Category Archive Home

USIACHE KUJIFUNZA NENO LA MUNGU

Neno la Mungu limefananishwa na MBEGU (Luka 8:11), na siku zote mbegu ina uhai na inapopandwa ndani ya mtu, ule uhai wake unajidhihirisha ndani ya mtu huyo kulingana na umeaji wa mbegu hiyo. Hivyo kwa jinsi ile mbegu inavyoendelea kukua ndipo tabia ya Yule mtu inavyoendelea kubadilika kidogo kidogo. Kumbuka hapo sio mtu anajibadilisha kwa jitihada zake hapana bali ni ile mbegu iliyopandwa ndani yake ndiyo inayombadilisha kutoka hatua moja hadi nyingine kulingana na ukuaje wake.

Bwana Yesu alitoa mfano huu.

Marko 4: 26 “Akasema, Ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga mbegu juu ya nchi;

27 akawa akilala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu ikamea na kukua, ASIVYOJUA YEYE.28 Maana nchi huzaa yenyewe; KWANZA JANI, tena SUKE, kisha NGANO PEVU, katika suke.

29 Hata MATUNDA yakiiva, mara atapeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika”.

Huu mfano unalinganishwa na jinsi Neno la Mungu linavyomea ndani ya mtu, kwanza linaanza kama mbegu, pale mtu anapoliruhusu lile Neno liingie ndani yake, hii inakuja kwa kutamani kujifunza kila siku Neno lile,kwa kutamani kumjua Mungu, na kujifunza maandiko, sasa kidogo kidogo, kwasababu ile mbegu imetengenezewa mazingira yanayostahili kumea yenyewe inaanza kukua taratibu taratibu pasipo hata yeye mwenye kuipanda kujijua ndio hapo unakuta mtu Yule anaanza kubadilika tabia zake na mwenendo wake, anaanza kujikuta anachukia mambo ya kidunia ambapo hapo mwanzo alikuwa hawezi, na hii haiji kwa jitihada za mtu hapana yeye mwenyewe tu anajikuta anapoteza hamu ya kufanya hivyo vitu, hapa mtu anajikuta vitu kama kiu ya sigara, pombe, uasherati, mavazi yasiyo na heshima n.k. vinakata vyenyewe, ataona tu ni kama vile kwa akili zake ameacha hayo mambo lakini hajui kuwa ni ile mbegu ambayo amekuwa akiiruhusu imee ndani yake ndiyo iliyotenda kazi ndani yake

Na kwa jinsi atakavyoendelea kuiwekea mazingira mazuri zaidi ya kukua, kwa kujifunza na kutamani kudumu zaidi katika Neno la Mungu sasa ile mbegu inageuka na kuwa JANI, hapa ni pale mtu ufahamu wake wa kumjua Mungu unaongezeka na kuwa mpana pasipo hata yeye mwenyewe kujijua kumbuka hii mbegu inachohitaji ni kuwekewa mazingira tu ya kutuzwa, kuhusu ukuaji huwa inajikuza yenyewe. Hatua hii inamfanya mtu ufahamu wake wa rohoni kuongezeka, yale mambo ambayo alikuwa hayaelewi kuhusu maandiko anaanza kuyaelewa taratibu taratibu.

Hatua inayofuata ni SUKE. Hatua hii mtu anakuwa anatoka katika ile hali ya “unyasi unaotikiswa na upepo”.

Waefeso 4: 14 “ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.

15 Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo”.

Hapa unakuwa umekomaa kutoka katika jani na kuwa suke gumu, hatua hii shetani hawezi kukuchukua tena na kila wimbi la mafundisho ya uongo kwa sababu Neno la Mungu limeshaweka mizizi migumu ndani yako. Unafika hatua ya kuwa na ujuzi wa kuitofautisha Kweli ya Neno na Uongo, kwasababu yale mafuta ya Roho yanakaa ndani yako. Mpaka hapo mtu anakuwa tayari kwa hatua inayofuata ya kuzaa matunda.

NGANO PEVU: Hii ni hatua ya kudhihirisha matunda, Hapa inatokea lile Neno lilipandwa ndani yako lenyewe linakupa uwezo wa kwenda kulipanda kwa watu wengine..na kuzaa matunda, Hapa ndipo Mungu kwa maarifa aliyoyaweka ndani ya mtu, anampa neema na uwezo wa kwenda kuwafundisha na wengine, na hii nguvu ya kufanya hivyo haiji kwa jitihada za mtu binafsi au kujilazimisha hapana bali mtu anajikuta anatamani mwenyewe kufanya hivyo kutoka ndani kwasababu ile nguvu za kuzaa matunda imeshajitengeneza ndani yake..,Ni kama tu vile mwanamke anapofikia wakati wa kuzaa, ule uchungu unapokuja hawezi kujizuia, vivyo hivyo na mtu akishafikia hatua hii, anajikuta mwenyewe anaanza kumzalia Mungu matunda.

Na hatua ya mwisho ni Mavuno: Hapa ndipo kazi ya kila mtu itavunwa na Bwana mwenyewe, na hii itakuja katika mwisho wa dunia.

Hivyo ndugu je! Ni mbegu gani imepandwa ndani yako?, Ni ya Neno la Mungu au ni ya Yule mwovu.?..Na kama ni ya Neno la Mungu, je! Mbegu hiyo imekuwa kwako katika hatua gani, ni jani?, ni suke au ni ngano?. Kama huna uwezo wa kushinda ulevi, uasherati, sigara, uzinzi, usengenyaji basi ujue ile mbegu imekufa ndani yako.. Kwasababu uliposikia Neno la Mungu hukutaka kuliwekea mazingira mazuri ya kukua lenyewe. Kumbuka mkristo yoyote anayezingatia kulitunza na kujifunza Neno la Mungu kila siku katika maisha yake, hatapata shida kuishida dhambi. Kwasababu Biblia inasema..

1Yohana 3: 9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao [MBEGU]wake wakaa ndani yake ; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.

Ni maombi yangu sisi sote tujue nguvu ya Neno la Mungu, tukijua kuwa tukilipinga Neno la Mungu ndani yetu ni kujitenga na uzima wetu wenyewe. Hivyo nakutia moyo ndugu usomaye haya usichoke kujifunza Neno la Mungu kila iitwapo leo, jifunze Biblia. Kwasababu hujui wewe lile Neno linatendaje kazi ndani yako. Wewe jifunze na kulitii tu, hata kama hutaona leo mabadiliko lakini fahamu tu, linakuwa kwa njia usioijua wewe, wakati Fulani ukipita ukiendelea hivyo utaona tofauti ya leo yako na jana yako ilivyokuwa.

Mungu akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Print this post

KAMA UNAPENDA MAISHA, NA KUTAKA SIKU YAKO IWE NJEMA.

Biblia inasema maisha yetu yamefananishwa na chombo chochote kinachoendeshwa chenye usukani, mfano wa vyombo hivi vinaweza vikawa ni: Gari, au Meli, au ndege, n.k. vyote hivi pamoja na kwamba vina uwezo mkubwa na nguvu nyingi ya utendaji kazi, lakini haviwezi kujiongoza vyenyewe pasipo USUKANI. Upepo unaweza ukawa mkubwa sana baharini na usifanikiwe kukipeleka chombo mahali kinapotakiwa kufika lakini usukani ni kitu kidogo chenye nguvu chache tu na kikafanikiwa kupindisha merikebu yote na kuielekeza inapotakiwa iende.

Kadhalika na maisha yetu ya Kikristo yanayo usukani wake, Na usukani huo ni nini? Tukisoma biblia tutapata majibu yote:

Yakobo 3: 2-12, Biblia inasema..

“Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.

3 Angalieni, twatia lijamu katika vinywa vya farasi, ili wamtii, hivi twageuza mwili wao wote.

4 Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote anakoazimia kwenda nahodha.

5 Vivyo hivyo ULIMI nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.

6 NAO ULIMI NI MOTO; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum.

7 Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu.

8 Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.

9 Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.

10 Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.

11 Je! Chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu?

12 Ndugu zangu, Je! Mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Kadhalika chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na maji matamu “.

Maandiko hayo yanaonyesha wazi kabisa kuwa usukani wa maisha yetu ni ULIMI. Na ulimi kama usukani ni wa kuuchunga sana kuliko vyote kwasababu Shetani akipata tu nafasi ya kuushika huo ataleta maangamizi makubwa kuliko hata angetumia njia nyingine za nje za dhoruba na tufani (ambayo ni majaribu).

Biblia inatuonya mtu anaweza akawa umezingatia kweli kuwa na Dini nzuri, kama kusaidia wajane, kutembelea yatima, kuvaa vizuri, kuzingatia ibada, kutoa sadaka, kufundisha watu,n.k (Yakobo 1:27). lakini kama hakuweza kuungoza usukani wake (Ulimi) basi dini yake yote na matendo yake mema mtu huyo yote yanakuwa ni sawa na bure. Soma.

Yakobo 1: 26 “ Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai. ”

Wewe ni mkristo lakini unakuwa mtu wa kusengenya, kila wakati kuzungumzia watu wengine kwa ubaya, kuchukua taarifa za mtu fulani kupeleka kwa mtu fulani, kutoa siri za mtu fulani na kumfunulia mwingine..Kila wakati unakuwa unatoa maneno yasiyokuwa na maana mdomoni, unatoa maneno ya mizaha ambayo ni aibu hata kwa mkristo kutamka, unatoa maneno ya uchochezi na fitna, unatamka matusi hata haionekani tofauti yako na mtu asiyeamini, kila wakati kuchangia mada zisizokuwa na maana, Sasa hapo hata kama unafanya ibada nzuri kiasi gani mbele za Mungu, au unahubiri kiasi gani, au unasaidia maskini kiasi gani, Dini yako ni bure mbele za Mungu..Ni kwasababu gani?..ni kwasababu Umeshindwa kuutawala usukani wa maisha yako ya kikristo, na umempa mwingine autawale naye ni shetani.

Wakati mwingine ajali nyingi zinazotokea huwa hazisababishwi na mazingira ya nje hapana!, unakuta nyingi zinasababishwa na matatizo ya kiuendeshaji (usukani) . Utakuta chombo ni kizuri tu, hakina matatizo yoyote, ni kipya, na kina uwezo mkubwa wa kupambana na mazingira mabaya ya nje, lakini kwa jambo dogo tu la uzembe katika uendeshaji inapelekea chombo kile kizima kupata ajali. Na ndicho hicho shetani anachokitafuta kwa wakristo, kukimbilia usukuni wa maisha yao (ULIMI) na akiupata huo kammaliza mtu huyo moja kwa moja.

Ndio hapo unajiuliza mbona najitahidi kusali, wakati mwingine kufunga, kutoa sadaka, kusaidia watu, kuhudhuria ibada, lakini siku yangu inakuwa mbaya, mbaya, sina amani na watu, sioni raha ya maisha, ni kwasababu kuna eneo moja la muhimu umemwachia shetani alitawale, usukani wako (Ulimi wako), shetani anapeleka maisha yako uliyoyajenga ya kikristo mahali anapotaka yeye,…Na ndio maana biblia inasema:

1Petro 3: 10 “Kwa maana, ATAKAYE KUPENDA MAISHA, NA KUONA SIKU NJEMA, AUZUIE ULIMI WAKE USINENE MABAYA, NA MIDOMO YAKE ISISEME HILA.

11 Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana.

12 Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya”.

Unaona hapo?. Shetani anaamka asubuhi kuziloga siku zako kwa kutumia ulimi wako mwenyewe, Mungu amekusudia kukumulikia jua lake la mema lakini anapokuja na kukukuta unamzungumzia ndugu yako vibaya, unamsengenya, anapokuja anakukuta unazungumza maneno ya mizaha, kinywa chako kinaimba nyimbo za kidunia, una laani watu, unawalaumu watu kila wakati,ukikwazwa kidogo tu basi unatoa maneno mengi na yasiyolingana na wokovu, basi na zile Baraka zako zinatoweka, mwisho wa siku, unajikuta mambo yako hayaendi sawa.

Mithali 10: 19 “Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili”.

Na pia inasema..

Mithali 21: 23 “ Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, Atajilinda nafsi yake na taabu. ”

Na njia pekee ya kuulinda ulimi wako haiji kwa kufunga na kuomba au kwa kuombewa na mtumishi, hapana! inakuja kwa kujizoesha maisha kuwa mbali na hayo mambo, unapoona kuna mazingira yoyote yanayokushawishi wewe kuzungumza maneno yasiyofaa au habari za mtu mwingine, suluhisho pekee ni kuyakataa hayo mazingira, ikiwa ni mtu anakuletea, habari hizo wewe zigeuze kumzungumzia kwa wema Yule mtu,..Ukiletewa mabaya ya mtu Fulani, wewe likumbuke lile moja jema ambalo mtu huyo alishawahi kulitenda na kulizungumzia hilo na yale tisini na tisa mabaya aliyoyatenda yapuuzie..Kwa kufanya hivyo utajikuta unabariki badala ya kulaani, unasifia badala ya kulaumu, unampenda badala ya kumchukia, unamfaurahia badala ya kumwonea wivu. Na ule uovu wote shetani alioupanga juu ya siku yako na maisha yako unayeyuka, Na kwa kufanya hivyo Mungu atakuona na kukuangazia siku zako na kuwa njema kwasababu umeweza kuutawala usukani wako.

Mithali 26: 20 “ Moto hufa kwa kukosa kuni; Na bila mchongezi fitina hukoma. ”..

Hivyo ndugu, huu ni wakati wa kuizoeza chemchemi yako kutoka maji matamu na sio machungu, kutoka Baraka na sio laana kwa faida zetu wenyewe, kwasababu kipimo kile kile tunachowapimia wengine biblia inasema ndio hicho hicho tutakachopimiwa. Baraka zile zile tutakazowabariki wengine ndio hizo hizo tutakazobarikiwa..kadhalika na laani zile zile tutakazowapimia wengine ndizo hizo hizo tukazopimiwa.

Mithali 18: 21 “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake. “

Swali ni je! Unapenda maisha na kuiona siku njema?? Kama ni ndio basi UZUIE ULIMI WAKO USISEME MABAYA …Na Bwana atakusaidia.

Zaburi 141: 3 Ee Bwana, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.

Bwana Yesu akubariki sana.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Print this post

CHANGIA SASA.

Asante kwa kutembelea Tovuti yetu, Maono yetu makuu ni kuisambaza injili ya Bwana wetu Yesu Kristo ili wokovu uwafikie watu wote ulimwenguni kote, sambamba na hilo tumelenga kutoa maarifa ya Neno la Mungu, kufuatana na mada mbalimbali katika  biblia.

Kwa mchango wako, utawezesha kazi hii ya Bwana kuendelea mbele, na tunachoamini ni kuwa mmoja hupanda mwingine hutia maji, lakini mkuzaji ni Mungu. Hivyo kwa matunda yazaliwayo kwa kupitia huduma hii, thawabu yetu ni moja mbinguni.

Waweza changia kupitia namba hizi:

  • AIRTEL-MONEY:  +255 789 001 312 
  • JINA:                    DEVIS MAGEMBE.

Au

  • M-PESA:         +255 767 992 434       
  • JINA:             DENIS MAGEMBE.

Bwana akubariki.

baruapepe(email) >> Info@wingulamashahidi.org

Shalom!

Print this post

KIMBIA! KIMBIA! KIMBIA!

Makanisa yanayohubiri injili ya mafanikio tu. Na kukwambia kuwa uthibitisho wa Mungu kuwa yupo na wewe, ni kuwa tajiri ...JIHADHARI NA HILO KANISA!

Makanisa yasiyohubiri toba ya msamaha na kuwafanya watu wajione ni kawaida kuishi na dhambi zao…JIHADHARI NA HILO KANISA!..Toba na msamaha ndio kiini cha Imani.

Makanisa yanayochanganya NENO la Mungu na siasa na vikundi vya kijamii, jambo ambalo huwezi kutofautisha jukwaa la siasa na kanisa, na makanisa yanayochanganya Neno la Mungu na mapokeo ya wanadamu….JIHADHARI SANA!

Makanisa yasiyohubiri utakatifu na kufundisha watu ukweli kulingana na Biblia…KUWA MWANGALIFU NA HILO KANISA..

Makanisa yanayohubiri ujumbe wa kutoa tu, na kuacha mafundisho ya adili kama upendo, utakatifu na imani,,,,JIHADHARI NA HILO KANISA KWA USALAMA WA MAISHA YAKO YA MILELE.

Kanisa lisilokufundisha wala kugusia kujiandaa kwenda katika unyakuo…KUWA MAKINI!

Kanisa lisiloruhusu karama za Roho kufanya kazi, kama uponyaji wa kiungu, unabii, lugha, miujiza n.k. jua hilo kanisa limekufa au lipo karibuni kufa. JIHADHARI NDUGU!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada zinazoendana:


Mada Nyinginezo:

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

USIACHE KUJIFUNZA NENO LA MUNGU

KWANINI MUNGU ANAMPA NABII HOSEA MAAGIZO YA KUMUOA MWANAMKE KAHABA? (HOSEA 3)

KUTOKA 10:1 “BWANA ANASEMA ATAMPA FARAO MOYO MGUMU, ASIMTII, JE! HAPO BWANA ATAMHUKUMU FARAO KAMA MKOSAJI SIKU ILE?”


Rudi Nyumbani

Print this post

NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.

NYAKATI SABA ZA KANISA.

Tangu kipindi cha Bwana Wetu Yesu Kristo kuondoka duniani mpaka sasa imepita miaka takribani elfu mbili na katika hichi kipindi cha miaka hii elfu mbili kanisa limekuwa likipitia katika vipindi tofauti tofauti saba vinavyoitwa NYAKATI SABA ZA KANISA, kulingana na kitabu cha..

Ufunuo 1:12-20″ Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu;

13 na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.

14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto;

15 na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.

16 Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking’aa kwa nguvu zake.

17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,

18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.

19 Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.

20 Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.

Amen.

Ufunuo huu alipewa Yohana na Bwana Yesu alipokuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, akionyeshwa jinsi kanisa litakavyokuja kupitia katika siku za mwisho. Leo hii si rahisi sana kuona kitabu cha ufunuo kikiguswa au kuelezewa katika kanisa, na shetani hataki watu wafahamu siri zilizoandikwa katika hiki kitabu maana ndio kinaelezea hatma ya mambo yote ikiwemo na shetani mwenyewe. Kwahiyo ndugu fungua moyo wako ujifunze na Mungu akusaidie unapoenda kusoma ujue ni wakati gani tunaishi na jinsi Bwana Yesu alivyo mlangoni  kurudi kuliko hata unavyoweza kufikiri.

Tafadhali pitia taratibu mpaka mwisho ili uelewe.

  • vile vinara saba vinavyozungumziwa ni makanisa saba tofauti tofauti ambayo yamepita tangu wakati wa Bwana Yesu alipokuwa hapa duniani hadi wakati tunaoishi sasa.

NYAKATI YA KWANZA:

Kanisa: Efeso

kipindi cha kanisa: 53AD -170AD

Tabia ya kanisa: limeacha upendo wake wa kwanza,tangu wakati wa mauaji ya wakristo yaliyoongozwa na Nero mtawala wa Rumi hadi kifo cha mtume Yohana. Na kipindi hiki ndipo matendo ya wanikolai yalianza kuingia katika kanisa (mafundisho ya kipagani). kuanza kujichanga na ukristo. ufunuo 2:1-7

onyo kwa kanisa- litubu lirudi katika upendo wake wa kwanza, lililopoteza.

Thawabu: Yeye ashindaye atapewa kula matunda ya mti wa uzima ulio katika bustani ya Mungu.

NYAKATI YA PILI;

Kanisa; Smirna

kipindi cha kanisa: 170AD -312 AD

Tabia ya kanisa; Ni kanisa lilopitia dhiki nyingi kutoka katika utawala mkali wa Diocletian wa Rumi , watakatifu wengi waliuawa katika hichi kipindi kuliko kipindi chochote katika historia ya kanisa.walichinjwa wengi, na wengine kutupwa kwenye matundu ya simba na wanawake kukatwa matiti na kuachwa mbwa walambe damu zao, na ukatili mwingi sana wakristo walitendewa katika hichi kipindi lakini walistahimili dhiki zote hizi soma kitabu cha (Foxe’s book of Martyr- kwenye archives zetu kinaelezea vizuri mauaji ya wakristo).

Japo wakristo walikuwa maskini sana  Lakini Kristo aliwafariji kuwa wao ni  Matajiri. ufunuo 2:8-11

Thawabu; Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.

NYAKATI YA TATU;

Kanisa ; Pergamo

Kipindi; 312AD -606AD

Tabia ya kanisa; Kanisa laingiliwa na mafundisho ya uongo zaidi, ambayo ndio yale matendo ya wanikolai sasa wakati huu yamegeuka kuwa mafundisho ya kidini. Ukristo ukaoana na upagani ukazaa Kanisa mama mfu Katoliki, katika baraza la Nikea AD 325 siasa na mafundisho ya miungu mitatu,ibada za sanamu na za wafu,sherehe na sikukuu za kipagani, ubatizo wa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, vyeo vya upapa n.k ndipo vilipochipukia. kwa mambo haya basi ikasababisha kanisa kuingia katika kipindi kirefu cha giza (Dark age). Ufunuo 2:12-17

Onyo kwa kanisa: litubu lirudi katika imani iliyoanzishwa na mitume wa Kristo

Thawabu; Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, ila yeye anayelipokea.

NYAKATI YA NNE:

Kanisa; Thiatira

Kipindi; 606AD -1520AD

Tabia ya kanisa; Japo kanisa lilikuwa na juhudi na bidii katika kumtafuta Mungu, lakini bado lilikuwa na mafundisho ya yule mwanamke kahaba Yezebeli yaani mafundisho ya Kanisa Katoliki.

Onyo; Litubu litoke katika mafundisho ya wanikolai. Ufunuo 2:18-29

Thawabu: Yeye ashindaye na kuyatunza matendo yangu hata mwisho nitampa mamlaka juu ya mataifa, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma.

NYAKATI YA TANO:

Kanisa; Sardi

kipindi; 1520AD -1750AD

Tabia; Ni kanisa lililokuwa linarudi katika matengenezo kutoka katika mafundisho ya yule kahaba mkuu kanisa katoliki. lakini lilikuwa bado na Jina lililokufa, wakishikilia baadhi ya mafundisho ya kanisa mama katoliki, huku ndiko chimbuko la walutheri lilipoanzia.Ufunuo 3:1-6

Onyo: litubu, lirejee kwenye mafundisho ya mitume.

Thawabu; Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri Jina lake mbele za baba yangu na mbele ya malaika zake.

NYAKATI YA SITA;

Kanisa;Filadelfia

Kipindi; 1750AD -1906AD

Tabia; Ni kanisa lililosifiwa kwa matendo yake mema, lilifanikiwa kujua na kuyarekebisha mafundisho ya uongo Kristo alisema ”tazama nakupa walio wa sinagogi la shetani wasemao kwamba ni wayahudi nao sio, bali wasema uongo, tazama nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda”.ufunuo 3:7-13

Thawabu;Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu, huo Yesalemu mpya ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe lile jipya.

NYAKATI YA SABA;

Kanisa; Laodikia

Kipindi;1906- Unyakuo

Tabia; Ni kanisa ambalo sio baridi wala moto, bali ni vuguvugu, Kristo anasema ni heri lingekuwa moto au baridi, hii ndiyo hali ya kanisa tunaloishi sasa mimi na wewe, uvuguvugu mbaya umeingia katika kanisa, watu wanajiona kuwa wanamwabudu Mungu katika uzuri wao wa majengo ya kanisa, kwaya.na injili ya mafanikio, wakidhani kuwa hivyo yatosha tu kumjua Mungu kumbe hawajui wameshaingia katika udanganyifu wa shetani pasipo wao kujua,

Watu wanasema kuwa wanampenda Mungu na bado wanapenda mambo ya ulimwengu huu kama fashion za mitindo ya kisasa wanawake kuvalia mavazi ya nusu uchi, michezo, miziki, muvi, ponography, ulevi. anasa,uasherati,na shughuli za ulimwengu huu ambazo zinawasonga wengi hususani kwa kizazi hichi cha ubize, watu wanapata muda wa kufanya kazi sana, lakini muda wa kumtolea Mungu hawana na bado ni wakristo., huu ndio uvuguvugu Kristo anaouzungumzia kwa kanisa letu la Laodikia.Hapa Kristo anasema unajiona kuwa tajiri kumbe ni maskini na mnyonge na uchi na unamashaka na kipofu, jiulize ni hali gani ya kanisa tulilopo sasa. 

Na hakutakuwa na kanisa lingine baada ya hili, na ndio linakaribia kuisha. jiulize umejiwekaje tayari kumpokea Bwana Yesu akirudi mara ya pili?

Onyo; Kristo anasema kanisa liwe na bidii likatubu na kumgeukia Mungu.

Thawabu;Yeye ashindaye nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na baba yangu katika kiti chake cha enzi. ufunuo 3:14-22

Watu wa Mungu hili ndilo kanisa la mwisho tunaloishi hakutakuwa na kanisa lingine baada ya hapa, tunaishi katika wakati ambao Kristo yupo mlangoni kulichukua kanisa lake teule, JIULIZE! UMEKWISHA KUJIWEKA TAYARI KUMLAKI BWANA, TAA YAKO INAWAKA??UMEMPOKEA ROHO MTAKATIFU??YEYE ALIYE NA SIKIO, NA ALISIKIE NENO HILI AMBALO ROHO AYAAMBIA MAKANISA.

Mungu akubariki

MARAN ATHA!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada zinazoendana:


Mada Nyinginezo:

MIHURI SABA

UBATIZO SAHIHI NI UPI?

ROHO SABA ZA MUNGU NI ZIPI? NA JE ZINATOFAUTIANA NA ROHO MTAKATIFU?

HUYU AZAZELI NI NANI TUNAYEMSOMA KATIKA(WALAWI 16:8)?


Rudi Nyumbani

Print this post

ROHO YA MPINGA KRISTO IKITENDA KAZI SIKU HIZI ZA MWISHO

Papa kiongozi wa kanisa katoliki duniani alipokuwa akihutubia mbele ya maelfu ya watu juni 25, 2014 St. Peter’s Square vatican akisema:

  •     katika ukristo hakuna hilo suala kama kumtafuta Kristo peke yako
  •     Mkristo yeyote ni lazima awe mshirika wa kanisa fulani 
  •     papa aliendelea kusema kwamba kuwa na mahusiano binafsi na Kristo, kwa kujaribu kufanya              hivyo ni hatari kubwa na yenye madhara
  •      papa alisema kwa mkristo yeyote jina lake la kwanza liwe la kwake na la pili liwe la kanisa kwa           mfano wewe unaitwa Maiko hivyo wewe utaitwa Maiko Mkatoliki, au Joseph Mlutheri n.k

    Mafundisho haya yanapingana na biblia ni mafundisho ya mpinga kristo,kulingana na ufunuo 17:5..”katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa kwa siri, BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI” katika maandiko mwanamke anawakilisha kanisa,kwa hiyo mwanamke huyu aliyezungumziwa hapa ni kanisa-kahaba,inamaanisha ni kanisa lililochanganya mafundisho ya neno la Mungu na ibada za sanamu  hivyo limemwacha Mungu na kumwabudu shetani ndio maana likafananishwa na mwanamke kahaba na kanisa hili sio lingine zaidi ya kanisa katoliki,

 hivyo basi tunaona hapa sio tu kahaba bali pia ni mama wa makahaba,amezaa mabinti ambao ni makahaba kama yeye, nao ni madhehebu yote na mashirika yote ya dini yaliyoiacha kweli ya neno la Mungu na kugeukia mafundisho kama ya mama yao ya kipagani.Leo hii tunaona makanisa yote ulimwenguni yanaungana na kanisa mama yaani katoliki, na kuiunda ile CHAPA YA MNYAMA,ambayo pasipo hiyo huwezi kuuza wala kununua katika kile kipindi cha dhiki kuu,itafika wakati kila mkristo itampasa asajiliwe  katika dhehebu lake kwa yeye kutambulika kama ni mkristo vinginevyo hautaweza kuuza wala kununua wala kuajiriwa,wala kufanya kazi yeyote usipokuwa na hiyo chapa ya mnyama ambayo ni..(utambulisho wako wa kidini au dhehebu lako) pia hautaruhusiwa kuabudu kwa uhuru kama unavyoabudu leo,..kwa yeyote atakayekaidi amri hiyo ataingia katika ile dhiki kuu.

    Na kwa jinsi tunavyoiona dunia ya leo vitendo vya ugaidi vimekithiri kutokana na itikadi kali za kidini, shetani ameunyanyua uislamu kuvuruga amani ya dunia kwa kigezo cha itikadi kali za dini,hivyo basi leo dunia inatafuta mtu wa kuleta amani naye ni lazima awe mtu wa dini ili amalize hili tatazo. na yupo mmoja tu duniani sasa anayekubalika na dini zote naye ni PAPA ambaye anajulikana kama mtu wa amani (man of peace) kiongozi wa kanisa katoliki, baadaye atapewa nguvu na dunia ili maandiko ya daniel 11:21 yatimie “Kisha badala yake atasimama mmoja, mtu astahiliye kudharauliwa, ambaye hawakumpa heshima ya ufalme; naye atakuja wakati wa amani, naye ataupata ufalme kwa kujipendekeza”, ataleta ustaarabu mpya wa dunia wa kuleta amani (NEW WORLD ORDER).

Hapo ndipo itakapompasa kila mtu asajiliwe kulingana na shirika lake la dini na dhehebu lake, kwa dhumuni la kuwatambua watu wote, na kukomesha ugaidi, wengi wataliona kuwa ni jambo zuri bila kujua kuwa ndio wanaipokea ile chapa ya mnyama, lakini baadhi ya wale wakristo waliobaki wasiokwenda katika unyakuo hawatakubali kusajiliwa katika madhehebu ya dini, kwasababu watajua kuwa hiyo ndio ile chapa ya mnyama 666 ndani yake, ni hao tu watakao pitia dhiki kuu wakisingiziwa kuwa wao ndio waondoa amani na magaidi, kwa kutokutaka kusajiliwa kwenye dini zao, watakataliwa na watu wote, hawataweza kuuza wala kununua wala kuajiriwa mahali popote, na mwishoni yule mnyama  atawauwa wote akiwa na roho ya mpingakristo

Mkristo leo hii anayedai kutafuta uhusiano binafsi na Mungu kulingana na papa alivyosema ni “hatari na yenye madhara” hii ni roho ya mpinga Kristo inatenda kazi ndani ya papa ikizungumza maneno haya ya makufuru…dhumuni kubwa ni kuizuia Roho ya Mungu ndani ya watu kutenda  kazi kwa sababu Roho ya Mungu aliachiwa kwa dhumuni moja tu kutuongoza katika kuijua kweli yote.. na pia yeremia 31:34..” Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana;….

Mtu ataijua kweli tu akiwa na Roho Mtakatifu na wala sio kwa kuwa mshirika wa kanisa lolote…biblia inasema  warumi 8:9 “..lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo huyo sio wake.”….warumi 8:14..”kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu” …na wala sio wanaoongozwa na kanisa.

(yohana 14:6 inasema “mimi ndimi njia na kweli na uzima mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi.” hivyo basi hatumfikii Baba kwa njia ya kanisa lolote,wala kwa njia ya kiongozi yoyote wa dini, wala kwa njia ya papa,wala kwa ukatoliki,wala kwa uanglikana,ulutheri,upentekoste,usabato, u-endtime,ubranhamite n.k

  Ukweli ni kwamba KUTOKUWA NA MAHUSIANO BINAFSI NA YESU KRISTO NI HATARI NA YENYE MADHARA MAKUBWA…..

MARAN ATHA!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada zinazoendana:


Mada Nyinginezo:

UTENDAJI KAZI WA MPINGA-KRISTO.

SIKU YA HASIRA YA BWANA.

JE! “MAJIRA NA SHERIA” MPINGA-KRISTO ATAKAYOKUJA KUBALISHA NI KUPINDUA SIKU YA SABATO NA KUWA JUMAPILI?


Rudi Nyumbani

Print this post

MVUTO WA TATU!

Bwana  wetu Yesu Kristo alipokuwa hapa duniani, huduma yake iligawanyika katika sehemu kuu tatu.

Ya kwanza:  huduma ya uponyaji, ishara na miujiza

Ya pili: kueleza siri za mioyo ya watu, kama vile kwa yule mwanamke msamaria,

Ya tatu: kuhubiri neno la Baba yake.

ndugu William Branham alifundishwa na malaika wa Bwana jinsi ya kuvua samaki WAKUBWA kutoka kwenye maji, na yule malaika alimwambia ni kwa namna hiyo hiyo Bwana Yesu Kristo aliitumia kuwavuta watu wake kwake kutoka kwenye dhambi alipokuwa hapa duniani

MVUTO WA KWANZA:

alielezwa kuwa baada ya kuweka mnofu wa kuwavutia samaki kwenye ndoano na kuitupa ndoano  majini baada ya muda kidogo utaivuta juu, wale samaki wadogo wataiona na kuifuata na kuizingira ila wale wakubwa watasogea tu karibu na tukio kuhakikisha kama ni chakula halisi, huo ndio mvuto wa kwanza.

MVUTO WA PILI:

baada ya muda tena kidogo utaivuta ndoano juu tena ila isitoke yote, na wale samaki wadogo waliokuwa wameizunguka ndoano, watakimbia lakini wale samaki wakubwa, watakikaribia na kukila na kunaswa,

MVUTO WA TATU:

baada ya wale samaki wakubwa kunaswa katika mvuto wa pili sasa ni wakati wa kumalizia mvuto wa mwisho.na huu ndio wa kumtoa samaki nje ya maji.

sasa kanisa la Mungu lipo katika mvuto wa tatu ambao ni NENO LA MUNGU, kuandaliwa kwenda kwenye unyakuo, ishara na miujiza haviwezi kutukamilisha hivyo vyote vilikuwa vinatuandaa kwa ajili ya mvuto wa tatu, ambao ni kusikia neno la Mungu,

tunawashauri wakristo wayatazame mafundisho haya, yameelezea vizuri zaidi kuhusu MVUTO WA TATU,

MUNGU AKUBARIKI

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada zinazoendana:

 

 

 


Mada Nyinginezo:

HISTORIA YA WILLIAM BRANHAM

JE! NI DHAMBI KUSHEREKEA SIKU YA KUZALIWA? BIRTHDAY!

JE! NI HALALI KWA MTU WA MUNGU KUTUMIA NJIA ZA UZAZI WA MPANGO?

JE! NI DHAMBI KWA MKRISTO KWENDA HOSPITALI AU KUTUMIA MITI SHAMBA ANAPOUGUA?


Rudi Nyumbani

Print this post

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

Moja ya maagizo muhimu sana ambayo Bwana YESU KRISTO aliyatoa kwa kanisa ni ubatizo.

Mengine yakiwemo kushiriki,kutawadhana miguu kwa wakristo,wanawake kufunika vichwa vyao wakati wa ibada.Kati ya hayo ubatizo ni muhimu sana kwa mwamini yeyote kwa ajili ya ondoleo la dhambi zake.Lakini ubatizo huu shetani ameuharibu usifanyike ipasavyo kwa sababu anajua una madhara makubwa katika kumbadilisha mkristo.na hiyo ndiyo imekuwa kazi ya shetani tangu awali kuyapindisha maneno ya Mungu na kuzuia watu wasimfikie Mungu katika utimilifu wote.

Makanisa mengi leo hii yanabatiza watu au watoto wachanga kwa kuwanyunyuzia maji. Wakibatiza kwa jina la BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU kulingana na mathayo 28:19. “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mtakatifu”..swali ni je! hili jina linatumiwa ipasavyo kubatizia?

Kwa kukosa Roho ya ufunuo na uelewa wa maandiko viongozi wengi wa dini wameacha kweli. Na kugeukia mafundisho ya kipagani na kibaya zaidi wengi wao wanaujua ukweli lakini wanawaficha watu wasiujue ukweli kwa kuogopa kufukuzwa kwenye mashirika yao ya dini. Watu kama hawa ni adui wa msalaba

 Bwana aliowazungumzia akisema 

Mathayo 23:13″ ole wenu waandishi na mafarisayo, wanafki! kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamuingii wala wanaoingia hamwaachi waingie.”

 Tukirejea tena kwenye maandiko

Yohana 5:42-43 “walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu.Mimi nimekuja kwa JINA LA BABA YANGU, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo.”

hapa tunaona dhahiri kabisa jina alilonalo Yesu ni jina la BABA yake. Kwa namna hiyo basi jina la baba yake ni Yesu.

Tukirudi tena kwenye maandiko yohana 14:26 Yesu Kristo alisema “lakini huyo msaidizi,huyo Roho mtakatifu ambaye baba atampeleka  KWA JINA LANGU, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.”na  hapa tunaona Roho Mtakatifu alitolewa kwetu kwa jina la Bwana Yesu. kwahiyo hapa biblia inatufundisha dhahiri kabisa kuwa jina la Roho Mtakatifu ni Yesu.

Na tena kwenye maandiko tunaona kuwa Roho Mtakatifu ndiye Baba mathayo 1:20 “…Yusufu, mwana wa Daudi usihofu kumchukua Mariamu mkeo maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu” kwahiyo Baba ndiye yule yule Roho na ndiye yule yule aliyechukua mwili na kuishi pamoja nasi kwahiyo hapa hatuoni ‘utatu’ wa aina yeyote ambao unahubiriwa leo hii na makanisa mengi.  Mungu ni mmoja tu!.

Kwahiyo jina la Baba ni Yesu na jina la Mwana ni Yesu na jina la Roho Mtakatifu ni Yesu; baba,mwana na roho ni vyeo na sio majina kwa mfano mtu anaweza akawa baba kwa mtoto wake,mume kwa mke wake,babu kwa mjukuu wake lakini jina lake anaweza akawa anaitwa Yohana na sio ‘baba,mume au mjukuu’ vivyo hivyo kwa Mungu.aliposema mkawabatize kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu alikuwa anazungumzia Jina la YESU KRISTO ambalo ndilo jina la baba na mwana na Roho Mtakatifu.

Katika biblia Wakristo na mitume wote walibatizwa na kubatiza kwa JINA LA YESU KRISTO na sio kwa JINA LA BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU. ubatizo huu wa uwongo ulikuja kuingizwa na kanisa katoliki katika baraza la Nikea mwaka 325 AD pale ukristo ulipochanganywa na upagani na ibada ya miungu mingi ya Roma.

Tukisoma matendo ya mitume 2:37-38 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao. wakamwambia Petro na mitume wengine , tutendeje, ndugu zetu? Petro akawaambia, tubuni mkabatizwa kila mmoja KWA JINA LAKE YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”

Tukisoma tena  katika maandiko Filipo alipoenda Samaria na wale watu wa ule mji walipoiamini injili walibatizwa wote kwa jina lake Yesu Kristo matendo 8:12 ” lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habati njema za ufalme wa Mungu na  JINA LAKE YESU KRISTO  wakabatizwa wanaume na wanawake”

Na pia matendo 8:14-17  inasema ” Na mitume walipokuwa Yerusalemu, waliposika ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu.wakawapelekea Petro na Yohana ambao waliposhuka wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila WAMEBATIZWA TU KWA JINA  LAKE BWANA YESU”

Tukirejea tena.

Matendo 10:48  Petro alipokuwa nyumbani mwa Kornelio alisema maneno haya “Ni nani awezaye kuzuia maji,hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vilevile kama sisi? akaamuru WABATIZWE KWA JINA LAKE YESU KRISTO”

Tukisoma tena katika matendo 19:2-6  hapa Paulo akiwa Efeso alikutana na watu kadha wa kadha akawauliza.” je! mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?, wakamjibu, la, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. Akawauliza, basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? wakasema, kwa ubatizo wa Yohana. Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani Yesu. Waliposikia haya WAKABATIZWA KWA JINA LA BWANA YESU”

Mitume wote hawa kuanzia Petro,Yohana,Filipo na mtume Paulo wote hawa walibatiza kwa jina la Yesu Kristo je? tuwaulize hawa viongozi wa dini wanaobatiza kwa jina la baba na mwana na roho mtakatifu wameutolea wapi??? na biblia inasema katika

Wakolosai 3:17 ” na kila mfanyalo kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote  katika Jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu baba kwa yeye”..

hii ina maana tukiomba tunaomba kwa jina la Yesu,tukitoa pepo tunatoa kwa Jina la Yesu, tukiponya watu tunaponya kwa jina la Yesu,tukifufua wafu tunafufua kwa jina la Yesu na tukibatizwa tunabatizwa kwa jina la YESU biblia inasema kwenye

Matendo 4:12 “…kwa maana hapana jina lingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo”

na hakuna mahali popote katika biblia mtu alibatizwa kwa jina la Baba na Mwana na Roho mtakatifu

na maana ya neno ubatizo ni “kuzamishwa” na sio kunyunyuziwa, kwahiyo ni lazima kubatizwa kwa kuzamishwa kwenye maji sawasawa na maandiko na hakuna mahali popote katika maandiko watoto wachanga wanabatizwa. Ubatizo ni pale mtu anapoona sababu ya yeye kutubu na kuoshwa dhambi zake ndipo anapoenda kubatizwa kwa jina la Yesu kwa ondoleo la dhambi zake.

Ewe ndugu Mkristo epuka mapokeo ambayo Yesu aliyaita “chachu ya mafarisayo” penda kuujua ukweli ndugu mpendwa na ubadilike na umuombe Roho wa Mungu akuongoze katika kweli yote usipende mtu yeyote achezee hatima yako ya maisha ya milele, uuchunge wokovu wako kuliko kitu chochote kile,Mpende Mungu, upende kuujua ukweli,ipende biblia..Mwulize mchungaji wako kwa upendo kabisa kwanini anayafanya hayo huku anaujua ukweli na kama haujui mwambie abadilike aendane na kweli ya Mungu inavyosema kulingana na maandiko.

Kama hujabatizwa au umebatizwa katika ubatizo usio sahihi ni vema ukabatizwa tena kwa jina la YESU KRISTO kwa ondoleo la dhambi zako kwani ubatizo sahihi ni muhimu sana..ukitaka kubatizwa tafuta kanisa lolote wanaoamini katika ubatizo sahihi tulioutaja hapo  juu au unaweza ukawasiliana nasi tutakusaidia namna ya kupata huduma ya ubatizo sahihi, karibu na mahali ulipo 0789001312

 Mungu akubariki 

  jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP             

  (ubatizo sahihi wa kuzamishwa na KWA JINA LA YESU KRISTO)

Muhtasari wa maelezo haya kwa njia ya video unaweza kuyapata hapa chini.

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=kuCSAZcnM80[/embedyt]

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada zinazoendana:


Mada Nyinginezo:

MAAGIZO YA BWANA YESU NI BORA KULIKO MAAGIZO YA DAKTARI:

SAUTI AU NGURUMO

JE, KAMA HAUNA UBATIZO SAHIHI HAUWEZI KUWA NA ROHO MTAKATIFU?

JE! NI HATUA ZIPI MUHIMU ZA KUFUATA BAADA YA UBATIZO?

UBATIZO WA MOTO NI UPI?


Rudi Nyumbani

Print this post

MIHURI SABA

Katika kitabu cha ufunuo sura ya tano, tunaona Mungu akiwa ameketi katika kiti chake cha enzi akiwa na kitabu katika mkono wake wa kuume, kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa mihuri saba. Na hapakuonekana mtu yeyote mbinguni wala duniani aliyestahili kukifungua hicho kitabu wala kukitazama,

Ni kitabu kilichobeba siri zote za ukombozi wa mwanadamu,kuanzia mwanzo wa mambo yote hadi mwisho wake, jambo lililomfanya Yohana alie machozi kwa kuwa hapakuona mtu yeyote aliyestahili kukifungua wala kukitazama. Lakini alionekana mmoja aliyestahili kukifungua hicho kitabu, naye ni BWANA YESU KRISTO haleluya!. (soma ufunuo sura ya tano yote.).

kitabu cha MIHURI SABA

MUHURI WA KWANZA:

Ufunuo 6:1-2, “Kisha nikaona napo Mwana kondoo alipofungua moja ya zile muhuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema, kama kwa sauti ya ngurumo, Njoo! nikaona na tazama, farasi mweupe na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda.”

Tunaona kuna wenye uhai wanne na farasi wanne.Wale wenye uhai wanne walioonyeshwa katika sura hii, wanaashiria nguvu ya Mungu iliyoachiwa kwa watu wake, kupambana na uovu na njama za yule adui.Mwenye uhai wa kwanza alikuwa mfano wa simba, na wa pili alikuwa mfano wa ndama na wa tatu kama mwanadamu, na wanne kama tai arukaye.

Kwahiyo muhuri wa kwanza ulipofunguliwa, yule mwenye uhai wa kwanza aliposema njoo! akatoka farasi mweupe, na aliyempanda juu yake ana uta (upinde wa mshale). Na hiyo ni roho ya mpinga Kristo ikianza kutembea katika kanisa la Mungu kwenye kanisa la kwanza, 2thesalonike 2:3 ” Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yeyote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu: akafunuliwa yule mwana wa kuasi, mwana wa uharibifu.”. kwahiyo hapo tunaona kuwa mwisho wa yote usingefika kabla ya ule uharibifu( ukengeufu) kuja kwanza na kuingia katika kanisa.

hii roho ya shetani ilianza kuingia katika kanisa la kwanza baada ya mitume kuondoka hapa Paulo anasema matendo 20:29 ” najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao.” 1Yohana 2:18 aliongezea kusema ” watoto ni wakati wa mwisho na kama vile mlivyosikia ya kwamba mpinga kristo yuaja, hata sasa wapinga kristo wengi wamekwisha kuwapo. kwasababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.

Walitoka kwetu lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wakwetu wangalikaa pamoja nasi.Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.”

Kwa hiyo hapa mitume walilionya kanisa juu ya mafundisho ya uwongo ambayo hayakuhubiriwa na mitume. Hivyo yule farasi mweupe ni roho ya mpinga kristo ikitembea katika kanisa la kwanza, na alionekana mweupe na aliyempanda ameshika uta (upinde). lakini hana mshale, kuashiria kutokuwa na madhara yoyote (yaani kuhusisha mauaji ya watakatifu) . roho hii ilanza kuingia kama mafundisho ya uwongo lakini Mungu aliachia Roho ya kuishinda iliyofananishwa na yule mwenye uhai wa kwanza ambaye ni Simba. Tabia ya simba ni mnyama asiyeogopa, mwenye ujasiri hivyo wadristo wa kipindi kile waliweza kuishinda ile roho ya mpinga kristo kwa ujasiri wa neno la Mungu.

Nyakati hii ilidumu kati ya kipindi cha 53AD-170AD. katika kanisa la kwanza ambalo ni Efeso.

Kristo alitoa pia angalizo kwa kanisa hili tunasoma katika kitabu cha ufunuo 2:2″ nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio ukawaona kuwa ni waongo……lakini unalo neno hili, ya kwamba wayachukia matendo ya wanikolai ambayo na mimi nayachukia.”.

MUHURI WA PILI:

ufunuo 6:3-4 ” Na alipoifungua muhuri ya pili, nikamsikia yule mwenye uhai wa pili akisema Njoo!. akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyeimpanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.”

Hapa tunaona shetani (mpinga kristo), baada ya kuona ameshindwa kuwazuia wakristo wa kweli kumwabudu Mungu katika Roho na kweli wakisimamia neno wakiongozwa na ile nguvu ya Mungu kwa mfano wa simba ambayo ndiyo ile Roho ya Mungu aliyoiachia kwa watu wake kumshinda shetani, Hivyo shetani akabadilisha mbinu zake za kuwashambulia wakristo, kwa kubadilika kutoka farasi mweupe kwenda kuwa farasi mwekundu, na runaona aliyempanda ni yule yule aliyekuwa anamwendesha yule farasi wa kwanza.

Tunasoma kuwa alipewa mamlaka ya kuiondoa amani na upanga mkubwa, kuashiria kuleta dhiki za mauaji kwa wale watu wanaomwamini Mungu na kuzishika amri zake.

Katika utawala wa Roma, Historia inaonyesha kuanzia mwaka 354AD hadi kufikia kipindi cha matengenezo ya kanisa utawala wa Rumi chini ya kanisa katoliki ulifanikiwa kuwauwa wakristo zaidi ya milioni 68, kwa dhumuni la kuimarisha itikadi za dini yao. kwa mtu yeyote kuwa na imani nyingine nje ya dini ya kikatoliki adhabu ilikuwa ni kifo. Wakristo na wayahudi wengi waliuawa kwa kusimamia imani yao. damu nyingi za watakatifu zilimwagika.

lakini Mungu aliachia Roho ya kuweza kuikabili hiyo nguvu ya mpinga kristo nayo ni nguvu iliyofananishwa na ndama. Ndama ni mnyenyekevu sana yupo tayari kwenda kuchinjwa na anaandaliwa kwa ajili ya kutolewa sadaka, hivyo wakristo wengi kwa kutaka wenyewe walijitoa maisha yao kwenda kuuawa kwa ajili ya imani yao bila kuogopa kwani Mungu ndiye aliyeachia hiyo Roho juu yao, walichinjwa, walisulibiwa, waliliwa na simba, waliburutwa lakini jinsi walivyozidi kuwauwa ndivyo walivyozidi kujitoa. warumi 8:36 ” …..kwa ajili yako tunauwa mchana kutwa, tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa” kipindi cha huyu farasi mwekundu kilidumu mpaka mwishoni mwa kanisa la pili.

Na hii roho ya mauaji dhidi ya wakristo bado inatenda kazi hata leo, katika baadhi ya nchi.


MUHURI WA TATU:

Ufunuo 6:5 “na alipoifungua muhuri ya tatu,nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake. Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wa nne, ikisema, kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia, wala usiyadhuru mafuta wala divai.”

Baada ya shetani kuona anawaua wakristo na bado wanaendelea kukubali kwenda kuuawa kwa kuishikilia imani yao akaamua kubadili mbinu ya kulivamia kanisa la Mungu kwa namna nyingine kwa kubadilisha rangi kutoka kuwa farasi mwekundu kwenda kuwa farasi mweusi

Hichi ni kipindi kinachojulikana na wanahistoria wengi kama kipindi cha giza (dark age) kilidumu kwa zaidi ya miaka 1000 kuanzia karne ya 5 mpaka karne ya 16. Ni kipindi ambacho utawala wa kipapa ulianza kuuza kile wanachokiita neno la Mungu kwamfano mtu akitaka kuoa au kuolewa ni lazima atoe fedha, ibada za kuwaombea wafu (ambazo ni kinyume na neno la Mungu) ni lazima utozwe pesa, kushiriki meza ya Bwana ni lazima utoe pesa, ukitaka kusamehewa dhambi unapaswa kutoa pesa, ukitaka kuombewa kama unaumwa ni lazima utoe pesa n.k ndio maana tunasoma yule mpanda farasi alikuwa amebeba mizani mkononi mwake hii inamaanisha kuwa ukitaka kitu lazima utoe kitu. Kwa njia hii kanisa katoliki likiongozwa na utawala wa papa lilijikusanyia utajiri mkubwa sio ajabu hata leo hii tunaona jinsi taifa la Vatican lilivyo na utajiri mkubwa na halifanyi biashara yoyote ya kuliingizia kipato.

Lakini pamoja na hayo Mungu aliachilia nguvu ya kulishinda hilo giza kwa watu wake,na ile sauti iliyosikika ikisema usiyadhuru mafuta wala divai. Mafuta yanaashiria Roho Mtakatifu na divai inaashiria ufunuo wa neno la Mungu, hivyo basi lile kundi dogo la Mungu lililopitia kwenye hichi kipindi kirefu cha giza Bwana aliachia Roho ya ufunuo juu yao kwa mfano wa uso wa mwanadamu ikiashiria hekima ya kibinadamu

Katika hichi kipindi cha giza hadi kwenye matengenezo ya kanisa Mungu alinyanyua watu waliotumia hekima kama Martin Luther alihubiri (mwenye haki wangu ataishi kwa imani) ambapo hapo mwanzo ilikuwa hairuhusiwi mtu yeyote kufundisha au kusoma biblia isipokuwa kwa viongozi tu wa kanisa katoliki tu!.hivyo Mungu aliendelea kunyanyua wengine wengi kama, Zwingli, Calvin, Knox,Bucer n.k kwa ajili ya matengenezo ya kanisa.

MUHURI WA NNE:

Ufunuo 6:7-8 “Na alipoifungua muhuri ya nne, nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wa nne akisema, Njoo! nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu na yeye aliyempanda jina lake ni mauti, na kuzimu ikafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, na kwa hayawani wa nchi.”

Tunaona hapa shetani ambaye ndiye mpinga Kristo alipoanza kubadilika kutoka kwenye farasi mweupe akaenda kwenye farasi mwekundu, akaenda tena kuwa farasi mweusi na sasa amekuwa farasi wa kijivu jivu. Rangi ya kijivujivu inaashiria mchanganyiko wa rangi zote tatu yaani nyeupe, nyekundu na nyeusi. ambayo pia inaashiria udanganyifu na mauti.

Hii ni roho ya mpinga kristo inayotembea sasa katika kanisa hili la mwisho (laodikia), farasi huyu amechanganyikana na anazo tabia zote tatu. Ameitwa kuzimu na mauti inamfuata kwasababu katika hichi kipindi cha mwisho anaonyesha rangi zake zote na kujifunua yeye ni nani kwa kuwaua watu na kuwapeleka kuzimu kwa mafundisho yake ya uongo, akiyaleta makanisa yote pamoja(world council of churches) na kuunda ile chapa ya mnyama. Na bado hazina yote ya dunia ipo Roma hii inaonyesha yule farasi mweusi pia bado anatembea katika utawala wa kanisa katoliki, na ni mwekundu kwasababu anawaua watu katika roho walewe kwa mvinyo wa uasherati wake na kuwafanya watu wengi wawe vuguvugu na bado pia atakuja kuwaua wakristo wengi na wayahudi katika kipindi cha dhiki kuu ambacho kiko mbioni kutokea pale mpinga kristo atakaponyanyuka kwa kupitia utawala wa kiPapa chini ya kanisa katoliki.

Pamoja na hayo Mungu ameachia nguvu ya kupambana na roho hii ya mpinga kristo nayo imefananishwa na Tai. Tai ana uwezo wa kuona vitu vya mbali na Bwana aliwafananisha manabii wake na Tai, hivyo basi katika kanisa hili la Laodikia ambalo ndio la mwisho Bwana ameachia Roho ya kinabii kuweza kuzitambua hila za yule adui, na kuturudishwa katika imani ya mababa na nguvu Mungu aliyoiachia ni ufunuo wa kumtambua Mpinga Kristo na chapa yake na ujumbe wa kutoka kwake na kutokushiriki mafundisho yake ya uongo..ufunuo 18:4 “…tokeni kwake, enyi watu wangu msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” Ikiwa wewe ni mkristo na hauna ndani yako Roho ya ufunuo ya kuona mbali kama Tai huwezi kamwe kumshinda shetani, utaangukia kumezwa na yule mnyama kwa mafundisho yake ya uwongo na unajua ni jambo gani linaambatana naye, biblia inasema ni MAUTI NA KUZIMU, hakuna namna yoyote utakayoweza kumshinda shetani kama upo kwenye mifumo ya madhehebu, umekwisha pokea chapa ya mnyama pasipo wewe kujijua, Kama hauna Roho Mtakatifu mwombe Mungu akupe na Roho ya ufunuo ya kulielewa neno lake.Amen!

MUHURI WA TANO:

Ufunuo 6:9-11 “Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi? Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vilevile kama wao.”

Hapa tunaona hakuna mwenye uhai yeyote akitangaza kufunguliwa kwa muhuri huu, hivyo hatuoni kanisa la mataifa likihusishwa. lakini ulipofunguliwa muhuri wa tano zilionekana roho nyingi chini ya madhabahu zikimlilia Mungu. Hizi roho ni wayahudi waliouawa kipindi cha utawala wa kimabavu wa Hitler (Holocaust), waliuliwa kwa sababu moja tu kuwa wao ni wayahudi, historia inasema Hitler aliwaua wayahudi zaidi ya milioni 6 katika kipindi cha vita ya pili ya dunia.

wana theolojia wengi wanasema kuwa hizi roho xilizo chini ya madhabahu ni wakristo waliouawa katika kipindi cha kanisa la kwanza chini ya utawala wa Roma, lakini hiyo sio kweli, hapa tunaona kuwa hawa walikufa kwa ushuhuda wao, na sio ushuhuda wa Yesu Kristo, na pia hawa wanamwomba Mungu alipize kisasi juu ya maadui zao, kwani kulingana na torati kulipiza kisasi ni desturi ya wayahudi. kwamfano tunaona kuna maandiko yanayosema jino kwa jino, jicho kwa jicho,n.k kwahiyo hatuwezi tukashangaa kwanini hapa walikuwa wanamwomba Mungu alipize kisasi juu ya maadui zao, lakini hiyo siyo desturi ya wakristo. Wakristo hawalaani wala hawaombi kisasi, bali wao husema baba uwasemehe, tunaona mfano wa Bwana wetu Yesu Kristo na Stefano walivyofanya.Hivyo hizi roho zinazozungumziwa hapa ni wayahudi na sio wakristo.

Pia tunaona walipewa nguo ndefu nyeupe, hizi zinaashiria kupewa neema ya wokovu kwa ushuhuda wao wenyewe walioushikilia, kwa lile agano Mungu alilomuahidia Ibrahimu na uzao wake,hawa ni wale wayahudi waliokuwa waaminifu na dini yao ya kiyahudi wakiishikilia torati kikamilifu hata kufa na sio wayahudi wote walio waliouliwa na Hitler walikuwa waaminifu na imani yao warumi 9:6 “Si kana kwamba neno la Mungu limetanguka. Maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli. “

wakaambiwa tena wangojee kwa kipindi kifupi mpaka idadi ya wajoli wao itimie ambao watakufa kama wao.hii inamaanisha katika kipindi cha ile dhiki kuu. Ambayo mpinga kristo atawaua wayahudi wengi na kulivunja lile agano atakalofanya na wayahudi ambalo limezungumziwa katika kitabu cha Danieli sura ile ya tisa.

(Wayahudi wakiwa katika kambi za mateso chini ya utawala wa Hitler,Nazi)

MUHURI WA SITA:

Ufunuo 6:12-17 ” Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi. Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. Na wafalme wa dunia, na wakuu na majemedari na matajiri, na wenye nguvu na kila mtumwa, na mungwana wakajificha katika pango la chini ya miamba ya milima, wakiiambia milima na miamba, tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye akitie juu ya kiti cha enzi, na hasira ya mwanakondoo kwa maana siku iliyokuu ya hasira yao imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?.”

Hapa tunaona muhuri huu ulipofunguliwa dunia nzima iliathirika na ndiyo ile siku kuu ya kuogofya ya Bwana kama Yesu Kristo alivyoizungumzia katika katika mathayo 24:29-30 ” Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi”. Hii siku ya Bwana itakuja mwishoni mwa miaka mitatu na nusu baada ya kumalizika ile dhiki kuu

Siku hii ya Bwana itadumu kwa kipindi cha siku 75. ikianzia kwa kumimina ghadhabu ya Mungu katika dunia, ambayo itahusisha vita vya harmagedoni. (ufunuo 19-21, zekaria 14:1-4, 12).ndani ya siku hizi 75 kutakuwa pia na kufufuliwa kwa watakatifu waliouawa katika kipindi cha dhiki kuu (ufunuo 11:18, 20:4). itamalizia na hukumu ya mataifa (mathayo 25:31-46) kabla ya kuingia katika matengenezo ya utawala wa miaka 1000 wa Bwana Yesu Kristo (mathayo 19:28).

hizi siku 75 zinapatikana kutoka katika zile siku 1335 zilizozungumziwa katika kitabu cha daniel 12:12. siku hizi 1335 ukitoa siku 1260 (au miezi 42) ambayo mpinga kristo atatawala baada ya kuikomesha sadaka ya kuteketezwa ya daima daniel 9:24-27″……Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.”

MUHURI WA SABA:

Ufunuo 8:1 “Hata alipoifungua muhuri ya saba, kukawa kimya mbinguni kama muda wa nusu saa. “

Mstari wa pili unaelezea juu ya wale malaika waliojiweka tayari kupiga baragumu ambayo ni habari nyingine isiyohusiana na muhuri wa saba, Huu ukimya mbinguni unaashiria kuna jambo linakwenda kutokea ambalo ndilo tunaloliona katika ufunuo sura ya kumi.

katika sura ya kumi.ufunuo 10:1-4 “Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake; na uso wake ulikuwa kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto. Na katika mkono wake alikuwa na kitabu kidogo kimefunguliwa. Akaweka mguu wake wa kuume juu ya bahari, nao wa kushoto juu ya nchi. Naye akalia kwa sauti kuu, kama simba angurumavyo. Na alipolia, zile ngurumo saba zikatoa sauti zao. Hata ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika. Nami nalisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Yatie muhuri maneno hayo yaliyonenwa na hizo ngurumo saba, usiyaandike.”

Malaika huyu anayeonekana hapa si mwingine bali ni Bwana Yesu Kristo akiwa ameshika kile kitabu kidogo. Na ndani ya muhuri huu wa saba ambao bado haujafunuliwa kwetu kwa sasa lakini utakapokuja kufunuliwa utampa bibi arusi wa Kristo imani ya kwenda katika unyakuo(ambayo siri hii imejificha katika zile ngurumo saba Yohana alizoambiwa asiziandike).Na muhuri huu wa saba utatimia kabla ya muhuri wa sita kutimia, kwasababu muhuri wa sita unaelezea siku kuu ya Bwana ambayo ni mwisho wa mambo yote.

kulingana na 1thesalonike 4:16-17 “Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele”.

Kuja kwa Bwana kutafuata hatua tatu, ya kwanza ni Bwana atakuja na mwaliko(shout) na ya pili ni sauti ya Malaika Mkuu na ya tatu ni parapanda ya Mungu. Hatua ya kwanza ya mwaliko ndiyo tuliyopo sasa hivi iliyoletwa na Mjumbe wa kanisa la saba(William Branham) yenye ujumbe wa kutuandaa sisi kumpokea Kristo na kuturudisha katika ukristo wa biblia.

Mathayo 25:6 “Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki” Mjumbe wa kanisa la saba alikuja kututangazia ujio wa Bwana Yesu Kristo ni wakati wa sisi kuzitengeneza taa zetu na kuwa tayari kumlaki Bwana Yesu mawinguni.

Hatua ya pili ni sauti ya Malaika mkuu. na ndiye tunayemwona katika ufunuo 10 na si mwingine zaidi ya Yesu Kristo. Na ujumbe wake utakuwa kwa yule bibi arusi aliyekwisha kujiweka tayari kumlaki, bikira safi ambaye taa yake inawakaa, huyu ni mkristo aliyebatizwa na Roho Mtakatifu. aliyejitenga na uasherati wa yule kahaba(katoliki na madhehebu yote) yasiyofanya neno la Mungu kuwa mwongozo wao na kushikilia mafundisho ya wanadamu na ibada za kipagani. Huyu bibi arusi pekee ndiye atakayeisikia sauti ya malaika mkuu ambayo itahubiriwa na zile ngurumo saba tunazoziona katika kitabu cha ufunuo 10:3-4 Yohana alizoambiwa asiziandike lakini mwingine yoyote asiye bikira mwenye busara hatoweza kuisikia sauti ya hizo ngurumo saba.

Ngurumo saba ni Sauti za watu saba ambao Mungu atawanyanyua katika kipindi hichi cha mwisho na kuleta uamsho duniani kote, ambazo kupitia hizi sauti saba tutapata imani itakayotuwezesha sisi kwenda katika unyakuo. Na hizi ngurumo saba zipo karibuni kutoa sauti zake..je? umejiweka tayari? unaye Roho Mtakatifu? watakaoweza kuupokea ujumbe wa ngurumo saba ni bibi arusi tu mwenye Roho wa kristo. Na wakati huo ukifika kutakuwa hakuna muda tena, ni wakati wa wewe kutengeneza mambo yako sasa vizuri kwa Bwana.

Hatua ya tatu na ya mwisho ni parapanda ya Mungu. katika kipindi hichi kila mmoja wetu aliye mkristo ataisikia sauti ya Mungu ikimwita na gafla tutaona mabadiliko ya miili yetu na kuchukuliwa juu mbinguni kwa Bwana milele na milele haleluya!.

Shalom!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

ROHO ZILIZO CHINI YA MADHABAHU:

MWANZI ULIOPONDEKA.

NENO “MASHEHE” TUNALIONA LIKITAJWA KATIKA BIBLIA(AGANO LA KALE); HAWA MASHEHE NI WAKINA NANI?

JE! NI SAHIHI KWA MKRISTO KUOA/KUOLEWA NA MTU WA IMANI NYINGINE?


Rudi Nyumbani

Print this post

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?

Kuna tofauti kati ya UBATIZO wa Roho Mtakatifu na UPAKO wa Roho Mtakatifu.

Watu wanachanganyikiwa wakidhani kuwa na upako, au nguvu za Roho Mtakatifu, ndio Umebatizwa na Roho Mtakatifu. Lakini hii sio kweli, mtu anaweza kuwa na upako wa Roho Mtakatifu, akaponya magonjwa, akafufua wafu, akanena kwa lugha, akaona maono, akatabiri au kuota ndoto na ikaja kutokea, na bado asiwe amebatizwa na Roho Mtakatifu. Tunaona kabla ya Pentekoste wanafunzi wa Yesu ikiwemo Yuda aliyemsaliti Bwana walikuwa wanafanya ishara zote hizi na bado walikuwa hawajabatizwa na Roho wa Mungu..

Biblia inasema Mathayo 5:45

“…..maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.”

Hii ni SIRI kubwa sana inayozungumzwa hapo, Bwana anaachia nguvu zake kwa waovu na wema, anaachilia nguvu zake za uponyaji,miujiza, kwa wote waovu na wema n.k. Hivyo kigezo cha mtu kufanya ishara na miujiza si tiketi ya yeye kuwa mwana wa Mungu, Bwana aliwaambia wanafunzi wake..

Luka 10:20″ Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.”

Unaona alituambia tusifurahi kwa sababu miujiza inatendeka na sisi bali kwasababu majina Yetu yameandikwa mbinguni hii ikiwa na maana,tunapaswa tufarahi tunapokuwa na mahusiano na Mungu na uhakika wa kwenda mbinguni na sio tunapokuwa na uwezo wa kutoa pepo au kufanya miujiza.

Katika kipindi hichi cha mwisho shetani amefanikiwa kuwadanganya wengi kwa njia hii, kwa kushindwa kutofautisha ubatizo halisi wa Roho Mtakatifu na Upako wa Roho Mtakatifu, si jambo la kushangaza kuona mtu anatoka kuvuta sigara na akaenda kunena kwa lugha, nabii katoka kuzini na bado akaenda kutoa unabii na huo unabii ukatimia kama ulivyo, mtu katoka kwenye ufisadi na akaenda kumwombea mtu akafufuka na bado anaota ndoto, ishara na miujiza vikifuatana naye, mtu katoka kutukana na bado akaenda kufundisha,na kutoa mapepo na bado nguvu za Mungu zikashuka na watu wakafunguliwa katika vifungo vyao..

lakini hiyo sio uthibitisho ya kwamba mtu huyo amepokea Roho Mtakatifu usidanganyike. Mungu anaweza kutumia chombo chochote kutenda kazi yake kama chombo cha kuazima tu, kazi ya hicho chombo ikiisha Mungu anaondoka. Kwa mfano tunaona katika biblia Mungu alimtumia Punda kuzungumza na Balaamu, lakini baada ya kuupeleka ujumbe yule punda akarudia katika hali yake ya mwanzo ya upunda.

Hivi ndivyo watu wanavyotumiwa na Mungu kama vyombo vya kuazima lakini wasiwe watu halisi wa Mungu, wamenyeshewa tu ile mvua ya upako ambayo inawanyeshea wote waovu na wema. Hii ni SIRI kubwa watu wanapaswa waijue.

Bwana Yesu alisema

Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.

Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.”

Mstari huu unajieleza wazi kabisa juu ya watu wanaojidhani kuwa wanafanya miujiza na ishara ndio uthibitisho kuwa wao ni wana wa Mungu.

LAKINI UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU NI UPI?

Uthibitisho wa Roho Mtakatifu pale anaposhuka juu yako anakufanya uwe kiumbe kipya (uzaliwe mara ya pili), anasafisha ile hali ya kutamani dhambi na kukufanya uwe mtakatifu na pia atakuongoza katika kuijua kweli yote tusome..

 Yohana 16:12 “Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa.
13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari”.

Jambo la kwanza Mkristo yeyote aliyepokea Roho Mtakatifu lazima Roho amuongoze katika kuijua ukweli, ikiwemo uelewa wa maandiko,kiu na shauku ya kumjua Mungu siku baada ya siku.na kufanywa ufanane na Yesu Kristo. Roho ya mafunuo itakuja juu yake, Hatafungwa na mambo ya dini bali na NENO la Mungu tu, na Roho atamweka mbali na ulimwengu, yaani kiu ya kuupenda mambo ya ulimwengu itaanza kufa ndani yake.

Jambo lingine ni Roho atashuhudia ndani yake kuwa yeye ni Mwana wa Mungu ( atakushuhudia katika maisha unayoishi)

Warumi 8:15 “Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.
16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu”;

Mtu huyo ataondokewa na hofu ya maisha kwa kuwa anajua anaye baba mbinguni, na Baba anamshuhudia ya kuwa yeye ni mtoto wake ndani yake. 

Kuna watu angali wakijidanganya kuwa wana Roho Mtakatifu lakini wamekosa haya mambo, ndani yao tamaa ya mambo ya ulimwengu imewavaa, Hawana uhusiano wowote  wao na Baba yao wa mbinguni, hofu na masumbufu ya maisha haya yamewasonga kana kwamba hawana Baba mbinguni, Wanalipinga siku zote NENO la Mungu, kuthibitisha dini zao na madhehebu yao(mfano wa mafarisayo na masadukayo), Hawapendi kuijua kweli halisi ya injili inayowapeleka watu mbinguni bali injili za pesa na mafanikio ya ulimwengu huu tu.

Sasa watu kama hao ni dhahiri kuwa hawajashukiwa na Roho wa Mungu bado, haijalishi wanafanya miujiza kiasi gani. Sio kwamba kuwa na hizo ishara ni mbaya, tofauti ni hii hawa wanakuwa wamenyeshewa mvua tu lakini hawana Roho, na wale waliobatizwa kweli kweli wanakuwa na vyote, 

Hivyo basi Roho wa Mungu anaposhuka juu ya mtu kwa mara ya kwanza huyo mtu anaweza akaanza kunena kwa lugha, au kuona maono, au kutabiri au akapata msisimko, au kushukiwa na nguvu za Mungu nyingi ndani yake,au akapata hisia ya tofauti ambayo hakuwahi kuisikia hapo kabla, wengine wakati Roho akishuka juu yao amani ya kipekee inawashukia,wengine hawasikii chochote lakini watafahamu kwa jinsi Roho wa Mungu anavyougua ndani yao, haya yote ni udhihirisho wa nje ambao hata wale wengine(magugu) wanaweza kuupata.

Lakini uthibitisho halisi ni jinsi maisha yako yatakavyokuwa yanaanza kubadilishwa na kufanywa kiumbe kipya siku baada ya siku kwa kutakaswa kwa Neno. na ubatizo wa Roho Mtakatifu unaambatana na karama za Mungu lakini kama tulivyosema mtu anaweza kuonyesha zile karama za Roho na asiwe amebatizwa na Roho Mtakatifu.

Na kuna mtazamo pia ya kuwa “kunena kwa lugha” kuwa ndio uthibitisho wa mtu kupokea Roho Mtakatifu, mtazamo huu si kweli mtu anaweza kunena kwa Lugha na asiwe amepokea Roho Mtakatifu kwasababu hichi ni kipawa cha Roho na kinamshukia yeyote kwa jinsi Roho alivyomjalia mtu, kumbuka hata mashetani wananena kwa lugha, Na kipawa hichi sio lazima kila mtu awe nacho,

kwasababu biblia inasema 

1wakoritho12:28 “Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.
29 Je! Wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza?
30 Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri”?

Si unaona hapo sio wote wenye hicho kipawa cha kunena kwa Lugha. Kwahiyo mtu anaweza akabatizwa na Roho Mtakatifu na asinene kwa lugha, bali akaonyesha karama nyingine tofauti na hiyo, aidha unabii, au karama ya uponyaji, au neno la maarifa, au miujiza n.k. kwa jinsi Roho atakavyokujalia.. Mafundisho ya kwamba kila mtu lazima anene kwa lugha sio sahihi mwisho wa siku kama mtu hajapewa hicho kipawa anaishia kunena kwa akili zake tu, na kutakuwa hakuna kufasiri 1wakoritho 14.

Kwahiyo mpendwa kama haujabatizwa na Roho Mtakatifu mwombe Bwana naye atakupa Luka 11:9-13..”Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa. Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.

Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki, badala ya samaki atampa nyoka? Au akimwomba yai, atampa nge? Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?” 

Kumbuka kutoa zaka, kusaidia yatima, kuhudhuria ibada kila jumapili, hayo hayatoshi hata watu wasioamini wanafanya hayo na zaidi ya hayo(mfano mzuri ni waislamu)

soma….

Mathayo 5:20″ Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. “

Hii haki inakuja kwa kuzaliwa mara ya pili, hauwezi kuingia katika ufalme wa mbinguni pasipo hiyo, na ukishabatizwa na Roho Mtakatifu ndio kuzaliwa mara ya pili.

Matendo 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.”

Kumbuka Roho mtakatifu ndiye MUHURI wa Mungu, (maana ya neno MUHURI ni kwamba “KAZI IMEKAMILIKA JUU YAKO”).waefeso 4:30 “Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi”. Pasipo huyo hauwezi kwenda mbinguni, kwa sababu biblia inasema warumi 8:9 “……….Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake”. 

Mungu akubariki!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

HATUA ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTUONGOZA

ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.

JE! KARAMA NI UTHIBITISHO WA KUWA NA MUNGU?

JIPE MOYO.

BWANA ALIPOSEMA “SIKUJA KUTANGUA TORATI BALI KUITIMILIZA” ALIKUWA ANAMAANISHA NINI?

rejeabiblia.com


Rudi Nyumbani

Print this post