Swali: Kitani ni nini, na Bafta ni nini? Kama tunavyosoma katika Isaya 19:9?
Jibu: Turejee.
Isaya 19:9 “Tena wao wafanyao kazi ya kuchana KITANI watafadhaika, na hao pia wafumao BAFTA”.
1.KITANI
“Kitani” ni aina ya mmea unaostawi kwa sana maeneo ya mashariki ya kati, mbegu za mmea huu hutumika kwa matibabu lakini pia nyuzi zake hutumika kati kutengenezea mavazi mbalimbali ikiwemo mavazi ya harusi.
Ufunuo 19:7 “Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari. 8 Naye amepewa kuvikwa KITANI NZURI, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu. 9 Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu”.
Ufunuo 19:7 “Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.
8 Naye amepewa kuvikwa KITANI NZURI, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.
9 Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu”.
Lakini si tu mavazi ya harusi bali pia ilitumika katika kutengenezea sanda za maziko.
Yohana 19:40 “Basi wakautwaa mwili wake Yesu, wakaufunga sanda ya KITANI pamoja na yale manukato, kama ilivyo desturi ya Wayahudi katika kuzika”
Mistari mingine inayozungumziwa mavazi ya Kitani ni pamoja na Mithali 31:22, Ezekieli 44:17, Danieli 10:4-5,Marko 14:51 na Ufunuo 18:16.
Vazi la kitani kiroho linafunua “Matendo ya Mtu” ikiwa ni kitani safi bali ni matendo safi, (Sawasawa na Ufunuo 19:8) lakini ikiwa ni kitani iliyoharbika, basi maana yake ni matendo yaliyoharibika.
2. BAFTA.
“Bafta” ni Kiswahili kingine cha “Pamba”.. Zao la pamba mbali ni kutumika katika matibabu, linatumika sana pia katika utengenezaji wa mavazi. Nyuzi za kitani zilitumika kutengeneza mavazi magumu nay ale ya nakshi, lakini pamba hutumika kutengenezea mavazi au mapazia yenye nyuzi laini na zenye kuhifadhi joto.
Ezekieli 9:11 “Na tazama, mtu yule aliyevaa bafta, mwenye kidau cha wino kiunoni, akaleta habari, akisema, Nimefanya kama ulivyoniamuru”.
Mistari mingine inayotaja mavazi na mapazia ya Bafta ni pamoja na Esta 1:6, Ezekieli 9:2 na Ezekieli 10:7.
Je unaye YESU maishani mwako?.. ni vazi gani ulilonalo kiroho?.. je ni kitani nyeupe? Au iliyoharibika? Je unayatunza mavazi yako au umeyaacha yaharibike?.. Kwa maarifa Zaidi ya namna ya kutunza mavazi yako kiroho fungua hapa >>USIYAACHE MAVAZI YAKO NA KWENDA UCHI!
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Naivera ni nini? Kwanini Daudi aliihitaji alipomtafuta Mungu?
JE! UNAYATUNZA MAVAZI YAKO?
VAA MAVAZI, USIVALIE MAVAZI.
MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.
MAUTI NA UZIMA HUWA KATIKA UWEZO WA ULIMI.
Rudi Nyumbani
Print this post