Swali: Bwana YESU alisema pepo anapomtoka mtu na baadaye akirudi na kukuta nyumba yake imefagiliwa na kupambwa huenda kuchukua pepo wengine saba,.. maaa yake nini kusafishwa na kupambwa?.. je mapepo wanapenda sehemu safi?
Jibu: Awali ya yote tuisome mistari hiyo.
Luka 11:24 “Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema,
25 Nitairudia nyumba yangu niliyotoka.
26 Hata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza”.
Sasa kabla ya kujua nini maana ya “kufagia na kupambwa” hebu tuelewe kwanza maana ya nyumba kiroho..
Maandiko yanasema Miili yetu ni Hekalu la Roho Mtakatifu..
1 Wakorintho 6.19 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu”.
Soma pia 1Wakorintho 3:16 utaona jambo hilo hilo..
Sasa kama miili yetu imekusudiwa iwe Hekalu/nyumba ya Roho Mtakatifu, maana yake ni kwamba isipokaliwa na Roho Mtakatifu basi itakaliwa na roho chafu za mapepo, maana yake badala ya mwili kuwa Nyumba ya Roho Mtakatifu, sasa inakuwa ni nyumba ya mapepo.
Hivyo mpaka hapo tumeshaelewa kuwa Nyumba inayozungumziwa hapo katika Luka 11:25-26, si nyingine zaidi ya miili yetu.
Sasa swali la pili: Nini maana ya kupambwa na kufagiliwa.
Hebu tena tutumie maandiko tujue mapambo ya nyumba ya Mungu (yaani miili yetu) ni yapi, na mapambo ya mapepo ni yapi.
1Petro 3:3 “Kujipamba kwenu, KUSIWE KUJIPAMBA KWA NJE, YAANI KUSUKA NYWELE; NA KUJITIA DHAHABU NA KUVALIA MAVAZI;
4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.
5 Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao”.
Angalia mstari wa tatu (3) anasema.. Kujipamba kwenu KUSIWE!, Zingatia hilo neno KUSIWE!!.. Maana yake ni kwamba mapambo yake ni kwamba mapambo yafuatayo si ya ki Mungu bali ni ya Ibilisi, ndio maana anasema hapo KUSIWE!.. Sasa hebu tuendelee tuangalie hayo mapambo..
…”Kujipamba kwenu, KUSIWE KUJIPAMBA KWA NJE, YAANI KUSUKA NYWELE; NA KUJITIA DHAHABU NA KUVALIA MAVAZI..”
Oo kumbe! kuweka wigi, kuvalia mavazi (ya kikahaba), na kuvaa dhahabu masikioni na shingoni na vikuku miguuni na mikononi ni mapambo ya mapepo, na tena tumeshaona kuwa “nyumba” tafsiri yake kiroho ni “miili yetu”, hivyo tunapoweka hereni masikioni, wigi kichwani, cheni shingoni na vikuku miguuni, tafsiri yake ni kwamba nyumba zetu (yaani miili yetu) tumeipamba kwa mapambo ya kipepo, ambayo yale mapepo yakiona yanafurahi na kwenda kutafuta pepo wengine saba, na kurudi kumwingia mtu.. Hii ni ajabu sana!.
Na ndio maana wengi (wanaume na wanawake) wanaopamba miili yao na kuvaa kikahaba wanakuwa wanasumbuliwa na mapepo na ndoto mbaya!, kwanini?..kwasababu miili yao ni nyumba iliyofagiliwa na kupambwa..
Sasa utauliza kufagiliwa ni kufanya nini?…Kufagiliwa ni maandalizi ya mapambo!..Maandalizi yote ya kiroho na kimwili kabla ya mtu kujitia mapambo ya nje ni “kufagia”..
Lakini hebu tuangalie mapambo ya ki MUNGU ni yapi!.. Tuendelee na mistari ile..
“Kujipamba kwenu, KUSIWE KUJIPAMBA KWA NJE, YAANI KUSUKA NYWELE; NA KUJITIA DHAHABU NA KUVALIA MAVAZI;
4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu”.
Bali anasema mapambo yetu yawe Utu wa moyoni, yaani Roho ya Upole, na utulivu (kwa ufupi utakatifu).
Je! mama, dada, au kaka ni mapambo gani unayo?..ya nje au ya ndani??.. ni kweli utaonekana wa kisasa, unayekwenda na wakati, lakini fahamu kuwa mapambo hayo ndio mapepo wanayoyaangalia.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10 atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.
Je mapepo au majini yanaweza kuviingia vitu visivyo na uhai?
SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.
Je kupiga miayo ni ishara ya mapepo?
Kwanini Bwana Yesu, aliruhusu yale mapepo yawaingie nguruwe?
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
SWALI: Nini Maana ya Mithali 15:24?
Kwa mtu mwenye akili njia ya uhai huenda juu; Ili atoke katika kuzimu chini.
JIBU: Hapo yapo mambo matatu,
Mtu mwenye akili ni mtu mwenye uwezo wa kufikiri/kupambanua vema na kufanya maamuzi sahihi katika maeneo mbalimbali ya maisha yake. Hivyo hapo anasema mtu mwenye akili anajua vema kuichagua njia yake ya uhai.
Anasema njia yake hutoka chini kuelekea juu. Kwa lugha ya picha ni barabara iliyopinduliwa na kusimamishwa wima kama ngazi, na sio mfano wa barabara hizi tulizonazo zilizolala chini, ambazo uelekeo wake ni aidha kaskazini na kusini, au mashariki na magharibi.
Sasa hapa anasema njia yake ya uhai huenda juu, ili atoke kuzimu chini. Akiwa na maana husafiri kutoka kuzimuni kuelekea uzimani juu kwa Mungu.
Hufunua nini?
Safari ya mtu mwenye akili, hufikiri kumtafuta Mungu juu alipo,
Wakolosai 3:1 Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. 2 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.
Hufikiri ukuaji wa kiroho, atokea hatua moja ya utakatifu kwenda nyingi, kiwango kimoja cha Imani kuelekea kingine kama Kristo (2Petro 1:5-10, Waefeso 4:13). Ni mtu ambaye kila siku anakwenda mbali na njia ya mauti. Mawazo yake yapo juu sikuzote kumjua Kristo na mapenzi yake yote.
Lakini kinyume chake ni ukweli, mtu asiye na akili barabara yake haijasimama wima, bali imelala. Atawaza atoke hatua moja kwenda nyingine lakini hakuna ukuaji wowote au kuongezeka kokote. Huwenda anachowaza tu sikuzote ni kutoka katika umaskini kwenda katika utajiri, kutoka katika kiwango kimoja cha elimu kwenda kingine, kutoka katika cheo kimoja kwenda katika kingine..Hatua zake ni za kidunia tu, akidhani ndio uzima wake upo hapo. Kumbe kapotea njia.
Si kwamba vinapingwa vya dunia hapana, ni vizuri na vinafaa, lakini havina uzima wa milele ndani yake. Ili uwe na akili hakikisha unampokea Kristo, kisha unaanza kukua kiroho, kila siku unafikiri njia ya kuyakimbia machafu ya kidunia. Hapo barabara yako itakuwa umesimama kama ngazi na hivyo utaiponya nafsi yako.
Je! Umeokoka?. Kama ni la! Basi wakati ndio sasa fungua moyo wako mkaribishe Yesu akuokoe hizi ni nyakati za hatari, tubu leo upokee wokovu. Ikiwa upo tayari kumkaribisha Kristo moyoni mwako, basi waweza kubofya hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba. Bwana akubariki. >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Mpumbavu ni nani katika biblia? (Zaburi 14:1, Mithali 10:14)
Biblia inasema nini kuhusu mtu ‘Mwenye kujipendekeza (Mithali 29:5)
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Zaburi 22:1 Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha? Mbona U mbali na wokovu wangu, Na maneno ya kuugua kwangu? 2 Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibu Na wakati wa usiku lakini sipati.
Maneno haya ukiyatafakari, utagundua ni ya mtu aliyefikia hatua mbaya sana ya kukaribia kukata tamaa kwasababu ya aidha magumu, au huzuni, au mateso yasiyoelekeza anayoyapitia, akiangalia kulia, haoni tumaini lolote, akiangalia kushoto haoni mkono wowote wa Mungu ukimsaidia licha ya kuomba na kulia sana, kwa muda mrefu.
Sehemu nyingine anasema, amekataliwa kila kona, amekuwa kama msikwao kwa ndugu zake.
Zaburi 69:10 Nilipolia na kuiadhibu roho yangu kwa kufunga, Ikawa laumu juu yangu.
11 Nilipofanya gunia kuwa nguo zangu, Nikawa mithali kwao. 12 Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za walevi hunidhihaki. 13 Nami maombi yangu nakuomba Wewe, Bwana, Wakati ukupendezao; Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Katika kweli ya wokovu wako.
14 Uniponye kwa kunitoa matopeni, Wala usiniache nikazama. Na niponywe nao wanaonichukia, Na katika vilindi vya maji. 15 Mkondo usinigharikishe, wala vilindi visinimeze, Wala shimo lisifumbe kinywa chake juu yangu.
16 Ee Bwana, unijibu, maana fadhili zako ni njema, Kwa kadiri ya rehema zako unielekee. 17 Wala usinifiche uso wako, mimi mtumishi wako, Maana mimi nimo taabuni, unijibu upesi.
Mwandishi huyu alikuwa ni Daudi, alipitia kipindi kirefu sana cha kujiona kama vile Mungu kamtupa, hadi kuna wakati akaona heri aende kuomba hifadhi kwa maadui zake wafilisti ambao hapo mwanzo aliwafukuza na kuwaita makafiri (wasio tahiriwa), lakini safari hii kwa unyenyekevu wote, anaenda kuwa mmoja wa askari wao, ili tu apate hifadhi, asiangamie kabisa. Huyo ni mtu ambaye maji ya shingo yalimfikia kwelikweli.
Sio kwamba alikuwa haombi, au hamlili Mungu?. Au kwamba ana dhambi kuliko wengine, mpaka awe mtu wa bahati mbaya hivyo Hapana, nyakati zote alikuwa mwombaji, lakini akafika mahali katika uhalisia wa kibinadamu aliona kama Mungu amemwacha kabisa.
Lakini kwasababu huruma za Mungu zilikuwa nyingi juu yake alimpa moyo mkuu, wa kuendelea kumngoja Bwana. Ndio maana sehemu nyingi katika Zaburi anasisitiza sana Neno hili ‘mngojeeni Bwana’ (Zaburi 37:7, 25:3, 31:24,38:15, 40:1).
Sasa moja ya maneno machache ya Daudi yaliyonikuliwa na Bwana Yesu lilikuwa ni hili.
Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha?
Mathayo 27: 45 Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa.
46 Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
Je! Unadhani kauli hiyo Yesu aliyoitoa alimaanisha kweli ameachwa?
Hapana, tangu mwanzo alikuwa anajua Mungu yupo pamoja naye, na kwamba saa yake imekaribia, muda si mrefu anakwenda kuinuliwa na kutukuzwa, tena sehemu nyingine anasema alishangalia pale msalabani (Wakolosai 2:15). Lakini kuinukuu kauli ile ni kuonyesha ubinadamu wetu, unavyoweza kutuhubiria tuwapo katikati ya shida, kwamba Mungu ametuacha hususani pale tunapopitia shida, na mateso.
Yesu alinukuu ubinadamu wetu kukumbuka mfano wa yale aliyoyapitia Daudi..
Lakini tunaona dakika chache baada ya pale, pindi tu alipokata roho, makaburi yakapasuka, wafu wakatoka makaburini, pazia la hekalu likapasuka, na baada ya siku tatu akafufuka, ukombozi wetu mkuu ukapatikana, ‘Lakini ni kwa maneno ya kudhaniwa kuwa Mungu amemwacha’.
Mathayo 27:50 Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.
51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka;
miamba ikapasuka; 52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; 53 nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.
Ndugu, upitiapo hatua hizo ambazo mawazo yako yanakufundisha kuwa Mungu hayupo na wewe tena, amekuacha, kwasababu ya shida unazozipitia muda mrefu, magonjwa yasiyokoma, umeomba mpaka umechoka, umelia hadi ukomo,wewe ona ni kawaida,…. Piga moyo konde Mngojee Bwana. Daudi alistahimili hatimaye akathibitishwa kwenye ufalme ambao ulidumu pamoja na vizazi vyake vingi tofauti na wafalme wengine wa Israeli. Mngojee Bwana, kimaombi, kwasababu baada ya joto huja mvua.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Nzi wa Misri, na Nyuki wa Ashuru vilimaanisha nini? (Isaya 7:18-20).
1Petro 2:9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
JIBU: Katika vifungu hivyo biblia inaeleza kwa ukubwa sifa zetu sisi tuliomwamini Yesu Kristo, jinsi zilivyo kuu, anasema sisi ni mzao mteule, na pia watu wa milki ya Mungu. Lakini sifa nyingine ndio hiyo ya ukuhani wa kifalme.
Angeweza kusema sisi ni ukuhani wa kisomi, au ukuhani wa kiroho, au ukuhani ki-mbingu, au ukuhani wa kitajiri. Lakini anatumia Neno ukuhani wa kifalme. Ikiwa na maana kuwa tunao ukuhani lakini si ukuhani tu bali wenye asili ya kifalme.
Sifa kuu ya kuhani, ni kuweza kumkaribia Mungu kusema naye, na kufanya upatanisho kwa ajili ya watu wengi. Mfano wa Haruni na uzao wake. Tunaona hawa tu ndio waliopewa neema ya kuweza kumkaribia Mungu katika kiti chake che rehema, kuzungumza naye na kuomba rehemu kwa taifa zima. Wengine wote walikaa nje ya hema.
Lakini pia sifa ya mfalme ni uweza, mamlaka, nguvu, na utajiri. Mfalme anatawala, mfalme ana nguvu ya kijeshi, mfalme ni lazima awe tajiri na mwenye utiisho.
Sasa tukirudi kibiblia, Haruni na walawi wote ambao waliopewa sifa ya kikuhani, hawakuwa na ukuhani wa kifalme ndani yao. Waliishia tu kukaa hemani, na sio ni makuhani na wakati huo huo ni wafalme, lakini pia wafalme wengi (Mfano wa Daudi, Sulemani n.k.)hawakuwa na ukuhani pia ndani yao.. Hivyo waliishia tu kutawala lakini sio kuingia hekaluni kuvukiza uvumba. Alitokea mfalme mmoja kujaribu kufanya kazi hizo mbili kwa wakati mmoja, aliishia kupata ukoma kwasababu hakukuwahi kutokea mtu mwenye uwezo huo wa kutembea katika vyeo vyote viwili kwa wakati mmoja (2Nyakati 26:16-21).
Lakini yupo aliyetabiriwa na manabii kuwa atakuwa kuhani mkuu lakini pia mfalme. Na huyo si mwingine zaidi ya Bwana wetu Yesu Kristo. (Waebrania 7:11-17), Yeye alikuwa kuhani lakini pia alitokea katika kabila la kifalme la Yuda, kwa jinsi ya mwili.
Na mpaka sasa anatawala kama kuhani mkuu wetu, lakini pia mfalme wetu. Amewazidi makuhani wote, amewazidi wafalme wote.
Hivyo na sisi tuliozaliwa na yeye, tunarithi vyote alivyonavyo, maandiko yanasema hivyo (1Petro 1:3-4), Tunafanyika sio tu makuhani, ambao tunamkaribia Mungu kusema naye ana kwa ana, na kuwapatanisha wengine na yeye, lakini pia tunafanyika wafalme wenye mamlaka yote, na nguvu, na utajiri.
Sisi tumepewa mamlaka ya kukanyaga nge na nyoka, na nguvu zote za Yule mwovu, mamlaka ya kupooza kila aina ya magonjwa na madhaifu, mamlaka ya kufungua na kufunga jambo lolote. Vilevile tumepewa na utajiri wote wa hekima na maarifa ndani ya Yesu Kristo (Waefeso 1:3).
Na zaidi mamlaka ya ufalme tuliyonayo itakuja kudhihirika vema mbeleni kwenye utawala wa miaka 1000 wa amani wa Yesu Kristo duniani. Jinsi tutakavyo milika na kutawala na yeye kama wafalme, na yeye akiwa kama mfalme wa wafalme. (Ufunuo 19:16)
Ufunuo 5:10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.
Je!, umeipokea neema hii?
Ni nini unachosubiri usimpe Kristo maisha yako? Tafakari ahadi kubwa namna hii unapewa bure, ni nani anayeweza kufanya hivyo? Saa ya wokovu ni sasa, na wakati uliokubaliwa na Mungu ndio huu, okoka leo, usamehewe dhambi zako, jina lako liandikwe katika kitabu cha uzima.
ikiwa upo tayari kumpokea Yesu, basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Nini maana ya “Uweza wa kifalme utakuwa begani mwake” (Isaya 9:6)?.
JIBU: Swali la kwanza la kujiuliza, je! mkristo ni mtu gani?..Mkristo ni mtu aliyemwamini,Yesu Kristo, kisha akapokea msamaha wa dhambi,kwa toba ya kweli, ubatizo na kutiwa muhuri na Roho Mtakatifu.
Mtu wa namna hiyo anakuwa na Kristo ndani yake. Na mtu mwenye Kristo Hawezi kuwa na mapepo, kwasababu Yesu hana pepo.
Vifungu hivi vinatuthibitishia kuwa hilo jambo haliwezekani;
1 Yohana 4:4
[4]Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.
2 Wakorintho 6:14
[14]Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
Kuonyesha kuwa giza na nuru haviwezi kuwepo sehemu moja, wakati mmoja.
Lakini swali linakuja inakuwaje kuna baadhi ya watu waliokoka wanaonekana kuwa na mapepo ndani yao?
Kama tulivyoona mkristo hawezi kuwa na mapepo, lakini ni vema kufahamu kuwa kuna tofauti kati ya kukaliwa na mapepo, na kushambuliwa na kipepo.
Mtu aliyeokoka hawezi kukaliwa na mapepo, lakini anaweza akashambuliwa au kusumbuliwa na uwepo wa mapepo, hicho ndicho kinachoweza kumtokea, lakini sio kwamba ana mapepo ndani yake.
Sababu zinazoweza mpelekea asumbuliwe nayo, ni hizi kuu tatu;
Tukianza na sababu ya kwanza.
Kukosa kujua nafasi na mamlaka uliyo nayo ndani ya Kristo, shetani anaweza kukusumbua kwelikweli. Na wakati mwingine kukutesa. mapepo yanaweza kuwasumbua watu kifikra na kwa kuwawekea mawazo machafu akilini mwao, kuwashitaki, kwa kuwatupia ndoto mbaya, au kuwakaba usiku, au kuwaletea majaribu mbalimbali, lakini huyu mtu akijua kuwa ameshakabidhiwa mamlaka yote ya kukanyaga nge na nyoka na nguvu zote za yule mwovu,(Luka 9:1), akaitumia vema, shetani atamwogopa kumsogelea kwasababu anajua nguvu ya kimamlaka iliyo ndani yake ni thabiti haitoki mdomoni bali inasukumwa na ufalme wa Mungu ulio nyuma yake.. Ni sawa na mtu anayetoa amri kwa kinywa chake mwenyewe na yule anayetoa kwa agizo la raisi watu watamwogopa yule anayetoa kwa mamlaka aliyopewa na raisi. Hivyo ni muhimu sana kuitafakari na kuiamini mamlaka uliyopewa na Kristo ndani yako ili hayo maroho unapoona dalili ya kutaka kukusumbua unatamka jina la Yesu mara moja tu yanatetemeka na kukimbia. Mamlaka hiyo amepewa mkristo yoyote aliyeokoka, haijaishi ni mchanga au mkomavu.
Ukiokolewa, kwasababu ya kutoondoka mara moja kwa baadhi ya tabia, au msingi au mienendo ya kale, hivyo tabia hizo mara nyingine zinakuwa ni upenyo wa uwepo wa kipepo kuzunguka zunguka karibu yako. Vitu vichanga sikuzote hushambulika kirahisi, unyasi ukiwa mdogo hutikiswa sana na upepo, Ndio maana ni lazima uanze kuukulia wokovu, kwa kujifunza Neno, kujizoesha utakatifu, maombi, ibada, mambo ambayo adui hapendi kwasababu ni kama moto kwao. Mtu asipokuwa mkristo wa vitendo, sikuzote atasumbuliwa na roho za kidunia, na hatimaye atajiona kama ni ana mapepo kabisa, na akiendelea kuishi hivyo, mpaka kurudi nyuma atakufa kiroho, na Roho Mtakatifu kuondoka ndani yake, na mapepo ndio yatapata nafasi ya kumtawala kabisa. (2Petro 1:5-10)
Mtu aliyeokoka, akaanza kutenda dhambi za makusudi, anarudia yale yale kila siku, jambo hilo ni upenyo mwingine wa mapepo kumsumbua, kwasababu anakuwa ameyapa nafasi, na maandiko yanasema tumsimpe ibilisi nafasi. (Waefeso 4:27).
Kwamfano umeacha ulevi, baada ya kuokoka, na umekuwa hivyo kwa muda mrefu sasa, halafu ghafla unaanza tena kuwa mlevi, Mungu anakuonya uache hutaki, unaendelea kunywa pombe..kitendo hicho kinaweza kukupelekea kusumbuliwa sana na mapepo. Mfano tu wa Yule ambaye anatawaliwa nayo.
Mathayo 12:43 Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika,asipate.
44 Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na
kupambwa.
45 Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye
mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.
Hivyo kwa hitimisho, ni kuwa mtu aliyeokoka, hawezi kukaliwa na mapepo, yaani kutawaliwa au kupagawishwa, au kuendeshwa nayo.. Isipokuwa anaweza kushambuliwa, kusababishiwa madhara, lakini kuvamiwa na uwepo wao. Ndio maana tumeambiwa tuvae silaha zote za haki, ili tuweze kumpinga shetani (Waefeso 6:10). Kwa kulijua Neno, utakatifu, maombi, na ibada.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Mbona ni maskini tu huwa ndio wanaolipuka mapepo, na sio matajiri?
DALILI TISA (9) ZA PEPO KUWEPO NDANI YA MTU.
Je mtu anaweza akawa hajaokoka akaombea mtu na Pepo likamtoka,
Je huu mji mtakatifu shetani aliomchukua Bwana katika Mathayo 4:5 ni mji gani?.. maana tunajua shetani hawezi kumiliki vitu vitakatifu?
Jibu: Turejee..
Mathayo 4:5 “Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu.
6 akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako”.
Mji Mtakatifu unaozungumziwa hapo ambao shetani alimpeleka Bwana YESU ni YERUSALEMU (Ya duniani) iliyopo pale Israeli..
Kumbuka ipo YERUSALEMU YA MBINGUNI, ambayo itakuja kushuka baada ya hukumu ya mwisho, na Yerusalemu hiyo Mpya shetani hawezi kufika wala watu ambao hawajamwamini Bwana hawataingia (kulingana na maandiko).
Ufunuo 21:1 “Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao”.
Ruka mpaka mstari wa 23-27..
“23 Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo.
24 Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.
25 Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku.
26 Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake.
27 Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo”.
Lakini Mji shetani aliompeleka Bwana ulikuwa ni Yerusalemu ya duniani, (ule mji ule wa Daudi), mahali pale ambapo Hekalu la Sulemani lilijengwa..Yerusalemu hii ya duniani shetani anaweza kufika wakati wowote na mtu mwingine yoyote anaweza kufika, (awe mtakatifu au asiwe mtakatifu), anaweza kufika, na hata leo watu wanafika pale..
Na shetani alimpomfikisha Bwana YESU katika Hekalu, alimpandisha mpaka kwenye kinara chake, na kumwambia ajirushe chini, kwa maana imeandikwa atawaagiza malaika nao watamwokoa na ajali ile (sawasawa na Zaburi 91:11-12).
Lakini Kwakuwa Bwana YESU alikuwa amejaa Roho Mtakatifu, alizijuza hila na mbinu zote za ibilisi, na aliweza kumjibu kwa Neno, kuwa imeandikwa tusimjaribu Bwana MUNGU wetu.
Ni jambo gani tunaweza kujifunza hapo?
shetani anapotaka kumjaribu mtu anayemcha MUNGU hampeleki kwa waganga wa kienyeji, wala hampeleki kwenye mazingira ya dhambi ili atende dhambi, bali anampeleka sehemu takatifu, kama kanisani, au katikati ya watu wanaomtafuta MUNGU,
Ndio maana utaona leo mtu amesimama lakini anaanguka/anaangushwa katika dhambi na mtu/watu wa kanisani.
Utaona Askofu, au mchungaji, au mwinjilisti, au Nabii, au Mtume au mwimbaji wa kwaya anaanguka katika uzinzi na watu wa kanisani, ni mara chache sana na watu wa nje, kwanini?.
Kwasababu shetani anajua sehemu pekee ya kumjaribu mtu aliyeokoka na kusimama ni kanisani, akimletea wanaojiuza huko barabarani ni ngumu kuanguka..
Ndicho alichotaka kujaribu kufanya kwa Bwana YESU kumpeleka Hekaluni, kwanini asingempekeka kwenye vinara vingine vya mahali pengine, badala yake akachagua Hekalu?.. ni kwasababu alijua hapo ni rahisi kumwangusha Bwana.
Hivyo na sisi tuliookoka ni muhimu kuwa makini katika nyumba ya MUNGU kwani huko huko shetani anaweza kupata nafasi.
Bwana atusaidie.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 2)
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 3)
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)
Je! Yesu aliwezaje kuchukuliwa na shetani juu ya kinara cha hekalu kujaribiwa?