Bwana Yesu alikuwa anamaanisha nini kusema Marko 2:19″walioalikwa harusini wawezaje kufunga maadamu bwana-arusi yupo pamoja nao?”

Bwana Yesu alikuwa anamaanisha nini kusema Marko 2:19″walioalikwa harusini wawezaje kufunga maadamu bwana-arusi yupo pamoja nao?”

Marko2:18 “Nao wanafunzi wake Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga; basi walikuja, wakamwambia, Kwani wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wa Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi?
19 Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kufunga maadamu bwana-arusi yupo pamoja nao? Muda wote walipo na bwana-arusi pamoja nao hawawezi kufunga.
20 Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana-arusi, ndipo watakapofunga siku ile.   

JIBU: shalom! Mfano huo sawa tu, na mwanafunzi aliye na mwalimu wake, pindi anapokuwa naye anao uwezo wa kumuuliza swali lolote na likajibiwa, au akampelekea mwalimu wake maswali yote magumu yanayomsumbua na yakatatuliwa pindi wakati yupo naye, lakini kikifika kipindi cha mitihani, labda mtihani wa NECTA, pale ambapo anawajibika kuketi mwenyewe kwenye chumba cha mtihani mahali ambapo mwalimu wake hawezi kuwepo tena hapo ndipo itampasa atumie nguvu na jitihada ya ziada kutatua maswali yote peke yake anayokutana nayo kwa maarifa aliyopewa na mwalimu wake, lakini hapo mwanzo angeweza kumpelekea tu kila swali linalokuja mbele yake na akasaidiwa pasipo hata kujishughulisha…  

Na ndivyo ilivyokuwa kwa mitume wa BWANA wetu YESU KRISTO wao walipewa neema ya kipekee kutembea na Mungu( BWANA YESU) duniani tofauti na wanafunzi wa Yohana au masadukayo, sasa unategemea vipi watu kama hao wafunge, au kujisumbua kwa lolote, wakati wanayemwomba wapo naye hapo hapo…wakiwa wanahitaji ufunuo wa jambo fulani si wanamkimbilia BWANA na kumuuliza kwasababu yupo nao hapo?!!!…

Na ndio maana akasema wakati utafika Bwana arusi atakapoondolewa…hapo ndipo watalazimika kufunga kama wenzao. Wakitaka ufunuo wa jambo fulani sasa itawapasa wafunge, wakitaka kutatua au kujua jambo fulani itawapasa wafunge kwanza na kuomba,Kwahiyo kile kitendo cha wao kutembea, kula, kuishi na kufundishwa na BWANA ndio kualikwa kwenyewe Harusini.   Kuna kipindi Bwana alimwamsha Petro na wenzake wasali, lakini walilemewa na usingizi wakalala, lakini baada ya Bwana kuondoka unamwona Petro anakuwa wa kwanza kusali na kufunga mpaka anazimia kwa njaa (Matendo 10:9).  

Kadhalika na sisi tunapompokea Kristo kwa mara ya kwanza kunakuwa na neema fulani ya kipekee inakuwa juu yetu, kila tuombalo tunalipokea haraka sana, kwasababu bado hatujajua umuhimu wa kuomba, hatujajua umuhimu wa kufunga, hivyo neema ya Mungu inakuwa juu yetu kubwa kama watoto wachanga, lakini unafika wakati Bwana anaipunguza ile neema, (Bwana arusi anaondolewa )unakuwa ili upate jambo fulani inakupasa uombe kwa bidii, wakati mwingine kwa kufunga, ili upate ufunuo wa Roho inakupasa kujifunza sana maandiko kwa muda mrefu n.k, kwasababu unakuwa sio mtoto tena, Bwana anakutoa hatua moja kwenda nyingine.  

Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.

MUNGU NDIYE ANAYEISHAWISHI MIOYO.

JIKANE NAFSI MTEULE WA MUNGU.

NINI MAANA YA HILI ANDIKO “USHUHUDA WA YESU NDIO ROHO YA UNABII” (UFUNUO 19:10)?

NGUVU ZA ZAMANI ZIJAZO:


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Edson Mugisha
Edson Mugisha
2 years ago

Aise, nimejifunza mambo makubwa hapa, hili ni jibu la swali ambalo limeleta gumzo kidogo. Atukuzwe BWANA kwa hili na mwalimu amuinue zaidi hakikaA