Nini maana ya maneno haya ya Bwana? “Nami nikiinuliwa juu ya nchi,NITAWAVUTA WOTE KWANGU”(Yohana12:32).

by Admin | 1 Septemba 2019 08:46 um09

JIBU: Tunaona wana wa Israeli baada ya kumkosa Mungu kule jangwani, Bwana aliwapiga kwa pigo la nyoka wa moto, na ndipo Musa akaambiwa atengeneze nyoka wa shaba na kumwinua juu ya nchi, ili kila amtazamaye apate kupona. Sasa Bwana wetu Yesu Kristo alifananishwa na yule nyoka wa shaba juu ya ule mti, kwamba na yeye aliinuliwa juu (Pale Kalvari) ili kila amtazamaye (kwa macho ya rohoni na kumwamini) apate uzima wa milele, na ndio maana alisema katika…

Yohana 3:14 ” Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;

15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.”

Kwahiyo hapo Bwana aliposema “Nami nikiinuliwa juu ya nchi,NITAWAVUTA WOTE KWANGU” alimaanisha kuwa “baada ya kusulibiwa pale msalabani” kwa ajili ya dhambi ya ulimwengu, itaachiliwa nguvu kubwa ya watu wengi kuvutwa kwake, na ndio maana ukiendelea kusoma mstari unaofuata utaona ameweka wazi kuwa kuinuliwa kunahusu mauti ya mwili wake..

Yohana 12:32 “Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu.
33 Aliyanena hayo akionyesha ni mauti gani atakayokufa”.

Ubarikiwe.


Mada zinazoendana:

MUNGU NDIYE ANAYEISHAWISHI MIOYO.

MWINUE YESU KRISTO KATIKA MAISHA YAKO.

DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?

AYUBU 28 : HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?

MAJI YA UZIMA.

UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?


Rudi Nyumbani:

WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/09/01/nini-maana-ya-maneno-haya-ya-bwana-nami-nikiinuliwa-juu-ya-nchinitawavuta-wote-kwanguyohana1232/