SWALI: Nini maana ya kuutia moyo ufahamu? Mtu anatiaje moyo wake ufahamu?
Danieli 10:12 “Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako”.
JIBU: Ukisoma kitabu cha Danieli chote utagundua Danieli alikuwa ni mtu ambaye si wa kuchulia mambo juu juu tu..alikuwa ni mtu anayechunguza na kufuatilia mambo baada ya kusikia
Kwa mfano angalia ile ndoto aliyoota Nebukadreza..ndoto ile hakuota Danieli, lakini baadaye alipoona ina maana kubwa alimwomba Mungu ampe kujua zaidi..Na ndio hapo utaona Danieli akifuniliwa kwa undani mkubwa sana mambo yahusianayo na ile ndoto, Juu ya zile Milki nne za ulimwengu. Soma Danieli 2,5,7
Ukisoma tena Danieli sura ya 9 utaona..alipokuwa anasoma vitabu akagundua kuwa kumbe imeshaandikwa na nabii Yeremia kuwa Israeli watakaa Babeli kwa muda wa miaka 70 tu..Hilo jambo lilimshangaza kwasababu hakuwahi kudhani kama Israeli ingekaa utumwani kwa muda mfupi vile. Hivyo hakukaa hivyo hivyo tu..Ndipo akaanza kumlilia Mungu kwa toba..baadaye Mungu akamfunilia jinsi itakavyokuwa mpaka mwisho.
Vivyo hivyo kuna wakati mwingine mbeleni biblia inatuambia Danieli alifunuliwa jambo lingine jipya..japokuwa jambo hilo halijaandikwa katika biblia ni lipi…lakini linaonekana lilikuwa ni la kutisha na ndio maana alisema ni vita vikubwa..Sasa alipofuniliwa kwa muhtasari tu,, kama kawaida yake hakukaa tu hivi hivi..bali aliingia katika maombi ya mfungo na maombolezo kwa muda wa wiki tatu nzima kumsihi Mungu amfunulie..
Tusome..
Danieli 10:1-3,
[1]Katika mwaka wa tatu wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, Danieli, ambaye jina lake aliitwa Belteshaza, alifunuliwa neno; na neno lile lilikuwa kweli; maana ni vita vikubwa; naye akalifahamu neno lile, akaelewa na maono hayo.
[2]Katika siku zile mimi, Danieli, nalikuwa nikiomboleza muda wa majuma matatu kamili.
[3]Sikula chakula kitamu, wala nyama wala divai haikuingia kinywani mwangu, wala sikujipaka mafuta kabisa, hata majuma matatu kamili yalipotimia”.
Unaona…Sasa tukiendelea kusoma mbeleni ndio tunaona akitokewa na yule malaika. Na kumwambia maneno haya;
Danieli 10:12
[12]Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako.
Kumbe kitendo cha Danieli kuzingatia jumbe alizopewa..mbinguni alikuwa anaonekana kama mtu aliyetia moyo wake ufahamu ili kutaka kujua.
Ni nini tunajifunza kwa Danieli?
Hata sasa, Mungu anatafuta watu kama hawa. Ni mara ngapi watu wanamsikia Mungu akizungumza nao kwa njia mbalimbali hususa kwa Neno lake lakini hawataki kutia mioyo yao ufahamu kusikia?.
Na ndio hapo utashangaa mtu anaona kila kitu ni sawa tu. Hajui kuwa ni Mungu anataka kumpigisha hatua nyingine..lakini yeye anaenda kwa desturi na mazoea ..kila siku kanisani ni kusikia tu Neno basi hatii moyo wake ufahamu wa kutaka kusikia sauti ya Mungu inamwambia nini nyuma yake(Maana yake kuwa hatilii maanani).
Na ndio maana hakuna badiliko lolote la maisha yake.
Mungu huwa anataka tutie mioyo yetu ufahamu kwanza ndipo aseme na sisi zaidi au kutuhudumia, kama alivyokuwa akifanya Danieli.
Shalom
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Je! Watu ambao hawajawahi kusikia injili kabisa siku ya mwisho watahukumiwa?
Yohana 9:39 “Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu”
Jibu: Ukisoma habari za Bwana Yesu utaona kuwa alikubaliwa na watu wanyonge na wenye dhambi lakini alikataliwa na watu wa Imani na wa dini (yaani Makuhani, waandishi, mafarisayo pamoja na masadukayo)..ambao wao walikuwa wanajiona wenye haki..
Sasa ili tuelewe vizuri hebu tujifunze katika mfano wa kawaida wa maisha.
Mtu anayetembea gizani na tochi yake mkononi, ule mwanga wa tochi akiutumia kumulika mbele yake katika njia anayoiendea utamfanya aone gizani, lakini akiigeuza ile tochi na kuyamulika macho yake, ule mwanga utamuathiri, utamfanya asione..
Ndivyo Mafarisayo na Masadukayo kilichowapata, walikuwa wanaenda kinyume na Nuru na maandiko yanasema Yesu ndiye Nuru ya ulimwengu (Yohana 8:12).Hivyo ile nuru ikawapofusha macho.
Laiti mafarisayo na Masadukayo wangeitumia nuru hiyo kumulika njia zao,wasingekuwa vipofu lakini kwasababu walikuwa wanaenda kinyume na ile Nuru, ikawapofusha macho kama ilivyompofusha Sauli alipokuwa anakwenda Dameski kuwaua watakatifu. (Soma Matendo 9:1-19).
Hiyo inatufundisha kuwa wanyenyekevu na kulitii Neno la Mungu..Tukijiona kuwa tunajua kila kitu au tunajua zaidi ya wengine wote, kama Mafarisayo na Makuhani na wala hatuhitaji kujua zaidi, wala kujifunza zaidi basi tujue tunakwenda kinyume na ile Nuru,Basi tufahamu kuwa Neno la Mungu litatupofusha macho, kama lilivyowapofusha mafarisayo, makuhani na Masadukayo.
1 Wakorintho 8:2 “Mtu akidhani ya kuwa anajua neno, hajui neno lo lote bado, kama impasavyo kujua”
Roho Mtakatifu atusaidie na kutubariki.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Maherodi walikuwa ni akina nani, Na kazi yao ilikuwa ni ipi?
Shalom tukisoma Mathayo 25:8 na Marko 16:8, tunaona habari mbili zinachanganya, kuhusu wale wanawake, sehemu moja inasema walikwenda kutangaza na sehemu nyingine inasema walikaa kimya hawakumwambia mtu, je ipi ni sahihi?
Jibu: Tusome.
Mathayo 25:5 “Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulibiwa.
6 Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa.
7 Nanyi nendeni upesi, mkawaambie wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu. Tazama, awatangulia kwenda Galilaya; ndiko mtakakomwona. Haya, nimekwisha waambia.
8 WAKAONDOKA UPESI KUTOKA KABURINI, KWA HOFU NA FURAHA NYINGI, WAKAENDA MBIO KUWAPASHA WANAFUNZI WAKE HABARI”.
Tusome tena habari hiyo hiyo katika Marko…
Marko 16:7 “Lakini enendeni zenu, mkawaambie wanafunzi wake, na Petro, ya kwamba awatangulia kwenda Galilaya; huko mtamwona, kama alivyowaambia.
8 Wakatoka nje, wakakimbia kutoka kaburini; KWA MAANA WAMEINGIA TETEMEKO NA USHANGAO; WALA HAWAKUMWAMBIA MTU NENO, MAANA WALIOGOPA”.
Hapo tunasona habari mbili zinazoelezea tukio moja, lakini ni kama vile habari hizo zinajichanganya, kwamba iweje Mathayo aseme ”wanawake walikwenda kuwapasha wanafunzi habari” na Marko aseme “hawakumwambia mtu neno”.. Swali ni je! Biblia inajichanganya?.
Jibu ni la! Biblia haijichanganyi hata sehemu moja, isipokuwa ni fahamu zetu ndizo zinazojichangaya…
Awali ya yote ikumbukwe kuwa kifo cha Bwana Yesu, kilihusisha Dini na vile vile kilihusisha Serikali. Kwa maana ya kuwa viongozi wa dini (yaani Makuhani na Waandishi) walimshitaki Bwana kwa Serikali(ambayo ilikuwa ni serikali ya kirumi), na Serikali hiyo ndiyo iliyomsulubisha Bwana Yesu. Na baada ya Bwana Yesu kufa kaburi lake liliwekewa walinzi kulilinda!. Lengo ni ili wanafunzi wake wasije wakamwiba na kusingizia kafufuka.
Hivyo kulikuwa na hofu kubwa sana, kwa mtu yeyote ambaye angezusha kuwa Kristo kafufuka!. Kwasababu Serikali ya kirumi ndio iliyokuwa inatawala, na ilikuwa ni serikali ya kikatili, endapo kingezushwa kitu chochote kilicho kinyume na itikadi zao au taratibu zao, sheria ilikuwa ni moja tu! Nayo ni Kifo.
Kwahiyo hata hawa wanawake ambao walitokewa na Malaika na kuwaambia kwamba Bwana kafufuka, wao waliamini, lakini haikuwa vyepesi kwenda kutangaza kwa watu wa nje!. Huko na huko kama Yule mwanamke Msamaria alivyofanya… Isipokuwa kwa watu wachache tu! Wenye imani moja na wao, ambao ndio wakina Petro na mitume wa Yesu.. Hao ndio wanawake waliwapelekea habari za kufufuka kwa Yesu, lakini watu wengine wa nje, kama Mafarisayo au masadukayo, maakida, au ndugu zao ambao hawakumwamini Bwana hawakuwapa taarifa zozote, zilibaki kuwa siri, ndio maana maandiko yanasema hapo hawakusema Neno kwa mtu yeyote.
Kwasababu hata katika hali ya kawaida, Mariamu Magdalena ataogopa vipi kumwambia Petro kwamba Bwana kafufuka?.. Kwani Petro angewafanya nini hao wanawake baada ya kupewa taarifa hizo?, angewapiga? Au angewashitaki kwa Herode?, bila shaka hilo ni jambo ambalo haliwezekani, kwasababu wote hao walikuwa upande mmoja, na tumaini lao ni moja..
Haiwezekani kuogopa kuambiana mambo yaliyojiri kumhusu Bwana wao… isipokuwa kwa watu wa nje, itabaki kuwa siri na fumbo.. ndio maana hata huyo Malaika hakuwaambia wakatangaze habari hizo kwa kila mtu tu!, bali kwa wanafunzi wa Yesu peke yao.
Hivyo hawa wanawake waliificha Siri kwa watu wa nje lakini waliiweka wazi kwa wanafunzi wa Yesu, kama maandiko yanavyosema hapo kwenye Mathayo.
Na hawakuwaambia watu wa nje kwasababu waliogopa!, aidha kuuawa, au kupitia dhiki fulani, kwasababu makuhani na maakida wangewasumbua kuwahoji ni wapi walipomficha..Ndio maana utaona sehemu zote baada ya kufufuka kwa Bwana, mitume pamoja na wanawake hawa, walikuwa wanajificha ndani na kujifungia kutokana na hofu ya kukamatwa, unaweza kuyathibitisha hayo katika mistari hii> Yohana 20:19, Yohana 20:26 na Matendo 2:1
Ni lipi tunaloweza kujifunza?
Kama kufufuka kwake Bwana Yesu kulivyokuwa kwa siri, kiasi kwamba ni watu wachache sana ndio waliojua na kuthibitisha kwamba Bwana kafufuka, wengine wote hawakujua chochote, Herode na Pilato hawakutokewa na Bwana wala malaika, hivyo hawakujua chochote, vile vile na watu wengine hawakutokewa na Bwana wala Malaika wake kuwajuza kuwa kafufuka, maandiko yanasema watu 500 tu ndio waliotokewa na Bwana baada ya kufufuka kwake kati ya Mamilioni waliokuwa wanaishi duniani,siku hizo..
Ndivyo itakavyokuwa katika siku ya unyakuo.. Itakuwa ni tendo la ghafla na la siri!. Siku parapanda ya mwisho itakapolia, kundi la watu wachache sana duniani litaondoka na kwenda mbinguni, na wengine wote hawatajua kitu…Hivyo hatuna budi kusimama imara katika Imani, ili siku hiyo ya unyakuo itakapofika tusiukose.
Marana atha
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
SWALI: Paulo alimaanisha nini kusema…”Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia;?
1Wakorintho 14:14 “Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda.
15 Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; mtaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia”.
JIBU: Hapa mtume Paulo alikuwa anaondoa mkanganyiko uliokuwa unaendelea katika kanisa kuhusiana na karama za rohoni, hususani karama ya lugha. Na mkanganyiko huu unaendelea hata sasa katika kanisa la Mungu.
Lakini kabla ya kufahamu mtume Paulo alikuwa anamaanisha nini hasaa hapo, ni vizuri tukajua jinsi hii karama inavyofanya kazi. Lugha zinazozungumziwa katika maandiko, ambazo Roho Mtakatifu anazishusha juu ya mtu kwa jinsi apendavyo yeye, zimegawanyika katika makundi mawili.
Kundi la kwanza: Ni lugha za kibinadamu. Mfano kichini, Kiswahili, kimasai n.k.
Kundi la Pili: Ni Lugha za malaika. Hizi hazijulikani na wanadamu,.
Sasa lengo kuu la hizi lugha ni kama zifuatavyo:
Mtu yeyote akimwomba Mungu ampe kunena kwa lugha, atapewa, (1Wakorintho 14:5).. Lakini pia haiwezi kuwa wakati wote, au ikaja kwa wepesi kama vile mtu yule aliyejaliwa karama hii na Mungu. Mtu aliyepewa karama hii, inakuwa ni rahisi sana kwake kunena, hususani pale anapoanza tu kuomba, hatumii nguvu nyingi, anashangaa ulimi wenyewe unaanza kuzungumza lugha nyingine gheni. Sasa kwa mtu kama huyu anapaswa kujua hiyo ni sehemu ya karama yake, na hivyo anapaswa aelewe ni nini anatakiwa afanye baada ya pale ili karama hiyo iwe ina manufaa kwa ajili ya kanisa la Mungu.
Sasa, jambo ambalo watu wengi hawajui ni kuwa hizi lugha zinaposhushwa ndani ya mtu, kwa kipindi cha mwanzoni, huwa haziji na tafsiri yoyote, zinakuwa ni kwa ajili ya yule mtu tu husika (mnenaji), na sio kwa kanisa, hapo ndipo utaona mtu anaweza kunena kwa lugha usiku kucha. Lakini kusiwe na kitu chochote unachokielewa yeye, au yule mwingine anayesikia.
Lakini baadaye kama ataichochea karama yake, kwa kumwomba Mungu, amjalie na tafsiri, ndio inapokuja na tafsiri ndani yake. Na hiyo inakuwa ni kwa faida ya kanisa la Kristo. Hivyo mtu ambaye karama yake inatenda kazi ni yule ambaye akinena katika kanisa, basi na Mungu anamfunulia tafsiri ya maneno yale aliyoyanena, kisha analiambia kanisa.. Na kanisa linajengwa, kwasababu hiyo.
Sasa tukirudi katika jambo ambalo Paulo alilisema.. kuhusiana na upungufu wa maarifa kuhusu karama hizi, ni kwamba watu walikuwa wananena kwa lugha mbele ya kanisa, lakini hakuna tafsiri yoyote ile. Ndipo hapo mtume Paulo akasema, Je! Yule anayesikia, ataelewaje?si atakuona wewe ni mwendawazimu? Akaongezea kusema, kama hutakuwa na tafsiri ya lugha hiyo, basi ni heri ukae kimya uombe kivyako vyako. Kuliko kusimama mbele ya kanisa na huku unatoa lugha ambazo hazieleweki kwa wasikiaji.
Ndipo hapo akasema..
Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; mtaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia..
Yaani, nitaomba kwa lugha, halafu wakati huo huo ninaomba kwa akili zangu, na sio tena tafsiri ya ile lugha niliyoizungumza bali maneno yangu mengine ya sikuzote.. kwamfano, mtu aanze kuzungumza kiharabu katikati ya mahubiri, bila kutolea tafsiri yoyote halafu anaendelea kuzungumza Kiswahili chake..wewe kama msikiaji utaelewa nini hapo?..
Ndicho kinachoendelea leo hii, mtu atasema ananena kwa lugha, anapohubiri, lakini hatoi tafsiri ya kile anachokisema, anaendelea na maneno yake ya Kiswahili. Katika mazingira kama hayo, wewe msikiaje unajengekaje?
Vilevile Roho Mtakatifu atakujalia kuimba hata wimbo katika lugha nyingine ya rohoni, halafu hutoi tafsiri yake, Je! Msikaji atajengekaje?
Naamini, kama na wewe ni mmojawapo mwenye karama hii, utafanya marekebisho katika hilo. Na kama umekuwa ukinena tu, huoni tafsiri, basi unawajibu wa kumwomba Mungu kwa bidi akupe na tafsiri, pindi uwapo mbele ya kanisa lake. Kwa msingi huu sasa, naomba upitie vifungu hivi hapa chini, ili uelewe Zaidi.
1Wakorintho 14:10 “Yamkini ziko sauti za namna nyingi duniani, wala hakuna moja isiyo na maana.
11 Basi nisipoijua maana ya ile sauti nitakuwa kama mjinga kwake yeye anenaye; naye anenaye atakuwa mjinga kwangu.
12 Vivyo hivyo na ninyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa.
13 KWA SABABU HIYO YEYE ANENAYE KWA LUGHA NA AOMBE APEWE KUFASIRI.
14 Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda.
15 Imekuwaje, basi? NITAOMBA KWA ROHO, TENA NITAOMBA KWA AKILI PIA; MTAIMBA KWA ROHO, TENA NITAIMBA KWA AKILI PIA.
16 Kwa maana wewe ukibariki kwa roho, yeye aketiye katika mahali pa mjinga ataitikaje, Amina, baada ya kushukuru kwako, akiwa hayajui usemayo?
17 Maana ni kweli, wewe washukuru vema, bali yule mwingine hajengwi.
18 Namshukuru Mungu ya kuwa nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote;
19 lakini katika kanisa napenda kunena maneno matano kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine, zaidi ya kunena maneno kumi elfu kwa lugha.
20 Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mkawe watu wazima.
21 Imeandikwa katika torati, Nitasema na watu hawa kwa watu wa lugha nyingine, na kwa midomo ya wageni, wala hata hivyo hawatanisikia, asema Bwana.
22 Basi, hizi lugha ni ishara, si kwao waaminio, bali kwao wasioamini lakini kuhutubu si kwa ajili yao wasioamini, bali kwa ajili yao waaminio”.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Jina kuu la Bwana na Mwokozi wetu na wa ulimwengu, Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tujifunze Neno la Mungu ambalo ndio taa iongozayo miguu yetu na mwanga wa njia yetu. (Zab 119:105).
Je unafanya kazi yoyote ya mikono?, ya kujiajiri au kuajiriwa?.. labda una shamba, au mifugo, au biashara, ambayo katika hiyo unategemea kukuingizia kipato?…
Je unayo shughuli ambayo ghafla umeshangaa mambo yameharibika!, yameenda kombo!..wakati mwingine unaweza kujiuliza ni nini chanzo, na ukashinda kujua..Leo nataka uone sababu ya mambo hayo kupitia maandiko?
Kama upo ndani ya Kristo, umesimama vizuri na ni mwaminifu kwa Bwana na mambo yamekuharibikia ghafla!, tambua kuwa chanzo ni kama kile kile cha Ayubu na wala si kingine..
Kwamba Shetani amekwenda kukushitaki mbele za Bwana, kwasababu ya haki yako, na hivyo Bwana akamruhusu aiharibu kazi yako,.. Na majaribu hayo mwisho wake ni mzuri, kwasababu ukiisha kuyashinda basi Bwana atakunyanyua mara dufu.. Ni majaribu ya kuwavusha watu wa Mungu kutoka hatua moja hadi nyingine.
Lakini kama upo nje ya Kristo (Yaani hujampokea Yesu na kumwamini, na kubatizwa, na kuishi maisha ya utakatifu yanayompendeza yeye), na ghafla umeona mambo yako yameharibika, kwa uharibifu usio wa kawaida..nataka nikuambie kuwa jambo ni lile lile lililomtokea Ayubu limekutokea na wewe, isipokuwa katika pande tofauti.
Ni kwamba shetani, au mapepo yake yamekwenda mbele za Mungu na kukushitaki na hivyo kupewa ruhusa ya kuja kuharibu kazi yako, au biashara yako au mifugo yako..na mwisho wa uharibifu huo ni mbaya kwasababu hauna tumaini la kuvipata tena vile ulivyopoteza.
Sasa hebu tusome habari moja katika biblia ambayo hiyo itatusaidia kuelewa vizuri.. tumsome mtu mmoja tajiri, ambaye alikuwa na biashara yake kubwa ya mifugo lakini iliharibika ghafla na wala hakupata kurejeshewa..
Marko 5:6 “Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia;
7 akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese.
8 Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu.
9 Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi.
10 Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi ile.
11 NA HAPO MILIMANI PALIKUWA NA KUNDI KUBWA LA NGURUWE, WAKILISHA.
12 PEPO WOTE WAKAMSIHI, WAKISEMA, TUPELEKE KATIKA NGURUWE, TUPATE KUWAINGIA WAO.
13 AKAWAPA RUHUSA. WALE PEPO WACHAFU WAKATOKA, WAKAINGIA KATIKA WALE NGURUWE; NALO KUNDI LOTE LIKATELEMKA KWA KASI GENGENI, WAKAINGIA BAHARINI, WAPATA ELFU MBILI; WAKAFA BAHARINI.
14 Wachungaji wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka walione lililotokea”.
Umeona hapo?.. huyu mtu pengine alikuwa tajiri sana mwenye nguruwe wengi (biblia inasema walikuwa nguruwe elfu 2), na akaajiri wachungaji wakawachunge kondoo wale milimani.. Na siku hiyo ghafla anakuja kuletewa taarifa kuwa nguruwe wake wote elfu mbili wamekimbilia baharini na wamekufa huko.
Bila shaka kwa haraka haraka angeweza kusema ni uchawi, au ana gundu!.. Lakini kumbe kuna jambo lililokuwa linaendelea katika roho juu yake na mali zake bila yeye kujua. Kwamba mapepo yalikwenda kwanza mbele za Bwana Yesu kuomba ruhusa yaingie kwenye kitega uchumi chake, ili yaiharibu kazi yake! Na Bwana Yesu akayapa ruhusa na wala hakuyakataza..
Kama vile tu!, shetani alivyokwenda mbele za Bwana kuomba ruhusa aharibu mifugo ya Ayubu, na Mungu akampa ruhusa wala hakumkataza.(Ayubu 1:9-12). Ndicho kilichomtokea huyu mtu mwenye nguruwe Elfu 2.
Lakini cha ajabu ni kwamba hatusomi tena habari za huyo tajiri aliyepoteza nguruwe wake, (hao elfu mbili kwa siku moja) kwamba alikuja kuwapata tena.. maana yake ni kwamba hakuja kuwapata tena.. kama ilivyokuwa kwa Ayubu.. Ayubu yeye alipopoteza mifugo yake maandiko yanasema alikuja kupata mara dufu.. Lakini huyu tajiri wa nguruwe hakuna chochote alichoambulia..zaidi ya kupata hasara tu!
Na kinachoshangaza zaidi ni kwamba hata Bwana hakumhurumia wala hakusikitika, yeye kupoteza nguruwe wote wali, Zaidi ya yote aliruhusu mapepo yaingie nguruwe wake.
Sasa ni kwasababu gani hatusomi ushuhuda wowote wa huyu tajiri kuja kupata tena alichokipoteza kama Ayubu?.. Jibu ni rahisi, ni kwasababu hakuwa ndani ya wokovu kama aliokuwa nao Ayubu.. hakutubu!, wala hakumwamini Yesu kabla wala baada ya hapo.. Zaidi ya yote maandiko yanasema wakuu wa miji pengine na yeye akiwemo miongoni mwao, walimfukuza Bwana Yesu atoke katika mipaka yao.
Ndugu unayesoma ujumbe huu, jitafakari je!, hiyo kazi unayoifanya ina usalama kiasi gani?..je upo ndani ya Kristo au nje!.. Unaweza kufikiri mali zako zitakusaidia, au mifugo yako..lakini nataka nikuambie mapepo kila siku yanazitaja hizo mali zako mbele za Mungu.. Na cha kuogopesha ni kwamba Mungu anaweza kuyaruhusu yazichukue au waziue ndani ya siku moja..
Kwasababu kama aliruhusu kwa mtumishi wake Ayubu, ambaye alikuwa mkamilifu mbele zake, wewe na mimi ambaye pengine si wakamilifu mbele zake ni wakina nani, Mungu asiruhusu mabaya hayo?
Jiulize je!, siku ya uharibifu itakapokuja ghafla kama ilivyokuja kwa huyu Tajiri wa nguruwe na Ayubu, utakuwa wapi?.. utakuwa na tumaini kama Ayubu au utapotea moja kwa moja kama huyu Tajiri.
Kama bado hujampokea Yesu, ni vyema ukampokea sasahivi, kwa usalama wa Roho yako na watoto wako, na mali zako na mifugo yako. Kwani usipofanya hivyo kuna hatari ya kukosa tumaini katika siku za kujaribiwa.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Kwanini Bwana aliwalenga mbwa na nguruwe tu katika Mathayo 7:6?
Nini maana ya “kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi?”
Katika Mathayo 9:2 tunasoma Bwana anamwita “Mkuu” Yule mtu aliyepooza ?.. Je ni sahihi na sisi kuitana wakuu?
Jibu: Tusome,
Mathayo 9:2 “Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, ALIMWAMBIA YULE MWENYE KUPOOZA, JIPE MOYO MKUU, MWANANGU, umesamehewa dhambi zako”.
Hapo ukisoma vizuri utaona Bwana hakumwita Yule mtu “Mkuu”.. Bali alimaanisha “ajipe Moyo Mkuu” yaani “moyo ulio mkuu”. Kwahiyo ni moyo mkuu ndio uliotajwa hapo, na si Mkuu kama mtu. Kristo hana Mkuu juu yake zaidi ya Baba, hivyo hawezi kumwita mtu yeyote duniani Mkuu, zaidi sana anatuita sisi WANAWE, kama mwishoni hapo alipomalizia.. “jipe moyo mkuu, MWANANGU, umesamehewa dhambi zako”
Kadhalika biblia haijaruhusu sisi kwa sisi kuitana “Wakuu”, kwasababu aliye Mkuu wetu sisi sote ni mmoja tu naye ni Kristo, (Soma Matendo 3:15 na Ufunuo 1:5). Sisi tukiitana majina yetu kama ndugu inatosha!..Vyeo vingine vya juu zaidi ya hivyo vinamhusu Bwana wetu Yesu peke yake (Mathayo 23:8-11).
Sasa hivi upo mtindo wa sisi kwa sisi kuitana “wakuu”, utaona mtu atazungumza maneno mawili matatu na mwenzie na katikati atataja neno “mkuu” kama kionjo cha kumpandisha hadhi Yule anayezungumza naye. Si sawa kufanya hivyo!.. Ni mtindo ambao chanzo chake ni kutoka kwa Yule adui yetu shetani.
Lakini pamoja na hayo, tunaweza kujifunza kitu kupitia hiyo habari!.. Bwana alimwambia Yule aliyepooza kwamba “jipe moyo mkuu ” na si “ajipe tu moyo”..bali “moyo mkuu”.. Maana yake tunapokuwa katika dhiki fulani, au tatizo fulani, au ugonjwa fulani.. Hatuna budi kujipa moyo mkuu wenyewe!.. Maana yake hatupaswi kukata tamaa.. Tunapaswa kuamini mpaka mwisho, ili tupokee uponyaji wetu, au Baraka zetu. Kama ni kuomba tunapaswa tuendelee kuomba kwa Moyo Mkuu, kama kutafuta tunapaswa tuendelee kutafuta kwa Moyo Mkuu, mpaka tukipate. Lakini tunapokata tamaa kirahisi ni ngumu kupokea au kupata kile tulichokuwa tunakitafuta.
Bwana atubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Je kualikwa kwenye sherehe za watu ambao si wakristo ni dhambi?
Tukisoma katika kitabu cha Ezekieli 14:9 tunasoma Mungu anaweza kumdanganya Nabii, sasa swali ni je Mungu anadanganya?
Jibu: Tusome
Ezekieli 14:9 “Na nabii akidanganyika, na kusema neno, MIMI, BWANA, NIMEMDANGANYA NABII YULE, nami nitaunyosha mkono wangu juu yake, na kumwangamiza, asiwe kati ya watu wangu Israeli.
10 Nao watauchukua uovu wao; uovu wa nabii utakuwa sawasawa na uovu wake yule amwendeaye aulize neno”
Kufuatia mstari huo ni rahisi kuamini kuwa Mungu anadanganya… lakini kiuhalisia ni kwaba, Mungu kamwe hawezi kudanganya na wala hasemi uongo!.. Yeye ni mtakatifu siku zote.. Isipokuwa Mungu anaweza kuruhusu roho ya upotevu kutoka kwa adui imwingine mtu, endapo mtu huyo atayakataa mema na kulazimisha mabaya katika maisha yake, ndivyo maandiko yanavyosema katika 2Wathesalonike 2
2Wathesalonike 2:10 “na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
11 Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo;
12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu”.
Sasa ili tuelewe vizuri Mungu anaiachiaje nguvu ya upotevu juu ya mtu, hebu tusome kisa kimoja cha Mfalme Ahabu katika maandiko..
1Wafalme 22:16 “Mfalme akamwambia, Mara ngapi nikuapishe usiniambie neno ila yaliyo kweli, kwa jina la Bwana?
17 Akasema, Naliwaona Waisraeli wote wametawanyika milimani, kama kondoo wasio na mchungaji. Bwana akasema, Hawa hawana bwana; na warudi kila mtu nyumbani kwake kwa amani.
18 Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Je! Sikukuambia, hatanibashiria mema, ila mabaya?
19 Mikaya akasema, Sikia basi neno la Bwana; Nalimwona Bwana ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kuume na wa kushoto.
20 Bwana akasema, NI NANI ATAKAYEMDANGANYA AHABU, ili akwee Ramoth-Gileadi akaanguke? Basi huyu akasema hivi; na huyu hivi.
21 Akatoka pepo, akasimama mbele za Bwana, akasema, Mimi nitamdanganya.
22 Bwana akamwambia, Jinsi gani? Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo kinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na kudiriki pia; ondoka ukafanye hivyo.
23 Basi angalia, BWANA AMETIA PEPO WA UONGO KINYWANI MWA MANABII WAKO HAWA WOTE; NAYE BWANA AMENENA MABAYA JUU YAKO”.
Umeona hapo?..Mfalme Ahabu alikuwa amemwacha Mungu na alikuwa anaabudu miungu na wala alikuwa hana mpango wa kubadili njia yake, na wakati huo huo anakwenda kumwuliza Mungu kwa habari ya vita iliyo mbele yake, huku moyoni amemwacha Bwana, yaani kwaufupi alikuwa anamgeuza Mungu kama mganga wa kienyeji kumtabiria mambo yake ya vita tu!
Lakini hapo tunasoma Mungu yeye mwenyewe hakumdanganya Ahabu, kwasababu yeye hasemi uongo, lakini aliiachia roho ya upotevu imfuate mfalme Ahabu.. Maana yake Mungu aliruhusu pepo liwaingie manabii wake 400, na kuwapa maono ya uongo, na kufikiri ni maono ya Mungu… Na hivyo Mfalme akadanganyika na maono yale na akaenda kufa katika vita badala ya kupona. Hivyo ni pepo ndilo lililomdanganya Ahabu na si Mungu, ingawa Mungu ndiye aliyeruhusu..hivyo ni sawa na kusema ni Mungu kamdanganya Ahabu..
Kama vile maandiko yanavyosema kuwa Mungu alimpiga Ayubu.. lakini kiuhalisia si Mungu aliyempiga bali ni shetani, isipokuwa kwa ruhusa ya Mungu..
Ndicho biblia pia ilichomaanisha hapo katika Ezekieli 14:9 “Na nabii akidanganyika, na kusema neno, MIMI, BWANA, NIMEMDANGANYA NABII YULE”.
Maana yake ni kwamba kama Nabii kamwacha Bwana moyoni mwake, Mungu anaweza kuruhusu pepo la uongo limwingie na kumpa maono ya uongo.. Sasa kitendo hicho cha Bwana kuruhusu upotevu umwingie mtu, ndio unaweza kutafsirika kama Bwana kamdanganya mtu huyo!.. Lakini kiuhalisia si Bwana aliyemdanganya bali ni mapepo ambayo yameruhusiwa na Mungu yamwingie na kumdanganya huyo mtu.
Sio jambo la ajabu pia Mungu anaweza kumuua mtu kwa kumweka mikononi mwa shetani..
Hivyo tunachoweza kujifunza ni kwamba hatuna budi kuwa makini sana na kutomgeuza Mungu kama waganga wa miungu ya kidunia, ambao unaweza kuwafuata wakutatulie matatizo yako, na kuondoka kuendelea kuishi maisha yako ya ulevi, ya uzinzi, au mengine yoyote.
Kwa Mungu wa mbingu na nchi sio hivyo, tunapomwendea hatuna budi kumkubali kwanza, na kujinyenyekeza chini yake na kufuata kile anachokitaka yeye katika maisha yetu, na si kile tunachokitaka sisi.. Maana yake ni kwamba tunapomwendea Mungu kumuuliza jambo na huku mioyoni mwetu bado tunapenda ulevi, na hatutaki kuacha, bado tunaabudu sanamu, bado ni wachawi, bado ni wazinzi n.k Bwana ataachia nguvu ya upotevu, kwasababu yeye hadhihakiwi alisema hivyo katika neno lake..
Ezekieli 14:1 “Ndipo baadhi ya wazee wa Israeli wakanijia, wakaketi mbele yangu.
2 Ndipo neno la Bwana likanijia, kusema,
3 Mwanadamu, watu hawa wametwaa vinyago vyao na kuvitia mioyoni mwao, nao wameweka kwazo la uovu wao mbele ya nyuso zao. Je! Ni laiki yangu niulizwe na wao katika neno lo lote?
4 Basi sema nao, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Kila mtu wa nyumba ya Israeli atwaaye vinyago vyake na kuvitia moyoni mwake, na kuliweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake, na kumwendea nabii; mimi, Bwana, nitamjibu neno lake sawasawa na wingi wa sanamu zake;
5 ili niwakamate nyumba ya Israeli kwa mioyo yao wenyewe, kwa sababu wamefarakana nami kwa vinyago vyao”.
Kama hujaokoka!, kumbuka kuwa Kristo ndiye njia kweli na Uzima, na hakuna njia nyingine ya kumfikia Baba zaidi yake yeye. Hivyo wote hatuna budi kumwamini na kumpokea ili tupate wokovu na ondoleo la dhambi zetu, na tunapata wokovu kwa kumwamini, na kutubu na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji tele na kwa jina la Bwana Yesu Kristo. Na Roho Mtakatifu atayakeyeingia ndani yetu atatuongoza katika kweli yote.
Marana tha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Kwanini Yakobo alimshinda Mungu, Je! Mungu huwa anashindwa na wanadamu?
SWALI: Naomba kuelewa kitendo cha Paulo, kuungana na wale watu wanne wenye nadhiri, alipoenda Yerusalemu kilimaanisha nini?. Au kinaelewekaje?
JIBU: Kama tunavyosoma katika maandiko tunaona ziara ya mwisho ya mtume Paulo kwenda Yerusalemu baada ya miaka mingi sana, kwa mara ya kwanza alikutana na Yakobo pamoja na wazee baadhi watakatifu wa Yerusalemu, na moja kwa moja alianza kuwasimulia mafanikio ya huduma yake, na jinsi alivyofanikiwa kuwavua watu wengi kwa Kristo na kuihubiri injili.
Yakobo na wazee wa kiyahudi waliposikia vile, walifurahi sana na kumtukuza Mungu, lakini walimpa taarifa nyingine ambazo, zilikuwa ni ngeni masikioni mwa Paulo. Kwamba, habari zake zimevuma kwa wayahudi wote wa kikristo waliokaa Yerusalemu kuwa yeye amekuwa akiwafudisha watu waipuuzie torati ya Musa, sio tu kwa watu wa mataifa bali pia kwa wayahudi waliokoka, wasishike sheria kama vile wasitahiriwe n.k.
Hivyo hiyo imemfanya Paulo aonekane kuwa ni mpingamizi mkubwa sana wa Torati kwa wayahudi, jambo ambalo sio kweli. Paulo aliwafundisha watu kwamba torati sio kipimo cha wokovu, bali neema inayotokana na kumwamini Kristo. Lakini hakuwa mpingamizi wa Torati kwa namna yoyote ile. Na ndio maana kuna wakati alimlazimisha hata Timotheo atahiriwe kwa ajili ya wayahudi. Kama angekuwa mpingamizi asingeruhusu hata kitendo cha kutahiriwa kufanyika(Matendo 16:1).
Hivyo, Yakobo, pamoja na wazee, walijua ukweli kuwa Paulo hawezi kufanya vile, ndipo hapo wakamashauri, kwamba ili kuondoa dukuduku hilo, hana budi kuwaonyesha wayahudi wote kuwa, yeye ahialifu torati hata kidogo. Ndipo wakamwambia, wapo watu wanne ambao wanakaribia kumaliza nadhiri zao (nadhiri ya mnadhiri), na kwamba aungane nao kuwahudumia, katika siku hizo, ili wayahudi watakapoona wajue kuwa Paulo, aihalifu torati.
Matendo 21:17 “Tulipofika Yerusalemu wale ndugu wakatukaribisha kwa furaha.
18 Hata siku ya pili yake Paulo akaingia kwa Yakobo pamoja nasi, na wazee wote walikuwako.
19 Na baada ya kuwaamkua, akawaeleza mambo yote moja moja Mungu aliyoyatenda katika Mataifa kwa huduma yake.
20 Nao waliposikia wakamtukuza Mungu, wakamwambia, Ndugu yetu, unaona jinsi Wayahudi walioamini walivyo elfu nyingi, nao wote wana wivu sana kwa ajili ya torati.
21 Nao wameambiwa habari zako, ya kwamba unawafundisha Wayahudi wote wakaao katika Mataifa kumwacha Musa, ukiwaambia wasiwatahiri watoto wao, wala wasizifuate desturi.
22 Basi, ni nini? Bila shaka watasikia kwamba umekuja.
23 Basi fanya neno hili tunalokuambia. Wako kwetu watu wanne waliofungwa na nadhiri.
24 Wachukue watu hao, ujitakase pamoja nao, na kuwagharimia ili wanyoe vichwa vyao, watu wote wapate kujua ya kuwa habari zile walizoambiwa juu yako si kitu, bali wewe mwenyewe unaenenda vizuri na kuishika torati”.
Sasa kwa kawaida, Mnadhiri kulingana na kitabu cha Hesabu 6, alikuwa haruhusiwi kuonyoa kichwa chake, wala kunywa divai, au mzabibu wa aina yoyote, wala kugusa maiti, mpaka siku zake zote zitakapotimia, Hivyo siku ya mwisho alikuwa anachukua, kondoo madume wawili na jike mmoja pamoja na vikapu vya unga, kwa ajili ya upatanisho.
Hivyo, kwa kuwa Paulo alilazimika kuungana nao katika nadhiri zao, basi, ilikuwa ni desturi uwahudumie kwa kuzichukua zao gharama zote za kinadhiri zilizohitajika. Hivyo Kwa kitendo hicho Paulo alionekana kuwa nay eye ni mtunzaji mzuri wa torati. Japo hilo pekee halikutosha kujiaminisha kwao kwa wayahudi, utaona walikuja kutaka kumkamata na kumuua.
Lakini Hiyo ndio sababu ya Paulo kuungana na wale watu wanne waliokuwa na nadhiri, ilikuwa ni ili kuwaonyesha wayahudi kuwa yeye haivunji torati.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Ni kweli Paulo alipuuzia maonyo aliyopewa ya kwenda Yerusalemu?
Maandiko yanasema katika 1Wathesalonike 4:17 tutakaa na Bwana milele mbinguni, sasa iweje tushuke tena kutawala na Yesu duniani kwa miaka 1000?.. Au tutarudi tena mbinguni, baada ya utawala huo kuisha?
Jibu: Tusome..
1Wathesalonike 4:16 “Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; NA HIVYO TUTAKUWA PAMOJA NA BWANA MILELE.
18 Basi, farijianeni kwa maneno hayo.
Kama ukitafakari maandiko hayo kwa makini yanasema “Tutakuwa pamoja na Bwana milele”. Na sio “tutaishi na Bwana mbinguni milele”..
Kuna tofauti ya kuwa na mtu milele na kuishi na mtu mahali fulani milele.
Kuwa na Yesu milele maana yake ni kwamba popote atakapokuwepo tutakuwepo naye, popote atakapokwenda tutakwenda naye..hatutamwacha wala yeye hatatuacha, kama alivyotuacha sasa na kwenda mbinguni.
Lakini baada ya sisi kwenda mbinguni huko alipo ,tutakuwa naye milele, hata wakati atakaporudi kwaajili ya hukumu ya vita vya harmagedon tutakuwa naye hatatuacha mbinguni..maandiko yanasema hivyo..
Yuda 1:14 “Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu”.
Umeona hapo?..
Kwahiyo mbinguni tutakwenda na vile vile tutarudi kutawala na Kristo kwa miaka elfu hapa duniani..
Kulingana na maandiko mbinguni tutakaa kwa kipindi cha miaka saba tu!..baada ya hapo tutarudi kutawala na Kristo hapa duniani kwa miaka elfu, na hatitarudi tena mbinguni..Kwani Mji wa kimbinguni Yesrusalemu mpya utashuka hapa, na hapa patageuzwa kuwa mbingu mpya na nchi mpya.
Kwa maelezo marefu kuhusu mbingu mpya na nchi mpya unaweza kufungua hapa >> Mbingu mpya na nchi mpya
Hivyo hatuna budi kupiga mbio ili tuweze kuwa miongoni mwa watakaokuwa na Bwana milele.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Tofauti kati ya ufalme wa mbinguni na ufalme wa Mungu ni ipi?
Naomba kufahamu Kwanini Bwana Yesu aliwaagiza wanafunzi wake wakanunue upanga?. Na tunafahamu kazi ya upanga si njema?
Tusome
Luka 22:35 “Akawauliza, Je! Hapo nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? Wakasema, La!
36 Akawaambia, Lakini sasa mwenye mfuko na auchukue, na mkoba vivyo hivyo; naye asiye na upanga, na auze joho yake akanunue”.
Maneno haya aliwaambia wanafunzi wake, alipokaribia mwishoni kabisa mwa huduma yake, akimaanisha kuwa majira yamebadilika, sasa sitawatuma, na kama siwatumi basi na faida zile zinazombatana na wito wangu mtazikosa, hivyo kama ulikuwa huna tabia ya kutunza pesa zako, basi sasa anza kuzitunza, maana yake jiwekee akiba kwenye mfuko wako, jihifadhie vitu vyako, kwa matumizi ya baadaye kwasababu kuna kupungukiwa huko mbele, vivyo hivyo na kama huna upanga, ukauze joho lako ukaununue!
Lakini swali linakuja kwanini uwe ni Upanga tena, wakati upanga ni wa kuulia?. Hata mitume nao walifikiri Bwana anamaanisha hivyo hivyo, kwamba wakanunue upanga kwa ajili ya kujilinda, au kuwapiga maadui zao pale wanapotaka kuwadhuru.. Na ndio maana muda huo huo wakamwambia Bwana maneno haya;
Luka 22:38 “Wakasema, Bwana, tazama, hapa pana panga mbili. Akawaambia, Basi”.
Wakidhani, kuwa Kristo alimaanisha wazitumie hizo kujilindia au kuwapiga maadui zao.. Utaona mawazo hayo bado yalikuwa vichwani mwao, hata baadaye kidogo, majeshi ya makuhani yalipokuja kumkamata Yesu, yakiwa na marungu na mapanga, utaona Petro alichukua upanga wake, na kwenda kumpiga na kumata sikio mtumwa wa kuhani Mkuu. Kitendo ambacho kilimuudhi sana Bwana, akawakemea, na kuwaambia auye kwa kwa upanga atauawa kwa upanga(Mathayo 26:52),.
Luka 22:49 “Na wale waliokuwa karibu naye walipoona yatakayotukia, walisema, Bwana, tuwapige kwa upanga?
50 Mmoja wao akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume.
51 Yesu akajibu akasema, Mwe radhi kwa hili. Akamgusa sikio, akamponya”.
Hapo ndipo wakagundua kuwa Panga walizoambiwa wakanunue si kwa lengo la kujihami au kuwadhuru wengine.
Bali Bwana alichomaanisha, aliposema mkanunue Panga, ni kwa lengo la kujipatia rizki, panga hapo linawakilisha vitu vyote vikali aidha vya kukatia, kuulia, kuchinjia, au kupasua. Kama vile kisu, shoka, mkuki, n.k. Kwamfano katika kupika utahitaji kisu tu mahali Fulani, kama huna kisu huwezi kukata nyama, au kitunguu, nyanya n.k. hivyo hapo mwanzo ulikuwa huna vitu hivi nyumbani kwako nenda kanunue kwasababu vitakufaa sana wakati huu.
Vilevile kama wewe ni mvuvi kama Petro utahitaji tu Kisu cha kuparulia samaki, hakuna namna utakikwepa. Kama wewe ni mwindaji, utahitaji mkuki au upanga, kama wewe ni mkulima utahitaji shoka, au rato n.k.
Hicho ndicho Bwana alichokimaanisha, kwamba wakajitafutie kitu chochote, kinachoweza kuwafaa kwa ajili ya kukidhi mahitaji yao ya mwilini, lakini sio upanga wa kuulia watu.
Ni nini Bwana anatufundisha katika kauli hiyo? Ni kuwa anapotuita katika utumishi wake tusiwe na wasiwasi tutakula nini, au tutakunywa nini, yeye mwenyewe atahakikisha anatuhudumia kwa kila kitu, kama alivyowahudumia mitume wake mpaka dakika ya mwisho, kwasababu anajua muda wote tunaupoteza kwake, hivyo yeye mwenyewe atahakikisha tunaishi kwa namna yoyote ile, Lakini kama hatupo katika utumishi wake, hatuna budi kuitunza mifuko yetu, kujiwekea akiba zetu, na kujitafutia mawindo yetu, na yeye atatubariki kwa njia hiyo.
Lakini baada ya pale, mtume walifurahia kuendelea na utume wa Bwana, hata siku ya pentekoste ilipofika, na kazi ya utume ulipoanza, Kristo alikuwa nao wakati wote akiwahudumia kama alivyowahidia katika Mathayo 28:20
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Kwanini Yesu aliwaambia wale wakoma wakajionyeshe kwa makuhani?