Title Devis

MPAKA UTIMILIFU WA MATAIFA UTAKAPOWASILI.

Hii neema tuliyonayo watu wa mataifa, haikuanzia kwetu, bali ilitoka kwa wengine lakini kwa huruma za Mungu walipokonywa wao tukapewa sisi. Israeli kama Taifa teule la Mungu walikuwa wameshafikia kilele cha kula matunda ya taabu yao kwa kuja kwake mkombozi ambaye ni Mesiya wao waliyemngojea kwa miaka mingi, ambaye angewaokoa na dhambi zao na maadui zao, lakini mambo hayakuwa kama yalivyo kwasababu badala ya wao kufaidi lile TUNDA, wakanyang’anywa na kupewa wengine ambao ndio sisi mataifa.

Hivyo mkombozi wa nafsi zao alipokuja Mungu aliwapiga upofu, wasiweze kumuamini kwasababu maalumu ili sisi (mataifa:mimi na wewe) tuweze kumwamini na kushiriki kipawa hicho cha neema.

Biblia inasema hivi juu ya Taifa la Israeli.

Warumi 11: 10 “Macho yao yatiwe giza ili wasione, Ukawainamishe mgongo wao siku zote.
11 Basi nasema, Je! Wamejikwaa hata waanguke kabisa? Hasha! Lakini KWA KOSA LAO WOKOVU UMEWAFIKILIA MATAIFA, ili wao wenyewe watiwe wivu.

12 Basi, ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa ulimwengu, na upungufu wao umekuwa utajiri wa Mataifa, je! SI ZAIDI SANA UTIMILIFU WAO?”.

Hii ni dhahiri tukiliangalia taifa la Israeli tangu kipindi kile Bwana Yesu alipokuja, mpaka sasa wayahudi wamekuwa wakiupinga ukristo, hawataki kumwamini Bwana Yesu kama ndiye Masia wao aliyetabiriwa, wanasema Yule ni mtu tu wa kawaida, Taifa zima haliamini habari za Yesu ni masalia tu (yaani watu wachache sana) waliopewa neema ndio wanaoamini lakini sio taifa, sio kwasababu ni waovu sana, hapana bali ni kwasababu Mungu mwenyewe kawapiga upofu makusudi wasilione hilo, kwa ajili yetu sisi mataifa, kwasababu mfano wangeamini sisi mataifa tusingekuwa na nafasi yoyote katika ufalme wa mbinguni. Kwasababu Mungu huwa hashughuliki na mataifa mawili kwa wakati mmoja. Alipotembea na Israeli, watu wa mataifa aliwaweka kando, vivyo hivyo na sisi.

Lakini hilo halitadumu milele, Mungu analipenda na analionea wivu taifa lake Israeli siku zote, ambalo hilo lingestahili kuwa la kwanza kupokea Baraka za mwokozi kwasababu hiyo basi utafika wakati Bwana atalirudia taifa lake tena, na watu wa mataifa waliobakia walioikataa neema watapigwa upofu wa mauti na kuondolewa. Ni kipindi cha hatari na kimeshaanza taratibu taratibu.

Ndugu tukishakifikia huo wakati hata uiweje watu hawataweza kuipokea injili tena, maana ili kuiamini inahitajika neema kutoka kwa Mungu mwenyewe, kwasababu biblia inasema

Yohana 6:44 “Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho”.

Hivyo hiyo nguvu ya kuvutwa kwa Mungu haitakuwepo tena kwa mataifa, kitu kitakachobakia kwa watu wa mataifa ni NGUVU YA UPOTEVU inayotoka kwa Mungu soma..

2Wathesalonike 2: 10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.

11 KWA HIYO MUNGU AWALETEA NGUVU YA UPOTEVU, WAUAMINI UONGO;

12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu”.

Watabakia katika dini zao na madhehebu yao wakidhani kuwa ndio wanamwabudu Mungu, kama wale mafarisayo na masadukayo walivyokuwa wakati ule neema ya Kristo ilipotolewa kwao, badala ya kumpokea kinyume chake walimsulibisha, ndivyo itakavyokuwa kwa watu wanaokataa KUIAMINI KWELI sasa hivi. Sasa kama wayahudi ambao walikuwa ni watu wa Mungu yaliwakuta mambo kama hayo Na sisi je! Tutawezaje kupona tusipouthamini wokovu mkuu namna hii??(Waebrania 2:3).

Biblia imetufananisha sisi watu wa mataifa kama mizeituni mwitu, na Israeli kama mzeituni halisi, kwamba wao walikatwa ili sisi tupandikizwe tulio mzeituni mwitu na tuzae matunda halisi ya mzeituni. Kama Mtume Paulo alivyoandika katika.:

Warumi 11:15-24 “15 Maana ikiwa kutupwa kwao{ISRAELI} kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! Kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhai baada ya kufa?

16 Tena malimbuko yakiwa matakatifu, kadhalika na donge lote; na shina likiwa takatifu, matawi nayo kadhalika.

17 Lakini iwapo matawi mengine yamekatwa, na wewe MZEITUNI MWITU ulipandikizwa kati yao, ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake,

18 usijisifu juu ya matawi yale; au ikiwa wajisifu, si wewe ulichukuaye shina, bali ni shina likuchukualo wewe.

19 Basi utasema, Matawi yale yalikatwa kusudi ili nipandikizwe mimi.

20 Vema. Yalikatwa kwa kutokuamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako. Usijivune, bali uogope.

21 KWA MAANA IKIWA MUNGU HAKUYAACHIA MATAWI YA ASILI, WALA HATAKUACHIA WEWE .

22 Tazama, basi, wema na ukali wa Mungu; kwa wale walioanguka, ukali, bali kwako wewe wema wa Mungu, ukikaa katika wema huo; kama sivyo, wewe nawe utakatiliwa mbali.

23 Na hao pia, wasipokaa katika kutokuamini kwao, watapandikizwa; kwa kuwa Mungu aweza kuwapandikiza tena.

24 Kwa maana ikiwa wewe ulikatwa ukatolewa katika mzeituni, ulio mzeituni mwitu kwa asili yake, kisha ukapandikizwa, kinyume cha asili, katika mzeituni ulio mwema, SI ZAIDI SANA WALE WALIO WA ASILI KUWEZA KUPANDIKIZWA KATIKA MZEITUNI WAO WENYEWE?.

Unaona hapo kuna wakati utafika ambao Mungu ameuamuru kwa watu wake Israeli, KUPANDIKIZWA TENA na sio siku nyingi. Na ukishafika huo wakati Israeli wote watafumbuliwa macho na kumpokea Bwana Yesu na kufahamu kuwa walifanya makosa kumsulibisha masihi wao, watamlilia na kumuombolezea biblia inasema hivyo (Soma Zekaria 12:9-14). Na neema hii itakaporudi Israeli itakuwa imebakia miaka 7 tu mpaka dunia iishe.

Kumbuka wakati huo Bwana atakuwa ameshamaliza kushughulika na watu wa mataifa, na shughuli hiyo itaishia na UNYAKUO wa kanisa, baada ya hapo ni giza kuu kwa mataifa yote na kufunuliwa kwa mpinga-kristo akitenda kazi katikakati ya wale waliobaki wasiokwenda kwenye unyakuo.

Ukiendelea mstari wa 25-27 utaona mtume Paulo anaendelea na kusema..

“25 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, MPAKA UTIMILIFU WA MATAIFA UWASILI.

26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao.”

Kwa miaka 2000 sasa, Mungu amekuwa akilia katika mioyo ya watu wa mataifa, akiwaambia “waje wanywe maji ya uzima bure”. Neema imekuwa kubwa kiasi kwamba Mungu analithibitisha Neno lake kwa ishara na miujiza ya kupita kiasi, wengine anawavuta kwa njia ya ndoto, wengine kwa maono, wengine kwa wahubiri, n.k. ili tu waingie katika karamu ya Mungu aliyowaandalia watu wake wa mataifa. Wapo ambao wameitii injili na kuiamini na kuifuata lakini cha kuhuzunisha ni kwamba wapo ambao wanaitupilia mbali NEEMA hii, na kumbuka kukatwa kwa mataifa kumeshaanza, kama tu vile kupandikizwa kwa Taifa la Israeli kunavyoanza.

Hauoni mataifa mengi hususani ya magharibi ambayo hapo kwanza yaliitwa ya kikristo na kutuletea sisi injili sasa hivi yamegeuka kuwa ni mataifa yanayo mpinga Kristo?. Hizo ni dalili za kukatwa, Na ukiangalia injili inamalizikia na Afrika(chini ya jangwa la Sahara) kwasababu ndio waliokuwa wa mwisho kupelekewa injili, na ndio inamalizikia hivyo, Irejee ilikotoka Israeli. Embu fikiri ni wakati gani huu tunaoishi??. Israeli inarudiwa na maandalizi ya kujenga Hekalu la Tatu huko Yerusalemu yameshakamilika. Miaka 70 sasa imeshapita tangu Israeli kupata uhuru wake baada ya kukaa zaidi ya miaka 2500 bila taifa. Leo hii mataifa yote macho yao yanaelekea Israeli ni nini kinachojiandaa kutokea?.

Ndugu Unyakuo ni muda wowote tokea sasa, tumeambiwa “KWA MTINI JIFUNZENI(ambalo ni Taifa la Israeli)”..Hivyo jitahidi kuingia katika huo mlango wa NEEMA sasa kabla haujafungwa, Biblia inasema

 Luka 13: 23-24 “Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia, Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.”

Tujitahidi ndugu.

Unapohubiriwa injili na kuipinga ndani ya moyo wako..ni dalili za awali kuwa neema inaondoka kwako.

Maombi yangu ni ufungue moyo wako sasa, Kristo ayabadilishe maisha yako.

2Wakoritho 6:1-2“ Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure. (Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;TAZAMA, WAKATI ULIOKUBALIKA NDIYO SASA; TAZAMA SIKU YA WOKOVU NI SASA)”.

Print this post

TABIA YAKO NI YA MNYAMA GANI?

Kila mnyama tunayemwona, kwa namna moja au nyingine yupo mwanadamu au jamii au taifa linalobeba tabia zinazofanana na huyo mnyama, Kwamfano Bwana Yesu kumwita Herode “Mbweha” hakuwa anamtukana, bali alikuwa anaelezea jinsi tabia yake inavyofanana na ya mbweha. Mbweha ni mnyama anayekaribia kufanana na mbwa, isipokuwa huyu anararau wanyama wadogo wadogo na pia tabia yake nyingine inayofanana na mbwa ni kuzaliana na mbweha mwingine yeyote bila mpangilio maalumu, hivyo tabia hizi zilionekana kwa Herode, Kwanza alikuwa muuaji: alimuua Yohana Mbatizaji nabii wa Mungu, na bado akaongeza kuoa mke wa ndugu yake, tabia zisizo na tofauti na mbweha.

Kadhalika kitabu cha Danieli kinaeleza juu ya zile Falme 4 zitakakuja kutawala mpaka mwisho wa Dunia, nazo pia zilifananishwa na tabia za wanyama, kwa mfano Babeli ilifananishwa na Simba, Umedi & Uajemi ilifananishwa na dubu, vivyo hivyo na Uyunani ulifananishwa na Chui.(Danieli 7)n.k.

Shetani naye alifananishwa na joka, kwasababu ya tabia aliyokuwa nayo nyoka ya kumdanganya mwanadamu kumuasi Mungu kwa kula tunda. Kama tu anavyoendelea kufanya sasa hivi kuudanganya ulimwengu watu wamwasi Mungu, waishie kwenda katika ziwa la moto.

Vivyo hivyo na BWANA wetu YESU KRISTO alifananishwa na mnyama fulani na huyu si mwingine zaidi ya MWANA-KONDOO.

KWANINI MWANA-KONDOO?

Tabia ya kwanza ya kondoo ni mnyenyekevu na mpole, na ni mnyama ambaye hawezi kujiongoza mwenyewe siku zote anategemea mchungaji wake kumuongoza tofauti na mbuzi, Mbuzi yeye anao uwezo wa kujichunga mwenyewe.

Na ndio maana tunaona sehemu zote Bwana Yesu aliitwa “mwanakondoo”, Yohana alimwona kama mwanakondoo achukuaye dhambi za ulimwengu, si ajabu hata kuzaliwa kwake kulikuwa ni kwenye hori la ng’ombe. YESU Alipoishi duniani alikuwa ni mpole na mnyenyekevu sana, kiasi kwamba japo alikuwa ni Mtakatifu lakini alikaa katikati ya watoza ushuru na makahaba, japo alikuwa ni mfalme lakini aliwaosha miguu wanafunzi wake. Biblia inamshuhudia alikuwa anawakemea waovu lakini moyoni mwake alijaa huruma. Yeye mwenyewe alishuhudia na kusema..

Mathayo 11: 28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa MIMI NI MPOLE NA MNYENYEKEVU WA MOYO; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”.

Ni mtu ambaye aliwaponya maadui zake waliokuja kumuua kwa mapanga na marungu, Alilia kwa dua nyingi na machozi kwa ajili ya ndugu zake(mimi na wewe).

Na kama vile kondoo wanaponyolewa manyoya yao kwa ajili ya sufu au wanapopelekwa machinjoni wanakaa kimya tofauti na mbuzi, ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana wetu Yesu, alitukanwa hakurudisha, alipigwa makofi hakurudisha, alitemewa mate, hakurudisha, japo alisikia maumivu kama mwanadamu mwingine yeyote lakini aliishia na kusema BABA WASAMEHE. Hii ilitoka ndani ya moyo wake kabisa na sio kinafiki.

Nabii Isaya alimwona miaka mingi sana kabla ya kuja kwake akaeleza habari zake..

Isaya 53:3-8 “Alidharauliwa na kukataliwa na watu; MTU WA HUZUNI NYINGI, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.

4 HAKIKA AMEYACHUKUA MASIKITIKO YETU, AMEJITWIKA HUZUNI ZETU; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

6 Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.

7 Alionewa, lakini ALINYENYEKEA, Wala hakufunua kinywa chake; Kama MWANA-KONDOO APELEKWAYE MACHINJONI, Na kama vile kondoo ANYAMAZAVYO Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, HAKUFUNUA KINYWA CHAKE.

8 Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani atakayeisimulia? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.”

Haikuishia hapo Zekaria naye alimuona miaka mingi iliyopita naye akamzungumzia na kusema…

Zekaria 9: 9 “Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; NI MNYENYEKEVU, amepanda punda, Naam, mwana-punda, mtoto wa punda.” Haleluya, Bwana Yesu alikuwa ni wa kipekee sana.

Vivyo hivyo Roho Mtakatifu alifananishwa na HUWA (yaani NJIWA)..Kutokana na tabia za njiwa huwa ni MPOLE. Na njiwa siku zote anatua sehemu zenye utulivu na amani..hawezi kutua sehemu nyingine yoyote kama Kunguru. Wanaofuga njiwa wanaelewa itakuchukua muda mrefu sana mpaka akuzoee kiasi cha kufikia hatua ya kutua kwenye mikono yako au mabegani mwako, Njiwa anayo desturi ya kuhakiki jambo Fulani kwa muda mrefu mpaka alizoee, inahitaji upole wa hali ya juu. Na inajulikana mahali palipo na makelele njiwa huwa hakai atahama hata kama anahudumiwa vizuri kiasi gani.

Na hapa tunaona ROHO mfano wa HUWA akitua juu ya Bwana Yesu Kristo kiashirio kuwa ni mahali sahihi penye utulivu wa kutua. Roho aliridhishwa na upole na unyenyekevu wa Bwana YESU kama mwanakondoo.

Marko 1: 9 “Ikawa siku zile, Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yordani.

10 Mara alipopanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kama hua, akishuka juu yake;

11 na sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.”

Vivyo hivyo na watoto wa Mungu wote wanafananishwa na wana-kondoo, na hao ndio ROHO WA MUNGU anaowashukia juu yao. Wanapaswa wawe wapole, wanyenyekevu, wanapotukanwa hawarudishi, wanapoudhiwa hawawaudhi wengine, hawasengenyi, wanawaombea wanaowaudhi, wanawapenda maadui zao na kuwasamehe kama Bwana alivyokuwa. Na zaidi ya yote hawajiongozi wenyewe kama mbuzi, wanamtegemea Mungu(Mchungaji mkuu YESU) kwa kila kitu, hawachukui maamuzi yoyote pasipo yeye, wanadumu katika NENO tu, hawaabudu miungu mingine, wanachofikiria ni utakatifu tu, wapo tayari hata kutoa uhai wao kwa ajili ya ndugu zao wengine kama yeye alivyoutoa uhai wake kwa ajili yetu. Watu kama hawa Roho wa Mungu anashuka juu yao na kuwafanya waendelea kuzaa matunda yote ya Roho.(wagalatia 5:22).

Lakini wasio wa Mungu wanafananishwa na mbuzi, wao huwa wanajiongoza wenyewe na kujiamulia mambo yao, hawana haja na mchungaji (yaani Bwana YESU), hawa hawawezi kuwa wanyenyekevu au wapole kwasababu wanajiona kuwa wanafahamu kila kitu.

Je! Wewe ni kondoo au mbuzi?. Kumbuka Roho wa Mungu hawezi kukaa juu ya mbuzi. Japo leo hii wanajificha katika kanisa la Mungu lakini utafika wakati wa kutengwa..KONDOO upande wa kuume, na MBUZI upande wa kushoto. Je! Utakuwa upande upi siku ile??

Mathayo 25: 32-46 “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;

32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;

33 ATAWAWEKA KONDOO MKONO WAKE WA KUUME, NA MBUZI MKONO WAKE WA KUSHOTO.

34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;

35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;

36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.

37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?

38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?

39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?

40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.

41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;

42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;

43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.

44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?

45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.

46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.

Print this post

NI MAONO YAPI HAYO UNAYOSUBIRIA?

Tunaposoma biblia tunajifunza mambo mengi sana, yahusuyo tabia za Mungu, na moja ya tabia ya kipekee sana ya Mungu ni “kutokumlazimisha mtu kufanya jambo Fulani”. Kuna kipindi nilitamani na nilimuomba sana Roho Mtakatifu anivae na kuniendesha pasipo mimi mwenyewe kujitambua kama vile mtu aliyepagawa na mapepo.

Kwasababu watu wenye roho za mashetani huwa wanaendeshwa mpaka wanakuwa hajitambui tena mfano vichaa. Niliendelea kuomba hivyo mpaka siku Bwana aliponipa ufahamu na kugundua kuwa Mungu hatendi kazi kwa namna hiyo japo anao uwezo huo, lakini hamvai mtu na kumfanya mateka kama vile pepo linavyofanya.

Roho Mtakatifu ni msaidizi na mshauri na pia ni mpole, kamwe hamlazimishi mtu kuchukua uamuzi Fulani, Na ndio maana mtu anapoamua kuwa mwovu, haendi kumlazimisha aokoke, yeye anachofanya ni kumshawishi na kumshauri na kumpa kila sababu ya kuacha dhambi, lakini akikataa anamwacha aendelee kufanya anachokitaka lakini akikubali anaendelea naye.

Na vivyo hivyo katika kuifanya kazi ya Mungu, wengi wanangojea waone maono kama mtume Paulo alivyoona, au watokewe na malaika, au washukiwe na uweza wa ajabu walazimishwe kama Yona, au wasikie sauti kutoka mbinguni ikiwaambia nenda, au watabiriwe n.k.

Napenda kukwambia ndugu ukitegemea njia hiyo mwisho wa siku utaishia kuvunjika moyo pale utakapoona hakuna jambo lolote lililotokea kwa kipindi ulichokuwa unasubiria na muda umeshakwenda. Njia kama hizo Mungu akizitumia ni kwa neema zake tu! Kwa kuonyesha uweza wake. Lakini sio njia aliyoikusudia kutumia kuwatuma watu wake katika kazi yake. Tunamtumikia Mungu kwa imani na sio kwa kuona, na Mungu anataka mtu afanye kwa moyo wake mwenyewe na sio kwa kulazimishwa.

Tunaweza tukajifunza mifano ya watu watatu katika biblia ambao wanaweza kutusaidia katika kujua njia sahihi ya kumtumikia Mungu.

1) DAUDI :

Daudi alikuwa ni mfalme wa Israeli, aliyepitia taabu nyingi katika maisha yake lakini Bwana alipomstarehesha, na kumpa ufalme na vitu vyote, alifikia wakati akaanza kumtafakari Mungu wake, dhamiri yake ikaanza kumchoma..akasema mimi Daudi naishi katika jumba la kifalme wakati Mungu wangu anakaa kwenye hema liliochakaa tena kwenye giza katika kijiji Fulani huko Shilo??. (Kwasababu wakati huo sanduku la Agano la Mungu lilikuwa linakaa Shilo). Ndio Daudi akaazimu moyoni mwake kumjengea Mungu nyumba nzuri ya kukaa kwa hiari yake mwenyewe.. Na alipofikiria hivyo tu biblia inasema..

1 Samweli 7: 1 “Ikawa, mfalme alipokuwa akikaa katika nyumba yake, hapo Bwana alipomstarehesha, asiudhiwe na adui zake waliomzunguka pande zote,

2 mfalme akamwambia Nathani, nabii, Angalia sasa, mimi ninakaa katika nyumba ya mierezi, bali sanduku la Mungu linakaa ndani ya mapazia.

3 Nathani akamwambia mfalme, Haya, fanya yote yaliyomo moyoni mwako; maana Bwana yu pamoja nawe.

4 Ikawa usiku uo huo, neno la Bwana likamfikia Nathani kusema,

5 Enenda, ukamwambie mtumishi wangu, Daudi, Bwana asema hivi, Je! Wewe utanijengea nyumba, nikae ndani yake?

6 Kwa maana mimi sikukaa ndani ya nyumba, tangu siku ile niliyowatoa wana wa Israeli katika Misri, hata leo, lakini nimekaa katika hema na maskani.

7 Mahali mwote nilimokwenda na wana wa Israeli wote, JE! NIMESEMA NENO LOLOTE NA MTU YEYOTE WA WAAMUZI WA ISRAELI?, niliyemwagiza kuwalisha watu wangu Israeli, NIKISEMA, MBONA HAMKUNIJENGEA NYUMBA YA MIEREZI?.

8 Basi, sasa, mwambie mtumishi wangu, Daudi, maneno haya, Bwana wa majeshi asema hivi, Nalikutwaa katika zizi la kondoo, katika kuwaandama kondoo, ili uwe mkuu juu ya watu wangu, juu ya Israeli;

9 nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina kuu, kama jina la wakuu walioko duniani.”

Ukizidi kusoma mbele utaona Daudi kwa kufanya hivyo aliahidiwa kuwa kiti chake cha enzi na ufalme utathibitika milele, Na ndio maana Mungu aliuchagua uzao wa Daudi kupitia yeye Kristo atokee huko, na mji wake Yerusalemu kuwa makao makuu ya MASIHI duniani.. Na Daudi ndiye aliyeupendeza moyo wa Mungu kuliko watu wote.

Sasa je! DAUDI ALINGOJEA MAONO YAMJIE ILI AMJENGEE MUNGU NYUMBA??.. Hapana aliona kila sababu ya kwanini asifanye vile kwa Mungu angali anao huo uwezo?. Na ndipo Mungu akampa thawabu kuu kwa maamuzi ya busara aliyoyafanya.

2) NEHEMIA:

Mfano mwingine tunamwona Nehemia, aliyekuwa mnyweshaji wa Mfalme wa Uajemi..Lakini siku moja ndugu zake walitoka Yerusalemu, na kumpasha habari kuwa nyumba ya Mungu, na Ukuta wa Mji umebomolewa. Habari zile zilimuhuzunisha sana hata akaamua afunge na kuomboleza na kulia kwa siku nyingi kwa ajili ya mji wake, na kumuomba Mungu dua na msamaha kwa Israeli, kumbuka Nehemia hakuwa nabii, alikuwa ni mtu tu! wa kawaida, mfanyaji wa kazi za ndani za mfalme wa mataifa.

Hivyo akawaza moyoni mwake tu, siwezi kukaa katika hali hii ya raha huku nyumba ya Mungu wetu kule Yerusalemu imekaa katika hali ya kuharibiwa. Kwa kufanya hivyo Mungu akamuhurumia na kumpa kibali cha mfalme kwenda Yerusalemu kukarabati nyumba na ukuta wa mji..

Japo alipitia taabu nyingi sana wakati wa kujenga ukuta, maadui waliwazunguka kila upande, mkono mmoja ulishika silaha na mwingine nyenzo za ujenzi, lakini kwa bidii yeye na wenzake walifanikiwa kumaliza kuujenga ukuta wa mji, mpaka akafikia kusema UNIKUMBUKE MUNGU WANGU, kwa taabu hizi..

Huyu naye pia hakuwahi kuona maono, wala kuota ndoto, au kuzungumza na malaika, au kushukiwa na upako aliona tu nyumba ya Mungu ipo katika hali mbaya inanipasa nifanye kitu!!.. Lakini leo hii tunaona ushujaa wa Nehemia Mungu kampa kumbukumbu lisilofutika leo tunakisoma kitabu chake japo hakuwa nabii wala kuhani wala mwandishi.

3) MWANAMKE KAHABA:

Mfano mwingine tunamwona Yule mwanamke mwenye dhambi aliyemwendea Yesu, pamoja na dhambi zake zote alizokuwa nazo aliona kuna mapungufu katika mwili wa Yesu, aliona kuwa miguu ya Yesu ni michafu, ndipo akaona kuna sababu ya kuiosha kwanza, hivyo akatumia machozi yake, badala ya maji, akatumia nywele zake kumfuta badala ya kitambaa, na baada ya kuona imesafishika akampaka mafuta yenye manukato ya thamani nyingi sana (thamani yake kwasasa ni sh. Milioni 6)…Kumbuka huyu hakuona maono aliamua tu mwenyewe kufanya hivyo baada ya kuona mapungufu, lakini baada ya tukio hilo Bwana Yesu aliwaambia..

Luka 7: 44 “Akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni, Wamwona mwanamke huyu? Niliingia nyumbani kwako, hukunipa maji kwa miguu yangu; bali huyu amenidondoshea machozi miguu yangu, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake.

45 Wewe hukunibusu; lakini huyu tangu nilipoingia hakuacha kunibusu sana miguu yangu.

46 Hukunipaka kichwa changu mafuta; bali huyu amenipaka miguu yangu marhamu. 

47 Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo.

48 Kisha alimwambia mwanamke, Umesamehewa dhambi zako.”

NI MAONO YAPI HAYO UNAYOSUBIRIA?

Kumbe iliwapasa wajue wao wenyewe kuwa miguu ya Bwana ni michafu na inahitaji kuoshwa, lakini wao walisubiria waambiwe..ndugu nataka nikuambie kama na wewe leo unasubiria Mungu akuambie nenda kafanye kitu fulani angali unafahamu kabisa kuna huo uhitaji,..jua tu hatakuambia …Ni jukumu lako wewe kuchukua hatua.

Ipo mifano mingi ya namna hii katika biblia yupo mwanamke mwingine alifanya kama huyu wa kwanza ukisoma Mathayo 26:13, utaona alimmwagia Bwana mafuta katika nywele zake, japo wengine waliona kama anatapanya pesa lakini Bwana alimwambia kuwa kwa kuwa amefanya vile Popote itakapohubiriwa injili, tendo hilo litatajwa kwa kumbukumbu lake. Huyu naye hakusubiria neema imshukie, au asubirie nabii amtabirie.

Hivyo ndugu, mahali ulipo,au kanisa ulilopo au chochote unachokifanya..je! unaugua kwa ajili ya kazi ya Mungu au unasubiri jambo Fulani Mungu akutendee ndipo uanze kumtumikia Mungu?. Mungu amekubariki katika Mali zako, zitumie hizo kufanya kazi ya Mungu, habari njema ziwafikie wengi kama wakina Martha, sio lazima uwe muhubiri, Nehemia hakuwa muhubiri, lakini alimfanyia Mungu kitu kinachoonekana, unaona choo kichafu kanisani, nyasi zimeota, unangoja uone maono juu ya hilo?.

Unaona kuna umuhimu wa kuwavuta watu kwa Kristo unasubiria kuitwa?? Utaitwa lini na huku umeshakaa katika ukristo kwa miaka mingi?. Lakini mtu atasema mimi sijui wito wangu..ndugu tumeitwa wote kuwa mashuhuda wa Kristo?.

Wewe ni fundi wa nyumba au technician unaona kuna kasoro katika nyumba ya Mungu embu kuwa kama Nehemia usingojee maono yakushukie kwenda kufanya hivyo, usisubirie mtu mwingine aajiriwe kuja kuifanya hiyo kazi angali ipo katika uwezo wa mikono yako.

Umepata nafasi ya kukaa mitandaoni na unaona kabisa kuna uhitaji wa watu kumjua Mungu usisubirie lolote kwasababu kamwe Bwana hatakuambia au kukulazimisha kufanya hicho kitu.. Inahitaji hekima tu kulitambua hilo.

Ni maombi yangu utachukua hatua sasa kwa kila sehemu Bwana alipokuweka kwa ajili ya Kristo. Mungu atakusaidia na kumbukumbuku lako halitaondoshwa milele.

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa mawasiliano, maombi/ushauri/ubatizo/ whatsapp: Namba zetu ni hizi: +255693036618/ +255789001312


Mada Nyinginezo:

USIISHIE KUTAZAMA JUU, ENDELEA MBELE.

MAMBO AMBAYO MALAIKA WANATAMANI KUYACHUNGULIA.

UCHUNGU WA KUIBIWA

JE! MKRISTO ANARUHUSIWA KULA NGURUWE, NA KUVUTA SIGARA NA KUNYWA POMBE?

JE! NI SAHIHI KWENDA KUMFUATA KIONGOZI WA DINI KWA MFANO PADRE NA KUMPIGIA MAGOTI KUMWELEZA DHAMBI ZAKO AKUSAMEHE?.


Rudi Nyumbani

Print this post

ZIKUMBUKE FADHILI ZA MUNGU

Ni rahisi KUANGUKA au KUPOA katika Imani kama hautajiwekea utaratibu wa Kujikumbusha matendo yote mema Mungu aliyokutendea nyuma katika maisha yako.

Jambo lililowafanya Wana wa Israeli kule jangwani washindwe kusonga mbele na kukwazwa na mabaya, lilikuwa si lingine zaidi ya KUSAHAU fadhili za Mungu walizotendewa nyuma, kwamfano walipotoka Misri, na kukutana na kikwazo cha bahari, walianza kunung’unika wakasahau siku chache tu nyuma Mungu aliwapigania kwa mkono hodari dhidi ya maadui zao wamisri,

vivyo hivyo mara baada tu ya kufanyiwa muujiza mwingine wa bahari kupasuka walimshangilia Mungu kwa furaha na kumwimbia nyimbo za shangwe lakini baada ya siku tatu mbeleni, manung’uniko yakaanza tena pale walipokosa maji ya kunywa, tatizo lilikuwa ni moja tu! Walisahau wema wa Mungu waliotendewa siku chache nyuma, laiti wangetilia maanani mema yale na kukumbuka fadhili zote zile, wasingeshindwa kustahimili majaribu waliyokutana nayo. Na ndivyo ilivyoendelea kuwa katika safari yao yote, manung’uniko kila walipokutana na changamoto.

Na ndio sababu Mungu aliwakataza Israeli wote wasile WANYAMA WASIO CHEUA, kwa mfano nguruwe au farasi nk. Unajua ni kwa sababu gani??, kwasababu katika roho wanafunua kitu Fulani. Mnyama anayecheua ni mnyama ambaye akila chakula anao uwezo wa kukirudisha tena kinywani mwake na kukitafuna kisha akimeze tena, kwa mfano ng’ombe analo tumbo la akiba, akila baadaye anarudisha na kukitafuna tena.

Hivyo wanyama wa namna hiyo hawakuwa najisi, kwa tabia hiyo tu. Ikifunua katika roho kuwa watu wote wasiokuwa na uwezo wa kuzikumbuka na kuzitafakari fadhili na sheria za Mungu ni NAJISI mbele zake. Watu wote wa Mungu wanapaswa wawe na uwezo wa kucheua, baada ya kusikia au kufanyiwa miujiza, sasa kinachofuata ni kuyarudisha tena katika akili na kuyatafakari hayo kila mara.

Yakobo 1: 22-25 “Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.

23 Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo.

24 Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo.

25 Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, ASIWE MSIKIAJI MSAHAULIFU, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.”

Kadhalika na kwa wakati tuliopo sasa, ili tusonge mbele au tuweze kusimama katika IMANI na kushinda wakati wa majaribu inatupasa tujiwekee utaratibu wa kutafakari na kujikumbusha kila siku mambo mema ambayo Mungu amewahi kututendea katika maisha yetu ya nyuma, Kwa mfano ulipowahi kupatwa na ugonjwa Fulani ambao ulikutesa sana na Bwana akakuponya, ni vizuri kujikumbushia jambo hilo kila siku, au ulimwomba Mungu jambo Fulani akakupa na kukufanikisha katika mambo yako na ukafahamu kabisa huyo ni Mungu aliyekutendea hivyo, unapaswa kulifikiria hilo kila siku usije ukasahau pale tatizo litakapokuja ili uweze kukabiliana nalo.

Kumbuka tena mahali Mungu alipokushindania ambapo unajua kabisa pasipo yeye usingeweza kufanikiwa, uwe unalitafakari hilo kila siku litakusaidia huko mbeleni ili umsimnung’unikie Mungu..Kuna hatari kubwa sana ya kuanguka kama hautajijingea huo utaratibu wa kukumbuka mambo uliyotendewa..

Sisi wanadamu tuna tabia ya kusahau hivyo ili usisahau ni vizuri uwe unaandika chini kila wema Mungu anaokufanyia kila siku.Kwa kufanya hivyo ndivyo utakavyoweza kudumu katika IMANI siku zote. Na pia unaposoma Neno la Mungu jenga tabia ya kujikumbusha kila wakati ili usisahau mapenzi ya Mungu katika maisha yako.

Wakati mwingine unajikuta unadondoka katika dhambi za usengenyaji, kwasababu unasahau Neno la Mungu, linakuwa halijakaa kwa wingi ndani yako, unajikuta unashindwa kusamehe kwasababu huna tabia ya kutafakari kila siku NENO LA MUNGU, Unajikuta wewe ni mkristo lakini unazungumza maneno ya mizaha, kwasababu mistari inayohusiana na mambo kama hayo imefutika ndani ya moyo wako, huna jambo la kukukumbusha kila wakati.

Ni maombi yangu utaanza kujenga utaratibu kuanzia leo wa kurekodi mambo yote mazuri Mungu anayokutendea ili yawe akiba kwa wakati wa shida au majaribu mbeleni. Na pia utaanza kutafakari NENO la Mungu kila siku. Sulemani kwa hekima ya Roho alituandikia sisi tulio watoto wa Imani na kusema;

Mithali 7:2 “Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako.

2 Uzishike amri zangu ukaishi, NA SHERIA YANGU KAMA MBONI YA JICHO LAKO.

3 ZIFUNGE KATIKA VIDOLE VYAKO; ZIANDIKE JUU YA KIBAO CHA MOYO WAKO.”

Na Daudi alisema;

Zaburi 119: 97 “Sheria yako naipenda mno ajabu, NDIYO KUTAFAKARI KWANGU MCHANA KUTWA.

98 Maagizo yako hunitia hekima kuliko adui zangu, KWA MAANA NINAYO SIKU ZOTE.

99 Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote, Maana shuhuda zako ndizo NIZIFIKIRIZO.

100 Ninao ufahamu kuliko wazee, Kwa kuwa nimeyashika mausia yako.”

Ubarikiwe na BWANA YESU.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa mawasiliano, maombi/ushauri/ubatizo/ whatsapp: Namba zetu ni hizi: +255693036618/ +255789001312


Mada Nyinginezo:

Nini maana ya “Kandake” (Matendo 8:27)

MAISHA ULIYOPITIA NYUMA NI USHUHUDA TOSHA WA WEWE KUMTUMIKIA MUNGU

MATOWASHI NI WAKINA NANI?

NINI MAANA YA HAYA MANENO ALIYOSEMA BWANA ; TULIWAPIGA FILIMBI WALA HAMKUCHEZA; TULIOMBOLEZA WALA HAMKULIA?


Rudi Nyumbani

Print this post

WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU

Naomba usome ushuhuda huu mfupi utakujenga,

“Mimi na ndugu yangu tumekuwa na desturi ya muda mrefu kukaa pamoja na kushirikishana NENO LA MUNGU mara nyingi ili kuepuka usumbufu wa watu tumekuwa tukiondoka na kwenda mbali na makazi ya watu, sehemu zenye utulivu na kutumia muda mwingi kulitafakari NENO LA MUNGU, pamoja na kutiana moyo katika safari yetu ya Ukristo. Siku moja wakati tunatembea muda wa mchana kama saa 7 huku tunazungumza habari za Mungu na kutafakari ghafla mbele yetu njiani umbali si mrefu sana, tulioana punda watatu wamefungwa NIRA wanafuata njia, wakikokota kigari cha mzigo wa majani na nyuma kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa akiwaendesha hao punda, lakini jambo moja lilitushangaza kidogo ni kuona punda 3 wamefungwa nira huku wakikivuta kile kigari wakati mara nyingi inakuwa ni punda wawili tu!.

Hivyo tulipokaribia kuwasogelea ili tuone vizuri, Yule punda aliyekuwa katikakati yao alitoweka wakabaki punda wawili kama kawaida. Wakati tunalishangaa hilo tukio lilitokea wale punda walifika mahali wakakuta na mtaro, uliokuwa mgumu kidogo kuvuka kutokana na ule mzigo waliokuwa wanauvuta, hivyo Yule Bwana wao aliokuwa anawaongoza alipoona wamesimama aliwachapa kwa fimbo yake aliyokuwa nayo, lakini japo ule mzigo ulikuwa ni mkubwa kwa wao kuuvukisha katika ule mtaro mwishoni walifanikiwa kupandisha na kuendelea na safari.

Tulibaki tunajiuliza maswali ni kitu gani tumeona? Ni mazingaumbwe au nini?. Ndipo Mungu akutupa ufahamu saa ile ile ni kwamba Mungu alitufumbua macho tuone jambo linaloendelea katika roho kuhusu sisi,”

Mathayo 18:20 “ Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.”

Biblia inasema Mathayo 18:20 “ Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.”

Tafsiri ya lile ono ni kuwa wale punda wawili wanatuwakilisha sisi wawili mimi na ndugu yangu, Yule punda wa tatu aliyekuwa katikati na kisha baadaye akaja kutoweka alimwakilisha Bwana YESU.

Na ule mzigo wale punda waliokuwa wameubeba ni SHERIA ZAKE, hivyo tunapokuwa wawili au zaidi Mungu anatufunga Nira yake mwenyewe sisi kwa sisi, na yeye akiwa katikati yetu kutusaidia mzigo wake(sheria zake), hivyo sheria zake zinakuwa nyepesi kuzishika.

Bwana Yesu pia alitupeleka kwenye hili andiko Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29 JITIENI NIRA YANGU, MJIFUNZE KWANGU; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30 KWA MAANA NIRA YANGU NI LAINI, NA MZIGO WANGU NI MWEPESI.”

Bwana alituonyesha kuwa anayo NIRA yake na MZIGO wake kwa watu wake, japo watu wa nje watauona kama ni mzigo mzito lakini Bwana akiwa katikati yetu unakuwa mwepesi kwasababu yeye anatusaidia, anakuwa anafanyika kama punda wa tatu katikati yetu.

> Kuishi maisha ya kuukataa ulimwengu huo ni mzigo wa Kristo aliokutwisha, na ndio maana wengine watakushangaa unawezaje kuishi maisha ya kutokufanya uasherati.

> Kufanya kazi yoyote ya Mungu ni mzigo wa Kristo, lakini yeye anakupa wepesi hususani mnapokuwa wawili au zaidi na ndio maana kila mahali Bwana alikuwa akiwatuma wawili wawili kazini kuhubiri injili.

Hivyo ndugu, kuna umuhimu mkubwa kuwa na mwenzako au wenzako mnaofanana imani, kwasababu mnapokuwa wawili au watatu au zaidi kwa jina lake lile NENO lazima litimie, ATAKUWA KATIKATI YENU. Mnakuwa mmefungwa NIRA na Kristo pamoja, hivyo mtajikuta kiurahisi mnazitimiza sheria za Bwana bila ugumu wowote tofauti na unapokuwa mwenyewe.

Umuhimu wa kuwa na mwenzako au kukusanyika na wenzako ni uwepo wa kipekee unashuka mahali mlipo, vitu kama faraja, kutiana moyo, kulindana, kushirikishana, mafunuo n,k. vinatoka huko kiasi kwamba hata shetani inamuwia ugumu kupata nafasi ya kukujaribu kwasababu yupo ndugu yako pembeni anayekuchunga.

Ndio maana biblia inasema katika 

Mhubiri 4:9-12 “Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.

10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!

11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto?

12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.”

Unaona hapo, kuna umuhimu wa kuwa karibu na ndugu anayeenda na wewe imani, Sisi baada ya Bwana kutufundisha hayo, tumekuwa tukikaa pamoja muda mrefu wakati mwingine kuanzia asubuhi mpaka jioni na tumekuwa tukimwona Mungu kwa namna ya kipekee isiyokuwa ya kawaida tofauti na pale mwanzo kila mtu alipokuwa kivyake.

Unawakumbuka wale watu wawili waliokuwa wanatoka Yerusalemu na kuelekea Emau, Njiani wakati wanazungumza habari za kufufuka kwake Yesu, Bwana mwenyewe aliwatokea na kuungana nao pasipo wao kujijua, baadaye kabisa mwishoni ndipo walipofunguliwa macho na kufahamu kuwa Yule alikuwa ni BWANA YESU mwenyewe(Luka 24).

Vivyo hivyo na wewe utakapojumuika na mwenzako au wenzako na kuanza kumzungumzia Bwana Lile Neno lake la ahadi lazima litimie. Na safari yako ya ukristo haitahitaji nguvu nyingi.

Natumai ushuhuda huu utakufanya uchukue uamuzi wa kujumuika na ndugu aliye  moja na wewe.

Bwana akubariki sana.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa mawasiliano, maombi/ushauri/ubatizo/ whatsapp: Namba zetu ni hizi: +255693036618/ +255789001312

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp


Mada Nyinginezo:

TUSIFUNGWE NIRA PAMOJA NA WASIOAMINI.

KWANINI TUWE WENYE BUSARA KAMA NYOKA?

DHAMBI YA ULIMWENGU.

NI KWELI MTU ANAWEZA AKAFA LAKINI ROHO YAKE IKAWA INATUMIKA KAMA MSUKULE (KUMILIKIWA NA MTU FULANI KWA WAKATI) MAHALI PENGINE?


Rudi Nyumbani

Print this post

USIMFANYIE JEURI ROHO WA NEEMA.

Kuna hatari kubwa sana kuidharau Neema ya Bwana YESU KRISTO, Katika agano la kale, kule jangwani Mungu alipokuwa anazungumza na wana wa Israeli katika mlima SINAI, Utukufu wa Mungu ulikuwa ni mkubwa kiasi kwamba hata watu wenyewe walikataa kuukaribia ule mlima kwa jinsi ulivyokuwa unatisha, kwa hofu na kwa kutetemeka walifikia hatua ya kumwambia Musa azungumze nao lakini sio Mungu. Mlima ule ulitisha sana hata kwa mnyama yoyote aliyeusogelea ilikuwa ni kifo.

Biblia inasema; katika Waebrania 12:18-25

18 Maana hamkufikilia mlima uwezao kuguswa, uliowaka moto, wala wingu jeusi, na giza, na tufani,

19 na mlio wa baragumu na sauti ya maneno; ambayo wale walioisikia walisihi wasiambiwe neno lo lote lingine;

20 maana hawakuweza kustahimili neno lile lililoamriwa, Hata mnyama akiugusa huo mlima atapigwa kwa mawe.

21 Na hayo yaliyoonekana jinsi yalivyokuwa ya kutisha, hata Musa akasema, Nimeshikwa na hofu na kutetemeka.

22 Bali ninyi mmeufikilia MLIMA SAYUNI, NA MJI WA MUNGU ALIYE HAI, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,

23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,

24 na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.

25 Angalieni msimkatae yeye anenaye. Maana ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya nchi, ZAIDI SANA HATUTAOKOKA SISI TUKIJIEPUSHA NA YEYE ATUONYAYE KUTOKA MBINGUNI;”.

Kama biblia inavyosema sisi tulio kwenye AGANO lililo bora la DAMU YA YESU KRISTO, tunaukaribia mlima wa mbinguni(SAYUNI YA MBINGUNI) mbali na wana wa Israeli wao waliukaribia mlima wa duniani(SINAI),.. Ni dhahiri kuwa wale walioukaribia mlima wa mbinguni, ambao maelfu ya malaika wamekusanyika ndio walio karibu zaidi na Mungu kuliko hao wengine.Hivyo hawa wa mbinguni ndio wanapaswa wawe na hofu kubwa zaidi na wawe makini zaidi, kwasababu wapo karibu na Mungu, hivyo kosa moja linaweza likakugharimu mauti ya kiroho.

Na ndio maana biblia inasema 

Wafilipi 2:12b-13 “ UTIMIZENI WOKOVU WENU WENYEWE KWA KUOGOPA NA KUTETEMEKA. 13 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.”

Hii tunayoiita NEEMA, ni kweli ni NEEMA lakini sio neema kwa wakati wote, Inapochezewa au kutupiliwa mbali inageuka kuwa laana mbaya kuliko zote. Biblia inasema hali ya mtu Yule aliyeidharau hali yake ya mwisho inakuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.

2Petro 2:20 “Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.

21 Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.

22 Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.”

Pale unapojiita mkristo halafu bado unakwenda kwa waganga ili upate kitu Fulani, ukijifariji kwamba utatubu tu siku moja, kwasababu neema bado ipo!! Usidanganyike NEEMA haifanya kazi kwa namna hiyo shetani anataka ufikirie hivyo ili ukumbane na mauti ya kiroho kutoka kwa Mungu mwenyewe.

Unapojiita mkristo halafu bado ni mwasherati, mlevi, mwabudu sanamu, na huku unafahamu kabisa hayo uyafanyayo sio sawa, ukijifariji utatubu, kwasababu tunaishi chini ya NEEMA, biblia inasema ingekuwa heri kwako kama usingeijua ile haki, Ndugu utaangukia hukumu ya kifo cha kiroho,na ukishafikia hiyo hatua, ndio pale injili kwako inageuka kuwa upuuzi tu masikioni mwako au hadithi za kutunga, ROHO MTAKATIFU anakuacha na kuondoka, na ile hali ya kuugua ndani juu dhambi inaondoka kwako, kutenda dhambi kunageuka kuwa ni kitu cha kawaida, hapo hata uhubiriweje injili huwezi kugeuka unasubiria moto wa jehanum.

Shetani ndiyo agenda yake sasa hivi, kuwapofusha watu na hili Neno “tunaishi chini ya neema” na kusema Mungu ataturehemu tu! Hata tuwe watenda dhambi.. Kumbuka Neema ina pande mbili, kwa Yule anayeikubali ndio italeta manufaa chanya kwake, lakini kwa Yule anayeidharau na kuitupilia mbali inageuka kuwa LAANI kubwa mno.

Waebrania 10:26-29 “Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, HAIBAKI TENA DHABIHU KWA AJILI YA DHAMBI;

27 BALI KUNA KUITAZAMIA HUKUMU YENYE KUTISHA, NA UKALI WA MOTO ULIO TAYARI KUWALA WAO WAPINGAO.

28 Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.

29 Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni KITU OVYO, NA KUMFANYIA JEURI ROHO WA NEEMA?”.

Unaona hapo usitende dhambi za makusudi ukidhani neema itaendelea kudumu siku zote maishani mwako, Ndugu huu ni wakati wa kujitazama tena maisha yako ni wapi haujakaa sawa, unalega lega au vuguvugu. Fanya bidii usimame imara angali bado Roho wa NEEMA analia ndani yako uache dhambi, fanya hima usimfanyie jeuri kabla haujachelewa, kwa maana wakati wa wokovu uliokubaliwa ni sasa.

Tubu mgeukie Kristo aliye mkuu wa uzima wako, naye ni mwaminifu atakuosha na kukupa uzima wa milele.

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa mawasiliano, maombi/ushauri/ubatizo/ whatsapp: Namba zetu ni hizi: +255693036618/ +255789001312


Mada Nyinginezo:

JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOWAFUNULIA WATU MAANDIKO.

USIMFANYIE JEURI ROHO WA NEEMA.

Je Malaika Mikaeli ndiye Yesu mwenyewe?

HABARI ILE YA PILATO KUCHANGANYA ZILE DAMU ZA WAYAHUDI NA PAMOJA NA DHABIHU ZAO,(LUKA 13) ILIHUSU NINI?


Rudi Nyumbani

Print this post

YATAFUTE YALIYO JUU SIKU ZOTE.

Wakolosai 3:1 “Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, YATAFUTENI YALIYO JUU KRISTO ALIKO, ameketi mkono wa kuume wa Mungu.

2 YAFIKIRINI YALIYO JUU, SIYO YALIYO KATIKA NCHI.”

Kama wasafiri hapa duniani, kila siku shabaha yetu inapasa iwe ni kufika mbinguni kwa gharama yoyote ile, Biblia imetuambia “tuyatafute” na “kuyatafakari” yaliyo juu, ikiwa na maana kuwa kwa bidii zote na nguvu zetu zote, tutafute kanuni za kutufanya sisi kuingia mbinguni, tumeambiwa tuutafute kama vile tunavyotafuta fedha au kama hazina iliyositirika (Mithali 2:4),

> Mambo ya ulimwengu huu yasiwe kikwazo cha wewe kuikosa mbingu, unapaswa utumie hekima popote ulipo usiwe na kisingizio kwamba kitu fulani kimekusonga usimtafute Mungu, kumbuka wapo katika dunia hii hii matajiri wakubwa kuliko wewe na bado wanayafikiria yaliyo juu, na maisha yao ni kama wasafiri tu hapa duniani, kama mfano wa akina Sulemani katika biblia, japo alikuwa ni tajiri lakini aliyatafakari sana yaliyo juu ,

> Wapo wenye vyeo vikubwa kuliko wewe katika kizazi hiki hiki unachoishi lakini fikra zao na mawazo yao yapo mbinguni, usiku na mchana wanamwomba Bwana ufalme wake uje!, mfano ni kama Danieli alivyokuwa katika biblia,japo alikuwa mwenye cheo kikubwa lakini kutwa mara tatu alikuwa akimwomba Mungu kuhusu hatma yake na watu wake.

> Vivyo hivyo wapo maskini kuliko wewe, hawana chakula wala nguo wala mahitaji yoyote lakini mawazo yao na fikra zao si katika mambo ya ulimwengu huu bali mbinguni, japo wanapitia magumu, wanaishi kama wasafiri tu hapa duniani…Wanaishi kama Lazaro wa kwenye biblia, ingawa alikuwa anakula makombo lakini hakutupa wokovu wake chini.

> Wapo wenye shida nyingi kuliko zako; wagonjwa, walemavu, hawana watoto, mayatima, lakini kwao hayo yote si kitu, mawazo yao na fikra zao zimeelekea juu mbinguni, siku kwa siku wakijihakiki maisha yao wasianguke, wakijiepusha na maovu wasije wakaikosa mbingu.

Na wewe je! UNAYATAFUTA YALIYO JUU! Au FIKRA ZAKO ZIMEELEKEA JUU MBINGUNI? Katika hali yoyote uliyopo?..Kumbuka vya duniani vinapita, hivyo visiwe sababu ya wewe kukusonga na kuikosa mbingu. Anza sasa kutamani kwenda mbinguni.

Tunaishi katika  muda wa nyongeza Bwana Yesu anakaribia kurudi.

Ubarikiwe.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.

DHAMBI YA MAUTI

MUNGU ALIKUWA ANAONGEA NA NANI ALIPOSEMA NA “TUMFANYE MTU KWA MFANO WETU”,(MWANZO 1:26)?

KATIKA BIBLIA KUNA UFUFUO WA AINA NGAPI?


Rudi Nyumbani

Print this post

JE! WEWE NI MBEGU HALISI YA KRISTO?

Huu ni wakati wa kuwa makini sana juu ya hatma ya maisha yetu ya rohoni, kwasababu tusipokuwa makini katika nyakati hizi na kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda tunaweza tukajikuta tunaangukia katika vifungo vya shetani pasipo hata kujijua.

Kumbuka shetani sasa hivi anatenda kazi ndani ya KANISA la Mungu, hawezi kutilia mkazo sana kwa watu wa nje walio waovu kwasababu hao ameshawapata siku nyingi..anakutafuta wewe unayejiita mkristo unayejiona umesimama. Na unadhani atakupatia wapi zaidi ya kanisani.? Huko ndiko kiti chake cha enzi alipokiamishia.

Bwana Yesu alizungumza hivi;

Mathayo 13:24-30

24 Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake;

25 lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.

26 Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu.

27 Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu?

28 Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye?

29 Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing’oa ngano pamoja nayo.

30 Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.

Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.

Kumbuka magugu na ngano ni vitu vinavyofanana sana, kwa kuviangalia huwezi ukavitofautisha mpaka vitakapokuwa vikubwa na kutoa mazao, Katika mfano huo tunafahamu kuwa aliyepanda hizo mbegu njema ni BWANA YESU na shamba lake ni KANISA. Tunaweza tukaona jinsi kanisa la kwanza lilivyokuwa safi, takatifu lisilojichanganya na mafundisho yoyote ya uongo au mapokeo yeyote ya kibinadamu, ni kanisa lililokuwa halina dosari,

Lakini baada ya shetani kuona hilo alianza kuja na mbinu za kuliharibu, hivyo aliiga njia ile ile ya kupanda mbegu kama vile Bwana alivyofanya. Ndipo akaanza kwanza kwa kupenyeza mafundisho ya uongo katikati ya kanisa la Mungu, kisha ile mbegu ya uongo ilipomea baadaye ikageuka na kuwa dini, na kukaa katikati ya kanisa la Mungu. Kuanzia hapo hizi mbegu mbili zikawa zipo pamoja zikishindana katika kanisani la Kristo.(Magugu na Ngano)

Mungu kwa kulifahamu hilo aliruhusu vyote vimee kwa pamoja mpaka wakati wa mavuno utakapowadia kwasababu kama tulivyoona magugu yakiwa machanga ni ngumu kuyatofautisha na ngano, yanafanana sana kwa tabia zao. Na Mungu aliposema yaache yakue pamoja ni kiashiria kuwa yote yapate mvua kutoka kwa Mungu.(Mathayo 5:45). Ikiwa na maana kuwa Mungu aliyaruhusu yafanikiwe katika njia zao kama vile tu zile mbegu njema zifanikiwavyo mpaka wakati wa mavuno utakapowadia. Yote yananyeshewa mvua, kumbuka hata manabii wa uongo wanatabiri kwa jina la Bwana na inatokea, wanaponya na kutoa pepo kwa jina la Yesu na yanawatii, lakini siku ile Bwana atawaambia siwajui nyinyi mtendao maovu. Kwasababu hawa walinyeshewa mvua moja na ngano halisi lakini ndani yao walikuwa ni magugu.

Hivyo Kanisa katoliki lilianza kujitokeza katika kanisa la Mungu kama GUGU la kwanza, enzi zile za kanisa la kwanza, lilianza na mafundisho tu (MBEGU), baadaye likaota mizizi na kujiundia dini inayofanana na ukristo katika kanisa, likazidi kusambaa katika shamba la Mungu na kusonga zile mbegu halisi za Mungu na ndio maana tunaona hili kanisa lilianza kuharibu mafundisho ya NENO LA MUNGU na kupachika mafundisho ya uongo na kama tunavyofahamu tabia halisi ya gugu ni kuharibu kile kilicho halisi, na ndio maana baadaye tunavyosoma katika historia liliuawa watakatifu wa Mungu zaidi ya milioni 68 waliojaribu kwenda kinyume na mafundisho yake ya uongo.

Na lilipofikia kilele likazaa na magugu mengine mengi yanayofanana ni hilo, yakifanya kazi moja, kuiharibu mbegu halisi ya Mungu. Lakini biblia inasema wakati wa mwisho ambao ndio tuliopo sasa, yale magugu na ngano vitatenganishwa, yale magugu yataanza kwanza kwa kufungwa matita matita kwasababu yapo mengi,

JE! HAYA MATITA MATITA NI NINI?..Haya si mengine zaidi ya MADHEHEBU, na watakaoyafunga ni akina nani? Hawa Si wengine zaidi ya wanaojiita viongozi wa dini lakini ndani ni mitume wa uongo (2Wakoritho 11:13).

Mhubiri yoyote anayekupeleka kwenye dini yake zaidi ya kukupeleka kwa Kristo huyo ni mvunaji anayekufunga katika mojawapo ya tita la magugu. Kiongozi anayekufundisha mafundisho yasiyotokana na utakatifu, anakuambia tu! Mungu ni wa rehema, huku hana habari na mambo ya toba au kuhubiri utakatifu yeye anakazania mambo ya ulimwengu huu tu, ujue huyo ni mvunaji anayetaka kukufunga katika mojawapo ya tita la magugu lililoandaliwa kwa ajili ya kuchomwa moto.

Mhubiri anayekuhubira kutwa kuchwa mafanikio tu! Agusii hata siku moja hatma ya maisha yako ya rohoni, anayekuhubiria Kristo harudi leo wala kesho..mkimbie huyo ni mvunaji wa siku za mwisho kazi yake ni kuwafunga watu wa namna hiyo wasiotaka kujihusisha na mambo ya Mungu bali wajihusishao na mambo ya ulimwengu huu tu.

Ukiona kanisa linakuambia hakuna kuzimu na mateso yake, au halitaki kudumu katika NENO LA MUNGU peke yake,linakuongoza katika ibada za sanamu ambazo Mungu amezipinga vikali, kimbia haraka sana hilo ni TITA la kukusanya watu wa dizaini hiyo wasiotaka kudumu kutenda mapenzi ya Mungu..

2Wathesalonike 2:10 “na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; KWA SABABU HAWAKUKUBALI KUIPENDA ILE KWELI, WAPATE KUKOLEWA.

11 Kwa hiyo Mungu awaletea NGUVU YA UPOTEVU, WAUAMINI UONGO;

12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.”

Na Kumbuka kila siku hawa wavunaji(Manabii wa uongo) na haya matita ya magugu yanazidi kuongezeka kuonyesha kuwa huu ni wakati wa mavuno wa siku za mwisho.

LAKINI NGANO HALISI NI IPI

Ukisoma mfano huo kwa makini utaona kuwa NGANO HALISI haijakusanywa katika matita matita mengi kama magugu yalivyofanywa, bali Ngano imekusanywa pamoja mara moja tu na kupelekwa ghalani. Kuonyesha kuwa bibi-arusi wa Kristo hatakuwepo kati ya mojawapo ya hivyo vikundi, Bibi-arusi hana utambulisho wa kimadhehebu. Baada ya kukusanywa maramoja atapelekwa ghalani (mbinguni). Ndugu tunaishi katika wakati wa bibi-arusi wa Kristo kukusanywa kwa ajili ya unyakuo. Na anakusanyikia wapi?.

Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake katika

Mathayo 24: 23 “Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki.

24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.

25 Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele.

26 Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki.”

Hii Ikiwa na maana kuwa katika siku za mwisho watatokea mitume na manabii wengi wa uongo, na zitatokea dini nyingi na madhehebu mengi ya uongo, na kila moja likidai kuwa lenyewe lina Kristo, ili tu yapate kuwakufunga watu kwenye matita yao..lakini Bwana alisema yatakapowafuata na kuwaambia hivyo msisadiki?. Na ndipo wanafunzi wake wakamuuliza..kama hatutawasidiki hao basi tukusanyike wapi sasa? Jibu lake lilikuwa ni hili.

Luka 17: 37 “Wakajibu, wakamwuliza, WAPI, BWANA? Akawaambia, ULIPO MZOGA, NDIPO WATAKAPOKUTANIKA TAI.”

Mzoga ni NENO LA MUNGU, na TAI ni BIBI-ARUSI, Hivyo katika siku hizi za mwisho bibi-arusi safi wa Kristo hatakusanyika katika madhehebu na dini bali atakusanyika katika NENO LA MUNGU tu..yeye hatafungwa na dini bali atafungwa, ‘’na nini NENO linasema’’ Hicho tu. Hii ndio ndio nguvu Mungu aliyoiachia sasa hivi kwa bibi-arusi wake, kurudi katika imani ya Mitume, Biblia.

Hivyo ndugu jitathimini je! na wewe umefungwa kama magugu kwenye matita tayari kwa kuchomwa au unakusanywa ghalani mwa Mungu kwa NENO lake?. Kama umefungwa huko toka, sio kwa miguu bali kwa kugeuzwa moyo wako na kuligeukia NENO linachosema na sio mapokeo ya dhehebu. Kwasababu biblia inatuambia 

1Petro 1:23 “Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; KWA NENO LA MUNGU LENYE UZIMA, lidumulo hata milele.”

Hivyo Umeona hapo? Bibi-arusi amezaliwa kwa mbegu isiyoharibika KWA NENO LA MUNGU tu, na sio kitu kingine.

Ni maombi yangu kuwa utazaliwa mara ya pili kwa NENO LA MUNGU na kumtazama Kristo peke yake aliyekufia msalabani ili ufanyike kuwa ngano na sio gugu.

Print this post

MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI.HATA UASHERATI NAO

“Moto hufa kwa kukosa kuni’’, na ndivyo ilivyo kwa uasherati


Mungu kamuumba kila mwanadamu na maamuzi yake binafsi yasiyoweza kuingiliwa na kitu kingine chochote, Mungu kayaheshimu maamuzi hayo kiasi kwamba hata yeye mwenyewe hajajipa mamlaka ya kuyaingilia japokuwa anao uwezo huo, si zaidi shetani? hawezi kumwamulia mtu mambo!!. Ukiamua kuwa mlevi hakuna kitu chochote kitakachoweza kukuzuia, ukiamua kuwa mchawi hakuna yeyote atakayeweza kukuzuia..Vivyo hivyo ukiamua kuwa mtakatifu hakuna chochote kitakachoweza kukuzuia.

Jambo analolifanya Roho Mtakatifu ni kumshawishi au kumpa mtu kila sababu ya yeye kutokufanya maamuzi ya jambo fulani ovu, na mtu anapoamua kutii ndipo Roho anapozidi kuwa msaada mkubwa kwake katika kuenenda katika mwenendo mtakatifu.

Vivyo hivyo na shetani naye anachofanya sio kumlazimisha mtu kufanya maamuzi fulani bali anamshawishi kwa kumjengea mazingira yote ya yeye kuchukua uamuzi wa kufanya uovu, na mtu anapomtii ndipo shetani anapapata nafasi zaidi ya kummiliki na kumuharibu. Mwisho wa siku unasikia mtu ana pepo la usherati, halikumwingia hivi hivi ni yeye mwenyewe alifungua mlango mahali fulani na kuliruhusu.

Mtu anaamua kuwa mzinzi mara baada tu ya kuyatii mahubiri ya shetani katika akili yake. Fahamu tu biblia inasema

 1Wakoritho 6: 18 “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.” 

Na pia inasema.. Mithali 6:32 “Mtu aziniye na mwanamke HANA AKILI KABISA; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.” . Unaona hapo?? mwasherati wa aina yoyote ile yupo katika HATARI kubwa sana kuliko mtu mwingine yeyote.

Kwanini wengi leo wanashindwa na dhambi ya uasherati?

Ni Kwasababu ile ile, wanachukuliana na mahubiri ya shetani katika maisha yao. na kuyatii. Na Mahubiri hayo ni yapi?.

1)Kutazama Picha na Video za kizinzi (Pornography).

Hii ni nyenzo kubwa sana shetani ameitumia kwa kizazi hiki kukiangamiza, Hii ni njia yenye ushawishi mkubwa kuliko zote, kiasi kwamba mtu akijiingiza huko uasherati hawezi akaukwepa kwa namna yoyote iwe ni ameshaingia kwenye ndoa au hajaingia, iwe ni kijana, au mzee haikwepeki, mtu huyo atabakia kuwa mwasherati au mzinzi daima. Na hapo shetani hajahusika kukufanya ukafanye uasherati hapana ni wewe mwenyewe kwa ufahamu wako kabisa na kwa miguu yako umeamua kuwa hivyo. Kama ingekuwa ni shetani kakuvaa ufanye hivyo, siku ile ya hukumu Mungu asingekuhukumu wewe angemuhukumu shetani.Lakini biblia inasema waasherati watahukumiwa… Na mtu anayetazama hivi vitu kama hatadondokea kwenye uasherati moja kwa moja basi ataishia kwenye masturbation ambayo nayo ni machukizo makubwa sana mbele za Mungu.

2) Njia ya pili ni ‘Mazungumzo mabaya’; 

Biblia inasema 1Wakoritho 15: 33 Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema . “ Haya ni mahubiri ambayo utakuta shetani anamuhubiria mtu pasipo hata yeye mwenyewe kujua, utakuta vijana au wazee kutwa kuchwa wanazungumza habari za wanawake, na wanawake vivyo hivyo utawakuta wana jadili habari za wanaume muda wote, lakini muda wa kutafakari mambo ya muhimu ya Mungu hakuna, sasa hapo watu kama hao ni rahisi sana kutawaliwa na roho za tamaa, kwasababu vichwa vyao wakati wote vimejazwa hayo mafundisho ya zinaa. Biblia inasema “hata uasherati usitamkwe kati yenu.”Utakuta kijana muda wote anaumalizia mtandaoni..ukitazama ni kitu gani anafanya, utagundua kuwa anachati katika magroup ambayo misingi yake ni uasherati, sasa kwa tabia hiyo haiwezekani wewe kuushinda uasherati hata uombeweje ni wewe tu kuamua kuacha hivyo vitu na kuanza kutii mahubiri ya Roho Mtakatifu ndani yako.

3) Mavazi: 

Vimini, suruali, kaptura, nguo zinazobana na zinazoonyesha vifua na migongo wazi kwa wanawake n.k., hivi vyote ni vichecheo vya uasherati, mavazi hayo yalibuniwa kwa kazi hizo, kuwavuta wazinzi wasogee karibu na wewe, hivyo mtu anayejiita mkristo na kuanza kuzivaa moja kwa moja anakaribisha uwepo wa uzinzi ndani yake.

4) Mziki na filamu za kidunia:

Kusikiliza miziki ya kidunia hii pamoja na filamu za kimapenzi ni kichecheo kikubwa cha kubebwa na roho hizi, asilimia 99 ya miziki yote ya kidunia zina mahudhui ya kiasherati ndani yake unategemea vipi uepukane na tabia hizo?. Na ndio maana utakuta mtu analalamika hawezi kuacha kuwa mzinzi/mwasherati wakati muda wote anaumalizia kwenye vitabu, filamu na tamthilia za kimapenzi. Viache hivi vitu kwanza na ndipo utakapoanza kuona wepesi.

Na mambo hayo yakishakaa ndani yako sana, sasa yanakuwa yakijirudia rudia yenyewe tu kwenye akili yako, mpaka inakuwa ngumu kuyakwepa kwasababu ndio yaliyoujaza moyo wako,

Hivyo ndugu ukitaka kuushinda uasherati usitafute kuombewa, dawa ipo ndani yako mwenyewe kwanza ni kuchukua uamuzi wa kukataa kutii mahubiri yote ya shetani, na kuanza kumtii Roho Mtakatifu anapougua ndani ya moyo wako, ukifahamu kuwa mtu atendaye mambo hayo mwisho wake ni kuzimu… kwa kufanya hivyo utampa Roho Wa Mungu nafasi ya kukutengeneza up mpaka mwisho wa siku unajikuta ile tamaa imezikwa kabisa, na kuweza kuishi maisha pasipo kutamani uasherati kabisa..Hivyo kataa hayo mahubiri yote ya shetani anayokuletea kupitia mtandao,(Pornography) na picha za uchafu, kwa kupitia kuchat katika mambo yasiyofaa, kwa kupitia mazungumzo mabovu, na kampani zisizo za ki-Mungu, kwa kupitia filamu, vitabu, tamthilia na miziki ya kidunia pamoja na mavazi ya kikahaba, Anza kukaa mbali kwanza na hivyo vitu vyote, na ndipo utakapoanza kuitawala mapenzi yako

Na pia mawazo machafu yanapokujia kichwani kwako ni kuyakataa kwa kutafakari NENO LA MUNGU badala yake, ukizingatia hayo kidogo kidogo Roho Mtakatifu anaanza kuyazika ndani yako, mpaka kufikia hatua ya kutoweka kabisa na kuwa na uwezo wa kujitawala. Kwasababu biblia inasema

(Mithali 26: 20a, “MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI”)….Hivyo uasherati pia hufa kwa kukosa vichochezi. Unapojitenga na vichocheo vyote hivyo hata ile tamaa ya kufanya uasherati inakuwa haipo. Roho Mtakatifu anaizika mpaka inafikia hatua watu watakushangaa unawezaje kuishi muda wote huo pasipo kuwa mwasherati?.

Lakini kama hutaki kuweka chini hivyo vitendea kazi vya uasherati kamwe hutaweza kumshinda shetani.Kwasababu biblia pia inasema WAASHERATI WOTE sehemu yao ni katika lile ziwa la Moto(Ufunuo 21:8)..Hivyo ndugu iogope hukumu ya Mungu, anza kubadilika sasa kimbia uasherati. Mwili wako ni Hekalu la Roho Mtakatifu, na mtu auharibuye Mungu kasema atamuharibu mtu huyo.

Print this post

HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?


Kitabu cha Ayubu sura ya 28, kinaeleza jinsi HEKIMA ilivyojificha mbali sana kiasi kwamba mwanadamu pamoja na ujuzi wake mwingi na maarifa yake mengi hajaipata, licha ya kwamba amefanikiwa kuchimba mahandaki makubwa ili kutafuta madini ndani yake lakini pia hajaipata, licha ya kwamba anayo teknolojia kubwa ya kuwa na vyombo maalumu vya kumfanya kutua mwezini, lakini alipofika na huko hakuikuta vile vile, biblia inasema wanyama nao hawajui inapatikana wapi, kadhalika na vitu vya asili kama bahari na milima havitambui ilipo,

AYUBU sura ya 28

Mstari wa 1-15

“1 Hakika kuna shimo wachimbako fedha, Na mahali wapatapo dhahabu waisafishayo.

2 Chuma hufukuliwa katika ardhi, Na shaba huyeyushwa katika mawe.

3 Binadamu hukomesha giza; Huyatafuta-tafuta hata mpaka ulio mbali, Mawe ya giza kuu, giza tupu.

4 Hufukua shimo mbali na makao ya watu; Husahauliwa na nyayo zipitazo; Huning’inia mbali na watu, huyumba-yumba huko na huko.

5 Katika ardhi ndimo kitokeamo chakula; Na chini yake hupinduliwa kama kwa moto. 

6 Mawe yake ni mahali zipatikanapo yakuti; Nayo ina mchanga wa dhahabu.

7 Njia ile hapana ndege mkali aijuaye, Wala jicho la tai halijaiona;

8 Wanyama wakali wajivunao hawajaikanyaga, Wala simba mkali hajaipita.

9 Huunyoshea mwamba wa gumegume mkono wake; Huipindua milima hata misingi yake.

10 Hukata mifereji kati ya majabali; Na jicho lake huona kila kito cha thamani

11 Hufunga vijito visichuruzike; Na kitu kilichostirika hukifunua.

12 BALI HEKIMA ITAPATIKANA WAPI? NA MAHALI PA UFAHAMU NI WAPI?

13 MWANADAMU HAJUI THAMANI YAKE, WALA HAIONEKANI KATIKA NCHI YA WALIO.

14 Vilindi vyasema, Haimo ndani yangu; Na bahari yasema, Haiko kwangu.

15 HAIPATIKANI KWA DHAHABU, WALA FEDHA HAITAPIMWA IWE THAMANI YAKE.”

BASI HEKIMA YATOKA WAPI? NA MAHALI PA UFAHAMU NI WAPI?.  21 Kwa kuwa imefichwa mbali na macho ya wote walio hai, Na kusitirika na ndege wa angani.

Biblia inaendelea kueleza kama Hekima ingekuwa inapatikana kwa thamani ya dhahabu au fedha basi ingeshapatikana na watu siku nyingi, au ingekuwa inapatikana kwenye vilindi au baharini ingekuwa ni heri, lakini huko kote mwanadamu ameshafika na hakuikuta. Lakini je! Inapatikana wapi?.

Biblia inaendelea…

“16 Haiwezi kutiwa thamani kwa dhahabu ya Ofiri, Wala kwa shohamu ya thamani nyingi, wala kwa yakuti ya samawi.

17 Dhahabu na vioo haviwezi kulinganishwa nayo; Wala kubadili kwake hakutakuwa kwa vyombo vya dhahabu safi.

18 Havitatajwa fedhaluka wala bilauri; Naam, kima cha hekima chapita marijani.

19 Yakuti ya rangi ya manjano ya Kushi haitasawazishwa nayo, Wala haitatiwa kima kwa dhahabu safi.

20 BASI HEKIMA YATOKA WAPI? NA MAHALI PA UFAHAMU NI WAPI?.

21 Kwa kuwa imefichwa mbali na macho ya wote walio hai, Na kusitirika na ndege wa angani.

22 Uharibifu na Mauti husema, Tumesikia habari zake kwa masikio yetu.

23 Mungu ndiye aijuaye njia yake, Naye anajua mahali pake.”

Viumbe vyote vya asili na visivyo vya asili na vyenyewe pia vinasema havijui makao yake, Ni Mungu pekee ndiye anayejua makao yake. Na tunasoma baada ya wote kushindwa kufikia makao ya HEKIMA na UFAHAMU, Ndipo Mungu naye akaazimu kuingilia kati na kuchunguza makao yao yako wapi?.. Naye pia kama mwanadamu aliingia katika uchunguzi wa kina na utafiti wa hali ya juu, akapanda milimani, akashuka vilindini, akashuka zaidi mpaka kuzimu, akarudi kwenye mbingu, akapitia sayari zote akazunguka kote kote kila mahali, akaingia mpaka kwenye mioyo ya wanadamu kuitafuta hekima, hakuna mahali ambapo hakufika. Ndipo mwishoni akaipata, na alipoipata akaihakiki na kuithibitisha, na ndipo akaja KUWAAMBIA WANADAMU.

Mstari wa 24-28 inaendelea kusema..

“24 Maana anatazama hata miisho ya nchi, Na kuona chini ya mbingu nzima.

25 Apate kuufanyia upepo uzito wake; Naam, anayapima maji kwa kipimo.

26 Hapo alipoiwekea mvua amri, Na njia kwa umeme wa radi.

27 Ndipo alipoiona na kuitangaza; Aliithibitisha, naam, na kuichunguza.

28 Kisha akamwambia mwanadamu, TAZAMA, KUMCHA BWANA NDIYO HEKIMA, NA KUJITENGA NA UOVU NDIO UFAHAMU.”

Maneno hayo ndiyo aliyomalizia Bwana, baada ya utafiti na uchunguzi wa hali ya juu, Na sisi tunajua hakuna mwanadamu mwenye Akili zaidi ya Mungu, Utafiti wa Mungu ni bora mara nyingi zaidi kuliko utafiti wa wanasayansi au wanajimu, na wanafalsafa. Kama wanasema HEKIMA ni kusoma sana, au kuwa na akili nyingi za kimasomo au ujasiriamali, au kuwa tajiri sana, kama wao wanasema hekima ni kuwa maarufu, kama wao wanasema ufahamu ni kuwa na ujuzi wa kufanya jambo fulani, lakini sisi tunajua Bwana katuonyesha HEKIMA ni nini, na ufahamu unapatikana wapi?.. NI KUMCHA YEYE, NA KUEPUKANA NA UOVU. Hilo tu.! Tukizingatia hayo mbele za Mungu tutakuwa ni watu wenye hekima sana na Ufahamu mkubwa.

Sulemani ingawa alikuwa ni mtu mwenye maarifa mengi na ufahari mkubwa ambao hakuna mtu aliyekuwa mfano wake, tangu wakati ule hata sasa, Ni mtu aliyekuwa na elimu pamoja na ujuzi wa viumbe vyote, ikiwepo miti, samaki, wanyama, alikuwa na ujuzi wa hali ya juu kiasi cha kutunga nyimbo na mashairi kwa hekima nyingi sana, alikuwa na uwezo wa kutenganisha hukumu ambapo vitu kama hivyo vilihitaji watu wenye akili nyingi kama mahakimu. Ilifika wakati yeye mwenyewe alikiri kuwa hakukosa lolote, wala hakujinyima nafsi yake kwa chochote. Lakini pamoja ya kwamba aliipata hekima yote ya kidunia, aliisahau HEKIMA MOJA YA MUNGU.

Kwa Kupuuzia amri za Mungu, na kuanza kwenda kuoa wake wageni, na kuabudu miungu migeni, akalitangua lile NENO walilopewa wafalme kwa amri ya Musa kwamba mtu yeyote atakayekuja kuwa mfalme kati yao, asijiongezee wake, wala mali kupita kiasi, wala asiabudu miungu mingine, zaidi ya yote anapaswa aandike amri za Mungu katika chuo ajifunze huko siku zote za maisha yake namna ya kumcha Mungu katika ufalme wake.(Kumbukumbu 17:14-20). Lakini yeye hakufanya hivyo akakaidi. 

Na alipogundua makosa yake kuwa aliiacha hekima hasaa inayopatikana katika kumcha Mungu, akaishia kusema UBATILI MTUPU, KILA KITU NI UBATILI.!

Sulemani alisema katika..

 Mhubiri 2: 10 “Wala sikuyanyima macho yangu cho chote yalichokitamani; wala sikuuzuia moyo wangu katika furaha yo yote; maana moyo wangu ulifurahi kwa sababu ya kazi yangu yote, na hii ilikuwa sehemu yangu katika kazi yangu yote.

11 Kisha nikaziangalia kazi zote zilizofanywa kwa mikono yangu, na taabu yote niliyotaabika katika kuzitenda; na tazama, YOTE NI UBATILI na kujilisha upepo, wala faida hakuna chini ya jua.”

Na mwisho wa siku Sulemani alimalizia na kusema….”

Mhubiri 12:13-14

“13 HII NDIYO JUMLA YA MANENO; yote yamekwisha sikiwa; MCHE MUNGU, NAWE UZISHIKE AMRI ZAKE, MAANA KWA JUMLA NDIYO IMPASAYO MTU.

14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.”

Hivyo ndugu, kweli zipo hekima nyingi duniani na sio kwamba ni mbaya ni nzuri na nyingine zinahitajika sana katika jamii zetu lakini usisahau, Mungu mbele zake HEKIMA NI MOJA TU!. Anayoitambua yeye, nayo ni KUMCHA BWANA , NA KUEPUKANA NA UOVU. Ni heri ukakosa hizo nyingine lakini usiikose hiyo. Ichukie dhambi mpe Bwana maisha yako, mche yeye, Elimu yako, ujuzi wako, mali zako ni vizuri kuwa nazo lakini zisije zikakufikisha mahali ukasema ni ubatili mtupu kama alivyofanya Sulemani, kwa jambo moja tu, ya kupuuzia amri za Mungu sasa. Kwasababu Bwana alishasema mwenyewe..Hekima ya ulimwengu huu ni upuuzi mbele zake (1Wakoritho 3:19). Hivyo kuwa makini unavyoenenda katika ulimwengu huu. Kumbuka YESU KRISTO ndiye HEKIMA YA MUNGU.(1wakoritho 2:6-9)

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

MUNGU AKIKUPITA LEO, HAIMAANISHI KUWA HAJAKUCHAGUA.

HUDUMA YA (ELIFAZI, BILDADI, NA SOFARI).

CHUKIZO LA UHARIBIFU

TOA SADAKA ISIYO NA KASORO KWA BWANA.

https://wingulamashahidi.org/2020/01/25/kwanini-mungu-alimtumia-musa-kwa-viwango-vile/


Rudi Nyumbani

Print this post