, hivyo wanaugeuza ule mti kuwa mungu wao..na shetani anatuma maroho yake kuwaingia wale watu wakati mwingine wanaanza kuota ndoto zinazoutukuza ule mti au wengine wanaona vitu vya ajabu kwenye ule mti n.k..lengo ni kutoa umakini wao kumhusu Mungu wa Mbinguni na kuwaleta kuamini miti na mawe kama miungu…Na haishii hapo akishajua watu wameuamini ule mti kupita kiasi..anawapa mpaka nafasi ya wao kuomba maombi yao au kupeleka mahitaji yao kwenye ule mti na akawafanyia…
Sasa roho hiyo hiyo ndio inayoingia kwa kasi katika kanisa katika siku hizi za mwisho, wengi wanaingizwa kwenye ibada za sanamu pasipo wao kujijua, shetani anahamisha umakini wa watu kumhusu Mungu wa Kweli wa Mbinguni na kuwatengenezea watu miungu ya kuiabudu, miti, mawe, sanamu n.k
Warumi 8: 35 “Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?……..
38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,
39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu”.
Ni matumaini yangu kuwa umepata kitu na utazidi kuchukua tahadhari juu ya hizi HADITHI ZA KIZEE, na kuanza kumtazama Mungu ili njia zetu ziwe zimenyooka siku zote.Na tuwe na Amani.
Ubarikiwe. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
SI SHETANI BALI NI WEWE. (CHAGUA MEMA)
JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.
Shalom, Mtu wa Mungu karibu tujifunze Injili, uweza wa Mungu uuletao wokovu, leo tutajifunza kwa ufupi juu ya NGUVU YA UFUFUO ILIYOPO NDANI YA YESU KRISTO. Katika kitabu cha Yohana tunasoma maneno yafuatayo aliyoyazungumza Bwana Yesu.
Yohana 5: 25 “Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja,na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai.
26 Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake.
27 NAYE AKAMPA AMRI YA KUFANYA HUKUMU KWA SABABU NI MWANA WA ADAMU.
28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini WATAISIKIA SAUTI YAKE.
29 Nao watatoka; wale waliofanya MEMA KWA UFUFUO WA UZIMA, na wale WALIOTENDA MABAYA KWA UFUFUO WA HUKUMU”.
Katika mistari hiyo Biblia inasema Mwana kapewa amri na Baba ya kufanya hukumu na tena amepewa uwezo wa kufufua wafu kama vile Baba alivyo na uwezo wa kufufua wafu, tunayasoma hayo juu kidogo katika Yohana 5: 21 “Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na MWANA AWAHUISHA WALE AWATAKAO”.
Kama wengi wetu tunavyofahamu kuwa kuna ufufuo utakaokuja baada ya maisha haya kuisha ambapo wale wote waliotenda haki watafufuliwa na kuurithi uzima wa milele, na wale wote waliotenda mabaya watafufuliwa kwaajili ya hukumu, na kila mmoja atahukumiwa kulingana na matendo yake na wale waovu watatupwa katika lile ziwa la moto, lenye moto usiozimika, waangamie milele.
Sasa jambo la kujiuliza hapa ni kwanini, Bwana Yesu awafufue wale waovu na kisha awahukumu na awatupe katika ziwa la moto…kwanini asingewaacha huko huko mautini, awahukumu huko huko na kuwatupa kwenye lile ziwa la moto wakiwa huko huko mautini, kuna umuhimu gani au haja gani ya wao kufufuliwa na tena wakati kuzimu wataenda tu??.
Kuna siri nzito sana hapo. Lakini kwa ufupi ni kwamba, siku ile ya hukumu watu wote waovu watavaa miili yao waliyokuwa nayo hapa duniani..yenye damu na mifupa na macho na moyo, na kusimama mbele za Bwana, na kisha kuongea naye ana kwa ana, kutoa hesabu kwa kila jambo na kila uovu waliokuwa wanaufanya, mbele ya kiti cha Hukumu…Jambo hilo halitafanyika mtu akiwa katika roho, hapana bali litafanyika mubashara kabisa katika mwili kama tulivyo hapa duniani…Na katika ziwa la moto mtu hatatupwa katika roho, bali atatupwa akiwa na mwili wake wa damu na nyama, na utaungua kule na ukiisha ndipo roho itaendelea nayo kuteseka milele kwenye huo moto milele.
Kwahiyo leo hatutaingia sana huko, lakini napenda tujifunze Nguvu ya ufufuo.
Ukiutafakari kwa makini mstari huo utakuja kugundua kuwa Kumbe Ufufuo sio tija. Kwasababu watu wote watafufuliwa, waovu na wema..kinachojalisha ni sababu ya kufufuliwa kwako. Kama mtu alikuwa mcha Mungu basi ufufuo kwake utakuwa wa maana, lakini kama alikuwa mwovu basi ufufuo kwake utakuwa ni laana.
Na ufufuo maana yake, ni “kukirudishia tena uhai au maisha kitu kile kilichokuwa kimekufa”..hiyo ndio maana ya ufufuo.
Sasa kuna ufufuo wa roho ambao unaendelea sasahivi, ambapo watu wote WANAISIKIA SAUTI YA MWANA WA ADAMU, na wanafufuka kutoka kwa wafu katika roho…Na sauti ya mwana wa Adamu ni Habari njema inayohubiriwa duniani kote leo, habari za msalaba na wokovu uliopo katika Kristo Yesu, sasa wapo ambao wanafufuka kwaajili ya uzima wa milele na wapo ambao wanafufuka kwaajili ya hukumu.
Wako ambao pindi tu wanapoisikia injili macho yao yanafumbuliwa (wanafufuka katika roho), hii inatokea pale ambapo wanachomwa dhamiri zao ndani ya mioyo yao, na kujijua kuwa njia zao sio sawa, hivyo kwa moyo mnyoofu wanaitii injili na kuokoka kikamilifu,wanaacha njia zao mbaya za kale, na kuzaliwa mara ya pili wakati huo huo na kuwa viumbe vipya.
Na wapo pia ambao wanapoisikia tu injili macho yao yanafunguka (wanafufuka) na kujua kabisa ndani ya mioyo yao Neno la Mungu ni kweli, na Roho Mtakatifu anawashuhudia kabisa kuwa Njia ya wokovu ni hii, na njia wanayoiendea wao sio sawa…Roho anawafufua katika roho zao, lakini kwasababu wanapenda giza kulika Nuru wanaikataa ile njia ya kweli,..na kwa makusudi, hawataki kugeuka na kutubu, wanaendelea na njia zao mbaya, hawa ndio wanaofufuliwa sasa kwa ajili ya hukumu. Wanayafumba macho yao kwa makusudi ingawa wamepewa neema ya kuona..Wanafahamu kabisa hata wakifa sasa hivi wanastahili Jeahanum ya Moto, lakini bado hawataki kutubu. Hawa wamefufuliwa kwa ajili ya Hukumu.
Kwahiyo ndugu unayesoma ujumbe huu, usifurahie tu Roho wa Mungu anapokushuhudia ndani yako kuwa KRISTO ndiye njia ya kweli na uzima, huo ni ufufuo tu! Ambao hata waovu wanapewa…hata waovu katika nyakati hizi za mwisho wanapewa neema hiyo mioyoni mwao kujua kuwa Kristo ni njia ya kweli na uzima, na kwamba hakuna uzima wowote nje yake yeye.. Hiyo ni neema ya ufufuo ambayo watu wote wanapewa waovu na wema..Lakini swali ni je! Unafufuliwa kwa sababu gani?.
Kama unaisikia injili kila siku inayokuambia ulevi, uasherati, utukanaji, rushwa,uvaaji mbaya ni dhambi, mustarbation, usagaji, na pornography…na ndani ya moyo wako unajua kabisa ni kweli ni dhambi kufanya mambo hayo..fahamu tu! Ufufuo uliopewa ni wa hukumu na sio wa uzima wa milele, haijalishi unayajua maandiko kiasi gani, au umezungumza na malaika kiasi gani,au umemwelewa Kristo kiasi gani, au umeponywa na Yesu kiasi gani,
Mtume Paulo kwa uwezo wa Roho aliandika habari za watu hawa wafanyao dhambi kwa makusudi huku wakijua kabisa wanayoyatenda sio sawa…Wameisikia injili (wakapata ufufuo katika roho zao)..lakini ufufuo wao ukawa ni wa mauti.
Warumi 1: 18 “Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.
19 Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, KWA MAANA MUNGU ALIWADHIHIRISHIA.
20 Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; HATA WASIWE NA UDHURU
21 kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.
22 Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;
23 wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo.
24 Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao.
25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.
26 Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;
27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.
28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,
30 wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao,
31 wasio na ufahamu, wenye kuvunjamaagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema;
32 ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao”.
Unaona Biblia inasema..”kwa maana walipomjua Mungu hawakumtukuza” na inasema “Mungu aliwadhihirishia ndani yao”..ikiwa na maana kuwa watu hawa, nuru ya haki iliwazukia ndani yao, au kwa lugha nyepesi tunaweza kusema ufufuo ulipita ndani ya roho zao, wakaiona kweli na kuiamini lakini walipoiamini hawakuifuata!..Hilo ndio jambo la kuogopesha, mtu anauona ukweli lakini haufuati…Nimewahi kuona madaktari bingwa ambao wanajua elimu yote ya biolojia ya ini na figo, na ni washauri wazuri wa kushauri watu wasitumie pombe na sigara kwani ni hatari kwa afya zao, lakini wao ndio watumiaji wakubwa wa mambo hayo, na wanakufa kwa magonjwa hayo hayo…Na ukiwauliza kwanini wanafanya hivyo na hali wanajua kwa kina na mapana madhara ya hivyo vitu katika mwili, zaidi hata ya watu wengine wanavyojua…wanakujibu basi tu! Nimeamua na nimependa kufanya hivyo, na atazidi kukuambia yupo tayari kufa na wala haogopi.
Sasa watu wa namna hii pia wapo katika Kanisa la Kristo, wanajua kabisa uzinzi ni dhambi, kwamba waasherati wote sehemu yao ni katika lile ziwa la moto, na wengine wamepewa maono na ndoto za jehanamu wameonyeshwa mahali wanawake wanaovaa vimini na suruali walipo lakini hao hao utawakuta wanaendelea kufanya hivyo bila uoga wowote. Ni kwasababu gani wanafanya hivyo? Ni kwasababu wapo katika ufufuo wa hukumu. Mpaka unaweza ukasema kwanini Mungu awafunulie mioyo yao waiamini injili halafu na bado wasiifuate si ni bora asingewapa kabisa neema hiyo..kuliko kuwapa halafu wasiifuate?..Jibu ni rahisi… “kila mtu lazima aisikie sauti ya mwana wa Adamu na kutoka kaburini aliko”.
Kadhalika pia usifurahie kwasababu kazi yako iliyokuwa imekufa ikafufuliwa tena, kwasababu huo unaweza ukawa ni ufufuo wa mauti kwako, furahia kazi yako kufufuka kwa ajili ya ufufuo wa uzima..
Unapokwenda kuombewa kazi yako au afya yako na kupona, na kisha maisha yako hayageuki hata kidogo, zaidi ya yote ndio unakuwa mbaya kuliko ulivyokuwa hapo kwanza, hujisikii vibaya kuendelea na uasherati wako, wala kiburi chako, nataka nikuambie hiyo ni dalili moja wapo ya kazi yako kufufuliwa kwa ajili ya hukumu yako mwenyewe,..hiyo kazi yako yako itakuwa kitanzi kwako cha kukuua na hatimaye kukupeleka katika ziwa la moto…Biblia inasema “…Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza Mithali 1:32”.
Kwahiyo furahia pale kazi yako inapofufuka na kustawi na inazidi kukufanya kuwa mtakatifu na mkamilifu mbele za Mungu, mali zako zinapoongezeka ndipo na kiwango chako cha usafi kinavyozidi kupaa..hapo kazi yako itakuwa imefufuliwa kwa ufufuo wa uzima. Haitakupeleka jehanamu.
Bwana akubariki sana, kama hujampa Yesu Kristo maisha yako…usikawie kawie, kama amezungumza nawe moyoni mwako zaidi ya mara moja na kukushuhudia kuwa njia unayoiendea sio sawa, na wewe mwenyewe umehakikisha jambo hilo moyoni mwako, usijaribu kwenda kutatufa visababu vya kujihalalishia njia zako. Mtii leo, yeye anawakubali wakosaji, na anasamehe dhambi, akikusamehe amekusamehe kweli kweli hana visababu sababu vidogo vidogo vya kukushitaki tena au kukulaumu..Unakuwa mpya kabisa mbele zako.
Waefeso 5.14 “Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza.”
kwahiyo Hapo ulipo tubu, dhamiria kuacha dhambi zote ulizokuwa unazifanya nyuma, Fufuka sasa katika ufufuo wa Uzima katika jina La Yesu, na sio ufufuo wa Mauti, mfanye Bwana kuwa tumaini lako kuanzia leo na kuendelea.. Na baada ya kutubu katafute ubatizo kwani ni wa umuhimu sana kukamilisha wokovu wako na ni maagizo ya Bwana mwenyewe aliyoyatoa kwamba ni lazima kila mtu aliyempokea yeye akabatizwe, na ubatizo sahihi ni wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo kulingana na Matendo 2:38, na Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake mtakatifu atakayekusaidia kushinda dhambi na kukuongoza katika kuijua kweli yote ya maandiko.
Bwana akubariki. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
UTALIPWA KATIKA UFUFUO WA WENYE HAKI
WALE WATAKATIFU WALIOFUFUKA NA BWANA YESU WALIKUWA WAPI KABLA YA KUFUFUKA KWAO?
NIFANYE NINI ILI NIIKWEPE HUKUMU
Shalom mtu wa Mungu, ni kwa rehema za Bwana tumeiona siku ya leo, hivyo hatuna budi kumshukuru sote pamoja kwa mema anayotutendea na pia kushiriki katika kujifunza maagizo yake kila iitwapo leo. Hivyo nakukaribisha tutafakari kwa ufupi juu ya haya “madaraka ya wakati mkamilifu” yanayozungumiwa kwenye maandiko, tutayaona ni yapi, na yatakuja wakati gani?.
Biblia inasema.
Waefeso 1:9 “akiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake, sawasawa na uradhi wake, alioukusudia katika yeye huyo.
10 Yaani, KULETA MADARAKA YA WAKATI MKAMILIFU atavijumlisha vitu vyote katika Kristo, vitu VYA MBINGUNI na vitu VYA DUNIANI pia. Naam, katika yeye huyo;
11 na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.”
Sasa Kama ukisoma huo mstari wa 10 kwenye tafsiri nyingine za biblia kwa lugha iliyo nyepesi unaweza kusomeka hivi,
“Wakati mkamilifu utakapofika, basi vitu vyote ya mbinguni na duniani vitajumuishwa pamoja kwa yeye huyo..Au wakati uliokusudiwa (wa Mwisho) basi mambo yote ya mbinguni na ya duniani yataletwa pamoja katika yeye huyo (KRISTO YESU)..”
Ndugu tukimjua Kristo, na ukuu wake na uweza wake, basi hatutaishi maisha ya kutokujali tu, tukiwa hapa duniani, hatutauchukulia ukristo wetu kama kitambulisho cha dini tu kama wengine wanavyofanya badala yake tutaishi kwa mitume wa zamani walivyoishi,..Leo Tunaishi maisha ya uvuguvugu na machafu kila siku na huku bado tunajiita ni wakristo, ni kwasababu tumekosa ufunuo wa kumjua Yesu Kristo ni nani katika maisha yetu, tumekosa shabaha ya kufahamu ni mambo gani na gani yalimfanya Yesu kuja duniani, tunadhani alikuja kufa tu msalabani halafu basi, na sasa ameketi mkono wa kuume wa Mungu mbinguni akisubiria kurudi tena kuja kunyakua watu wake….Hatujui mengine zaidi ya hayo.
Hiyo ndio sababu inayotufanya tunaishi maisha ya kuukinai wokovu, tunaposoma habari za watu ambao walijitoa maisha yao, watu ambao hawakupenda maisha yao hata kufa kwa ajili ya Bwana, tukisoma habari ya Ibrahimu ambaye japo Mungu alimpa kila kitu lakini aliishi kama mpitaji hapa duniani kukaa kwenye mahema, akiutazamia mji wenye misingi (YERUSALEMU MPYA),sio hii ya sasa inayoharibika,(Waebrania 11:8)…watu ambao Mungu aliwapa kila kitu lakini hawakupumbazwa na vitu walivyopewa, macho yao wakati wote yalielekea juu, mfano wa Ibrahimu na Ayubu…Sio kana kwamba walikuwa hawajipendi hapana bali waliona mbele, walipokea ufunuo wa mambo yanakuja na hivyo wakaanza kujijengea misingi mizuri kuanzia hapa duniani ili wakifika kule, iwe heri kwao. Lakini sisi tunaona wokovu ni kama kitu-baki, ni kitu tu cha ziada, na sio kila kitu katika maisha yetu.
Hatujui kuwa Kristo sasa yupo katika hatua za mwisho kabisa za kutimiliza mambo yake yote, na yeye mwenyewe hakutuficha siku anakwenda kwa Baba alisema, “ninakwenda kuwaandalia makao”,
Sasa ni vizuri kufahamu kuwa Kristo alipokuwepo duniani alikuja kufanya upatanisho wa kitu vikuu vitatu.
1) UPATANISHO KATI YA SISI KWA SISI
2) UPATANISHO KATI YA SISI NA MUNGU
3) UPATANISHO KATI YA MBINGU NA DUNIA.
Kristo alikuja kutupatanisha sisi kwa sisi, kumbuka hapo mwanzo wayahudi (yaani Waisraeli) walikuwa hawachangamani na mataifa kabisa, Israeli limekuwa likijulikana ni Taifa teule la Mungu, Mungu alilolibariki kupitia Ibrahimu. Ilikuwa hakuna namna yoyote ile sisi watu wa mataifa tungeweza kumfikia Mungu, lakini kwa kupitia Bwana Yesu, sisi ambao tumezaliwa mara ya pili ni mamoja sawa na wayahudi, mbele za Mungu hakuna aliye juu ya mwenzake, bali wote tunakubaliwa sawa kwa kupitia damu ya Kristo. Hiyo ni nafasi kubwa sana ya upendeleo..Jaribu kufikiria taabu walizozipata wengine kwa muda mrefu sisi tunakuja kuzila kiuwepesi namna hiyo. Ni neema kubwa sana. Jambo hilo unaweza kulipata katika kitabu cha Waefeso..
Waefeso 2: 11 “Kwa ajili ya hayo kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa Wasiotahiriwa na wale wanaoitwa Waliotahiriwa, yaani, tohara ya mwilini iliyofanyika kwa mikono;
12 kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.
13 Lakini sasa, KATIKA KRISTO YESU, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo.
14 Kwa maana yeye ndiye amani yetu, ALIYETUFANYA SISI SOTE TULIOKUWA WAWILI KUWA MMOJA; AKAKIBOMOA KIAMBAZA CHA KATI KILICHOTUTENGA.
15 Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani.
16 AKAWAPATANISHA WOTE WAWILI NA MUNGU KATIKA MWILI MMOJA, KWA NJIA YA MSALABA, AKIISHA KUUFISHA ULE UADUI KWA HUO MSALABA.
17 Akaja akahubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali, na amani kwao wale waliokuwa karibu.
18 Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja.
19 Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu”.
Hali kadhalika Kwa kumwamini tu Yesu na uweza katika damu yake, basi moja kwa moja tunakuwa tumepatanishwa na Mungu na hivyo tunakuwa na uwezo wa kupakaribia patakatifu pa patakatifu mahali Mungu alipo juu sana, na kuzungumza naye uso kwa uso katika roho, na kupokea rehema itokayo kwake. mambo ambayo hapo mwanzoni hayakuwepo, ilikuwa ni kuhani mkuu tu, alipelekea maombi yake katika maskani iliyofanywa na wanadamu huku chini mfano wa ile ya mbinguni, kisha Kerubi wa Mungu pale chini ndiye aliyekuwa anayachukua hayo maombi na kuyasogeza mbele ya kiti cha enzi cha Mungu huko juu mbinguni, lakini sasa kwa kupitia damu ya Yesu, sisi wenyewe tuingia moja kwa moja mbinguni kwa damu ya Yesu, na kupeleka haja zetu na majibu ya maombi yetu, sawa tu na makerubi na malaika wa Mungu walio mbinguni, sisi na wao hatuna tofauti yoyote, mbele za Mungu tukiwa ndani ya Kristo ni kitu kimoja.
2 Wakorintho 5: 17 “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
18 Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, ALIYETUPATANISHA SISI NA NAFSI YAKE KWA KRISTO, NAYE ALITUPA HUDUMA YA UPATANISHO;
19 yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho”.
Na Jambo lingine la mwisho Kristo aliloleta NI KUIJUMUISHA MBINGU NA NCHI KUWA KITU KIMOJA..vitu vya mbinguni na vitu vya dunia, Sasa Hakuna yoyote ambaye angeweza kufanya jambo hili, inahitaji nguvu ya ajabu inayovuka viwango vya fikra za kibinadamu, inahitaji iwe muumba kufanya shughuli hii..
Wakolosai .1:9 “Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae;
20 na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; KWA YEYE, IKIWA NI VITU VILIVYO JUU YA NCHI, AU VILIVYO MBINGUNI”.
Sasa jambo hilo ndilo linalokuja kutokea katika WAKATI MKAMILIFU ULIOKUSUDIWA, Yesu aliposema naenda kuwaandalia makao, ili nilipo mimi na nyinyi muwepo, na makao hayo yamegawanyika katika sehemu tatu, ya kwanza ni makao ya roho zetu ambayo hata sasa sisi tuliopokea Roho Mtakatifu tupo ndani yake,
Waefeso 2: 6 “Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;”
Na makao ya pili ni MIILI MIPYA ambayo tutaipokea tukifika mbinguni miili isiyoharibika, na makao ya tatu ndio hiyo NCHI MPYA NA MBINGU MPYA…Ambayo hiyo sasa itashuka kutoka mbinguni na kutua hapa duniani…Itashuka Hapa hapa duniani hatutaishi mbinguni milele, makao yetu yatakuwa ni hapa maandiko yanasema hivyo.
Na ndio hapo hilo neno linalosema “atavijumlisha vitu vyote katika Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya duniani pia.” Ndipo litakapotimia,
Ndugu yangu Kristo anayo nafasi kubwa sana maishani mwetu, kwanza kati yetu sisi wanadamu, pili kati yetu sisi na Mungu na tatu kati ya makao yetu ya sasa na ya yale ya baadaye..Embu jaribu kufikiria, ikiwa leo hii hutaweza kuzishiriki Baraka za Ibrahimu tu ambazo Mungu alimwahidia yeye na uzao wake (Wayahudi) kuwa watakuja kuirithi nchi, japo kweli walikuwa vile lakini bado hawakuweza kumkaribia Mungu, sasa wewe ambaye sasa ni mtu wa mataifa na bado huna habari na Kristo siku ile utaonekania wapi?..Itawezekanikaje kumfikia Mungu, au utamshawishi vipi Mungu hata akusikie maombi yako sasa wewe ambaye unasua sua katika mawazo mawili.
Hujapatanishwa, na Wayahudi, hujapatanishwa na Mungu, bado hujapatanishwa na hayo makao mapya yanayokuja huko mbeleni, unatagemea vipi, Mbingu utaiona ndugu?. Matumaini yako ni nini?, tegemeo lako lipo kwa nani?…
Muda umekaribia wa madaraka ya wakati mkamilifu kuanza, Kristo kuvileta vitu vyote pamoja, chini ya mikono ya MUNGU..lakini wale wote wanaopinga, biblia inasema kitakachosalia kwao ni kuangamizwa milele.
Yesu yupo mlangoni ndugu yangu, fanya uamuzi sasa, wakati ndio huu, pokea kuponi yako sasa ya kuwa na uhakika wa maisha baada ya kufa, ulimwengu huu unaousumbukia unakuahidia nini miaka yako 100 mbeleni kama sio ukomo wa mauti?.
Kwanini usikubali NEEMA HII YA UPATANISHO inayokuja kwako bure, ingekuwa ni wanadamu ungejaza fomu ngapi ili ukubaliwe tu uwe raia wa taifa fulani?, ungejaza fomu ngapi ili ukubaliwe kuwa mrithi wa taifa fulani?, ungejaza form ngapi ili ufikie tu kigezo cha kumfika raisi wa taifa fulani?. Lakini kwa Mungu haipo hivyo, vyote hivyo ni bure, na vinapatikana hata hapo ulipo sasa hivi.
Chukua maamuzi sasa, kabla ya mlango wa neema kufungwa. Unachopaswa kufanya hapo ulipo ni kutubu kabisa dhambi zako kwa kukusudia kuziacha,..unakusudia kuacha ulevi, anasa, wizi, uasherati uongo, uvaaji usio na maadili, na kila aina ya uchafu, Kisha hatua inayofuata ni kwenda kubatizwa, hakikisha unabatizwa katika ubatizo ulio sahihi wa kimaandiko, yaani ni ule wa kuzamishwa katika maji mengi, na kwa jina la YESU KRISTO, (zingatie hilo uwe ni kwa jina la YESU) sawasawa na maandiko (Matendo 2:38, 8:16, 10:48, 19:5), ili upate ondoleo la dhambi zako. Na baada ya hapo Mungu mwenyewe atakupa kipawa cha Roho Mtakatifu, atakayekusaidia kushinda dhambi na kukuongoza katika kuijua kweli yote ya maandiko Yohana 16:13.
Na kuanzia hapo utakuwa na nafasi ya kuwa mshirika wa mambo yote ya kimbinguni Mungu aliokusudia kuwafunulia watoto wake.
1Wakorintho 2:9 “lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.”
Ni maombi yangu utafanya hivyo sasa.
Tafadhali “SHIRIKI” ujumbe huu na wengine.Bwana akubariki sana. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada zinazoendana..
DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
Shalom, Mtu wa Mungu karibu tujifunze Neno la Mungu, ambapo leo kwa Neema za Bwana tutajifunza kwa sehemu juu ya ufunuo uliopo katika ufalme wa Mbinguni. Biblia inasema katika..
Mathayo 13.45 “Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta LULU NZURI;
46 naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua”.
Mfano huu ulitolewa na Bwana Yesu Kristo, alipokuwa anawafundisha makutano maana ya ufalme wa Mbinguni..Kama ukichunguza kwa makini utagundua kuwa Bwana Yesu alikuwa anapenda kutumia mifano ya kidunia hii kuifananisha na ufalme wa mbinguni Ikiwa na maana kuwa mambo mengi au shughuli nyingi za ulimwengu huu zimebeba kwa sehemu Fulani siri za ufalme wa Mbinguni ndani yake..Katika shughuli za haki au za uovu ndani yake kuna hekima za Kimungu..ndio maana utaona mahali pengine Bwana anatoa mfano wa Mpanzi aliyekwenda kupanda mbegu zake shambani…na mahali pengine Bwana Yesu anatoa mfano wa mwizi (kwamba atakuja kama mwivi usiku wa manane)…ikiwa na maana kuwa hata katika WIZI kuna hekima ya kiMungu ndani yake…ingawa kwa kusema hivyo sio kwamba anahalalisha wizi, sehemu nyingine anatoa mfano wa yule kadhi dhalimu..ikiwa na maana kuwa hata katika udhalimu pia ipo hekima ya Mungu ndani yake..nk
Lakini leo tutajifunza juu ya huu mfano wa Mfanyabiashara aliyekuwa akitafuta lulu ya thamani na alipoiona alikwenda kuuza kila alicho nacho ili kuinunua.
Sasa LULU ni nini?.
Lulu ni madini fulani ya thamani sana..ambayo hayachimbwi kutoka ardhini kama madini mengine yachimbwavyo bali asili yake ni baharini…Madini haya yanatengenezwa ndani ya mwili wa samaki, wanaojulikana kama “Oyster”…na samaki hawa sio kama samaki wa kawaida tunaowajua wenye mapezi na mikia na macho, hapana bali jamii ya hawa samaki hawana mapezi wala macho, wala mikia na wala hawaogelei ogelei kama viumbe wengine wa majini, bali wapo kama kokwa la embe hivi lililokauka na wanakaa katika sakafu ya bahari chini kabisa, hawaruki ruki huko na huko, wakati wote wanakuwa wametulia tu chini ya habari, …Hivyo ni ngumu kuwaona kwani unaweza ukapita ukadhani ni mawe tu yamelala kumbe ni samaki.
Sasa hayo madini yanayoitwa LULU yanaanza kujitengeneza kama chembe ndogo ya mchanga, tumboni mwa hao samaki, na kwa kadiri muda unavyozidi kuendelea..yanaongezeka ukubwa kidogo kidogo na hata kufikia ukubwa wa kama hizi gololi wanazochezea watoto wadogo..kwa jinsi inavyokuwa kubwa ndivyo thamani yake inavyozidi kuongezeka. Watu wanaokwenda kuyatafuta madini hayo baharini wanatumia gharama nyingi na muda mwingi na hatari nyingi..kwasababu inawagharimu waende mbali kwenye vilindi vya maji na wazame chini mpaka kwenye sakafu ya bahari na kuanza kuangalia angali huku na huko kama mtoto anayetafuta hela aliyoiangusha njiani..inawaachua hata siku nzima kukaa chini maji, hana hiyo inaweza kwenda kwa miezi kadhaa, Na kwa tabu nyingi wakibahatika kuwapata hao samaki wanawachukua na kwenda kuwapasua na kutoa hayo madini..
Sasa kutokana na madini hayo kuwa adimu na kuwa mazuri kupita kiasi, thamani yake nayo inakuwa kubwa zaidi…lulu moja ya ukubwa wa juu, thamani yake inaweza ikafika mpaka sh.milioni 250 za kitanzania. Hiyo ni moja tu!
Sasa tukirudi kwenye huo mfano Bwana Yesu alioutoa unaosema…ufalme wa Mungu umefanana na mfanya biashara aliyeona LULU ya thamani akaenda kuuza kila kitu alicho nacho ili kuinunua, alikuwa na maana kuwa, huyu mfanya biashara, alikwenda mahali akakuta LULU inauzwa kwa thamani ya chini…tuchukue mfano hiyo lulu yenye thamani ya sh.milioni 250 akaikuta inauzwa sh.milioni 100. Na alipoiona kwasababu yeye anaijua thamani yake halisi, na hana hela ya kutosha akatumia akili ya kwenda kuuza vyote alivyo navyo kama ni mashamba, kama ni nyumba kama ni mifugo yake, vyovyote vile…ili kwamba apate hela ya kutosha, akainunue hiyo lulu inayouzwa kwa bei ya chini..
Sasa kumbuka Bwana Yesu anamwita huyu mtu mfanyabiasha, na unajua mtu akiwa mfanyabiashara yupo kimaslahi zaidi, uyo kwaajili ya kupata faida.
Hivyo yeye kuuza kila kitu ili akainunue ni alijua siku atakapokwenda kuiuza kwa thamani yake halisi atapata faida kubwa na hivyo atakwenda tena kununua mashamba mazuri kuliko hata yale aliyouza, atakwenda kununua tena mifugo mingine mingi, atakwenda kujenga tena nyuma yenye thamani kama ile ya kwanza na bado atabakiwa na faida yake juu..
Kwahiyo huyu mfanyabiashara hakuwa mjinga, kwamba auze kila kitu halafu akae na lulu ndani kama urembo…hapana kumbuka yeye ni mfanya-biashara, aliinunua ili akaiuze.
Ndugu yangu Bwana Yesu Kristo ndio hiyo LULU YA THAMANI, Anapatikana BURE lakini HAPATIKANI KIRAHISI. Kama tu Lulu Baharini inavyopatikana bure lakini si kirahisi, kadhalika na Bwana Yesu, ndio maana alisema katika Luka 14.33 “Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, HAWEZI KUWA MWANAFUNZI WANGU”.
Unapousikia ujumbe huu, mimi ninayekuhubiria ni kama mfanya biashara ninayekuletea YESU KRISTO kwa bei ya chini..na wewe unayesikia ni kama mfanya-biashara mwenye kutafuta lulu hii ya thamani, hivyo unachopaswa kufanya ni kwenda kuuza kila ulicho nacho..ili upate pesa ya kutosha kumnunua huyu Yesu Kristo moyoni mwako, na kisha nenda kamwuze nawe kwa wengine ndipo utaona faida. Na gharama za kumnunua ndio hizo…”kuuza kila kitu cha ulimwengu huu unachokishikilia sasa kinachokufanya uwe mbali na Mungu wako” kuacha kila kitu kiovu, kukubali kuacha kila aina ya dhambi maishani mwako, kukubali kuingia gharama ya kuacha anasa, na mambo ya kiulimwengu, kukubali kuacha uasherati na uzinzi, kukubali kuacha utumiaji mbaya wa mitandao, kuchat mambo yasiyofaa mitandaoni, kukubali kuacha ulevi, na utazamaji wa pornography, kukubali kuacha kuvaa nguo fupi na zinazobana na suruali na vimini, kukubali kuacha kampani mbaya za watu wenye mizaha, na matusi, kukusudia kuuza muda wako wote kwa Mungu, kukusudia kumgeukia Mungu kwa moyo wako wote, na kwa akili zako zote, na kubeba msalaba wako na kuelekea Kalvari. Ndugu yangu wa thamani mtu asikudanganye kuwa utampa Bwana Yesu nje ya njia hiyo…yeye mwenyewe alisema katika..
Luka 14.25 “Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia,
26 Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
27 Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”
Maneno haya ni magumu, lakini ndio ukweli wa mambo…ukitaka kwenda kununua lulu ya thamani Yule anayekuuzia atakwambia usipofikia kiwango Fulani cha fedha, huwezi kuipata..sio kwamba anataka kukuumiza hapana bali huo ndio ukweli wa mambo kwamba kitu unachokitafuta ni cha thamani ya juu, hivyo anaweza kukushauri uende ukauze hata shamba au nyumba ili upate fedha ya kutosha ya kuinunua..lakini kama usipotaka basi ni sawa uamuzi ni wakwako.
Hivyo ndugu unayesoma ujumbe huu ambaye hujampa Bwana Yesu maisha yako, au upo mguu mmoja nje, mguu mmoja ndani na unataka kuwa na maisha mazuri ya hapa duniani na huko mbinguni, unataka kupata faida hapa duniani na mbinguni, basi fahamu kuwa NJIA YA MSALABA haikwepeki. Ni lazima ujikane nafsi tu! Ni lazima uache KILA KITU CHA ULIMWENGU HUU, Ni lazima umgeuke yeye kikweli kweli, hakuna njia ya mkato..wengi wanapenda kufarijiwa kwamba kwa Bwana Yesu ni mteremko tu! Usidanganyike..Kristo ni LULU YA THAMANI. Kama alitoka mbinguni mahali penye utukufu atakuwaje wa bei rahisi huyo??..hebu chukua muda mtafakari huyu MFALME WA WAFALME!!.
Kwahiyo Bwana Yesu anatupenda na ataka tupate faida ndio maana, alitupa mfano huo wa mfanyabiashara, anataka na sisi tuwe wafanya biashara werevu tunaotafuta faida na si hasara, anataka tuingie gharama kupoteza vitu vidogo vya muda vya kitambo visivyo na maana ili tupate vitu vikubwa vya muda mrefu vyenye faida..huoni kama hiyo ni fursa nzuri kwetu??..Ndio ni fursa nzuri sana na ya faraja…ndio maana wanafunzi walipopata mashaka ya kupoteza mambo yao yote kwa ajili ya Kristo, yeye mwenyewe aliwapa faraja akawaambia watapata mara 100 hapa duniani na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.. Tunayasoma hayo katika…
Marko 10:28 “Petro akaanza kumwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe.
29 Yesu akasema, Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili,
30 ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; NA KATIKA ULIMWENGU UJAO UZIMA WA MILELE”.
Hivyo Kama hujampa Bwana Yesu maisha yako, ni wakati wako sasa wa kufanya hivyo, unachopaswa kufanya ni kutubu kwa kumaanisha na kudhamiria kuziacha dhambi zako zote, na kumaanisha kutokuzifanya tena, (UNAZIACHA KABISA) Kama ulikuwa mlevi, unaacha ulevi, kama ulikuwa unatanga tanga kwa uasherati, unauacha uasherati, kama ulikuwa unavaa vibaya unaacha, na kisha baada ya kufanya hivyo nenda katafute ubatizo sahihi popote pale kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako, kulingana na matendo 2:38 na ubatizo sahihi ni wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO, baada ya kufanya hivyo Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu atakayekusaidia kushinda dhambi na kukuongoza katika kuijua kweli yote ya Biblia.Na hapo utakuwa umezaliwa mara ya pili.
Bwana akubariki sana.
Tafadhali “share” ujumbe huu na wengine na Bwana akubariki. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
UFALME WA MUNGU HAUPATIKANI KIRAHISI
SHETANI ANATOLEA WAPI FEDHA, ANGALI TUNAJUA FEDHA NA DHAHABU NI MALI YA BWANA?
Wakati nikiwa shule ya msingi, kuna mwalimu mmoja aliyetufundisha somo lijulikanalo kama “stadi za kazi”, mwalimu huyu wanafunzi wote tulimpenda sana kwasababu alikuwa tofauti kidogo na walimu wengine, kwani yeye kila alipokuwa akija darasani, alituambia watoto tumchangie hela ya karanga atutoe nje michezoni (lakini kiukweli hakuitumia kwa karanga bali alikwenda kununulia pombe).Na kama unavyojua watoto wanavyopenda michezo, hawapendi kukaa muda wote darasani kufundishwa, hivyo suala la kujitolea kila mtu sh.5 au sh.10 halikuwa ni jambo kubwa sana kulinganisha na raha tuliyokwenda kuipata kwenye michezo!.
Hiyo ndio ilikuwa desturi yake, na walimu wengine walipokuwa wanaona watoto wanacheza nje muda wa masomo, walipoulizwa mnafanya nini nje muda huu, wote wanajibu ni sehemu ya somo mwalimu ametutoa nje!, na ni kweli katika somo la stadi za kazi michezo inayo nafasi yake. Lakini baadaye likaja kuleta madhara mengine.
Hiyo ikapelekea watoto kupoteza hamu ya kufundishwa darasani somo lile, na hivyo kutokuwa na maarifa ya mambo mengine muhimu yahusuyo stadi za kazi, mfano ujenzi, ususi, uchongaji, ufugaji, ukulima, ushonaji n.k. wakabakia kufikiri stadi za kazi ni michezo tu ya kuruka ruka nje. Na mwisho wa siku mtihani wa mwisho ukifika watoto wanafeli. Kwasababu wanakuwa wamekosa maarifa ya kutosha juu ya somo lile…Unaona hapo tatizo mama lipo kwa yule mwalimu ambaye angepaswa atimize wajibu wake wa kuwafungulia wanafunzi wake mlango wa maarifa kwa kuwafundisha mambo yote katika uwiano, badala yake yeye ndiye anayekuwa wa kwanza kuufunga mlango huo kwa faida zake mwenyewe.
Jambo la namna hiyo lipo hata katika kanisa la Mungu, biblia inasema katika.
Luka 11:52 “Ole wenu, enyi wana-sheria, kwa kuwa MMEUONDOA UFUNGUO WA MAARIFA; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia”.
Unaona, Mungu alishaweka ufunguo mlangoni, kilichokuwa kimebaki ni kufunguliwa tu na kuingia katika maarifa ya kumjua Mungu kwa mapana na marefu yake na sio kuhangaika hangaika tena, lakini hapa tunaona wana-sheria (yaani watu waliobobea katika kuisoma sheria/torati), au kwasasa tunaweza kusema waalimu wa biblia, wachungaji, maaskofu,manabii n.k. wao ambao ndio wangepaswa wawe wa kwanza kuuzungusha ule ufunguo ili waingie katika maarifa ya kumjua Mungu pamoja na watu wao, badala yake wao ndio wanaokuwa wakwanza kuundoa ule ufunguo na wanafanya hivyo kwa makusudi kabisa,…na mtu akishautoka ufunguo ni nani awezaye kuingia tena?.
Viongozi hawa wanajua kabisa watu wengi hawapendi, kufundishwa maneno ya Mungu katika mapana yake na marefu yake, kwasababu ni wachanga hawajui umuhimu wake kwasasa, na wao bila hata ya kuwahurumia, wanawalazimisha hivyo hivyo wajifunze na hayo mengine hata kama hawataki kwa usalama wa maisha yao,..Wao wanawafundisha yale ambayo watu wanataka tu kusikia, watu wanapenda tu, na kibaya zaidi pale wanapoona matoleo yanaongezeka kwa injili kama hizo, ndipo wanapoamua kutia nanga na kufundisha hizo hizo tu siku zote, na kuacha mambo ya msingi.
Viongozi hawa wanafahamu kuwa injili za mafanikio zinapendwa na watu wengi, lakini kwa makusudi kabisa huku wakijua kabisa hakuna mlevi yoyote atakayeurithi ufalme wa mbinguni, wala mtu yoyote ambaye sio mtakatifu atakayemwona Mungu, (Waebrania 12:14), wala wazinzi, wala muabudu sanamu, lakini wao hawana muda wa kugusia mambo hayo…
Viongozi hawa wanafahamu kabisa kuwa wale watu ni wachanga, na kama ni wachanga ni lazima watapenda vitu vilaini laini tu, na yeye kama mwalimu badala azingatie kuwa mchezo peke yake haitoshi kumpa mtu maarifa yote ya kufaulia mtihani bali achanganye na maarifa mengine yote..Yeye hilo halizingatii na matokeo yake mwisho wa siku watoto wote wanafeli, na ndio huko watu wanaishia shimo la kuzimu.
Ndugu jiulize injili unazozisikia mara kwa mara, JE! ZINAKUJENGA PANDE ZOTE AU UPANDE MMOJA TU WA MAFANIKIO YA KIMWILI?…Unafahamu kuwa haya maisha yatakuwa na mwisho?..ulishawahi kulitafakari hilo?, kama unyakuo hautakukuta basi ujue siku yoyote unaweza ukaondoka hapa duniani, na huko uendako je! utakuwa mgeni wa nani? Huko uendako umejiwekea hazina gani?..BWANA YESU ANASEMA ITAKUFAIDIA NINI UUPATE ULIMWENGU MZIMA, NA HUKU UMEPATA HASARA YA NAFSI YAKO?, upate nyumba nzuri, upate gari, upate umaarufu, upate ukubwa na kila kitu na huku unapata hasara ya nafsi yako kwa kumkosa Kristo moyoni mwako??
Siku ile utakapokufa utasema laiti ningejiwekea huku hazina, nisingekuwa mahali hapa pa taabu, Leo hii unafurahia injili ya kuburudishwa na vichekezo na comedy kwenye madhabahu, na huku unajua kabisa umefarakana na Mungu moyoni mwako, na hata ukifa leo unakwenda kuzimu, hujui kuwa kizazi unachoishi ndio kizazi kilicho katika hatari kubwa sana kuliko vyote vilivyotangulia, ni kizazi kilicho katika hatari ya kuuona uharibifu utakaoijilia dunia nzima, hujui kuwa kulingana na kalenda ya kimbinguni tunaishi katika lile kanisa la Mwisho lijulikanalo kama Laodikia ambalo ndilo litakaloshuhudia kurudi kwa pili kwa Kristo?. Hufahamu kuwa hatua za Unyakuo zimeshakwisha anza, na wewe huna habari, haujui kuwa kazi za mpinga-kristo sasa zipo dhahiri na kiti chake kinajulikana sasa mahali kilipo, wewe upo buzy kukimbilia injili za vichekesho, na kufarijiwa, na huku unadhani upo sawa…Kaa mbali na hao viongozi! Na hizo injili ambazo zimekosa uwiano.
Tunaonywa tuwe makini, huu ni wakati wa kutafuta kwa bidii mahusiano yetu binafsi na Mungu, kupata maarifa ya kina juu ya mapenzi yake kwetu sisi wanadamu, na maarifa haya yanakuja kwa kulitafakari na kuliishi Neno la Mungu.
2Petro 1:4 “Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa WASHIRIKA WA TABIA YA UUNGU, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
5 Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu MAARIFA”,
Hivyo ni maombi yangu, tutaanza mwanzo mpya sasa, ikiwa tulishampa Bwana maisha yetu, embu tuongezee na maarifa ya kumjua Mungu na uweza wake..Tutafakari zaidi mambo ya mbinguni kwasababu mtihani mkubwa sana upo mbele yetu, na tusipokuwa na maarifa ya kutosha ya kuyajua mapenzi ya Mungu, basi tujue kufeli kupo mbele yetu, na kufeli kwenyewe ni kuishia kuzimu..Lakini tukiwa na maarifa ya kutosha kuhusu Mungu wetu, hiyo itatusaidia kuishi maisha ya uangalifu sasa katika huu ulimwengu kama wapitaji hapa duniani na mwisho wake tutafaulu na kuishia Mbinguni milele.
Kama hujampa Bwana maisha yako kihakika, au unasita sita katika mambo mawili, au umezamishwa katika hizi injili za mafanikio zisizokuwa na uwiano za kuchuja mbu na kumeza ngamia, hebu tenga muda jaribu kuweka mambo yote kwenye mizani, jaribu kulitilia mkazo lile lenye uzito mkubwa zaidi na hayo mengine yafuate baadaye.
Mathayo 23:23 “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.
24 Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia”.
Hivyo tuwe tayari kuzisikia habari zote, za ufalme wa mbinguni, kwa uwiano wote, na Mungu atatusaidia, La kwanza liwe ufalme wa mbinguni, na hayo mengine yafuate.
Wakolosai 1.9 “Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ILI MJAZWE MAARIFA YA MAPENZI YAKE KATIKA HEKIMA YOTE NA UFAHAMU WA ROHONI;
10 mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu;”
Mungu akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, libarikiwe.
Karibu tujifunze Neno la Mungu, na leo tutajikumbusha kazi mojawapo ya Yesu Kristo iliyomleta Duniani…Tukiachilia mbali kazi ya UKOMBOZI na KUTUONYESHA NJIA YA KUMWELEKEA BABA..kazi nyingine iliyomleta Bwana duniani ni UPONYAJI. Na uponyaji upo wa rohoni na mwilini. Leo kwa ufupi tutajifunza juu ya uponyaji wa mwili.
Yesu Kristo sio daktari, ingawa tukimwita ni daktari mkuu tutakuwa hatujakosea sana..lakini yeye ni zaidi ya hapo…yeye ni mwumbaji..daktari atamtibu mtu, lakini litabaki kovu (hana uwezo wa kukirudisha kitu kama kilivyokuwa katika uhalisia wake)..Lakini Mungu ni zaidi ya hapo hatibu bali anaponya..
Katika huduma yake, Tangazo lake la kwanza alilowatangazia wayahudi ni hili.
Luka 4: 18 “ROHO WA BWANA YU JUU YANGU, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.
20 Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.
21 AKAANZA KUWAAMBIA, LEO MAANDIKO HAYA YAMETIMIA MASIKIONI MWENU”.
Huyo ni Bwana Yesu aliyezungumza maneno hayo baada ya miaka mingi wana wa Israeli kusubiria tumaini kutoka kwa Mungu, na sasa tumaini hilo limewafikia, Na tunaona ni Bwana pekee ndiye aliyeanza kufanya miujiza isiyo ya kawaida ambayo haikuwahi kutokea katika historia ya mwanadamu kwa vizazi vyote. Vipofu walikuwa wanaona, viwete wanatembea..na wenye magonjwa ya kila namna yalikuwa yanaponywa.
Ndugu nataka nikuambie Kristo Yesu mpaka leo anaishi, na kazi alizozifanya wakati akiwa hapa duniani bado anazifanya hata leo, kwa kupitia watu wake. Na yeye sio mwongo kama sisi wanadamu. Maneno yake ni ya ukweli wote. Tumeshuhudia mara nyingi kwa macho yetu watu wakiponya papo kwa hapo. Na mimi mwenyewe alishawahi kuniponya papo kwa hapo na sio mara moja.
Nimewahi kusikia shuhuda kadha za watu kuponywa magonjwa ambayo yamewatesa muda mrefu na wamekosa suluhisho kila walikokwenda, nimewahi kuwaombea watu kadhaa na Bwana akawaponya magonjwa ambayo yamewatesa kwa miaka mingi, na nimewahi kusikia shuhuda kadha za watu ambao Mungu kawaponya watu pasipo hata kuombewa. Hayo yote ni kuthibitisha kuwa Yesu Kristo si mwongo.
Sasa ni muhimu kufahamu ni jinsi gani uponyaji wa kimungu unashuka juu ya mtu. Wengi wetu tunadhani Mungu anatuponya au anatupa afya kwa utakatifu wetu tulionao….hiyo kwa sehemu Fulani ina ukweli kwa baadhi ya watu…kwasababu kama mtu anaisikia injili kwa miaka na miaka na hataki kubadilika, na anakuwa ni mtu wa kusitasita, leo anakwenda mbele, kesho anarudi nyuma, leo anakwenda kanisani kesho ni mwasherati, mtu wa namna hiyo ulinzi wa kimungu umeondoka juu yake, hivyo inakuwa ni rahisi kwake kuvamiwa na roho za uharibifu, ndio unakuta zitakazomsababishia magonjwa ya ajabu na hata wakati mwingine mauti.
Lakini kama mtu ni mwaminifu kwa Mungu au hakuwahi kuisikia kabisa INJILI au yupo katika hatua za awali za kumpa Yesu maisha yake halafu baadhi ya mambo yamemtokea, kama vile magonjwa pengine yasiyojulikana hata chanzo chake ni nini, na akaenda kutafuta uponyaji kutoka kwa Mungu kwa moyo wa kumgeukia yeye..Nataka nikuambie Ipo dawa!!, YESU NDIYE DAWA!!. Biblia inasema Yesu ni yeye Yule jana, leo na hata milele ikimaanisha kuwa anao uwezo wa kukirudisha kitu kiwe kama kilivyokuwa jana, na anao uwezo wa kukileta kitu leo kiwe kama kitakavyokuwa miaka 100 mbele au milele ijayo..Kwahiyo yeye hana muda wala hajachelewa…wanadamu sisi ndio tunao usemi unaosema “basi tena haiwezekani” lakini Yesu sio hivyo yeye hana muda, anaponya sasahivi na anarudisha kitu kama kilivyokuwa jana.. aliirudisha ngozi ya Naamani iliyokuwa na ukoma ikawa kama ngozi ya mtoto mchanga….
2 Wafalme 5: 13 “Watumishi wake wakamkaribia, wakamwambia, wakasema, Baba yangu, kama yule nabii angalikuambia kutenda jambo kubwa, usingalilitenda? Je! Si zaidi basi, akikuambia, Jioshe, uwe safi?
14 Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; NAYO NYAMA YA MWILI WAKE IKARUDI IKAWA KAMA NYAMA YA MWILI WA MTOTO MCHANGA, AKAWA SAFI.
15 Akamrudia yule mtu wa Mungu, yeye na mafuatano yake yote. Akaja, akasimama mbele yake;”
Sasa kama wewe ni mgonjwa na huo ugonjwa umekutesa sana kwa muda mrefu, labda ni UKIMWI, au CANCER, au KISUKARI au ugonjwa wowote ule na unakuogopesha na hujui huo ugonjwa sababu yake ni nini, unachotakiwa kufanya sasahivi, ni kutulia, usiogope wala usikuogopeshe wala usipanic, tenga dakika chache mahali ulipo, tubu dhambi zako na maovu yako, na umwahidi Bwana endapo akikuponya huo ugonjwa utamfanyia nini…
Baada ya kutubu na kumwahidi…nataka utafakari mfano huu kisha uutumie huo kupokea uponyaji wako sasahivi. Hebu tafakari siku ulipojikata na kisu na baada ya muda Fulani kile kidonda kikapona..je! ulitumia utakatifu gani hapo kufanya ngozi yako ijirudie kama ilivyokuwa kwanza?…au siku upele ulipokuota kwenye ngozi yako na kesho asubuhi ukaukuta umepotea ulitumia utakatifu gani kuufanya upotee…hebu tafakari siku ulipojisikia kichwa kinauma na baada ya muda kikaisha chenyewe labda baada ya kulala na kuamka asubuhi, ulitumia utakatifu gani kukiponya? Kama hukutumia utakatifu wowote kijiponya kadhalika na ugonjwa ulio nao sasahivi hauhitaji utakatifu wowote…Siku ile ni Mungu alikiponya kichwa chako bure kwa Neema yake pasipo hata wewe kujijua, ukadhani ni mwili wako umejiponya mwenyewe, kumbe hujui ni Mungu ndiye aliyekuponya. na kila siku anauponya mwili wako pasipo hata wewe kujijua wala kumwomba, anakuponya kwa neema zake tu! Bureee…ngozi ya mguu wako kila siku inachubuka lakini kila siku Bwana anakutengenezea ngozi mpya ndio maana kiatu chako kinachakaa na unakibadilisha viatu kila siku lakini mguu wako hauchakai na wala haubadilishi, ndio maana nguo zako zinachakaa lakini mwili wako uko vile vile siku zote. Huo ni uponyaji wa kiMungu unaoendelea mwilini mwako pasipo matendo ya sheria.
Hivyo kwa kanuni hiyo hiyo ya kuponywa pasipo matendo, basi itumie hiyo hiyo kwa ugonjwa ulionao hapo ulipo, kama una HIV, au KISUKARI, au KANSA, au UTASA au Vidonda vya tumbo, au tatizo la figo, au ini, au moyo, au ni kiziwi, au kipofu, au ni kiwete, au tatizo lolote lile katika mwili wako. Kinachohitajika kwako ni IMANI tu!!..Usianze kujishaurishauri wala kuwa na mashaka mashaka, yakatae hayo mashaka, hata kama wakati mwingine bado unaona kuna udhaifu mwilini, hapo ulipo simama juu sema nimeshapona kwa jina la YESU. Kifo kimeshaingia kwenye huo ugonjwa..haupo tena huo ugonjwa, hata kama bado unahisi maumivu yasikuogopeshe tayari kifo kimeshaingia kwenye huo ugonjwa..unaukumbuka ule mtini Bwana Yesu alioulaani?…haukunyauka palepale lakini tayari ulikuwa umeshakufa ndani kwa ndani, hauna uzima tena, mizizi ilikuwa imeshaoza, baada ya masaa kadhaa wanafunzi wanafunzi walipouona umenyauka ndipo wakaelewa kuwa kumbe mti ulikuwa umeshakufa tangu jana Bwana alipoulaani, na sio leo, na ndivyo itakavyokuwa leo kwako na huo ugonjwa ulio ndani yako, usiangalie hali uliyo nayo hapo, amini kwamba tayari kiini cha ugonjwa hakipo…
Sasa kwa ajili ya kuwathibitishia wengine uponyaji wako..Nenda sehemu ambayo unafanyaga check/up ukifika waambie nimekuja kuchukua cheti ya uzima wangu, waambie wakupime na wakupe majibu ili ukatangaze matendo makuu ya Mungu, na watakupa majibu ambayo wao wenyewe watashangaa, yachukue hayo nenda mtaani kwako waonyeshe watu wengine kuwa YESU KRISTO SIO MZIMU YUPO HAI na anatenda kazi zake hadharani.
Nakuombea kwa Mungu, imani yako isitetereke, mwamini Bwana Yesu, fanya kama nilivyokwambia na wewe mwenyewe utashuhudia kwa macho yako matendo makuu ya Mungu. Alifanya kwa wengine, alifanya kwangu, atafanya na kwako, na atafanya kwa wengine kwa kupita ushuhuda wako wewe.
Bwana akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!
JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOKUJA JUU YA MTU.
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, Mkuu wa Uzima libarikiwe. Karibu tujifunze Neno la Mungu, ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo ya ndoa ambapo leo tutajifunza juu ya ndoa takatifu jinsi inavyofungwa ..kwa kufuata misingi ya kimaandiko.
Kwanza ni muhimu kufahamu kuwa kuna ndoa za aina mbili, kuna ndoa zetu sisi wanadamu, zinazohusu mwanaume na mwanamke, na Pia kuna ndoa ya kimbinguni inayomuhusu Yesu Kristo na Kanisa lake. Na ndoa ni kitu cha kimaandiko kabisa na ni mpango wa Mungu kamili. Na shetani siku zote hapendi ndoa takatifu inayofungishwa na Mungu mwenyewe, kwasababu anajua itamzuilia mambo yake mengi maovu ambayo angeweza kuyafanya kwa mtu husika au jamii kama ndoa isingekuwepo. Na ndio maana biblia inasema katika siku za mwisho “yatatokea mafundisho ya uongo ya kuwazuia watu wasioe” Tutaelewa jambo hili kwa undani zaidi kwa jinsi tunavyoendelea kujifunza.
Tukianza kwa kuzizungumzia kwa ufupi ndoa zetu za kibinadamu; Kwanza ni lazima ziwe na utaratibu, kwasababu Mungu ni wa utaratibu, ndoa ya kwanza ilifungishwa Edeni na Mungu mwenyewe, lakini unaona Mungu alikuwa na utaratibu katika kuifungisha ile ndoa..Tunaona alimwumba kwanza Adamu ambaye ni mwanaume kabla ya Hawa kufunua kuwa mwanamume ndiye kiongozi wa ile ndoa, na kabla hajamwumba Hawa, alimpa Adamu Majukumu ya kuilima na kuitunza Bustani, ili mkewe ajapo akute kila kitu kipo tayari, awe kama ni msaidizi tu, na sio aanze kuteseka nayeye kufanya hivi na vile. Kwahiyo unaona huo ni utaratibu mzuri, kwamba mwanamume akitaka kwenda kuoa ni sharti aandae mazingira ya atakapomweka mke wake na tayari awe ameshajiweka tayari kiakili kwa majukumu yaliyopo mbele yake.
Hivyo baada ya ndoa ya kwanza kufungishwa na Mungu mwenyewe utaratibu ulibadilika haikuwezekana tena ndoa nyingine zinazofuata wanawake watoke kwenye ubavu wa mwanamume, au Mungu atoe maagizo moja kwa moja tena kutoka mbinguni kama hapo kama kwanza, hapana bali ni lazima watu wazaliwe..kwahiyo mwanadamu akapewa jukumu na uwezo wa kutengeneza mwanadamu mwingine kutoka katika tumbo lake na viuno vyake. Hii ikiwa na maana pia azisimamie kwa utaratibu ndoa zote zitakazofuata mbele yake, kwamba zizaliwe kupitia kwenye mikono ya ya watu wa Mungu, kwamba lazima ndoa ihalalishwe mbele za Mungu kwa kupitia watu.
Hivyo huo utaratibu ukaendelea hivyo vizazi na vizazi, mwanamume anapotaka kumwoa mwanamke ni lazima ataratibu ufuatwe, kwanza wazazi washirikishwe, na sheria za Mungu zihusike ndipo hiyo ndo iwe halali. Sio sawa na sio jambo la kimaandiko kabisa watu wawili kuchukuana pasipo utaratibu wowote na kuishi pamoja na kusema wameonganishwa na Mungu, hapo hawajaunganishwa na Mungu bali shetani. Kwasababu Mungu ni Mungu wa utaratibu. Adamu hakumwona Mzazi kwasababu alikuwa hana wazazi, na kadhalika Hawa…Lakini baadaye unaona Mungu anasema “mwanamume atamwacha babaye na mamaye na kuungana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja”. Kumwacha pale mzazi sio kumwacha kwa shari bali kwa heri..
Kuna usemi unaosema kuwa Agano la kale hakukuwa na utaratibu wa kuoa..na hivyo watu walikuwa wanajitwalia wake tu! manabii walikuwa wanajitwalia wake, usidanganyike ndugu, utaratibu ulikuwepo. Na leo tutaenda kujifunza huo utaratibu.
Katika desturi za kiyahudi (yaani waisraeli) utaratibu wa ndoa ulikuwa kama ifuatavyo. Kulikuwa na hatua mbili kuu za ndoa, ilikuwa baada ya mwanamume kumpenda mwanamke na kutaka kumwoa, anakwenda kutoa taarifa kwa wazazi wake, na kisha wazazi wake wanakwenda nyumbani kwa mwanamke na kuzungumza na wazazi wa mwanamke, na endapo wazazi wakiridhia hatua nyingine zinafuata.
Hatua ya kwanza ni KUPOSA: Hatua hii inahusisha mwanaume Pamoja na washenga, kutoka kwao na kwenda nyumbani kwa mwanamke, ambapo watatoa mahari, kufanya karamu ndogo, na kikubwa zaidi WATABADILISHANA VIAPO na kuwekeana mkataba kwamba watakuwa waaminifu wote wawili mpaka siku Harusi itakapofungwa. Hivyo baada ya kukamilisha hiyo hatua, mwamume na mwanamke wanakuwa wamefungwa na hicho kiapo, mpaka siku ya Harusi yenyewe itakapofika.
Hapo mwanamume anakuwa huru kurudi kwao, na kuendelea kutengeneza maisha yake, ataendelea kuandaa nyumba ya kumweka mkewe, kama alikuwa hana, na mambo mengine ya muhimu ya kifamilia, na hapaswi kuwa na mahusiano na mwanamke mwingine yeyote, na mwanamke naye ni hivyo hivyo, hapaswi kujihusisha na mahusiano yoyote na mwanamume mwingine, na katika kipindi hichi pia wapendwa hawa wawili hawapaswi kukutana kimwili kabisa (yaani kufanya tendo la ndoa)..Mpaka siku ya harusi itakapofika, ingawa wana ruhusa ya kuitwa mume na mke, Na kipindi hichi cha matengano kinaweza kikadumu kwa miezi kadhaa au hata zaidi ya mwaka, inategemea na hali ya kimaisha ya mwanamume.
Kipindi hichi ndicho kipindi ambacho Mariamu alionekana ana mimba, ya Bwana Yesu Kristo, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, baada ya kuposwa na Yusufu.
Na hatua ya PILI inayofuata baada ya KUPOSWA Ni Harusi yenyewe. Katika siku hiyo ya arusi, Mwanamume atatoka kwao pamoja na kundi la wanaume wenzake, na ndugu zake wakiume atakwenda kwa matarumbeta na shangwe nyumbani kwa mwanamke, na kisha atamchukua mwanamke na kwenda naye nyumbani kwa mwanamume (kwa Baba wa mwanamume) na kule watakwenda tena kurudia vile VIAPO walivyotoa wakati wa kuposa. Na watakuwepo Marabi ambao watasoma maandiko machache ndani ya TORATI, yanayohusiana na ndoa Na baada ya kufanya hivyo hiyo ndoa inakuwa ni halali na Takatafu na inabarikiwa. Na mfano wa mazungumzo hayo ni huu:
Mwanzo 24: 57 “Wakasema, Na tumwite huyo msichana, tumwulize mwenyewe.
58 Wakamwita Rebeka wakamwuliza, Je! Utakwenda na mtu huyu? Akasema, Nitakwenda.
59 Ndipo wakampeleka Rebeka ndugu yao, na yaya wake, na mtumishi wa Ibrahimu, na watu wake.
60 Wakambarikia Rebeka, wakamwambia, Ndugu yetu, uwe wewe mama wa kumi elfu, mara elfu nyingi, na wazao wako waurithi mlango wa hao wawachukiao.
61 Rebeka akaondoka na vijakazi wake, nao wakapanda juu ya ngamia, wakamfuata yule mtu. Naye huyo mtumishi akamchukua Rebeka akaenda zake”.
Baada ya ndoa hiyo kufungwa, bibiarusi anajitenga na mumewe kwa siri kwa siku saba, ambapo kuanzia hapo wanaruhusiwa kukutana kimwili na kuendelea na mambo mengine.
Huo ndio ulikuwa utaratibu wa ndoa kwa Wayahudi wa agano la Kale, na hakuna mahali popote watu walijitwalia wake kienyeji na kuishi nao, labda tu watu hao wawe si wayahudi.
Sasa Ndoa ya rohoni nayo pia ina utaratibu huo huo.
Bwana Yesu aliacha enzi na Mamlaka mbinguni kwa Baba yake, akalipenda kanisa lake (ambaye ndio mke wake), ubavu wake, akaja duniani ambapo ndio makao ya mke wake yalipo, Na akaliposa kanisa kwa kulitolea mahari, na mahari hiyo ilikuwa ni DAMU yake iliyomwagika pale Kalvari. Na baada ya kulinunua kanisa(ambaye ndio mke wake)..Ilimpasa aondoke arudi nyumbani kwa Baba yake ili kumwandalia mkewe makao, ili baadaye aje kumchukua tena…
Kama ilivyo desturi za wayahudi kwamba ni lazima mwanamume baada ya kuposa aondoke kwa kipindi fulani kwenda kumwandalia mke wake makazi na kisha baadaye aje kumchukua tena kwa shangwe na tarumbeta na nderemo aende kwake, ndivyo Kristo alivyofanya na atakavyofanya, siku atakaporudi mara ya pili kulichukua kanisa lake, naye atarudi kwa parapanda ya Mungu pamoja na kundi la malaika, na kumchukua mkewe kwenda kwenye makao ya Baba yake,(mbinguni) ambapo huko mbinguni kutakuwa na karamu kubwa ambayo haijawahi kutokea..na bibi arusi atakaa na Bwana arusi mbinguni kwa kipindi cha miaka saba, wakati huo duniani kutakuwa na dhiki kuu, na baada ya hiyo miaka saba ya karamu kuisha Bwana Yesu atashuka na kanisa lake, duniani kuja kuitawala dunia na dunia hii itageuka na kuwa mbingu mpya na nchi mpya, wataishi kwa furaha isiyo na kifani milele na milele.
Na kama inavyopaswa mwanamke aliyeposwa awe mwaminifu siku zote, wakati mume wake anakwenda kumwandalia makao, ndivyo inavyotupasa na sisi wakristo tunaoishi sasa, wakati tunamngojea Bwana twende mbinguni kwenye karamu tunapaswa kuwa watakatifu na wasafi katika roho zetu, kwa kujiepusha na uzinzi wa kiroho, kama ibada za sanamu, uasherati, ulevi, anasa na mambo mengine yote machafu. Ili ajapo atukute bado ni waaminifu katika lile agano aliloingia nasi pale Kalvari.
Kwahiyo kwa muhtasari huo mfupi unaweza ukaona ndoa iliyo katika utaratibu ni mpango wa Mungu kabisa..kwasababu ndani yake imebeba siri ya Kristo na kanisa lake.
Hivyo katika Ukristo pia, ni lazima hatua za kufunga ndoa zifuatwe, Baada ya mwanamume kumpenda mwanamke, anapaswa awashirikishe wazazi wa pande zote mbili, ili awaache wazazi wake kwa amani, kisha Mahari itolewe kulingana na makubaliano ya pande zote mbili, kama familia ya mwanamke haitaki mahari basi ni sawa, lakini ni lazima wamtoe Binti yao kwa moyo mweupe, Na baada ya mahari mipango ya ndoa inaanza, hapo ni kipindi cha matengenezo inaweza ikawa baada ya wiki,mwezi au hata mwaka inategemea na maamuzi ya upande wa mwanamume, kisha hatua ya mwisho ni kanisani…
Kwaajili ya kubadilishana viapo, sasa viapo vinavyobadilishwa hapa sio viapo vya upumbavu ambavyo biblia imevikataza, kwamba tusiape kabisa, bali viapo vinavyozungumziwa hapa ni viapo vya ahadi, mtu anaahidi kusema ukweli wa moyo wake wote..ambavyo ni lazima mtu aahidi, kuishi na mume wake/mke wake mpaka kifo kitakapowatenganisha, anaahidi kumpenda na kumjali siku zote za maisha yake…viapo hivi ni NADHIRI, na hivyo havina kugeuka nyuma, mtu atakayoyasema kutoka kwenye kinywa chake yanakuwa yanarekodiwa mbinguni, akiyavunja hayo basi atahukumiwa. Baada ya hapo ndipo ndoa hiyo inajulikana mbinguni na kupigwa muhuri.
Lakini ndoa nyingine inayofungwa nje ya utaratibu huo, sio halali mbele za Mungu, wengi hawapendi kuambiwa hivi kwasababu wameshafanya makosa na hawataki kuyarekebisha makosa yao, hivyo wanatetea uovu wao kwa kutumia maneno ambayo hayapo kwenye biblia.
Wewe kama umeishi na mwanamke/mwanamume ambaye mlichukuana tu! pasipo kufuata utaratibu, na ulifanya hivyo kwa kutokujua, ni rahisi tu kujirekebisha, tubu kwa Mungu wako kwa maana yeye anakuhurumia na kukupenda, kisha anza hizo hatua haraka sana, nendeni kwa wazazi wa pande zote, kama huyo mwanamke hana wazazi basi ndugu zake wa karibu,na mwisho kanisani..Mungu atawabariki, lakini kama umesikia na hutaki kutubu kwa kisingizio kuwa ni wapi manabii walifungishwa ndoa..Umekwisha kuusoma hapa utaratibu wa ndoa ulivyokuwa katika agano la kale..kwahiyo siku ile hutasema hukusikia.
Ni maombi yangu kuwa Bwana atakusaidia katika hilo, na pia kama hujampa Bwana maisha yako, nakushauri ufanye hivyo leo, ukubali kujiunganisha na Bwana, Ndoa ya Muhimu na ya msingi ambayo mtu hapaswi kuikosa ni hii ya rohoni (yaani muunganiko wa Kristo na kanisa lake).Kosa hiyo ya mwilini lakini usikose hii ya rohoni, Mpokee leo Kristo na IKUBALI MAHARI YA DAMU YAKE aliyoitoa pale Kalvari, Hakuna mahari kubwa kama hiyo ambayo ilishawahi kutolewa, ni UPENDO WA AJABU SANA, aliouonyesha Bwana, na baada ya hapo ishi katika uaminifu katika hichi kipindi kifupi tunachomngoja arudi, ili atakapokuja tuingie naye karamuni tusifananishwe na wale wanawali wapumbavu ambao Bwana wao alipokuja hawakuwa na mafuta ya ziada na hivyo wakatupwa nje..Hebu kwa kumalizia chukua muda kutafakari mfano huu wa wanawali na ujifunze kitu.
Mathayo 25 : 1-13
“1 Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi.
2 Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara.
3 Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao;
4 bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.
5 Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi.
6 Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki.
7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao.
8 Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.
9 Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie.
10 Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.
11 Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie.
12 Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi.
13 Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.”
Bwana akubariki.
Tafadhali “share” ujumbe huu na wengine na Bwana akubariki
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
ALIPO NA ATAKAPOKUWEPO BIBI-ARUSI WA YESU KRISTO.
ULE MFANO WA WANAWALI 10 (MATHAYO 25), YALE MAFUTA YA ZIADA KATIKA CHUPA ZAO YANAWAKILISHA NINI?
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, Mkuu wa Uzima libarikiwe…Karibu tujifunze Neno la Mungu, na leo kwa Neema zake tutajifunza Maana ya kumheshimu Mungu ni ipi?, Tukijifunza kupitia maandiko matakatifu.
Maana ya kumpa mtu heshima…haina tofauti sana na “kumpandisha mtu hadhi”, Biblia inaposema “waheshimu Baba yako na Mama yako” haina tofauti sana na kusema fanya jambo lolote ambalo likawaletea wazazi wako heshima mbele za Mungu na mbele za jamii inayowazunguka…Kwa kufanya hivyo ni sawa na umewaheshimu wazazi wako.
Kwamfano mtoto anapokuwa ni msafi wa tabia na mwenendo, anasalimia wakubwa, mpole, mtulivu, msikivu, mwelekevu na watu wote wa nje wakamwona..jambo la kwanza watu watakwenda kuwatazama wazazi wake na kuwasifia wazazi kwamba wanajua kumlea mtoto katika maadili, hivyo wazazi wa yule mtoto wanapata heshima kwa kupitia mwanao.Kwahiyo hapo huyo mtoto tayari katimiza amri ya Mungu ya kuwaheshimu mzazi wake, hata kama wazazi wake nyumbani hawajamfundisha hayo maadili.
kadhalika kijana wa kike, anapovaa mavazi ya nusu uchi na anatembea mtaani au barabarani, hata kama kapewa ruhusu ya kuvaa hayo mavazi na wazazi wake mwenyewe lakini bado mbele za Mungu na wanadamu HAJAWAHESHIMU MZAZI WAKE..Ni kwasababu gani?..Ni kwasababu Kwa mavazi yale anasababisha kuwadhalilisha wazazi wake na ndugu zake mbele za watu walio nje na mbele za Mungu. Na hili ndio tatizo kubwa kwa vijana wengi wa kike wanadhani kwasababu tu wazazi wao wanavaa nguo fupi na zaidi ya yote wanapewa ruhusa na wao kuvaa nguo fupi kama za wazazi wao, basi wanadhani mbele za Mungu tayari wanawaheshimu wazazi wao.
Wanaona wazazi wao wanakunywa pombe, na pengine hata wazazi wao wanawaacha na wenyewe wanywe pombe, wanadhani kuwa ndio wanawaheshimu wazazi wao.
Binti usijidanganye kumheshimu mzazi wako sio kumtii tu! bali ni kumpa hadhi kama mzazi, hata kama mzazi wako anakuruhusu au anakuhimiza uvae nguo za nusu uchi, au vimini, au suruali wewe kataa..mwambie Mama/Baba sitaki kukuvunjia heshima kwa kuvaa hizo nguo,.
Na pia kwa kijana wa kiume hata kama mzazi wako anatoboa masikio, au anakuruhusu nawe utoboe masikio, au anafuga rasta au anakunywa pombe hivyo anataka na wewe uwe mlevi kama yeye…wewe usikubali kwani kinyume chake kwa kukataa kwako ndiko utakuwa umemheshimu…ukitii kwa kukubali kuwa mlevi kama yeye, utakuwa hujamheshimu, hivyo kama maandiko yanavyosema “wote wasiowaheshimu wazazi wao watakuwa na siku chache za kuishi duniani”..Na wewe utakuwa ni mmoja wao..Lakini endapo ukakataa na watu wakikuona wewe sio mlevi kama baba yako, hata kama watamdharau baba yako kwa ulevi wake lakini pia kwa sehemu fulani watampa heshima baba yako kwa kulea mtoto mwenye adabu mbele za watu.
Na hivyo wewe kijana utakuwa umempandisha hadhi mzazi wako(umempa heshima yake).N.k Na mambo mengine yote ambayo unaweza kufanya yakampandisha hadhi mzazi wako mbele za Mungu na mbele za wanadamu, ukiyafanya hayo ndio utakuwa umemheshimu mzazi wako na kwa Mungu wa Mbingu na nchi.
pia ni hivyo hivyo, hatumheshimu Mungu wetu kwa KUMPA SHIKAMOO hapana! Mungu haheshimiwi hivyo, Yapo mambo matatu tunayoweza kufanya yakampa Mungu HESHIMA kubwa sana, nayo ni 1) IMANI… 2)UTAKATIFU…….3)MWONEKANO
Hayo mambo matatu ndio yatakayomfanya Mungu apate heshima kutoka kwetu., Lakini leo hatutazungumzia hayo mawili ya kwanza, bali tutazungumzia hilo moja la mwisho, ambalo ni MWONEKANO, tutaliangalia ni kwa namna gani litampa Mungu heshima.
Mavazi yamekuwa ni tatizo kubwa sana, kwa watu wanaojiita ni watu wa Mungu, hasa hasa kwa wanawake..Utakuta mwanamke hata kwenye Ibada anakwenda na suruali, au kimini, au anakwenda kajipaka uso rangi na mdomoni kaweka kila rangi. Na anaujasiri wote wa kukaa kiti cha mbele kabisa na anapaza sauti yake kwa nguvu akiabudu na kusifu, na ni kila siku anafanya hivyo.
Binti unayesoma haya, nakwambia kwasababu pengine uliambiwa lakini hukuelewa au ulipuuzia…Kwa mwonekano huo HUMWESHIMU MUNGU HATA KIDOGO. Kama tu ni aibu kutembea na Baba yako mzazi njiani ukiwa umevaa hizo nguo, si zaidi KUSIMAMA MBELE YA MUNGU WA MBINGU NA NCHI ukiwa na hizo nguo?..Hebu chukua muda kutafakari hili jambo, usilichukulie kiwepesi tu! Usidhani pale unapokwenda kuabudu hakuna macho ya Mungu, yapo na anaangalia kama tunavyoangalia sisi wanadamu, kwasababu Mungu huyo huyo aliyeuimba roho ndio huyo huyo aliyoumba mwili. Kwahiyo acha kusikiliza Ubeti wa shetani uliotungiwa kuzimu kwamba MUNGU ANAANGALIA ROHO HAANGALII MWILI.
Hebu tujifunze kwenye maandiko kidogo watu waliomheshimu Mungu kwa mwonekano wao.
Yohana 21 : 1-25
“1 Baada ya hayo Yesu alijidhihirisha tena kwa wanafunzi wake, penye bahari ya Tiberia, naye alijidhihirisha hivi.
2 Simoni Petro, na Tomaso aitwaye Pacha, na Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, na wana wa Zebedayo, na wengine wawili wa wanafunzi wake, walikuwapo pamoja.
3 Simoni Petro aliwaambia, Naenda kuvua samaki. Nao wakamwambia, Sisi nasi tutakwenda nawe. Basi wakaondoka, wakapanda chomboni; ila usiku ule hawakupata kitu.
4 Hata asubuhi kulipokucha, Yesu alisimama ufuoni; walakini wanafunzi hawakujua ya kuwa ni Yesu.
5 Basi Yesu akawaambia, Wanangu, mna kitoweo? Wakamjibu, La.
6 Akawaambia, Litupeni jarife upande wa kuume wa chombo, nanyi mtapata. Basi wakatupa; wala sasa hawakuweza kulivuta tena kwa sababu ya wingi wa samaki.
7 Basi yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda akamwambia Petro, Ndiye Bwana. Naye Simoni Petro, aliposikia ya kwamba ni Bwana, akajifunga vazi lake, (maana alikuwa uchi), akajitupa baharini.
8 Na hao wanafunzi wengine wakaja katika mashua; maana hawakuwa mbali na nchi kavu; ila yapata dhiraa mia mbili; huku wakilikokota lile jarife lenye samaki.
9 Basi waliposhuka pwani, wakaona huko moto wa makaa, na juu yake pametiwa samaki, na mkate”.
Ukisoma habari hiyo kwa makini utaona kwamba Petro alikuwa anavua na wenzake akiwa uchi (sasa uchi unaozungumziwa hapo sio uchi kabisa wa kukosa nguo zote, hapana bali ni uchi ambao mtu anakuwa amebakiwa tu na nguo ya ndani). Kutokana na desturi za uvuvi, wavuvi wengi wanapunguza nguo zao wakati wa kuvua ili wawe wepesi wa kuogelea na wanakuwa vile kwasababu wanakuwa wanaenda mbali na makazi ya watu, kwahiyo kwa mwonekano wao hawawezi kuiharibu jamii..
Kwahiyo hapa Petro alikuwa yupo na nguo ya ndani tu, gafla akatokea Bwana ufukweni na hawakumtambua lakini walipomtambua tu! PETRO ALIVAA VAZI LAKE HARAKA NA KISHA AKAJITUPA BAHARINI!.
Hebu tafakari hilo tukio!! Petro huyo ni mwanaume, na akatokea Yesu ambaye pia ni mwanaume kama yeye lakini Petro kwa kumheshimu Bwana akavaa haraka vazi lake, na hata baada ya kuvaa akaona haitoshi, ili kujisitiri zaidi akajitupa kwenye maji. Kwasababu anajua aliyesimama mbele yake ni nani?…alijua kabisa ni zaidi ya mwanadamu ni Mungu, na hivyo mbele zake anapaswa ajisitiri.
Kwa tukio hilo unaweza ukaona kabisa kamwe wanafunzi wa Yesu walikuwa hawajiachii mbele zake, ikiwa na maana kuwa walikuwa wanajisitiri mbele zake kila wakati, walikuwa hata hawadhubutu kubaki kifua wazi mbele zake ingawa wote walikuwa ni wanaume kama yeye.
Sasa kama hawa wanafunzi wa Bwana Yesu walio wanaume walikuwa wanajisitiri hivyo mbele za Bwana, unadhani wale wanawake waliokuwa wanamfuata walikuwaje mbele zake??..unadhani wakina Mariamu Magdalena walikuwa wanavaaje mbele zake, unadhani wangeweza hata kuonyesha vifua vyao mbele yake? walikuwa wanajisitiri kuliko kawaida, pengine hata walikuwa wanaficha wakati mwingine hata nyuso zao mbele zake.
Lakini leo hii unamwambia binti wa Mungu, kwa kumhurumia na kwa upendo, jisitiri unapoingia mbele za Mungu, na sio tu mbele za Mungu bali kila mahali, uendako unamwonyesha na maandiko kuhusiana na yeye kujisitiri (1Timthotheo 2:9)…anakuambia Mungu haangalii mavazi anaangalia roho, Injili ambayo haijulikani ilitoka wapi.
Mwanaume hawezi kwenda kwenye ibada na kaptura, au malapa lazima kuna kitu ndani yake kitamhukumu, na ukiona kaenda na malapa basi ni kweli huyo mtu hana viatu au anamajeraha..Lakini mwanamke ataingia kapaka wanja, lipstick, kapaka uso rangi, kapuliza pafyumu mita 5 mbele watu wanasikia, mgongo wote uko wazi, kavaa sketi fupi ambayo ni aibu kuelezea mfano wake, na ndani hakuna kitu kinamchoma!! Lazima kuna tatizo ndani ya huyo mtu.
1 Samweli 2: 30 “Kwa sababu hiyo, Bwana, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; LAKINI SASA BWANA ASEMA, JAMBO HILI NA LIWE MBALI NAMI; KWA MAANA WAO WANAONIHESHIMU NITAWAHESHIMU, NA WAO WANAONIDHARAU WATAHESABIWA KUWA SI KITU”.
Mwanamke unapokwenda kwenye ibada na mwonekano usio wa heshima, jua unakwenda kukutana na Bwana Yesu mwenyewe, unamshushia Yesu Kristo heshima yake, na hivyo na yeye hawezi kukuheshimu ndivyo Neno lake linavyosema, Watu wasio wakristo wanasema dini yenu ni ya namna gani? watu wanamwabudu Mungu uchi. Jina la Mungu linatukanwa kwa ajili yako. Utajikuta unakwenda kujitafutia laana badala ya Baraka..Hata kama hilo kanisa unalokwenda mchungaji wake anawaruhusu wanawake kuvaa hivyo au haongei chochote…wewe usiende kujitafutia laana mbele za Mungu, vaa kwa kujisitiri, vaa nguo za heshima jisitiri mbele za Mfalme Mkuu Yesu Kristo, na mbele za wanadamu Kama Petro aliyeteuliwa na Bwana alijisitiri mbele zake, na alikuwa ni mwanamume alifanya hivyo wewe mwanamke ni nani usifanye hivyo. Vaa nguo yako ndefu, funika kichwa chako, hata watu wasione kifua chako ndivyo utakavyokuwa UMEMHESHIMU MUNGU, na HIVYO MUNGU ATAKUHESHIMU.
Ni matumaini yangu kuwa Bwana atakupa macho ya kuyaona hayo ewe mwanaume/mwanamke..kwamba utamheshimu Mungu kwa mwonekano wako ili naye akuheshimu.
Mungu akubariki sana.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
Tukiachilia mbali ule waraka wa kwanza ambao Mtume Yohana aliuandika kwa watu wote, zile nyaraka mbili za mwisho zilizosalia hakuzielekezwa kwa watu wote, bali kwa watu husika, na tunaona ndio zimekuwa nyaraka fupi kuliko zote katika biblia nzima, lakini zimebeba ujumbe wa msingi sana, kwa makundi ya watu waliozungumziwa huko..Kwa mfano kama tukiutazama ule waraka wa tatu, tunasoma mtume Yohana aliuelekeza kwa ndugu mmoja anayeitwa GAYO.
Sasa wengi wanaupenda mstari mmoja maarufu sana unaotoka katika kitabu kile unaosema..”MPENZI NAOMBA UFANIKIWE KATIKA MAMBO YOTE NA KUWA NA AFYA YAKO, KAMA VILE ROHO YAKO IFANIKIWAVYO.(3YOHANA 1:2)”..Ni mstari unaopendwa na kila mmoja kwasababu ni mstari unatoa Baraka na mafanikio..Lakini tunashindwa kuelewa kuwa waraka ule haukuandikwa kwa watu wote bali kwa mtu anayeitwa GAYO peke yake ndio aliyeambiwa maneno yale ya baraka, na ni lazima ujue ni kwanini Baraka zile alizistahili yeye na si mwingine kutoka kwa Mungu, na kwa kujifunza kupitia yeye na sisi ndio tunaweza kustahili kupata Baraka kama zile, kwa ufupi kama ukisoma pale utagundua kuwa mtu huyu alikuwa na moyo wa kipekee sana, aliwakaribisha wageni waliokuwa wanasafiri kwa ajili ya kazi ya Mungu, alijitoa kwa ajili ya Bwana kweli kweli, aliwahudumia watumishi wa Mungu waliokwenda kuhubiri nchi za ugenini, kwa hali na mali kiasi cha kwamba hata watumishi hao waliosafirishwa na yeye wakawa hawana mahitaji yoyote kutoka kwa watu wasioamini, Hivyo sifa zake zikavuma katikati ya makanisa yote mpaka kuwafikia mitume..Na ndipo ukija kusoma utaona maneno hayo ya Baraka yanatamkwa mbele yake..
Sasa leo utamwona mtu ni mkristo lakini hata kutoa kitu kidogo kwa Mungu wake anaona shida, na huyo huyo bado ndio wa kwanza kumwambia Mungu, ulisema nifanikiwe katika mambo yote..Hajui kuwa ili Mungu akubariki kwa Baraka kama hizo kuu na nono sio hivi hivi tu..BALI KWA WATU WENYE TABIA KAMA ZA GAYO. Watu ambao hawapo tayari kuona kazi ya Mungu haikwamishwi na kitu chochote.
Vile vile na leo tutaona kwa ufupi juu ya ujumbe ulio katika huu Waraka wa PILI wa Yohana, je! Unamhuhusu nani?. Ni vema ukapata muda wa kuusoma wote peke yako. kwanza ni mfupi na pia itakusaidia tuende pamoja katika uchambuzi huu tunaokwenda kuuangalia..
Tunasoma…
3Yohana 1:1 “Mzee, kwa MAMA MTEULE, na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na wote waijuao ile kweli;
Awali ya yote tunaona Hapa mtume Yohana anajitambulisha kama MZEE, na sio kama mtume, au mtumwa wa Kristo, kufikisha ujumbe kama mkomavu, mtu aliyekula chumvi nyingi, anafahamu mambo mengi yahusuyo kanisa na shamba la Mungu kwa ujumla, anayejua jinsi ya kupambanua mitego ya Yule mwovu aliyowahi kuiona katika maisha yake ya kikristo, na jinsi mitego hiyo inavyoweza kunasa makundi mbali mbali ya watu na namna yake, “kijana kwa wazee”, watoto kwa wakubwa, waume kwa wake, n.k.
Hivyo hapa waraka huu tunaona moja kwa moja anaulekeza kwa MAMA MTEULE..Na sio mama tu wa kawaida, Bali anasema mama MTEULE tena pamoja na watoto wake..Hivyo ni wazi kuwa ujumbe huu unawahusu WANAWAKE WOTE, WALE WALIO WATEULE WA KRISTO, ambao wameshaokolewa, ambao walishaoshwa dhambi zao kwa damu ya Yesu Kristo, ambao neema ya Mungu tayari ipo juu yao siku zote, ambao ni watakatifu tena wenye watoto,.
Sasa yapo mambo 3 makuu yalipaswa yazingatiwe au yaonekane katikati wanawake watuelu wa Mungu wa namna hiyo..Na ndio hayo tutayatazama leo katika vipengele vyake. Jambo la kwanza ni..
1) KUWAONGOZA WATOTO KATIKA KWELI:
Kama ukisoma hapo utaona mzee huyu alianza kwanza kwa kuchunguza hali ya watoto wa mama Yule mkristo, katika nyumba yake, na kutamani sana kuona jinsi alivyoweza kuwajali watoto wake au watu wa nyumbani kwake kwa kuhakikisha kuwa wanamcha Mungu, wanadumu katika utakatifu, alitamani kumwona mama huyu jinsi ambavyo angejitoa katika kuangalia hali ya kiroho ya watoto wake kuliko kitu kingine chochote wakifanyacho.. na kama tunavyosoma ni kweli mwanamke huyu mteule alikuwa nacho Tunasoma.
1:1 “Mzee, kwa mama mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na wote waijuao ile kweli;
2 kwa ajili ya hiyo kweli ikaayo ndani yetu, nayo itakuwa pamoja nasi hata milele.
3 Neema, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo Mwana wa Baba, zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.
4 Nalifurahi mno kwa kuwa nimewaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba”.
Unaona hapo mstari wa 4 anasema.
“4 Nalifurahi mno kwa kuwa nimewaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba.”
Hivyo ikiwa wewe ni mama, na unataka kuitwa MTEULE wa Kristo, Swali ni je!.unahakikisha watoto wako wanaenenda katika misingi ya kumjua Mungu?, Unawakemea wanapotenda dhambi au unawaangalia tu, je! Unafuatia hali zao za kiroho, au kila wakati upo buzy kufuatilia tu mahudhurio yao ya shuleni na huku mahusiano yao na Mungu yanadorora kila siku. Watoto wako mstari mingapi ya biblia wanaifahamu mpaka sasa, lakini nyimbo za kidunia kila siku unawasikia wakiimba lakini huwasemeshi? Na bado unajiita MAMA MTEULE wa Kristo unayempenda Mungu….Huo sio uteule mama, siku ile hautakuwepo katikati ya wanawake wateule wa Kristo kama wakina SARA na HANA, na wengineo ikiwa utawaona watoto wako wanapotea na wewe huwasemeshi kitu, ikiwa utawaona hawamjui Mungu na wewe hutaki kuwafundisha, unawanunulia kila siku vitabu vipya vya shuleni lakini biblia huwanunulii, unawalipia tution kila siku lakini fellowship na bible study huwapeleki…Huo sio uteule mama…Hali kadhalika na wewe ambaye bado hujawa na watoto, je! Hayo malengo yapo kwenye kichwa chako?
2) KUWA NA UPENDO:
Jambo la pili Mzee huyu alilotamani kuliona katikati ya mwanamke huyu mteule wa Kristo ni UPENDO.
Tunasoma.
“5 Na sasa mama, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane.
6 Na huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. Hii ndiyo ile amri, kama mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo”.
Unaona hapo? Anasema Hii ndiyo ile amri, kama mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo. Sasa Amri hiyo aliyokuwepo tangu mwanzo ni ipi?
Marko 12:29 “Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;
30 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.
31 Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.”
Umeona hizo mbili zote alitazamia kuziona kwa mwanamke huyu, ahakikishe kuwa kumpenda Mungu kupo ndani yake siku zote, juu ya kulea watoto katika kweli lakini pia kumcha Mungu kuwepo ndani yake, awe na amani kuwepo uweponi mwa Bwana, awe mwombaji, au msomaji wa Neno.
Na pia awapende ndugu, kwa furaha kabisa kama vile biblia isemavyo upendo huvumilia, upendo hauhusudu, upendo haujivuni, upendo hauhesabu mabaya,.
Lakini mwanamke anayesema ameokoka, lakini hana habari na Mungu, hataki kujifunza maneno ya Mungu, hata kusali kwake ni shida, huruma hana, ni msengenyaji wakati wote, hana uvumilivu ndani yake, akiudhiwa kidogo tu, yeye naye anaanza kusengenya. Na suala hili limekuwa hafifu kwa wanawake wengi, na hivyo kimekuwa kikwazo kikubwa sana cha UTEULE WAO pasipo wao kujijua, Hivyo kama wewe ni mwanamke na unajiita mteule fanyia kazi hilo kwa bidii, shindana na usengenyaji huo mpaka uushinde.
3) KUJILINDA NA WADANGANYIFU.
Hili ndio jambo la tatu na la mwisho mzee huyu mwenye hekima alimwomba mama huyu mteule alizingatie. Hapa anaendelea kusema..
“7 KWA MAANA WADANGANYIFU WENGI WAMETOKEA DUNIANI, wasiokiri ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo.
8 Jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda, BALI MPOKEE THAWABU TIMILIFU.
9 Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu. Yeyeadumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba na Mwana pia.
10 Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu.
11 Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu”.
Tazama hapo anasema “KWA MAANA WADANGANYIFU WENGI WAMETOKEA DUNIANI”,…Sasa kumbuka kama wadanganyifu hawa walitokea wakati ule, watatokea na sasa, na pia zingatia jambo hili ili usichanganyikiwe roho ya mpinga-kristo ni ile ile, lakini utendaji wake kazi unabadilika kulingana na nyakati na majira. Wadanganyifu waliokuwepo wakati ule wa mitume walikuwa na kazi moja tu, yaani Kumkana Kristo kuwa hakufufuka..Kwasababu habari ya ukristo ndio kwanza zilikuwa zinaanza kuhubiriwa, Hivyo shetani ili kuuuwa ukristo usiaminiwe na wengi kwa wakati ule, alitumia udanganyifu wa kuwa Kristo hajafufuka, na pia hawezi kurudi katika mwili..Hao ndio walioitwa wapinga-kristo wa wakati ule, na ndio hao Mzee huyu alikuwa anamwonya mama huyu MTEULE ajitenge nao pamoja na mafundisho yao…Kwasababu kwa uzoefu wake wa rohoni Mungu aliompa aliona kuwa wanawake wengi wateule ndio wanaokuwa rahisi kuchuliwa na wimbi hili na wapinga-kristo zaidi ya wanaume wateule,.(sisemi kuwa wanaume hawadanganyiki), hapana bali wengi ni wanawake.
Lakini roho ile ile ya udanganyifu, inatenda kazi hata sasa isipokuwa kwa namna ya ujanja mkubwa zaidi, mpaka kufikia hatua Bwana Yesu kusema wakati huo watawadanganya yamkini hata walio WATEULE…Hivyo roho hii ya udanganyifu haiji tena kwa kusema Yesu hakufufuka, au haikuambii Yesu hatarudi, kwani mpaka sasa shetani anafahamu kuwa hakuna mkristo asiyejua kuwa Kristo alifufuka, na Yesu siku moja atarudi..kila mtu analijua hilo, lakini badala yake anakuja na udanganyifu mwingine nao ndio huu “Kushusha thamani ya wokovu na injili ya YESU KRISTO.”
Kuwafanya watu wasichukulie tena kwa uzito na umakini habari za wokovu, watu wajue kuwa ni kweli Yesu anaokoa lakini maisha yao yasiathiriwe na wokovu huo, anahakikisha kuwa mtu anakuwa vuguvugu, nusu kwa Mungu nusu kwa dunia, injili ya kisasa, injili ya I don’t care, injili ya “haijalishi!”..injili ya kutabiriwa tu mafanikio basi, lakini mambo ya toba yasigusiwe kabisa..Na hali hiyo inawalewesha hata wale ambao walikuwa wamesimama waanze kuwa vuguvugu.
Na roho hii inawakamata sana sana wakina mama, tena hata wale wateule, na ndio maana hapo Mtume Yohana anamwambia. “9 Kila apitaye cheo, wala asidumu katika MAFUNDISHO YA KRISTO, yeye hana Mungu”.
Umeona, njia pekee ya kuwatumbua hao ni kudumu katika mafundisho ya Kristo (Yaani Neno la Mungu)…
Webrania 12: 14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
Hivyo ikiwa wewe ni mwanamke mteule unayetaka kupokea THAWABU TIMILIFU kama huyu mama, hakikisha unaufanya imara uteule wako kama maandiko yanavyosema, kwa kuzingatia hayo mambo matatu kuwa yapo ndani yako.
2 Petro 10 “Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na UTEULE WENU; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe”.
Mungu akubariki. Tafadhali “Share” ujumbe huu kwa wengine. Na Bwana atakubariki zaidi.
Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA TATU WA YOHANA.
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU
Ni nani aliyeidharau siku ya mambo madogo?…Ni swali Bwana alilouliza.
Jina la Bwana Yesu Kristo, libarikiwe, karibu katika kujifunza Neno la Mungu, Leo kwa Neema za Mungu, tutajifunza namna ya kusimama imara siku ya mambo madogo?.
Najua unajiuliza SIKU YA MAMBO MADOGO NDIO NINI?...Lakini kabla ya kufikia huko kuelezea siku ya mambo madogo, hebu tujikumbushe kidogo historia fupi ya Taifa la Israeli, ambapo kwa kupitia hiyo tutaelewa kwa undani nini maana ya “siku ya mambo madogo”.
Kama wengi wetu tunavyojua Mungu aliwatoa wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri, na kuwaingiza katika nchi ya ahadi, ambapo ndani ya nchi ile aliwaahidia kula mema yote endapo wataishi kwa kuzishika amri zake, na kama ni msomaji mzuri wa biblia utagundua kuwa vipo vizazi vilivyofanya vizuri kwa kwenda katika sheria za Mungu, ambavyo viliishi kwa raha na kwa amani, na vipo pia vizazi vya wana wa Israeli ambavyo havikufanya vizuri, vilikengeuka na kuacha kuyashika maagizo ya Mungu waliyopewa na badala yake vikapitia vipindi vya tabu sana.
Na utaona pia baada tu ya Israeli kugawanyika na kuwa sehemu mbili yaani YUDA NA ISRAELI …ndio kipindi ambacho wana wa Israeli walipozidi kukengengeuka kwa viwango vya hali ya juu. Kuanzia kipindi cha Mfalme Yeroboamu mpaka kipindi cha mfalme Hosea wa Israeli kulikuwa hakuna unafuu kabisa, watu waliabudu mabaali na sanamu wazi wazi na kuvukiza uvumba katika sehemu za juu. Na kwasababu ya maasi kuwa mengi, Bwana alituma idadi kubwa sana ya manabii wake katika kipindi hichi kuliko vipindi vyote vilivyotangulia ili kuwaonya wana wa Israeli wageuke na kuacha njia zao mbovu, hivyo kuanzia huo wakati manabii wengi sana walitokea kama wakina Eliya, Elisha, Nathani, Yona, Habakuki,Sefania, Hosea, Mika, Yeremia,Isaya, Obadia, Amosi,Nahumu,Ezekieli,Yoeli,Mika, Zekaria n.k Wote hawa walitokea ndani ya kipindi cha wafalme wa Israeli..Lakini hawakusikia, kinyume chake waliwaua wengine na kuwapiga kwa mawe.
Hivyo maovu yalipozidi hata kufikia kikombe cha ghadhabu ya Mungu kujaa, kukawa hakuna tena kusamehe, Mungu akaahidi kuwa watakwenda utumwani, na Miji yao yote itachomwa moto, na watu wengi sana watauawa kwa upanga, na wengine watakufa kwa njaa, na wengine kwa Tauni. Na lile hekalu ambalo mfalme Sulemani alilitengeneza kwa gharama nyingi litavunjwa na kuteketezwa kabisa..Na kweli wakati ulipowadia Neno la Bwana lilitimia, Israeli ilichukuliwa utumwani Ashuru na wale waliosalia wa Yusa ,Wakaldayo(yaani watu wa Babeli)..walifika Yerusalemu wakauteketeza mji wao kwa moto, wakalivunja lile hekalu kama Ilivyotabiriwa wakawaua watu wengi kwa upanga; wanawake, kwa watoto na wachache waliobakia waliwachukua utumwani kwenda nao Babeli. Israeli Mji ambao ulipata sifa na kuogopeka na mataifa yote ulimwenguni ukageuka kuwa kama jalala.
Lakini Mungu ni wa rehema aliwaahidi kuwa hawatakaa huko utumwani milele, bali watakaa huko wakimtumikia Mfalme wa Babeli kwa miaka 70 tu! na baada ya hiyo miaka 70 kuisha watarejeshwa tena kwao.
Sasa ndio tunaelekea kwenye kiini cha somo letu, baada tu ya wana wa Israeli kutimiza ile miaka 70, wakiwa Babeli Mungu aliwafungulia mlango wa kurudi tena nchini mwao, lakini waliporudi kule walikuta tayari kuna watu wengine ambao walikuwa wanakaa pale, ambao sio waisraeli, ambao mfalme wa Uajemi aliwaweka wakae kule…Lakini Hao watu walipoona wana wa Israeli wamerudi tena nchini mwao wakaanza kuwapiga vita.
Wakati wana wa Israeli wanapanga kumjengea tena Mungu Hekalu lingine jipya baada ya lile la kwanza kuharibiwa na Mfalme wa Babeli miaka 70 iliyopita, wanakutana tena na changamoto nyingine ya kusumbuliwa…hivyo kwasababu ya hao watu iliwafanya waishiwe nguvu kabisa ya kuijenga tena nyumba ya Mungu, kwasababu pia kwa idadi yao waliorudi Israeli walikuwa ni wachache sana.
Lakini ulipofika wakati Mungu aliwanyanyua manabii wake wawili HAGAI na ZEKARIA kuwatabiria wana wa Israeli kwamba wasimame imara waijenge nyumba ya Mungu wasiogope changamoto zilizopo mbele yao, ijapokuwa hawana fedha wala utajiri lakini Bwana atakuwa nao katika UDOGO WAO. Bwana akamwambia Hagai maneno haya awaambie wana wa Israeli.
Hegai 2: 1 “Katika mwezi wa saba, siku ya ishirini na moja ya mwezi, neno la Bwana lilikuja kwa kinywa cha Hagai nabii, kusema,
2 Sema sasa na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, liwali wa Yuda, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na hayo mabaki ya watu, ukisema,
3 Miongoni mwenu amebaki nani aliyeiona nyumba hii katika utukufu wake wa kwanza? Nanyi mnaionaje sasa? Je! Mbele ya macho yenu, siyo kama si kitu?
4 Lakini sasa uwe hodari, Ee Zerubabeli, asema Bwana; nawe uwe hodari, Ee Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, nanyi iweni hodari, enyi watu wote wa nchi hii, asema Bwana; MKAFANYE KAZI, kwa kuwa mimi ni pamoja nanyi, asema Bwana wa majeshi;
5 KAMA NENO LILE NILILOAGANA NANYI MLIPOTOKA KATIKA NCHI YA MISRI; NA ROHO YANGU INAKAA KATI YENU; MSIOGOPE.
6 Kwa maana Bwana wa majeshi asema hivi, Mara moja tena, ni kitambo kidogo tu, nami nitazitikisa hizo mbingu, na hii nchi, na bahari, na nchi kavu;
7 nami nitatikisa mataifa yote, na vitu vinavyotamaniwa na mataifa yote vitakuja; nami nitaijaza nyumba hii utukufu, asema Bwana wa majeshi.
8 FEDHA NI MALI YANGU, NA DHAHABU NI MALI YANGU, asema Bwana wa majeshi.
9 Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema Bwana wa majeshi; na katika mahali hapa nitawapa amani, asema Bwana wa majeshi”.
Unaona maneno hayo?..Bwana anawatia moyo wana wa Israeli kuwa WASIOGOPE! Utukufu wa hekalu la pili utakuwa mkubwa kuliko utukufu wa lile Hekalu la Kwanza. Hivyo wasonge mbele, wakafanye kazi, wasiangalie umaskini walio nao, wala shida waliyo nayo wasonge mbele kwasababu utukufu wa nyumba ya pili utakuwa ni mkubwa kuliko utukufu wa nyumba ya kwanza, na FEDHA NA DHAHABU NI MALI ya Bwana.. haleluya!! Haleluya!!.
Zaidi ya hayo wakati wana waisraeli wakiongozwa na kiongozi wao aliyeitwa ZERUBABELI wanatazama kuwa kujenga nyumba na uchache wao, na umaskini wao, pamoja na wingi wa maadui uliowazunguka ni jambo lisilowezekana, ni kama mlima mkubwa umewekwa mbele yao halafu uusawazishe kwa beleshi..Lakini jicho la Mungu lilikuwa linaona tofauti..Na ndio Bwana akampa nabii Zekaria maono mengine miezi miwili baada ya yale maono ya Hagai na kusema..
Zekaria 4: 5 “Ndipo malaika aliyesema nami akajibu, akaniambia, Hujui vitu hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu.
6 Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, SI KWA UWEZO, WALA SI KWA NGUVU, BALI NI KWA ROHO YANGU, ASEMA BWANA WA MAJESHI.
7 NANI WEWE, EE MLIMA MKUBWA? MBELE YA ZERUBABELI UTAKUWA NCHI TAMBARARE; NAYE ATALILETA LILE JIWE LA KUWEKWA JUU KABISA PAMOJA NA VIGELEGELE VYA, NEEMA, NEEMA, ILIKALIE.
8 Tena neno la Bwana likanijia, kusema,
9 Mikono yake Zerubabeli imeiweka misingi ya nyumba hii, na mikono yake ndiyo itakayoimaliza; nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwenu
10 MAANA NI NANI ALIYEIDHARAU SIKU YA MAMBO MADOGO? Kwa kuwa watafurahi, nao wataiona timazi katika mkono wa Zerubabeli…..”
Unaona hapo anasema NANI WEWE, EE MLIMA MKUBWA? MBELE YA ZERUBABELI UTAKUWA NCHI TAMBARARE, Mbele ya changamoto zote zinazoonekana kama ni milima, mbele za masihi wa Bwana zitakuwa ni nchi tambarare…na sio kwa uwezo wa Zerubabeli wala kwa nguvu zao bali kwa roho yake Bwana ndio watausawazisha huo mlima.
Na zaidi ya yote Bwana anamwambia Zerubabeli.. “MAANA NI NANI ALIYEIDHARAU SIKU YA MAMBO MADOGO”…
Sasa siku ya mambo madogo ndio ipi?..Ndio hiyo siku ambayo walikuwa hawana chochote, siku ambayo walikuwa wanaona hakuna chochote kinachoweza kufanyika, siku ambayo walikuwa wanaona ndio kwanza mambo bado hata hayajaanza, siku ambazo nguvu zao ni chache, hizo ndio siku za mambo madogo?..Na Bwana anawauliza ni nani anayezidharau siku hizo??…Ni nani anayesema kwamba jambo hilo la kuisimamisha nyumba yenye utukufu mwingi halitafanikiwa?..Ni nani anayesema kuwa katika udhaifu huo hakuna chochote kinachoweza kufanyika?!…sentensi hiyo huwa inamuhuzunisha Mungu sana.
Ndugu somo hili ni la kukutia moyo tu! wewe ambaye upo katika safari ya kwenda mbinguni, kuwa USIIDHARAU SIKU YA MAMBO MADOGO.
Kama ndio kwanza unaanza kumtafuta Mungu, usizidharau siku hizi ambazo unajiona huwezi kuitenda kazi ya Mungu, siku inafika utakayoleta matunda mengi kwa Kristo, endapo hutazimia unachopaswa kufanya ni kuendelea kusonga mbele kwa bidii zote bila kukata tamaa,…Mtaji ulionao moyoni mwako uzalishe, kwasababu ni kama mbegu ndogo, na itakapokuwa itakuletea faida nyingi sana mbeleni. Mwingine aliniambia jana siwezi kumgeukia Mungu kwasasa sina kazi,..ndugu hata ukipata bilioni 100 leo bado utajiona tu hujafika, anza leo na Bwana.
Na pia katika maisha ya kawaida ya kujitafutia riziki, ikiwa wewe ni mkristo na kwanza ndio shughuli uzifanyazo zinaanza kuchipuka, upo kama fukara tu! au una mtaji kidogo, au kazi yako ni ya hadhi ya chini sana, na ukiangalia mbele unaona milima mikubwa, hiyo milima isikuogopeshe, ITAKUWA NCHI TAMBARARE…. Usidharau siku ya mambo madogo nenda kakifanyie kazi hicho kidogo, kakizalishe!! Usimvunjie Mungu heshima kwa kutomwamini endelea kutenda haki katika utakatifu wote kwa sababu fedha na dhahabu ni mali yake, mwisho wa siku atakunyanyua tu! kama alivyomnyanyua Zerubabeli na haitakuwa kwa nguvu zako wala kwa uwezo wako bali kwa ROHO WA MUNGU,…NI NANI WEWE UNAYEIDHARAU SIKU YA MAMBO MADOGO! Mungu mwenyewe haidharau wewe ni nani uidharau na mtu mwingine yoyote yeye ni nani hata aidharau siku ya mambo yako madogo!!..Hata kama unauza mchicha usizidharau hizo siku.
Na mwisho kabisa tunaona baada ya Zerubabeli kupata unabii ule kutoka kwa Bwana, kwa vinywa vya Hagai na Zekaria Manabii wa Bwana, alipata nguvu mpya yeye pamoja na Yoshua na wana wa Israeli wote na kwenda kuijenga nyumba ya Mungu, na baada tu ya kutia nia ya kwenda kuijenga nyumba, wakati huo huo vibali vikaanza kufunguka, mara mfalme anatoa amri wapewe ruhusa ya kujenga pasipo kusumbuliwa, mara mfalme anasema wapewe fedha na wasilipishwe kodi yoyote na fursa nyingi na upendeleo mwingi waliupata kutoka kwa watu na mfalme, nyumba ya Mungu ilipatikana na dhahabu nyingi na fedha nyingi, na ikamalizika chini ya mikono ya Zerubabeli salama sawasawa na unabii Bwana alioutoa.
Hivyo ndugu, Bwana ndiye anayenyanyua na ndiye anayeshusha, kama alikushusha chini wakati mwingine ni kwasababu ya maovu yako (ingawa sio kila kushushwa chini ni kwasababu ya maovu, nyingine ni kwa utukufu wa Mungu kama Ayubu), kama ilivyo tu kufanikiwa, sio mafanikio yanatoka kwa Mungu…lakini kama maisha yako yalikuwa hayampendezi Mungu huko nyuma na akakushusha ni kwasababu anakupenda anataka akupe tumaini tena, kama alivyowashusha wana wa Israeli kukaa Babeli miaka 70, na walipotubu aliwarudisha tena katika nchi yao na kuwapa faraja kubwa kama hiyo, na kuwanyanyua tena! Kwanini na wewe asikufanyie hivyo endapo utatubu kabisa kwa kumaanisha kuziacha dhambi zako na kumgeukia yeye. Na kumbuka USITUBU! Kwasababu tu unataka KUPATA UTAJIRI WA ULIMWENGU HUU, tubu kwasababu unataka kwanza kupata UTAJIRI WA ULIMWENGU UNAOKUJA!…..Huo ukiupata hata huu wa ulimwengu hauhitaji kuuhangaikia, Bwana alisema TUTAZIDISHIWA, kuzidishiwa sio kusumbukia, kitu cha kutafuta ni Ufalme wa Mungu, huo ndio tumeambiwa tuutafute kwa bidii zote …“ Mathayo 6:33..utafute kwanza ufalme wake na haki yake, na hayo mengine mtazidishiwa”.
Hivyo Kama hujampa Bwana maisha yako, huu ndio wakati wako wa kufanya hivyo, kabla mlango wa Neema haujafungwa, Roho wa Mungu anataka utii thabiti kutoka ndani ya moyo wako na sio kulazimishwa, anataka utubu kabisa kwa kudhamiria KUACHA, sio KUPUMZIKA, hapana bali kuacha dhambi, unakusudia kuacha kwa vitendo usengenyaji, uasherati, rushwa, utukanaji, ulevi, uvaaji usio na heshima(vimini na suruali kwa wanawake), unakusudia kuacha anasa zote za ulimwengu, na ukisha tubu hatua inayofuata ni ubatizo sahihi, na ubatizo sahihi ni wa maji Mengi na kwa Jina la Yesu Kristo, kulingana na Matendo 2:38, na kisha baada ya ubatizo Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu atakayekusaidia kushinda dhambi. Na hapo utakuwa umezaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho.
Mungu akubariki sana.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
SHETANI ANATOLEA WAPI FEDHA, ANGALI TUNAJUA FEDHA NA DHAHABU NI MALI YA BWANA?.