Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe! Karibu tujifunze Biblia. Leo kwa Neema za Bwana tutajifunza juu ya “swali kuu la kujiuliza katika maisha yetu”.
Hebu jaribu kutengeneza picha labda kuna mtu, kakukamata halafu kakufunga macho na kisha akakusafirisha na kukupeleka labda tuseme nchi ya India, na ulipofika pale hakukwambia kama upo India, badala yake akakutelekeza kwenye moja ya mitaa ya India na kukimbia, na baadaye ulipofanikiwa kufungua kile kitambaa mbele yako ukaona mazingira ambayo hujawahi kuyaona, mitaa ambayo ni mipya kwako, watu ambao huwajui, lugha inayozungumzwa ni ngeni kwako, ulipotazama kulia ukaona kuna watu wanacheza mpira kiwanjani, ulipotazama kushoto ukaona kuna mgahawa wa chakula, watu wanakwenda pale kula, ulipotazama nyuma ukaona kuna watu wanakimbilia kupanda gari la usafiri, na pembeni mwa barabara ukaona kuna kama soko Fulani la mboga mboga na matunda na wafanyabiashara wengi, mbele yake kidogo unaona nyumba nzuri za kifahari na bustani nzuri za kumpumzika..
Jiweke katika hiyo nafasi halafu uniambie..ungekuwa ni wewe ungekimbilia kipi cha kwanza?..inawezekana ukasema ningekimbilia kucheza mpira, au kwenye mgahawa wa kula, au sokoni kula matunda. Lakini kama umefikiria mojawapo ya hivyo basi ni wazi kuwa utakuwa umefikiria jambo la kipumbavu la mtu asiyefikiri.
Kwanini ni jambo la kijinga?…Ni kwasababu baada ya kujikuta tu pale, swali la kwanza ambalo ungetakiwa kujiuliza HAPA NI WAPI? Na NI KWANINI NIPO HAPA?..Hilo ndio jambo la kwanza kabisa la kujiuliza kabla ya kufanya jambo lolote au kujiunga na kitu chochote kule..Utajiuliza kwa makini sana HAPA NI WAPI?..Niko wapi hapa?..na baada ya hilo swali kujiuliza litakalofuata ni NI KWANINI NIPO HAPA?.
Sasa majibu ya maswali haya utayapata kutoka kwenye vyanzo viwili tofauti…Swali la kwanza linalouliza HAPA NI WAPI au NIKO WAPI HAPA…Jibu lake utalipata kwa kwenda kuwauliza watu wanaokuzunguka, labda utaenda pale mgahawani na kumwuliza mtu mmoja na kuwambia “samahani eti hapa ni wapi?”…Pengine Yule mtu anaweza akashangaa kidogo kuulizwa swali kama lile anaweza akafikiri wewe ni kichaa lakini mwisho wa siku atakwambia hapa ni INDIA.
Na baada ya kujua kuwa upo INDIA, swali litakalofuata ni NANI aliyenileta hapa, na ni kwa dhumuni gani yeye kunileta hapa?..sasa jibu la hili swali huwezi kulipata kwa wale watu tena wanaokuzunguka, kwasababu ukienda kuwauliza watakuona umerukwa na akili…Hivyo itakugharimu kufanya uchunguzi wako kumjua aliyekupeleka pale na dhumuni lake, hapo ndipo itakugharimu uchunguzi kidogo Kumtafuta Na kama Yule aliyekuleta atapenda kujidhihirisha kwako, ili kukueleza sababu ya yeye kukuweka pale basi atakupa sababu zote, na dhumuni lake lote, kisha ukishatimiza mapenzi yake, yeye ndiye atakayekuonyesha njia ya kurudi katika nchi uliyotoka. Huo ni mfano tu!.
Sasa katika maisha tunayoishi ndio hivyo hivyo….Sisi wanadamu wote tumezaliwa katika hii dunia, TUMEJIKUTA TU! TUMETOKEA HAPA ULIMWENGUNI. Hatukukaa katika kikao cha makubaliano na yeye aliyetuleta hapa ulimwenguni. Tumejikuta tu! Tupo tayari ulimwenguni ni kama tumetekwa mateka na kuletwa mahali tusipopajua. Na wote tulipozaliwa tayari tumekuta kuna mambo yanaendelea duniani, tumekuta kuna michezo, kuna burudani, kuna shughuli hizi na zile, kuna kumbi za starehe na mambo mengi, kuna fursa nyingi kila mahali…Lakini swala ni lile lile litakuwa ni jambo la kipumbavu kujiunga na hayo mambo kabla ya kujiuliza baadhi ya maswali..KWAMBA MIMI NI NANI? NIMETOKA WAPI? NIPO WAPI? NA NI NANI ALIYENILETA HAPA? NA KWA DHUMUNI GANI?…Hayo ndiyo maswali ya kwanza ya muhimu ya kujiuliza ya mtu mwenye akili kabla ya kujiunga na taasisi yoyote ile, kabla ya kujiunga na chuo Fulani, kabla ya kujiunga na biashara Fulani, kabla ya kuanza kupanga mipango fulani ya maisha…hayo ndio maswali ya msingi ya kujiuliza.
Na baadhi ya majibu ya hayo maswali unaweza kuyapata kwa wanadamu wenzako lakini kuna ambayo huwezi kuyapata kutoka kwa wanadamu, kwamfano ukienda kumwuliza mtu hapa ni wapi? Atakuona mwendawazimu lakini mwisho wa siku atakupa jibu hapa ni duniani, na atakupa mpaka historia ya dunia ilipotokea n.k.
Na swali la kwamba ni nani aliyekuleta hapa duniani, unaweza ukajibiwa tu kirahisi kuwa ni MUNGU..Lakini dhumuni la yeye kukuleta hapa ni lipi? Hakuna atakayekujibu!..hapo itakugharimu wewe utafute, hakuna mtu anayeweza kukupa jibu la dhumuni la Mungu kukuleta hapa duniani?..Kwasababu kila mtu anakusudi lake la kutimiza hapa duniani tofauti na mwingine.
Sasa utajuaje kusudi la aliyekuleta hapa duniani (Yaani kusudi la Mungu)..juu yako?
1) Kwanza Ni lazima umpate huyo aliyekuleta duniani, na namna ya kumpata huyo ni kwa kupitia kitu kimoja kinachoitwa MSALABA..Kwa kupitia YESU KRISTO, Hakuna namna nyingine yoyote utakayoweza kumjua Mungu nje ya huyu YESU KRISTO, Huo ndio ukweli ndugu yangu, na huyu unampata tu kwa kumwamini na kwa kutubu dhambi zako na kumgeukia yeye kikweli kweli, na kwa kubatizwa na kwa kupokea Roho Mtakatifu. Hapo utakuwa umempata huyu aliyekuleta ulimwenguni.
2) Baada ya kumpata kwa kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, sasa moja kwa moja ataanza kuongea na wewe na kukuongoza katika lile kusudi alilokuitia duniani, hajakuleta hapa duniani bure bure tu! Wala hajakuleta hapa ili uwe mfanyabiashara, au uwe maarufu, au uwe milionea, hapana lipo kusudi lingine ambalo ndilo alilokuletea hapa, na hilo kusudi linafanya kazi kwa silaha alizoziweka ndani yako tayari (yaani karama aliyoiweka ndani yako), kwa kupitia huyu Roho wake Mtakatifu atakufunulia hilo kusudi, na ukishalijua hilo kusudi ndipo amani ya ajabu ya kuishi duniani itakujia, kwasababu umeshajua dhumuni la wewe kuletwa duniani. Na kusudi hilo ndilo litakalokufanya uishi kama mpitaji tu katika hii dunia, ukijua kuwa hapa duniani, sio kwako, ni kama umetekwa tu na umeletwa ili utimize kusudi Fulani, na huku ukijua kabisa aliyekuleta sio mjinga kwamba akulete humu duniani na kisha ashindwe kukuhudumia mahitaji yako ya mwilini, kwahiyo utakuwa unaishi kwa bajeti ya aliyekuleta, sio bajeti yako wewe, huku ukiangalia na kulitazama kusudi lake. Na lolote utakalolifanya ndani yake utafanikiwa.
Ndugu unayesoma ujumbe huu, swali ni lile lile? UNAJUA UPO WAPI?…UNAJUA SABABU YA WEWE KUWEPO HAPA?...Ni jambo la kuhuzunisha kama unaishi katika hii dunia na unafanya anasa, unaendelea na shughuli zako za kiuchumi…lakini hujui sababu ya wewe kuishi duniani, ni sawa na Yule mtu aliyetweka na kufumbuliwa macho na pasipo hekima yoyote akaanza kukimbilia mgahawani kula chakula, pasipo hata kujiuliza yupo wapi…Hivyo ndiyo unavyoonekana mbele za Muumba wako wewe usiyetaka kuyatafakari msingi wa maisha yako?..unaonekana mpumbavu mbele zake kwa kutokutambua kusudi lako na uwepo wake na wako..wewe na mtu asiyeamini kuwa Mungu yupo hamna tofauti.
Zaburi 14: 1 “Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu….”;
Kama leo hii umeamua kufumbua macho yako na kutafuta kujua kusudi la Mungu juu ya maisha yako, hatua ni nyepesi za kufuata, ndio hizo hapo juu…kwanza tubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kutokuzitenda tena, kusudia moyoni kuacha uasherati, uzinzi, utazamaji wa pornography, masturbation, usengenyaji, ulevi, uvutaji wa sigara, rushwa, utoaji mimba, ulawiti,wizi, utukanaji na mengineyo..kisha ukishadhamiria kuacha hayo mambo…hatua inayofuata ni kwenda kubatizwa, kumbuka ubatizo sahihi ni wa muhimu sana na ni wa kuzamishwa mwili wote katika maji tele na kwa JINA LA YESU KRISTO, Ubatizo wa udogoni sio sahihi kulingana na maandiko, kama ulibatizwa hivyo, hukufanya dhambi kwasababu ulikuwa hujui, ulifanyiwa pasipo kujua lakini sasa umejua ukweli,nenda kabatizwe tena upya kwa Imani, kwasababu ni maagizo ya Bwana YESU mwenyewe. Kulingana na Matendo 2:38. Na baada ya kumaliza hatua hizo muhimu..Nguvu ya Ajabu ya Roho Mtakatifu itaingia ndani yako, hiyo itakuongoza katika kuijua kweli yote ya biblia na kukufunulia kusudi la Mungu juu ya maisha yako, na jinsi ya kulitimiza hilo kusudi hatua kwa hatua..Na huyo huyo Roho atakusaidia kulitimiliza mpaka mwisho wa siku zako.
Wafilipi 1: 6 “Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu”;
Anza leo kazi njema, Timiza kusudi la aliyekuleta hapa ulimwenguni, na siku ile upokee Taji ya Uzima.
Bwana akubariki sana.Tafadhali “share” na wengine ujumbe huu.
Kwa Maombezi, Ushauri, au Ratiba za Inada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +225789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Zinazoendana:
AYUBU 28 : HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?
NGUVU YA HEKIMA NA AKILI
JE! UBATIZO SAHIHI NI UPI?
Rudi Nyumbani
Print this post
Shalom mtu wa Mungu, karibu tujifunze Maneno ya uzima, Leo hii ukimwuliza mtu yeyote aliye mkristo swali.. ‘chakula cha rohoni ni nini?’….atakujibu pasipo kusita sita kuwa ni NENO LA MUNGU. Na ndivyo ilivyo Neno la Mungu ndio chakula cha Roho zetu. Ni swali ambalo jibu lake linajulikana na watu wote.
Wapo wengi wanaofahamu umuhimu wa Neno la Mungu, lakini vile vile si wengi wanaofahamu kazi ya Neno la Mungu katika maisha yao ya hapa duniani na huko wanakokwenda.
Leo tutatazama kwa ufupi kazi ya Neno la Mungu juu ya maisha yetu ya kikristo.
Kwanza kabisa kama tunavyojua wengi wetu kuwa Neno la Mungu linafananishwa na chakula, na pia kama tunavyojua mtu hawezi kukua vizuri au kuongezeka kimo au unene pasipo kula vizuri..Moja ya kazi ya chakula ni kutufanya tukue kimwili na kuwa na afya njema.
Kadhalika katika roho, ili tusitawi katika roho vile ipasavyo ni lazima tule vizuri rohoni, na chakula hakiliwi mara moja kwa mwaka, vinginevyo utakufa, bali kinaliwa mara tatu kwa siku, angalau huo ndio tunaweza kusema ni mlo ulio sahihi.
Lakini licha ya faida mojawapo ya chakula ambayo ni ya kuukuza mwili, ipo pia faida nyingine ya muhimu sana ambayo wengi wetu hatuifahamu, au kama tunaifahamu basi hatuitilii maanani.
Na faida hiyo ni kuupa MWILI NGUVU.
Mtu anapokula chakula, kile chakula kinaingia tumboni, na kuchanganyikana na baadhi ya vimeng’enyo na kisha kuna baadhi ya hatua zinaendelea pale, kile chakula kinavunjwa vunjwa na hatimaye kunapatikana virutubisho ambavyo vinaweza kuupa mwili nguvu, ndio hapo mtu anapata nguvu ya kuweza kusimama, kutembea, kufanya kazi, kukimbia, kuongea, kuona n.k. kama alikuwa ni mtu wa mapambano vitani anapata nguvu ya kupambana vizuri zaidi na kushinda.
Na Neno la Mungu ni hivyo hivyo, halitusaidii tu kukua kiroho, kama wengi wetu tunavyojua, bali pia linatupa nguvu za kila siku zinazoweza kutusaidia kufanya kazi za kiroho, kusimama katika roho, kukimbia katika roho, kushindana katika roho na kushinda. Ndio maana mtu mwenye afya njema utakuta anakula mara tatu kwa siku na anakula mlo kamili. Na mtu wa namna hiyo ni ngumu kuwa mdhaifu au kushambuliwa na magonjwa.
Kadhalika ni wajibu wetu hata sisi kulitafakari Neno si mara moja tu kwa siku au kwa wiki, hapana hata ikiwezekana mara tatu au mara nne kwa siku, ili kujiweka katika hali ya kuwa na afya njema katika roho. Kwasababu nguvu za rohoni kila siku zinapungua na zinahitaji kuongezwa chaji kwa kula chakula kizuri cha roho…Mtu asikudanganye eti! Kuwa nguvu za rohoni, hazipungui au haziishi,!! Huo ni uongo ndugu!! Watu wote nguvu zao zinaisha kila siku kwasababu zinatumika katika roho kufanya shughuli nyingi..hivyo ni lazima kila siku ziongezwe na zinaongezwa kwa kula chakula cha rohoni (Neno la Mungu).
Ndio maana biblia inatuambie “yeye ajidhaniaye kuwa amesimama aangalie asianguke 1Wakorintho 10:12”..Ikiwa na maana kuwa tunajukumu kila siku la kujiongeza nguvu za rohoni. Hata vyombo vya elektroniki kama simu, hakuna kifaa kinachokaa na charge muda wote ni lazima kuna wakati kinakwenda kuongezewa nguvu kwa kuchajiwa…Watu tu wa imani nyingine katika mambo yao wanaweza kufanya dua mara tano kwa siku, lakini wakristo hatuwezi kufanya lolote.
Ni kwanini wakati mwingine mtu anashambuliwa na nguvu za giza?..Ni kwasababu nguvu zake za rohoni ni chache, kila kukicha wachawi wanakusumbua, na magonjwa ya ajabu ajabu yasiyofahamika chanzo chake..mengi ya hayo (ingawa sio yote) yanasababishwa na roho yako kutokula vyema. Mara ya mwisho ulikula wiki iliyopita unategemea vipi usiwe dhaifu?, usishambuliwe na wachawi?.
Nguvu za rohoni hazipatikani kwa kulisoma Neno siku moja na kwenda zako?, haiko hivyo kabisa, Tunahitaji kujifunza Maandiko kila siku ili tuishi. Hata kama tutarudia chakula kile kile kila siku ni afadhali kufanya hivyo kuliko kutokula kabisa.
Ni afadhali kurudia kile kile nilichojifunza jana na juzi kuliko kutoshika kabisa Biblia na kujifunza maandiko, ndugu zipo hatari nyingi sana za kutolitafakari Neno la Mungu.
Ili siku yako, mwezi wako, mwaka wako uende vizuri unahitaji Neno la Mungu rohoni mwako, ili roho yako iwe salama unahitaji kujifunza Neno la Mungu kila siku, ili ukue katika maarifa ya ki-Mungu na ili umjue yeye zaidi, Kujifunza Neno lake kila siku hakukwepeki. Hiyo ndio siri ya kuishi pasipo kusumbuliwa na shetani na kuendelea mbele, Ni kwa kula tu chakula kilicho sahihi.
Zaburi 119: 105 “Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu”.
Sikiliza maneno haya ya YEHOVA…
Kumbukumbu 11:18 “Kwa hiyo yawekeni maneno yangu mioyoni mwenu na rohoni mwenu; yafungeni yawe dalili juu ya mikono yenu, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yenu. 19 Nayo wafunzeni vijana vyenu kwa kuyazungumza uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. 20 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako; 21 ili siku zenu zifanywe nyingi, na za vijana vyenu nao, juu ya nchi Bwana aliyowaapia baba zenu kuwa atawapa, kama zilivyo siku za mbingu juu ya nchi”.
Kumbukumbu 11:18 “Kwa hiyo yawekeni maneno yangu mioyoni mwenu na rohoni mwenu; yafungeni yawe dalili juu ya mikono yenu, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yenu.
19 Nayo wafunzeni vijana vyenu kwa kuyazungumza uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
20 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako;
21 ili siku zenu zifanywe nyingi, na za vijana vyenu nao, juu ya nchi Bwana aliyowaapia baba zenu kuwa atawapa, kama zilivyo siku za mbingu juu ya nchi”.
Wakolosai 3: 16 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu”.
Ubarikiwe!
Kwa Maombezi, Ushauri, au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036613/ +225789001312
NJAA IPO!, USIACHE KULA ASALI.
MANA ILIYOSHUSHWA KUTOKA MBINGUNI.
CHAKULA CHA ROHONI.
MAJI YA UZIMA.
Shalom! shalom!, karibu tuongeze maarifa katika mambo yetu yahusuyo wokovu wetu hapa duniani. Wengi wanadhani mtu akiingia tu katika wokovu basi, akili yake huwa inafutwa na kugeuzwa kuwa kitu kingine cha kimbinguni, Na hivyo vitu kama wivu, hasira, ghadhabu, visasi, vinyongo, chuki, huzuni, hofu, vinakuwa vimeondoka kabisa ndani ya huyo mtu, Na ikionekana kuwa havijaondoka basi huyo mtu bado hajafanyika kiumbe kipya.
Mimi hapo nyuma niliomuomba sana Mungu aniondolee hivyo vitu ndani yangu, kwasababu nilikuwa ninachukia ninapoona hasira inakuja ndani yangu na mimi ni mkristo, wakati mwingine hofu Fulani,.hayo yalinifanya nijione kama bado sijawa mkristo. Lakini baada ya kuona ninaomba sana viondoke bila ya kuona mafanikio yoyote, ndipo Mungu akanifumbua macho yangu ya ndani nikaona…
Nikaja kugundua kuwa nilikuwa ninamuomba Mungu aniondolee vitu ambavyo ameniumbia ndani yangu, na kama hiyo haitoshi, yeye mwenyewe anavyo…Nikafikiria nikasema ni kweli ukitafakari utaona Mungu anao wivu, amejitaja mwenyewe kuwa yeye ni Mungu mwenye wivu (Kutoka 20), amejitaja kuwa yeye ni Mungu mlipiza kisasi, amejitaja yeye ni Mungu mwenye hasira nyingi na ghadhabu, isitoshe amejionyesha sehemu nyingi kuwa anahuzunika wakati mwingine,..Sasa kama hivyo vitu vipo ndani yake kwanini mimi nimwombe aniondolee?..Na yeye katuumba sisi kwa mfano wake, biblia inasema hivyo.
Kiuhalisia vitu hivi Mungu hakuviumba kwa ubaya ndani yake na ndani ya watu wake, bali ni kwa nia njema kabisa na ya Upendo. Embu jaribu kufikiria kama mtu asingekuwa na wivu hata kidogo kwa mpenzi wake, inamaanisha kuwa hata angemwona mtu mwingine anam-baka mke wake, asingeshuhulika kufanya lolote angemwacha tu, kwasababu ndani yake hakuna chembe chembe za wivu, ambazo hizo zingemsaidia kumpigania mke wake asifanyiwe kitendo kama kile..
Jaribu pia kufikiria kama mtu asingekuwa na hofu ndani yake, angeweza hata kwenda kuchukua kisu na kumchoma mtu mwingine, au angeweza hata kwenda kusimama juu ya ghorofa refu na kujitupa chini, kwasababu ndani yake hakuna hofu ya kuogopa chochote, unadhani tungekuwa na madhara mengi na makubwa kiasi gani duniani?. Jamii zetu zingesimamaje?
Au fikiria ungekuwa hauna hasira hata kidogo ungekuwa wewe ni wa kuonewa au kuudhiwa tu kila saa, au unadhulumiwa haki yako, lakini kama mtu akiona umekasirika, ataogopa na kuacha kile alichokuwa anakifanya kwasababu anajua akiendelea madhara yoyote yanaweza kumtokea..Hivyo unaona hasira hapo inasimama kama ulinzi kwa mtu asionewe au asidhulumiwe au asiudhiwe.
Vivyo hivyo na vitu kama ukali, na vinginevyo. Ni mambo ambayo Mungu ametuumbia ndani yetu, ili yatumikie katika mahali papasapo,..Lakini leo hii ni kwanini tunaona , Wivu ni kitu kibaya, hasira ni kitu kibaya, kisasi ni kitu kibaya, chuki ni kitu kibaya, kinyongo ni kitu kibaya….Ni kwasababu tunavitumia mahali ambapo Mungu hakutaka vitumike na ndio hapo vinaonekana kuwa ni vitu vibaya visivyofaa kuonekana ndani ya mtu yeyote.
Embu tuangalie mfano wa wivu mzuri, Tuchukulie mfano wa Bwana wetu Yesu, yeye kuna wakati alishikwa na WIVU wa kushindwa kuvumilia mpaka kufikia hatua ya kuleta madhara na vurugu..Hayo yalitokea pale alipokwenda Hekaluni na kukuta watu wanafanya biashara mahali ambapo pangepaswa pawe mahali pa Ibada…ndipo tuona akapindua mezi zile na kuwachapa wale waliokuwa wanafanya biashara mule ndani. ..Mpaka wanafunzi wake wakakumbuka kuwa iliandikwa hivyo (Yohana 2:17 ….Wivu wa nyumba yako utanila.).
Unaona huo ni mfano mzuri jinsi wivu ulivyotumika jinsi ipasavyo. Lakini tujiulize ingekuwa na sisi tupo pale na yeye je! Tungeshirikiana naye kufanya kile kitendo? Ni rahisi kusema ndio. Lakini ikiwa leo hii tunaona Injili ya YESU KRISTO Bwana wetu inageuzwa na kuwa taasisi za kibiashara, na hakuna chochote kinachotukuna ndani yetu?..Badala yake wivu wetu unajidhihirisha katika mambo mengine yasiyokuwa na umuhimu sana, pale tunapoona wafanyakazi wenzetu wanatuibia ofisini, ndio tunakuwa na wivu, pale tunapoona mafisadi wanaaiibia nchi, wanapitisha magendo, ndio tunazungumza mpaka mshipa ya shingo inatutoka, na kibaya zaidi pale tunapoona majirani zetu wanafanikiwa, ndipo tunatafuta namna zote juu chini za kuwashusha ili wasiendelee mbele …
Sasa kama wivu wa namna hii ndio Mungu kaukataa, kama upo ndani yetu basi tujue umetumika isipovyopasa na hivyo unahesabika kuwa ni dhambi mbele za Mungu..Nguvu hizo hizo unazotumia kuhakikisha adui yako hafanikiwi kwanini usizipeleke mbele za Mungu wako kuhakikisha adui yako MKUU shetani hafanikiwi na kazi zake mbovu?..Kwanini tunaona kazi ya Mungu inachezewa na sisi tunakaa kimya, wachekeshaji wameingia mpaka madhabahuni wanamfanyia Mungu dhihaka na sisi tunafurahi pamoja nao,..
Halikadhalika KISASI ni kitu chema ambacho kimeumbwa ndani yetu ili kitimize kusudi Fulani..Na kusudi hilo si lingine zaidi ya kumpiga shetani. Fikiria Ulipokuwa katika dhambi ulivyokuwa unateseka na magonjwa, ulivyokuwa unateswa na nguvu za giza au mapepo au wachawi au jinsi ulivyokuwa unakesha Disco na kupoteza muda mwingi na pesa nyingi, hata kwa wiki mara mbili ukimwabudu shetani kule..Lakini sasa umekuwa mkristo, kuna kitu Fulani ndani yako unapaswa ukihisi kitu kama kisasi kumlipizia shetani kukupotezea muda wako, na kukutesa na mambo mabaya, Hivyo sasa utahakikisha muda wako hata kwa wiki mara tatu unakesha katika kumsifu Mungu na na katika kuomba nakuziharibu kazi za shetani katika kuwavuta watu kwa Kristo..Hicho ndio kisasi Mungu anachokitafuta, ulikuwa unaimba nyimbo za kidunia, sasa umeokoka ni wakati wa kumwimbia na kumsifu Mungu kwa nguvu zaidi kulipiza kisasi kwa vile shetani alivyokutenda..
Ulikuwa ni msengenyaji na mmbea wa kupelekea taarifa za watu kwa watu wengine mpaka mtaa wa tatu sasa umeokoka ni wakati wa kutumia kipawa kilekile kumlipizia shetani kisasi kwa kusambaza habari za Yesu kwa nguvu wa watu wengine zaidi ya pale ili kumkomesha shetani. Hivyo ndio visasa ambavyo Mungu anavihitaji.
Vivyo hivyo tumeumbiwa hofu. Ulikuwa unamwogopa shetani na wachawi kiasi kwamba hata wewe mwenyewe ulikwenda huko huko kumwomba akupe hirizi kama kinga yako. Lakini sasa umeokoka, ile hofu imerudi mahali ipasapo, itumie hiyo kumwogopa Mungu wako na sio adui yako tena..kama Bwana Yesu alivyotuambia
Luka12:5 “Lakini nitawaonya mtakayemwogopa; mwogopeni yule ambaye akiisha kumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanum; naam, nawaambia, Mwogopeni huyo.”
Hofu yako ikiwa kwa Mungu utaogopa kwenda kuzini, utaogopa kutukutana, utaogopa kusema uongo, utaogopa kufanya mambo maovu, kama haipo hautamjali Mungu n.k.
Chuki iliyopo ndani yako, ndugu hiyo Mungu hakukuumbia kwa ajili ya kuwachukia ndugu zako, ni wazi kuwa huwezi kumwekea chuki mdogo wako au kaka yako au mama yako aliyekuzaa, utakuwa na chuki sana na Yule ambaye uliyemwona akimchoma mdogo wako moto bila huruma., Vivyo hivyo chuki hasaa ya ki-Mungu ipo ndani yetu kumchukia SHETANI pamoja na mapepo yake yote, na kazi zake zote, na sio wanadamu wenzetu ambayo hayo ndiyo yamekuwa sababu ya ndugu zetu wengi mamilioni kuwepo kuzimu leo hii.. Na hivyo kama hiyo chuki itatumika ndani yetu kisawasawa leo hii tutaweka mikakati kabambe ya kumwangamiza shetani na kazi zake kwa KUHUBIRI INJILI YA YESU KRISTO kwa watu wote.
Hivyo kwa kumalizia, ni maombi yangu kuwa vipawa vyote na tabia zote Mungu alizoziweka ndani yako, usiruhusu shetani azitumie vibaya kwa faida zake, bali badala yake, tuziteke zikaleta manufaa makubwa katika ufalme wa mbinguni. Leo hii usimwombe Mungu akuondolee hasira ndani yako, haitaondoka hiyo, ili uwe mfano wa Mungu lazima uwe nayo, badala yake pale inapokuja basi ukumbuke lile Neno kuwa je! Mahali ninapoiachilia ni mahali pafaapo, kama hapafai, moja kwa moja ikatae hiyo hali na yenyewe itatulia,. Lakini ikiwa ni sehemu ifaayo yaani ni sehemu yenye manufaa kwa ajili ya ufalme wa mbinguni na kumkandamiza shetani..basi usiizuie kwani hiyo imevuviwa na Mungu kutimiza kusudi lake.
Ubarikiwe sana na Bwana Yesu.
HISIA YA MUNGU ILIYO MBAYA KULIKO ZOTE.
TUSIPOUTHAMINI WOKOVU TUTAPATAJE KUPONA?
JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?
KIFAA BORA CHA MATUMIZI.
Mhubiri 1:1 “Maneno ya Mhubiri mwana wa Daudi,mfalme katika Yerusalemu. 2 Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili. 3 Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua? 4 Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima. 5 Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake. 6 Upepo huvuma kusi, hugeuka kuwa kaskazi; hugeuka daima katika mwendo wake, na upepo huyarudia mazunguko yake. 7 Mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena. 8 Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia. 9 Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua. 10 Je! Kuna jambo lo lote ambalo watu husema juu yake, Tazama, ni jambo jipya? Limekwisha kuwako, tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi”.
Mhubiri 1:1 “Maneno ya Mhubiri mwana wa Daudi,mfalme katika Yerusalemu.
2 Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili.
3 Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua?
4 Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima.
5 Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake.
6 Upepo huvuma kusi, hugeuka kuwa kaskazi; hugeuka daima katika mwendo wake, na upepo huyarudia mazunguko yake.
7 Mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena.
8 Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia.
9 Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua.
10 Je! Kuna jambo lo lote ambalo watu husema juu yake, Tazama, ni jambo jipya? Limekwisha kuwako, tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi”.
Shalom karibu tujifunze Neno la Mungu, Sulemani alipewa na Bwana hekima kuliko watu wote wakati huo, alichunguza mambo mengi na kupata jawabu moja ya mambo hayo na kusema yote ni UBATILI.
Ubatili maana yake ni “kitu kisichokuwa na maana”…au “kitu ambacho kwa nje kinaonekana kina thamani kubwa lakini ndani yake hakina maana”..hiyo ndio maana ya Neno UBATILI.
Umewahi kujiuliza kwanini Sulemani aliishia kusema mambo yote ni Ubatili??…Hebu tujifunze kidogo ni kwanini alisema hivyo..
Ukisoma mstari wa 4, 5,6 na wa 7 hapo juu utapata picha ni kwanini Sulemani anasema mambo yote ni Ubatili. Utaona kuwa aliyajaribu kutafiti mambo kadhaa akidhani kuwa atapata jambo jipya ndani yake lakini kinyume chake akagundua kuwa mambo yote yanamrudisha kwenye jambo lile lile la kwanza, akachukia na kuhuzunika akasema sasa inafaida gani kujitaabisha na kitu ambacho hatma yake ni kule nilikotokea.
Alilitafakari jua, alilichunguza linapozama huwa linaenda wapi…pengine akatafakari labda linapotea na kutokea jua jingine jipya…lakini alipozidi kuchunguza akagundua jua ni lile lile moja, hakuna jua jipya, ni lile lile lipo kwenye mzunguko wake..
Akatafakari tena ni wapi maji masafi yanatengenezwa, akachunguza milimani ni sehemu gani hiyo inayoyatengeneza safi kila siku malita ya maji mapya yanayotiririka chini ya milima na kuishia baharini, alipochunguza sana akitazamia agundue jambo jipya, akaishia kugundua kuwa hata hakuna mahali maji mapya yanapotengenezwa, maji ni yale yale yanajisafisha na yapo kwenye mzunguko wake..yanaingia kwenye bahari yanarudi milimani na kutiririka tena, akaona tabu yote aliyoipata kuchunguza inamrudishia jibu lile lile kuwa hakuna jipya.
Hakuishia hapo, akaanza kuutafakari tena na upepo, akitafuta upepo, baada ya kumpuliza mtu unaenda wapi, akitazamia kugundua kuwa kuna mahali upepo mpya unajitengeneza kila siku na ule wa zamani kuna mahali unakwenda kuishia…Lakini Mwisho wa siku akagundua kuwa hakuna upepo mpya, upepo ni ule ule upo kwenye mzunguko wake. Akachukia kwasababu alitumia muda mwingi kuchunguza akitegemea kuvumbua kitu kipya ndani yake, kinyume chake alipata majibu madogo.
Ili kuuelewa vizuri uchungu wa kupoteza muda Hebu tafakari mfano huu: mtu mmoja asiyeijua Jeografia ya dunia aliamua kuanza safari ya kwenda mbali na makazi yake ili kuutafuta mwisho wa dunia, akitumaini kuwa pale upeo wa macho yake unapoishia ndio kutakuwa ni mwisho wa dunia, kwahiyo akaanza kufunga safari na kusafiri mamia ya maili huku kila siku anaongeza mamia ya maili katika safari yake, akajifariji kuwa kashafika mbali sana, hivyo akazidi kusafiri miezi na miezi na hatimaye miaka, akisema akilini mwake kuwa nataka nifike mwisho wa dunia, nitasafiri maisha yangu yote mpaka nifike mwisho wa dunia mahali atakapokuta kuna ukomo wa ardhi. Akavuka bahari na mito, na ghafla pengine baada ya miaka 50 ya safari yake anakuja kujikuta katokea tena pale pale alipoanzia safari yake….
Baadaye sana ndio anakuja kugundua kuwa dunia ni duara..utakapoanzia ndipo utakapomalizia..Unafikiri mtu huyo atajisikiaje?? Ni wazi kuwa atakasirika na kuchukia, kwasababu kapoteza miaka mingi kutafuta kitu kisichokuwa na maana, na pengine atajiona mjinga na kapoteza muda wake mwingi kwasababu alifikiri anavyozidi kusafiri ndipo anapokwenda mbali zaidi kumbe ndivyo anavyozidi kuukaribia mwanzo wake.
Ndio maana unaona katika kitabu hichi Mfalme Sulemani haanzi na salamu, wala maneno ya hekima kama alivyoanza katika mithali..badala yake anaanza kama mtu aliyeonja kitu na kukitema haraka na kusema hakifai!! hakifai!! Kimeoza!! Kimeoza kimeoza!!…na ndio tunaona anasema hapa ubatili!! Ubatili!! kila kitu ni ubatili!!…Hiyo ni sentensi ya kuwaonya wale watu ambao bado hawajaonja!! Kwamba wasijaribu kuonja! Kwasababu watakuta kitu ambacho hawajakitegemea, na mwisho wa siku watapata hasara.
Mhubiri 1: 12 “Mimi, Mhubiri, nalikuwa Mfalme wa Israeli katika Yerusalemu. 13 Nikatia moyo wangu ili kuyatafuta yote yanayotendeka chini ya mbingu, na kuyavumbua kwa hekima; ni taabu kubwa ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake. 14 Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kujilisha upepo”.
Mhubiri 1: 12 “Mimi, Mhubiri, nalikuwa Mfalme wa Israeli katika Yerusalemu.
13 Nikatia moyo wangu ili kuyatafuta yote yanayotendeka chini ya mbingu, na kuyavumbua kwa hekima; ni taabu kubwa ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake.
14 Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kujilisha upepo”.
Anatuonya sisi tulio watoto, ndugu tusisubiri tufike mwisho ndio tugundue kuwa tulikuwa tunapoteza muda. Mfalme Sulemani anatosha kutufanyia utafiti na sisi tusiurudie tena huo utafiti ambao hauna matumaini yoyote mwisho wake.
Ndugu Mwanzo wa Mwanadamu ndio Mwisho wa mwanadamu. UMETOKA KWA MUUMBA WAKO UTARUDI KWA MUUMBA WAKO. Watu wengi ambao wapo katika dhambi hawalijui hilo…hawajui maisha ni DUARA kama vile DUNIA ilivyo duara..unapoanzia ndipo utakapoishia..haijalishi utajiona umepiga hatua kiasi gani kutoka katika mwanzo wako..lakini siku moja utaparudia tu pale ulipokuwa penda usipende, Na siku hiyo utajichukia na kujiona mjinga na umepoteza muda mwingi.
Ndio maana Sulemani huyu huyu sura za mbeleni anasema “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako Mhubiri 12” ..
kwasababu siku za uzee wako ndio siku za kuurudia mwanzo wako..Usiku unavyozidi sana ndipo asubuhi inavyokaribia…
Utajiona umefanikiwa katika mambo yako, kwahiyo huna haja ya kutubu wala kumkumbuka muumba wako, utajiona umekuwa na majukumu mengi hivyo huna haja ya kulisoma Neno lake na kulitafakari, utajiona umekwenda mbali sana kiteknolojia na kisayansi hivyo mambo madogo madogo yanayohusu Imani, na wokovu hayana maana tena kwako, utajiona una afya nyingi na ulinzi mkubwa hivyo hakuna haja ya kutafuta ulinzi wa maisha yangu ya milele…Siku zinazidi tu kwenda unajishughulisha na mambo tu yasiyokuwa na maana, Lakini nataka nikuambie HAKUNA JIPYA CHINI YA JUA..ULIPOANZIA NDIPO UTAKAPOMALIZIA. Hujui kuwa Unakaribia kumaliza duara la maisha yako, kurejea mwanzoni, pasipo wewe kujijua na siku hiyo ndio utakayofahamu kuwa yote uliyokuwa unajitaabisha nayo hayana maana.
Sulemani anasema..Mkumbuke Muumba wako kabla roho yako haijamrudia yeye aliyoitoa..
Mhubiri 12: 6 “Kabla haijakatika kamba ya fedha; Au kuvunjwa bakuli la dhahabu; ……… 7 Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, NAYO ROHO KUMRUDIA MUNGU ALIYEITOA”.
⏩Anamalizia kwa kusema maneno haya..
Mhubiri 12: 8 “Mhubiri asema, Ubatili mtupu; mambo yote ni ubatili! 9 Walakini, kwa sababu huyo Mhubiri alikuwa na hekima, aliendelea kuwafundisha watu maarifa, naam, akatafakari, akatafuta-tafuta, akatunga mithali nyingi. 10 Huyo Mhubiri akatafuta-tafuta ili apate kuona maneno yapendezayo, na yale yaliyoandikwa kwa unyofu, YAANI, MANENO YA KWELI. 11 Maneno yao wenye hekima huwa mfano wa michokoo; na kama misumari iliyogongomewa sana; ndivyo yalivyo maneno yao walio wakuu wa makusanyiko, ambayo yatoka kwa mchungaji mmoja. 12 Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo; hakuna mwisho wo wote wa kutunga vitabu vingi; na kusoma sana huuchosha mwili. 13 Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; MCHE MUNGU, NAWE UZISHIKE AMRI ZAKE, MAANA KWA JUMLA NDIYO IMPASAYO MTU. 14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.
Mhubiri 12: 8 “Mhubiri asema, Ubatili mtupu; mambo yote ni ubatili!
9 Walakini, kwa sababu huyo Mhubiri alikuwa na hekima, aliendelea kuwafundisha watu maarifa, naam, akatafakari, akatafuta-tafuta, akatunga mithali nyingi.
10 Huyo Mhubiri akatafuta-tafuta ili apate kuona maneno yapendezayo, na yale yaliyoandikwa kwa unyofu, YAANI, MANENO YA KWELI.
11 Maneno yao wenye hekima huwa mfano wa michokoo; na kama misumari iliyogongomewa sana; ndivyo yalivyo maneno yao walio wakuu wa makusanyiko, ambayo yatoka kwa mchungaji mmoja.
12 Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo; hakuna mwisho wo wote wa kutunga vitabu vingi; na kusoma sana huuchosha mwili.
13 Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; MCHE MUNGU, NAWE UZISHIKE AMRI ZAKE, MAANA KWA JUMLA NDIYO IMPASAYO MTU.
14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.
Jumla ya mambo yote ndio hiyo MCHE Mungu uzishike amri zake, je! Swali linakuja unazishika amri?, je wewe ni mlevi? Mwasherati? Mshirikina? Mtazamaji pornography?, mwizi? Msengenyaji? Je ni mfanyaji masturbation?..je ni mtukanaji? Je ni mtoaji mimba? Ni msagaji au shoga?..au ni mfanyaji wa dhambi kwa siri? Watu nje wanakuona uko sawa lakini ndani yako hakufai kumeoza?.
Usisubiri mwisho wako ufike, kwasababu wengi siku ile watatazamia wafike sehemu mpya, wengine watafikiri baada ya kufa kutakuwa hakuna maisha, lakini watajikuta wamerudi pale pale kwa mwokozi wao waliomkimbia mwanzo, leo wewe usiwe mmoja wao. Kristo yupo hai , na anawapokea wenye dhambi na wote wanaomkimbilia, unachopaswa kufanya hapo ulipo ni kutenga dakika chache kutubu dhambi zako zote kwa kudhamiria kuziacha sasa angali muda upo..unadhamiria kwa vitendo kuacha ulevi, sigara, pornography, utukanaji, usengenyaji, wizi n.k, na ndipo Mungu atakapokupa NGUVU ya kuvishinda ……hapo ulipo yeye yupo haihitaji mtu akuombee, kwa Imani amini yupo hapo anakusikia..Mwambie akuoshe dhambi zako zote na yeye ni mwaminifu na si mwongo atakupokea na kukufanya mpya na kukusamehe..
Kisha baada ya kutubu nenda katafute ubatizo sahihi kama hujafanya hivyo, mahali popote karibu na wewe kumbuka ubatizo ni wa kuzamishwa mwili wote katika maji mengi na kwa Jina la YESU, na baada ya kubatizwa, Roho atafanya kazi ndani yako kwa namna isiyo ya kawaida na uwezo wa ajabu wa kushinda dhambi utashuka ndani yako, na uwezo mkubwa wa kuyaelewa maandiko utaingia ndani yako..Hapo utakuwa umezaliwa mara ya pili na kuwa na uhakika wa kuiona mbingu.
Bwana akubariki sana.
FANYA MAAMUZI KABLA HAZIJAKARIBIA SIKU ZA HATARI.
NAMNA GANI NITAPOKEA NGUVU ZA BWANA YESU?
Kwanini Bwana aliwaaita waandishi na mafarisayo wana wa majoka?, Na hao wana wa majoka kwasasa wanawawakilisha watu wa namna gani?.
Najua ulishawahi kuyasoma haya maandiko, lakini naomba usome tena kwa utulivu lipo jambo nataka ulione la tofauti naamini litakufungua macho yako na kukuponya katika uelekeo ambao pengine ulidhani upo sawa kumbe haupo sawa.
Mathayo 23:29 “Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki, 30 na kusema, KAMA SISI TUNGALIKUWAKO ZAMANI ZA “BABA ZETU”, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii. 31 Hivi mwajishuhudia wenyewe, ya kwamba ninyi ni wana wao waliowaua manabii. 32 Kijazeni basi kipimo cha baba zenu. 33 ENYI NYOKA, WANA WA MAJOKA, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum? 34 Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji; 35 hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria bin Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu. 36 Amin, nawaambieni, Mambo hayo yote yatakuja juu ya kizazi hiki.”
Mathayo 23:29 “Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki,
30 na kusema, KAMA SISI TUNGALIKUWAKO ZAMANI ZA “BABA ZETU”, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii.
31 Hivi mwajishuhudia wenyewe, ya kwamba ninyi ni wana wao waliowaua manabii.
32 Kijazeni basi kipimo cha baba zenu.
33 ENYI NYOKA, WANA WA MAJOKA, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?
34 Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji;
35 hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria bin Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu.
36 Amin, nawaambieni, Mambo hayo yote yatakuja juu ya kizazi hiki.”
Amen.
Jaribu kufikiria hawa watu kauli waliyokuwa wanaitumia siku zote za maisha yao… KAMA SISI TUNGALIKUWAKO ZAMANI ZA “BABA ZETU”, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii…
Hiyo ni uthibitisho tosha, kutuonyesha kuwa wao walikuwa sio wana wa manabii, sio uzao wa watu waliomcha Bwana, walikuwa na baba zao tofauti na wale tunaowasoma habari zao kwenye biblia, walikuwa tofauti na wakina Musa, tofauti na wakina Samweli, tofauti na wakina Eliya, tofauti na akina Daudi, tofuati na makuhani wote wa kweli wa Mungu..Tunasoma wanaafikiana kabisa na kuthibitisha kuwa kweli BABA zao walikuwa na huduma moja tu duniani nayo ni hiyo, kama sio kuwapiga watu wa Mungu, na kuwafukuza miji kwa miji basi waliwasulibisha na kuwaua hadharani.
Maneno hayo yakiwa yanatoka katika vinywa vyao kwa ujasiri, tunamwona Bwana Yesu akiwashangaa na kuwauliza,..mwajishuhudia kabisa mkisema kama “sisi tungalikuwako zamani za BABA ZETU!!!….ati nini? …BABA ZETU!!
kumbe wale ni BABA zenu??, Baba zenu nyie sio mitume na manabii waliouliwa na wale wauaji, lakini wale ndio mnaowaona kuwa ni baba zenu..Mnajishughudia kabisa kuwa nyie ni watoto wa wauaji,!! Mnajishuhudia kabisa nyie ni wana wa majoka, mnasubiri kukua mkomae kama baba zenu ili nanyi mfanye kazi zile zile walizokuwa wanazitenda baba zenu za kuwapiga manabii wa Mungu na kuwaua na kuwasulibisha… Kwasababu WANAJISHUHUDIA WENYEWE.
Lakini cha kusikitisha ni kwamba hata leo hii, katika kanisa la Mungu jambo hili hili linajirudia..Leo hii ndugu nataka nikuambie kabla haujapinga neno lolote hapa, au kutoa maneno ya kejeli naomba nikuulize swali BABA ZAKO NI WAKINA NANI?..Unajishuhudia kwa mababa wapi?..Usije ukajikuta na wewe upo miongoni wa watoto wa MAJOKA yaliyowaua mababa wa Kweli wa Mungu, ukijidanganya kuwa wewe nawe ni miongoni mwa wana wa mitume…Jitathimini.
Kabla hujafikiria kusema mimi ni mshirika wa dini Fulani, au dhehebu Fulani embu fanya utafiti kwanza, hao mababa zako au waanzilishi wao walikuwa na historia gani huko nyuma? Chimbuko lao ni lipi?.
Cha kuhuzunisha sana KANISA la kirumi ( KATOLIKI) ambalo leo hii ndio kanisa lenye washirika wengi ulimwenguni, na washirika wake na wengi wa washirika wake wanajivunia kuitwa Wakatoliki, lakini tukilitazama chimbuko lake ni la kushtusha sana, nasema tena sio kidogo, bali ni sanaa!!..Hivi karibuni viongozi wa kanisa hilo likiongozwa na PAPA kiongozi wao mkuu wanaomba msamaha kwa mauaji ya wakristo na watakatifu wengi wa Mungu zaidi ya MILIONI 68 yaliyofanywa tangu kipindi cha kanisa la kwanza hadi wakati wa matengenezo. ..
Wanakiri kuwa ni kweli “BABA” zao walifanya hivyo, na ndio maana wanawaombea msamaha, ..Ingekuwa sio baba zao wasingejisumbua kuwaombea msamaha, lakini sasa wanakiri kuwa Baba zao, ndio waliohusika na mauaji yale mabaya na ya kikatili hawakuwa mitume watakatifu wa Mungu ambao hatujawahi kuona hata siku moja katika maandiko mtume mmoja kamnyooshea mtume mwanzake kidole, sembuse kuua na kusulibisha watakatifu zaidi ya milioni 68, kama sio MAJOKA haya ni NINI tena??. Tuwe wawazi.
Na kibaya zaidi ndugu zetu wengine wasiojua historia ya kanisa vizuri, wanaungana nao na kujiita wao ni watoto wa Kanisa hilo la damu. Hawajui kuwa na wao mbele za Mungu wanaingizwa katika hatia moja na baba zao wanakuwa wana wa majoka.. Ndugu usidhani haya mambo hayafanyiki hata sasa, mimi nakueleza kitu nilichokishuhudia na kukionja mwenyewe, siongelei kidini au kishabiki, au kwa chuki, nami pia nilikuwa huko kwa neema za Bwana nikatoka..Kwa ujasiri wote nataka nikuambie Hasira ya Mungu ipo juu ya kanisa hili la uongo KATOLIKI. Ndugu tenga muda usome historia ya kanisa, usikubali tu! Kurithishwa kitu pasipo kujua asili yake..
Na ndio maana Bwana Yesu bila unafiki aliwaambia..
32 Kijazeni basi kipimo cha baba zenu. 33 Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum? 34 Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji; 35 hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria bin Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu. 36 Amin, nawaambieni, Mambo hayo yote yatakuja juu ya kizazi hiki.”
33 Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?
Usipotaka kutoka huko, katika kanisa la damu, ujue hukumu ipo juu yako, na wewe pia utakuwa umeshiriki katika kuwaangamiza watakatifu wa Mungu bila hata ya wewe kujua, wakati huo kama sio sasa, utadhani unamtolea Mungu Ibada kwa watu wa Mungu kufa, kumbe umeshakomaa katika viwango vya juu vya baba zako kwa uuaji. Usidhani utagundua, hutagundua hilo mpaka siku ile ya hukumu ndio utajua ni jinsi gani umeshiriki katika damu za watakatifu wengi.
Bwana Yesu aliwaonya mitume wake mapema akawaambia..
Yohana16 :1 ‘Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa. 2 Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada.
Yohana16 :1 ‘Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa.
2 Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada.
Lakini hilo halitadumu siku zote, wakati wao umeshawekwa tayari, wote watakuja kuangamizwa katika ile siku ya Bwana, kwa yale mapigo makuu ya mwisho yatakayoachiliwa juu ya dunia nzima.(Ufunuo 16) watapewa kwanza wainywe damu ya watakatifu waliyoimwaga tangu Habili mpaka mtakatifu wa mwisho atakayeuliwa na wao, na baadaye watauliwa na kunyokea katika lile ziwa la moto.
Na ndio maana injili tuliyonayo sasa, si tu ya kuwaambia watu watoke dhambini, bali pia ni ya kuwahubiriwa watu kutoka katika DINI ZA UONGO. Watu wasije wakafa kwa kukosa kuzijua hila za shetani.
⏩ Mwisho kabisa, sauti ya Mungu kwetu ni hii:
Ufunuo 18: 4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU, MSISHIRIKI DHAMBI ZAKE, WALA MSIPOKEE MAPIGO YAKE.15 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake’’.
Hivyo kama wewe ni mtu wa Mungu, na sio wana wa majoka yaliyohusika kuua watu wa Mungu wasio na hatia watakatifu zaidi ya milioni 68, na bado wanaendelea sasa kwa siri, na watazidi sana katika kile kipindi cha dhiki kuu,..leo hii unaisikia sauti yake ikisema na wewe na kukumwambia mwanangu TOKA HUKO!!!
Usifanye moyo wako mgumu. Ondoka! Kwa furaha zote, uipishe ghadhabu ya Mungu.
Ukiulizwa wewe ni nani, sema mimi ni Mkristo hiyo inatosha..kwasababu ndio watakatifu wa kwanza, maBABA zetu wa imani mitume na manabii walivyoitwa, na hakukuwahi kuonekana dosari yoyote ya mauaji, au ya fitina ndani yao…Hao ndio mababa wetu. Tuwafuate wao.. BIBLIA TAKATIFU NENO LA MUNGU. Haleluya!!
Lakini Hawa mababa wengine hatujui watokako, asili yao ni upande mwingine wa adui…ni maadui wa msalaba, katika mavazi ya kondoo.
Ubarikiwe.
Kwa Maombezi, Ushauri, au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba..
UZAO WA NYOKA.
MPINGA-KRISTO
NINI MAANA YA KUTOKA KATIKA MADHEHEBU?
HATUA ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTUONGOZA.
Shalom Mtu wa Mungu, karibu tujifunze Maneno ya Mungu, Uzima wetu na Taa yetu ituongozayo katika njia sahihi ya kufika mbinguni…
Sulemani Mfalme wa Israeli mwana wa Daudi, Ni mtu aliyempendeza Mungu sana hata kufikia hatua ya kuambiwa aombe lolote naye atapewa…Tunaona Mfalme akachagua kuomba Hekima badala ya Mali, na Maarifa badala ya Ufahari na nguvu za kijeshi…sio kwamba alichagua hivyo kwasababu alikuwa hapendi utajiri au ufahari, hapana alikuwa anaupenda na kuutamani, lakini alipiga hesabu awe na utajiri na nguvu za kijeshi kuliko wafalme wote duniani, halafu akose akili ya namna ya kuwaongoza na kutatua matatizo ya watu wake itamfaidia nini?..Kwahiyo akaona jambo la kwanza la kuchagua ni akili na hekima kwanza , na hayo mengine yatafuata mbele ya safari kama yatakuwa na ulazima.
Hebu leo tupewe na sisi nafasi kama hiyo, Mungu atuambie tuombe lolote naye atatupa…Utaona wengi wetu mambo tutakayoyakimbilia kwanza, tupewe mali nyingi na utajiri ili tuishi kwa raha sisi na familia zetu, na ndugu zetu na ukoo mzima…Lakini ni wachache sana watachagua Mungu awape Hekima na akili za kuwapenda wenzi wao na ndugu zao, na akili na maarifa ya kuwalea watoto wao katika njia inayopasa kutokujali kiwango cha utajiri au umaskini walichonacho…Hilo ndio lingetakiwa liwe jambo la kwanza la kuomba kisha hayo mengine ndio yafuate..
Kwasababu itakufaidia nini, uwe na fedha nyingi na utajiri mwingi na kuwatimizia watoto wako mahitaji yote na Mwisho wa siku wanakuja kuwa mashoga au makahaba? Si ni afadhali wale chakula cha kawaida kila siku lakini ni matajiri wa akili na hekima, walizozipata kutoka kwako na mwisho wa siku watakapokuja kuwa wakubwa watakuwa msaada kwako na kwa wengine?..au itakufaidia nini uwe na mali nyingi na fedha nyingi lakini mke wako au mume wako haoni raha ya kuishi na wewe?..unapata mali lakini unakosa hekima ya jinsi ya kuishi na mume/mke. Hiyo ni hatari sana…
Ndio maana biblia inasema katika Mithali 16:16 “ SI AFADHALI KUPATA HEKIMA KULIKO DHAHABU? NAAM, YAFAA KUCHAGUA UFAHAMU KULIKO FEDHA.” ..Hayo ni maneno ya mtu aliyekuwa tajiri kuliko wote duniani anakushauri hivyo, kwasababu yeye ameyapitia mengi na kuyaona mengi…Ni afadhali na Njiwa wanakaa kwenye viota vilivyotengenezwa na nyasi lakini upendo wao ni wa milele, kuliko kuishi kwenye kasri ambalo ni malumbano kutwa kuchwa.
Mhubiri 4:6 Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kujilisha upepo.
Sulemani aliliona hilo akachagua Kuwa na Hekima, ambayo hekima hiyo biblia inasema ilizidi ikapita mpaka wana wote wa Mashariki,
1 Wafalme 4: 29 ‘Mungu akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko pwani. 30 Hekima ya Sulemani ikapita hekima ya wana wote wa mashariki, na hekima zote za Misri. 31 Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote yaliyozunguka. 32 Naye akanena mifano elfu tatu, na nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano. 33 Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko Lebanoni hata hisopo umeao ukutani; pia akanena habari za wanyama, na za ndege, na vitambaavyo, na samaki. 34 Wakaja wa mataifa yote ili waisikie hekima ya Sulemani, toka wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamepata habari za hekima yake”.
1 Wafalme 4: 29 ‘Mungu akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko pwani.
30 Hekima ya Sulemani ikapita hekima ya wana wote wa mashariki, na hekima zote za Misri.
31 Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote yaliyozunguka.
32 Naye akanena mifano elfu tatu, na nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano.
33 Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko Lebanoni hata hisopo umeao ukutani; pia akanena habari za wanyama, na za ndege, na vitambaavyo, na samaki.
34 Wakaja wa mataifa yote ili waisikie hekima ya Sulemani, toka wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamepata habari za hekima yake”.
Aliona kuliko awe tajiri kama baba yake na kuwa na nguvu nyingi za kijeshi kama baba yake halafu kila kukicha ni kutokuwa na maelewano ndani ya nchi yake, kila kukicha kupambana vita na maadui zake, aliona huo ni udhaifu mkubwa sana…akamwomba Mungu ampe hekima na akili ya namna ya kutawala, na Mungu akampa…Ndio maana utaona Sulemani hakukumbana na vita yoyote kama baba yake, lakini utawala wake ulikuwa na nguvu kuliko wa Daudi baba yake..hakushika upanga kwenda vitani lakini Maadui zake walikuwa wanamwogopa. Hakumuua Goliathi kwa upanga wala kwa kombeo, lakini Wafilisti walimwogopa. Kwa ufupi hakuna mtu aliyekuwa anadhubutu kupanga vita juu ya Sulemani kwasababu walikuwa wanamwogopa na wanamheshimu. Kwa hekima yake ya kutatua mambo. Alikuwa anao uwezo wa kusulihisha mambo mengi ikiwemo vita kabla hata halijafikia katika vilele vyake, kwa hiyo hekima ambayo Mungu alimpa.
Hivyo ndivyo Sulemani alivyokuwa anatawala, na kwasababu alikuwa hapambani vita, hakutumia gharama zozote vitani, na hivyo uchumi wake ulikuwa unakuwa kwa kasi, tofauti na Baba yake Daudi au Sauli, wao kukitokea ugomvi ni rahisi kuingia kwenye mapambano pasipo mazungumzo, kwasababu walikuwa wanaamini Mungu kuwa amewapa vyote na maadui zao watakuwa chini yao siku zote, kila watakapokanyaga kama ni mapenzi ya Mungu, Mungu atawamilikisha na kweli ndivyo ilivyo, Mungu alikuwa na Daudi kila mahali alishinda vita nyingi..Lakini walitumia gharama nyingi zisizokuwa na maana na muda mwingi vitani jambo ambalo lingeweza kusulihishwa kwa njia ya hekima au akili, ndio maana unaona haikuwa hivyo kwa Sulemani, Mungu alimshindia vita Sulemani pasipo kupambana vita, alimpa Hekima kama Silaha yake badala ya mapanga na nguvu. Haleluya!!.
Ndugu Hekima ni silaha kubwa sana…Ndio maana utaona ni kwanini mtu mmoja anakaa na mke wake au mume wake mwenzi mmoja au mwaka mmoja wameachana, na mwingine hana fedha wala si tajiri lakini wameishi na mwenzi wake miaka zaidi hata ya 40 na bado wanapendana na kuvumiliana, ni kwasababu ya hekima iliyopo ndani ya hao wawili..Sio kwamba hawajawaji kukosana kabisa, wanakosana lakini kila kukitokea kutokuelewana kidogo tu! Mmoja wao anatumia hekima ya kiMungu kutatua hilo tatizo kabla hawajafika mbali kabla hawajakwenda kumwambia mama mkwe au babamkwe au marafiki, hekima iliyo ndani yao inawapeleka kwenye unyenyekevu, upendo, uvumilivu, ustaarabu, kusitiriana, kuchunguza jambo kabla ya kuchukua hatua, kujaliana, kusameheana nk.
Lakini hao wengine waliokosa hekima utaona kukitokea tatizo kidogo tu! Moja kwa moja mguu wa kwanza ni kwa marafiki na mashosti kuwaelezea kinachoendelea kati yao na wenzi wao..Na ndio huko huko shetani anapata nafasi wanapata ushauri wa kipepo wa kuachana na kuaibishana wakati mwingine, na mwisho wa siku ndoa inavunjika. Na sio tu katika Nyanja ya ndoa, bali katika Nyanja zote za maisha Hekima ni silaha kubwa.
Ndugu kama haya yanaendelea kwako, achana na hayo maombi unayoomba au unayoombewa kila siku ya mafanikio ya biashara yako na kazi yako, anza kuomba hekima..Biblia inasema..
Mithali 16:16 “ SI AFADHALI KUPATA HEKIMA KULIKO DHAHABU? NAAM, YAFAA KUCHAGUA UFAHAMU KULIKO FEDHA.”
Ukiona matatizo kama hayo yamekutokea na unashindwa namna ya kuyatatua ni dhahiri kuwa umepungukiwa hekima na sio kingine..Na kupungukiwa hekima sio dhambi, ni udhaifu tu ambao kila mtu anazaliwa nao, na hivyo unaweza ukaondoka endapo mtu akitaka uondoke!..Kwahiyo unachotakiwa kufanya ni KUOMBA HEKIMA KWA MUNGU!.
➽Yakobo 1: 15 ‘’LAKINI MTU WA KWENU AKIPUNGUKIWA NA HEKIMA, NA AOMBE DUA KWA MUNGU, AWAPAYE WOTE, KWA UKARIMU, WALA HAKEMEI; NAYE ATAPEWA.
6 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
8 Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote”.
Neno limetushauri kama tumepungukiwa na Hekima na tuombe, Sulemani aliomba hekima kwasababu aliona amepungukiwa..na sisi vivyo hivyo, tunapaswa tuombe! Kama tu nyimbo ya taifa letu TANZANIA, tunapoiimba tunamwambia Mungu aibariki nchi yetu, huku tukisema HEKIMA ni ngao yetu…yatupasaje sisi tunaoamini? Tunapaswa tuombe Ili tuongezewe hekima! Lakini tunapaswa tuombe kwa imani na pasipo kusitasita.
Sasa Maana ya kuomba kwa imani ni nini?.
Maana yake unapaswa uombe, ukiwa ndani ya IMANI ya YESU KRISTO, na ukiwa na uhakika kwamba Mungu unayemwomba anakusikia na anawapa thawabu watu wajinyenyekezao kwake!..ukiwa nje ya Imani ya Yesu Kristo ni ngumu kupokea hiyo hekima, kwasababu hiyo Hekima ndio Yesu Kristo mwenyewe. Na pia hutakiwi kusita sita..Maana ya kusitasita ni kuwa na mawazo mawili… “mawazo ya ..aa sijui itawezekana, sijui nimesikiwa?”..na mawazo ya kushika hili na lile kwa wakati mmoja!! Kwasasa lenga jambo moja tu! Kumwomba Mungu hekima, usianze kuomba; Bwana naomba hekima, unipe na utajiri nipate hela, unipe na magari matatu, nyumba, unipe maisha marefu, unipe na biashara kubwa ya kimataifa n.k
HUKO NI KUSITA-SITA KWENYE MAWAZO MAWILI na hakumpendezi Mungu, ni sawa na mwanajeshi anayekwenda vitani na kumwomba kamanda wake ampe bunduki tatu za kubeba, mabomu sita, ampe na ndege ya vita na kifaru cha kisasa, ampe na mboksi matatu ya risasi, visu ishirini, ampe na kombora moja la nyuklia..Ni wazi kuwa huyo mwanajeshi hajiamini na hafai kwenda vitani..Na sisi hatupaswi kuwa hivyo.Kusita sita kwa kushika mambo mawili kwa wakati mmoja, Tunatumia silaha MOJA YA HEKIMA KWANZA, hizo nyingine zitakuja baadaye. Kama Sulemani alivyofanya hakuanza kumwambia Mungu naomba hekima, unipe na watoto sita waje kuwa wafalme, unipe na maisha marefu, unipe na utajiri, unipe na umaarufu na ufahari dunia nzima wanijue…hapana hakufanya hivyo hakusitasita kwenye mawazo mawili aliomba jambo moja kuu kwanza HEKIMA, na hayo mengine Mungu atayafungua mbele ya safari.
Tunasoma..
1 Wafalme 3; 9 “Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi?
10 Neno hili likawa jema machoni pa Bwana, ya kuwa Sulemani ameomba neno hili. 11 Mungu akamwambia, Kwa kuwa umeomba neno hili, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho za adui zako; bali umejitakia akili za kujua kuhukumu; 12 basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe. 13 NA MAMBO YALE USIYOYAOMBA NIMEKUPA, MALI NA FAHARI, HATA HAPATAKUWA NA MTU KATIKA WAFALME KAMA WEWE, SIKU ZAKO ZOTE”.
10 Neno hili likawa jema machoni pa Bwana, ya kuwa Sulemani ameomba neno hili.
11 Mungu akamwambia, Kwa kuwa umeomba neno hili, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho za adui zako; bali umejitakia akili za kujua kuhukumu;
12 basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe.
13 NA MAMBO YALE USIYOYAOMBA NIMEKUPA, MALI NA FAHARI, HATA HAPATAKUWA NA MTU KATIKA WAFALME KAMA WEWE, SIKU ZAKO ZOTE”.
Unaona Mungu anamwambia Sulemani nimekupa HATA YALE MAMBO USIYOYAOMBA! Tatizo kubwa lililopo katika Ukristo leo hii, ni kushindwa kuelewa kuwa Mungu anajua mahitaji yetu kabla hata ya sisi kumwomba, hata pasipo kumwambia anaweza kukutimizia mahitaji yako endapo utakuwa UMESHIKA JAMBO MOJA KUU NA LA MUHIMU.
Mungu si mwanadamu, au hana udhaifu wa kibinadamu wa kusahau kuwa hitaji moja linategemea lingine, umemwomba kiatu anajua kabisa utahitaji na soksi, kwasababu huwezi kuvaa kiatu bila soksi, kwahiyo siku atakapokujibu ombi la kiatu atakupa na soksi hapo hapo..atakutengenezea na mazingira ya kupata fedha ya kwenda kukisafisha na kukipiga rangi pia… Lakini tanguliza kwanza ombi la msingi la kuomba kiatu, ili hayo mengine Bwana akuongezee.
Na leo hii shika jambo hili moja kuu na la Muhimu “HEKIMA” Itafute hiyo na hayo mengine yote utazidishiwa, mali, maisha marefu, watoto, heshima, n.k lakini la kwanza ni Hekima.
Mungu akubariki sana.Tafadhali “share” Ujumbe huu kwa wengine.
+225789001312/ +225693036618
HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?
UMEFUNULIWA AKILI?
KUNA TOFAUTI GANI KATI YA SALA NA DUA?
Ni kweli kitendo cha Kufa na kufufuka kwa Bwana Yesu kilikuwa kimeshatabiriwa hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote na kufufuka, Lakini pia tujiulize kwanini kufufuka kwake kulikawia kidogo, mpaka zikafika siku tatu, au kwanini zisiendelee na kuwa 10 au 20, kwanini ziwe ni zile tatu tu. Ndio tunaweza kusema hiyo ilikuwa ni kupisha muda wa kwenda kuzimu, lakini huko kuzimu kwanini kusingechukua siku moja au wiki, Ukweli ni kwamba siku ile ile aliyokufa, angepaswa afufuke siku hiyo hiyo, na angekuwa hajayatangua maandiko yoyote yale. Lakini kukaa kwake kaburini siku tatu, kulisababishwa na baadhi ya watu, ambao leo tutawaona, tunaweza kudhani kitendo kile ni kizuri sana kama watu wanavyodhani..Lakini nataka nikuambie ndugu tunapaswa tujitathimini sana.
Kumbuka wale watu Bwana aliokuwa nao (Wayahudi) sikuzote walikuwa ni watu wa kutokuamini, japo Mungu alijidhihirisha kwao kwa namna nyingi kwa kupitia manabii wake wengi huko nyuma lakini bado walikuwa hawataki kuamini mpaka waone ishara Fulani, sio kwamba Mungu alikuwa hawapi ishara alikuwa anawapa ishara nyingi njema lakini bado wakipewa walikuwa hawasadiki vile vile, mpaka ilipofikia wakati Mungu anakaribia kumleta Yesu duniani, Mungu aliwatangulizia Yohana mbatizaji kwanza kwa roho ya Eliya, lakini bado hawakutaka kuamini. Yaani kwa ufupi ni watu ambao walikuwa hawaeleweki wanataka kitu gani, au waone ishara ya aina gani ili waamini..Na ndio maana Bwana Yesu alisema..
Mathayo 11:16 ‘Lakini nitakifananisha na nini kizazi hiki? Kimefanana na watoto wanaokaa sokoni, wanaowaita wenzao, wakisema, 17 Tuliwapigia filimbi, wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia.18 Maana Yohanaalikuja, hali wala hanywi, wakasema, Yuna pepo. 19 Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwakazi zake. 20 Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ndani yake ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu haikutubu. 21 Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu. 22 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi. 23 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujizailiyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo. 24 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe”.
Mathayo 11:16 ‘Lakini nitakifananisha na nini kizazi hiki? Kimefanana na watoto wanaokaa sokoni, wanaowaita wenzao, wakisema,
17 Tuliwapigia filimbi, wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia.18 Maana Yohanaalikuja, hali wala hanywi, wakasema, Yuna pepo.
19 Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwakazi zake.
20 Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ndani yake ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu haikutubu.
21 Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu.
22 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi.
23 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujizailiyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo.
24 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe”.
Pamoja na Kwamba Bwana Yesu alikuwa anawafanyia miujiza mikubwa kama ile, na ishara nyingi kiasi kile, lakini bado walikuwa wanataka waonyeshwe ISHARA nyingine zitakazowashawishi wamwamini
Hilo tunalithibitisha kwenye vifungu hivi vya maandiko:
Yohana 6:30 “Wakamwambia, Unafanya ishara gani basi, ili tuione tukakuamini? Unatenda kazi gani? 31 Baba zetu waliila mana jangwani kama vile ilivyoandikwa, Aliwapa chakula cha mbinguni ili wale. 32 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Siye Musa aliyewapa chakula kile cha mbinguni, bali Baba yangu anawapa ninyi chakula cha kweli kitokacho mbinguni. 33 Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima”.
Yohana 6:30 “Wakamwambia, Unafanya ishara gani basi, ili tuione tukakuamini? Unatenda kazi gani? 31 Baba zetu waliila mana jangwani kama vile ilivyoandikwa, Aliwapa chakula cha mbinguni ili wale.
32 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Siye Musa aliyewapa chakula kile cha mbinguni, bali Baba yangu anawapa ninyi chakula cha kweli kitokacho mbinguni.
33 Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima”.
Unaona? ni watu wa kupenda ishara tu, na hata walipopewa walikuwa bado hawaamini.Jiulize dakika chache tu nyuma Yesu aliwavunjia ile mikate 5 wakala maelfu ya watu, hilo hawakuliona kama ni ishara kwao inayofanana na ile ile ya Musa..hilo hawakuliona, Watu wa namna hiyo unadhani wataonyeshwa jambo gani waridhike?
Biblia imeweka wazi kabisa Wayahudi ni watu wa kupenda Ishara, soma (1Wakorintho 1.22) kwasababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima;
Sasa mambo hayo yalipozidi Bwana hakupendezwa nao kabisa, Na ndio akawaambia maneno haya.
Luka 11:29 “Na makutano walipokuwa wakimkusanyikia, alianza kusema, Kizazi hiki ni kizazi kibaya; kinatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ILA ISHARA YA YONA. 30 Maana, kama vile Yona alivyokuwa ishara kwa Waninawi, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu kwa kizazi hiki”.
Luka 11:29 “Na makutano walipokuwa wakimkusanyikia, alianza kusema, Kizazi hiki ni kizazi kibaya; kinatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ILA ISHARA YA YONA.
30 Maana, kama vile Yona alivyokuwa ishara kwa Waninawi, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu kwa kizazi hiki”.
Sasa wakati mwingine tunapaswa tujiulize ni kwanini Bwana hakuwachagulia ishara ya aina nyingine bali ile ya Yona?, kwanini asingewapa ishara kama ya Eliya kushusha moto, au ya Joshua kusimamisha jua, bali kawapa ile ya Yona?.
Embu turudi kumchunguza Yona kidogo, kumbuka Yona hakutumwa kwenda kuwaokoa wana wa Israeli, wala hakutumwa kwenda kutoa tu unabii na kuondoka kama alivyokuwa anafanya huko nyuma katika Taifa la Israeli, hapana bali alitumwa Ninawi kwenda kutangaza hukumu. Kwamba baada ya siku 40 Ninawi inaangamizwa kama wasipotubu..Sasa Hekima ya Mungu ilivyokuwa kubwa aliruhusu Yona akengeuke, ili amezwe na Yule samaki, ili akae siku tatu usiku na mchana kwenye tumbo lile. Na siku atakapotapikwa aende kuwahadithia watu wa Ninawi mambo yote yaliyomkuta…kwamba wale watu watathimini wenyewe kama yeye kwa kosa moja tu! La kutokuisikiliza sauti ya Mungu yamemkuta hayo, itakuwaje wao ambao maisha yao yote yapo kwenye dhambi watapataje kupona kama wasipotubu?.
Unaona Vivyo hivyo Mungu aruhusu Kristo amalize siku tatu kaburi, mfano wa Yona, ili somo lieleweke vizuri, kama ISHARA kwa WAYAHUDI. Lakini onyo haliendi kwao Bali linakuja kwetu sisi watu wa mataifa. Kama vile Yona hapo mwanzo alikuwa ni nabii wa Israeli tu, lakini ili afikie mataifa ilimpasa siku tatu zipotelee kwenye tumbo la samaki. Sasa leo hii tunafurahia Yona katapikwa na Yule samaki, lakini hatufahamu ujumbe Yona anaotuletea sisi, kuwa TUTUBU, kwani baada ya siku 40 mataifa yote yataangamizwa.
Upo usemi unaosema siku za mwizi ni 40, hiyo haimaanishi kuwa ni siku 40 kweli kweli hapana, bali ni lugha tu iliyopenda kutumia neno 40 kama kiashiria cha neema. Vivyo hivyo zile siku 40 za watu wa Ninawi walizopewa watubu ndio siku 40 zetu sisi katika roho watu wa mataifa..
Injili inahubiriwa miaka 2000 sasa, unaopoona kufa kwa Yesu na kukaa kwake kaburini siku tatu unaona ISHARA GANI NZURI HIYO?, Amefufuka na kutoka Kaburini ili kukuhubiria kuwa yapo mabaya mbeleni yanakuja kama hutatubu.
Ndugu hizi ni nyakati za mwisho, UNYAKUO upo karibu sana kutokea, vile vile na maangamizi ya dunia hii yapo karibu sana kutokea Biblia imesema hivyo. Tumepewa kipindi kirefu hichi cha kutubu, tusipofanya hivyo kama unyakuo hautatukuta basi kifo ni lazima, sasa tutawezaje kupona siku ile. Tutajitetea vipi mbele za Mungu kuwa hatukuwa na muda. Na ndio maana Bwana alimalizia na kuwaambia wale watu maneno haya.
“……32 WATU WA NINAWI WATASIMAMA SIKU YA HUKUMU PAMOJA NA KIZAZI HIKI, NAO WATAKIHUKUMU KUWA NA HATIA; KWA SABABU WAO WALITUBU KWA MAHUBIRI YA YONA, NA HAPA PANA MKUBWA KULIKO YONA”.
Yona alihubiri siku tatu akaenda kukaa kule mlimani akisubiria maangamizi, lakini Sisi tumekuwa tukiisikia injili ya Yesu Kristo kila siku na bado tunaendelea kusikia injili masikioni mwetu kwa njia mbalimbali kuonyesha ni jinsi gani Kristo anavyotuhurumia tusiangamie kwa hayo mambo mabaya yanayokuja huko mbele.
Ni maombi yangu, ikiwa bado upo katika dhambi utatubu leo, kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi zako, na hakika Bwana atakupokea na kukufanya kuwa kiumbe kipya..Na ikiwa pia wokovu wako ni wa kusua sua, mguu moja huku mwingine kule, ni vizuri leo ukafanya maamuzi ya kusimama imara, Hakikisha pia baada ya kutubu kwako, tafuta mahali ukabatizwe katika ubatizo ulio sahihi wa kimaandiko kukamilisha wokovu wako. Na ubatizo sahihi ni ule wa kuzamishwa katika maji tele na uwe katika Jina la YESU KRISTO.
Nakutakia kila la heri katika safari yako ya wokovu hapa duniani. Na Bwana akubariki.
Pia kwa Maombezi, Ushauri au Ratiba za Ibada basi Wasiliana nasi kwa namba
SAUTI NYUMA YA ISHARA.
INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA
MWEZI NI ISHARA GANI KWETU?
TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.
Kuna maswali mengi tunajiuliza juu ya mwonekano wa nje wa Bwana wetu Yesu Kristo ulikuwaje! Je alikuwa ni mweupe au mweusi, je alikuwa ni mrefu au mfupi, je alikuwa ni mnene au mwembamba?, je! Alikuwa mzuri au wa kawaida?..Biblia inasema nini juu ya jambo hilo?.
Sehemu pekee tunayoweza kuisoma kwenye maandiko na kutupa walau picha ndogo ya mwonekano wake ni Isaya 53:2 Inasema: “Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; YEYE HANA UMBO WALA UZURI; NA TUMWONAPO HANA UZURI HATA TUMTAMANI”.
Mstari huo unaonyesha kuwa Bwana wetu, alikuwa ni mtu mwenye mwonekano wa kawaida sana..mtu kusema hana umbo inamaanisha kuwa ukimweka katikati ya wanaume wanaovutia unaweza ukashangaa sana, kwenye uzuri tukisema tunamweka katikati ya wenye sura nzuri (ma-handsome) yeye anaweza akawa miongoni mwa wale wa mwisho mwisho pengine,..Ni mtu ambaye mtu akipishana naye barabarani hawezi kuyateka macho yako, kama mtu wa ajabu au ageuke nyuma amtazame, alikuwa ni wa kawaida sana kimwonekano, na ndicho kilichowakuta hata watu aliokuwa nao wakati ule, japo alijulikana sana, umaarufu wake ulienea duniani kote, lakini ilikuwa bado tu ni shida watu kumkariri sura yake, kwasababu si sura ambayo huwezi ukaitilia maanani ukimwona, alikuwa ni mtu wa kawaida. Bwana Yesu hakuwa kama hao watu wanaoonekana kwenye sinema, na kwenye picha wazuri, wanavutia. Sio kwamba alikuwa ni mtu mbaya kwa sura, kwasababu hakuna mtu mbaya duniani, watu wote ni wazuri, lakini tunaweza kusema alikuwa ni mtu wa kawaida.
Unajua kama ulishawahi kugundua jambo mfano umeenda mahali tuseme kwenye ofisi Fulani, ukakutana na wanafanyakazi wa pale, ukikaa tu dakika chake kuyasoma yale mazingira utaweza kumgundua boss wao ni nani, hata kabla ya kuambiwa chochote…utamgundua pengine kwa kiti chake anachokalia, utamgundua kwa wafanyakazi jinsi wanavyomnyenyekea, au anavyowaamrisha, utamgundua hata wakati mwingine kwa mavazi yake, na utembeaji wake…Lakini kwa Bwana YESU haikuwa hivyo, alipokaa na mitume wake kwa miaka zaidi ya mitatu na nusu bado makuhani, na watu wengi walishindwa kumtambua alipoketi katikati ya makutano au wanafunzi wake. mpaka walipotaka kumkamata iliwabidi wakaombe msaada kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wake awasaidie.
Hilo tunalithibitisha siku ile Bwana aliyokuja kusalitiwa na Yuda..
Yohana 18:3 “Basi Yuda, akiisha kupokea kikosi cha askari na watumishi waliotoka kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, akaenda huko na taa na mienge na silaha. 4 Basi Yesu, hali akijua yote yatakayompata, akatokea, akawaambia, NI NANI MNAYEMTAFUTA? 5 Wao wakamjibu, Ni Yesu Mnazareti. Yesu akawaambia, NI MIMI. Yuda naye aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao. 6 Basi alipowaambia, Ni mimi, walirudi nyuma, wakaanguka chini. 7 Basi akawauliza tena, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti. 8 Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni ya kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao”.
Yohana 18:3 “Basi Yuda, akiisha kupokea kikosi cha askari na watumishi waliotoka kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, akaenda huko na taa na mienge na silaha.
4 Basi Yesu, hali akijua yote yatakayompata, akatokea, akawaambia, NI NANI MNAYEMTAFUTA?
5 Wao wakamjibu, Ni Yesu Mnazareti. Yesu akawaambia, NI MIMI. Yuda naye aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao.
6 Basi alipowaambia, Ni mimi, walirudi nyuma, wakaanguka chini.
7 Basi akawauliza tena, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti.
8 Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni ya kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao”.
Unaona?, Unaweza kudhani wale watu walikuwa wanajifanya kutokumjua, utauliza walishindwaje wakati kila siku walikuwa wanamwona Hekaluni akifundisha, lakini ni kweli ilikuwa ni ngumu kumtambua Bwana, hata wewe ungekuwepo bado ungehitaji msaada wa kusaidiwa kumtambua. Hiyo yote ni kwasababu ya mwenendo wake wa unyenyekevu, hakuwa na nguo za kipekee sana kumtofautisha na mitume wake, hakuwa mzuri wa uso zaidi ya mitume wake, hakujipiga scrabing kujionyesha kuwa yeye anatunzwa zaidi ya mitume wake, wala hakuwahi kujionyesha kuwa yeye ni mkuu zaidi ya wengine, kama ingekuwa ni hivyo wale watu wasingetumia nguvu kumtambua, lakini hawakuweza mpaka YESU alipowathibitishia mara mbili ya kuwa yeye ndiye.
Unyenyekevu wa Bwana wetu Yesu Kristo ulikuwa ni mkuu sana, na sisi tunapaswa tuuige mfano huo, unakumbuka pale alipokuwa anawatawadha wanafunzi wake miguu aliwaambia maneno haya: “Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo” (Yohana 13:13), lakini mimi mbele yenu ni kama atumikaye..nami nimewapa kielelezo kama mimi nilivyowatendea ninyi nanyi mkatende vivyo hivyo.” Akamalizia na kusema..
“MKIYAJUA HAYO HERI NINYI MKIYATENDA.”
Tusipende kuitwa wakuu, tusipende kujionyesha sisi ni tofauti na watu wengine hata kama Mungu katupa vipawa vikubwa kiasi gani, Heshima ya utumishi wako haipo katika uzuri wa sura yako ndugu mchungaji, ndugu nabii, ndugu mwalimu… heshima ya utumishi wako haipo katika mavazi unayoyabadilisha kila siku na magari na ma bodyguards, unaotembea nao na msafara au nyumba yake kama raisi. na kuwaonyesha ili watu wote wakuone..Usijidanganye ukidhani hapo ndipo umeupa heshima utumishi wako Mbele za Mungu, kama hutataka kujinyenyekeza kuna hatari mbele.
Imefikia hatua mpaka akionekana mtumishi yeyote wa Mungu anatembea kwa miguu au havai nguo zinazovutia kama watu wengine, anaonekana mlokole aliyekosa maarifa, hamjui Mungu, watu hawamsikilizi tena, Nataka nikuambie ungekuwa kipindi cha mwokozi wako wakati upo hapa duniani ungemfanyia hivyo hivyo tu. Sio kwamba na support uvaaji mbaya hapana, lakini vipo vipimo tofauti tofauti kulingana na mtu, huyu hivi Yule vile, usiutafute uzuri wa nje wa Bwana, hautaupata…kwasababu uso wake haukuwa wa umuhimu sana kwetu zaidi ya Maneno yake, ndio maana karuhusu maneno yake yahifadhiwe mpaka leo na hajaruhusu picha ya uso wake ihifadhiwe mpaka leo.
Kwahiyo ni vizuri kubadilika na kuwa kama YESU KRISTO, Tuipende kweli, tuuishi kweli na kuishika. Tukifahamu kuwa Uzima wa mtu haupo katika urembo alionao au wingi wa vitu alivyonavyo.
Na pia kama hujampa Bwana maisha yako, bado hujachelewa ni vyema ukafanya hivyo leo, saa ya wokovu ni sasa, maadamu mlango wa Neema bado haujafungwa, utafika wakati utafungwa na wengi watatamani kuingia wasiweze, hebu wewe usiwe mmoja wao, hivyo unachopaswa kufanya hapo ulipo ni kutubu kwa kudhamiria kuacha maisha yote ya nyuma ya dhambi ya uasherati, ya wizi, utukanaji, uzinzi, ulevi, uvaaji mbaya, nk na baada ya kutubu tafuta haraka sana kushiriki na wengine kanisani, ili upate kubatizwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako kama hujafanya hivyo..kumbuka ubatizo ni wa muhimu sana katika kukamilisha wokovu wako na ubatizo sahihi ni wa kuzamishwa mwili wote kwenye maji na kwa jina la Bwana Yesu Kristo (kulingana na Matendo 2:38) na Baada ya hapo Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu atakayekuongoza katika kuielewa biblia na kuijua kweli yote ya maandiko na atakayekusaidia kushinda dhambi, kwasababu kwa nguvu zako mwenyewe hutaweza kushinda dhambi hata kidogo.Kwahiyo Huu ndio wakati wa kukimbilia msalabani kwa Imanueli kusafishwa dhambi zako.
Ikiwa umebarikiwa na ujumbe huu.(naomba u – Share) kwa watumishi wengine na watu wengine nao wapone. Mungu akubariki.
Pia kwa Maombezi, Ushauri au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
MJUE SANA YESU KRISTO.
NI KWASABABU YA YESU KRISTO.
UKIAMINI NA UKIMKIRI YESU KWA KINYWA CHAKO, UTAOKOKA.
SIRI YA MUNGU.
WhatsApp
Shalom! Mtu wa Mungu karibu tujifunze Neno la Mungu, ambalo ndio Taa yetu ituongozayo uzimani.
Jinsi ufalme wa mbinguni unavyotenda kazi, kwa sehemu kubwa sana unafanana na namna ufalme wa duniani unavyotenda kazi, kwahiyo tukiulewa vizuri jinsi ufalme wa duniani unavyotenda kazi, tutauelewa pia vizuri jinsi ufalme wa mbinguni unavyofanya kazi.
Kwamfano katika ufalme wa duniani tunaona kunakuwa na wafalme, na mfalme mkuu, au kunakuwa na Raisi..Kadhalika na ufalme wa mbinguni ni hivyo hivyo, wapo wafalme na yupo mfalme wa wafalme (Yesu Kristo). Na kama vile hukumu za mwisho huwa zinapitishwa na Raisi wa hiyo nchi au Mfalme, na katika ufalme wa mbinguni ni hivyo hivyo hukumu ya Mwisho inapitishwa na Yesu Kristo aliye Mfalme wa wafalme.
Lakini pia tunaweza kujifunza katika jambo lingine linalofanyika katika ufalme wa ulimwengu huu, ambalo pia linafanyika katika ufalme wa mbinguni pasipo wengi wetu kulijua. Na jambo hilo si lingine zaidi ya UCHUMI, Yaani mzunguko wa fedha.
Kama wengi wetu tunavyojua, jamii kubwa karibia yote ya wananchi wa Taifa hili wanatafuta FEDHA, kama chombo cha kubadilishana, ili wayafikie mahitaji yao waliyotaka kwa wakati fulani, na kutimiza mipango yao, wengi wanautafuta utajiri kwa nguvu zote, ambao sio jambo baya ni jambo zuri. Na utajiri maana yake ni kuwa na fedha nyingi, kwahiyo tafsiri yake ni kwamba ni lazima mtu atafute fedha nyingi ndio awe tajiri.
Sasa FEDHA NI NINI?.. fedha ni kitu chochote ambacho kimekubaliwa na jamii husika kitumike kama chombo cha kubadilishana huduma au bidhaa,, kinaweza kuwa kuwa karatasi au safaru” na hicho kinakuwa kimepewa heshima ya kubeba THAMANI fulani, mahususi kwa ajili ya kununua kitu chenye thamani ya hiyo fedha…Hivyo Bila kuwa na fedha ni vigumu kupata huduma zile unazozihitaji.
Sasa ukichukua sarafu au NOTI labda tuseme ya shilingi elf 10 au elfu 5 , utagundua kuwa ina pande mbili, upande wa kwanza utaona ina alama fulani fulani hivi, pengine utaona picha zinazozungumzia utajiri wa nchi, au utaona kuna picha ya kiongozi wa nchi mkubwa aliyewahi kupita, au utamaduni wa nchi, na baadhi ya viishara ishara kama nembo ya taifa n.k..huo ni upande wa mbele na upande wa pili wa nyuma..utaona kuna picha za wanyama. Mambo hayo yote yanafunua kuwa fedha ina roho nyuma yake…Ukiipata katika njia sahihi itakuletea mafanikio makubwa kama inavyoonekana katika upande wa mbele, lakini pia usipoipata kwa njia halali, au ukiitumia kwa njia isiyopasa..ina roho ya unyama upande wa pili, itakuharibu badala ya kukujenga…Ndio maana unaona wengine fedha zinawashusha wengine fedha hizo hizo zinawapandisha n.k
VIvyo hivyo katika Ufalme wa mbinguni kuna UCHUMI, na pia kuna fedha..Na kila mtu ili aweze kudumu katika ufalme wa mbinguni ni lazima awe na fedha za kimbinguni, Na fedha hizo pia zipo katika mfumo wa makaratasi..NA HIZO SIO NYINGINE ZAIDI YA NENO LA MUNGU NDANI YA BIBLIA TAKATIFU. Biblia inasema Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu..(Wakolosai 3:16)..Ina maana kuwa Neno la Mungu ni kama fedha, tunapaswa tuwe nalo kwa wingi ili tuweze kujikimu na mahitaji yetu yote ya rohoni. Ukipungukiwa na Neno la Mungu basi utapungukiwa na mahitaji yote ya kiroho, hutaweza kufanya chochote katika roho ni wazi kuwa utashambuliwa na matatizo ya kila aina.
Biblia pia inasema katika Mathayo 11:12 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.”..ikiwa na maana kuwa kama vile vile fedha inavyopatikana kwa nguvu na ufalme wa mbinguni ni hivyo hivyo..Wale wote wenye utajiri wa Neno la Mungu mioyoni mwao ndio wanaoteka baraka zote za rohoni, hawababaishwi na mapepo, wachawi, hofu, mashaka au chochote kile kwasababu wameupata utajiri mioyoni mwao.
Na kama vile tulivyojifunza kuwa fedha ina pande mbili, upande mmoja unaelezea utajiri wa nchi, nembo ya nchi, shughuli za kiuchumi za nchi, na nyuso za viongozi wakubwa waliotangulia, kadhalika pia katika NOTI za kimbinguni (yaani Neno lake)..Ina pande mbili…Upande mmoja unaelezea Uzuri wa Ufalme wa mbinguni, Mbingu mpya na nchi mpya ulivyo, na pia upande huo huo wa mbele unaonyesha nyuso za viongozi wakubwa waliotangulia..Ndio maana tukisoma Biblia tunaona maisha ya Mitume na Manabii, tunaona mashujaa wa Bwana kama wakina Paulo wakiishindania Imani waliokabidhiwa watakatifu mara moja tu! Hivyo Bwana akaruhusu maisha yao yawekwe kwenye alama ya fedha ya ufalme wa mbinguni Na utaona pia Bwana wetu YESU KRISTO KAMA MFALME WA WAFALME anatokea karibia katika kila Noti, (kila kitabu katika Biblia)..oo haleluya!! Lakini pia sehemu hiyo hiyo ya mbele utaona kunakuwa na Nembo ya nchi, inayoonyesha utamaduni na miiko ya nchi, na katika Biblia (ambayo ndio noti yetu ya kimbinguni) ndani yake tunasoma namna ya kuishi kulingana na utamaduni na utaratibu wa ufalme wa mbinguni.
Lakini pia haiishii hapo, Neno la Mungu (noti ya kimbinguni) inayo upande wa nyuma pia..Ambao huo una picha za wanyama..Kuonyesha kuwa Katika maandiko matakatifu wapo wanyama pia, na kama unavyojua tabia ya wanyama..ni kurarua na kuua, hawana akili..kadhalika katika maandiko matakatifu tunaonywa kuhusu MNYAMA ATAKAYEKUJA KUTOKA BAHARINI, kuwatia CHAPA WALE WOTE, WASIOKUWA NA MUHURI WA MUNGU (soma Ufunuo 13 & 17). Ikifunua kuwa yeyote Yule atakayeupokea ufalme wa mbinguni isivyopaswa ataangamizwa, na kuraruliwa na roho ya Yule mnyama anayetoka kuzimu..Kwahiyo ni kuwa makini sana na fedha hii ya kimbinguni. Ina UTAJIRI, na BADO INA HUKUMU.
Ufunuo 13: 1 “Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru. 2 Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi. 3 Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama Yule”.
Ufunuo 13: 1 “Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.
2 Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.
3 Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama Yule”.
Ufunuo 17: 3 “Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi. 4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake. 5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI. 6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu”.
Ufunuo 17: 3 “Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.
5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu”.
Kwahiyo kwa kujifunza hayo tunaweza kuona ni jinsi gani, tunapaswa tuwe makini sana, tunapoutafuta ufalme wa mbinguni, kwamba tuutafuta kwa njia halali kama tunavyotafuta fedha, ili utupe utajiri wa rohoni, lakini tusipoutafuta kwa njia halali utatuangamiza na tutajikuta tumeangukia chini ya mikono ya Yule mnyama atokaye baharini, na huyo mnyama si mwingine zaidi ya Mpinga-Kristo, ambaye hivi karibuni atanyanyuka…naye atapewa kufanya kazi yake kuwaua wale wote watakaokataa kuipokea chapa ya mnyama. Na mnyama huyo sasa ameshaanza kufanya kazi, na anafanya kazi chini ya Kanisa la Kirumi (Kanisa Katoliki), sasahivi yupo katika hatua za mwisho mwisho kukusanya madhebebu yote na dini zote ili kuunda Umoja wa dini zote na madhehebu yote, na itafikia wakati mtu yeyote au kanisa lolote likikataaa kuwa mshirika wa umoja huo, litafutiwa usajili, na mtu yeyote atakayekataa kuwa mshirika wa umoja huo hataweza kununua wala kuuza, na hataweza kufanya kazi maana ajira zote zitataka wahusika wawe katika ushirika huo, na yeyote atakayekubali kujiunga na ushirika huo (atakuwa tayari amepokea chapa ya mnyama)..katika usahili wa kuingizwa katika umoja huo vitatumika vitu mbali mbali, kama micro-chips kuingizwa katika mwili…mfumo wa chips utatumika sana sana kwa nchi zilizoendelea, na hizo chips sasahivi zipo tayari, zinasubiri wakati tu wa kuanza kutumika.
Kwa nchi zinazoendelea, sehemu baadhi zitatumika hizo chips lakini sehemu kubwa vitatumika vitambulisho vya kawaida tu, lakini vyenye taarifa zote za dini ya mtu husika, kila mtu atalazimishwa kwenda kuhakiki upya taarifa zake za msingi, na ndani ya kuhakiki huko watalazimishwa wataje ni madhehebu yao au dini zao ambazo zipo kwenye huo umoja..Na endapo mtu atakataa au atakuwa sio mshirika wa mojawapo wa muunganiko huo, ni wazi kuwa hatapata utambulisho huo, hivyo ataonekana ni muhalifu tu! Na hataweza kusafiri wala kwenda popote pale, kazini atafukuzwa, na kadi yake ya benki na ya simu itafungiwa kwasababu hajakamilisha usajili. Jambo hilo litakapoanza dunia yote, itafurahiwa itaonekana ni mfumo mzuri mpya, lakini wengi hawatajua kuwa ndio wanapokea chapa ya mnyama hivyo. Wakati huo unyakuo utakuwa umeshapita! Na kumbuka unyakuo utakuwa ni siri sana, sio wote watajua kuwa unyakuo umepita, hakutatokea ajali mabarabarani kama inavyosemekana, zitasikika habari chache tu za chini chini kwamba baadhi ya watu wametoweka (uvumi fulani tu)…wengi hawataamini kwasababu siku hizi yapo matukio mengi ya watu kutoweka, kwahiyo wengi watajua ni kutoweka kwa kawaida tu! Hivyo watapuuzia, na haitachukuliwa kwa uzito huo.
Baada ya huyo mnyama kumaliza kazi yake ya kuwatia chapa yake wale wote walioachwa kwenye unyakuo, ataanza kuwaua wale waliokataa kusajiliwa kwenye mfumo wake, atatumia nguvu ya serikali, atahimiza serikali zote ziwatoe hao waliokataa kupokea mfumo wao na watu wengi wataonyesha ushirikiano kumpa support huyo mnyama..ndugu atamsaliti ndugu yake ili auawe..kutakuwa hakuna kujificha siku hiyo, baba utaona anamkana wazi wazi mwanae, na kusema huyu mwanangu alikataa kwenda kuhakiki taarifa zake, ana kiburi mkamateni, watakamatwa watu wengi na kupelekwa magerezani na hatimaye kwenye kambi za mateso, sasa hao ndio watasingiziwa kuwa ndio chanzo cha matatizo yote yanayotokea kwenye jamii na duniani, hata kama kulikuwa na mtu ameiba mtaa wa pili, lawama zote watatupiwa hao, wataachwa huru wale wauaji na magaidi, watawageukiwa wao, kama vile tu Yesu, alivyofunguliwa Baraba muuaji akasulibiwa yeye. watateswa mateso yasiyokuwa ya kawaida kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu..Ni matezo ambayo hajawahi wala hayataka yatokee.
Ndugu yangu, sio kipindi kizuri hicho kikukute, mimi sitaki kinikute na wewe nakuambia sasa ili nawe kisikukute, kipo karibuni sana kutokea…leo hii itii injili ya Yesu Kristo, Utafute ufalme wa mbinguni kwa bidii zote kama unavyotafuta fedha, maana mwenye nguvu ndio wanaoupata..Anza kujikusanyia utajiri wa kimbinguni kwa kujifunza na kulitii neno lake ambalo ndio Noti yetu. Ndipo utakaposalimika katika dunia hii..
Mithali 2: 1 “Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, Na kuyaweka akiba maagizo yangu; 2 Hata ukatega sikio lako kusikia hekima, Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu; 3 Naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu; 4 Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika; 5 Ndipo utakapofahamu kumcha Bwana, Na kupata kumjua Mungu. 6 Kwa kuwa Bwana huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;”
Mithali 2: 1 “Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, Na kuyaweka akiba maagizo yangu;
2 Hata ukatega sikio lako kusikia hekima, Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu;
3 Naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu;
4 Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika;
5 Ndipo utakapofahamu kumcha Bwana, Na kupata kumjua Mungu.
6 Kwa kuwa Bwana huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;”
Usisahau, noti ina pande mbili, na biblia imetupa NJIA mbili za kuchagua kufuata..NJIA YA UZIMA na NJIA YA MAUTI. (Yeremia 21: 8 Nawe waambie watu hawa, Bwana asema hivi, Tazama naweka mbele yenu njia ya uzima, na njia ya mauti).
Ni maombi yangu kuwa utachagua njia ya uzima, kama hujampa Bwana Yesu Kristo maisha yako, ndio wakati wakufanya hivyo sasa, usisubiri leo ipite, kwasababu hujui lisaa limoja mbele nini kitatokea, hapo ulipo mwambie Bwana akusamehe makosa yako yote, na mwambie hutaki tena kuishi maisha ya dhambi, na baada ya kuomba sala hiyo, dhamiria ndani ya moyo wako kuacha dhambi kweli kweli, dhamiria kuacha pombe, sigara, rushwa, uasherati, uvaaji mbaya wa vimini na suruali na mapambo ya kidunia hii, dhamiria kuacha kampani mbovu, na mambo mengine yote yasiyofaa..Ukimaanisha kutoka moyoni mwako kuacha hayo mambo, nguvu ya ajabu itashuka juu yako kukusaidia kuyashinda hayo mambo yasikurudie tena…na ukishamaliza hiyo hatua nenda mahali popote wanapoamini ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo, ubatizwe hapo, na Bwana mwenyewe atakusaidia kufanya yaliyosalia..
Bwana akubariki sana, tafadhali pia “share” kwa wengine nao waokoke.
EPUKA MUHURI WA SHETANI
ALAMA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO.
CHAPA YA MNYAMA
TUNAPOSEMA TUISHI KWA NENO, INAMAANISHA TUISHI MAISHA YA NAMNA GANI?
Shalom Mwana wa Mungu, karibu tuyatafakari maandiko na kujifunza.
Leo kwa Neema za Bwana tutajifunza, ni kwanini Mungu aruhusu katika agano la kale wana wa Israeli waoe mke zaidi ya mmoja. Huu umekuwa ni mjadala mkubwa sana, usio na mwisho miongoni mwa wakristo wengi wasio na ufunuo kamili wa Roho Mtakatifu kuhusu maandiko hayo.
Kwanza kabisa ni muhimu kufahamu kuwa Mungu hajawahi kumwagiza mtu yoyote mahali popote aoe mke zaidi ya mmoja. Hakuna mahali popote Mungu alishawahi kumpa Mwanadamu hayo maagizo…utaniuliza mbona kwenye kumbu 21:15 na kumbu 25:5 inazungumzia habari ya mtu kuwa na mke zaidi ya mmoja?. Ni kweli habari hizo zinazungumzia kuhusu kuwa na mke zaidi ya mmoja, lakini hiyo bado haimfanyi Mungu kuhalalisha mke zaidi ya mmoja..Nitakuthibitishia hilo leo kwa maandiko.
kulielewa vizuri hili suala, hebu tusome maandiko yafuatayo na kisha tuyatafakari..
Kumbukumbu 17: 14 “Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako ukaimiliki, na kukaa humo; nawe utakaposema, Nitaweka mfalme juu yangu mfano wa mataifa yote yaliyo kando-kando yangu; 15 usiache kumweka yule atakayechaguliwa na Bwana, Mungu wako, awe mfalme juu yako; umweke mmoja katika ndugu zako awe mfalme juu yako; usimtawaze mgeni juu yako, ambaye si ndugu yako. 16 Ila asifanye farasi wake kuwa wengi, wala asiwarudishe watu Misri, ili apate kufanya farasi kuwa wengi; kwa kuwa Bwana amewaambia, Tangu sasa msirudie tena njia ile. 17 Wala asijizidishie wake, ili moyo wake usikengeuke; wala asifanye fedha zake na dhahabu kuwa nyingi mno. 18 Tena na iwe, zamani aketipo juu ya kiti cha ufalme wake, ajiandikie nakala ya torati hii katika chuo, kufuata hicho kilicho mbele ya makuhani Walawi; 19 na awe nayo, asome humo siku zote atakazoishi; ili apate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wake, ayashike maneno yote ya torati hii na amri hizi, kwa kuyafanya; 20 moyo wake usije ukainuliwa juu ya ndugu zake, wala asikengeuke katika maagizo, kwa mkono wa kuume wala wa kushoto; ili apate kuzifanya siku zake kuwa nyingi katika ufalme wake, yeye na wanawe, katikati ya Israeli”.
Kumbukumbu 17: 14 “Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako ukaimiliki, na kukaa humo; nawe utakaposema, Nitaweka mfalme juu yangu mfano wa mataifa yote yaliyo kando-kando yangu;
15 usiache kumweka yule atakayechaguliwa na Bwana, Mungu wako, awe mfalme juu yako; umweke mmoja katika ndugu zako awe mfalme juu yako; usimtawaze mgeni juu yako, ambaye si ndugu yako.
16 Ila asifanye farasi wake kuwa wengi, wala asiwarudishe watu Misri, ili apate kufanya farasi kuwa wengi; kwa kuwa Bwana amewaambia, Tangu sasa msirudie tena njia ile.
17 Wala asijizidishie wake, ili moyo wake usikengeuke; wala asifanye fedha zake na dhahabu kuwa nyingi mno.
18 Tena na iwe, zamani aketipo juu ya kiti cha ufalme wake, ajiandikie nakala ya torati hii katika chuo, kufuata hicho kilicho mbele ya makuhani Walawi;
19 na awe nayo, asome humo siku zote atakazoishi; ili apate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wake, ayashike maneno yote ya torati hii na amri hizi, kwa kuyafanya;
20 moyo wake usije ukainuliwa juu ya ndugu zake, wala asikengeuke katika maagizo, kwa mkono wa kuume wala wa kushoto; ili apate kuzifanya siku zake kuwa nyingi katika ufalme wake, yeye na wanawe, katikati ya Israeli”.
Sasa ukisoma mistari hiyo kwa makini, utaona kuwa Bwana anawapa maagizo wana wa Israeli jinsi mfalme wao anavyopaswa awe siku watakapokuja kumchagua…utaona Mungu anawaambia, mfalme huyo anapaswa asiwe mtu wa kujiongezea mali nyingi wala asiwe wa kujiongezea wake..
Sasa kwa maagizo hayo haimaanishi kuwa Mungu, tayari ndio kawapa amri ya wao kuja kuwa na Mfalme, haikuwa mpango wa Mungu kabisa wana wa Israeli waje kuwa na Mfalme, kwani mfalme wao ni mmoja tu yaani YEHOVA, lakini kwasababu Mungu aliona Mbele kwamba watakuja kukengeuka na kutaka kuwa na mfalme kama mataifa mengine walivyokuwa nao ndio hapo akamwambia Musa awape maagizo ya mfalme atakavyopaswa kuja kuwa..Kwahiyo kile kitendo chao cha kuwa na tamaa ya kutaka mfalme ilikuwa ni dhambi kubwa sana, na Mungu hakupendezwa nacho. Tunasoma hayo katika…
1 Samweli 8: 4 “Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama; 5 wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; BASI, TUFANYIE MFALME ATUAMUE, MFANO WA MATAIFA YOTE. 6 Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba Bwana. 7 Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; KWA MAANA HAWAKUKUKATAA WEWE, BALI WAMENIKATAA MIMI, ILI NISIWE MFALME JUU YAO. 8 Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe”.
1 Samweli 8: 4 “Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama;
5 wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; BASI, TUFANYIE MFALME ATUAMUE, MFANO WA MATAIFA YOTE.
6 Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwomba Bwana.
7 Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; KWA MAANA HAWAKUKUKATAA WEWE, BALI WAMENIKATAA MIMI, ILI NISIWE MFALME JUU YAO.
8 Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe”.
Umeona hapo kitu Mungu anachomwambia Nabii samweli?…
“hawakukukataa wewe bali wamenikataa mimi nisiwe mfalme juu yao”….Sasa ingekuwa Mungu amehalalisha wana wa Israeli kuwa na Mfalme kule nyuma kwenye Kumbukumbu la Torati 17 …asingekasirika hapa kuona wana wa Israeli wanataka mfalme…asingelaumu, lakini badala yake unaona Mungu anachukizwa sana na kitendo hicho cha wana wa Israeli kutaka mfalme.
Umeona? Kwahiyo ni wazi kuwa kule kwenye kumbukumbu 17, Mungu alipotoa maagizo ya namna mfalme atakavyopaswa kuwa sio kwamba ndio alitoa ruhusa wana wa Israeli wawe na mfalme, badala yake ni maagizo yatakayotumika baada ya wao kukengeuka akili na kutaka mfalme..(Kwasababu ya mioyo yao kuwa migumu)
Kadhalika na katika suala la ndoa. Mungu alitoa maagizo katika agano la kale namna watakavyoishi endapo watajiongezea wake…lakini sio kwamba alitoa amri ya watu kuoa mke zaidi ya mmoja! Au kutoa talaka…Mungu hakuwahi kumwagiza mtu kufanya hivyo vitu, wala kumpa hayo maagizo…alizungumzia namna ya kuishi na mke zaidi ya mmoja ndio, na maagizo ya talaka kwasababu aliona tayari wana wa Israeli walishakengeuka na watazidi kuja kukengeuka na kuweka mioyo yao migumu na kuwa na shingo ngumu, kwa kutaka kila mtu kuwa na mke zaidi ya mmoja, na kila mtu kutaka kumwacha mkewe….na kwasababu walishamkataa Mungu katika fahamu Mungu naye akawaacha wafuate akili zao…Kama vile tu walivyomkataa Mungu asiwatawale na kujichagulia mfalme wao wenyewe, Mungu aliwaacha katika akili zao hizo. Lakini haukuwa mpango kamili wa Mungu tangu awali.
ndio maana Bwana Yesu alikuja kusema mambo hayo hayakuwa hivyo tangu mwanzo.…
Mathayo 19: 3 “Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? 4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, 5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? 6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe. 7 Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha? 8 Akawaambia, Musa, KWA SABABU YA UGUMU WA MIOYO YENU, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi”.
Mathayo 19: 3 “Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?
4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
7 Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?
8 Akawaambia, Musa, KWA SABABU YA UGUMU WA MIOYO YENU, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi”.
Kwahiyo kwa maandiko hayo yanatufundisha kuwa mke ni mmoja tu na mume ni mmoja tu! Na hairuhusiwi kumwacha mwanamke, kwasababu yoyote ile isipokuwa ya uasherati tu!..Mtu anayeoa wake wengi na bado anajiita ni mkristo, azini, asitumie kisingizio cha kuwa agano la kale liliruhusu, YESU ni mkuu kuliko nabii yoyote maandiko yanasema kuwa “katika yeye utimilifu wote wa Mungu unakaa kwa jinsi ya kimwili (Wakolosai 2:9)”.
2 Timotheo 2:15 “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.”
Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine..
Pia kwa Maombezi, Ushauri au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba hizi…..
+225693036618
+225789001312
Mada Zinazoendana
UNALITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI?.
NDOA NA TALAKA
BIBLIA INASEMA ASKOFU ANAPASWA AWE MUME WA MKE MMOJA! JE! WALE WASIOOA KWA AJILI YA INJILI HAWAWEZI KUWA MAASKOFU?
NDOA NA HARUSI TAKATIFU.
MAANA YA KUISHI NA MKE KWA AKILI.