SWALI: ‘Siku ya uovu’ inayozungumziwa katika Waefeso 6:13 Ni ipi? Waefeso 6:13 “Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
JIBU: Ikiwa umedumu katika wokovu kwa muda mrefu utaelewa, si wakati wote mambo yatakwenda sawa kama unavyotaka wewe,
Bwana Yesu aliweka wazi kabisa juu ya suala hilo..akasema..
Mathayo 18:7 “Ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha…
Unaona anasema, hayana budi kuja..Hiyo haijalishi wewe ni mtakatifu au la!. Si wakati wote shetani atakuwa anakuangalia ukiufurahia wokovu wako kwa kwa amani na utulivu, kuna wakati atapanga mashambulizi ya kukuangamiza, au kukufanya utetereke kwenye imani, au ya kukuudhi, kipindi hicho ukikipitia basi ujue hiyo ndio “siku ya uovu” inayozungumziwa hapo.
Kwahiyo kama siku hiyo ikikukuta halafu ulikuwa hujajiweka tayari, ni ngumu sana kumshinda shetani, ni rahisi kupoa au kuurudia ulimwengu kabisa, katika eneo lolote ulilopo hata katika utumishi wako, anaweza kukuletea vitisho visivyo vya kawaida, anaweza kukuletea majaribu, anaweza kukuletea magonjwa, anaweza kukuletea mashahidi wa uongo, anaweza kukubambikizia hata kesi, anaweza kukujia kwa njia yoyote ile, lengo ni kukuangusha, yalimkuta Yusufu, yalimkuta Danieli, yalimkuta Ayubu, yakamkuta Bwana wetu Yesu Kristo, yakawakuta mitume, mimi na wewe ni nani yasitukute?. Hivyo usipojua namna ya kukabiliana na mitego hiyo inapokuja kwa ghafla, utaanguka mara moja.
Na ndio maana mtume Paulo anatoa suluhisho baada ya mstari huo, anasema;
Waefeso 6:13 “Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama 14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; 16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; 18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote”
Waefeso 6:13 “Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama
14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;
16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;
18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote”
Umeona, vigezo vimeshatolewa hapo juu, ili kumshinda shetani wakati wote, kusema tu umeokoka haitoshi, na huku hujijengei desturi ya kuwa mwombaji wa mara kwa mara, husomi Neno, huifanyi kazi ya Bwana kwa jinsi Mungu alivyokupa karama, Ukiwa ni mkristo wa dizani hiyo ni ngumu kustahimili vishindo vya adui siku ya uovu ikifika, maana ni lazima ije.
Ni sawa na mtu anayejisifia nyumba yake kubwa ya kisasa yenye mali nyingi za thamani, lakini ndani amekosa vifaa vya uokozi kama vile zima moto, au waya wa Earth. Anaweza kuifurahia kweli nyumba yake nzuri kaijenga na kuipamba kwa muda mrefu, lakini siku janga kama la moto litakapotokea kwa ghafla na kuteketeza mali zake zote, pamoja na nyumba yake yote, au umeme unapozidi ndani ya nyumba au radi itakapopiga nyumba, ndipo atakapojua kuwa alikosa vifaa muhimu sana ndani ya nyumba yake.
Vivyo hivyo, tukitaka na sisi tuwe wakristo tuliokamilika, ni lazima tuzingatie vigezo tajwa vyote hapo juu. Tuyafanye maombi kuwa sehemu ya maisha yetu kama tahadhari, Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yetu kutuongezea imani, na tutumie karama zetu kuwapelekea na wengine habari njema.
Bwana atutie nguvu.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
MWANANCHI WA UFALME WA MBINGUNI
MAPAMBANO DHIDI YA SHETANI.
WALIO NA HEKIMA NDIO WATAKAOELEWA.
KUOTA UPO KANISANI.
FAIDA ZA MAOMBI.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Shalom, mtu wa Mungu..karibu tujifunze Biblia…
Katika kisiwa cha Patmo, Bwana Yesu alimtokea Yohana alipokuwa ametelekezwa kule na kumwambia maneno mengi sana kama tunavyoyasoma katika kitabu cha Ufunuo. Na moja ya maneno aliyomwambia ni haya.
Ufunuo 1:17 “Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, 18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu”
Ufunuo 1:17 “Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu”
Mtu aliye na funguo maana yake yeye ndie mwenye uwezo wa kuingia na kutoka, au ana uwezo wa kumruhusu mtu mwingine aingie au atoke. Ana uwezo pia wa kumfungia mtu nje au akamfungia ndani. Vilevile huwezi kuzungumzia funguo bila mlango.
Sasa kuna Malango makuu matatu katika maisha 1) Lango la MAUTI na 2) Lango la KUZIMU na 3) Lango la UZIMA WA MILELE
Lango la mauti ni hatua ile ya mwisho kabisa mtu anapouacha mwili na kufa..Anakuwa anaingia katika upeo mwingine, ambao sio wa maisha haya ya duniani. Huko anakwenda kukutana na vitu vipya ambavyo havipo hapa duniani aidha vizuri au vibaya. Katika huu mlango au geti kabla ya agano jipya ilikuwa haiwezekani mtu aliyeenda huko arudie tena huku ulimwenguni. Ukifa hakuna kurudi, wanaoingia mautini wanakuwa wamefungiwa huko huko milele. Lakini baada ya Kristo na kuzitwaa funguo za Mauti, ndipo ukazaliwa uwezekano mpya wa wafu kurudia tena uhai… Na huo ulianza na Yesu mwenyewe kutoka kaburini na kurudia uhai, na siku ile tu alipokufa wapo wengine waliotoka makaburini Pamoja naye, wale waliokufa katika haki wakati wa agano la kwanza.
Lango hili mtu analiingia baada ya kifo, Mtu aliyekufa katika dhambi, pasipo kutubu..anapokufa baada ya kuvuka lango la kwanza la Mauti, anaingia lango la pili la kuzimu. Huko ni sehemu mbaya isiyofaa. Na huko nako kuna malango mengine madogo madogo kumtenganisha mwovu na mwovu..hatutaingia huko sana. Lakini katika lango hili kuu la kuzimu, waliokuwa wamekufa katika uovu katika agano la kale, ilikuwa haiwezekani kutoka huko milele. Lakini Kristo alizitwaa funguo, na siku moja wafu waliopo kuzimu watatolewa huko kwaajili ya hukumu na wakiisha hukumiwa watatupwa katika ziwa la moto.
Yohana 5:27 “Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu. 28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu”.
Yohana 5:27 “Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu.
28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.
29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu”.
Hivyo hata wafu waliopo kuzimu siku moja watatolewa huko kwaajili ya hukumu. Ufunuo 20:13 “Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake”. Ufufuo huu sio mzuri kabisa kwasababu ni wa hukumu.
Na roho ya malango ya kuzimu inafanya kazi hata kabla ya mauti, roho hiyo ndiyo inayowavuta watu wengi waiendee njia iliyopotea, shetani na majeshi yake wanafanya kazi kwa nguvu sana kuhakikisha ni kundi kubwa linataingia kuzimu.
Lango hili ni ndio la lenye maana kwetu wanadamu, kwasababu ndio lango la uzima wa milele. Tofauti na malango hayo mengine ambayo yanahitaji kifo ndipo uyaingie.. Lango hili la uzima wa milele halihitaji mtu ufe, linaanzia hapa hapa duniani..wakati huu huu mtu anapumua na kuishi katika mwili wake. Lango hili ni bure kuingia lakini linahitaji kupambana sana, kwasababu yupo mwingine adui yetu ambaye hatamani hata mmoja wetu aingie.
Lango hili ni lile Bwana Yesu alilolisema katika kitabu cha Luka..
Luka 13:24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze. 25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama NA KUUFUNGA MLANGO, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako; 26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu. 27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu. 28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje”.
Luka 13:24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama NA KUUFUNGA MLANGO, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu. 27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.
28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje”.
Kama tunapenda uzima wa milele basi lango hili lipo wazi mbele yetu leo, Bado Bwana Yesu hajalifunga na tunaingia ndani ya lango leo hili kwa kuyatii maneno yake yanayohubiriwa katika biblia takatifu na yanayohubiriwa na watumishi wake. Lakini tukiyakataa maneno yake basi mlango huu utafungwa mbele yetu.
Wapo watu wanaoishi hapa duniani ambao tayari wameshafungiwa mlango huu.(kwamfano watu waliomkufuru Roho Mtakatifu tayari wameshafungiwa, hao kamwe hawawezi kusamehewa tena kadhalika na watu baadhi ambao wameisikia injili kwa muda mrefu sana, wamepigiwa kelele sana, injili imerudiwa na kurudiwa masikioni mwao lakini hata kujigusa hawajigusi, wengi wameshafungiwa huu mlango hivyo kamwe hawataweza kusikia tena ile hamu ya kutubu na kuvutwa kwa Mungu).
Yesu ndiye mwenye funguo za hili lango na funguo hizo pia amewapa watumishi wake..Hebu tusome maandiko yafuatayao ili tuelewe Zaidi..
Yohana 20:21 “Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. 22 Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu. 23 Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa”.
Yohana 20:21 “Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi.
22 Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.
23 Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa”.
Umeona hapo? Wale waliotumwa na Yesu kuhubiri wamepewa amri ya kuwafungia watu dhambi..Na hawawafungii kwa kutamka mdomoni kwamba “Fulani nakufungia dhambi” hapana hiyo sio tafsiri yake..Tafsiri ya kuwafungia watu dhambi iliyozungumziwa hapo ni hii >>
Mathayo 10:14 “Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung’uteni mavumbi ya miguuni mwenu. 15 Amin, nawaambia, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma na Gomora kustahimili adhabu ya siku ya hukumu, kuliko mji ule”.
Mathayo 10:14 “Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung’uteni mavumbi ya miguuni mwenu.
15 Amin, nawaambia, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma na Gomora kustahimili adhabu ya siku ya hukumu, kuliko mji ule”.
Kwahiyo mtu anaposikia injili na kuidharau tena kuikejeli..Yule mtumishi wa Mungu Roho Mtakatifu anapomwongoza aondoke mahali pale..hao waliosalia hapo nyuma, ndio Habari yao imeisha!..hawatapata tena neema kamwe, wataendelea katika njia hiyo hiyo! Mlango umefungwa tayari. Hali kadhalika wanapoikubali na kuitii, basi wanafunguliwa mlango ambao malango ya kuzimu hayataiweza..maana yake hao watu watakaoitii injili inayohubiriwa na mtu yule aliyetumwa na Mungu..basi ni ngumu sana kupotea…Watakuwa wana ulinzi Fulani wa daima ambao hata wakirudi nyuma kidogo nguvu ya Mungu itawarudisha kwenye mstari kwasababu tu! Waliitii injili ya Kristo. Bwana Yesu alimwambia maneno haya Petro.
Mathayo 16:18 “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. 19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni”
Mathayo 16:18 “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni”
Petro ni mfano wa watu wote waliothibitishwa na Mungu na kuwekwa wakfu kwa ajili ya kazi yake.
Hivyo dada/kaka unayesikia maneno haya. Kama unapenda kuishi Maisha yasiyo na mwisho…miaka milioni kwa mamilioni yasiyo na shida wala taabu, wala uchungu…Njia ni moja tu, nayo ni Yesu. Yeye ndiye mwenye funguo za Uzima wa Milele, na funguo hizo amewapa watumishi wake pia..Ukitaka kuishi, ukitaka uzima..Mkubali Yesu. Ukimkubali Yesu malango ya kuzimu yatakukwepa..kuna nguvu fulani itaachiliwa juu yako ambayo atakuweka katika mstari uliyoonyooka..Lakini kama hutaki kuishi milele, basi malango ya Mauti na kuzimu yanakungoja, hivyo chagua chaguo jema, Yesu ndiye lango na anakupenda!
KUZIMU ni mahali pa namna gani, Je! huko wanaishi watu wakifa na kwenda kupata mateso au ni vinginevyo?
USIUZE URITHI WAKO.
HASIRA YA MUNGU KUKUWAKIA, KWA KUTOMZUNGUZIA TU MUNGU IPASAVYO.
FAHAMU MAJIRA ULIYOPO NA NINI UNAPASWA UWE NACHO.
MWANAMKE ULIYEKOMAA KI-UMRI, ITAMBUE HUDUMA YAKO.
NI KITU GANI PETRO NA YOHANA WALIKIGUNDUA KABURINI?
UHARIBIFU HAUNA KIFUNIKO.
Kuna ufufuo wa aina ngapi?
Mwezi wa Abibu ni upi?
Huu ni mwezi wa kwanza kwa kalenda ya Kiyahudi. Ambao kwa kalenda yetu hii ya ki-gregory unaangukia katikati ya mwezi Machi, na Aprili, kutegemeana na mwaka wenyewe jinsi ulivyokuja.
Upo mwaka ambao mwezi huu wa Abibu unaanza katikati ya mwezi wa tatu, na upo mwaka, unaanza mwanzoni mwa mwezi wa nne.
Mwezi huu ni mwezi muhimu sana kwa wayahudi, kwasababu ndio mwezi wa kumbukizi yao ya kutoka katika nchi ya Misri(Nchi ya Utumwa).
Kutoka 13:4 “Ninyi mwatoka leo katika mwezi wa Abibu”.
Ndani ya mwezi huu, Siku ya 14 walikuwa wanasheherekea sikukuu iliyojulikana kama sikukuu ya pasaka, Na kuanzia tarehe 15-21, walisheherekea sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu.
Kumbukumbu 16:1 “Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie pasaka Bwana, Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku Bwana; Mungu wako. 2 Nawe umchinjie pasaka Bwana, Mungu wako, katika kundi la kondoo na la ng’ombe, mahali atakapochagua Bwana apakalishe jina lake”.
Kumbukumbu 16:1 “Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie pasaka Bwana, Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku Bwana; Mungu wako.
2 Nawe umchinjie pasaka Bwana, Mungu wako, katika kundi la kondoo na la ng’ombe, mahali atakapochagua Bwana apakalishe jina lake”.
Mwenzi wa Abibu ulijulikana kwa jina lingine kama mwezi Nisani.
Esta 3:7 “Basi mwezi wa kwanza, ndio mwezi wa Nisani, mwaka wa kumi na mbili wa mfalme Ahasuero, wakapiga Puri, yaani kura, mbele yake Hamani; siku kwa siku, na mwezi kwa mwezi, hata mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari”.
Soma pia. Nehemia 2:1
Sasa wayahudi kila wanapoiungia huu mwezi wa Abibu/Nisani, huwa wanakumbuka siku ya kutolewa kwao utumwani..
Lakini swali linakuja kwako wewe mkristo, Siku yako ya Nisani ni ipi?
Abibu/Nisani yetu ni pale tunapookoka, siku tunapoamua kuacha dhambi na kumfuata Kristo, na kwenda kubatizwa, basi kuanzia siku hiyo nasi pia tunakuwa tumejumuishwa katika kalenda ya ki-Mungu. Hivyo rohoni tunaonekana kuwa tumeshauanza mwezi wa Abibu/Nisani.
Na faida yake ni kuwa, kuanzia huo wakati unakuwa unaanza kutembea katika mpango wa Mungu wa kimbinguni, wewe unakuwa sio mwana-haramu tena, Mungu anaanza kutenda kazi zake ndani ya maisha yako, kipindi kwa kipindi, Na hilo utalishuhudia mwenyewe, kwa jinsi siku zitakavyokuwa zinakwenda. Utaona tofauti yako ya mwezi uliopita na mwezi huu, utaona tofauti yako ya mwaka ule uliookoka, na ile mingine iliyopita nyuma.
Lakini kama upo katika dhambi, wewe bado kalenda ya ki-Mungu haijaanza kuhesabiwa kwako. Na hivyo Mungu anakuwa hana mpango wowote na wewe, unakuwa ni kama mwana haramu tu. Shetani atajiamulia kufanya lolote atakalo katika maisha yako, atakuharibia maono yako, atafanya chochote ajisikiacho na mwisho wa siku utapotea na kwenda kuzimu. Na kuishia katika majuto ya milele
Lakini ukitubu dhambi zako, leo na ukawa tayari kuanza maisha mpya na Kristo, basi ni uhakika kuwa utaanza kutembea katika huo mpango wa Mungu. Hivyo bila kupoteza muda Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki,
pia fungua vichwa vingine vya masomo chini, upate mafundisho mengine ya rohoni.
SIKUKUU 7 ZA KIYAHUDI ZINAFUNUA NINI KWETU?
Israeli ipo bara gani?
ESTA: Mlango wa 8, 9 & 10. (SIKU KUU YA PURIMU)
MAVUNO NI MENGI
KRISIMASI (CHRISTMAS) NI NINI? JE IPO KATIKA BIBLIA?
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
CHUKIZO LA UHARIBIFU
UNYAKUO.
SWALI: Nimrodi ni nani? Na je! Alikuwa ni mtumishi wa Mungu?
Nimrodi ni kitukuu cha Nuhu kwa kupitia uzao wa Hamu,
Biblia inatuambia alianza kuwa mtu Hodari, na sio Hodari tu, bali alikuwa ni Hodari wa kuwinda mbele za Bwana, Mpaka enzi hizo ukatungwa msemo maarufu kwa jina lake (Soma Mwanzo 10:9),
Hivyo aliendelea na huo uhodari wake mpaka akafikia hatua ya kuwa na nguvu nyingi za kuanza kujenga miji mikubwa, ikiwemo Babeli na Ninawi.
Mwanzo 10:8 “Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi. 9 Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za Bwana. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za Bwana. 10 Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari. 11 Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala; 12 na Reseni, kati ya Ninawi na Kala, nao ni mji mkubwa”
Mwanzo 10:8 “Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.
9 Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za Bwana. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za Bwana.
10 Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari.
11 Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala;
12 na Reseni, kati ya Ninawi na Kala, nao ni mji mkubwa”
Lakini japokuwa alikuwa ni Hodari, alikuwa ni mwovu katika fikra zake na matendo yake, nakala nyingi za kale zinaonyesha, hata nia yake ya kutaka kuujenga mnara wa Babeli ilikuwa ni kumlipizia Mungu kisasi, kwamba kwanini aliwaua mababu zake, hivyo akaunyanyua mnara ule juu sana kuelekea mbinguni kiasi kwamba hata Mungu akileta tena mafurukio mengine asiweze kuwaangamiza.
Lakini jitihada zake hazikufika mbali, tunajua kilichotokea ni nini baada ya pale, ni kwamba walichafuliwa lugha zao na semi, ndoto zao zote zikayeyukia palepale, Kwasababu Mungu hadhihakiwi.
Lakini Pamoja na hayo bado tunakuja kuona Babeli iliendelea kuwepo kwa miaka mingi mbeleni, mpaka ikaja kuwa kitovu cha machafuko yote duniani, Na ndio hawa wababiloni baadaye wakaja kulichukua taifa la Israeli utumwani tena. Kama ulikuwa hujui ni kwamba chimbuko la ibada zote za sanamu na miungu, ilianzia huko, Hii miungu ya Rumi ya kuabudu mungu mke na katoto chake (ambayo kwa sasa wameipachika majina ya watakatifu kama Mariamu ) chimbuko lake lilikuwa ni huko,
Na ndio maana Babeli hiyo mpaka siku hizi za mwisho bado inaonekana kuishi, isipokuwa safari hii inatenda kazi rohoni. Katika kivuli cha dini.
Sasa muhasisi wa hayo yote alikuwa huyu Nimrodi.
Biblia inasema..
Mithali 1:32 “Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza”
Usifurahie mafanikio ya kipumbavu hata kama utasifiwa na ulimwengu mzima, shetani naye alikuwa ni Hodari hivyo hivyo kabla ya kuasi, lakini ulikuwa ni uhodari unaokwenda kinyume na mapenzi ya Mungu.
Ezekieli 28:14 “Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto. 15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako. 16 Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto. 17 Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama. 18 Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao. 19 Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele”.
Ezekieli 28:14 “Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.
15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.
16 Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto.
17 Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.
18 Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao.
19 Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele”.
Nasi pia tusiige mifano hiyo, tuwe wanyenyekevu kwa Mungu, tuishi kwa kuyafanya mapenzi yake, Hilo tu linatosha Sio kila jambo linalofanywa na watu Hodari wa mataifa yaliyoendelea na sisi tuigee, Ni heri tubakie na ushamba wetu kuliko tuige utukanaji, ushoga, au upagani, au uvaaji wa mavazi yasiyo na heshima mbele za Mungu na wanadamu.
Imemfaidia nini Nimrodi kuupata ulimwengu mzima, halafu amepata hasara ya roho yake?
Bwana atusaidie.
YEREMIA
Kuungama ni nini?
Je! msalaba kaburini una umuhimu wowote?
UMEFUMBULIWA MACHO YAKO YA KIROHO?
HERI YULE ATAKAYEKULA MKATE KATIKA UFALME WA MUNGU.
WhatsApp
Swali: Sabato tatu ni nini? Kama tunavyosoma katika Matendo 17:2
Jibu: Tusome,
Matendo 17:1 “Wakiisha kupita kati ya Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambapo palikuwa na sinagogi la Wayahudi. 2 Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko SABATO TATU, 3 akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo”.
Matendo 17:1 “Wakiisha kupita kati ya Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambapo palikuwa na sinagogi la Wayahudi.
2 Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko SABATO TATU,
3 akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo”.
Mstari huo haumaanishi kwamba kuna aina tatu za sabato au sabato zipo tatu. Hapana, bali unamaanisha Sabato tatu mfululizo.
Kwamfano tafakari hii sentensi.. “Yohana baada ya kuokoka alihudhurua kanisani JUMAPILI TATU mfululizo za mwezi uliopita”. Sasa hapo simaanishi jumapili zipo za aina tatu, bali namaanisha ni jumapili za majuma matatu. Ndivyo Paulo alichomaanisha hapo katika sabato tatu. Maana yake kwa sabato tatu mfululizo aliingia hekaluni kuhojiana nao kwa maneno ya maandiko.
Sasa unaweza kuuliza je! kwa mantiki hiyo na sisi tunapaswa tuishike sabato?
Jibu ni la! Sabato halisi katika agano jipya sio siku moja maalumu, bali ni kila siku ya maisha yetu tunayoishi, sasa kwanini hapo Paulo aingie kuhojiana nao wakati wa sabato?. Ni kwasababu kwa wakati huo wayahudi (yaani waisraeli), walikuwa bado wana desturi ya kuishika sabato. Hivyo siku pekee ya kuweza kukutana nao ni siku ya sabato katika masinagogi yao, siku nyingine zozote wasingeweza kupatikana ndio maana hapo Paulo alikwenda kukutana nao katika siku yao ya kuabudu.
Ni sawa leo utafute namna ya kuwapata watu wa dini Fulani kuhojiana nao kuhusu imani, huwezi kuwapata nje na ile siku yao wanayokutana kuabudu. Kama ni ijumaa, au jumamosi au jumapili, au siku nyingine yoyote ile, sasa kitendo cha wewe kuwafuata ili uwashuhudie katika siku yao ya Ibada haimaanishi kwamba na wewe umeihalalisha siku ile.
Kufahamu zaidi kuhusu Sabato halisi ni ipi, mwisho wa somo hili chini kabisa utaona orodha ya mada hizo zinazohusiana na sabato, zifungue uzisome.
Bwana akubariki.
Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?
BABA YANGU ANATENDA KAZI HATA SASA!.
Je! “majira na sheria” mpinga-kristo atakayokuja kubalisha ni kupindua siku ya sabato na kuwa jumapili?
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
KIAMA KINATISHA.
Karibu tujikumbushe mambo machache, ambayo yanaonekana ni madogo lakini ni ya umuhimu sana, katika mapambano ya Imani.
Kuna tofauti ya sadaka na msaada. Unapomsaidia maskini huo ni msaada, na una thawabu zake mbele za Mungu..lakini sadaka ina matokeo makubwa zaidi kuliko msaada.
Sadaka ni nini?
Sadaka ni matoleo yoyote yanayohusisha madhababu!.. Katika agano la kale, sadaka iliyokuwa inakubalika kwa Mungu ni ile iliyokuwa inapelekwa mbele ya madhabahu ya Mungu katika nyumba ya Mungu…iwe ni kafara ya kondoo, au sadaka ya mazao au chochote kile. Vigezo ni lazima ipelekwe katika hema ya kukutania au katika nyumba ya Mungu.
Usipeleke sadaka yako kwa maskini, ukifanya hivyo utakuwa hujatoa sadaka bali umetoa msaada, utabarikiwa kwa ulichotoa lakini si kama ungeitoa kama sadaka. Sadaka ni lazima ihusishe madhabahu ya ki-Mungu.
Hata watu wanaokwenda kwa waganga huwa wanapewa masharti ya kupeleka sadaka..Na ile sadaka wanapewa maagizo ya kuiacha pale kwenye madhabahu zao, ili ilete matokeo wanayoyataka, kama ni kuku ataambiwa ampeleke hapo wamchinjia hapo hapo na kumwacha pale pale…Huwezi kusikia wanapewa maagizo na waganga na kuambiwa wakachinje jogoo mweusi nyumbani halafu wakawape maskini, au wakaipeleke kwa mganga mwingine,! Huwezi kusikia hicho kitu!.watakuambia leta hapa (kwenye hii madhabahu) hiki au kile kama sadaka yako, kwasababu ili kitu kiwe sadaka ni lazima kihusishwe na madhabahu.
Kwahiyo hakuna sadaka pasipo madhabahu.
Bwana Yesu alisema maneno haya katika
Mathayo 23:18 “Tena, Mtu atakayeapa kwa madhabahu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amejifunga”.
Maneno hayo yanaelezea uhusiano uliopo kati ya sadaka na madhababu.
Kwahiyo kama wewe ni mkristo, sadaka yako peleka kanisani na mahali unapokuzwa kiroho (kwamfano kwenye mikutano ya injili, semina n.k), ndipo utakapobarikiwa Zaidi… Bila kusahau kusaidia maskini na wenye uhitaji ambako pia kuna thawabu kubwa kutoka kwa Mungu. Lakini sadaka ina nguvu mara nyingi Zaidi ya hiyo, endapo utaelewa ufunuo wake!.. Ongeza bidii sana katika kutoa sadaka kuliko kupeleka michango yako sehemu nyingine.
Kuna fikra mbaya sana ambayo shetani kaisambaza kwenye akili za watu wengi, ambayo imewasababishia watu wengi kukosa baraka zao. Na hicho ni saikolojia ya kwamba ukiipeleka sadaka kanisani basi ni kuwatajirisha wale wachungaji na watumishi!, na hivyo ni afadhali kuipeleka kwa maskini, Hiyo ni saikolojia ya Adui, usikubali ikutawale.
Bwana Yesu alisema pia maneno haya..
Mathayo 5:23 “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako”.
Mathayo 5:23 “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,
24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako”.
Mambo haya yanaonekana ni madogo machoni pa wengi, lakini yana umuhimu mkubwa sana. Hivyo ni muhimu sana kuyafahamu na kuyazingatia. Zaka yako ipeleke nyumbani kwa Bwana, Sadaka zako za shukrani vilevile ipeleke nyumbani kwa Bwana.
Mungu akubariki sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 693036618/ 0789001312
TUMTOLEE MUNGU VILE VINAVYOTUGHARIMU ZAIDI.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
Ubatizo wa moto ni upi?
MASOMO MBALIMBALI YA NENO LA MUNGU.
UWEPO WA BWANA HATA KATIKATI YA MATESO.
JE KUVAA PETE NI DHAMBI?
JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe daima, Nakukaribisha tena tuyatafakari maneno ya uzima.
Leo tutatazama kwa ufupi Habari ya watu wawili. Wakwanza ni mtu mmoja anayeitwa Yairo mkuu wa sinagogi, na wa pili ni mwanamke mmoja aliyekuwa anatokwa na damu kwa muda mrefu lakini baadaye alikuja kuponywa na Bwana Yesu kwa kulishika tu pindo la vazi lake.
Sasa lipo jambo moja la kusisimua nataka ulione kwa hawa watu wawili ambalo kila mmoja lilikuwa kichwani mwake. Embu tusome kidogo;
Luka 8:40 “Basi Yesu aliporudi mkutano ulimkaribisha kwa furaha, maana walikuwa wakimngojea wote. 41 Na tazama, mtu mmoja akaja, jina lake Yairo, naye ni mtu mkuu wa sinagogi, akaanguka miguuni pa Yesu, akamsihi aingie nyumbani kwake; 42 kwa kuwa binti yake yu katika kufa, ambaye ni mwana pekee, umri wake amepata miaka kumi na miwili. Na alipokuwa akienda makutano walimsonga. 43 Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote, 44 alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma”.
Luka 8:40 “Basi Yesu aliporudi mkutano ulimkaribisha kwa furaha, maana walikuwa wakimngojea wote.
41 Na tazama, mtu mmoja akaja, jina lake Yairo, naye ni mtu mkuu wa sinagogi, akaanguka miguuni pa Yesu, akamsihi aingie nyumbani kwake;
42 kwa kuwa binti yake yu katika kufa, ambaye ni mwana pekee, umri wake amepata miaka kumi na miwili. Na alipokuwa akienda makutano walimsonga.
43 Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote,
44 alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma”.
Sasa ukiangalia hapo, utaona huyu Yairo, alikuwa na binti yake aliyepatwa na matatizo katika umri wake wa miaka kumi na miwili (12), Na wakati huo huo alikuwepo yule mwanamke alitokwa na damu kwa muda wa miaka kumi na miwili (12). Ipo sababu kwanini biblia imeutaja umri wa mtoto na muda wa mwanamke kutokwa damu.
Kwamfano biblia inatuambia huyu Yairo hakuwa na mwana mwingine isipokuwa yule binti tu, pengine alimlea kwa taabu na shida, akiwa na matumaini kuwa huyu ndiye atakayekuja kuwa heshima yake ukubwani, pengine aliona mwelekeo mzuri wa binti yake, kama vile Yokebedi(mama yake Musa) alivyoona uzuri wa Musa tangu akiwa mdogo, akaamua kumficha ambapo kweli baadaye tunaona akaja kuwa nyota ya Israeli mwokozi wa Israeli,
Vivyo hivyo pengine huyu Yairo naye alimwona binti yake kuwa ni mzuri atakuja kuwa mcha Mungu kama Hana, au Sara, na kumletea fahari kwake, hivyo pengine akajitahidi kumlea katika maadili tangu anapozaliwa, mpaka anafikisha umri wa miaka 11, lakini alipofikisha umri wa miaka 12, ghafla akaanza kuona mabadiliko katika afya ya mtoto wake, miezi ya kwanza kwanza, hali inaanza kuwa mbaya mpaka inakaribia miezi ya katikati mtoto ndio yupo mauti uti kabisa,..katika hali kama hiyo anawaza afanyaje mtoto wake anakwenda kufa?
Je! Aruhusu maono yake yafe katika umri wa miaka 12,akizingatia kuwa ndio mwana pekee aliye naye? au afanye nini?. Lakini kama tunavyosoma habari, hakuruhusu jambo hilo litokee, hakuruhusu ndoto zake alizozihangaikia tangu zamani zizimwe na shetani katika mwaka wake wa 12 wa Maisha ya mwanawe, hapo ndipo akaanza safari ya kumtafuta Yesu.
Lakini huku nako upande wa pili, kulikuwa na mwanamke aliyetokwa na damu naye kwa muda mrefu, ambaye pia harakati zake za kutafuta uponyaji, zilianza tangu kipindi yule binti anazaliwa, tangu mwaka wa kwanza, akaendelea hivyo hivyo mpaka mwaka wa 2,..3…4, bila mafanikio mpaka mwaka wa 11, (Biblia inasema alikuwa ameshapoteza pesa zake nyingi kwa madaktari bila mafanikio) na ulipofika mwaka wa 12 bado hajapata alichokuwa anakitafuta, lakini naye siku moja akasikia Yesu yupo mjini..akasema sitakubali uponyaji wangu niliokuwa ninautafuta kwa miaka yote hii 12, leo hii ukatishwe na kukata tamaa, nitakwenda kukutana na Yesu.
Hivyo wote hawa wawili kila mmoja akaanza safari yake kivyake, na kama tunavyoisoma Habari Kristo aliwaponya wote, na wakapata walichokuwa wanakihangaikia, na kukiongojea.
Hata leo, tunapaswa tujifunze kuwa upo wakati wa kuyashindania yale maono ya kumtumikia Mungu ambayo tulikuwa tumeshaanza kuyafanya tangu zamani,haijalishi leo hii ni kipingamizi kikubwa kiasi gani kimesimama mbele yako, tunapaswa tuyashindanie…
Kwa kumkabidhisha Yesu hayo matatizo bila kuruhusu yaangamie kabisa..
Wapo watumishi ambao walishaanza kumtumikia Mungu,na walishapiga hatua fulani lakini pengine wakapitia vitisho Fulani vya ibilisi wakaacha kuhubiri, au kutumika. Ndugu usiruhusu taabu yako uliyoisumbukia iwe bure.
Kumbuka wapo wengine wamekuwa wakimwomba Mungu wapate kama tu hicho ulichonacho kwa muda mrefu, pengine tangu ulipoanza wewe kutumika, lakini bado hawajakipata, na hawakati tamaa kumwomba Yesu, na atawapa, kwanini wewe uruhusu kukata tamaa?
Mwaka wa 12 wa mtoto ya Yairo, Sio sawa na miaka 12 yule mwanamke aliyokuwa anangojea uponyaji wake..Hivyo na wewe, tatizo lako mpito lisikwamishe katika kazi yako ya utumishi Mungu aliyoiweka ndani yako.
Ili tushinde, ni lazima tushindane, Hivyo songa mbele.
Na sio tu kwenye kuifanya kazi ya Mungu, bali pia katika vitu vingine vyote unavyovitafuta vilivyo mapenzi ya Mungu, hupaswi kukata tamaa kabisa.
Bwana akubariki sana.
Shalom.
MWAKA WA BWANA ULIOKUBALIWA.
NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE
KUOTA UMEFUNGA NDOA.
NENO LA MUNGU NI DAWA ILIYO TOFAUTI NA DAWA NYINGINE.
FUKUZA TAI WOTE JUU YA SADAKA YAKO.
Kuota upo gerezani kunamaanisha nini?
Ndoto ya namna hii inaanguka katika makundi makuu matatu (3) ya watu.
Sasa ni vizuri ukajitathmini kwanza wewe mwenyewe na ukajijua upo katika kundi lipi kati ya hayo, ili upate tafsiri sahihi ya ndoto yako. Sasa tukianzana na kundi la kwanza.
Ikiwa wewe unajijua kabisa umeokoka, na umesimama katika Imani na hakuna chochote kinachokuyumbisha, Lakini cha kushangaza umejikuta katika ndoto upo gerezani, au kifungoni na hujui utatokaje. Nataka nikumbie hupaswi kuwa na hofu,.Shetani anaona Imani yako, na bidii yako kwa Mungu, na hivyo atafanya kila njia kukuzuia, au pengine ameshaanza kufanya hivyo katika Imani yako, wewe kusonga mbele, atajaribu kukusonga usifike mahali Fulani, lakini hawezi kufanikiwa.
Ipo mifano kadha wa kadha katika biblia, utaona magwiji wote wa Imani walipokuwa wanafanikiwa katika kumcha Mungu shetani hakutulia tu hivi hivi, badala yake alinyanyua vikwazo vya vifungo. Kwamfano utamwona Yusufu, wakati alipokataa kulala na mke wa Boss wake (Potifa), alisingiziwa na kutupwa gerezani na akakaa kule kwa muda wa karibu miaka 2..Lakini Yusufu hakuacha kumcha Mungu, kwasasababu, vifungo haviwezi kumshika mteule wa Mungu daima, Na sote tunajua ni nini kilikuja kumpata Yusufu baada ya lile jaribu, ilikuwa ni kufanyika kuwa waziri mkuu wa Misri,
Vilevile utamwona Yeremia naye, alifungwa gerezani kwasababu alikuwa anawatabiria Israeli Habari za kweli za Mungu,(Soma vitabu vya Wafalme na Yeremia chote)
Utamwona tena Yohana Mbatizaji, yeye naye walimshika na kumtupa gerezani kisa tu, alimweleza mfalme Herode kosa lake la kuzini na mke wa ndugu yake, (Marko 6:17)
Halikadhalika utawaona mitume wa Kristo, akina Petro na Yohana vifungo viliwakuta, Paulo alipokuwa kuwa anasafiri katika ziara zake za kuhubiri injili Roho Mtakatifu alimshuhudia kabisa na kumwambia;
Matendo 20:23 “ isipokuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na dhiki vyaningoja.24 Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo”.
Wakati mwingine alipokuwa na Sila, walimkamata na kumtupa gerezani, lakini wakiwa kule gerezani, hawakufadhaika, bali walimwimbia Mungu na kumsifu,
Matendo 16:25 “Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza”.
Vivyo hivyo na wewe, ikiwa ni mkristo ambaye unajijua umesimama kikamilifu katika Imani, unaweza ukawa unapitia sasahivi vipingamizi vya kiimani, au vitakuja mbele yako kipindi sio kirefu, utakutana na shetani kutaka kukuzuia usisonge mbele na hicho unachomfanyia Mungu, basi usiogope, wewe fanya kama Paulo na Sila, zidi kumwimbia Mungu na kumsifu, na kuomba kwa bidii, kwasababu ipo hatua nzuri Zaidi Mungu anataka kukuvukisha.
Na ndio maana umeoteshwa ndoto kama hiyo upo gerezani, kifungoni. Usiogope, zidisha matendo yako kwa Mungu, wewe ni shujaa..
Lakini kama wewe ni mkristo ambaye ni vuguvugu au ulishaanza kupoa, hapo mwanzo ulikuwa umesimama lakini sasahivi ni kama vile umerudi nyuma, na umeota ndoto kama hii upo gerezani, Hiyo ni tahadhari kubwa sana kwako.
Kumbuka shetani anakuwinda usiku na mchana,..Kwenye biblia alikuwepo mtu mmoja aliyeitwa Samsoni, yeye ni mfano wa wakristo vuguvugu wa leo, alilaghaiwa na uongo wa shetani mpaka akatoa siri ya nguvu zake. Na wote tunajua kilichomkuta baada ya pale ni nini?.
Alitobolewa macho, akatupwa gerezani na kufanyishwa kazi hata Zaidi ya punda..
Waamuzi 16:21 “Wafilisti wakamkamata, wakamng’oa macho; wakatelemka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza”
Ndivyo ilivyo hata na wewe, Mungu amekuotesha upo gerezani, ni kwamba upo karibuni kutekwa na ibilisi au pengine tayari ameshakuteka kabisa..Biblia inasema kurudi kwake nyuma mpumbavu kutamwangamiza.
Hivyo unachopaswa kufanya ni kutubu na kumgeukia Mungu haraka sana, kama unafanya mambo ambayo hayampendezi heri uache mara moja, Kwasababu Mungu hataki uangamie. Na ndio maana kakupa tahadhari hiyo.
Lakini sasa kama wewe, upo dhambini tangu zamani, hujawahi kuwa na Habari na Mungu, kisha umeota upo gerezani,..Ni Mungu anazungumza na wewe, na kukuonyesha hali yako ilivyo rohoni. Kwamba upo vifungoni, shetani amekunasa, shetani anaitesa roho yako.
Lakini habari njema ni kuwa lengo kuu mojawapo la Yesu kutumwa duniani ilikuwa ni kuwafungua na kuwaacha huru waliofungwa na ibilisi..
Hivyo ikiwa wewe ni mkristo jina tu, au mwislamu, au muhindu, au mpagani,.. Sikiliza unabii Mungu aliompa Yesu zamani..alisema.
Isaya 42:6 “Mimi, Bwana, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa; 7 kuyafunua macho ya vipofu, KUWATOA GEREZANI WALIOFUNGWA, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa. 8 Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu”
Isaya 42:6 “Mimi, Bwana, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa;
7 kuyafunua macho ya vipofu, KUWATOA GEREZANI WALIOFUNGWA, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.
8 Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu”
Na ndio maana Yesu alisema..
Zaburi 61:1 “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, KUWATANGAZIA MATEKA UHURU WAO, NA HAO WALIOFUNGWA HABARI ZA KUFUNGULIWA KWAO”.
Hivyo leo umejiona upo vifungoni, pengine unateseka kutafuta njia ya kutoka huwezi, Yesu anakuita leo akuokoe,.
Zaburi 69:33 “Kwa kuwa Bwana huwasikia wahitaji, Wala hawadharau wafungwa wake”.
Ukimpokea Yesu, atafanya mabadiliko makubwa katika Maisha yako, atakufungua katika laana nyingi ambazo hata wewe mwenyewe hukuwahi kuzijua, laana za ukoo, na laana za mapepo na majini, ikiwa utakuwa tu tayari leo kusema Bwana Yesu njoo niokoe yote hayo yatafanyika kwako.
Kwahiyo Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Na ukimaliza kufanya hivyo basi Kristo anaanza sasa kuyafanya mabadiliko hayo moyoni mwako, na utaona jinsi anavyokufungua kifungo kimoja mpaka kingine. Kama alitufanyia sisi hivyo, atakufanyia na wewe, Hivyo amini tu na fungua moyo wako!
Pia tazama mafundisho mengine chini tayakusaidia kiroho sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au kwa namba hii +255 789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
RABI, UNAKAA WAPI?
TAZAMA, MWISRAELI KWELI KWELI, HAMNA HILA NDANI YAKE!
TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.
MTETEZI WAKO NI NANI?
KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?
Jina la Bwana libarikiwe.
Kuna kitu kimoja cha kipekee ambacho Mungu katuumbia sisi wanadamu “nacho ni uponyaji wa asili”
Huu uponyaji wa asili upo katika miili yetu na vile vile upo katika roho zetu. Na huo Uponyaji tumepewa bure wanadamu wote kama zawadi na Mungu wetu, na huo hauhitaji uwe mkristo au utumie jina la Yesu kuupata. Upo tu Mungu kauweka ndani ya kila mtu.
Kwamfano unapojikata na kisu mkononi kwa bahati mbaya, inaweza kukuchukua wiki kadhaa tu kupona na nyama yako ikarudi vile vile, au unapoanguka na kuchubuka sehemu ya mwili wako, baada ya wiki kadhaa au mwezi Ngozi yako itakuwa imesharudia katika hali yake kama ilivyokuwa mwanzo, litabaki kovu tu lakini si jeraha!..
Kwahiyo ni kitendo cha muda tu..lakini mwisho wa siku utapona majeraha yako yote. Vinginevyo Mungu wetu asingeuweka huo uponyaji wa asili basi dunia ingekuwa ni jehanamu..pangekuwa si mahali pa kuishi.
Na katika roho ni hivyo hivyo, yapo majeraha ya rohoni ambayo mtu unaweza kuumizwa au kujiumiza mwenyewe. Majeraha hayo yanaweza kutokana na mambo Fulani Fulani ya kimaisha, na hayo pia Mungu kayawekea uponyaji wake wa asili…
Ndio maana unaweza ukakasirika sana sasahivi, ukapita muda kadhaa ile hasira inaanza kutulia na mwishowe inaisha kabisa… hapo ni uponyaji unafanya kazi yake.
Hivyo kama vile tunavyotumia njia za kuponya majeraha ya nje tutumie njia hiyo hiyo kuyatibu yale ya ndani.
Tukiumia kwa majeraha ya nje kama vidonda, huwa tunavisafisha vizuri, tunavipaka dawa na kisha tunavifunga..na kikubwa Zaidi tunahakikisha hatuvitoneshi, baada ya siku moja au mbili tunarudia tena hilo zoezi, mpaka mwishoni tunapona kabisa. Sasa zoezi hilo la kukisafisha na kukifunga na kuzuia kukitonesha ndilo litasaidia kidonda kile kipone haraka, lakini kisipofanyiwa matunzo hayo..basi hakitapona haraka, na matokeo yake kinaweza kuzidi kuwa kikubwa Zaidi na kutengeneza tatizo lingine likubwa zaidi.
Na majeraha ya ndani tunayaponya kwa njia hiyo hiyo. Pale tunapoumizwa na watu au mazingira Fulani kama wakristo, njia ni hiyo hiyo;
Yohana 8:32 “tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru”.
Fanya hivyo siku ya kwanza, rudia tena siku zinazofuata, kila siku soma maandiko, funga, omba na usijikumbushe kumbushe…Kwa kufanya hivyo nakuambia ukweli..Haitapita kipindi kirefu utaona mabadiliko makubwa sana. Utapona majeraha yako ya muda mfupi sana. Kwasababu umeiwekea mazingira yanayofaa, ile nguvu ya uponyaji wa asili kufanya kazi ndani yako.
Lakini usipofanya hivyo..Utakuwa na majeraha ambayo hayaponyeki kila kukicha…Utaishi Maisha ya kuumia kila siku, na ya chuki, na ya vinyongo. Kila mtu utamwona ni adui yako, na kila Neno litakuwa linakuumiza. Utakuwa na majeraha ya miaka 20 iliyopita ambayo hayajapona bado! Utakuwa mtu wa kutokusamehe…Nakuambia ukweli sio mpango wa Mungu kuwa na majeraha ya rohoni kwa miaka 10..Ukiona una kinyongo, au bado unaumia kwa jambo lililotokea miaka 10 au 20 iliyopita..jaribu kutafuta suluhisho mapema..kwasababu kuna uwezekano nguvu ya msamaha haipo ndani yako, na jeraha unapozidi kuliacha huwa ndio linazidi kuwa kubwa kila siku na kuweza kuzaa tatizo kubwa Zaidi ya hilo.
Zaburi 38:5 “Jeraha zangu zinanuka, zimeoza, Kwa sababu ya upumbavu wangu”
Na sababu ya kutopona majeraha ndio hizo hapo juu kutofunga jeraha na kutoweka dawa!.. Unaweza kuwa unatatizo la kutopata mtoto, na ukasikia watu wanakusema vibaya..na hilo likawa ni jeraha kwako!..lakini kama Neno la Mungu halipo ndani yako; kama hujui Habari za akina Sara na wengineo ambao Mungu aliwafungua matumbo katika uzee wao, kama hujui Habari za Hana na Raheli ambao walisemwa kupita maelezo, basi hutaweza kupona haraka jeraha ulilonalo. Kwahiyo Neno la Mungu ndio dawa, inayoharakisha uponyaji wa ki-Mungu.
Zaburi 147:3 “Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuziganga jeraha zao”
Ndicho kinachowakuta watu wasiolijua Neno la Mungu (watu wa kidunia), wanahangaika na majeraha ya muda mrefu yasiyopona kwasababu hawana dawa, wala hawaijui dawa..Hivyo jeraha lolote lililo ndani yako, lisiwe kikwazo cha wewe kuikosa mbingu anza sasa kuusafisha moyo wako.
Mwisho kama hujaokoka, wakati umeenda sana, wakati wowote Kristo anarudi, biblia inasema..itatufaidia nini tuupate ulimwengu mzima halafu tupate hasara za nafsi zetu?. Mambo ya ulimwengu yanapita lakini Neno la Mungu lipo pale pale. Mgueukie leo Kristo, utubu dhambi zako, uoshwe kwa damu yake, ukabatizwe na kisha upokee Roho Mtakatifu, ambaye atakuongoza katika kuijua kweli yote ya maandiko.
Maran atha
SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.
ALIJARIBIWA SAWASAWA NA SISI KATIKA MAMBO YOTE.
MKARIBIE BWANA ZAIDI ILI UFANYIKE NGUZO.
NAO WAKADHANI YA KUWA YUMO KATIKA MSAFARA;
UTASIMAMA PEKE YAKO SIKU ILE.
JIRANI YANGU NI NANI?
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
WAKAKAA KWAKE SIKU ILE. NAYO ILIKUWA YAPATA SAA KUMI.
Shalom, karibu tena tujifunze maneno ya uzima ya Mungu wetu YEHOVA.
Kuna wakati Mungu anaweza kukaa kimya na kuruhusu mambo Fulani yatokee, ili aone watu wake watamzungumziaje kuhusu jambo hilo, Na hapo ndipo tunapopaswa tuwe makini, kwasababu mtu akikosa kujua makusudi ya Mungu ni nini, halafu akamzungumzia tu kutokana na mawazo yake au uonavyo yeye, anaweza kujisababishia hasira yake iwake juu yako.
Kuna jambo moja la namna hiyo ambalo lipo hasaa kwetu sisi watu wa kanisa la Laodikia, ambalo tunamzunguzia Mungu isivyopasa. Kosa hilo lilifanywa na watu wa kale na sisi bado tunataka kulirudia Na leo hii tutaliona katika biblia.
Kosa lenyewe lilifanywa na wale marafiki watatu Ayubu (yaani Elfazi, Sofari na Bildadi). Mawazo yao yalianzia pale, walipoona Mungu kamletea Ayubu majanga makubwa kama tunavyoyasoma katika biblia.. Walipoona ghafla mali za Ayubu zimepukutika, baadaye tena familia yake ikaondoka, na zaidi ya yote, magonjwa ya mauti yakawa yanamwandama…
Hivyo hawa marafiki zake watatu ambao walikuwa ni wenye hekima kweli kama yeye, na wakati mwingine wenye upendo, kiasi kwamba kufunga safari toka mbali kuja kumfariji Rafiki yao, na kulia naye, ni jambo la upendo mwingi..Lakini walikosa kujua kitu kimoja..Wao walidhani kigezo pekee cha mtu kukubaliwa na Mungu ni kuwa na mali, na utajiri, na mafanikio na Maisha mazuri basi…
Hivyo watu wote waliokuwa wanawaona barabarani kama matajiri, na wenye mali, walihitimisha kuwa ni marafiki wa Mungu wakubwa, Halikadhalika wale wanaopatwa na matatizo na shida, wanatumika chini ya laana kubwa ya Mungu..Hilo tu ndilo lilikuwa kikwazo kwao, lakini mengine yote hawakuwa na hatia..
Sasa ulipofika wakati wa Rafiki yao kipenzi Ayubu kukutwa na majanga kama yale, ndipo wakahitimisha kuwa Ayubu sasa kuna mahali alimkosea Mungu, tena mahali pakuwa sana, na hivyo ni lazima akiri, na atubu makosa yake, wakawa wanamshurutisha kwa nguvu, wakijaribu kushuhudia mabaya yake kwa kila namna..kwa kumwambia maneno kama haya:
Ayubu 4:7 “Kumbuka, tafadhali, ni nani aliyeangamia akiwa hana hatia? Au hao waelekevu, walikatiliwa mbali wapi? 8 Kama mimi nilivyoona, hao walimao maovu, Na kupanda madhara, huvuna yayo hayo. 9 Kwa pumzi za Mungu huangamia. Na kwa kuvuma kwa hasira zake humalizika”.
Ayubu 4:7 “Kumbuka, tafadhali, ni nani aliyeangamia akiwa hana hatia? Au hao waelekevu, walikatiliwa mbali wapi?
8 Kama mimi nilivyoona, hao walimao maovu, Na kupanda madhara, huvuna yayo hayo.
9 Kwa pumzi za Mungu huangamia. Na kwa kuvuma kwa hasira zake humalizika”.
Ayubu 8:3 “Je! Mungu hupotosha hukumu? Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki? 4 Kwamba watoto wako wamemfanyia dhambi, Naye amewatia mkononi mwa kosa lao; 5 Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii, Na kumsihi huyo Mwenyezi; 6 Ukiwa wewe u safi na mwelekevu; Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako, Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa. 7 Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka sana.
Ayubu 8:3 “Je! Mungu hupotosha hukumu? Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki?
4 Kwamba watoto wako wamemfanyia dhambi, Naye amewatia mkononi mwa kosa lao;
5 Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii, Na kumsihi huyo Mwenyezi;
6 Ukiwa wewe u safi na mwelekevu; Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako, Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa.
7 Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka sana.
Ayubu 15:34 “Kwa kuwa jamii ya hao wasiomcha Mungu watakuwa tasa, Na moto utateketeza mahema yenye rushwa”.
N.k n.k, hatuwezi kuorodhesha mistari yote hapa, lakini soma kitabu cha Ayubu kuanzia sura ya 4-25, utaona, msimamo wao hao watu jinsi ulivyokuwa mkali na ule ule, Kwamba Ayubu kupatwa na misiba ile ni matokeo ya uovu wake aliomtendea Mungu, Pamoja na familia yake..
Lakini kwasababu Ayubu alikuwa anamjua Mungu vizuri, hakuhitimisha kuwa kupitia shida, au mtu kuwa maskini au kupungukiwa ni kwamba Mungu amekukataa, badala yake alianza kuwaeleza siri ambayo walikuwa hawaijui akawaambia, wapo watu ambao wamemkataa Mungu, ambao hawaamini hata uweza wa Mungu, lakini Mungu huyo huyo anawapa, afya, amebariki kazi za mikono yao, amewafanikisha kwa kila kitu watakacho, na zaidi ya yote wamepewa Maisha marefu, lakini mwisho wa siku watakufa na watashuka kuzimu kwa ghafla…Hivyo kigezo cha kufanikiwa sio kigezo kuwa Mungu amekukubali..
Ayubu 21:7 “Mbona waovu wanaishi, Na kuwa wazee, naam, na kuongezeka kuwa na nguvu? 8 Kizazi chao kinathibitika nao machoni pao, Na wazao wao mbele ya macho yao. 9 Nyumba zao zi salama pasina hofu, Wala fimbo ya Mungu haiwapigi. 10 Fahali wao huvyaza wala hapungukiwi na nguvu; Ng’ombe wao mke huzaa, asiharibu mimba. 11 Huwatoa kama kundi watoto wao. Na watoto wao hucheza. 12 Huimba kwa matari na kwa kinubi, Na kuifurahia sauti ya filimbi. 13 Siku zao hutumia katika kufanikiwa, Kisha hushuka kuzimuni ghafula. 14 Walakini walimwambia Mungu. Tuondokee; Kwani hatutaki kuzijua njia zako. 15 Huyo Mwenyezi ni nani, hata tumtumikie? Nasi tutafaidiwa nini tukimwomba? 16 Tazama, kufanikiwa kwao hakumo mkononi mwao; Mashauri ya waovu na yawe mbali nami. 17 Je! Ni mara ngapi taa yao waovu huzimishwa? Na msiba wao kuwajilia? Na Mungu kuwagawanyia uchungu kwa hasira yake? 18 Ili wawe kama mabua makavu mbele ya upepo, Kama makapi yaliyochukuliwa na dhoruba”?
Ayubu 21:7 “Mbona waovu wanaishi, Na kuwa wazee, naam, na kuongezeka kuwa na nguvu?
8 Kizazi chao kinathibitika nao machoni pao, Na wazao wao mbele ya macho yao.
9 Nyumba zao zi salama pasina hofu, Wala fimbo ya Mungu haiwapigi.
10 Fahali wao huvyaza wala hapungukiwi na nguvu; Ng’ombe wao mke huzaa, asiharibu mimba.
11 Huwatoa kama kundi watoto wao. Na watoto wao hucheza.
12 Huimba kwa matari na kwa kinubi, Na kuifurahia sauti ya filimbi.
13 Siku zao hutumia katika kufanikiwa, Kisha hushuka kuzimuni ghafula.
14 Walakini walimwambia Mungu. Tuondokee; Kwani hatutaki kuzijua njia zako.
15 Huyo Mwenyezi ni nani, hata tumtumikie? Nasi tutafaidiwa nini tukimwomba?
16 Tazama, kufanikiwa kwao hakumo mkononi mwao; Mashauri ya waovu na yawe mbali nami.
17 Je! Ni mara ngapi taa yao waovu huzimishwa? Na msiba wao kuwajilia? Na Mungu kuwagawanyia uchungu kwa hasira yake?
18 Ili wawe kama mabua makavu mbele ya upepo, Kama makapi yaliyochukuliwa na dhoruba”?
Unaona? Hata baada ya kuelezwa maneno hayo, hilo halikuwafanya marafiki wa Ayubu wabadilishe mitazamo yao, msimamao wao bado ulikuwa ni ule ule, kwamba Ayubu kakosea mahali!, ndio maana yale yote yamempata…Mungu kamwe hawezi kuruhusu mabaya kama yale yamkute mja wake..hilo haliwezekani,
Lakini mwisho kabisa mwa kitabu cha Ayubu tunaona Mungu anasimama na kuanza kuzungumza sasa, akamwambia Ayubu maneno yafuatayo..
Ayubu 42:7 “Basi ikawa, baada ya Bwana kumwambia Ayubu maneno hayo, Bwana akamwambia huyo Elifazi Mtemani, HASIRA ZANGU ZINAWAKA JUU YAKO, na juu ya hao rafiki zako wawili; kwa kuwa ninyi HAMKUNENA YALIYO SAWA KATIKA HABARI ZANGU, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu. 8 Basi sasa, jitwalieni ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba, mkamwendee mtumishi wangu Ayubu, mjisongezee sadaka ya kuteketezwa; na huyo mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi; kwa kuwa nitamridhia yeye, nisiwatende sawasawa na upumbavu wenu; kwani ninyi HAMKUNENA MANENO YALIYONYOKA KATIKA HABARI ZANGU, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu”
Ayubu 42:7 “Basi ikawa, baada ya Bwana kumwambia Ayubu maneno hayo, Bwana akamwambia huyo Elifazi Mtemani, HASIRA ZANGU ZINAWAKA JUU YAKO, na juu ya hao rafiki zako wawili; kwa kuwa ninyi HAMKUNENA YALIYO SAWA KATIKA HABARI ZANGU, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu.
8 Basi sasa, jitwalieni ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba, mkamwendee mtumishi wangu Ayubu, mjisongezee sadaka ya kuteketezwa; na huyo mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi; kwa kuwa nitamridhia yeye, nisiwatende sawasawa na upumbavu wenu; kwani ninyi HAMKUNENA MANENO YALIYONYOKA KATIKA HABARI ZANGU, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu”
Ni lipi tunafundishwa?
Kwa bahati mbaya, hata sasa mawazo kama haya mabovu yapo vichwani mwa baadhi yetu (Hususani wahubiri wa leo). Tunamwazia Mungu katika utajiri tu na mafanikio? Na mahubiri yetu kila siku ni hayo, na tunatumia mistari baadhi baadhi ya kusimami, kama walivyofanya wakina Bildadi, Sofari na Elfazi.
Ndugu unayosoma ujumbe huu, ikiwa na wewe unamnenea Mungu maneno kama hayo, ikiwa na wewe unamuhubiri Mungu kwa njia hiyo tu, ikiwa biblia unayoisoma unaona mistari tu kufanikiwa kimwili, na unawafundisha wengine hivyo..angalia sana..Hasira ya Mungu isije ikawa juu yako.
Kumbuka: (Sio kwamba tusihubiri mafanikio, la! Kwa Mungu yapo mafanikio, makubwa sana! lakini usihubiri kwamba wote ambao hawajafanikiwa na maskini wamepungukiwa na kitu kwa Mungu wao, hapo utakuwa hujamzungumzia Mungu vizuri). Hata ufanyaje huwezi elewa njia zote za Mungu, hivyo epuka kulazimisha kila jambo, na kutaka liwe kama wewe unavyotaka liwe. Sio kila mtu mwenye ulemavu ana laana!, sio wote wenye magonjwa ya muda mrefu yasiyopona kafungwa na nguvu za giza!..sio vipofu wote unaowaona au viziwi ni laana inawafuata… Wengine Mungu karuhusu wawe hivyo kwa makusudi yake yeye (kasome Yohana 9:1-3)
Yakobo 2:4 “ Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?”
1Wakoritho 10:11 “Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. 12 Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke”.
1Wakoritho 10:11 “Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.
12 Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke”.
Maran atha!
Je Mungu anawapenda watu wote au ana chuki?
TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.
Jehanamu ni nini?
JAWABU LA MAISHA YA MTU.
KUMTEGEMEA MWOKOZI Lyrics/Swahili.