Mwanzo 2:8-9 “Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.
9 Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya”.
Tukisoma katika mistari hii hapa juu, tunaona kabisa mwanzoni Mungu alipopanda bustani mashariki mwa Edeni Mungu aliiweka miti ya aina tatu bustanini nayo ni:
Hapa usichanganye hii ni miti aina tatu tofauti yenye tabia tatu tofauti tofauti, tukianzana na mti wa kwanza,
Sasa mti wa aina hii unaozungumziwa hapa biblia inasema Mungu alichepusha katika ardhi ”KILA” mti unaofaa kwa chakula, tunaona hili neno “KILA” linamaanisha ni miti mingi na sio mti mmoja, mfano wa miti hii ni mapeasi, matofaa, maembe,mananasi, ndizi, mapasheni,mapapai n.k. hii ni miti aina ya kwanza ya mti ambayo Mungu aliichepusha katika ardhi kwa ajili ya chakula cha mwanadamu kumfaa kwa ajili ya mwili wake na mahitaji yake akiwa bustanini, yeye pamoja na wanyama wake wote Bwana aliompa. Adamu hakupewa masharti juu ya miti hii alikuwa na uhuru wa kula jinsi apendavyo na jinsi atakavyo kama biblia inavyosema.
2. Mti wa uzima katikati ya bustani.
Huu ni mti aina ya pili ambao Bwana aliuweka bustanini, tunaona kuwa mti wa pili na watatu imebeba tabia, na hii miti miwili ya mwisho ipo mmoja, mmoja tu. sio mingi kama ile aina ya kwanza ya mti, sasa huu mti wa uzima. Huu mti ulikuwa hauonekani kwa macho, kama miti mingine, na ulikuwa ni mti ambao ukila matunda yake (sio kula kwa mdomo) unapata uzima ambao umebeba ule uzima wa milele. Kwahiyo huu mti Mungu aliuweka kama hazina kwa Adamu endapo ikitokea wameupoteza ule uzima, waende kula matunda yake wapate uzima tena, Mungu kwa kujua kuwa mwanadamu baadaye atapoteza uzima aliuumba huu mti kuwa kama akiba ya tiba baadaye. Na huu mti Adamu hakuwa na matumizi nao kwasababu tayari alikuwa na uzima wa milele ndani yake.
Lakini tunaona baadaye Adamu alipodondoka kwenye dhambi na kupoteza uzima ndani yake alitamani kwenda kula matunda ya mti wa uzima lakini njia yake ilikuwa imeshafungwa ikilindwa mpaka wakati ulioamuriwa wa hiyo njia kufunguliwa ufike.kwahiyo ilipasa mwanadamu aijue hiyo njia ni ipi. soma mwanzo 3:24. kuanzia hapo wanadamu ndipo walipoanza kufa na kuanza kutafuta suluhisho la kuishi milele tena, na ndipo hapo wanadamu walipoanza kuliitia jina la BWANA, mwanzo 4:26
Lakini sasa sisi tunaoishi wakati huu wa neema tunajua NJIA ni ipi?… na huo MTI WA UZIMA ni nani?… na MATUNDA yake ni nini?..na tunajua sio mwingine zaidi ya BWANA wetu YESU KRISTO mwokozi wetu Haleluya!! .Kwa ufafanuzi mfupi wa jambo hili tusome maandiko yafuatayo…
Yohana 14:6″ Yesu akamwambia, Mimi ndimi NJIA, na KWELI, na UZIMA; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” Unaona hapo!?? hakuna njia yoyote sisi tunaweza kumfikia Baba kama ilivyokuwa hapo mwanzo kabla ya Adamu kuasi isipokuwa kwa njia ya YESU tu! na pia tena ukisoma
Yohana 6:47-51″ Amin, amin, nawaambia, Yeye aaminiye yuna UZIMA WA MILELE.
48 Mimi ndimi chakula cha uzima.
49 Baba zenu waliila mana jangwani; wakafa.
50 Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mtu akile wala asife.
51 Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ATAISHI MILELE. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.”
Maandiko hayo hapo juu yanaonyesha wazi kabisa kuwa hakuna uzima wa milele mahali pengine popote nje ya BWANA YESU KRISTO, matunda ya porini siku zote hayajawahi kumpa mtu uzima wa milele, kwahiyo mtazamo wa kuwa matunda ya mti wa uzima ni matunda yafananayo na ya mwituni sio sahihi,(ni kukosa tu Roho ya mafunuo) kwasababu matunda ya kawaida hayawezi kutupa sisi uzima wa milele, biblia inasema hakuna wokovu wowote nje ya Yesu Kristo, Hivyo basi maana ya kula matunda ya mti wa uzima ni kulitafakari na kuliamini NENO la Bwana Yesu tu, na kusafishwa kwa damu yake ambaye yeye ndiye huo mti wa uzima. Na hili NENO la Mungu ndilo liletalo Utii,Upendo,Amani,Uvumilivu,Fadhili,Kiasi,Utakatifu,Utu wema,Hekima,Haki n.k.
Wagalitia 5:22″ Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria”.
3.Mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
Kama tulivyouona mti wa pili, haukuwa mti wa kawaida kama ule wa kwanza, ndivyo ulivyo na huu pia, mti huu nao upo mmoja na umebeba tabia ya kipekee kwamba ukila matunda yake, utapata maarifa ya ujuzi wa mema na mabaya na ndio mti pekee Mungu aliomkataza mwanadamu asiule, alimwambia kabisa siku atakapokula tu matunda ya mti ule atakufa hakika. Lakini mwanadamu alikaidi akala na ikapelekea hata sisi wote tukaingia katika hali ya laana ambayo tunayo mpaka sasa, lakini ashukuriwe Mungu njia ya mti wa uzima (YESU KRISTO) imeshafunguliwa tunao ukombozi wetu.
Huu mti asili yake ni mauti, na mauti inaletwa na shetani, kama vile uzima unavyoletwa na Yesu Kristo vivyo hivyo mauti inaletwa na shetani. Kwahiyo huu mti alikuwa ni “shetani” mwenyewe, na matunda yake ni “kwenda kinyume na NENO la Mungu” ndio huko unazaliwa uongo,uasherati,uuaji,ulevi,wizi,ulafi,sanamu,ufisadi,wivu, usengenyaji, n.k. ambayo mwisho wake ni mauti.
sasa kilichotendeka Edeni. shetani ambaye ndio ule mti wa ujuzi wa mema na mabaya, alimwingia nyoka. na nyoka akaenda kumdanganya Hawa kwa mafundisho yake ya uongo aliyoyatoa kwa baba yake shetani. kumbuka Mungu alimwonya mwanadamu adumu katika maagizo yake, asitafute maarifa mengine nje na Neno lake, lakini kwa kuwa shetani alijua mwanadamu anapenda maarifa ambayo Mungu alimkataza mwanadamu asiyatafute, na shetani siku zote ni mpingamizi wa Mungu hivyo alimjaribu katika hayo hayo, ndipo alipomwingia nyoka, na kumshawishi Hawa kutokumtii Mungu. na njia shetani aliyotumia ni ushawishi wa kufanya uasherati, kwa maana nyoka alimwambia ukila matunda haya utafanana na Mungu ukijua mema na mabaya. kumbuka kuwa nyoka hakuwa mnyama “reptilia” kama tunavyomwona leo, bali alikuwa ni mnyama anayekaribiana sana na mwanadamu, alikuwa na uwezo wa kuongea, kutafakari, alikuwa anatembea kwa miguu miwili, kwa ufupi alikuwa kama mtumwa wa mwanadamu.Baada ya kulaaniwa ndipo alipotembea kwa matumbo, na kula mavumbi.
Kwahiyo baada ya nyoka kuingiwa na shetani na kwenda kufanya uzinzi na Hawa, Hawa naye akaenda kumpa tunda (kuzini) na mumewe, ikapelekea Hawa kubeba mimba ya mapacha wawili wasiofanana, akamzaa Habili na Kaini kila mmoja akiwa na baba yake. Baba yake Habili alikuwa ni Adamu na baba yake Kaini alikuwa ni nyoka. kumbuka nyoka hakuwa kama nyoka tunayemwona leo.(kwa ufafanuzi mrefu fuatilia somo langu liitwalo UZAO WA NYOKA.)
Tujue kuwa kitendo cha kula matunda ya porini kama peasi, embe au papai, hakuwezi kumfanya mtu ajione kuwa uchi, na kama walikula matunda yale kwa midomo hiyo midomo ndiyo ingetakiwa ilaaniwe na sio viungo vya uzazi, tunaona kabisa baada ya kula tunda (kuzini) walikimbilia kwenda kujifunika sehemu zao za siri, kiashirio kuwa hizo sehemu zao ndizo zilizohusika katika tendo lile.
Ni dhahiri kabisa kuwa mwanadamu ni vigumu kushawishika kwa matunda ya porini, kwa sababu alikuwa na matunda mengine mengi kwanini sasa aende kula lile la katikati ya bustani ya Edeni? Jibu ni dhahiri kuwa ni dhambi ile ile ya asili ambayo shetani alifahamu atampata nayo mwanadamu kirahisi na ndiyo hiyo hiyo anayowapata nayo wanadamu hata leo na hii sio nyingine bali ni dhambi ya uasherati.
Mungu ni yeye yule jana, na leo na hata milele, alichokichukia Edeni ndio hicho hicho anakichukia hata leo. Kama ilikuwa kula tunda kama tunda la kawaida ni makosa angeendelea kukichukia na kukikemea hicho kitu mpaka leo. lakini ni dhambi ya uasherati Mungu anayoichukia hata leo na ndiyo inayowaangusha watu wengi, kwa wanaojiita wakristo na wasio wakristo. kwahiyo hili tunda la kutokuliamini neno la Mungu (ambalo kwa mara ya kwanza shetani alilitangaza kwa kivuli cha uzinzi) hadi leo watu wanalila hili tunda. kama vile tu watu wa Mungu wanavyoendelea kula matunda ya mti wa uzima (kama tulivyosema ni kuliamini na kuliishi Neno la Mungu) ili wapate uzima wa milele vivyo hivyo hadi leo watu wanaendelea kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya kama uasherati, n.k. kwa ajili ya mauti yao wenyewe. Akipandacho mtu ndicho atakachovuna.
Kwahiyo ndugu jambo lile lile lililotendeka Edeni linaendelea kutendeka hadi leo, je! unakula matunda ya ule mti wa ujuzi wa mema na mabaya huku ukijua kabisa Mungu amekataza usiyale ambayo tunayajua matunda yake ndiyo haya, uasherati, na mengine ni uongo, ulevi,ufisadi, usengenyaji, ushoga, ulafi, anasa, kuupenda ulimwengu, wizi, rushwa, tamaa mbaya, chuki, wivu, n.k. unafahamu kabisa mwisho wa haya ni mauti kama Mungu alivyosema pale Edeni, siku utakapokula matunda hayo utakufa hakika. Apple haliwezi likakufanya ufe! na biblia inasema mshahara wa dhambi ni mauti. Kimbilia kwa Yesu sasa ukale matunda ya Mti wa uzima, upate uzima wa milele, Bwana Yesu alisema itakufaidia nini uupate ulimwengu mzima na kupata hasara ya nafsi yako au utatoa nini badala ya nafsi yako. Kuzimu ipo, tazama miti miwili ipo mbele yako, chagua moja MTI WA UZIMA au MTI WA MAUTI.
Warumi 6:16 Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki.
Chaguo lipo kwako. Wakati umekwenda sana na mlango wa neema unakaribia kufungwa, je! umejiweka tayari.?? Umejazwa Roho Mtakatifu,??
Neema ya Mungu iwe pamoja nawe.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
JE! NYWELE ZAKO ZINAOTA AU ZIMESIMAMA?
Kizazi au Uzao wa Nyoka ni upi kwa mujibu wa maandiko?
Leo tutauzunguzia ule uzao wa nyoka… Ni vizuri tuanze kujifunza kula vyakula vigumu pia ili tukue tuzidi kumjua Kristo katika utimilifu wake wote, Leo tuutazame uzao wa nyoka mwanzo wake na ulipofikia sasa..
Mathayo 12:34 “Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake”
Mahali pengine Bwana Yesu alisema:
Mathayo 23:31-33 “Hivi mwajishuhudia wenyewe, ya kwamba ninyi ni wana wao waliowaua manabii.
32 Kijazeni basi kipimo cha baba zenu.
33 Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?”
Na Yohana mbatizaji aliyarudia haya maneno, tunayaona kwenye Luka 3:7
“ Basi, aliwaambia makutano ya wale waliomwendea ili awabatize, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?”
Maneno haya yanathibitisha kuwa uzao wa nyoka upo, na ndio umekuwa adui wa uzao wa Mungu tangu vizazi hata vizazi, Tuufatilie huu uzao wa nyoka umeanzia wapi, na chimbuko lake ni wapi, na ni akina nani hawa wanaitwa uzao wa nyoka?.Tumeona jinsi mti wa uzima na mti wa ujuzi wa mema na mabaya una maana gani, kama hujafahamu soma somo nililoliandika kabla ya hili ” MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA” ili tuteremke vizuri pamoja.
Tunafahamu kuwa kitendo kilichotendeka kwenye bustani ya Edeni ni kwamba Hawa alifanya uasherati na nyoka kisha akaenda kufanya na mume wake ikapelekea Hawa kubeba mimba ya watoto wawili mapacha wasiofanana, kila mmoja akiwa na baba yake tofauti, Habili baba yake akiwa ni Adamu na Kaini baba yake akiwa ni nyoka.
Jambo hili linawezekana kibaolojia na ni jambo la kawaida linalotokea mara kwa mara duniani, kwamba mama mmoja ana uwezo wa kukutana kimwili na wanaume wawili tofauti na kusababisha kubeba mimba ya watoto wawili wa baba tofauti tazama picha hapa chini,
Ni dhahiri kuwa nyoka hakuwa kama jinsi tunavyomuona leo akitambaa kwa tumbo, hana mikono wala miguu bali alikuwa hivyo baada ya kulaaniwa, lakini kabla ya kulaaniwa alikuwa ni mnyama anayekaribiana sana na mwanadamu soma mwanzo 3:14, hivyo baada ya mwanadamu alikuwa anafuata nyoka kisha nyani, kisha wanyama wengine, kwahiyo nyoka alikuwa ana uwezo wa kuzungumza kama mwanadamu,kutafakari, na alikuwa na mikono na miguu miwili kama mtu, Mungu alimuumba kwa kusudi la kumsaidia mwanadamu katika shughuli zake za karibu na kama biblia inavyosema amelaaniwa kuliko wanyama wote ina maanisha alikuwa juu ya wanyama wote na alikuwa mwerevu mbali na wanyama wengine.
Lakini tunaona shetani baadaye alikuja kumwingia nyoka na kwenda kumdanganya Hawa asimtii Mungu ikapelekea kwenda kufanya kitendo kile cha uasherati. mwanzo 3:20 “Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio hai.” ..biblia ilimwita Hawa kuwa mama wa wote walio hai lakini haikumwita Adamu baba wa wote walio hai. Hii ikiwa na maana kwamba wote walitoka kwa Hawa lakini sio wote waliotoka kwa Adamu.
Jambo linalowachanganya wengi ni pale mwanzo 4:1 inaposema”
1 Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana.
2 Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi.
3 Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana.”
Hapa tunaona Adamu alimjua Hawa mara moja tu, na sio mara mbili, maana tunasoma Hawa alimzaa Kaini akamwongeza na Habili…Sio Adamu akamjua Hawa akamzaa Kaini na kisha tena akamjua Hawa akamzaa Habili..Hapana!.. ni kitendo kimoja tu cha Adamu kilichofanyika….
Na kitendo cha “kuongeza” hakimaanishi “kumjua” tena. Na pia ukisoma kwa makini utaona pia sio Adamu aliyesema kwamba Amepata mtoto mwanamume kwa Bwana…bali utaona ni Hawa ndiye aliyesema vile..Adamu asingeweza kusema vile kwasababu si mwanawe wa damu.
Na ni wazi kwa hakuna mwanamke yoyote ambaye akizaa mtoto hata kama kabakwa si wa baba aliyesahihi atamchukia mwanawe..hakuna mwanamke wa namna hiyo.
Tukisoma pia mwana wa pili wa Adamu aliyeitwa Sethi ndiye aliyezaliwa kwa sura na mfano wa Adamu…Ikifunua kuwa Kaini hakuwa mwenye mfano na sura ya Adamu..Tunasoma hayo katika..
Mwanzo 5:3 “Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi”.
Na pia kuna jambo lingine la kuzingatia katika kitabu cha mwanzo jinsi kilivyoandikwa…Huwa matukio yake hayajakaa katika mfululizo, huwa kuna kwenda mbele na kurudi nyuma. kwamfano ..
*Kwenye sura ya kwanza Mungu aliziumba mbingu na nchi na miti na wanyama, na wanadamu huko huko(mwanamke na mwanaume) akamaliza kila kitu na siku ya 7 akapumzika,
* Lakini kwenye sura ya pili tunaona tena Mungu anamwumba Adamu tena kutoka ardhini, na Hawa akaja kumuumba baadaye kutoka kwa Adamu, kitendo ambacho tunajua kilishakamilika tangu sura ya kwanza, vivyo hivyo na mimea na wanyama, waliumbwa kutoka ardhini tena.
* Vivyo hivyo kwenye sura ya tatu inaeleza Adamu na Hawa walivyokula tunda na kufukuzwa katika bustani ya Edeni,
*Lakini sura ya nne inaelezea ni jinsi gani Adamu Alivyokula lile tunda kwa kumjua mkewe na kupata mimba na kuzaa watoto wawili.
Hivyo tukirudi kwa Kaini.. alipozaliwa alibeba tabia za baba yake nyoka na ndio maana tunaona tu baada ya kutoka bustanini alimwamkia ndugu yake na kumuua,hakuwa hata na muda wa kutubu, wivu na hasira vilimtawala hivyo tujiulize alivitolea wapi hivi? kwanini ndugu yake Habili hakuwa navyo jibu ni dhahiri kabisa alivibeba kutoka kwa baba yake nyoka, tunaona ni ile ile roho ya shetani ambayo ilitenda kazi ndani ya nyoka mwanzoni ndiyo inayotenda kazi ndani ya Kaini.
Jambo hili hili tunaona likizidi kuendelea katika uzao wa Kaini, ukifuatilia vizuri utaona Lameki mzao wake alikuwa ni muuaji kushinda hata baba yake Kaini
Mwanzo 4:23-24″3 Lameki akawaambia wake zake, Sikieni sauti yangu, Ada na Sila; Enyi wake za Lameki, sikilizeni usemi wangu; Maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha; Kijana kwa kunichubua;
24 Kama Kaini akilipiwa kisasi mara saba, Hakika Lameki atalipiwa mara sabini na saba.”
na pia tunaona tabia nyingine za kuoa wanawake wengi zilitokea katika huu uzao wa Kaini(ambao ni uzao wa nyoka). Lameki alioa wake wawili kitu ambacho Mungu hakumwagiza Adamu wala uzao wake wala hakikuonekana mahali popote katika uzao wa Mungu.
Pia tunaona huu uzao kutoka kwa baba yao Kaini Mungu aliwatia alama, baada ya Kaini kumuua ndugu yake
Mwanzo 4:13-15 ” Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.
14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.
15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga. “
Kwahiyo hii alama Bwana aliyomtia Kaini sio alama kama chapa fulani kwenye mwili wake (tatoo) , Bali Mungu alimwongezea ukubwa wa mwili wake na akili nyingi (inteligency) yeye na uzao wake, tunaona katika kipindi cha Nuhu ule uzao wa Kaini ulikuwa ni wa watu wakubwa walioitwa “majitu (wanefili)”.
kwahiyo kwa ukubwa huu mtu yeyote asingeweza kupigana nao au kuwatishia, na kwenye upande wa akili tunaona katika mwanzo 4 wana wa Kaini walianza kuwa na ustaarabu mkubwa kwa haraka kama ugunduzi wa vyuma, shaba, ustadi wa vyombo vya miziki n.k.waliitwa watu hodari na wenye sifa wakati ule (soma mwanzo 6:4) inaelezea..wao ndio waliotengeneza mapiramidi ambayo yamesimama mpaka leo, kama tunavyojua hata leo taifa lenye ujuzi mwingi kwa teknolojia kubwa ni dhahiri kuwa taifa hilo litaogopeka na hakuna mtu atayakayedhubutu kwenda kulidhuru ndivyo ilivyokuwa kwa Kaini na uzao wake, Mungu alimpa ukubwa na ujuzi mwingi ambao ulikuwa kama ulinzi kwake ili mtu atakapomuona asimdhuru..
Lakini ule uzao mwingine wa Adamu ambao ni uzao wa Mungu wao walikuwa ni wafugaji tu na wakulima, na walikuwa ni wanadamu wenye miili ya kawaida. hawakuwa hodari katika nchi, mtazamo wao ulikuwa kwa Mungu na ndio maana tunaona walianza kuliitia tu jina la Mungu pale walipoanza kukaa katika nchi,
Mwanzo 4:25-26″ Adamu akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pa Habili; kwa sababu Kaini alimwua.
26 Sethi naye akazaa mwana; akamwita jina lake Enoshi. Hapo ndipo watu walipoanza kuliitia Jina la Bwana. ”
Tunaona katika kipindi hicho chote uzao wa Adamu ulikuwa dhahiri na unaonekana kwa macho na uzao wa nyoka pia ulikuwa dhahiri na unajulikana kwa tabia na kwa kuutazama.
Wana wa Adamu wote walikuwa wanaitwa ”WANA WA MUNGU” na wana wa Kaini walikuwa wanaitwa “WANA WA BINADAMU” kulingana na
Mwanzo 6:1-4 ” Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,
2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.
3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.
4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa. “
Kuna baadhi ya mitazamo inayosema kuwa hawa wana wa Mungu walikuwa ni malaika, na kwamba walikuja na kuzini na wanadamu, ndipo wakazaliwa wanefili lakini mtazamo huo sio kweli kwasababu, kwanza tunaona wanafili walikuwepo duniani kabla hata ya hao wana wa Mungu kuzini na binti za binadamu, na pia malaika hawana miili zile ni roho zitumikazo (Soma waebrania 1:14), ..Hivyo hawawezi kukutana kimwili na wanadamu, lakini pia tunaona baada ya wana wa Mungu kuzini ni binti za binadamu Mungu aliwahukumu wanadamu na sio malaika kuonyesha kuwa ni wanadamu ndio waliohusika na hicho kitendo na sio malaika (mwanzo 6).
Tuendelee kujifunza..
Baada ya watu kuongezeka na kuwa wengi duniani, wana wa Mungu(uzao wa Adamu) waliwatamani binti za wanadamu(binti za Kaini) waliwaona ni wazuri, wenye mitindo ya kisasa, wanaopaka lipstick,wanaovalia nusu-uchi,wanaopaka wanja, wenye ujuzi wa kujipamba kwa manukato ya kila aina,waliojaa macho ya uasherati na ukahaba,wanaoenda na wakati(fashion) kwa mitindo ya kisasa huu ni mfano tu dhahiri wa wanawake tulionao sasa.
Waliacha kwenda kuoa wake zao(binti za Mungu) ambao walikuwa ni wacha Mungu,wastaarabu, wanaojiheshimu kwa mavazi na tabia njema, mabikira, wasioendana na fashion za ulimwengu, lakini wao wakawaona kama washamba, hawafai, wakaenda kujitwalia binti za wanadamu wakazaa nao watoto Ikapelekea kuchanganya mbegu,
Wana wa Mungu wakaacha kumwangalia BWANA tena, wakaanza kuupenda ulimwengu kitu kilichomkasirisha sana Mungu na ndipo Bwana akaghairi na kusema Moyo wangu hautashindana na mwanadamu milele,basi maovu yakaendelea kuzidi kuwa mengi duniani, vitendo viovu, ukatili,ushoga,uuaji, usengenyaji, uzinzi, ulevi,rushwa kukawa hakuna tena wacha Mungu, Dunia ikaharibika sana, mambo yasiyofaa yaliujaza ulimwengu kama siku zetu hizi za leo, maana Bwana alisema kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu ndivyo itakavyokuwa katika siku za kuja kwake mwana wa Adamu. Na ndipo hapo Mungu akakusudia kuiteketeza dunia katika gharika.
Lakini Nuhu ambaye alikuwa ni wa uzao wa Mungu (uzao wa Adamu) alipata neema, japo na yeye alikuwa na mke aliyechanganyikana na uzao wa Kaini, na kusababisha kupata watoto wale watatu waliochanganyikana Hamu,Shemu na Yafethi..
Tunafahamu Bwana Mungu aliuangamiza ule uzao wote halisi wa nyoka kwenye gharika, Ule uzao wote uliondoka Hakukuwa tena na uzao halisi wa nyoka baada ya pale, lakini kutokana na kile kitendo cha kuchanganyikana mbegu kulisababisha na wana wa Mungu kubeba zile tabia za nyoka ndani yao, japo hawakutokea katika ule uzao wa nyoka.
Na ndio maana tunaona zile tabia ambazo zilikuwa kipindi cha nyuma zilianza kujidhihirisha tena katikati ya wale watoto wa Nuhu, tunafahamu Hamu alikuja kuuona uchi wa baba yake, hii ni dhahiri kuwa haikuwa tabia ya uzao wa Mungu lakini kwasababu mbegu zimeshachanganyikana sio jambo la kushangaza vitendo kama hivyo vya wanyama kutokea maana wanyama ndio wanafanya vitendo kama hivyo, hivyo kwa nje mtu anaweza akaonekana kuwa ni mwanadamu lakini ndani anayo ile asili (mbegu) ya nyoka.
Na tabia hizo hizo zikaendelea kwa vizazi vyote hadi kufikia wakati wa agano jipya Bwana Yesu Kristo alipoifichua hii “SIRI YA UASI ” alipowaambia watu ni wa uzao wa nyoka, sasa unaona asili ya huu uzao wa nyoka umetokea wapi, mtu yeyote ambaye hajazaliwa mara ya pili haijalishi wewe ni nani una asili ya nyoka ndani yako fahamu tu wewe ni mzao wa nyoka, na mtu atauliza nitafahamuje kama mimi ni mzao wa Mungu au uzao wa nyoka? ..jibu ni rahisi kabisa kama haujazaliwa mara ya pili wewe ni mzao wa nyoka, na uzao wa nyoka wote utateketezwa kwenye lile ziwa liwakalo moto na kiberiti.
Mungu aliiumba mbegu halisi ya mwanadamu lakini baada ya Adamu kuiharibu ile mbegu halisi kwa kuichanganya na mbegu nyingine ikapelekea wote tuingie katika hali ya uharibifu na mauti, hivyo basi Mungu alimuumba Adamu wa pili yaani Yesu Kristo kwa mbegu nyingine isiyoweza kuchanganyikana ili tukizaliwa katika yeye tupate uzima wa milele 1 Petro1:23″Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele. ” unaona jinsi ilivyo muhimu kuzaliwa mara ya pili?? Bwana Yesu alisema
Yohana 3:3-5″Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.”
Je! umabatizwa kwa maji na kwa Roho ipasavyo? kubatizwa kwa maji ni kuzamishwa na ni katika jina la BWANA YESU KRISTO kulingana na Matendo 2:38, na pia unapaswa ubatizwe kwa Roho Mtakatifu(huko ndiko kuzaliwa mara ya pili) ambao huo ndio utimilifu na muhuri wa Mungu juu yako kulingana na Waefeso 4:30, biblia inasema wote wasio na Roho wa Mungu hao sio wake warumi 8:9″ Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho.
Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.” kwa hiyo Roho wa Mungu tu peke yake ndiye anayeweza kutoa asili ya uzao wa nyoka ndani ya mioyo ya watu. usijidanganye kwa namna yoyote kuwa unatenda matendo mema, unaenda kanisani, unatoa fungu la 10,unasaidia yatima n.k ukidhani unampendeza Mungu, ndugu kama haujazaliwa mara ya pili kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu hauwezi kuingia katika ufalme wa mbinguni.
Maombi yangu ni wewe ujazwe ROHO MTAKATIFU,
naomba umalizie kwa kusoma kifungu kifuatacho:
Luka 11:9-13″ Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.
10 Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
11 Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki, badala ya samaki atampa nyoka?
12 Au akimwomba yai, atampa nge?
13 Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?
Mungu akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa mawasiliano/Ushauri/kuokoka/Whatsapp. Namba zetu ni hizi
+255693036618/+255789001312
Mada Nyinginezo:
MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.
AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA!
Moja ya maagizo muhimu ambayo Bwana wetu Yesu Kristo aliyatoa kwa wanafunzi wake na kwa kanisa kwa ujumla ni kitendo cha kushiriki meza ya Bwana, pamoja na wakristo kutawadhana miguu na mengineyo yakiwemo ubatizo , na wanawake kufunika vichwa vyao wakiwemo ibadani. lakini leo tujifunze hayo mawili ya kwanza.
MEZA YA BWANA:
Mathayo 26:26-28″ Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu
27 Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki;
28 kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. “
Tukisoma pia…
Yohana 6:52-56″ Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao wakisema, Awezaje mtu huyu kutupa sisi mwili wake ili tuule?
53 Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.
54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.
55 Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.
56 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake.
57 Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi. “
Tunaona kuwa haya ni maagizo ya Bwana kwa kila mkristo kushiriki meza ya Bwana kikamilifu.
1wakoritho 11:26 inaeleza umuhimu wa jambo hili kwamba tunapoumega mkate na kukinywea kile kikombe tunaitangaza mauti ya Bwana katika miili yetu wenyewe, hii inamaana kuwa tunakubaliana na lile jambo la kufa na kufufuka kwa Bwana Yesu pale msalabani vivyo hivyo na sisi tunayachukuwa yale mateso ya Bwana Yesu katika miili yetu( kwamba tunakubali kudharauliwa, kuchukiwa na hata kuuawa kwa ajili ya yake kama yeye alivyouawa).hivyo picha ya Kristo inajengwa ndani yetu
Wafilipi 1:29″Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake;
“2Timotheo 2:12″ Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi; ” Kwahiyo Huko pia ndiko kutangaza mauti ya Kristo.
1Wakoritho 10:16″ Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?
17 Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.
18 Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je! Hawana shirika na madhabahu?
19 Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu?
20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.
21 Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. “
kwa mistari hii inaonyesha kabisa kuna mahusiano makubwa ya rohoni kati ya mtu na Bwana, pale anaposhiriki meza ya Bwana. Kama tu vile mtu anapokwenda katika madhabahu za mashetani na kula vitu vya mashetani ni dhahiri kabisa nguvu za giza zitamwandama huyo mtu, vivyo hivyo pia na kwa mtu anayeshiriki meza ya Bwana anashiriki pia neema ya Bwana na baraka za Bwana, na roho za unyemelezi za shetani kama roho za magonjwa, hofu, n.k. Mungu anazifukuzia mbali maana Bwana Yesu alisema mtu asipokula mwili wangu na kuinywa damu yangu hana uzima ndani yake.(yohana 6:53). kwahiyo tunapoula mwili wake na kuinywa damu yake tunakuwa na uzima ndani yetu kila siku.
Luka 24:13″
13 Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili.
14 Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia.
15 Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao.
16 Macho yao yakafumbwa wasimtambue.
17 Akawaambia, Ni maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao.
18 Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! Wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi?
19 Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote;
20 tena jinsi wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulibisha.
21 Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipotendeka mambo hayo;
22 tena, wanawake kadha wa kadha wa kwetu walitushitusha, waliokwenda kaburini asubuhi na mapema,
23 wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosema kwamba yu hai.
24 Na wengine waliokuwa pamoja nasi walikwenda kaburini wakaona vivyo hivyo kama wale wanawake walivyosema, ila yeye hawakumwona.
25 Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii!
26 Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake?
27 Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.
28 Wakakikaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, naye alifanya kama anataka kuendelea mbele.
29 Wakamshawishi wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha. Akaingia ndani kukaa nao.
30 Ikawa alipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa.
31 Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua; kisha akatoweka mbele yao.
32 Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia maandiko? “
tunaona hapa umuhimu wa jambo lingine tena kuwa watu hawa wasingemtambua Bwana kama wasingeumega mkate, vivyo hivyo na sisi kwa kufanya hivyo Mungu anaachilia Roho ya kumjua yeye na Neno lake vizuri siku baada ya siku pale ambapo tulikuwa hatumuelewi vizuri tunapata ufahamu mpya wa kumwelewa vizuri, hivyo ni muhimu kwa kila mkristo kushiriki meza ya Bwana.
Vitu vinavyohitajika ni mkate usiotiwa chachu( yaani usiotiwa hamira), na uwe ni unga wa ngano, Ni vizuri kutumia ngano ambayo haijakobolewa iliyosagwa japo kwa mazingira ya sasa hivi ni ngumu kupata ngano ambayo haijakobolewa isiyochanganywa na chochote hivyo unaweza ukaenda tu masokoni kununua ngano na kwenda kuisaga mwenyewe mashineni kama wanavyosaga unga wa mahindi nusu kilo/kilo moja inatosha kwa matumizi ya muda mrefu, kwahiyo wakati unaanza kuandaa chukua unga mkono mmoja(sasa inategemea na idadi mnaokutanika kushiriki) idadi inapaswa iwe ni watu wawili na kuendelea haiwezekani kushiriki peke yako, kanisa ni kuanzia watu wawili na kuendelea.
ukishapima unga mkono mmoja, tia mafuta yoyote mazuri ya kupikia kama kijiko kimoja (wengi wanapenda kutumia mafuta ya mizeituni), lakini kwa huku kwetu yanayopatikana sana ni ya alizeti, kisha tia chumvi kidogo, kisha weka maji kidogo halafu kanda kama vile unavyokanda chapati, (angalizo : usitie hamira wala vyombo unavyotumia visiwe na hamira vioshe kabla haujatumia).
ukishamaliza kukanda sukuma kama unavyosukuma chapati, usipoteze muda mwingi katika kukanda na kutengeneza umbo, maana unavyozidi kukawia unga utaumuka kutokana na hamira ya asili hivyo jitahidi kuwa haraka kidogo. ukishamaliza tia jikono usiweke chochote tena baada ya kuuweka jikoni, acha kama dakika mbili tatu, ili uwe mgumu wa kuvunjika ukishaiva toa. Na mkate wako utakuwa upo tayari.
Divai inayohitajika ni ile ya mzabibu, na sio fruto au juisi ya zabibu hapana, kilichotumika kushiriki kwa mitume na kanisa la kwanza ni divai(yenye kiwango fulani cha kileo ndani yake). Kama utahitaji divai hizi zinapatikana kila mahali hapa nchini kwetu, zinaitwa “Alter wine”. zimetengenezwa maalumu kwa ajili ya kushiriki meza ya Bwana, ukinunua utaona zimechorwa alama ya msalaba na zimeandikwa “Alter wine”.
Kwahiyo baada ya kuandaa mkate wako na divai mkishakwisha kushukuru mnaweza mkaumega kama Bwana alivyoagiza muda wa jioni ni mzuri zaidi.(tazama picha yake hapa chini)
KUTAWADHANA MIGUU:
Yohana 13:3-17″ Yesu, hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu,
4 aliondoka chakulani; akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni.
5 Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga.
6 Hivyo yuaja kwa Simoni Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi?
7 Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye.
8 Petro akamwambia, Wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Kama nisipokutawadha, huna shirika nami.
9 Simoni Petro akamwambia, Bwana, si miguu yangu tu, hata na mikono yangu na kichwa changu pia.
10 Yesu akamwambia, Yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote.
11 Kwa maana alimjua yeye atakayemsaliti; ndiyo maana alisema, Si nyote mlio safi.
12 Basi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Je! Mmeelewa na hayo niliyowatendea?
13 Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo.
14 Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi.
15 Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.
16 Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka.
17 Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda. “
Maagizo hayo yanajitosheleza kabisa kwamba yatupasa sisi kutawadhana miguu hii inaonyesha picha ya unyenyekevu na kujishusha jambo hili linapuuziwa sana na watu wengi na katika makanisa lakini ni la muhimu sana na faida zake ni nyingi, unaposhika miguu ya mwenzako na kuiosha mambo yote na sababu zote mbaya ambazo shetani ameziweka za uadui baina yako na ndugu yako zinayeyuka, utashangaa ghafla chuki na ndugu yako inapotea, wivu, masengenyo, kutokumjali kunapotea na jinsi utakavyofanya mara kwa mara ndivyo upendo na mahusiano yanavyozidi kuongezeka zaidi na zaidi.
si ajabu leo tunakosa umoja wa Roho kanisani baina ya ndugu, kwasababu tumeyaacha maagizo kama hayo kila mmoja na mambo yake, mkristo mmoja hamjui mwumini mwenzake kanisani. matabaka kati ya maskini na matajiri yanakuwepo kanisani ni kwasababu hakuna mtu anayetaka kujinyenyekeza kwa mwenzake, Bwana Yesu alisema mkiyajua hayo heri ninyi mkiyatenda, kama Bwana wetu alituosha sisi miguu inatupasaje sisi?? tunapaswa tufanye haya zaidi na zaidi.
Kwahiyo mambo haya mawili makuu (kushiriki meza ya Bwana na kutawadhana miguu), sio lazima yatendeke tu kanisani hata nyumbani tunapokusanyika katika Bwana iwe ni wawili au watatu au wanne, n.k. jambo hili linaweza likatendeka. Na tukizingatia haya hali zetu za kiroho zitazidi kuimarika pamoja na upendo kati ya ndugu na ndugu.
Mungu akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa mawasiliano/Ushauri/kuokoka/Whatsapp. Namba zetu ni hizi
+255693036618/+255789001312
Mada Nyinginezo:
JE! NI SAHIHI KUMUITA MARIA MAMA WA MUNGU?
Bwana YESU ni yeye yule jana, na leo na hata milele hajabadilika wala hana kigeugeu, na NENO lake ni lile lile. Kama maandiko yanavyosema mwanamke wa kikristo anapaswa avae mavazi ya kujisitiri.(1Timotheo 2:9) hilo Neno hata leo bado linaendelea kufanya kazi kwa binti za Mungu.
Leo hii vichaa wapo wengi mitaani tunawaona, lakini ni mara chache sana kumuona kichaa mwanamke akitembea uchi barabarani, ingawa vichaa wanaume ni rahisi kuwaona wakiwa uchi, lakini sio kwa wanawake vichaa utawakuta wamevaa matambara na kujisitiri mwili mzima japo ni vichaa. Je! ni kwanini iwe hivi?? Jibu ni Kwasababu uchi wa mwanamke ni wathamani zaidi kuliko wa mwanamume hivyo unastahili muda wote usitiriwe.
Lakini leo hii mwanamke mwenye akili timamu ambaye uchi wake unathamani ambaye angepaswa afunikwe, ndiye anayeongoza kwa kutembea uchi barabarani, SASA HAPO KICHAA NI NANI? lakini mwanamume ambaye uchi wake usiokuwa na thamani nyingi utakuta kajisitiri, kafunika shingo yake kwa shati na tai, huwezi kuona mgongo wake uko wazi wala mapaja yake wazi akitembea barabarani, miguu yake imesitiriwa yote kwa viatu na soksi, ni mtu huyo ambaye uchi wake hauna thamani sana, Leo hii huwezi kuona mwanaume anaenda na vesti kazini, lakini hili jambo ni la kawaida kwa wanawake kutembea migongo wazi na vifua wazi hata sasa imekuwa kawaida mpaka kwenye sehemu za ibada.
Swali ni Je! roho gani ipo hapo katikati? jibu ni rahisi ni ile ile roho iliyokuwa kwa mwanamke Yezebeli wa kwa maana yeye ndiye mwanamke pekee aliyekuwa anapaka uso rangi katika biblia.Lakini tuna wadada hao hao ambao Bwana Yesu amewaambia yeye mwenyewe wasifanye mambo kama hayo na wametii yaani, kujipodoa uso, kupaka wanja, kuvaa vimini, suruali, kaptura, vesti, tight, pedo, kupaka lipstick, kupachika kucha, wigi n.k. lakini cha ajabu utamkuta mdada mwingine anajiita mkristo na anadai amepokea Roho Wa Mungu lakini bado anajiona salama kufanya vitu hivyo.
Jiulize ni roho gani iliyoko ndani yako? kwanini YESU yule yule amkataze dada yule kufanya hivyo vitu na wewe asikukataze? jiulize sana, kama Roho wa Mungu kweli anakaa ndani yako atakushuhudia kwamba haya mambo hayafai na yanakupeleka kuzimu.
Lakini kaa ukifahamu tu, wanawake wote wanaofanya hivyo sehemu yao ni katika lile ziwa la moto HIVI ASEMA BWANA.. (warumi 1).
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa mawasiliano/Ushauri/kuokoka/Whatsapp. Namba zetu ni hizi
+255693036618/+255789001312
Mada Nyinginezo:
CHACHU YA MAFARISAYO NA CHACHU YA HERODE
Tukisoma kitabu cha mwanzo 1, Biblia inasema Hapo mwanzo, Mungu aliziumba mbingu na nchi. Lakini tunaona hakueleza aliumbaje umbaje hii mbingu na nchi yaani, miti, jua, mwezi, milima, wanyama, mwanadamu n.k.
Lakini tukija kusoma kwenye kitabu cha waebrania 11:3 tunaona
” Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri. “
Kwahiyo siri inaonekana hapo ni kwamba mbingu na nchi ziliumbwa kwa NENO la Mungu.
Sasa swali linakuja hili NENO ni nini?
Tukisoma Yohana 1:1-3″
1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. “
Kwahiyo kulingana na mstari huu biblia inaeleza kuwa Neno lilikuwapo kwa Mungu, na lilikuwa ni Mungu, maana halisi ya “Neno” kulingana na tafsiri ya Kigiriki iliyotumika ni WAZO au NIA. Kwahiyo wazo lilikuwapo ndani ya Mungu, Na hivyo vitu vyote vilivyoumbwa vimetoka katika hilo wazo la Mungu mfano dunia, malaika, wanadamu, sayari, miti n.k.
Mfano mzuri ni kama wewe kitu chochote ulichokitengeneza kama nyumba, kiti, meza, nguo, vilitoka kwanza katika wazo lako au nia yako. Hii ikiwa na maana kwamba kama usingekuwa na hilo wazo usingeviumba vitu hivyo vyote, Vivyo hivyo na kwa Mungu pia kama WAZO lake (ambalo ni Neno lake) asingekuwa nalo hapo mwanzo asingeweza kuumba chochote.
Kwahiyo kabla ya mwanadamu kuasi hili NENO lilikuwa pamoja na mwanadamu, Mtu alikuwa na ushirika na Mungu kwa asilimia zote, kwasababu NENO lilikuwa ndani yake kama lilivyokuwa ndani ya Mungu kitu kilichomfanya mpaka mwanadamu kuonekana kuwa kama mfano wa Mungu, Adamu alikuwa na mamlaka yote duniani, kama vile YESU leo alivyo na mamlaka yote duniani na mbinguni biblia inasema hivyo. Na ndio maana utajua sababu ya Mungu kutuita sisi ni miungu duniani, Na yeye ni MUNGU WA miungu.
Lakini baada ya anguko Adamu aliyapoteza yote aliyokuwa nayo kwasababu alijitenga na NENO la Mungu kwa kutokutii. Hivyo yeye na NENO (nia ya Mungu) vikawa ni vitu viwili tofauti. Kuanzia wakati huo baada ya anguko, lile NENO likaanza kumtafuta tena mwanadamu limrudishe tena katika ile hali ya kuwa na mahusiano na Mungu na mamlaka yote aliyokuwa nayo kabla hajayapoteza. Na ndio maana kuna mahali Yesu alisema sio ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua nyinyi.
Sasa tangu huo wakati lile NENO likaanza kutafuta njia nyingi za kumrejesha mwanadamu, likaanza kuzungumza na wanadamu kwa kupitia MBINGU, nyota,sayari na kwa vitu vya asili, kwa dhumuni la kumrejesha tu, lakini mwanadamu bado hakutaka kutega sikio lake kusikia.
Baadaye lile NENO likaanza kuzungumza kupitia watu, mfano manabii wa Mungu, tunaona manabii kama Henoko, Nuhu, Ibrahimu, Musa, Eliya, Danieli, Yeremia, Isaya n.k..lilisema nao kwa nguvu na kwa udhihirisho mwingi liliwapigia kelele wanadamu wamrudie Mungu, warudi katika ule ushirika waliokuwa nao kwanza na Mungu. Lakini wanadamu bado hawakutega sikio lao kulisikia, zaidi ya yote waliwaua manabii waliotumwa kwalo.
Lakini japokuwa NENO hili limezungumza mara zote hizi kwa vizazi na vizazi kupitia vitu vya asili na manabii, bado ule uhusiano uliokusudiwa mwanadamu awe nao na Mungu wake haukufanikiwa kurejeshwa kwasababu ya ugumu wa mioyo ya wanadamu.
Ndipo wakati ulipofika lile Neno likaona liuvae mwili, lije lenyewe katika mwili,liishi na wanadamu, lihubiri mambo yote lililohubiri ndani ya manabii na vitu vya asili kwa kusudi lile lile la kumrejesha mwanadamu kwa muumba wake. Hili jambo linazungumziwa kwenye..
Waebrania 1:1-2″ Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. ”
Sasa umeona mwisho wa yote Neno limekuja kuzungumza na sisi kupitia nini? sio kanisa wa chochote bali mwana.
Hili NENO likajichagulia mwili unaoitwa YESU KRISTO, Haleluya! ni furaha kiasi gani Mungu alivyojirahisisha kwetu sisi ili tukae na hilo NENO kwa jinsi ya kimwili, likiongea, likifundisha, likijibu maswali, likitembea na sisi wazi kabisa, linafurahi na sisi, kitu ambacho hapo mwanzo ilikuwa ni ngumu kulielewa lizungumzapo lakini hapa lipo pamoja nasi (IMANUELI)..Embu tutazame mstari ufuatao;
1 Yohana 1:1-3″
1 Lile lililokuwako tangu mwanzo, TULILOLISIKIA, TULILOLIONA kwa macho yetu, TULILOLITAZAMA, na mikono yetu IKALIPAPASA, kwa habari ya NENO la uzima;
2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);
3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.”
Habari hiyo inaelezea lile NENO ambalo zamani lilikuwepo lakini sasa limefanyika mwili na lipo katikati yetu kama mwanadamu.
Hivyo basi BWANA YESU KRISTO alipokuja akaanza kutufundisha na kuturejesha katika utimilifu wote na Mungu tuliokuwa nao pale Edeni hata na zaidi ya pale.,Jambo la kwanza alilolifanya ni kutupatanisha sisi na Mungu kwa kumwaga damu yake kwa ajili ya ondoleo la dhambi zetu maana biblia inasema pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo (waebrania 9:22).
Na jambo la pili ni kutufanya sisi kuwa wana wa Mungu (miungu)
Yohana 1:12 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; “
Tukisoma
2 Wakoritho 5:18-19 “Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho; yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu NENO la upatanisho. “
Kama tulivyosema lile NENO ni wazo/nia ya MUNGU nalo ni Mungu, ikiwa na maana usiipotii nia ya Mungu haujamtii Mungu. Na nia ya Mungu ni nini? Ni kuturujesha sisi tuwe na mahusiano naye kama ilivyokuwa hapo mwanzo ili tumwabudu MUNGU katika Roho na Kweli. Na ndio maana WAZO/NIA yake iliuvaa mwili kwa dhumuni la kutuhubiria sisi tumgeukie Baba.
Kwasababu hiyo basi Yesu Kristo ndiye NJIA, NA KWELI, NA UZIMA, MTU HAFIKI KWA BABA ISIPOKUWA KWA NJIA YAKE YEYE.(Yohana 14:6), alisema aliyeniona mimi amemwona BABA, usipomtii YESU KRISTO na kumwamini umeukataa mpango wa Mungu kwa wanadamu na viumbe vyake vyote kama shetani alivyofanya.
Natumaini utakuwa umeshaiona sababu ya YESU KRISTO Kutokea ni nini?, ni hiyo hapo juu, Neno la Mungu liliuvaa mwili, kutuhubiria sisi na kuturejesha kwa Mungu wetu ili tumwabudu yeye katika roho na kweli.
Wakolosai 2:9 “Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. “
Kwahiyo Mungu hana nafsi tatu, Nafsi ya Mungu ni moja tu. Mungu kuonekana katika mwili hakumfanyi yeye kuwa na nafsi tatu. Alifanya hivyo tu ili kutupatanisha sisi na yeye. Kama tusingeanguka katika dhambi kulikuwa hakuna haja ya yeye kuuvaa mwili na kuja duniani, Yeye ni Roho nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
NEEMA YA BWANA YESU KRISTO IWE PAMOJA NAWE!
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa mawasiliano/Ushauri/kuokoka/Whatsapp. Namba zetu ni hizi
+255693036618/+255789001312
Mada Nyinginezo:
VIUNO VYENU VIWE VIMEFUNGWA NA TAA ZENU ZIWE ZINAWAKA
VIUMBE VINATAZAMIAJE KUFUNULIWA KWA WANA WA MUNGU?
NINI MAANA YA MSIMWITE MTU BABA DUNIANI?
Je! Manabii wa uongo ni wapi?
Mathayo 7:15 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?
17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.
18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.
19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.
20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.
21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. “
Kuna watu wanasema usizihubiri hizi habari, we fundisha TU watu watubu wawe wakristo inatosha ndiyo kazi yako!. Swali ni je! ukishakuwa mkristo ndio mwisho wa safari?, unahitaji kukua na ndio safari inapoanzia na sio inaishia. Hivyo basi unahitaji chakula ili ukue, na ujue ni chakula gani unapaswa ukile, maana vyakula ni vingi vijengavyo na vibomoavyo, Hivyo ni kuwa makini kujua ni chakula kipi ule na kipi usile kwa usalama wa roho yako na hatma yako ya milele.
Tunaishi katika kipindi cha hatari ambacho hakijawahi hata kutokea katika vizazi vyote vya nyuma, ambacho kina mchanganyiko mkubwa wa MANABII WA UONGO NA MANABII WA KWELI, Na wote wanafanya kazi moja ya KUVUNA ROHO ZA WATU, aidha kuzipeleka kuzimu au mbinguni, ni kipindi cha hatari sana tunachoishi. Ni muhimu kufahamu unavunwa upande gani, ili usije ukajikuta unadondokea sehemu ambayo haujatarajia.
Jambo kubwa linalowachanganya watu wengi ni kuona pale mtu anayejiita mtumishi wa Mungu halafu bado ni mwasherati, mtukanaji, mlevi, anapenda anasa, na bado miujiza inatendeka na yeye, anafufua wafu, anaombea watu wanaponywa, anatabiri na unabii unakuja kutimia, ananena kwa lugha n.k.
Kiasi ambacho kinamfanya mtu mchanga ashindwe kuelewa inawezekanikaje huyu mtumishi anafanya mambo ya kidunia lakini bado ishara na miujiza zinatendeka na yeye, Na wala hatumii uchawi ila anatumia jina la YESU na nguvu za Mungu zinashuka. “HII NI SIRI” na ni jukumu kwa kila mkristo anayethamini maisha yake ya kiroho kufahamu..kumbuka (kuna wanaotumia nguvu za giza kutenda miujiza, siwazungumzii hao, hao ni rahisi kuwagundua lakini nawazungumzia wale wanaotumia nguvu za Mungu ambao ni ngumu kuwatambua.)
Tusome, mstari ufuatao unawazungumzia hao wanaotumia nguvu za Mungu ; Kumb.13:1-5″
1 Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu,
2 ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo;
3 wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote.
4 Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.
5 Na yule nabii, au yule mwotaji wa ndoto, na auawe, kwa kuwa amesema yaliyopotoka juu ya Bwana, Mungu wenu, aliyewatoa katika nchi ya Misri, akakukomboa katika nyumba ya utumwa, apate yule mtu kukupotoa katika njia aliyokuamuru Bwana, Mungu wako, uiendee. Ndivyo utakavyouondoa uovu utoke katikati yako. “
Unaona hapo? Huyo nabii hapo katoa unabii kwa uweza wa nguvu za Mungu na ikatokea, lakini anawafundisha watu waende kinyume na maagizo ya Mungu. Vivyo hivyo na hata sasa katika kipindi hichi cha mwisho Mungu ameamua kuachia mvua yake (UPAKO) kwa watu wote waovu na wema kutujaribu sisi kama TUNAMPENDA BWANA NA KUYASHIKA MANENO YAKE AU LA!.
Mtu anaweza akaja kwako na kutoa unabii na ukatimia na kufufua wafu, na kuponya wagonjwa lakini akafundisha injili nyingine akakwambia ulevi ni sawa, wanawake kwenda na mitindo ya kisasa ni sawa (anasema Mungu haangalii mavazi anaangalia roho ), akakufundisha kuupenda ulimwengu ni sawa, kuoa wake wengi ni sawa, Dunia haiishi leo wala kesho kula maisha, kuwa na pesa nyingi ndio kigezo cha kubarikiwa na Mungu, Mungu siku zote ni Mungu mzuri na hawezi kuwahukumu watu aliowaumba. n.k. na bado mtu huyo akatoa mapepo na kufufua wafu.
Na wewe kwasababu NENO na kumpenda Mungu hakupo ndani yako, ukadhani anazungumza ukweli au katumwa na Mungu kwasababu tu! ametoa unabii ukatokea, NDUGU USIDANGANYIKE UMEPOTEA!! . Biblia inasema jiepushe na huyo mtu, CHUKUA TAHADHARI KWA USALAMA WA MAISHA YAKO..KIMBIA! HARAKA SANA NI BWANA NDIYE ANAYEKUJARIBU KUONA KAMA UNAMPENDA KWELI NA KULIFUATA NENO LAKE AU LA!
Leo hii wewe unayejiita mkristo unapenda injili za kufarijiwa tu! siku zote unapendwa kuambiwa “ALL IS WELL” ulimwengu hautakuja kuteketezwa,tunaishi chini ya neema, mafundisho unayoyapenda wewe ni KUTABIRIWA MAFANIKIO TU!. Lakini fahamu jambo moja BWANA YESU hakuacha enzi na mamlaka mbinguni ili aje kutufia sisi mlabani tuwe MABILIONEA, bali kwa ajili ya dhambi zetu.(hicho ndicho kiini cha injili) yeye mwenyewe alizungumza ..Mathayo 16:24-27
” Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
Leo mkristo anadai anamfuata YESU, lakini kigezo cha kumfuata YESU ni kuwa na MSALABA wako, sasa wewe MSALABA WAKO UKO WAPI?, Jihadhari na haya mafundisho ya uongo yanawapeleka maelfu wa waaminio kuzimu kila siku pasipo wao kujua.
Hawa manabii wa uongo, Bwana Yesu alisema tutawatambua kwa MATUNDA YAO na sio kwa upako wao, kwasababu Mungu anaweza akamtumia mtu kama chombo tu cha kuazima akishamaliza shughuli nacho anakiacha, mfano tunaona Mungu alimtumia Punda kuongea na Nabii Balaamu kumpa ujumbe, lakini baada ya punda kutoa ujumbe alirudia katika hali yake ya kawaida ya upunda, vivyo hivyo na Balaamu mwenyewe alikuwa ni MCHAWI lakini Mungu alimtumia yeye kuwabariki Israeli, (hesabu 22:21-29),
Na pia Mungu aliwatumia wale manabii 400 kumdanganya mfalme Ahabu kwasababu Mungu alikuwa amekusudia mabaya juu yake. (1 wafalme 22:6). Kwahiyo kuwa na upako mtu kuona maono, au kuwa nabii, au kunena kwa lugha au kuponya au kufanya miujiza yoyote ile, sio kigezo cha huyo mtu kuwa NABII WA MUNGU. Tutatawatambua kwa matunda yao (AMBAYO NI NENO LA MUNGU). Nabii wa ni yule anayekuja na ishara pamoja na NENO lakini lililokuu ni NENO.
Kipime mtu anachokuambia je! kinaendana na NENO la Mungu? kama hakiendani na NENO la Mungu weka kando haijalishi anawashirika wengi kiasi gani, au anakubalika kiasi gani, au kanisa ni kubwa kiasi gani, au anaupako kiasi gani. KIMBIA! HILO NI SINAGOGI LA SHETANI!..
Jiulize Wewe unayejiita mkristo tangu ulipoamini, maisha yako ya kiroho yamesonga mbele kiasi gani. utakuwaje mkristo halafu biblia husomi!?? sasa utawatambuaje manabii wa uongo au manabii wa ukweli kwa namna hiyo watakapokujia na mafundisho yao??. Utakuwa unapelekwa na kila upepo unaokuja wa elimu yoyote. Maana njia pekee ya kumpima nabii wa uongo au Nabii wa ukweli ni kwa NENO TU!.
Na sio kitu kingine. Jijengee kila siku tabia ya kusoma NENO na kuomba. Hizi ni nyakati za hatari tunaishi zile zilizotabiriwa kuwa watatokea manabii na makristo wengi wa uongo nao watawadanganya wengi yamkini hata walio wateule. Kumbuka ni wateule ndio wanaozungumziwa hapo kuwa wanaweza wakadanganywa sasa jiulize wewe ambaye sio mteule utaonekania wapi? wewe ndio hautaelewa chochote kinachoendelea utaishia kuwashangilia na kuwasifia kama Bwana Yesu alivyotabiri juu ya manabii wa uongo.
2 Petro 1:10″ Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.”
KWAHIYO NDUGU HUU NI WAKATI WA MUNGU KUTUJARIBU SISI KAMA TUNAMPENDA YEYE NA KULISHIKA NENO LAKE AU LA!. Biblia inasema, MPENDE BWANA MUNGU WAKO, KWA MOYO WAKO WOTE, KWA ROHO YAKO YOTE, KWA NGUVU ZAKO ZOTE, NA KWA AKILI ZAKO ZOTE.
Mungu hadhihakiwi usipoweza kufanya hivyo jua tu utaangukia kwenye huu mstari ufuatao;
2 Thesalonike 2:10-12″… na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
11 KWAHIYO MUNGU AWALETEA NGUVU YA UPOTEVU, WAUAMINI UONGO;12 ILI WAHUKUMIWE WOTE ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu. “
MARAN ATHA!
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa mawasiliano/Ushauri/kuokoka/Whatsapp. Namba zetu ni hizi
+255693036618/+255789001312
Masomo Mengineyo
Kutoka 21:2-6 ” Ukimnunua MTUMWA wa Kiebrania, atakutumikia muda wa miaka sita; mwaka wa saba atatoka kwako HURU bure.
3 Kwamba aliingia kwako peke yake tu, atatoka hivyo peke yake; kwamba ameoa, mkewe atatoka aende pamoja naye.
4 Kwamba ni bwana wake aliyempa huyo mke, naye amemzalia wana, wa kiume au wa kike; yule mke na wanawe watakuwa ni mali ya bwana wake, naye mume atatoka peke yake.
5 Lakini huyo mtumwa AKISEMA WAZIWAZI, Mimi nampenda bwana wangu, na mke wangu na watoto wangu; SITAKI MIMI KUTOKA NIWE HURU;
6 ndipo hapo huyo bwana wake atamleta mbele ya Mungu na kumleta mlangoni, au penye mwimo wa mlango; na bwana wake ATALITOBOA SIKIO LAKE KWA UMA; ndipo ATAMTUMIKIA SIKU ZOTE. “
Biblia inaeleza wazi kabisa kulingana na maandiko hayo hapo juu, Mtumwa yule aliyetangaziwa uhuru wake baada ya kutumika miaka 6 akakataa (Yaani akaona ni vyema kuendelea katika utumwa wake.). Jambo linalotokea ni hili bwana wake huyo mtumwa atachukua sindano na kutoboa SIKIO lake, kuwa kama MUHURI wa kukataa kuwekwa huru, Hivyo basi huyo mtumwa atamtumikia bwana wake milele, Na kama tunavyofahamu sikio likishatobolewa haliwezi kurejea tena katika hali yake ya kwanza. Na ndio maana ilikuwa inatumika kama ISHARA YA MAPATANO(MUHURI).
Vivyo hivyo kwa wanadamu wa leo, Kristo alikuja kututangazia uhuru wetu kutoka katika UTUMWA WA DHAMBI kulingana na
Mathayo 11:28-29 (Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; “),
Kwasababu Bwana Yesu alisema Yohana 8:34-36″ ….Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote. Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli. “
Bwana Yesu pia alisema maneno haya luka 4:18-19″ Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma KUWATANGAZIA WAFUNGWA KUFUNGULIWA KWAO, Na vipofu kupata kuona tena, KUWAACHA HURU WALIOSETWA,Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. “
Kwahiyo injili ililetwa kwetu mahususi kwa kutuweka HURU mbali na dhambi. Hapo anaposema
“kuutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa” akiwa na maana kuwa ndio mwaka wa maachilio, ule mwaka wa saba ( Kwa maana mahali pengine anasema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia; tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa.
2 Wakoritho 6:2). Kwahiyo tunaona MBIU YA MAACHILIO IMESHAPIGWA watu wote wawe HURU kwa YESU KRISTO BWANA. Lakini cha kusikitisha wapo baadhi ya watumwa (watumwa wa dhambi), wanakataa kuupokea uhuru WAO waliotangaziwa na Bwana wanapenda kuendelea kumtumikia bwana wao shetani ambaye hapo mwanzo alikuwa anawatumikisha na kuwatesa. Embu tuitazame hii mihuri inampataje mtu.
Mungu anao MUHURI wake, na shetani pia anao muhuri wake kwa watoto wake. Wale waliokubali kuwekwa huru na BWANA wanatiwa MUHURI WA MUNGU nao ni ROHO MTAKATIFU kulingana na
waefeso 4:30″(Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa MUHURI hata siku ya ukombozi). , na pia biblia inasema katika
2 Wakoritho 3:17 .. walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru. “.
Kwahiyo unaona unapoukubali UHURU Mungu anakupa zawadi ya kupokea Roho Mtakatifu kama Muhuri wa uhuru wako. Lakini kama hauna Roho wa Mungu wewe bado ni mtumwa wa dhambi na UNAJUA MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI. Warumi 8:9″….Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. ”
Kwa wale waliokataa uhuru kwa makusudi angali wakijua kabisa wapo kwenye utumwa na wangepaswa wawe huru, lakini wakapenda kumtumikia bwana wao shetani katika dhambi zao kuliko kumtumikia Mungu nao pia wanatiwa MUHURI. Na mihuri hiyo YA SHETANI wanatiwa katika MASIKIO YA MIOYO YAO, maana yake ni hii HAWATAKUWA TENA NA NEEMA YA MUNGU JUU YA MAISHA YAO!,baada ya kuisikia injili na kuikataa Haiwezekani wao kumgeukia Mungu tena, Hata waelezweje injili hawawezi kusikia tena wageuke hao wameshakuwa mali halali ya shetani. Hii ni hatari sana tuwe makini tunaposikia wito wa Mungu.
Na huu muhuri wa shetani mpaka sasa hivi unaendelea kuwapiga watu,
leo hii umeshaisikia injili mara ngapi, umehubiriwa uache uzinzi mara ngapi ewe kijana ewe binti,? umehubiriwa utubu dhambi zako mara ngapi? lakini umekuwa wa kwanza kufanya mizaha? umehubiriwa uache ulevi mara ngapi? unavuta sigara, unaangalia pornoghaphy, unafanya mustarbation, binti unasagana, umekuwa shoga kijana, unaenda kwa waganga, unajifurahisha katika anasa na miziki ya kidunia,
Mwanamke unavaa suruali, vimini, unapaka rangi kucha, kijana unanyoa mitindo isiyofaa na kusuka nywele ,na tatoo kwenye mwili wako, wanawake usengenyaji na umbea, mtukanaji, unajichanganya na watu waovu kwa jinsi isivyopasa, unachati nao mambo maovu, huku ukijua kabisa watu wanaoyafanya hayo wataishia katika jehanum ya moto, JE! UNADHANI NEEMA YA MUNGU ITAENDELEA KUDUMU JUU YAKO MILELE?.
Mungu hadhihakiwi apandacho mtu ndicho atakachokivuna. Tutawezaje kupona tusipouthamini wokovu mkuu namna hii?.
Unashindwa kuona jinsi unavyozidi kutiwa ule MUHURI wa shetani? kwa kuukataa uhuru wako ambao BWANA aliokutangazia pale KALVARI?. Maana kama unasikia sauti ya Mungu kila siku ikisema moyoni mwako UTUBU lakini unaipuuzia nakwambia ukweli utafika wakati HAUTAKAA UISIKIE TENA NDANI YAKO!!,
Na unajua ni kitu gani kitaenda kukutokea? Ni kwamba utafika wakati utaona mambo yote kuwa ni sawa, kuwa ulevi ni sawa,utaona uasherati hauna ubaya wowote, Mungu aliyetuumba hawezi kutuhukumu, hautaamini tena kama kuna jehanamu, utaishia kuwaona watumishi wote wa Mungu ni waongo, utaishia kuukosoa kila siku ukristo na biblia ukisema hayo mambo ni ya kale.
Utaanza kujiona kuwa ni haki yako kuishi unavyotaka hata kujichubua, kubadili maumbile, kuvaa unavyotaka ni sawa, Utajiona kutukana ni sehemu tu ya maisha ya binadamu hakuna kosa lolote kwasababu Roho Wa Mungu hayupo tena ndani yako kwasababu UMESHATIWA MUHURI, utaanza kuona kujipenda mwenyewe ni sawa, Kutazama pornography na kufanya musturabation ni sehemu maisha ya kila mwanadamu ukijidanganya kuwa Mungu hawezi kumuhukumu mtu kwa kufanya hivyo, unajikuta unaanza kupenda kufuatilia mafundisho ya mashetani kuliko mafundisho ya Mungu, Biblia hutaki kusoma kusoma lakini habari za freemasons, na zi kichawi, na filamu pamoja na vitabu kama , harryporter, twightlight, vampires,n.k. ndivyo vinavyokuvutia kusoma na kuangalia, jiulize ni roho gani inakuendesha? n.k.
Ndugu ukishaanza kuona dalili ya mambo kama hayo yanakuja ndani yako, jua kabisa neema ya Mungu ndivyo inavyoondoka kwako kidogo kidogo na ndo unavyoupokea MUHURI wa shetani hivyo, maana jua tu wewe unayeisikia injili kila siku unaambiwa utubu hautaki, neema yako haiwezi kuwa sawa na mtu yule ambaye hajawahi kusikia injili kabisa. soma mstari ufuatao;
2 Wathesalonike 2:10-12 ” na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
11 KWAHIYO MUNGU AWALETEA NGUVU YA UPOTEVU, WAUAMINI UONGO;
12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu. “
Kwahiyo ndugu maneno hayo hayakuogopeshi?? TUBU! yamkini hii sauti ya upole inayokuambia kila siku utubu bado inaendelea KULIA NDANI YAKO! ..itii na ugeuke maana upo katika HATARI, Maana hiyo sauti haitadumu milele ndani yako. Na ikishaondoka hakutakuwa na njia ya kurudi tena. YAANI MOYO WA KUTUBU hautakuwepo tena ndani yako utafanana na hao watu unaowaona huko ulimwenguni watendao matendo ya giza si kana kwamba hawasikii au hawakusikia injili hapana lakini mioyo yao imeshatiwa MUHURI, hawatakaa wasikie tena na kubadilika, ndugu usifanane nao. Mtii Mungu tubu dhambi zako muda umeenda sana kuliko unavyofikiria.Yesu yupo mlangoni kurudi.
Maana biblia inasema…
Ufunuo 22:10 “Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia. MWENYE KUDHULUMU NA AZIDI KUDHULUMU; na MWENYE UCHAFU AZIDI KUWA MCHAFU; na MWENYE HAKI AZIDI KUFANYA HAKI; na MTAKATIFU NA AZIDI KUTAKASWA.Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. “
Naomba umalizie kwa kuyatafakari maneno yafuatayo ujue hatma ya WALIOUKATAA UHURU WAO KUTOKA KWA BWANA;
Warumi 1:24” Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao.
25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.
26 HIVYO MUNGU ALIWAACHA WAFUATE TAMAA ZAO ZA AIBU, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;
27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, WAKAPATA NAFSINI MWAO MALIPO YA UPOTEVU WAO YALIYO HAKI YAO.
28 NA KAMA WALIVYOKATAA KUWA NA MUNGU KATIKA FAHAMU ZAO, MUNGU ALIWAACHA WAFUATE AKILI ZAO ZISIZOFAA, WAYAFANYE YASIYOWAPASA.
29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,
30 wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao,
31 wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema;
32 AMBAO WAKIJUA SANA HUKUMU YA HAKI YA MUNGU, YA KWAMBA WAYATENDAYO HAYO, WAMESTAHILI MAUTI, WANATENDA HAYO, WALA SI HIVYO TU, BALI WANAKUBALIANA NAO WAYATENDAYO.Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa mawasiliano/Ushauri/kuokoka/Whatsapp. Namba zetu ni hizi
+255693036618/+255789001312
Mada Nyinginezo:
WAKATI WA JIONI KUTAKUWAKO NA NURU.
NUHU ALIWALETAJE LETAJE WANYAMA KWENYE SAFINA?
NINI TOFAUTI KATI YA 1) KUOKOKA, 2) WOKOVU, 3) KUONGOKA?
UAMSHO MKUU UMEKARIBIA!!
Yoeli 2:28-32″ Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;
29 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.
30 Nami nitaonyesha MAMBO YA AJABU KATIKA MBINGU na KATIKA DUNIA, DAMU, na MOTO, na MINARA YA MOSHI.
31 JUA LITAGEUZWA KUWA GIZA, na MWEZI KUWA DAMU, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo.
32 Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama Bwana alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao Bwana.
Tukisoma mistari hiyo Nabii Yoeli alionyeshwa maono ya uvuvio mkubwa wa Roho ya Mungu ambao ungekuja katika siku za mwisho, Na ni dhahiri kabisa kwa wasomaji wa biblia wanafahamu sehemu ya huo unabii ulitimia wakati wa PENTEKOSTE, pale Roho wa Mungu alipowashukia wale watu 120 kwa mara ya kwanza, na kuwapa vipawa vikubwa na vya ajabu, ishara na miujiza mingi ikifanywa na mitume na wale wote waliojazwa Roho Mtakatifu.
Mvua hii ya Roho Mtakatifu Mungu aliyoiachilia kwa mara ya kwanza pale Pentekoste inajulikana kama “MVUA YA AWALI/MASIKA” ( kwa kiingereza former Rain). Lakini pia Mungu aliahidi kuileta mvua nyingine tena ambayo ni “MVUA YA BAADAYE/ VULI” ( kwa kiingereza Latter Rain). Kwa ufafanuzi wa maelezo haya tusome;
Yoeli 2:23 “Furahini, basi, enyi wana wa Sayuni, mkamfurahie Bwana, Mungu wenu; kwa kuwa yeye huwapa ninyi MVUA YA MASIKA, kwa kipimo cha haki, naye huwanyeshea mvua, MVUA YA MASIKA, na MVUA YA VULI, kama kwanza.”
Kwahiyo hii mvua ya pili (MVUA YA VULI) mbali na ile ya kwanza iliyotokea wakati wa Pentekoste, Tukisoma katika historia ya ukristo Bwana aliishusha tena mwaka 1906, kwenye uamsho uliotokea mtaa wa AZUSA, huko Calfornia Marekani ambapo Bwana alimwaga ROHO wake na kushusha vile vipawa tena vya Roho Mtakatifu kama ilivyokuwa katika Pentekoste ya kwanza baada ya kanisa la Kristo kukaa muda mrefu bila uamsho kwa muda wa karne nyingi, lakini kuanzia huu mwaka 1906 tunaona vipawa vyote vilirejeshwa watu wakaanza kunena kwa lugha, kutabiri, kuponya magonjwa, ishara na miujiza, unabii n.k. vitu ambavyo havikuwahi kutenda tangu wakati wa kanisa la kwanza.
Hivyo basi Mungu alimtuma mjumbe wake William Branham kama mjumbe wa kanisa la mwisho LAODIKIA, ufunuo 3, Mungu alimtumia kwa ishara nyingi na miujiza ya ajabu ambayo haikuwahi kufanyika hapo kabla ikiwemo na utambuzi wa siri za mioyo ya watu, tafsiri za ndoto kama ilivyokuwa kwa Nabii Danieli, na ishara zilizoweza kuonekana wazi na kunaswa katika picha za kimagnetiki, n.k.
Ndipo Mungu akaendeleza kuimwaga hiyo roho kwa watumishi wake wengi waaminifu duniani kote kwa mfano wa William Branham kama oral Robert, Billy Granham, TL Osborn, nk..
( tazama ushuhuda mfupi juu ya huduma na maisha ya William Branham,)
Mvua hii ya mwisho itatimizwa katika huu wakati wa mwisho Bwana aliahidi sehemu hii ya maandiko itaenda kutimia
Yoeli 2:29 “tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.
30 Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, na minara ya moshi.
31 Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo.
Kumbuka katika mvua iliyoachiliwa mara ya kwanza, tuliona unabii, lugha, maono, ndoto, ishara, n.k. lakini hatukuona mambo ya ajabu katika dunia na katika mbingu kama jua kutiwa giza, mwezi kuwa damu, moto, minara ya moshi, n.k. tumezoelea kuona unabii na uponyaji, lakini haya mambo mengine yaliyosalia yanaenda kutimilika katika hii mvua ya mwisho na yatakuja na hukumu sio kwa kuwaburudisha watu, Tunaona mfano uliotokea kwa mapigo ya Musa na Eliya. Ni mambo ya kutisha yanakuja. Na ishara ambazo hata hazijawahi kurekodiwa wala kufanywa mahali popote pale katika historia ya dunia.
Kumbuka hakuna ishara isiyokuwa na ujumbe nyuma yake. Hivyo hizi ishara zitakuja na ujumbe, na ujumbe wake utakuwa ni wa kipekee, ukisoma kitabu cha ufunuo 10:4-11″ Inaelezea zile NGURUMO SABA ambazo Yohana aliambiwa asiziandike, ni siri zilizofichwa tangu zamani nazo hazijaandikwa mahali popote katika biblia.
Zipo siri nyingi ambazo hazijulikani kwamfano “Tutakapofika kwenye utawala wa miaka 1000 ni shughuli gani zitakuwa zinaendelea , na tukienda mbinguni tutakuwa tunafanya nini huko, siri za kwenda kwenye unyakuo na siri za kurudi kwa pili kwa Yesu, kuanguka kwa shetani, na mambo yaliyokuwa yanatendeka kabla ya Adamu kuumbwa nk,(huu ni mfano tu, zinaweza zikawa nyingine tofauti ya hizo au zaidi ya hizo ) .Siri hizi zitakuja kufunuliwa katika wakati huu ambao upo karibu katika mvua hii inayokuja kunyesha.
Ndugu William Branham kabla ya kufariki kwake alionyeshwa na Bwana huu uvuvio mkubwa jinsi utakavyokuja kuwa kiasi kilichomfanya yeye mwenyewe atamani kuwepo katika huo uamsho. Katika hilo ono alionyeshwa uponyaji wa kiungu wa ajabu ukitendeka watu wengi walikuwa wakiponywa kabisa kabisa.
lakini tukisoma
Mathayo 24:14″Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.”
Mstari huu unaelezea jambo litakalofanyika kwanza kabla ya Bwana YESU kurudi, Huu uamsho unaokuja ndio utakaokuwa wa mwisho na utapita duniani kote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote, kwasababu mambo dhahiri na ishara za ajabu zitaonekana kwa watu wote na bibi-arusi naye atakusanyika pamoja kwa ajili ya unyakuo na ndipo ule mwisho utakapokuja.
Ndugu hizi siku zipo karibu, wakati huo utakapofika kama leo haujajiweka tayari kule hautaweza kwasababu zitakuja na hukumu kutoka kwa Bwana, utaishia kupinga na kusema ni vya shetani, kwasababu utasikia mambo ambayo pengine hayajarekodiwa mahali popote kwenye biblia, na hautapata uhakiki wa mambo hayo sehemu yeyote kama hauna ROHO MTAKATIFU kwasababu ni mambo mapya kabisa na hautaweza kupambanua utabakia kuwa mtu wa nia mbili kama unyasi utikiswao na upepo hutajua wapi usimame, ikiwa leo tu huwezi kumtambua yupi nabii wa kweli na yupi nabii wa uongo, utawezaje kuelewa yatakayokuja huko mbele ambapo mambo mapya yatakuja kuhubiriwa??.
Tafakari ndugu tunaishi katika siku za mwisho, ijue kalenda ya Mungu katika maisha yako na wakati tuliopo, usije ukafanana na wale wanawali wapumbavu ambao hawakuwa na mafuta ya ziada katika taa zao. Maana ya yale mafuta ya ziada ni roho ya mafunuo ambayo mkristo wa dini tu hawezi kuwa nayo.
Ndugu kaa ukifahamu Huu uamsho utaanza duniani kote hivi karibuni, na mambo ya ajabu yataenda kutendeka na kuhubiriwa, kwa waovu itakuwa ni hukumu bali kwa wenye haki itakuwa ni kwa kuandaliwa kwa ajili ya unyakuo. Maandalizi ni sasa.
“Tumeandika makala hii kuwakumbusha bibi arusi wa Kristo wote popote walipo kuwa kuna uamsho mkuu unakuja mbeleni na kuna baadhi ya watumishi wa Mungu waaminifu wachache wamekwisha anza kuonyeshwa katika maono na Bwana Yesu, jinsi utakavyokuwa. Tazama chini shuhuda chache za watu hawa;”
USHUHUDA WA STEPHEN POWELL’S
Stephen Powell’s ni muhubiri wa kimarekani hivi karibuni tarehe 21 April 2017. Bwana alimwonyesha maono yafutayo na haya ni maneno yake yaliyonukuliwa;
Kulingana na historia, “NEMBO” (Coat of Arms) ni ishara muhimu ya utaratibu wa urithishaji uliotumika katika zama za kati huko Ulaya, Ilitumika mahususi kama utambulisho katika vita, Nembo zilianzishwa kuashiria ukoo wa familia fulani, urithi, umoja, umiliki, na pia katika taaluma fulani .
Bwana kwasasa anaenda kupitisha NEMBO hii ya thamani sana kwa kizazi chenye utukufu anachokinyanyua leo duniani!, Mungu anaenda kuachilia uhalali fulani, ujuzi fulani, na urithishwaji katika roho!. Nisikilize kwa makini kitu ninachokwenda kusema sasa…
Hivi karibuni katika mfululizo wa maono niliyopewa, nilichukuliwa mbinguni nikaonyeshwa vitu vingi. Mara ya mwisho nilijikuta nimerudi katika hali yangu ya kawaida nikiwa na akili zangu juu ya kitanda changu katika hotel moja huko west Virginia. Na nilipokuwa nimelala pale nilisikia BWANA akisema ” NINARUDISHA TENA NEMBO YA VITA ALIYOKUWA AMEIVAA WILLIAM BRANHAM “. Kisha nikaona ono Bwana akishika bega la askari mmoja ambaye kwenye nguo yake kulikuwa na kitu kama NEMBO hivi ingawa sikuweza kuikariri jinsi ilivyokuwa. Kisha Bwana akaniambia ataenda kuachia vipawa vya miujiza katika mikono ya wana wake na binti zake katika hichi kipindi, kama ilivyokuwa kwa William Branham alivyopewa sio tu kuona maono bali pia kipawa katika viganja vyake.
Katika vita askari huwa wanavaa vazi fulani la nje (surcoat) kuzuia dirii isipate kutu. Hichi ndicho nilichokiona usiku ule, na ninaamini NENO la Bwana kuwa ni hili: Bwana anaenda kuendeleza haya katika roho mwaka huu hapa Marekani na itakuwa ni kwa mwendelezo wa William Branham. Dirii ya huyu mtu haitaendelea kushika kutu itatokea tena kwa mara nyingine Marekani katika huu mwaka, wamekwisha vikwa hawa matenda miujiza wapya ambao wataanza kutenda kazi mwaka huu.
Kama vile Mungu alivyoweka fimbo katika mkono wa Musa na kumwambia aende kufanya miujiza kule Misri, vivyo hivyo Mungu ataenda kufanya miujiza kupitia mikono ya hawa mashujaa ambao watatokea katika mwendelezo wa William Branham.
Branham alipewa maagizo mwaka 1946, Mungu alimwambia “miujiza itafanyika kupitia mikono yake”. Moja ya hii miujiza ilifanya kazi katika mkono wake wa kushoto na akapewa uwezo wa kupambanua roho hata kuweza kugundua uwepo wa magonjwa ya kipepo au udhaifu. Ishara ya pili aliyopewa ni kipawa cha ajabu cha maono aliweza kutambua siri za mioyo ya watu kwenye mimbari na kuwasaidia watu kuishinda roho ya kutokuamini (kitu ambacho kinazuia miujiza mingi isitendeke hapa Marekani). Mungu aliyafanya haya yote kupitia maisha ya huyu mtu na huduma yake, Hata hapa Marekani Mungu anaenda tena kufanya haya katika wakati wetu. Anaendeleza Nembo iliyokuwa kwa William Branham.
Bwana alisema msiwe na mitazamo hafifu juu ya uvuvio unaokuja wa Mungu, kwasababu ikiwa haupo katika sehemu ya huo uamsho, ni rahisi wewe kuingia katika hatari ya kumruhusu shetani aufanye moyo wako kuwa mgumu kama hautakuwa makini.
“Kuweni makini sana katika huu wakati mchunge laana mnazotoa katika midomo yenu juu ya huo uamsho unaokuja na kuuita kazi ya Mungu kuwa ni ya shetani. Kwasababu hata mafarisayo walisema maneno hayo hayo japo walikuwa wanauona uwepo dhahiri wa Mungu ukitembea katika dunia. Sio mara zote ni rahisi kufahamu kipi kinatoka kwa Mungu na kipi kinatoka kwa shetani kwahiyo usiwe mwepesi kuhukumu kimakosa huo uvuvi unaokuja. Jinyenyekezeni viongozi wangu, ” Bwana anasema ” Na kwa utulivu hukumuni kazi ya Mungu hichi kipindi kinachokuja, sana sana kama katika kazi za kanisa”
“Kwasababu mimi BWANA nitaijaribu mioyo ya viongozi wangu katika huu uvuvio unaokuja; kwasababu uvivio unaokuja unahitaji kuujaribu uongozi. Mimi BWANA nitafichua siri za mioyo yenu, na kuyakemea mawazo yenu kwa vitu ambavyo hamjawahi kusikia wala msivyovielewa. Lakini kama mkijinyenyekeza na kuwa wavumilivu katika hukumu zenu katika hichi kipindi, Mimi Bwana nitawafunulia kazi zangu ni zipi na za shetani ni zipi.
“Mimi Bwana nitawafanya mtambue tofauti kati ya mwanga na giza. Lakini hawatapewa ujuzi huo viongozi wote wenye majigambo na wenye kujikweza na kujidhani kuwa wana mamlaka yote. Hawatapewa watu wanaojiona wanajua vitu vya Mungu. Siri za Mungu hawatapewa watu wale waliowepesi kuhukumu bali wale wanyenyekevu ndio watakaopewa kuzijua hizi siri.
Katika huu uamsho unaokuja kutafunuliwa vitu vya ajabu, siri zilizojificha, na vitu ambavyo huwezi kuvitegemea, Mimi Bwana nitaleta watenda miujiza na sio tu waponyaji, hawa watafanya miujiza ambayo hamjawahi kusikia wala kuona. Lakini msiogope kwa hivyo vitu msivyovielewa, Kwa kuwa mimi Bwana nitakuwa pamoja nanyi nami nitawapa uwezo wa kutambua. Nitaenda kuwasaidia, viongozi wangu, Mitume wangu, Manabii wangu, Wachungaji wangu, lakini muwe wanyenyekevu na msiwe wepesi kuhukumu. Hili ndilo Neno nalowapeni leo kuwaanda ninyi katika huo uvuvio unaokuja.
Love & Blessings,
Stephen Powell,
Lion of Light Ministries.
Hivi karibuni ndugu Sadhu ambaye ni nabii mwenye asili ya India Bwana amekuwa akimtumia kutoa nabii nyingi na kuja kutimia ikiwemo ushindi wa Obama 2008 na Donald Trump 2016 , mafuriko na matetemeko ya ardhi, mengi pamoja na tetemeko litakalokuja kutokea Calfornia Marekani hivi karibuni, Alionyeshwa na Bwana Yesu Katika maono kwamba nguvu ya uvuvio iliyokuwepo juu ya nabii William Branham itarejeshwa tena ikiwa na nguvu mara saba”, kwa vijana wadogo ambao Mungu ataenda kuwanyanyua. Bwana alimwonyesha katika maono mengine mengi kuwa nguvu ambayo itaenda kuachiliwa katika huu wakati ukifika itakuwa ni kubwa sana na miujiza isiyokuwa ya kawaida itatendeka alisema. bofya hapa kutazama video .
Na kuna manabii wengi wameonyeshwa uamsho huo utakao kuja duniani, baadhi yao ni Rick jonyer, Kenneth Hagin, Neville Johnson, Vincent selvakumar n.k.
Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitika. Katika neema tulionayo sasa hivi umejiwekaje tayari umepokea Roho Mtakatifu?. Jitahidi utubu ndugu injili zinazokuja huko mbele sio za kuwafanya watu watubu tena bali ni kwa ajili ya hukumu na ushuhuda kwa watu tu , wakati wa kutubu ndio sasa, wakati wa kupita katika mlango ulio mwembamba ndio sasa, Tafuta mahusiano yako binafsi na Mungu epuka kamba za madhehebu uwe tayari maana Bwana yupo mlangoni kurudi. Ndugu huu ni wakati wa kukaa chini na kumtafuta muumba wako, kalenda ya Mungu isikupite usilemewe na mambo ya ulimwengu huu, Bwana Yesu alisema tukeshe ili siku hiyo isitujie kama mwivi maana ndivyo itakavyoujia ulimwengu mzima. Kukesha sio kujizuia kulala bali ni kuwa macho rohoni, ujumbe wa Mungu unapokushukia uufahamu.
Luka 13:23-28″ Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,
24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.
27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.
28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje”.
Mungu akubariki.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa mawasiliano/Ushauri/kuokoka/Whatsapp. Namba zetu ni hizi
+255693036618/+255789001312
Mada Nyinginezo:
HATUA ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTUONGOZA
ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.
NINI MAANA YA HUU MSTARI “NIMEVIPIGA VITA VILIVYO VIZURI, MWENDO NIMEUMALIZA, IMANI NIMEILINDA”?
HISTORIA YA WILLIAM BRANHAM
Hii neema tulionayo leo itafika mwisho, kuna baadhi ya misemo imekuwa ikisemwa kuwa Mungu wa agano la kale leo hii hayupo, kama yupo zile ishara alizokuwa anatenda agano la kale ziko wapi leo?. Lakini SIKU YA BWANA inakuja ndugu usitamani uwepo! USITAMANI UWEPO! ni mambo ya kuogopesha ambayo usingetamani hata adui yako yampate, Mungu kuzuia ghadhabu yake ni kwa ajili yetu sisi tutubu lakini tusipotubu hukumu itatukuta.
vitasa saba
Kuna vitu vitatu vinavyokuja huko mbeleni, 1) DHIKI KUU, 2) SIKU YA BWANA, 3) ZIWA LA MOTO. Leo tutaitazama hii SIKU YA BWANA ni ipi, itakuja lini na itakuwa inamuhusu nani.
Kwa ufupi ndugu, DHIKI KUU itakuja na tunafahamu itakuwa kwa wakristo watakaokataa kuipokea ile alama/chapa ya mnyama. Hii itamuhusu mpingakristo akiwatesa wakristo wale waliokataa kuipokea ile chapa ya mnyama wale ambao hawakwenda kwenye unyakuo, Ambapo mwishoni mpinga-kristo atafanikiwa kuwaua kikatili wote wasioipokea chapa. Na hii dhiki itadumu kwa muda wa miaka mitatu na nusu, ni wakati wa kutisha sana unakuja mbeleni. Kwahiyo wakati wakristo wachache wanapitia dhiki kuu, wengine wote waliosalia watakuwa wanaendelea kujifurahisha na mambo yao ya dunia wakimfurahia mpinga kristo na utawala wake.
Sasa SIKU YA BWANA itaanza mara tu baada ya DHIKI KUU kuisha ambapo wale wanawali wapumbavu wote watakuwa wameshaondoka,(wameuliwa na mpingakristo) na unyakuo utakuwa umeshapita wakati huo, lakini hao waliobakia walioipokea chapa ya mnyama itawapasa waingie kwenye adhabu kali sana ya Mungu mwenyewe, Kwasababu wameshirikiana na mpinga kristo kuwaua watu wa Mungu na kwasababu wamekataa kumcha Mungu na kuzishika amri zake, ndugu Hii SIKU YA BWANA usitamani uwepo. Kumbuka haitakuwa jehanamu ya moto, bali itakuwa ni adhabu ya hapa hapa duniani.
maandiko yanasema:
Amosi 5:18 “Ole wenu! Ninyi mnaoitamani SIKU YA BWANA; kwani kuitamani siku ya Bwana? Ni giza, wala si nuru.
19 Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma.
20 Je! Siku ya Bwana haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga.“
Pia tukisoma…
Isaya 13:6″ Pigeni kelele za hofu; maana SIKU YA BWANA i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu.
7 Kwa sababu hiyo mikono yote italegea, na moyo wa kila mtu utayeyuka.
8 Nao watafadhaika; watashikwa na utungu na maumivu; watakuwa na utungu kama mwanamke aliye karibu na kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto.
9 Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.
10 Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.
11 Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali;
12 nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri.”
Maandiko yanaposema SIKU YA BWANA hayamanishi ni siku kama siku moja, bali inamaanisha ni kipindi fulani cha WAKATI ambacho Bwana amekitenga kwa kusudi fulani. Kama maandiko yanavyotueleza ni kipindi ambacho kimetengwa cha GHADHABU NA HASIRA ya Mungu kulipiza kisasi kwa wanadamu wote wasiomcha Mungu.
Kipindi Hichi cha SIKU YA BWANA kitadumu kwa muda wa siku 75, Hizi zimepatikana kutoka katika kitabu cha Nabii Danieli 12:12, ambapo tunaona kipindi cha ile dhiki kuu kitadumu kwa muda wa siku 1260, na hapo zimeongezeka siku nyingine kutoka siku 1260 mpaka kufikia siku 1335, kwahiyo ukichukua hizo siku 1335-1260=75.
Kwahiyo hizi siku 75 zilizoongezwa ni mahususi kwa ajili ya BWANA kujilipizia kisasi kwa wanadamu wote waliosalia juu ya uso wa nchi.
Kabla ya SIKU hiyo ya BWANA kuanza Kutakuwa na baragumu saba zitakazopigwa kuitangulia , Hizi Zitabeba hukumu kwa watu wote, kama onyo watu watubu kumgeukia Mungu, Dunia itapigwa kwa mapigo mengi ya ajabu ukisoma Ufunuo 8 utaona hili, ikiwemo, theluthi moja ya maji kuwa damu, theluthi ya maji duniani kutiwa uchungu,theluthi ya mwezi na jua na nyota kupigwa,hebu tafakari kutakuwaje duniani wakati huo mchana kutakuwa kama jioni, giza litakuwa nene usiku na baridi kali sana, nzige wa ajabu watapandishwa kutoka kuzimu, maumivu yao ni kama ya kung’wata na nge, na meno yao ni kama meno ya simba, n.k.
Biblia inasema watu watakitamani kifo lakini hawatakiona, kumbuka hapo bado SIKU YA BWANA haijaanza huo ni mwanzo wa utungu tu, unatangaza hukumu KUU ya Bwana inayokuja mbeleni kwa urefu soma ufunuo sura ya 8 na ya 9. inaelezea haya mapigo ya baragumu saba za Mungu.
Lakini pamoja na mapigo yote hayo ya baragumu biblia inasema watu watakaokuwa juu ya uso wa nchi hawatatubu maovu yao kwasababu roho ya uovu imeshakaa juu yao kwa kuwa wote wamekwisha ipokea ile chapa ya mnyama neema ya Mungu imeondoka juu yao hawawezi kutubu tena.
Kwahiyo mara baada ya dhiki kuu ya mpinga-Kristo kuisha hapo tayari unyakuo ulishapita siku nyingi na wanawali wapumbavu kuuliwa, Sasa Hawa wanadamu waliobaki ndio watakaoingia katika mapigo ya vitasa Saba vya Mungu , katika hayo ghadhabu ya Mungu imetimia : Hebu tutazame vitasa hivi kimoja baada ya kingine.
Ufunuo 16:1 ” Nikasikia sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Enendeni, mkavimimine vile vitasa saba vya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi.
2 Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na JIPU BAYA, BOVU, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake.”
Sasa adhabu hizi zitakuwa ni kwa Dunia nzima na sio theluthi tena ya dunia kama ilivyokuwa kwa zile baragumu saba. Majipu haya tunaona ni mfano wa yale yale waliopigwa wamisri, Kutakuwa na majipu ya ajabu usidhani ni haya ya kuwaida uliyoyazoea, biblia imeyaita ni MAJIPU MABOVU bado hajatokea kabisa duniani, huo ugonjwa bado haujazuka, Tuna magonjwa mengi ya hatari duniani lakini biblia haijayataja yote hayo, lakini ni huu ugonjwa wa MAJIPU tena jipu bovu ndio umetabiriwa utakuja, homa yake itakuwa sio kama hizi za kawaida tulizozizoea. Ndugu usitamani kuwepo huko wewe unayesema Mungu wa agano la kale haishi, siku hiyo utayaona haya wazi wazi.
Ufunuo 16:3 “Na huyo wa pili akakimimina kitasa chake juu ya bahari, ikawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa.” .
Duniani kutakuwa na harufu kama ya damu ya mtu aliyekwisha kufa, fikiria jambo hilo dunia nzima kutoa uvundo, hakutakuwa na kiumbe chochote baharini chakula kitapungua duniani, maji yataisha, shughuli za usafirishaji baharini nk. vitakwama, mvua zitaacha kunyesha duniani kutakuwa sio sehemu ya kuishi tena mwanadamu, taabu itaongezeka duniani, hofu kuu itawaingia watu wakitazama ni mambo gani haya yameipata dunia?.. lakini bado mapigo yatakuwa yanaendelea,
Ufunuo 16:4-7 ” Na huyo wa tatu akakimimina kitasa chake juu ya mito na chemchemi za maji; zikawa damu.
5 Nami nikamsikia malaika wa maji akisema, Wewe u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako, Mtakatifu, kwa kuwa umehukumu hivi;
6 kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; nao wamestahili.
7 Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, ni za kweli, na za haki, hukumu zako. “
Baada ya bahari kugeuzwa kuwa damu ya mizoga, watu wote tunajua wangekimbilia kutafuta maji katika mito na kwenye chemchemi za maji, kutokana na kiu kikali, lakini Bwana atayapiga pia maji ya mitoni na chemchemi, wakati huo fedha itakuwa haifanyi kazi tena, Mtu tajiri atakuwa ni mwenye kikombe cha maji safi mkononi mwake na sio fedha, Kwahiyo Bwana atawalazimisha kuyanywa hayo maji ya DAMU kwasababu walishirikiana na yule mnyama kumwaga damu ya watakatifu wa Mungu, hivyo nao Bwana amewapa wainywe. Na kwasababu ya kiu kali watakunywa hiyo damu, na wanadamu wengi wataangamia na kufa kwa pigo hilo.
Ufunuo 16:8-9 “Na huyo wa nne akakimimina kitasa chake juu ya jua, nalo likapewa kuwaunguza wanadamu kwa moto.
9 Wanadamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, nao wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo; wala hawakutubu wala kumpa utukufu.”
Baada ya pigo la maji kuwa damu, jua litashushwa chini, maunguzo yatakuwa ni makubwa sana, joto litaongezeka duniani kwa nyuzi joto kubwa kuliko kiwango cha kawaida. Mimea yote itakauka, dunia itafanana na jangwa ndani ya muda mfupi sana, jaribu kutafakari jipu linapigwa na jua kali halafu hakuna maji hata kidogo ya kujipooza,ni dhiki kiasi gani? ni mambo ambayo huwezi dhania yatatokea lakini yapo mbioni kutokea. Lakini pamoja na hayo mapigo yote biblia inasema watu watamtukana Mungu hawatatubu. Mfano tu wa kizazi chetu hichi watu wanapopatwa na majanga badala wageuke na kumuuliza Mungu ni kwanini na kutubu, wao wanalaani.
Ufunuo 16:10-11 “Na huyo wa tano akakimimina kitasa chake juu ya kiti cha enzi cha yule mnyama; ufalme wake ukatiwa giza; wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu,
11 wakamtukana Mungu wa mbingu kwa sababu ya maumivu yao, na kwa sababu ya majipu yao; wala hawakuyatubia matendo yao. “
Sasa pigo hili linamuhusu sana sana yule mnyama aliyewakosesha wanadamu wote kuipokea ile chapa, mahali kiti chake cha enzi kilipo ambapo ni VATICAN, Roma, Mungu ataachilia laana kwa mataifa ya ulaya ambayo ndio zile pembe kumi, zitamchukia na kumwangamiza yule mwanamke kahaba (Kanisa Katholiki) ambalo makao yake makuu ni VATICAN.
Hii ni kutokana na kwamba yale mataifa ambayo yalimtumaini mpinga kristo ayaletee amani duniani, hayajaletewa zaidi ya yote mpingakristo (PAPA) ameiongezea dunia matatizo hivyo basi watamchukia na kumwangamiza, tangu wakati huo utawala wa Roma, pamoja na mpinga kristo (PAPA) na Vatican yake hawatakuwepo tena ufalme wao umekwishatiwa giza.
Soma
ufunuo 17:16″ Na zile pembe kumi ulizoziona, na huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto. ”
Ufunuo 16:12 “Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.
13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.
14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.
15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)
16 Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.”
Kitasa hichi kunazungumzia ile vita kuu ya HAR MAGEDONI ambayo itakuwa ni vita kati ya Mungu mwenyezi akilipigania taifa la Izraeli dhidi ya wafalme wote wa dunia. karibu kila taifa litaunga mkono vita hii wakiongozwa na mataifa kutoka mawio ya jua. Haya mataifa ya mawio ya jua ni mataifa ya mashariki, nayo ni CHINA,JAPAN, KOREA n,k. Wakati huo Vatican itakuwa haipo, Marekani itakuwa haipo, Urusi itakuwa haipo yatatoweshwa katika vita vilivyoelezwa katika ezekieli 38 & 39,
Kwahiyo zile roho chafu ambazo zilikuwa zinaendesha Vatican na Marekani zitahamia kwenye haya mataifa ya mashariki yaliyosalia kwa ajili ya vita dhidi ya Izraeli. Wakati huo ndio Bwana YESU atakapotokea kuwapigania watu wake Izraeli. Ndugu wakati huo dunia itakuwa mfano wa sayari ya Zebaki, hakutakuwa na maji, chakula, magonjwa, joto litakuwa juu sana,maji yote damu, machafuko pamoja na vita, usitamani ndugu yangu uwepo nakuombea Mungu usiwepo itakuwa ni vilio na kusaga meno, siku hiyo watu watatamani siku hizi za neema tulizonazo leo hawataziona.
Ambacho ndio hasaa kinaizungumzia ile siku ya Bwana..
Ufunuo 16:17-21 ” Na huyo wa saba akakimimina kitasa chake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu, katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa.
18 Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo.
19 Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.
20 Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena.
21 Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.”
Hili ni pigo la mwisho, na katika hili ghadhabu ya Mungu imetimia tukisoma pale muhuri wa sita ulipofunguliwa ulitoa picha halisi jinsi hii siku itakavyokuwa soma Mathayo 24:30-31 na pia Ufunuo 6:12-17
Ufunuo 6:12-17 ” Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,
13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.
14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.
15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.
17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?”
Pigo la saba la mwisho kama tunavyosoma ni baya kuliko yote yaliyotangulia maana jua linaondolewa, mwezi utakuwa damu, nyota zitatoweka, unaweza kuona kutakuwa na giza kiasi gani duniani, na baridi kiasi gani,litakuwaa ni giza zito sana, hakutakuwa na chanzo chochote cha umeme, shughuli zote za kimaendeleo zilishamalizwa katika mapigo yaliyotanguliwa, hadi kufikia hapa watu wachache sana watakuwa wamesalia duniani, kumbuka hapo bado ziwa la moto linasubiri watu, Hichi ni kisasi cha hapa hapa duniani.
Mvua ya mawe kubwa sana itanyesha, mawe kama talanta,(talanta 1 ni kama kg 34), Huwezi kujificha kwenye nyumba yako ya bati au ya kigae, kg 34 ni uzani mkubwa sana itaambana na tetemeko ambalo halijawahi kutokea, kiasi cha kwamba visiwa vitahama, kisiwa cha zanzibar kitapotea, Milima itatapika volkano, kumbuka hayo yote yatafanyika katikati ya giza nene, hakuna mawasiliano. hapo hakuna mfalme wala mtumwa, raisi wala mwananchi wote waliosalia watatamani wafe kuliko kuishi, watatamani milima iwaangukie waikwepe ghadhabu ya Mungu, Hapo ndipo itakapoonekana ishara ya mwana wa Adamu mawinguni.
Soma
Mathayo 24:29 “Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; 30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. “
Rafiki haya mambo ni kweli yatatokea, ndivyo yatakavyokuja kuupata ulimwengu na dalili zote zinaonyesha kuwa yatatokea katika kizazi chetu tunachoishi mimi na wewe, Bwana amekwisha kutuonya mbele, Nia yake ni sisi tuiepuke hiyo ghadhabu na ndio maana kuna mahali alisema alipokuwa katikati ya kitasa cha sita (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake). Kwahiyo ametuonya tukeshe na kuyatunza mavazi yetu, maana hii siku ya ghadhabu itakuja ghafla.
Ndugu kimbia injili ambazo zinakufanya usifikiri hatma ya maisha yako ya milele badala yake inakupeleka kutazama mambo ya ulimwengu huu. Hii ni roho ya shetani inawapumbaza wengi wafikiri mambo hayo yatakuja kutokea baada ya miaka 2000 mbele, usidanganyike ni uongo wa shetani, ndugu dalili zote zinaonyesha, unabii wote umetimia kwamba tunaishi katika kizazi cha hatari sana.
Chunguza maisha yako angali neema ipo, mambo hayatakuwa hivi siku zote, pale mlango wa neema utakapofungwa kutakuwa hakuna kurudi nyuma itakuwa ni vilio na maombolezo, kimbilia kalvari sasa tubu dhambi zako, uoshwe kwa damu ya Yesu, na Upokee Roho Mtakatifu kabla ya huo wakati kufika. Kumbuka adhabu ya hii SIKU YA BWANA, sio jehanamu ya moto, baada ya mapigo hayo ndipo ziwa la moto ziwa la moto litafuata.
Ikiwa unataka kumpa Bwana Yesu maisha yako na kugeuka leo tubu mwenyewe moyoni mwako au fuatiliza sala hii kwa imani:
Sema:
“Bwana Yesu, Leo hii nasogea mbele zako nikiwa mwenye dhambi, natubu makosa yangu yote niliyokukosea, naomba unisamehe, nimeamua kugeuka leo, nisaidie Bwana Yesu, neema yako iwe juu yangu, nikuishie wewe, siku zote za maisha yangu, asante Bwana Yesu kwa kunisikia na kunisamehe. AMEN! “.
Baada ya kutubu unahitaji kubatizwa, Hivyo basi tafuta kanisa linalobatiza ubatizo sahihi nao ni kwa kuzamishwa kwenye maji mengi na ni kwa jina la YESU KRISTO, Kwa kufanya hivyo Bwana atakupa kipawa cha Roho Mtakatifu na utakuwa umekamilisha wokovu wako.
MUNGU AKUBARIKI.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Kwa msaada zaidi, wa kanisa, au mafundisho, au ushauri, piga namba hizi
+255693036618/ +25578901312
Mada Nyinginezo:
KIKOMBE CHA GHADHABU YA MUNGU KINAJAA…TUBU UMGEUKIE MUNGU
NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.
JE! SISI NI WAFALME NA MAKUHANI KWA NAMNA GANI?
PETRO ALIAMBIWA NA BWANA YESU UKIONGOKA WAIMARISHE NA NDUGU ZAKO. JE! KUONGOKA MAANA YAKE NINI?
Mpinga-Kristo ni nani?
Vita kubwa inayoendelea duniani leo ni vita kati ya MUNGU na SHETANI. Mungu anatafuta roho za watu vile vile shetani naye anawinda roho za watu. Hizi roho mbili zimekuwa zikipingana siku zote tangu ulimwengu ulipoanza kukaliwa na wanadamu.
Lakini baada ya mwanadamu kuanguka Mungu alitumia njia zote kwa Roho wake kumvuta kwake tena, mwishoni akaona vema kumleta mwanawe mpendwa YESU KRISTO kwa dhumuni moja tu! kutupatanisha sisi na Mungu, ili katika yeye sisi sote tuokolewe.
Vivyo hivyo shetani naye, kwa kuona hivyo kwa roho yake ya uovu, alitumia njia zake zote za kuweza kumtoa mwanadamu katika kusudi la Mungu na kumvuta kwake, jambo hili lilianza tangu Edeni, tunaona shetani jinsi alivyomtumia Nyoka kumdanganya Hawa ili aipate roho yake. Hivyo basi ulipofika wakati alipoona Mungu amemleta mwokozi katika mwili yaani YESU KRISTO na kuwavuta wengi kwa BABA, yeye naye alianza mipango ya kumwandaa mtu mmoja ambaye atakuwa na kazi maalumu ya kuwavuta watu kwake na kwenda kinyume na huyo mmoja Mungu aliyemteua (yaani YESU KRISTO). Sasa mwana huyu wa shetani ndiye anayeitwa MPINGA-KRISTO.
Kumbuka vita vya kwanza kabla ya Kristo kuja vilikuwa ni roho kwa roho (yaani Roho wa Mungu dhidi ya roho ya shetani), lakini vita vya mwisho ni MTU dhidi ya MTU (yaani YESU KRISTO dhidi ya MPINGA-KRISTO).
Wakristo wengi wanapokosa shabaha ni pale wanaposhindwa kumfahamu YESU KRISTO ni nani na MPINGA-KRISTO ni nani?. Ukishindwa kumfahamu YESU KRISTO ni nani huwezi kumfahamu MPINGA-KRISTO ni nani.
Hawa wote wawili waliandikwa kwenye NENO la Mungu katika “SIRI”. Ikiwa na maana utendaji kazi wao ulihitaji “UFUNUO wa ROHO” Kuutambua. Embu kwa ufupi, tutazame siri iliyopo kwa YESU KRISTO ambayo ilikuwa imefichika kwa Muda mrefu na hata sasa baadhi ya watu bado imefichika machoni pao.
1 Timotheo 3:16 ” Na bila shaka SIRI YA UTAUWA NI KUU. Mungu alidhihirishwa katika MWILI, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.”
Ukisoma hapo utaona kuwa jambo hili Mungu aliliweka liwe SIRI,na sio kitu cha wazi ya kwamba Yesu Kristo alikuwa ni MUNGU KATIKA MWILI. Yaani ni Roho ya Mungu ikitenda kazi katika mwili, lakini wengi hawakulijua hilo walimkataa na kumsulubisha,na hata leo wengi hawalifahamu hilo. maana Bwana Yesu alisema “Yohana 5:43 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo. “ unaona huyo mwingine BWANA YESU aliyemzungumzia akija kwa jina lake mtampokea ni MPINGA-KRISTO mwenyewe..tusome tena mstari ufuatao
1 Wakoritho 2:6-8″ Walakini iko HEKIMA tusemayo KATI YA WAKAMILIFU; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika;
7 bali twanena HEKIMA YA MUNGU KATIKA SIRI, ILE HEKIMA ILIYOFICHWA, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;
8 ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, WASINGALIMSULIBISHA BWANA WA UTUKUFU; “.
Kwa maandiko hayo hapo juu, hata leo watu katika mioyo yao wanamchukulia YESU KRISTO kama ni mtu wa kawaida kama walivyofanya watu wa kipindi kile, wanayadharau maneno yake sio kwa mdomo bali kwa matendo, lakini hawajui kuwa wanamkataa na kumsulibisha Mungu mwenyewe ambaye ni BWANA WA UTUKUFU, kwa heshima aliitoa damu yake, imwagike kwa ajili ya dhambi zetu kutupatanisha sisi na yeye lakini bado leo hii unaichezea hii damu ya thamani, itafika wakati hii neema haitakuwepo tena.
2 Wathesalonike 2:3 “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; AKAFUNULIWA YULE MTU WA KUASI , MWANA WA UHARIBIFU;
4 YULE MPINGAMIZI, AJIINUAYE NAFSI YAKE JUU YA KILA KIITWACHO MUNGU AMA KUABUDIWA; hata yeye mwenyewe kuketi katika HEKALU LA MUNGU, AKIJIONYESHA NAFSI YAKE KANA KWAMBA YEYE NDIYE MUNGU.
5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?
6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.
7 Maana “ILE SIRI YA KUASI” HIVI SASA INATENDA KAZI; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.
8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule ASI, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;
9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;
10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.”
Ukisoma habari hiyo mstari wa saba inazungumzia SIRI YA KUASI ambayo inatenda kazi duniani, na hii siri ya kuasi inatenda kazi ndani ya yule ASI (ambaye ndio mpinga-kristo mwenyewe) kama maandiko yanavyomtaja kwenye mstari wa 9, kuwa “kutenda kwake kazi ni mfano wa kutenda kwake shetani mwenyewe”. Kama tu vile SIRI YA UTAUWA ilivyokuwa inatenda kazi ndani ya YESU KRISTO, na kutenda kwake kazi Yesu kulikuwa ni mfano wa kutenda kwake Mungu mwenyewe vivyo hivyo na huyu (Mpinga-kristo) siri ya kuasi inatenda kazi ndani yake na kutenda kwake kazi kutakuwa ni mfano wa shetani.
Baada ya shetani kuona kuwa hawezi kuwapata wanadamu wengi kwa kutaka wamwabudu moja kwa moja kama wanadamu wamwabuduvyo Mungu, aliamua kujibadilisha na kujifanya kuwa kama malaika wa Nuru (2Wakoritho 11:14), ili awapate wale wanaoonyesha dalili ya kuipenda Nuru. Kumbuka shetani hafanyi vita na watu wa ulimwengu huu, kwasababu hao alishawapata na siku zote wapo gizani, kwahiyo ili awapate wale wa nuruni ni lazima ajigeuze kuwa mfano wa malaika wa Nuru, vivyo hivyo na watumishi wake nao ni lazima wajigeuze kuwa kama watumishi wa nuru. Hapo ndipo penye vita vikali pale mbwa-mwitu anapokuja kwa vazi la kondoo. Hivyo inahitaji hekima ya Roho Mtakatifu kumtambua mpinga-kristo vinginevyo hawatakaa ufahamu adui yako yupo wapi na anatendaje kazi.
Ndugu kuna vikundi vingi vya kishetani na kichawi, vinavyosifika kama freemason, rotary clubs, iluminati, ku klux klan, brotherhood, n.k. vimekuwa vikiogopeka kana kwamba hivyo ndio makao makuu ya shetani, usidanganyike vikundi hivyo shetani anavitumia kuwadaka watu wasiokuwa wakristo na wakristo wachache wenye imani isiyothabiti kwasababu mkristo wa kweli yoyote hawezi kwenda kwa mganga na shetani analijua hilo, wala hawezi kujiunga kwenye mojawapo ya hivyo vikundi wala kupiga ramli, au kupunga-pepo, shetani anajua kabisa kama angetegemea njia hiyo tu, basi angewakosa wakristo wengi sana duniani. Anafahamu kuwa mkristo mahali pake pekee anajihisi atakutana na Mungu ni kanisani na ndiko huko huko anapowafuata wakristo.
Kumbuka, shetani anatenda kazi katika SIRI, na ndiyo maana ikaitwa “SIRI YA UASI”. na inatenda kazi ndani ya Kanisa la Mungu pale shetani anapovaa mavazi ya kondoo lakini ndani ni MBWA-MWITU(Hii ni SIRI). kuharibu roho za watu(wakristo wa kweli) na kuwapeleka kuzimu. Anatumia hila zake kuwafanya watu waone kama wanamwabudu Mungu, kumbe wanamwabudu yeye.
Anaingia kanisani na kuwafanya watu wajione kuwa wapo katika njia sawa, lakini mwisho wake ni kuzimu,. Na anaowapeleka kuzimu kwa njia hii ni kubwa sana kuliko hata hizo njia nyingine ndogo ndogo kama uchawi, freemason n.k. HAPA NDIPO KRISTO ALIPOTUTILIA MSISITIZO KWAMBA “TUJIHADHARI NA MANABII WA UONGO, WANAOVAA MAVAZI YA KONDOO LAKINI NDANI NI MBWA-MWITU WAKALI”..Ndugu, Bwana hakutuonya tujihadhari na wachawi au wapiga-ramli, au freemason, au wapunga-pepo hilo ni jambo dogo sana ambalo kwa namna ya kawaida mkristo yoyote anaweza kujihadhari nayo.
Baada ya shetani kujiingiza kwa siri kwenye kanisa la Mungu na kukomaa kwa muda mrefu, tunaona alianza kwa kuharibu mafundisho ya Mungu ya kweli na kupachika mafundisho ya kipagani kama ibada za wafu, ibada za miungu mitatu, kuongeza vitabu katika NENO la Mungu, Ibada za sanamu kanisani, kubariki pombe kanisani, na kupindisha maandiko na utaratibu uliokuwepo wa kanisa kwa kupotosha ubatizo sahihi wa maji, na wa Roho Mtakatifu, kwa kuua karama za roho, kuingiza siasa na vyeo katika kanisa visivyotakana na Mungu,kuua mafundisho ya uponyaji wa kiungu, n.k.
Kwa kuendelea hivyo alifanikiwa kutengeneza kanisa lake moja “MFU” lenye jina linalofanana na lile kanisa la mwanzo la kweli lakini sio, watu wakidhani kuwa ndio lile kanisa la kwanza (la Mitume) kumbe wamepotea pasipo wao kujua ROHO MTAKATIFU ameshaondoka muda mrefu imebaki roho ya shetani ikitawala, Kwahiyo shetani akalipa jina hili kanisa lake akaliita UNIVERSAL CHURCH yaani KANISA LA ULIMWENGU (KANISA KATOLIKI).
Na yeye (shetani) akiwa kama mungu wa hilo kanisa aliweka watumishi wake, Na akaweka cheo cha juu zaidi kabisa katika hilo kanisa ambacho ndio cheo kile cha UPAPA (hichi ndicho cheo cha MPINGA-KRISTO mwenyewe) kisimame kwa niaba yake duniani kama Yesu Kristo alivyosimama kwa niaba ya Mungu duniani.
Tunafahamu katika historia chombo chake kiteule alichokitumia shetani kupambana na uzao wa Mungu ni KANISA KATOLIKI,na si kingine, lilifanikiwa kuua zaidi ya wakristo milioni 68, waliojaribu kuenda kinyume na mifumo yake ya kipagani. Na hadi leo kanisa hili linaendelea kuuwa watu wengi kiroho, kwa kudhani wanamwabudu Mungu kumbe wanamwabudu shetani katika hilo kanisa. Na litakuja kuuwa wengi zaidi katika kipindi cha ile dhiki kuu. HAYA NDIYO MALANGO YA KUZIMU.
Hivyo basi roho ya mpinga-kristo inakaa katika cheo cha UPAPA, kwahiyo mtu yeyote atakayekikalia hicho cheo atakuwa amekidhi vigezo vyote kuwa MPINGA-KRISTO.
Injili iliyopo leo hii, kulingana na wakati tunaoishi sio injili tu ya kuwavuta watu kwa Kristo, kwasababu wengi wameshampokea Kristo lakini hawajui kuwa wanamwabudu shetani pasipo wao kujua katika madhehebu yao wakidhani kuwa wapo sawa kumbe hawapo sawa. Ndugu Mungu kashatoa laana juu ya kanisa Katoliki na madhehebu yote yasiyokaa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, (maana haya kwa pamoja ndiyo yanayounda ile chapa ya mnyama). Kwa kufahamu zaidi kwa undani juu ya chapa ya mnyama unaweza kusoma soma tuliloliandika linaloitwa “CHAPA YA MNYAMA”.
Haya ndiyo maneno ya Bwana mwenyewe.
Ufunuo 18:4-5″ Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU, MSISHIRIKI DHAMBI ZAKE, WALA MSIPOKEE MAPIGO YAKE.
5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. “
Bwana anatuonya tutoke (sio kutoka kwa miguu bali kwa roho. Yaani kujihadhari na mafundisho yote yasiotoka na Mungu, ukiri ukristo wa biblia usiukiri udhehebu) Toka katika kamba za madhehebu, umwabudu Mungu katika roho na kweli kwasababu hayo yamefanya uasherati wa kiroho kwa kuchanganya NENO la Mungu na mafundisho ya kipagani hivyo Bwana ameyahukumu na yoyote atakayeshirikiana nayo atashiriki katika mapigo yake yote yaliyoandaliwa kwasababu yameshiriki katika kumwaga damu nyingi za watakatifu wa Mungu.
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo: