Luka 12:35 “VIUNO VYENU na viwe vimefungwa, na TAA ZENU ziwe zinawaka; 36 nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara. 37 Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia. 38 Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao.”
Luka 12:35 “VIUNO VYENU na viwe vimefungwa, na TAA ZENU ziwe zinawaka;
36 nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.
37 Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.
38 Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao.”
Lakini hapa limetokea jambo ambalo linamgharimu Bwana wao kuchelewa, hivyo inamlazimu kuwasihi wamsubirie wasilale mpaka atakaporudi kutoka Harusini ili waje kumfungulia pindi tu atakapogonga malango ya nyumba … Unajua Kwa hali ya kawaida, wapo watumwa wengine watasema, huyu bwana amevunja mkataba tulioingia naye hivyo sisi hatutaweza kumngojea mpaka muda huo, kwanza katufanyisha kazi mchana kutwa tena na bado hapa anataka tukeshe mpaka usiku wa manane, atatupa fedha ya ziada? Wengine watasema sisi tutamngojea lisaa limoja au mawili na asipoonekana tutalala.
Lakini wengine wakarimu watasema hapana tusifanye hivyo bwana wetu huwa hana desturi ya kutufanyia hivi sikuzote, imekuwa ni dharura tu,na ni leo tu kesho haitakuwa hivi, hivyo tuvumilie kwa siku hii moja tumngojee bwana wetu asije akalala nje! Kwenye hatari nyingi.
Hivyo ni wazi kuwa wapo watakaokataa na watakaokubali. Lakini habari hiyo inaendelea kutuambia nini?
“37 Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo ATAWAKUTA WANAKESHA. Amin, nawaambieni, ATAJIFUNGA NA KUWAKARIBISHA CHAKULANI, ATAKUJA na KUWAHUDUMIA.”
Unaona hapo mfano huo unaturudisha pia kuitafakari habari ya wana wa Israeli siku ile ambayo Mungu aliona vema kuwatoa utumwani baada ya kukaa miaka 430 katika hali ya mateso, Kwa kuwa hatuna muda wa kuelezea matukio yote lakini tunafahamu siku ile ya mwisho ya wao kukaa katika nchi ya Misri Mungu aliwapa maagizo, na ikumbukwe kuwa hawakutoka nchi ya Misri MCHANA, hapana bali ilikuwa ni USIKU wa manane kwasababu ndio uliokuwa mpango wa Mungu watoke usiku.
Lakini kabla ya kutoka kwao Mungu aliwapa maagizo na maagizo na mojawapo ya maagizo hayo ilikuwa ni KUFUNGWA MKANDA VIUNONI na KUVALIWA kwa VIATU. Tunafahamu mtu akienda kulala ni lazima azilege nguo zake, atoe mikanda kisha azime taa na alale. Lakini kama nguo zako bado zimebanwa na mkanda pamoja na viatu ni wazi kuwa mtu huyo yupo katika mazingira ya kutoka muda wowote.
Lakini wana wa Israeli hawakujua uzito wa wao kuambiwa hivyo, mpaka tunavyosoma pale Farao na wamisri wote wakiwafukuza wenyewe kutoka Misri pamoja na zawadi nyingi usiku ule ule, hapo ndipo walipotambua kuwa kumbe! KUVAA KULE NDIO ILIKUWA NI KUONDOKA! Wengine waliwaza mbona! imekuwa Ghafla ghafla tu, hili jambo si lingesubiria walau asubuhi tu, tuanze kuweka vitu vyetu vizuri, tuwaage majirani zetu, tuwafuate wadeni wetu watulipe kwanza?, tukavune ngano zetu tupate chakula cha kusafiria? Nk. Lakini mbona jambo hili Mungu kaliharakisha mapema hivi?….Tunasoma usiku ule ule safari ilianza (Kutoka 12), lakini jaribu kifikiria kama mwisraeli mmoja asingetiii yale maagizo na kwenda kuamua kujifungia ndani kwake na kuvua nguo zake na kulala, unadhani atakapoamka ni jambo gani atakutana nalo?, WENZAKE HAWAPO!!. Na ndivyo itakavyokuwa katika siku hizi za mwisho Bwana alisema.
“VIUNO VYENU na viwe vimefungwa, na TAA ZENU ziwe zinawaka; 36 nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka ARUSINI, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara. 37 Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia. 38 Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao.”
“VIUNO VYENU na viwe vimefungwa, na TAA ZENU ziwe zinawaka;
36 nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka ARUSINI, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.
Unaona hapo, laiti kama hawa watumwa wote wangekuwa tayari kumngojea bwana wao mpaka atakaporudi kutoka arusini ili wamfungulie, kwa fadhila Bwana wao asingewaambia laleni mpumzike, hapana badala yake kwa kuwa VIUNO VYAO VIMESHAFUNGWA ikiashiria utayari wao wa kuondoka.
Moja kwa moja yeye mwenyewe atawakaribisha katika karamu yake aliyokwenda kuiandaa baada ya kutoka arusini, na kuwahudumia kwa kila kitu ambacho wangekihitaji, usiku ule ule wangeondoka pale nyumbani na kwenda mahali pengine kabisa kula raha ya daima. Kadhalika wao nao wangestaajabia kwanini Bwana wetu asingesubiri walau asubuhi ifike tuoge, tuvae vizuri tuwaambie na wenzetu kisha ndio tuende kwa pamoja huko kwenye hiyo karamu aliyotuandalia…kwanini kachukua maamuzi ya haraka haraka usiku huu?.. Lakini hivyo ndivyo ilivyompendeza Bwana wao.
Ndugu siku ya kuondoka kwa wana wa Mungu hapa duniani hakutakuwa kwa kukutazamia kama wengi wanavyodhani. Utakuwa ni wakati usiofaa kwa wengi hata katikati ya watumishi wake waaminifu.
Bwana alipotupa maagizo kwamba TUKESHE, TAA ZETU ZIWE ZINAWAKA na VIUNO VYETU VIWE VIMEFUNGWA. Alijua kabisa itakuwa ni wakati wa usiku wa manane ndio muda utakuwa wa kurudi kwake . Na sasa ndio tupo hicho kipindi ambapo dunia ipo katika kilele cha giza kuu kuliko hata vizazi vyote vya nyuma vilivyotutangulia. Maovu yameongezeka kuliko hata kipindi cha Sodoma, ushoga unahalalishwa hata mahali patakatifu. Hizo ndio dalili madhubuti kuonyesha kwamba tupo katika giza nene la usiku wa manane.
Lakini kumbuka pia Bwana wetu yupo karibu kurudi kutoka katika arusi ya faragha aliyoalikwa na BABA yake mbinguni. Na watakaokwenda naye ni wale tu ambao TAA zao zinawaka na VIUNO vyao vimefungwa, yaani wale ambao kila siku macho yao yapo mbinguni. Biblia inasema “jifungeni KWELI kiunoni” na kweli ni NENO LA MUNGU (Waefeso 6:14). Hivyo wale wote wataokadumu katika msingi ya Neno la Mungu wakielekeza macho yao mbinguni bila kujali mambo yanayopita ya ulimwengu, kadhalika pia wale ambao TAA zao zinawaka, kumbuka ili taa iwake inahitaji mafuta, na mafuta ni ROHO MTAKATIFU, Hivyo wale ambao waliotajazwa Roho na kila wakati wanaufanya uteule wao na wito wao imara bila kumzimisha Roho wa Mungu ndani yao, hao ndio siku ile BWANA atakapogonga watamsikia na kuingia kwenye Karamu aliyoiandaa yeye mwenyewe. Na pia ili taa iwake lazima kuwe na giza, taa haiwezi kuwashwa wakati wa mchana, hivyo wakati huu ambapo dunia imejaa matendo ya giza, ndio wakati wa kuzifanya taa zetu ziwake.
Lakini wengine wote waliosalia, wapendao matendo ya giza hawatajua lolote, itakapopambazuka tu ndipo watakapogundua kuwa wenzao hawapo, na ndiko kutakako kuwa na kilio na kusaga meno. Katika dhiki kuu, na katika siku ile ya BWANA.
Ni kwanini leo maisha yako yasiuhakisi wokovu?, Ni kwanini bado upo usingizini?. Na uzingizi hauna nguvu mchana,JE! Unao huhakika hata Bwana akija leo, utakuwa mwepesi kumsikia akigonga mlango wa moyo wako?, Mambo ya ulimwengu huu yanakusonga?, Unawatazama wanadamu? Hao watakusaidia nini endapo umesikia unyakuo umekupita, ? na wewe umebaki? ujana wako, mali zako na nguvu zako zitakuwa msaada gani kwako katika siku hiyo?
BWANA ANASEMA..
Waefeso 5:14 “……AMKA, WEWE USINZIAYE, UFUFUKE KATIKA WAFU, Na Kristo atakuangaza. 15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16 MKIUKOMBOA WAKATI KWA MAANA ZAMANI HIZI NI ZA UOVU.”
Waefeso 5:14 “……AMKA, WEWE USINZIAYE, UFUFUKE KATIKA WAFU, Na Kristo atakuangaza.
15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
16 MKIUKOMBOA WAKATI KWA MAANA ZAMANI HIZI NI ZA UOVU.”
Kama haujatubu ndugu fanya hivyo sasa, huu si wakati wa kuishi maisha ya kubahatisha, UKOMBOE WAKATI! nenda ukabatizwe katika ubatizo ulio sahihi wa maji mengi katika jina la YESU KRISTO haraka baada ya kutubu dhambi zako ili upate ondoleo la dhambi (Matendo 2:38) …Kumbuka kuzaliwa mara ya pili ni kutubu, kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho, na kuishi maisha matakatifu katika Kristo, na si vinginevyo. Ikiwa bado hujapitia hatua hizo zote hapo bado hujazaliwa mara ya pili. Na Bwana alisema mtu wa namna hiyo hawezi kuuona ufalme wa mbinguni (Yohana 3:5).
Fanya bidii utubu na Bwana atakuangazia neema yake.
Ubarikiwe sana.
Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine, Na Bwana atakubariki
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
KAMA MWIZI USIKU WA MANANE:
BEI YA UFALME WA MBINGUNI:
JE! UMECHAGULIWA TANGU ASILI?
ZILE TUNU (DHAHABU, UVUMBA NA MANEMANE) MAMAJUSI WALIZOZITOA KWA BWANA (MATHAYO 2) . ZILIWAKILISHA NINI?
SAYUNI NI NINI?
Rudi Nyumbani
Print this post