Jibu: Labda tuanzie mstari ule wa 18, ili tupate kuelewa vizuri.
Isaya 3:18 “Siku hiyo Bwana atawaondolea uzuri wa njuga zao, na kaya zao;
19 na pete za masikio, na vikuku, na taji zao;
20 na dusumali, na mafurungu, na vitambi, na vibweta vya marashi, na matalasimu;
21 na pete, na azama,
22 na mavazi ya sikukuu, na DEBWANI; NA SHALI, NA VIFUKO”
Hayo ni aina ya mavazi waliovaa watu wa zamani, na baadhi ya hayo hata sasa yanavaliwa.. Sasa hapo yametajwa mengi, ikiwemo Dusumali, kwa urefu kuhusu Dusumali basi fungua hapa>>Dusumali ni nini katika biblia?
Lakini tutatazama hayo matatu yaliyotajwa katika huo mstari wa 22 ambayo ni “DEBWANI, SHALI, na VIFUKO”.
1. DEBWANI.
Debwani ni vazi refu linaloanzia mabegani mpaka miguuni, vazi hili linavaliwa na wanawake, (Tazama picha chini juu).
2. SHALI.
Shali ni vazi linalofanana na Debwani isipokuwa lenyewe linafunika kuanzia kichwa mpaka miguu, na hili linaweza kuvaliwa na jinsia zote, kwani kazi yake kubwa ni kujikinga na hali ya hewa, (baridi au mvua au upepo mkali), Shali ni Kiswahili cha “Overcoat” (Tazama picha chini).
3. VIFUKO
Vifuko si vazi bali ni mikoba inayobebwa na wanawake katika safari fupi. (Tazama picha chini)
Je umempokea Bwana YESU?
Kama bado ni nini kinachokusubirisha? Fahamu kuwa hizi ni siku za mwisho na Bwana amekaribia sana kurudi, je ni nini kipo katika akili yako wewe kama Baba, au mama au kijana?. Je unawaza nini?.. kujenga maisha ya kimwili, kula, kunywa na kuvaa??..au unawaza nini Zaidi.
Kama unawaza kupendeza na kujifanya mzuri kwa mavazi na mitindo ya kidunia, Neno la Mungu linasema siku inakuja ambayo Mungu atawaondolea watu wote uzuri wa njuga zao watu wote waliomwacha yeye..
Isaya 3:18 “Siku hiyo Bwana atawaondolea uzuri wa njuga zao, na kaya zao;
19 na pete za masikio, na vikuku, na taji zao;”
Achana na mapambo na fasheni za kidunia, mpokee YESU leo ukaoshwe dhambi zako.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MANENO YA MUNGU YANAPINDULIWAJE?
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 12 (Kitabu cha Isaya)
Ni kwa jinsi gani Mungu anapatiliza maovu ya baba zetu sawasawa na Kutoka 20:5-6?
About the author