Category Archive Maombi ya kujikuza kiroho

MANENO SABA YA YESU MSALABANI.

Kabla ya Bwana wetu YESU KRISTO, Mkuu wa Uzima, Mfalme mwenye Nguvu, Mwamba Mgumu, na Mkombozi, na Mfalme wa wafalme, kuutoa uhai wake, ili baadaye aurudishe tena (Yohana 10:17), yapo maneno saba (7) aliyasema pale msalabani, ambayo tunayapata katika zote nne (yaani Mathayo, Marko, Luka na Yohana), na maneno hayo ni kama yafuatayo.

  1. BABA UWASAMEHE, KWA KUWA HAWAJUI WATENDALO.

Luka 13:34 “Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura”.

Hili ndilo Neno la Kwanza Bwana YESU kulisema akiwa pale msalabani, kuonyesha upendo wa hali ya juu na huruma kwetu, ijapokuwa yeye tayari alishawasamehe, lakini alijua pia umuhimu wa kuwaombea msamaha kwa Baba, kwani si kila msamaha unaoweza kutoa wewe ukawa pia umetolewa na MUNGU, waweza kumsamehe mtu lakini Baba wa mbinguni akawa hajamsamehe huyo mtu bado, hivyo tunajifunza hata sisi kuwaombea wengine msamaha kwa Baba yetu wa mbinguni, kama alivyofanya Bwana wetu YESU KRISTO.

  2. AMIN, NAKUAMBIA LEO UTAKUWA PAMOJA NAMI PEPONI.

Luka 13:42 “Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.

43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi”.

Hili ni neno la Pili Bwana kuzungumza msalabani, kuonyesha huruma za Bwana YESU hata katika hatua za mwisho kabisa za maisha ya mtu.

    3. MAMA TAZAMA MWANAO, NA KISHA AKAMWAMBIA YULE MWANAFUNZI TAZAMA MAMA YAKO.

Yohana 19:26 “Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao.

27 Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake”.

Hili ni neno la tatu, lenye ujumbe wa kuangaliana sisi kwa sisi, kwani kwa kufanya hivyo tunaitimiza amri ya Kristo la upendo.

    4. MUNGU WANGU, MUNGU WANGU MBONA UMENIACHA?

Mathayo 27:46 “Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”

Hili ni neno la nne, lenye kuonyesha Uzito wa dhambi Bwana wetu alizozibeba kwaajili yetu, zilikuwa ni nyingi kiasi cha kuuzima uwepo wa MUNGU mbele zake pale msalabani.

   5. NAONA KIU.

Yohana 19:28 “Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu”.

Hili ni neno la tano, lenye kuonyesha uzito wa mateso ya Bwana YESU kuwa yalikuwa ni makuu.

   6. IMEKWISHA

Yohana 19:30 “Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake”.

Hili ni neno la sita, lenye kutangaza mwisho wa utumwa wa dhambi.. na kuanza kwa majira mapya, hakuna tena mateso, wala kilio wala uchungu kwake YESU, na kwa wote watakaokuwa ndani yake.

  7. BABA MIKONONI MWAKO NAIWEKA ROHO YANGU.

Luka 23:46 “Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu”.

Hili ni neno la mwisho, kabla ya kukata roho.

Maneno haya yalifunga kauli ya Bwana duniani na baada ya siku tatu, alitoka kaburini, Mauti ilimwachia, na akaja na ushindi MKUU, Wokovu kwetu, Haleluyaa!…

Je bado upo dhambini?.. bado huoni ni gharama gani aliyoiingia YESU kwaajili yako?.. Tubu leo na kumkaribisha maishani mwako kabla ya nyakati mbaya na hatari zinazoikaribia dunia kufika.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kwanini tarehe ya pasaka inabadilika kila mwaka?

PASAKA NI NINI? NA JE TUNARUHUSIWA KUSHEHEREKEA?

Nini tofauti kati ya kileo na divai?

Je kibiblia ni sahihi kuadhimisha jumapili ya mitende?

Ipi tofauti kati ya Sheria na kanuni kibiblia.

 

Print this post

NAMNA BORA YA KUIOMBA SALA YA BWANA

Huu ni mwongozo maalumu ya njia bora ya kuiomba sala ya Bwana. Wengi wetu tunaiomba aidha kwa kukariri au kwa kukosa ufahamu wa jinsi ipasavyo kuombwa, kulingana na majira ya nyakati za agano jipya. Lakini kama tukijua namna ya kuiomba ipasavyo basi tutaweza fungua milango mingi sana rohoni, ukizingatia kuwa ni sala ambayo Bwana wetu mwenyewe alitufundisha kwasababu ndio hiyo hiyo hata yeye alikuwa anaiomba.

fungua chapisho hili lililo katika pdf kwa kubofya download uweze kusoma;

Kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Mafundisho mengine:

MWONGOZO WA MAOMBI YA KUJIKUZA KIROHO.

Ni lazima mtu aongozwe sala ya toba ili awe ameokoka?


 

https://wingulamashahidi.org/2023/04/01/jinsi-ya-kupigana-maombi-ya-vita/.

Print this post

MWONGOZO WA MAOMBI YA FAMILIA

 

Huu ni mwongozo wa maombi maalumu kwa ajili ya familia yako. Kama watakatifu, ni wajibu wetu kuziombea familia, Lakini sio kuziombea tu, bali kufahamu maeneo muhimu ya kugusia kwenye maombi hayo. Huu ni mwongozo maalumu wa maombi ya familia. Bofya juu ufungue chapisho hilo (pdf)

Pia Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MWONGOZO WA MAOMBI YA ASUBUHI.

TEMBEA NDANI YA SUKOTHI YAKO.-Maafundisho maalumu kwa watumishi

Print this post

Ni kelele gani zinazozungumziwa hapo katika Waefeso 4:31.

Waefeso 4:31 “Uchungu wote na ghadhabu na hasira NA KELELE na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya”.

Kelele zinazozungumziwa hapo ni kelele za  “Maneno” , kelele za “Maombi” na kelele za “Nyimbo”

1.KELELE ZA MANENO.

Hizo ni zile kelele zinazotokana na malumbano yasiyo na msingi wa kiroho, au mashindano ya maneno. Watu wagomvi huwa wana kelele, watu wabishi huwa wana kelele, watu wakorofi huwa wana kelele, na yote ni matunda ya dhambi ambayo hayapaswi kuwa ndani ya mtu aliyeokoka.

2. KELELE ZA MAOMBI

Kuna mambo ambayo mtu akiomba ni kelele mbele za Mungu, na mfano wa hayo ni yale yasiyotokana na Neno, maana yake mtu anaomba kitu kwa tamaa zake na ambacho si mapenzi ya Mungu, na tena anatumia sauti kubwa, (maombi kama haya ni kelele mbele za Mungu na pia hayana majibu.)

Yakobo 4:3 “Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu”.

3. KELELE ZA NYIMBO.

Amosi 5:23 “NIONDOLEENI KELELE za nyimbo zenu; kwa maana sitaki kuzisikia sauti za vinanda vyenu”.

Si nyimbo zote ni kelele mbele za Mungu, zipo zinazomtukuza Mungu na wanaoimba pia wanamtukuza Mungu.. Lakini zipo nyimbo ambazo hazimtukuzi Mungu ingawa zina majina na sifa za kumtukuza Mungu,

Vile vile zipo nyimbo ambazo zina maneno mazuri ya kumtukuza Mungu, lakini wanaoimba ni watu wasio na mahusiano yoyote na MUNGU, nyimbo za namna hiyo ni KELELE mbele za MUNGU.

Vile vile nyimbo zenye midundo ya kidunia, lakini zina maneno ya kibiblia, hizo nazo ni kelele, na si kelele tu bali pia ni machukizo.

Jihadhari na kelele.

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NIONDOLEENI KELELE ZA NYIMBO ZENU (Amosi 5:23)

WAKINYAMAZA HAWA, MAWE YATAPIGA KELELE.

Nini maana ya Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu?

LAKINI USIKU WA MANANE, PAKAWA NA KELELE.

Je ni kweli Tumejengwa juu ya Mitume na Manabii? (Waefeso 2:20)

Rudi Nyumbani

Print this post

MWONGOZO WA MAOMBI YA KUJIKUZA KIROHO.

Ikiwa wewe umeokoka, na una kiu kweli ya kumkaribia Mungu wako katika viwango vya juu. Basi fahamu huna budi ujikuze kiroho. Na ukuaji huo hutegemea mambo mawili makuu “Neno pamoja na maombi”. Katika tovuti hii yapo mafundisho mbalimbali yatakayokusaidia kupiga hatua hizo.

Makala hii imeegemea zaidi katika Maombi. Hivyo huu ni mwongozo wa Wiki kwa Wiki, mfululizo wa vipengele muhimu vya kuombea. Uwapo nyumbani, uwapo kanisani. Jiwekee ratiba Kisha kuwa mwombaji. Na hakika baada ya wakati fulani utaona matokeo makubwa sana ndani yako.

Wiki ya Kwanza:

Wiki ya pili:

Wiki ya Tatu:

Wiki ya Nne:

Wiki ya Tano:

Wiki ya Sita:

Wiki ya Saba:

Wiki ya Nane:

Mwendelezo utakuja…

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mafundisho mengine:

MASOMO MBALIMBALI YA NENO LA MUNGU.

MAFUNDISHO MAALUMU KWA WAONGOFU WAPYA.

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1

Orodha ya mafundisho yote.

KUONGOZWA SALA YA TOBA

Rudi nyumbani

Print this post