Swali: Je Bwana YESU alikuwa amemfunga shetani wakati wa kuzaliwa kwake Kulingana na Mathayo 12:29?
Jibu: Turejee.
Mathayo 12:29 “Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, ASIPOMFUNGA KWANZA yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake”.
Jibu ni kwamba shetani hakuwa amefungwa wakati wa kuzaliwa Bwana YESU, na hata sasa shetani hajafungwa!, kwani Ingekuwa shetani amefungwa wakati wa kuzaliwa Bwana, basi Herode asingetafuta kumwua mtoto..
Mathayo 2:13 “Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize”.
Tukio hilo linaeleweka vizuri katika Ufunuo 12:1-6.
Vile vile Ibilisi asingesimama kumjaribu Bwana kule jangwani..
Mathayo 4:1 “Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ILI AJARIBIWE NA IBILISI. 2 Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa. 3 Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate”
Mathayo 4:1 “Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ILI AJARIBIWE NA IBILISI.
2 Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.
3 Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate”
Na ikiwa shetani amefungwa leo, maasi yasingeendelea kuwepo na maandiko yasingetuonya kuwa tusimpe nafasi..
Waefeso 4:28 “wala msimpe Ibilisi nafasi. 28 Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji”.
Waefeso 4:28 “wala msimpe Ibilisi nafasi.
28 Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji”.
Maandiko yametabiri shetani kuja kufungwa katika ule utawala wa miaka elfu wa Bwana wetu YESU hapa duniani. Na utawala huo utaanza baada ya dhiki kuu kuisha, na hukumu ya Mungu kwa mataifa kupita (Ufunuo 16), hapo ndipo utawala wa miaka elfu moja utakapoanza na shetani (pamoja na majeshi yake) kufungwa kwa kipindi hiko.
Ufunuo 20:1 “Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. 2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; 3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache”.
Ufunuo 20:1 “Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake.
2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu;
3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache”.
Kwahiyo shetani kwasasa yupo na hakuwahi kufungwa wakati wowote huko nyuma, lakini atakuja kufungwa baada ya hukumu ya Mungu kwa mataifa inayotajwa katika Ufunuo 16.
Sasa swali kama ni hivyo je! Maandiko hayo katika Mathayo 12:29 yana maana gani?….
Turejee tena..
Haya ni maneno ambayo Bwana YESU aliyasema, akifundisha nguvu iliyo kuu/kubwa inapoingia mahali basi inateka au inafunga ile nguvu iliyo dhaifu.
Na ukisoma kuanzia juu kidogo utaona ni wakati ambapo Mafarisayo walimwona akitoa pepo kwa uweza wa Mungu, lakini wakasema yeye hatoi kwa uweza wa Mungu bali kwa uwezo wa Pepo mkuu aitwaye Beelzebuli, ambaye ni shetani mwenyewe.
Na Bwana akawahoji, akiwauliza yawezekanaje Shetani amtoe shetani mwenzake?..jambo ambalo haliwezekani!, vinginevyo ufalme wa giza hauwezi kusimama, lakini kama wakiona pepo katolewa maana yake katolewa kwa uweza wa Mungu, kwasababu kamwe shetani hawezi kumtoa shetani mwenzake.
Na ili kulifanya hilo lizidi kueleweka vizuri ndipo akatoa mfano mwingine kwamba… “Awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, ASIPOMFUNGA KWANZA yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake”
Ikifunua kuwa Bwana anapotoa pepo, kwanza anauteka ule ufalme wa giza (maana yake wote unakuwa chini ya amri yake) halafu ndipo anaamrisha pepo zitoke na kwenda atakako yeye soma Mathayo 8:28-32.
Sasa kitendo cha Bwana YESU kusimama na kuamrisha, maana yake mamlaka yake ni KUU inayoteka, na kufunga, na kuhamisha.. Na mamlaka hiyo hajabaki kwake tu pake yake, bali pia amewapa na wale wote wanaomwamini na kufanya mapenzi yake, kwamba kwa jina lake wanateka, na wanafunga na kuhamisha kila falme za giza.
2Wakorintho 10:4 “(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) 5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; NA TUKITEKA NYARA KILA FIKIRA IPATE KUMTII KRISTO; 6 tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia”.
2Wakorintho 10:4 “(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; NA TUKITEKA NYARA KILA FIKIRA IPATE KUMTII KRISTO;
6 tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia”.
Kwahiyo mantiki ya Bwana YESU hapo ya KUFUNGA, haikuwa ya kumfunga shetani asiwepo duniani, bali katika kuzifunga kazi za ibilisi na majeshi yake zisisimame mbele yetu. (lakini shetani yupo, na ataendelea kuwepo na kuwasumbua wale wote wasiomwamini na kumfuata Bwana YESU), lakini walio na Bwana shetani hana nguvu juu yao.
Mathayo 18:18 “Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni”.
Je umeokoka??..Hizi ni siku za hatari na BWANA anarudi. Na shetani anajua wakati wake uliobaki ni mchache sana, hivyo anafanya kazi kwa kasi sana kusudi asiende kwenye lile ziwa la moto peke yake.
Ufunuo 12:12 “Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu”
Je bado wewe ni rafiki wa dunia?, bado ni mshabiki wa mipira, bado unacheza Kamari, bado unavaa kidunia na kuupenda ulimwengu?
1Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. 16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. 17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”
1Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Shetani anaishi wapi, Je! Amefungwa au yupo kuzimu?
MUNGU MWENYE HAKI.
NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?
USIMPE NGUVU SHETANI.
ZIFAHAMU KAZI KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.
Rudi Nyumbani
Print this post