Mwandishi na uchambuzi wa kitabu cha Yakobo.

Mwandishi na uchambuzi wa kitabu cha Yakobo.

Kitabu hiki kama kinavyoanza na utambulisho wake. Kiliandikwa na Yakobo aliye mtumwa wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo. (Yakobo 1:1).

Yakobo huyu sio yule mmoja wa mitume kumi na mbili wa Yesu, (yaani ndugu yake Yohana wana wa Zebedayo)..Hapana bali ni mmoja wa ndugu  za Yesu wa kunyonya aliozaliwa nao (kimwili) kupitia Mariamu. Na huyu ndiye baadaye aliyekuwa kama moja ya nguzo ya kanisa la Yerusalemu. Wengine wakiwa ni Petro na Yohana.

Inaonekana wakati Petro alipotoka na kwenda kusimamisha makanisa katika mataifa ya mbali, yeye ndiye aliyebakia kama msimamizi mkuu kwa kanisa la Yerusalemu,

Vilevile majaribu na dhiki mbalimbali zilizolikumba kanisa hili tukiachia mbali janga la njaa kubwa lililotokea wakati ule, mpaka wakapelekewa misaada kutoka kwa makanisa mengine (Matendo 11:28–30), lakini pia na dhiki walizozipata kwa wayahudi wasioamini, mtume huyu Yakobo alizifahamu sana.

Ndio maana katika sehemu kadha wa kadha za waraka huu Yakobo anayazungumzia majaribu,

Huku yeye akiyachukulia katika taswira nyingine, tofauti na kama yangepaswa kuchukuliwa, akielezea  kwamba Majaribu na dhiki, sio jambo la kukaa na kuhuzunika, kinyume chake tuyaone kama ni fursa nzuri ya sisi kuimarishwa na kuthibitishwa kiimani.

Lakini Maudhui kuu ya waraka huu, ni kueleza mahusiano kamili yaliyo katika imani, na matendo yake. Kwamba hivi vitu viwili haviwezi kutenganishwa.

Waraka huu aliuelekeza kwa wayahudi wote waliotawanyika ulimwenguni kote (kwa wakati ule). Ambao kwasasa unatuhusu sote.

Huu ndio ufupisho wake katika maeneo makuu SITA (6).

Yakobo anaeleza.

 1) Imani iliyo kamili huvumilia majaribu na dhiki (1:2-18)

  • Inapopita katika majaribu haivunjiki moyo bali hufurahi na kustahimili (1:2-4,),
  • Lakini pia hutambua kuwa chanzo cha majaribu si Mungu, bali ni tamaa za mtu mwenyewe. Hivyo asiwe na fikra kuwa Mungu anawajaribu watu kwenye dhambi (1:13-15)

 

2) Imani kamilifu huonekana katika hekima ya ki-Mungu.

  • Hekima ya ki-Mungu huwa ni safi, ya amani na upole, haiwi katika wivu, uchungu na ugomvi (3:13-17)
  • Hivyo pale tunapopungukiwa hekima tunapaswa tuombe (1:5-8),

3) Imani/Dini ya kweli huwachukulia watu kwa usawa bila kujali matabaka yao

  • Matajiri wanapaswa wasiwakandamize maskini katika kazi zao(Yakobo 5:1-6),
  • Vilevile katika kanisa kusiwe na upendeo kwa watu matajiri zaidi ya maskini (2:1-13)

4) Imani ya kweli huiweka huthibitika kwa matendo yake (1:19-2:26)

  • Tunapaswa tuwe wepesi wa kusikia, zaidi ya kuongea (1:19-20)
  • Tuzitumie ndimi zetu vema. Yatokea yaliyo sahihi tu (1:26, Yakobo 3:1-12)
  • Tusiwe msikiaji tu wa Neno bali pia mtendaji (1:21-27).Kwa kwenda kuwatazama wajane, yatima (1:26)
  • Kuonyesha kimatendo wokovu tuliopokea, vinginevyo ni imani mfu ijulikanayo kama ya mashetani (2:14-26)

5) Imani ya kweli inazalika katika kujinyenyekeza (4:1-17)

  • Kwa kukataa kuwa rafiki wa dunia, (4:1-6)
  • kwa kujisogoza karibu na Mungu, kwa maombolezo, kulia, (4:7-17)
  • Kwa kuepuka kuwahukumu wengine (4:11-12)
  • Kwa kukataa kujivunia kesho (4:13-16)

6) Imani ya kweli huthibitika katika Maombi, upendo na uvumilivu (5:1-20)

  • Kuna baraka katika kuwa wavumilivu mpaka kutokea kwake Bwana (mfano wa Ayubu 5:7-12)
  • Kuna heri kuwa waombaji wenye bidii kama Eliya (5:13-18)
  • Kuna heri kuonyesha upendo kwa waliopotea, kwasababu tunaponyeka pia sisi (5:19-20).

Kwa ufupi mtume Yakobo kwa uvuvio wa Roho alilenga kuimarisha watakatifu katika eneo la utendeaji kazi imani. Na hiyo pengine ilidhaniwa au kufikiriwa kuwa wokovu ni kuamini tu, bila kuonyesha matendo yoyote. Lakini katika waraka huu analiweka sawa kwa kuonyesha matendo na imani hivitenganiki, kama mtu akijaribu kuacha kimoja, basi ni kifo mfano wa roho na mwili visivyoweza kutenganika.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Uchambuzi na Mwandishi wa kitabu cha Wagalatia.

Fahamu Mwandishi wa kitabu cha Waebrania ni nani.

Mgawanyo wa Vitabu vya Biblia

Fahamu ni nani aliye mwandishi wa kitabu cha Mathayo.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments