Mkumbuke Mke wa Lutu..
Luka 17:28 “Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga;
29 lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote.
30 Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu.
31 Katika siku ile, aliye juu ya dari, na vyombo vyake vimo ndani ya nyumba, asishuke ili kuvitwaa; na kadhalika, aliye shambani asirejee nyuma.
32 MKUMBUKENI MKEWE LUTU.
33 Mtu ye yote atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza; na ye yote atakayeiangamiza ataiponya”.
Ni wazi kuwa kizazi tunachoishi kinafananishwa na kile cha Sodoma na Gomora, kadhalika kinafananishwa pia na kizazi cha Nuhu, Na ni kwanini ni hichi na sio kizazi kingine?. Ni kwasababu yale mambo yaliyokuwa yanafanyika kule wakati ule ndio yanayofanyika sasa na zaidi hata ya pale, Kumbuka Jambo kuu lililopelekea Miji ya Sodoma na Ghomora kuteketezwa ni tabia ya ulawiti na ushoga, tafsiri ya neno lenyewe Sodoma ni Ulawiti, Hivyo wakati ule hiyo roho ya kuingiliana kwa watu kinyume na maumbile ilikuwa imekithiri jambo ambalo lilianza tena kuonekana likijirudia kwa kasi sana mwanzoni mwa karne ya 20 na kuendelea mpaka sasa.
Roho hii imekithiri katika karne hizi 2 kuliko vizazi vingine vyote vya nyuma vilivyotangulia. Mpaka sasa hivi vitendo hivyo vimehalalishwa kisheria, kwamba vimepewa haki ya kuitwa ndoa kama ndoa nyingine halali, Kama Bwana Yesu alivyotabiri siku hizo watu watakuwa wakioa na kuolewa. Sasa Kuoa na kuolewa kwenyewe kunakozungumziwa hapo sio ndoa za mke na mume hapana, bali ni ndoa za mume na mume, na mke na mke. Mambo ambayo tunayaona sasahivi yakihalalishwa hata katika nyumba zinazojiita ni za ibada.
Sasa madhara ya haya mambo ni nini?
Madhara yake ni kupelekea jamii nzima kuathiriwa na adhabu hata watu wanaoonekana kutokuwa na hatia wanashiriki adhabu yao. Kwamfano tukitazama katika kipindi cha Nuhu, makosa ya wanadamu yaliwasababisha hata wanyama wasiokuwa na hatia kuangamizwa, ilisabababisha nchi na mimea isiyokuwa na hatia kuharibiwa, ilisababisha watoto wachanga wasiotenda hayo makosa kuteketezwa pia. Kadhalika na katika kipindi cha Lutu vivyo hivyo Na ndivyo itakavyotokea hata katika kizazi hiki cha siku za mwisho, wataathirika hata na watu wengine na viumbe vingine visivyokuwa na makosa (visivyostahili hayo madhara).
Lakini kabla Bwana hajaleta maangamizi huwa anatuma kwanza wajumbe wa kuwaonya watu wajitenge na kizazi hicho, Na ndio tunakuja kuona katika wakati wa Nuhu waliotii sauti ya Mungu ni watu wachache (yaani watu 8 tu! kati ya mamilioni), Kadhalika katika wakati wa Lutu waliotii ni watu 4 tu lakini Yule wanne (ambaye leo tutajifunza habari zake) alilikuja kuangamia, na kupelekea watu 3 tu kupona kati ya maelfu na mamilioni waliokuwa mijini.
Siku zote tunajua ni jambo la kawaida kwa mwanadamu kufuata au kuamini kitu kinachopendwa na watu wengi, hata kama ni cha kipuuzi kiasi gani, kikiwa kimekubaliwa na wengi basi ni rahisi kupata wafuasi wengi pasipo hata kupata ukinzani.kwamfano jamii nyingi za zamani watu walikuwa na hofu ya kumiliki televisheni katika manyumba yao wakiogopa kuwa zinaweza kuharibu maadili ya familia au jamii zao, lakini kwa jinsi zinavyozidi kuongezeka na kuaminiwa na wengi, zinakuja kuwa ni kitu cha kawaida kadri muda ulivyozidi kuendelea hata wale wachache waliokuwa wanazitilia mashaka wanaanza kuona kama ulikuwa ni ushamba kuogopa kumiliki televisheni,
Kadhalika pia zamani mtoto mdogo kumiliki simu ya mkononi wengi iliwashangaza sana, kuona kama mtoto ataharibikiwa, lakini kutokana na simu kuwa nyingi na wazazi wanaowawaruhusu wanao kuzitumi kuongezeka, inapelekea hata wale wazazi waliokuwa wanazipinga zisimilikiwe na watoto wao, wajione kama walikuwa washamba na wanahofu ya bure tu!, hii inakuja kutokana na presha ya watu wengine, hivyo husababisha yale madhara yalikuwa yanadhaniwa mwanzo kumezwa na mabadiliko ya kijamii.
Mfano mwingine ni kuwasili kwa fasheni, zamani ilikuwa mwanamke akionekana amevaa suruali alijulikana kama ni kahaba Fulani hivi, lakini kwa siku zilivyozidi kwenda na wavaaji kuongezeka, suruali zikaanza kuonekana kuwa ni kitu cha kawada sana kwa wanawake, hata wale wachache waliokuwa wanazipiga vita wanaanza kujiona kuwa walikuwa ni washamba..Na ndivyo ilivyo hata kwa ushoga, zamani ilikuwa hata kutamkwa hilo neon tu, ilikuwa ni aibu lakini leo hi kutokana na kwamba mambo haya yanazidi kuongezeka hata Eneo linalojiita la Kanisa mada hizo zinazungumziwa na kupewa kipaumbele na kuhalalishwa, limekuwa ni jambo la kawaida hata wale waliokuwa wanapinga mwanzoni, wanaanza kujiona kama walikuwa watu wa itikadi kali…Kwahiyo roho hii ya kubadilika kutokana na mikumbo ya watu wengi imeendelea mpaka sasa katika kanisa la Mungu..
Sasa mambo haya ndivyo yalivyokuwa katika zama za Lutu, Na Mungu kwa kumuhurumia Lutu na familia yake akamwambia atoke, lakini kabla ya wao kutoka walipewa nafasi ya kwenda kuwahubiria ndugu zao pia , lakini biblia inasema walionekana kama wanacheza mbele zao (mwanzo 19:24), Hivyo ikawalazimu watoke wao tu.
Tukizidi kusoma habari ile tunaona, Mkewe Lutu alikuja kugeuka nyuma na kuwa nguzo ya chumvi.
Kwanini Mke wa Lutu ageuke nyuma na anamwakilisha nani Sasa?
Mke wa Lutu anamwakilisha MKRISTO ambaye alishaokolewa huko nyuma, kumbuku Mke wa Lutu mwanzoni aliitika kabisa wito wa kutoka Sodoma, kwa kuyatambua maovu yote yaliyokuwa yanatendeka kule, kwamba wale watu walikuwa wanastahili hukumu , kwa kujua hilo aliamua kabisa kuyaacha mambo ya Sodoma na kuondoka, Lakini baadaye katikati ya safari alianza kujiona anavutiwa na mambo ya nyuma kuliko ya mbele, akianglia mbele haoni majumba, mali, wala raha, akiangalia nyuma anaona fahari, mali, starehe, karamu, mashamba, n.k. Hivyo akaanza kushawishika kidogokidogo kuyafikiria na kuyatamani aliyoyoaacha nyuma Hivyo matokeo yake akageuka, akaangamia na kuwa jiwe la chumvi.
Mke wa Lutu alidanganyika kama vile kanisa linavyodanganyika leo, pengine aliambiwa maneno haya na wale watu aliowahubiria huko nyuma;…,
aah! Ni nyie tu wanne Mungu aliowaona ndio watakatifu kuliko watu wote hapa Sodoma!, Vipi kuhusu watoto,? Unataka kusema watoto wasio na hatia Mungu atawaangamiza pia?, Na vipi kuhusu viongozi wetu wa kidini tulio nao huku, wao nao wataangamizwa, nyie ni bora kuliko wao? Na majengo yetu, na masinagogi yetu Mungu ataanzia wapi kuyaangamiza?..
Kwa kosa gani kubwa hivyo mji wote uteketezwe?..Nyie ni lazima mtakuwa mmesikia roho zidanganyazo..ambazo haziwatakii mema, zinawataka muache mali zetu mkimbilie milimani na kufa huko!…Vipi kuhusu mifugo kwani nayo imemkosea nini Mungu, hata iangamizwe? Mungu ni wa haki bwana, hawezi kufanya hivyo vitu….wapo wengi waliojaribu kama nyie wakapotea, embu tulieni hapa, muwe kama sisi acheni hizo itikadi zenu kali rudini kwenu, msije mkawa vichaa.
Ndivyo mke wa Lutu alivyodanganyika wakati akiwa katikati ya safari yake kwa kuyatafakari hayo maneno, akagundua kweli inawezekana ni upuuzi anaoufanya, kwamba hakuna kitu kama hicho, Mungu hawezi kuleta madhara kama yale kwa idadi kubwa ya watu kama ile,ni kweli vipi kuhusu mali zetu, vipi kuhusu mifugo yetu, vipi kuhusu ndugu zetu na watoto, vipi kuhusu viongozi wa kidini n.k…Kwa ushawishi mwingi kama huo Mke wa Lutu akageuka nyuma moja kwa moja na kuangamia milele.Na ndio maana Bwana alisema “Mkumbukeni mkewe Lutu”
Ulikuwa mkristo mzuri zamani ulipoamini, macho yako yalikuwa yapo mbinguni, hukujali ulimwengu unakuchukuliaje, ulijua kabisa unaishi katika siku za mwisho na siku yoyote ghadhabu ya Mungu itamwagwa juu ya nchi, ulikuwa tayari kuacha sigara, pombe, uasherati, anasa, disco, ulawiti, usagaji, pornography, mustarbation, mizaha, matusi, vimini, suruali, mapambo yote ya kikahaba n.k. na zaidi ya yote ulikuwa umeshajumuika na wenzako katika safari ya kuukimbia ulimwengu.. Lakini ulifika wakati ukaanza kuona kama safari yako ni ngumu na ni wachache tu mpo, ukaanza kukumbuka mafundisho ya ya mashetani uliyohubiriwa huko nyuma..yaliyokuwa wanakuambia: Yesu haji leo wala kesho, ukakumbuka pia mtu mmoja alishawahi kukwambia dunia haiwezi kuangamizwa Mungu hawezi kuangamiza watu wasiokuwa na hatia, hawezi kuangamiza watoto wadogo, hawezi kuteketeza viongozi wetu wa kidini, kwani ni nyie tu kikundi kichache kinachojiona kitakatifu ndio mtakao okoka,? Mungu haoni wengine? Mungu ni Mungu wa upendo, Na zaidi ya yote unaacha uzuri wako, unaacha kujipa raha kama kijana unaenda kuwa mshamba,..utakumbuka kuna mwingine alikwambia kuna watu waliopita njia kama yako na mwisho wake ukawa ni matatizo, utakumbuka kuna kiongozi wa kidini alikuambia uzichunguze hizo roho…watakambia hizo ni roho za shetani zinazowafanya mtoke katika hali ya kawaida na kuwa katika hali ya kutazamia mambo yasiyokuwepo ya uongo n.k..
Sasa hapo na wewe unashawishika na kuyatazama mambo ya nyuma, ndugu/dada usigeuka nyuma maana kabla ya kurudi nyuma utakuwa umeshakuwa JIWE LA CHUMVI. Biblia inasema.
2Petro 2: 20 “Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.
21 Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.
22 Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni”.
Ndugu yangu mkumbuke MKE WA LUTU. Kumbuka dunia ya leo hii imejaa maovu ya kila namna, hivyo usitazame wimbi la watu wengi wanafanya nini, usitazame kwasababu vijana wote wanafanya anasa na wewe ufanye, kwasababu wanawake wote wanavaa vimini na wewe uvae kwasababu watu wote wanazini na wewe uzini, Biblia ilishatabiri katika siku za mwisho watakatifu watakuwa wachache, na upendo wa wengi utapoa, kama zilivyokuwa katika siku za Nuhu na siku za Lutu, Hivyo ukiwa wewe ni mkristo na umeacha mambo ya ulimwengu huu, zidi kujitakasa, maana siku si nyingi Mungu atauteketeza huu ulimwengu kabisa na watakaopona ni watakatifu ambao watakuwa ni wachache sana, mimi na wewe tuwe miongoni mwao….
2Petro 3: 3 “Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,
4 na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.
5 Maana hufumba macho yao wasione neno hili ya kuwa zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu;
6 kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.
7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.
8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.
9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.
10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,
12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?”
Ubarikiwe.
Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine na Mungu atakubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
MAANA YA KUISHI NA MKE KWA AKILI.
TABIA YA KIPEKEE USIYOIJUA KUHUSU NENO LA MUNGU.
ULE MSALABA UNAOWEKWA KWENYE KABURI, NA ILE IBADA INAYOFANYWA VINA UMUHIMU WOWOTE KWA MKRISTO?
Neno la Mungu limefananishwa na MBEGU (Luka 8:11), na siku zote mbegu ina uhai na inapopandwa ndani ya mtu, ule uhai wake unajidhihirisha ndani ya mtu huyo kulingana na umeaji wa mbegu hiyo. Hivyo kwa jinsi ile mbegu inavyoendelea kukua ndipo tabia ya Yule mtu inavyoendelea kubadilika kidogo kidogo. Kumbuka hapo sio mtu anajibadilisha kwa jitihada zake hapana bali ni ile mbegu iliyopandwa ndani yake ndiyo inayombadilisha kutoka hatua moja hadi nyingine kulingana na ukuaje wake.
Bwana Yesu alitoa mfano huu.
Marko 4: 26 “Akasema, Ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga mbegu juu ya nchi;
27 akawa akilala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu ikamea na kukua, ASIVYOJUA YEYE.28 Maana nchi huzaa yenyewe; KWANZA JANI, tena SUKE, kisha NGANO PEVU, katika suke.
29 Hata MATUNDA yakiiva, mara atapeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika”.
Huu mfano unalinganishwa na jinsi Neno la Mungu linavyomea ndani ya mtu, kwanza linaanza kama mbegu, pale mtu anapoliruhusu lile Neno liingie ndani yake, hii inakuja kwa kutamani kujifunza kila siku Neno lile,kwa kutamani kumjua Mungu, na kujifunza maandiko, sasa kidogo kidogo, kwasababu ile mbegu imetengenezewa mazingira yanayostahili kumea yenyewe inaanza kukua taratibu taratibu pasipo hata yeye mwenye kuipanda kujijua ndio hapo unakuta mtu Yule anaanza kubadilika tabia zake na mwenendo wake, anaanza kujikuta anachukia mambo ya kidunia ambapo hapo mwanzo alikuwa hawezi, na hii haiji kwa jitihada za mtu hapana yeye mwenyewe tu anajikuta anapoteza hamu ya kufanya hivyo vitu, hapa mtu anajikuta vitu kama kiu ya sigara, pombe, uasherati, mavazi yasiyo na heshima n.k. vinakata vyenyewe, ataona tu ni kama vile kwa akili zake ameacha hayo mambo lakini hajui kuwa ni ile mbegu ambayo amekuwa akiiruhusu imee ndani yake ndiyo iliyotenda kazi ndani yake
Na kwa jinsi atakavyoendelea kuiwekea mazingira mazuri zaidi ya kukua, kwa kujifunza na kutamani kudumu zaidi katika Neno la Mungu sasa ile mbegu inageuka na kuwa JANI, hapa ni pale mtu ufahamu wake wa kumjua Mungu unaongezeka na kuwa mpana pasipo hata yeye mwenyewe kujijua kumbuka hii mbegu inachohitaji ni kuwekewa mazingira tu ya kutuzwa, kuhusu ukuaji huwa inajikuza yenyewe. Hatua hii inamfanya mtu ufahamu wake wa rohoni kuongezeka, yale mambo ambayo alikuwa hayaelewi kuhusu maandiko anaanza kuyaelewa taratibu taratibu.
Hatua inayofuata ni SUKE. Hatua hii mtu anakuwa anatoka katika ile hali ya “unyasi unaotikiswa na upepo”.
Waefeso 4: 14 “ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.
15 Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo”.
Hapa unakuwa umekomaa kutoka katika jani na kuwa suke gumu, hatua hii shetani hawezi kukuchukua tena na kila wimbi la mafundisho ya uongo kwa sababu Neno la Mungu limeshaweka mizizi migumu ndani yako. Unafika hatua ya kuwa na ujuzi wa kuitofautisha Kweli ya Neno na Uongo, kwasababu yale mafuta ya Roho yanakaa ndani yako. Mpaka hapo mtu anakuwa tayari kwa hatua inayofuata ya kuzaa matunda.
NGANO PEVU: Hii ni hatua ya kudhihirisha matunda, Hapa inatokea lile Neno lilipandwa ndani yako lenyewe linakupa uwezo wa kwenda kulipanda kwa watu wengine..na kuzaa matunda, Hapa ndipo Mungu kwa maarifa aliyoyaweka ndani ya mtu, anampa neema na uwezo wa kwenda kuwafundisha na wengine, na hii nguvu ya kufanya hivyo haiji kwa jitihada za mtu binafsi au kujilazimisha hapana bali mtu anajikuta anatamani mwenyewe kufanya hivyo kutoka ndani kwasababu ile nguvu za kuzaa matunda imeshajitengeneza ndani yake..,Ni kama tu vile mwanamke anapofikia wakati wa kuzaa, ule uchungu unapokuja hawezi kujizuia, vivyo hivyo na mtu akishafikia hatua hii, anajikuta mwenyewe anaanza kumzalia Mungu matunda.
Na hatua ya mwisho ni Mavuno: Hapa ndipo kazi ya kila mtu itavunwa na Bwana mwenyewe, na hii itakuja katika mwisho wa dunia.
Hivyo ndugu je! Ni mbegu gani imepandwa ndani yako?, Ni ya Neno la Mungu au ni ya Yule mwovu.?..Na kama ni ya Neno la Mungu, je! Mbegu hiyo imekuwa kwako katika hatua gani, ni jani?, ni suke au ni ngano?. Kama huna uwezo wa kushinda ulevi, uasherati, sigara, uzinzi, usengenyaji basi ujue ile mbegu imekufa ndani yako.. Kwasababu uliposikia Neno la Mungu hukutaka kuliwekea mazingira mazuri ya kukua lenyewe. Kumbuka mkristo yoyote anayezingatia kulitunza na kujifunza Neno la Mungu kila siku katika maisha yake, hatapata shida kuishida dhambi. Kwasababu Biblia inasema..
1Yohana 3: 9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao [MBEGU]wake wakaa ndani yake ; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.
Ni maombi yangu sisi sote tujue nguvu ya Neno la Mungu, tukijua kuwa tukilipinga Neno la Mungu ndani yetu ni kujitenga na uzima wetu wenyewe. Hivyo nakutia moyo ndugu usomaye haya usichoke kujifunza Neno la Mungu kila iitwapo leo, jifunze Biblia. Kwasababu hujui wewe lile Neno linatendaje kazi ndani yako. Wewe jifunze na kulitii tu, hata kama hutaona leo mabadiliko lakini fahamu tu, linakuwa kwa njia usioijua wewe, wakati Fulani ukipita ukiendelea hivyo utaona tofauti ya leo yako na jana yako ilivyokuwa.
Mungu akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali share ujumbe huu kwa watu wengine na Mungu atakubariki.
Mada Nyinginezo:
NENO LA MUNGU KATIKA UTIMILIFU WOTE.
ALIPO NA ATAKAPOKUWEPO BIBI-ARUSI WA YESU KRISTO.
NINI MAANA YA USIPUNGUZE WALA KUONGEZA NENO LA MUNGU?
JE! NI DHAMBI KUSHEREKEA SIKU YA KUZALIWA? BIRTHDAY!
JE! NI HALALI KWA MTU WA MUNGU KUTUMIA NJIA ZA UZAZI WA MPANGO?
Biblia inasema maisha yetu yamefananishwa na chombo chochote kinachoendeshwa chenye usukani, mfano wa vyombo hivi vinaweza vikawa ni: Gari, au Meli, au ndege, n.k. vyote hivi pamoja na kwamba vina uwezo mkubwa na nguvu nyingi ya utendaji kazi, lakini haviwezi kujiongoza vyenyewe pasipo USUKANI. Upepo unaweza ukawa mkubwa sana baharini na usifanikiwe kukipeleka chombo mahali kinapotakiwa kufika lakini usukani ni kitu kidogo chenye nguvu chache tu na kikafanikiwa kupindisha merikebu yote na kuielekeza inapotakiwa iende.
Kadhalika na maisha yetu ya Kikristo yanayo usukani wake, Na usukani huo ni nini? Tukisoma biblia tutapata majibu yote:
Yakobo 3: 2-12, Biblia inasema..
“Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.
3 Angalieni, twatia lijamu katika vinywa vya farasi, ili wamtii, hivi twageuza mwili wao wote.
4 Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote anakoazimia kwenda nahodha.
5 Vivyo hivyo ULIMI nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
6 NAO ULIMI NI MOTO; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum.
7 Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu.
8 Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.
9 Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.
10 Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.
11 Je! Chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu?
12 Ndugu zangu, Je! Mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na maji matamu “.
Maandiko hayo yanaonyesha wazi kabisa kuwa usukani wa maisha yetu ni ULIMI. Na ulimi kama usukani ni wa kuuchunga sana kuliko vyote kwasababu Shetani akipata tu nafasi ya kuushika huo ataleta maangamizi makubwa kuliko hata angetumia njia nyingine za nje za dhoruba na tufani (ambayo ni majaribu).
Biblia inatuonya mtu anaweza akawa umezingatia kweli kuwa na Dini nzuri, kama kusaidia wajane, kutembelea yatima, kuvaa vizuri, kuzingatia ibada, kutoa sadaka, kufundisha watu,n.k (Yakobo 1:27). lakini kama hakuweza kuungoza usukani wake (Ulimi) basi dini yake yote na matendo yake mema mtu huyo yote yanakuwa ni sawa na bure. Soma.
Yakobo 1: 26 “ Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai. ”
Wewe ni mkristo lakini unakuwa mtu wa kusengenya, kila wakati kuzungumzia watu wengine kwa ubaya, kuchukua taarifa za mtu fulani kupeleka kwa mtu fulani, kutoa siri za mtu fulani na kumfunulia mwingine..Kila wakati unakuwa unatoa maneno yasiyokuwa na maana mdomoni, unatoa maneno ya mizaha ambayo ni aibu hata kwa mkristo kutamka, unatoa maneno ya uchochezi na fitna, unatamka matusi hata haionekani tofauti yako na mtu asiyeamini, kila wakati kuchangia mada zisizokuwa na maana, Sasa hapo hata kama unafanya ibada nzuri kiasi gani mbele za Mungu, au unahubiri kiasi gani, au unasaidia maskini kiasi gani, Dini yako ni bure mbele za Mungu..Ni kwasababu gani?..ni kwasababu Umeshindwa kuutawala usukani wa maisha yako ya kikristo, na umempa mwingine autawale naye ni shetani.
Wakati mwingine ajali nyingi zinazotokea huwa hazisababishwi na mazingira ya nje hapana!, unakuta nyingi zinasababishwa na matatizo ya kiuendeshaji (usukani) . Utakuta chombo ni kizuri tu, hakina matatizo yoyote, ni kipya, na kina uwezo mkubwa wa kupambana na mazingira mabaya ya nje, lakini kwa jambo dogo tu la uzembe katika uendeshaji inapelekea chombo kile kizima kupata ajali. Na ndicho hicho shetani anachokitafuta kwa wakristo, kukimbilia usukuni wa maisha yao (ULIMI) na akiupata huo kammaliza mtu huyo moja kwa moja.
Ndio hapo unajiuliza mbona najitahidi kusali, wakati mwingine kufunga, kutoa sadaka, kusaidia watu, kuhudhuria ibada, lakini siku yangu inakuwa mbaya, mbaya, sina amani na watu, sioni raha ya maisha, ni kwasababu kuna eneo moja la muhimu umemwachia shetani alitawale, usukani wako (Ulimi wako), shetani anapeleka maisha yako uliyoyajenga ya kikristo mahali anapotaka yeye,…Na ndio maana biblia inasema:
1Petro 3: 10 “Kwa maana, ATAKAYE KUPENDA MAISHA, NA KUONA SIKU NJEMA, AUZUIE ULIMI WAKE USINENE MABAYA, NA MIDOMO YAKE ISISEME HILA.
11 Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana.
12 Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya”.
Unaona hapo?. Shetani anaamka asubuhi kuziloga siku zako kwa kutumia ulimi wako mwenyewe, Mungu amekusudia kukumulikia jua lake la mema lakini anapokuja na kukukuta unamzungumzia ndugu yako vibaya, unamsengenya, anapokuja anakukuta unazungumza maneno ya mizaha, kinywa chako kinaimba nyimbo za kidunia, una laani watu, unawalaumu watu kila wakati,ukikwazwa kidogo tu basi unatoa maneno mengi na yasiyolingana na wokovu, basi na zile Baraka zako zinatoweka, mwisho wa siku, unajikuta mambo yako hayaendi sawa.
Mithali 10: 19 “Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili”.
Na pia inasema..
Mithali 21: 23 “ Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, Atajilinda nafsi yake na taabu. ”
Na njia pekee ya kuulinda ulimi wako haiji kwa kufunga na kuomba au kwa kuombewa na mtumishi, hapana! inakuja kwa kujizoesha maisha kuwa mbali na hayo mambo, unapoona kuna mazingira yoyote yanayokushawishi wewe kuzungumza maneno yasiyofaa au habari za mtu mwingine, suluhisho pekee ni kuyakataa hayo mazingira, ikiwa ni mtu anakuletea, habari hizo wewe zigeuze kumzungumzia kwa wema Yule mtu,..Ukiletewa mabaya ya mtu Fulani, wewe likumbuke lile moja jema ambalo mtu huyo alishawahi kulitenda na kulizungumzia hilo na yale tisini na tisa mabaya aliyoyatenda yapuuzie..Kwa kufanya hivyo utajikuta unabariki badala ya kulaani, unasifia badala ya kulaumu, unampenda badala ya kumchukia, unamfaurahia badala ya kumwonea wivu. Na ule uovu wote shetani alioupanga juu ya siku yako na maisha yako unayeyuka, Na kwa kufanya hivyo Mungu atakuona na kukuangazia siku zako na kuwa njema kwasababu umeweza kuutawala usukani wako.
Mithali 26: 20 “ Moto hufa kwa kukosa kuni; Na bila mchongezi fitina hukoma. ”..
Hivyo ndugu, huu ni wakati wa kuizoeza chemchemi yako kutoka maji matamu na sio machungu, kutoka Baraka na sio laana kwa faida zetu wenyewe, kwasababu kipimo kile kile tunachowapimia wengine biblia inasema ndio hicho hicho tutakachopimiwa. Baraka zile zile tutakazowabariki wengine ndio hizo hizo tutakazobarikiwa..kadhalika na laani zile zile tutakazowapimia wengine ndizo hizo hizo tukazopimiwa.
Mithali 18: 21 “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake. “
Swali ni je! Unapenda maisha na kuiona siku njema?? Kama ni ndio basi UZUIE ULIMI WAKO USISEME MABAYA …Na Bwana atakusaidia.
Zaburi 141: 3 Ee Bwana, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.
Bwana Yesu akubariki sana.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali share kwa marafiki zako ujumbe huu, na Mungu atakubariki.
Mada Nyinginezo:
MWISHO WA HAO WAMSAHAUO MUNGU.
ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!
JE! KUFANYA MASTURBATION (PUNYETO) NI DHAMBI?
Asante kwa kutembelea Tovuti yetu, Maono yetu makuu ni kuisambaza injili ya Bwana wetu Yesu Kristo ili wokovu uwafikie watu wote ulimwenguni kote, sambamba na hilo tumelenga kutoa maarifa ya Neno la Mungu, kufuatana na mada mbalimbali katika biblia.
Kwa mchango wako, utawezesha kazi hii ya Bwana kuendelea mbele, na tunachoamini ni kuwa mmoja hupanda mwingine hutia maji, lakini mkuzaji ni Mungu. Hivyo kwa matunda yazaliwayo kwa kupitia huduma hii, thawabu yetu ni moja mbinguni.
Waweza changia kupitia namba hizi:
Au
Bwana akubariki.
baruapepe(email) >> Info@wingulamashahidi.org
Shalom!
Makanisa yanayohubiri injili ya mafanikio tu. Na kukwambia kuwa uthibitisho wa Mungu kuwa yupo na wewe, ni kuwa tajiri ...JIHADHARI NA HILO KANISA!
Makanisa yasiyohubiri toba ya msamaha na kuwafanya watu wajione ni kawaida kuishi na dhambi zao…JIHADHARI NA HILO KANISA!..Toba na msamaha ndio kiini cha Imani.
Makanisa yanayochanganya NENO la Mungu na siasa na vikundi vya kijamii, jambo ambalo huwezi kutofautisha jukwaa la siasa na kanisa, na makanisa yanayochanganya Neno la Mungu na mapokeo ya wanadamu….JIHADHARI SANA!
Makanisa yasiyohubiri utakatifu na kufundisha watu ukweli kulingana na Biblia…KUWA MWANGALIFU NA HILO KANISA..
Makanisa yanayohubiri ujumbe wa kutoa tu, na kuacha mafundisho ya adili kama upendo, utakatifu na imani,,,,JIHADHARI NA HILO KANISA KWA USALAMA WA MAISHA YAKO YA MILELE.
Kanisa lisilokufundisha wala kugusia kujiandaa kwenda katika unyakuo…KUWA MAKINI!
Kanisa lisiloruhusu karama za Roho kufanya kazi, kama uponyaji wa kiungu, unabii, lugha, miujiza n.k. jua hilo kanisa limekufa au lipo karibuni kufa. JIHADHARI NDUGU!
Mada zinazoendana:
Mada Nyinginezo:
USIACHE KUJIFUNZA NENO LA MUNGU
KWANINI MUNGU ANAMPA NABII HOSEA MAAGIZO YA KUMUOA MWANAMKE KAHABA? (HOSEA 3)
Tangu kipindi cha Bwana Wetu Yesu Kristo kuondoka duniani mpaka sasa imepita miaka takribani elfu mbili na katika hichi kipindi cha miaka hii elfu mbili kanisa limekuwa likipitia katika vipindi tofauti tofauti saba vinavyoitwa NYAKATI SABA ZA KANISA, kulingana na kitabu cha..
Ufunuo 1:12-20″ Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu;
13 na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.
14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto;
15 na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.
16 Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking’aa kwa nguvu zake.
17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
19 Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.
20 Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.
Ufunuo huu alipewa Yohana na Bwana Yesu alipokuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, akionyeshwa jinsi kanisa litakavyokuja kupitia katika siku za mwisho. Leo hii si rahisi sana kuona kitabu cha ufunuo kikiguswa au kuelezewa katika kanisa, na shetani hataki watu wafahamu siri zilizoandikwa katika hiki kitabu maana ndio kinaelezea hatma ya mambo yote ikiwemo na shetani mwenyewe. Kwahiyo ndugu fungua moyo wako ujifunze na Mungu akusaidie unapoenda kusoma ujue ni wakati gani tunaishi na jinsi Bwana Yesu alivyo mlangoni kurudi kuliko hata unavyoweza kufikiri.
Kanisa: Efeso
kipindi cha kanisa: 53AD -170AD
Tabia ya kanisa: limeacha upendo wake wa kwanza,tangu wakati wa mauaji ya wakristo yaliyoongozwa na Nero mtawala wa Rumi hadi kifo cha mtume Yohana. Na kipindi hiki ndipo matendo ya wanikolai yalianza kuingia katika kanisa (mafundisho ya kipagani). kuanza kujichanga na ukristo. ufunuo 2:1-7
onyo kwa kanisa- litubu lirudi katika upendo wake wa kwanza, lililopoteza.
Thawabu: Yeye ashindaye atapewa kula matunda ya mti wa uzima ulio katika bustani ya Mungu.
NYAKATI YA PILI;
Kanisa; Smirna
kipindi cha kanisa: 170AD -312 AD
Tabia ya kanisa; Ni kanisa lilopitia dhiki nyingi kutoka katika utawala mkali wa Diocletian wa Rumi , watakatifu wengi waliuawa katika hichi kipindi kuliko kipindi chochote katika historia ya kanisa.walichinjwa wengi, na wengine kutupwa kwenye matundu ya simba na wanawake kukatwa matiti na kuachwa mbwa walambe damu zao, na ukatili mwingi sana wakristo walitendewa katika hichi kipindi lakini walistahimili dhiki zote hizi soma kitabu cha (Foxe’s book of Martyr- kwenye archives zetu kinaelezea vizuri mauaji ya wakristo).
Japo wakristo walikuwa maskini sana Lakini Kristo aliwafariji kuwa wao ni Matajiri. ufunuo 2:8-11
Thawabu; Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.
Kanisa ; Pergamo
Kipindi; 312AD -606AD
Tabia ya kanisa; Kanisa laingiliwa na mafundisho ya uongo zaidi, ambayo ndio yale matendo ya wanikolai sasa wakati huu yamegeuka kuwa mafundisho ya kidini. Ukristo ukaoana na upagani ukazaa Kanisa mama mfu Katoliki, katika baraza la Nikea AD 325 siasa na mafundisho ya miungu mitatu,ibada za sanamu na za wafu,sherehe na sikukuu za kipagani, ubatizo wa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, vyeo vya upapa n.k ndipo vilipochipukia. kwa mambo haya basi ikasababisha kanisa kuingia katika kipindi kirefu cha giza (Dark age). Ufunuo 2:12-17
Onyo kwa kanisa: litubu lirudi katika imani iliyoanzishwa na mitume wa Kristo
Thawabu; Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, ila yeye anayelipokea.
Kanisa; Thiatira
Kipindi; 606AD -1520AD
Tabia ya kanisa; Japo kanisa lilikuwa na juhudi na bidii katika kumtafuta Mungu, lakini bado lilikuwa na mafundisho ya yule mwanamke kahaba Yezebeli yaani mafundisho ya Kanisa Katoliki.
Onyo; Litubu litoke katika mafundisho ya wanikolai. Ufunuo 2:18-29
Thawabu: Yeye ashindaye na kuyatunza matendo yangu hata mwisho nitampa mamlaka juu ya mataifa, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma.
Kanisa; Sardi
kipindi; 1520AD -1750AD
Tabia; Ni kanisa lililokuwa linarudi katika matengenezo kutoka katika mafundisho ya yule kahaba mkuu kanisa katoliki. lakini lilikuwa bado na Jina lililokufa, wakishikilia baadhi ya mafundisho ya kanisa mama katoliki, huku ndiko chimbuko la walutheri lilipoanzia.Ufunuo 3:1-6
Onyo: litubu, lirejee kwenye mafundisho ya mitume.
Thawabu; Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri Jina lake mbele za baba yangu na mbele ya malaika zake.
NYAKATI YA SITA;
Kanisa;Filadelfia
Kipindi; 1750AD -1906AD
Tabia; Ni kanisa lililosifiwa kwa matendo yake mema, lilifanikiwa kujua na kuyarekebisha mafundisho ya uongo Kristo alisema ”tazama nakupa walio wa sinagogi la shetani wasemao kwamba ni wayahudi nao sio, bali wasema uongo, tazama nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda”.ufunuo 3:7-13
Thawabu;Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu, huo Yesalemu mpya ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe lile jipya.
Kanisa; Laodikia
Kipindi;1906- Unyakuo
Tabia; Ni kanisa ambalo sio baridi wala moto, bali ni vuguvugu, Kristo anasema ni heri lingekuwa moto au baridi, hii ndiyo hali ya kanisa tunaloishi sasa mimi na wewe, uvuguvugu mbaya umeingia katika kanisa, watu wanajiona kuwa wanamwabudu Mungu katika uzuri wao wa majengo ya kanisa, kwaya.na injili ya mafanikio, wakidhani kuwa hivyo yatosha tu kumjua Mungu kumbe hawajui wameshaingia katika udanganyifu wa shetani pasipo wao kujua,
Watu wanasema kuwa wanampenda Mungu na bado wanapenda mambo ya ulimwengu huu kama fashion za mitindo ya kisasa wanawake kuvalia mavazi ya nusu uchi, michezo, miziki, muvi, ponography, ulevi. anasa,uasherati,na shughuli za ulimwengu huu ambazo zinawasonga wengi hususani kwa kizazi hichi cha ubize, watu wanapata muda wa kufanya kazi sana, lakini muda wa kumtolea Mungu hawana na bado ni wakristo., huu ndio uvuguvugu Kristo anaouzungumzia kwa kanisa letu la Laodikia.Hapa Kristo anasema unajiona kuwa tajiri kumbe ni maskini na mnyonge na uchi na unamashaka na kipofu, jiulize ni hali gani ya kanisa tulilopo sasa.
Na hakutakuwa na kanisa lingine baada ya hili, na ndio linakaribia kuisha. jiulize umejiwekaje tayari kumpokea Bwana Yesu akirudi mara ya pili?
Thawabu;Yeye ashindaye nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na baba yangu katika kiti chake cha enzi. ufunuo 3:14-22
Watu wa Mungu hili ndilo kanisa la mwisho tunaloishi hakutakuwa na kanisa lingine baada ya hapa, tunaishi katika wakati ambao Kristo yupo mlangoni kulichukua kanisa lake teule, JIULIZE! UMEKWISHA KUJIWEKA TAYARI KUMLAKI BWANA, TAA YAKO INAWAKA??UMEMPOKEA ROHO MTAKATIFU??YEYE ALIYE NA SIKIO, NA ALISIKIE NENO HILI AMBALO ROHO AYAAMBIA MAKANISA.
Mungu akubariki
MARAN ATHA!
Mada zinazoendana:
Mada Nyinginezo:
ROHO SABA ZA MUNGU NI ZIPI? NA JE ZINATOFAUTIANA NA ROHO MTAKATIFU?
HUYU AZAZELI NI NANI TUNAYEMSOMA KATIKA(WALAWI 16:8)?
Papa kiongozi wa kanisa katoliki duniani alipokuwa akihutubia mbele ya maelfu ya watu juni 25, 2014 St. Peter’s Square vatican akisema:
Mafundisho haya yanapingana na biblia ni mafundisho ya mpinga kristo,kulingana na ufunuo 17:5..”katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa kwa siri, BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI” katika maandiko mwanamke anawakilisha kanisa,kwa hiyo mwanamke huyu aliyezungumziwa hapa ni kanisa-kahaba,inamaanisha ni kanisa lililochanganya mafundisho ya neno la Mungu na ibada za sanamu hivyo limemwacha Mungu na kumwabudu shetani ndio maana likafananishwa na mwanamke kahaba na kanisa hili sio lingine zaidi ya kanisa katoliki,
hivyo basi tunaona hapa sio tu kahaba bali pia ni mama wa makahaba,amezaa mabinti ambao ni makahaba kama yeye, nao ni madhehebu yote na mashirika yote ya dini yaliyoiacha kweli ya neno la Mungu na kugeukia mafundisho kama ya mama yao ya kipagani.Leo hii tunaona makanisa yote ulimwenguni yanaungana na kanisa mama yaani katoliki, na kuiunda ile CHAPA YA MNYAMA,ambayo pasipo hiyo huwezi kuuza wala kununua katika kile kipindi cha dhiki kuu,itafika wakati kila mkristo itampasa asajiliwe katika dhehebu lake kwa yeye kutambulika kama ni mkristo vinginevyo hautaweza kuuza wala kununua wala kuajiriwa,wala kufanya kazi yeyote usipokuwa na hiyo chapa ya mnyama ambayo ni..(utambulisho wako wa kidini au dhehebu lako) pia hautaruhusiwa kuabudu kwa uhuru kama unavyoabudu leo,..kwa yeyote atakayekaidi amri hiyo ataingia katika ile dhiki kuu.
Na kwa jinsi tunavyoiona dunia ya leo vitendo vya ugaidi vimekithiri kutokana na itikadi kali za kidini, shetani ameunyanyua uislamu kuvuruga amani ya dunia kwa kigezo cha itikadi kali za dini,hivyo basi leo dunia inatafuta mtu wa kuleta amani naye ni lazima awe mtu wa dini ili amalize hili tatazo. na yupo mmoja tu duniani sasa anayekubalika na dini zote naye ni PAPA ambaye anajulikana kama mtu wa amani (man of peace) kiongozi wa kanisa katoliki, baadaye atapewa nguvu na dunia ili maandiko ya daniel 11:21 yatimie “Kisha badala yake atasimama mmoja, mtu astahiliye kudharauliwa, ambaye hawakumpa heshima ya ufalme; naye atakuja wakati wa amani, naye ataupata ufalme kwa kujipendekeza”, ataleta ustaarabu mpya wa dunia wa kuleta amani (NEW WORLD ORDER).
Hapo ndipo itakapompasa kila mtu asajiliwe kulingana na shirika lake la dini na dhehebu lake, kwa dhumuni la kuwatambua watu wote, na kukomesha ugaidi, wengi wataliona kuwa ni jambo zuri bila kujua kuwa ndio wanaipokea ile chapa ya mnyama, lakini baadhi ya wale wakristo waliobaki wasiokwenda katika unyakuo hawatakubali kusajiliwa katika madhehebu ya dini, kwasababu watajua kuwa hiyo ndio ile chapa ya mnyama 666 ndani yake, ni hao tu watakao pitia dhiki kuu wakisingiziwa kuwa wao ndio waondoa amani na magaidi, kwa kutokutaka kusajiliwa kwenye dini zao, watakataliwa na watu wote, hawataweza kuuza wala kununua wala kuajiriwa mahali popote, na mwishoni yule mnyama atawauwa wote akiwa na roho ya mpingakristo
Mkristo leo hii anayedai kutafuta uhusiano binafsi na Mungu kulingana na papa alivyosema ni “hatari na yenye madhara” hii ni roho ya mpinga Kristo inatenda kazi ndani ya papa ikizungumza maneno haya ya makufuru…dhumuni kubwa ni kuizuia Roho ya Mungu ndani ya watu kutenda kazi kwa sababu Roho ya Mungu aliachiwa kwa dhumuni moja tu kutuongoza katika kuijua kweli yote.. na pia yeremia 31:34..” Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana;….
Mtu ataijua kweli tu akiwa na Roho Mtakatifu na wala sio kwa kuwa mshirika wa kanisa lolote…biblia inasema warumi 8:9 “..lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo huyo sio wake.”….warumi 8:14..”kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu” …na wala sio wanaoongozwa na kanisa.
(yohana 14:6 inasema “mimi ndimi njia na kweli na uzima mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi.” hivyo basi hatumfikii Baba kwa njia ya kanisa lolote,wala kwa njia ya kiongozi yoyote wa dini, wala kwa njia ya papa,wala kwa ukatoliki,wala kwa uanglikana,ulutheri,upentekoste,usabato, u-endtime,ubranhamite n.k
Ukweli ni kwamba KUTOKUWA NA MAHUSIANO BINAFSI NA YESU KRISTO NI HATARI NA YENYE MADHARA MAKUBWA…..
MARAN ATHA!
Mada zinazoendana:
Mada Nyinginezo:
UTENDAJI KAZI WA MPINGA-KRISTO.
Bwana wetu Yesu Kristo alipokuwa hapa duniani, huduma yake iligawanyika katika sehemu kuu tatu.
Ya kwanza: huduma ya uponyaji, ishara na miujiza
Ya pili: kueleza siri za mioyo ya watu, kama vile kwa yule mwanamke msamaria,
Ya tatu: kuhubiri neno la Baba yake.
ndugu William Branham alifundishwa na malaika wa Bwana jinsi ya kuvua samaki WAKUBWA kutoka kwenye maji, na yule malaika alimwambia ni kwa namna hiyo hiyo Bwana Yesu Kristo aliitumia kuwavuta watu wake kwake kutoka kwenye dhambi alipokuwa hapa duniani
MVUTO WA KWANZA:
alielezwa kuwa baada ya kuweka mnofu wa kuwavutia samaki kwenye ndoano na kuitupa ndoano majini baada ya muda kidogo utaivuta juu, wale samaki wadogo wataiona na kuifuata na kuizingira ila wale wakubwa watasogea tu karibu na tukio kuhakikisha kama ni chakula halisi, huo ndio mvuto wa kwanza.
MVUTO WA PILI:
baada ya muda tena kidogo utaivuta ndoano juu tena ila isitoke yote, na wale samaki wadogo waliokuwa wameizunguka ndoano, watakimbia lakini wale samaki wakubwa, watakikaribia na kukila na kunaswa,
MVUTO WA TATU:
baada ya wale samaki wakubwa kunaswa katika mvuto wa pili sasa ni wakati wa kumalizia mvuto wa mwisho.na huu ndio wa kumtoa samaki nje ya maji.
sasa kanisa la Mungu lipo katika mvuto wa tatu ambao ni NENO LA MUNGU, kuandaliwa kwenda kwenye unyakuo, ishara na miujiza haviwezi kutukamilisha hivyo vyote vilikuwa vinatuandaa kwa ajili ya mvuto wa tatu, ambao ni kusikia neno la Mungu,
tunawashauri wakristo wayatazame mafundisho haya, yameelezea vizuri zaidi kuhusu MVUTO WA TATU,
MUNGU AKUBARIKI
Mada zinazoendana:
Mada Nyinginezo:
HISTORIA YA WILLIAM BRANHAM
JE! NI DHAMBI KUSHEREKEA SIKU YA KUZALIWA? BIRTHDAY!
JE! NI HALALI KWA MTU WA MUNGU KUTUMIA NJIA ZA UZAZI WA MPANGO?
JE! NI DHAMBI KWA MKRISTO KWENDA HOSPITALI AU KUTUMIA MITI SHAMBA ANAPOUGUA?
Moja ya maagizo muhimu sana ambayo Bwana YESU KRISTO aliyatoa kwa kanisa ni ubatizo.
Mengine yakiwemo kushiriki,kutawadhana miguu kwa wakristo,wanawake kufunika vichwa vyao wakati wa ibada.Kati ya hayo ubatizo ni muhimu sana kwa mwamini yeyote kwa ajili ya ondoleo la dhambi zake.Lakini ubatizo huu shetani ameuharibu usifanyike ipasavyo kwa sababu anajua una madhara makubwa katika kumbadilisha mkristo.na hiyo ndiyo imekuwa kazi ya shetani tangu awali kuyapindisha maneno ya Mungu na kuzuia watu wasimfikie Mungu katika utimilifu wote.
Makanisa mengi leo hii yanabatiza watu au watoto wachanga kwa kuwanyunyuzia maji. Wakibatiza kwa jina la BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU kulingana na mathayo 28:19. “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mtakatifu”..swali ni je! hili jina linatumiwa ipasavyo kubatizia?
Kwa kukosa Roho ya ufunuo na uelewa wa maandiko viongozi wengi wa dini wameacha kweli. Na kugeukia mafundisho ya kipagani na kibaya zaidi wengi wao wanaujua ukweli lakini wanawaficha watu wasiujue ukweli kwa kuogopa kufukuzwa kwenye mashirika yao ya dini. Watu kama hawa ni adui wa msalaba
Mathayo 23:13″ ole wenu waandishi na mafarisayo, wanafki! kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamuingii wala wanaoingia hamwaachi waingie.”
Tukirejea tena kwenye maandiko
Yohana 5:42-43 “walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu.Mimi nimekuja kwa JINA LA BABA YANGU, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo.”
Tukirudi tena kwenye maandiko yohana 14:26 Yesu Kristo alisema “lakini huyo msaidizi,huyo Roho mtakatifu ambaye baba atampeleka KWA JINA LANGU, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.”na hapa tunaona Roho Mtakatifu alitolewa kwetu kwa jina la Bwana Yesu. kwahiyo hapa biblia inatufundisha dhahiri kabisa kuwa jina la Roho Mtakatifu ni Yesu.
Na tena kwenye maandiko tunaona kuwa Roho Mtakatifu ndiye Baba mathayo 1:20 “…Yusufu, mwana wa Daudi usihofu kumchukua Mariamu mkeo maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu” kwahiyo Baba ndiye yule yule Roho na ndiye yule yule aliyechukua mwili na kuishi pamoja nasi kwahiyo hapa hatuoni ‘utatu’ wa aina yeyote ambao unahubiriwa leo hii na makanisa mengi. Mungu ni mmoja tu!.
Kwahiyo jina la Baba ni Yesu na jina la Mwana ni Yesu na jina la Roho Mtakatifu ni Yesu; baba,mwana na roho ni vyeo na sio majina kwa mfano mtu anaweza akawa baba kwa mtoto wake,mume kwa mke wake,babu kwa mjukuu wake lakini jina lake anaweza akawa anaitwa Yohana na sio ‘baba,mume au mjukuu’ vivyo hivyo kwa Mungu.aliposema mkawabatize kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu alikuwa anazungumzia Jina la YESU KRISTO ambalo ndilo jina la baba na mwana na Roho Mtakatifu.
Katika biblia Wakristo na mitume wote walibatizwa na kubatiza kwa JINA LA YESU KRISTO na sio kwa JINA LA BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU. ubatizo huu wa uwongo ulikuja kuingizwa na kanisa katoliki katika baraza la Nikea mwaka 325 AD pale ukristo ulipochanganywa na upagani na ibada ya miungu mingi ya Roma.
Tukisoma matendo ya mitume 2:37-38 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao. wakamwambia Petro na mitume wengine , tutendeje, ndugu zetu? Petro akawaambia, tubuni mkabatizwa kila mmoja KWA JINA LAKE YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”
Tukisoma tena katika maandiko Filipo alipoenda Samaria na wale watu wa ule mji walipoiamini injili walibatizwa wote kwa jina lake Yesu Kristo matendo 8:12 ” lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habati njema za ufalme wa Mungu na JINA LAKE YESU KRISTO wakabatizwa wanaume na wanawake”
Na pia matendo 8:14-17 inasema ” Na mitume walipokuwa Yerusalemu, waliposika ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu.wakawapelekea Petro na Yohana ambao waliposhuka wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila WAMEBATIZWA TU KWA JINA LAKE BWANA YESU”
Matendo 10:48 Petro alipokuwa nyumbani mwa Kornelio alisema maneno haya “Ni nani awezaye kuzuia maji,hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vilevile kama sisi? akaamuru WABATIZWE KWA JINA LAKE YESU KRISTO”
Tukisoma tena katika matendo 19:2-6 hapa Paulo akiwa Efeso alikutana na watu kadha wa kadha akawauliza.” je! mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?, wakamjibu, la, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. Akawauliza, basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? wakasema, kwa ubatizo wa Yohana. Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani Yesu. Waliposikia haya WAKABATIZWA KWA JINA LA BWANA YESU”
Mitume wote hawa kuanzia Petro,Yohana,Filipo na mtume Paulo wote hawa walibatiza kwa jina la Yesu Kristo je? tuwaulize hawa viongozi wa dini wanaobatiza kwa jina la baba na mwana na roho mtakatifu wameutolea wapi??? na biblia inasema katika
Wakolosai 3:17 ” na kila mfanyalo kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika Jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu baba kwa yeye”..
hii ina maana tukiomba tunaomba kwa jina la Yesu,tukitoa pepo tunatoa kwa Jina la Yesu, tukiponya watu tunaponya kwa jina la Yesu,tukifufua wafu tunafufua kwa jina la Yesu na tukibatizwa tunabatizwa kwa jina la YESU biblia inasema kwenye
Matendo 4:12 “…kwa maana hapana jina lingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo”
na maana ya neno ubatizo ni “kuzamishwa” na sio kunyunyuziwa, kwahiyo ni lazima kubatizwa kwa kuzamishwa kwenye maji sawasawa na maandiko na hakuna mahali popote katika maandiko watoto wachanga wanabatizwa. Ubatizo ni pale mtu anapoona sababu ya yeye kutubu na kuoshwa dhambi zake ndipo anapoenda kubatizwa kwa jina la Yesu kwa ondoleo la dhambi zake.
Ewe ndugu Mkristo epuka mapokeo ambayo Yesu aliyaita “chachu ya mafarisayo” penda kuujua ukweli ndugu mpendwa na ubadilike na umuombe Roho wa Mungu akuongoze katika kweli yote usipende mtu yeyote achezee hatima yako ya maisha ya milele, uuchunge wokovu wako kuliko kitu chochote kile,Mpende Mungu, upende kuujua ukweli,ipende biblia..Mwulize mchungaji wako kwa upendo kabisa kwanini anayafanya hayo huku anaujua ukweli na kama haujui mwambie abadilike aendane na kweli ya Mungu inavyosema kulingana na maandiko.
Kama hujabatizwa au umebatizwa katika ubatizo usio sahihi ni vema ukabatizwa tena kwa jina la YESU KRISTO kwa ondoleo la dhambi zako kwani ubatizo sahihi ni muhimu sana..ukitaka kubatizwa tafuta kanisa lolote wanaoamini katika ubatizo sahihi tulioutaja hapo juu au unaweza ukawasiliana nasi tutakusaidia namna ya kupata huduma ya ubatizo sahihi, karibu na mahali ulipo 0789001312
Mungu akubariki
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
(ubatizo sahihi wa kuzamishwa na KWA JINA LA YESU KRISTO)
Muhtasari wa maelezo haya kwa njia ya video unaweza kuyapata hapa chini.
[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=kuCSAZcnM80[/embedyt]
Mada zinazoendana:
Mada Nyinginezo:
MAAGIZO YA BWANA YESU NI BORA KULIKO MAAGIZO YA DAKTARI:
JE, KAMA HAUNA UBATIZO SAHIHI HAUWEZI KUWA NA ROHO MTAKATIFU?
JE! NI HATUA ZIPI MUHIMU ZA KUFUATA BAADA YA UBATIZO?