Madirisha ya mbinguni ni nini/yapi?(Mwanzo 7:11)

Madirisha ya mbinguni ni nini/yapi?(Mwanzo 7:11)

Ni neno lenye maana zaidi ya moja, kwamfano katika vifungu hivyo, Lilimaanisha chemchemi za maji zilizokuwa juu ya anga, Mungu alizifungua, mvua ikaanza kunyesha bila kipimo au kiasi, usiku na mchana kwa  siku arobaini.

Mwanzo 7:11 Katika mwaka wa mia sita wa maisha ya Nuhu, mwezi wa pili, siku ya kumi na saba ya mwezi, siku ile chemchemi zote za vilindi vikuu zilibubujika kwa nguvu, madirisha ya mbinguni yakafunguka.  12 Mvua ikanyesha juu ya nchi, siku arobaini mchana na usiku

Utakumbuka kuwa katika siku ile ya pili ya uumbaji, Mungu aliyatenga maji ya juu na ya chini (Mwanzo 1:6-7). Sasa yale ya juu, aliyaachia yote, yakawa yanashuka juu ya nchi na matokeo yake yakaifunika tena dunia. Hayo ndio madirisha ya mbinguni yaliyofunguliwa.

Ni neno pia linalomaanisha, Baraka za Mungu nyingi.

Kwamfano katika vifungu hivi, lilimaanisha hivyo;

Wafalme 7:2 Basi yule akida, ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu, akasema, Tazama, kama Bwana angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula.

Hichi ni kile kipindi, Israeli imepitia njaa kali kiasi cha watu kulana, lakini Elisha akatokea na kumwambia Yule mkuu wa mfalme, kwamba Bwana atawaletea Baraka nyingi siku hiyo, na chakula kitakuwa kama si kitu tena Israeli. Yeye akadhihaki na kusema hata kama Mungu akifungua milango yake yote ya mbinguni  (Baraka) hilo jambo haliwezekani ndani ya siku moja. Elisha akamwambia utaliona kwa macho yako, lakini hutakula chochote katika hivyo.

Vilevile katika vifungu hivi, utaona vikimaanisha Baraka pia;

Malaki 3:10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

Bwana anataka tumjaribu kiutoaji, ndipo atafanya muujiza wa kutufungulia Baraka zake nyingi ambazo hazitatosha hata mahali pa kuzihifadhia.

Hivyo Neno hili kibiblia lilimaanisha, hukumu ya Mungu iliyopitiliza, au Baraka za Mungu zilizopitiliza kufuata na tukio lenyewe lililoambatana nalo.

Bwana akubariki.

Je! Unatamani kushiriki Baraka zote za Mungu rohoni? Unatamani madirisha ya mbinguni yafunguliwe juu yako. Kama ni ndio basi sharti uokoke, umkabidhi Kristo maisha yako, kwa kutubu dhambi zako na kuwa tayari kumfuata Kristo, ili upate ondoleo la dhambi zako.

Ikiwa utapenda mwongozo wa sala ya kumpokea Kristo, baada ya toba yako ya kweli. Basi fungua hapa kwa sala hiyo>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

NUHU WA SASA.

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU BARAKA

Nini maana ya huu mstari; Mithali 10:22 “Baraka ya Bwana hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo”

JE NI KIKOMBE KIPI UTAKINYWEA SIKU ILE?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments